Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 22 | 23 | (Page 24) | 25 | 26 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 02/04/13--10:31: Mdau Linda anatafuta mchumba

 • Habari yako kaka Michuzi jr. Mimi naitwa Linda naishi nje ya Tanzania kwa sasa, nimeona na mimi nijitokeze  kwenye blogu yako kuwa natafuta rafiki ambaye Mungu akijalia tunaweza kufika mpaka kwenye ndoa. Kwa kweli natafuta rafiki ambaye anajitambua, yupo serious na maisha, ambaye hajawahi kuoa wala hana watoto. 

  Mwenye kupenda maendeleo na mwenye malengo ya maisha. Umri wake uwe kuanzia miaka 35 na kuendelea. Awe mwepesi sana wa mawasiliano. Asiwe mbabe na pia awe mpole na mwenye kujiheshimu.Yule ambaye hayupo serious tafadhali naomba asiniandikie. Elimu kuanzia chuo kikuu.
   
  email yangu ni:

  0 0

  Shamba lenye ukubwa wa heka moja na nusu linauzwa maeneo ya Kiromo, Bagamoyo, liko jirani na Kiromo View Resort kwenye barabara kuu iendayo Bagamoyo mjini, kiasi cha 10 tu. Lina kibanda cha vyumba vinne, linafaa kwa uwekezaji wa shughuli mbalimbali za kibiashara, kwani liko barabarani kama picha zinavyoonesha. Bei ni maelewano.
  KWA MAELEZO ZAIDI, PIGA SIMU: +255 657 803139

  0 0


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuzindua  ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.

   Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Phillipe Dongier akitoa hotuba kwa kiswahili fasaha wakati wa sherehe za  uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw Phillipe Dongier, wakifunua kitambaa cha jiwe la msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa Kigoma wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw Phillipe Dongier, wakipiga makofi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na viongozi wengine baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw Phillipe Dongier, wakisalimiana wakati wa kuweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
    Msanii Diamond na kundi lake wakitumbuiza wakati wa sherehe za  uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi mbalimbali wakipata maelezo juu ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma toka kwa mhandisi George Sambali
  wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Muungano eneo la Kibaoni wilayani Uvinza, Kigoma, akiwa njiani kuelekea mjini Kigoma, akitokea kukagua ujenzi wa daraja la Mto Malagarasi leo.


  0 0

  Afisa mauzo wa Ecobank Jackline Nyangoe (kushoto) akifafanulia jambo wageni waliofika katika banda la maonyesho la benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Februari 3 2013.
  Wakazi wa Dar es Salaam na wageni mbalimbali wakiangalia bidhaa za benki ya Ecobank katika banda la maonyesho la benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina zilizofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam juzi.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata taarifa kutoka kwa Balozi wa China Nchini Tanzania Lu Yuquing wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, na Kaimu Mkuu wa Mkoa, Pia Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. (Picha na Mpigapicha Wetu)
  ---
  Ecobank Tanzania ambayo ni mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33 Africa, inazidi kukuza uwezo wa wanabiashara Tanzania katika kushiriki biashara kati ya Tanzania na China kwa kupunguza garama za uendeshaji biashara kati ya nchi hizi.

  Wakishiriki katika sherehe ya mwaka mpya ya China Jumapili hii katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Ecobank ilionyesha nia yake ya kusaidia jamii ya waendesha biashara kati ya Tanzania na China zikiwepo huduma zinazorahisisha wafanyabiashara wa Tanzania na wawekezaji wa Kichina kushiriki katika uagizaji na mauzo ya nje kati ya nchi hizi.

   "Sisi tunayo nia ya kutoa huduma za garama nafuu na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hizi kuwezesha sekta hii inayokua kwa kasi sana. katika mwongo uliopita kumekuwa na uwekezaji wa $ 868 bilioni wa china ndani ya Tanzania, huduma zetu zinajaza pengo la kurahisisha biashara hii "anasema Bw Enoch Osei-Safo, Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Tanzania.

  Ecobank inazindua huduma ya kubadilisha hela ya Tanzania kupata sarafu za kichina (RMB) moja kwa moja, ambapo hapo awali hapa Tanzania, wanabiashara walilazimika kubadili TZS kwa Dola za kimarekani ili kununua RMB. Katika mfumo huo wa awali, wanabiashara walipoteza kiasi kikubwa cha mtaji lakini sasa, Ecobank itatwawezesha wanabiashara kupunguza garama hizi kwa kueneza huduma hii hapa Tanzania.

  " Sisi hatuwezi kupuuza matokeo ya biashara ya China juu ya Afrika, ambayo inafikia zaidi ya dola bilioni 200 katika mwaka 2012 kwa uagizaji na 5% ya mauzo yote ya Afrika kwenda nchini China, ushirikishwaji wa kifedha kukuza sekta hii ni muhimu, na ndiyo maana Ecobank Group imeonyesha nia ya kurahisisha uendeshaji wa biashara hii na kuwezesha Afrika kuwa na ushindani na nchi zingine duniani.” Enoch aliongeza.

  Ecobank Tanzania katika miezi michache ijayo itakua kituo cha kutoa huduma za uendeshaji biashara kati ya Tanzania na China kwa kutoa huduma ya ubadilishaji wa sarafu ya kichina na pia kulipia kodi ya forodhani kwa TRA papo kwa papo kupitia huduma ya Asybank katika matawi yote ya Ecobank.

  0 0


   Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu NBTS Dk. Efesper Nkya akimkabidhi cheti cha kushukuru mchango wa tigo kuchangia damu mkoa wa Lindi mwaka jana kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez kulia ni bi. Woinde Shisael Afisa wa  Ushirika wa Jamii wa Tigo.

  TigoTanzania leo imekabidhiwachetichashukrani kutoka kwa Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwamsaadawake mkubwa wa kuhamasisha umma juu yaumuhimu wa kuchangia damukupitia mpango wa kuchangia damu salama  ambao ulifanyikakatika mkoa wa Lindi mwezi mwaka jana.


  Mpango huuulifanyika katika mkoa wa LindiUwanja wa ILULU, na ulianza tarehe 25 Novemba 2012  naulihitimishwaDesemba 1, 2012 kuashiria sikuya Ukimwi Duniani. Lengo kuula zoezi hilo lilikuwakuwaalika nakuhamasisha wachangiaji wa damu kwa njia ya hiari,pamoja nakutoafursa kwa wanajumuia kupima VVUnakuelimishwabure juu yaumuhimu watabiahatarishizamaambukizi ya VVU. 

  Mpango huu ulikuwa na mafanikio makubwakwani zaidi yauniti 300zadamuzilikusanywakutoka kwa waleambao walishiriki.Maadhimisho ya mpango huo yaliongozwa na mheshimiwaRais wa Jamhuri yaMuunganowaTanzania, Dr JakayaMrishoKikwete,ambaye alikuwamgeni rasmikatikaSiku yaUkimwidunianiiliyofanyika  mkoa wa Lindi mwaka jana.


  Mpango huo ulifanikiwa kuwaelimisha wanajamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu na jinsi zoezi rahisi kama hili linaweza kuokoa maisha ya mwanadamu, kwa kupunguza vifo vya uzazi, watoto wachanga, na mama wajawazito kwa kiwango cha  asilimia 80% kati ya wapokeaji damu. 

  "Sisi kama Mpango wa Taifa wa Damu Salama tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu kwa Tigo Tanzania kwa msaada wao mkubwa katika programu hii na imeonyesha kwamba  wao wana moyo wa kuwasaidia Watanzania kuhakikisha wanaishi maisha bora na afya njema", alisema Dk Efesper Nkya,Meneja wa Programu NBTS wakati akikabidhi cheti.


  Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bwana Diego Gutierrez alisema akipokea cheti kuwa “kamaTigotunajisikiaheshima nafahari kubwa kuwa sehemuyampango huu wa kuhamasisha ummajuu yaumuhimu wamchangowa damusalama, na tunafurahi kuwachangia Watanzania ili waishimaishaboranaafya njema.Ni furahakubwa kwangu mimikukubalihati yashukranikwa niaba yaTigo Tanzaniananapenda kuchukuafursa hiikushauri na kuwahamasisha Watanzaniawotekuchangia damu salama, kwanimchango wao unaweza kuwasababu kubwa katika kuokoa maisha  ya mwanadamu mwingine".  Kuhusu Huduma ya kutoa Damu ya Taifa:


  NBTSilianzishwa mwaka2004nani mpangochini yaWizara ya AfyanaUstawi wa Jamii(MoHSW) na mamlakayakuhakikisha upatikanaji wadamu salama ya kutoshakupitiaserikali kuuni uratibu wahuduma ya kuongezewadamunchini Tanzania.

  Malengo makuu ni:

  1. Kuongeza uwezo wa kukusanya, usindikaji na kusambazaji wa kutosha wa damu salama na damu kutoka kwa wafadhili wa hiari ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa.
  2. Ili kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kutosha na kupatikana ya damu salama kutoka kwa  wafadhili  wa  damu  kutokana na idadi ya watu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  3. Kuanzisha ufuatiliaji na tathmini ya mfumo wa kudumisha ubora, na ufanisi wa Huduma ya
  Damu ya Taifa.


  NBTS inafanya kazi nchi nzima na JWTZ na TRCs kama washirika wake kupitia vituo vyake sita ambavyo ni  Kanda ya Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Mtwara, Mbeya na Moshi.
  Kama mdau TACAIDS wamechangia sana katika kuzuia VVU / Ukimwi, tangu kuanzishwa kwake, na kupunguza kwa kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU, na ni miongoni mwa wafadhili damu kutoka% 7-10 mwaka 2004 hadi 1.2% katika 2012.  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Bi. Irina Bokova's (kushoto) akitoka katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro akiwa ameambatana na Msaidizi wake pamoja Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka (kulia) tayari kuanza rasmi ziara yake nchini mapema leo asubuhi.

  Bi. Irina Bokova's akiingia kwenye gari tayari kuanza rasmi ziara yake.

  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka kabla ya kuanza mkutano na Menejimenti ya Umoja wa Mataifa nchini katika Ofisi za Shirika la UNESCO Tanzania. Kushoto ni Bi. Irina Bokova's.

  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (kushoto) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's ( wa pili kushoto) ofisini kwa Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (kulia) kabla ya kuanza mkutano na Menejimenti ya Umoja wa Mataifa pamoja na wafanyakazi wa Ofisi za UNESCO Tanzania.

  Dkt. Alberic Kacou akizungumza jambo na Bi Irina Bokova's kwenye ofisi za UNESCO Tanzania mapema leo asubuhi.  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi.Irina Bokova's akisalimiana na baadhi ya viongozi wa matawi ya Umoja wa Mataifa nchini kabla ya kuanza kwa mkutano.

  Bi. Irina Bokova's akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa matawi ya Umoja wa Mataifa nchini.

  Bi.Irina Bokova's akiendesha kikao cha Menejimenti ya Umoja wa Mataifa nchini na kugusia Agenda muhimu za kuboresha sekta ya Elimu nchini. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen.

  Mkutano ukiendelea.

  Baadhi ya viongozi wa matawi ya Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini.

  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi.Irina Bokova's na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka wakiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Menejimenti ya Umoja wa Mataifa nchini.

  Bi. Irina Bokova's akisalimiana na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin wakati wa mkutano na wafanyakazi wa UNESCO uliofanyika katika Ofisi za shirika hilo nchini.

  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's akimsalia mmoja wa wafanyakazi wa UNESCO Tanzania Bi. Rahma.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi za UNESCO nchini wakisikiliza nasaha za Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's (hayupo) mapema leo asubuhi.
  Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj (kushoto) akimuongoza kuelekea kwenye chumba cha mikutano kuzungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaa.
  Bi. Irina Bokova's akisalimiana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa.
  Bi.Irina Bokova's akiwa kwenye mkutano na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa ( wa pili kushoto) na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) wakijadili changamoto mbalimbali na mbinu mbadala za kunyanyua sekta ya elimu nchini kwa kusaidia na Shirika lake la UNESCO.
  Bi.Irina Bokova's akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
  Bi.Irina Bokova's akifanyiwa mahojiano na Capital Television baada ya mkutano wake na mawaziri hao.
  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa tayari kuelekea visiwani Zanzibar.

  0 0


   Baadhi ya Wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja,mapema leo asubuhi mara baada ya kumaliza mkutano wao na Wanahabari ndani ya ukumbi wa hoteli ya Bell Monte,jijini Dar.
  Mmoja wa wasanii mahiri,Mr Blue,ambaye pia  atashiriki kutumbuiza kwenye tamasha hilo akitoa vionjo kwa Wanahabari (hawapo pichani). 
   Mratibu wa tamasha hilo kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Lumuliko Mengele a.k.a Dj Mully B akifafanua kuhsiana na maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika kwenye ufukwe wa Coco beach,februari 10 jijini Dar Es salaama,Shoto kwake ni baadhi ya wasanii watakaoshiriki tamasha hilo.
  Pichani shoto ni Meneja wa chapa ya Tigo Bwana William Mpinga akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi huo akisema "Tigo ina fahari kubwa kwa jinsi ambavyo inawajali na kuwapa thamani wateja wake kupitia bidhaa zake mbalimbali za mawasiliano.

  Tigo kufanya tamasha kubwa la Muziki kuzindua msimu wa Tabasamu!


  Kampuni ya simu za Mikononi ya Tigo inatarajia kufanya tamasha kubwa la kuzindua msimu wa Tabasamu ambao umetokana na Tigo kubadilisha kauli mbiu yake ya zamani kutoka Jielezee mwenyewe” kuwa “Tabasamu! upo na Tigo”.

  Meneja wa chapa ya Tigo Bwana William Mpinga alielezea kuhusu uzinduzi huo akisema "Tigo ina fahari kubwa kwa jinsi ambavyo inawajali na kuwapa thamani wateja wake kupitia bidhaa zake mbalimbali za mawasiliano. Mabadiliko haya ya kauli mbiu yanatupa fursa ya kuonyesha dhamira yetu ya kuwajali Watanzania pamoja na kuwahakikishia kwamba tutakuwa nao sambamba kwa kila jambo, wakati wote. Wateja wetu ni msukumo wa kila tufanyacho Tigo, hivyo tunajitahidi kuhakikisha tunawatimizia mahitaji yao yote ya mawasiliano. Lengo letu linabakia kujenga na kutoa huduma za unafuu , zinazopatikana kila mahali na kwa wote."

  "Uzinduzi wa msimu huu wa Tabasamu unalengo la kuhakikisha watu wengi zaidi wanatabasamu kutokana na bidhaa zetu zenye thamani, mtandao wenye ubora wa juu na huduma nzuri kwa wateja kama ishara ya shukrani kwa nafasi yetu muhimu kwenye maisha ya  Watanzania. Tumekuwa ni sehemu ya maisha yako na tunataka kuwa na wewe siku zote hivyo Tabasamu, upo na Tigo! " Alihitimisha Bwana Mpinga.

   Tamasha hili litafanyika katika ufukwe wa Coco (Coco Beach) Jumapili ya tarehe 10 Februari 2013 kutoka  saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni na litashirikisha burudani kali kutoka kwa Enika, Roma Mkatoliki, TMK Wanaume, Tip Top Connection, Juma Nature, Recho, Mr. Blue na wachezaji dansi wa THT .
  Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa Tigo bwana Alex Msigara alisema juu ya tamasha kwamba "ukiachana na burudani kutoka kwa wanamuziki hao mahiri vilevile kutakuwa na zawadi kubwa za kushindaniwa na promosheni na ofa za kusisumua. Tutakuwa na bidhaa na huduma mbalimbali za ofa za Tigo hivyo tunatarajia ujio mkubwa na tunawahakikishia burudani kali ya kuanza mwaka na tabasamu”

  Msimu huu wa tabasamu unahusisha ofa, promosheni, zawadi na bidhaa mbalimbali za thamani kutoka Tigo ambazo zitawalenga wateja wa vipengele vyote na mahitaji yao yote.


  0 0


  Naomba kuuliza wizara ya elimu watueleweshe kuhusu maana ya michango ya ushirikishi shuleni kila siku. maana katika shule ya msingi Boko wilaya ya kinondoni imekuwa ni kero kwa watoto na wazazi watoto wanapigwa kwa ajili hilo mfano darasa la saba kila siku asubuhi ni lazima waende na sh. 300 na wanaambiwa ni lazima vinginevyo wanapigwa sasa nimepiga mahesabu kama watoto ni 300 kila siku kila kipindi kinakusanya sh. 300 x 300 = 90,000/= hizo hela zinaenda wapi.

  Ukiuliza wazazi wanasema kwenye kikao cha shule walisema sio lazima  kwa hiyo aina maana mzazi asipompa mtoto hela lazima apigwe. Nawaomba Wizara ya Elimu watueleweshe kama ni kitega uchumi cha walimu? au inakuwaje?
  Mdau 

  0 0


  Kwa niaba ya CCM UK Napenda kutoa salamu za kusheherekea miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwa watanzania wana CCM wote na popote pale duniani. 
  Nimeattach maelezo mafupi ya salamu zetu toka hapa CCM UK.
  Ni matumaini nitapata ushirikiano wa kutosha kufikisha salamu hizi.

  Wasalaam

  Abraham Sangiwa
  ..........................................
  Nb. Katibu Itikadi Siasa na Uenezi
  Chama Cha Mapinduzi Tawi la Uingereza

  0 0  Mhe. Balozi Tuvako Manongi, akimsomea  Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar maneno yaliyoandikwa kwenye zawadi ambayo  alipewa na  Maafisa Wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa wakati wa hafla fupi ya kumuanga na kumshukuru Balozi Maajar kwa  ushirikiano mzuri wa kikazi baina ya  Balozi hizo mbili. Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki hapa New York.


  =====   ======  ======    ======

  WATANZANIA MAREKANI JIANDAENI KUTOA MAONI YA KATIBA-MAAJAR


  Na Mwandishi Maalum.


  Watanzania wanaoishi nchini Marekani wametakiwa kujiandaa kutoka maoni yao kuhusu Katiba mpya  pale muda  wa  kufanya hivyo utakapofika .Wito huo umetolewa na  Balozi wa Tanzania nchi Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar wakati  wa hafla fupi ya kumuaga iliyokuwa imeandaliwa na Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa pia na  viongozi wa  Jumuiya ya Watanzania  New York.

  “    Ninapoagana nanyi,  napenda kutumia fursa hii kuwahimiza  mujiandae kutoa maoni yenu.Mabalozi tumepokea   taarifa ya kwamba watanzania waishio ughaibuni  nanyi pia  mtapata fursa ya kutoa mchango wenu na kwamba wajumbe wa Tume ya kukusanya maoni watafika kusikiliza hoja zenu. Rai yangu ni hiyo jiandaeni”. Akasisitiza Balozi Maajar.


  Akizungumza zaidi  kuhusu uhusiano kati  watanzania waishio Marekani na Ofisi za Ubalozi,  kwanza, Balozi Maajari amewataka watanzania wenyewe kwa wenyewe kuheshimiana, kusaidiana, na kupendana bila ya kujali  wanatoka wapi au itikadi zao za kisiasa.


  “ Mkishirikiana, mkipendana na kuheshimiana ,  siyo tu mnajijengea mazingira mazuri ya kuishi  lakini pia mnakuwa na ari ya kusaidia maendeleo yenu kule mlikotoka na mnazifanya  Ofisi zetu pia ziwe karibu nanyi na kushirikiana nanyi kwani ni sehemu ya   jukumu letu” akasema Maajar.  Na kuongeza kwamba serikali ya awamu ya nne imetoa mkazo mkubwa wa kuhakikisha kwamba watanzania wanaoishi nje  nao wanakuwa na fursa kubwa kuchangia  maendeleo ya nchi yao na  ndio maana  imeanzisha kwa makusudi kabisa  Idara ya Diaspora ambayo ipo  katika Wizara ya Mambo ya  Nchi za Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa, na  kuwataka kuitumia  Idara hiyo  kikamilifu.


  Pamoja na kuwahimiza  watanzania waishio nchini Marekani kujiandaa kwa fursa hiyo ya kutoa maoni, pia ameelezea kuridhishwa  kwake na namna ambavyo Balozi za Tanzania nchini Marekani na  katika  Umoja wa Mataifa  zinavyofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa licha ya kwamba  zinatofautiana kimajukumu. Na kwa sababu hiyo amesisitiza haja na umuhimu wa ofisi hizi mbili kuendeleza jadi hiyo  ili kuongeza Tija kwa Taifa.

  Awali akimkaribisha Balozi   Maajar kusalimiana na  wafanyakazi wa Ubalozi na baadhi ya watanzania waliohudhuria hafla hiyo, Balozi Tuvako Manongi amwelezea  Balozi Maajar kama  kiongozi ambaye ameiwakilisha vema Tanzania nchini Marekani ikiwa pamoja na  Uingereza alikoanzia.


  Aidha akasema Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa,  unamshukuru kwa ushirikiano wake na  kwa kufanya kazi kwa karibu na ubalozi hali iliyochangia sana kwa namna moja ama nyingine utekelezaji wa majukumu yake. Na akamtakia kheri katika majukumu yake mapya.


  Balozi Manongi akabainisha kwamba  moja ya changamoto anayoiacha ni ile ya kuhakikisha kwamba  Jumuiya za Watanzania zinaendelea  kuimarika na kuwa zenye maslahi kwa wanachama wake na Taifa kwa ujumla.  0 0

  Watangaza Vita Mpya ya "KUZIBA NYUFA" katika mpasuko wa Jamii!
  Habari za uhakika tena nyeti vimevuja kutoka katika kambi ya bendi
  maarufu ya muziki  wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU yenye makazi  yake  nchini Ujerumani.

  Kuwa bendi hiyo inayofanananishwa na kikosi kazi FFU imeingia kambini
  katika msimu  wa barafu huko ughaibuni,   kwa kujifua na kujiandaa kwa kuwaletea washabiki vitu vipya ! Pia   Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja   
  mwanamuziki mwenye mjina mengi ya kutisha tisha kama vile kamanda wa  
  FFU,Kolokoloni namba 1,mfalme   
  Hui Hui wa gagagigikoko n.k,kamanda alikaririwa mwanzoni mwa Januari   
  2013 kuwa Bendi hiyo inaenda kambini   
  Kujiandaa na vita ! alipoulizwa vita gani? alijibu vita vipya vya   
  "KUZIBA NYUFA" zilezojitokeza katika jamii yetu!  Ndio kusema Kamanda wetu wa FFU Ras Makunja kaingia kambini na kikosi
  chake kujiandaa na vita?   vita venyewe vya kuziba nyufa na mimomonyoko au mipasuko katika jamii   yetu! kauli ya kamanda Ras Makunja

  inaonekana inadarubini ya mtazamo mkali unaoona mbali! katika
  mahojiano na jarida la africa analysis la Uingereza,


  Ni siku chache tu bendi hiyo yenye tabia za ki-FFU ilionekana katika
  uwanja wa ndege wa Bremen,wakiwa wanaondoka   lakini wakusema wapi wanako elekea, "wanamuziki wa bendi hiyo wakiwa   na mizigo" nyusoni wakiwa seriously tena  hawakuwa   
  tayari kujibu chochote wanachoulizwa ! tena katika msimu wa baridi na   
  barafu wanaenda kambini? tena haijulikani nchi gani?   
  kama Serbia au Bosnia ? pengine Israel ! hakuna anayejua !
  Kamanda Ras Makunja na ffu wa Ngoma Africa Band wapo kambini,kwa
  kujiandaa na vita vya kuziba nyufa, na mwaka huu pia bendi hiyo inatimiza miaka 20 tangu izaliwe mwaka  1993 hadi mwaka huu 2013 ni umri mkubwa.  Washabiki wanasubiri kwa hamu kubwa kuona na kujiunga na na vita
  vilivyotangazwa na bendi hiyo chini ya kamanda  
  Ras Makunja mwenye kichwa kigumu au mkuu wa "Watoto wa Mbwa" Ngoma.

  Africa ukipenda FFU . 

  0 0


  NA RAMADHANI ALI/HABARI MAELEZO .
                                              
  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi zake za kuimarisha ustawi wa wananchi kupitia sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo sekta ya Elimu.

  Akizungumza na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ambao Wizara zao zinapata misaada  kupitia UNESCO, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bi. Erina Bokova amesema juhudi zinazochukuliwa na Serikali zimepelekea mabadiloko makubwa ya maendeleo visiwani humo.

  Amesema UNESCO itaendelea kusaidia sekta ya Elimu kwani inafahamu  kwamba kuimarika kwa sekta hiyo ni muelekeo mzuri wa kuimarika kwa sekta nyengine za maendeleo ikiwemo kilimo, utalii na masuala ya Utamaduni nchini.

  Ameipongeza Wizara ya Elimu kwa hatua kubwa  iliyofikia ya kuwasomesha watoto wote waliofikia umri wa kusoma na ameeleza matumaini yake kwamba sera mpya ya Elimu ya Zanzibar itazidi kuimarika kwa sekta hiyo.

  Bi. Erina amesema suala la kuijengea uwezo Wizara ya Elimu na kuwaongezea ujuzi watendaji wake ni miongoni mwa masuala yatakayoendelea  kupewa kipaumbele na UNESCO.

  Akizungumzia  kuimarishwa  Mji Mkongwe wa  Zanzibar, ambao ni moja kati ya miji iliyopata heshma ya kuwa ya Urithi wa Kimataifa, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO amesema hatua ya Serikali kuendelea kuuhifadhi mji huo ni hatua ya kupigiwa mfano.

  Amesema mabadiliko madogo madogo aliyoyaona  katika baadhi ya majengo ya Mji Mkongwe hayaonyeshi kuondosha mandhari ya asili ya mji huo bali yanalenga zaidi kubuni vianzio vya ajira kwa wananchi wanaoishi ndani ya  mji huo.
   
  Amesisitiza kwa Taasisi zinazosimamia Mji huo kuhakikisha kwamba malengo ya kuufanya mji huo kuwa mji wa urithi wa Kimataifa linaendelezwa na linasimamiwa vizuri zaidi.

  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO amefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukubali kuanzishwa kwa vituo vya  Redio Jamii Micheweni na  Mtegani Makunduchi na amesema hiyo ni moja ya hatua ya kuwapelekea maendeleo wananchi wa vijiji hivyo.

  Amesema UNESCO itaendelea kusaidia utaalamu na vifaa mbali mbali kwa vituo hivyo na vituo vyengine vya aina hiyo ambavyo jamii za vijijini zitaamua kuvianzisha.

  Akizungumza  katika mkutano huo ulioshirikisha wajumbe wa UNESCO na viongozi wa ngazi za juu wa Serikali katika Hoteli ya Serena Shangani, Waziri wa Habari, Utamduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alisema vituo vya Redio Jamii vimekuwa na mchango mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya wanajamii wenyewe.

  Amesema vituo hivyo vimekuwa tegemea kubwa kwa wanajamii na vimeleta mabadiliko makubwa ya maisha  yao hasa katika masuala ya kupunguza umaskini na kukuza sekta ya Utalii ambayo imekuwa tegemeo kubwa kwa wananchi wa vijijini.

  Katika ziara yake ya siku mbili hapa Zanzibar, Ujumbe  wa UNESCO, ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, ulitembelea sehemu mbali mbali za Mji Mkongwe wa Zanzibar zikiwemo sehemu za kihistoria na baadhi ya vivutio vya Utalii vilivyomo ndani ya mji huo. 

                     IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Mlinzi Athman Mohamed wa Mundu( kulia) akimiliki mpira mbele ya Ameir Amour wa Chuoni.Pambano la ligi kuu ya Grand Malt ya Zanzibar kati ya timu ya Chuoni na Mundu kwenye uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar jana. Chuoni iliichabanga Mundu mabao 2 - 0.
   Mlinzi wa Chuoni, Ahmed Salum (kushoto) akipambana na mshambuliaji Japhet Mamboleo wa Mundu kwenye uwanja wa Mao Tse Tung jana, ligi kuu ya Grand Malt ya Zanzibar. Chuoni 2 Mundu 0.
   Rajab Mzee wa Chuoni (kushoto) akipambana na Alias Juma wa Mundu, ligi kuu ya Grand Malt ya Zanzibar, uwanja wa Mao Tse Tung jana.  Chuoni 2 Mundu 0.Picha zote na INTELLECTUALS COMMUNICATIONS LIMITED

  0 0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk.Maliki Juma Akili akipata maelezo kutoka kwa fundi Tall wa Karakana ktk sehemu ya kipimo cha Injector pump alipokuwa akigagua shuhuli mbali mbali za Karakana Kuu ya Serekali ya Zanzibar. Picha na Nafisa M.Ali-Maelezo Zanzibar.


  0 0


   Rais Jakaya Kikwete jana amefanya ziara ya siku moja mkoani Kigoma na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi wilayani Uvinza mkoani Kigoma. Picha Zote na IKULU.

  Rais Kikwete alitembelea daraja hilo na kuzungumza na wananchi wa eneo jirani na daraja hilo na kuwataka walitumie vyema katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutumia ardhi yao kwa kilimo na si kuiuza kwa watu wengine.

  Kikwete amewaambia wakazi hao kuwa wasikubali kulubuniwa na wageni wanaokuja kama wawekezaji na kununua maelfu ya hekta za ardhi yao.

  0 0  0 0

  STATE HOUSE ZANZIBAR
  OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
  PRESS RELEASE
      Zanzibar                                                                                           
     
  SERIKALI ya Oman imeeleza azma yake ya kuendelea kuunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu kwa kuanzia na elimu ya juu kupitia Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).

  Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Dk. Rawya Saud Al Busaid, aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu Mjini Zanzibar.

  Katika maelezo hayo, Waziri Dk. Rawya alimueleza Dk. Shein kuwa akiwa Zanzibar yeye na Ujumbe wake utapata nafasi ya kujadili zaidi Makubaliano ya Awali  ya mashirikiano kati ya Zanzibar na Oman kupitia sekta ya elimu yaliotiwa saini katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ziara yake nchini humo hivi karibuni.

  Dk. Rawya alieleza kuwa Serikali ya Oman imetoa ahadi ya kuwapatia nafasi wanafunzi wa Zanzibar katika Nyanja mbali mbali za masomo kupitia Mfuko wa  Mfuko wa Maendeleo ya Elimu wa Sultan Qaboos kwa ajili ya Zanzibar  (SQAP).

  Alisema kuwa katika mchakato huo Chuo Kikuu hicho cha Taifa cha Zanzibar ndio kitakachoamua ni eneo gani kitataka kuimarishwa zaidi kwani tayari Serikali hiyo ya Oman imeshajipanga vyema kutoa ushirikiano huo kwa chuo hicho ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi za masomo ya Uzamili na Uzamifu.

  Dk. Rawya alisema kuwa katika Mpango wa Muda mrefu Serikali hiyo ya Oman itajikita zaidi katika kuunga mkono kwenye maeneo makuu matatu ikiwa ni pamoja na kukisaidia Chuo hicho cha SUZA.

  Pia, kusaidia taasisi mbali mbali za serikali ambazo baadae zitakuwa ni sehemu ya chuo kikuu hicho na kuasaidia wanafunzi watakaomaliza masomo ya Sekondari kuwapa nafasi za masomo katika vyuo mbali mbali duniani ili baadae waje kutoa utaalamu wao katika Chuo Kikuu hicho.
    
  Aidha, Waziri huyo wa Elimu wa Oman alisema kuwa Oman pia, ina mpango wa kuiunga mkono Serikali katika kuwapatia wanafunzi wa Zanzibar nafasi za masomo katika vyuo vikuu mbali mbali duniani gharama ambazo zote zitatolewa na nchi hiyo na kupata huduma zote zinazostahiki za kimasomo kama anazozipata mwanafunzi wa Oman.

  Dk. Rawya alisema kuwa mipango ya Serikali ya Oman katika kukiimarisha chuo hicho Kikuu cha SUZA ikifanikiwa chuo hicho kinaweza kupatanafasi maalum ndani ya serikali hiyo ya Oman ambapo chuo hicho kitaweza kuunganishwa na vyuo kadhaa duniani na kuweza kupata mafanikio.

  Sambamba na hayo, Dk. Rawya alimueleza Dk. Shein kuwa  kuna wananchi wengi wa Oman wenye asili ya Zanzibar ambao wako tayari kuiunga mkono Zanzibar na kutoa misaada yao mbali mbali lakini bado hawajajua taratibu zilizopo ili kufanikisha azma yao hiyo kwa ndugu zao wa Zanzibar.

  Alieleza kuwa Waomani waliowengi ambao wanaasili ya Zanzibar wamevutiwa kuisaidia Zanzibar katika sekta ya afya ikizingatiwa kuwa kuna Madaktari wengi nchini humo wenye asili ya Zanzibar wakiwemo Madaktari Bigwa.

  Nae Dk. Shein kwa upande wake alieleza kuwa Zanzibar inathamini sana uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati yake na Oman huku akisisitiza kuwa azma ya nchi hiyo kuiunga mkono Zanzibar katika sekta ya elimu kupitia SUZA ni jambo la busara na lenye matumaini makubwa katika maendeleo ya Zanzibar


  Dk. Shein pia, alieleza kuvutiwa kwake na hatua ya nchi hiyo ya kuiunga mkono Zanzibar katika sekta ya afya na kusisitiza kuwa kupitia Idara maalum ya Diaspora aliyoinda katika afisi yake kutaandaliwa utaratibu maalum wa jinsi ya kuwasiliana na wataalamu hao na baadae wizara ya Afya itafanya taratibu husika.

  Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alitoa ahsante kwa ujio wa Waziri huyo hapa Zanzibar huku akisisitiza uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya pande mbili hizo utaimarishwa.

  Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Ali Juma Shamuhuna alisema kuwa Waziri huyo wa Elimu akiwa na Ujumbe wake huo upo nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano mwema na Zanzibar katika sekta ya elimu.

  Alisema kuwa ujumbe huo tayari umeshafanya ziara ya kukitembelea Chuo hicho cha SUZA pamoja na kuwa na azma ya kutembelea taasisi nyengine za elimu zikiwemo Chuo cha Afya, Skuli ya Lumbumba na nyenginezo huku baadhi ya wajumbe wakiahidi kwenda kisiwani Pemba ili kuangalia maendeleo katika sekta hiyo ya elimu nchini.

  Wakati huo huo, Dk. Shein alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),  Mama Irina Bokova, ambapo Shirika hilo limeeleza azma yake ya kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo elimu, Uhifadhi wa Mji Mkongwe Kimataifa, Utamaduni, Mazingira na mengineyo.

  Nae Dk. Shein kwa upande wake alitoa pongezi kwa Mama Bokova kwa ujio wake hapa nchini na kutoa pongezi kwa Shirika hilo kutokana na juhudi zake za kuiunga mkono Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo.

  Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza Mkurugenzi Mkuu huyo kuwa   Zanzibar imevutiwa na juhudi za UNESCO katika uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar na kusisitiza haja ya kuyafayia ukarabati majnego ya mji huo ikizingatiwa kuwa ni kivutio kikuu cha watalii wanaoitembelea Zanzibar.

  Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
  Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

  0 0


  Na  Khadija Khamis-Maelezo Zanzibar  05/02/2013.

  JAJI Mkuu wa Zanzíbar Omar Othmani Makungu amesema  kuwepo kwa Mahakama ya watoto nchini kutasaidia kupunguza mrundikano wa kesi zinazowakabili watoto mahakamani na kupatikana haki zao kwa wakati.

  Jaji Makungu ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mahakama ya Watoto Zanzibar huko Vuga ikiwa ni shamra shamra ya siku ya Sheria duniani inayoazimishwa Februari 7 kila mwaka.

  Amesema lengo la kufunguliwa Mahakama hiyo ni kukabiliana na changamoto ya ongezeko la kesi zinazohusu Watoto na kuwapatia haki zao za msingi kwa wakati. Aidha ameongeza kuwa Mahakama hiyo itakuwa ni mazingira rafiki kwa watoto ambayo yatawasaidia kuweza kujieleza pamoja na kutoa ushahidi bila ya hofu.

  Jaji Makungu amefahamisha kuwa wanatarajia kuanzisha Mahakama ya Watoto kwa upande wa Pemba sambamba na kuweka mahakama ndogo ndogo katika kila wilaya ili kuweza kuondoa usumbufu kwa wananchi.

  Nae katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii maendeleo ya Wanawake na Watoto Fatma Gharib Bilali amewataka wazee kushirikiana na mahakama hiyo ili kuweza kutatua matatizo mbali mbali yanayowakabili watoto ikiwemo kurekebisha tabia na kukufatilia nyendo zao.

  “Maendeleo yeyote lazima yawe na changamoto zake jamii lazima iwasaidie watoto kuwalinda na vishawishi vya watu wabaya” alisema Katibu huyo.

  Nao Wawakilishi kutoka Mashirika ya Kimataifa ya UNICEF na Save The Children wameishukuru Mahakama Zanzibar kwa ushirikano wao wa kuweza kuanzisha mahakama ya watoto ambayo itaweza kutetea na kulinda haki za mtoto na ustawi wake.

  IMETOLEWA NA  MAELEZO ZANZIBAR  05/02/2013.

  0 0


  Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj akisalimiana na Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji kwenye hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro wakati Balozi Begum Taj akisubiri kumsindikiza Airport Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO aliyeondoka nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea jijini Paris. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen.

  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's akisindikiza kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (katikati). Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa UNESCO Bi. Robertine Raonimahari aliyeambatana na Bi. Irina Bokova's nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili iliyomalizika jana.(Picha zote na Zainul Mzige wa Mo Blog).
  Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo akisalimiana na Mh. Mohammed Dewji.
  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's akielekea kwenye gari la maalum tayari kwa safari ya Airport.
  Bi. Irina Bokova's akiwasili VIP Terminal na kulakiwa na Bi. Rahma wa Ofisi za Unesco Tanzania.
  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi.Irina Bokova's akizungumza jambo na Mh. Mohammed Dewji walipokutana Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mw. Julius Nyerere VIP Terminal. Kushoto ni Msaidizi wa Mh. Dewji Bw. Cosmas Mtesigwa na Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mh. Begum Taj.
  Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's aliyeondoka nchini usiku wa kuamkia leo baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.
  Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Kitengo cha Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka akipkea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo kabla ya kuondoka nchini usiku wa kuamkia leo.
  Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo alifanya hivyo pia kwa Naibu Mkurugenzi wa UNESCO Bi. Robertine Raonimahari hii ikionyesha jinsi gani watanzania walivyokuwa wakarimu kwa wageni.
  Safari ya kuelekea kupanda ndege iliwadia.....Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akiteta jambo na Bi. Irina Bokova's wakati akimsindikiza kupanda ndege ya shirika la KLM usiku wa kuamkia leo.
  Mama Rahma wa Ofisi za Unesco Tanzania akigana na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Kitengo cha Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka pamoja na Naibu Mkurugenzi wa UNESCO Bi. Robertine Raonimahari (kulia).
  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen wakiwa ndani gari maalum linalowapeleka sehemu ilipopaki ndege ya shirika la KLM.

  0 0


  Na Thehabari.com

  IMEELEZWA kuwa hali ya elimu nchini kwa sasa si shwari hivyo ni wakati muafaka kwa wananchi na Serikali kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hii.

  Changamoto hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo anuai vya habari kuzungumzia mustakabali wa elimu nchini.

  Alisema shule zetu zinapaswa kutoa elimu inayomwezesha mwanafunzi kujitambua na kumpa maarifa yatakayomsaidia kumudu mazingira yake jambo ambalo halifanyiki kwa sasa kutoka na sera hafifu. “Wakati tukijaribu kutafakari changamoto hizi katika sekta ya elimu ni muhimu tukajiuliza tumefikaje hapa tulipo?,” alisema.

  “Matatizo ya mfumo mbovu wa elimu yamechangia kwa kiasi kikubwa na kutokuwa na dira ya elimu, ambayo inatolewa na sera kwa takribani miaka mitano sasa Serikali imekuwa ikiahidi kukamilisha na kupitia sera ya elimu ya mafunzo ya mwaka 1995. 
  Watanzania wamekosa dira ya elimu waitakayo kwa sababu Serikali imeshindwa kukamilisha uandaaji wa sera mpya ya elimu,” alisema. 

  Alisema Serikali imekuwa ikiandaa sera tangu mwaka 2007, lakini kwa sababu zisizojulikana imekuwa ikisuasua katika ukamilishaji sera hiyo mwaka hadi mwaka. 

  “Sera ilianza kuandaliwa tangu mwaka 2007, Serikali kwa sababu zisizo julikana imebaki ikipiga danadana kila mwaka. Ni dhahiri kwamba kutokana na mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa nchini inahitajika sera mpya itakayotupa dira sahihi ya sura ya elimu tunayoitaka, pia kuandaa kutoelekeza mipango sahihi kuboresha mfumo wa elimu hapa nchini,” alisema Bi. Missokia.

  Alisema kikwazo kingine ni migogoro sugu katika sekta ya elimu inachangia kudorora kwa elimu ya msingi na sekondari, kwani kwa kipindi kirefu sasa sekta ya elimu imegubikwa na migogoro mingi ikiwemo madeni ya walimu ambayo mgogoro wake umedumu kwa zaidi ya miaka minane. 

  Akizungumzia mvutano ulioibuka bungeni juu ya uwepo wa mitaala ya elimu ama  kutokuwepo, Meneja Utafiti na Uchambuzi wa Sera wa HakiElimu, Godfrey Bonivetura alisema taasisi hiyo haijawahi kuona mtaala wowote wa elimu licha ya wao kuomba mara kadhaa.

  “Kwa mantiki hiyo sisi tunaamini mtaala haupo na kinachofanyika sasa walimu hutumia muktasari wa masomo kufundishia…mwaka jana tulifanya utafiti mmoja ambapo tulizungumza hadi na walimu nao walikuwa wakidai hata wao hawajawahi kuona mtaala,” alisema.

  Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari cha HakiElimu, Nyanda Shuli aliitaka Serikali kuwa wazi juu ya suala hilo na kama kweli inayo mitaala iiweke katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili wananchi na wadau mbalimbali wa elimu waweze kuuona. “Ukiwauliza watendaji wa Serikali juu ya suala la mtaala wanasema upo ukiuomba uuone utapigwa danadana hadi unakata tamaa...," alisema Nyanda.

  Aidha aliiomba Serikali kuacha kuingiza siasa katika kushughulikia masuala ya elimu kwani hali hiyo ndiyo iliyoifikisha elimu yetu hivi sasa.

  Hivi karibuni ulizuka mjadala bungeni kuhusu kuundwa kwa kamati ya kuchunguza mitalaa, sera na mihutasari ya elimu, hoja binafsi ambayo iliibuliwa na Mbunge wa Kuteuliwa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akilitaka bunge kuunda Kamati kuchunguza suala hilo.

older | 1 | .... | 22 | 23 | (Page 24) | 25 | 26 | .... | 1898 | newer