Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 243 | 244 | (Page 245) | 246 | 247 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0

  Picture-055

  Hoyce Temu a communication specialist at the United Nations in Tanzania has been selected as one of the inspirational southern African women and a rising star in the region. Temu has been involved in the social works by helping the communities in various ways and sharing what she has to make the world a better living for everyone.

  On the International Women’s Day, the MISA announced the first annual MISA’s Women to Watch.

  MISA is honoring 12 dynamic­­ and inspirational southern African women who embody both the official United Nations theme for International Women’s Day 2014 - Equality for women is progress for all – as well as the theme designated by non-governmental organisations around the world –Inspiring Change.

  MISA Regional Director, Ms Zoe Titus said, “We chose women who we see as rising stars in the region, women whose achievements to date are a promise of more great work to come, making them women to watch.”

  You can download MISA’s Women to Watch in 2014 as an electronic magazine in two parts:
  You can also read extended profiles of the women on our website, by following the links below.

  MISA’s Women to Watch in 2014

  Alisa Amupolo, a technology entrepreneur from Namibia;
  Ana Margoso, a newspaper journalist from Angola;
  Chikondi Mphande,a radio journalist from Malawi;
  Emma Theofelus,a high school student from Namibia who is the Junior Mayor of the City of Windhoek;
  Hoyce Temu, a communications specialist and former Miss Tanzania;
  Jean Chalungama, a radio journalist from Malawi and one of the only female sports journalists in the country;
  Mboni Masimba,a talk show host from Tanzania;
  Mwiza Zulu, a teenage radio and television presenter in Zambia;
  Nellie Kanyemba,a journalist from Malawi;
  Nontobeko Tshabala, a newspaper journalist from Swaziland;
  Nyasha Chingore-Munazvo,a human rights lawyer from South Africa; and
  Solange Dos Santos,a photographer from Mozambique.
  Source misa.org
  1456005_1817516041720649_704041018_nUntitled1

  0 0

  Photo Credits: happyholidays2014.com
  Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
  Kipindi hiki kilirushwa moja kwa moja (live) Jumamosi Machi 8, 2014
  Katika kipindi cha wiki hii, mjadala ulijikita zaidi katika SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ambapo wageni Mary Ndaro akiwa Wichita Kansas na Mch. Tumaini Mwanyonga  walijadili kwa mapana suala hili.
  Wamegusa mengi mema ambayo ni muhimu kuyasikiliza.


  0 0

   Hakuna kazi rahisi,na kila kazi inahitaji kujituma,ubunifu na umakini wa kutosha ili kupata kilicho bora.Pichani ni Mwandishi mtayarishaji,Mtangazaji na mpiga picha mahiri  wa kituo cha televisheni cha Star TV,chenye makao yake makuu jijini Mwanza,Mpiganaji Abdallah Tilata akirekodi juu na chini matukio ya mapokezi ya mgombea Ubunge wa CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa katika Jimbo la Kalenga, alipokuwa akiwasili kata ya Kalenga-Iringa vijijini kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.


  0 0
 • 03/10/14--21:55: Article 21


 • 0 0

  Muimbaji Erica Lulakwa na wimbo wa Hongera Wanawake aliyoimba kwenye sherehe za Kilele cha maadhimisho ya mwanamke Duniani, iliyoandaliwa na kundi zima la Tano Ladies siku ya Jumamosi March 8, 2014 ndani ya Ukumbi wa Hampton Inn Jijini Maryland nchini Marekani.
  (Picha na Swahilivilla.blogspot.com)

  0 0

   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhwan Kikwete akionesha fomu aliyochukua ya kugombea ubunge jimbo la hilo kulia kwake ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo, Kongo Kamate na Mbunge wa viti maalum wa jimbo la Charinze Subira Mgalu.

  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akijaza fomu ya kugombea jimbo hilo.
   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea jimbo hilo

   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akiongozana na wanachama wa CCM kwenda kuchukua fomu fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya Bagamoyo.
  =======  =========
  Ridhwani achukua fomu za Ubunge Chalinze.


  MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete jana alichukua fomu katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi wilayani  Bagamoyo na leo anatarajia kurudisha fomu hiyo.


  Akisindikizwa na mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM wa jimbo la Chalinze na Bagamoyo, Ridhwani alimhakikishia  ofisa wa uchaguzi wa wilaya ya Bagamoyo Shija Andrew, kuwa atazingatia taratibu zote za uchaguzi na kutoendesha kampeni za matusi na vurugu.


  Baada ya kuchukua fomu hiyo pamoja na nakala nyingine muhimu za uchaguzi aliongozana tena na mamia ya wafuasi wake kuelekea kwenye ofisi za CCM Bagamoyo ambapo alizungumza na waandishi wa habari.

  Katika mazungumzo yake hayo Ridhwan alitaja vipaumbele vyake kwa kuleta maendeleo kwa wakazi wa Chalinze ambapo alisisitizia kuimarisha upatikanaji wa maji salama na ya uhakika, kuimarisha afya, elimu pamoja na kukuza ajira kwa vijana.


  "Kama  mnavyofahamu kuwa Chalinze ni eneo ambalo linakabiliwa na changamoto nyingi kama vile maji, umeme na hata suala zima la ajira kwa vijana sasa pindi ambapo nikipata Ubunge kwangu mimi nitahakikisha kuwa napunguza kama sio   kumaliza kabisa tatizo hilo"alisema Ridhwan. Aliongeza kuwa "Mimi nimeguswa na changamoto mbalimbali zinazowakuta wakazi wa wilaya hii na kama ambavyo nilisema kuwa sikushinikizwa ila ni kwa matakwa yangu mwenyewe naona kabisa kuwa nipo katika hali na nguvu ya kushirikiana na wananchi kumaliza shida za Chalinze".

  Ridhwan pia alisema kuwa atasaidia kutatua ugomvi wa mara kwa mara unaowakumba wakulima na wafugaji na kuwataka wakazi wa Chalinze kumchagua kwa kishindo. Wakati huo huo mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey akizungumza baada ya kuchukua fomu alisema kuwa anavyo vipaumbele vingi kimojawapo ikiwa ni kuinua maisha ya wakazi wa Chalinze.
  Leo Ridhwan anatarajiwa kurejesha fomu za kugombea ubunge katika ofisi ndogo za uchaguzi.

  Uchaguzi wa jimbo la Chalinze unakuja kufuatia kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ramadhan Bwamdogo aliefariki Januari 22 mwaka huu.


  0 0

  Kwa kutambua umuhimu wa mashabiki wake, SMARTCODES inawapa nafasi mashabiki wake wa Facebook, Twitter na Instagram (Wanao wa follow kwenye akaunt yao ya @SmartCods). Kwa kila mtandoa yao ya kijamii atachaguliwa mshindi moja Kwenda kuaangalia Premier Movie ya 3D300: RISE OF AN EMPIRE” Ijumaa tarehe 14 Marchi 2014, pale CINEMAX Mlimani City


  Namna ya ushiriki:

  unatakiwa ku Like, kisha Share na muhimu Zaidi tuambie vitu vitatu unahisi vinalingana na huduma zetu ukiangalia nembo yetu ya kampuni. Jibu lako lianze na #smartbird @smartcods

  Kwenye TWITTER; unatakiwa ku follow @SmartCods, retweet na kisha tweet vitu vitatu unahisi vinalingana na huduma zetu ukiangalia nembo yetu ya kampuni. Jibu lako lianze #smartbird @smartcods

  Kwenye INSTAGRAM; unatakiwa kutufollow @SmartCods, ku repost na kucomment vitu vitatu unahisi vinalingana na huduma zetu ukiangalia nembo yetu ya kampuni, jibu lako likianza na #smartbird @smartcods

  Watembelee Hapa: www.smartcodes.co.tz
  0 0   Lori la kubeba taka likiwa eneo kituo cha gereji barabara ya mandela ,huku likiwa limebeba uchafu baada ya kuharibika na limekaa hapo siku mbili.


   Huo unaonekana kwa juu ni uchafu uliooza na unatoa harufu kali kituoni hapo. eneo la kituo cha gereji mandela road

   Uchafu uliobebwa na Lori hilo,lililoharibika eneo la kituo cha gereji mandela road


  Abiria wanaotumia kituo cha gereji barabara ya mandela kwa siku mbili mfululizo wamekuwa wakipata kero ya harufu kali inayosababishwa na gari ya kubebea taka iliyopaki kwenye kituo hiko.Wakiongea na mtandao wa wetu huu wa Dj sek abiria hao wamesema kwamba gari hiyo iliharibika ikiwa inaelekea kumwaga uchafu huo na wakaisogeza kituoni hapo ili waweze kuitengeneza, lakini badala yake dereva na wasaidizi wake wakaitelekeza gari iyo toka juzi.Wakiendeleaa kuongea na mtandao wetu wamesema eneo lote la kituoni hapo linatoa harufu kali ambayo ni kero kwa wao wanaosubilia usafiri eneo hilo.

  Mwandishi wa blog hii nilishuhudia mwenyewe na kupiga picha pia kuonja adha ya harufu kali inayotoka kwenye gari hiyo.Manispaa ya kinondoni na wasimamizi wa usafi mnaombwa kufuatilia hili na kuweza kulitatua kwani ni kero kwa watumiaji wa kituo hiki.

  0 0


  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti wa Kamati ya Uundaji wa Kanuni zitazotumika katika bunge Maalum la Katiba Prof. Costa Ricky Mahalu akisoma azimio la kutunga na kupitisha kanuni za bunge Maalum.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba akiiunga Mkono Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt. Fransis Michael akiwaomba wajumbe wa bunge maalum la katiba kuunga mkono na Kupitisha Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba ili kuwa na umoja na kutekeleza jukumu hili la kitaifa leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba na Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Mhagama akiunga Mkono Azimia la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. James Mbatia akiunga Mkono Azimia la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba na kuwataka wajumbe wengine kufanya hivyo ili kuanza kikao cha bunge maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Panya Ally Abdalah(Mwenye mtandio wa Zambarau) akiiunga Mkono Azimia la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Sheikh. Mussa Kundecha akiwataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Kuwa wamoja na Kupitisha Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Amon Muhagachi akiunga mkono Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba na kuwataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuunga mkono azimio kwa maslahi ya Taifa.
  Mwenyekiti wa Muda wa Bynge Maalum la Katiba akiwaleza jambo wajumbe wa Bunge Hilo kabla ya kuahirishwa mpaka kesho jioni na Kuwataka wale wanaotaka kuchukua fomu ya uenyekiti kuanza kuzichukua leo.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Frederick Msigala akiunga Mkono Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba.(Picha na Hassan Silayo-MAELEZO)


  0 0

   Cosmas Njingo-afisa habari na mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro akichangia mada.
    Zadock Kitomary-Mkulima bora mara mbili mfululizo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha akitoa mada.

  Ayubu Nnko-Msimamizi wa Jarida kwa upande wa Tanzania akitoa mada katika Semina hiyo.

    Coroline Nyakundi- Meneja Mradi The Organic Farmer& jarida la Mkulima mbunifu akitoa mada.


    John Cheburet-Mtayarishaji wa vipindi vya Redio kutoka jarida la Mkulima mbunifu .
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali na Mafunzo katika semina hiyo
  ******
  Na Arusha yetu Blog
  IMEELEZWA kuwa Watanzania ni wavivu wa kusoma Majarida mbali mbali yanayoweza kuwaongezea upeo ukilinganisha na nchi zingine. 
  Hayo yamebainishwa na Mmoja wa maafisa wa Jarida la Mkulima Mbunifu, Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya, wakati akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari za kilimo na wataalamu wa kilimo yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Arusha Crown ya Mjini hapa.
  Ameongeza kuwa kunatofauti kubwa ya Mwitikio wa kusoma machapisho kati ya Raia wa Tanzania ukilinganisha na Kenya ambako imeelezwa kuwa wanauhitaji mkubwa wa kujifunza mbinu mpya za kilimo tofauti na Watanzania ambao hawana uhitaji wa kusoma na kutaka kujua zaidi.

  Akieleza Mikakati ya Jarida la Mkulima Mbunifu mmoja katika ya Maafisa wa Jarida hilo, Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya, amesema tangu kuzinduliwa kwa jarida hilo Juni,2011 limeonesha mwitikio mkubwa kutokana na kupata taarifa nyingi kutoka kwa wakulima wakilihitaji ili kujua zaidi habari za Kilimo.
  Amesema Jarida hilo limelenga zaidi maoni na mahitaji ya Mkulima kutokana na mawazo yao ambayo wamekuwa wakiyatoa katika jarida hilo mara kwa mara jambo linaloonesha Mkulima kufikiwa na Jarida hilo na kwa wakati.


  0 0


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Mafunzo ya wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi Nchini, mafunzo hayo yanafanyika katika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete (Katikati) na Mkurugenzi wa mazingira Dkt. Julius Ningu (Kulia) wakimsilikiza Bw. Julio Esterban Mshauri Mwelekezi kutoka UNIDO akitoa ufananuzi kwa wakufunzi kutoka Vyuo vya ufundi nchini.


  Sehemu ya washiriki wa warsha wakifatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa mgeni rasmi.
   Washiriki wa Mafunzo wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete watatu kutoka kulia mara baada ya ufunguzi wa warsha.
  =========  =======  =========
  Lulu Mussa na Rashda Swedi

  Ofisi ya Makamu wa Rais

  Dar es Salaam


  Serikali inaendelea na jitihada za kutoa elimu kwa umma juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi ili kulinda tabaka la Ozoni. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Mafunzo kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali vya Ufundi Nchi.

  Katika Hotuba yake Bi Madete amesema kuwa kemikali haribifu zinauwezo mkubwa kuharibu tabaka la Ozoni na kuongeza joto angani. Kutokana na sababu hizo, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jamii za kimataifa zimekubaliana kufanya jitihada za kuondoa kemikali  hizo hatarishi.


  Bi Madete ameainisha baadhi ya kemikali hizo kuwa ni methyl bromide, halons na chloroflorocarborns ambazo hutumika kama vipozi katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya  kuzima moto, usafishaji chuma, ufukizaji wa mazao katika maghala na utengenezaji wa magodoro ambazo huleta madhara kwa tabaka la ozoni na adhari zake hutokea kwa binadamu, mimea na viumbe hai.


  Katika awamu ya kwanza, Tanzania imefanikiwa kuondoka tani  296 za kemikali hizo haribifu ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba wa Montreal na Vienna ambayo Tanzania iliridhia mwaka 1993.


  Aidha, Bi Madete ameyataja madhara yatokanayo na uharibifu wa Tabaka la Ozoni kuwa ni kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya ngozi,uharibifu wa macho maarufu mtoto wa jicho, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi.  Athari hizi kwa kiasi kikubwa zinatokana na shughuli za kibinadamu kama vile matumizi ya kemikali haribifu na zisizo rafiki kwa mazingira. 


  Warsha hii ya siku mbili imeratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na inajumuisha wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi vya Zanzibar na Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Mbeya na Mwanza. 


  0 0

  Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa kuanza rasmi utaratibu wa kugawana mirabaa na watengenezaji na wasimamizi wa kazi zake za sanaa.

  Maamuzi haya yamekuja chini ya mkataba mpya ambao CPwaa ameingia na "Record label" yake ya "Brainstormusic" ambayo itazinduliwa rasmi siku za usoni.Maamuzi haya ni magumu kwa wasanii wengi lakini kwa wale wafuatiliaji na wadau wa muziki hakika wanatambua biashara ya muziki inafanyikaje na jinsi kila muhusika anavyotakiwa kupata share zake kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na pande zote kupitia sheria za kitaifa na kimataifa za haki miliki.

  CPwaa ambaye amakuwa akifanya kazi na "Brainstormusic" kwa miaka mingi tayari amekuwa na mafanikio makubwa kimuziki kupitia uongozi na usimamizi wa kampuni hiyo.Ukiacha tuzo 3 za Kilimanjaro Muisc awards,nomination za tuzo za kimataifa kama Channel O ,CPwaa anaendelea kufaidika kupitia mikataba  mizuri ya shows na endorsements kwenye makampuni mbalimbali kupitia label hiyo.

  .."Kupitia Brainstormusic nimejifunza vitu vingi sana kuhusu sanaa ya muziki baadaa kufanya kazi na makampuni ya hapa Tanzania na nje.Nimesafiri nchi nyingi Africa na Asia kupitia muziki na kusema ukweli Tanzania kuna mambo mengi sana bado hayako sawa kwenye biashara ya muziki" Umefika muda wa sasa kushare experience na knowledge na kama tukifata utaratibu huu hakuna mtu atadhulumiwa wala kulalamika.Kila mdau anahusika.".....aliongezea CPwaa!!

  Kwenye utayarishaji wa muziki kila muhusika huwa anakuwa kiwango fulani cha asilimia ya mapato anapata kutokana na mchango wake.Kwa kawaida mapato ya muziki "Royalties" hugawanywa kati ya Songwriter ( mtunzi wa nyimbo ambae ndio mmliki halali wa nyimbo), Producer ( Mtayarishaji), Performing Artist ( Muimbaji wa nyimbo) na Publisher au Record label ( wasambazaji na wasimamizi). 

  Mgawanyo unatokana na kiwango cha mchango wa kila muhusika na mara nyingi huwa makubaliano kati ya wahusika. Kimataifa au kawaida mtunzi huchukua asilimia kubwa na wengine hupata sehemu tu mirabaa itakayokusanywa.Serikali haihusiki na makubaliano ya asilimia za mirabaa kati ya wahusika au hatua za awali za hiyo sanaa ila inahusika kwenye kuweka na kutoza kiwango fulani kinacholipwa na vyombo vyote vinavyotumia kazi za sanaa na kisha kugawa mirabaa kwa wale wamiliki wa hizo sanaa.

  Kuanzia mwaka huu Producer yeyote atakayefanya kazi na CPwaa chini ya usimamizi wa "Brainstormusic" basi atafaidika si tu kwenye malipo ya awali ya utengenezaji wa beat na studio time ila pia asilimia fulani ya mapatao ya mirabaa itakayoingizwa na kazi hiyo. Kimataifa producer huchukua kati ya 20 - 25% kutokana na kwamba yeye kama mtengenezaji wa beat basi ndio mmliki wa ile beat. 

  Huu ni utaratibu mpya utakuwepo kwa maproducer wote watakaofanya kazi na CPwaa au Brainstormusic kuanzia mwaka huu:

  1.Kazi zote zitaandaliwa na kufanywa chini ya makubaliano yaliyoandikwa na kusainiwa na pande zote.Invoice na risiti zitahusika.
  2.Brainstormusic ikinunua beat pamoja na haki miliki zake ( yaani producer akiuza beat jumla) basi hatapata share za mirabaa.
  3.Kama Brainstormusic au Msanii wake atahusika kwenye hatua za utayarishaji beat,vionjo,idea,upangiliaji basi asilimia fulani ( Chini ya makubaliano) ya mirabaa itatolewa na Brainstormusic kwa Producer wa kazi hiyo.
  4.Kama producer atahusika mwanzo mwisho kutengeneza na kukamilisha beat hiyo bila uhusika wa Brainstormusic au msanii wake basi producer atapata asilimia fulani kubwa zaidi ( Chini ya makubaliano) ya mapato ya mirabaa ya kazi hiyo.
  5. Ukiacha mapato ya mirabaa Brainstormusic itamlipa Producer au Studio gharama za kawaida ( Delivery / Studio Fee) kama utaratibu ulivyo sasa.

  Brainstormusic ni Record label ya kujitegemea inayofanya kazi na wasanii,maproducers na makampuni mbalimbali.Mwaka huu imedhamiria kujitanua kwenye Music Publishing hivyo kupitia mikataba yake itahakikisha producer analipwa asilimia yake kutoka makampuni mbalimbali kama ikiwemo Music Stores,makampuni ya milio ya simu na PROs ( Performance Rights Organization) kama COSOTA. 

  Bado hakuna utaratibu mzuri nchini Tanzania unaotumika kwenye utendaji na usimamizi wa kazi za sanaa kuanzia hatua za awali."Brainstormusic" tunatambua mchango na kuheshimu kila mtu kwenye "Food Chain" ya sanaa na hivyo tutafanya kazi kufuata miongozo ya kitaifa na kimataifa ambapo kila mtu anapata maslahi kutokana na mchango wake. Utaratibu huu hautaishia kwa CPwaa tu bali wasanii wote watakaokuwa wakisimamiwa na "Brainstormusic".

  Asanteni sana.

  By CPwaa's Management.

  0 0

  TIMU ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na Taswa Queens kesho zitacheza mechi maalum za kirafiki dhidi ya Chuo Cha Uandishi wa Habari, Mawasiliano ya Umma na Utawala kijulikanacho kwa jina la Dar es Salaam City College (Dacico).

  Mechi hiyo imepangwa kufanyika Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.

  Majuto alisema kuwa  mechi hizo zimepangwa kuanza saan 9.00 alasiri na zimeandaliwa ili kuendeleza uhusiano baina yao na chuo hicho maarufu na bora nchini.Alisema kuwa wanatarajia kuondoka jijini saa 5.00 asubuhi na kabla ya kucheza mechi hizo, watapata fursa ya kutembelea mazingira ya chuo hicho na baadaye kuzungumza na wanafunzi na walimu.

  “Tumepokea mwaliko na naamini watataka kujifunza kutoka kwetu, sisi ni waandishi wa habari ambao tupo tayari kazini na pale kuna wanafunzi ambao wanataka kuja kufanya kazi tunayofanya sisi, hivyo hii ni ziara muhimu sana mbali ya kucheza michezo,” alisema Majuto.

  Alisema kuwa kocha mkuu wa timu ya soka, Ali Mkongwe na msimamizi wa timu ya netiboli, Sharifa Mustapha waliendesha mafunzo mazuri kwa wachezaji kwenye mazoezi na lengo kubwa ni kupata ushindi.

  Mkurugenzi wa Dacico, Idrisa Mziray alisema kuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya mechi hizo na lengo kubwa ni kuongeza mtandao wa chuo chao ambacho kina matawi handi mikoani. Mziray alisema kuwa wanafunzi wao wa tawi la Mbeya nao wamefika kwa ajili ya ziara hiyo na kuonyesha uwezo wao katika michezo.

  “Tupo tayari kwa ajili ya mechi hizo, tunajua Taswa FC na Taswa Queens ni timu nzuri nah ii imetokana na kufanya vyema katika mechi zao mbali mbali, tupo tayari kwa changamoto,” alisema Mziray.

  0 0

  Na Jovina Bujulu, Maelezo Dodoma.


  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wameunga mkono azimio la kutunga na kupitisha kanuni za bunge Maalum la katiba. Wakiongea kwa nyakati tofauti ndani ya ukumbi wa bunge baadhi ya wajumbe waliopata nafasi waliwataka wajumbe wengine kuunga mkono na kupitisha azimio hilo kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.

  Aidha wajumbe hao waliwapongeza wajumbe walio katika kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni itakayotumika kuongoza bunge hilo kwa kazi waliyoifanya tangu kuanza kwa semina ya marekebisho ya kanuni hizo. Pia wajumbe walimpongeza mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Bw. Pandu Ameir Kificho kwa kuongoza bunge hilo la uandaaji wa kanuni kwa umakini na busara.

  Naye mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Bw. Pandu Ameir Kificho aliwataka wajumbe wenye nia ya kugombea uenyekiti wa Bunge hilo kwenda kuchukua fomu za maombi za nafasi hiyo katika ofisi za katibu wa bunge.


  Kuhusu suala la Makamu mwenyekiti wa Bunge hilo Bw. Kificho alisema kwamba nafasi hiyo itajazwa pale mwenyekiti atakapopatikana kwani matakwa ya sheria ya bunge hilo yanataka nafasi hizo kuwa na wawakilishi toka pande zote mbili za Tanzania.


  “Tunasubiri kumpata mwenyekiti kwanza kabla ya makamu mwenyekiti kwani sheria inasema iwapo mwenyekiti atatoka Tanzania bara basi makamu wake atatoka Zanzibar na vilevile kama mwenyekiti atatoka Zanzibar basi makamu wake atatoka Tanzania bara.” Alisema Kificho.


  Mpaka jioni ya leo wajumbe 4(nne) wameshachukua fomu hizo wakiwamo Samwel Sitta, Theresia Huviza, John Lifa Chipaka na Hashim Rungwe.  0 0

  Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kushoto) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wake Bw. Said Lugumi, kukabidhi msaada wa Pump ya maji inayotumia umeme na fedha taslimu shilingi milioni kumi kwa Afisa Elimu Takwimu (W) Sekondari bw. John M. Mangu  katika makabidhiano yaliyofanyika viwanja vya shule ya Sekondari ya Magu.
  Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari Magu wakati wa makabidhiano ya msaada wa pumpu ya maji inayotumia umeme pamoja na fedha taslimu shilingi  milioni kumi kwaajili ya kukamilisha nyumba ya walimu.
  Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kulia) akiwaongoza wanafunzi wa Magu Secondary kushusha vifaa vya pump ya maji inayotumia umeme ikiwa ni sehemu ya msaada alioukabidhi jana kwa shule hiyo.
  Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kulia) akiwaongoza wanafunzi wa Magu Secondary kushusha pump ya maji inayotumia umeme ikiwa ni sehemu ya msaada alioukabidhi jana kwa shule hiyo kutimiza ahadi iliyowekwa mwaka jana kwenye maafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne na Mkurugenzi wake Bw. Said Lugumi.
  Hili ni sehemu ya kusanyiko la baadhi ya wanafunzi wa Shule ya sekondari Magu waliohudhuria makabidhiano hayo. 
  Afisa Elimu Takwimu Sekondari Wilaya ya Magu John M.Mangu (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya sekondari Magu Mwl. Geoffrey Mikenze kiasi cha shilingi milioni kumi alichopokea kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe ili kukamilisha ujenzi wa nyumba ya walimu shuleni hapo.
  "Msaada wa Fedha tuliopokea ni huu" Mkuu wa Shule ya sekondari Magu Mwl. Geoffrey Mikenze (kulia) akiwa na wanafunzi wake.
  Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akipata picha ya pamoja na baadhi ya walimu, wakuu wa idara Shule ya sekondari Magu. 


  Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akipata picha ya pamoja na Mkuu wa shule na viongozi wa wanafunzi wavulana Shule ya sekondari Magu. 
  Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akipata picha ya pamoja na Mkuu wa shule na viongozi wengine wa wanafunzi wavulana Shule ya sekondari Magu. 
  Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akipata picha ya pamoja na Mkuu wa shule na viongozi wa wanafunzi upade wa wasichana Shule ya sekondari Magu. 
  Serikali ya wanafunzi Shule ya sekondari Magu.
  Aksante....
  MAGU.
  KAMPUNI ya  Lugumi Enterprises Ltd & Ran It Solution imedhamilia kumaliza kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi na salama katika Shule ya Sekondari ya Magu baada ya kutoa msaada wa Pampu mpya ya kusukuma maji ili kukabiliana na kumaliza kabisa kero hiyo Wilayani hapa.


  Pamoja na msaada huo Kampuni hiyo pia imetoa kiasi cha fedha shilingi milioni 10 tasilimu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la nyumba ya walimu familia mbili (two in one) ambalo lilishindwa kukamilika kutokana na kukosekana fedha jambo ambalo sasa litakamilishwa na fedha zilizotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo iliyo na tawi lake jijini Mwanza.


  Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi Pampu hiyo na kiasi hicho cha fedha katika viwanja vya shule hiyo Mjini Magu jana, Meneja wa Kampuni hiyo Eligod Sangawe  aliyemwakilisha Mkurugenzi wake Bw. Said Lugumi alisema kwamba utekelezaji wa msaada huo unatokana na ombi la wanafunzi na walimu wa shule hiyo wakati wa sherehe za Mahafali ya 24 ya 2013 kuwaaga wahitimu wa kidato cha nne kwenye risala yao kwa Mgeni rasmi siku hiyo.

  Sangawe alisema lengo kubwa ni kuhakikisha ukarabati na miundombinu ya kufikisha maji shuleni hapo inaimarishwa na kuwezesha maji safi na salama yanapatikana ili kuondoa adha ya kero ya muda mrefu iliyopo katika baadhi ya maeneo ya Mji wa Magu ikiwemo Sekondari hiyo jambo ambalo litawapatia fursa wanafunzi takribani 1,100 waliopo shuleni hapo kutumia muda mwingi katika masomo.


  “Jitihada hizi zitasisimua mwamko wa jamii na wadau wengine wa elimu kuona kwamba wanayo nafasi ya kuchangia na kusukuma mbele gurudumu la elimu hapa nchini, hivyo sisi Lugumi Enterprises Ltd & Ran It Solution tunayo matumaini kuwa msaada huu utatatua suala la mahitaji ya maji kwa asilimia 75 huku ule wa kompyuta utawasaidia kukimbizanana na mapinduzi ya Teknohama kutoka mfumo wa analojia na kuingia kwenye mfumo wa kidigitali" 

  Meneja Sangawe alisema kuwa kutokana na kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekondari hiyo, Kampuni hiyo hapo awali iliweza kusaidia uboreshaji wa Maabara kwa kutoa vifaa ikiwemo Gesi na zana muhimu, kuboresha mfumo wa maji wa maabara shuleni hapo pamoja na  kukabidhi Computer 3 za ofisi ikiwemo moja ya kufundishia masuala ya sayansi na Teknohama.


  Naye Mkuu wa Sekondari hiyo Geoffrey Mikenze alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo na Meneja wake kwa kuamua kutoa msaada huo italeta chachu ya mafanikio ya kielimu kwa shule yake.


  “Kwenye risala yetu tulieleza kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji safi kwenye shule yetu, ukosefu wa rasilimali fedha kwa ajili ya kukamilisha nyumba ya walimu yenye vyumba nane ikiwemo, sebule mbili, stoo mbili (Two in One) Kampuni hii imetusaidia kiasi cha shilingi milioni 10 ili kukamilisha wa ujenzi” alisema Mkuu huyo.  Ametoa wito kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na wananchi ambao walipata kusoma katika sekondari hiyo kuiga mfano ulionyeshwa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Kizalendo ya Lugumi Enterprises Ltd & Ran It Solution katika kusaidia kutatua changamoto nyingine zilizobaki kama upungufu wa vitabu vya kiada na rejea, upungufu wa matundu ya vyoo nane vya wavulana na vitano vya wasichana ili wanafunzi kufaulu vyema na walimu kutoa taaluma bora. 


  0 0  Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akipokea Fomu kutoka kwa Ofisa wa Bunge Bi. Lidya Mwaipyana Katikati ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangala.
  Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akionesha fomu ya uenyekiti aliyochukua leo Kushoto niMjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangala na Kulia ni Mjumbe wa Bunge hilo Bw. Paul Makonda.
  Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akiongea na waandishi wa habari Mara baada ya Kuchukua fomu hizo na kuahidi kufanya kazi kwa KasinaViwango. 
  (PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Meki Sadiki (kushoto) akizungumza na  mkazi wa eneo la Mloganzila Bw. Fredy Justine Masondole (kulia) ambaye aliweka pingamizi kuzuia miundombinu ya maji, umeme na barabara kupita katika eneo lake , Hata hivyo mkazi huyo aliruhusu ujenzi kuendelea baada ya mazungumzo ya kupatikana kwa muafaka kufikiwa. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchian Mramba. 
   .Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Meki Sadiki (katikati) akizungumza jambo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS) lililo kwenye mpaka wa wilaya ya Kisarawe na mkoa wa Pwani leo.Wengine kutoka  kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi.Therezia Mmbando,Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Bw. Archard Mutalemwa na Meneja wa Tanroad mkoa wa Dar es salaam Bw. Ndyamukana Julius.
   Mkazi wa eneo la Mloganzila Bw. Fredy Justine Masondole (Katikati) akiwapeleka katika eneo la nyumba yake lenye mgogoro viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meki Sadiki (upande wa nyuma katikati), mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jordan Lugmbana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando.
  Mafudi wakiendelea na ujenzi wa awali wa ofisi za muda katika eneo itakapojengwa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS) lililo kwenye mpaka wa wilaya ya Kisarawe na mkoa wa Pwani leo
  Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

  =========  ========  =========
  WALIOKWAMISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU MLOGANZILA SASA WARUHUSU UJENZI KUENDELEA .

  Na. Aron Msigwa.
  11/3/2014, Dar es salaam.

  Baadhi ya wakazi wa eneo la Mloganzila waliokuwa wamezuia maeneo yao kutumiwa kupitisha miundombinu ya maji, barabara na umeme kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS) wamekubali kuyatoa maeneo yao ili kuruhusu kuendelea kwa ujenzi wa miundombinu hiyo.

  Wakazi hao waliozuia ujenzi huo kwa madai ya kutolipwa fidia na baadhi yao kwenda mahakamani wamefikia uamuzi  huo leo mara baada ya mazungumzo baina yao na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Meki Sadiki aliyetembelea eneo la mradi huo.

   Akiwa katika eneo la ujenzi wa mradi huo unaojengwa na Kampuni ya Colon Global Corporation kutoka Korea, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Meki Sadiki amesema kuwa mradi huo kwa muda umeshindwa kuendelea kutokana na kukosekana kwa maji,umeme na miundombinu ya barabara.

  Amesema mkandarasi alikwisha onyeshwa eneo hilo la ujenzi toka Februari 23 na kuongeza tayari makabidhiano ya eneo hilo lililo mpakani mwa wilaya ya Kisarawe na mkoa wa Pwani yamekwishafanyika.

  “Ujenzi wa hospitali hii kubwa na chuo Kikuu cha Afya na Tiba ni moja ya ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, Mh. Rais aliahidi na kama  mnavyoona ujenzi huu umeanza lakini umekwamishwa na baadhi ya wananchi wachache na kama serikali tumeona si vema tuendelee kuchelewesha ujenzi wake” Amesema.

  Amesema mkoa kwa kushirikiana na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) na Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) umekaa kwa pamoja ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huo ili kuruhusu kuanza kwa ujenzi wa mradi huo haraka iwezekanavyo.

  “Tumekua na mazungumzo na wenzetu hawa na leo tulikua na kikao cha pamoja ili tupate ufumbuzi wa suala hili na tayari wakazi hawa wawili ambao nyumba zao ziko kwenye eneo yatakapopita mabomba ya maji, nguzo za Umeme na Barabara tumezungumza nao na tayari wamekubali na kesho ujenzi unaendelea” Amesisitiza. Ameongeza kuwa wamiliki wa maeneo hayo wamekubali busara itumike kwa wao kuruhusu mradi huo uendelee na kufafanua kuwa tathmini ya nyumba na maeneo yao inaendelea kufanyika ili waweze kulipwa stahiki zao.

  “Tumeamua busara itumike ili kuokoa muda unaozidi kupotea na kuchelewesha ujenzi wa mradi huu mkubwa wenye manufaa kwa wananchi,licha ya kwamba baadhi yao wamekwishapeleka madai yao mahakamani”
  Kuhusu sehemu ya eneo la mradi huo linalomilikiwa na JWTZ, Mh. Sadiki amesema kuwa atakwenda kuzungumza na Mamlaka husika ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo na kutoa wito kwa wananchi ambao tayari wamekwisha pokea fidia zao kupisha ujenzi wa mradi huo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchian Mramba akiwa katika eneo la tukio ameeleza shirika lake limeshindwa kufikisha umeme katika eneo husika kutokana na zuio lililowekwa na wananchi hao na kuongeza kuwa muafaka uliofikiwa leo ni faraja kwao kuwezesha kazi hiyo kuendelea. “Sisi baada ya maelewano haya ni kazi kuendelea na kesho kazi ya kupitisha nguzo na nyaya inaendelea” amesisitiza.

  Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Bw. Archard Mutalemwa amefafanua kuwa tayari wao kama wahusika wakuu wa usambazaji wa miundombinu ya maji wameshalaza miundobinu hiyo kwa 50%, kujenga mnara wa tenki kubwa la maji, kununua vifaa na kuongeza kuwa wamejipanga kukamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa.

  Naye Meneja wa TANROAD mkoa wa Dar es salaam Bw. Ndyamukana Julius ameeleza kuwa ujenzi wa barabara za eneo hilo utakamilika mwezi Agosti mwaka huu.
  “Sisi tumejipanga vizuri kukamilisha ujenzi huu kwa kushirikiana na wenzetu ili kufikia tarehe 22 Agosti  mwaka huu tukamilishe kazi” Amesema.

  0 0

    Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Makete Shaaban Mkakanze.
   

  Hatua hiyo imefikiwa baada ya mkutano wa wanachama uliofanyika jumamosi machi 8, mwaka huu kwa pamoja kuazimia kuung'oa madarakani uongozi uliokuwepo baada ya kujadiliana kwa kina katika mkutano huo

  Miongoni mwa viongozi waliong'olewa ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Makete Bw. Sahaaban Mkakanze na katibu wake pamoja na uongozi mzima uliokuwa ukiongoza chama hicho wilayani.
  Mkutano huo ambao pia uliowashirikisha viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo mwenyekiti Bw. Lulandala, ulibaini kuwa kasi ya kukua kwa chama hicho wilayani Makete ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine licha ya jitihada zinazofanywa na ndiyo maana wakaona wabadilishe uongozi

  Katika mkutano huo waliazimia kuchagua uongozi wa muda ambao umepewa miezi miwili ya matazamio kuhakikisha wanakiimarisha chama katika kata zote za wilaya ya Makete ikiwemo kuunda uongozi wa kila kata ambao unaweza kufanya kazi kama inavyotakiwa

  Viongozi wa wa muda waliochaguliwa kushikilia chama hicho ngazi ya wilaya kwa muda ni Bw. Ibrahim Ngogo ambaye ni mwenyekiti, Bw. Ilomo ambaye ni katibu na Bw. Stephano Kasanga ambaye ni katibu mwenezi

  Mkutano huo umewapa miezi miwili ya kukiimarisha chama kabla ya kuitishwa mkutano mwingine ambao utakuwa wa uchaguzi wa wanachama kuwachagua viongozi wa wilaya wa kukiongoza chama hicho.

older | 1 | .... | 243 | 244 | (Page 245) | 246 | 247 | .... | 1897 | newer