Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 242 | 243 | (Page 244) | 245 | 246 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Kiongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) akipata maelezo ya maendeleo ya Mradi wa Maji ya Mtiririko Kijiji cha Igurusi kutoka kwa Mshauri wa Mradi huo Mhandisi Kimambo.
   Wakaguzi walipata bahati ya kujionea chanzo cha maji hayo kutoka nje kidogo ya Kijiji cha Igurusi.
   Kikazi Zaidi.. Timu ya ukaguzi pia ilikagua maendeleo ya Tanki la kuhifadhia maji la mradi huo. Pichani, Kiongozi wa Ukaguzi, Bibi Florence Mwanri akipanda ngazi kwenda kujionea maendeleo ya ujenzi wa Tanki.
   Ujenzi unaendelea.. Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi huku wakaguzi hao wakikagua. Tanki hilo lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita laki tano ambalo limeshakamilika kwa asilimia 90. Hadi kukamilika kwake Mradi utagharimu jumla ya Shilingi zaidi ya Milioni 830.
   Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Aliyenyanyua Mkono) akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Maji wa Iwalanje wakati Timu ya Ukaguzi ilipotembelea Mradi huo.
   aonja Maji.. Kiongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye nguo nyeusi) akionja maji kutoka moja ya njia za kusambazia maji ya Mradi wa Maji wa Iwalanje. Kukamilika kwa Mradi huo kumetoa suluhisho la adha ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa Kijiji cha Iwalanje na Taasisi mbalimbali za Serikali zinazohudumiwa na Mradi huo.


   Timu ya Ukaguzi pia ilishuhudia Tanki la kuhifadhia maji la Mradi huo lenye uwezo wa kuhifadhi lita 43,000. Mradi huo umegharimu jumla ya Shilingi milioni 273, ambapo mpaka sasa Mradi unahudumia zaidi ya kaya 2, 506.
   Viongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Prof. Longinus Rutasitara (Wanne Kushoto aliyenyanyua mkono) na Bibi Florence Mwanri (Watatu Kushoto) wakipata maelekezo ya Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe. Pichani ni ujenzi wa sehemu wa kukaa abiria ukiendelea.
   Meneja uwanja wa ndege wa Songwe jijini Mbeya, Eng. Valentino Kadeha (Kulia) akitoa maelekezo kwa Timu yaUkaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea Mradi huo. Kwa Mujibu wa Mhandisi Kadeha Uwanja huo umeshakamilika kwa aslimia 70 na utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria zaidi ya 300 kwa saa.
   Ukaguzi wa Hospitali.. Kwa kutambua umuhimu wa afya kwa maendeleo ya nchi, Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pia ilitembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya. Timu hiyo ilishuhudia maendeleo ya ujenzi wa jengo la Kitengo cha Dharura (linaloonekana nyuma).
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr  Sankey (Wapili Kulia) akieleza changamoto zinazozikabili Hospitali hiyo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pia ilipotembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya. Aliyeambatana nae ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Humphrey Kiwelu (Kulia). Picha zote na Saidi Mkabakuli

  ======  =====  =======
  MBEYA WAANZA KUNEEMEKA NA MPANGO WA MAENDELEO

  Na Saidi Mkabakuli

  Wakazi wa mkoa wa Mbeya na vitongoji vyake wameanza kufaidi matunda ya uwekezaji wa kimkakati uliobainishwa na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 – 2016) kupitia ujenzi wa miundombinu ya maji, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, pamoja na ujenzi wa jengo la Kitengo cha Dharura katika Hospitali ya Rufaa iliyopo mkoani humo.

  Hayo yalibainika wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara ya ukaguzi wa baadhi miradi ya maendeleo kushuhudia hali ya utekelezaji wa miradi iliyopo mkoani humo.

  Akizungumza wakati wa ukaguzi huo mmoja wa Kiongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri anayeshughulikia Huduma za Jamii na Maendeleo ya Idadi ya Watu, alisema kuwa katika kutambua changamoto zinazowakabili wakazi wa mkoa huo, Mpango wa Maendeleo uliweka bayana uanzishaji na uendelezaji miradi ya maendeleo ili kutoa huduma za kijamii kwa Watanzania wote.

   “Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa ikiwemo miradi hii tunayokagua leo,” alisema Bibi Mwanri.

  Bibi Mwanri aliongeza kuwa kwa kutambua changamoto za uhitaji wa maji kwa baadhi wakazi wa vijijini wa mkoa wa Mbeya, Serikali iliwekeza zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya maji ya Mradi wa Maji ya Mtiririko Kijiji cha Igurusi na Mradi wa Maji wa Iwalanje.

  “Hii ni baadhi ya miradi inayonufaisha wakazi wa mkoa huu ambayo tumetembelea. Kukamilika kwa Miradi hii kumetoa suluhisho la adha ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa Mbeya na vitongoji vyake pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali zinazohudumiwa na Miradi hii,” alisema.

  Naye Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara ambaye alikuwa kiongozi mwenza wa ukaguzi huo, alisema kuwa maendeleo ya miradi hiyo ni ishara tosha kuwa wakazi wa Mbeya na vitongoji vyake wataanza kuneemeka na uwekezaji huo wa Serikali kwa kupata fursa mbalimbali za kimaendeleo kupitia miradi hio.

  Akitolea mfano wa uwekezaji katika Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Prof. Rutasitara alisema kuwa kukamilika kwa Uwanja  huo ambao umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 70, sio tu kutaongeza shughuli za kiuchumi mkoani Mbeya bali kunatoa fursa za kufungulia za kuwezesha ukuaji mpana wa uchumi wa nchi.

  “Uwanja wa Songwe unatoa fursa za misingi wa uchumi kwa watu walio wengi, hizi ni juhudi za makusudi za Serikali za kuondoa vikwazo vilivyopo hivi sasa katika kutumia utajiri mkubwa wa rasilimali zilizopo mkoani Mbeya,” alisema Prof. Rutasitara.

  Serikali imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Mpango huu utadumu kwa mwaka 2011/12 - 2015/16 na utakuwa  wa kwanza katika mfululizo wa mipango mitatu  itakayotekelezwa kwa awamu. Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.


  0 0

  DSCF3003Mgeni rasmi katika sherehe ya maadhimisho siku ya wanawake duniani  iliyondaliwa na Phenomenal Women Group, Mama Regina Lowassa akikata keki kuashiria ufunguzi rasmi wa kikundi hicho,Hafla iliyofanyika jana Machi 8/2014 katika ukumbi wa World Garden Moshono jijini Arusha, ambapo kampuni Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 ilishiriki kudhamini siku hiyo ya wanawake duniani.
  DSCF3007Mgeni rasmi Mama Regina Lowassa akifungua chupa ya wine,kushoto kwake ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi.Youthness Godfrey
  DSCF2993Mgeni Rasmi katika halfa ya siku ya Wanawake Duniani, Mama Regina Lowassa akisoma hotuba huku akisisitiza wanawake kujitambua pamoja na kujikubali hali itakayosaidia wao kushiriki katika maendeleo na kuchangia pato la Taifa
  DSCF2975Wageni waalikwa wakiangalia burudani kutoka kwa mwanamuziki Snura,
  hayupo pichani.
  DSCF2976Wakinamama wakionekana na nyuso za furaha katika hafla ya siku ya wanawake duniani.

  DSCF3003Mgeni rasmi katika sherehe ya maadhimisho siku ya wanawake duniani  iliyondaliwa na Phenomenal Women Group, Mama Regina Lowassa akikata keki kuashiria ufunguzi rasmi wa kikundi hicho halfa iliyofanyika jana Machi 8/2014 katika ukumbi wa World Garden Moshono jijini Arusha ambapo kampuni Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 ilishiriki kudhamini siku hiyo ya wanawake duniani.
  DSCF3007Mgeni rasmi Mama Regina Lowassa akifungua chupa ya wine,kushoto kwakwe ni mwenyekiti wa kikundi hicho Bi.Youthness Godfrey
  DSCF2993Mgeni Rasmi katika halfa ya siku ya wanawake dunia Mama Regina Lowassa akisoma hotuba huku akisisitiza wanawake kujitambua pamoja na kujikubali hali itakayosaidia wao kushiriki katika maendeleo na kuchangia pato la Taifa
  DSCF2975Wageni waalikwa wakiangalia burudani kutoka kwa mwanamuziki Snura
  DSCF3012
  DSCF2972Aliyevalia sare za jeshi ni Ispekta Mariam 
  DSCF2976Wakinamama wakionekana na nyuso za furaha katika halfa ya siku ya wanawake duniani.


  DSCF3015Kushoto ni Dk.Msuya ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika hospitali ya St.Thomath jijini Arusha
  DSCF2992Mwenyekiti wa kikundi cha Phenomenal Women Group Youthness Godfrey akisoma risala kwa mgeni rasmi
  DSCF3016Mama Regina Lowassa akiwa katika zoezi la kuwamiminia akina mama wine mara baada ya kugungua kuashiria ufunguzi rasmi wa kikundi cha Phenomenal Women Group
  DSCF3020Kushoto Sarah Keiya Meneja masoko wa kampuni Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha akiwa katika picha ya pamoja na Pamela Sioi
  DSCF2997Muonekano wa baadhi ya wanakikundi  wa Phenomenal Women Group
  DSCF3022Sarah Keiya Meneja masoko wa kampuni Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa kikundi hicho Youthness Godfrey
  DSCF3023Wadau wakishow love na Pamela Sioi,mtoto wa Mama Regina Lowassa
  DSCF3026Hapa wadau wakiwa katika pozi na mgeni rasmi Mama Regina Lowassa
  DSCF3024kushoto niMmiliki wa jamiiblog akishow love na wadau
  DSCF3029
  DSCF2979Muonekana wa keki pamoja na wine kabla havijatumika.


  DSCF2989Mwanamuziki maarufu Snura akiwaburudisha wanawake katika halfa hiyo iliyoandaliwa na kikundi cha Phenomenal Group
  DSCF2985Wacheza show wa Snura wakitoa burudani

  0 0


  0 0

   Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na mmoja wa wanakijiji,mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni wa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo,uliofanyika katika kijiji cha Wenda kata ya Mseke-Iringa Vijijini,huku kukiwa na mvua kubwa ikinyesha,ambayo hata hivyo haikuzuia kufanyika kwa mkutano huo.Wananchi wa Kijiji hicho walionekana kuw ana shauku kubwa ya kutaka kumsikiliza Mgombea huyo bila kujali kulowana na mvua.Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Machi 16.
   Wanakijiji cha Wenda wakimpungia Mgombea Ubunge wa CCM,jimbo la Kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,huku shangwe na vifijo vikiwa vimetawala eneo hilo pasina kujali mvua kubwa ilioyokuwa ikiendelea kunyesha eneno hilo.
   Pamoja na Mvua kubwa iliyokuwa inanyesha katika kijiji cha Wenda kata ya Mseke-Iringa Vijijini,wanakijiji wa eneo hilo walionekana kuvutiwa mno na sera za mgombea ubunge wa CCM,Godfrey Mgimwa alipozungumza nao kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.Kama uonavyo pichani baadhi ya Wanakijiji wakilikimbiza gari ya mgombea huyo mara baada ya kumaliza mkutano wake.Mgombea huyo aliwaomba wampigie kura za ndio na kumpa ridhaa ya kuwaongoza kama Mbunge wa jimbo hilo,ili wayamalizie yale yaliyokuwa yameachwa na Mbunge aliyekuwepo hapo awali,Marehemu Dk Willliam Mgimwa.

  0 0   
   
  RETIREMENT PLANNING COURSE

  A unique opportunity for employeesto develop Entrepreneurship, Financial Literacy and Retirement Planning Skills. The longer prior to retirement you take this course, the more you will benefit.

  Approach and Contents
  The course is delivered by highly experienced facilitators using experiential methods. Participants are guided to recognize opportunities and challenges of retirement; their talents and other tangible and intangible assets and liabilities; alternative  post-retirement “careers”;  to choose when to retire; and to continuously build their asset base, streams of income and fulfilling lives after retirement. They are exposed to good practices in starting and running a business, personal finance and health management; expected pension benefits and investment schemes tailored to retirees. They leave with self awareness, a Retirement Vision and look forward to their exit from employment.

  Dates, Fee and Registration
  24th - 27th March, 2014, Morogoro. Tuition is Tshs 500,000/= per person. Apply: info@imedtz.org or 0718-942314 (Ulrich) and
  0754-548248 (Hellen) or visit us at Mwalimu House, 7thFloor, Uhuru Road, Ilala, Dar es Salaam or www.imedtz.org to pick the Registration Form.
  We also offer Certificate and Diploma courses in Entrepreneurship and Business Management registered by NACTE

  0 0

   Afisa Uhusiano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (kushoto) akizungumza na mmoja wa wanakikundi  cha Tumaini Kijiji cha Lemguru,Kata ya Kisongo wilaya ya Arumeru,Elizabeth Daniel ambaye ameanzisha ufugaji baada  kupata mafunzo kutoka asasi  isiyo ya kiserikali ya Ace Africa iliyopewa fedha kiasi cha dola za Marekani 64,000.
   Meneja Mauzo wa kampuni ya Bia(TBL)Kanda ya kaskazini,Wilderson Kitio(kulia)akizungumza na maafisa wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Ace Africa  wakati wa ziara ya kutembelea miradi iliyofadhiliwa na TBL kupitia asasi hiyo mkoani Arusha hivi karibuni
   Afisa Uhusiano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (kulia) akizungumza na mmoja wa wanakikundi  cha Tumaini Kijiji cha Lemguru,Kata ya Kisongo wilaya ya Arumeru,Naserian Mayase wakati wa ukaguzi wa miradi ilifadhiliwa na TBL kupitia taasisi isiyo ya kiserikali ya Ace Africa.Picha na Mpigapicha Wetu
  Afisa Miradi wa asasi isiyo ya kiserikali ya Ace Africa,Baraka Mshana(katikati) akiwapa maelezo ya umuhimu wa matumizi ya majiko banifu kwaajili ya kulinda mazingira,Meneja Mauzo wa kampuni ya Bia Kanda ya Kaskazini,Wilderson Kitio(kushoto)na  Afisa Uhusiano wa TBL,Doris Malulu .

  0 0

  WAKATI  siku zikikaribia kuelekea kwenye Tamasha la Pasaka katika zoezi la upigaji kura kuchagua waimbaji, mikoa na mgeni rasmi katika tamasha hilo, waimbaji kadhaa wamechomoza kwenye mchakato wa kutoa huduma ya uimbaji katika tamasha hilo.

  Kwa mujibu  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama waimbaji hao wamepata nafasi hiyo kupitia mfumo wa upigaji kura kupitia ujumbe mfupi wa maandishi ya simu za mkononi.

  Msama aliwataja waimbaji hao kuwa ni pamoja na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Voice  Acapela na Sarah Kiarie kutoka Kenya. Aidha Msama alisema taratibu za upigaji kura kuelekea tamasha hilo zinaendelea, hivyo alitoa wito kwa mashabiki kuendelea kupiga kura kuchagua maeneo hayo matatu yatakayofanikisha tamasha hilo.

  0 0


  Mjumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Ally Kessy akiwaeleza jambo jambo Wajumbe wenzie Bw. Edward Lowassa (katikati) na Almas Maige ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta (kulia) akimweleza jambo Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
  Mjumbe wa bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni zitakazotumika katika Bunge maalum la Katiba Bw. Prof. Costa Mahalu akiwaeleza jambo wajumbe wa bunge hilo wakati wa semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma. 

  Mjumbe wa bunge Maalum la Katiba Bw.  Augustino Mrema akimweleza jambo Mjumbe mwenzie Bw. Islaim Aden Rage leo Mjini Dodoma.
  Wajumbe wa Bunge Maalumla Katiba na Wajumbe wa kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni zitakazotumika katika Bunge maalum la Katiba Bw. Prof. Costa Mahalu (Kulia) na Tundu Lissu wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma.
  Wajumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Hamadi Rashidi (kushoto) Juma Alawi (katikati) na Thumwein Thuwein wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma.
   (PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO)

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Seif Rashidi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, kuhusu  maadhimisho ya wiki ya  afya ya Figo itakayoanza tarehe 10 hadi 14, na kuadhimishwa kitaifa tarehe 13 mjini Dodoma katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, kauli mbiu  ya maadhimisho hayo ni “Figo huzeeka , kadiri mtu anavyozeeka. Jali afya ya Figo zako”.( Lorietha Laurence-Maelezo)

  0 0


  "Haya Mheshimiwa Mbunge sasa nakata utepe kuzindua rasmi usambazaji dawa za serikali ulio chini ya MSD" ni Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe akishuhudiwa na Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Tibaijuka (Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini) .
  "Haya tupige makofi kwa pamoja kuashiria kukubali uzinduzi huu" Naibu Waziri Dk. Kebwe (Kulia), Waziri Prof. Tibaijuka (Katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu MSD Bw. Mwaifwani.
  Afisa Habari wa MSD Makao Makuu (Mwenye Kipeperushi cha Bendera ya MSD) na Baadhi ya watumishi wakifuatilia kwa umakini shughuli za uzinduzi wa Kituo kipya
  Meneja wa MSD Kanda ya Mwanza Tabula akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof. Tibaijuka ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Mtulia (Mwenye suti) wapili Kulia, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe (Nyuma mwenye suti) na Mkurugenzi MSD Kanda Makao Bw. Tell (Mwenye miwani aliyevaa shati nyeupe nyuma) 

   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Alli Mtulia akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa nchini (MSD) akitoa taarifa fupi ya MSD kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo kipya.
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Stephen Kebwe Aliyemwakirisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamerd Ghalib Bilal akihutubia viongozi, watumishi wa MSD na wananchi wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha MSD Wilayani Muleba
  Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka  ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitoa hotuba ya shukurani za wananchi wa Wilaya ya Muleba na Mkoa wa Kagera kwa kuzinduliwa kwa kituo kipya cha MSD Wilayani Muleba.
  Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali ya uzinduzi wa kituo kipya cha MSD Muleba.
  Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini ambaye ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka akisindikizwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya MSD (Kulia) Prof. Idris Alli Mtulia na Kushoto kabisa ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa nchini (MSD) Bw. Cosmas Mwaifwani wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kituo cha kuhifadhi na usambazaji dawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera. 
  Baadhi ya wanawake wakifuatilia tukio la uzinduzi .  Kakao Bandi wakiwa kazini kutumbuiza wakati wa sherehe 

  Kazi ni moja tu kushambulia ndani ya viwanja vya uzinduzi wanamuziki wa Kakao Bandi.
  Ramani kuonyesha Mfumo wa Usambazaji Dawa kutoka MSD kwa kauli mbiu yake kufikisha dawa moja kwa moja hadi vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa ni Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya na Teule, Mkoa na Rufaa maeneo yote nchini.
  Baada ya kumalizikehe kwa sherehe za uzinduzi Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini alianzisha maandamano ya Amani kuunga mkono juhudi za serikali kufikisha huduma ya dawa na vifaa tiba kupitia Bohari Kuu ya Madawa (MSD) nchini kote ili kupunguzi vifo vya mama na watoto, mapambanaona ugonjwa  wa UKIMWI na Malaria.

  Kituo kipya cha muda cha Kutunza na Usambazaji Dawa cha Bohari Kuu ya Madawa (MSD) kilichozinduliwa Jumamosi na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (Akimwakirisha Makamu wa Rais Dk. Mohamerd Ghalib Bilal ) kilichopo eneo la Mahalahala Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera. 
  MKurugenzi wa MSD Kanda Makao Makuu Dar es salaam Mr Tell akiteta jambo na Meneja wa MSD Kanda ya Mwanza Tabula Byekwaso kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa Kituo kipya cha muda cha Kutunza na Usambazaji Dawa cha eneo la Mahalahala Wilayani Muleba March 8 Mwaka huu.
  Wanawake ambao ni wananchi wa Wilaya ya Muleba na maeneo ya jirani na Kituo kipya wakijumuika na baadhi ya watumishi wa MSD kusakata dansi la Bendi ya Muziki ya Kakao eneo la uzinduzi Mahalahala Wilayani Muleba.
  Waibaji na wacheza show wa Bebdi ya Kakao wakitumbuiza kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo kipya cha MSD eneo la Mahalahala Muleba.
  Viongozi Jukwa Kuu wakishiriki kusakata rumba la Kakao Bandi

  Na Peter Fabian.
  ALIYEKUWA MULEBA.

  MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kufanya msako endelevu ili kuwafichua, kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaopatikana na Dawa za Serikali kinyume cha taratibu na sheria zilizopo.

  Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Stephen Kebwe (MB) wakati wa ufunguzi rasmi wa Kituo cha Kutunza na Usambazaji Dawa (Bohari ya MSD) cha muda kilichopo eneo la Mahalahala kwenye Hospitali inayojengwa ya Wilayani Muleba juzi alisema wizi na upotevu wa dawa hizo zinazotolewa na serikali hufanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

  Alieleza kwamba Kituo cha Muleba (Bohari ya Madawa ya MSD) cha muda kitakuwa na jukumu kubwa la kusambza dawa na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali na Vituo vya Afya katika maeneo yote ya Wilaya za Mikoa ya Kagera (Vituo 270 ) na Geita (Vituo 64) kuanzia mwezi julai mwaka 2013 mfumo huu wa usambazaji dawa ulianza kabla ya kufunguliwa rasmi.

  Makamu wa Rais Dk. Katika hotuba hiyo ameipongeza Bohari Kuu ya Madawa (MSD) nchini kwa kuanzisha utaratibu wa kuweka alama ya Government Of Tanzania (GOT) katika dawa zinazosambazwa na kusema kuwa hatua hiyo itasaidia dawa za serikali kutambulika kiurahisi kwa wananchi pamoja na kuthibiti wauzaji wa maduka ya dawa baridi wanaopelekewa zinazoibiwa na watumishi wa serikali.

  “Lengo kubwa la kufunguliwa kituo hichi ni kupunguza vifo vya akina mama na watoto, kupambana na ungonjwa wa UKIMWI na Malaria ikiwa ni kuanza kutumia mfumo wa fikisha dawa karibu na wananchi na kwa wakati ili kufanikisha lengo mahususi la serikali ya awamu ya nne huku ufatiliaji wake uwe chini ya usimamizi wa karibu na matumizi ya dawa zinazosambazwa kwenye vituo vya huduma ” alisisitza

  Kwa upande wake Naibu Waziri Dk. Kebwe amesikitishwa na taarifa ya kasi ya wizi na upotevu wa dawa zinazopelekwa na serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) katika Wilaya za Ngara, Kerwa, Biharamulo na Muleba huku akizipongeza Wilaya za Karagwe na Bukoba vijijini kwa kuweka jukumu la udhibiti wizi na upotevo wa dawa hizo kutoka kwa watumishi wasio waadilifu.

  Dk. Kebwe ameungana na Makamu wa Rais Dk. Bilal kuzitaka Kamati za ulinzi na usalama za Mikoa ya Kagera na Geita na zile za Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri zote kufatilia kwa ukaribu huku akitaka taarifa za upokeaji dawa na utolewaji kwa wananchi utolewe kwenye Vikao vya Kamati ya Ushauri na Maendeleo (RCC) za Mikoa yote.

  “Tusikubaliane na wajanja wachache wa Idara za Afya kutumia mwanya wa kuiba dawa na kuziuza kwenye maduka waliyoanzisha na kisha kujinufaisha kwa kununua magari, kujenga vyumba za kifahari nasi kuwashangilia eti muda mchache jamaa ana gari zuri ambapo makusanyo ya mapato kutoka vituo vya afya kuonyesha ni asilimia 50 tu huku zingine zikiliwa na wajanja wachache” alisema.

  Dk. Kabwe alisema kuwa Wizara yake itatumia bilioni 6 kwa mwaka katika Dawa zote zitakazotolewa na kituo hicho na kila mwezi kitasambaza dawa za kiasi cha shilingi milioni 150 huku Bajeti ya Wizara ikionekana kutumia Bilioni 80 za Dawa, Vifaa tiba na Vitenganifu na kupitia kituo hicho ndani ya siku 14 Hospitali na Vituo vya Afya vitapeka oda na kupatiwa dawa.

  Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Porfesa Idrisa Mtulia kuzinduliwa kwa kituo hicho ni mkombozi mkubwa wa wananchi wa Mkoa ya Kagera na Mkoa wa jirani wa Geita na Wilaya zake zote ambapo kitawezesha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na viunganifu vya kutolea huduma ya afya kwa Bohari ya madawa kufikisha haraka huduma zake kwa wateja.

  Prof. Mtulia alisema kwamba pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili MSD itahakikisha inashirikiana na serikali na wadau wengine kuendelea kutoa huduma bora na kufikisha dawa zenye ubora na bei nafuu wakati wote kwa manufaa ya watanzania wote  huku akihimiza Halmashauri zote nchini kukunua dawa kutoka MSD kwa kutumia vyanzo vyake vingine vya fedha.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) nchini Cosmas Mwaifwani alisema kwamba kutokana na ukubwa wa Kanda ya Ziwa na idadi kubwa ya wingi wa watu zaidi ya milioni 13 kutokana na matokeo ya Sensa ya mwaka 2012 kuwepo na malalamiko ya wadau mbalimbali juu ya huduma za MSD Kanda ya Mwanza kutokidhi kwa wakati huduma ya utoaji wa dawa.

  Kaimu huyo alieleza kuwa imefungua kituo hicho cha muda kuhakikisha upatikanaji na usambazaji wa Kituo cha Muleba kinafanikisha lengo la MSD na kupunguza usumbufu wa Mkoa wa Kagera kufata huduma hiyo Jijini Mwanza na Kanda ya Tabora ambapo ilionekana kuchelewesha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba vyenye ubora na kwa bei nafuu kwa watanzania wote.

  Ufunguzi wa Kituo hiki cha usambazaji dawa Mkoani Kagera na Mkoa wa jirani wa Geita ni mchango mkubwa wa utekelezwaji wa Malengo ya Millenia hususani kupunguza vifo vya mama na watoto na kupambana na Ukimwi na Malaria ambayo imekuwa ni magonjwa ya mlipuko katika maeneo mengi ya Wilaya za Muleba ” Alisema Mwaifwani.

  Mbunge wa Muleba Kusini Porfesa Anna Tibaijuka ambaye ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwahakishia Naibu Waziri Dk. Kebwe na uongozi wa MSD kuwa eneo la Ekhali 5 zilizotolewa na Halmashauri Wilaya ya Muleba linaachwa wazi ili kutoa nafasi kwa MSD kujenga Ofisi kuu na Maghala ya kuhifadhiwa dawa Mkoani humo.

  “Kituo hiki ni wajibu wetu kukilinda na kukitunza vizuri ili kiendelee kutoa huduma, lakini Mkurugenzi wa Halmashauri naomba utumia sheria za ardhi zilizopo kuhakikisha unawaondosha watu wanaovamia eneo tulilotenga kwa ajili ya shughuli za MSD hili ni agizo natoa kama Waziri nila serikali siyo langu kama Mbunge wa Jimbo hili” alisisitiza.

  Mbunge huyo aliongeza kuwa kutokana na waathilika wakubwa ni Kimama na watoto pamoja na Wilaya hiyo kukubwa na magojwa ya mlipuko hususani Malaria ambayo yalipelekea serikali na Wizara ya Afya kutuma wataalamu na kufanya utafiti kisha kuanzisha mkakati wa kupulizia dawa ya Ukoko kwenye nyumba za Wilayah ii ili kudhibiti ugonjwa huo uliokuwa ni janga kwa wananchi.


  0 0


  MKUU WA MKOA WA GEITA NA KAIMU MKUU WA MKOA WA MWANZA SAID MAGARULA AKIMKARIBISHA  JANA 9/3/2014 MKE WA WAZIRI MKUU MAMA TUNU PINDA MKOA WA MWANAZA AMBAPO ALIFUNGUA TAMASHA LA WANAWAKE (WOMEN DIALOGUE FRONT 2014) IKIWA NI SEHEMU YA MAANZIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI YALIYOFANYIKA KATIKA HOTELI YA JB BELMONT YA JIJINI MWANZA. HAFLA HIYO ILIYO ANDALIWA NA MIKAELA WOMEN EMPOWERMENT INITIATIVES.PICHA PMO 

   MKE WA WAZIRII MKUU MAMA TUNU PINDA AKIPOKEA SHADA LA MAUA KUTOKA KWA MTOTO RAIYAH ADAM MARA BAADA YA KUTUA KWENYE UWANJA WA NGEGE WA MWANZA JANA TAYARI KWA KUFUNGUA TAMASHA LA WANAWAKE (WOMEN DIALOGUE FRONT 2014) IKIWA NI SEHEMU YA MAANZIMISHO YA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YALIYOFANYIKA KATIKA HOTELI YA JB BELMONT . TAMASHA HILI LILILOANDALIWA NA MIKAELA.ALIYESIMAMA NYUMA NI KAIMU MKUU WA MKOA NA MKUU WA MKOA WA GEITA SAID MAGARULA NA KATIKA NI EDITH MUDOGO MWENYEKITI WA MIKAELA  NA MWISHO NI MARGARETH KAZI MSHAURI WA MIKAELA.  

  PIX 2 NI KATIBU WA MIKAELA IDDA ADAM AKIMPOKEA MKE WA WAZIRI MKUU MAMA TUNU PINDA MKOA WA MWANZATAYARI KUFUNGUA TAMASHA LA WANAWAKE JANA 9/03/2014  LILILO ANDALIWA NA MIKAELA IKWA NI SEHEMU YA KUSHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI .PICHA NA PMO

  ==============  ==========  ========


  MKE WA WAZIRI MKUU, Mama Tunu Pinda amewaasa wanawake nchini kwa kuwataka wawe na nidhamu ya matumizi ya fedha za mikopo wanayochukua kwa ajili kuendeshea miradi kama kweli wanataka kufanikiwa na kutimiza malengo waliyojiwekea.


  Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili, Machi 9, 2014) wakati akifungua Tamasha la Wanawake (Women Dialogue Front -2014) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililofanyika kwenye hoteli ya JB Belmont, jijini Mwanza.

  Akizungumza na washiriki wa tamasha hilo lililoandaliwa na asasi ya Mikaela Women Empowerment Initiatives  ya jijini Mwanza, Mama Tunu Pinda alisema: “Japokuwa kwenye ujasiriamali kuna changamoto nyingi lakini kuna wenzenu walioweza kufanikiwa. Hivyo nina imani kubwa kuwa nanyi mtafanikiwa, ili mradi muwe na nia ya dhati katika kutekeleza malengo mliyojiwekea.”

  Akisisisitiza haja ya kuwa na uthubutu kwenye ujasiriamali, Mama Pinda alisema: “...Lakini niwatake wanawake wenzangu kuwa wajasiri na wenye kuthubutu na kuwa na mipango inayotekelezeka ili muweze kutimiza ndoto zenu.”

  “Sisi wanawake tunapaswa kujitambua na kuzitumia fursa zilizopo ambazo kama tutazizingatia ipasavyo, zitatusaidia kujenga ustawi wa maisha yetu na jamii kwa maana kukua kwa uchumi kwa mwanamke ni kukua kwa uchumi wa familia, kaya na jamii pia.”

  Aliwataka akinamama nchini watumie vizuri fursa za mikopo na wawe waaminifu katika kutumia na kurejesha mikopo hiyo. “Tumieni fursa za mikopo kwa kukopa kwa uaminifu, kimkakati na kwa malengo ili kuendeleza miradi yenu na jamii kwa ujumla,” alisisitiza.

  Kwa upande wake, Mama Tunu Pinda alisema ana imani kwamba taasisi za fedha zitatoa kipaumbele katika kutoa mikopo yenye riba na masharti nafuu kwa wanawake wajasiriamali ili kuleta maendeleo ya kweli miongoni mwa akinamama.


  Akizungumzia kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) katika jiji la Mwanza, Mama Tunu Pinda aliwataka wanawake hao kuwa makini kwa kujikinga na maambukizi mapya ya VVU kwa vile Jiji hilo lina kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa huo.

  “Utafiti unaonyesha kwamba Jiji la Mwanza linashika nafasi ya 11 kati ya mikoa 30 ya Tanzania sawa na asilimia 4.2. Na kati ya hao wanawake ndio wanaongoza kuliko wanaume. Hii inasababishwa na wengi wao kukosa uelewa wa kutosha katika masuala ya afya ya UKIMWI pamoja na kukosekana kwa usawa wa kijamii, kiuchumi na unyanyasaji wa wanawake na wasichana walio ndani na nje ya mahusiano,” alisema Mama Pinda.

  Alisema takwimu hizo zinaonyesha ni jinsi gani mwanamke anaweza akuchukua tahadhari mapema na ya haraka katika kupambana na ugonjwa huo hatari. “Lakini pia mimi niseme tu, mwanamke una nafasi kubwa sana katika kupambana na ugonjwa huu kwa kuchukua hatua za dhati na za makusudi katika kujikinga wewe na familia yako kama mwanamke unayejitambua,” aliongeza.

  Mapema, akisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa asasi ya Mikaela Women Empowerment Initiatives, Bibi Edith Mudogo alisema asasi hiyo inayojishughulisha na utoaji wa mikopo midogodogo kwa akinamama, ina jumla ya wanachama 102 ambao wanajihusisha na biashara, kilimo na ufugaji.

  Alisema wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo kunyimwa mikopo na taasisi za kifedha kutokana na masharti yasiyo rafiki yaliyowekwa na taasisi hizo; ukosefu wa fedha unaowanyima fursa ya kuwafikia wanawake waishio vijijini na usumbufu unaopatikana katika kukopa na kurejesha mikopo ingawa ni kwa kiasi kidogo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 3021,
  DAR ES SALAAM.

  JUMATATU, MACHI 10, 2014.

  0 0

   Meneja Mikataba wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Taddious Theodore akimkabidhi  msaada wa Shuka Julieth Mchanga  kwa niaba ya wazee wenzake 45,  wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walitembelea kituoni hapo kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam, vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
   aadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  wakiwa katika picha ya pamoja na wazee wasiojiweza wa kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation ilichopo Yombo Kilakala wakati walipokwenda kuwapa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mashuka, blanketi,vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 2.5 
   Wafanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink   wakiwa na mizigo mbalimbali ya vyakula wakati  walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika eneo la Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,  wanaolelewa na Kituo cha  Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchere na mafuta ya chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
   Mhasibu wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Joyna Mwafute akimlisha  chakula mmoja wa wazee waishio katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo kilakala Bi.Tabu Juma( 65) wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipofika kituoni hapo kutoa misaada wa vyakula,mafuta ya kula,blanketi na mashuka vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
   Meneja  Mafunzo na Uendelezaji wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink,Maxine Makenzie, akimpatia soda mmoja wa wazee wasiojiweza wanaotunzwa katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo kilakala jijini Dar es Salaam,wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipofika kituoni hapo kutoa msaada wa Vitu mbalimbali vikiwemo mashuka,blanketi na vyakula mbalimbali kwa wazee 45 waishio katika kituo hicho.
   Meneja  Mafunzo na Uendelezaji wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink,Maxine Makenzie,akihudumia chakula baadhi ya wazee wasiojiweza   wanaoishi katika kituo cha Tushikamane Pamoja kilichopo Yombo Kilakala jijinin Dar es Salaam,wakati wafanyakazi wa Kampuni ya hiyo walipokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile Mashuka,blanketi na vyakula mbalimbali. 
   Mhasibu wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Joyna Mwafute akisalimiana na Bi,Julieth Mchanga (80)  wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika kituo hicho cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo  Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam.Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  vikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5

   Mfanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  Maria Chundu akiteta jambo na Bi.Khadija Sultan (78) wa kituo cha kulelea wazee cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala mara walipotembelea kituo hicho kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika kituo hicho.Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.

   Mfanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Zabida Kibiki akimvisha shuka baada ya kumkabidhi msaada huo John Shitundu ambaye ni miongoni mwa wazee waliopo chini ya kituo chaTushikamane Pamoja Foundation wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa kituo hicho Rose Mwapachu.
  Baadhi ya wazee wanaoishi na kutunzwa katika Kituo cha  Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,wakicheza pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  walipowatembelea wazee hao mahususi kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.  0 0

  MILIONI 80KUNUNUA GARI YA WANAFUNZI IFUNDA

  Na Denis Mlowe,Iringa

  ZAIDI ya shilingi milioni 80 zinatarajia kutumika katika ununuzi wa gari ya wanafunzi wa shule ya wasichana Ifunda iliyoko katika wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.

  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Zaina Salingwa alisema hayo katika harambee iliyofanyika sambamba na mahafari ya nane ya kidato cha sita shuleni hapo kuwa kuna changamoto kubwa ya usafiri wa wanafunzi katika shule hiyo na wanatarajia kukusanya fedha hiyo kuweza kuondokana na hali hiyo.

  Alisema shule inakabiliwa na wakati mgumu inapojitokeza dharula katika kutekeleza majukumu ya shule na wanafunzi wanapohitaji gari wakipatwa na matatizo hususani katika kipindi cha ugonjwa.

  “Tunaomba wadau mbalimbali, wazazi na makampuni mbalimbali kutuchangia katika ununuzi wa gari la wanafunzi ambalo bei yake ni kubwa hivyo tunategemea sana misaada kutoka kwao” alisema Salingwa

  Aidha alisema kuwa shule hiyo ina upungufu wa vitabu kwa wanafunzi  na tatizo la walimu katika masomo ya Hisabati, Fizikia, Kemia na baiolojia na kuongeza kuwa shule ina walimu wawili wa somo la hisabati, walimu wawili kemia na mwalimu mmoja wa somo la fizikia huku idadi ya wanafunzi wanaosoma sayansi ni kubwa na kuitaka serikali kuwaongezea walimu.

  Salingwa alisema miundo mbinu ya shule imechakaa kutokana na kujengwa zaidi ya miaka 30 iliyopita na kukabiliana na uchakavu wa vyoo, jiko, mifumo ya umeme na maji taka.

  “ Shule hii inakabaliwa na uchakavu wa maeneo yake hii inahatarisha usalama wa mali za shule, mali za wanafunzi na maisha yao, tunaomba serikali na wadau  mbalimbali pia katika hili watusaidie ukarabati unaohitaji fedha nyingi.” Alisema Salingwa

  Kwa upande wao wanafunzi wa wanaotarajia kuhitimu kidato cha sita katika risala iliyosomwa na Hildegarda Colman walisema gari la shule imekuwa changamoto kubwa katika shule hiyo na mara nyingi mwanafunzi anapougua na kulazimika kusafirishwa kwenda hospitalini nyakati za usiku inawawiha vigumu kupata usafiri.

  Colman alisema shule inakabiliwa na upungufu wa vitabu kwa masomo yanayotolewa hapo ya sayansi japokuwa kila mwaka vinanunuliwa lakini vimekuwa havitoshelezi kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi.

  Aidha alisema shule ya wasichana Ifunda inakabiliwa na ukosefu wa maktaba hivyo wanalazimika kutumia chumba cha darasa kwa matumizi ya maktaba ambayo hata hivyo haikidhi mahitaji ya wanafunzi.

  “Tunakabiliwa na ukosefu wa kompyuta hata moja kwa matumizi ya wanafunzi kama unavyojua mabadiliko ya dunia, mitaala inabadilika, kukosekana kwa kompyuta kunatunyima fursa ya kuendana mabadiliko hayo, tunaomba tusaidiwe hata komputa chache tujifunze na tuzitumie kutafuta maarifa ya kitaaluma” alisema Colman

  Katika harambee Kampuni ya Asasi ilichangia jumla ya shilingi milioni 3 na jumla ya fedha zilizopatikana ni shilingi milioni 9.7 zilipatikana kati ya hizo fedha taslimu shilingi milioni 5.5 na ahadi shilingi milioni 4.2.

  0 0

  picha kwa hisani ya mitandao ya kijamii.

  Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mh.PETER MSIGWA  kwa mara nyingine amefikishwa leo  katika mahakama  kuu ya mkoa , kufuatia tuhuma inayomkabili ya kufanya vurugu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya nduli manispaa ya iringa.

  Tukio hilo limetoke tarehe 6 ya mwezi wa pili ambapo  SALUM  KEITA mjumbe wa kampeni hizo kupitia  chama cha mapinduzi alidai kufanyiwa vurugu na mbunge wa jimbo la iringa mjini kwa kumpiga.


  Kesi hiyo imesomwa leo  katika mahakama ya wilaya ya Iringa mbele ya jaji   ALOYCE  MASUA na kesi hiyo imeahirishwa na kutajwa kusikilizwa

  tarehe 9 ya mwezi wa 4 mwaka huu.  0 0

  Mabadiliko ya hali ya nchi kwa asilimia  90 yanasababishwa na shughuli za wananchi, kutokana na kilimo pamoja na viwanda ambavyo huongeza hali joto angani.


  Hayo yamesemwa na afisa mradi wa maji mazingira na afya  kutoka  shirika lisilo la kierikali la IDYDC lilopo mkoani hapa   CASTOR DAVID nakusema kuwa zaidi ya asilimia 60 ya eneo la nchi kavu la dunia limeumbwa na milima kutokana na kuongezeka kwa joto duniani.


  CASTOR  ametaja baadhi ya athari ambazo zimeweza kutokea kutokana na kuongezeka kwa joto duniani. Naye afisa mradi wa mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi katika asasi isiyokuwa ya kiserikali  mazombe mahenge development association(MMADEA) BI FELISTA KASUGAametaja baadhi ya matukio ambayo huweza kusababisha mabadiliko ya hali ya nchi duniani.
    
  WAKAZI WA MAFINGA WAITAKA MAMLAKA YA MAJI KUTATUA TATIZO LA MAJI WILAYANI MUFINDI.

  Wakazi wa mji wa  mafinga wilayani mufindi mkoani hapa ,wameitaka mamlaka ya maji wilayani humo kutatua tatizo la maji ili jamii iweze kupata maji ya kutosha na  kujenga vyoo vya kisasa.


  Wakizungumza kwa  nyakati tofauti  wakazi wa mji mdogo wa mafinga wamesema uwezekano wa  kujenga vyoo vya kisasa upo,  tatizo ni serikali kushindwa kuwahakikishia uwepo wa maji ya  kwa wakazi hao.  Joseph Kishame miongoni  wa miliki wa hoteli pamoja na nyumba za kulala wageni mjini mafinga amesema jitihada za  ujenzi  wa vyoo bora zinaendelea  ili kuwa na vyoo bora kwa watumiaji, na  wana lazimika kutumia njia za  kawaida katika ujenzi  kutokana na changamoto ya ukosefu wa maji ya kutosha.


  WANANCHI WA SAO HILL WAMLALAMIKIA DIWANI KWA KUTOWATEMBELEA.


  Wananchi wa kata ya Sao hill  mji mdogo wa mafinga  wilayani Mufindi,wamemlalamikia diwani wa  kata hiyo  PASILI   MGODA  kushindwa kuwatembelea wakazi wa kata hiyo na kujua matatizo yanayowakabili.


  Akizungumza  diwani MGODA amekiri kutoitisha  mikutano kwa muda mrefu  kwa  kuwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kiafya.


  amewataka wananchi wake kuwa na subira na kuahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi hao,ikiwemo changamoto ya ukosefu wa  maji  na umeme .


  Aidha Mgoda amesema kata hiyo inashindwa kupata mapato ya kutosha kutokana na sehemu ya kata yake kuwa  finyu na  kushindwa kuwa na mapato ya kutosha .
  0 0

  D92A4042

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyewahi kuwa mkuu wa kitengo cha maafa katika ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Bakari Shaabani huko Ada Estate jijini Dar es Salaam jana.Marehemu amezikwa nyumbani kwao huko Unguja Zanzibar Jana.
  D92A4062
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa aliyewahi kuwa mkuu wa kitengo cha Maafa katika ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Bakari Shaabani nyumbani kwake Ada Estate jijini Dar es Salaam jana.
  D92A4091
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha maafa meja Jenerali Bakari Shaabani nyumbani kwake Ada Estate jijini Dar es Salaam jana.Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda Zanzibar na kuzikwa.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Mgombea Ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bwa.Mathayo Torongei akizungumza na wanahabari mapema leo baada ya kutangazwa na Kiongozi wa Kampeni jimbo la Chalinze,Bwa.John  Mrema,ambaye ndio kiongozi wa kampeni za chalinze kuwa ndiye atakayeibebe bendera ya chadema jimboni humo kupambana na mgombea wa CCM,Ndugu Ridhiwani Kikwete. 


  0 0

  Makamu Mwenyekiti (BARA) wa CCM,Ndugu Philip Mangula akihutubia kwenye kumtano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga,mapema leo jioni kwenye Kata ya Kalenga-Iringa vijijini.

  0 0

  Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga,Godfrey Mgimwa akiwa emebebwa juu na Wananchi na wanachama wa CCM wakielekea kwenye eneo la Mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Wakazi wa Kalenga A,wakifurahia jambo wakati wa mkutano wa kampeni za Ubunge kupitia CCM zilizofanyika leo.
  Wakifuatilia kwa makini
  Makamu Mwenyekiti (BARA) wa CCM,Ndugu Philip Mangula akihutubia kwenye kumtano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga,mapema leo jioni kwenye Kata ya Kalenga A-Iringa vijijini.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga,kupitia tiketi ya CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akiwahutubia wakazi wa kata ya Kalenga A mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akipokea kadi ya Chadema iliyorudishwa na Ndugu Said Omary Mbilinyi ambaye amerudi CCM baada ya kutoelewa sera na siasa za Chadema.


  Baadhi ya Wananchi wakifautailia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kampeni
  Msanii maarufu Tanzania mwenye vipaji vya kuigiza ,kucheza na kuimba Dokii akiimba na kucheza pamoja na Diwani wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa UWT Iringa Vijijini Ndugu Shakira Kiwanga wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge za CCM kwenye kitongoji cha Tosamaganga.
  Wananchi wakifurahia jambo
  Wanafuatilia kwa makini

  Usijali kijana wetu,tayari ushindi ni wako-
  Sister Paula Msambwa mwenye umri wa miaka 73 na aliyewahi kuwa mwalimu wa Marehemu William Mgimwa kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne ambapo alimfundisha somo la hisabati, amesema amefarijika kumuona mtoto wa mwanafunzi wake akigombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Kalenga.pichani shoto ni Mgombea Ubunge wa jimbo hilo,kwa tiketi ya CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akisikiliza kwa makini
  Godfrey Mgimwa akipewa mkono wa kila la kheri na Sister Paula,kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu
  Wanachama wa CCM wakiserebuka na Mgombea wao wakielekea kwenye kata ya Kalenga A

  Wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiserebuka na Mgombea wao wakielekea kwenye kata ya Kalenga A kwa ajili ya mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo.

  0 0

  DSC_0128
  Jaji wa Mahakama ya Rufani, Edward Rutakangwa akifungua rasmi mafunzo ya siku nne juu ya sheria za kimataifa za kazi kwa majaji na wasajili wa mahakama nchini yalioandaliwa na Shirika la Kazi Duniani mjini Bagamoyo.

  Musindo amesema katika mafunzo hayo yatatoa fursa kwa majaji na wasajili wa Mahakama kujifunza sheria za kimataifa za kazi na utatuzi wa migogoro katika sehemu za kazi.
  Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mgaya amesema kwa kuwa sheria ya kazi ni mpya ya mwaka 2004 bado kuna majaji na wasajili wa mahakama haifahamu vya kutosha ili kukidhi haya ya jamii.

  Amesema mafunzo hayo ya siku nne ni fursa pekee kwa majaji na wasajili wa mahakama kujifunza sheria za kimataifa za kazi ili kuleta tija katika maamuzi yao mbalimbali.
  DSC_0094
  Baadhi ya majaji na wasajili wa mahakama nchini wanaohudhuria mafunzo ya siku nne juu ya sheria za kimataifa za kazi yalioandaliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mjini Bagamoyo.
  DSC_0061
  Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la kazi duniani (ILO) kwenye nchi nne Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, Alexio Musindo akizungumza na washiriki kwenye mafunzo hayo mjini Bagamoyo.
  DSC_0099
  Jaji Regina Rweyemamu kutoka Mahakama ya kazi, akizungumza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kama majaji katika mahakama za kazi nchini.
  DSC_0139
  Baadhi ya majaji na wasajili wa mahakama nchini wakifuatilia yanayojiri kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku nne yaliyoandaliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) yanayoendelea mjini Bagamoyo.


  DSC_0020
  DSC_0079
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw. Nicholas Mgaya akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo ya siku nne kuhusu changamoto katika mahakama za kazi, upungufu wa majaji na vitendea kazi kama moja ya vitu vinavyochangia mrundikano wa kesi katika mahakama hapa nchini.
  DSC_0089
  Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri (ATE) Wakili, Cornelius Kariwa akitoa hotuba yake kwa niba ya chama cha waajiri nchini umuhimu wa kufahamu sheria za kimataifa za kazi duniani.
  DSC_0015
  Baadhi ya wasijili wa Mahakama ya kazi wakiwa kwenye mafunzo ya siku nne yanayoendelea mjini Bagamoyo.
  DSC_0144
  Mgeni rasmi Jaji wa Mahakama ya Rufani, Edward Rutakangwa (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la kazi duniani (ILO) kwenye nchi nne Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, Bw. Alexio Musindo wakati wakielekea kupiga picha ya pamoja. Kulia ni Afisa Mipango mwandamizi wa shirika la kazi duniani (ILO) Anthony Rutabanzibwa.
  DSC_0152
  Mgeni Rasmi Jaji wa Mahakama ya Rufani, Edward Rutakangwa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo ya siku nne yanayoendelea mjini Bagamoyo.
  DSC_0003
  Mgeni rasmi Jaji wa Mahakama ya Rufani, Edward Rutakangwa (katikati) akiwasili kufungua rasmi mafunzo ya siku nne juu ya sheria za kimataifa za kazi kwa majaji na wasajili wa mahakama nchini yalioandaliwa na Shirika la Kazi Duniani mjini Bagamoyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la kazi duniani kwenye nchi nne Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, Alexio Musindo.

  Na Damas Makangale, Bagamoyo, MOblog Tanzania
  JAJI wa Mahakama ya Rufani, Tanzania, Edward Rutakangwa amesema bado kuna upungufu mkubwa wa majaji katika mahakama za Tanzania kiasi cha kusababisha mrundikano wa kesi katika mahakama hapa nchini. MOblog inaripoti.

  Akifungua rasmi mafunzo ya siku nne kwa majaji, wasajili na wasajili wasaidizi wa Mahakama ya Kazi, Jaji Rutakangwa amesema kwamba pamoja na Mheshimiwa wa Rais kuteua majaji bado kuna upungufu mkubwa wa majaji nchini. “Tatizo la majaji kuwa wachache ni la muda mrefu pamoja na juhudi za Mheshimiwa rais kupunguza ukubwa wa tatizo kwa minajili ya kuleta ufanisi katika idara ya mahakama,” amesema Jaji Rutakangwa

  Amesema mafunzo hayo ya siku nne yataleta matokeo mazuri kwa majaji na wasajili wa mahakama katika kuleta haki kwa wafanyakazi na kufanya kazi kwa viwango vya kimataifa vya kazi duniani.
  DSC_0010
  Meza kuu ikipitia makabrasha yao kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mafunzo hayo.
  Jaji Rutakangwa alilisisitiza kwamba kuna umuhimu wa majaji kujua haki na sheria za kazi kwa hiyo mafunzo hayo yatatoa fursa kwao kuelewa sheria za kazi ili kuwawezesha kutoa hukumu kwa kuzingatia sheria na haki za wafanyakazi nchini.

  Amesema kuna umuhimu wa majaji na wasajili wa mahakama kuelewa kwa kina sheria za kimataifa za kazi na jinsi ya kuzitumia katika mahakama za ndani ya nchini. Kwa upande, Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la kazi Duniani, Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda, Alexio Musindo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekuwa walifanya mabadiliko kadhaa ya kijamii na kiuchumi.
  DSC_0030
  Mmoja wa wawezeshaji kutoka Ghana akijitambulisha kwa washiriki wa mafunzi hayo.
  Amesema moja ya mipango ya serikali hizo mbili ni kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya soko huria pamoja na kuweka vyombo vya kudhibiti soko hilo kama vile Mahakama ya kazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

  “Shirika la kazi duniani litaendelea kufanya kazi kwa karibu na mahakama ya kazi pamoja na Tume Usuluhishi katika kuleta ufanisi katika sekta ya kazi kwa kujali maslahi ya wafanyakazi katika maeneo ya kazi duniani,” amesema Musindo.

older | 1 | .... | 242 | 243 | (Page 244) | 245 | 246 | .... | 1897 | newer