Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 244 | 245 | (Page 246) | 247 | 248 | .... | 1897 | newer

  0 0

  1 (2)  
  Rais Jakaya Kikwete wa pili kushoto akipata maelezo kuhusu msaada wa magari 11 kutoka kwa Mkurugenzi  wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir (katikati)na  kulia ni   Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa  na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili  katika hifadhi za Serengeti Selous na Maswa.4 (1)Mkurugenzi  wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir(katikati) akitoa hotuba yake kuhusu msaada  magari 11 waliyoyatoa kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili  katika hifadhi za Serengeti ,Selous na Maswa,kushoto wa pili ni Rais Jakaya Kikwete na wa kwanza ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel na kulia wa pili  Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.6 (1)  
  Rais Jakaya Kikwete wa pili kushoto akionesha moja ya ufunguo wa msaada wa magari 11 mara baada ya kukabidhiwa na  Mkurugenzi  wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir (  kulia wanne) katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili  katika hifadhi za Serengeti ,Selous na Maswa.9  
  Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel akizungumza jamabo wakati wa hafla hiyo  iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.IMG_0461 
  Rais Jakaya  Kikwete  akitoa hotuba yake kushukuru  msaada  magari 11 ulioyatolewa na Mkurugenzi  wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili  katika hifadhi za Serengeti,  Selous na Maswa. Picha na Magreth Kinabo -MAELEZO

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akionyesha mfano wa karatasi la kupiga kura kwa wanachama wa CCM wanaoishi kwenye kitongoji cha Ulete,Kijiji cha Muwimbi mkoani Iringa .
   Mgombea wa kiti cha Ubunge jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM Ndugu Godfrey Mgimwa akiomba kura kwa wakazi wa kitongoji cha Ulete ,kijiji cha Muwimbi mkoani Iringa ambapo aliwaambia tusikilize sera za kuleta maendeleo na si porojo zisizo na tija kwa Taifa letu.
   Katibu wa UWT CCM Arusha mjini Ndugu Rehema Mohamed akiwahutubia wakazi wa kitongoji cha Ulete kijiji cha Muwimbi na kuwaambia Mgimwa atasukuma maendeleo ya Jimbo hilo na atakuwa muwakilishi mzuri wa jimbo hilo kwa wananchi Bungeni na kwa madiwani.

   Mwakamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akihutubia viongozi na Mabalozi 26 wa CCM waKata ya Ifunda,kijiji cha Mfukulembe ambapo aliwasihi kuwa makini na zoezi zima la upigaji kura na kutupilia mbali kauli za vyama pinzani zinazosema zitalinda kura kwa helkopta kwani kila chama kinatoa wakala wake wa kusimamia wakati wa zoezi la kupiga kura.Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) aliendelea kuhutubia bila kujali mvua.
   Baadhi ya Viongozi wa CCM kata ya Ifunda wakiangaia mfano wa karatasi la kupigia kura ambapo wameshauria kusimamia watu wao kushiriki kupiga kura siku ya tarehe 16 March 2014.
  Godfrey Mgimwa mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM akihutubia viongozi na mabalozi 26 wa CCM wa kata ya Ifunda kijiji cha Mfukulembe na kuwaambia kwa kutumia ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo atavipa kipaumbele elimu, afya , na ujenzi wa barabara.

  0 0

  MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi. TUNAOMBA SANA MSAADA WENU MTOTO ATIBIWE KWANI ANATESEKA SANA MTOTO HUYU

  Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya Thobias Mwalyego baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari alilazimika kwenda hadi mtaa wa Maendeleo Iyunga ili kupata maelezo ya kina kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa zozote juu ya mtoto huyo.  Baba wa mtoto huyo Joseph Njavike amesema wakati wa tukio yeye alikuwa hayupo nyumbani .

  Mama mzazi wa Adorotea  Milika Kibelege.  Hatimaye Wazazi wa mtoto Adorotea Njavike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne wamewasili Jijini Mbeya kutoka Mkoani Njombe baada ya kutafutwa kwa muda mrefu kutolea maelezo ya ajali ya mtoto aliyeungua moto miezi saba iliyopita.


  Ajali hiyo imepelekea ulemavu mkubwa kwa mtoto huyo ambapo ngozi ya kidevu imeungana na kifua na kumsababishia ulemavu unaomfanya kushindwa kula vizuri na macho kushindwa kufumba.


  Baba wa mtoto huyo Joseph Njavike amesema wakati wa tukio yeye alikuwa hayupo nyumbani kwani mtoto alibaki na mama yake mzazi aitwaye Milika Kibelege.


  Milika amesema kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa mbili usiku alipokuwa anapika na yeye kupigwa na kitu kichwani kisha mtoto kudondokea motoni nay eye kuzirai kabla ya mtoto kuokolewa na majirani baada ya kusikia kilio kikali kutoka kwa mtoto.


  Milika  amesema kuwa baada ya tukio mtoto alikuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kijiji cha Wanzali na kwamba yeye alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo hali iliyomlazimu Dada yake kumchukua mwanae hadi Mbeya ili aweze kupatiwa matibabu zaidi.


  Kutokana na uduni wa maisha wameshindwa kufika Mbeya kumjulia hali mtoto wao hadi walipofuatwa na Dada yake Machi 8 mwaka huu kuwa wanahitajika Mbeya  ili kibali kitolewe mtoto asafirishwe kwenda Hospitali ya Mhimbili kwa matibabu zaidi.


  Mama Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye alitoweka na mtoto huyo amesema anaomba radhi kwa kuondoka bila kuaga na mtoto huyo kwani alichanganyikiwa alipoambiwa mtoto itabidi asafirishwe kwenda India na matibabu yake yatachukua miezi sita hivyo akaona ni bora awafuate wazazi wa mtoto huko njombe wakajadiliane

  Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya Thobias Mwalyego baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari alilazimika kwenda hadi mtaa wa Maendeleo Iyunga ili kupata maelezo ya kina kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa zozote juu ya mtoto huyo.


  Mwalyego amesema kuwa kuanzia sasa ataendelea kufuatilia maendeleo ya mtoto huyo kuhakikisha anapatiwa huduma zinzostahili ukiwemo msamaha wa matibabu kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya.


  Kwa upande wa wazazi wamewashukuru wasamaria wema waliojitokeza kuchangia matibabu ya mtoto wao na madaktari wanaofanya juhudi za kuhakikisha mtoto huyo anapatiwa upasuaji wa haraka.


  Aidha amekubali kuandamana na mwanae katika matibabu endapo ataruhusiwa kwenda kokote na Afisa Ustawi wa Jamii alishauri pia Mama mkubwa kuongozana na Familia hiyo kutokana na udhaifu wa mama Adorotea


  Na Mbeya yetu

  0 0


  Tunawaomba RADHI kutokana na kutoonekana kwa vipindi vyetu hewani kuanzia  jumamosi tarehe 8. Hii imetokana na sisi Kama waandaaji kuwaomba TBC KUSITISHA kurusha vipindi.


  Kipindi cha kwanza kilirushwa saa 4.20 usiku, cha pili kikarushwa saa 4.50 usiku, cha tatu kikarushwa saa 3 usiku na cha nne (cha jumamosi) HAKIKURUSHWA KABISA!

  Kwa kuwa jambo hili linahusisha makubaliano, tunaomba muwe na subira wakati tukirekebisha mambo ili muweze kuitazama Maisha Plus SEHEMU na muda UNAOELEWEKA ndani ya siku chache zijazo. Tunawaomba RADHI kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

   


  Imetolewa na Uongozi
  dMb Co. Ltd

  0 0

  Baadhi ya wananchi wa Namanyere wilayani Nkasi wakichangia damu katika siku ya uzinduzi wa siku ya Utepe mweupe. Baadhi ya wananchi wa Namanyere wilayani Nkasi wakichangia damu katika siku ya uzinduzi wa siku ya Utepe mweupe.Mmoja wa wananchi akichangia damu huku akisaidiwa na daktari Mmoja wa wananchi akichangia damu huku akisaidiwa na daktariMkuu wa Wilaya ya Nkasi, Idd Kimanta akiwa na Mkurugenzi wa Evidence for Action, Craig John wakiwa kwenye viwanja vya Sabasaba ambapo mamia ya wananchi walijitolea damu. Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Idd Kimanta akiwa na Mkurugenzi wa Evidence for Action, Craig John wakiwa kwenye viwanja vya Sabasaba ambapo mamia ya wananchi walijitolea damu.[/caption] [caption id="attachment_43806" align="aligncenter" width="640"]Mratibu wa Mtandao wa Utepe mweupe, Bi. Rose Mlay akiwapongeza mke na mume waliojitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wanawake wajawazito. Mratibu wa Mtandao wa Utepe mweupe, Bi. Rose Mlay akiwapongeza mke na mume waliojitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wanawake wajawazito.[/caption] MTANDAO wa Utepe Mweupe na Uzazi Salama (White Ribbon Allience for Safe Motherhood) umekemea vikali tabia zinazofanywa na baadhi ya watumishi wa hospitali na vituo vya afya ya kuuza damu ambayo kimsingi inatakiwa kutolewa bure kwa wahitaji. 

  Kauli hiyo ya pamoja imetolewa jana wilayani Nkasi na wanaharakati wa mtandao huo walipokuwa katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya Utepe Mweupe wilayani hapa, mkoani Rukwa. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ‘Evidence for Action’ ambao wanatekeleza mradi ujulikanao kama ‘Mama Ye’, Craig John, alisema wamepata malalamiko toka kwa wananchi ya kuwa kuna tabia ya baadhi ya watendaji kwenye sehemu za kutolea huduma za afya huwauzia wagonjwa damu kitu ambacho hakikubaliki.

   “...Wakati tunapita pita mitaani kuhamasisha wananchi kuja kujitolea damu kwa ajili ya akinamama wajawazito wanaohitaji kuongezewa damu, wananchi walituambia kuwa baadhi ya watendaji wa afya wamekuwa kero kwao kwani wanawauzia damu pindi wanapokuwa wanaihitaji,” alisema Craig. Naye Mratibu wa Utepe Mweupe nchini, Bi. Rose Mlay aliitaka serikali kutenga bajeti mahususi katika mwaka wa fedha 2014/2015 ili kuhakikisha vituo vya afya wanatoa huduma za dharura ikiwemo upasuaji na damu salama.

   “...kama mtoto amekaa vibaya tumboni kwa mama au hata kama amepigwa mwanamke huyu anaweza kusaidiwa kwa kufanyiwa upasuaji na kuongezewa damu salama pekee, hivi ndivyo vitakavyo muokoa,” alisema Rose. Sherehe za kilele cha Wiki ya Utepe Mweupe zinatarajiwa kufanyika Machi 15, 2014 wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.

  0 0


  Jumla ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) ifikapo tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika shule za Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo 5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada).

  Orodha rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa itatangazwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) ifikapo tarehe 15 Machi, 2014.

  Walimu wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri walikopangiwa ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja.
  Inasisitizwa kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi zifanyiwe kazi na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili 2014 na hivyo kuepuka ulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza ajira.

  Mwalimu yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za msingi zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo. Ikumbukwe kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa mahitaji ya walimu. 

  Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba na nauli ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu atakayeripoti kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri walikopangwa walimu hao. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri alikopangwa.

  Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kufanya kazi walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho baada ya mwalimu kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.

  Ni vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya. Walimu ambao tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao na kuendelea na kazi.

  IMETOLEWA NA
  JUMANNE A. SAGINI
  KATIBU MKUU
  OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


  TAARIFA KWA UMMA


  UZINDUZI WA SIKU YA TAIFA YA KUTUNDIKA MIZINGA

  TAREHE 18 MACHI 2014


  Siku ya Taifa ya Kutundika Mizinga itaadhimishwa kitaifa mkoani Katavi katika wilayani Mlele tarehe 18 Machi 2014. Aidha, siku hiyo mikoa mingine itaadhimisha kimkoa katika wilaya na vijiji vilivyochaguliwa.  Kauli Mbiu ya mwaka huu ni: “Boresha Ufugaji Nyuki, Linda Ubora wa Mazao Yake”.


  Madhumini ya siku hii ni kuendeleza Ufugaji Nyuki unaolenga kuongeza idadi ya wafuga nyuki, usimamizi bora wa makundi ya nyuki na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa kuzingatia ubora na teknolojia za kisasa. Aidha, siku hii inatumika kuhamasisha uhifadhi endelevu wa raslimali za misitu na nyuki.


  Siku hii itakuwa chachu ya kuwahamasisha wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki kwa wingi katika ufugaji nyuki wa kisasa. Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb), ambaye atashiriki kutundika mizinga katika msitu wa Mlele Kusini eneo la Kanembela na baadaye kuhutubia wananchi.

  Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa wito kwa wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kufanikisha siku hii kwenye maeneo yaliyopangwa na maeneo binafsi.  MAENEO YATAKAYOTUNDIKWA MIZINGA KATIKA MIKOA MBALIMBALI TANZANIA BARA

  NA

  MKOA

  WILAYA

  KIJIJI

  MHUSIKA/

  WAHUSIKA

  ENEO LA KUFUGIA

  1

  Simiyu

  Busega

  Mkula

  Kikundi cha Imarika

  Msitu wa Kikundi na Kijiji

  2

  Geita

  Geita

  Itina

  Kikundi cha Itina

  Msitu wa Kijiji (Ngitiri)

  3

  Mwanza

  Ilemela

  Kasamwa

  Kikundi

  Ngitiri ya kijiji

  4

  Mara

  Musoma


  Magereza

  Msitu wa Magereza

  5

  Kagera

  Missenyi

  Kenyana

  Kikundi cha Shubira

  Miti katika Mashamba

  6

  Ruvuma

  Songea

  Mtyangimbole

  Kamati ya Usimamizi Shirikishi Misitu

  Misitu wa Songea Fuel

  7

  Mtwara

  Mtwara

  Mnivata

  Kikundia

  Msitu wa Halmashauri Mtiniko Mnivata

  8

  Lindi

  Ruangwa

  Liuguru

  Kikundi cha Ufugaji Nyuki

  Msitu wa Kijiji Liuguru

  9

  Iringa

  Iringa

  Mgera na Mngalali


  Msitu wa Ubena

  Mufundi

  Shamba la Miti Sao Hill

  Shamba la Miti Sao Hill

  Shamba la Miti Sao Hill

  10

  Mbeya

  Momba

  Chilanu na Nzoka

  Vikundi vya Ufugaji Nyuki

  Mlima Malinde

  11

  Njombe

  Ludewa

  Mapogoro na Mavale

  Vikundi vya Ufugaji nyuki

  Msitu wa Sikaranyumbo

  12

  Rukwa

  Kalambo

  Kisumba, Kafukoka

  Vikundi vya ufugaji nyuki

  Msitu wa mto Kalambo

  Nkasi

  Vijiji (5) Chala A, B, na C, Chalakima na Chatekelesha

  Vikundi vya ufugaji nyuki kila kijiji mizinga 10

  Msitu wa Mlima Chale

  13

  Tanga

  Korogwe

  Mkwakwani Myusi

  Kikundi cha Ufugaji Nyuki

  Hifadhi ya asili Amani

  14

  Arusha

  Arumeru

  Nkwenankoli

  Kamati ya Maliasili ya Kijiji

  Hifadhi ya Msitu wa TFS

  15

  Kilimanjaro

  Moshi

  Kahe

  NGO

  Msitu wa Halmashauri

  16

  Tabora

  Sikonge

  Utyatya

  Kikundi cha Wafugaji Nyuki Nyahua

  Bwawa la Utyatya

  17

  Kigoma

  Uvinza

  Uvinza

  Kazaroho beekeepers cooperative society

  Msitu wa Basanza

  18

  Shinyanga

  Shinyanga

   Ukimbagu

  NAFRAC na Kikundi cha Wafugaji Nyuki Ugimbagu

  Shamba la Albano Malila

  19

  Katavi

  Mlele

  Kanembela

  Kikundi cha Ufugaji Nyuki

  Msitu wa Mlele

  20

  Morogoro

  Ulanga

  Mselezi

  Kikundi cha ufugaji Nyuki SEMA

  Msitu wa Hifadhi Mselezi

  Gairo

  Msingisi

  TFS – Meneja Wilaya

  Msitu wa Hifadhi Msingisi

  21

  Pwani

  Bagamoyo

  Msinune

  Kikundi cha Ufugaji Nyuki

  Msitu wa Simbo

  Mkuranga

  Kibuyuni

  Kamati ya Maliasili na Mazingira ya kijii

  Msitu Masanganya

  22

  Dodoma

  Kongwa

  Nyamkonga

  Kikundi cha Ufugaji Nyuki

  Msitu wa Halmashauri ya Wilaya

  23

  Singida

  Mkalama

  Nkungi

  Kikundi cha ufugaji Nyuki

  Msitu wa Kijiji

  24

  Manyara

  Babati

  Haraa

  Kikundi cha ufugaji Nyuki

  Msitu wa Kijiji


  Imetolewa na:  S.Gesimba

  Naibu Katibu Mkuu,

  Wizara ya Maliasili na Utalii,

  11/03/2014

  0 0

   Mtendaji Mkuu Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo akiwasilisha Rasimu ya awali ya Sera ya Filamu wakati wa moja ya kikao cha wadau cha kujadili rasimu ya awali ya Sera ya Filamu kilichofanyika hivi karibuni, kulia ni Mkurugenzi msaidizi kutoka Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Verediana Mushi, na Kushoto ni mdau wa filamu Bw. John Kitime.

  Wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu wakijadiliana wakati wa kikao cha wadau cha kujadili rasimu ya awali ya Sera ya Filamu kilichofanyika hivi karibuni.(Picha na Genofeva Matemu).
  ========  ======= =======
  SERIKALI YAJIPANGA KUWA NA SERA YA FILAMU

  Na: Genofeva Matemu – Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHVUM
   Serikali ya Tanzania imejipanga kuendeleza kwa dhati TASNIA ya Filamu ili kuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa wasanii na pia kuongeza uchumi wa nchi.
  Ni dhahiri kuwa sekta ya filamu ni njia madhubuti ya kutambulisha jamii kiutamaduni, kisiasa na kijamii  na pia katika kukuza na kuongeza fursa za nchi katika uwekezaji na utalii.
  Filamu na Makala za Filamu zikitumika vizuri zitaweza kuhamisha na kuondoa tofauti  mbalimbali zilizopo ndani ya jamii na hivyo kuongeza umoja na mshikamano baina ya watu wa makabila na watu wenye asili mbalimbali, hivyo kuutambulisha utamaduni wa Mtanzania.
  Kazi na shughuli za Filamu nchini zimekuwa zikisimamiwa na Sera ya Utamaduni ambayo ilitayarishwa na kupitishwa mwaka 1997 pamoja na Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza na 4 ya mwaka 1976.


  Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 2013 kumekuwepo na maendeleo  makubwa katika Tasnia ya Filamu nchini hivyo kuisababishia Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kutokidhi baadhi ya mahitaji ya tasnia ya filamu na kupelekea mahitaji ya kurekebisha Sera ya Utamaduni kama Sera mama na kutungwa kwa Sera ya Filamu.


  Mnamo Desemba 12 mwaka 2013, wadau mbalimbali kutoka Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo, Bodi ya Filamu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi walishiriki katika kikao cha wadau cha kujadili rasimu ya awali ya Sera ya Filamu.

   Wadau wengine ni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Kazi na Ajira, BASATA, Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mtandao wa Muziki, Swahili Films, ROSAF, TAPAF, Umoja wa Mashirikiano wa Filamu, Filamu Cental, Chama cha Hakimiliki Tanzania, Shirikisho la Sanaa za Maonyesho pamoja na G&S Associates and Advocates.
  Hata hivyo wadau ambao hawakushiriki walipewa nafasi na Serikali kuwasilisha maoni yao ambapo mwitiko umekuwa mzuri na maoni yanaendelea kupokelewa ili hatimaye kuwa na Sera bora na shirikishi.
  Katika kikao hicho Rasimu ya awali ya Sera ya Filamu iliwasilishwa kwa kuelezea historia fupi ya filamu nchini, vikao vya wadau vilivyofanyika vya mapendekezo ya kuwa na Sera ya Filamu kati ya mwaka 2004 na 2013, nyaraka kama Mpango Mkakati wa Bodi ya Filamu unaoonyesha haja ya kuwa na Sera ya filamu pamoja na kuelezea malengo mahususi na matamko ya Sera mpya inayopendekezwa kutungwa.
  Aidha, wadau walijadili uzoefu wa nchi nyingine kama Kenya, Nigeria, China, Afrika Kusini, Marekani, Canada, India na Uingereza na matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanyika pamoja na Changamoto zinazoikabili Tasnia ya Filamu nchini.
   Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na wadau ni pamoja na kuwa Sera itamke uanzishwaji wa  Chuo cha Taifa cha Filamu, Sera itamke kuwepo kwa Mfuko ambao utasaidia katika kuimarisha Sekta ya Filamu na Sanaa za maonyesho kwa ujumla, Sera itoe tamko kuhusu kusimamia  maadili katika tasnia ya  Filamu na kudhibiti ukatili wa kijinsia katika  tasnia ya Filamu.
  Pia walipendekeza kuwa hoja na matamko yawe na takwimu zaidi, Sera itamke namna ya kumlinda msanii wa Tanzania, mzalishaji wa ndani na wawekezaji, pamoja na kupiga vita udhalilishaji wa watoto wa kike.

  Kwa upande mwingine, wadau hao walitoa pongezi kwa Wizara kwa kuandaa Rasimu ya awali ya Sera ya Filamu iliyotokana na maoni mbalimbali ya wadau, Sera ambayo itaiwezesha Tasnia ya Filamu kupata mwelekeo bayana na kukidhi matakwa ya kila mdau katika tasnia ya filamu.


  Wizara inapenda kuujulisha umma kuwa imekua na inaendelea kushirikiana na wadau wa Filamu kwa kila hatua ili hatimaye ifanikishe azma ya kuwa na nyaraka zote muhimu katika kuendeleza, kusimamia, kuratibu na kukuza tasnia ya filamu nchini.

  0 0

    Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji  Mstaafu Damian Lubuva akifafanua jambo kwa msisitizo kuhusia na maandalizi ya mwisho ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika Machi 16,mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya Siasa,vyombo vya usalama na wadau wengine
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji  Mstaafu Damian Lubuva akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo,kuhusu uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga katika kikao cha pamoja na vyama vilivyosimamisha wagombea kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulioko Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini.Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Machi 16.Ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ameeleza kuwa idadi ya wapiga kura jumla yao ni 71,765.
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji  Mstaafu Damian Lubuva akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kwenye mkutano uliohusu kupeana taarifa ya maandalizi ya mwisho ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika Machi 16,mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya Siasa,vyombo vya usalama na wadau wengine,mkutano huo umefanyika leo asubuhi kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo zilizomo ndani ya Ofisi za Halmashauri Wilaya ya Iringa.
   Mkurugenzi wa Oparesheni wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi wa Kalenga,Benson Kigaila wakisalimiana kwa furaha na Mmratibu wa kampeni CCM Kalenga Miraji Mtaturu.
  Mkurugenzi wa Oparesheni wa chama cha demokrasia na maendeleo katika uchaguzi wa Kalenga Benson Kigaila aliyesimama kwa nyuma akizungumza na mratibu wa kampeni ccm Kalenga Miraj Mtaturu  kulia kwake ni mratibu wa uchaguzi wa ccm Taifa Edwin Millinga.
   Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akijadiliana jambo na Afisa msajili msaidizi wa vyama vya siasa Sisty Nyahoza.
   Wanahabari wakijadiliana jambo.
  Baadhi ya Wanahabari wakiwa katika kikao cha Tume ya Uchaguzi n Vyama vya siasa na baadhi ya wadau wa usalama.

  0 0

   Wafanyakazi wanawake wa Airtel wakitoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi wenzao wakati wa tafrija fupi waliyoiandaa kwa dhumuni la kukusanya fedha ili kuwachangia wagonjwa wa kansa waliopo hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam. jana
   Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akichangia fedha kwa huduma ya Airtel Money kupitia simu wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa Airtel Tanzania kwa dhumuni la kuwachangia wanawake wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa waliopo hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam. 
  Mmoja kati ya wafanyakazi wa Airtel, Bw. Deodatus Hondo akichangia fedha wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa Airtel Tanzania kwa dhumuni la kuwachangia wanawake wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa waliopo hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.
  ========  =======  =======

   Wafanyakazi Airtel wachangisha fedha kwa ajili ya wanawake wanaougua kansa

  Umoja wa wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania unaofahamika kwa jina la Airtel Divas leo wameandaa halfa ya kuchangisha pesa kwa ajili yakina mama  wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa katika hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.

  Halfa hiyo ya kuchangisha pesa ilifanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Tanzania  na kushirikiksha wafanya kazi wa Airtel Tanzania kwa ujumla

  Akizungumza kwa niaba ya  Airtel Ofisa Mahusiano na matukio Dangio Kaniki alisema” Airtel Tanzania kupitia Umoja wa wanawake Airtel Divas” tumeamua kuchangisha pesa kwaajili ya kina mama wenzetu ambao ni wagonjwa mahospitalini,  ambapo leo tumeaandaa kifungua kinywa kwa wafanyakazi wote wa Airtel na kiasi cha pesa kitakachopatikana kitaenda kusaidia wanawake wanaougua ugonjwa wa kansa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Saalam.

  Tunatambua jamii inayotuzunguka ina changamoto nyingi ikiwemo maradhi, na ndio sababu umoja wa wanawake wa Airtel tumeamua kuchangisha pesa kwa dhumuni la kuwasaidia wagonjwa hususani wakina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa kansa. Tunaamini zoezi hili tunalolifanya leo litatuwezesha kufanikisha lengo letu.  Mpango huu wa kusaidia jamii zinazotuzunguka ni endelevu, na tumejipanga kutoa misaada ili  kuchangia katika kutatua vikwazo mbalimbali vya maisha na kujenga jamii iliyo bora. alisema Kaniki.

  Kwa upande wa wafanyakazi Bi Doris Kibassa ambaye ni mmoja ya wanachama wa Airtel Diva alisema “ najisikia furaha kuwa sehemu ya kusaidia jamii,  mbali na kampuni yetu kuwa na shughuli za kijamii bado sisi  kama mfanyakazi tunanafasi ya kushiriki na kutoa msaada  kwa jamii. Tunaamini mchango huu tunaoutoa leo utaweza kunusuru maisha ya baadhi ya watanzania na hivyo basi tunaziasa asasi nyingine kuiga mfano huu  na kushiriki katika kuokoa maisha ya watanzania walio wengi,”

  Airtel Tanzania imekuwa ikitoa michango kwa jamii kutupitia shughuli zake za huduma kwa jamii, Airtel kwa kushirikisha wafanyakazi wake pia inatoa huduma kwa jamii nchini.

  0 0

  MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.
   
  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa msanii huyo amepata kura nyingi kutoka kwa mashabiki waliompendekeza.

  “Tunashukuru kwamba baada ya mapendekezo ya mashabiki tuliwasiliana na Rebecca ambaye ameonesha uungwana wa hali ya juu na kutukubalia ombi letu.

  “Lakini pamoja na kukubali ana ratiba ya maonesho sehemu nyingine huko kwao, hivyo ametuambia hatatumbuiza katika mikoa yote ambayo tamasha litafanyika mwaka huu, hivyo tutaangalia wapi tumpangie kulingana na ratiba yake. 

  “Lakini niwahakikishie mashabiki wetu kwamba msanii huyo tutakuwa naye na sasa ni suala la Kamati ya Maandalizi kuona ratiba yake ilivyo na kisha nasi tumuweke kwenye ratiba yetu ili mashabiki wafurahi,” alisema Msama.


  Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).


  Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao tayari wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro, Rose Muhando na kwaya ya Kwetu Pazuri wote wa Tanzania.

  0 0

   Sehemu ya wakufunzi kutoka vyuo vya ufundi Mbeya, Mwanza na Mkunazini – Zanzibar wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kutumia njia rafiki ya kuhudumia majokofu na viyoyozi bila ya kuharibu tabaka la Ozoni.
  Kundi la washiriki kutoka mkoa wa Dar es Salaam wakielekezana jinsi ya kutumia vifaa rafiki ya kuhudumia Majokofu na Viyoyozi siku ya pili ya mafunzo jijini Dar es Salaam.Picha na  Rashda Swedi.

  0 0

  )


  0 0

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda akimweleza Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon, Mipango mbalimbali inayofanywa na Tanzania kuimarisha uhusiano na Korea Ikiwamo ufunguaji wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea, wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon akimweleza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda mpango wa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala yatakayochangia maendeleo kwa nchi na wananchi husika.
  Wajumbe wa Kamati za Mambo ya Nje za Tanzania na Korea wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda akimpa zawadi Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon wa Mwisho kulia ni Mkurugenzi Mkazi Ujirani Mwema, leo Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon akimpa zawadi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda , leo Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.  (Picha na Hassan Silayo)

  Na Jovina Bujulu, Maelezo Dodoma

  Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na mpango wa kuanzisha ubalozi Tanzania Nchini Korea.

  Hayo yamesemwa leo na Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelewa na Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Mjini Dodoma leo.

  Spika Makinda alisema kuwa serikali itaendelea kulisimamia suala hili ikiwa ni njia moja wapo ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.

  “Tuna kila nia ya kufungua ubalozi wa Tanzania nchini Korea na hii tunafanya tukiwa na nia ya kuendelea kuujenga uhusiano kati yetu” Alisema Spika Makinda.

  Aidha Spika Makinda alisema kuwa bunge la Tanzania limeweka mikakati mbalimbali ili kuliimarisha na kulifanya kuwa la kimataifa ikiwamo kuridhia uanzaji wa bunge la kimtandano (E-parliament).

  Akizungumzia kuhusu uanzishaji wa Radio ya Bunge Spika Makinda spika alisema kuwa bunge linampango wa kuwa na Radio ya bunge ili kupunguza gharama za kutumia radio za taifa kama wanavyofanya sasa.

  Pia Spika Makinda alimtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon kushirikiana katika kuanzisha chama cha ushirikiano cha wabunge wa Korea na Tanzania.

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano ambaye ni mbunge wa bunge la Korea Bw. Ahn Hong Joon, alimuahidi Spika Makinda kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwamo mpango wa Tanzania kuwa na Bunge la kimtandao.


  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa alishukuru Serikali ya Korea hasa kutokana na Misaada mbalimbali wanayopata kutoka Serikali ya Korea ikiwamo ujenzi wa chuo cha Afya  na Ujenzi wa Daraja la Malagarasi.

  0 0

   Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uwekezaji Mhandisi Decklan  Mhaiki (katikati) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo  (kushoto) pamoja na Waandishi wa habari moja ya mashine za kufua Umeme zitakazofungwa katika  eneo la Kinyerezi I jijini, Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Mradi wa ujenzi huo, Bw. Shaun Moore.

   Mmoja wa mitambo ya kufua umeme ambao utafungwa katika eneo la Kinyerezi I mara baada ya ujenzi kukamilika. Mitambo hiyo, inatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati za umeme 150 ambazo zitaunganishwa katika gridi ya Taifa.

   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji kutoka TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wa kampuni inayojenga kituo hicho ya Jacobsen Elektro.  

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha Kinyerezi I, Bw. Shaun Moore, wakati akimweleza maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

  ========  ========   ======
  Megawati 150 kuongezeka katika Gridi ya Taifa


  Na Asteria Muhozya na Jema Marko, Dar es Salaam

  Megawati 150 zinatarajiwa kuongezeka katika gridi ya Taifa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mitambo ya kufua umeme eneo la Kinyerezi I pamoja na kukamilika kwa ufungaji wa mitambo hiyo, ambapo shughuli zima inatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Disemba mwaka 2014.


  Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo  hicho  alieleza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa  kituo hicho  ni  hatua  mojawapo ya kutimiza azma  ya Serikali ya kuongeza umeme katika gridi ya Taifa.


  Aidha, aliwataka watanzania na wateja wa umeme kujenga imani na Shirika la Umeme Tanzania kutokana na mabadiliko ambayo tayari yamefanyika katika shirika hilo ikiwemo utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kuhakikisha kunakuwa na umeme wa uhakika.


  “Nataka Watanzania muelewe kuwa, Tanesco ya sasa sio kama ya zamani. Umeme utapatikana. Kampuni ya Jacobsen Elektro ambao wanafanya kazi ya ujenzi ni wazoefu katika shughuli hizi, tuna imani kazi itakwenda vizuri kama tulivyopanga. Tanesco itatatua tatizo la umeme”. Alisema Waziri Muhongo.


  Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo   alieleza kuwa, asilimia 98 ya kampuni za kitanzania kupata   kandarasi katika ujenzi huo ni fursa mojawapo ambazo watanzania wanatakiwa kuzitumia katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia katika uchumi wa gesi.


  Akizungumzia kuhusu fedha za ujenzi wa kituo cha kinyerezi I na ujenzi wa vituo vingine vya kinyerezi II, III na IV, Waziri Sospter Muhongo alieleza kuwa,  fedha  za ujenzi wa kituo cha Kinyerezi I zimetolewa na Serikali kupitia TANESCO.  Ujenzi wa kituo cha kinyerezi II fedha itatokana  na ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Japani , wakati ujenzi wa kinyerezi III na IV fedha zitatokana na kuingia ubia kati ya Serikali  na kampuni ya Kichina.


  Wakati huo huo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uwekezaji, wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Decklan Mhaiki, aliongeza kuwa, katika kituo hicho zitafungwa jenereta nne ambapo kila moja itakuwa na uwezo wa kuzalisha kiasi cha megawati 37.5, hivyo kufanya jumla ya megawati 150 kutoka kituo hicho.


  Vilevile, alieleza kuwa, katika jitihada za kuhakikisha kwamba Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linatatua tatizo la Umeme nchini, tayari shirika hilo na mkandarasi anayejenga kituo hicho, kampuni ya Jacobsen Elektro wameanza mazungumzo ili kuongeza kiasi kingine cha megawati 200 ili kituo cha kinyerezi I kiweze kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 350.


  Akielezea kuhusu ubora wa jenereta zitakazofungwa kituoni hapo, Mhaiki alieleza kuwa, generator hizo ni za kisasa na hazina athari za kimazingira ikiwemo kelele.


  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Mradi huo kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro, Bw.  Shaun Moore, akielezea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, alieleza kuwa, ujenzi wa kituo hicho unaendelea vizuri kutokana na kampuni hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri na kampuni za kitanzania zilizochukua kandarasi tofauti tofauti za ujenzi wa kituo hicho, ambapo takriban asilimia 98 ya kandarasi  na wafanyakazi ni kutoka  kampuni za kitanzania.

  0 0

   A group photo with students, teachers and coordinators of Connecting Classrooms Programme at Kisutu Secondary School after her visits.
   HC Dianna Melrose follows one of the program of the Connecting Classrooms Programme at Kisutu Secondary School
   HC Dianna Melrose listens to a beneficiary student of Connecting Classrooms Programme at Kisutu Secondary School
   HC Dianna Melrose listens to a beneficiary students of Connecting Classrooms Programme at Kisutu Secondary School
   HC Dianna Melrose listens to Prof Eustella Bhalalusesa, Commissioner of Education from the Ministry of Education and Vocational Training during the visits at Kisutu Secondary School
  HC Dianna Melrose talks to students at Kisutu Secondary School.

  0 0

  Mkurugenzi wa Oparesheni wa chama cha demokrasia na maendeleo katika uchaguzi wa Kalenga Benson Kigaila aliyesimama kwa nyuma akizungumza na mratibu wa kampeni ccm Kalenga Miraj Mtaturu  kulia kwake ni mratibu wa uchaguzi wa ccm Taifa Edwin Millinga.
  ……………………………………………………….
  Na Bashir Nkoromo, Iringa
  WAWAKILISHI wa Chadema wakiongozwa na Mratibu wa Kampeni za chama hicho katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Benson Kigaiya leo wameumbuka baada ya kushindwa kuonyesha mbele ya jombo la Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) sheria ambayo wawakilishi hao wa Chadema waling’ang’ania kuwa ipo kuwaruhusu wafuasi wa vyama kukaa mita mia kusubiri matokeo au kulinda kura.

  Chadema walizidi kutahayari kia
  si cha mwanasheria wa chama hicho, John Malya, aliyeambatana wa wawakilishi hao, kwenye mkutano wa Tume na vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo utaofanyika Machi 16, mwaka huu, naye kukiri kwamba hakuna sheria ambayo awali ilikuwa imedaiwa na Kigaia kuwa ipo.
  “Madai haya ya kuwepo sheria inayoruhusu wafuasi au kundi la watu kukaa mita mia kutoka kituo cha kupigia kura kwa lengo lolote ikiwepo kusubiri matokeo au kulinda kura, yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na baadhi ya vyama vya siasa, lakini nasi tumekuwa tukiwaambia kwamba hakuna sheria hiyo, na kuwataka yeyote anayejua kifungu cha sheria hiyo atuonyeshe, Kigaia wewe unasema ipo hebu tuonyeshe kifungu hicho”,  alisema, Mjumbe wa Tume hiyo Jaji Mstaafu John Mkwawa.

  Mapema Kigaia alisisitiza kuwa kwa upande wa Chadema wanaona kuwa sheria ipo na kutokana na kuwepo sheria hiyo, kwa hiyo itakuwa ni haki ya msingi kwa wafuasi wa chama hicho kukaa mita 100, wakisubiri matokeo ya kura zao na pia kulinda ukiukwaji wowote unaoweza kufanyika kwa watu kutoa rushwa au kupiga kampeni za chini chini wakati wa uchaguzi.

  Maelezo hayo ya Kigaia yalipingwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, akisema, sheria iliyopo ni inayotaka kuanzia mita mia moja kutoka kituo cha kupigia kura pasiwepo nembo au ishara zozote za utambulisho wa chama chochote kinachoshiriki uchaguzi.

  Akitoa taarifa ya Tume hiyo kwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo ambavyo ni CCM, Chadema na CHAUSTA, Mwenyekiti wa Tume, pamoja na mambo mengine, alisema, mi marufuku kwa kundi au mtu yeyote kukaa kwenye kituo cha kupigua kura au karibu na kituo hicho baada ya kupiga kura.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu ( kushoto), akizungumza na Tajiri wa Nne Duniani, Bw Howard Buffet ( kulia), akiwa na Wasaidizi wake  ofisini Mpingo House, Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhe. Lazaro Nyalandu ( kulia),akitafakali neno na Tajiri wa Nne Duniani, Bw. Howard Buffet ( kushoto) alipotembelewa Ofisi kwake Mpingo House, Wizara ya Maliasili na Utalii. Wengine ni wasaidizi wake alioambatana nao.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (katikati) akielezea        jambo kwa Tajiri  wa Nne Duniani, Bw. Howard Buffet ( kulia) , akiwa na msaidizi wake , mara baada ya kutembelewa Ofisini kwake Mpingo House, Wizara ya Malisili na Utalii.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia), akiongozana na Tajiri wa Nne Duniani, Bw. Howard Buffet ( kushoto), mara baada ya mazungumzo waliyofanya Ofisini kwake Mpingo House, Wizara ya Maliasili na Utalii.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kutoa agizo kwa viongozi na watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanawaondoa na kuwachukulia hatua za kisheria wanaovunja sheria za jiji kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika maeneo yasiyoruhusiwa.
  Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna (CP) Suleiman Kova akitoa ufafanuzi ameeleza kwa waandishi wa habari kuhusu wakazi wa jiji la Dar es salaam hususan madereva wa bodaboda na Bajaji kufuata sheria za barabarani na kajenga tabia ya kufanya tathmini ya safari zao iwapo wanakidhi vigezo vya usalama barabarani ili kuepusha madhara.
  Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu sheria inayosimamia usafiri wa Bajaji na Bodaboda nchini. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.


  0 0

  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowasa na Anna Tibaijuka wakimpongeza Mwenyekiti Mpya wa Bunge maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta Mara baada ya Kutangazwa Kuwa Mshindi wa Nafasi hiyo kwa Idadi ya Kura 487 dhidi ya Hashim Rungwe aliyepata kura 69 na kura zilizoharibika  ni 7.

  PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na moja ya mjumbe wa bunge hilo wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.

   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na moja ya mjumbe wa bunge hilo wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.

   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na moja ya mjumbe wa bunge hilo wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.
   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na moja ya mjumbe wa bunge hilo wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.

  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na moja ya mjumbe wa bunge hilo wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.

   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wasira akiwa na Mjumbe mwenzie wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.

   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na moja ya mjumbe wa bunge hilo wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.

older | 1 | .... | 244 | 245 | (Page 246) | 247 | 248 | .... | 1897 | newer