Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

Taarifa kwa Umma:Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa


Kwetu Pazuri lapigiwa kura Tamasha la Pasaka

$
0
0

WAKATI zoezi la upigaji kura kwa waimbaji, mgeni rasmi na mikoa likiendelea, kundi la Ambassadors of Christ, ‘Kwetu Pazuri,’ limepigiwa kura na Watanzania  kwa ajili ya kushiriki kwenye Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Aprili 20.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Abihudi Mang’era, kundi hilo limeanza kupigiwa kura siku chache zilizopita wakati baadhi ya waimbaji wa Tanzania wakiongoza katika zoezi hilo. Akizungumza na Pata Habari, Mang’era alisema kundi hilo linaendelea kupigiwa kura kwa wingi za uwepo wao katika tamasha hilo licha ya kuwa baadhi ya waimbaji wanaongoza kwa kuwa na kura nyingi.

“Tumewapa nafasi Watanzania wafanikishe taratibu za kupatikana kwa mgeni rasmi, mkoa  na waimbaji lakini tumeona wameanza kuchagua na waimbaji wengine kutoka nje na kura zao nyingi zimeangukia kundi la Ambasadors.” Alisema.

Mang’era alisema baada ya kuona hilo na kutaka kuwafurahisha watanzania, wanafikiria kufanya mazungumzo ya kundi hilo ili  kufanikisha mapendekezo ya wapiga kura. “Tunafikiria kufanya mazungumzo nao hivi karibuni, bila shaka kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga kwa watanzania kupata kile wanachohitaji kwa maana ya Neno la Mungu kupitia kwa waimbaji watakaowachagua,” alisema Mang’era.

Aidha Mangera amewaomba na kuwakumbusha watanzania namna ya kuwapigia kura kwa waimbaji, mgeni rasmi na mikoa ambako ukitaka kumpigia mwimbaji andika neno pasaka acha nafasi kisha andika jina la mwimbaji unatuma kwenda namba 15327.

Pia kwa mgeni rasmi  andika neno pasaka acha nafasi kisha andika jina la mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda 15327, wakati mikoa unaandika pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura tuma kwenda namba 15327 piga kura uwezavyo ili upate mwimbaji na mgeni rasmi na mkoa unaopenda tamasha lifanyike.

Bank of Africa Tanzania and European Investment Bank partnership

$
0
0
 Mr. Pim van Ballekom, European Investment Bank Vice President for Africa and Mr. Ammish Owusu-Amoah, Managing Director of BANK OF AFRICA - TANZANIA at the signing of MOU between the two parties to unlock Euros 7 M in Tanzania.

==========   ========  ==============

New lending programme to benefit small businesses across Tanzania

 The European Investment Bank, Europe’s long-term lending institution, has agreed a new lending programme with Bank of Africa Tanzania that will support investment by small companies across the country. The European Investment Bank will provide EUR 7 million (over 15 billion Tanzanian shillings) that will be matched by Bank of Africa.

The new initiative was formally agreed in Dar es Salaam by Pim van Ballekom, European Investment Bank Vice President for Africa, and Ammish Owusu-Amoah, Managing Director of Bank of Africa Tanzania. The signature was witnessed by Ambassador Filiberto Ceriani, Head of the European Union Delegation to Tanzania.


“Investment by small and medium sized companies is essential to create new jobs and unlock business opportunities. We are pleased to have signed a new partnership today with Bank of Africa Tanzania. The European Investment Bank is committed to supporting private sector investment across Africa and today’s new initiative demonstrates our continued commitment to Tanzania.” said Pim van Ballekom, European Investment Bank Vice President. 

MKUU WA WILAYA YA KIBONDO VENANCE MWAMOTO AMTAKIA KILA LAKHERI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA,GODFREY MGIMWA

$
0
0
 Pichani Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo,Mkoani Kigoma Mh.Venance Mwamoto akisalimiana na kumtakia kila la kheri mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Godfrey William Mgimwa,katika mchaka mchaka wake wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga,Iringa Vijijini na hatimae kuibuka mshindi.

Uchaguzi wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 16 machi 2014,ambapo wananchi wa jimbo hilo wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo la upigaji kura na hatimae kumchagu kiongozi (Mbunge) wamtakae kwa maendeleo ya jimbo lao.Aidha Vyombo vya Usalama pia vimetoa rai kwa Wananchi kuwa watulivu kwa wakati wote wa kampeni na uchaguzi,ili kuhakikisha amani na utulivu vinatawala muda wote pasi na vurugu. 
"Kila lakheri Mdogo wangu"-Venance Mwamoto.

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA PHENOMENA L WOMEN GROUP

First Tanzania Diaspora HOMECOMING conference

First Tanzania Diaspora HOMECOMING conference

WAFANYA BIASHARA WA KARIAKOO KUJIACHIA COCO BEACH

$
0
0
Msemaji wa Hazina Capital, Rachel Ndauka (kulia) na William Joseph (kushoto) wakiongea na wanahabari (hawapo pichani).

Hazina Capital tunapenda kujitambulisha/kuwatangazia Watanzania juu ya soko jipya la biashara litakalojumuisha wafanyabiashara wa bidhaa za aina mbalimbali kutoka Kariakoo na kuwapa nafasi ya kuonyesha pamoja na kuuza bidhaa zao Coco Beach ambalo tumeliita ‘Kariakoo at Coco Beach’ linalotarajiwa kuanza kuanza Machi 29 na 30 mwaka huu na kila mwisho wa wiki ya mwisho wa mwezi.

Soko hili litatatoa nafasi pia kwa wananchi ambao huwa hawaendi Kariakoo au hata wanaoenda, kununua bidhaa zinazopatikana Kariakoo katika ufukwe huo wa bahari na kwa bei ileile na hata ya chini zaidi.
Pia watu wanaweza kuja na familia zao kwa sababu kutakuwa na vitu vingi kama michezo ya watoto na n.k.

Lengo la soko hili siyo kuwafanya watu wanunue tu, bali pia kuwasogezea karibu zaidi wananchi huduma ili waweze kupata mahitaji yao katika mazingira mazuri ya utulivu, ya furaha na usalama.

Pia lengo letu ni kuendeleza na kukuza wafanyabiashara pamoja na kupanua zaidi masoko yao lakini pia kuwawezesha kufikia malengo na mafanikio na kulitangaza soko letu maarufu la Kariakoo, Tanzania.

Hazina Capital inapenda kuwashukuru waandaaji wenza ambao ni Ndauka Promotion na Real Stars pamoja na Hazina Lounge kuturuhusu kutumia mahali hapa.

Tunapenda kuvishukuru vyombo vya habari kwa ushirikiano.

STAMICO yaipongeza SUMA JKT

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Uzalishaji Mali  la Jeshi la Kujenga Taifa,  SUMA JKT, limepongezwa kwa juhudi zake katika kuhakikisha ulinzi unaimarika katika maeneo ya mgodi wa STAMIGOLD uliopo Biharamulo Kagera.

Mgodi huo kwa sasa umekabidhiwa kwa serikali ambapo unaendeshwa chini ya shirika la madini la STAMICO.

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  wa STAMICO,  Rumisha Kimambo katika kikao kilichojumuisha Bodi yake na uongozi wa mgodi wa huo kilichofanyika mgodini hapo  hivi karibuni.

Mwenyekiti huyo ambae pia alipata fursa ya kutembelea eneo la westzone na mojamoja uliopo Mgodi huo alionesha kuridhishwa na mfumo wa mbinu shirikishi zinazotumiwa na mgodi huo katika kulinda mgodi bila ya kuharibu uhusiano kati ya mgodi huo na wananchi.

“Tumefurahishwa sana na kazi inayofanywa na SUMA JKT hapa STAMIGOLD kwani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana  kuondoa tatizo la wachimbaji haramu na wavamizi ndani ya  mgodi.” 

Alisema kuwa wachimbaji haramu wengi katika migodi ni tatizo na kunakuwa na njia mbadala katika kuwakabili kitu ambacho SUMA JKT imefanikiwa.

Shughuli za uchimbaji katika mgodi huo zinatarajiwa kuanza  mwezi April mwaka huu baada ya kukamilika kwa barabara ya urefu wa takribani Kilometa 3.9 kutoka eneo la ofisi za Mgodi kuelekea kwenye maeneo ya uchimbaji.

Mapema mwezi huu kampuni ya African Barrick Gold  iliyokuwa ikimiliki mgodi wa TULAWAKA ilifanikiwa kuhamisha  kibali  na baadhi ya leseni  za uchimbaji  katika eneo la westzone na mojamoja kwa shirika la madini STAMICO hivyo kuwezesha shirika hilo kuwa katika nafasi nzuri ya kuendeleza sekta ya madini hapa nchini.

PROIN PROMOTIONS LIMITED KUANZA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI NCHINI TAREHE 1 APRIL 2014

$
0
0
Meneja wa Mradi wa Kusaka Vipaji Vya Uigizaji Tanzania (Tanzania Movie Talents) Bw Joshua Moshi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakutambulisha kampeni mpya ya kusaka Vipaji vya uigizaji kutoka kampuni ya Proin Promotions Limited mapema leo katika Ofisi za Proin Promotions Limited, Mikocheni, Mtaa wa Ursino, Pembeni ni Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Bw Evance Stephen.

Muigizaji wa Filamu za Kitanzania Single Mtambalike almaarufu Richie Richie ambae pia ni mmoja wa majaji katika Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited akiongelea jinsi washindi watakavyopatikana katika shindano hilo linalotarajia kuanza tarehe 1 Aprili 2014
 Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Runinga Cha Channel Ten, Bw Fredy Mwanjala akiuliza swali kwa Meneja Mradi wa Tanzania Movie Talents, Bw Joshua Moshi (hayupo pichani) kuhusiana na Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji nchini.

 Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen (wa kwanza kushoto) akionyesha stika za TRA ambazo zinaonyesha Uhalali wa filamu za Proin Promotions lakini Pia Wateja watakaonunua Filamu kutoka Proin Promotions wanatakiwa kutuma namba zilizopo kwenye stika hizo za TRA kwaajili ya kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kutoka Proin Promotions kama Vile TV za Samsung na deki zake

MZUNGU TAPELI ANASWA NA MAHERA KIBAO FEKI HAPA BONGO

$
0
0
  Kamanda Suleiman Kova
 JAN ELOFF AKITOLEWA  NJE YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM
JAN ELOFF AKIHOJIWA NDANI YA CHUMBA MAALUM KILICHOPO NDANI YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY

Yule mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae amekamtwa akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki.

Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa South Africa aliyefahamika kwa jina la  JAN ELOFF ambae anaishi maeneo ya Msasani Jijini Dar. 

Taarifa zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi (jina kapuni) na DTV Bw. Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU, pamoja na Kutoa Euro Feki.

Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni raia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukamatwa mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana nao.Kufuatia kukamtwa kwa mzungu huyo wananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha kukamatwa mzungu huyo. 

Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi 'kupigwa' na mzungu huyo basi wafike haraka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo.
Habari na Kili Nyepesi

OPERATION KOKORO YAVUNA WANACHAMA 1800 WILAYA YA MWANGA.

$
0
0
Ziara ya Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro Komredi Japhar Mghamba akiongozana na Katibu Msaidizi wa Mkoa Maalum wa Vyuo Vikuu Komredi Daniel Zenda inaendelea kwa mafanikio makubwa katika wilaya hiyo ambapo mpaka sasa imefanikiwa kuingiza Vijana 1800 katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) pamoja na Chama.


Ziara hiyo iliyobeba jina la Operation Kokoro iliyoanza wiki iliyopita ilipata misikosuko hasa baada ya moja ya msafara wake kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Operation hiyo inayolenga kuhamasisha Vijana wa Upinzani na wasio na vyama kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhamasisha Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu pamoja na kukagua, kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya utekelezaji wa Ilani ya chama kwa kauli mbiu "CCM Mwanga Ukimya sasa Basi"



Operation kokoro tayari imeshapita katika kata ya Kisangara, na kuendelea katika milima ya upareni maeneo ya Ugweno, Msangeni, Kifula, Mamba na Kikweni. Viongozi hao wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wametembelea vikundi mbalimbali vya bodaboda, makundi ya wajasiriamali wadogo na wakubwa pamoja na kukagua miradi iliyoainishwa kwenye Ilani ya Chama ambayo inayoendelea kutekelezwa wilayani humo na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.



Viongozi hao wakiwa wanahutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Msangeni wamesema kuwa wananchi waendelee kuiamini CCM kwani ndio Chama Bora Cha siasa ambacho kinasikiliza kero za wananchi wake na kuzitafutia ufumbuzi na kutaja kero mbalimbali ambazo tayari zimepatiwa ufumbuzi wa kudumu wilayani humo.



Ziara hiyo inaendelea katika kata na maeneo mengine ya wilaya ya Mwanga.

 


Matukio Bunge Maalum la Katiba Dodoma leo.

$
0
0

Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (Kushoto) akimweleza jambo mjumbe mwenzie Bw. Saleh Pamba baada ya Bunge hilo kuahirishwa, leo Mjini Dodoma
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Mansoor Hiran akiongea na wanahabari baada ya Semina ya ya uundwaji wa kanuni zitakazoongoza bunge maalum la katiba kuahirishwa leo mjini Dodoma.
Baadhi wa wajumbe maalum wa katiba wakibadilishana Mawazo Nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Semina ya ya uundwaji wa kanuni zitakazoongoza bunge maalum la katiba kuahirishwa leo mjini Dodoma.

Wanafunzi watakiwa kuchukua hatua wanapokutana na aina yeyote ya udhalilishaji wa kijinsia.

$
0
0

Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka, Wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari leo Mjini Dodoma. Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Jovina Bujulu.
Baadhi ya Waandishi waliohudhuria katika Mkutano wa Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana katika ukumbi wa Idara ya Habari leo Mjini Dodoma.

(PICHA NA HASSAN SILAYO)

Na Jovina Bujulu, Maelezo Dodoma.

Wanafunzi nchini wametakiwa kuripoti katika sehemu husika ikiwamo kwenye madawati ya kijinsia iwapo watakumbana na aina yeyote ya udhalilishaji wa kijinsia.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana wakati wa Mkutano na waandishi wa habari leo Mjini Dodoma.

Dkt. Pindi alisema kuwa kumekuwepo na malalamiko kwa wanafunzi  hasa wa vyuo vikuu kukumbana na udhalilishaji wa kijinsia katika kipindi cha utoaji wa matokeo ya mitihani.

“Tumekuwa tukipata malalamiko sana kwa  wanafunzi wa hasa wa vyuo vikuu kukumbana na udhalilishaji wa kijinsia hasa katika kipindi cha matokeo ila wito wetu kwao ni kuripoti katika sehemu husika na Madawati ya kijinsia na sisi kama serikali tunaahidi kusaidiana nao kutokomeza tatizo hili”Alisema Dkt. Pindi.

Akizungumzia kuhusu Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka Dkt. Pindi alisema kuwa dhumuni kuu la siku hii ni kuiwezesha jamii kupima utekelezaji wa maazimia, Matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za kimataifa zinazohusu masuala ya wanawake ili kuhakikisha haki za wanawake zinalindwa.

Aidha, Dkt. Pindi aliongeza kuwa wananchi hawana budi kuongeza juhudi katika kufichua, kubaini na kuchukua hatua za kukomesha ukatili na kunyimwa haki kwa wanawake kwani wanaofanyiwa hivi ni dada zetu, watoto wetu, mama zetu na wengine ni bibi zetu.

Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika katika ngazi za mikoa kwa kila mkoa kuandaa utaratibu wa maadhimisho haya na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia”.

TASAF NA MKAKATI WA KUKABILIANA NA TATIZO LA LISHE DUNI NCHINI.

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF

 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF

 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF

 Baadhi ya washiriki wa mkutano uliondaliwa na TASAF kujadili namna bora ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini sana nchini wakimsikiliza mkurugenzi Mtendaji wa TASAF , Ladislaus Mwamanga ( hayupo pichani) wakati alipofungua mkutano huo kwenye ukumbi wa CEEM ,jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF

===========  ===========   ============
TASAF NA MKAKATI WA KUKABILIANA NA TATIZO LA LISHE DUNI NCHINI.



Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF kupitia Mpango wa kunusuru kaya masikini sana na zilizo katika mazingira hatarishi ,PSSN umekutana na wadau wa sekta mbalimbali za kiserikali kujadili namna ya kushirikiana katika kuhakikisha kuwa suala la lishe bora linapewa umuhimu mkubwa ili kupambana na tatizo la utapiamlo hususani kwa watoto nchini.


Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa sekta za afya na lishe kwenye ukumbi wa CEEMI jijini DSM,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga amesema jitihada zaidi zinapaswa kuelekezwa katika kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuboresha afya kwa kutumia lishe bora hususani kwa watoto ili kujenga makuzi sahihi ya ubongo wao.


Mwamanga amesema TASAF kwa upande wake imeweka mfumo imara wa kuwahusisha watalaamu wake ambao wamesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini kote na kutoa rai ya kuwahusisha katika kampeni mbalimbali za kuwaelimisha wananchi juu  ya matumizi sahihi ya vyakula kwenye maeneo husika.


Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesisitza kuwa pamoja na TASAF kuanza utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi ambapo suala la lishe ni moja ya vipengele muhimu, ni vema sekta nyingine pia zikashirikiana na taasisi yake katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata elimu sahihi juu ya namna bora ya kuboresha lishe hususani kwa watoto na akinamama wajawazito.


Mwamanga pia ametoa rai kwa wataalam kutumia mbinu mbalimbali za kuwasilisha ujumbe sahihi wa masuala ya lishe na kuzisambaza kwa walengwa jambo litakalosaidia kupambana na tatizo la kudumaa kwa makuzi na ubongo kwa watoto ambapo kwa sasa inakadiriwa kuwa asilimia 42 ya watoto nchini wamedumaa kimakuzi.


Mapema akizungumza katika mkutano huo ulioshirikisha wadau kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wizara ya mifugo na Uvuvi ,Wizara ya Kilimo,Taasisi ya Lishe na Chakula na wataalamu kutoka TASAF,Mkurugenzi wa uratibu wa Shughuli za Serikali katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Obeyi Assery amesema suala la kudumaa katika makuzi ya mtoto ni tatizo kubwa nchini ambalo linapaswa kutatuliwa kwa nguvu za wadau mbalimbali .



Naye mkurugenzi msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey amepongeza jitihada za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF kwa kubuni mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi ambapo suala la lishe litawekewa msukumu mkubwa kama moja ya vigezo vya kuzisaidia kaya zitakazoingizwa kwenye mpango huo mkubwa wa aina yake. 


WAKULIMA NCHINI KUSHIRIKI MKUTANO NA MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO APRIL MWAKA HUU

$
0
0
 Mratibu wa Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo kutoka Kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd, Dk.Ellen Otara-Okoedian akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusu mkutano na maeonesho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini hapa.Kulia ni Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni John Matiko
 Mratibu wa Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo kutoka Kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd, Dk.Ellen Otara-Okoedian akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusu mkutano na maeonesho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini hapa.Kulia ni Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni John Matiko
 Mratibu wa Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo kutoka Kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd, Dk.Ellen Otara-Okoedian akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusu mkutano na maeonesho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini hapa.Kulia ni Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni John Matiko
Mmoja wa wanahabari ambaye ni mpiga picha wa Televisheni ya Tumaini (katikati), akiuliza swali kwenye mkutano wa wanahabari na kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd iliyoandaa Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini hapa. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.


=========  ========  =======
Na Frank Mvungi-MAELEZO.


TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano na Maonesho  ya Kilimo (AGRITECH) 2014,  yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kuanzia April 10 mwaka huu na kuwashiriksha waoneshaji wan je na ndani ya nchi katika Nyanja mbalimbali za kilimo.


Hayo yamesemwa na Mratibu wa mkutano huo Dkt.Ellen Otaru- Okoediankatika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Iadara ya Habari-MAELEZO leo jijini Dara es salaam.


Dkt Ellen amesema mkutano huo unalenga uwezeshaji katika kilimo ambapo wakulima wa Tanzania watapata fursa ya kukutana na wadau wakubwa wa kilimo kutoka ndani na nje ya nchi ili kujadili na kuona namna bora ya kuinua sekta ya kilimo nchini.


Alisema mkutano huo  pia utawahusisha wadau wa kilimo wakiwemo wauzaji wa pembejeo,mbolea, na madawa ya mimea, matrekta, wanaohusika na umwagiliaji, vyuo vya kilimo, biashara,  za mazao, watafiti, Taasisi za biashara za ndani na nje ya nchi, wakulima na wafugaji, Wizara zote  husika na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali.

Aliongeza kuwa katika mkutano huo unaotarajiwa kuanza tarehe 10 hadi 12 aprili 2014 wakulima watapata fursa ya kuelewa umuhimu wa zana bora  za kilimo,utafiti , jinsi teknolojia ya simu za mkononi inavyoweza kubadili kilimo hapa nchini.


“Mkutano huu pia utajadili fursa mbalimbali zilizopo kwenye kilimo na mchango wa Taasisi za fedha katika kukuza kilimo hapa nchini na washiriki watapata fursa ya kujadili na kutoa mawazo yao juu ya namna bora ya kuongeza tija katika kilimo ili kupambana na janga la njaa  hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla” alisema Dk. Ellen.


Dkt. Ellen amesema mkutano huo utajumuisha washiriki toka mataifa takribani 20 yakiwemo Ujerumani, Marekani, Ufaransa, China, Japani, Kenya, Uganda na Malawi.

Naye Meneja Maonesho  na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, John Matiko alitoa wito kwa wakulima hapa nchini na wadau wote wa Sekta ya kilimo kujitokeza katika mkutano huo na pia kushiriki katika maonesho yatakayofanyika wakati wa mkutano huo.


Kwa mujibu wa Matiko, mkutano huo utakuwa na Kaulimbiu isemayo “Nguvu ya Teknolojia katika Mapinduzi ya Kilimo”.

TAASISI YA KANUMBA " KANUMBA THE GREAT FOUNDATION KUZINDULIWA APRIL 7 JIJINI DAR

$
0
0
Uzinduzi wa taasisi ya marehemu Steven Kanumba ijulikanayo  kwa jina la Kanumba The Great Foundation utafanyika Aprili 7 kwenye ukumbi maarufu wa Dar Live uliopo Mbagala, jijini. Uzinduzi huo utaenda sambamba na maadhimisho ya miaka miwili tokea kufariki kwa marehemuKanumba ambaye alifariki dunia Aprili 7.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa alisema kuwa wameamua  kuanzisha taasisi hiyo ili kuendelea kumuenzi mtoto wake na kuendeleza kile ambacho alikuwa akikifanya wakati wa uhai wake.

Alisema kuwa taasisi yao itajihusisha na utoaji wa elimu, kusaidia watoto yatima, kuibua vipaji vya waigizaji chipukizi na kuviendeleza na mambo mbali mbali ya jamii na tasnia ya filamu na muziki. “Kwa njia hii, jamii itaendelea kumkumbuka kila siku na si kusubiri maadhimisho ya siku yake aliyokufa tu, siku hii (Aprili 7 kila mwaka) itabaki kuwa ya kukumbukwa, lakini tutajihusisha na mambo mengine ya maendeleo na kusaidia jamii,” alisema Mtegoa.

Alisema kuwa wameamua kuipa jukumu kampuni ya Vannedrick  Tanzania Limited kufanya shughuli za uzinduzi wa taasisi hiyo kutokana na uadilifu wao na kuvunia na jinsi inavyojihusisha na mambo mbali mbali katika jamii.

Mkurugenzi kuu wa Vannedrick Tanzania Limited Frederick Mwakalebela alisema kuwa siku hiyo mbali ya kuwa na Red Carpet, pia kutakuwa na burudani mbali mbali za muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya na vichekesho kutoka kwa wasanii maarufu hapa nchini.

Alisema kuwa kutakuwa na maonyesho ya filamu mbali mbali za marehemu Kanumba ikiwa pamoja na script alizokuwa akiandika yeye mwenyewe, nyimbo alizotunga na vingienvyo. “Pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Movie ambao wameanza maandalizi kwa ajili ya siku hiyo maalum kwa waigizaji na mashabiki wa filamu nchini, tunawamba wadhamini wajitokeze ili kufanikisha siku hiyo,” alisema.

Serikali, UNDP, PATH wakubaliana njia bora ya kukabiliana na TB, Malaria na magonjwa kwenye nchi za joto

$
0
0
DSC_0773
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Neema Rusibayila, akifungua rasmi warsha ya mradi wa upatikanaji na utekelezaji wa pamoja kati ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) na Shirika la Kimataifa lisilokuwa la Kiserikali (NGO) PATH kwenye sekta ya Afya katika utumiaji na uanzishwaji wa Teknolojia mpya katika kupamba na magonjwa ya TB, Malaria na magonjwa yaliyoachwa katika nchi za joto. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkazi, Oparesheni wa UNDP, Bw. Titus Osundina.
DSC_0730
Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo ya siku moja ambayo ilikuwa inazungumzia mradi wa pamoja wa upatikanaji na utekelezaji kati ya UNDP na PATH jinsi ya uanzishwaji wa Teknolojia mpya katika kupamba na magonjwa ambayo yanapatikana katika nchi za joto.
DSC_0789
DSC_0732
DSC_0804
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Neema Rusibayila akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Bw. Titus Osundina wakati wa warsha ya Upatikanaji na Utekelezaji wa pamoja katika miradi ya utathimini na mipango inayowashirikisha UNDP na PATH.
DSC_0723
Picha juu na chini ni Kaimu Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Neema Rusibayila, akibadilishana mawazo na kusalimiana na baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
DSC_0708

NANI KUIBUKA MSHINDI WA SAFARI YA BRAZILI WIKI HII?

$
0
0
Tiketi ya kwanza ya kwenda Brazili na Serengeti kutolewa wiki hii:

Machi 4, 2014; Kampuni ya Bia ya Serengeti inatarajia kuchezesha droo ya nne ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti ambapo mshindi wa kwanza wa kwenda Brazili atapatikana. Licha ya zawadi kibao kutoka kampuni hiyo kama ving’amuzi, ipad, bia za bure, na fedha taslimu kufaidisha wateja wengi wa bia ya Serengeti kwa wiki tatu za mwanzo na zinazoendelea, wiki hii kutakua na zawadi kubwa zaidi ya promosheni hiyo ya safari ya kwenda Brazili ambapo mshindi atalipiwa gharama zote kwenda kutembea nchini humo.


Wakiongea kwa nyakati tofauti washindi wa wiki ya tatu ya promosheni hiyo wameonesha furaha zao kwa kupata zawadi hizo huku wakiishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwajali wateja wake huku wengi wao wakiwa na shauku ya kupata zawadi kubwa zaidi ya promosheni hiyo ya kwenda nchini Brazil ambayo droo yake itachezeshwa wiki hii huku gharama zote zikilipwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.


Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika mapema wiki hii mmoja wa washindi wa Samsung tablet Vedastus Kalinga kutoka Mbeya alisema amefarijika sana kupata zawadi ya simu hiyo ya mkononi kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti kwani itamsaidia kufanya vitu vyake kwa urahisi zaidi katika ulimwengu huu wa dijitali ingawa ndoto yake ni kupata safari ya kwenda Brazili.


Naye Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo alisema mpaka sasa washindi watano wameshakabidhiwa simu aina ya ‘Samsung Galaxy tab 3’ na kumi na nne wameshapata ving’amuzi kupitia promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti. Promosheni hiyo  zaidi ya zawadi za washindi wa droo za kila wiki pia kuna washindi wa bia za bure za papo hapo na fedha taslimu ambapo zaidi  ya wateja 716 wameshajipatia fedha taslimu Tsh 5000 na washindi 400 wameweza kujipatia Tsh 10,000 .


“Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kuwa wiki hii kutakuwa na droo kubwa yakupata mshindi wa kwanza wa safari ya Brazili ambaye atalipiwa gharama zote na Kampuni ya Bia ya Serengeti. Zawadi hii kubwa ni kwaajili ya wateja wetu chakufanya ni kufungua bia yako ya Serengeti kokote nchini na fuatilia maelezo ya promosheni na uweza kuwa mshindi wetu wa wiki inayokuja. Pia unaweza kufuatilia kupitia ukurasa wetu wa facebook www.facebook.com/serengetipremiumlager. Hivyo hatuna budi kuwashukuru wateja wetu kwa ushirikiano wanaotupa”, aliongeza Rugambo.


Kunywa kwa tahadhari. Inauzwa kwa wenye miaka 18+.

SHULE BINAFSI NA MCHANGO WAKE WA PEKEE KATIKA SEKTA YA ELIMU HAPA NCHINI

$
0
0

 SHULE binasi zina mchango wa pekee katika sekta ya elimu hapanchini,  kwa kutambua wingi wa watoto na ufinyu wa nafasi za shule za serikali


zilizopo.

Hiyo imefanya serikali kuchagua wale wenye uelewa wa juu pekee
kujiunga na shuleza elimu ya juu, huku wale ambao pengine kwa bahati  mbaya wamekwama kufikia alama zilizowekwa na serikali, wakiokolewa na


shule binafsi.

Hii imesaidia idadi kubwa ya watoto nchini kupata elimu ya sekondari
tofauti na miaka ya nyuma ambapo watoto wengi waliokuwa wakifeli na
kukosa shule basi huishia nyumba.

Shule za Filbert Bayi, nazo ni miongoni mwa shule binafsi zilizokuwa
na mchango wa pekee, hususani katika elimu ya sekondari.

Miaka  tangu kuanzishwa kwa shule ya Sekondari Filbert Bayi, na miaka
sita ya mahafali ya kidato cha nne, imeweza kuonyesha maajabu ya aina
yake kwa kufuta kabisa daraja sifuri.

Shule ilianza ikiwa na wanafunzi 28 na hadi sasa wamefikia 380, na
Mkurugenzi wa shule hizo Anna Bayi anasema wamefikia idadi hiyo kwa
sababu  ya kuchagua watoto wanaokidhi viwangovilivyowekwa na shule.

"Tungekuwa tunachukua watoto wa kila aina, basi nadhani idadi ingekuwa
kubwa zaid, lakini kwanza hatupokei watoto we na wenye utovu wa
nidhamu na wenye uelewa  wa hali ya chini.

Anasema ingawa wanachangamoto  ya kuachiwa watoto wasio na uelewa
sana, kwa kuzingatia wote wanaofanya vizuri kuchukuliwa shule za
serikali, lakini bado wameweza kutoa watoto bora kielimu.

Hata  hivyo, nao huwachuja na kupata wenye uelewa wastani, na tangu
wameanza kufanyamitihani yakidatocha nne hawajawahi kupata daraja
sifuri.

"Tulianza kwa kupata dara la nne, ambapo walikuwa wachache sana,na
tulishuka hadi akabaki mmoja, na mwaka jana hatukupata daraja la nne,
na badala yake daraja moja na mbili ndio walikuwa wengi huku daraja la
tatu wakiwa wachachekabisa,"anabainisha.

Kutokana na matokeo hayo, shule ya sekondari Filbert Bayi iliyoko
Kibaha mkoani Pwani, imefanikiwa kushika nafasi ya sita kimkoa, kati
ya shule 105,na nafasi ya 71 kitaifa kati ya shule zaidi ya 3000 na
nafasi ya nne kiwilaya.

Pamoja na mafanikio hayo, lakini shule hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kubwa ya kunyoosha maadili ya watotona hatimaye
kuwa wamoja.

"Kila mmoja anatoka kwenye mazingira na makuzi ya aina yake, na
anapofika hapa tunataka awe na tabia zenye kupendeza machoni mwa watu,
na kama unavyojua watoto wengi wa sekondari wanafika wakiwa na umri wa
kufanya matendo ya kipumbavu, basi tunahangaika nao hadi  wanakaa
sawa,"anaongeza.

Anasema ingawa yeye ni mkurugenzi lakini kuna wakati anasimama kama
mama, akielewa fika wazazi wengi siku hizi malezi yao hayasimama sawa
kimaadili.

Anna anasema wazazi wengi hawakai na watoto wao na wengi hawajui pia
tabia za watoto hao, kitu ambacho si sawa hasa nyakati hizi za sayansi
na teknolojia.

"Unaweza ukamuita mzazi aje kusikiliza matatizo ya mwanaye anayevaa
nguo fupi ama mlegezo, na anapokuja anakuwa kavaa kama mwanaye, kiasi
hata maneno ya kumkanya mtoto unakosa,"anabainisha.

Ili kuwafanya wanafunzi wabobee katika masomo na si kitu kingine,
anasema wameweka mitihani ya majaribio mara mbili kwa wiki, na hivyo
siku za mapumziko huzitumia kuajindaa na mitihani.

Anaongeza kuwa mazingira ya shule yamewekwa kirafiki na wanafunzi, na
ni lazima mtoto akutwe nakitabu cha kujisomea wakati wote awapo eneo
la shule.

Licha ya kusimama kitaaluma, pia shule hizo huongoza katika sekta ya
michezo pamoja na stadi nyingine za maisha.

Anasema huwapa watoto kazi za mikono kwa ajili ya ujasiriamali, ambapo
kuna wanaofuga kuku wa mayai na nyama, walima bustani za mbogamboga,  wanaofundishwa upambaji pamoja na mapishi.



Mkurugenzi huyo anasema kunapokuwa na shughuli yoyote shuleni
inayohitaji kupamba maeneo, basi wanafunzi ndio hufanya kazi hiyo,
kwa matokeo ya ufanisi mkubwa.


"Tunamjenga mtoto kuwa mbunifu katika maisha na anapotoka hapa,
anakuwa na shughuli za kufanya huko nyumbani, ni elimu ambayo hata
wenyewe wanaifurahia sana nainawajenga kiakili pia,"anaongeza.

Anaongeza kuwa suala la kufuta daraja sifuri si dogo hasa kwa shule
ambayo inachukua watoto wenye uelewa wa chini.

Hivyo, ili kuzidi kuwapa moyo walimu, hutoamotisha ya  sh. milioni
mojakwa kila mwalimu wa somo lililofanya vizuri.

"Nina walimu 10 wanaofundisha kidato cha nne, ambao wote kwa mwaka huu
wanastahili sh.milioni moja moja, na nimewaandaliwa hafla maalum ya
kuwakabidhi vitita vyao, hii italeta faraja na motisha kwao ili wazidi
kufundisha kwa juhudi,"anafafanua.

Anasema kifuta jasho hicho huwa hakitoki katika mitihani ya taifa tu,
bali hata mitihani ya mwisho wa mwaka kwa walimu ambao masomo yao
yatafanya vizuri.

Pia anasema ili mtoto aweze kufanya vizuri anastahili kuwa msafi yeye
pamoja na eneo linalomzunguka, hivyo wameandaa vikombe ya usafi
ambavyo hushindaniwa kila mwezi.

"Tunashindanisha usafi wa kuanzia vyumbani, madarasani ndani na
kuzunguka nje na mavazi kwa ujumla, na bweni litakalopata kikombe,
linaandaliwa hafla ndogo yenye vitafunwa vya sambusa na soda,"anasema.

Kuna watoto ambao kwa ujumla hawapendi kuandika, na wanapogundulika,
Anna anasema hupewa adhabu ya kali za kuwajenga, zikihusisha kuandika
notisi nyingi zaidi kuliko alizokwepa.

"Katika somo la hesabu nakoni shida, hivyo tunawapa watoto wakariri
tebo ya kuzidisha na tunaandaa mashindano kabisa, kwa wale wasiofanya
vizuri kwa kweli tunakuwa wakali sana,"anasema.

Hata wanapokuwa likizo majumbani, pia hupewa kazi za shule za kwenda
kufanya na pindi mtoto anaporudi shuleni bila kukamilisha hurudishwa
na mzazi.

Kwenye changamoto za kiuendeshaji anasema kwa kiasi kikubwa zinatokana
na serikali, ambayo imekuwa ikiwarundikia kodi na michango ya kila
aina hata kusababisha shule nyingine kufungwa.

"Serikali  haituoni sisi kama wasaidizi katika kuinua sekta ya elimu
hapa nchini balitunaonekana tofauti, tunabambikiwa ada nyingi kweli,
wanataka hicho kidogo tunachopata tugawane nusu kwa nusu.

"Mfano mdogo ni hapa kwangu, ada sh. milioni mbili tu, lakini hiyo
hiyo mtoto ale vizuri na apate huduma zote muhimu, huku kodi ya
ukaguzi wa elimu, sh. 2000 kila mtoto ikinisubiri, bado Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Zimamoto, Usalama kazini, mitihani na majengo,
wakati huo huo ukichunguza kodi zote zinafanana matumizi
yake,"anaongeza.

Anasema kwa wao waliochukua mikopo ya kujenga shulekuna muda
wanakwama, na pia serikali imekuwa ikiongeza gharama kila wakati bila
kujali na wala kushirikishwa wakati mwingine.

Anaongeza kuwa kama wangeshirikishwa katika masuala mengi basi elimu
ya Tanzania ingefika mbali mno.

Na hilo pia linagusa hata katika ratiba zamitihani ambayo serikali
imetoa amri na shulebinafsi kufanya, na wakati mwingine husababisha
ratiba kuingiliana na za shule husika, na yoteni kutokana na
ushirikishwaji haba.

Anna anabainisha kuwa wanashindwa kuchangia elimu elimu ya serikali,
kama vile kusaidia vitabu katika shule za kata, madawati na msaada
mwingine kwa sababu wanabanwa na kodi.

Anasema kodi hizo wakati mwingine zinasababisha mmiliki wa shule
asitengeneze watoto wanaotakiwa kuwa katika ulimwengu wa maendeleo.

Akirudi kwa upande wa mikakati ya shule, anasema kuanzia mwaka jana
wameanza kuchukua watoto wa kikepekee, ili baadaye shule hiyo iwe kwa
ajili ya wasichana tu.

Anasema hata ukifika sasa shuleni, utaona wavulana ni wachache, na
lengo ni kuwainua wanawake hapo baadaye waje kuongoza sekta
mbalimbali.

"Kusimamia watoto wa kike ni rahisi zaidi kuliko wanaume, hivyo
tunataka kutumia muda mzuri kuwaandaa na baadaye tuje kujivunia kutoa
viongozi na hata Rais,"anasema.

Shule za msingi za Filbert Bayi nazo zimekuwa zikifanya vizuri, na
anasema hadi sasa zina wanafunzi 860 kampasi zote.

Anna anasema amendeleo ya shule hizo ni mazuri na ufaulu wao kwa
darasa la saba ni wa asilimia  100.

"Hata darasa la nne nao wamefaulu vizuri tu na pia kuna motisha kwa
walimu wa shule za msingi wanaofanya vizuri, hatutoi motisha kwa shule
za sekondari tu,"anaongeza.

Kwa sasa wanajenga uwanja mkubwa wa michezo, ambao utakuwa na daraja
la kimataifa, na ni matumaini yake kwamba michezo mingi itakayofanyika
mkoani wa Pwani, itatumia uwanja huo.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images