Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

KAMPENI UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA,CCM YAZIDI KUIVURUGA CHADEMA,YAMNG`OA MWENYEKITI WAKE.

$
0
0

 Wananchi wa Kijiji cha Kikombwe wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa CCM,jimbo la Kalenga ,wakimsikiliza mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akijinadi na kuwaomba kura kwa ridhaa yao awaongoze kama Mbunge
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Lupembelwasenga, Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Kibiki akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini Delfina Mtavilalo, baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo hilo, leo katika kata ya Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema. 
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akijinadi na kuwaomba kura kwa ridhaa ya kuwaongoza kama Mbunge,Wanakijiji  wa Lupembe lwasenga,katika kata ya Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema leo jioni.

 Mkutano ukiendelea wa kumnadi mgombea Ubunge kupitia tiketi ya chama cha CCM,katika kijiji cha kijiji cha Kikombwe leo
 Aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA,ambaye kwa sasa ni Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akimnadi Godfrey Mgimwa, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, uliofanyika katika kijiji cha Kikombwe leo.
 Baadhi ya Wanakijiji wakifuatilia mkutano (CCM) wa kampeni wa chaguzi ndogo wa jimbo la Kalenga,katika kijiji cha Lupembe lwasenga,katika kata ya Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema leo jioni
 Baadhi ya Wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa kampeni wa chaguzi ndogo wa jimbo la Kalenga,katika kijiji cha Lupembe lwasenga,katika kata ya Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema leo jioni
 Akina mama wa kata ya Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema wakifuatilia mambo yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,kwa ajili ya kumnadi mgombea wao.
 Godfrey Mgimwa akinadiwa na kuombewa kura kwa wanakijiji cha kata ya Lwamgungwe,Iringa Vijini mapema leo
 Wakiwasili kijiji cha Kikombwe leo kwa ajili ya kampeni 
 Pichani wa pilia shoto ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga,Godfrey Mgimwa akiwasili katika kijiji cha Kikombwe leo,kwa ajili ya mkutano wa kampeni.
Amekwenda kusikiliza yanayosemwa kwenye mkutano wa kampeni.
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Salum Mtenga akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi ya CCM ya mkoa huo, kuhusu mambo yanavyoendelea katika kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga.

MAMA AISHA BILAL MGENI RASMI WOMENS CELEBRATION

$
0
0
MKE WA MAKAMU WA RAIS MAMA AISHA BILAL ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA SHUGHULI YA #WOMENSCELEBRATION ITAKAYOFANYIKA MARCH 8 KATIKA UKUMBI WA DIAMOND VIP HALL SAMBAMBA NAE ANAONGOZANA NA KIKUNDI CHA WAKE WA VIONGOZI CHA MILLENIUM WOMEN GROUP
WOMENS CELEBRATION INAYOANDALIWA NA KWA MARA YA TATU MWAKA HUU N BLOG YA 8020 FASHIONS ITAHUDHURIWA NA WANAWAKE KUTOKA KADA MBALIMBALI JIJINI.

NA MADA KUU YA MWAKA HUU NI KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE AMBAPO TUNAWEZA KAMPENI YA OXFAM NDIO WANATAKAOTUPA SOMO JUU YA KUPAMBANA NA UKATILI .

NA SPONSOR WA SHUGHULI HII NI TUNAWEZA KAMPENI,PSPF,SHEAR ILLUSIONS,MAZNAT BRIDAL CARE,PIXEL BASE,SIMPLY MADINI MICHUZI MEDIA GROUP NA AMERICAN NAILS.

TAZAMA PICHA TOFAUTI ZA MAMA AISHA BILAL AKIWA KATIKA HAFLA TOFAUTI mama aisha  bilali
#AFRICANPRINT NDIO KIVAZI CHA SIKU
Blog-Ad-High-Res mmg

Wajumbe Bodi ya Wakurugenzi NSSF Watembelea Ujenzi Mradi wa 'Dege ECO Village'

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF walipotembelea mradi wa Dege ECO Village wa Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu akifuatilia. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF walipotembelea mradi wa Dege ECO Village wa Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu akifuatilia.

======  ======  ======
WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) leo wametembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaojulikana kwa jina la Dege ECO Village unaojengwa eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 

Ujenzi huo wa mji wa kisasa ambao utakuwa na nyumba za kuishi za kisasa za watu wa kipato cha kati unajumuisha ujenzi wa nyumba zaidi ya 7,000 zikiwa na huduma zote za kujamii eneo moja. Akizungumzia mradi huo mkubwa unaotekelezwa kati ya NSSF kwa ushirikiano na kampuni ya Azimio, Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo aliwaeleza wajumbe wa Bodi ya shirika hilo kuwa ujenzi wa makazi hayo ya kisasa kwa wananchi wa kipato cha kati unaendelea vizuri.

 Alisema eneo hilo litakuwa na nyumba bora na za kisasa zikiwa na huduma zote za msingi kwa jamii kama maduka, shule, hospitali, masoko, viwanja vya michezi, kituo cha polisi, kituo cha zimamoto, eneo la ujenzi wa majengo ya ibada, majengo ya burudani pamoja na miundombinu ya kisasa ya maji safi na maji taka.

 Alisema ujenzi wa mradi huo wa kisasa utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchukua watu takribani elfu 30 ambao watapata makazi bora nay a kisasa katika eneo hilo la Kigamboni. Akifafanua zaidi Mhandisi Msemo alisema ujenzi wa nyumba hizo utakuwa na awamu tatu; ambapo awamu ya kwanza itakamilika mwaka 2016 ikiwa na nyumba 2,500, huku awamu ya pili ya ujenzi itakamilika 2017 ikiwa na nyumba bora na za kisasa 2,500.

 “…Awamu ya tatu tunatarajia ikamilike mwaka 2018 hii itakuwa na nyumba 2,460,” alisema Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi Msemo akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari juu ya mradi huo. Aidha akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa NSSF, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dk. Ramadhan Dau alisema nyumba zote zitakazojengwa katika mradi huo zitauzwa kwa watu wenye kipato cha kati watakaohitaji.

 Alisema zipo zitakazouzwa kwa fedha taslimu na nyingine kwa makubaliano ya mikopo kadri ya utaratibu utakavyotolewa na shirika hilo pamoja na mwekezaji walieshirikiana naye kutekeleza mradi huo, yaani kampuni ya Azimio.

 Alisema bei ya nyumba moja inakadiriwa kuuzwa kuanzia dola za Kimarekani elfu 80 hadi 130, na tayari wameanza kupokea fedha na maombi kwa watakaohitaji au kulipa kidogo kidogo kwa utaratibu utakao kubalika. Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa bodi walipongeza juhudi za uongozi wa NSSF kwa kubuni mradi huo wa kisasa ambao utawasaidia wengi na hivyo kushauri kuna haja ya kutekelezwa na mikoa mingine.

WANAKALENGA HAWATOPIGA KURA KWA KUTISHWA-KATIBU WA CCM MKOA IRINGA

Mkazi wa Bukoba ashinda milioni 50 za Airtel ‘Mimi ni Bingwa’

$
0
0
 Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde(kulia)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa droo ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ iliyochezeshwa Jumanne jioni katika ofisi za makao makuu ya Airtel. Bw. Rashid Jackob Kagombola, mkazi wa Bukoba  mkoani Kagera alitangazwa mshindi wa shilingi milioni 50. Kushoto ni Mkaguzi mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Bw. Bakari Maggid.
Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde (kulia) akimwonyesha Mkaguzi mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Bw. Bakari Maggid namba ya katika droo kubwa ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ iliyochezeshwa Jumanne jioni katika ofisi za makao makuu ya Airtel.  Bw. Rashid Jackob Kagombola, mkazi wa Bukoba mkoani  Kagera alitangazwa mshindi wa shilingi milioni 50.

=========  =======  =========
Mkazi wa Bukoba ashinda milioni 50 za Airtel ‘Mimi ni Bingwa’

KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kupitia promosheni yake ya ‘Mimi ni Bingwa’ imemfanya Bw. Rashid Jacob Kagombola, mkazi wa Bukoba mkoani Kagera kuwa tajiri baada ya kujishindia milioni 50 katika droo kubwa ya bahati nasibu iliyochezeshwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Akimtangaza mshindi Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “Leo hii tumefikia mwisho wa promosheni yetu ya ‘Mimi ni Bingwa’ ambayo imewanufaisha watanzania walio wengi. Limekuwa ni zoezi lenye mafanikio makubwa likiwa na idadi kubwa ya wateja wakijiunga katika promosheni na kujishindia zawadi katika vipengere tofauti. 

“Ningependa kuwashukuru wateja wetu kwa kushiriki katika promosheni hii tangu ilipoanza mwishoni mwa mwezi November mwaka jana. Airtel bado mipango mingine mingi inakuja, tukilenga kuendelea kurudisha kile tulichonacho kwa wateja wetu na kuisaidia jamii inayotuzunguka kukuza viwango vyao vya kuishi,” alisema Mmbando. 

Alisisitiza kuwa mbali na zawadi kubwa ya milioni 50 kutolewa, washindi wa awamu ya pili na ya tatu wa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya moja kwa moja ‘live’ ya klabu ya Manchester United wataondoka nchini mwezi huu pale klabu hiyo ikitarajia kucheza tena katika uwanja wa Old Trafford.  
Kwa upande wake, milionea mpya akizungumza kupitia simu kutoka Bukoba aliipongeza Airtel Tanzania kwa kuanzisha promosheni zinazosaidia kuyabadilisha maisha ya wateja wake na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na nchi nzima kwa ujumla.

“Hii ni miujiza inayotokea maishani mwangu. Siwezi kuamini nami nimeingia katika orodha ya mamilionea Tanzania. Ni kama ndoto kwangu imekuwa kweli sababu ya Airtel. Naishukuru Airtel Tanzania kwa msaada wao si tu kwa wateja wake bali pia kwa jamii yote inayoizunguka. Hizi milioni 50 hakika zitabadilisha maisha yangu kabisa na zawadi nitakayoipatia Airtel ni kubaki kuwa mteja wao mwaminifu wakati wote,” alisema Bw. Kagombola.

“Nimejiunga na promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ tangu ilipoanza mwezi November, na nilikuwa nikicheza pale tu nitakapokuwa na salio la kutosha. Ilikuwa ni changamoto kuweza kupata pesa ili kuongeza salio la muda wa maongezi, lakini siwezi kuamini leo hii mimi ni milionea! Shukrani ziende kwa promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ kwa kubadilisha maisha yangu,” aliongeza. 

Promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ imeanza mwezi Novemba mwaka jana, ikiwa ni matokea ya ushirikiano katika ya klabu ya Manchester United na kampuni hiyo ya simu, haikulenga kuwazawadia wateja pekee, bali pia kuwaunganisha washiriki na soka la kimataifa na kusaidia kukuza hari ya michezo miongoni mwa watanzania.                                                             
 Wakati wa promosheni hiyo, washiriki wawili wa Mimi ni Bingwa walizawadiwa shilingi milioni 2 kila siku, wawili wakijishindia shilingi milioni 5 katika droo za kila wiki na mmoja kujishindia tiketi mbili za safari iliyogharamiwa kila kitu kwenda Old Trafford.

AKWILOMBE KUTOKA MTWARA AFUNGUA TURBO ZAKE KALENGA MKOANI IRINGA

$
0
0
KATIBU WA CCM KUTOKA MTWARA,NDUGU SHAIBU AKWILOMBE AMBAYE PIA ALIWAHI KUWA NAIBU KATIBU MKUU WA CHADEMA,AKIZUNGUMZA KWENYE MKUTANO WA HADHARA WA KAMPENI YA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KALENGA,KATIKA KIJIJI CHA KIKOMBWE,IRINGA VIJIJINI

MANGULA AISIMANGA CHADEMA KALENGA, ASEMA CCM LAZIMA ISHINDE

$
0
0
................................................................................................
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amekifananisha chama cha CHADEMA sawa na wachuuzi wa biashara za mkononi (wamachinga) kwa kutokuwa na maeneo rasmi ya kuendesha shughuli zao.Mangula amesisitiza kuwa CCM imejipanga na ina uhakika wa kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini.Kiongozi huyo wa juu wa CCM aliyasema hayo jana katika kijiji cha Mugama kata ya Mugama wilayani humo wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya kata hiyo. 

  Mangula alitoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi huo katika kata ya Mugama ambapo Katibu wa CCM kata ya Mugama Sylvester Samon kueleza kuwa chama cha CHADEMA ambacho ni mshindani wa CCM katika uchaguzi huo hakina dalili kushinda. 

  Samson alisema CHADEMA haina ofisi hata moja katika kata nzima ya Mugama jambo linalokitia hofu chama hicho na kulazimika kutumia mbinu chafu ikiwemo kushusha bendera za CCM na kuchana mabango ya mgombea wake. Baada ya kuelezwa hayo, Mangula alisema CHADEMA kimekosa mwelekeo ndani ya kata hiyo na jimbo zima la Kalenga kwa kuwa kimekuwa sawa na wamachinga kwa kutokuwa na na ofisi ambazo ni dalili ya kukubalika na kuwa na wanachama kwenye eneo husika. 

  “CHADEMA hakina hata ofisi moja katika kata nzima, hivi unaweza kusema kina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwenye eneo hili au wanatakakuwalaghai na kuwarubuni wananchi,” alisema. Alisema CCM imejipanga kupata ushindi wa kishindo kutokana na mafanikio na utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo mambo mbalimbali ya maendeleo yamefanikiwa kutekelezwa. 

  Kwa mujibu wa Mangula, uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya mbunge wa CCM hivyo ni vyema wana-Kalenga wakamrudisha mwana-CCM ili akamilishe ahadi zilizotolewa na Chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Mugama, Betha Luhavi, alisema Chama kina taarifa kamili kuhusu wapiga kura wa eneo hilo hivyo hakuna mtu kutoka nje ya eneo hilo atakayepewa nafasi ya kujipenyeza ili kuvuruga uchaguzi huo. 

  Betha alisema hadi sasa tayari CCM imefanikiwa kuyazunguukia matawi yote yaliyo kwenye kata hiyo kwa lengo la kuhamasisha makada na wapenzi wake siku ya kupiga kura wajitokeze kupiga kura. Alisema viongozi na wapenzi wa CCM watakuwa mstari wa mbele kuhamasisha amani kipindi chote cha kamepeni na siku ya uchaguzi ili kuhakikisha ubnafanyika kwa amani. Aidha, alisema CCM itashirikiana na vyombo vya dola kufichua uhalifu wa aina yoyote unaolenga kuvuruga uchaguzi na amani katika kata hiyo na jimbo la Kalenga kwa jumla. 

  Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu ambapo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa kuwa mgombea wake atakaechuana na wagombea wengine. uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake Dk. William Mgimwa kufariki dunia Januari mwaka huu wakati akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.

Wajumbe wa Bodi Wavutiwa na Teknolojia ya Utengenezaji Kadi ya Mwanachama NSSF

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu (mwenye kofia nyeupe) akimkabidhi kadi ya uanachama wa NSSF, Ester Msalahi, ambaye ni mwalimu katika shule moja ya msingi ya binafsi. Kadi hilo iliandaliwa ndani ya saa moja kwa teknolojia mpya ya kisasa 'Mobile POS' ya utengenezaji kadi ya mwanachama wa shirika hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu (mwenye kofia nyeupe) akimkabidhi kadi ya uanachama wa NSSF, Ester Msalahi, ambaye ni mwalimu katika shule moja ya msingi ya binafsi. Kadi hilo iliandaliwa ndani ya saa moja kwa teknolojia mpya ya kisasa 'Mobile POS' ya utengenezaji kadi ya mwanachama wa shirika hilo.Wajumbe wa Bodi ya NSSF pamoja na viongozi wa shirika hilo wakipata maelezo juu ya Mobile POS inavyofanya kazi. 
Wajumbe wa Bodi ya NSSF pamoja na viongozi wa shirika hilo wakipata maelezo juu ya Mobile POS inavyofanya kazi.Mmoja wa wafanyakazi wa NSSF tawi la Ilala (katikati) aliyezungukwa akitoa maelezo namna Mobile POS inavyorahisisha kazi ya utengenezaji kadi ya mwanachama wa NSSF kwa muda mfupi. Mmoja wa wafanyakazi wa NSSF tawi la Ilala (katikati) aliyezungukwa akitoa maelezo namna Mobile POS inavyorahisisha kazi ya utengenezaji kadi ya mwanachama wa NSSF kwa muda mfupi.


TBL YAKABIDHI MAJENGO YA KIWANDA KWA CHUO KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA STEPHANO MOSHI

$
0
0
Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya kaskazini,Salvator Rweyemamu (kulia) akimkabidhi mkataba wa kukabidhiana majengo ya TBL yaliyopo Moshi, kwa Katibu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Dayosisi Kanda ya Kaskazini, Julius Mosi, katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Moshi, mkoani Kilimanjaro. Majengo hayo yatakayotumika kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stephano
SMMUCO) yalikuwa ya Kiwanda cha Bia cha Kibo kilichonunuliwa na TBL.
Katibu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi Kanda ya Kaskazini, Julius Mosi akikabidhi mkataba kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stephano (SMMUCO) Prof,Arnod Temu kwa ajili ya
kutmiwa na chuo hicho chini ya dayosisi hiyo iliyokabidhiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Moshi, mkoani Kilimanjaro.Awali majengo hayo yalikuwa ya Kiwanda cha
Bia cha Kibo kilichonunuliwa na TBL.
Baadhi ya majengo yaliyokabidhiwa
Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya kaskazini,Salvator Rweyemamu, AKIELEZEA SABABAU ZA TBL kukabidhi majengo hayo kwa chuo hicho.


Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stephano (SMMUCO) Prof,Arnod Temu akitoa shukurani kwa TBL
bAADHI YA WANANCHI WALIOHUDHURIA SHEREHE HIYO
Viongozi wa TBL, dAYOSISI NA cHUO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA
Ndani ya moja ya majengo hayo
Sehemu ya ndani ya moja ya majengo hayo
Viongozi wa TBL pamoja na viongozi wa chuo hicho wakitembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho kujionea hali ilivyo kwa sasa.PICHA NA MDAU DICKSON BUSAGAGA

Airtel yazindua huduma ya Breaking news kupitia simu

$
0
0
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Mwananchi, Francis Nanai akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakati wa uzinduzi wa huduma ya kuwapasha habari wananchi kwa njia ya simu (Breaking News) iliyofanyika katika ofisi za Mwananchi jijini Dar es Salaam


Dar es Salaam, Airtel imezindua huduma mpya ya utaoaji wa taarifa za hapo kwa papo .

Huduma hiyo inayojulikana kama Airtel Mwananchi Breaking news itahusisha utoaji wa habari kupitia wateja wa simu za mkononi wanaotumia mtandao wa Airtel kwa kushirikiana na Kampuni ya Mwananchi Communications inayochapisha magazeti ya Mwananchi.

 Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mwananchi Francis Nanai alisema pamoja na mambo mengine mpango huo unalenga kuwafikisha watanzania habari sahihi kwa wakati.

Alisema kwa kutambua maendeleo ya teknolojia matumizi ya simu za mkononi katika kutoa taarifa yanazidi kuongezeka na kuwa sehemu ya maisha ya kila siku.

<  Kadiri siku zinavyokwenda teknolojia inaonekana kukua na simu za mkononi kutumika kama njia mojawapo ya kuwasilisha taarifa kutokana na hilo Mwananchi kwa kushirikiana  na Airtel tumekuja na ushirikiano huu ambao utawawezesha wateja wetu kupata taarifa sahihi na kwa wakati > alisema Nanai.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso  alisema kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kubuni njia mbalimbali zinazorahisisha utoaji wa huduma za mawasiliano na taarifa kwa wateja wake.

Alisema kupitia huduma hiyo watanzania watapata fursa ya kupata habari zinazotokea hapo kwa papo kutoka katika kila kona ya dunia.
Airtel tuko mstari wa mbele kuanzisha huduma ambazo zinalenga kumrahisishia mawasiliano mteja  na kupitia huduma hii ni matumaini yangu watanzania watapata nafasi ya kupata habari mahali popote walipo >alisema Colaso

Alisema kwa kuanzia wateja wa Airtel watapata huduma hiyo bure kwa muda wa siku saba na baada ya hapo watatozwa Sh 120 kwa siku.
 Meneja Masoko wa MCL Bernad Mukasa alisema taarifa zitakazotolewa kwa wateja wa Airtel zitakuwa katika sehemu tatu hivyo mteja atakuwa na uamuzi wa kuchagua habari anazozitaka ambazo zitahusisha habari za kawaida,burudani na michezo.

<  Sasa hivi wateja watakuwa na uamuzi wa kuchagua taarifa wanazohitaji kama ni habari za kawaida,michezo au burudani kwa mujibu wa matakwa ya kila mmoja >alisema Mukasa

WAPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

$
0
0
 Naibu meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibu katika ukumbi wa Hallfare na kudhaminiwa na kampuni ya Vannedrick ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana asasi isiyo ya kiserikali ya TCDA.
 Fredrick Mwakalebela akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibu katika ukumbi wa Hallfare na kudhaminiwa na kampuni ya Vannedrick ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana asasi isiyo ya kiserikali ya TCDA.
 kulia ni mratibu wa mafunzo hayo Anzawe Chaula akiwa na baadhi ya washiriki waliohudhuria mafunzo hayo akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibu katika ukumbi wa Hallfare na kudhaminiwa na kampuni ya Vannedrick ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana asasi isiyo ya kiserikali ya TCDA.

=======  ======  ==============
WAPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

Na Denis Mlowe,Iringa

KAMPUNI ya Vannedrick ya jijini Dar es salaam kwa kushirikiana asasi isiyo ya kiserikali ya TCDA wametoa msaada wa kielimu kwa wajasiriamali zaidi ya 200 walioko mkoani Iringa kwa lengo la kuwainua kiuchumi na kuondokana na umasikini.

Mratibu wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibu katika ukumbi wa Hallfare, Anzawe Chaula alisema baada ya kubaini wajasiriamali mkoani Iringa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa elimu ya biashara ndogondogo na kusababisha wengi wao kushindwa kuendeleza biashara zao wanazozianzisha.

Alisema mafunzo hayo yatawasaidia wajasiriamali kutambua fursa zilizopo katika mkoa wa Iringa na kuwataka kuyafanyia kazi mafunzo hayo waliyopatiwa katika kujikomboa kiuchumi.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa mafunzo hayo Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa Iringa Gervas Ndaki akizungumzia kuhusu mafunzo hayo alisema kuwa ni muhimu kwa wajasiriamali kwani ni kati ya fursa za kielimu ambazo zinaweza kuwakwamua na kuondokana na umaskini wakizingatia kwa umakini.

Alisema wajasiriamali hao watanufaika na mafunzo hayo na uwezekano wa kupata mabadiliko makubwa kiuchumi upo kwa sehemu kubwa na hivyo hali ya utegemezi kwa baadhi ya wanawake itapungua.

Ndani alisema pamoja na mafanikio hayo kuna tatizo ambalo kama halitatatuliwa kwa wajasiriamali hao kupatiwa mafunzo kwa ujumla yatakuwa hayana manufaa na kuishia kuwa na kumbukumbu za kwenye daftari na kuwataka waifanyie kazi elimu hiyo waliyopata bure na kuwashukuru wafadhili hao.

“Ni kweli mafunzo haya yamewapa mwelekeo wa maisha wengi hatukuwa na chochote katika ujuzi, lakini mafunzo haya yanahitaji mali ghafi na mitaji lakini kutokana na mafunzo haya utajua ni sehemu gani ya kuanzia na kuweza kujinufaisha katika maisha yako na kuongeza uchumi wa nchi yako na wewe mwenyewe kwa ujumla na itakuwezesha  kuendesha miradi inayoibuliwa ”alisema Ndaki.

Ndaki aliwataka wajasiriamali hao kuwa wabunifu katika kuzitumia fursa za elimu na kusikitika kwa kiasi kubwa kwa wajasiriamali wa Iringa kushindwa kujitokeza kwa wingi kama ilivyokuwa malengo ya wafadhili wa mafunzo hayo kukadilia zaidi ya wajasiliamali 1000 kujitokeza.

Aidha alizitaka taasisi za kibenki kupunguza masharti ya mikopo kwa wajasiriamali na kuiomba serikali kutoa hamasa kwa asasi za kifedha za kiserikali na zisizokuwa za kiserikali kuangalia uwezekano wa kuwapa mikopo wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuongeza uzalishaji na kukuza pato la Taifa.

BENKI YA NMB YAFANYA MKUTANO ELEKEZI KWA WADAU WAKE JIJINI MWANZA

$
0
0
Baadhi ya wateja wakubwa wa benki ya NMB na wafanyabiashara jijini Mwanza wakimsikiliza meneja wa mahusiano wa biashara,Wogofya Mfalamagoha wakati wa mkutano elekezi kwa wateja wa benki hiyo uliofanyika katika Chuo cha Benki Kuu jijini Mwanza leo.

ONDOA KITAMBI NDANI YA SIKU KUMI NA NNE.

$
0
0


 ONDOA  KITAMBI  NDANI  YA  SIKU  KUMI  NA  NNE.

Neema  Herbalist  & Nutritional  Foods  Clinic  ni  wauzaji  wa   dawambalimbali  za  asili.  Tunayo  dawa  nzuri  ya  asili  inayo  ondoa kitambi  na kulifanya  tumbo  lako  kuwa  flat  kabisa  ndani  ya siku  kumi  na  nne.

Dawa  ni  ya  asili  kabisa " Pure  Herbal", haijachanganywa  na kemikali  yoyote  na  haina  side  effects  kwa  mtumiaji .

BEI  YAKE  NI  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU ( Tshs.50,000/=)

Tunapatikana jijini  Dar  Es  salaam, katika  eneo  la  CHANGANYIKENI karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.

Kwa  wasio weza  kufika  ofisini  kwetu tunawapelekea  dawa  mahali
walipo  ( DELIVERY )

Kwa  wateja  wa  mikoani, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  mabasi,
kwa  wateja  walipo  Zanzibar  tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  meli
na  kwa  wateja  waliopo  nje  ya  Tanzania, tunawatumia  dawa  kwa
njia  ya  DHL.

    Tunapatikana  kwa  SIMU : 0766538384.

           Kwa  maelezo  zaidi  tembelea


Pinda, Mengi, Askofu Gamanywa, Mzee wa Upako wachuana Tamasha la Pasaka

$
0
0

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mizengo Pinda amechomoza kwenye zoezi la upigaji kura kuchagua mgeni rasmi katika tamasha hilo linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa Tanzania.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era sambamba na Waziri Mkuu, wengine wanaofuatia katika zoezi hilo ni Mkurugenzi wa kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi  na Askofu Mkuu wa Taasisi ya WAPO Mission International, Sylvester Gamanywa,  mchungaji wa kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat Gwajima, Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ pia wanamfuatia Waziri Mkuu katika zoezi la upigaji kura linaloendelea.

Mang’era anaendelea kuwakumbusha watanzania namna ya kuwapigia kura waimbaji, mgeni rasmi na mikoa ambako ukitaka kumpigia mwimbaji andika pasaka acha nafsi kisha andika jina la mwimbaji unatuma kwenda namba 15327.

Pia kwa mgeni rasmi  andika neno pasaka acha nafasi kisha andika jina la mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda 15327, wakati mikoa unaandika pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura tuma kwenda namba 15327 piga kura uwezavyo ili upate mwimbaji na mgeni rasmi na mkoa unaopenda ili tamasha lifanyike.

Aidha Mang’era mbali ya viongozi hao wa dini na serikali, pia waimbaji Jescar BM  na Bahati Bukuku ni mojawapo ya waimbaji wanaoonekana kuelekea kupata nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo kwa kuwa na kura nyingi.

Mang’era alisema mikoa ambayo inaongoza kupigiwa kura nyingi ni pamoja na Mwanza, Mbeya, Kigoma na Dar es Salaam inapigiwa kura nyingi kwa ajili ya kufanyika kwa tamasha hilo.

Makamu Mwenyekiti huyo alisema kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo wanazingatia na kutekeleza yale ambayo yanayotakiwa na wadau ambao wanachagua wanachopenda.

TAMASHA LA PASAKA KUTIMIZA MIAKA 14 TANGU KUANZISHWA KWAKE NA MSAMA PROMOTIONS YA JIJINI DAR

$
0
0
TAMASHA la Pasaka mwaka huu limetimiza miaka 14 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam imekuwa ikijiongezea umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa kiroho kupitia matamasha hayo.

Umaarufu wa matamasha hayo pamoja na mambo mengine, unatokana na ukweli kuwa yamekuwa yakifanyika kwa ubunifu na umakini mkubwa huku kila mwaka yakiongezeka na kubadili waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi.

Imebainika kuwa tamasha hilo ni kivutio kwa watu mbalimbali kiasi cha kuwafanya kila linapoandaliwa Tamasha la Pasaka na Krismasi, Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam ambao umekuwa ukitumika kwa kazi hiyo, kufurika watu nao kutoka wakiwa na mioyo iliyotakasika kupitia nyimbo na waimbaji hao.

Hapana shaka kuwa ubunifu huu ndio ulichangia hata Serikali kupitia Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenela Mukangala, kumteua Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, kuwa Mjumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Matamasha haya yanapambanuliwa na wadau mbalimbali ambao wanayaelezea ubora wake lakini wengi wanasema, yanapata umaarufu na mvuto kwa kuwa washiriki hususan waandalizi na wasanii (waimbaji), wanajiandaa na kujua kinachohitajika kwa jamii, hivyo kukiwasilisha kadiri ya mahitaji ya jamii.

Waimbaji mbalimbali wakiwamo wa kutoka nje ya nchi, wamekuwa wakikonga nyoyo za wananchi kwa kushirikiana vizuri na wazawa.
Sababu ya Kamati za Maandalizi za Matamasha haya kuleta waimbaji kutoka nje ni pamoja na hasa, kuleta ladha tofauti kwa nia ya kupata mahubiri au Neno la Mungu kwa ladha tofauti kutoka kwa waimbaji hao.

Wapo waimbaji wengi wenye uwezo wa kimataifa kutoka nje, lakini hawa ambao wamekuwa wakishiriki katika matamsha haya, ni pamoja na Marehemu Angela Chibalonza (Kenya) ambaye naye aliwahi kutikisa katika Tamasha hili mwaka 2000 lilipoanza, kwa kuimba nyimbo zake. Baadhi ya nyimbo zake zilizotikisa na kukonga nyoyo ni “Yahwe Uhimidiwe” na “Uliniumba Nikuabudu.”

Wengine walioweka historia nchini ni pamoja na Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini. Mwimbaji huyo aliweza kuvunja rekodi ya waimbaji wote licha ya kuwa hafahamu lugha ya Kiswahili vilivyo, lakini aliweza kuimba nyimbo kadhaa za Kiswahili kama Mwambamwamba ili kwenda sawa na Watanzania aliokonga nyoyo zao kwa kuwapa Neno la Mungu kupitia muziki wa Injili.

Sipho Makhabane, Rebeka Malope nao kwa nyakati tofauti, waliweza kufanya vizuri ukiachilia mbali waimbaji wengine kama Ephraim Sekeleti kutoka Zambia; Ambassadors of Christ (Rwanda), Faraja Ntaboba na Solomoni Mukubwa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) 24 Elders (Uganda) na Anastazia Mukabwa (Kenya).

Lengo la Msama kuanzisha matamasha haya ni kukusanya mapato kupitia chagizo za viingilio ili kuwasaidia Watanzania wenye uhitaji maalum wakiwamo wajane, walemavu na kuwasomesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Kwa kiasi kikubwa, Kamati hii imeweza kufanikisha malengo hayo.
Katika matamasha hayo yanayofanyika kila mwaka, wamekuwa wakija waimbaji kutoka nchi tofauti ambapo kwa mwaka huu haijajulikana kwamba ni mwimbaji wepi watakaoshiriki kutoka nje kwa sababu kazi hiyo iko mikononi mwa wananchi ambao wanatakiwa kupiga simu kuchagua mikoa litakapofanyika tamasha hilo, mgeni rasmi na waimbaji.

Uchunguzi wa makala haya kupitia mazungumzo na wadau mbalimbali umebaini kuwa, kila mwaka linapofanyika Tamasha la Pasaka limekuwa likiongezeka ubora ikiwa ni pamoja na kuleta waimbaji wa kimataifa ambako ni wazi kamati hii siku za usoni ikaleta waimbaji wakubwa kutoka nchini za Ulaya  na baadaye Marekani.

Kila mwimbaji au kundi la waimbaji linakuwa na vionjo tofauti hivyo tunaamini siku moja kwa kazi nzuri inayofanywa na Msama Promotions, ina uwezo mkubwa wa kuwaleta waimbaji kutoka Marekani kama akina Yolanda Adams, Michael Smith, Martha Carson, Tasha Cobbs na wengine wengi.

Achilia mbali hao,  waimbaji wengine kutoka nchi mbalimbali za Afrika ni pamoja na Joyous Celebration, Benjamin Dube, Uche  Keke, Sarah K, Paul Kigame na Marion Shako.

“Kamati hii itaendelea kufanya makubwa, hivyo Watanzania na mashabiki wa tamasha hili watarajie kuona mapya tofauti na matamasha mengine yaliyowahi kufanyika ikiwa ni pamoja na kupata Neno la Mungu kupitia waimbaji wapya,” anasema Msama.

Bado ni kitendawili kisichiojulikana kuwa ni mwimbaji gani atakayetoka nje  safari hii  na kuvunja rekodi ya Solly Mahlangu aliyeimba katika Tamasha Dada la Krismasi lililofanyika Desemba mwaka jana.

Kauli mbiu ya Tamasha hilo ambayo ni ‘Uzalendo Kwanza, Haki huinua Taifa’ itakayochochea na kuimarisha maendeleo ya Tanzania ijayo.

SHIGONGO AFAFANUA MADHARA YA UGONJWA WA INI

$
0
0
Shigongo akizungumza kwa masikitiko jinsi watu wengi walivyo kwenye hatari ya kufa kwa ugonjwa wa ini.
…Akiwa na jopo la madaktari. Kushoto ni Dk. Mtebe Majigo, Mganga Mkuu wa Amana, Meshack Shing'wela (wa pili kulia) na Daktari Kiongozi Andrew Method.
Ndeonasio Towo kutoka Damu Salama akielezea umuhimu wa wananchi kupima damu kubaini maradhi mbalimbali bila kusahau virusi vya homa ya ini.
Mwakilishi kutoka SD Tanzania ambao ni wadau wa ugonjwa huo, Phillip Sawe, akielezea umuhimu wa kupima mapema ugonjwa huo kabla mwili haujashambuliwa.


Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Amana, Andrew Method (kulia) akisistiza jambo.
Mapaparazi kazini.
Shigongo akimueleza jambo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho (kushoto) na Mwakilishi kutoka Sanofa, Edwin Kisimbo, wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kikiendelea.
Dk. Majigo (wa pili kulia) akielezea ugonjwa huo unavyoambukiza kwa njia ambazo huambukiza Ukimwi.
Meshack Shing'wela akifafanua jambo.
…Akimshukuru Shigongo kwa kuanzisha kampeni za kutokomeza ugonjwa huo.
MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, na wadau mbalimbali wa afya leo walizungumzia madhara ya ugonjwa hatari wa homa ya ini kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana Jijini Dar.
Miongoni mwa wadau waliokuwa kwenye mkutano huyo ni madaktari mbalimbali, Sanofa ambao huhusika na vipimo vya ugonjwa huo, Damu Salama ambao huhusika na upimaji wa damu na SD Tanzania.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

MAPACHA WATATU WAZALIWA SALAMA HOSPITALI YA AICC ARUSHA

$
0
0
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Elishilia Kaaya akiwa amebeba watoto watatu mapacha Catherine, Caroline na Cathrine ambao walizaliwa mwanzoni mwa wiki hii katika Hospitali ya AICC Jjiini Arusha. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Hospitali ya AICC Prof. Sendui Ole Nguyaine (kushoto), mama mzazi wa watoto hao, Janeth Kimario (katikati) pamoja na wauguzi wa Hospitali hiyo. (Picha kwa hisani ya AICC). Mama huyo alijifungua kwa njia ya oparesheni wakiwa na afya njema. (Picha na AICC)

HOSPITALI YAKUMBWA NA MAFURIKO,WAUGUZI NA MADAKTARI WASITISHA KUTOA HUDUMA KWA WAGONJWA KUFUATIA MVUA KUBWA KUNYESHA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mapema mchana wa leo kumetokea mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es salaam, kumesababisha usumbufu mkubwa baada ya maeneo mengi kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara , nyumba za watu pamoja na maeneo mbalimbali.

Mvua hizo kubwa ambazo hata mamlaka ya hali ya hewa wametahadhalisha kwamba zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014 hadi Tarehe 7.03.2014  zimesababisha usumbufu mkubwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza - Palestina kujaa maji kila kona na kupelekea wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya Meza na viti wakikwepa maji hayo. Na wengine kukimbia katika eneo hilo kuhofia maji hayo.

Walikwepa maji hayo kutokana na kwamba si ya mvua tuu lakini yalikuwa ni Machafu yaliyochanganyikana na maji kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya maji machafu imepita hapo.

Baada ya mvua hiyo kwisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa zaidi ya dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila chumba.

Akiongea kwa Simu Mganga Mkuu wa Hospitalu hiyo amekili kwamba kuna usumbufu mkubwa wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo zinanyesha kwa kiasi kikubwa. 

Ameongeza kwa kusema kwamba kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.
Nao baadhi ya wagonjwa ambao wengine walikuwa katika hali ambayo si nzuri wamesema  wanaiomba serikali itazame tatizo hilo maana licha ya maji hayo kuwa mengi lakini pia ni hatari kwa afya zao kwa ujumla.

Hii ndio picha halisi ilivyokuwa katika picha hizi..
 Huu ni mtaro wa kupitisha maji taka ambao umepita kati kati ya Hospitali ya Palestina amapo ulifumuka na kusababisha kusambaa kwa maji machafu katika kila kona ya Hospitali hiyo
 Mmoja wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kwisha
 Haya ni maji machafu ambayo yametapakaa kila sehemu ya hospitali
 Kushoto ni Mgonjwa akiwa amelala juu ya Benchi ambapo pembeni kuna maji na matope ambayo yamechanganyikana na kinyesi kutoka katika vyoo mbalimbali katika makazi ya watu.
 Hii ndio hali halisi ya Chemba hii ambayo ipo ndani ya Hospitali ya  Sinza Palestina
 Hizi ni chemba zaidi ambazo zipo nje na pia zimeungana na zilizopo ndani ya Hospital hiyo
 Wagonjwa zaidi wakingojea waganga kufika pia kumalizia kusafishwa kwa vyumba hivyo ili wapate hudumiwa
 Moja ya Chumba ambacho kilikuwa kimejaa tope kikingojea kusafishwa
 Hapa hata hapapitiki
 Baadhi ya viti vikiwa vimeegeshwa kwa ajili ya kungoja kufanya usafi
 Hakuna mtu katika maeneo haya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha

 Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa hiyo kunyesha
 Baadhi ya vifaa vya kutibia wagonjwa vikiwa juu ya moja ya kitanda cha kutibia wagonjwa huku watu wakingoja huduma ya matibabu.
 Huu ndio Mtaro wa maji machafu ambapo maji kutoka nje yamepita ndani ya hospitali hiyo na kusababisha maafa baada ya Mtaro huo kuziba. Picha zote na Dar es salaam yetu.

MKUU WA WILAYA YA MAKETE AKABIDHI BATI 183 KWA WAATHIRIKA WA KIMBUNGA WILAYANI HUMO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro (kushoto) akimkabidhi bati Bi. Ami Mahenge, ambaye ni mmoja kati ya waathirika wa kimbunga katika kijiji cha Ndulamo, Makete. 
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Josephine Matiro akiwa na waathirika hao muda mchache kabla ya kuwakabidhi.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na waathirika wa kimbunga katika ofisi za kijiji cha Ndulamo.
 Kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Peter Mwagilo akizungumza na waathirika wa kimbunga (hawapo pichani) wakati wa kuwakabidhi bati kama walivyoahidiwa na serikali.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza kabla ya kukabidhi bati kwa waathirika wa kimbunga katika kijiji cha Ndulamo.
 Bati zenyewe.(Picha zote/habari na Edwin Moshi)
=====
Kufuatia maafa yaliyokikumba kijiji cha Ndulamo wilayani Makete mkoa wa Njombe ya nyumba 10 kuezuliwa na kimbunga mwishoni mwa mwezi februari mwaka huu, halmashauri ya wilaya ya Makete kwa kushirikiana na mfuko wa jimbo, hii leo wamekabidhi bati 180 kwa waathirika wa maafa hayo

Akizungumza na waathirika wa tukio hilo wakati wa kukabidhi bati hizo zenye thamani ya tsh. milioni 2.5, mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro amesema kufuatia mkutano uliofanyika baina ya serikali na wananchi wa kijiji hicho, waligawana majukumu ambapo serikali iliahidi kutoa bati kwa wananchi hao, na hii leo imetekelezwa

Mh. Matiro amesema ingawa msaada huo haukuwa asilimia 100 kwa waathirika wote lakini wamepatiwa zaidi ya robo tatu hivyo kiasi kilichobakia ni kidogo na kuwaomba wananchi hao kumalizia gharama zilizobaki

"Mfano mtu alikuwa ameharibikiwa nyumba yenye bati 24, hapa serikali inampa bati 20 na hizo nne anatakiwa azigharamie yeye mwenyewe, na hii ni kutokana na msaada huo kuhitajika katika vijiji vingine viwili vya makete ambavyo vilikumbwa na maafa tena ili kila mmoja apate kidogo kidogo" amesema Matiro

Amesema kwa hivi sasa hawana budi pia kumshukuru mbunge wa jimbo la Makete ambaye pia ni waziri wa mazingira Dkt. Binilith Mahenge kwa jitihada zake na uongozi wa wilaya kwa ujumla kuhakikisha wananchi hao wanapata bati hizo na kuwaomba wananchi hao kuzitumia kwa makusudi yaliyopangwa na si kuziuza

Awali akimkaribisha mkuu wa wilaya, kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Peter Mwagilo amesema ilifanyika tahmini ya kina na wataalamu wa halmashauri mara baada ya maafa hayo kuwakumba wananchi hao, na hivyo kila mwananchi atapewa bati kulingana na ukubwa wa tatizo lake

"Kwa mfano wapo waliopata maafa kidogo wanahitaji bati chache, wengine bati mbili hao watapata zote mbili, lakini wale waliopata maafa makubwa watapata bati nyingi ila kila mmoja atagharamia kiasi kidogo pale palipopelea" alisema kaimu mkurugenzi

Naye mmoja wa waathirika hao akizungumza na mwandishi wetu baada ya kukabidhiwa bati zake Bi. Ami Mahenge amesema anaishukuru serikali kwa msaada huo aliopewa na kuongeza kuwa kutokana na maafa hayo yaliyomkumba hakujua hatima ya maisha yake, ukizingatia yeye kukosa uwezo wa kifedha lakini msaada huo umekuwa mkombozi wa maisha yake

Bi. Mahenge ametoa wito kwa waathirika wenzake kuhakikisha wanatumia ipasavyo msaada huo, kwa kuwa kumekuwa na kasumba ya kutumia vibaya misaada na baadaye wanaishia kulalamika

MTEMVU AONGOZA MKUTANO MKUU WA KATA YA 14 TEMEKE

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la TemekeAbbas Mtemvu  akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi kata ya 14(CCM) Mohamedi Kidungu

Diwani kata ya Tandika Mariam Mtemvu (kushoto) akisikiliza kwa makini , alipokua akizungumza Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya 14 Temeke

Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (kushoto),akipokea kadi toka kwa mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Musa Ramadhani , ambaye alikua Mwenyekiti wa kata ya 14 Temeke na Mwenyekiti Vijana wa chadema Wilaya amehamia Chama cha  Mapinduzi (CCM),Dar es Salaam mwishoni mwa wiki .
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (kushoto),akipokea kadi toka kwa mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Musa Ramadhani , ambaye alikua Mwenyekiti wa kata ya 14 Temeke na Mwenyekiti Vijana wa chadema Wilaya amehamia Chama cha  Mapinduzi (CCM),Dar es Salaam mwishoni mwa wiki 

Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbs Mtemvu akianyesha kadi ya mwanachama huyo na akiwa anavishwa Tisheti na Katibu Uchumi kata ya 14 Temeke, Celina Tilya .












Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images