Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 239 | 240 | (Page 241) | 242 | 243 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava akifungua kikao kazi hicho

   Mtaalamu mwelekezi kutoka Norway Bw.  Farouk Al Kasim akiwasilisha mada

  Mtaalamu mwelekezi kutoka Norway Bw.  Farouk Al Kasim akiwasilisha mada.


  =========   =======  ======
  Wadau  kutoka Taasisi za Serikali waanza kupitia  rasimu ya kwanza ya sera ya petroli.


  Na Greyson Mwase, Bagamoyo

  Wadau mbalimbali kutoka  taasisi za serikali wameanza kupitia  rasimu ya kwanza ya sera ya petroli katika kikao kazi kilichofanyika katika hoteli  ya Millenium Sea Breeze iliyopo  huko Bagamoyo.


  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava amesema kuwa, kikao hicho  ni  maalum na muhimu kwa ajili ya kupata michango ya wadau hao  ili kuboresha rasimu ya sera ya petroli.


  Mhandisi Mwihava aliongeza kuwa awali rasimu hiyo iliandaliwa na timu maalumu kwa kushirikiana  na mtaalam mwelekezi kutoka  Norway Bw.  Farouk Al Kasim. Timu hiyo  ilijumuisha watalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Rais –Tume ya Mipango, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Nishati na Maji Zanzibar, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na  Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)


  Mhandisi Mwihava aliongeza kuwa lengo la kamati  iliyoundwa lilikuwa ni kuandaa rasimu ya  sera itakayolenga maeneo  yote muhimu yanayohusiana na sekta ya petroli.


  Mhandisi Mwihava alisisitiza kuwa wakati wa uandaaji wa sera hiyo, kamati ilipitia sera za petroli za nchi nyingine kama Norway, Uganda, Ghana, Sierra Leone, Pakistan ili kupata uzoefu.


  Alisema pia kamati hiyo ilitembelea nchi ya Norway ikiwa ni pamoja na kufanya majadiliano ya kina na taasisi za serikali ya Norway zinazosimamia sekta ya petroli ikiwa ni pamoja na kupitia sera zake kwa ajili ya kuongeza ujuzi na uzoefu.


  Aliongeza kuwa sera hii itatumika kama msingi wa kuboresha usimamizi wa sekta ya petroli ikiwa ni pamoja na sheria na kanuni, uendelezaji wa taasisi husika ikiwa ni pamoja uendelezaji wa mpango mkakati wa kukuza uchumi wa nchi.


  Mhandisi Mwihava alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali ya Norway kwa ushirikiano iliyoonesha kwa nchi ya Tanzania katika uandaaji wa sera ya petroli.


  Wakati huo huo  mtaalam mwelekezi kutoka Norway, Bw.  Farouk Al Kasim akiwasilisha mada alisema kuwa  sera ya petroli inahitaji umakini mkubwa sana huku ikishirikisha wadau mbalimbali.


  Bw. Kasim alisema mambo yanayotakiwa kugusiwa kwenye sera ya petroli ni pamoja na  mkakati wa usimamizi, ushirikishwaji wa wananchi,  uwekezaji kwenye mafunzo kwa wazawa ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji.


  Akielezea changamoto katika sekta ya petroli kutokana na uzoefu wake kwa nchi zilizoanza uchimbaji wa petroli Bw. Kassim aliongeza kuwa  kumekuwepo na taarifa  zinazopotoshwa na baadhi ya watu kwa ajili ya maslahi fulani, kutoa matumaini makubwa zaidi ya matarajio ya wananchi, kuingia mikataba mibovu na wawekezaji,  usimamizi mbovu ikiwa ni pamoja na kutokuzingatia usalama wa mazingira.


  “Ndugu zangu  uandaaji wa sera ya petroli unahitaji umakini mkubwa sana, kwani ni sekta inayoweza kutajirisha nchi ikisimamiwa ipasavyo, ikisimamiwa vibaya inaweza kugeuka kuwa laana badala ya baraka.” Alisisitiza Bw. Kasim.


  Naye Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli  Mhandisi Hosea Mbise alisema  kuwa kutokana na kuongezeka kwa kasi ya utafutaji wa mafuta na gesi umepelekea serikali kuandaa sera ya petroli.


  Mhandisi Mbise aliongeza kuwa sera hiyo inalenga uendelezaji wa maeneo ya utafutaji na uchimbaji wa petroli, usimamizi wa sekta ya petroli, sheria ikiwa ni pamoja na usimamizi wa mazingira. Mhandisi Mbise aliongeza kuwa serikali imeanza kupeleka wataalamu nje ya nchi kama moja ya maandalizi ya usimamizi wa sekta ya petroli.

  0 0


  Dereva wa Bodaboda, akiwa na abiria wake, wakinyanyua miguu kukwepa kulowa na maji ya mvua yaliyofurika kwenye barabara ya Mbozi, Chang'ombe jijini Dar es Salaam jana. Mvua ya siku mbili tu tayari imeanza kuleta kasheshe, si kwa wenye magari pia wenye bodaboda, watembea kwa miguu.

  Mto Msimbazi ukionekana Alhamisi Machi 6, 2014 baada ya mvua ya siku mbili jijini Dar es Salaam
  PICHA ZOTE KWA HISANI YA K-VIS BLOG.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Saleh Jidawi Akifungua Warsha ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na Mangariba juu ya Kutahiri watoto wa kiume ili kuepukana na Ugonjwa wa Fistula. 
   Mwenyekiti wa Taasisi ya Interplast ya nchini Uholanzi Dkt. Rein Zeeman kushoto akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya Waandishi wa habari  juu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na Mangariba juu ya Kutahiri watoto wa kiume ili kuepukana na Ugonjwa wa 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Saleh Jidawi katika picha ya pamoja na Wanachama wa Taasisi ya Interplast baada ya Ufunguzi wa Warsha ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na Mangariba juu ya Kutahiri watoto wa kiume ili kuepukana na Ugonjwa wa Fistula.Fistula Zanzibar. PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Interplast ya nchini Uholanzi Dkt. Rein Zeeman aliyesimama mbele akiendesha Warsha ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na Mangariba juu ya Kutahiri watoto wa kiume ili kuepukana na Ugonjwa wa Fistula.

  ========  ========  =====

  Faki Mjaka- Maelezo Zanzibar .

  Taaluma ndogo katika kutahiri Watoto wa kiume imeelezwa kuwa ni miongoni mwa Vyanzo vya Ugonjwa wa Fistula ambapo Watoto waliotahiriwa huwa na njia zaidi ya moja ya kupitishia Mkojo.
  Hali hiyo imepelekea Taasisi ya Interplast ya nchini Uholanzi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kuandaa Warsha ili kukabiliana na tatizo hilo kwa Watoto wa Zanzibar.

  Akizungumza katika uzinduzi wa Warsha hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Saleh Jidawi amesema ni vyema Mangariba wakapatiwa mafunzo kutoka kwa Wataalam ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Amesema kupatikana kwa taaluma ya kutosha kutalifanya tatizo hilo kupungua na kupelekea Afya za watoto kuimarika.

  “Sisi Serikali kazi yetu ni kuhakikisha  Wananchi wanaondokana na Matatizo ndio maana tukashirikiana na Taasisi hii ya Interplast ili kuwajengea uwezo Mangariba wetu juu ya tatizo la Fistula” alisema Dkt. Jidawi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Interplast Dkt. Rein Zeeman amesema wamekuja Zanzibar kwa ajili ya kutoa elimu na ushauri ili Mangariba waweze kupata mbinu bora za kufanya kazi zao. Amefahamisha kuwa Jamii inapaswa kuelewa kwamba kazi ya Kutahiri inahitaji kufanywa kwa taaluma na tahadhari kubwa kama inayochukuliwa katika Upasuaji wa binadamu.

  “Jamii inapaswa kujua kuwa Kutahiri ni jambo la hatari na hivyo linapaswa kufanywa tu na watu waliopatiwa mafunzo ya kutosha” Alisisitiza Dkt. Zeeman. Naye Mshauri wa Taasisi ya Interplast Bi. Ruth Lester amesifia mashirikiano ya kutosha wanayoyapata kutoka kwa Wananchi na Serikali kwa ujumla.

  Ameongeza kuwa matarajio yao nikuona kazi ya Ungariba haifanywi na kila mtu badala yake ifanywe na Wataalam waliosajiliwa ili kuepukana na Tatizo la Fistula kwa Watoto. Amesema utafiti waliofanya wamegundua kuwa kila Watoto 1,000 Wakiume waliotahiriwa Zanzibar wawili hadi watatu wamepata tatizo la Vistula kutokana na kutahiriwa vibaya.

  “Tumefanya utafiti katika sehemu mbali mbali duniani kuhusu kutahiri,kwa mfano Mji wa Birmingham Watoto 50,000 waliotahiriwa hakuna aliyegundulika na tatizo lakini kwa Zanzibar kila Watoto 1,000 Wawili hadi watatu wamepata tatizo” Aliongeza Dkt. Semina hiyo ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Afya na Mangariba imefanyika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View mjini Unguja ambapo pia itaendelea katika Kisiwa cha Pemba ili kuondokana na ugonjwa wa Fistula kwa Watoto Zanzibar. IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  John Lisu .
  WAKATI zoezi la upigaji kura wa kuchagua maeneo matatu ya kufanikisha Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika kuanzia Aprili 20 mwaka huu, waimbaji mahiri wa muziki wa injili hapa Tanzania, Rose Mhando na John Lisu wameonesha shukrani kwa wapiga kura kwa kuwapigia kura nyingi kuelekea tamasha hilo.

  Waimbaji hao wanaoonesha kukubalika na wadau mbalimbali kushiriki katika tamasha hilo kutokana na sababu mbalimbali za uwasilishaji wao wa Neno la Mungu kwa wadau wa tamasha hilo, ingawa zoezi hilo likiendelea. John Lisu amewashukuru Watanzania kwa kuonesha kumkubali katika utoaji wake wa huduma za kufanikisha Neno la Mungu kupitia uimbaji wa nyimbo za injili, huku zoezi la upigaji kura likiendelea.

  Lisu anasema Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amekuwa baraka kwa Mungu kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa kuwaleta waimbaji mbalimbali wa Kimataifa katika tamasha hilo. “Mchango wa Msama kwa jamii ni mkubwa hasa katika maendeleo, hivyo natoa shukrani kwa Msama kwa kufanikisha kufanyika kwa matamasha ya kufikisha neno la Mungu ambayo ni Pasaka na Krismasi,” alisema Lisu.
  Rose Muhando amesema kupata kura nyingi ambazo zinaashiria kipimo cha kuonekana na Mungu  na watu mbalimbali wanaopenda kazi za mikono yake kwamba anastahili kutoa huduma ya Neno la Mungu katika tamasha hilo.

  Muhando anasema kwa sababu Mungu na Watanzania wameona umuhimu wa yeye kushiriki kutoa huduma katika tamasha hilo, anawashukuru kwa hatua hiyo ingawa zoezi bado linaendelea, kwani ni mwelekeo mzuri kwao kuelekea katika tamasha hilo. “Namshukuru Mungu na watanzania wenzangu walionipigia kura kwa wingi ikiwa ni njia pekee ya kufanikisha kuhudumu katika Tamasha la Pasaka,” alisema Muhando.

  Muhando anasema sababu zinazofanikisha kupata uteuzi wa mara kwa mara ni kwamba mara nyingi anapenda kazi yake ijieleze yenyewe na anaamini kwamba kazi yake inatamka neno ambalo linagusa mioyo ya wanadamu ambao wanatakiwa kumfikishia Mungu matatizo yao. Anatumia fursa hiyo kuishukuru kampuni ya Msama Promotions kwa kufanikisha matamasha ya kumuimbia na kumtukuza Mungu kupitia waimbaji mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa ambao kwa pamoja wanatoa elimu kwa jamii kuhusu kumuabudu Mungu.

  Muimbaji huyo amesema atajisikia vibaya iwapo atakosa nafasi ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa sababu tamasha hilo ni kubwa kwani hata ingekuwa kuhudumu bure yuko tayari kwa sababu ibada yake inafika vilivyo kwa Mungu kwa sababu ya wingi wa wanaohudhuria. Muhando anatumia fursa hiyo kuwaeeleza Watanzania kwamba iwapo atapata nafasi ya kuwemo kwenye orodha ya waimbaji katika tamasha hilo, atawasilisha albamu yake ya tano ya Kamata Pindo la Yesu yenye nyimbo nyingi ikiwemo Facebook.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama waimbaji hao wamepigiwa kura na wadau wa muziki huo ambao wanakubali kazi zao.
  Msama amesema  Tamasha la Pasaka la mwaka huu limekuja katika mfumo mwingine kabisa ambao ni wa upigaji kura ili kuchagua maeneo matatu yatakayofanikisha kufanyika kwa tamasha hilo ambalo limekuwa likitumika katika kufanikisha kuwasaidia wenye uhitaji maalum ambao ni pamoja na wajane, walemavu na yatima.

  Kupitia matamasha yanayoandaliwa na Msama, viingilio vinavyopatikana katika matamasha hayo vinafanikisha mipangilio ya kujenga kituo cha wenye uhitaji maalum katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambacho kinajulikana kama Jakaya Mrisho Kikwete, rafiki wa wasiojiweza.
  Msama anasema kwa kuanzia kuelekea tamasha hilo linalotarajia kuanza Aprili 20 jijini Dar es Salaam, ambalo litaendelea katika mikoa mingine zaidi ya nane hapa nchini ambapo kauli mbiu ya tamasha hilo ni ‘Uzalendo Kwanza, Haki huinua Taifa’ inayochochea na kuimarisha amani na kudumisha maendeleo ya Tanzania ijayo.

  Msama anatoa wito kwa kuwakumbusha Watanzania namna ya kuwapigia kura wahusika ambapo utaratibu wa kupiga kura tayari umebainishwa kwa wale ambao watahitaji kufanya hivyo kwa kuandika Pasaka acha nafasi kisha andika jina la mwimbaji unatuma kwenda namba 15327.

  Pia kwa mgeni rasmi  andika neno Pasaka acha nafasi kisha andika jina la mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda 15327, wakati mikoa unaandika Pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura tuma kwenda namba 15327,  pia imebainishwa kuwa kila mmoja anaruhusiwa kupiga kura kadri awezavyo ili kupata mwimbaji na mgeni rasmi na mkoa husika ili tamasha hilo liweze kufanyika katika mkoa husika.

  Msama anasema mojawapo ya  wadhamini wa tamasha hilo ni magazeti ya Dira ya Mtanzania na Pata Habari ambayo ni sehemu ya kampuni ya Msama Promotions na kutoa wito kwa wadhamini wengine kujitokeza kufanikisha tamasha hilo.
  “Tamasha la Pasaka linahitaji wadhamini wengine ambao watasaidia kufanyika kwa ufanisi, hivyo wajitokeze kutusaidia kufanikisha, kwa sababu lina nia njema kwa Tanzania,” alisema Msama

  0 0


  0 0

  Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Wilayani Mufindi,Ndugu Miraji Mtaturu akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama hicho,Ndugu Godfrey Mgimwa mapema leo jioni mbele ya wanakijji cha Mfukulembe,(hawapo pichani),kata ya Ifunda,Iringa vijijini mkoani humo.
  Mgombea Ubunge Jimbo la Kaleta (CCM),Ndugu Godfrey Mgimwa akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Mabikimitali,kata ya Ifunda katika jimbo hilo,mkoani Iringa leo jioni.Godfrey amewaomba wananchi hao kumuamini na kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa kumoigia kura zote za ndiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika machi 16 mkoani humo.
  Mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,kupitia chama cha Mapinduzi,wa kumnadi mgombea wa chama hicho ukifanyika leo jioni kwenye kijiji cha Mibikimitali,kata ya Ifunda Iringa Vijijini
   Ndugu Mwampamba akimuombea Kura,Mgimbea Ubunge jimbo la Kalenga,kupitia chama cha CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa jioni ya leo katika kijiji cha Mibikimitali,kata ya Ifunda,Iringa Vijiini.
   Baadhi akina Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,kupitia chama cha Mapinduzi,mapema leo jioni kwenye kijiji cha Mibikimitali,kata ya Ifunda Iringa Vijijini,ambapo mgombea wa chama hicho,Ndugu Godfrey Mgimwa ndiye amesimamishwa kwenye jimbo hilo kuomba ridhaa ya kuonngoza.
  Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
   Baadhi ya Wanakijiji cha Mibitimitali wakishangilia jambo
   Baadhi ya Wadau wa CCM,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni ya Uchaguzi,jimbo la Kalenga,Iringa vijijini,uliofanyika katika kijiji cha Mfukulembe,kata ya Mafinga,mkoani Iringa mapema leo jioni.

  0 0


  CHADEMA JIMBO LA CHALINZE

                                     TAARIFA KWA UMMA

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Chalinze kimeanza mchakato wa ndani wa kupata mgombea ubunge kwa ajili ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Aprili, mwaka huu, ambapo fomu za uteuzi zimeanza kutolewa kwenye Ofisi Jimbo, kuanzia tarehe 4 Machi na mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu hizo itakuwa tarehe 7 Machi 2014, saa 10.00, jioni.


  Kura za maoni ndani ya chama, zitafanyika tarehe 8 Machi katika Mji wa Chalinze na kufuatiwa na kikao cha kamati ya utendaji ya jimbo ili kufanya uteuzi wa awali kwa mujibu wa Katiba ya chama na hatimaye kikao cha Kamati Kuu kufanya uteuzi wa mwisho ili kupata mgombea atakayeshindana na wagombea wa vyama vingine.


  Mpaka sasa wagombea waliochukua fomu kwenye ofisi ya jimbo ni watatu (3) na wagombea wengine watatu (3) wamechukulia fomu Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam, hivyo hadi sasa idadi ya wagombea waliotambuliwa rasmi ni sita.


  Tunatumia nafasi hii kuujulisha umma wa Watanzania, hususan wanachama wa CHADEMA, kuwa fomu za kuwania uteuzi wa ndani zinaendelea kupatikana sehemu tatu, Makao Makuu ya Chama, Ofisi ya Jimbo la Chalinze na kwenye tovuti ya chama www.chadema.or.tz


  Imetolewa Machi 5, 2014 

  Iddi Omary Ucheche


  Katibu wa CHADEMA, Jimbo la Chalinze


  0 0


  0 0

   Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini,Bwa.Sistyl Nyahoza akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari  (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Ruaha International,mkoani Iringa kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la kalenga, ikiwa ni pamoja na Sheria ya gharama za Uchaguzi kwa wagombea na vyama husika vinavyoshiri katika Uchaguzi huo utakaofanyika machi 16 mwaka huu.
  Pichani wa tatu kulia ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini,Bwa.Sistyl Nyahoza akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Ruaha International,mkoani Iringa kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la kalenga, ikiwa ni pamoja na Sheria ya gharama za Uchaguzi kwa wagombea na vyama husika vinavyoshiri katika Uchaguzi huo utakaofanyika machi 16 mwaka huu.Shoto ni Bwa.Mihayo Kadete,Erald Martin na kulia ni Isaya Makoko ambao wote ni Maofisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
  Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano uliondaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusiana na Uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kalenga mapema leo asubuhi,na pia Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa kujtambulisha uwepo wake katika zoezi zima la uchaguzi wa Kalenga sambamba na kuwafahamisha Wananchi zinazofanywa na Ofisi za Msajili wa vyama vya siasa tangu Maafisa wa Ofisi hiyo wafike mjini Iringa.
  Msajili  wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akifafanua jambo kwa Wanahabari mapema leo asubuhi,mkoani Iringa.

  0 0

  Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga,Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko akikabidhi kadi UVCCM kwa mmoja wa vijana wa kambi ya JUDO ya Vijana wilayani Lushoto.
  jumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga,Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko akipandisha bendera ya CCM kwenye moja ya mashina ya chama hicho.

  ======= ======  ========
  Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko amefunga tawi la Chadema katika Kijiji Cha Lukozi na kupandisha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza Ufalme mpya wa Chama hicho cha siasa.

  Tukio hilo limetokea jana tarehe 6th March 2014 katika kijiji cha Lukozi, wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga, ambapo sambamba na kuasisi tawi hilo la Chama Cha Mapinduzi pia kiongozi huyo wa UVCCM ameingiza wanachama wapya 206 ambapo wengi wao walikuwa ni wanachama wa Chama Cha Demokrasia  na Maendeleo (CHADEMA)

  Mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM, alifungua mashina sita yakiwemo ya Manyara, bodaboda, n.k pia alifanya vikao vinne vya ndani ambapo alizungumza na wanaCCM juu ya hali ya Uimara wa Chama na kuhoji kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Kijiji hicho ndani ya Wilaya ya Lushoto pamoja na kufanya mkutano wa hadhara ambao ulihudhuriwa na wananchi wengi wa Lukozi.

  Pamoja na vikao hivyo lakini pia Husna alitembelea vikundi vya ujasiriamali vya  akinamama pamoja na kambi ya JUDO ya Vijana wilayani Lushoto na kujadili nao Changamoto wanazokutana nao na kushirikiana nao kuzipatia ufumbuzi.

  Husna anafanya ziara za kawaida katika Mkoa mzima wa Tanga katika kuhamasisha Vijana kujiunga na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Vijana.

  0 0

  Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (kulia)akiteta na Afisa Mnadhimu wa Polisi Kinondoni, Bibie Juma Athumani (wa kwanza kushoto)baada ya Airtel kukabidhi viti na meza kwa ajili ya polisi wa kituo cha oysterbay hivi karibuni.Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa Polisi wa kituo hicho.
  Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (kulia) akisalimiana na Afisa Mnadhimu wa Polisi Kinondoni, Bibie Juma Athumani baada ya Airtel kukabidhi viti na meza kwa ajili ya polisi wa kituo cha oysterbay hivi karibuni.Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa kituo hicho.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea kuunga mkono serikali kupitia jeshi la polisi usalama barabarani kwa kuwapatia vifaa vya ofisi kwa ajili ya kituo cha Usalama Barabarani cha Oysterbay kilichopo wilaya ya Kinondoni.
    
  Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Afisa uhusiano na matukio wa Airtel  Dangio Kaniki alisema “Airtel inatambua umuhimu wa kazi inayofanywa na Kitengo cha Usalama Barabarani katika kusimamia na kuhakikisha usalama wa watanzania na kuamua kushirikina nao katika kuboresha mazingira ya kufanyia kazi. Leo tunatoa meza pamoja viti vya ofisi kwa kitu hiki cha polisi oystebay tukiamini   kwamba tutaongeza ari na moyo wa kujituma kwa maofisa hawa  na kuleta ufanisi wa kazi ,”

  kwa miaka mitano mfululizo sasa Airtel imekuwa ikishirikiana na jeshi la polisi katika kufanikisha zoezi la usalama barabarani hivyo tumeonelea ni vyema kuendelea kushirikiana nao  ili kuleta mafanikio makubwa katika kutekeleza kazi zao  nchini.

  Airtel itaendelea na dhamira yake  yakushirikiana na jeshi la polisi katika juhudi za kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa na kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kwa kiasi kikubwa nchini

  Kwa upande wake, Afisa Mnadhimu wa Polisi  Kinondoni, SSP. Bibie Juma Athuman alisema “Naishukuru sana Airtel kwa kutoa mchango wa vifaa vya ofisi kwenye kituo changu kwani tulikuwa na uhaba mkubwa wa viti na meza za kukalia wafanyakazi pindi wakiwapo ofisini. Msaada huu utasaidia kutatua matatizo tuliyokuwa nayo na kuboresha mazingira ya wafanyakazi wa kituo hiki kuwa mazuri zaidi.  Tunawaomba makampuni mengine pia yashiriki katika kuwawezesha jeshi la polisi na kuchangia katika kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa kama wanavyofanya wenzetu wa Airtel.”

   Msaada huo ni muendelezo wa mpango wa Airtel kusaidia Polisi  Usalama Barabarani hapa nchini ambapo mwezi Septemba mwaka jana kampuni hiyo imetoa T-shirt zenye ujumbe Maalum wa Usalama Barabarani, stika zenye ujumbe wa kuelimisha na mafunzo kwa ajili ya kuelimisha Usalama Barabarani kwa waendesha bodaboda mkoani Mwanza.

  0 0

    


  RETIREMENT PLANNING COURSE


  A unique opportunity for employeesto develop Entrepreneurship, Financial Literacy and Retirement Planning Skills. The longer prior to retirement you take this course, the more you will benefit.


  Approach and Contents

  The course is delivered by highly experienced facilitators using experiential methods. Participants are guided to recognize opportunities and challenges of retirement; their talents and other tangible and intangible assets and liabilities; alternative  post-retirement “careers”;  to choose when to retire; and to continuously build their asset base, streams of income and fulfilling lives after retirement. They are exposed to good practices in starting and running a business, personal finance and health management; expected pension benefits and investment schemes tailored to retirees. They leave with self awareness, a Retirement Vision and look forward to their exit from employment.


  Dates, Fee and Registration

  24th - 27th March, 2014, Morogoro. Tuition is Tshs 500,000/= per person. Apply: info@imedtz.org or 0718-942314 (Ulrich) and

  0754-548248 (Hellen) or visit us at Mwalimu House, 7thFloor, Uhuru Road, Ilala, Dar es Salaam or www.imedtz.org to pick the Registration Form.  We also offer Certificate and Diploma courses in Entrepreneurship and Business Management registered by NACTE 


  0 0


  0 0


  Jhikoman,  Tanzania´s great Reggae Ambassador to represent Africa…SUNDAY MAGAZINE - Nairobi, KENYA
    Having internationally toured, Jhikoman and the Afrikabisa band has performed in well-known international music festivals such Mela in Oslo, Norway, World Village festival / Maalma Kylassa in Helsinki, Finland;  Exeter Respect Festival in Exeter City-Devon UK and locally at ZIFF- Zanzibar International Film Festival, and Sauti za Busara in Zanzibar as well as Bagamoyo International Art  Festival.

   This true son of Africa is honoured at home and abroad and has earned himself abundant recognition, “No more bloodshed for our liberation…to free our own minds is the last and permanent solution “ with this message to the world and having been granted audience to perform at recognized International festivals such as The International African Festival Tübingen and the 1st African Tourism Exhibition tradefair Germany, Afrikabisa Band under leadership of Ras JhikoMan- Tanzanian Singer/composer  base in Bagamoyo,Tanzania wish to make use of this opportunity to thrill fans in Europe this Summer 2014. To meet it´s target, the Band is therefore soliciting for sponsorship and support.  

  0 0

  Wahamiaji Haramu hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole katika kata ya Ruaha Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi likiwa katika doria ya kawaida na kulitilia mashaka gari hilo lililokuwa limebeba matenga ya Nyanya.

   Kiongozi wa Wahamiaji Haramu,akiwagawia wenzake mikate  ilionunuliwa na wanahabari waliokuwepo kwenye tukio hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani humo.
   Kiongozi wa Wahamiaji Haramu,akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na sakata lao la kukamatwa nchini Tanzania,anasema wamesafiri nchini kwao Ethiopia mpaka Tanzania kwa siku 21
   Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akizungumza na Waaandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye makao ya Polisi ya mkoani humo,akithibisha kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao wakiwa katika roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga wakitokea nchini Ethiopia kuelekea nchini Afrika Kusini.
   Roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga ndilo lililotumika kuwabeba wahamiaji hao.
   Matenga ya Nyanya ambamo Wahamiaji hao walikuwa wamekaa.PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-IRINGA
  =======  =======  ======  WAHAMIAJI HARAMU 46 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI

  Na Denis Mlowe,Iringa

  JESHI la Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 46 kutoka Ethiopia waliokuwa wakielekea nchini Afrika ya Kusini.

  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amethibitisha kukamatwa wahamiaji hao wakiwa katika roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga..

  Mungi alisema wahamiaji hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole katika kata ya Ruaha Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi likiwa katika doria ya kawaida na kulitilia mashaka gari hilo.

  “Jeshi la polisi lilipata habari za kiintelejensia kuwa kuna roli limebeba wahamiaji haramu vijana wakajipanga na kufanikiwa kuwakamata wakiwa katikakati matenga ya nyanya yaliyopangwa kwa pembeni na na kufanikiwa kuwakamata vijana hao 46 akiwemo mtoto wa miaka 17” alisema Mungi.

  Alisema kuwa dereva wa gari hilo anashikiriwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na kusema baadhi ya Waethiopia hao 6 kati yao wana hati ya kusafiria (passport).

  Katika hali kuonyesha ukarimu kwa wageni hao haramu waandishi wa habari walioko katika kampeni za jimbo la Kalenga wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa waliwapatia msaada wa vyakula wahamiaji hao baada ya kuonyesha wanakabiliwa na njaa kali na kiu ya maji.

  Waandishi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa Iringa (IPC), Frank Leonard walichangishana na kupatikana kiasi cha shilingi elfu 50 na kufanikiwa kuwapatia vyakula hivyo.  0 0


  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo wajumbe wenzie Bi. Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Richard Ndassa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sumve, kabla ya kuingia katika Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli akimweleza jambo Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo Bw. John Mnyika Mapema leo Mjini Dodoma.
  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Ismail Aden Rage (mwenye kanzu) na Hashim Rungwe wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo Mjini Dodoma
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwaeleza jambo wajumbe wa Bunge maalum la Katiba Edward Lowassa (mwenyeshati Jeupe) na Philemon Ndesamburo, Ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mufti, Sheikh Thabit Noman Jongo akiongoza  dua ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Mstaafu Donald Mtetemela akiongoza sala ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma. (PICHA NA HASSAN SILAYO)

  0 0


  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai .

  (Na Jovina Bujulu, MAELEZO DODOMA).

  Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar ni jambo la kujivunia kwa watanzania wote na katika bara la Afrika.

  Hayo yamesemwa leo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai wakati wa mahojiano katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC ONE.

  Mh. Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema kuwa jambo la Muhimu tunalotakiwa kufanya kwa sasa ni kuimarisha na kuboresha Muungano ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo.

  “Hatuna budi kuendelea kuuimarisha muungano uliopo ikiwa ni kichocheo cha maendeleo, tumeona mifano kwenye nchi kadha wa kadha zilizo katika muungano mfano nchi Marekani imekuwa mfano bora duniani kimaendeleo hasa kutokana na Muungano uliopo” Alisema Ndugai.

  Mh. Ndugai aliongeza kuwa hata Muasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akitukumbusha mara kwa mara kuusimamia muungano wa Tanzania na kuudumisha.

  “Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiasa Watanzania wote kuudumisha Muungano wa Tanzania na kuepuka viashiria vyote vinavyoonekana kuvunja muungano, hivyo tushikamane katika kuudumisha”. Alisema Ndugai.

  Naye Mjumbe wa Bunge hilo ambaye mjumbe wa secretariati ya marekebisho kanuni za Bunge Maalum Mhesh. Evod Mmanda alisema kwamba miaka 50 ya muungano ni faraja na jambo la kujivunia.

  “hatuna budi kwa pamoja kukaa na kuufikiria zaidi Muungano na kutatua changamoto zote zinazojitokeza ili kuudumisha muungano huu na Wasiopenda Muungano  hawana sababu za kutosha” Alisema Mh. Mmanda.

  0 0


  0 0

  Na Jovina Bujulu ,MAELEZO DODOMA.

  Serikali itaendelea kuchukuwa hatua za utekelezaji katika maeneo ya kijamii ili kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia nchini. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh. Dkt. Pindi Chana hivi karibuni Mjini Dodoma.

  Akizataja hatua hizo hizo Dkt. Pindi alisema kuwa serikali imemekuwa ikiwajengea  wanawake uwezo wa kisheria ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha na jamii kwa ujumla.

  “Sheria kadhaa zimekuwa zikitungwa na nyingine zikifanyiwa marekebisho, ikiwemo sheria ya makosa ya kujamiiana ya Mwaka 1998, sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004 na sheria ya mtoto ya mwaka 2009 na hii yote ni kuhakikisha tunawajengea wanawake mazingira bora” Alisema Dkt. Pindi.

  Aidha, Dkt. Pindi aliongeza kuwa kumekuwepo na ongezeko la ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi, Ongezeko hilo linatokana na marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1995 ambapo viti maalum viliongezwa na kuwa asilimia 15 kwa Tanzania bara na asilimia 20 kwa upande wa Zanzibar.

  Pia Dkt. Pindi alisema kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa maendeleo ya wanawake unaotoa mikopo ya uanzishwaji wa biashara na shughuli nyingine za kiuchumi ili kuwawezesha wanawake nchini.

  Aliongeza kuwa serikali imeandaa sera ya mitaji midogo midogo ya mwaka 2000 ambayo imeweka mazingira mazuri kwa taasisi binafsi za fedha  kama PRIDE, FINCA, BENKI YA WANAWAKE NA CATSBY kutoa mikopo kwa wanawake.

  Madhumuni ya kuazimisha siku ya Wanawake duniani ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa unaofanywa na wanawake katika kuleta maendeleo na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na kijamii.

  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kijiji cha Wangama, Fred Mgata (kulia) akikabidhi kadi za chyama hicho kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga baada ya yeye na wanachama wengine 50 wa Chadema kuamua kukihama na kujiunga CCM katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika  katika Kijiji hicho kilichopo Kata ya Luhota, Iringa Vijijini leo. Mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chadema ambaye ni mzaliwa wa kijiji hicho,  Grace Tendega alikuwa chini ya uongozi wa Mgata.
   Mgata akisalimiana na mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa
   Mgata akipongezwa na wafuasi wa CCM kwa kitendo chake cha kuamua kuihama Chadema na kujiunga na CCM
   Ofisa wa Umoja wa Vijana wa CCM Makao Makuu, Mariana Shonzaakimuombea kura  mgombea ubunge wa CCM, Mgimwa.
   Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akihutubia katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Wangama.
   Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa 9kulia) akilakiwa kwa shangwe na vigeregere na wananchi wa Kijiji cha Ikuvilo, Kata ya Luhota alipowasili kwa ajili ya mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo leo Iringa Vijijini.
   Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu wakiungana na wananchi wa Kijiji cha Wangama alichozaliwa mgombea ubunge wa Chadema, Grace Tendega, wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Luhota, Iringa Vijijini leo.
   Baadhi ya mabalozi wa CCM wa Kijiji cha Wangama wakinyoosha juu mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.
   Mkazi wa Kijiji cha Wangama akifurahia sera za CCM zilizokuwa zinatolewa kwenye mkutano huo.
   Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Rehema Mohamed akionesha moja ya majeraha  yaliyvyomuathiri mguuni wakati wa vurugu zilizofanywa katika maandamano ya Chadema mkoani Arusha. Rehema ambaye kabla ya kuhamia CCM alikuwa Diwani wa Chadema, alikuwa akihutubia katika mkutano wa kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa leo katika Kijiji cha Ikuvilo, katika Kata ya Luhota, Iringa Vijijini leo.
   Mfuasi wa CCM, Sabinus Segerela akishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Ikuvilo, Kata ya Luhota, Iringa Vijijini leo.
  Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Seif Shaaban Mohamed, akihutubia katika mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa katika katika Kijiji cha Ikuvilo, Kata ya Luhota, Iringa Vijijini leo. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

older | 1 | .... | 239 | 240 | (Page 241) | 242 | 243 | .... | 1898 | newer