Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 232 | 233 | (Page 234) | 235 | 236 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Kutoka kushoto ni Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Kata ya Masekelo(Chadema),na Kulia ni Sebastian Peter aliyekuwa diwani kata ya Ingokole(Chadema) wakitambulishwa mbele ya umati wa watu na Katibu wa NEC itikadi na uenezi Nape Nnauye kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini ambao kwa moyo mmoja wamejiunga na CCM.


  0 0

   Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Allan Chonjo akitangaza majina ya washindi wa droo ya tatu ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti mbele ya wana habari(hawapo pichani)mara baada ya kuchezesha droo mapema leo jijini Dar es Salaam, anayemshuhudia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Mrisho Milao.
   Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Allan Chonjo akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti wakati wa droo hiyo mapema leo.


  Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Allan Chonjo akitoa maelezo kwa wana habari mara baada ya kupatikana kwa washindi wa droo ya tatu ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti mapema leo jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Afisa Mwandamizi kutoka PWC Golder Kamuzora.
  ========   =======  ======

  PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI YAENDEENDELEA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KATIKA DROO YA TATU.


  Wawili wajishindia simu za kisasa kutoka Bia ya Serengeti.


  Kwa wiki mbili zilizopita Kampuni ya Bia ya Serengeti imeweza kupata washindi kutoka mikoa mbali mbali  kama vile Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam katika promosheni yake inayoendelea nchi nzima ya WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI. Katika droo iliyochezeshwa leo kiwandani hapo washindi wawili wa ‘Samsung tablet’ walitangazwa ambako bahati hiyo iliangukia kwa Bw Mikidadi Omari (45) kutoka Mbagala, Dar es Salaam na Eddy Kisanga (67) kutoka Moshi, Kilimanjaro.

  Droo hiyo iliyochezeshwa mapema leo huku ikishuhudiwa na wana habari, Maafisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, PWC na Push Mobile Media. Mbali na washindi wa droo za kila wiki kama waliopatikana leo pia kuna washindi wa bia za bure, fedha taslim na ving’amuzi kwa wiki iliyopita. Promosheni hii bado ina wiki tisa mbele za zawadi za kutosha ikiwemo ile kubwa zaidi ya safari ya Brazili.


  Bw Eddy liyejawa furaha alielezea furaha yake na kutoamini kama atamiliki kifaa cha kisasa cha mawasiliano, washindi wote waliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwa na ofa kabambe kwa wateja wao kila kukicha. Eddy alisema “ninafuraha sana kuwa moja ya washindi wa promosheni hii, nilifahamu kuhusu kampeni hii kupitia vyombo vyetu vya habari vya hapa nchini na nilihamasika kushiriki. Nilisita kushiriki promosheni hii lakini  kwa ushindi huu nitaendelea kushiriki promosheni hii huenda nikabahatika tena na kupata safari ya Brazili.


  Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Allan Chonjo alieleza kuwa promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inaendelea vizuri na washindi wanapatikana kutoka kote Tanzania. Allan aliongeza  “Tuna washindi kutoka sehemu mbalimbali kama Mwanza, Moshi, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam, kwetu hili ni moja ya mafanikio makubwa kufanikisha kuwafikia wateja wetu waliopo maeneo tofauti. Promosheni hii ni ya nchi nzima na si kwa wateja wa Dar es Salaam tu ila ni pamoja na wateja wetu wote hata wale waliopo mikoani.”


  Washindi wa wiki iliyopita waliojipatia ving’amuzi ni Godbles Sehaba na Karushe Mathias ambao tayari wameshakabidhiwa zawadi zao na siku ya Jumamosi tunategemea kukabidhi zawadi kwa washindi wetu mkoani Mwanza Bw Jacob Nnko aliyetangazwa mshindi wa ‘Samsung tablet’ wiki iliyopita na Deus Mwikitalu aliyejishindia king’amuzi.


  Kunywa kwa tahadhari. Inauzwa kwa wenye miaka 18+


  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  leo imetangaza kudhamini tuzo za Mwanamakuka zenye lengo la kusaidia wanawake kutoka katika maeneo mbalimbali kujiinua kiuchumi

  Tuzo za Mwanamakuka zinaandaliwa na The Unity of Women friends kila mwaka zikiwatambua wanawake jasiri waliopambana kubadili maisha yao kutoka katika hali ngumu, duni na umaskini

  Akiongea kuhusu udhamini wa Tuzo hizo Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Airtel inaamini kwamba ujasiriamali ni muhimu katika kufikia maendeleo ya kiuchumi na kuondoa umaskini. Kwa kudhamini tuzo hizi za mwanamakuka tunajikita katika kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kuwa sehemu ya shughuli za maendeleo ya wanawake nchini”.

  Kwa miaka mitatu mfululizo Airtel tumekuwa moja ya wadhamini wa tuzo hizi za mwanamakuka ambazo zimebadili maisha ya wanawake na kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wenye mafanikio. Tutaendelea kuonyesha dhamira yetu katika mipango ambayo itasaidia wanawake walio katika mazingira magumu kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleo ya taifa."

  Jane aliongeza kwa kusema , kuna msemo unaosema ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii nzima. Airtel tumejipanga kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani tunaamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewezesha jamii kwa ujumla

  Kwa upande wake mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo alisema” Tunashukuru Airtel kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha tuzo hizi ambazo ushirika huu umekua wa mafanikio makubwa. Lengo la tuzo hizi ni kuwahamasisha na kuwavutia wanawake  kufikia ndoto zao. Lakini hasa tuna hakikisha kuwa zoezi hili na matokeo yake yanaleta mafanikio ya kudumu na kubadili maisha yao”

   Tuzo za mwanamakuka za mwaka huu zitafanyika sambamba na kusherehekea siku ya wanawake Dunia, Mwanamakuka family bonanza itafanyika tarehe 15 machi 2014 , siku ya Jumamosi katika viwanja vya Escape 1 Dar es Saalam kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 2 Usiku.

  0 0

  CHAMA cha Mapinduzi (ccm), kimejiingiza matatani baada ya kuwapangisha wafanyabiashara wawili katika flemu moja la kufanyia biashara.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam mfanyabishara Charles Msigwa alisema aliingia mkataba na Mecy Mziray ambaye kwa sasa ni marehemu na aliendelea kumlipa kodi ndugu wa marehemu Vesta Haule.Alisema wakati akiendelea kufanya biashara katika banda hilo alishangazwa na viongozi wa CCM tawi la Vigaeni Kata ya Ndugumbi kumfuata wakitaka aingie mkataba upya na chama hicho.
  index
  “Nimekuwa nikiendesha shughuli zangu za biashara kwa muda wa miaka minne ndipo nilipofuatwa na viongozi wa CCM na kunishauri nichukue mkataba nao ili chama kipate mapato,”alisema Msigwa. 

  Aliongeza kuwa viongozi hao walimuita kwenye ofisi ya tawi na kumuhakikishia hakutakuwa na tatizo lolote juu ya mkataba huo.“Viongozi hao waliniambia kuwa mabanda hayo hayarithishwi hata hivyo aliyeachiwa amekuwa msumbufu wa kodi mwenye banda alishafariki kwa hiyo banda huwa linarudi na kuwa mali ya chama,”alisema.

  Msigwa alisema kuwa aliujaza mkataba huo na kuurudisha ofisini kwao alipotaka kuulipia akawa anazungushwa zungushwa.“Nilipeleka malalamiko yangu Kwa uongozi wa Wilaya ambapo uliwaandikia barua ya kwamaba wanitafutie banda jingine iwapo nikiwa tayari kutimisha masharti ya kuwa mpangaji wa chama hicho na nilikubali lakini uongozi huo haukufanya kama ulivyo agizwa,”alisema Msigwa. 

  Awali Chama cha mapinduzi (CCM) kiliingia mkataba wa kujenga banda hilo na Marehemu Mecy Mziray gharama zake na asingeweza kutoka mpaka gharama zake za ujezi zitakapo malizika.

  0 0

   New Arrivals Funzone at Shamo Tower Mbezi Beach Tanki Bovu, KWA MAWASILIANO ZADI PIGA NO. 0654 149749.


  0 0

  Baadhi ya madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana katika mabanda mbalimbali katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya Bangkok Gems and Jewelry Fair.
  Mfanyabiashara wa madini na Afisa Masoko wa Kampuni ya Tom Gems Tanzania, akimwonesha mgeni aliyefika katika banda la Tanzania kuona madini ghafi ya Tanzanite yanayozalishwa Tanzania pekee. Wageni wengi wamefika katika banda hilo kuona Tanzanite halisi kutoka Tanzania.
  Mwenyekiti wa Madini ya Viwandani Bw. Kassim Iddi Pazi, akimwonesha mgeni madini ya Ruby. Kutokana na maelezo ya Bw. Pazi, ameeleza kuwa, madini hayo yametoka katika maeneo ya Winza Dodoma na Matombo Morogoro.
  Mfanyabiashara wa Madini kutoka Kampuni ya Tom Gems Bw.Benjamin Mtalemwa akimwonesha mgeni madini mbalimbali alipotembelea banda la Tanzania. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mthamini wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Edward Rweymamu, Wa pili kulia ni Afisa Madini kutoka Shirika la Madini Tanzania (STAMICO). Bw. Peter Maha, na wa kwanza kulia ni Afisa toka Wizarani Bibi. Margareth Muhony.

  Na Asteria Muhozya, Bangkok

  Madini ya Tanzanite yamekuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya‘’Bangkok Gems and Jewelry Fair’’, yanayoendelea katika eneo la kibiashara la ‘Impact Challenger’, jijini Bangkok.

  Madini ya Tanzanite yanayozalishwa nchini Tanzania pekee duniani, yamekuwa kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea maonesho hayo ikiwemo wauzaji, wanunuzi na wafanyabiashara ambao wamefika katika banda la Tanzania kutaka kuona Tanzanite halisi kutoka Tanzania.

  Aidha, pamoja na kwamba madini ya Tanzanite yanazalishwa na Tanzania pekee, lakini katika maonesho hayo ya Bangkok, madini hayo yanapatikana kwa kiasi kikubwa katika mabanda ya washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani jambo ambalo linaonesha namna madini hayo yalivyo na muhimu katika sekta za kibiashara na kiuchumi.

  Akizungumzia suala la uwepo wa madini ya Tanzanite kwa kiasi kikubwa katika soko la kimataifa, na katika maonesho hayo, Kamishna Msaidizi wa Madini , Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hamis Komba, ameeleza kuwa, uwepo wa Tanzanite katika soko la kimataifa unaashiria mahitaji makubwa ya madini hayo duniani na umuhimu wake katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania, na nchi nyinginezo ikiwemo thamani yake katika soko la kimataifa na upekee wake.

  Aidha, , aliongeza kuwa, hiyo ni changamoto katika uthibiti wa madini hayo katika soko la kimataifa kutokana na uwiano wa takwimu za kiasi cha madini kinachotoka kwa kufuata taratibu za usafirishaji madini hayo nje ya nchi na uwingi halisi unaoonekana katika soko la Kimataifa.

  “Uwiano wa takwimu za uzalishaji Tanzania na idadi halisi ya madini iliyopo katika maonesho ya kimataifa ni tofauti. Hii ni changamoto katika udhibiti wa madini haya” Amesema Kamishna Komba.

  Hivyo, ameongeza kuwa, Serikali inalifanyia kazi suala hili kwa lengo la kufanikisha usimamizi na biashara endelevu ya madini ya Vito na usonara.

  Mbali na madini ya Tanzanite kuwa kivutio, katika banda la Tanzania, vinyago vinavyotengenezwa kutokana na mawe aina ya Zoisite, Basalt, Limestone, Travertine, Granite na White marbale yanayopatikana Tanzania  ambayo yametengenezwa mapambo mbalimbali ya majumbani yamekuwa kivutio kikubwa katika maonesho hayo kwa wageni waliotembelea banda la Tanzania kutoka nchi za Ulaya na Asia, akiwemo pia Rais wa Shirikisho la wafanyabiashara wa vito na usonara Bw. Somchai Phornchindarak, ambaye pia alitembelea Banda la Tanzania na kuonesha kuvutiwa na kushangazwa na mapambo hayo.

  Akizungumzia kuhusu ushiriki wake katika maonesho hayo, Mratibu wa kituo cha Tanzania Geomological Center, Bw. Musa Shanyangi, amesema kuwa, maonesho hayo yamekuwa ya manufaa katika soko la madini ya mawe kutokana na wageni wengi kuonesha kuvutiwa nayo.

  Shanyangi, ameongeza kuwa, tayari kituo hicho kimeanza kufanya ukarabati wa miundombinu na kuandaa mitaala ya kufundishia , hivyo chuo kitaanza kutoa mafunzo ya uchongaji wa vinyago, ukataji wa madini ya vito, uchongaji wa mawe, mafunzo ya utambuzi wa madini ikiwemo pia maabara itakayotumiwa kwa ajili ya shughuli hizo.

  Hivyo, amewataka vijana wa kitanzania kuitumia fursa hiyo kupata mafunzo hayo ili waweze kuingia katika sekta ya madini kwa kuwa itawasiadia kujiajiri, kuinua vipato vyao na kuchangia katika ukuaji wa uchumi. Aidha, amewataka wadau katika sekta ya madini kuona umuhimu wa kuongeza thamani ya madini.

  “ Maonenesho hayo, yamekuwa na manufaa kwa Tanzania, kituo chetu kimepata fursa ya kufaa kwa bidhaa za mawe, kwasababu nimejaribu kuzunguka katika mabanda mengi sana sijaona bidhaa kama hizi. Hiyo ni fursa kwetu na kwa vijana wa Tanzania katika soko hili. Amesema Shanyangi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Madini ya Viwanda Tanzania (FEMATA), Bw. Kassim Iddi Pazi akielezea ushiriki wake katika maonesho hayo na soko la madini kimataifa ameeleza kuwa, maonesho hayo yamefungua fursa kubwa ya biashara kutokana na kupata oda nyingi za madini mbalimbali yakiwemo madini ya ruby na zoisite. Ameongeza kuwa, wamegundua mambo mengi ya muhimu yatakayowasaidia wachimbaji katika sekta hiyo na hasa madini ya viwandani.

  “Hakuna kitu muhimu kama kushiriki maonesho. Ruby yetu ni bora na imependwa sana hapa. Wengi walijua Ruby inatoka Bama lakini uwepo wetu umewafanya kujua Ruby safi inatoka Tanzania. Namshukuru Sana Mhe. Rais na Wizara kwa kutuwekea mazingira mazuri katika sekta hii na kutuwezesha kushiriki maonesho haya”. Amesema, Pazi.

  Aidha, ameongeza kuwa, kama viongozi wa shirikisho hilo, wanao wajibu wa kuwasaidia wachimbaji wengine kupata taarifa mbalimbali kuhusu sekta hiyo kutokana na uzoefu walioupata na hivyo amewataka kufanya kazi na Serikali kwa ushirikiano.

  Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza maonesho hayo ya 53 ya Kimataifa ya ‘Bangkok Gems and Jewelry Fair, ambapo mwaka 2013 ilishiriki kama nchi mwalikwa ambapo kiongozi wa ujumbe wa Tanzania alikuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Mhe. Stephen Masele.

  0 0

  Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura likiwa ndani ya Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam tayari kwa Ibada maalum ya kumuombea Marehemu huyo iliyofanyika mchana wa leo kanisani hapo.
  Viongozi wa Kanisa hilo la Mt. Peter wakiwaongoza waomboleazaji kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiwaongoza waomboleazaji mbali mbali kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Prof. Rwekaza Mkandala (mbele) Sir George Kahama,pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akimfariji Mjane wa Marehemu pamoja na watoto wakati wa Ibada maalum ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura,iliyofanyika kwenye kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.


  Familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura ikiwa kanisani hapo sambamba na waombelezaji wengine mbali mbali.
  Watoto wa Marehemu Balozi Fulgence Kazaura wakizungumza jambo,pamoja na Mama yao (katikati).
  Mtoto Mkubwa wa Marehemu Balozi Fulgence Kazaura,Kamugisha Kazaura akisoma risala fupi ya baba yake wakati wa Ibada Maalum ya kutoa heshima za mwisho,iliyofanyika mchana wa leo kwenye Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
  Mzee Samuel Tassa ambaye alikuwa ni mtu wa karibu la Marehemu Balozi Fulgence Kazaura,akimzungumzia namna walivyoweza kuishi pamoja katika kipindi chote cha Uhai wake.
  Muwakilishi wa Mabalozi wastaafu nchini,Balozi Anthony Nyaki akitoa ujumbe wa Mabalozi wenzake namna walivyoguswa na msiba huo wa Mwenzao,Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.
  Ibada ikiendelea kanisani hapo.
  Mh. Mkapa akilishwa Mkate wa Bwana.
  Prof. Mkandala akilishwa Mkate wa Bwana.
  Sir George Kahama.  0 0

   Hii ni sehemu moja tu ya Mlimani City Mall ambayo kuna mlinzi mmoja tu eneo la kupaki magari hii ni hatari sana kwa wananchi wanaokuja na magari yao eneo hili maana hakuna ulinzi wa kutosha. Hivi kweli mtu huyu mmoja anaweza kulinda eneo lote la Mlimani City au kuna mchezo unachezwa.
   Sehemu hii pia haina mlinzi anayelinda magari yanayopaki Mlimani City  Mall hii ni hatari kwa watu wenye magari yao maana wezi ni wengi eneo hili kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi mzuri. Unaweza kujiuliza hivi kweli hakuna walinzi wa kutosha wa kukaa kwenye sehemu hii maana kwa siku magari yanayoingia na kutoka Mlimani City ni zaidi ya 400.
  Hivi kweli uongozi wa Mlimani City Mall unafanya hata ukaguzi eneo hili kuona kama kuna tatizo, mpaka blog yetu hii ilipopita hapo na kuliona hili tatizo kwa wakati mdogo. Ukitizama katika picha hiyo ya hapo juu unaona hakuna walinzi sehemu hizo mbili . Hivi kweli wizi ukitokea eneo hili nani atarahumiwa kati ya uongozi na walinzi wa Mlimani City.
  Huu ndio mwenekano halisi wa magari yakiwa yamepaki na kuna mlinzi mmoja kwa juu ambaye hawezi kuona magari yote kwa kupitia juu.

  0 0


   Wahariri wakiwa katika picha ya pamoja a viongozi wa TBL wakati wa ziara hiyo.
   Wahariri wa Vyombo vya Habari wakitembelea eneo la upikaji bia wakati wa ziara yao iliyofanyika  kwenye Kiwanda cha Bia Tanzania cha Dar es Salaam
   Mtalaam wa Upishi Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Benjamin Budigida akitoa maelezo ya jinsi bia inavyopikwa kwa kutumia njia ya kisasa ya kompyuta  wakati wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.
   Meneja wa Usimamizi wa Ubora wa Bia wa TBL, Conchesta Ngaiza (kulia) akielezea jinsi wanavyodhiti ubora wa bia.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Nevile Meena wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo  vya habari katika Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Kelvin O'Flaherty.


   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kulia) akielezea utendaji wa kampuni hiyo, wakati wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea  Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.
   Robin akisalimiana na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Habari Leo, Joseph Kulangwa
   Wahariri wa Vyombo vya Habari wakitembelea idara ya uchachuaji wa bia wakati wa ziara yao iliyofanyika  kwenye Kiwanda cha Bia Tanzania cha Dar es Salaam
   Fundi wa Upishi Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Benjamin Budigida akitoa maelezo ya jinsi bia inavyochujwa  wakati wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea juzi Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.
  Mhariri kutoka Gazeti la Mwananchi, Rashid Kejo akifurahia kupata zawadi yake
   Joseph Kulangwa wa Gazeti la Habari Leo, Joseph Kulangwa akipatiwa zawadi
   Mhariri wa  Gazeti la Uhuru, Jane Mihanji akipokea zawadi ya bia baada ya kumaliza ziara TBL
   Meneja Mawasiliano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Orio akifafanua jambo mbele ya wahariri
                    Rashid Kejo wa gazeti la Mwananchi akipokea zawadi ya bia baada ya ziara
  Wahariri wakizuru Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam

  0 0
 • 02/26/14--13:10: KINGWENDU AJA NA FAZA HAUSI
 • MSANII wa filamu nchini Athumani Lali 'Budege' baada ya kucheza filamu za watu sasa ameamua kuja na filamu zake mwenyewe na kuwawezesha wasanii wenzie kuwa na kipato kizuri baada ya kuamua kufungua kampuni yake binafsi inayokwenda kwa jina la AJM Entatainment ambayo ina husika na maswala ya filamu za kibongo
  Athumani Lali 'Budege'
  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Lali amesema kuwa kwa sasa yupo katika atua za mwisho kwa ajili ya kutoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la Faza Hausi ambayo imeshilikisha wasanii wakongwe ndani yake akiwemo Mohamed Nurdini 'Chekbudi' ,Esha Buheti, Rashidi Mwishehe 'Kingwendu' Muogo Mchungu .

  Filamu hiyo itakayo tolewa na Kampuni hiyo ya jijini Dar es salaam itakuwa moto wa kuotea mbali kwani si ya kukosa kabisa kwa mashabiki wa filamu nchini.

  filamu hiyo ya Faza Hausi itakuwa mtaani wakati wowote kuanzia sasa kwani takribani vitu vyote muhimu vimeshafanyika hivyo wadau wakae mkao wa kula kwani filamu hii si yakuikosa
  Ambapo itapatikana Tanzania nzima nikianzia Dar es salaam na mikoa yote filamu hiyo itawafikia

  0 0

  Tunamtafuta Bibi Husna ambaye asili ya kimalaysia, aliolewa na Mtanzania Baba yake ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa ni Bw. Said Abdullah Belwal.


  Kwa taarifa Husna ni Muuguzi (Nurse) ila haifahamiki hospitali gani na mji gani.

  Mume wake ni Mwanajeshi na ndoa yao ilifungwa kijeshi.  Tafadhali atapopata tangazo hili au yeyote mwenye taarifa zake awasiliane na namba hizi

  Mob: +60102987357

  Tel: +60342517603

  Kuala Lumpur, Malaysia
  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia matembezi ya mshikamano wakati yakiingia uwanjani kabla hajaanza kuhutubia wakazi wa Shinyanga mjini.
   Wakazi wa Shinyanga mjini wakiwa na Furaha ya kuwakaribisha wanachama wapya ambao walikuwa madiwani kwa kupitia Chadema ambao tarehe 25 walijiuzuru na tarehe 26 Februari 2014 kujiunga na CCM.
   Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Masekelo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo na kuwaambia wananchi hao ameamua kurudi CCM kutokana na ufisadi na ukiukwaji ya maadili ya Uongozi ndani ya Chadema.
  Sebastian Peter maarufu kama Obama aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Ingokole akihutubia wananchi kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsaidia kufunga vifungo vya shati Ndugu Sebastian Peter aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ingokole ambaye amerudisha Kadi yake ya Chadema na kupokelewa rasmi CCM kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjni Shinyanga.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wakazi wa Shinyanga mjini na kuwaambia Huu ndio Mwanzo tu,aliwaambia CCM imejengwa kwa misingi imara hivyo itaendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa ushauri Mbunge wa Shinyanga Mjini Ndugu  Stephen Masele juu ya VETA mkoani hapo kutoa kozi zinazoendana na mahitaji ya Soko la Viwanda vya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini tarehe 26 Februari 2014.

  0 0

   Mbunge wa Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Ndugu Stephen Masele akizungumza kwenye mkutano na wakina Mama na Baba Lishe wa Shinyanga mjini ambapo aliwasaidia kufungua SACCOS na kuwaongezea mtaji wa biashara yao.
   Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakishangilia jambo wakati wa hotuba ya Mbunge wao Ndugu Stephen Masele,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.
   Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakishangilia baada ya kuwezeshwa pesa kwenye mitaji ya biashara yao Mbunge wao Ndugu Stephen Masele,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.
  Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakipeana mikono na  Mbunge wao Ndugu Stephen Masele baada ya kuwawezesha kuwa na SACCOSS pia kuwasaidia mtaji wa zaidi ya shilingi milioni nane,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.

  0 0  0 0


  0 0
 • 02/27/14--08:41: FLAVANITE is BACK


 • FLAVANITE is BACK ndani ya MzalenDo pUb, MiLLennium tOwers, JUMAMOSI  hii ni Rasmi na Kila SATURDAY chini ya dj BONILUV, dj MACKAY & dj OSCA wakiburudisha na OLDIES, NAIJA, SOUTH, AFRICAN na Zoote kaLi.
  Thanks in Advance

  0 0


  TANZANIA Horticultural Association (TAHA) and the USAID funded 
  Tanzania Agriculture Productivity Programe (TAPP) have agreed in  
  principal to engage other public and private partners in efforts to 
  up-scale technologies for better access and use by actors within and 
  outside the value chains using various platforms and or mechanisms.

  According to the Executive Director for TAHA, Jacqueline Mkindi, said 
  "I wish to inform you of this exciting initiative expecting to deliver 
  tangible impact to horticultural communities in Tanzania, and also, to
  let you know that, in the process, we shall be directly engaging with 
  government research and training institutions such as Sokoine
  University of Agriculture (SUA), Uyole Research Institution in Mbeya,
  Horticulture Research and Training Institution (HORTI-Tengeru), and
  Kizimbani Research Center in Zanzibar in establishing the PTCs."

  Ms. Mkindi said that the objectives of this initiative are also in
  line with the MAFC-TAHA infrastructure development project aiming at
  establishing farmer service centers in Morogoro, Njombe, Dar es Salaam
  and Coast regions.

  She noted that establishment of Practical Training Centers (PTCs)
  where innovative technologies will be packaged and demonstrated which
  has been identified as one of the most viable vehicles to; provide an
  opportunity to farmers and other stakeholders to practically learn of
  the innovations around production and handling of perishables.

  Others are to create a window for input dealers to showcase their
  quality products, while at the same time allowing farmers chance to
  participate in the selection of best input varieties, and enhancing
  their knowledge and understanding of available technologies for
  improved production and productivity; and Ensure sustainability in
  providing practical technical capacity services to industry
  stakeholders.

  TAHA and the TAPP are prime partners in supporting horticultural value
  chains in Tanzania. The two partners are actively involved in capacity
  building of value chain actors thereby introducing innovative and
  affordable technologies for improved production and productivity along
  with increasing market access of horticulture products from rural
  farmers.

  TAHA is an apex private sector member based organization and has
  participated effectively in transforming the Tanzania horticulture
  since its establishment in year 2004. The association is currently the
  fastest growing farmer organization in the region which catalyzes
  actions and commitment in support of the industry development and
  inclusive growth.

  As a result of TAHA interventions, the horticultural industry has
  attracted enormous support from a number of partners including the
  government of Tanzania and the Development Partners such as USAID,
  BEST-AC, the Royal Netherlands Embassy, ITC, and Finnish Government.
  As a business oriented organization, TAHA offers an industry mouth
  piece, a voicing platforms safeguarding and promoting the interests of
  all the value chain actors in the horticultural industry namely
  producers, exporters, processors, and service providers of flowers,
  fruits, vegetables, spices, herbs and horticultural seeds.

  TAPP is a USAID funded five year programe implemented by Fintrac Inc.
  in conjuction with TAHA. It is designed to increase smallholder
  farmers' incomes through enhanced productivity, crop diversification
  and improved market access.

  0 0

  *       Initiative to generate US$1.2 billion revenue
  *       2 million people will be lifted out of poverty
  *       10,000 small-scale growers will be commercialised

  By Our Reporter
  GROWERS associations have signed a Memorandum of Understanding (MoU)
  to strengthen farmers participation in the design and implementation
  of the Southern Agriculture Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT).

  The associations which have signed the MoU include; Agriculture Council of Tanzania (ACT), Agricultural Non-State Actors Forum (ANSAF), the SAGCOT Centre Ltd,   and Tanzania Horticulture
  Association (TAHA).

  The actors will jointly facilitate the engagement of civil society and
  farmers in SAGCOT initiatives.  Their concerted efforts aim to
  mobilize and monitor inclusive investments in agriculture and improve
  policy reforms that promote and encourage growth in the agriculture
  sector.

  The first phase of implementation of the agreement is funded through a
    grant provided by BEST-AC. The MoU is one of the outcomes of a
  Non-State Actor consultation session, facilitated by UNDP, where
  non-state actors called for a more structured engagement in SAGCOT.

  According to SAGCOT Centre Ltd, CEO Geoffrey Kirenga, this agreement
  symbolizes the partnership approach that is required to ensure that
  investments in the Corridor are inclusive, engage and benefit farmers.

  The MoU is considered a landmark for the farmers lobby by Mrs Janet
  Bitegeko, Executive Director of ACT. "The coalition underpins what we
  have all along advocated for; working in partnership. Through the
  Tanzania Agriculture Partnership program (TAP), ACT has long
  championed the multi-stakeholder partnership approach in agriculture.
  I can assure you that ACT is ready for action."

  Mr. Audax Rukonge, Executive Director of ANSAF stated that the MoU
  aims at providing a platform to the smallholder farmers to raise their
  voices and marks the start of deeper involvement of smallholder
  farming communities in SAGCOT. "We look forward to contribute to the
  promised outcomes from the SAGCOT initiative"

  Ms Jackie Mkindi, the CEO of TAHA, said that the most viable way to
  sustainably address the numerous challenges faced by farmers is
  through transformational partnerships. "This MoU will define our roles
  and responsibilities as partners in catalyzing actions and commitments
  to strengthen farmers' involvement in agriculture value chains as
  business partners."

  SAGCOT which was launched in 2010 is a multi-stakeholder partnership
  that seeks to transform the agriculture sector of Tanzania by building
  inclusive agribusinesses in the country's southern region.

  Its innovative model brings together various partners - including food
  companies, processors, service providers, and farmers' associations -
  to develop viable agricultural value chains and enhance the
  profitability of farmers, especially those which are small-scale.

  SAGCOT's ambitious goals include bringing 350,000 hectares into
  profitable production; transitioning 10,000 small-scale farmers into
  commercial farming; creating 420,000 new employment opportunities;
  lifting 2 million people out of poverty; and generating $1.2 billion
  in annual farming revenue by 2030.

  0 0

  Na Teresia Mhagama


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ameeleza kuwa ujenzi wa eneo la mitambo ya kusafisha gesi asilia katika kijiji cha Madimba mkoani Mtwara utaanza mwezi wa tatu mwaka huu.


  Katibu Mkuu aliyasema hayo mbele ya viongozi wa dini wa mikoa ya Lindi na Mtwara waliofika katika eneo la ujenzi wa mitambo hiyo ili kupata elimu ya shughuli zitakazofanyika katika eneo hilo na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi watakaoishi katika eneo hilo ili kuendesha mitambo ya kusafisha gesi asilia.


  Katibu Mkuu alieleza kuwa ili kuhakikisha ajira zinabaki maeneo ambayo gesi inazalishwa serikali imeamua mitambo ya kusafisha gesi asilia ijengwe katika maeneo hayo.


  Alieleza kuwa mitambo hiyo katika eneo la Madimba itakuwa na uwezo wa kusafisha gesi asilia futi za ujazo milioni 210 kwa siku na itatoka katika eneo la Mnazi Bay, Ntorya na bahari ya kina kirefu.


  Katibu Mkuu alieleza kuwa kukamilika kwa mitambo hiyo kutaiwezesha serikali kuzalisha umeme wa uhakika na hivyo kuondokana na gharama kubwa zinazotokana na ununuaji wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme ambayo inaigharimu serikali kiasi cha shilingi trilioni 1.6 kwa mwaka.


  Naye mtaalamu wa masuala ya gesi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Sultan Pwaga aliwaleza viongozi hao wa dini kuwa mitambo mingine yenye uwezo wa kusafisha gesi asilia kiasi cha futi za ujazo milioni 140 kwa siku itajengwa katika kijiji cha Songosongo mkoa wa Lindi na itasafisha gesi asilia itakayozalishwa katika eneo la Songosongo, Kiliwani na maeneo ya jirani.


  Mtaalamu huyo kutoka TPDC alieleza kuwa usimikaji wa mitambo ya kusafisha gesi katika eneo hilo unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu na majaribio ya mitambo  hiyo yataanza mwezi Januari mwaka 2015.


  Bw. Sultan Pwaga, aliwaeleza viongozi hao kuwa katika eneo hilo kutajengwa mitambo ya kusafishia maji ambapo kijiji cha Madimba kitapatiwa maji safi kiasi cha lita 60,000 kwa siku. Kuhusu ajira, Bw. Pwaga alieleza kuwa ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi katika eneo hilo umetoa ajira kwa watanzania wapatao 351 na raia wa kigeni wasiozidi 35.

  Kongamano la viongozi wa dini wa mikoa ya Lindi na Mtwara limefanyika tarehe 25 na 26 mkoani Mtwara na ambapo Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake za Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) zilishiriki ili kutoa elimu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu sekta za Nishati na Madini.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipowasili kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. Nyuma yake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandara na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe saidi Meck Sadick.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waombolezaji wengine kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji familia ya marehemu kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. Kwa Picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 232 | 233 | (Page 234) | 235 | 236 | .... | 1896 | newer