More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 4641 to 4660 of 37959)
- 02/25/14--04:16: _TAARIFA KWA UMMA: ...
- 02/25/14--14:00: _Serikali yatangaza ...
- 02/25/14--07:45: _UFUNGUZI WA MAADHIM...
- 02/25/14--12:25: _MWANAFUNZI CHUO CHA...
- 02/25/14--12:26: _TASWIRA ZA LAKE GAS...
- 02/25/14--12:27: _MTEMVU AKABIDHI MIK...
- 02/25/14--12:30: _MWILI WA BALOZI KAZ...
- 02/25/14--12:44: _MAONESHO YA 53 YA K...
- 02/25/14--22:26: _Okoa gharama na mud...
- 02/26/14--01:02: _MSAADA TUTANI: Nina...
- 02/26/14--01:04: _Serikali yaahidi us...
- 02/26/14--01:30: _ MAJINA YA WAANDISH...
- 02/26/14--02:22: _semina ya mkakati w...
- 02/26/14--02:30: _Article 5
- 02/26/14--05:01: _Article 4
- 02/26/14--05:23: _MKUTANO MKUU WA TAT...
- 02/26/14--05:25: _Kipindi cha familia...
- 02/26/14--05:29: _UZINDUZI RASMI WA K...
- 02/26/14--07:00: _Last respect and fu...
- 02/25/14--13:05: _President Kikwete L...
(showing articles 4641 to 4660 of 37959)
Channel Description:
Karibuni Jamvini Wanajamii
0 |
|
0 |
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
TAARIFA KWA UMMA
RATIBA YA UZIMAJI WA MITAMBO YA UTANGAZAJI YA ANALOJIA AWAMU YA PILI
Ndugu wananchi, napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kuwa Awamu ya Pili ya Uzimaji wa Mitambo ya Utangazaji ya Analojia itaanza rasmi mwezi Machi mwaka huu. Awamu hii ya Uzimaji inaanza baada ya Serikali kujiridhisha na matokeo ya tathmini ya uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya analojia awamu ya kwanza kwenye miji saba ya Dar e salaam, Tanga, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Moshi na Arusha. Tathmini hiyo imeonyesha kuwa asilimia 89% ya watanzania kwenye miji hiyo wamehamia kwenye mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali.
Ninaamini kuwa asilimia kumi na moja ya watanzania waliobaki kwenye miji hiyo watakuwa wameingia katika mfumo wa dijitali hadi hivi sasa.
Ndugu wananchi, Awamu ya Pili ya Uzimaji wa Mitambo ya Utangazaji ya Analojia itaanza mwezi Machi mwaka huu katika miji tisa na kukamilika mwezi Oktoba 2014. Miji hiyo ni Singida, Tabora, Musoma, Bukoba, Kigoma, Morogoro, Kahama, Iringa na Songea.
Natoa wito kwa wadau na wananchi wote kushirikiana na Serikali katika kutekeleza vema zoezi hili la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya analojia kwa manufaa ya Taifa letu na wananchi wote kwa ujumla.
Asanteni sana.
Imetolewa na:
Prof. Makame M. Mbarawa (MB.)
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
DAR ES SALAAM
21/02/2014
0 |
|
0 |
|
Serikali inapenda kuwaarifu waombaji wa nafasi za kazi kwa tangazo la tarehe 27 Novemba, 2013 wa kada za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Udereva kuwa usaili utaanza tarehe 4 Machi, 2014 takriban katika mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema hayo leo ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya wadau waliomtembelea kwa lengo la kufahamu masuala mbalimbali ya uendeshaji wa mchakato wa ajira serikalini.
Amesema usaili huo unaoanza tarehe 4 Machi katika mikoa takribani yote nchini utahusisha jumla ya wasailiwa 6,087 wa fani za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na udereva kwa kada ambazo sio za Maofisa. Amefafanua kuwa vigezo vya kupanga mikoa ya usaili vimetokana na anwani ambazo waombaji waliwasilisha katika barua zao za maombi husika ya kazi.
Daudi alibainisha kuwa kila mwombaji aliyekidhi vigezo na kuchaguliwa kwa ajili ya usaili anapaswa kwenda kufanyia usaili katika mkoa aliopangiwa kama anwani yake inavyoonyesha katika tangazo kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira, isipokuwa kwa waombaji wa mkoa wa Katavi wao wataenda kufanyia usaili mkoa wa Rukwa na waombaji waliotumia anwani za mkoa wa Singida wao watafanyia usaili mkoa wa Manyara kutokana na sababu zisizozuilika.
Aliongeza kuwa kwa mwombaji ambae hatazingatia anwani, siku na muda aliopangiwa na kuamua kwenda mkoa mwingine tofauti na utaratibu uliopangwa ajue wazi hatasailiwa kwa kuwa ratiba na idadi ya majopo ilishapangwa kwa kila mkoa na haitabadilishwa ili kuweza kurahisisha kazi hiyo kukamilika kwa ufanisi.
Aidha, amewataka waombaji wote wa tangazo hilo kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni http://www.ajira.go.tz/ wao wenyewe ili kuweza kujua kiundani endapo wamechaguliwa kufanya usaili, kufahamu tarehe, mahali na muda wa kuanza usaili ili kuepuka usumbufu usiokuwa na lazima.
Daudi aliendelea kufafanua kuwa kwa waombaji waliotumia anuani za mkoa wa Dar es Salaam kwa nafasi ambazo sio za maofisa usaili utafanyika tarehe 11 Machi, 2014.
Aidha, kwa nafasi za Maofisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wote usaili wao utafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 10 hadi 14 Machi, 2014.
Katibu amewataka waombaji wote kuhakikisha pindi wanapoenda kwenye usaili wawe wamejiandaa vya kutosha ikiwemo kubeba nyaraka muhimu hususani vyeti halisi vya taaluma zao maana vitahitajika kwa ajili ya uhakiki siku ya usaili. Aidha, amewasihi waombaji wa matangazo mengine ya nafasi za kazi kuwa na subira wakati uchambuzi ukiendelea na pindi utakapokamilika wahusika watataarifiwa.
Alimaliza kwa kuwasisitiza wadau wa Sekretarieti ya Ajira kuwa pindi wanapoona matangazo ya kazi, ikiwemo kuitwa kwenye usaili au kupangiwa vituo vya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari hususani baadhi ya mitandao ya kijamii wajiridhishe kwanza kwa kuangalia taarifa hizo katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira, ili kuepuka taarifa zisizokuwa za kweli ambazo zimekuwa zikitolewa nyakati nyingine na baadhi ya watu wasio waaminifu kwa lengo la kupotosha Umma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 21 Machi, 2014
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
0 |
|
0 |
|
-Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi M.K Tarishi akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu, kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Ruvuma Bw. Severin Tossi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi M.K Tarishi akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Kumbukizi ya Vita ya Majimaji katika ukumbi wa Songea Club,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw Joseph.J. Mkirikiti na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Severin Tossi.
Philip Maligisu, Mhifadhi Kiongozi Makumbusho ya Majimaji akitoa maelezo kwa wajumbe katika eneo ambalo lilikuwepo kanisa katoliki la kwanza nchini.
========== ======== ========
HOTUBA YA KATIBU MKUU, WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, BI. TARISHI M.K WAKATI WA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA UTALII WA UTAMADUNI NA KUMBUKIZI YA VITA YA MAJIMAJI TAREHE 25 FEBRUARI 2014, UKUMBI WA MALIASILI, MJINI SONGEA-RUVUMA
========== ======== ========
Awali ya yote, nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuifikia siku ya leo. Ninayo furaha kubwa kupewa heshima ya kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho haya muhimu kwa historia ya nchi yetu. Nimefurahi kwa sababu hii imekuwa ni fursa kubwa na ya pekee kwangu kukutana na kufahamiana na wadau wa urithi wa utamaduni kutoka Kanda ya Kusini hususan mkoa wa Ruvuma. Kupitia fursa hii, nitapata nafasi ya kubadilishana uzoefu nanyi wadau wetu muhimu mnaotusaidia katika jukumu la kuhifadhi, kulinda, kuendeleza rasilimali za urithi wa utamaduni na utalii katika ukanda huu wa Kusini.
Ndugu wageni waalikwa na wadau wetu,
Nimefurahishwa pia na utaratibu huu wa wadau kukutana na kujadili namna ya kuendeleza utalii wa utamaduni na kuenzi mchango wa Mashujaa wetu wa Vita ya Majimaji. Utaratibu huu ni mzuri kwa sababu unatekeleza Sera na Sheria zetu ambazo zinaelekeza ushirikishwaji wa wadau katika kuhifadhi na kuendeleza kumbukumbu za kihistoria na kutunza maeneo ya urithi wa utamaduni. Aidha, napenda kuwakumbusha kuwa sote kwa ujumla wetu tunawajibika kuuenzi kwa kutambua na kutumia kiundelevu urithi wa utamaduni uliopo katika maeneo yetu. Kila mdau anayo nafasi katika kuendeleza na kuimarisha rasilimali hizi kwa manufaa ya Taifa letu.
Ndugu wadau wenzangu,
Nimefahamishwa kuwa katika maadhimisho haya tutapata fursa ya kutembelea baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo katika Mkoa wa Ruvuma. Aidha, nimefahamishwa kuwa baada ya kutembelea vivutio hivyo, kutakuwa na warsha ya wadau ambapo jumla ya mada nne zinazolenga katika matumizi endelevu ya urithi wa utamaduni na uendelezaji wa utalii katika Ukanda huu zitawasilishwa na kujadiliwa. Nimefahamishwa pia kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuwawezesha mfanye ulinganifu baina ya hali mtakayokuwa mmeiona wakati mkitembelea vivutio vya utalii na mada zitakazowasilishwa ili muweze kutushauri kulingana na hali halisi ya vivutio husika.
Ndugu Wadau,
Napenda niwakumbushe kuwa wakati mtakapokuwa mnatembelea vivutio vya utalii na kujadili mada zitazowasilishwa, zingatieni kuwa lengo kuu la Serikali ni kushirikisha wadau wote katika kutunza, kuhifadhi, kuendeleza urithi wa utamaduni na utalii ili kuchangia katika kujenga uchumi imara, endelevu na unaolenga katika kuboresha maisha ya Watanzania wote.
Wadau mnayo nafasi kubwa ya kuchangia katika majadiliano haya kwani mawazo na michango yenu ndio itasaidia kufikia lengo linalokusudiwa. Ninaamini kuwa kupitia uzoefu wenu, mtaweza kutushauri sisi watendaji tunaohusika na usimamizi wa shughuli za kuendeleza urithi wa utamaduni na utalii. Nami nawaahidi kuwa Ofisi yangu itashirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Ruvuma kushughulikia ushauri wote mtakautoa.
Ndugu wadau,
Naomba nichukue fursa hii kumkaribisha rasmi Profesa Audax Z.P Mabulla, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika Wizara ya Maliasili na Utalii na kumwaahidi kuwa Wizara iko tayari kumwezesha ili aweze kutekeleza majukumu ya utunzaji wa urithi wa utamaduni na kuwawezesha Watanzania kufurahia na kuuenzi urithi wetu ikiwa ni pamoja na kuendeleza kusimamia na kuratibu hili tamasha la Utalii wa Utamaduni na Kumbukizi ya Vita ya Majimaji.
Ndugu wadau,
Mwisho nimalizie kwa kuwashukuru tena nyote kwa kukubali kushiriki katika maadhimisho haya. Baada ya kusema hayo machache, ninawatakie maadhimisho mema na kutamka kwamba maadhimisho ya Utalii wa Utamaduni na Kumbukizi ya Vita ya Majimaji kwa mwaka 2014 yamefunguliwa rasmi.
0 |
|
0 |
|
Meneja Masoko wa Be forward Tanzania,Bwa Kohei Shibata (kulia) na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Isaac Mbinile wakimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa gari aina ya Noah Marco Hingi (katikati) ambaye ni mwanafunzi wa kutoka hosipitali ya bungando, jijini mwanza.
Meneja Mkuu wa kampuni ya uagizaji na usambazaji magari ya Be forward Tanzania Issac Mbinile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi gari aina ya noah mshindi (kulia). hafla hiyo ilifanyika leo makao makuu ya kampuni hiyo katika bustani za Palm Resdency , mkabala na hospitali ya saratani 'ocean road' jijini dar es salaam.
Meneja Masoko wa kampuni ya Be Forward,Kohein Shibataa akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar baada ya kutoa gari aina ya Noah kwa mshindi.
Kampuni ya uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka JAPAN ya BEFORWARD imeendesha shindano la kuwapata washindi 25 duniani kote waliojielezea jinsi wanavyoweza kuitumia kampuni hiyo katika shughuli za maendeleo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook ambapo mtanzania MARCO HINGI ameibuka mshindi na kujishindia gari.
Akizungumza jijini DSM Afisa masoko wa kampuni hiyo KOHEI SHIBATA amesema shindano hilo liliendeshwa wakati wa sikukuu ya CHRISMASS ambapo wateja waliotembelea ukurasa wa facebook wa befoward walipata nafasi ya kuulizwa maswali na kujibu mambo kadha wa kadha
Kati ya washindi hao Tanzania imepata nafasi mbili ambapo mwanafunzi wa chuo cha afya cha BUGANDO MWANZA bwana MARCO HINGI ameibuka mshindi
Makabidhiano ya zawadi ya gari aina ya NOAH yenye thamani ya shilingi milioni 11.8 yamefanyika leo jijini DSM kati ya Afisa masoko wa kampuni hiyo KOHEI SHIBATA na Mshindi MARCO HINGI ambapo SHIBATA amesema hiyo ni moja ya mikakati yao ya kuongeza mauzo kwa kuwafanya wateja kuwa na imani nao kama anavyoeleza meneja mkuu ISAAC MBINILE
Kwa upande wake MARCO HINGI ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha afya BUGANDO mwanza amesema aliwaomba BEFORWARD kumpatia gari la kubebea wagonjwa kutokana na mradi wake alioubuni wa kusaidia mama wajawazito vijijini.
Aidha HINGI ameongeza kuwa baada ya kujibu swali la BEFORWARD walijitokeza watu wengi waliolipenda wazo lake kwa kuandika ‘like’ na hatimaye kuibuka mshindi.HINGI amesema atalitumia gari hilo kubebeea wagonjwa katika mradi huo waliouanzisha mkoani MWANZA
0 |
|
0 |
|
Dj akiwa makini kuhakikisha watu wanaburudika na miziki
mizuri ya Kihindi wakati wa Tamasha la LAKE GAS INDIAN FOOD
Mandhari ya eneo la tukio
Palipendeza
Mama na mwanae akionekana ni mwenye furaha
Mstahiki Meya wa Kinondoni Mhe Yusuf Mwenda
akipokea zawadi ya unga kutoka kwa mwakilishi wa banda la Azam
Mstahiki Meya wa Kinondoni Mh.Yusufu Mwenda(kushoto)
akifatiwa na balozi wa India Mhe. Debnath Shaw na familia zao.
0 |
|
0 |
|
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimkabidhi ufunguo wa gari aina ya Noah katibu Mkuu wa Saccos ya Tujikwamue ya Chang'ombe, Dar es Salaam, Itika Mwankenja katika hafla ya Taasisi ya PFT ya kukabidhi mikopo ya magari, bajaji, pikipiki na fedha kwa vicoba mbalimbali, Temeke, Dar es Salaam juzi. Mtemvu ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Itika akiangalia wakati Mtemvu akiliwasha gari hilo.
Mtemvu akikabidhi mkopo wa bajaji kwa moja ya wana vicoba
Mwenyekiti wa Mpakani B Vicoba, Mwaimuna Ali akikabidhiwa funguo wa bajaji kwa niaba ya wenzie
Ni furaha iliyoje kwa kikundi hicho kupata mkopo wa bajaji
Moja ya Vicdoba ikipatiwa mkopo wa pikipiki
Viongozi wa VICOBA ya VAMAU wakipatiwa funguo za pikipiki baada ya kukopeshwa na PFT
Waombolezaji wakisukuma jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), marehemu Balozi Fulgence Kazaura ulipowasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni hii , kutoka India. (PICHA NA KHAMIS MUSSA)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick akwafariji ndugu wa marehemu
Ndugu wakifunua jeneza kuutengeneza mwili wa marehemu Kazaura.
Mwili ukipakiwa kwenye gari tayari kupelekwa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Kairuki, Mikocheni
Ujumbe wa Tanzania katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya Bangkok katika picha ya pamoja na Rais Rais wa Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak (aliyeshika kinyago cha mamba kilichochongwa kutokana na mawe ya madini yanayopatikana nchini Tanzania. Kinyago hicho kimechongwa na Kituo cha 'Tanzania Geomological Center' kilichopo Arusha.) Wa tatu kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la madini na usonara la Thailand Bw. Peter Brooke.
Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Thailand Mhe. Ruby Marks (katikati) katika picha ya pamoja na wafanyabiashara ya madini( wa kwanza kushoto, Bw. Sam Mollel mwakilishi kutoka Tanzania Geomological Center (wa tatu kulia) Bw. Musa Shanyangi Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Kamati ya Vito ya Shirikisho la Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Bw. Gregory Kibusi.(nne kulia).
Kamishna Msaidizi wa Madini ,Wizara ya Nishati na Madini , Mhandisi Hamis Komba akiongea jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Thailand Mhe. Srirat Rastapana mara baada ya kufungua maonesho ya 53 ya “Bangkok Gems & Jewelry Fair” mapema leo. Nyuma ya Kamishna ni Bw. Edward Rweymamu ni Mthamini wa Madini ya Almas Wizara ya Nishati na Madini. Kushoto Mhe. Dora Mushi mfanyabiashara wa madini kutoka Arusha.
Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak akiangalia madini ya Almas katika banda la Tanzania. Anamwelekeza jambo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vito ya Shirikisho la Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Bw. Gregory Kibusi. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya ujumbe wa Tanzania unaoshiriki maonesho hayo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sam Mollel wa pili kulia akionesha Hati ya Maridhiano ya kuendeleza ushirikiano wa tasnia ya madini ya vito na usonara baada ya kusaini kati yake na Rais wa Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak. Wanaoshuhudia ni Kamishna msaidizi wa Madini, Mhandisi Hamis Komba (Wa kwanza kulia) na Makamu wa Rais wa Shirikisho la madini na usonara la Thailand Bw. Peter Brooke.
Wakati Watanzania, katika miaka ya karibuni wamekuwa wakijitahidi kuboresha maisha yao hususan katika suala zima la ujenzi wa nyumba zilizo bora na za kisasa, upande wa pili wa harakati hizi umekuwa ni wa changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi katika kuzifikia ndoto zao hizo, hasa kwa upande wa gharama za vifaa vya kufanikisha ujenzi huo, lakini pale ambapo wameweza kujitahidi kuweza kufikia gharama hizo,
Katikati ya sintofahamu hii, kumekuwa na Watanzania ambao wamekuwa wakijitahidi kuwaza ni namna gani wataweza kuwasaidia wananchi wenzao katika kukabiliana na changamoto hizo, ambapo miongoni mwao ni wamiliki wa kampuni ya Mega Woodcraft Products (T) Ltd, kampuni ambayo imelenga kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya ujenzi nchini kwa kutambulisha mfumo wa kisasa wa ujenzi wa
Kifupi, Mega Panel, ni Mega Panel ni polystyrene (EPS) iliyoimarishwa kwa wavu wa chuma cha pua uliopakwa zinc na kuunganishwa kwa nguvu ya umeme ili kuwa kiini cha mkingiko wa waya zilizopenyeza kwenye polystyrene ambapo polystyrene iliyochomekwa katikati ya wavu wa chuma cha pua huzuia moto na umeme na ingawa panel hii ni nyepesi ina sifa ya kuifanya iwe kifaa cha ujenzi imara na kinachodumu.
Inaweza kufungwa na kujengwa haraka na ni imara kuliko matofali au matofali yenye uwazi.Mfumo huu wa ujenzi ilianza Marekani, licha ya kuwa kitu kigeni nchini, lakini umeshatumika katika nchi kadhaa na kuonyesha mafanikio makubwa nchi kama Japan, China ,Korea, Afrika Kusini, Msumbiju, Botswana na ata majirani zetu Kenya wanatumia mfumo huu wa ujenzi ,
Manufaa ya ujezi huu ni ujenzi mwepesi na rahisi, hutumia asilimia hamsini (50%) tu ya ujenzi ukilinganisha na ujenzi wamatofali, hupunguza asilimia thelathini (30%) ya saruji , hupunguza gharama za usafirishaji na unajenzi (installation cost), haitaji msingi mkubwa kwa sababu Mega Panels ni nyepesi sana ukilinganisha na matofali hivyo ni rahisi kuongezea gorofa (Vertical extension), kutoka kwenye nyumba ya chini ni rahisi kujengea maumbo maalum (design configuration), imara sana kutonana na wavu wa chuma cha pua (wire mesh reinforcement), hupunguza joto kwa asilimia ishirini(20%) kutokana na polystyrene, pamoja na mambo yote hayo mfumo huu ni rafiki wa ikolojia.
Ili kujua zaidi kuhusu mfumo huu, wasiliana na Mega Panels kupitia tovuti yao www.mega.co.tz , ikiwa ni pamoja na mbinu za ujenzi wake nk. na ikiwa bado una maswali zaidi, unaweza kuwatembelea Mega Woodcraft Products (T) Ltd ofisini kwao, mtaa wa Bungoni, kiwanja namba 508, au kwa barua pepe jonathan@mega.co.tz
Habari za leo ndugu, ninakuomba unisaidie kuweka waraka wangu kwenye blogu yako, ili watu wenye uwezo wa kunisaidia hata kwa ushauri tu, waweze kunisaidia kwani nipo katika wakati mgumu sana sasa hivi Natanguliza shukurani zangu za dhati kwako.
Kwa ufupi mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 26 . Ninaishi Dar Es salaam na kazi yangu ni mfanyabishara. Baada ya maisha kunipiga sana, niliamua kwenda kuomba ushauri kwa mdada mmoja jirani yetu ambaye yeye mambo yake yalikuwa yamemnyookea sana.
Dada huyo aliniunganisha na mmama mmoja ambaye alikuwa anaishi Masaki, mama huyo akanipeleka kwenye klabu ya wanawake wasagaji ambao ni matajiri ambako niliingizwa kwenye utaratibu wa ibada (matambiko ) yao. Hekalu la wanawake hawa matajiri lipo katika wilaya ya Kinondoni.
Waganga wakuu wa hekalu hilo wapo watatu, kuna wanaume wawili ambao ni vijana vijana tu na mwanamke mdada mmoja ambaye yupo kwenye umri wa kama miaka arobaini hivi na ushee.
Watu hawa watatu ni wachawi wenye nguvu za ajabu sana na pindi unapojiunga na klabu hii, unakula kiapo cha kutii na kufuata masharti yao katika siku zote za maisha yao. Wanao kiuka masharti yao huwa wanapata matatizo makubwa sana.
Katika hekalu hilo, zinafanyika ibada za uchi za kila mwisho wa wiki na huwa zinahusisha mamia ya wanawake. Niliingia katika klabu hii tangu mwaka jana (2013) mwanzoni, kweli nilipoingia nilitajirika sana baada ya muda mfupi tu. Kila kitu nilichokitaka katika maisha yangu nilikipata.
Hata hivyo pamoja na kupata mali na utajiri kupitia klabu hii, mimi ninataka kujitoa ingawa nashindwa kwa sababu naogopa kupata adhabu ya kuvunja kiapo cha watu hawa.
Ninataka kujitoa kwa sababu, kwanza sina amani moyoni mwangu. Nafsi yangu inanisuta sana kupata mali ambazo zinatokana na kujiunga na klabu ambayo memba wake wanamuabudu shetani, vilevile ninajiona mkosaji sana kwa ninacho kifanya kwa sababu ni kama nimekuwa muabudu shetani.
Tatizo linalo nikabili ni kwamba, ninataka kujitoa lakini ninashindwa kwa sababu ninaogopa kupata adhabu ya kukiuka masharti ya klabu( dini ) hii ambayo kwa kweli ni magumu sana kwangu.
Ni tamaa tu ndio iliyo niponza, naomba mnisaidie ndugu zangu japo hata kwa kunipa ushauri. Vilevile ninawasihi akina dada wa hapa Dar Es salaam, ambao nawaona kwa wingi sana wanaingia katika klabu hii.
Kuweni makini sana wadada wenzangu, hakuna hela wala mali za bure, kila kitu kina gharama yake, utakapo fika wakati wenu wakulipa gharama zake, mtakielewa ninacho kizungumzia hapa.
Nipeni ushauri kupitia barua pepe yangu ambayo ni : tunukondo@gmail.com
Mwenyekiti wa maandalizi ya Kongamano la Viongozi wa Dini mikoa ya Lindi na Mtwara MohamedSenani akiwakaribisha wajumbe katika kongamano la viongozi hao katika ukumbi wa VETA mjini Mtwara. Kongamano ambalo viongozi hao walijadiliana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizungumza na viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa kongamano la viongozi hao lililohusu rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madinikwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Baadhi ya wajumbe wa kongamano la viongozi wa dini wakiwasili eneo la Mnazi Bay kujionea shughuli za namna visima vya gesi vinavyofanya kazi na kuzalisha gesi ambayo ni moja ya chanzo cha nishati ya umeme kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu.
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
0 |
|
0 |
|
0 |
|
0 |
|
wadau wa Taasisi mbalimbali wakisikiliza na kutoa maoni ya Rasimu ya kwanza ya mkakati wa Mawasiliano ya Mazingira Endelevu wa Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania. . katika Ukumbi wa NIMRI
Mkurugenzi Msaidi wa Ofis ya Makamu wa Raisi Idara ya Mazingira Bi Magdalena J.Mtenga (wa kwanza kushoto) akifunguwa rasmi Semina ya Rasimu ya kwanza ya Mkakati wa Mawasiliano ya Mazingira Endelevu wa ukuaji wa u chumi na kupunguza Umaskini Tanzania. na kulia ni Alhaji.Selemani Kisimbo ni Kaimu Mkurungezi wa Idara ya Mazingira na wadau wa Taasisi mbalimbali.
Mkurugenzi Msaidi wa Ofis ya Makamu wa Raisi Idara ya Mazingira Bi Magdalena J.Mtenga akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Taasisi mbalimbali katika Semina ya kutoa maoni ya Rasimu ya kwanza ya Mkakati wa Mawasiliano ya Mazingira Endelevu wa Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania .katika Ukumbi wa NIMRI.PICHA OFIS YA MAKAMU WA RAIS
Entries to the 2014 African Blogger Awards (http://www.africanbloggerawards.com), the continent’s very first awards programme that measures online and social influencers’ reach and influence through data analysis, are open to bloggers, Instagrammers, Tweeters and YouTubers across Africa.
Infographic “The African Digital Frontier”:http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/photos/140226.png
The Awards have been divided into 36 categories, providing the opportunity for influencers on these platforms to be measured objectively against their peers, and duly recognised for their achievements.
Categories are diverse, and include sectors such as Advice, Fashion and Beauty, Events and Nightlife, Education, Sports, Political, Technology and Gadgets, and Youth Culture among others. “The African Blogger Awards are the first completely impartial, objective awards for online and social influencers on the African continent because winners will be determined by data analytics provided by Webfluential, and not through peer nominations,” says Mike Sharman, co-founder of the African Blogger Awards.
The Awards will also give brands and the marketing industry, including advertisers, public relations agencies and media buyers in each country, an impartial measurement of the most relevant online and social influencers to include in their campaigns, making sure that they achieve the greatest possible impact for their marketing spend.
There is no cost to enter, but entrants are required to register their blog, Twitter, Instagram or YouTube profile (or a combination thereof) on Webfluential (http://www.webfluenti.al), a platform designed to quantify the reach, resonance and relevance of bloggers, Instagrammers, Tweeters and YouTubers with over 1000 active, legitimate followers. Evaluation of the entrants will be managed primarily through Webfluential (https://webfluenti.al)
Reach measures the size of an influencer’s audience (following) per social media network.
Resonance is a measure of how widely the content that an influencer shares reaches outside of their own community.
Relevance is a measure of the response from the influencer’s community in the form of likes, comments, retweets. Bloggers, Instagrammers, Tweeters and YouTubers who are permanent residents of any African country are eligible to enter the African Blogger Awards.
Entries for the awards close on 9 March 2014 at midnight GMT+2, and results will be announced on 16 April 2014 via the competition’s Twitter profile, @African_Blogger, from 11h00 GMT+2. Overall awards for Africa’s Top Blogger, Top Instagrammer, Top Tweeter and Top YouTuber will be announced on 18 April 2014 at a celebration hosted in Johannesburg, South Africa.
Winners in each category will receive a web banner announcing their achievement that can be personally-leveraged through their social network and a commemorative trophy.
“As the competition grows, we plan to host the awards ceremony in other cities on the African continent each year, in recognition of the enormous influence that the online community has on news, lifestyle, media and marketing across the continent,” says Murray Legg, co-founder of the African Blogger Awards.
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinti, akizindua huduma mpya ya PSPF Pamoja nawe na PSPF call centre, itolewayo na mfuko wa Pensheni wa PSPF, baada ya kufungua Mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo Feb 26.2014.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (kushoto), akimkaribisha mjumbe wa bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambaye pia ni katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimatifa, John Haule alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimtaifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, kuhudhuria mkutano mkuu wa tatu wa Mfuko wa PSPF wa wadau Februari 26.2014.
Wakurugenzi wa idara mbalimbali za mfuko wa Pensheni wa PSPF, mstariu wa mbele, wakiwa miongoni mwa wajumbe wanaohudhuria mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Februari 26, 2014
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akishuka kwenye gari lake, huku naibu waziri wa fedha, Adam Malima (kushoto), akiwa tayari kumpokea kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo, kufungua Mkutano Mkuu wa Tatu wa Wadau wa mfuko wa pesnheni wa PSPF.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo.
Photo credits: moneymanagement.org
Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Katika kipindi hiki, tumeingia katika sehemu ya pili ya mjadala kuhusu BAJETI KATIKA FAMILIA ambapo mbali na historia ya bajeti, pia tumesisitizwa kuhusu umuhimu wake, namna ya kulitekeleza na mengine mengi.
Wachangiaji studio walikuwa ni Amos Cherehani ambaye ni mtaalamu wa masuala ya fedha, Denzel Musumba na Mubelwa Bandio
KARIBU UUNGANE NASI
0 |
|
0 |
|
Jaji Mkuu Mstaafu Mh. Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi wa uzinduzi wa Rasimu ya pili ya Katiba
Mkurugenzi Mtendaji wa Haki za Binadamu Bi. Helen Simba akieleza kuhusika kwa haki za Binadamu katika Rasimu ya Pili katiba kwa wananchi.
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akitoa hotuba kabla ya uzinduzi Rasmi wa kampeni ya Taifa ya kusambaza uelewa wa Rasimu ya Pili ya Katiba kwa Wananchi
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua Rasmi Kijitabu kidogo kilicho andikwa Rasimu ya Pili ya Katiba Inasemaje? Chapisho la Lugha nyepesi
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua rasmi vipeperushi vilivyo andikwa , Mambo Saba makubwa ya kuungwa mkono na wananchi katika Rasimu ya Katiba pamoja na mambo makubwa matano yanayokosekana katika Rasimu ya Katiba na Kipeperushi cha pili kinacho sema 'Taifa ni letu na Katiba ni yetu Husika tupate Katiba Bora.
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akigawa vipeperushi hivyo kwa ishara ya uzinduzi rasmi.
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua Rasmi Jarida la Rasimu ya Pili ya Katiba
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua Flash Disk maalum zenye Rasimu ya Katiba ambazo zitagawiwa kwa waendesha Bodaboda ili abiria akipanda nae apate kusikiliza Rasimu hiyo.
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua Rasmi, DVD, VCD pamoja na AUDIO CD kwa ajili ya walemavu.
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua Rasmi Tovuti 'Blog' inayo itwa Taifa ni letu www.taifaniletu.blogspot.com ambayo ni maalumu kwa ajili ya Rasimu ya Pili ya Katiba.
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akitoa pongezi kwa jinsi mchakato unavyokwenda ikiwa ni pamoja na kutumia Teknolojia ya hali ya juu ili kila mtu afikiwe na Rasimu ya Pili ya Katiba
Kundi la watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wakiwa wamefika katika uzinduzi wa kampeni ya taifa ya kusambaza uelewa wa Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wananchi wote
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani wakiwa katika uzinduzi wa kampeni ya taifa ya kusambaza uelewa wa Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wananchi wote,ambapo pia kulikuwa na shule zengine Kama Azania ,Mazimbwi na Chamazi.
Kwaya kutoka Haki za Binadamu wakitumbuiza kwa moja ya nyimbo zao
Sehemu ya watu waliohudhuria katika Uzinduzi huo.
Picha na Dar es salaam Yetu Blog
0 |
|
0 |
|
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete(Centre seated) in a group picture with senior government officials and members of the Private sector organizations shortly after he launched Improving Business Environment Lab at Kunduchi Beach Hotel in Dar es Salaam this evening. Others in the picture seated from left is the Vice President Dr.Mohamed Gharib Bilal, The CEO of the Presidential Delivery Bureau Mr.Omar Issa(second left), Malaysian Cabinet Minister and Expert in Development Affairs Prof. Idris Jala(Fourth left) and extreme right is the Chairman of Tanzania Private Sector Foundation Dr. Reginald Mengi. Photo by Freddy Maro.