Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

MKOSAJI MKUU WA HAKI ZA BINADAMU NI SERIKALI - JAJI MSTAAFU MIHAYO

$
0
0
DSC_0259
Mjumbe wa Bodi ya Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini (Tanzania Human Rights Defenders Coalition) Dkt. Hellen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha watetezi wa Haki za Binadamu nchini na Jeshi la Polisi jijini Dar leo.
.Asema dunia nzima inajua mvunjifu wa kwanza wa haki za binadamu ni dola
.Polisi pia ni binadamu wanahitaji kutetewa na mitandao ya haki za binadamu nchini

Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
MKOSAJI na mvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ni serikali kutokana na mazingira halisi ya utendaji na mfumo mzima wa utawala katika serikali nyingi duniani. Imeelezwa.

Akizungumza kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) kwa wakuu na makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo amesema kwa mfumo wa utawala katika nchi nyingi duniani mkosaji mkuu wa haki za binadamu ni serikali.

“dunia nzima inajua kwamba serikali ndio mkosaji mkuu wa haki za binadamu na maana halisi ya serikali ni dola na mahakama tu kwisha,” amesema Jaji Mihayo
Jaji Mihayo amesema kuwa kwa hali ya kawaida dola ikimkamata mtu au mhalifu lazima mpeleke katika mahakama ili sheria ichukue mkondo wake wa kawaida.
DSC_0316
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Abdurahman Kaniki, akitoa hotuba yake ya ufunguzi kwa niaba ya IGP Ernest Mangu, kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Dkt Helen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi amesema warsha hiyo inatoa fursa nzuri kwa watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi kuboresha kazi zao za utetezi wa haki za binadamu nchini. Amesema kwa ujumla haki za binadamu hazipewi bali ni haki ya msingi ambayo mtu anazaliwa nayo ili zinaminywa aidha kupitia mtu kwa mtu au taasisi au mfumo wa utawala.

“Kazi za watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi zinaendama na msingi ni utetezi wa haki za binadamu pamoja na mali zao,” alisisitiza
Naye, Mratibu wa kitaifa wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake ya (The Concept of Protection and Security Management for Human Rights Defenders and Social Organization) amesema kuwa taaluma inaweza kutumika kutetea haki za binadamu katika maeneo mengi hapa duniani.
DSC_0334DSC_0379
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, umuhimu wa kushirikiana kati ya Jeshi hilo na Asasi za kutetea Haki za Binadamu ili kuleta tija katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Amesema pia kupitia mada hiyo kwamba jamii inadhani kwamba anayepaswa kutetewa ni mwananchi tu lakini pia hata polisi naye ni binadamu anapaswa kuwa na mtetezi pale ambapo haki yake ya msingi inapovunjwa.

“Mpaka sasa Tanzania haina sheria yeyote inayomlinda mtetezi wa haki za binadamu lakini tunaendelea na mchakato na ni matumaini yetu serikali itaridhia kuwa na sheria hiyo hapa nyumbani,” alilisitiza
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki amesema kuwa jeshi la polisi nchini litaendelea kuimarisha mahusiano kati ya jeshi hilo na watetezi wa haki za binadamu nia ni kudumisha amani na utulivu nchini.
DSC_0325
Sehemu ya makamishina na makamanda wa mikoa na maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku moja jijini Dar es Salaam.

“majukumu ya jeshi la polisi na watetezi wa haki za binadamu nchini yanafanana kwa kila hali ni kulinda na kutetea haki za wananchi na mali zao,” amesema Naibu IGP Kaniki,Kamishina Kaniki alilisitiza kwamba ni muhimu wadau wote kuzingatia sheria za nchi, taratibu na kanuni katika kutafuta haki mbalimbali ili kudumisha amani na utulivu nchini.

“nachukua nafasi kuwakaribisha wadau wote wa haki za binadamu na makundi mengine kushirikiana na jeshi la polisi katika kulinda na kutetea haki za binadamu nchini,” alisisitiza.Kamanda wa Polisi Arusha, RPC Liberatus Sabas amesema kwa muda mrefu watu wa utetezi wa haki za binadamu na makundi mengine huwa wanasahau kwamba polisi pia ni binadamu nao wanahitaji utetezi kutoka kwa watetezi hao wa haki za binadamu.
DSC_0375DSC_0417
Naibu Inspekta General wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki (kushoto), Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oparesheni, Kamishina Paul Chagonja wakifuatilia mbalimbali ilizokuwa ikitolewa na washiriki wa warsha hiyo.


DSC_0291
Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake juu ya Ulinzi na utawala wa haki za binadamu kwa mashirika ya watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na Polisi.
DSC_0355
Pichani juu ni Meza kuu na chini ni Baadhi ya Wakuu na Makamishina wa Jeshi la Polisi nchini wakifurahia jambo wakati wa uwasilishwaji wa mada mbalimbali kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
DSC_0362DSC_0413
Kamishina wa kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova akichangia mada katika warsha ya siku moja kuhusu Haki za Binadamu na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
DSC_0397
Kamanda wa Polisi, Arusha Liberatus Sabas akizungumza umuhimu wa kujali pia askari polisi kwa sababu na wao pia ni Binadamu wanahitaji utetezi kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea Haki za Binadamu nchini.
DSC_0390
Kamanda wa Polisi, Lindi, RPC Zeloithe Stephen akitoa nasaha kuhusu miiko na kanuni za Jeshi la Polisi jinsi zinavyotetea na kulinda Haki za Binadamu (Police General Order).
DSC_0438
Picha ya pamoja kati ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini na mgeni rasmi Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini.
DSC_0441
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Malya (kulia) akiteta jambo na Kamishina wa kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova baada ya kupiga picha ya pamoja.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAPOKEA MSAADA KUTOKA SHIRIKA LINALOSHUGHULIKIA IDADI WATU DUNIANI (UNFPA).

$
0
0

TANGAZO LA AJIRA KUTOKA WAIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

 


   




TANGAZO


Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia Wauuguzi  wa ngazi ya Astashahada na ngazi ya Stashahada waliohitimu mafunzo mwaka 2013 wawasilishe maombi ya kupangiwa  vituo vya  kazi. Waombaji wanatakiwa kupendekeza maeneo matatu wanayotaka wapangiwe kazi.


Maeneo  yenye nafasi za kazi yameainishwa kwenye tangazo la kazi kwenye tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  (www.moh.go.tz).


Maombi wayawasilishwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawiwa Jamiikwa anuani ya hapa chini kabla ya tarehe 14 Machi, 2014.


Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,

S.L.P. 9083,

DAR ES SALAAM.


IN EVERLASTING MEMORY OF OUR BELOVED MOM MWL IDA KULWA MAGANGA (27-02-2014)

$
0
0
                                                        
2 Timothy 4:7

“I have Fought a Good Fight, I have Finished My Course, and I have Kept the Faith”


 Mama

Days have turned into weeks, weeks into months, and months into a year since you left us on that Wednesday the 27th February, 2013.


Your love for your husband and children was like nothing else in this World; it knew no law and dared all things.  Your faith in God was immeasurable which you instilled in all of us, we are immensely grateful for that. The wonder and strength of our Almighty Lord, has enabled us to remember you with memories of your unfailing love. 

Mama.


You are always in our hearts, prayers, thoughts and conversations and we believe in our Almighty Lord that one day, we will be together. Deeply missed and remembered by your loving husband Dr Matthew J. Maganga, your children Stella,Reynaltha, Eng Joe, Glory, Benedicta,Adv. Patricia, Florence, Dr AlfredMzee” and Adv. Christina. Also missed by your grand and great grand children, your in laws, brothers and young sisters, the Maganga, Magolo and Maswa’s families, Friends Neighbours and Relatives.

Mama

We thank the Almighty Lord for your life and we will celebrate your life in Tabora on the 22ndApril 2014, where you would have turned 79 years.

A BEATIFUL FLOWER HAS BEEN SENT BACK TO THE LORD’S HEAVENLY GARDEN


R.I.P Mama

RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI MTAMBO WA KUHAKIKI TAKWIMU ZA MAWASILIANO JIJINI DAR LEO.

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama. 

CCM YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA MKOANI IRINGA LEO,MWIGULU AMNADI MGOMBEA WA CCM KWA KISHINDO

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Mwigulu Nchembba akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ifunda, Iringa Vijijini.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa, akizungumza na kuomba kura kwa wakazi wa mji Ifunda mapema leo jioni katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ifunda, Iringa Vijijini.
 Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga,Iringa .
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga,Iringa .
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Mwigulu Nchemba akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ifunda mapema leo,wakati wa mkutano uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ifunda, Iringa Vijijini.
 Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga,Iringa .
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Bi.Pindi Chana akimpigia kampenni mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Kalenga,Godfrey Mgimwa mapema leo jioni,na kulia ni Mwigulu Nchemba
 Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM  ukiendeleo mapema leo jioni,kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ifunda, Iringa Vijijini.

Mjadala kuhusu Mitandao ya kijamii kutoka Jamii Production (UPDATED)

$
0
0

Karibu katika kipindi hiki cha kwanza cha moja kwa moja (Live) kilichorushwa toka studio zetu za Washington DC Katika kipindi hiki, mjadala ulikuwa juu ya MITANDAO YA KIJAMII.
Washiriki walikuwa Prof Nicholas Boaz. Mwalimu wa Mawasiliano kutoka Chuo kikuu cha Maryland.

Mzee Emmanuel Muganda. Mtangazaji mkongwe aliyefanya kazi zaidi ya miaka 30 katika Idhaa za Sauti ya Amerika (VOA) na pia Denzel Musumba. Mmiliki wa Border Media Group ambaye kwa miaka mingi amekuwa akitangaza kupitia mitandao ya kiJamii.

Kwa njia ya Skype tuliungana na Jeff Msangi. Mwandishi, Blogger na mwanaharakati aliyejiunga nasi kutoka Ontario Canada .Na kutoka nchini Tanzania tulimsikia mwakilishi wetu Ahmad James Nandonde aliyeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mara na watu wengine.
Karibu sana

NB: Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa sauti katika baadhi ya sehemu za kipindi.

Kaya zaidi ya 5000 za manispaa ya Iringa kufikiwa na maji safi na salama

$
0
0
 Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Kulia) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wataalam hao waliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Watatu Kulia mwenye koti jeusi) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Wapili Kulia).
 Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Kulia) wakitaka ufafanuzi juu ya maendeleo ya mradi.
 Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
 Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (aliyenyanyua mkono) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya tanki la kuhifadhia maji kwa ajili ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa.
 Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto wa Uwanja wa Ndege wa Iringa (Nduli) ambao ni wanufaika wa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa , Bw. Ranier Nyimbo (Mwenye Fulana nyeusi) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwenye uwanja huo.
 Baadhi ya wanavijiji wa Nduli na Kigonzile kutoka manispaa ya Iringa wakichota maji katika bomba pekee linalopatikana katika mpaka wa vijiji hivyo. Adha hii itaisha mwezi Juni mwaka huu mara baada ya kukamilika  kwa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ikiwemo wanavijiji hawa.
 Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Watatu Kulia) akiwaonesha wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango moja ya mabomba yatakayotumika kusambaza maji. PICHA NA SAIDI A. MKABAKULI

==========  ========  =========
Kaya zaidi ya 5000 za manispaa ya Iringa kufikiwa na maji safi na salama

Katika kukamilisha ahadi na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 – 2016), Serikali imejidhatiti kuwafikishia maji safi na salama wakazi wa zaidi ya kaya 5000 za Manispaa ya Iringa kufikia katikati ya mwaka huu wa fedha.

Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayodhaminiwa na serikali na wafadhili.

Bibi Mwanri alisema kuwa katika kutimiza Mpango wa huo wa Maendeleo Serikali inawekea mkazo katika Kuendeleza adhma yake ya utekelezaji wa miradi ya maji iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hasa katika maeneo sugu yenye upungufu wa maji hasa maeneo ya vijijini ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuuendelea kuimarisha usimamizi vyanzo vya maji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William alisema kuwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo wa Miaka Mitano zaidi ya vijiji 10 vya mkoa wa Iringa vitanufaika na miradi hiyo ya maji ambayo inagharimu zaidi ya milioni 600.

Maji ni eneo mojawapo la kipaumbele la kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaoratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Maeneo mengine ya vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango ni pamoja na: miundombinu ya usafiri, nishati; kilimo; viwanda; maendeleo ya rasilimali watu; na huduma za jamii.

WANAFUNZI WA KITANZANIA THAILAND WAZUNGUMZIA MADINI

$
0
0
 Kamishna Msaidizi wa Madini  Mhandisi Hamis Komba katikati akiwa pamoja na Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand. Wa kwanza kulia ni Agatha Mwinuka, anayefuata ni Emmanuel Minja na wa kwanza kushoto ni Doricas Moshi.

 Wanafunzi wa Kitanzania nchini Thailand, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali , ambao wamelitembelea  banda la Tanzania.

Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini katika picha ya pamoja na wanafunzi hao katika banda la Tanzania.

=======  ======= ========
Wanafunzi wa Tanzania Thailand Waizungumzia sekta ya Madini.


Na Asteria Muhozya, Bangkok


Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand, wamewataka wadau wa tasnia ya madini ya vito na usonara nchini Tanzania kuichukua sekta hiyo kwa umakini mkubwa kutokana na  mchango wake kiuchumi.


Aidha, wameeleza kuwa, nchi ya Thailand imepiga hatua kubwa katika sekta ya madini ukilinganisha na Tanzania lakini bado Tanzania inaweza kufaidika zaidi katika sekta hiyo ikiwa kila mdau atatimiza wajibu wake kikamilifu ili madini ya vito yaongeze mchango katika pato la taifa.


Wameongeza kuwa, Tanzania bado ina nafasi ya kujipanga upya kuhusu kuboresha zaidi sekta hiyo kama ilivyo kwa nchi nyingine  endapo mipango mikakati ya maboresho itatekelezwa  na kusimamiwa kikamilifu.


Wanafunzi hao wameyasema hayo, wakati walipolitembelea banda la Tanzania katika maonesho ya 53 ya Vito vya Usonara na Madini yanayoendelea katika jiji la Bangkok ambapo nchi zaidi ya 150 zinashiriki maonesho hayo.


“Thailand wamejipanga vizuri katika sekta ya madini. Wafanyabiashara wa madini wana umoja. Wadau wa madini wanatakiwa kuelewa  kuwa madini yanawakilisha utajiri wetu tulionao”. Amesema Agatha Mwinuka.


Aidha, wameitaka serikali na  wadau wa Tanzania  wanaoshiriki maonesho hayo kujifunza kutokana na changamoto wanazozipata kutoka kwa nchi nyingine, jambo ambalo litasaidia kuboresha sekta ya madini na vito, ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kuhakikisha  kuwa wanafuata sheria na taratibu zilizopo.


“Tunaiomba serikali iendelee kuendeleza viwanda vya kukata madini. Ni jambo zuri kama shughuli hizi za kukata madini zitafanyika ndani ya nchi badala ya nje. Jambo hili linasaidia sana kuongeza thamani ya madini.  Ameongeza, Emmanuel Minja.


Akiongelea kuhusu umuhimu wa kuendeleza na kuboresha kituo cha Tanzania Geomological Center,  Doricas Moshi, ameeleza kuwa,  kituo hicho kinaweza kutoa mchango mkubwa katika tasnia hii hasa katika nyanja ya ukataji madini  na uthamini wa madini hivyo, ameitaka Serikali kukiongezea nguvu kituo hicho kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya  Tanzania.


“Chuotunachosoma hapa kinatumia sana mifano ya madini ya Tanzania katika kufundisha.  Mengi yametoka nyumbani, hii ni ishara nzuri. Serikali iliangalie hili. Ameongeza Doricas.


Aidha, wameeleza kuwa, soko la kimataifa kwa madini ya Tanzania lipo, hivyo, wamewataka wadau wote kuhakikisha wanashirikiana vizuri na serikali kuendeleza sekta hiyo kutokana na umuhimu na mchango wake kwa taifa.


Akizungumzia  mipango iliyopo ya kuboresha sekta hiyo, Kamishna Msaidizi wa Madini, Mhandisi Hamis Komba, amesema kuwa, Serikali kupitia Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), inatekeleza mikakati ya kuwasaidia wachimbaji wadogo na wa kati  ili waweze kuendana na   mahitaji ya soko la kimataifa kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kukata madini, kuyaongezea thamani na  kuwapatia mikopo kupitia Benki ya TIB.


“STAMICO imepewa jukumu la kuwaendeleza wachimbaji wadogo katika sekta ya madini hususani katika masuala ya uchimbaji, uongezaji thamani madini na biashara ya madini. Serikali imejipanga vizuri katika hilo”. Ameongeza Kamishana.


Ameongeza kuwa, Serikali inatambua kwamba wachimbaji wengi wapo katika sekta ya madini ya vito na usonara hivyo, jitihada za kuwaendeleza  zitasaidia kufikia kiwango bora cha utendaji wao wa kazi.


Vilevile, ameongeza kuwa, kutokana na kuboreshwa kwa Sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inaiwezesha STAMICO kumiliki asilimia 50 ya hisa katika mgodi wa Tanzanite One, jambo ambalo linaifanya Serikali kuwa mmiliki katika mgodi huo.

DTBi - COSTECH WATILIANA SAINI YA USHIRIKIANO NA SILION VALLEY YA MAREKANI

$
0
0
Mr Carl Davis Jr, President of the Silicon Valley Black Chamber of Commerce and Eng. George Mulamula, CEO of DTBi sign MOU copy
Bw.Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi (kulia) wakisaini MOU.

Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
KAMPUNI tanzu ya Tume ya sayansi na teknolojia ya DTBi-COSTECH na Silicon Valley Black Chamber of Commerce’s Center for Entrepreneurial Development (SVCED) wametiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) ambapo pande zote mbili zitashirikiana kwa njia mbalimbali kwa ajili ya ukuaji wa wajasiriamali.

Mkataba huo, kati ya DTBi na SVCED utawezesha pande hizo mbili kukuza ujasiriamali na kujenga uwezo katika Habari, Teknolojia na Mawasiliano kwenye sekta zote za kiuchumi.

Mkataba huo wa MoU utawafanya wadau kufanya shughuli za biashara kwa kuanza na mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kupitia njia ya mtandao na kusaidia wale walio na ubunifu katika nyanja mbalimbali za biashara.
Mr Carl Davis Jr, President of the Silicon Valley Black Chamber of Commerce and Eng. George Mulamula, CEO of DTBi shake hands after signing MOU copy
Bw. Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi kupeana mikono baada ya kusaini MOU.

Mkataba huo pia utasaidia wajasiriamali kuweza kukua na kufanya biashara kwa kutumia mifumo habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ujasiriamali na kuanzisha mfumo wa kubadilishana uzoefu katika kuendeleza biashara na ukuaji wa ujasiriamali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Injinia. George Mulamula amesema mkataba MOU utatoa ushirikishiano ambao utaruhusu wajasiriamali wa Tanzania kufaidika na ujuzi, maarifa ya Silicon Valley ya ujasiriamali.

Amesema hii itasaidia nchi ya Tanzania kuruhusu uanzishwaji wa biashara kupitia njia ya mtandao na mifumo ya Habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ajira na kuchangia pato la taifa.
Mr Mulamula explains the partnership to the press copy
Eng.George Mulamula akielezea ushirikiano kwa vyombo vya habari.
Baada ya kutiliana saini ya MOU, Bw Carl Davis Jr, alikuwa na semina kwa wajasiriamali yenye jina la “The Mindset of the Silicon Valley Entrepreneur: Lessons for the Tanzania Entrepreneur/Innovator”.

Mr Davis Jr amesema anaweza kuwasaidia “wajasiriamali kuelewa jukumu la uzinduzi na ujasiriamali na jinsi Wajasiriamali hapa nchini jinsi wanavyoweza kujiinua katika kufikiri chanya kwenye maeneo ya biashara.
Mr Carl Davis Jr,  gives a talk to Tanzanian entreprenuers at DTBi copy
Bw. Carl Davis Jr, akitoa majadiliano DTBi kwa wajasiriamali wa Tanzania juu ya jinsi ya kuwa mwekezaji mwenye mafanikio.
Attendee contributing to the discussion copy
Mshiriki akichangia mjadala.

Article 0

SIKINDE YAANZA KUIPUA NYIMBO MPYA

$
0
0
Hatimaye bendi kongwe, bendi pekee ambayo imepata kuwa mabingwa wa muziki nchini mara zote mbili ambazo mashindano hayo yamepata kufanyika, bendi ya Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae” imeanza kuipua nyimbo zake mpya zitakazokuwa katika album mpya ya “Jinamizi la Talaka” itakayozinduliwa mwaka huu 2014. 

Album hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 7,ambapo mpaka sasa Sikinde wameishazitoa nyimbo tatu.

Nyimbo hizo ni Jinamizi la Talaka, Za Mkwezi Mbili,Nikipata Nitalipa. Nyimbo hizo unaweza kuzisikiliza online au ku-download kwenye mtandao wa https://www.hulkshare.com/sikindeNyimbo 4 zilizobakia ambazo nazo zitatolewa muda wowote kuanzia hivi sasa ni 1. Kibogoyo, 2. Dole Gumba, 3. Ng'ombe Haelemewi na Nundu na 4. Tabasamu.

 Hii ni album ya kwanza kutolewa tokea mwaka 2009 iliporekodiwa album ya “Supu Umeitia Nazi” album iliyomfanya mwimbaji wake Karama Regesu kuchukua Zawadi ya Tuzo katika Kili Music Award ya mwaka 2009 kwenye category ya “Mtunzi Bora wa Muziki”.

MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA KUOKOA MAISHA YA MTOTO ADOLOTEA NJAVIGE

$
0
0
MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.
Mdau Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo

MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.

Akizungumza kwa masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.

Anasema tukio hilo lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya kula na kufurahi na wenzake.

Anasema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.

Ameongeza kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.

Aidha kutokana na kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.

Amesema anahitaji zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri matibabu ya Mwanaye.

Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.


Na Mbeya yetu.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MEYA WA MJI WA VALLEJO WA MAREKANI, IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya sanamu ndogo ya mji wa Vallejo toka kwa Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis na ujumbe wake walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani. PICHA NA IKULU 

TPA yaendesha semina kwa wakuu wa idara na wawakilishi wa Wafanyakazi ya mkataba wa huduma kwa mteja

$
0
0
Mwenyekiti wa kikao Phares Magesa kushoto akiongoza semina ya mkataba wa huduma kwa wateja ya wakuu wa idara na wawakilishi wa Wafanyakazi wa TPA, kulia ni mwezeshaji Mrs. Ndaba ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utumishi toka Wizara ya Uchukuzi, TPA iko katika hatua ya mwisho ya utengenezaji wa mkataba wa kuhudumia wateja "Customer Service Charter".
Baadhi ya wajumbe wakisikiza kwa makini semina hiyo.

MAMBO 6 YANAYOMFANYA MTU AWE KIONGOZI BORA NA SIO BORA KIONGOZI

$
0
0
leadtheway_21x16-5

Tukiacha mbali picha ambayo mara nyingi au kwa miaka mingi imekuwa ikijengwa  vichwani mwa wengi wanapoona na kudhani kwamba fulani ni kiongozi bora [pengine kwa muonekano tu], au kwa sababu anashuka kutoka kwenye gari kwa mbwembwe, tabasamu baada ya kufunguliwa mlango na mkanda na kisha kupokelewa briefcase yake, yapo mambo kadhaa ambayo yanamfanya mtu awe kiongozi bora na sio bora kiongozi. Na kadri siku zinavyokwenda, taswira ya kiongozi kwa muonekano tu inazidi kupotea. Vitendo,maadili,mafanikio, uvumbuzi na maendeleo vinachukua mstari wa mbele.


Tofauti na miaka ile ambayo picha ya kiongozi bora ilikuwa kama hiyo hapo juu, siku hizi viongozi bora wapo na wanajitokeza katika hali tofauti tofauti kabisa. Anaweza kuwa asiyevaa suti kama Dalai Lama na akawa kiongozi bora. Au asiyevaa suti bali t-shirt na jeans tu kama alivyokuwa Steve Jobs wa Apple au Mark Zuckerberg boss wa Facebook. Mifano ya viongozi hawa ipo mingi.

Kituo cha utafiti na mafunzo ya uongozi cha Dale Carnegie cha jijini New York nchini Marekani kinasema katika utafiti wao wamegundua kwamba kinachomfanya mtu awe kiongozi bora sio suti, briefcase, tabasamu[ hususani lile la uongo] bali uwezo na nia ya dhati katika kuamsha ari, kuwawezesha unaowaongoza, kuwafanya wajiamini na kuwapa motisha watu unaowaongoza. Pamoja na hayo, na kutokana na ukweli kwamba leo hii tuna kila aina ya viongozi, yapo baadhi ya mambo yanayowatofautisha viongozi bora na bora viongozi. Haya hapa ni baadhi yake;

HABARI ZAIDI BOFYA HIYO LINK

Tamasha la Pasaka, CXC, NSSF wadhamini mkutano TASWA

$
0
0
KAMPUNI ya CXC ya jijini Dar es Salaam, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na waandaaji wa Tamasha la Pasaka wamejitosa kupiga tafu Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika kesho.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, alisema NSSF imetoa udhamini wa ukumbi wakati CXC na Tamasha la Pasaka kila mmoja ametoa Sh milioni moja kwa ajili ya mkutano huo utakaoenda pamoja na Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.
 
“Tunashukuru Kampuni ya CXC ya jijini Dar es Salaam,  waandaaji wa Tamasha la Pasaka kampuni ya Msama Promotions na shirika la NSSF wametusaidia kwa kiasi fulani mkutano wetu.
 
“Bajeti yetu ni kubwa sana ni zaidi ya Sh milioni 10 maana licha ya wanachama wa Dar es Salaam pia tuna wanachama kutoka mikoani, ambapo wengine wanatoka Morogoro, Tanga, Zanzibar na Arusha,” alisema Mhando na kuongeza kuwa wanatarajia wanachama 150 washiriki mkutano huo.
 
Alisema mkutano utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront Dar es Salaam na kwamba wanachama kutoka nje ya Dar es Salaam wanatarajia kuwasili leo tayari kwa mkutano huo wa aina yake.

MAISHA PLUS ‘REKEBISHA’ WASHIRIKI KAZI ZA JAMII

$
0
0
 Washiriki wa maisha Plus wakichimba shimo kwa ajili ya kujenga choo cha shule ya msingi Igula. 
 Baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus 'Rekebisha' wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya kazi ya kuchumba matundu ya choo katika shule ya msingi Igula tarafa ya Ismani mkoani Iringa kulikokuwa na kijiji cha awali cha mashindano hayo.
 Baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus 'Rekebisha' wakiwa wamepumzika baada ya kufanya kazi ya kuchimba matundu ya choo katika shule ya msingi Igula tarafa ya Ismani mkoani Iringa kulikokuwa na kijiji cha awali cha mashindano hayo.
 Moja ya nyumba za watu wasiojiweza ikiendelea kukarabatiwa na washiriki wa maisha plus 'Jirekebishe'
Baadhi ya washiriki wa shindano la Maisha Plus 'Rekebisha' wakigawana chakula.


MAISHA PLUS ‘REKEBISHA’  WASHIRIKI KAZI ZA JAMII

Na Denis Mlowe,Iringa

WASHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus walioko katika kijiji cha awali cha Igula kilichoko tarafa ya Ismani kata ya Kihorogota wameshiriki katika kazi za kijamii zikiwemo ujenzi wa choo katika shule ya Msingi Igula.

Washiriki hao 20 wakiongozwa na mwenyekiti Yasinta Hokororo wamefanikiwa kukarabati baadhi ya nyumba ambazo zinakaliwa na wazee wasiojiweza na kufanya shughuli za kilimo kwa walezi wanaoishi nao kijijini hapo.

Akizungumza,Hokororo alisema maisha wanayoishi kijijini hapo ni kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kijiji ikiwemo kuwasaidia wazee wasiojiweza kuwahudumia shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo.

Alisema changamoto wanazokutana nazo zimewafanya kuwa mahiri katika utendaji wa kazi tofauti na maisha yao ya nyumbani.

Hokororo alisema maisha wanayoishi katika kijiji cha awali lengo kuu ni kurekebisha changamoto wanazokumbanazo wananchi wa kijiji husika zikiwemo za kilimo kwa kuwapa mbinu mbalimbali za kujikwamua na kupata mazao bora.

“Moja ya Changamoto ambazo tumekutana nazo hapa ni masuala ya kilimo na wanafunzi wa shule ya msingi Igula kukosa choo bora hivyo sisi kama vijana tukaamua kuanza na ujenzi wa choo kwa wanafunzi hao na kisha kwenda mashambani kusaidia kazi za walezi wanaotulea.” Alisema Hokororo

Kwa upande wake mkuu wa usanifu wa Maisha Plus Kaka Bonda alisema shindano la mwaka huu limekuja na kauli mbiu ya ‘Maisha Plus 'Rekebisha’ likiwa na lengo la kuingia ndani ya jamii na kuibua na kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo na kuzitatua kwa njia mbadala.

Bonda alisema washiriki wa  shindano hilo watakuwa na jukumu la kufanya kazi za kijamii zaidi na kuwasaidia watu wasiojiweza katika maisha ya kijijini na kurekebisha baadhi ya vitu ambavyo kwa namna moja au nyingine wanakumbana nazo.

“Kama unavyoona vijana wameanza kutengeneza choo cha shule ya msingi Igula, na wanaendelea na ukarabati wa nyumba ya mzee asiyejiweza baada ya kuanguka na mvua ndio kazi ambazo kwa mwaka huu wa maisha plus rekebisha watahusika nazo washiriki.” Alisema Bonda

Alisema shindano la mwaka huu litakuwa la kimataifa zaidi kwa kushirikisha washiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Tanzania.

Alisema maisha plus kipindi cha televisheni kinachoonyesha maisha halisia ya Vijana na Wakulima Wanawake ambao ni mama shujaa wa chakula hivyo washiriki wanaohitajika kuingia katika fainali ni 9 kati ya 19 walioko katika kijiji na kisha wataelekea kijiji cha awali cha Zanzibar.

BODI YA VYAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YAKUBALIANA NA MFANYA BIASHARA KUREJESHWA MCHELE MBOVU PAKISTAN.

$
0
0
 Mmiliki wa Mchele uliodhibitishwa kuwa mbovu na kutofaa kwa chakula na Bodi ya vyakula, dawa na vipodozi Zanzibar Bwana. Mohamed Mauly akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la kurejeshwa kwao Mchele huo wenye wingi wa Nani 26 sawa na kg 2,600 katika Gonauni lake kwerekwe Zanzibar. 
 Mchele mbovu uliodhibitishwa na Bodi ya vyakula, dawa na vipodozi Zanzibar ukiwa kweye Godauni Mwanakwerekwe ukisubiri kurejeshwa Pakistan ulipo nunuliwa. 
 Wachukuzi wakipakia Mchele kwenye gari kwaajili ya kusafirishwa kurejeshwa ulipotoka.
Mmiliki wa Mchele Bwana. Mohamed Mauly akionyesha Mchele mbovu ulithibitishwa na Bodi ya vyakula, dawa na vipodozi Zanzibar na mwenyewe kuridhika na majibu hayo, nakusema sio aliouagizia hivyo ameshapeleka madai na kutakiwa aurudishe ili kupewa haki zake na Kampuni ya Bilal Rice Mills ya Pakistan. Picha na Makame Mshenga wa Maelezo-Zanzibar.

Afisa mstaafu wa NMB afariki dunia kwenye ajali ya Basi na Treni

$
0
0
DSC06845
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni, Dk.Kitundu Jackson ,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya mapokezi ya majeruhi wa basi la bunda lililogonga kichwa cha Treni leo.Picha zote na Nathaniel Limu.
DSC06809
Bbasi la Bunda lililokuwa likitokea mjini Dodoma linakwenda jijini Mwanza na kugonga kichwa cha Treni maeneo ya mjini Mnayoni,linavyoonekana katika picha baada ya kugonga.
DSC06818
Baadhi ya majeruhi wa basi la Bunda lililogonga kichwa cha Treni mjini Manyoni,wakiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni.
DSC06819
Na Nathaniel Limu, Manyoni.

AFISA Mstaafu wa NMB benki tawi la Manyoni mkoani Singida ambaye kwa sasa alikuwa Mhasibu wa SACCOS ya chama cha walimu Tanzania Manyoni,Belida Kombo amefariki dunia baada ya basi la kampuni ya Bunda alilokuwa akisafiria kugonga kichwa cha treni na kujeruhi abiria wengine 39.

Basi hilo T.782 BKZ aina ya scania lililokuwa Farak Adamu lilikluwa likitokea Dodoma mjini kuelekea jijini Mwanza,liligonga kichwa cha treni eneo la makutano ya barabara kuu ya Dodoma – Singida na reli eno la round about ya Manyoni mjini leo saa moja na nusu asubuhi.

Bi Kombo ambaye alipandia basi hilo katika kituo cha mabasi cha Manyoni mjini na alifariki dunia dakika chake wakati akihangaika kutafuta kiti.Pia ndugu zake waliomsindikiza wakiwa bado hawajaondoka eneo lam kituo cha mabasi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni,Dk.Kitundu Jackson amekiri kwamba amepokea majeruhi 39 wa ajali ya treni na basi na kati yao sita wana hali mbaya. Amesema majeruhi walio na hali mbaya ni pamoja na kondakta wa basi Masage Bunyema na kwamba baadhi watapewa rufaa ya kupelekwa hospitali ya mkoa wa Dodoma na wengine katika hospitali ya misheni ya St.Gasper Itigi.

“Tayari majeruhi wawili tumeisha wapa rufaa kwenda kupata matibabu katika hospitali ya mkoa ya Dodoma mjini na sista mmoja tumempeleka katika hospitali ya misheni ya St.Gasper Itigi”,alifafanua zaidi Dk.Kitundu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Fatma Toufiq ameiangiza mamlaka ya TRL na TANROADS kujenga haraka kuweka mtumishi wa kutoa angalizo kwa vitambaa juu ya gari la moshi linapopita katika eneo hilo ambali kumetokea ajali tatu katika kipindi kifupi kilichopita.

Aidha,mashuhuda wa ajali hilo,wamedai kuwa hicho kichwa cha treni kilichokuwa kikitokea katika kijiji cha Aghondi,dereva wake alijitahidi kupiga honi kali ili kumwonya dereva wa bunda basi lakini dereva huyo hakujali.Kama haitoshi,dereva wa hiece aliyekuwa apishane na basi hilo,alimumulika kwa taa akimwonya asimame ili kipisha kichwa hicho,lakini hakujali pia.

Watu hao wamedai kuwa dereva wa basi hilo alikuwa kwenye mwendo kasi wakati akipewa onyo hilo la kupisha kichwa cha treni lipite.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images