Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

LIBENEKE LA UJIO WA "ALOYSON TV"

$
0
0
 UJIO NA UTAMBULISHO WA "aloysonTv"www.youtube.com/aloysontv

ITAZAME VIDEO HII HAPA CHINI


aloyson.com Inapenda kuitambulisha "aloysonTv" itakayokuwa ikiwakusanyia na nkuwaletea matukio ya picha mwendo (video) katika habari nyingi ambazo aloyson.com watakuwa wakiyaripoti.

Pia kwa nia ya dhati kabisa inapenda kukitambulisha kipindi cha MY ZONE kitakachokuwa kikifanya vipindi mbalimbali kwa watu maarufu na wasio maarufu ili kuleta uwiano wa habari zisizopata wasaha mzuri wa kuwafikia watu wengi.

aloysonTv, imevutiwa zaidi na kuguswa kuhakikisha inapata habari zaidi za wazee ambapo katika ulimwengu huu wa teknolojia iliyokuwa kwa kiasi kikubwa na kuwasahau sana. Tutapata kujua nini hasa wazee wetu huvutiwa na ulimwengu huu, nini wanavutiwa toka kwa vijana na pia fashion zinavyotofautiana hasa kwa vijana na wazee toka enzi hizo na za sasa na mengine mengi yanayojiri miongoni mwao.

Hii yote inaambatana na kutambua umuhimu wa wazee wetu waliotuleta na kutulea sisi ambao ndiyo vijana na nguvu kazi ya sasa na tunaohitajika kama tegemezi kwao.

OMBI KWA WADAU WA HABARI:
Msaada wenu unahitajika sana katika kusaidia yale yote mazuri ambayo jamii inastahili kufikiwa. Bila nguvu ya ushirikiano wenu sitaweza kuyatimiza haya yote na hivyo basi kwa dhati kabisa nawaomba kutoa msaada kuzisambaza habari hizi ikiwa ni nguvu kazi na ubunifu wa vijana tunaopenda kujituma na kuitumikia jamii kwa maendeleo jamii yetu ya Tanzania.

MWISHO:
Shukrani za dhati ni kwa M/Mungu na kwenu wanahabari, wadau wa habari na wasomaji au wafuatiliaji wa habari, heshima za dhati sana kwenu nyote na Mungu awejalie mema mengi.
 Aloyce Mlawa || Aloyson mmiliki wa aloyson.com
Juma Omary || Omry, Director of Photography.

Imeandikwa na;
Aloyce Mlawa,
(Aloyson)
Blogger
www.aloyson.com
aloyson@live.com

MSHINDI WA MILIONI 10 ZA CHAMPIONI SHINDA MAHELA AKABIDHIWA MPUNGA WAKE

$
0
0
Mkurugenzi wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Marsha Bukumbi akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 mshindi wa shindano la Championi Mahela, Kizito George Chuma (kushoto).
Kizito George Chuma akiwa ameshika mfano wa hundi yake ya milioni 10.
Kizito George Chuma akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 na Global Publishers Ltd.
Meneja wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (katikati) akimtambulisha mshindi wa milioni 10 za shindano la Championi Mahela kwa wanahabari (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Global Publishers Ltd, Marsha Bukumbi (wa kwanza kushoto) akipozi na mshindi wa milioni 10 pamoja na wakala wa Magazeti ya Global aliyejishindia pikipiki aina ya Skymark kutoka kampuni ya Shinyanga Emporium.


Mkurugenzi wa Kamapuni ya Shinyanga Emporium, Ritesh Monami (kushoto) akimkabidhi pikipiki wakala wa magazeti ya Global Publishers Ltd, Majid Hamis.
Timu ya Championi ikipozi na mshindi wa milioni 10.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akimpongeza mshindi wa milioni 10.
Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula (kulia) akimpongeza Kizito.
Msanifu Kurasa wa Global, Huruma Bujiku (aliyekaa) akimuonyesha mshindi wa milioni 10 namna gazeti linavyoandaliwa. Aliyesimama kulia ni Meneja Masoko wa Global, Benjamin Mwanambuu.
...Kizito akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Ojuku Abraham.
Mhariri wa Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Mohamed Kuyunga (kulia) akimpongeza Kizito kwa kulamba M10.
Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Amani na Risasi Jumamosi, Erick Evarist (kushoto) akimkpongeza Kizito. Kizito akisalimiana na Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Oscar Ndauka (kushoto).
Kizito akifurahia jambo na Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Aziz Hashim (kulia). Kushoto ni Walusanga Ndaki.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

MAKAMU WA RAIS,DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA ZIWA,JIJINI MWANZA LEO

$
0
0
  Mgeni Rasmi katika Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo,uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
 Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo,uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo ambaye ndie Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,akizungumza na washiriki wa Kongamano hilo (hawapo pichani) wakati ufunguzi wake uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.
 Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuja kuzungumza na Washiriki wa Kongamano hilo,jijini Mwanza leo.
Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania,Mh. Thamduycse Chilliza (katikati) akifatilia Kongamano hilo sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC),Julieth Kairuki (kushoto).Kulia ni Msaidizi wa Balozi wa Afrika Kusini,Terry Govender.
Waheshimiwa Mawaziri wakishiriki pamoja na Wajumbe wa Kongamano hilo,kuimba wimbo wa Taifa.
Baadhi ya waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Wadau wa Bodi ya Utalii.


Washiriki mbali mbali wa Kongamano hilo.
Watumishi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Wadau wakifatilia kwa umakini Kongamano hilo.



Picha ya pamoja na Waheshimiwa Mawaziri na Wakuu wa Mikoa.
Picha ya Pamoja na Watumishi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

NYUMBA INAUZWA GONGO LA MBOTO MWISHO WA LAMI

$
0
0
Nyumba inauzwa iko, Gongo la Mboto mwisho wa Lawi,
Mita 50 kutoka barabara kuu,
Gari inafika mpaka mlangoni bila matatizo yeyote,
Nyumba ina vymba vitatu, kimoja master bedroom,
Inajiko, dinning na sebure kubwa na uwa mkubwa
Nyumba ina Umeme na Ac 2,
Kwa mawasiliano zaidi piga namba 0715 001 975 au 0787 999 774
Muonekano wa mbele wa nyumba hiyo...
Muonekano wa mpaka wa nyumba hiyo.
Nguzo ya umeme...ambayo ipo katika ukuta.
Madirisha ya kisasa kabisa...
Mlango wa ndani...
Korido ya kuendelea vyumbani...

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY KWA STYLE YA KIPEKEE.

$
0
0
 Mmoja wa Wakurugenzi wa Skylight beach Haruna Said akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusiana na matayarisho ya Burudani ya kipekee ya Valentine's day na Fullmoon Party litakalofanyika kwenye ufukwe wa ziwa Victoria, Skylight Beach Resort Malimbe jijini Mwanza. 
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kabla ya ufunguzi wa Ukumbi wa burudani wa Disko kuanza wamejipanga kuanza kutoa burudani ya ufukweni maarufu Foolmoon Beach Part ambayo itakuwa inafanyika kila mwezi mara moja kwa lengo la kutambulisha bidhaa mbalimbali zitakazopatikana Skylight Beach Resort.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Syklight Group Ltd, ‘Jembe ni Jembe’ Innocent Maletho (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kutambulisha burudani zitakazo kuwepo usiku wa Valeentine pande za Skylight Beach Resort Malimbe jijini Mwanza.

Alisema kuwa katika siku hii ya shangwe kwa wakazi wa Rock city, kututakuwa na burudani mbalimbali toka kwa MAdj wakali,  DVJ Frank,  DVJ Denis na DVJ Davy ambao watatambulisha mfumo mpya wa burudani ya kiwango cha kimataifa. Pia tutakua na Dj mgeni (Guest DJ),kutoka Dar es salaam, DVJ MAFUVU Atakayedondosha ngoma kali kwa watakao hudhuria.

Wandishi wa habari wakijadiliana juu ya tukio hilo huku wakiweka kumbukumbu kwa yale yanayopaswa kuwafikia walaji wa habari aka jamii.
Kona ya wanahabari.
Baadhi ya wadau wa Skylight Beach Resort Mwanza wakiweka mambo sawa kubainisha huduma zitakazo kuwa zikitolewa kwenye kiota hicho kipya chenye hadhi ya kitalii nchini. Kutoka kushoto ni meneja masoko wa Skylight Beach Resort, Ombeni Charles, Afisa masoko Innocent Maletho, mmoja kati ya wakurugenzi wa 'Jembe ni Jembe' Haruna Said, Dvj Frank na Mdau wa kitengo cha huduma vinywaji Skylight Beach Resort Mwanza.  
Meneja Ubunifu Matukio wa Skylight Beach Resort Albert G. Sengo (Pichani) amesema kuwa ujio wa Skylight Beach Resort umekuja kwa nia ya kuitikia wito wa Serikali ya Mkoa wa Mwanza kwa wadau wake wazalendo na wageni kuwekeza katika jiji hilo kwa nia ya kukuza Sekta ya Utalii sambamba na uboreshaji wa huduma za mahoteli Kanda ya Ziwa. 
Mkare Front Bar ni mmoja kati ya maeneo ya kiota hicho cha Skylight Beach Resort Mwanza, kitakacho tambulishwa ambapo Part hilo la Valentine linalo ambatana na tukio la Foolmoon Party litafanyika.
This is Skylight Beach Resort. 


MWANZA.


KITUO kipya cha Burudani cha Skylight Beach Resort, kilichopo Sweya Kata ya Mkolani Wilayani Nyamagana kuzinduliwa rasmi siku ya Wapendanao (Valentines Day) kwa Tamasha kubwa la burudani ya ufukweni mwa mwambao wa Ziwa Victoria Jijini hapa.


Kufunguliwa kwa kituo hiki ni moja kati ya hatua za kuitikia wito wa serikali kwa wazalendo kuwekeza katika sekta ya utalii na burudani kwenye  maeneo mbalimbali ya Majiji , Manispaa na Halmashauri za Wilaya.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini humo jana, Mmoja wa Wakurugenzi wa Skylight beach Haruna Said alisema kwamba, Kituo hicho kilichojengwa kwa hadhi ya Kimataifa na chenye madhari nzuri ambacho kwa sasa ni gumzo na cha kwanza kwa ubora Jijini hapa.


Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kabla ya ufunguzi wa Ukumbi wa burudani wa Disko kuanza wamejipanga kuanza kutoa burudani ya ufukweni maarufu Foolmoon Beach Part ambayo itakuwa inafanyika kila mwezi mara moja kwa lengo la kutambulisha bidhaa mbalimbali zitakazopatikana Skylight Beach Resort.


“Tumeazimia kuutangaza utamaduni mpya wa Party kila mwezi kwa wakazi wa Jiji hili na wale wanaotoka maeneo ya Mikoa ya jirani na nchi za jirani wanapofika kupata ladha mpya ya burudani ikizingatiwa kituo hiki chenye hadhi ya kitalii kiko kilomita 10 kutoka Chuo Kikuu cha SAUT kilichopo Malimbe Katani hapa”alisema


Aliongeza kuwa kufuatia siku hiyo kuangukia siku ya wapendanao “Valentines Day”ambapo vilevile siku hiyo imeangukia kwa tukio la mwezi kuonekana kikamilifu (Umbo la duara) klabu hiyo imenuia kuwapa fursa watu wa burudani wa Jiji la Mwanza na wageni kusherehekea matukio hayo kwa Tamasha la Skylight Fullmoon Party ikiwa ni juhudi za kukuza utalii na uchumi.


“Moja ya bidhaa zitakazo nadiwa siku hiyo ya Februari 14 mwaka huu kwa Watalii wa ndani na nje ambapo watapata fursa maalumu ya wao kupata bidhaa  ambazo ni vionjo vipya vya Skylight Beach yaani Mamba Squre, Kiboko Tarrace na Mkare Front Bar ambapo kwa watakaoingia watapata ladhaa na mitindo mipya kabisa” alisisitiza.


Naye Afisa Masoko wa Kampuni ya Syklight Group Ltd, ‘Jembe ni Jembe’ alisema kuwa katika siku hii ya shangwe kwa wakazi wa Rock city, kututakuwa na burudani mbalimbali toka kwa MAdj wakali,  DVJ Frank,  DVJ Denis na DVJ Davy ambao watatambulisha mfumo mpya wa burudani ya kiwango cha kimataifa. Pia tutakua na Dj mgeni (Guest DJ),kutoka Dar es salaam, DVJ MAFUVU Atakayedondosha ngoma kali kwa watakao hudhuria.

.


“Tumejianda kutatoa zawadi kibao kwa waliopendeza na kuvalia mavazi rasmi ya Valentine, huku vinywaji vya KVant Gin vikitolewa bure mlangoni, Pia tutatoa Red roses na Rollypop  kwa akinadada 100 wa kwanza watakauingia Resort na viile vile zawadi kibao kushindaniwa siku hiyo” alisema



Wito kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na wageni wapenzi wa burudani wafike kujionea burudani mpya ya kiwango ambayo kwa mara ya kwanza itaanza kutolewa kwenye madhari ya fukwe kwa mitindo tofauti kwa kusherehekea na kufanya utalii kwa kingilio cha shilingi elfu kumi tu mlangoni huku ulinzi wa wateja na mali zao ukiimarishwa kwa asilimia 100.

DIWANI WA KATA YA MBWENI BONIFACE MNYACHIBE (CCM) AFARIKI DUNIA-.

$
0
0
Marehemu Boniface Mnyachibwe Enzi za Uhai wake


TANZIA.

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inapenda kutangaza kifo cha Diwani wa kata ya Mbweni Mh. Boniface Mnyachibwe kilichotokea leo ghafla saa tatu asubuhi.

Tunatoa pole kwa familia yake, wakazi wa Mbweni, Wananchi wa Kinondoni pamoja na Chama chake cha CCM.

Mchango wake mkubwa ktk kuboresha maisha ya wakazi wa Mbweni na Kinondoni kwa kujituma na uadilifu kamwe hautasahaulika. Aidha, kifo chake cha ghafla leo wakati jana tulikuwa naye mpaka saa moja na nusu jioni kwenye vikao vya bajeti ni uthibitisho wa uzalendo wake na mapenzi yake kwa anaowawakilisha na Kinondoni kwa ujumla.

Dua zetu na sala zetu ziende kwa familia yake na wote aliokuwa anawawakilisha.

Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi-AMIN.
Imetolewa na Manispaa Ya Kinondoni

WATATU WAHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI CCM

$
0
0

 Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye akiwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma tayari kwa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili.
 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa akizungumza na Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye kabla ya kuanza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma.
 Ndugu William Ngeleja akisubiri kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama.
 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa kizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo alisema mazungumzo yalikuwa mazuri,yalikuwa yenye nia ya kukijenga chama kwa ajili ya uchaguzi 2015.
Waandishi wa Habari wakiwajibika kuandika habari nje ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo viongozi watatu walihojiwa na Kamati ndogo ya Maadili.

Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula  leo imewahoji watu watatu ambao wawili walishawahi kuwa Mawaziri Wakuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Mawaziri hao waliohojiwa leno ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa,Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema Ndugu William Ngeleja ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

 Kamati hiyo bado ina kazi ya kuwahoji viongozi wengine watatu ambao leo walishindwa kufika baada ya kuomba udhuru kwani walikuwa na majukumu mengine ya kiserikali, ambao hawajafika leo ni Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe ambaye yupo safarini nje ya nchi ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen Wassira na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu Januari Makamba.

RAIS KIKWETE APENDEKEZA KUPIGWA MARUFUKU KWA BIASHARA YA MENO YA NDOVU NA PEMBE ZA FARU DUNIANI

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete akiongea kuhusu mbinu za kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na pembe za faru, ambapo katika mkutano maalumu wa tatizo hilo leo huko Lancaster House jijini London, Uingereza leo, mependekeza kupigwa marufuku kwa biashara hiyo ulimwenguni kote ili kuua biashara hiyo.

MTU MMOJA AKAMATWA NA VIPANDE 21 VYA MENO YA TEMBO MKOANI SINGIDA LEO

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani SINGIDA limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43. 

 Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika kijiji cha Mwamagembe  wilayani Manyoni  zikisafirishwa kwenda Itigi, mkoani Singida. 
 Mtu mmoja  George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno  hayo ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria.
 Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili kilichoko katika kijiji Ukimbu, kata  ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida RPC Geofrey Kamwela (katika video) amesema vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni 43 na vyote vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani Itigi."Meno haya yanaashiria kuuwawa kwa tembo wanne", alisema Kamanda James.

Vitendo vya ujangili wilayani MANYONI vimekuwa vikiongezeka ambapo mwaka 2013 askari mmoja wa jeshi polisi alipoteza maisha katika mapambano na majangili wilayani humo.

Tukio hili la limekuja wakati leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria mkutano maalumu wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo na pembe za Faru jijini London, Uingereza. Katika mkutano huo amependekeza kupigwa marufuku biashara hiyo ili kuweza kudhibiti ujangili duniani kote.

YUNEDA MKOMBOZI WA WASANII BONGO:Kusambaza filamu ya Why Linah? Jumatatu hii.

$
0
0
KAMPUNI mpya ya usambazaji wa filamu Bongo ya Yuneda Entertainment imeingia katika biashara ya usambazaji baada ya kilio cha wasanii kukosa sehemu za kuuza filamu zao au kusambaziwa, kampuni hiyo inayojali ubora kwa kazi za sinema imeingia nchini kuanza kwa kusambaza filamu ya Why Linah?

Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya filamu Bongo kama Hemed Suleiman ‘Phd’, Rose Ndauka, Charles Magali ‘Mzee Magali’, pamoja na wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahilihood, filamu hiyo inaingia leo jumatatu.


Wasanii wamefurahia sana ujio wa kampuni hiyo kwani wanaamini kuwa wengi wataweza kusambaziwa kazi zao kwani moja ya sifa hiyo ni ya kizalendo inayojali maslahi ya wasanii, na inaongozwa na wazalendo wanaojua hali halisi ya soko la filamu nchi Tanzania.


Hivyo kwa kuzingatia umakini na ubora wa filamu Yuneda Entertainment wanakuletea filamu yenye viwango vya kimataifa ya Why Linah?.

MIFUKO YA BIMA YA AFYA (NHIF) NA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) SINGIDA YAHIMIZWA KUWA MAKINI KWA MADAI YA KUGHUSHI

$
0
0
DSC06603
Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki, akifungua kikao cha waratibu wa mfuko wa Taifa Bima ya Afya na wale wa mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambacho kilitumika kukumbushana juu ya utoaji huduma bora kwa wananchama.Kulia ni afisa matekelezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida,Isaya Shekifu na kushoto ni Edwin Mwangajilo afisa udhibiti ubora NHIF.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC06615
Afisa matekelezo na uratibu wa mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Singida, Isaya Shekifu akitoa mada yake kwenye kikao cha wataribu wa mfuko wa NHIF na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkoa wa Singida.Kikoa hicho kililenga kubadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi,ili kuboresha zaidi huduma za mifuko hiyo.Kushoto ni meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
DSC06606
Afisa udhibiti ubora NHIF mkoa wa Singida, Edwin Mwangajilo,akitoa mada yake kwenye kikao cha waratibu wa NHIF na CHF kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.Kushoto ni meneja NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
DSC06607
Baadhi ya waratibu wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wale wa mfuko wa Afya ya Jamii mkoa wa Singida, waliohudhuria kikao cha kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi, ili kuboresha huduma zaidi.
DSC06616
Picha ya pamoja.

Na Nathaniel Limu, Singida.

WARATIBU wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkoani Singida,wamehimiza kuwa makini zaidi kukabiliana na wimbi la madai ya kughushi, kwa madai kwamba vitendo hivyo,vitachangia kudhoofisha huduma zinazotolewa na mifuko hiyo.

Wito huo umetolewa na meneja wa NHIF mkoa wa Singida,Agnes Chaki,wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha waratibu wa NHIF na CHF mkoani hapa, kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa kanisa katoliki mjini hapa.

Alisema kuna baadhi ya watoa huduma si waaminifu na wanaleta madai ya kugushi, na mfuko umejiandaa kikamilifu kuhakikisha unadhibiti vitendo hivi ili kutimiza lengo la msingi la kuwapa huduma bora wanachama wake.

"Ninyi waratibu ninawaomba ndugu zangu, tusaidiane katika kupambana na hili tatizo.Mnapokutana na watoa huduma,naomba mjaribu kuwaelimisha kuwa wawe wanatibu kwa kuzingatia miongozo ya NHIF na ile ya wizara.Wahakikishe kile wanachokitoa kinakuwa ni sawa na wanacho wasilisha NHIF....mfano katika dawa",alisema Chaki.

Aidha,meneja huyo wa mkoa, alisema mwanachama,mratibu au kiongozi ye yote akisikia au kuona kuna vitu/vitendo vinafanyika kinyume na taratibu za NHIF,tafadhali atoe taarifa mapema ofisi za NHIF mkoani hapa,ili ziwezekufuatiliwa mapema kabla havijaleta madhara kwa mfuko.

Kwa upande wake afisa matelekezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida,Isaya Shekifu,akitoa mada yake ya majukumu ya waratibu wa NHIF/CHF,aliwataka waratibu hao kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa uadilifu na kwa ushirikiano baina yao ili kuongeza ufanisi na pia wanajitambulisha kikamilifu katika vituo vyao vya kazi,ili wanachama wa mifuko hiyo,waweze kuwafahamu na kuwatambua .

"Pia hakikisheni mnatatua mapema matatizo/kero zinazohusu wanachma wa NHIF/CHF pamoja na watoa huduma na muandae taarifa za utekelezaji kila baada ya miezi mitatu",alisema Shekifu.
Afisa huyo wa maelekezo na uratibu,alisema NHIF inategemea endapo waratibu watatimiza majibu wao kwa uhakika, malalamiko kuhusu huduma za NHIF yatapungua na huduma zitaboreka.

Pia afisa udhibiti na uhakiki ubora wa NHIF mkoa wa singida ,Dr.Edwin Mwangajilo aliwasisitizia waratibu wa NHIF kuhakikishia wanapitia madai kwa uangalifu ili kuepusha makosa ambayo yanaweza kupunguza kiasi cha malipo ya madai kwa watoa huduma.
"Tunategemea mtafanya kazi zenu kwa ufanisi na uadilifu na kuhakikisha mnasimamia vituo vyote vile vya serikali,binafsi na mashirika ya dini ili wanachama wetu wa NHIF na CHF wapate huduma bora ,alifafanua Mwangajilo.

BENKI YA WANAWAKE TANZANIA YAJITOSA KUPIGA JEKI MAANDALIZI YA TUZO YA MWANAMAKUKA 2014

$
0
0
 Meneja Mradi wa Mwanamakuka Bi.Maryam Shamo akizungumzia maandalizi ya tuzo hizo.Mkurugenzi wa benki ya Wanawake Tanzania,Bi Margareth Chacha akizungumzia namna benki yake inavyoweza kuwasaidia Wanawake nchini,ambaye pia ni Mdau mkubwa wa Tuzo za Mwanamakuka

CCM YABAKI NA MFUMO WA SERIKALI MBILI

$
0
0

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo aliwaeleza kuwa Kikao cha NEC kilikamilika vizuri ambapo wajumbe waliijadili Rasimu vizuri na CCM kubaki na msimamo wa Serikali mbili .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma na kuwaambia CCM bado imebaki na msimamo wake wa muundo Serikali mbili wenye maboresho.

WAFANYE WATABASAMU WATEMBELEA WATOTO WA SOS CHILDREN'S VILLAGES JUZI

$
0
0
Mchora vibonzo na Mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala, akiongea na baadhi ya watoto wa Kituo cha SOS Children’s Villages cha Dar es Salaam wakati wa ziara ya mafunzo ya uchoraji katika kituo hiko, Juzi. Ziara hiyo iliyohusisha wachoraji na marafiki kadhaa ililenga kuibua vipaji na kuwatabasamisha watoto. (Picha zote na Wafanye Watabasamu).
 Mchora vibonzo Abdul King O  ‘Kaboka Mchizi’, akitoa maelekezo ya jinsi ya ‘kutupia’ rangi kwa watoto wa SOS Children’s Villages, juzi.
 Hili ndilo haswaaa lengo la Wafanye Watabasamu; elimu, ukuzaji vipaji na tabasamu.
 Baadhi ya Makomredi wa Wafanye Watabasamu wakiwa wamekula pozi katika SOS Children’s Villages, juzi. Kutoka kulia, Godfrey ‘Mzee wa Beche’, Evaris Chikawe ‘Rasta bila masharti’ na Said Michael ‘Wakudata.’
 Watoto wa SOS Children’s Villages cha Dar es Salaam, ‘wakizishambulia’ rangi wakati walipotembelewa na marafiki wa Wafanye Watabasamu, juzi.
‘Si umesema wewe ndiye mchora kibonzo ITV, tuoneshe?’ Baadhi ya watoto wa SOS Children’s Villages wakimdadisi mchora vibonzo Nathan Mpangala, mara baada ya zoezi la uchoraji kwisha.Kulikuwa na ubunifu wa kila aina. Picha zaidi bofya: https://www.facebook.com/pages/Wafanye-Watabasamu-Make-Them-Smile/140812046112398

UNIC YAHAMASISHA VIJANA MKOANI DODOMA KUANZISHA VILABU VYA UMOJA WA MATAIFA MASHULENI

$
0
0
DSC_0029
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akibadilishana mawazo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kikuyu Mwl. Zaituni Mkoyi alipotembelea shuleni hapo kwa lengo la kuwahamasisha wanafunzi kuanzisha vilabu vya Umoja wa Mataifa. Katikati ni Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo Bw. Francis Tumaini.
DSC_0032
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akisaini kitabu cha wageni cha shule ya Sekondari Kikuyu iliyopo mkoani Dodoma.
DSC_0081
Afisa habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akizungumza na vijana wa shule za sekondari Kikuyu iliyopo mkoani Dodoma, kuwaelezea umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa (UN Clubs) vinavyoanzishwa mashuleni kwa lengo la kuwasaidia kujitambua na nafasi yao kama vijana katika kutekeleza agenda mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Bi. Ledama amefafanua kuwa, kuanzisha vilabu hivyo shuleni hapo kutawawezesha kujifunza shughuli za Umoja wa Mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali ikiwemo na masuala ya Kidiplomasia.

Bi. Usia pia amewafafanulia vijana hao kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa na mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya kufanya kazi za kujitolea.

Pia amewagusia suala la kujiepusha na marafiki wenye tabia mbaya itakayowapelekea kujihusisha na vitendo visivyo vya kimaadili ikiwemo uvutaji bangi na matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili Tanzania kwa sasa, aidha amewasaa kutojihusisha na ngono pindi wawapo mashuleni ili kujiepusha na gonjwa hatari la Ukimwi. (Pichani kushoto ni Mwalimu Cecilia Mwolo na Mwalimu Elias Ndangula na Kulia ni Bw. Laurean Kiiza kutoka UNIC Dar es Salaam).
DSC_0059
Mmoja wa wanafunzi shule ya Sekondari Kikuyu akiuliza swali kwa Afisa Habari wa Kitengo cha Habari (UNIC) hayupo pichani.
DSC_0084
Sehemu ya Wanafunzi vidato mbalimbali wa shule ya Sekondari Kikuyu wakimsikiliza Bi. Usia Nkhoma Ledama.
DSC_0043

SHEREHE ZA JUBILEE YA MIAKA 25 YA KKKT - DMZV ZILIVYOFANA JANA JIJINI MWANZA.

$
0
0
Askofu mkuu wa Dayosisi ya Mwanza Ziwa Victoria (DMZV) Andrew Gulle kabla ya kufunua jiwe maalum la Jubilee alikata utepe kuashiria safari ya maadhimisho hayo kuanza rasmi, ambapo kilele chake kitakuwa tarehe 31 Agosti, 2014.  
Jiwe la jubilee.
Maaskofu waalikwa toka makanisa mbalimbali kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Baada ya tukio la kuzindua jiwe la Jubilee Maaskofu na mamia ya waumini walielekea kwenye jengo la Kanisa kuu la Mwanza kwaajili ya kulizindua.
Kabla ya Uzinduzi wa kanisa la Imani KKKT Mwanza historia ya ujenzi wa kanisa hadi kukamilika ilisomwa naye Bw. Serafin Kimaro. Jumla ya shilingi bilioni moja na milioni 500 zimetumika kukamilisha ujenzi huo uliotumia miaka takribani 13 hadi kukamilika.
Akishuhudiwa na mamia ya waumini na viongozi wa makanisa mbalimbali Kanda ya ziwa na mikoa mingine nchini ukafika wakati sasa wa mgeni rasmi Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa kukata utepe kuzindua kanisa la KKKT Imani Makongoro Mwanza. 


Kisha mgeni rasmi Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa aligonga malango ya kanisa na kuingia ndani kwa mara ya kwanza ikiwa ni rasmi.
Mgeni rasmi Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa alikuwa ni wa kwanza kuongoza msafara wa maaskofu, wachungaji na mamia ya waumini waliohudhuria Jubilee hiyo.
Mkuu wa KKKT Askofu Dr. Alex Geaz Malasusa (kulia) akiongoza ibada ya kuweka wakfu kanisa la KKKT Imani Makongoro akiwa ameambatana na Askofu Andrew P. Gulle wa Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria (DMZV) katikati aliyemshikia kipaza sauti.
Ibada inaendelea.
Kwaya ya Imani KKKT.
Wageni toka mataifa mbalimbali ulimwenguni nao pia wameshiriki maadhimisho ya Jubilee hiyo.
Kwaya alikwa ya KKKT Kijitonyama toka jijini Dar es salaam iliipamba Jubilee.


Nyimbo nzuri nzuri zilisikika.
Wanamuziki wa KKKT Kijitonyama.
Maandari ya kanisa toka juu na upande wa kulia.
Kushoto na kulia hadi mbele kwenye madhabahu.
Kanisa hili limejengwa kwa nguvu za waumini wa ushirika wa Imani, waumini wa sharika nyinginezo na marafiki wa usharika huo na DMZV.
Sehemu waliyoketi Kamati ya maandalizi ya Jubilee na Ujenzi.
KKKT Imani wakitoa huduma ya kiroho kwa njia ya uimbaji.
Sherehe za Jubilee ya miaka 25 ya DMZV ziliambatana na harambee ya ujenzi wa Imani Lutheran Schools mradi endelevu unaotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili za kitanzania hadi utakapokamilika.

Harambee ilifanyika ikiwa na makusudi ya kukusanya zaidi ya shilingi milioni 250 kwaajili ya kuanza ujenzi ambapo kamati ilivuka malengo kwa kukusanya kiasi cha shilingi  milioni 259,280,000/= zikiwemo ahadi, na taslimu ilikuwa kiasi cha shilingi milioni 58,869,000/=.

WAHITIMU WATAKIWA KUELIMISHA JAMII KUTANGAZA BIDHAA ZA TANZANIA

$
0
0
DSCF2810Kulia ni mgeni rasmi Adam Shayo,ambaye ni mkurugenzi wa Taasisi ya elimu ya Sila(SILA VOCATION TRUST ARUSHA) katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu katika  mahafali ya kwanza  chuo cha Biashara na Teknohama Arusha. kushoto ni mkurugenzi wa chuo hicho Valentune Ndanu
DSCF2801Meza kuu wakijiandaa kukabidhi vyeti kwa wahitimu 
DSCF2800Mgeni rasmi Bw. Adam Shayo akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitumu,wapili ni mkurugenzi wa chuo hicho Bw.Valentune Ndanu
DSCF2804Burudani nayo ilichukua sehemu yake
DSCF2797Baadhi ya waalikwa wakiwa wanaangalia burudani
DSCF2798Meza kuu wakijiandaa kukabidhi vyeti kwa wahitimu ngazi ya stashahada
DSCF2807Mgeni rasmi Bw. Adam Shayo katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu

Na Pamela Mollel,Arusha.

Wahitimu katika chuo cha Biashara na Teknohama Arusha(IBICTA)wametakiwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutafuta masoko nje ya nchi kwaajili ya kutangaza  bidhaa za Tanzania hali itakayo saidia  uchumi wa Taifa kuwa juu

Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Sila( SILA VOCATION TRUST ARUSHA) Bw. Adam Shayo juzi wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza chuo cha Biashara na Teknohama Arusha

Alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni pamoja na bidhaa za Tanzania kutotambulika katika soko la kimataifa huku akidai kuwa asilimia kubwa ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zinaubora ukilinganisha na nchi zingine

Aidha aliwata wahitimu kutumia  stashahada zao katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutafuta masoko nje ya nchi kwaajili ya bidhaa zinazozalishwa hapa Nchini

Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho Bw.Valentune Ndanu alisema kuwa waliohitimu  katika chuo hicho ni wanafunzi 10 huku akidai kuwa elimu waliyoipata  wahitimu hao itawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu 

Pia alitaja faida nyingine  watakayofaidika nayo ni pamoja na kutambua fursa  zilizopo sanjari na kujiingiza katika ujasiriamali hali itakayowasaidia kuwa na ajira ya kudumu

Malengo ya chuo hicho ni kutoa digrii ya biashara na teknohama hali itakayosaidia vijana kujiingiza katika ujasiriamali,

WAZEE WA NGWASUMA WALIVYOWAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA MWISHONI MWA WIKI

$
0
0

DSCF2780Wazee wa ngwasuma wakiburudisha mashabiki  ndani ya triple a night club-Arusha siku ya wapendanao tarehe 14/2/2014 kwa udhamini mnono wa kampuni ya Megatrade  Investment kupitia kinywaji chake cha K-vant Gin
DSCF2770Wapili kushoto ni Meneja mauzo na masoko Goodluck Kway wa kampuni ya Megatrade  Investment akiwa katika meza ya pamoja na wadau siku ya valentine’s day
DSCF2771Lema moters a. k.a mutu ya pesa naye alikuwepo kwa wazee wa ngwasuma
DSCF2759Mashabiki wakiwatunza wazee wa masauti”Fm Academia”
DSCF2766Mpiga drum akifanya yake siku ya valentine day
DSCF2772Wadau wakishow love ndani ya FM ACADEMIA
DSCF2783Mashabiki wakifanya yao wakati wazee wa ngwasuma wakitoa burudani
DSCF2778Jailos Joseph wa Megatrade akiyarudi ndani ya stage…kushoto ni mdau wa jamiiblog
DSCF2781
DSCF2784Wazee wa masauti wakifanya yaooooooooooooooooo
DSCF2788Meneja mauzo na masoko Goodluck Kway wa kampuni ya Megatrade  Investment akiwa katika picha ya pamoja na warembo waliopendaza siku ya valentine day mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao
DSCF2768

Tanzania kushirikiana na ufaransa katika masuala ya mabadiliko ya Tabianchi

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mheshimiwa Dr Bilinith Mahenge (wa kwanza kushoto) akifutiwa na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Bwana Marcel Escure( kulia)Ofisini kwa Waziri wa Mazingira, wakizungumzia masuala ya Mazingira kuhusu mabadiliko ya Tabianchi na jinsi Tanzania itakavyoweza kushirikiana na ufaransa katika kufanya kazi kwa pamoja . Picha zote kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mheshimiwa Dr Bilinith Mahenge (wa kwanza kushoto)akizungumza na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Bwana Marcel Escure (pili kushoto), jinsi Tanzania itakavyoweza kushirikiana na Ufaransa katika kukabiliana na masuala ya mabadliko ya Tabianchi na watakavyofanyakazi kwa pamoja. Wa pili kulia ni Msaidizi wa Balozi wa Ufaransa Bwana Frangois Leonardi na ( wa kwanza kulia) ni Mkurungenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Richard Muyungi anayeshughulikia masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais.

TANGAZO RASMI KUTOKA UONGOZI WA SWAHILI MEDIA GROUP

$
0
0
Uongozi wa Swahili Media Group unapenda kuufahamisha umma kuwa Alex Kassuwi sio mtendaji wala mkurugenzi katika kampuni hii na tunapenda kuwatahadharisha wadau wote  kuacha kuwasiliana  au kufanya mikataba  ya aina yeyote kwa jina la Swahili Media Group na  kampuni zake tanzu na Kassuwi kwani haitatambuliwa.

Kuhusu taarifa potofu ambazo zimekuwa zikitolewa na aliyekuwa hisa  mwenza  katika kampuni hii Bwana Alex Kassuwi.


Kwa mujibu wa kumbukumbu zetu, Alex Kassuwi sio mmiliki na hahusiki na uendeshaji wa Swahili Media Group kuanzia mwezi Januari 21, 2014 baada ya wanahisa na menejimenti  kumuondoa kwa maslahi ya kampuni hii ni baada ya  kumsimamisha tangu mwezi Octoba 2013 kutokana na ubadhilifu wa mali za kampuni ambao aliufanya akiwa mmoja wa wakurugenzi wa  Swahili Media Group.


Katika kikao hicho Bwana Alex alikiri kuiba mali za kampuni zenye thamani ya zaidi ya dola $15,000 na kuzipeleka kuweka rehani (Pawn Shop) bila ya idhini ya uongozi, alikubaliana na hukumu ya kusimamishwa katika nafasi ya menejimenti na kubakia mwana hisa tu.ushahidi wa nyaraka za wizi kutoka Pawn Shops na mazungumzo ya mkutano yalirekodiwa.


 Januari 8,2014 Bwana Alex aliomba  arudishwe kwenye  menejimenti na uendeshaji wa siku kwa siku wa kampuni, kwa njia ya email baada ya jitihada zake za kuomba kwa njia ya simu na text kushindikana, menejimenti ilikataa ombi lake la kumrudisha kazini hasa ikizingatiwa kwamba  nafasi hiyo itaweza kumuweka karibu na vyombo vya ofisi ikiwemo vile  ambavyo aliviiba awali lakini alifahamishwa kuwa hisa zake zitaendelea kuwepo.


Januari 19, 2014 Bwana  Alex aliomba kujiondoa rasmi kwenye kampuni kama mmoja wa wanahisa ombi  ambalo lilikubaliwa rasmi Januari 21 baada ya kikao cha wanahisa na menejimenti kumkubalia.


Kwa taarifa hii, tunawaomba wadau wote kutambua  kuwa Alex Kassuwi sio mfanyakazi wala mkurugenzi  na hivyo haruhusiwi kuisemea  wala kufanya  mikataba yeyote ya Swahili Media Group ikiwemo maidhinisho kwa niaba ya Swahili Media Group.


Uongozi wa Swahili Media Group unamtakia Mafanikio mema bwana Kassuwi popote aendako.

Uongozi


Swahili Media Group / Swahili Media International.

Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images