Mgombea wa Chadema jimbo la Kalenga Grace Tendega akipunga mkono kwa wanachama wa chama hicho waliompokea katika eneo la Igumbiro Km 8 toka mjini Iringa
Jeshi la polisi likiwa tayari limejipanga kuweza kuwazuia wanachama wa Chadema waliokuwa wametoka kumpokea mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga na askari akiwa mbele ya gari la waandishi akiwazuia kupita (picha zote na Denis Mlowe)
Baadhi ya wanachama wa Chadema wakiwa katika foleni ya kumsindikiza mgombea wao Grace Tendega kuchukua fomu za kugombea jimbo la Kalenga
Jeshi la polisi likiwa tayari limejipanga kuweza kuwazuia wanachama wa Chadema waliokuwa wametoka kumpokea mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga na askari akiwa mbele ya gari la waandishi akiwazuia kupita (picha zote na Denis Mlowe)
Msamamizi wa Uchaguzi jimbo la Kalenga Pudenciana Kisaka akimkabidhi fomu za kugombea uchaguzi wa ubunge jimbo la hilo Grace Tendega wa Chadema katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa jana.
========== ========= =========
TENDEGA ACHUKUA FOMU ZA UBUNGE JIMBO LA KALENGA
Na Denis Mlowe,Iringa.
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema), Garce Tendega jana amechukua fomu ya kuwani kiti hicho huku msafara wake ukikumbana na kizuizi cha Jeshi la Polisi Mkoani hapa kutokana na kutokuwa na kibali cha kuandamana na kumshikiria diwani wa kata ya Mivinjeni Frank Nyarusi.
Msafara huo ulipokelewa maeneo ya Igumbiro kilometa 8 toka Iringa mjini ukiwa unasindikizwa na pikipiki zaidi ya 50 na magari ya M4C zaidi ya 4 na gari nyingine ndogondogo 6 na kusababisha msafara huo kusimama zaidi ya saa moja baada ya jeshi la polisi kuwazuia katika mlima Ipogoro.
Maafisa wa Polisi waliofika kuzuia masafara huo walisemna wasengeweza kuruhusu kupita katikati ya mji kwa madai hayo ni maandamani batili na kusababisha ubishani kati ya uongozi wa jeshi hilo na waratibu wa mapokezi ya mgombea huyo.
Akizngumza mara baada ya kuchukua fomu, Grace Tendega alisema moja ya changamoto ambayo inampa nafasi ya kushinda uchaguzi huo mdogo ni wapinzani kujenga woga hadi kufikia hatua ya kutumia jeshi la polisi kuwazuia kwenda kuchukua fomu za kugombea.
“ Huu ni mwanzo tu wa mapambano ya kulikomboa jimbo la Kalenga kutoka kwa chama tawala ambacho kwa miaka zaidi ya Hamsini maisha ya wananchi wamebaki kuwa na maisha yale yale ni zamu yetu sasa kuwakomboa wanakalenga na Tanzania kwa jumla hivyo wananchi wakinipa ridhaa hakika nitawaletea maendeleo kwa kushirikiana nao” alisema Tendega.
Mgombea huyo alisema Chadema kimejiandaa kushinda na kilichotokea katika msafara wake ni mwanzo tu wa mapambano hivyo chama kiko tayari kwa mapambano ya kuwapata wapiga kura wataoweza kuwaondoa madarakani .
Tendega aliwataka wakazi wa Jimbo la Kalenga kutokuwa na hofu kutokana na matukio yanayoweza kujitokeza kama lilivyotokea la kuzuiliwa na jeshi la polisi ila wajitokeza kwa wingi kuunga mkono harakati hizo za ukombozi.
Alisema wananchi wa jimbo la Kalenga wanatakiwa wachague kiongozi atakayewafaa na si kuwatesa na kuwatumiakia na sio kuwatawala katika kuwaletea maendeleo ya jimbo la Kalenga.
Mgombea huyo alifanikiwa kuondoka maeneo hayo baada ya jeshi la polisi kumruhusu kuondoka maeneo hayo bila msafara wa magari na pikipiki hizo hadi katika ofisi zaMsimamizi wa uchaguzi Pudenciana Kisaka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jimbo la Iringa Vijijini na kukabidhiwa nyaraza mbalimbali za tume ya taifa ya uchaguzi zikiwamo sheria kanuni na katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa na mgombea wa Chadema atapambana na mtoto wa marehemu Dk Mgimwa anayejulikna kwa jina la Godfrye Mgimwa.