Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 224 | 225 | (Page 226) | 227 | 228 | .... | 1903 | newer

  0 0

   WAKATI taratibu za kupatikana kwa kibali cha Tamasha la Pasaka mwaka huu zikifanyika, mikoa nane ya Tanzania bara imeomba tamasha hilo lifanyike kwenye mikoa hiyo. 

  Kwa mujibu wa habari kutoka katika mikoa hiyo, wanalihitaji tamasha hilo kwa sababu mbalimbali zikiwemo kumtukuza Mungu kupitia nyimbo na Mapambio kupitia waimbaji wa Kitaifa na Kimataifa.

  Walisema manufaa mengine wanayoyapata kupitia tamasha hilo ni kutoa michango yao kwa wenye uhitaji maalum hasa utekelezwaji wa kituo cha wenye uhitaji maalum kitakachojengwa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

  Mikoa ambayo iliomba kufikiwa na tamasha hilo ni pamoja na Morogoro, Iringa, Dodoma, Mbeya, Kahama, Mwanza, Njombe na Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ndio waandaaji wa Tamasha hilo, Alex Msama alisema hivi sasa wanasubiri taratibu za upatikanaji wa kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili waanze taratibu za kufuatilia tamasha hilo.

  Msama alisema  tamasha la mwaka huu wamejipanga kuwafikia wadau wengi zaidi ili kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu kupitia Waimbaji wa ndani na nje.

  Aidha Msama alisema hawana cha kuwaeleza wadau hao wa mikoani kwa sababu taratibu za kibali hazijakamilika, lakini wanayafanyia kazi.

  0 0

   Moja ya mabango yaliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru nchini. Hafla hii ilifanyika muda mfupi kabla Rais Kikwete hajapanda ndege kuelekea London, Uingereza, kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kupanga mikakati ya kupambana na ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na faru.
   Rais Jakaya Kikwete (kulia) akibofya kwenye kompyuta kuzindua rasmi  mabango hayo ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru  kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Mahamoud  Mgimwa. 
   Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Far baada ya kuyazindua rasmi kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam 
   Moja ya mabango hayo likiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
   Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Farubaada ya kuyazindua rasmi kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk. Mahamoud  Mgimwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said  Meck Sadick.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji amewapongeza Wakuu wa Mikoa wa Kanda ya Ziwa katika juhudi zao za kuhakikisha Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa linafanyika.

  Mikoa ambayo itashiriki katika Kongamano la Uwekezaji la Kanda ya Ziwa ni Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga Kongamano ambalo kwa pamoja litawakutanisha Wawekezaji pamoja na Serikali katika kujadili vivutio vya Uwekezaji vinavyopatikana katika mikoa hiyo ya kanda ya Ziwa.

  Kituo cha Uwekezaji Kimejizatiti kushirikiana na Mikoa katika kuhakikisha kuwa wawekezaji wanapatiwa huduma zinazohitajika katika Mikoa.

  Kituo cha Uwekezaji na Mikoa wamekubaliana kushirikiana na kuhakikisha kupatikana kwa Ardhi katika Mikoa ili iweze kuwekwa kwenye Benki ya Ardhi kwa ajili ya kupatia Wawekezaji na pia kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu sheria na taratibu zinazomtaka muwekezaji kuzifuata kabla ya kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

  Kituo cha Uwekezaji pia kitafanya kazi na Makatibu Tawala wa Mikoa ili kujenga uwezo ili nao waweze kusimamia utoaji wa huduma vizuri kwa wawekezaji katika mikoa yao.

  Kwa maelezo zaidi kuhusu Kongamano la Uwekezaji Tanga na Vivutio vya Uwekezaji vinavyopatikana Kanda ya Ziwa tembelea tovuti ya www.lakezoneinvestmentforum.go.tz
  Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji TIC,Bi Juliet R. Kairuki (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa mikoa ya kanda ya ziwa,toka kushoto ni Mhe. Chief Kishosha Pascal Mabiti (Mkuu wa Mkoa Simiyu); Eng. Evarist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa Mwanza) Mhe. Magalula Said Magalula (Mkuu wa Mkoa, Geita); Mhe. John Gabriel Tuppa (Mkuu wa Mkoa Mara); Col Phabian Massawe (Mkuu wa Mkoa Kagera); Mhe. Ali Nassor Rufunga (Mkuu wa Mkoa Shinyanga)

  0 0

   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ilala, Jesca Njau (kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi wodi ya watoto wachanga Katika Hospitali ya Rufaa ya Amana Ilala iliyokarabatiwa kwa msaada kampuni hiyo, Dar es Salaam jana.  Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali hiyo, Dk. Mtagi Kibatala, Mhandisi wa TBL, John Malisa na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Meshack Shimwela. TBL ilitumia sh. mil. 68 kukarabati wodi hiyo na miundombinu yake. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Jesca Njau akipongezwa na Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali hiyo, Dk. Mtagi Kibatala,
   Dk. Kibatala akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo ambao alidai umepunguza kwa asilimia kubwa kupunguza adha kwa wazazi waliozaa watoto njiti.

   Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Shimwela akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo mkubwa wa ukarabati wa wodi ya wazazi na miundombinu ya maji.
   Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu  akielezea mikakati ya kampuni hiyo katika kusaidia jamii katika sekta ya maji, ambapo katika mkoa wa Dar es Salaam TBL imetumia sh. mil 450 kuboresha sekta ya maji katika vituo mbalimbali vya afya.
   Mzazi alyejifungua mtoto njiti Mariam Mbwambo, akitoa shukurani kwa TBL kwa msaada huo ambao alisema umesaidia kupunguza kero waliyokuwa wanaipata kukaa na watoto hao ambao wanahitaji uangalizi mkubwa.


   Mjkazi wa Msimbazi Bondeni, Febi Joramu akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo muhimu wa wazazi.
   Jesca Njau akizungumza na Mariamu baada ya kukabidhi eneo hilo lililokarabatiwa.
                                                     Moja ya vyoo vilivyokarabatiwa
   SDehemu ya mabomba yiliyokarabatiwa

  Muuguzi Kiongozi wa Wodi ya Wazazi, Mercy Maleko akionesha choo kilichokarabatiwa cha watumishi wa wodi hiyo.

  0 0

   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets British Foreign Secretary William Hague in his London office this evening. The two leaders then held talks on bilateral issues concerning their two countries.
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, British Foreign Secretary William Hague and Tanzania’s Minister for Foreign Relations and International Cooperation Bernard Membe pose for a photograph shortly after they met Mr.Hague in his London office this evening.President Kikwete is in London to attend the London Conference on Illegal Wildlife Trade
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete with British Foreign Secretary William Hague in London  this evening after the  two leaders  held talks on bilateral issues concerning their two countries. Photos by Fred Maro

  0 0

   Mwezeshaji  wa jamii wilaya ya Mtwara, Yusufu namoto, akisoma majini ya kaya masikini zitakazoingia katika mpango wa kunusuru kaya masikini katika mkutano wa kijiji cha Chawi wilayani humo ambapo ujumbe wa tasaf makao makuu ukiongozwa na mkurugenzi mtendaji. Ladislaus Mwamanga, mwakilishi wa benki ya dunia Ida manjolo.
  Wananchi katika mkutano wa kijiji cha Chawi 

   Mkurugenzi  Mtendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF) Bw. Ladislaus Mwamanga, (mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji cha Chawi wilaya ya Mtwara mkoani hapa mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kijiji uliothibitisha majina ya kaya masikini zitakazoingia katika mpango wa kunusuru kaya masikini, kushoto kwake ni mwakilishi wa benki ya dunia Ida Manjolo
  Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini. Ladislaus Mwamanga, (mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji cha Chawi wilaya ya Mtwara mkoani hapa mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kijiji uliothibitisha majina ya kaya masikini zitakazoingia katika mpango wa kunusuru kaya masikini, kushoto kwake ni mwakilishi wa benki ya dunia Ida Manjolo .  =========   =======  ========
   Na Hassan Simba, Mtwara 
  IMEELEZWA kuwa kufikishwa kwa elimu juu ya mpango wa kunusuru kaya masikini unaoendeshwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini tasaf awamu ya tatu, ndio chachu ya mafanikio ya mpango huo yaliyokwishaanza kuonekana kwa jamii ya wakazi wa Mtwara. 
  Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa mfuko huo Bw. Ladislaus Mwamanga, alipokuwa anaongea na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Idd Mshili, ofini kwake alikokwenda kumtembelea kabla ya kwenda vijijini kujionea namna mpango huo unavyotekelezwa wilayani humo. 
  Bw. Mwamanga alisema kuwa chini ya mpango huo wawezeshaji wamelimishwa vizuri na wao wanaweza kufikisha ujumbe kwa jamii na baada ya kuanza kuelewa ndio maana kumekuwa na mwitikio chanya katika maeneo yote ambako mradi huo umeanza kutekelezwa. 
  "Ndugu mkurugenzi hayo mafanikio unayoanza kuyaona hata kabla ya kuanza kutolewa kwa ruzuku kwa kaya masikini ni matokeo ya elimu ambayo tumewapatia jamii...kwa hakika tumepata mwitikio mzuri kila tulikoenda na hii inatutia faraja na kutuongezea hali ya kufanyakazi kwa bidii", alisema Mwamanga. 
  Mkurugenzi huyo aliyasema hayo baada ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuueleza ujumbe wa tasaf makao makuu uliomuhusisha mwakilishi kutoka benki ya dunia.Idda Manjolo. kwamba tayari mafanikio ya mpango huo yameshaanza kuonekana katika wilaya yake hata kabla ya ruzuku kuanza kutolewa kwa kaya masikini. 
  "Nataka niwaambie tu kwamba wakati nyinyi mnasema mpango huu upo katika hatua ya pili ambayo ni kutambua kaya masikini na hatua ya tatu ndio itakuwa ya kuanza kutoa ruzuku lakini hapa kwetu tumeanza kuona mafanikio...uandikishaji wa watoto wa darasa la kwanza umevuka lengo na wakinamama wanaohudhuria kliniki imeongezeka mara dufu", alisema Mshili. 
  Mshili alisema kuwa kwakua mpango huo unalenga pia kutoa ruzuku kwa kaya masikini ambazo watoto wao wanahudhuria shuleni kaya nyingi zimehamasika kuandikisha watoto wao na kufuatilia mahudhurio yao ili kuweza kupata sifa ya kupata ruzuku hiyo na hjivyo kufanya maeneo mengi kuvuka malengo ya uandikishaji waliyojiwekea.
   Mkurugenzi huyo alisema kuwa hiyo ni hatua kubwa ya mafanikio kwani katika kipindi cha nyuma wataalamu wake wamekuwa wakiwahimiza wananchi kuwapeleka watoto wao shuleni na wakinamama kuhudhuria kliniki lakini mwitikio ulikua mdogo kulinganisha na baada ya kuanza kwa mpango huo wa tasaf. 
  Akiwa katika kijiji cha Chawi alikukonda kuona namna ambavyo wanakijijikupitia mkutano wao mkuu wa kijiji wanachaguana kuongoza kamati ufuatiliaji na kuthibitisha majina ya kaya masikini, mkurugenzi huyo alisifu uwazi katika uendeshaji wa zoezi na uelewa mkubwa wa wawezeshaji juu yanmpango huo. 
  Mwamanga alisema chini ya mpango huo uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete 2012 na kuanza kwa majaribio katika wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino, kaya masikini zinapatiwa ruzuku katika elimu, afya na kujikimu kimaisha kila mwezi kwa miaka mitatu ambapo hadi sasa halmashauri 22 zimekwishafikiwa. 

  Mwamanga alisema kwa namna walivyojipanga hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu halimashauri zote kwa upande wa Tanzania bara na visiwani zitakuwa zimefikiwa na mpango huo ambao unalenga kupunguza umasikini miongoni mwa jamii nchini.

  0 0

  Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (wakatikati) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wanne wa kujadili juu ya viwango na uzibiti wa ubora kwenye bidhaa, uliofanyika Zanzibar Beach Resort Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
   Afisa Mkuu wa Viwango Jumuiya ya Africa Mashariki Willy Musinguzi akielezea changamoto wanazokabiliana nazo juu uzibiti wa bizaa zisizo na viwango katika Mkutano wa bodi ya ufundi ya nchi za Africa (EASC) uliofanyika Zanzibar Beach Resort nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
   Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akifungua Mkutano wanne wa kujadili juu ya viwango na uzibiti wa ubora kwenye bidhaa, uliofanyika Zanzibar Beach Resort nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

   Wajumbe wakimsikiliza wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (hayupo pichani) katika Mkutano wa bodi ya ufundi ya nchi za Africa (EASC) wakujadili viwango na uzibiti wa ubora kwenye bidhaa uliofanyika Zanzibar Beach Resort.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akishuka kwenye ndege wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo,tayari kwa ufunguzi Kongamano la uwekezaji kwa Kanda ya Ziwa,linaotarajiwa kuanza kesho kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini,Mh. Charles Kitwanga.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ambao ndio waratibu wa Kongamano hilo,Bi. Julieth Kairuki,wakati wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo.Makamu wa Rais yupo jijini Mwanza kwa ajili ya Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji kwa Kanda ya Ziwa,linalotarajiwa kuanza kesho kwenye Hoteli ya Malaika,jijini humo. 
   Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanali Mstaafu Fabian Massawe wakati walipotembelea hoteli ya Malaika kukagua maendeleo ya Maandalizi ya Kongamano hilo litakalofunguliwa na Makamu wa Rais,Dkt. Mohammed Ghalib Bilal.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ambao ndio waratibu wa Kongamano hilo,Bi. Julieth Kairuki 


  0 0
 • 02/12/14--21:40: Article 20


 • 0 0

  DSC_0046

  Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama, akitoa mafunzo ya maadili na jinsia kwa waandishi wa habari na watangazaji wa Redio za Jamii nchini yanayolenga kuwajengea uwezo katika utendaji wa kazi zao kwenye vituo vyao.
  Mafunzo hayo ya siku tano yamefadhiliwa na Shirika la UNESCO kupitia mradi wa Demokrasia na Amani kuelekea uchaguzi 2015.
  DSC_0012
  Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa somo kwa washiriki wa Semina ya siku tano ya Maadili na Jinsia inayolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari na watangazaji wa Redio za Jamii nchini iliyofadhiliwa na UNESCO kupitia mradi wa Demokrasia na Amani kuelekea uchaguzi 2015 inayoendelea mjini Dodoma.
  DSC_0020
  Pichani juu na chini ni Baadhi ya watangazaji na waandishi wa habari kutoka Redio mbalimbali za Jamii wakifuatilia mafunzo hayo yanayoendelea mjini Dodoma.
  DSC_0009DSC_0052DSC_0119
  Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari na watangazaji wa redio za jamii wakichangia maoni kwenye mafunzo ya siku tano yanayoendelea mjini Dodoma.
  DSC_0134DSC_0169
  Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka redio Triple A FM ya jijini Arusha Grace Damian akizungumzia changamoto mbalimbali zinazozikabili Redio za Jamii nchini.

  0 0

   Mkurugenzi wa Mipango Mikakati wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Jaffar Machano akifungua mkutano huo wa hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano.
  ********

  Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank) na Benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Development Bank of Southern Africa, DBSA) zimeingia mkataba wa makubaliano ya kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini jana jioni.

  Makubaliano hayo yatasaidia kufufua miundombinu ya uchukuzi ikiwemo Reli ya Kati, Viwanja vya Ndege vya Arusha na Mwanza pamoja na Upanuzi wa Bandari. Zifuatazo ni picha mbalimbali za hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana jioni.
   Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Peter Noni akizungumza na wadau wakati wa hafla hiyo.
   Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (DBSA), Patrick Dlamini akizungumza na wadau katika hafla hiyo.
   Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Kiserikali,Bunge na Binafsi wakifuatilia matukio ya hafla hiyo.
   Kutoka kushoto ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick Dlamini, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Peter Noni wakifuatilia kwa makini sehemu ya matukio wakati wa hafla hiyo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank), Peter Noni (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick Dlamini (wa pili kushoto) wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi huku ukishuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia waliosimama) na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia waliosimama). Kushoto (waliokaa) ni Meneja Mkuu wa Fedha wa DBSA, Bane Makene na Mwanasheria wa Bodi ya TIB Development Bank, Martha Maeda (kulia). 
   Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank), Peter Noni (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick Dlamini (wa pili kushoto) wakibadilishana nyaraka baada ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Fedha wa DBSA, Bane Makene na Mwanasheria wa Bodi ya TIB Development Bank, Martha Maeda (kulia).
  Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe wakizungumza na washiriki wa hafla hiyo.

  0 0

  DSCF2699Kaimu kamishna Mkuu wa wa Mamlaka ya mapato Tanzania Rished Bade akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha kuhusu mgomo wa wafanyabiashara hapa Nchini
  DSCF2695Waandishi wa habari wakiwa kazini
  DSCF2697Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo
  DSCF2713Mr.Jangala ambaye ni Ajenti wa usafirishaji wa magari ya mikoani akilalamikia hali ya wafanyabiashara kugoma ambapo anadai kuwa imemuathiri kwa kiasi kikubwa kukosa abiria wanaokuja kununua bidhaa za jumla
  DSCF2700
  DSCF2706Shughuli mbalimbali zilidorora hata zile za M-pesa
  DSCF2711Hapa maduka yakiwa yamefungwa kama inavyoonekana katika picha eneo la maduka ya stendi mabasi yaendayo Moshi
  DSCF2712
  DSCF2708Muonekano katika stendi kubwa ya mabasi baada ya mgomo wa wafanyabiashara

  Na Pamela Mollel,Arusha
  Wafanyabiashara hapa nchi wametakiwa kutoendeleza mgomo  wa mashine za kieletroniki za EFD’S na badala yake wafungue maduka na kuendelea na biashara zao kwa kutumia mashine  kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza masharti ya kufanyabiashara.

  Rai hiyo aliitoa jana Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania Rished Bade wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha ambapo alisema kuwa kitendo cha kutumia mashine kwa wafanyabiashara itawawezesha kuweka  kumbukumbu sahihi.

  Alisema kuwa kodi ya ongezeko la dhamani ilikuwa kwenye awamu ya kwanza hivyo  awamu ya pili wafanyabiashara hawatahusika kulipa kodi kama wengine wanavyodai
  “siyo kweli kwamba wakitumia mashine watafilisika bali watakuwa na kumbukumbu sahihi…na kuna watu wachache wanapotosha wafanyabiashara kwa hili” alisema Bade.

  Aidha aliwataka wafanyabiashara kutokubali kutumika na wasiowafanyabiashara ambao wamekuwa  wakiwashawishi kufunga maduka ili kushinikiza serikali bali wawaripoti katika mamlaka husika ili sheria ichukue mkondo wake

  0 0

   Mkuu wa Huduma za Utangazaji na Mawasiliano ya redio kutoka Shirika la Utangazaji la Kimataifa (ITU), Pham Nhu Hai akiwasilisha mada katika kongamano hilo.
   Mjadala ulifautiliwa kwa umakini na washiriki
   Muongozaji wa mjadala huo, Simon Spanswick (kushoto) ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ITU akiwa katika mjadala la na Pham Nhu Hai.

   Maswali na maoni mbalimbali yalitolewa kutoka kwa washiriki wa kongamano hilo la uhamaji wa mfumo wa utangazaji kutoka Analojia kwenda Dijitali.
   Mkurugenzo Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkoma nae alishiriki kikamilifu katika mijadala mbalimbali ukiwepo ule wa namna gani nchi za Afrika zitaendelea katika kipindi cha miaka 5 - 10 katika sekta ya utangazaji.
   Mhandisi Mwandamizi wa Utangazaji kutoka TCRA, Andrew Kisaka ambaye aliwasilisha mada juu ya majitaji ya kiufundi katika matumizi ya DVB-T.
   Baadae palikuwa na tafrija kidogo ya 'Mkia wa Tausi' Cocktail na mambo yalienda vyema kwa mazungumzo ya hapa na pale ya wadau.

   Mkurugenzi wa Azam TV nae alikuwepo kufuatilia mijada hiyo na hapa akiwa na wadau wenzake.
   
   Ilikuwa ni bata kwenda mbele kwa washiriki.
   Burudani kutoka kwa kundi la kimasai lilikuwepo na kumfanya Katibu Mtendaji wa Shirika la Utangazaji la Jumuia ya Madola (CTO), Tim Unwin kuamua kuchukua taswira zao
   Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi alikuwa akipita akifuatisha midundo ya Kimasai
   Burudani hapa ilinoga vilivyo.

  0 0

   Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea barua kutoka kwa Mhe. Spika wa BUNGE la Jamhuri ya Muungano Tanzania ya kuiarifu uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Kalenga lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. William Mgimwa aliyefariki dunia tarehe 1/1/2014. Baada ya taarifa hiyo Tume imepanga ratiba ya Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga kama ifuatafyo:-

  1.     Uteuzi wa Wagombea Ubugne utafanyika tarehe 18-Februari-2014 

  2.     Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 19-Februari-2014 hadi 15-Machi-2014 

  3.     Siku ya kupiga kura ni Jumapili terehe 15-Machi-2014 

  Wagombea wanatakiwa kuwasilisha Fomu za Uteuzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa JImbo la Kalenga siku ya Uteuzi si zaidi ya Saa 10:00 Alasiri. Tume inawataarifu Wananchi wote pamoja na Vyama vya Siasa kufuata ratiba iliyotolewa pamoja na kushiriki katika mchakato mzima wa Uchaguzi kuanzia siku ya Uteuzi hadi siku ya Kupiga Kura ili watimize haki yao ya Kikatiba ya Kuchagua viongozi wanaowataka.

  Tume inawasisitiza wananchi wote katika maeneo husika kujitokeza kukagua taarifa zao wakati wa kuweka wazi Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuona kama kuna marekebisho madogo yanahitajika kufanyika kuwawezesha kupiga Kura bila malalamiko yoyote. Ikumbukwe kwamba hakutakuwa na uandikishaji mpya wa Wapiga Kura.


  J. Mallaba
  MKURUGENZI WA UCHAGUZI  0 0

   Naibu Katibu Utumishi  Bw.HAB Mkwizu (kushoto) akizungumza na wataalam wa kujitolea kutoka Japan katika hafla fupi ya kuwakaribisha nchini iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais,Utuimishi.Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa JICA Tanzania Bw. Shinya Tomonari.
  Naibu Katibu Mkuu  Utumishi Bw.HAB Mkwizu (wa pili kutoka kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa kujitolea  wa fani mbalimbali kutoka Japan waliokuja kutoa huduma katika sekta mbalimbali nchini.

  0 0

  Yametimia polisi  wamemakamata  mwenyekiti wa chama cha  waandishi wa habari  mkoa  wa Iringa (IPC) Frank Leonard (kushoto) ambae ni mwandishi wa magazeti ya  serikali  wakimtuhumu kupiga  picha mahakamani ,hadi  sasa amewekwa  chini ya ulinzi wa polisi huku kesi ya mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi ikiendelea kusomwa. Picha na Francis Godwin-Iringa. 

  0 0

    Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia akieleza kwa waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) kuhusu Mikakati Madhubuti ya ukusanyaji mapato na Matumizi bora ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri zote nchini, wakati wa Mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene.
   -Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano wa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia, Katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Hassan Silayo.  MAELEZO YA WAZIRI WA NCHI OWM-TAMISEMI KWA VYOMBO YA HABARI KUHUSU USIMAMIZI NA UDHIBITI WA FEDHA KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

  1.                 UTANGULIZI

  Usimamizi wa fedha katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa unaongozwa na Sheria, Kanuni na Taratibu mbalimbali ambazo ni pamoja na:-

  i.       Sheria ya Fedha ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Sura ya 290  ambayo inaainisha Mamlaka na taratibu mbalimbali zinazohusu Usimamizi wa fedha kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

  ii.    Sheria ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 na kanuni zake za Mwaka 2005.

  iii.Kanuni za Usimamizi wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo ni Mwongozo katika utaratibu na Usimamizi wa fedha kama ifuatavyo:-

         Memoranda ya usimamizi wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 1997 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009 (Local Government Financial Memorandum),

         Kanuni za Kudumu za Halmashauri,

         Kanuni za uanzishaji na uendeshaji wa Bodi za Zabuni katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za mwaka 2007,

         Mwongozo wa uhasibu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (Local Authority  Accounting Manual) wa mwaka 2009,

         Mwongozo wa ukaguzi wa ndani wa mwaka 2005, na

         Mwongozo wa mipango na bajeti unaotolewa kila mwaka.

  Usimamizi wa Sheria na Kanuni tajwa hapo juu ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora katika usimamizi wa fedha. Katika masuala haya, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI inasimamia kwa karibu kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatekeleza majukumu yake inavyopaswa.

  Usimamizi wa fedha katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa umegawanyika katika maeneo makuu yafuatayo:-

  1.     Vyanzo vya fedha (Financing Resources) - fedha za kuendeshea shughuli mbalimbali za Halmashauri;

  2.     Utumiaji wa fedha (Uses of Finance) - matumizi ya fedha zilizokusanywa na kupokelewa; na

  3.     Udhibiti wa rasilimali (Controlling of Resources) - Namna ya kudhibiti ubadhirifu au upotevu wa aina yeyote ile unaohusu rasilimali za Serikali za Mitaa.


  2.                 VYANZO VYA FEDHA ZA MAMLAKA ZA SERIKALI  ZA MITAA

  Wajibu wa msingi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ni kutoa huduma za msingi za kijamii na kusimamia Utawala Bora. Gharama za utoaji huduma hizo unatokana na mapato ya kodi, ushuru na ada mbalimbali, ruzuku toka Serikali Kuu, pamoja na misaada toka kwa Washirika wa Maendeleo na Mikopo kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za fedha. Hivyo vyanzo vya fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa kisheria vimegawanyika katika makundi matatu yafuatayo:-

  2.1            Mapato ya Ndani (Own Source Revenue).

  Kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali  za Mitaa Sura ya 290 Kifungu cha 6, 7, 8 na 9 vyanzo mbalimbali vya mapato vimeainishwa kwa Halmashauri za Jiji, Miji, Wilaya na Vijiji. Vyanzo vilivyotajwa katika Vifungu hivyo vinatoa nafasi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa husika kutunga Sheria Ndogo zitakazowezesha Mamlaka hizo kukusanya mapato kutokana na vyanzo hivyo. Miongoni mwa mapato hayo ni ushuru wa leseni, ushuru wa kodi ya huduma, ushuru wa mazao, Kodi ya majengo, ushuru wa magulio na masoko na ada za kuegesha magari.

  Mapato ya Halmashauri kutoka vyanzo vyake vya ndani kwa miaka nane (2005 -2013) iliyopita yanaonesha kuwa makisio na makusanyo ya mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekuwa yanaongezeka. Mfano, kwa miaka mitano iliyopita yaani Mwaka 2008/09 makisio yalikuwa ni shilingi bilioni 107.6 na makusanyo halisi yalikuwa shilingi bilioni 93.7 ambayo ni asilimia 87 ya makadirio. Kwa mwaka wa fedha 2009/10 makadirio yalikuwa shilingi bilioni 130.9 ambapo makusanyo yalikuwa shilingi bilioni 117.8 sawa na asilimia 90 ya makadirio. Mapato haya yameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kufikia Mwaka 2012/13 makadirio yalikuwa kukusanya shilingi bilioni 328.4 na makusanyo yalikuwa shilingi bilioni 240.9 sawa na asilimia 73.3. Ongezeko la makadirio kwa miaka hii nane yaani kutoka 2005/06 hadi 2012/13 ni sawa na asilimia 512.9wakati makusanyo yameongezeka kwa asilimia 389. Mtiririko wa mapato hayo kwa kipindi hicho ni kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo:

  Mwenendo Wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri kuanzia Mwaka 2005/6 Hadi Mwaka 2012/13

  Mwaka

  Makadirio

  Makusanyo Halisi

  % Ya Makusanyo

  2005/06

  53,593,591,293

  49,291,049,660

  92.0

  2006/07

  63,385,237,737

  61,411,259,961

  96.9

  2007/08

  80,136,598,991

  79,770,210,999

  99.5

  2008/09

  107,628,203,817

  93,752,903,592

  87.1

  2009/10

  130,887,328,313

  117,783,506,345

  90.0

  2010/11

  175,084,789,727

  158,279,374,601

  90.4

  2011/12

  310,962,562,609

  195,524,503,634

  62.9

  2012/13

  328,450,131,918

  240,908,504,656

  73.3


  Mwenendo wa ukusanyaji wa mapato unaonesha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeendelea kujitahidi katika ukusanyaji. Hata hivyo Serikali inaendelea kuzijengea uwezo Halmashauri ili ziweze kufikia malengo ya ukusanyaji waliojiwekea. Kwa sasa Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo imeendelea kufanya yafuatayo:-

  ·        OWM – TAMISEMI imekamilisha utafiti wa vyanzo vya mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 30 (za majaribio) katika kipindi cha Julai – Septemba, 2013, ambapo vyanzo mbalimbali vipya vinavyoweza kutozwa Kodi vimeibuliwa kama Kodi ya majengo kwa Halmashauri za Wilaya, Ushuru wa Mifugo, Ushuru wa Minara ya Simu, Ushuru wa nyumba za kulala wageni uliofutwa awali nk. Maeneo hayo yatapanua wigo wa mapato wa Halmashauri pamoja na maeneo yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho ya Kisheria (Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 1982) ili kuongeza wigo wa mapato. Vile vile, utafiti huo umeangalia njia za kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato pamoja na njia za malipo rahisi ili kupunguza kero na umbali kwa walipaji hasa katika kulipa kupitia teknolojia rahisi za malipo kwa kutumia M- Pesa, Tigo – Pesa, Max- Malipo, n.k.


  ·        OWM-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara imerudisha Ada za Leseni za Biashara kuanzia mwezi Julai, 2013 ili kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kuongeza vyanzo vya ukusanyaji wa mapato.


  ·        OWM-TAMISEMI itaendelea kusimamia kikamilifu Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuhakikisha zinakusanya mapato yake ya ndani ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa mapato yaani “Local Government Revenue Collection System (LGRCS)” na “i-TAX” kwa lengo la kuboresha usimamizi na udhibiti wa mapato ya ndani ya Halmashauri na kuhakikisha mapato haya yanatumika inavyopaswa.


  ·        Halmashauri zimeendelea kuchukua hatua za Kisheria kwa Mawakala wote ambao hawajawasilisha makusanyo ya mapato pamoja na wale wote wanaokwepa kulipa ushuru kulingana na taratibu zilizopo. Mfano mwaka 2011/12 Mawakala 35 wa ukusanyaji mapato katika Halmashauri mbalimbali wamefikishwa Mahakamani kwa kutowasilisha makusanyo kulingana na makubaliano.


  ·        OWM-TAMISEMI imeendelea kuzielekeza Halmashauri zote nchini kubuni vyanzo vipya vya mapato kulingana na uwezo na uchumi wa maeneo yao ili kuwaongezea kipato. Kadhalika, maelekezo yametolewa kwa Halmashauri kuhakikisha kodi zinazotozwa sasa zinakusanywa kikamilifu na kwamba mbinu za ukusanyaji zinaboreshwa ili kuongeza mapato. Mikoa nayo imeagizwa kutekeleza jukumu lake la msingi la kuzisaidia na kusimamia Halmashauri ipasavyo ikiwemo eneo la ubunifu wa vyanzo vya mapato.


  2.2            Ruzuku toka Serikalini na kwa Washirika wa Maendeleo

  Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa zinapaswa kupokea ruzuku toka Serikali Kuu ili kulipia gharama za utoaji wa huduma mbalimbali kama Afya, Elimu, Kilimo, Barabara na maji. Ruzuku hii ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida, Mishahara na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Suala la kupeleka fedha za ruzuku katika MSM linategemea upatikanaji wa fedha za makusanyo ya ndani ya Serikali na kutoka kwa Washirika wa Maendeleo. Pale ambapo Serikali Kuu imekusanya mapato kidogo kutoka katika vyanzo hivyo, upelekaji wa fedha katika MSM nao huwa mdogo.


  2.3            Mikopo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa

  Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Kifungu cha 11 cha Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa Sura 290  zina fursa ya kukopa kutoka katika Taasisi za fedha na Mabenki ili kupata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Hadi kufikia Juni, 2013 Halmashauri zipatazo 21 zimepatiwa Mikopo kupitia Taasisi za binafsi za Fedha. Pia Kifungu na 12 cha Sheria hiyo kinatoa nafasi kwa Halmashauri kutumia fedha zaidi ya akiba iliyopo Benki kwa kupata kibali cha Waziri mwenye Dhamana ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

  Kadhalika, Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaruhusiwa kukopa fedha kutoka Bodi ya Mikopo ya  Serikali za Mitaa. Hadi kufikia Septemba, 2013 Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa imeweza kutoa mikopo ya jumla ya Shs. 6,935,736,734/=. Aidha, zipo Halmashauri zilizowasilisha maombi ya mikopo ambayo yanaendelea kushughulikiwa ili yaweze kupata vibali vya kukopa. OWM – TAMISEMI imendaa Mwongozo maalum unaozielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia taratibu muhimu za kufuatwa kabla ya kuwasilisha maombi ya Vibali vya mikopo.


  3.                 UTUMIAJI WA FEDHA

  Usimamizi katika matumizi ya fedha za Umma unaanzia katika utengenezaji wa bajeti. Serikali huandaa Mwongozo wa namna ya kuandaa bajeti kila mwaka ambapo Mamlaka za Serikali za Mitaa huutumia kuandaa bajeti zao kwa kuzingatia ushirikishwaji wa jamii katika kuibua Miradi ya Maendeleo kulingana na mahitaji ya eneo husika. Katika Usimamizi wa Mapato na Matumizi ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kanuni za Usimamizi wa Fedha wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (LAFM, 2009) zimeainisha wajibu na majukumu ya makundi mbalimbali ya Viongozi na Watendaji katika Mamlaka hizo ambao wana wajibu wa kusimamia matumizi hayo kama ifuatavyo:

  3.1            Waziri mwenye Dhamana ya Mamlaka za Serikali za Mitaa

  Kuhakisha kuwa upo usimamizi madhubuti wa mapato na matumizi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa; kuwezesha kuwepo kwa usalama wa fedha kwa ajili ya shughuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuhakikisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatekeleza shughuli zake kwa mujibu wa mipango na bajeti ikiwemo kuziwezesha ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi. Kadhalika kuchukua hatua stahiki kwa Watendaji watakaobainika kufanya ubadhirifu wa mali ya umma.


  3.2            Mkuu wa Mkoa.

  Kuhakiki na kupitia taarifa za mapato na matumizi ikiwemo zile za utekelezaji wa miradi ya maendeleo za kila robo mwaka; kutoa ushauri katika mipango na bajeti za Halmashauri; kupitia taarifa za Mkaguzi wa Ndani za kila robo mwaka; kupitia taarifa za Kamati za Ukaguzi (Audit Committee),kufanya ukaguzi maalum wa masuala ya fedha na kuchukua hatua stahiki kulingana na Sheria, Taratibu na Kanuni zilizopo.


  3.3            Baraza la Madiwani.

  Baraza la Madiwani lina wajibu wa kutoa maamuzi katika masuala yote ya usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo kuidhinisha mipango na bajeti za Halmashauri; kujadiliana, kukubali au kukataa mapendekezo ya taarifa za utekelezaji zilizowasilishwa na Kamati za Kudumu pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa watumishi walioenda kinyume na Sheria.  3.4            Kamati ya Fedha na Uongozi.

  Kudhibiti na Kusimamia Mapato na Matumizi ya Halmashauri kwa kupitia taarifa za mapato na matumizi ya kila mwezi; taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya kila robo mwaka; taarifa za Mkaguzi wa ndani na zile za Kamati ya Ukaguzi. Pia kuidhinisha mipango na bajeti ya mwaka ya Halmashauri; kupitia taarifa za Bodi ya Zabuni; kupitia taarifa za Kitengo cha Manunuzi cha Halmashauri (PMU),  na kusimamia uwasilishaji wa  taarifa za mwisho wa mwaka wa fedha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. 


  3.5            Menejimenti ya Halmashauri.

  Mkurugenzi ndiye Afisa Masuuli wa Halmashauri kwa hiyo kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara, anao wajibu wa kuhakikisha kuwa Halmashauri ina mfumo rasmi na wa kuridhisha wa usimamizi wa fedha; Sheria, Kanuni na Miongozo ya Usimamizi wa fedha inafuatwa kwa ukamilifu na Idara zote katika utekelezaji wa shughuli za Halmashauri; kusimamia Mapato, Matumizi, Mali na Madeni yote ya Halmashauri; kujibu Hoja za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mkaguzi wa Ndani na Kamati zozote za Ukaguzi kwa wakati na ukamilifu; pamoja na kuhakikisha kuwa Madiwani wanapewa taarifa zinazohusu masuala ya fedha kwa wakati.

  Katika kutekeleza majukumu haya ya usimamizi kwa upande wa matumizi, zipo taarifa mbalimbali zinazoandaliwa katika ngazi zote zinazoonesha mapato yaliyopatikana na namna fedha hizo zilivyotumika. Lengo ni kuona fedha hizi zimetumika katika maeneo yaliyokusudiwa na kwamba thamani ya fedha hizo inaonekana ili hatimaye kutoa huduma za msingi kwa wananchi.

  Taarifa hizi huonesha mapato na matumizi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo miradi ya maendeleo na  hupitiwa na Vikao na Kamati mbalimbali  zikiwemo; Baraza la Madiwani, Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Huduma za Kiuchumi na Kamati ya Fedha na Uongozi/Mipango).


   Kamati ya Fedha na Uongozi inakutana kila mwezi. Baraza la Madiwani na Kamati za Huduma za Jamii na Huduma za Kiuchumi hukutana angalau mara moja kila robo mwaka. Kamati hizi hujadili  na kujiridhisha kama taarifa hizi ni sahihi na kama zinawakilisha matakwa ya wananchi kwa mujibu wa mipango na bajeti za kila mwaka. Matakwa ya wananchi yanapatikana kwa kuwahusisha na kuwashirikisha katika Vikao vya kupanga na kuamua vipaumbele vinavyotokana na mazingira, nyakati na mahitaji waliyonayo.


  Taarifa hizi hupelekwa ngazi ya Mkoa ambapo huthibitishwa usahihi wake, kuunganishwa na kuwasilishwa OWM-TAMISEMI kwa uchambuzi na kutoa maamuzi mbalimbali.


  4.                 UDHIBITI WA RASILIMALI

  Serikali inawajibika kwa wananchi ambao ni walipa kodi na Washiriki wa Maendeleo wanaotupatia misaada kuhakikisha kuwa fedha zao zinatumika kwa maendeleo ya nchi na hazifujwi.


  4.1             Mfumo wa Usimamizi wa Fedha (Epicor 9.05)

  Ili kuhakikisha kunakuwepo matumizi sahihi ya fedha na utoaji taarifa, Serikali ilianzisha mfumo wa kudhibiti matumizi ya fedha yaani “Intergrated FinancialManagement System (IFMS)”. Katika Serikali kuu maboresho haya yalianza na Wizara 5 za Kisekta na upande wa Serikali za Mitaa mfumo huu ulifanyiwa majaribio kwenye Halmashauri 38 mwaka 1999-2002.  Mfumo wa IFMs (Epicor 9.05) ulioanzishwa unasaidia utunzaji wa kumbukumbu za kihasibu na usimamizi wa fedha ikiwa ni pamoja na utumiaji wa mfumo katika kutunza hesabu za Halmashauri. Hadi sasa Mikoa 21 na Halmashauri 133 zimeunganishwa kwenye mfumo huu na mpango wa Serikali hadi kufikia mwaka wa fedha 2014/2015 ni kuunganisha pia Mikoa na Halmashauri mpya zote zilizoanzishwa.

  Mfumo huu wa usimamizi wa fedha upo ili kudhibiti upotevu na matumizi mabaya na pia unauhakikishia umma kwamba kuna matumizi mazuri ya fedha  na rasilimali nyingine, uwajibikaji, uwazi, na kwamba matumizi ya fedha hizo yanaonesha thamani halisi ya fedha zilizotumika (value for money).


  4.2             Vyombo vingine vya udhibiti

  Pamoja na kuwepo kwa maelezo ya wazi kuhusu wajibu na majukumu ya kila Kiongozi na Mtendaji, Sheria, Kanuni na Taratibu za usimamizi wa fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa  zimeainisha mfumo na vyombo vinavyoangalia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri zilizopangwa ikiwemo kuhakikisha miongozo bora ya Uhasibu na utunzaji fedha inazingatiwa. Vyombo hivyo ni pamoja na:-


  a.     Mkaguzi wa Ndani

  Halmashauri zinapaswa kuwa na Mkaguzi wa Ndani kwa mujibu wa Kifungu cha 45 cha Sheria za Mamlaka za Serikali za Mitaa. Wajibu wake ni kukagua na kutathmini umadhubuti na ukamilifu wa Mfumo wa Udhibiti wa ndani ambao umewekwa kuhakikisha malengo ya Taasisi yanafikiwa. Serikali imeendelea kuboresha Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Halmashauri kwa kuwapatia vitendea kazi na mafunzo mbalimbali ili kuwajengea uwezo katika kuhakikisha udhibiti wa rasilimali za Halmashauri unaimarika.


  b.    Kamati ya Ukaguzi ya Halmashauri

  Kamati ina wajumbe wa ndani na nje ya Halmashauri. Wajibu wake ni kutathmini mpango kazi na taarifa za Mkaguzi wa Ndani,  kuhakikisha taarifa za Mapato na Matumizi ni sahihi, za kuaminika na kamilifu (accurate, reliable and complete), hivyo kupunguza/kuondoa uwezekano wa kupata hati chafu za Ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.  Kadhalika kutoa maoni na ushauri kwa Afisa Masuuli kuhusu masuala yanayohusu hoja mbalimbali za ukaguzi na udhaifu wa usimamizi wa fedha ili kurekebisha kasoro zilizobainika na hatimaye kuwezesha rasilimali kutumika kwa uadilifu na kwa madhumuni yaliyokusudiwa.


  c.      Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)

  Kamati hii ina wajibu wa kupitia taarifa za fedha zinazowasilishwa na Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za kila mwaka pamoja na majibu ya hoja hizo; kuchambua na kuhakiki taarifa za mapato, matumizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na kuhakiki miradi ya maendeleo na matumizi ya mifuko ya pamoja. Katika kutekeleza majukumu hayo, Kamati hufanya Vikao ambapo Halmashauri hutakiwa kuwasilisha taarifa zao za mapato na matumizi na kisha kujadiliwa na kupewa maelekezo au mapendekezo ya namna ya kuboresha utendaji wa kazi. Aidha Kamati pia hutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kulingana na mipango ya Halmashauri ili kuona kama thamani ya fedha imepatikana na huduma hizo zinakidhi mahitaji ya wananchi.

  OWM – TAMISEMI inaendelea kushirikiana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa ili kuhakikisha kuwa Sheria, Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali za Mitaa zinafuatwa na kila mhusika, pamoja na kuona kuwa Halmashauri zinajirekebisha na kuendelea kupata Hati Safi. Vilevile Ofisi hii pia imeendelea kuhakikisha kuwa inawachukulia hatua za kinidhamu Watendaji ambao siyo waadilifu katika masuala ya fedha kwa mujibu wa Sheria.


  d.    Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.


  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mujibu wa Kifungu namba 48 cha Sheria ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa amepewa Mamlaka ya kukagua rasilimali, mifumo ya uendeshaji, utekelezaji wa shughuli za Miradi ya Maendeleo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, na kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi namba 19/2008 anapaswa kukagua na kutoa taarifa yenye hati za maoni kuhusu taarifa za fedha jinsi zinavyoonesha utekelezaji wa shughuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa kila mwaka pamoja na Kufanya ukaguzi maalum pale inapobidi.


  Kiuhalisia Halmashauri zimeendelea kufunga vitabu na kuwasilisha hesabu hizo kwa Wakaguzi kwa wakati. Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, hali ya usimamizi na utunzaji wa vitabu vya hesabu za fedha kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa imeendelea kuimarika. Mtiririko wa Hati kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa unaonesha kuwa hati zisizoridhisha zimeendelea kupungua, mfano mwaka 2011/12 hakuna Halmashauri iliyopata Hati isiyoridhisha ikilinganishwa na Halmashauri nne za mwaka 2005/06. Kadhalika kwa miaka nane iliyopita hati safi zimeendelea kuongezeka ambapo mwaka 2011/12 Halmashauri 104 sawa na asilimia 78 zilipata Hati Safi ikiwa ni ongezeko la Halmashauri 51 kutoka Halmashauri 53 za mwaka 2005/06.

  Mwenendo wa matokeo ya Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa miaka nane (8) ni kama inavyoonekana katika jedwali linalofuata.


  Mwaka

  Hati Safi

  Asilimia

  Hati Yenye shaka

  Asilimia

  Hati Chafu

  Asilimia

  Hakuna maoni (Disclaimer

  Asilimia

  Jumla

  2004/5

  62

  53%

  51

  44%

  4

  3%

                     -  

            -  

        117

  2005/6

  53

  43%

  67

  54%

  4

  3%

                     -  

            -  

        124

  2006/7

  100

  81%

  24

  19%

                      -  

            -  

                     -  

            -  

        124

  2007/8

  72

  54%

  61

  46%

                      -  

            -  

                     -  

            -  

        133

  2008/9

  77

  58%

  55

  41%

  1

  1%

                     -  

            -  

        133

  2009/10

  66

  49%

  64

  48%

  4

  3%

                     -  

            -  

        134

  2010/11

  72

  54%

  56

  42%

  5

  4%

                     -  

            -  

        133

  2011/12


  104


  78%


  29


  21%

                      -  

            -  

  1

  1

        134


  Ni mategemeo ya Serikali kuwa Halmashauri nyingi zaidi zitaendelea kupata hati safi kutokana na jitihada mbalimbali za udhibiti na usimamizi wa fedha zinazoendelea ikiwemo matumizi ya mfumo wa IFMS-Epicor 9.05, pamoja na uimarishwaji wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Halmashauri pamoja na Ofisi za Mikoa zinazosimamia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kwa karibu zaidi.


  HATUA ZA KINIDHAMU ZILIZOCHUKULIWA KWA WATENDAJI

  Pamoja na kuimarika kwa usimamizi wa rasilimali za MSM, kumekuwepo na vitendo vya baadhi ya Watendaji katika ngazi hizo kufuja mali za umma kinyume na taratibu zilizopo. Hata hivyo Serikali imeendelea kuwachukulia Watumishi hao hatua za Kinidhamu na Kisheria kulingana na makosa waliyofanya. Hatua hizi ni pamoja na kufukuzwa kazi, kupewa onyo, kuvuliwa madaraka, kushushwa mshahara, kufikishwa Mahakamani pamoja na kutakiwa kurejesha fedha zilizopotea. Hatua hizo zimekuwa zikichukuliwa pale inapobainika au kuthibitika Watumishi wameshindwa kutekeleza wajibu wao. Hadi kufikia mwezi Septemba, 2013 hatua za Kinidhamu/Kisheria zimechukuliwa kwa Watumishi mbalimbali waliofanya ubadhirifu kama inavyoonesha katika mchanganuo hapa chini:-


  Jumla ya Wakurugenzi 53, Wakuu wa Idara 65 na Watumishi wengine 749 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kufuatia kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha za umma kama ifuatavyo:-


  1.     Wakurugenzi;                

  (i)               Waliofukuzwa Kazi ni mmoja (1),

  (ii)            Waliosimamishwa kazi ni sita (6),

  (iii)         Waliovuliwa Madaraka ni ishirini na tano (25),

  (iv)          Waliopewa ONYO ni kumi na mbili (12),

  (v)             Waliofikishwa Mahakamani ni nane (8) na

  (vi)          Walioshushwa mshahara ni mmoja (1).  2.     Wakuu wa Idara;

  (i)               Waliofukuzwa kazi ni 14,

  (ii)            Waliosimamishwa kazi ni 12,

  (iii)     Waliopewa ONYO ni 16,

  (iv)     Waliovuliwa madaraka ni tisa (9),

  (v)             Waliofikishwa Mahakamani ni 13 na

  (vi)     Waliofikishwa Polisi na TAKUKURU ni mmoja (1).  3.     Watumishi wengine;

  (i)               Waliofukuzwa kazi ni 217,

  (ii)            Waliosimamishwa kazi ni 168,

  (iii)         Walioshushwa cheo ni wanne (4),

  (iv)          Walioshushwa cheo ni 28,

  (v)             Waliopewa ONYO ni 85,

  (vi)          Waliofikishwa Mahakamani ni 212 na

  (vii)       Waliofikishwa Polisi na TAKUKURU ni 35.


  CHANGAMOTO ZINAZOZIKABILI MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

  Pamoja na jitihada za Serikali za kuhakikisha MSM zinawezeshwa ili kutoa huduma bora kwa wananchi bado, zipo changamoto mbalimbali ambazo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi. Miongoni mwao ni pamoja na:-

  1.     Utegemezi mkubwa wa fedha za Ruzuku kutoka Serikali Kuu ili kutekeleza shughuli za maendeleo. Mapato ya ndani ya Halmashauri yanayokusanywa hayatoshi kukidhi mahitaji ya wananchi hivyo kuzifanya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutegemea Ruzuku na Misaada ya Washiriki wa Maendeleo. Hata hivyo, Halmashauri zimeendelea kuhimizwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuhakikisha vile vilivyopo vinakusanywa kwa ukamilifu.

  2.     Baadhi ya watumishi kutokuwa waaminifu na kuendelea kutumia fedha za umma isivyo halali.

  3.     Uhaba wa watumishi na vitendea kazi.

  4.     Baadhi ya wadau mbalimbali kutokukubali Mfumo wa usimamizi wa fedha ulioanzishwa wa IFMS – Epicor 9.05.


  MIKAKATI ILIYOWEKWA KUONGEZA UWAJIBIKAJI NA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI NA KUDHIBITI UBADHIRIFU WA MALI/FEDHA ZA UMMA

  Mikakati iliyowekwa na Serikali ili kuongeza uwajibikaji na udhibiti wa mali za Umma ni kama ifuatavyo:-

  1.     Kutoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kufanya ukaguzi wa mara kwa mara hususan katika miradi ya maendeleo kwa kutumia vyombo vifuatavyo:-

  a.     Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT),

  b.    Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango,

  c.      Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani,

  d.    Kamati ya Ukaguzi ya Halmashauri, na

  e.     Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


  2.     Kuendelea kuzijengea uwezo Sekretarieti za Mikoa ili ziweze kushauri na kusimamia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ikiwemo ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuchukua hatua stahiki wa watumishi watakaobainika kufanya ubadhirifu.

  3.     Kuendelea kuimarisha Kitengo cha Ukaguzi wa Awali  na Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Halmashauri kwa kuwapatia Wakaguzi wa ndani vitendea kazi ili kurahisisha ufuatiliaji katika maeneo yao, sambamba na kuendelea kufanya mafunzo kwa Wakaguzi wote wa Ndani  wa Halmashauri na wale walio Mkoani.

  4.     Viongozi wa OWM-TAMISEMI pamoja na Wataalam kuendelea kufuatilia na kufanya ukaguzi kwa Mikoa na Halmashauri kwa lengo la kuangalia uendeshaji wa shughuli za Halmashauri ikiwa ni pamoja na Miradi ya Maendeleo. Pia kupeleka nyenzo kama magari, pikipiki na Kompyuta. 

  5.     Kuendelea kuimarisha mifumo ya uhasibu na udhibiti wa ndani  kupitia Mfumo wa usimamizi wa fedha wa IFMS-  EPICOR 9.05 kwa upande wa “technical“ na “application“ ili kuhakikisha nidhamu ya bajeti na taratibu za matumizi ya fedha vinafuatwa. Hii itahusisha marekebisho katika Mtandao wa mawasiliano hususan Halmashauri za pembezoni pamoja na kukamilisha “module” mbalimbali zitakazotumika katika uaandaji wa taarifa za fedha na ufungaji wa Hesabu. Mfumo pia utaendelea kutumika kufuatilia kwa karibu na kudhibiti matumizi yanayofanywa na Halmashauri moja kwa moja kulingana na Sheria za Fedha.

  6.     Kufunga Mfumo wa IFMS-EPICOR 9.05 katika Halmashauri na Mikoa mipya iliyoanzishwa pamoja na kutoa mafunzo kwa Waweka Hazina na Wahasibu wa Halmashauri JUU ya namna ya kuutumia ipasavyo.

  7.     Kuendelea kutoa miongozo mbalimbali kwa Mikoa na Halmashauri juu ya matumizi sahihi ya fedha za Umma pamoja na kuendelea kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wanaobainika kufanya ubadhirifu wa mali ya Umma kulingana na Sheria zilizopo.

  8.     Kuendelea kutoa mafunzo kwa watendaji wa Halmashauri na Mikoa juu ya usimamizi wa fedha, manunuzi, ukaguzi na majukumu yao kwa wananchi pamoja na uwajibikaji.
  0 0

   Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba akitoa hotuba yake wakati wa kufunga kongamano la siku tatu la uhamaji wa mfumo wa utangazaji kutoka Analojia kwenda Dijitali kwa Afrika (DBSF) 2014 katika Hoteli ya Naura Spring jijini Arusha. Kongamano hilo la 9 liliandaliwa na Shirika la Utangazaji kwa Nchi za Jumuia ya Madola (CTO) kwa ushirikiano mkubwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Srikali ya Tanzania ambao ndio wenyeji.
   Mgeni rasmi katika ufungaji wa Kongamano hilo la DBSF 2014, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (wapili Kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (kushoto) Katibu Mtendaji wa CTO, Tim Unwin (wapili kulia) na  Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka TCRA, Habbi Gunze. 
   Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (kulia) akizungumza kabla ya Mgeni rasmi kufungaji  Kongamano hilo la DBSF 2014 katika Hoteli ya Naura jijini Arusha leo. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (Kushoto),  Katibu Mtendaji wa CTO, Tim Unwin (katikati) na  Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka TCRA, Habbi Gunze. 
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (kulia) akizungumza kabla ya Mgeni rasmi kufungaji  Kongamano hilo la DBSF 2014 katika Hoteli ya Naura jijini Arusha leo 
   Katibu Mtendaji wa CTO, Tim Unwin akisema neno la shukrani kwa washiriki na wageni wote kwa kufanikisha kongamano hilo la DBSF 2014 katika Hoteli ya Naura Spring jijini Arusha.
   Waandishi wa habari wakiwajibika wakati wa ufungaji.

   Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba akifanya mahojiano maalum na waandishi wa habari jijini Arusha.
  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa CTO, Tim Unwin baada ya kufunga kongamano hilo jijini Arusha leo.

  0 0


  DAR ES SALAAM, Tanzania
  RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi ameipongeza Taasisi ya Aga Khan kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia Jamii ya Watanzania kimaendeleo


  Pia, amesema maonyesho ya Aga Khan yanayoendelea kufanyika nchini yanaonyesha ushirikiano wa dhati uliopo baina ya taasisi hiyo na Tanzania.  Mwinyi (picahni juu), aliyasema hayo jana jioni, alipotembelea maonyesho hayo huku akiwa ameambatana na Waziri Mkuu Mstaafu, Samwel Malicela, alisema taasisi yab Aga Khan imefanya mambo mengi nchini.  Alisema binafsi amebahatika kukutana na Imam Aga Khan zaidi ya mara mbili, ambapo zote amekuwa akizungumza mambo mengi ya maendeleo kuhusiana na Tanzania.  "Imam Aga Khan muda wote amekuwa na akisisitiza maslahi na mafanikio ya watanzania hayo yanatokana na kuwa na mapenzio mema na watanzania,''alisema.  Alisema jambo hilo ndio maana lilimfanywa kuwa mstari wa mbel katika kuboresha sekta ya elimu na afya, ambayo imekuwa tegemeo kubwa la watanzania kunufaika na huduma hizo.  Hivyo, alisema maonyesho hayo yameonyesha ni namna gani Aga Khan amekuwa akiisaidia nchi bila kujali dini, rangi au kabila yeye anachojari ni utu.


  Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Taasisi ya Shia Ismailia Tanzania, Kamal Khimji alisema maonyesho hayo wanayatumia kuonyesha upendo na namna gani wanavyojitahidi kuisaidia wananchi.
  Makamu wa Rais wa Taasisi ya Aga Khan Tanzania, Kanal Khimj akitoa manano ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mzee Mwinyi kuzungumza.

  Mzee Mwinyi akizungyumza na viongozi hao kwenye chumba cha mapumziko
  Mzee Mwinyi akizungumza na Makamu  wa Rais wa Taasisi hiyo hapa nchini, Kanal Khimji
  Waakiendelea na mazungumzo kwenye chumba cha mapumziko.
  Mzungumzo yakiendelea chumba cha mapumziko
  Mmoja wa viongozi wa Taasisi hiyo, Altaf Hirani akizungumza na Mzee Malecela ukumbini
  Mzee Malecela akiwa na viongozi wa Taasisi hiyo ya Aga Khan
  Wageni ukumbini
  Wageni ukumbini
  Ukumbini
  Wageni ukumbini wakimsubiri Mzee Mwinyi
  Mzee Mwinyi akiingia ukumbini na Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam.


  Mzee Mwingi akiketi meza kuu
  Mzee Mwinyi akiwa ameketi meza kuu na viongozi wa Tasisi hiyo ya Aga Khan
  Mzee Mwinyi akizungumza
  "Hekima ikiongezeka Maneno yanapungua", akisema Mzee Mwinyi mwishoni mwa hotuba yake iliyojaa hekima. Imetayarishwa na theNkoromo Blog.
   Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akikaribishwa katika hafla ya Maonyesho ya picha kuhusu Taasisi ya Aga Khan, jana kwenye ukumbi wa Diamod Jubilee jijini Dar es Salaam.
  Mzee Mwinyi akisalimia viongozi mbalimbali wa taasisi hiyo
  Mzee Mwinyi akiendelea kusalimia 
  Salam
  Salam
  Salam na viongozi
  Salam na viongozi
  Salam na viongozi
  Mwisho wa salam na viongozi
  Sheikh Mkuu Mufti wa Tanzania, Sheikh Simba Shaaba (kushoto), Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Waziri Mkuu mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu John Malecela wakimsubiri Mzee Mwinyi kwenye hafla hiyo 
  Mzee Mwinyi akikaribishwa kwenye chumba maalum cha mapumziko na viongozi wa taasisi hiyo ya Aga Khan
  Sheikh Mkuu, Muft wa Tanzania akiingia ukumbini

  0 0

   Frank Mvungi-Maelezo 
  Serikali imesema itaendelea kuboresha Sekta ya elimu nchini ili kuongeza wataalamu watakaosaidia kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa  nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Mh. Hawa Ghasia  wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Waziri Ghasia alisema kuwa baada ya Serikali kwa kushirikiana na wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini kukamilisha ujenzi wa shule za kata hatua inayofuata ni kuhakikisha kuwa shule hizo zinakuwa na vitabu, maabara za kisasa pamoja na walimu wakutosha.

  Akifafanua zaidi alisema shule kongwe za Sekondari nchini ni miongoni mwa shule zitakazoboreshwa ili kutoa wanafunzi wenye ubora na uwezo ili kulisaidia taifa katika siku za usoni kuwa na wataalamu wakutosha katika maeneo yote yatakayosaidia kuwaletea wananchi maendeleo.

  Pia Waziri Ghasia alieleza kuwa maboresho hayo yanakwenda sambamba na kuongeza idadi ya vyuo vya Elimu ya kati na vile vya Elimu ya juu .

  Katika kutekeleza mpango wa kuboresha elimu Waziri Ghasia amesema kila Mtendaji katika Mkoa na halmashauri zote nchini anatakiwa kusimamia vyema utekelezaji wa mpango huo ili kuinua kiwango cha elimu na wale watakaoshindwa Serikali itawachukulia hatua kali za kinidhamu.

  Katika Hatua nyingine Waziri Ghasia amesema Serikali itahakikisha kuwa mfumo mpya wa ukusanyaji mapato katika Halmashauri zote nchini unafungwa kufikia mwaka 2015/16 ili kusaidia kuongeza mapato na kuboresha  huduma za jamii kama hosipitali, Elimu na maji.

  Alitaja Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kuwa miongoni mwa halmashauri zilizokwisha anza kutumia mfumo wa kielektroniki katika kukusanya mapato yake ambapo mfumo huo unaainisha vyanzo vyote vya mapato katika eneo husika hivyo kurahisisha ukusanyaji wa mapatao hayo.

   Akifafanua zaidi alibainisha kuwa kufuatia maboresho yanayoendelea Kufanywa na Serikali hati safi katika Halmashauri zimeongezeka kutoka halmashauri 53 za mwaka 2005/2006 hadi Halmashauri 104 za mwaka 2011/12.


  Pia Serikali Imeendelea kuchukua hatua za kinidhamu na Kisheria kwa watumishi wachache waliobainika kujihusisha na ufujaji wa mali za umma ambapo hadi Septemba, 2013 jumla ya wakurugenzi 53, Wakuu wa Idara 65 na watumishi 749 walichukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha za umma.


older | 1 | .... | 224 | 225 | (Page 226) | 227 | 228 | .... | 1903 | newer