Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

KIZITO ASHINDA MILIONI 10 ZA 'CHAMPIONI MAHELA' AKIWA KWENYE DALADALA

0
0
MC Chaku (kushoto) akiwa na mmoja ya wakazi wa Mbagala tayari kwa kuchagua mshindi wa Championi Shinda Mahela.
...Kuponi za Championi Shinda Mahela zikiwa tayari kwa ajili ya droo.
Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao (kushoto), Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (katikati) na kulia ni Ofisa Masoko wa Shinyanga Emporium, Herman Bernard wakiendelea kufuatilia droo.
...Mchezesha droo akichambua kuponi katika Viwanja vya Mbagaka Zakhem jijini Dar.
MC Chaku akimfunga kitambaa mkazi wa Mbagala ili amchague mshindi wa Championi Shinda Mahela
Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao (kushoto) akikabidhiwa kuponi ya mshindi wa milioni 10 za Championi Shinda Mahela.


MC Chaku (kulia) na mkazi wa Mbagala wakitaja jina la mshindi wa milioni 10 za shindano la Championi Shinda Mahela ambaye ni Kizito George.
MC Chaku akimwaga kuponi za Championi Shinda Mahela wakati wa mchakato wa kumpata mshindi wa milioni 10.
...MC Chaku akiweka sawa kuponi hizo.
Msomaji wa Championi kutoka Mbagala akitafuta mshindi wa tisheti.
Mr Championi (kushoto) akimkabidhi mshindi tisheti.
...Wakazi wa Mbagala wakiendelea kufuatilia Bahati Nasibu ya shindano la Championi Shinda Mahela.
Wasomaji wakijaza kuponi za Championi Shinda Mahela kabla ya Bahati Nasibu kuanza.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akiongea na wanahabari baada ya kupatikana mshindi wa Championi Shinda Mahela ambaye ni Kizito George.
Burudani wakati wa droo hiyo ya mwisho.
Burudani ikiwa imepamba moto Viwanja vya Mbagala Zakhem kabla ya droo ya mwisho ya kumpata mshindi wa milioni 10 kupatikana.
BAADA ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye, mshindi wa milioni 10 amepatikana kupitia droo ya Shinda Mahela na Championi ambaye ni Kizito George Chuka.
Droo hiyo iliyochezeshwa mbele ya Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao kwenye Viwanja vya Mbagala- Zakhem jana Jumanne.
Akizungumza Kizito ambaye ni makazi wa Kawe jijini Dar alipopigiwa simu na muendeshaji wa shughuli hiyo MC Chaku, mshindi huyo alikuwa ndani ya daladala hivyo hakuwa na mengi ya kuongeza zaidi ya kushukuru kwa kujinyakulia kitita hicho.
Kizito, 43 alionekana kufurahia kutokana na sauti yake kusikika akichekelea na haijafahamika kama aliwasilimulia abiria wenzake aliokuwa nao ndani ya daladala hiyo.
Hata hivyo keshokutwa Alhamisi anatakiwa kuja Ofisi za Global Publishers kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuchukua mkwanja wake huo.
“Nimefurahi sana lakini sasa hivi nipo ndani ya daladala naomba muda nikifika nitakupigia,” alisema Kizito.
Washindi wengine ambao walipatikana siku hiyo ni Athuman Yusuph, 40, mkazi wa Mwanza aliyejinyakulia shuka za kisasa na Amiri Kinguaba, 60 aliondoka na simu kali aina ya Samsung Galaxy.
(PICHA/HABARI: DENIS MTIMA NA LUCY MGINA/GPL)

ITV News goes undercover to expose Tanzania's illegal ivory trade

0
0

KAMATI KUU YAMTEUA MGOMBEA WA CCM JIMBO LA KALENGA

0
0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha kwa waandishi wa habari, mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa, Godfrey William Mgimwa (kushoto), leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Nape amemtambulisha Godfrey ambaye ni mtoto wa Marehemu Dk. William Mgimwa, baada ya Kamati Kuu ya CCM kumpitisha, leo kuwania nafasi hiyo ya Ubunge. (Picha na Bashir Nkoromo)

TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR (ZBS) NA TASISI YA VIWANGO TANZANIA (TBS) ZAKUBALIANA KUFANYA KAZI PAMOJA.

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum akimkabidhi ripoti ya Kamati ya pamoja ya mashirikiano Mhe. Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi katika Mkutano uliofanyika Amani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi (alie simama) akizungumza katika Mkutano wa uzinduzi wa kamati ya mashirikiano ya (TBS) na (ZBS) kulia ni Mkurugenzi Mkuu ZBS Bwa. Khatib Mwalim na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Viwango TBS Bwa. Leandr Kinabo.
Mwenyekiti wa kamati ya pamoja ya mashirikiano kati ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na la Zanzibar (ZBS) Bwa. Suleiman Masoud Makame akiitambulisha kamati ya watalamu yenye wajumbe nane wanne kutoka Bara na wane Zanzibar kwa Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi katika Mkutano uliofanyika Amani Zanzibar.
Baadhi ya watendaji wakuu wa tasisi mbili wakiskiliza nasaha za Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi (hayupo pichani) mara baada ya kuizindua Kamati yawatalamu katika Mkutano uliofanyika ofisi ya Viwango Amani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Thuwaiba Edington Kisasi katika picha ya pamoja na watenandaji wa Tasisi mbili zinazoshuhulikia ubora wa viwango Tanzania. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo-Zanzibar). 

MHE. RAZA AZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI.

0
0
 Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassan Dharamsi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhoji matumizi ya pesa za Mapinduzi Cup zilivyotumika, katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar. kushoto Afisa habari Wizara Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana na Watoto Bi. Sharifa Maulid na kulia Afisa habari Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Bi. Miza Kona.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassan Dharamsi (hayupo pichani) katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
 Mwandishi wa Habari wa coconat Redio  Jacson Sekiete akimuuliza swali mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamedraza Hassan Dharamsi katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

HABARI MSETO KUTOKA MKOANI IRINGA LEO.

0
0
Bodi na kamati za usimamizi wa hospital ,vituo vya afya na zahanati katika halimashuri ya manispaa ya Iringa vimezinduliwa rasmi hii leo  katika ukumbi wa halimashauri ya maniapaa.

Akizungumza mstahiki meya wa manispaa, AMANI MWAMWINDI kwa niaba ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Iringa RETISIA WALIOBA katika uzinduzi huo, amesema kuwa wajumbe pamoja na kamati ya bodi wasitumike kama vyanzo vya migogolo bali walete mafanikio.

Amesema kuwa bodi na kamati zinapaswa kuhakikisha kuwa zinaboresha na kubuni mbinu zitakazozalisha uchumi na kusaidia upatikanaji wa huduma kiurahisi kama vile upatikanaji wa dawa pamoja na kuwapatia elimu  wajumbe ili kuwajengea uwezo katika kazi zao. 
Hata hivyo amesema kuwa bodi hiyo inapaswa kusimamia na kuhakikisha wanaondoa kero zinazoikabili sekta ya afya katika manispaa kwa kuwajibika kuzifanyia kazi changamoto zilizopo.

Ameongeza kwa kusema kuwa serikali imeahidi kuwaletea dawa,vifaa na watalamu huku akiitaka jamii ishirikiane na bodi ili kuleta maendeleo katika sekta ya afya. Aidha kwa upande wake naibu meya GEREVAS NDAKI ameipongeza kamati pamoja na bodi iliyochaguliwa na kusema kuwa anategemea watafanya kazi kwa umoja huku akiwataka wawe wa kwanza kujiunga na tika kabla ya kuwashawishi wengine.


WAKAZI WA IRINGA WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA WIZARA YA AFYA IKIWA SAMBAMBA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA.

Wananchi kwa kushirikiana na Halmashauri ya manispaa ya iringa wametakiwa kufuata taratibu za wizara ya afya ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira. 

Hayo yamesemwa na Dk NICOLUS NTABAYE   wakati akizungumza na Nuru FM na kusema kuwa baadhi ya wananchi wamekua hawana taratibu ya utunzaji wa mazingira na badala yake wamekua vyanzo vya uharibifu wa mazingira.

Amesema kuwa  jitihada mbalimbali zinazofanywa na halmashauri ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria kwa wale wanaokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa hata hizo wananchi wamekuwa hawazitekelezi.

NTABAYE ameelezea umuhimu wa jamii katika kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kuepuka  magonjwa mbalimbali hususani magonjwa ya mlipuko katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.

TAHADHARI KUTOKA MAMLAMKA YA HALI YA HEWA:MATARAJIO YA KUWA NA VIPINDI VYA MVUA KUBWA,UPEPO MKALI NA MAWIMBI MAKUBWA.

0
0

SUPER D AIPIGA TAFU GYM YA UHURU KARIAKOO VIFAA VYA NGUMI

0
0

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akikadhi vifaa vya mchezo wa masumbwi Gloves pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo kwa Kocha wa GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo  Mohamed Chipota kwa ajili ya kuhamasisha mchezo  wa masumbwi katika eneo hilo na kuwapa moyo wa kuendelea na mazoezi, wanaoshudia wengine wa pili kushoto ni Atanasi kibwe,Omari Bai, Raymond Mbwago na Mussa Sindano. Vifaa hivyo pamoja na Dvd vina thamani ya shilingi laki mbili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na baazi ya mabondia wanaofanya mazoezi katika
GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo kutoka kushoto ni
Atanasi kibwe,Omari Bai, Raymond Mbwago ,Mussa Sindano Vifaa na kocha wa GYM hiyo Mohamed Chipota .




Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akikabizi vifaa vya mchezo wa masumbwi Gloves pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo kwa Kocha wa GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo  Mohamed Chipota kwa ajili ya kuamasisha mchezo  wa masumbwi katika eneo ilo na kuwapa moyo wa kuendelea na mazoezi wanaoshudia wengine wa pili kushoto ni Atanasi kibwe,Omari Bai, Raymond Mbwago na Mussa Sindano Vifaa hivyo pamoja na Dvd vina thamani ya shilingi laki mbili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa katika picha ya pamoja  na baadhi ya mabondia wanaofanya mazoezi katika
GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo baada ya kuwakabizi vifaa vya mchezo huo kutoka kushoto ni
Atanasi kibwe,Raymond Mbwago,kocha wa GYM hiyo
Mohamed Chipota,Mussa Sindano na
Omari Bai, Vifaa na
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ameipiga tafu   GYM ya mchezo wa ngumi ya  Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo Dar es salaam kwa kuwapati vifaa vya mchezo huo

akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Super D alisema amevutiwa na uanzishwaji wa GYM hiyo ambayo ina uwezo mkubwa wa kuwatoa mabondia wazuri kipindi kijacho

aliongeza kwa kusema kuwa unajua hizi GYM za mtaani zipo chache sana na wana uhaba wa vifaa vya kufundishia hivyo mimi nimeamua kujitolea gloves mikono mitatu kwa kuanzia ili  wapate moyo wa kuendelea na mazoezi pamoja na DVD za mafunzo mana ndio timu ambazo tunazitegemea kwa siku za usoni kutuletea mabondia wakali watakaoweza kutuletea medali na kutupa sifa nchi hii

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo  Kocha wa GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo  Mohamed Chipota amesema vifaa hivi pamoja na DVD za mafunzo ya ngumi zimekuja wakati muhafaka kwa kuwa tulikuwa na huaba wa vifaa kama hivi

hivyo tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutupa sapoti kama alivyofanya Super D yeye ni kocha wa Mkoa wa Kimichezo Ilala sasa hapa kama amewekeza mabondia wa ilala sasa watatokea hapa kwa siku za usoni

tumeanza hivi karibuni lakini mategemeo yangu ni kuibua vipaji vyipya kabisa vya mchezo wa masumbwi nchini alisema Chipota

Super D ambaye ujihusisha na uhuzaji wa DVD za mafunzo ya ngumi pamoja na vifaa vya mchezo huo ikiwemo, Gloves,Gum shit, Clip bandeji dambel,Protecta,bukta, singrend na vifaa vyote vya mchezo wa masumbwi

MWALIMU AJITOKEZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

0
0
 Mwalimu Vitus Lawa akikabidhi fomu ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Kalenga kwa Katibu wa Wilaya ya Iringa Vijijini Felix Nyondo katika ofisi za chama hicho zilizoko kata ya Gangilonga mjini Iringa.
 Mwalimu Vitus Lawa akizungumza na wadau waliomsindikiza kurejesha fomu za kuwania kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa chadema jimbo la Kalenga
Mwalimu Vitus Lawa akizungumza na waandishi baada ya kurudisha fomu za kuwania kuchaguliwa kuwania ubunge wa jimbo la Kalenga katika ofisi za chama hicho zilizoko kata ya Gangilonga. (Picha zote na Denis Mlowe)
Mwalimu Vitus Lawa akizungumza na wadau waliomsindikiza kurejesha fomu za kuwania kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa chadema jimbo la Kalenga
========  ======  ========
MWALIMU AJITOKEZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

Na Denis Mlowe,Iringa

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngwelo iliyoko Lushoto mkoani Tanga, Vitus Lawa (41) amejitokeza kuwania ubunge katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akitumia msemo wa neno ‘Jembe ambao kila herufi imebeba maana ya ujumbe, Lawa aliyesindikizwa na baadhi ya wanachama wa Chadema wa kata ya Kalenga alilirudisha fomu za Chadema kwa kuwapa moyo wakazi wa Kalenga kuwa mkombozi wa kweli amefika katika kuwaletea maendeleo.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kurudishafomu  mbele ya Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa Vijijini Felix Nyondo, Lawa alisema uwezo wa kuwakomboa na kuwaletea maendeleo wakazi wa Kalenga umefika hivyo ni wakati wake wa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo katika kushirikiana na kushikamana katika kuleta maendeleo.

Alisema endapo atapatiwa nafasi atatumia ajenda tano ambazo zinamaana ya neno jembe, imebeba maana kubwa sana katika maisha ya binadamu kwa uwezo wangu wa akili na ubunifu,neno hilo lina maana ya jamii bora ambayo itatokana na kuwajengea uwezo kwa wajasiliamali wote na elimu bora pia inawezekana kwa wakazi wa Kalenga kwa kusimamia upatikanaji elimu iliyobora kwa taasisi husika na wadau wake.

Lawa alisema endapo chama kitampitisha kuwania ubunge kwa jimbo la Kalenga atawaletea maendeleo  wakazi hao kwa kuhakikisha miundo mbinu inakuwa bora kwa wilaya hiyo kwa kuanzisha shirika la wakandarasi ambao watasimamia kitengo hicho.

Aliongeza kuwa kuwainua wafanyabiashara wa jimbo la Kalenga kupitia mafunzo ya ujasiliamali na kuanzisha shirika la wafanyabiashara wa kalenga walioko nje na ndani ya mkoa wa Iringa.

“Nitaakikisha naanzisha kundi la wana Kalenga waishio ndani na nje ya mkoa kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo ya jimbo kwa mtindo wa egima hivyo najiamini nina uwezo wa kuwasaidia wananchi wa Kalenga na siasa safi kwa wananchi ni JEMBE” alisema Lawa

Hadi sasa kuna wanachama  13 wa Chadema wamejitokeza katika ofisi za chama hicho wilaya ya Iringa vijijini kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Kalenga katika Uchaguzi mdogo wa kujaza kiti hicho kilichoachwa wazi na Dk William Mgimwa aliyefariki Januari 1, mwaka huu, utafanyika Machi 16, mwaka huu.

Wananachama wengine waliojitokeza  kuomba kugombea nafasi hiyo kuwa ni pamoja na Lawa ni Zubery Mwachura , Dr Evaristo Mtitu, Akbar Sanga, Grace Tendega, Rehema Makoga, Sinkala Mwenda, Henry Kavina, Aidan Pungili, Mussa Mdede, Mchungaji Samweli Nyakunga,  Daniel Luvanga na Anicent Sambala.

Article 18

0
0
                                             

Registration is NOW open for CISA Review Class for the forthcoming CISA exam on 14th June, 2014. Our Reviews are due to begin on Monday 24Th February, 2014. Get discount of $75 if you register for the Exam before 12 February, 2014

This CISA Review Class focuses exclusively on the essential areas covered in the CISA exam. This review class covers the core sections and a series of sample exam questions that provide participants with a "feel" of the format and the types of questions encountered on the CISA exam.


Our trainers are qualified Professionals with technical experience, skills and knowledge of specific domain(s). Participants will gain an overall understanding of the relevant CISA Examination DOMAINS.


At the end of the course the MOCK EXAM will be set which will provide the participants with a general idea of the examination questions format. 


Course Contents

Domain 1

Domain 2

Governance and Management of IT

Domain 3

Info Systems Acquisition, Dev & Implementation

Domain 4

Info Systems Operations, Maint & Support

Domain 5

Protection of Information Assets


Two Separate  Mock Exams with 200 Questions Each


                                                           

Study Materials

Our Courses utilize official ISACA presentations and study materials provided by our head office in USA. We will inform you about recommended materials upon your enrolment authorized by us.

Fees- 1,200,000 Tshs.  per Participant (Ask for available discounts in various groups and  possibility of instalment payments)


WARNING:

Any training institution offering review has to be approved by ISACA Tanzania Chapter   before it begins to offer review classes.


For more details about the course and online registration visit our website www.isaca.or.tzwww.isaca.org or contact - info@isaca.or.tz. Mobile No 0754 274491/0715274491 

shule ya makete girls yamkuna mkuu wa mkoa wa Njombe

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi(katikati) akikagua majengo ya shule mpya wa wasichana wilayani Makete, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro na kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka.
 Ukaguzi huo ukiendelea.
 Wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Msangi(hayupo pichani) akizungumza nao
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akizungumza kwenye mkutano shuleni hapo
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi akizungumza na wananchi shuleni hapo.
========  ======  =======
Habari/picha na  Edwin Moshi, Makete.

Kufuatia kukamilika kwa kiasi kikubwa majengo ya shule mpya ya sekondari ya wasichana Makete iliyojengwa katika kijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilayani Makete, mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Asseri Msangi ameagiza shule hiyo iandikishwe ili ianze kutumika.

Mkuu wa mkoa ametoa agizo hilo hii leo Februari 11, 2014 wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya elimu wilayani Makete, ambapo baada ya kufika shuleni hapo ameridhishwa na ujenzi wa shule hiyo na kuona haina sababu ya shule hiyo kuendelea kukaa bila kuandikishwa ili ianze kupokea wanafunzi.

Akizungumza na wananchi wa vijiji viwili vinavyojenga shule hiyo ambavyo ni Utweve na Masisiwe, mkuu huyo wa mkoa mbali ya kupokea na kutjibu kero za wananchi, amekasirishwa na tabia ya wazazi wa vijiji hivyo kuwaambia watoto wao wafeli kwa makusudi ili wasiendelee na masomo ya sekondari.

"Ndugu zangu dunia tuliyopo sasahivi, si ile tuliyoishi zamani, mtoto asiposoma ni matatizo kwake, na ninyi wazazi wenye tabia ya kuwaambia watoto wenu wafeli kwa makusudi mnatupelekea taifa letu kaburini na sisi hatutakubali, tunaomba muiache hiyo tabia, somesheni watoto wenu" alisema Msangi.

Katika hatua nyingine Kapteni Msangi amechangia kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya shule hiyo maalum kwa ajili ya wasichana kama njia mojawapo ya kusaidia ujenzi wa shule hiyo ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Shule hiyo pekee ya wasichana wilayani Makete inajengwa na serikali kwa kushirikiana na wazawa wa Makete wanaoishi nje ya wilaya hiyo, wananchi pamoja na wadau mbalimbali.

MIUNDO MBINU YETU:MVUA MAKETE ILIVYOMKWAMISHA MKUU WA MKOA WA NJOMBE KWENYE TOPE

0
0
Gari la mkuu wa mkoa wa Njombe likiwa limekwama kwenye tope kijiji cha utweve makete. 
 Wadau wakisukuma gari hilo, na huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Utweve akijitahidi kusukuma.
 Hali tete hapa, gari hilo likiwa limenasa mtaroni
 wadau wakijitahidi kuvuta gari hilo
 jitihada zikiendelea.
Gari la mkuu wa mkoa wa Njombe, kapteni mstaafu Aseri Msangi limekwama kwa zaidi ya saa kadhaa katika kijiji cha Utweve wilayani Makete wakati akiwa ziarani kukagua maendeleo ya sekondari ya wasichana makete inayojengwa kijijini hapo

Adha hiyo ilimkumba mkuu wa mkoa baada ya mvua kubwa kunyesha wakati akifanya mkutano na wananchi shuleni hapo mara baada ya kuikagua shule hiyo na kuridhishwa na jinsi ilivyojengwa

Mtandao huu wa eddy blog umeshuhudia magari mengine yaliyokuwa yametangulia gari la mkuu wa mkoa yakipita eneo hilo lililokuwa na utelezi mwingi huku gari hilo la mkuu wa mkoa likikwama kutokana na utelezi huo

Jitihada za kulinasua gari hilo zilifanywa na msafara mzima ulioambatana na mkuu wa mkoa pamoja na wananchi wa kijiji hicho ambapo zoezi hilo lilichukua zaidi ya saa moja kutokana na mvua kuzidi kunyesha zaidi

Jitihada hizo zilizaa matunda na hatimaye gari hilo lilinasuliwa na mkuu wa mkoa kuendelea na safari yake, na hakuna madhara yoyote yaliyotokea

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL A AHUDHURIA MAONESHO YA MIALE YA NURU

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa onesho maalum la Miale ya Nuru, iliyoandaliwa na Taasisi ya Aga Khan kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, jana usiku Feb 11, 2014. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Mipango wa Aga Khan, Navroz Lakhan, wakati alipokuwa akitembelea kujionea maonesho ya kumbuku ya Miale ya Nuru, iliyoandaliwa na Taasisi ya Aga Khan kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, jana usiku Feb 11, 2014. 
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisikiliza maelezo wakati alipokuwa akitembelea kujionea maonesho ya kumbuku ya Miale ya Nuru, iliyoandaliwa na Taasisi ya Aga Khan kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, jana usiku Feb 11, 2014. Picha na OMR

WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI TAMASHA LA KWANZA LA KIPEKEE LA KUWAWEZESHA WANAWAKE NA VIJANA

0
0
Pichani wa tatu kulia ni  Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa Kampuni ya Angels Moment ya jiji Dar,akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Serena Hotel,kuhusiana  tamasha la kwanza na la aina yake kufanyika nchini Tanzania, lenye lengo la kuongeza na kuchochea uelewa wa wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiwekea akiba.

 “Tamasha hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada na maonesho,” alisema Bi Pamela. Pichani kulia ni Meneja  Mawasiliano wa kampuni ya Angels Moment,Bi.Beatrice Millinga,Mratibu wa Matangazo na Mahusiano kutoka kampuni ya AZAM/Bakharessa,Bwa.Mohameda Ramadhani (Mdhamini wa tamasha hilo),pamoja na mwisho kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo kutoka kampuni ya MONTAGE LTD,Bi,Teddy Mapunda.
Pichani ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Angels Moment ya jiji Dar wakiwa katika picha ya pamoja,mara baada ya mkutano kumalizika.
========  ======= =========
Na Beatrice Millinga
Kampuni ya Angels Moment ya jijini Dar es Salaam imetoa wito kwa wadau wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo kujitokeza na kudhamini tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana lililopewa jina la Mwanamke na Akiba na linalotarajiwa kufanyika kuanzia Februari 19 - 21, 2014 kwenye Ukumbi wa  Dar Live - Mbagala, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa wahabari katika ukumbi wa Serena leo, Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa Kampuni ya hiyo, Bibi Pamela David amesema kuwa makampuni na mashirika mbalimbali yatapata fursa ya kujitangaza,  na kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao kwa wanawake na vijana wa Kitanzania.
“Kwa kudhamini Tamasha hili wadau watapata sio tu fursa ya kutangaza biashara na huduma zao bali kujitangaza wao wenyewe na kutoa elimu kwa umma maana si wananchi wote wanauelewa wa huduma zitolewazo na mashirika na makampuni mbalimbali hapa nchini,” alisema Bi Pamela.
Kwa mujibu wa Bi Pamela, Tamasha hilo ni la kwanza na la aina yake kufanyika nchini Tanzania lenye lengo la kuongeza na kuchochea uelewa wa wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiwekea akiba.
“Tamasha hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada na maonesho,” alisema Bi Pamela.
Aliongeza kuwa washiriki watapata fursa ya kupata elimu juu ya kukabiliana na hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na usimamizi wa fedha.
Akizungumza mfumo utakaotumika kuendesha tamasha hilo, msemaji wa kampuni, Bi Pamela alisema “Tamasha litakuwa kwenye mfumo wa maonesho pamoja na vipindi vinne vya uwasilishaji wa mada mbalimbali toka kwa wanawake wafanyabiashara waliofanikiwa na wataalamu waliobobea kwenye nyanja hizo.
Kwa mujibu wa msemaji huyo watoa mada wanaotarajiwa kuwasilisha ni pamoja na Naibu Gavana Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Natu Mwamba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)  Bibi Irene Isaka.
Tamasha linatarajia kuwavutia washiriki 5,000 na waonyesha bidhaa 50 kutoka maeneo mbalimbali katika sekta ya usimamizi wa fedha. Pia, inatarajiwa kuvutia washiriki toka sekta nyingine ikiwemo biashara zenye mahusiano na suala zima la uhifadhi wa fedha na uwekaji wa akiba kwa wanawake.
Mgeni rasmi wa Tamasha hili anategemewa kuwa Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal.
Mualiko wa Mama Asha kwenye Tamasha hili unachagizwa na ujasiri na mchango wake, pamoja na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kusaidia wanawake, vijana na makundi mbali mbali yenye uhitaji nchini Tanzania.
Tamasha limedhaminiwa na Said Salim Bakhresa (SSB), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Benki ya CRDB, STANBIC, FINCA, Mamlaka ya  Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Wadhamini wengine ni pamoja na Mfuko wa UTT, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) na Kampuni ya Ashton Media.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA TAFAKURI MARIDHIANO KUELEKEA KATIBA MPYA, JIJINI DAR LEO.

0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, baada ya kufunguliwa rasmi rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia
 Picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo. 
 
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo.
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakijadiliana jambo
 Meza Kuuu.
 Picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiagana na wajumbe walioshiriki Kongamano hilo baada ya ufunguzi uliofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, baada ya kufunguliwa rasmi rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia.  Picha na OMR

MSANII NEMO KUPIGA SHOO LADY IN RED 2014

0
0
Na Andrew Chale.

MKALI  wa R&B na Afro Pop,  ambaye aliwahi pia kushiriki shindando la BSS,  Nemo, anayetamba na wimbo wa ‘My Number One’ aliyomshirikisha Ommy Dimpoz anatarajia  kupafomu kwenye  shoo ya miaka 10 ya onyesho la mavazi lijulikanalo kama ‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’ linalotarajiwa kufanyika Februari 14, kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions inayoandaa onyesho hilo , Asia Idarous Khamsin, alisema tayari msanii huyo ameingizwa kwenye listi ya wasanii watakaotoa burudani kali nay a aina yake siku hiyo ya Februari 14. Asia Idarous alisema msanii Nemo  anatarajia kuimba vibao vyake mbali mbali vikiwemo vya “Vumilia”, “Wife” na wimbo ulio kwenye chati ndani na nje ya Tanzania unaotamba kwa sasa wa  “My Number 0ne”.

“Hii ni ‘Surprise’ kwa wapendanao  katika onyesho letu la Miaka 10 ya jukwaa la Lady in red’ hivyo mbali na kushuhudia mavazi ya ubunifu yaliyobuniwa na wabunifu magwiji na wale wanaochipukia kwenye fani hii, pia watakonga nyoyo zao kwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa Msanii Nemo” alisema Asia Idarous.
Aidha, katika onyesho hilo, mbali na  Nemo,  pia kunatarajia kuwa na burudani kutoka mwanamuziki wa nyimbo za asili, Wanne Star na bendi ya Babloom Trio.

 Kwa upande wa wabunifu magwiji watakaopamba steji hiyo  siku hiyo ni pamoja na Mustapher Hasanal , Ally Remtulla, Lucky Creation, Martin Kadinda, Ghymkana Hilali,  Paka wear, Gabriel Molel, Fransiska Frankoo,  Shirima, Salim Ally, Ameed Abdul, Mgese Makory, Kiki Collection, Rose fashion, Diana Magesa, Rio Paul na wengine.

 Kwa upande wa wabunifu chipukizi: Faustin Simon, Water Edward, Brian Hango, Benedict Mnzava,Crissiwelly Uissoson,Willex Willibard, Jackson, Gumbala, Jabir Jumanne, Alabama King, Agusta Masaki, Nelson Tomas, Bebi Juliet Mtandu, Ummi fashion/Ummi Investiment Comapany, Asmahan Eva, Hassan Nasor, Juniper Mafuru, Ante Ngongi, Adam Hassan, Jaquline, Kijangwa na Waiz Shelukindo.

Katika onyesho hilo ambalo litafanyika siku hiyo ya Februari 14, ambayo pia itakuwa ni siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ , kiingilio kitakuwa sh 30,000 kwa viti vya kawaida huku viti maalum ikiwa sh 50,000. Tayari tiketi za onyesho hilo zimeanza kuuzwa ikiwemo vituo vya duka la Fabak fashion, lililopo mikocheni mkabala na kituo cha Mwalimu Nyerere huku kwenye hoteli ya Serena, zikipatikana mapokezi.

 Kwa mwaka huu onyesho hilo limedhaminiwa na adhamini mbalimbali wakiwemowadhamini wakuu ambao ni kinywaji cha Zanzi pamoja na kampuni ya nywele ya Darling.  Wengine ni CXC, Times fm, Clouds media, Vijimambo blog, michuzi media group, channel ten, Elite Computer, Eventlites, One touch-solution, Raysa Style, Paka Wear, Dj Bula, Magic fm, DTV, Jambo Leo, I View media, Vayle Spring, Voice of American na wengine wengi.

warsha ya mafunzo ya kemikali zinazodumu kwenye mazingira kwa muda mrefu

0
0
 Bi Magdalena Mtenga, Mkurugenzi msaidizi Idara ya mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, akimsikiliza mmoja wa washiriki hayupo pichani katika warsha  ya mafunzo ya kemikali zinazodumu kwenye mazingira kwa muda mrefu,jijini Dar es Salaam leo.
 Washiriki katika warsha ya mafunzo ya ya kemikali zinazodumu katika mazingira kwa muda mrefu wakimsikiliza muwezeshaji katika siku ya pili ya mafunzo hayo jijini Dar es Salaam leo.
 Dkt Roland Weber Consultant wa masuala ya kemikali zinazodumu kwenye mazingira kwa muda mrefu,ambae ni mumwezeshaji katika warsha ya mafunzo inayofanyika jijini Dar es Salaam akitoa mada katika warsha hiyo.
Washiriki wakifuatilia mada katika siku ya pili ya warsha ya mafunzo jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Evelyn Mkokoi)

Serikali yapongeza Tamasha la Krismasi

0
0

 SERIKALI kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) imeipongeza Kampuni ya Msama Promotions kufanikisha tamasha jipya la Krismasi lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Licha ya kampuni hiyo kupitia Kamati ya Maandalizi kukumbana na changamoto mbalimbali, Basata limeipongeza kampuni hiyo  kwa kuanza vema katika mikoa mitano lilikofanyika.

Akizungumza katika Kikao cha kuwasilisha ripoti ya tathmini ya Tamasha la Krismasi iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Basata, Ofisa Sanaa  wa Basata, Rajabu Zubwa alipongeza licha ya kwamba imekumbana na changamoto ikiwa pamoja na kulipeleka mkoa wa Tanga ambao una idadi kubwa ya waislamu ni wengi.

Zubwa pamoja na kupongeza alitoa mapendekezo yatakayopunguza gharama katika tamasha hilo na ili kufanikisha gharama ambazo zitawafikia walengwa ambao ni wenye uhitaji maalum, Kamati hiyo inatakiwa kupunguza  waimbaji kutoka nje  kwa kuwa viingilio ni vidogo. “Mnapoandaa tamasha jaribuni kutulia sehemu moja kwa ajili ya kukwepa hasara pia punguzeni idadi ya watu ni kubwa, gharama haiwezi kurudi,” alisema Zubwa.

Naye Ofisa Sanaa Mkuu, Philemon Mwasanga alipongeza Msama kuandaa tamasha hilo na kueleza lilikuwa zuri  na aliishauri Kamati kuwa makini na ualikaji wa waimbaji kutoka nje ya nchi kwa kuwa wengi  wamekuwa wakifanya kinyume  na maadili ya ufikishaji wa Neno la Mungu  kwa njia ya uimbaji.

Alisema waimbaji  wengi wa sasa wamemuweka Yesu nyuma hawana tofauti na wanamuziki wa Bongo Fleva huku akitaka ziwekwe sheria za tamasha kwa waimbaji hao zitakazodhibiti mambo mbalimbali  ikiwemo mavazi, nidhamu  na mengineyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Abihudi Mang’era alisema wamekumbana na changamoto nyingi ikiwa pamoja na kutopata wahudhuriaji wengi katika mkoa wa Tanga.  

Mang’era alisema changamoto nyingine ni viingilio vidogo hasa ukizingatia hakuna wadhamini kabisa na alitumia fursa hiyo kuwaomba Basata kuliona hilo na kuwasaidia katika matamasha yake yajayo.     

VIONGOZI WA KINONDONI MNALIONA HILI; KITUO CHA DALADALA CHA BIAFRA CHAGEUZWA DAMPO

0
0
Uchafu ukiwa nyuma ya kituo cha Biafra na ukitizama picha vizuri kuna abiria amekaa lakini cha kusikitisha nyuma yake kuna uchafu ambao unatoa harufu mbaya na pia kuna wafanya biashara katika eneo hili. Sehemu hii imekuwa kero kwa abiria wanaoshuka na hata wanaopanda magari kwenye hiki kituo cha Biafra kilchopo Kinondoni kwani kuna uchafu mwingi unaotupwa na wakazi wa eneo hilo mpaka kituo hiki kubadilishwa na kuwa dampo.
 Hii ndio hali halisi ya kituo cha Biafra kilichopo kwenye wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kilichogeuzwa kama sehemu ya kutupia takataka.
Jambo la kujiuliza ina maana hapa Biafra hakuna Dampo? Au uongozi wa eneo hili umelala mpaka kituo hiki kuwa na hali kama hii inasikitisha sana. 

PICHA NA PAMOJA BLOG

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAENDESHA DROO YA KWANZA YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI

0
0
 
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Allan Chonjo akitangaza washindi wa droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na kampuni hiyo nchini kote, kushoto kwake ni Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo, na kulia kwake ni Afisa Mwandamizi kutoka PWC Bwana Tumain iliyofanyika mapema leo jijini Dar es Salaaam.
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia  Serengeti Allan Chonjo akiongea kwa njia ya sinu na moja wa washindi wa droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti iliyochezeshwa mapema leo jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo.  Ambapo washindi wawili wamejishindia 'Samsung tablets' ambao ni  Mwl. John Yesaya(49) kutoka mkoani Kilimanjaro na  Salehe Mohamed(25) kutoka jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo(kulia)akizungumza na wana habari(hawapo pichani)katika droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti, jijini Dar es Salaam.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images