Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 222 | 223 | (Page 224) | 225 | 226 | .... | 1903 | newer

  0 0


  Kikosi cha Timu ya Golani Veteran ya Kimara Jijini Dar es salaam Kilichofanya Ziara Mkoa wa Morogoro.
  Kikosi cha Timu ya Moro Veteran Kilichoanza . 
  Moja ya Hekaheka katika Lango la Golani Veterani katika Mchezo wa Kirafiki Uliopigwa Katika Uwanja Wa Jamuhuri Mkoani Morogoro.
  Beki wa Golani Veteran Akiondosha Moja ya Hatari Katia Lango lake.
  Mshambuliaji  wa Zamani wa Timu ya Polisi Morogoro Ambaye kwa sasa anaichezea Timu ya Moro Veteran Mokil Rambo Akitafuta Mbinu za Kuwatoka Mabeki wa Golani Veteran Katika Mchezowa Kirafiki  Uliochezwa Katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro .
  Mchezaji wa Zamani wa Timu za Morogoro Adam Seleman wa Moro Veteran akiwa katika Hekaheka  za Kutafuta Mbinu za Kuwatoka Mabeki wa Timu ya Golani Veterani ya Kimara Dar es Salaam katika Mchezo wa KirafikiUliopigwa Katika Dimba la Jamuhuri Mkoani Morogoro.

  Wachezaji wakongwe wa Golani Veteran Ambao walikuwa Kivutio Katika Mchezo wa jana.

  Mwenyekiti wa Timu ya Moro Veteran Khamis Madole akipongezwa na Mchezaji Mwenzake Aliyefahamika kwa Jina la Seif  Baada ya Kuipatia Timu ya Moroveteran Goli na nne

  Timu ya Soka ya Moro Veteran ya Mkoani Morogoro jana  Wameichapa Timu ya Golani Veteran ya Kimara Dar es Salaam jumla ya Magoli 4 kwa Moja.Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Ulikuwa wa Kasi na Upinzani wa hali ya Juu.

  Hadi Mapumziko Matokeo Yalikuwa Sare ya Bila Kufungana.
  Kipindi cha Pili Moro Vetrani Walifungua Karamu ya Mgoli Katika Dk 50 Goli lilofungwa Na Seif baada ya Kupewa Pasi na Kufumua Shuti lilomshinda Golikipa.

  Moro Veterani Waliendela Kulishambulia Goli la wapinzani Wao Na Kufanikiwa Kupata Mabao Mawili Katika Dakika za 67 na 70 Kupitia kwa Mshambulizi wao Khamis .

  Magoli hayo yaliwachanganya Benchi la Ufundi la Gorani Veterani hali Iliyowafanya Kufanya Mabadiliko Haraka  na Kuwasaidia Kupata Bao La kufuta Machozi Katika Dk 79 ya Mchezo.Wakiwa Bado  wanaimani wanaweza Kuzudisha Magoli mawili yaliosalia walijisahau Na kukuta wakipigwa Goli na 4 katika Dk 87 Ya Mchezo Goli Lililofungwa na Khamisi Madole.

  Hadi Mwisho Moro Veteran 4 Golani Veteran 1
  Na MATUKIO NA VIJANA BLOG

  0 0

   Baadhi ya wasafiri waliokwama wakiangalia greda inayojaribu kutengeneza njia ili waweze kupita.
   Wasafiri wakiwa wamekwama eneo la hedaru
   Maroli na mabasi yakiwa kwenye foleni baada ya njia kuzibwa na mafuriko ya maji
   Wakandarasi wakijadiliana jambo ili kuweza kupata ufumbuzi
   Umati wa wasafiri wakiwa wanashangaa jinsi barabara ilivyozuiwa na maji
  Hii ndio hali halisi inavyoonekana malori yakiwa yamekwama katikati ya barabara.Magari zaidi ya 3000 yamekwama mda huu eneo la hedaru baada ya barabara kufungwa na kuzibwa na maji mengi yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha eneo hilo.Wasafiri wamekwama eneo hili kwani magari na mabasi pia magari ya mizigo yanashindwa kupita kwa kuwa njia haionekani.


  Kampuni ya ujenzi inayojenga barabara hiyo wanajitaidi kuchimba maeneo ya pembeni ili kuweza kuhamisha maji ili angalau njia iweze kuonekana.Hali ni mbaya eneo hili hivyo serikali inatakiwa kuwahi kwenda kutoa msaada wa kuweza kupunguza maji na hatimaye magari yaweze kupita.


  0 0

  JamiiProduction . jamiiproduction@gmail.com 12:57 PM (31 minutes ago) to bcc: me
  Bwn Solomon, Sunday Shomari na Herriet Shangirai wakijadili jambo ndani ya studio za Jamii Production. Washington DC
  Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
  Katika kipindi hiki, tumejadili suala la BAJETI KATIKA FAMILIA.
  umuhimu wake, namna ya kulitekeleza na mengine mengi.
  Wachangiaji studio walikuwa ni Herriet Shangirai, Sunday Shomari, Solomon na Mubelwa Bandio
  KARIBU UUNGANE NASI

  0 0

  MAFOTO PRODUCTION & ENTERTINMENT KWA MAHITAJI YAKO YA STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING, MUSIC & Mc's KATIKA SHEREHE YA AINA YEYOTE. 

  KAZI NYINGINEZO:- VIDEO EDDITING, COVER DISGNING, PPS ZA DK 3, POSTERS ZA AINA MBALIMBALI COVER CD PRINTING, BURNING CD N.K. WASILIANA NASI KWA NO, 0787 200005/0754, 0655-306109/0714 656660 

  BARUA PEPE:- muhidinuk@yahoo.co.uk,sufianimafotoblog@gmail.com AMA TEMBELEA www.sufianimafoto.com

  OFISI ZETU ZIPO KIJITONYAMA NYUMA YA KITUO CHA POLISI MABATINI, BARABARA YA SPIKA WA BUNGE

  0 0

  IMG_1007Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Balozi wa Israel nchini,  Mhe. Gil  Haskel, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe toka Umoja wa Ulaya (EU) kutoka kwa Mkurugenzi wa EU pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  Mkurugenzi wa EU pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Koen Vervaeke (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa EU nchini Tanzania Balozi  Filiberto Ceriani Sebregondi, bada ya kukutana nao  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  ujumbe toka Umoja wa Ulaya (EU) ukiongozwa na  Mkurugenzi wa EU pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu Bw. Koen Vervaeke, Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014. 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Burham Philbrook wa Shirika la Global Volunteers la Minnestota, Marekani, akishuhudiwa na Askofu Dkt. Owdenburg M. Mdegella wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Iringa walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jarida toka kwa  Bw. Burham Philbrook wa Shirika la Global Volunteers la Minnestota, Marekani, akishuhudiwa na Askofu Dkt. Owdenburg M. Mdegella wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Iringa walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014. PICHA NA IKULU


  0 0

  Na Andrew Chale
  WABUNIFU mbali mbali watakaopamba miaka 10 ya onyesho la mavazi lijulikanalo kama ‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’ linalotarajiwa kufanyika Februari 14, tayari majina yao yamewekwa hadharani. Onyesho la mwaka huu linatarajia kufanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam, Februari 14, huku asilimia ya mapato ya fedha hizo zinatarajia kusaidia wathirika wa dawa za kulevya wa kituo cha Kikale Kilichopo Mkoani Pwani.
  Akiongea na wandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fabak Fashions inayoandaa onyesho hilo, Asia Idarous Khamsin, alisema kila mwaka onyesho hilo huja kitofauti ikiwemo kuongeza vionjo mbalimbali katika kufikia mafanikio kwenye tasnia ya ubunifu  na mitindo ya mavazi hapa nchini.
  “Safari hii, steji ya Lady in red’, inatimiza miaka 10, huku ikijivunia kuibua vipaji vya wabunifu wengi hapa nchini, na wengine kwa sasa wanamajina makubwa kwenye yasnia hiyo, hivyo tutaendelea kutoa nafasi kwa wabunifu chipukizi mara kwa mara ilikufikia malengo yao” alisema Asia Idarous.
  Asia Idarous aliwataja wabunifu magwiji watakaopamba steji hiyo kuwa ni pamoja na Khadija Mwanamboka, Mustapher Hasanal , Ally Remtulla, Lucky Creation, Martin Kadinda, Ghymkana Hilali,  Paka wear, Gabriel Molel, Fransiska Frankoo,  Shirima, Salim Ally, Ameed Abdul, Mgese Makory, Kiki Collection, Rose fashion, Diana Magesa, Rio Paul na wengine.
  Kwa upande wa wabunifu chipukizi watakaopamba ni pamoja na Faustin Simon, Water Edward, Brian Hango, Benedict Mnzava,Crissiwelly Uissoson,Willex Willibard,  Jackson, Gumbala, Jabir Jumanne, Alabama King, Agusta Masaki, Nelson Tomas, Bebi Juliet Mtandu, Ummi fashion/Ummi Investiment Comapany, Asmahan Eva, Hassan Nasor, Juniper Mafuru, Ante Ngongi, Adam Hassan, Jaquline, Kijangwa na Waiz Shelukindo.
  Aidha, Asia Idarous aliongeza kuwa, kwenye onyesho hilo, pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo kutoka bendi ya Babloom Trio na Mwanamuziki mahiri wa nyimbo na ngoma za asili, Wanne Star. Katika onyesho hilo ambalo litafanyika siku hiyo ya Februari 14, ambayo pia itakuwa ni siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ , kiingilio kitakuwa sh 30,000 kwa viti vya kawaida huku viti maalum ikiwa sh 50,000.
  Tayari tiketi za onyesho hilo zimeanza kuuzwa ikiwemo vituo vya duka la Fabak fashion, lililopo mikocheni mkabala na kituo cha Mwalimu Nyerere huku kwenye hoteli ya Serena, zikipatikana mapokezi.
  Kwa upande wa wadhamini wakuu wa shindano hilo ni pamoja na kinywaji cha Zanzi pamoja na kampuni ya nywele ya Darling. Wengine ni CXC, Times fm, Clouds media, Vijimambo blog, michuzi media group, channel ten, Elite Computer, Eventlites, One touch-solution, Raysa Style, Paka Wear, Dj Bula, Magic fm, DTV, Jambo Leo, I View media, Vayle Spring, Voice of American na wengine wengi.

  0 0

   Hapa ni maeneo maarufu ( kama mtaa wa congo dar) sana mkoani Iringa,panajulikana kama Miyomboni kukiwa kimya kutokana maduka yote ya bidhaa muhimu yamefungwa na wananchi wanaendelea kupata taabu kutokana na mgomo wa kutumia mashine za kutolea risiti za TRA.(picha zote na Denis Mlowe )

  0 0


   Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Februari 10, 2014 juu ya Kongamano la  9  la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) ambao utafanyika kuanzia 11 – 14 Februari, 2014 Naura Springs Hotel, Arusha Tanzania. Katikati ni Katibu Mtendaji wa CTO, Prof. Tim Unwin, akifuatiwa na Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mahsriki (EACO) Hodge Semakula.

   Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Februari 10, 2014 juu ya kukamilika kwa maandalizi ya Kongamano la  9  la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) ambao utafanyika kuanzia 11 – 14 Februari, 2014 Naura Springs Hotel, Arusha Tanzania. Kulia ni Katibu Mtendaji wa CTO, Prof. Tim Unwin.
   Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze akifafanua zaidi juu ya Kongamano hilo 9  la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF)
   Katibu Mtendaji wa Commonwealth Telecommunications Organisation (CTO) Prof. Tim Unwin, akizungumza na wanahabari wa jijini Arusha juu ya kukamilika kwa maandalizi ya mkutano huo unaoanza Februari 11-14, 2014 katika hoteli ya Naura Spring Arusha.Kushoto ni Habbib Gunze, Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kulia ni Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), Hodge Semakula.
   Katibu Mtendaji wa Commonwealth Telecommunications Organisation (CTO) Prof. Tim Unwin, akizungumza na wanahabari wa jijini Arusha juu ya kukamilika kwa maandalizi ya mkutano huo unaoanza Februari 11-14, 2014 katika hoteli ya Naura Spring Arusha.
   Viongozi TCRA, CTO na EACO wakizungumza na wanahabari
   Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
   Wanahabari na maofisa wa TCRA wakiwa katika mkutano huo.
   Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), Hodge Semakula akielezea zoezi la uhamaji kutoka mfumo wa Analojia kwenda Dijitali kwa nchi za Afrika Mashariki hasa Tanzania ulivyofanikiwa. 
  Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombelezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72)  aliyefariki  dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI)  jijini Dar es Salaam.

  Marehemu Qorro ambaye wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwamo Waziri mdogo wa Kilimo na Ushirika na baadaye kuwa waziri kamili wakati wa awamu ya pili, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvuja damu kwenye mzunguko wa kichwa kulikosababishwa na hitilafu ya figo.
  Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. James Bwana, Marehemu anatarajiwa kuagwa rasmi kesho kabla ya kusafirishwa Jumatano hadi Kijiji cha Mbulumbulu, wilayani Karatu, mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Dkt Martha Qorro na wanafamilia wengine nyumbani kwa  aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72)  aliyefariki  dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI)  jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

  0 0


  NAPE NNAUYE

  DAR ES SALAAM, Tanzania.

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23. 

  Akitoa shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.

  Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa wananchi.

  Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.

  "CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini," alisema.

  Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata CCM ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na  Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo, Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro) na Mrijo (Dodoma).

  0 0

  Brazil is calling! Don’t miss the World Cup and Copacabana beach !
  On Wednesday last week, MOblog hosted an exclusive Q and A interview with the Brazilian Ambassador to Tanzania, Hon. Francisco Luz, ahead of the upcoming World Cup Tournament. Read On;
  DSC_0076
  MOblog Tanzania’s Chief Editor, Damas Makangale in an exclusive interview with the Brazilian Ambassador to Tanzania, Hon Francisco Carlos Soares Luz at his office.

  By Damas Makangale, MOblog Tanzania
  MOblog: What was your initial reaction when you heard that Brazil will host the 2014 World Cup?

  Ambassador Luz: I think like every Brazilian who is crazy about football, I was very excited with the news. At a time we knew that there was no competition since Columbia had retired its candidate so Brazil was standing alone. We knew [the World Cup] was supposed to happen in South America, so we are very happy and excited with the opportunity of hosting the world cup again after 64 years.

  MOblog: Brazilians are going to the world cup with a squad of younger and very promising players compared to Spain, Germany and Argentina. To what extent do you think it will help the team to win the trophy?


  Ambassador Luz: I think Scolari has done the right thing. He has mixed the team with young, talented players who are ready to present themselves to the world and become national heroes like Neymar da Silva Santos but he has included veterans; mature and experienced players.

  MOblog: Do you think Brazil will benefit from a home advantage and go on to win their first World Cup since 2002?

  Ambassador Luz: We have won the confederation cups and a home advantage will be a factor during the world cup finals. We believe that the home ground will make a difference to us.


  To read more click here

  0 0

   TIMU ya wasichana ya Tanzania imekabidhiwa zawadi ya Sh milioni 16 baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika Septemba mwaka jana nchini Nigeria.

  Timu hiyo ilitwaa taji hilo baada ya kuifunga Kenya bao 1-0 lililofungwa na Donisia Daniel katika fainali hiyo. Akipokea fedha hizo jana (Februari 10, 2014) Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Msanifu Kondo alisema.

  wanaishukuru Kampuni ya Airtel kwa kutimiza ahadi yao ya zawadi ya fedha hizo na tayari wamezikabidhi kwa makocha na wachezaji wa timu hiyo.

  Alisema kila mchezaji amepewa Sh 850,000 wakati kocha mkuu wa timu hiyo Rogasian Kaijage amepewa Sh milioni moja na laki mbili na kocha msaidizi amepewa Sh milioni moja.  “Tunawashukuru Airtel kwa kutoa fedha hizo za zawadi kwa timu hii na sisi tumewakabidhi wahusika,” alisema.

  Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema wao kama wadhamini wa mashindano hayo wametimiza ahadi yao kwa kukabidhi fedha hizo kwa mabingwa hao.

  “Kwa niaba ya Airtel Tanzania tunaipongeza timu ya wasichana ya Tanzania kwa kutwaa ubingwa huo, lakini pia tumetekeleza ahadi yetu ya kukabidhi zawadi, kama mnavyofahamu kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia mambo ya kijamii lakini pia michezo ikiwemo soka kupitia michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars kwa kushiriki na klabu ya Manchester United,” alisema.

  Mohamed Mharizo
  Ofisa Habari wa DRFA

  Februari 11, 2014

  0 0

   Bi Galvana Erlinda, mwakilishi kutoka, shirika la maendele la umoja wa Mataifa akisema machache katika warsha hiyo..
   Dkt Julius Ningu, Mkurugenzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais akimkaribisha mgeni rasmi katika warsha ya mafunzo ya kupitia mpango wa utekelezaji wa mkataba wa Stockholm unaohusu kemikali zinazodumu kwenye mazingira kwa muda mrefu.
   Sehemu ya washiriki wakisikiliza  katika warsha ya mafunzo ya kupitia mpango wa utekelezaji wa mkataba wa Stockholm unahohusu kemikali zinazodumu kwenye mazingira kwa muda mrefu.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula akifungua Warsha ya mafunzo ya kupitia mpango wa utekelezaji wa mkataba wa Stockholm unaohusu kemikali zinazodumu katika mazingira kwa muda mrefu, leo Jijini Dar Salaam.
  Picha ya pamoja wa washiriki katika warsha hiyo.(Picha zote na Evelyn Mkokoi).

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  (Picha na Freddy Maro).

  0 0

   Meneja katika Kitengo cha Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Dorothea Mabonye akibonyeza kitufe ili kumpata mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Mteja wa benki hiyo, Mary Malifedha Popote kutoka Kigoma amejishindia gari jipya aina ya Suzuki Swift lenye thamani ya shs milioni 28. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Abdallah Hemedy, Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Gaudence Shawa na Mkuu wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Musa Jallow. 
    Mkuu wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Musa Jallow (katikati) akizungumza katika hafla ya droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Gaudence Shawa,   Kaimu Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa NBC, Raymond Mutagahywa na Meneja wa Kanda w NBC, Rachel Mwalukasa.
  Meneja wa Kanda wa Benki ya NBC, Rachel Mwalukasa (katikati) akizungumza na mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa NBC, Raymond Mutagahywa na Mkuu wa Kitengo cha Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe.  

  0 0

  Jumuiya za Watanzania Italy,kwa pamoja walifanya mkutano mkuu wa kihistoria siku ya jumamosi tarehe 8/2/2014.

   Mkutano huo uliofanyika mjini Napoli,ulikuwa na madhumuni matatu makubwa.  kwanza kuimarisha mshikamano baina ya Jumuiya za Watanzania nchini Italy, na pili kuzungumzia kero na matatizo ya Watanzania wanaoishi Italy.Wajumbe walichangia yote yaliyokusanywa katika mikutano na vikao vya awali.

  Yote yaliyojadiliwa yatafanyiwa kazi na kufikishwa kunakostahili kwa ufumbuzi wa kudumu.

  Jambo kubwa la tatu, Wajumbe waliunda kamati ya pamoja ya diaspora yenye wajumbe kutoka NAPOLI,ROMA,MODENA,GENOVA NA PADOVA. Na kuweka majukumu. Wajumbe pia walimchagua:
   Ndugu Kagutta N.Maulidi  (Mwenyekiti)
   Ndugu Ricky JG.Bondo ( kaimu m/kiti)
  Ndugu Andrew Chole Mhela (katibu) 
   Ndugu Mwinyimwaka Sarai (kaimu/katibu),
  Ndugu LIlian Luhende (hazina)
  Ndugu Abdulrahaman A.Alli (mjumbe)
  Ndugu Erasmus Luhoyo (Mjumbe)
  Ndugu Livinus Mwereke (Mjumbe)
  Ndugu Awadhi Sulaiman (Mjumbe)
  Ndugu Judith Joseph  (Mjumbe)
  Ndugu Zacharia Madjid Mhessa (Mjumbe)

  Wajumbe wa mkutano wamependekeza kuwa baada ya kipindi cha miaka miwili  utafanyika mkutano wa kutathmini utendaji wa kamati kwa  ujumla.
  Mwisho mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy mh Abdulrahaman A.Alli aliwapongeza baadhi ya viongozi na wajumbe kwa kuwatunukia shahada za uongozi bora na uhadilifu.
  Pichani Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia Mh Abdulrahaman A.Alli(aliyeshika cheti)  akimtunukia cheti cha uadilifu na uongozi bora Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma Mh. Andrew Chole Mhela. 

  Mwenyekiti wa kamati ya Diaspora Mh Kagutta N.Maulidi akionyesha cheti alichotunukiwa na mh Mwenyekiti kwa uadilifu na uongozi bora wa jumuiya ya Watanzania Italy .

  Wajumbe wakifuatilia mkutano kwa makini

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italia Mh Abdulrahaman A.Alli nae alikabidhiwa cheti cha uongozi bora, anaemkabidhi ni mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Roma Mh.Erasmus Luhoyo. wengine ni Katibu Andrew Mhela(mwenye kitambaa shingoni) na wa pili ni Katibu mkuu mh Kagutta N.Maulidi na pembeni aliyevaa jacket ni katibu wa jumuiya ya watanzania wa Napoli Mjini Mh Livinus Mwereke.

  viongozi katika picha ya pamoja


  hii ndio kamati ya Diaspora  Mwenyekiti wa kamati ya Diaspora katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati.

  Kaimu Mwenyekiti wa Diaspora Mh Ricky JG.Bondo akifafanua jambo kwa mjumbe ndugu Mohamed Mnondwa, baada ya kikao.

  0 0


  duka_1_63817.jpg
  Mkuu wa mkoa wa Iringa, Dr. Christina Ishengoma leo amezungumza na wafanya biashara wa manispaa ya Iringa katika ukumbi wa community centre uliopo eneo la Kitanzini katika manispaa ya Iringa, mada kuu ilikuwa inahusu mgomo wa wafanya biashara kupinga mashine mpya za kutoa risiti zilizotolewa na TRA ili zitumike katika biashara zao.
  duka_2_19543.jpg
  baadhi ya wafanya biashara walio hudhuria katika mkutano huo uliofanyika leo.
  duka_9_e1545.jpg
  Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Iringa,Bw. Lucas Mwakabunge, akizungumza na wafanya biashara katika mkutano huo.
  duka_5_a19b2.jpg
  duka_3_dc400.jpg
  Pichani ni baadhi ya Wafanyabiashara wakimsikiliza Mkuu wa
  Mkoa katika mkutano huo.

  Mkuu wa mkoa huyo alisisitiza kuwa elimu inatakiwa kutolewa kwa wafanya biashara hao kuhusu umuhimu wa mashine hizo kwa kuwa wafanya biashara wengi wameonesha hali ya kutoridhishwa nazo na hata kufanya maandamano ya nchi nzima wakipinga matumizi ya mashine hizo na kutaka kendelea kutumia mfumo wao wa zamani wa kutumia vitabu.

  Mkuu wa mkoa huyo alidai kuwa yeye sio muhusika mkuu wa suala hilo lakini kama ilivyo, ni wajibu wake kuzungumza na hata kuwasaidia watu wake hivyo aliwataka wafanya biashara hao fungua maduka kwani kilio chao kimesikika na serikali inalifanyia kazi suala hilo.
  PICHA ZAIDI INGIA MJENGWA BLOG.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd cha Dar es Salaam (TPI), Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kusambaza dawa bandia na kusababisha hasara ya Sh148.3 milioni.

  Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi aliwataja washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo kuwa ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TPI, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msofe, Mhasibu Msaidizi, Fatma Shango pamoja na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), Sadick Materu na Evans Mwemezi.

  Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Nyigulile Mwaseba, Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro alisema katika shtaka la kwanza, Aprili 5, 2011, Madabida, Shamte, Msofe na Shango wakiwa na nyadhifa hizo kwenye kiwanda cha TPI walisambaza makopo 7,776 ya dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV) aina ya Antirectroviral.
  Kimaro alidai kuwa washtakiwa hao, walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 76 (1)(2) cha Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2003, wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halali na kwamba zimetengenezwa Machi, 2011 na muda wake wa kutumika unakwisha 2013 wakati wakijua kuwa si kweli.

  Katika shtaka la pili, Wakili Kimaro alidai kuwa Aprili 11, 2011, Madabida, Shamte, Msofe na Shango walisambaza na kuuza makopo 4,476 ya dawa bandia aina ya Antiretroviral walizokuwa wakijaribu kuonyesha kuwa zilikuwa na viambatanisho vya Starudine 30mg, Nevirapine 200mg, Lamivudine 150mg pamoja na fungu namba OC 01.85.

  Alidai kuwa washtakiwa hao waliweka viambatanisho hivyo wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halisi na kwamba zilitengenezwa Machi 2011 na muda wake wa kutumika ulikwisha Februari 2013 huku wakijua kwamba ni uongo.

  Katika shtaka la tatu wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kinyume na Kifungu cha 302 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
  Wakili Kimaro alidai kuwa kati ya Aprili 12 na 29, 2011, washtakiwa hao wakiwa na nia ya kulaghai, walijipatia Dola za Marekani 98,506 sawa na Sh148,350,156.48 wakijaribu kuonyesha kuwa kiasi hicho cha fedha ni malipo halali ya makopo 12,252 ya dawa aina ya Antirectrovial yaliyokuwa katika fungu (batch) namba OC 1.85.

  Alidai pia kuwa washtakiwa hao walikuwa wakionyesha dawa hizo bandia zilikuwa zimetengenezwa Machi, 2011 na kwamba muda wake wa kumalizika kutumika ni Februari, 2013 na wakafanikiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka MSD.

  Katika shtaka la nne, Materu na Mwemezi wakiwa ni Meneja wa Udhibiti Viwango na Ofisa Udhibiti Viwango wa MSD, kati ya Aprili 2 na 13, 2011 huku wakijua nia ya kutendeka kwa makosa hayo ya usambazwaji wa dawa bandia, walishindwa kuzuia kinyume na Kifungu cha Sheria namba 383 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

  Katika shtaka la tano, wakili huyo wa Serikali alidai kuwa kati ya Aprili 5 na 30, 2011, washtakiwa Madabida, Shamte, Msofe, Shango pamoja na Materu na Mwemezi, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi, walishindwa kutekeleza majukumu yao wakiwa watendaji.

  Alidai kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao kwa pamoja walishindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kusambaza makopo 12,252 ya dawa bandia wakijaribu kuonyesha kuwa zilitengenezwa Machi 2011 na kwamba zitakwisha muda wake wa kutumika Februari 2013 na kuisababishia mamlaka hiyo ya Serikali hasara ya Sh148,350,156.48.

  Washtakiwa wote walikana mashtaka yanayowakabili na upande wa mashtaka ulisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Akitoa masharti ya dhamana, Hakimu Mwaseba alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao wanafanya kazi kwenye taasisi zinazotambulika kisheria na kwamba kila mdhamini angesaini bondi ya Sh6,181, 256.

  Pia alimtaka kila mshtakiwa kutoa kiasi cha Sh12, 362,513 milioni taslimu mahakamani hapo au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha. Madabida na Materu waliachiwa huru baada ya kukamilisha masharti hayo huku wenzao wakipelekwa mahabusu kusubiri kuyakamilisha.
  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 24, mwaka huu itakapotajwa.

  0 0

   
   Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akifuatilia hotuba mbalimbali katika ufunguzi wa Kongamano la 9 la uhamaji wa mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda dijitali Afrika  2014 (DBSF)ulioanza leo jijini Arusha. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano kwa nchi za Jumuia ya Madola (CTO), Tim Unwin akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkomwa.

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkomwa akizungumza.
  Baadhi ya waalikwa ambao ni viongozi wa Vituo vya televisheni nchini Tanzania
   Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya TCRA wakifuatilia mijadala katika kongamano hilo.
    Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akifuatilia hotuba mbalimbali katika ufunguzi wa Kongamano la 9 la uhamaji wa mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda dijitali Afrika  2014 (DBSF)ulioanza leo jijini Arusha. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano kwa nchi za Jumuia ya Madola (CTO), Tim Unwin akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkomwa.
  Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy ambaye pia ndiye Mwendeshaji wa kongamano hilo, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habbi Gunze wakati wa kongamano hilo leo.
   Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano kwa nchi za Jumuia ya Madola (CTO), Tim Unwin akizungumza.

  Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akitoa hotuba kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Tanzania ambaye alipaswa kuwa mgeni rasmi.


   
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Waziri wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo jijini Arusha leo.
   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akishikana mkono na Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano la Jumuia ya Madola (CTO) Tim Unwin (kulia) baada ya Waziri Mukangara kufungua kongamano la tisa la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) mjini Arusha jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (katikati)
   Meza kuu katika picha mbalimbali za pamoja na washjiriki wote wa kongamano hilo la 9 la CTO na Uhamaji wa mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda Dijitali
   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Umoja wa mashirika ya Posta Afrika (PAPU), Younouss Djibrine (kushoto) baada ya Waziri Mukangara kufungua kongamano la tisa la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) mjini Arusha leo. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano la Jumuia ya Madola (CTO) Tim Unwin (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (wapili kushoto)
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akizungumza jambo na Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano la Jumuia ya Madola (CTO) Tim unwin (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (katikati)  baada ya Waziri Mukangara kufungua kongamano la tisa la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) mjini Arusha leo.

older | 1 | .... | 222 | 223 | (Page 224) | 225 | 226 | .... | 1903 | newer