Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Msama awapigia magoti wadhamini

$
0
0
 KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka na Krismasi, Kampuni ya Msama Promotions imewaomba wadau wenye nia ya kufanikisha maendeleo ya matamasha hayo kuwasaidia katika muendelezo wa matamasha yanayoandaliwa na kampuni hiyo, Aprili  mwaka huu kampuni hiyo iko mbioni kuandaa Tamasha la Pasaka.  

Kutokana na hali hiyo, wadau mbalimbali ambao wamepata kutoa ahadi za namba mbalimbali katika matamasha hayo wameombwa kutekeleza ahadi zao ili zitumike katika malengo yaliyokusudiwa. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema wadau mbalimbali wa muziki wa Injili, wakiwemo baadhi ya viongozi wamekuwa wakitoa ahadi ambazo utekelezaji wake umekuwa mgumu.
 
“Wapo baadhi ya watu wanakuja katika matamasha yetu, wanatoa ahadi nzito hasa za fedha, lakini tamasha likishamalizika wanashindwa kutekeleza ahadi zao na ndiyo huwaoni tena, tunashukuru wapo wengine huwa wepesi kutimiza walichoahidi.“Huwa haya matamasha tunayaandaa kwa malengo maalum, ukitaja ahadi yako huwa tunaipa thamani kubwa na ukishindwa kuitimiza unatuangusha na hilo ndilo linatuharibia sana mipango yetu,” alisema Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi.

Aliwaomba baadhi ya viongozi na wadau wengine ambao wamepata kutoa ahadi mbalimbali kwenye Tamasha la Pasaka kuhakikisha wanatekeleza ahadi zao kama walivyozitoa na kusisitiza kuwa hakuna sababu ya kuwataja majina kwani wenyewe wanajitambua.

“Tunaamini pengine wana mambo mengine ndiyo sababu tumeandika barua kuwakumbusha wakati huu tukielekea katika maandalizi ya Tamasha la Pasaka,” alisema. 

TAHA yapata mwenyekiti mpya

$
0
0

TAASISI inayoshughulika na kilimo cha maua na mboga mboga nchini (TAHA) imemteua Bw. Eric Ng'imaryo kama Mwenyekiti wake mpya kuchukua   nafasi iliyoaachwa wazi na Bw. Colman Ngalo, ambaye ameiendesha    taasisi hiyo kwa mafanikio kwa takribani miaka kumi ya utawala wake.



Sambamba na uteuzi huo pia Bw. Ng'imaryo, pia taasisi hiyo ilimpata
Makamu Mwenyekiti mpya pamoja na wajumbe nane wa Bodi ya TAHA pia
walichaguliwa katika Mkutano Mkuu wa TAHA (AGM) uliofanyika hivi
karibuni jijini Arusha.

Miongoni mwa wanaounda Bodi mpya ya taasisi ya TAHA ni pamoja na: Bi.
Fatma Riyami , Bw. Ravi Bhalerao, Bw. Herald Peeters , Bw. Juma
Lossini , Bw. Robert Daniel, Bw. Tjerk Scheltema na Bw. Adrian Moss.
Bw. Juma Ally Juma amechaguliwa kama mwakilishi kwenye taasisi ya Bodi
ya TAHA kutoka jimbo la uchaguzi Zanzibar.

Taasisi hiyo ya TAHA kwa sasa imekuwa ikikuza msendeleo ya wakulima
nchini ambayo hatua inayoonesha kujitolea katika kukuza maendeleo ya
sekta ya maua na mboga mboga nchini.

Kablya ya uteuzi huo, Bw. Ng'imaryo alikuwa Mwenyekiti wa Arusha
Blooms Company Limited, kampuni ambayo ni mwanachama wa TAHA na moja       ya wazalishaji wakubwa wa mboga mboga nje ya nchi na nchini. Bw.


Ng'maryo kitaalamu ni mwanasheria ambaye amekuwa akifanya kazi zake za     kisheria katika Tanzania tangu mwaka 1987. Hata hivyo, Mwnyekiti huyo   mpya ni mfanyabiashara, mkulima na mwandishi mahiri.



"Nimepata heshima kubwa na ya kipekee kabisa kuweza kuchaguliwa kuwa
Mwenyekiti mpya wa TAHA na niuangalia uteuzi huu kutekeleza wajibu na
majukumu kwa kufanya kazi na Bodi na Sekretarieti ili kuhakikisha
kwamba dira yetu inatekelezwa. Nami nitakuwa sehemu ya kuifanya
taasisi yetu ya TAHA kuwa na mafanikio zaidi katika siku zijazo.
Ninapenda pia kuwashukuru Bw. Colman Ngalo, Mwenyekiti anayemaliza
muda wake, kwa uongozi wake mzuri.


Bw. Ngalo amekuwa nguzo ya TAHA kwa miaka kumi iliyopita. "Bw.
Ng'imaryo pia alitoa shukrani zaidi kwa Bi. Jacqueline Mkindi ,
Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA, samabmba na Sekretarieti nzima ya TAHA
kwa mchango wao mkubwa kwa taasisi na sekta nzima ya maua na mboga
mboga. "Jacqueline amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa mfano. Utendaji wake   
wa kazi umeijenga taasisi yetu uaminifu na heshima kutoka kwa Serikali    
na Washirika wa Maendeleo."

Katika hotuba yake, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Bw. Ngalo
ameusifu uamuzi wa TAHA wa kuweza kumchagua Bw. Ng'imaryo ambapo
ameleelezea kuwa na imani na uongozi wake ambao utaleta mageuzi ya
kweli kwenye sekta ya maua na mboga mboga. "Kwa niaba ya Bodi ya TAHA
inayomaliza muda wake, napenda kumpongeza Bw.Eric kwa kuchaguliwa
kwake kuwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TAHA na ni mategemeo yangu kuwa      
tutaendelea kufanya kazi pamoja naye katika miaka ijayo.

Mchanganyiko wa ujuzi wake katika sekta ya maua na mboga mboga na
uzoefu mkubwa sambamba na utaalamu unafanya kuwa mtu bora kuchukua
nafasi ya Uenyekiti wa TAHA na sekta yenye maendeleo endelevu. Napenda
pia kuishukuru Sekretarieti ya TAHA na wanachama wake kwa ushirikiano
wao bora katika muongo uliopita. Kwa ushirikiano tumepata mafanikio
mkubwa. Mimi ninajisikia fahari kubwa kukabidhi taasisi hii yenye
mafanikio ambayo bado ina fursa kubwa kwa ukuaji zaidi katika TAHA na
sekta nzima kwa ujumla."

TAHA ni taasisi ambayo ni mwanachama wa sekta binafsi ambapo imekuwa
ikishiriki kwa ufanisi katika kubadilisha kilimo cha sekta ya maua na
mboga mboga toka kuanzishwa kwake mwaka 2004.

Kutokana wa hatua za uwepo wa TAHA , sekta ya maua na mboga mboga
nchini na kufanikiwa kuvutia washirika mbali mbali kutoa misaada
mikubwa ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania na Washirika kama vile
USAID, BEST- AC, Ubalozi wa Uholanzi , ITC, na Serikali Finland.

TAHA inatoa sapoti mbali mbali kwa wadau wa sekta ya maua na mboga
mboga ikiwemo kuwajengea uwezo kwenye majukwaa, kulinda na kukuza
maslahi ya watendaji katika sekta hiyo ya maua yaani wazalishaji ,
wauzaji, wasindikaji, na watoa huduma ya maua, matunda , mboga, viungo
, mimea na mbegu za maua.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion,Alex Msama azindua albam ya dvd ya kwaya.

$
0
0


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion,Alex  Msama,(katikati) akizindua Album ya Dvd ya kwaya ya Mtakatifu Benedicto ya Kanisa la Kathoriki kigogo Luhanga Jijini Dar es salaam,msama alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la uzinduzi wa album hiyo ambapo alichangia Shilingi milioni 1,500,000/kulia ni Mratibu wa tamasha la Pasaka,John Melele,(kushoto)ni Paroko wa kanisa hilo Father Vitus Sedlmair.

MTEMVU ANOGESHA MASHINDANO YA SERIKALI ZA MITAA TEMEKE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Jamaica ya Mtaa wa Keko Molemo, Paulo Peter zawadi ya sh. 300,000 baada ya kuifunga timu ya DotmondMtaa wa Jamaica  ya Mtaa wa Keko Magurumbasi katika mechi ya kuchagua wachezaji wa kuunda timu ya kombaini ya Kata ya Keko jana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Elimu (DUCE), Chang,ombe Dar es Salaam . Jamaica lishinda mabao 3-1. Pia timu ya Dotmond ilizawadiwa sh. 200,000.
Abbas Mtemvu  akimkabidhi Nahodha wa timu ya Dotmond ya Maa wa Keko Magurumbasi zawadi ya sh. 200,000 baada ya kuwa washndi wa pili katika mchezo huo.
Bakari Hemed wa timu ya Dotmond akka mca Mbegu 
Wapenzi wa soka wakiangalia mechi hiyo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

BONANZA LA JOGGING & GLOBAL BREAKING NEWS LAFANA NDANI YA DAR LIVE

$
0
0
Washiriki wakimalizia mbio zao kutokea Uwanja wa Taifa mpaka Ukumbi wa taifa wa Burudani wa Dar Live.
Klabu mwenyeji, Kejo Community wakiwa jukwaani wakicheza kwa furaha katika Bonanza hilo.
Msanii wa Msondo Music Band, Hassan Moshi (mwenye Mic) akikosha nyoyo za wana Jogging waliohudhuria kwenye Bonanza la Jogging & Global Breaking News leo.
Timu ya klabu ya Jogging ya Magenge 20 wakipepetana na Spurs (jezi nyeupe) katika mchezo wa pete hatua ya nusu fainali, katika bonanza hilo.
Wacheza drafti John Gwile (kushoto) na Mohamed Abdallah wakichuana kwenye Bonanza la Jogging & Global Breaking News leo.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtevu akimpatia cheti cha shukrani Mratibu wa Dar Live, Luqman Maloto kilichotolewa na klabu mwenyeji, Kejo Community.


Mratibu wa Dar Live, Luqman Maloto akionesha cheti cha Heshima kwa Dar Live, kilichotolewa na klabu ya jogging ya Kejo kutoka Temeke.
Msondo Music Band, wakifanya yao jukwaani katika Bonanza la Jogging & Global Breaking News ndani ya Dar Live.
Washiriki kutoka klabu mbalimbali wakiwa tayari kuanza mbio zao kutoka Uwanja wa Taifa kuelekea Ukumbi wa taifa wa Burudani, Dar Live, katika Bonanza la Jogging & Global Breaking News.
Gari la huduma ya kwanza (kushoto) nalo lilikuwepo katika mbio za jogging kwa ajili ya kunusuru wale watakaopata matatizo.
Mkali wa staili ya 'Mapanga' kutoka TMK Halisi, Rashid Ziada 'KR Mulla' akifuatilia kwa karibu shoo ya Msondo ndani ya Dar Live.
(PICHA ZOTE NA NICODEMUS JONAS / GPL)

MTOTO WA MGIMWA ASHINDA KURA ZA MAONI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

$
0
0
 Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu Dkt William Mgimwa, akiongea kwa niaba ya familia wakati wa mazishi ya baba yake kijijini Magunga jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Na Francis Godwin, Iringa

Mtokeo  ya  kura  za maoni  ndani ya  CCM yametangazwa usiku wa kuamkia leo  huku mtoto wa aliyekuwa mbunge  wa  jimbo hilo Godfrey Mgimwa akishinda kwa  kishindo  katika  nafasi hiyo, akifuatiwa na Jackson Kiswaga katika matokeo hayo.

Godfrey Mgimwa amepata  kura 342 huku Kiswaga  akipata kura 170 na mkuu wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa akiambulia  kura 42 .

Matokeo hayo  yaliyotangazwa  katika  ukumbi wa shule ya  sekondari  Mwembetogwa mjini Iringa yanaonesha mgombea Peter Mtisi kapata  kura 33, Msafiri Pangagira kura 8, Bryson Kibasa kura 7, Edward Mtakimwa kura 3 na Thomas Mwiluka akiambulia kura 2

HATIMAYE MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KWA AJILI YA MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA YATANGAZWA RASMI.

$
0
0
 Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) , Sharon Mariwa  Meneja wa Mahusiano OXFAM, Francis Bonda(Kaka Bonda) Mkurugenzi wa Usanifu katika Kampuni ya DMB pamoja na Mkamiti Mgawe Afisa utetezi wa haki za kiuchumi OXFAM, wakati wa kutangaza rasmi majina ya waliochaguliwa katika Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula leo.
Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) akielezea Mchakato mzima wa kazi ilivyokuwa kabla , wakati wa kuwatafuta washiriki wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula na kutaja rasmi majina ya waliochaguliwa katika usahili huo.

   Meneja wa Mahusiano OXFAM Sharon Mariwa  akielezea utaratibu utakao fuatia baada ya kutangazwa rasmi majina ya waliochaguliwa katika shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula
 Francis Bonda(Kaka Bonda) Mkurugenzi wa Usanifu katika Kampuni ya DMB akitilia mkazo baadhi ya mambo wakati wa kutangaza rasmi majina ya waliochaguliwa kuingia Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
 Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) akijibu Maswali yaliyo ulizwa na waandishi wa Habari.

Baadhi ya Waandishi wa Habari na wadau Mbalimbali wakiwa wanasikiliza kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa katika Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.




*************
Majina ya waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wa Mama Shujaa wa Chakula / Maisha Plus 2014.
Usaili:
Mama Shujaa watapigiwa kura mtandaoni ili kupata washiriki 20 ambao wataingia kijijini Maisha Plus. Zoezi la kuwapigia kura litafanyika baada ya uhakiki ‘verification’ pamoja na upigaji picha kuthibitisha taarifa walizojaza kwenye fomu.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake. INALIPA.
Vijana wa Maisha Plus watagawanywa katika makundi mawili ya watu 20 na kupelekwa katika vijiji vilivyochaguliwa Iringa na Zanzibar, huko wataishi pamoja na familia zilizochaguliwa na kutakiwa kuishi maisha sawa na familia hizo. Zoezi kuu litakuwa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa vijiji hivyo kama changamoto za maji, n.k.
Baada ya siku 7 wanakijiji watatakiwa kuwapigia kura vijana hao ili kupata jumla ya vijana 18 watakaopelekwa katika kijiji cha Maisha Plus kuungana na wenzao 12 kutoka nchi za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni Maisha Plus REKEBISHA.

Majina

Mama Shujaa wa Chakula
  1. Amina Kupela Chikaponya – Mtwara
  2. Anna James Yuda – Morogoro
  3. Anna Mwanilyela Chrisant – Katavi
  4. Bahati Muriga –Mwanza
  5. Clara Ancilla Ibihya – Pwani
  6. Cristina Kurwa Malale – Zanzibar
  7. Dina Rusoti – Mara
  8. Dionisia Rashidi Karata – Tanga
  9. Doricus Msafiri Shumbi – Singida
  10. Edina Jamas – Mbeya
  11. Elinuru Moses Pallangyo – Arusha
  12. Elizabeth Matayo – Geita
  13. Elizabeth Simon – Morogoro
  14. Ezeleda Chedego – Dodoma
  15. Fredina M. Said – Shinyanga
  16. Gladness Ebenezery Mmary – Kilimanjaro
  17. Grace G.D. Mahumbuka – Kagera
  18. Janeth Niima – Manyara
  19. Kuruthumu Ramadhani Mwengele – Tanga
  20. Leah Dominick Mnyambugwe – Dodoma
  21. Mary Athanaz Ndasi – Rukwa
  22. Mary John Mwanga – Singida
  23. Mary Kessy – Dar es salaam
  24. Neema Robert – Simiyu
  25. Nyachum Haji Ame – Zanzibar
  26. Pendo Musa – Morogoro
  27. Santina Mapile – Njombe
  28. Thereza Kitinga – Mwanza
  29. Zaituni Shedrack Kalenbi – Kigoma
  30. Zamda Daniely Mgonganga – Iringa

Vijana wa Maisha Plus

  1. Adolph Anacleth - Mwanza
  2. Agatha Kalesu – Rukwa
  3. Ally Thabit - Mwanza
  4. Anastazia John – Mara
  5. Asumta Mwingira – Dar es salaam
  6. Ausi Abdul Moyo – Ruvuma
  7. Bakari Khalid – Shinyanga
  8. Boniphace Meng’anyi Nyankena – Dar es salaam
  9. Charles Daniel – Simiyu
  10. Douglas Said Msalu - Arusha
  11. Ellymathew Kika – Njombe
  12. Elizabeth Joachim - Tabora
  13. Fahamni Kaite Mwadini – Zanzibar
  14. Farida Ally – Pwani
  15. Fadhili Isanga - Kilimanjaro
  16. Flora John - Singida
  17. Frederick Joseph Ndahani – Singida
  18. Hyasinta T. Hokororo - Mtwara
  19. Jane Julio Kalinga – Iringa
  20. John Sylvester Malima - Geita
  21. Joyce Jacob Mushy - Arusha
  22. Marriam Mosses - Shinyanga
  23. Mary Nicholaus Kavishe – Manyara
  24. Mbonimpaye N. Nkoronko – Rukwa
  25. Mohammed Selemani Lipemba - Lindi
  26. Moureene K. Daud - Kagera
  27. Nelson Daniel – Dar es salaam
  28. Ngoma Abdallah – Kigoma
  29. Osama Norman – Mbeya
  30. Otilia Selestin Simime - Mbeya
  31. Said Salum – Katavi
  32. Salumu Saidi Johari – Mtwara
  33. Scholastica Deusidedith – Geita
  34. Seif Mohamed Salum - Tabora
  35. Shaaban Masoud Shaaban – Zanzibar
  36. Shida Keneth Mganga – Dodoma
  37. Shishira G. Mnzava - Morogoro
  38. Thomas P. Mgazwa – Dodoma
  39. Yassini Hamisi Suddi – Dar es salaam
  40. Zaharani Yusuph Hossen – Tanga



Taarifa zaidi Tembelea : www.maishaplus.tv

CCM WASHINDA KATA ZOTE TATU MKOA WA IRINGA, CHADEMA YASHINDA NJOMBE MJINI

$
0
0
 Wafuasi wa CCM Iringa  wakimpongeza kaimu katibu  wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kwa kufanikisha  chama  hicho kushinda  uchaguzi mdogo kata ya  Nduli.
Wafuasi wa CCM kata ya Nduli  wakiwa  wamemnyanyua  juu  juu  aliyekuwa mgombea  udiwani kata ya Nduli Bw Mtove  baada ya  matokeo kumpa ushindi wa kishindo leo 
...........................
CHAMA  cha  mapinduzi (CCM)  mkoa  wa  Iringa  kimefanikiwa  kutetea kata  zake  zote tatu ambazo  leo   wananchi  wameshiriki  kupiga kura  kuwachagua madiwani  kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki  dunia.

Wafuasia  wa  CCM  walimpongeza  aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na  kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa  Hassan Mtenga na kudai kuwa  kazi  yake  inaonesha  wazi  safari yake ya  kulitwaa jimbo la Iringa mjini.

Matokeo katika vituo vyote  tisa  ambavyo  wananchi  wa Nduli  walipata  kuvitumia kupiga kura  ,kituo cha Mawasiliano  CCM (57),Chadema(28),Zahanati  CCM( 114), Chadema ( 47), Shule Nduli  CCM(70) Chadema(39), KIngonzile shule CCM(105) Chadema(82),Mibata CCM(48) Chadema(103), MTalagala CCM(95),Chadema(54),Godauni   CCM(138 ,Chadema(52),Njiapanda CCM (75) Chadema (52),Msisina  CCM (156 ) Chadema (31)

Katika  Matokeo hayo ambayo hadi sasa  majira ya saa 12.50  bado msimamizi wa uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 854 huku  hadema  wakifuatia kwa kura 487,Mbali ya  matokeo  hayo ya kata ya  Nduli pia  CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za  wilaya ya  Kilolo.

Katika kata ya  Njombe mjini mgombea  wa  Chadema amembwaga mgombea wa CCM ambapo  matokeo yanaonyesha  mpinzani wake ameongoza katika kituo kimoja pekee   kwa tofauti ya  kura  2  huku  katika vituo vyote  Chadema ikiibuka kidedea.

CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII ZANZIBAR CHAFANYA SHEREHE ZA MAHAFALI YA TANO.

$
0
0
  Mkurugenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Bi. Zulekha Khamis Omar akitoa maelezo juu maendeleo ya Chuo katika Mahafali ya tano Chuoni hapo.
  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Khamis Mussa Omar akieleza machache kuhusu muelekeo wa Chuo hicho na kumkaribisha Mgeni rasmin kutunuku vyeti kwa wahitimu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizunguza na wahitimu mbalimbali (hawapo pichani) mara baada ya kuwatunuku vyeti na stashahada katika Mahafali ya tano Chuoni hapo, (kulia yake) Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Khamis Mussa Omar na (kushoto) Kaimu Mwenyekiti Bi. Naila Jidawi.
 Baadhi ya wahitimu wa Mapishi ya vyakula na Uokaji wakiwa wamesimama mara baada ya kutunukiwa vyeti na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk katika sherehe zilizofanyika Chuoni hapo. 
 Baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika sherehe ya Mahafali ya tano ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii  Maruhubi Zanzibar. 
 Baadhi ya wahitimu wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (hayupo pichani) ambae ni mgeni rasmin wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi Zanzibar. 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akimpa zawadi ya mlango kwa niaba ya wanafunzi wa ICT & ACCOUNT, Maalim. Hassan Mrisho Haji katika sherehe ya Mahafali iliyofanyika Chuoni hapo.


Wapiga Picha nao wakiuza picha zao mara baada ya kumaliza kwa Mahafali chuoni hapo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

Article 0

TAI YATOA MAFUNZO KWA VITENDO JUU YA KUNAWA MIKONO NA KUSAFISHA KINYWA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KILIMANI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Aspiration Initiatives - TAI Bw. Gwamaka Mwabuka akitoa maelekezo kwa mwanafunzi wa darasa la pili shule ya Msingi Kilimani Juma Abdul jinsi ya kunawa mikono kwa usahihi ili kuipeka magonjwa. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wanafunzi toka Denmark waliopata mualiko na TAI kupitia taasisi ya Global Platform. 

  Wanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Kilimani wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kusafishwa kinywa na kuepukana na magonjwa yanayotokana na kutosafisha kinywa.

1Baadhi ya wanafunzi w shule ya awali ya Kilimani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waliowatembelea kuwafundisha swala zima la usafi shuleni hapo kupitia miradi ya Mikono Ming’avu (MiMi) na Kinywa Kisafi (KiKi) chini ya Taasisi isiyo ya kiserekali ya Tanzania Aspiration Initiatives – TAI. 


=========      ==========   ==========

TAI YATOA MAFUNZO KWA VITENDO JUU YA KUNAWA MIKONO NA KUSAFISHA KINYWA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KILIMANI JIJINI DAR ES SALAAM

10 Februari, 2014, Dar es slaam, Tanzania

Taasisi isiyo ya kiserikali ya TAI - Tanzania Aspiration Initiatives imefanya mafunzo ya kulinda afya kwa vitendo kwa wanafunzi Zaidi ya 200 wa Darasa la Kwanza, la pili na darasa la awali katika shule ya msingi Kilimani iliyopa Sinza Uzuri wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa miradi miwili inayojulikana kama Mikono Ming’avu (MiMi) na Kinywa Kisafi (KiKi).

Miradi yote ina lengo kuu la kupambana na magonjwa yanayoweza kuzuilika kama Magonjwa ya tumbo na yale ya meno na kinywa yanayoathiri zaidi watoto. Mafunzo hayo pia yalishirikisha Vijana wengine kutoka nchini Denmark walio nchini katika ziara ya kimasomo chini ya Jukwaa la kimataifa la Global Platform.

Mikono Ming’avu (MiMi) ni mradi uliyojikita katika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa watoto wa shule za msingi kutatua tatizo la magonjwa yanayosababishwa na mikono michafu kama vile Pneumonia na homa ya Matumbo (Diarrhea). Mradi huu tayari umeshawafikia Zaidi ya watoto 1000 katika baadhi za shule za msingi jijini Dar es salaam huku malengo ni kufikia shule zote za msingi Tanzania nzima.

"Hatua hizi za TAI ni baada ya kuona Watanzaia wengi hawana tabia ya kunawa mikono na sabuni kwa ufasaha ambapo ni moja ya sababu inayochangia magonjwa yanayoweza kuzuilika, lakini pia yanaathiri ukuaji wa mtoto. Kila mwaka watoto Zaidi ya milioni 3.2 duniani walio chini ya miaka 5 wanakufa kwa sababu ya homa ya matumbo na pneumonia yakiwa ni magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo kwa watoto baada ya malaria hasa katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara, Tanzania ikiwepo" alisema Bw. Gwamaka Mwaibuka, Katibu Mkuu wa TAI. 

Kinywa Kisafi (KiKi) ni ni moja kati ya mradi ya TAI ukiwa na lengo la kupunguza tatizo la magonjwa ya Kinywa na meno kwa watoto ambapo taasisi hiyo hufanya mafunzo kwa vitendo kwa kushirikiana na wataalam kuwafundisha watoto njia sahihi za kufanya usafi wa meno na kinywa na kuhimiza tabia ya kusafisha kinywa kuanza tangu utotoni.

TAI ni taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha maisha ya kila mmoja katika jamii hasa watu wanaoushi katika mazingira magumu na umasikini kupitia sekta tano za Elimu, Afya, Ujasiriamali, Teknolojia ya Habari na Mazingira. Kwa taarifa Zaidi ingia www.tai.or.tz au Tufuate katika ukurasa wetu wa Facebook www.facebook.com/tai2012

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAKABIDHI MISAADA KWA VITUO VITATU VYA JIJINI DAR.

$
0
0
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa Islamic Orphans,Halima Mpeta (kushoto),hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya kulipia ada za shule za watoto hao
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akiwapa vifaa vya shule watoto wa kituo cha TOVICHIDO.
Sehemu ya misaada hiyo ya vitu mbalimbali iliyotolewa na Kampuni ya Msama Promotions, kwa vituo vitatu vya watoto waishio katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa Islamic Orphans,Halima Mpeta (kushoto),akipkea msaada wa vitu mbalimbali kutoka katika mfuko wa Tamasha la Pasaka,Kutoka kwa Kampuni ya Msama Promotions Ltd.
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akimkabidhi kiasi cha shilingi laki saba Mlezi wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha TOVICHIDO,Honoratha Michael kwa ajili ya kulipia ada za shule za watoto hao.
=======  ========  =========

Msama akabidhi misaada kwa vituo vitatu


KAMPUNI ya Msama Promotions waandaaji wa  Matamasha ya Krimasi na Pasaka, jana ilikabidhi misaada mbalimbali kwa vituo vitatu vya jijini Dar es Salaam, ikitimiza ahadi ya kuisaidia jamii kabla ya Tamasha la mwaka huu linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama misaada hiyo iliyogharimu shilingi milioni 7 imekabidhiwa katika vituo vya TOVICHIDO cha Temeke Maganga, Malaika Kids cha Mwananyamala na kituo cha Yatima cha Mwandaliwa.

Msama alisema katika sehemu ya msaada huo pesa taslim shilingi milioni 2.9 ni ada kwa wanafunzi na nyingine ni kwa vifaa mbalimbali yakiwemo madaftari, sabuni za mche, unga, mafuta ya kupaka na  sukari. Aidha Msama alisema misaada hiyo imetokana na mfuko wa Tamasha la Pasaka kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la Krismasi ambalo walikabidhi misaada ya shilingi milioni 4.

Mkurugenzi wa TUVICHIDO, Honarata Michael alimpongeza Msama kwa kuwajali watoto na jamii kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa, Halima Mpeta alisema anamshukuru Msama kwa kujali jamii kwani katika kituo chake si mara ya kwanza kukisaidia na amezidi kumuomba aendelee na moyo wa kukisaidia kituo chake na vingene vyenye mahitaji.

VALENTINES DAY @ SHEKINAH GARDEN

SHULE 22 ZAPATIWA MSAADA WA VITABU WILAYA YA KILOLO

$
0
0
 Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akizungumza na baadhi ya wakuu wa shule za sekondari zilizoko katika wilaya ya kilolo baada ya kukabidhi vitabu katika shule hizo. Kushoto kwake Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Ilula
 Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akionyesha moja ya vitabu ambavyo amekibadhi kwa shule 22 za wilaya ya Kilolo halfa zilizofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ilula.
 Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akimkabidhi Mwenyekiti Huduma za Jamii wa Halmashauri ya wilaya Kilolo, Anna Kulanga moja ya mfano wa vitabu walivyokabidhi katika shule za sekondari wilaya ya Njombe.
 Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilula.
 Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi mwenye nguo ya njano akiwa na walimu wa shule za sekondari zilizopatiwa msaada wa vitabu kutoka shirika la CAMFED.(Picha zote na Denis Mlowe)
Baadhi ya Maboksi ya Vitabu yaliyokabidhiwa kwa shule 22 zilizoko wilaya ya kilolo.

========  =======  =========
SHULE 22 ZAPATIWA MSAADA WA VITABU WILAYA YA KILOLO

Na Denis Mlowe,Ilula

Katika kuhakikisha kiwango cha elimu nchini kinakua,shirika lisilo la Kiserikali la Campaign for Female Education (CAMFED)  chini  ya mpango wake kuwasomesha watoto wa kike limetoa misaada ya vitabu 54,935 kwa shule 22 za sekondari zilizoko katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa vyenye thamani ya shilingi milioni 55.

Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Ilula mwishoni mwa wiki mgeni rasmi Mwenyekiti Huduma za Jamii wa Halmashauri ya wilaya Kilolo, Anna Kulanga alilishukuru shirika hilo kwa msaada huo kwa kuweza kuwafikia wanafunzi wa shule za Iringa vijijini.

 “Tumefurahi sana kupata vitabu mbalimbali kwani shule ya sekondari za hapa zina  changamoto ya upungufu wa vitabu hasa vya sayansi na kulifanya somo hilo kuwa na wanafunzi wa chache, lakini hivi sasa kutokana na msaada wa vitabu vilivyo tolewa vitaongeza ufaulu kwa wanafunzi wetu kutokana na uwingi wa vitabu wenyewe kwa shule zilizofaidika na msaada huo” alisema Kulanga

Aliwataka walimu na wanafunzi  wavitumie vitabu hivi vizuri kwa kuvitunza kwa lengo la kutumika kwa muda mrefu wakati wa masomo yao na kuamini kwamba vitabu vivyo vitaleta ufanisi  katika kukuza uelewa wa mwanafunzi katika matumizi sahihi ya lugha ya kiingereza.

Aidha alisema vitabu hivyo vitumike kwa wanafunzi wote kwa wa shule husika na kuwaasa wanafunzi wa shule zilizofaidika na msaada huo kuacha tabia mbaya ya kuuza vitabu na kuwataka walimu wa shule hizo kufatilia kwa makini wanafunzi wote watakaopatiwa vitabu hivyo.

Naye Mwalimu mkuu wa sekondari ya Irole Laurence Maluka akiongea kwa niaba ya wakuu wa sekondari 22 zilizofaidika na msaada huo wa vitabu alisema msaada huo wa vitabu utaweza kuwa saidia wanafunzi kuwa na uweza wa kujisomea zaidi na kuwawezesha kufaulu hadi kwenda chuo kikuu,kwani hapo awali kulikuwa na changamoto kubwa katika shule zetu ambapo uwiano ulikuwa kitabu kimoja wanafunzi  5 lakini kwa sasa ni vitabu 5 kwa mwanafunzi mmoja.

“Ni jambo la kulishukuru sana shirika la CAMFED kwa msaada huu utapunguza zaidi, kwa kweli huu ni msaada mkubwa katika kuboresha taaluma na kuinua ufaulu hivyo tunaomba program hii ya shule zetu iendelee ili kuwafikiwa wanafunzi wengi zaidi katika wilaya ya Kilolo” alisema Maluka

Kwa upande wake Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi amewataka wanafunzi wa sekondari zote wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuongeza uwezo wa kujisomea ufaulu wa wanafunzi unaongezeka kupitia msaada unatolewa na shirika hilo.

Alisema  vitabu hivi vitunzwe ili viweze kuwafaidisha wanafunzi wengi kwa kuwa  vitaleta faida kwa wanafunzi wengi zaidi katika kujisomea na kuwataka walimu wakuu wawapatie wanafunzi kila mmoja vitabu vitano na kwenda navyo nyumbani hadi amalizapo elimu ya sekodari na kuweza kuvirudisha.
 
Alizitaja shule zilizofaidika na msaada huo ni shule ya sekondari Ilula, Nyalumbu, Mazombe, Irole,Lundamatwe, Selebu, Ngangwe, Uhambingeto, Lukosi, Mlafi Na Ndekwa.

Shule nyingine ni shule za za sekondari za Mtitu, Kilolo, Lulanzi,Ukwega, Udzungwa, Dabaga, Kitowo, Mawambala, Masisiwe, Madege na Makwema.

UMOJA WA MATAIFA WASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA UTAMADUNI MZURI WA KUENZI WANAWAKE WANAOLETA MABADILIKO KWENYE JAMII

$
0
0
DSC_0017
Picha juu na chini ni Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za jijini Dar es Salaam na kuwaonyesha picha na kuwapa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo wakinamama wamekuwa wakifanya kwa mustakabali kwa kuleta usawa na haki za wanawake duniani.

Shirika la Ufaransa la Alliance Francaise de Dar es Salaam liliandaa safari ya maonyesho iliyopewa jina “women in Resistance by the talented French photo-journalist Pierre-Yves Ginet.
Mwandishi wa habari huyo mpiga picha Pierre-Yves Ginet ambaye alifanya kazi ya kutafuta wanawake wanaojituma katika maisha yao ya kila siku na kazi zake zimeweza kuwapa ari na moyo wakinamama wengi Afrika.

Kati ya 2001 na 2006, alisafiri zaidi ya nchi 17 akipiga picha za wakinamama ambayo katika shughuli zao waliweza kufungua ukurasa mpya na kubadilisha historia katika kizazi cha leo.
Katika shughuli na katika njia tofauti walizotumia katika kubadilisha maisha wa wakinamama wengi duniani, wanawake kupitia kazi za picha Ginet wameweza kuwa na dhamira moja kubwa nayo ni kubadilisha maisha ili kuweza kuwa matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi kwa sasa na baadaye.

Maonyesho hayo ya lengo la kuwapa usawa wakinamama wote kupitia mabara yote hapa duniani na hasa nchi zinazoendelea, sehemu za vita.
Na sehemu kubwa ya picha hizo zinaonyesha jinsi wakinamama wanavyopambana ili kujikwamua katika unyonge na ukandamizaji wa aina yoyote hapa duniani.
DSC_0025
DSC_0071
Mmoja wa wananfunzi akibadilishana mawazo na Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet anayetumia maonyesho ya picha mbalimbali kuelimisha jamii kupitia picha hizo.
DSC_0065
Afisa Habari kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwa wanafunzi wa shule za sekondari mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani inayoambatana na siku ya Wanawake Duniani ni kufikisha sifuri katika kuondoa swala ukeketaji duniani.

Ujumbe unasema kwamba ukeketaji umepungua katika sehemu kubwa ya dunia na takwimu zinasema kwamba zaidi ya wanawake na wasichana 125 milioni ambao wanaishi katika dunia ya leo katika nchi 29 za Afrika na Mashariki ya kati walifanyiwa vitendo vya ukeketaji, na kama swala hii likiendelea zaidi ya wasichana 86 milioni duniani watafanyiwa vitendo vya ukeketaji kufikia mwaka 2030.
DSC_0102
Salome Anyoti kutoka shirika la umoja wa mataifa la wanawake akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa sekondari wa kutoka shule mbalimbali hapa Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kuangali picha za wakinamama walioleta mabadiliko katika maisha yao na wengine kwa ujumla.
DSC_0069
DSC_0030
Hizi ni baadhi ya picha za wanawake nchini Tanzania ambao wameleta mabadiliko katika maisha yao na wengine hapa nchini.
DSC_0028
DSC_0048
Baadhi ya picha zinazoonyesha matukio mbalimbali yaliyokusanywa na Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet.
DSC_0051

TUWASAIDIE WATOTO WAISHIA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-MSAMA

Twanga Pepeta kupagawisha Wapendanao Mzalendo Pub Ijumaa

$
0
0
Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ watafanya onyesho maalum siku ya wapendanao ‘Valentine Day’, kwenye ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Onyesho hilo litakalofanyika Ijumaa litajulikana kama Dodoma Wine Valentine Show. 

Mratibu Joseph Kapinga amesema onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Dodoma Wine, Freditto Entertainment na Saluti5. 

Kapinga alisema siku hiyo Twanga Pepeta watatambulisha nyimbo na staili mpya ya uchezaji. Mratibu huyo alisema kuwa siku hiyo Twanga Pepeta pia itapiga nyimbo zao za zamani zilizowapatia umaarufu. 
Baadhi ya nyimbo hizo ni Kisa Cha Mpemba, Fainali Uzeeni, Mtu Pesa, Safari 2005, Aminata, Busu 2000 na nyinginezo. 

Bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigono pia itapiga nyimbo zao za kisasa kama Nyumbani ni Nyumbani, Dunia Daraja, ‘Mwana Dar es Salaam’, ‘Shida ni Darasa’, ‘Rafiki Adui’, ‘Mwisho wa Ubaya ni Aibu’, ‘Nazi Haivunji Jiwe’ na ‘Sitaki Tena’. 

Bendi hiyo inaundwa na wanamuziki kama Kalala Junior, Dogo Rama, Saleh Kupaza, Luiza Mbutu, Badi Bakule, Greyson Semsekwa, Rama Pentagon, Mirinda Nyeusi, Kala Junior, na Janet Isinika katika safu ya uimbaji. 
 Kwa upande wa upigaji vyombo wapo James Kibosho, Jojo Jumanne, Moshi Kinanda, Miraji Shakashia, Gody Kanuti, Kaposho, huku safu ya unenguaji ikiwa, Saidi Matongee, Mandela, Abdilayi Zingu, Sabrina Pazi, Vicky, Hamida na Grace.

Rays of Light Exhibition imprints its foot on the Land of the Kilimanjaro

$
0
0
Rt. Hon. Mizengo Peter Pinda, the Prime Minister of the United Republic of Tanzania (left) and mr. Jehangir Bhaloo, President of the Aga Khan Council for Tanzania officially cutting the ribbon at the opening ceremonies of
Rt. Hon. Mizengo Peter Pinda, the Prime Minister of the United Republic of Tanzania (left) and Mr. Jehangir Bhaloo, President of the Aga Khan Council for Tanzania, officially cutting the ribbon at the opening ceremonies of the Rays of Light Exhibition at the Diamond Jubilee Hall in Dar es Salaam, Tanzania. (Photo: RAYSOFLIGHT/Aly Z. Ramji).
Rt. Hon. Mizengo Peter Pinda, the Prime Minister of the United Republic of Tanzania listens to Karim Kanji, (tour guide)  articulating a point  on  the Rays of Light Exhibition. Photo_ Aly Z. Ramji
Rt. Hon. Mizengo Peter Pinda, the Prime Minister of the United Republic of Tanzania and Mr. Jehangir Bhaloo, President of the Aga Khan Council for Tanzania, receiving a tour from Karim Kanji(tour guide) for the Rays of Light Exhibition. (Photo: RAYSOFLIGHT/Aly Z. Ramji).

After visiting France, Portugal, United States, United Kingdom, UAE, Uganda, and Canada, the Rays of Light: Glimpses into the Ismaili Imamat, finally makes its hallmark debut on Tanzanian soil. The much-anticipated Exhibition marks a significant milestone for Tanzania as it coincides with the upcoming 50th Anniversary of the Union of Tanganika and Zanzibar.

Opened officially today at the Diamond Jubilee Hall in Dar es Salaam, by the Rt. Honourable Mizengo Peter Pinda, the Prime Minister of the United Republic of Tanzania, the Ismaili Jamat and the peoples of Tanzania will have an exclusive peek into the world of the Shia Ismaili Imamat and the role of the Aga Khan development(AKDN) Globally.

The vision of both the late Sir Sultan Mohamed Shah(Aga Khan III) and a glimpse of the work of H H the Aga Khan over the past 50 years, are demonstrated through the varied projects that are in existence today.

During the opening ceremony, amid the joy and fanfare at the Diamond Jubilee Hall, Honorable Mizengo Pinda, thanked the Aga Khan Shia Imami Ismaili Council for Tanzania for organizing the event, and stated "We are here to celebrate this historic event worldwide, which indeed reflects the life and work of His Highness Prince Aga Khan, a true pioneer and one of Tanzania's most committed and trusted friends. A person whose family and community have been the pride of the great things we are proud of as a Country."

For Tanzanians, this marks a truly exclusive occasion; many of the featured projects demonstrate AKDN’s rich history in the country. The Imamat initiatives, specifically in socio-economic and cultural programs date back over a century in Tanzania, with the establishment of the first Aga Khan Girls School in Zanzibar in 1905. By the 1960’s there were nearly 65 Aga Khan Schools across the nation. The Aga Khan Education Services is currently planning the construction of a $30 million Aga Khan Academy, which will be affiliated with all other Aga Khan Academies globally.


Another integral program in the country is the current establishment of the Aga Khan University in Arusha. The AKU plays an integral role in educating skilled professionals with an ethic of social responsibility and commitment to serving their community. The AKU Arusha Campus will boast professional graduate schools in management, law, government and public policy, journalism and tourism to name a few.

The Aga Khan Health Services Tanzania has had a major impact in the country, with the first dispensary being established in 1929. Since then, numerous other health initiatives through AKHST have been established; these include the Aga Khan Hospital, as well as numerous Outreach Health Centers in Mwanza, Morogoro, Mbeya, Iringa, Arusha, Dodoma and Mbezi Beach, and of course the newly inaugurated Oncology wing, which was opened in January 2014..

The historical association between Tanzania and the Ismaili Imamat span over a century exemplified by H H the Aga Khan’s presence at the Independence of Tanganyika in 1961, it was in 1991, that the Aga Khan signed an Accord of Cooperation for Development with the then President, H.E. Ali Hassan Mwinyi. Just a decade later, in 2001, former President H.E. Benjamin William Mkapa signed an official protocol with H H the Aga Khan enhancing the collaboration between the AKDN and Tanzania, by formalizing the establishment of a mission and enabling it to facilitate the optimal utilization of resources for the AKDN’s objectives.

President of the Aga Khan Council for Tanzania, Mr. Jehangir Bhaloo during his opening remarks stated, "The Rays of Light’ is a celebration of a life. Not just any life. It is a celebration of the life and work of the Imam of the time. In our Shia ethical tradition, the Imam leads not only in the interpretation of the faith but also in the effort to improve the quality of life of his community and of wider societies within which the community lives. A guiding principle of the Imamate’s institutions, according to His Highness Aga Khan is to “replace walls that divide with bridges that unite.”

With far too many development programs to list, it is known that the cooperation between Tanzania and the AKDN has significantly impacted the lives of many Tanzanians. Given this unique history with Tanzania, the Rays of Light Exhibition will also be visited by H.E. Dr. Mohamed Gharib Bilal, the Vice President of the United Republic of Tanzania, as well as former Tanzanian Presidents H.E. Al-Haj Ali Hassan Mwinyi and H.E. Benjamin William Mkapa.

kituo cha mabasi cha makambako kam a kinonekavyo pichani.

$
0
0
 Stand ya makambako kama inavyoonekana ikiwa imejaa matope kutokana na mvua zinazoendelea mkoani Njombe na Iringa. Imekuwa kero kwa wakazi wa hapo na wafanyabiashara katika stand hiyo. 
 Wamachinga wakiendelea kufanya biashara katika mabasi yanayoingia katika stand ya Makambako. (Picha zote na Denis Mlowe).

Mkuu wa jeshi la polisi mstaafu ashinda kwenye promosheni ya Airtel Tanzania Mimi ni Bingwa

$
0
0
Afisa Uhusiano wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania Jane Matinde, (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu PhilemonNathaniel Mgaya aliyejishindia shilingi milioni tano (5m/-) ikiwa ni zawadi ya wiki katika promosheni ya Mimi ni Bingwa. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishini mwa wiki katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
========  ======  ========
Mkuu wa jeshi la polisi mstaafu ashinda kwenye promosheni ya Airtel Tanzania Mimi ni Bingwa

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu PhilemonNathaniel Mgaya anakila sababu za kuwa na furaha baada ya kuibuka mshindi wa shilingi milioni tano (5m/-) za Airtel Tanzania Mimi ni Bingwa promosheni zinazotolewa kila wiki.

Hili linakuja wakati bado wiki chache tu kampuni hiyo ya mawasiliano kutangaza mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 ambaye atapatikana katika kilele cha promosheni hiyo.  Akizungumza wakati wa droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Jane Matinde, Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania alisema matokeoi mazuri ya promosheni hiyo inadhihirisha dhamira na jitihada za kampuni za kuwasaidia wateja wake.

“Airtel kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa leo hii inaendelea kuzawadia wateja wengine, tukielekea katika droo kubwa ambayo itachezeshwa hivi karibuni, droo itakayomwezesha mshindi mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni 50.

“Philemon Nathaniel Mgaya ambaye anapokea hundi yake leo hii, ni mmoja kati ya washindi wetu wa kila wiki aliyejishindia shilingi milioni 5 katika promosheni hii iliyobadilisha maisha ya watanzania wengi.

“Tangu promosheni ya Mimi ni Bingwa ianze katikati ya mwezi Novemba mwaka jana, tumeona watanzania wengi wakishinda kila siku na kila wiki. Airtel kupitia Airtel Money imekuwa ikihakikisha wanaojishindia zawadi za chini ya shilingi milioni 5 wanapokea pesa zao ndani ya masaa 24 bila ya kukatwa garama za kutoa, wakati wale waliojishindia shilingi milioni 5 wanapata pesa zao kupitia akaunti zao za benki,” alisema Jane.

Alisema kuwa wateja wote wa Airtel bado wananafasi ya kujishindia milioni 50 pesa taslim, kutokana na kuwa mshindi atapatikana kupitia bahati nasibu.

“Kwa mujibu wa vigezi na masharti ya promosheni, kila namba iliyojisajili kwenye promosheni, hata kama mteja amejibu swali moja tu, atakuwa ameingia kwenye droo kubwa.

“Huu ni wakati sasa wa wateja wengine wa Airtel ambao hawajajisajili kwenye promosheni waingie kwenye promosheni kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neon “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo, unaweza kuwa mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50,” alisema Jane.

Alisema kuwa washindi wa tiketi wa awamu ya kwanza ya safari iliyogharamiwa kila kitu kwenda Old Trafford wamesharejea kutoka Uingereza na kuongeza kuwa wale wa awamu ya pili wataondika nchini hivi karibuni wakifuatiwa na wa awamu ya tatu na ya mwisho kabla ya mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.

Mara baada ya kupokea hundi yake ya shilingi milioni 5, Philemon Nathaniel Mgaya alisema pesa alizopokea zitamsaidia kutanua biashara yake aliyoianzisha baada ya kustaafu kazi katika Jeshi la Polisi.

“Ninafuraha ya pekee kuweza kushinda milioni 5 za Mimi ni Bingwa, nitazitumia pesa hizi kwa makini kwa kuongezea mtaji katika biashara yangu. Naishukuru Airtel kwa hili na napenda kuwahakikishia wateja wengine wa Airtel kuwa nao wanaweza kushinda katika promosheni hii. Nitaendelea kujibu maswali zaidi na zaidi ili nijiweke katika nafasi nzuri ya kujishindia zawadi kubwa ya shilingi milioni 50,” alisema Philemon.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images