Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA ‘FOUNDATION FOR BENEFACTOR OPPORTUNITY EDUCATION

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Joe Ricketts Kiongozi wa ‘Foundation for Benefactor Opportunity Education’, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Februari  7, 2014 kwa mazungumzo. Kulia ni Martin Russell Kiongozi wa Taasisi hiyo nchini Tanzania.   Ujumbe huo una lengo la kusaidia Tanzania kuboresha mfumo wa utoaji elimu kwa matumizi ya ‘Tablet’. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib BIlal, akizungumza na ujumbe wa ‘Foundation for Benefactor Opportunity Education’, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 7, 2014 kwa mazungumzo.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.  Makame Mbarawa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, pamoja na ujumbe wa ‘Foundation for Benefactor Opportunity Education’, baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam. Picha na OMR


MKUU WA WILAYA YA MAKETE AWAKUTANISHA POLISI NA MADEREVA WA BODABODA

$
0
0
Na Edwin Moshi, Makete
Kutokana na ukosefu wa elimu ya sheria barabarani miongoni mwa madereva bodaboda wilayani Makete mkoani Njombe kunakopelekea madereva hao kukamatwa na askari wa usalama barabarani mara kwa mara, mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro amefanya kikao na waendesha bodaboda hao

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete, waendesha bodaboda hao walipata fursa ya kutoa kero zao na kuuliza maswali ambayo yalikuwa yakijibiwa papo kwa papo na Muu wa polisi wilaya ya Makete, askari wa usalama barabarani na Meneja msaidizi wa TRA Makete

Akizungumza kwenye kikao hicho Mkuu wa polisi wilaya ya Makete (OCD) Alfred Kasonde amekanusha vikali tuhuma zinazoelekezwa kwa askari wake kuwa wanakula fedha wanazotoza kama faini kwa vyombo vya usafiri wanavyotoza kutokana na makosa mbalimbali na kuongeza kuwa ni vingumu kwa askari ambaye amekuandikia faini ya kosa lako kwenye kitabu cha serikali kula fedha hiyo

Bw. Kasonde amesema askari wake hawana vitabu vya risiti na hawaruhusiwi kutembea navyo kwa kuwa jeshi la polisi lina wahasibu wanaokusanya fedha hizo, hivyo kwa wilaya ya Makete dereva akiandikiwa faini na askari, askari haruhusiwi kupokea fedha na badala yake atakuandikia karatasi maalum maarufu kama notification na baada ya hapo dereva huyo atakwenda kulipa faini hiyo kituoni

Amewataka madereva hao kuacha kuwapa fedha ya faini askari hao na badala yake wahakikishe askari aliyewakamata anaandika kosa hilo kwenye kitabu cha faini, huku akionesha rundo la risiti za madereva bodaboda ambao wamelipia faini lakini hawajafika kuchukua risiti zao kwa madai kuwa fedha walizotoa zililiwa na askari

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro amewataka madereva hao kuhakikisha wanajikamilisha kwa vitu vyote vinavyohitajika kama sheria za usalama barabarani zinavyolelekeza ili kuepukana na adha ya kukamatwa mara kwa mara na askari na kutozwa faini

Mh Mariro amesema ni kweli madereva wengi hawajui sheria za usalama barabarani lakini sheria hazitambui kuwa hawafahamu sheria, hivyo ili kuepukana na adha hiyo wanatakiwa kuwa na vitu vyote vinavyohitajika kama leseni ya udereva, leseni ya biashara, bima, kadi ya pikipiki, stika ya nenda kwa usalama, kofia ngumu(helment 2) pamoja na pikipiki yenye vyake vifaa vyote

Amesema kwa kulitambua hilo mkuu huyo atafanya mazungumzo na chuo cha VETA Makete kifanye mafunzo maalum kwa madereva hao kwa gharama nafuu ili wazifahamu sheria za usalama barabarani pamoja na kupata leseni za udereva

Katika kikao hicho madereva hao walikuwa wakiuliza maswali mengi ya ufahamu ambapo walijibiwa maswali yao yote na kuondoka kwa furaha na uelewa wa mambo mbalimbali ya usalama barabarani
 Kikao cha waendesha bodaboda kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete hii leo.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akionesha kitabu cha polisi kwa ajili ya kutoza faini za makosa ya usalama barabarani.
Mkuu wa polisi(OCD) wilaya ya Makete Alfred Kasonde akionesha risiti za faini ambazo zimetelekezwa na baadhi ya madereva ambao wengi wao wamekuwa wakilalamika kuwa fedha hizo zimeliwa na askari.
 Meneja Msaidizi wa TRA Makete Hamis Zumba akifafanua jambo kwa madereva bodaboda Makete.
 Dereva bodaboda aliyejitambulisha kama Alex akiuliza swali kwenye kikao hicho
 Mwalimu wa VETA Makete Bw. Mathew Komba akifafanua jambo kwenye kikao hicho

CHAMA CHA WANANCHI CUF CHAFANYA MKUTANO NA WANDISHI WA HABARI OFISINI KWAO VUGA MJINI ZANZIBAR.

$
0
0
  Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha Wananchi CUF Salum Bimani akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ofisi yao, Vuga Mjini Zanzibar.
 Mwandishi wa Habari wa ZBC Dennis Bilal akiuliza swali kwenye mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa na Chama cha CUF Ofisni kwao Vuga, Mjini Zanzibar leo. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa CUF (hayupo pichani) Salum Bimani katika Ofisi ya Vuga, Mjini Zanzibar.
===========  ========  ==========
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar  

Chama cha Wananchi (CUF) kimeilalamikia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutokana na jinsi ilivyosimamia uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliofanyika tarehe 2 mwezi huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya CUF, Vuga Mjini Zanzibar leo, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa Chama hicho Salim Bimani amesema Uchaguzi huo haukuwa huru na haukuwa wa haki.Amesema vitendo vya  kuvurugwa uchaguzi huo vilianza kujitokeza kuanzia  wakati wa  kampeni na siku ya uchaguzi lakini pamoja na kutoa taarifa kwa Tume ya Uchaguzi hakuna hatua yoyote iliyochukua.

‘’Chama cha CUF kilibaini tokea mapema maandalizi ya fujo na matumizi mabaya ya nguvu za dola pamoja na Vikosi vya Serikali, ambavyo viliandaliwa kwa dhamira ya makusudi ya kuwapa haki wasiostahiki na pia kuwanyima watu wengi haki yao ya kufanya maamuzi ya kidemokrasi’’, alisema Salim  Bimani. Aliongeza kuwa upo ushahidi kwamba Vikosi vilitumika kuwalinda na kuwasafirisha wapigakura mamluki kutoka sehemu  nyengine kuja kupiga kura  bila ya hatua yopyote ya kisheria kuchukuliwa.

Bimani alidai kuwa vikosi hivyo vilithubutu kuwatisha  baadhi ya wananchi waliopaza sauti kupinga mwenendo huo haramu wa uchaguzi. “ Wananchi na Chama cha Wananchi, CUF , walijenga matumaini makubwa ya kuona Uchaguzi huru na wa haki ukifanyika katika zama hizi ambazo Zanzibar inaongozwa na Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, chini ya misingi ya maradhiano ya kisiasa, inayozingatia amani, utulivu, demokrasi na mshikamano kupitia siasa za kistaarabu’’, aliongeza Mkurugenzi  Bimani .

Alisema kutokana na kasoro nyingi katika uchaguzi huo mdogo, CUF imekosa imani na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Daftari la Kudumu la wapigakura kutokana na kuchezewa na halipo kwa misingi ya kutekeleza demokrasia, Haki na Uadilifu. Bimani alirejea kauli ya Chama hicho kutaka Tume ya Uchaguzi (ZEC) ivunjwe ili kutoa fursa ya kupatikana Mamlaka nyengine huru itakayoweza kusimamia Uchaguzi wa Haki na wa Kidemokrasia.

Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki ulifanyika kufuati  kujiuzulu aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Mansour Yussuf Himid mwishoni mwa mwaka jana.

Finally its happening in London, Mfalmeeeeee,

$
0
0

 Finally its happening  in London, Mfalmeeeeee,


The one and only, Mzee Yusuf  akijulikana kama King of Taarabu, anakuja London kwa show moja tu Show yenye hadhi, show ya watu wanaojuwa raha za Pwani na show ambayo hupaswi kukosa kuhudhuria.



Ni kwa kiingilio cha Twenty Pound Only ndani ya The Ville 640 Ripple Road BARKING.
Njoo upandishwe Jahazini, Njoo Tulambe na Njoo unukie marashi huku tukionja raha za Mpenzi Chocolate,



Yaaaani itakuwa Hatari Bin Dangerrrr

Rais Kikwete akutana na Rais wa Kampuni ya TBEA ya China,pia afanya mazungumzo na Lord Mandelson

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Kampuni ya China Tebian Electrical Apparatus Stocks Company(TBEA) ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kampuni hiyo inashughulika na ujenzi wa miundombinu ya umeme.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Lord Mandelson ikulu jijini Dar es Salaam leo.Lord Mandelson amewahi kushika nyadhifa za uwaziri katika serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu Tony Blair na Gordon Brown.Lord Mandelson kwa sasa ni mwenyekiti wa taasisi ya Global Counsel.(picha na Freddy Maro) 

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Kairuki Azindua Kampeni Care For Me!

$
0
0
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hizo za kuhamasisha jamii na makundi mbalimbali kuchangia na kumjali mtoto aliye katika mazingira hatarishi na yatima zinalenga kuwasaidia watoto zaidi ya 12,000 hadi kufikia mwisho wa kampeni yaani mwaka 2016.  
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hizo za kuhamasisha jamii na makundi mbalimbali kuchangia na kumjali mtoto aliye katika mazingira hatarishi na yatima zinalenga kuwasaidia watoto zaidi ya 12,000 hadi kufikia mwisho wa kampeni yaani mwaka 2016.Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akitia saini sehemu maalumu kutoa ujumbe wake mara baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine fedha zitakazopatikana katika kapeni hiyo zitahakikisha zinaongeza idadi ya vituo vya SOS kuwasaidia watoto yatima na waliopo katika mazingira hatarishi. Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akitia saini sehemu maalumu kutoa ujumbe wake mara baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine fedha zitakazopatikana katika kapeni hiyo zitahakikisha zinaongeza idadi ya vituo vya SOS kuwasaidia watoto yatima na waliopo katika mazingira hatarishi.Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Anna Maembe akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua kampeni. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Anna Maembe akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua kampeni.Watoto wa Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam wakiwa kwene hafla hiyo. Watoto wa Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam wakiwa kwene hafla hiyo.Mkurugenzi wa SOS Tanzania, Mr. Anatory M. akizungumza na wageni waalikwa kabla ya uzinduzi. 
Mkurugenzi wa SOS Tanzania, Mr. Anatory M. akizungumza na wageni waalikwa kabla ya uzinduzi.Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akiwa katika moja ya darasa la awali liloloendeshwa na Kijiji cha SOS, darasa hilo pia linatumiwa na watoto wa kawaida ambao hufundishwa pamoja na wale wa kituo hicho. Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akiwa katika moja ya darasa la awali liloloendeshwa na Kijiji cha SOS, darasa hilo pia linatumiwa na watoto wa kawaida ambao hufundishwa pamoja na wale wa kituo hicho.Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akiwa katika moja ya darasa la awali liloloendeshwa na Kijiji cha SOS, darasa hilo pia linatumiwa na watoto wa kawaida ambao hufundishwa pamoja na wale wa kituo hicho. Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akiwa katika moja ya darasa la awali liloloendeshwa na Kijiji cha SOS, darasa hilo pia linatumiwa na watoto wa kawaida ambao hufundishwa pamoja na wale wa kituo hichoMwakilishi wa Kituo cha SOS kutoka nchini Kenya akizungumza na wageni waalikwa katika hafla za uzinduzi huo. Mwakilishi wa Kituo cha SOS kutoka nchini Kenya akizungumza na wageni waalikwa katika hafla za uzinduzi huo
.Burudani mbalimbali za ngoma na sarakasi kwa wageni waalikwa. 
Burudani mbalimbali za ngoma na sarakasi kwa wageni waalikwaMeza kuu katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo. Meza kuu katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leoBurudani mbalimbali kwa wageni waalikwa. Burudani mbalimbali kwa wageni waalikwa.Ofisa Mkuu kutoka Kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Ujerumani nchi Tanzania, Jan Dieter Gosink ambao ni moja wa wafadhili wa kituo hicho akizungumza na wageni waalikwa kabla ya uzinduzi wa kampeni za 'Nijali Mimi!' (Care For Me!) leo katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam. Ofisa Mkuu kutoka Kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Ujerumani nchi Tanzania, Jan Dieter Gosink ambao ni moja wa wafadhili wa kituo hicho akizungumza na wageni waalikwa kabla ya uzinduzi wa kampeni za 'Nijali Mimi!' (Care For Me!) leo katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam.Mratibu wa kampeni ya Care For Me kutoka SOS taifa, John Baptista akiwakaribisha wageni waalikwa katika hafla hiyo. 
Mratibu wa kampeni ya Care For Me kutoka SOS taifa, John Baptista akiwakaribisha wageni waalikwa katika hafla hiyo.Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Kijiji cha SOS wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Care For Me! iliyoandaliwa na kituo hicho. Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Kijiji cha SOS wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Care For Me! iliyoandaliwa na kituo hicho.Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Kijiji cha SOS wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Care For Me! iliyoandaliwa na kituo hicho. Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Kijiji cha SOS wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Care For Me! iliyoandaliwa na kituo hichoNaibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Kairuki Azindua Kampeni Care For Me! Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Kairuki Azindua Kampeni Care For MeNaibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akitembelea nyumba zinatumika kulala watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kabla ya kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo. 
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki akitembelea nyumba zinatumika kulala watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kabla ya kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni za 'Care For Me!' katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam leo.

NAPE ALAANI VITENDO VYA KINYAMA VINAVYOFANYWA NA CHADEMA

$
0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.Nape alisema kitendo cha wana CCM kushambuliwa ni kitendo cha kinyama na kinatakiwa kikemewe na kila mtu,pia alisisitiza Vijana wa CCM kuwalinda wapigaji kura wao siku ya kupiga kura.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa Habari kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitazama picha ya X-Ray  ya Sebastian Masonga Katibu wa UVCCM kata ya Majengo Wilaya ya Kahama,Masonga amevunjika mkono wa kushoto baada ya kupigwa na wafuasi wa Chadema wakati walipokua wanarejea kwenye mikutano ya  kampeni za Udiwani.
Katibu wa NEC Itikadi na uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akimpa pole Afisa Mtendaji wa Kata ya Ubagwe wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambaye alipigwa na kutobolewa macho na wafuasi wa Chadema .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoka nje ya jengo la hospitali ya Bugando akiongozana na baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza ambapo waliwatembelea na kuwajulia hali majeruhi walioumizwa na wafuasi wa Chadema mjini Kahama.

Rais Kikwete amwandalia Bwana joe Ricketts Chakula cha Usiku

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Bwana Joe Ricketts ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Opportunity Education Foundation ya Marekani.Rais Kikwete alimwandalia mgeni wake chakula cha usiku.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipa zawadi ya kinyago cha mpingo Bwana Joe Ricketts wakati wa chakula cha usiku alichomwandalia ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.Bwana Ricketts amezifadhili shule kadhaa hapa nchini kwa teknolojia ya teknohama kwa kuzipatia tablets kuboresha mbinu za kisasa za kujifunza.(picha na Freddy Maro) .

Mh. Lowassa akana umiliki wa kurasa za mitandao ya kijamii

$
0
0
Kumekuwa na kurasa (accounts) mbalimbali zenye jina la Mh. Edward Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mitandao ya kijamii Kama vile Facebook,Twitter,Instagram nk.

Zinazoonye kuwa mmiliki wake ni Mh. Edward Lowassa.

Ukweli ni kwamba hizo kurasa zote hazimilikiwi na Mh. Lowassa.

Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo,hazihusiani kwa namna yoyote na Mh. Lowassa. 

Hata hivyo Mh. Lowassa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ya ruhusa yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.

Imetolewa na 
Ofisi ya Mh. Edward Ngoyai Lowassa 
Mbunge wa Jimbo la Monduli.

MASHINDANO YA NGUMI NELSON MANDELA OPEN BOXING CHAMPIONSHIP YAZIDI KUNOGA KAWE

$
0
0

Bondia Habasi Hamisi wa Kigoma akikwepa konde la Mustafa Murinho  wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open Championship yaliyofanyika katika  viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam Morinho alishinda kwa point mpambano huo na kuingia fainal
Bondia Finias Genga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Swanga wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Openchampion ship yaliyofanyika katika viwanja vya  Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam Swanga alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza na kufanikiwa kuingia fainal ya mashindano hayo Picha Na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Haruna Swanga akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake
Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis akisaidia kufunga mlingoti wa taa katika mashindano hayo.

Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare akimwelekeza ofisa habari wake Viduka  jinsi ratiba ya mahindano yanavyokwenda kushoto ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
Diwani wa Kata ya Kawe Othumani Kipete Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis na
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare wakifatilia kwa makini Mashindano hayo
Aisha Vonialis




Na Mwandishi Wetu Kawe

Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis amesema wanawake wanatakiwa wawe na msukumo mkubwa katika kuhakikisha wanajitokeza kwenye mchezo wa masumbwi

akizungumza wakati wa mashindano ya kumuenzi Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela Open Boxing Championship yaliyofanyika katika viwanja vya  Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam 

Mjumbe huyo alitoa wito kuwa wanawake wanaweza hivyo wajitokeze katika kucheza mchezo wa ngumi na kuangalia mchezo huo kama michezo mingine akitolea mfano unaona katika mashindano haya wanawake ndio walio ongoza kuja kwa wingi kwa kuwa wanapenda mchezo siku zote tulizo kuwepo hapa katika viwanja hivi wanawake wanakuja kushingilia sana tu

aliongeza kwa kusema kuwa wanaomba mashilika,makampuni tasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi kuja kusaidia mchezo wa masumbwi upate wadhamini wa kutosha kwani mashindano hayo yamekutanisha mikoa mbalimbali nchini kwa sasa hivyo wadau wote wanaombwa kujitokeza kudhamini mchezo huo 

katika mashindano hayo ya kuingia fainali bondia Mustafa Morinho alimsambalatisha Abbasi Hamisi uku Jonson Swanga akimpiga Disson Everest na Abuu Said akimdunda Frank Msindo na Haruna Swanga akimwazibu bila huluma bondia Finias Genga kwa TKO ya raundi ya kwanza

NAPE:KUWAZUIA WATU KUPIGA KURA NI KUHUJUMU DEMOKRASIA

$
0
0
 Katibu wa NEC tikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Nyasura wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani ambapo aliwaeleza wananchi haikuwa rahisi kuwaleta watanzania pamoja,hivyo basi wakatae kabisa vyama viinavyotaka kuwatenganisha kwa misingi ya udini na ukabila.
 Wakazi wa kata ya Nyasura wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani zinazoendelea nchi nzima ambapo kata 27 zitafany uchaguzi wa madiwani.
 Wakazi wa Kata ya Nyasura wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Nape Nnauye ambaye aliwaambia safari hii CCM haipo tayari kuhujumiwa na kutaka watu wengi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na kutoa wito kwa vijana kulinda wapiga kura wa CCM.
Mgombea wa Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Nyasura  Ndugu Alexander Mwikwabe akiomba kura toka kwa wananchi wa Nyasura kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Nyasura ambapo mgeni wa heshima alikuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Februari 7,2014.

ALAT TAWI LA MOROGORO WAFANYA MKUTANO WAO

$
0
0

Mwenyekiti wa ALAT Tawi la Morogoro Ambaye pia ni Meya w Manispaa ya Morogoro Mh Amir Juma Nondo Akifungua Mkutano wa Alat Tawi la Morogoro Kulia Ni Katibu wa ALAT Tawi la Morogoro Ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji Kutoka Wilaya ya Ulanga Mh Isabella Chilumba Akifuatilia Kwa Makini Hotuba ya Ufunguzi w mkutano Huo.

Makamu Mwenyekiti wa ALAT Tawi la Morogoro Na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro Vijijini Mh Kibena Kingu (Kushoto) Akiwa Pamoja na Mwenyekiti wa ALAT Tawi la Morogoro Ambaye pia ni Meya w Manispaa ya Morogoro Mh Amir Juma Nondo (Katikati) Wakimsikiliza Katibu wa ALAT Tawi la Morogoro Ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji Kutoka Wilaya ya Ulanga Mh Isabella Chilumba Akiongoza Kikao Hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mh Jonas Zerand Akichangia Hoja katika Mkutano wa ALAT Tawi la Morogoro Uliofanyika jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya Ya Mvomero.

Wakurugenzi watendaji wa Wilaya  za Mvomero Kilombero na Morogoro manispaa ambao ni wajumbea wa ALAT Tawi la Morogoro wakifuatilia kwa Makini Mkutano hu.

Wajumbe wakifuatilia kwa Makini Ajenda Zinazoendelea wakati wa Mkutano wa ALAT Tawi la Morogoro.

Katika Mkutano Huo Ulioudhuriwa na Wajumbe Kutoka Wilaya Zote Zinazounda Mkoa w morogoro Walijadili Mengi Likiwemo Kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Katia ya ALAT ya 1984 Pamoja na Kulichukulia kwa Uzito wa Juu Swala la Mgogoro wa Wakulima na Wafugajikatika Mkoa wa Morogoro.

ALAT Tawi la Morogoro wamiomba Serikali Kuliangalia Tatizo Hilo la Migogoro ya Wakulima na wafugaji kwa kuwa Limezidi Kuichafua Sura ya Mkoa wa Morogoro na Litakuja Kuleta Matatizo Makubwa kama halitachukuliwa kwa uzito mkubwa sasa.Aidha Wajumbe wa ALAT Tawi la Morogoro Wameiomba Serikali Kuwashirikisha Kila Jmabo Ambalo wamepanga Kufanya kwajili ya Maendeleo ya Wanchi wa Mkoa wa Morogoro kwa kuwa wao ndio Watendji Ambao wako Karibu Zaidi na Wananchi.

THE FIRST IBF FEMALE WORLD TITLE FOR AFRICA - HELEN JOSEPH READY TO LOCK HORNS WITH SANTANA IN THE "RUMBLE OF THE BEAUTIES"

$
0
0

ACCRA, REPUBLIC OF GHANA, FEB. 08, 2014: The Ghanaian GoldenMike Boxing Promotions Syndicate managed byMichael Tetteh a.k.a "Muttu" has made history that will be written in golden ink for many years to come. Upon winning the first bid for the African continent to host the First Female IBF World Title, GoldenMike Boxing Promotion Syndicate is on the whirlwind to setup one of the major tournament Ghana and in deed Africa has ever staged.


This come on the wheels of its victory for the IBF Female featherweight championship of the world between Ghanaian based Nigerian Princess of Africa boxing Helen  Joseph against IBF Female Featherweight champion Dahianna Santana from the city of San Domingo in the the Dominican Republic.


The GoldenMike Bixing Promotions Syndicate a subsidiary of Goldenconcept Busjness Conglomerant has scheduled the tournament to take place April 25, 2014 at the Accra Sports Stadium. This is the same place where Helen Josephannihilated Marriana Gulays from Hungary to snatch the IBF Feameke Fetherweight Intercont8ennatkl Title last year.
 
Theweigh-in will take place April 24, 2014 at the famous Press Center.


The Princess of African Boxing Helen Joseph is in the hands of Kofi Daku-Rickets who is regarded as one of the greatest professional boxing trainers in Ghana today. Kofi Daku-Rickets has bigger plans for Helen as she aim to the great heights.


The derby to be fought on 10 rounds of 2 minutes each has been heralded as one of the greatest news that Africa has every received in recent years. For a boxer to win the world title under IBF is a golden opportunity for those who would climb that stairs.


Helen, a boxer who has gone through the IBF Africa & Middle East's progression path is young, beautiful, calm and has the serenity to charm anyone around her. She is typical African Princess the like of Princess Cleopatra who harbors great ambitions for her and her continent of Africa.


Nigeria 
home to the Princess of African boxing Helen Joseph 
is known for producing the first world boxing champion from Africa. Dick Tiger, the man who sent fear shivers to many of his opponents across the Atlantic 
ocean
 is the Africa's pride whose history and achievements in boxing are written by the golden ink.


Africa 
continent 
is known as home and bedrock for boxing because many years ago, boxing started in Abyssinia now Ethiopia and was used to measure manhood and heroes. That Africa has been home to several world class boxing champions; it is not a surprise at all.
Helen Joseph (Left) Pummeling Dahianna Santana (right)


In the 21st century boxing cannot be written without the inclusion of female boxing. Women have brought feminine favor to boxing which was missing before. Nowadays boxing is more attractive than during the days of bareknuckle and all this thanks to the inclusion of women to the sweet science which makes it sweeter!


We have already read stories of the meticulous rise and dominance of Dick Tiger, Azumah Nelson, Welcome Ncita, Harry Simon and other boys in the ring but, it is time now we read about the role of women in the sport of professional boxing and most particularly, the story of Helen Joseph, known as "The Princess of boxing in Africa" or "Iron Lady" from Nigeria.


Helen Joseph is a beautiful young lady who found her calling to boxing early on when she was still a toddler. She wanted to be a nurse so that she could attend to the needs of others but then, there was desires of being a protector to others and particularly women. Helen could not stand when she saw other girls from South West Nigeria being mistreated. For that she swore that one day she would do something about it.


Her desires to help and protect other women drove to boxing and as fate would have it, she climbed the ladders so quick that she would realize that time was running so fast with her.


He
 r
 first duty was in January 10, 2004 when she met Margaret Ibiam in Lagos, Nigeria and did a hurried work by KOed her in the 1st round. The bout became an eye opener to the Nigerian boxing promoters that the champion has arrived.


Three months later on 03, Mrch 2004, she met and disposed Ndidi Okafor in Lagos, Nigeria only 2 rounds of their 4 rounder bout.

The Princess of African Boxing Helen Joseph (Right) Zeroing Dahianna Santana (Left)


Victim number three was Esther Haruna when Helen did her in the third round of their 4 rounder bouts on June 16, 2004 before she met and mauled  Toyin Omorayi by points on 29th January 2005.


Helen continued her meticulous rise in professional boxing and this was apparent when she met Busola Obi on 25 June 2005 by stopping her in the 4th round of their 6 rounder bout in Lagos Nigeria before travelling to Ibadan, Nigeria on October 15, 2005 only to knock out Mariam Joseph in 2nd round of their 6 rounder bout.


Helen's first foreign bout came calling in June 03rd, 2006 when she travelled to the Capital City of Lome in Togo and metYarkor Chavez Annan for the 4 rounder bout which ended in Helen's favor by points.


Her whirlwind tour of West African took her to Burkina Faso in August 05, 2006 where she met Kahide Kazeem at the Maison du Peuple, Ouagadougou, Burkina Faso and outpointed her in their 6 rounder bout.


The Burkinabe boxing stakeholders demanded that she went back to the country of the Stallion again to showcase her prowess and she did so in July 28, 2007 when to meet Ameley Turkson at the same venue the Maison du Peuple, Ouagadougou, Burkina Faso. Ameley Turkson would lose the fight on points to Helen in their 6 rounder bout.


Time now to the Southern African Hemisphere when Helen calling saw her putting camp in Lusaka, Zambia to meet their national pride Mable Mulenga for the minor WIBF Intercontinental Bantamweight Title at the famous Nationalist Stadium, Lusaka, Zambia. Mable Mulenga could not stand Helen onslaught and she lost on points in their 10 rounder duel.


Helen next outing took her to the Rainbow nation of South Africa in the city of Igoli (JoBurg) when she met and lost controversially on points to Unathi Myekeni in their minor World Boxing Foundation International Female featherweight title.


Namely Emilia of Ghana had to take all of Helen's fury in September 23, 2011 at the Prison's Canteen, Accra, Ghana when she was TKOed in round 6 of their 6 rounder bout.


The Princess of African Boxing Helen Joseph (Left) Santana (Right)


Helen's other controversial bout in the Rainbow nation and in the same Igoli city of JoBurg came in March 24, 2012 when she met Unathi Myekeni at the Carnival City Casino, Brakpan, Gauteng, South Africa and the fight was declared a draw to the amazement of all the attending boxing stakeholders.


But, the world's top boxing body the IBF saw her ability and gave her a shot at its world featherweight title against the title holder Dahiana Santana of Dominican Republic. Helen's trip to The Dominican Republic was rescheduled twice because of the visa problems and her team led by her promoter Henry Manly-Spain, the CEO of GoldenConcept Business Group that owns GoldenMike Boxing Promotion Syndicate of Accra, Ghana.


In the end Helen arrived in The Dominican Republic after traveling long way from Ghana, to Spain, Brazil and then Dominican Republic. She has no time to rest and on arrival she was whisked to the weigh-in to face her nemesis Santana who was fighting on her home turf.


The fight was held at the Dominican Fiesta Hotel & Casino, Santo Domingo, Dominican Republic in December 17, 2012 under the supervision of the IBF Chairman of ratings Committee Anibal MiremontesThe fight saw both boxers kissing the carpet and at the of it Santana came better of the two and retained her title.


The IBF rewarded Helen's courage with the I/C Featherweight title and in May 03, 2013 she had to show the boxing fraternity the type of the boxer she was when she met the stubborn Hungarian Iron Lady Marianna Gulyas and sent her packing in the shortest fight of the year  0:28 second in the first round.


The win and her IBF I/C Featherweight title on hand enabled Helen to retain her number one contender to the Featherweight world title.


The Princess of Africa Boxing Helen Joseph with Onesmo Ngowi, IBF Africa & Mideast President (Left) and her trainer Kofi Daku-Ricketts (Right)  after winning the IBF Inter Continental Title last year


Africa is excited with the news of 
Helen Joseph stab at the 
world title and many boxing fans across the continent are planning to travel to Ghana to watch the awesome fight.


Africa's hopes are highly invested on Helen Joseph, the "Princess of African Boxing" to bring back the honors that her predecessors Dick Tiger, Azumah Nelson, Welcome Ncita, Harry Simon and others brought to Africa some years ago.

They call it Africa. We call it HOME

Semina na Mwl.Mwakasege Arusha Mjini

KONGAMANO LA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU MKOANI MBEYA KUELEKEA MIAKA HAMASINI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

$
0
0
 picha ya pamoja ya baadhi ya washiriki katika kongamano la Muungano lililohusisha vyuo vya elimu ya juu, mjini Mbeya leo (Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais).
 katikai mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abas kandoro akifungua kongano la Muungano kwa vyuo vya elimu ya juu mjini mbeya leo, kushoto ni Naibu katibu Mkuu Ofisi ya makamu wa Rais Bi Angelina madete,na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya muungano kutoka Ofisi ya makmau wa Rais Baraka Rajab
Waziri wa Nchi Ofisi Ya Makamo wa Rais Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akifafanunua kuhusu masuala ya Muungano katika kongamano lililohusisha vyuo vya elimu ya juu mkoani Mbeya leo
 Washiriki wa Kongamano la Muungano mkoani Mbeya ambao ni wanafunzi wa vyuo ya elimu ya juu wakifuatilia mjadala katika kongamano hilo mjini Mbeya leo

==========    =========   ==========

KONGAMANO LA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU MKOANI MBEYA KUELEKEA MIAKA HAMASINI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.


Ni wajibu wa kila Mtanzania kutambua kwamba uandikishwaji wa katiba mpya unalenga kuweka misingi ya kuijenga Tanzania ya sasa naya siku nyingi zijazo.


Hayo yameelezwa leo na mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abas Kandoro katika ufunguzi wa kongamano la vyuo vya elimu ya juu mkoani humo,lililohusu masuala mbali mbali ya muungano kuelekea maadhimisho ya miaka hamsini ya muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar.


Katika Kongamano hilo Bwana Kandoro aliongeza kwa kusema kuwa  jambo hili ni kubwa na linahitaji umakini wa hali ya juu saana katika kila hatua ili kufanikisha mchakato huu, aidha Bwana kandoro aliwakumbusha washiriki wa kongamano hilo kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu nyingi lakini kubwa ni kuwepo kwa mahusiano ya karibu kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika Nyanja mbali mbali kama vile undugu wa damu, biashara,utamaduni lugha na mahusiano ya karibu ya kisiasa.


Bwana kandoro aliendelea kusema kuwa, Muundo wa muungano wetu umeweka mfumo wenye vyombo mbalimbali vyenye mamlaka za utendaji, kutunga sheria na kusimamia shughuli za umma na utoaji haki.

“Pamoja na hiyo mifumo, na kuwepo sababu nyingi nzuri na za msingi za kuwepo Muungano, bado ndani ya jamii yetu kuna wanaohoji  uhalali wake kupitia maoni yaliyotolewa mbele ya tume ya mabadiliko ya katiba mahakama na mijadala mingine, alisisitiza.”


Mkuu wa Mkoa alisema kuwa yawezekana kabisa kuwa washiriki wanaweza kuwa na hoja zinazofanana na hizo..na hivyo mada zitakazotolewa zinaweza kusaidia kujibu baadhi ya hoja. Katika Kongamano hilo wasomi hao wametoka na kauli mbiu inayosema “MUUNGANO IMARA NI MUSTAKABALI WA TAIFA LETU.”

Kungamano hili linaondeshwa na Idara ya Muungano ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mikoa ya Mbeya ya Iringa ni moja ya makongamano katika vyuo vikuu nchini kuelekea maadhisho ya miaka hamsini ya Muungano


EVELYN MKOKOI

AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS

KONGAMANO-MUUNGANO

MBEYA

8/2/2014



Waziri Mukangara azindua rasmi mashindano maalum shule za sekondari Dar kwa kishindo.

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara akipiga mpira na kumchambua Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano maalum kwa shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Mashindano hayo yanayotimua vumbi yataanza  katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.

========  =======  =======
Waziri Mukangara azindua rasmi mashindano maalum shule za sekondari Dar kwa kishindo.

·        Shule 12 kutoka wilaya tatu za mkoa huo kutoana jasho
Dar es Salaam Februari 8, 2014 … Mashindano maalum yanayozikutanisha shule kumi na mbili za sekondari kutoka wilaya tatu tofauti za mkoa wa Dar es Salaam yamezinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara katika viwanja vya shule ya sekondari ya Turiani.

Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa na ya aina yake yatahusisha shule kumi na mbili za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam kutoka wilaya zake tatu; kwa wilaya ya Kinondoni shule zitakazoshiriki ni Turiani, Mugabe, Kawe na Kiluvya; Ilala ni Benjamini William Mkapa, Mnazi Mmoja, Majani ya Chai na Juhudi; Temeke ni Kibasila, Temeke, Pendamoyo na Mtoni Relini.

Mashindano hayo yanaanza kutimua vumbi kuanzia Februari 8 na kuhitimishwa siku ya tarehe 23 ya mwezi huu. Viwanja vitakavyotumiwa ni vitatu yaani kimoja kutoka kila wailaya ambavyo ni Kibasila (Temeke), Benjamini Mkapa (Ilala) na Turiani (Kinondoni).

Akizungumza wakati wa mashindano hayo mheshimiwa waziri Dk. Fenella Mukangara alibainisha kuwa ni kwa muda mrefu sasa michezo mashuleni imekuwa ni ya kusuasua kitu ambacho kinapelekea vipaji vya wachezaji wachanga kutoonekana.

“Ni muda sasa tangu michezo mashuleni  kama vile UMITASHUMTA kufanyika, kipindi kile michezo ya aina mbali mbali kama vile mpira wa miguu, netiboli, riadha na mingineyo ilikuwa ikiwakutanisha wanafunzi na kuonyesha vipaji vyao. Tunataka kurudisha hayo mashindano kama ilivyokuwa zamani, naamini kwa kushirikiana na wizara husika pamoja na wadau mbali mbali lengo letu tutafanikiwa.” Alisema Dk. Mukangara

Aliongezea kwa kusema mashindano haya yatafungua njia na kurudisha ari ya wanafunzi kupenda michezo na kuwa ni sehemu ya masomo yao. Hatutaki iwe ni nadharia tu kwamba michezo ni muhimu kwa afya ya mwili na akili.

“Kwa kuanza na shule hizi chache za mkoa wa Dar es Salaam tunaamini mashindano yatakuwa ni yenye msisimko na ushindano mkubwa na tunategemea zoezi hili kusambaa mikoa tofauti ya Tanzania. Ningependa kutoa rai kwa shule zilipata fursa ya kushiriki kuitumia nafasi hiyo ipasavyo, nawatakia maandalizi mazuri, mtuonyeshe soka safi na hatimaye kuibuka na ushindi.” Alimalizia mheshimiwa waziri

Rekodi katika michuano ya Olimpiki Sochi

$
0
0
Michuano ya 22 ya Olimpiki ya majira ya baridi imeanza jana huko Sochi nchini Russia. Mabadiliko mengi yametokea katika miaka sita na nusu ya maandalizi yake Na wakati mamilioni ya watu duniani wakiwa wameelekeza macho na masikio yako huko, kujua nani atashinda nini na nani atavunja rekodi gani, tayari rekodi kubwa zaidi katika michuano hiyo imevunjwa hata kabla ya kuanza kwake. Na tuipitie safari safari ya maandalizi ya michuano hii mpaka ilipofikia na baadhi ya vikwazo ilivyopambana navyo Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Majina ya wajumbe wa Bunge maalumu la katiba haya hapa.

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Florence Turuka akitangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum la katiba   jioni hii katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jioni hii jijini Dar es salaam.
Wanahabari wakimsikiliza  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mhe.  Florence Turuka akitangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum la katiba  yakitangazwa jioni hii katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam. Bunge la Katiba litakalokuwa na wajumbe 640, litakutana kwa siku 70 (na kuongezewa siku 20 kama hawatoafikiana)  kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Desemba 30, mwaka jana. 
Kupata orodha kamili ya majina hayo  BOFYA HAPA

MASHINDANO YA NGUMI YA NELSONI MANDELA OPEN CHAMPIONSHIP YAMALIZIKA KAWE

$
0
0


Bondia Rudia Mashala kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ratifa Khalidi wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open Champion Ship yaliyo malizika katika viwanja vya Kawe Dar es salaam .Ratifa alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ezira Paur wa Kigoma akipambana na Hafidhi Kassimu wa Ngome wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open CHampion Ship yaliyomalizika kawe Dar es salaam Paur alishinda kwa point.
Baadhi ya watu waliofulika kuangalia michuano hiyo
Meya wa Kinondoni akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo
Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis katikati akiwa na mabondia wa kike waliopigana na kunyakuwa zawadi mbalimbali
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yussuph Mwenda akimkabidhi,  Mwenyekiti wa timu ya Mkoa wa Kigoma  Eddie Kikwesha  baada ya kuibuka timu yenye Nidhamu katika mchezo wa masumbwi, katikati ni Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis

Katika picha ya pamoja

Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare akimzawadia kocha wa timu ya kawe baada ya kuibuka washindi wa tatu katika mashindano hayo.


NAIBU WAZIRI WA MAENDELO YA JAMII PINDI CHANA APOKELEWA KWA KISHINDO WILAYANI RUDEWA.

$
0
0
 
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana akimkaribisha Mama yake mzazi Regina Mlowe kuzungumza machache katika sherehe za kumkaribisha zilizofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Rudewa
 Mama mzazi akiwashukuru wananchi wa Rudewa katika sherehe za kumkaribisha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana.
 baadhi ya wanachama wa CCM wakiwa katika sherehe za kumkaribisha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana.
 Mkuu wa Wilaya ya Rudewa Juma Solomon Madaha akizungumza wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana. (Picha zote na Denis Mlowe).
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana akicheza muziki na baadhi ya viongozi wa ccm wilaya ya Rudewa

Viewing all 46313 articles
Browse latest View live




Latest Images