Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 219 | 220 | (Page 221) | 222 | 223 | .... | 1898 | newer

  0 0

  makada  wa ccm  wakimsaidia kijana Salum aliyejeruhiwa   

  Polisi  Iringa  wakiyaongoza magari ya  CCM na Chadema ambalo  amepanda  mbunge Msigwa kuingia  kituo cha  polisi baada ya  kuibuka  vurugu kubwa 
  Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwa  chini ya ulinzi wa  polisi . 
  Polisi  akiliongoza  gari la  mbunge Msigwa   baada ya  kukamatwa kwa  vurugu katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya  Nduli 
  gari la mbunge Msigwa  likiwa  polisi  usiku  wa jana.
  MBUNGE  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amekamatwa na  polisi kufuatia vurugu   kubwa  zilizoibuka jana,   katika  uchaguzi mdogo  wa udiwani kata ya  Nduli jimbo la Iringa mjini baada ya  wafuasi wa chama  cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)  kuwashambulia  wafuasi wa CCM .


  Tukio  hilo  limetokea  jioni  ya jana  baada ya  wafuasi wa Chadema  kuwashambulia  kwa mawe na nondo  wafuasi wa CCM na kupelekea  kijana mmoja wa UVCCM Salum Kaita   kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hospital ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa .


  Wakizungumzia tukio hilo  baadhi ya mashuhuda waliozungumza na mtandao huu wa matukio daima   walidai kuwa   Chadema  walikuwa na mkutano  eneo la Nduli na  vijana  hao wa CCM  walikuwa  mbali na eneo la mkutano  wakiendelea  na shughuli zao kabla ya  kuvamiwa na makada wa Chadema.


  Hata  hivyo  wakati  wa  vurugu  hizo  zikitokea  inadaiwa mbunge Msigwa alikuwa akishuhudia  tukio zima na  kutuhumiwa  kuhusika kufanya  njama  za  kuwashambulia vijana  hao.


  Naibu  meya wa Manispaa ya  Iringa Gervas Ndaki  amemweleza mwandishi wa habari hizi kuwa ana    sauti ya mbunge Msigwa inayoelezea  jinsi ambavyo mbunge  huyo alivyopanga  kufanyika kwa  vurugu  hizo.


   Huku  mmoja kati ya makada wa Chadema  mjini hapa akidai  kuwa  CCM ndio  ambao   walihusika na vurugu  hizo kutokana na kupita  eneo hilo la mkutano wa Chadema wakati  wao  hawakuwa na ratiba  ya kufanya mkutano  eneo hilo.


  Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia  askari wa FFU  mkoa  wa Iringa  wakiwaongoza  wafuasi wa Chadema  zaidi ya  20  waliokuwa katika  gari la matangazo pamoja na mbunge Msigwa ambae  alikuwa  chini ya  ulinzi na kufika kituoni hapo kwa gari lake  la  ubunge .


  Kamanda wa  polisi mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi  hakuweza  kupatikana  kuelezea  undani wa   tukio hilo na jitihada za  kumtafuta  zinaendelea  japo  hadi sasa  saa moja  hii  usiku  mbunge Msigwa yupo  kituo cha  polisi  akihojiwa .source hapa  0 0


  wananchi  wachache  leo  walifika katika viwanja  vya mahakama  kuu kanda ya  Iringa  kushuhudia  mbunge Msigwa akifikishwa mahakamani  hapo na kalandinga la polisi  huku ile hamasa  kubwa ambayo  ilikuwa  ikitokea  katika  kesi yake ya Machinga  kwa jana  haikuwa hivyo  baada ya mbunge  huyo kukosa  wafuasi wa  kwenda  kumuunga mkono mahakamani kama zamani .

  Mbali ya  polisi  wa FFU  kutanda kila  kona na mahakamani  hiyo  na polisi ila bado polisi  hawa  hawakuwa na kazi  nzito kama  siku  nyingine kutokana na utulivu mkubwa wa  wafuasi  kama 30  waliofika mahakamani hapo  kushuhudia  kesi  hiyo.Chanzo hapa

  0 0

   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Nasoro Hamid akizungumza na ujumbe toka Norway ulipofika ofisini kwake kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya namna  nchi hiyo ilivyoweza kunufaika  kwa  kuwekeza katika sekta ya gesi  mnamo miaka ya 1970. Anayesaini kitabu ni Bw. Alaf Jakobson Meya wa mji wa Hammerfest nchini Norway.

  Meya wa mji wa Alstahaug Bw. Bard Anders  akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika ofisini kwa Meya wa mji wa Lindi Bw. Frank Magali mwenye miwani.

  ==========  ========  ========
  Elimu ipewe kipaumbele Ili kuwawezesha wananchi wa kusini kunufaika na rasilimali ya gesi – Norway


  Na Nuru Mwasampeta,

  Serikali ya Norway imeeleza kuwa, iliichukua takribani miaka ishirini kwa nchi hiyo kuanza kufaidika na matunda ya uwekezaji mkubwa katika sekta ya gesi.


  Hayo yalibainishwa na balozi wa Norway nchini Bi. Ingunn Klepsvik alipokuwa akizungumza katika ziara ya Mameya toka nchi hiyo mjini Lindi ikiwa ni sehemu ya kutoa uzoefu iliyoupata baada ya kuingia katika uchumi huo mkubwa.


  Bi. Ingunn alisema tangu kuwepo ugunduzi wa gesi katika miaka ya 1960 iliwachukua miaka 20 kuanza kuzalisha gesi ambapo uzalishaji ulianza miaka ya 1980 na kurudisha gharama za uwekezaji kwa miaka ishirini, na hivyo kuchukua kipindi cha jumla ya takribani miaka arobaini hadi walipoanza kunufaika na rasilimali hiyo ya gesi.


  Aidha,  mameya wa miji ya Alstahaug na Hammerfest  walisistiza umuhimu  wa kuwepo na mipango madhubuti ambayo itawawezesha wazawa kunufaika ikiwemo pia mikakati itakayowabana wawekezaji ili kuhakikisha kuwa eneo linalochimbwa  rasilimali hiyo pia linanufaika ili wananchi waweze kunufaika na uwepo wa  rasilimali hiyo.


  Kwa upande wake Meya wa mji wa Alstahaug Bw. Bard Anders, alieleza kuwa nchi ya Norway iliwekeza zaidi katika elimu lengo likiwa kupata watendaji wazuri katika sekta za gesi na mafuta.


  Vilevile alieleza kuwa, wanaamini kuwa kwamba wananchi wakielimishwa ni rahisi kwao kushiriki kikamilifu katika masuala ya maendeleo lakini pia hali hiyo itawajengea uwezo wa kutumia fursa zilizopo na mipango endelevu juu ya namna ya kuboresha vipato vyao.


  Akizungumzia kuhusu namna uchumi wa gesi ulivyoinufaisha nchi hiyo kielimu, Bw. Bard alieleza kuwa, nchini Norway elimu inatolewa bure  kwa elimu ya awali na sekondari  ambapo watoto kuanzia mwaka mmoja hadi sita wanapelekwa katika shule za awali kabla ya kujiunga na  shule za msingi  na sekondari.


  Akizungumzia kuhusu elimu ya juu, alieleza kuwa, elimu hiyo nchini Norway inatolewa kwa mkopo toka serikalini ambapo aliyekopa anarejea baada ya kuanza kazi.  ‘‘Watu wote Norway wanahaki sawa ya kupata elimu’’ alisisitiza Bard.

  Katika ziara hiyo ujumbe huo uliishauri Serikali ya Tanzania kuwa na sera zinazowabana wawekezaji ikiwemo pia kuhakikisha kunakuwa na asilimia nyingine ya mapato inayobaki kwa ajili ya  kusaidia  kuboresha huduma mbalimbali katika eneo husika kwa  kuzingatia vipaumbelea vya wananchi  ikiwemo miundombinu, elimu, afya pamoja na kuinua hali ya maisha ya wananchi  wa eneo husika.


  Kwa upande wa viongozi wa mikao ya Lindi na Mtwara waliupokea ushauri wa ujumbe huo na kujadiliana pamoja masuala mbalimbali kuhusu namna watakavyoweza kushiriki na kunufaika na rasilimali ya gesi iliyogunduliwa katika maeneo yao.


  Pamoja na kujadili masula ya gesi na mafuta ujumbe huo ulipata fursa za kutembelea mashamba ya samaki yanayoendelezwa  na wananchi wa Lindi pamoja na chuo cha Ufundi Veta kinachotarajiwa kuelimisha wananchi wa mtwara juu ya masuala ya uvuvi na kuogelea pamoja na ufundi mwingine.


  0 0  THE UN SECRETARY-GENERAL

  --

  MESSAGE ON THE INTERNATIONAL DAY OF ZERO TOLERANCE FOR FEMALE GENITAL MUTILATION.


  “Preserve the Best in Culture and Leave Harm Behind”

  6 February 2014


  As Secretary-General of the United Nations, I hold high the banner of empowering women and girls, promoting their health and defending their rights. The International Day of Zero-Tolerance for Female Genital Mutilation is an opportunity to confront this persistent problem – and to find hope in initiatives proving that it can end.


  We should strive to preserve the best in any culture, and leave harm behind.


  There is no developmental, religious or health reason to cut or mutilate any girl or woman. Although some would argue that this is a ‘tradition,’ we must recall that slavery, so called honour killings and other inhumane practices have been defended with the same weak argument. Just because a harmful practice has long existed does not justify its continuation. All ‘traditions’ that demean, dehumanize and injure are human rights violations that must be actively opposed until they are ended.


  FGM causes grave harm to individuals. The immediate and long-term health consequences include constant pain, infections, incontinence and sometimes deadly complications in pregnancy and childbirth.


  The practice is declining in almost all countries but it is still frighteningly widespread. Although firm statistics are difficult to obtain, it is estimated that more than 125 million girls and women alive today have been cut in 29 countries in Africa and the Middle East, where FGM is most prevalent and data exist.If current trends continue, some 86 million young girls worldwide are likely to experience some form of the practice by 2030. Asia, Europe, North Americaand other regions are not spared and must be equally vigilant in addressing the problem.


  Fortunately there are positive signs of progress in our global push to end this harmful practice.


  Girls themselves instinctively understand the dangers of being cut, and many mothers who have seen or experienced the trauma want to shield their daughters from suffering. It is encouraging that an increasing number of communities are coming together and agreeing publically to end FGM and ensure a better life for their girls.


  Recently, Uganda, Kenyaand Guinea-Bissauadopted laws to end FGM. In Ethiopia, those responsible have been arrested, tried and penalized, with full media coverage further raising public awareness.


  The United Nations and our partners are engaged in valuable, culturally sensitive activities that aim to stop FGM without scolding or shame.


  In Sudan, we are seeing social change from a campaign called “Saleema,” the Arabic word that implies complete, intact, whole and untouched. One father moved by the effort who decided to leave his daughters uncut explained simply, “A girl is born Saleema, so leave her Saleema.”  Hundreds of communities have embraced this initiative, expressing their support through songs, poetry and clothes in the campaign’s trademark bright colours. Other countries are emulating Saleema or coming up with solutions tailored to their local needs, such as Kenya, where Meru community elders have prohibited FGM and vow to impose a fine on anyone who conducts or abets the practice


  In addition to prevention, the United Nations is working with partners to help those who have been affected by FGM. Pioneering medical advances now allow doctors to repair women’s bodies and restore their health. I recall the words of one physician working in Burkina Fasowho described “the relief that overwhelms women” following the surgery, which she said is 100 per cent effective. The many women who lack the resources needed to travel to the right facilities and the programmes that offer proper treatment deserve generous support.


  The General Assembly’s landmark resolution proclaiming this commemorative Day was sponsored by every country in Africa and embraced by the entire membership of the United Nations. This breakthrough shows the great value of the United Nations in rising as one to defend universal human rights. Now our challenge is to give real meaning to this Day by using it to generate public support, trigger legal and practical advances, and help girls and women at risk of or affected by FGM.


  The effect on individuals will be profound, sparing them pain and spurring their success. The benefits will reverberate across society as these girls and women thrive and contribute to a better future for all.
  0 0


  Wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa jimbo  la kalenga wametakiwa kuzingatia unyeti wa jukumu la kusimamia uchaguzi,kuzingatia katiba,sheria,kanuni na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi kikamilifu ili kudhihilisha demokrasia na kuepusha malalamiko yasiyo ya msingi.
   
  Hayo yamesemwa leo katika ufunguzi wa semina ya mafunzo ya msimamizi wa uchaguzi,wasimamizi wasaidizi ngazi ya jimbo na kata ya jimbo la kalenga pamoja na wandishi wa habari  na mkuu wa wilaya ya Iringa RETISIA WALIOBA ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa siasa na kilimo uliopo manispaa ya Iringa.
   
  Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya tume ya uchaguzi mawakala wa vyama vya siasa  hawapaswi kuwepo katika vituo vya kupigia kura jambo ambalo litasaidia kudhihirisha uwazi katika zoezi zima la uchaguzi.
   
  Amesema kuwa wajibu wa mawakala wa vyama vya siasa ni kuangalia sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa na tume zinazingatiwa katika mchakato wa kupiga kura hadi wakati wa kutangaza matokeo.
   
  Hata hivyo amesema kuwa wananchi wahamasishwe na elimu ya kutosha itolewe kwa wapiga kura wote huku akitoa wito kwa wananchi kujiandaa kwa ajiri ya uchaguzi na kuhakikisha wanatunza kadi za kupigia kura na wajiepushe kurubuniwa kwa namna yoyote ili wasiweze kupiga kura.
   
  Aidha ameongeza kwa kusema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi inaendesha program ya elimu ya mpiga kura ambapo mabango,vipeperushi na matangazo kwa kutumia vyombo vya habari huku akiwataka wasimamizi kutopendelea chama chochote wala kuonesha ushabiki wa chama chake bali watumie demokrasia.
   
  Akitoa ratiba ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi PUNDENCIANA KISAKA amesema kuwa muda wa kuanza kuchukua fomu ni kuanzia tarehe 9 hadi 18 na kufanyika kwa uteuzi kabla ya saa kumi,kampeni zitaanza tarhe 19 hadi 15 mwezi wa tatu na upigaji kura utafanyika tarehe 16 mwezi wa tatu .

  0 0

  JAJI mkuu mstaafu Raymond Mwaikasu amependekeza Viongozi wa jeshi la magereza waingizwe  katika rasimu ya katiba kwa sababu ni watekelezaji wa sheria za nchi  husika   hivyo viongozi wakuu wa magereza washirikishe katika kamati ya ulinzi na usalama wa taifa kwa sababu ni sehemu ya nchi washirika.

  Akizungumza katika warsha iliyofanyika  mjini Iringa yenye lengo la kuwajengea  uelewa wa katiba pamoja na mchakato wa marekebisho ya katiba kwa wananchi waishio wilaya ya Iringa vijijini,  alisema kuwa viongozi wa Magereza waingizwe katika kamati ya ulinzi na usalama wa Taifa ili kuweza kutoa taarifa kwa kamati juu ya yanayotokea gerezani na wanayokabiliana nayo katika magereza.

  Kwa upande wake  MKurugenzi mkuu John Msika alisema kuwa jeshi la magereza halijatajwa kama ni sehemu ya muungano hivyo halimtambui katika kuidhinisha adhabu.

  “Mkuu wa jeshi la magereza aidhinishe kama mmoja wa wanakamati na mjumbe katika kamati kuu ya ulinzi na usalama “alisema Msika
  Naye mkurugenzi wa mafunzo na utafiti Erick Nyato alisema kuwa Muundo wa serikali tatu utahimiza na kujari maadili na miiko ya viongozi wa umma kupunguza mamlaka ya Rais katka uteuzi wa viongozi mbali mbali.

  Suala la serikali tatu sio kuvunja amani hili ni suala la uongozi kama itashindikana ni kubadilisha uongozi kwa sababu ni maamuzi yetu wenyewe wananchi . 

  0 0


  Askari wa Kikosi cha kutuliza Fujo Akizima  Moto uliowashwa na wakulima waliofunga barabara ya Morogoro Iringa Leo Asubuhi.Wakulima hao walifunga Barabara hiyo kwa Lengo la kushinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Joel Bendera  Ili kutatua Mgogoro uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopo katika vijiji hivyo.Askari wa jeshi la Polisi walilazimika Kutumia Mabomu ya Machozi mara baada ya Wananchi wao kugoma Kuonana na Kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mvomero Ikiongozwa na Mkuu Wa Wilaya ya  mvomero.
   Wananchi wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wameshika mawe na Silaha za Jadi wakikataa kabisa kufungua barabara hiyo wakitaka Mkuu wa Mkoa kuja Kuoanana Nao.

  Mabomu ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji. 

  Wakulima wa kijiji cha Mangae wilaya Mvomero wamefunga barbara kuu ya Morogoro Wakulima hao ambao wanalima katika Mashamba yaliopo eneo la Mkangazi  baada ya wananchi kuvamiwa na kupigwa wakulima hao walikusanyikajana usiku na kufikia maamuziWakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.

  Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha mgongamano mkubwa wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa. Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.Wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo
  Askari wa Jeshi la Polisi Wakiwa Onyo wakulima wa Kijiji Hicho Kabla ya Kuanza Kutumia Mabomu ya Kutoa Machozi kwa Lengo la Kuwatanya.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo wakati akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa rasimu ya katiba kwa viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
  viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na wenyeviti wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad   wakiongozana na Sehemu ya viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa,wakitoka katika mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Picha na Issa Michuzi.

  0 0

   NOTICE IS HEREBY Given that a General Meeting of the foundation will be held at Cine Club, Mikocheni/Msasani, Dar es Salaam on Saturday, 8th February, 2014 at 10.00hrs.

  Mkutano wa Weruweru Alumnae Foundation utafanyika Jumamosi tarehe 8 Februari 2014, Cine Club, Mikocheni/Msasani, Dar es Salaam kuanzia saa Nne (4) asubuhi ,Tafadhali mtaarifu Golden Girl mwingine


  0 0  Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa SSRA, Bagamoyo leo.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka, akisoma hotuba yake na kisha kumkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

  Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji, Sarah Kibonde Mkataba wa Huduma kwa Wateja, wakati wa uzinduzi huo. Kushoto niMkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka.
  Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, akimkabidhi Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa SSRA. Kulia anayepiga makofi ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawa wa wizara hiyo, Noah Mwaikuka.
  Mwakilishi wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Athuman Juma, akisoma risala ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo, wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi, lililozinduliwa naWaziri wa Kazi na Ajira, Gaudetia Kabaka, Hoteli ya Millenium Sea Breeze, Bagamoyo, mkoani Pwani leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

  Baadhi ya wafanyakazi wa SSRA, wakiwa katika mkutano wa uzinduzi huo, Bagamoyo, mkoani Pwani leo. 
  Baadhi ya wafanyakazi wa SSRA, wakiwa katika mkutano wa uzinduzi huo, Bagamoyo, mkoani Pwani leo.

  Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kulizindua baraza hilo leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka.
  Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi huo leo. Kulia niMkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka.
  Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa na na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, Wakurugenzi wa na wafanyakazi wa SSRA, pamoja na wageni waalikwa, mara baada ya uzinduzi huo.
  Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa na na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, baadhi ya Wakurugenzi na wageni waalikwa, wakiwa katika picha ya pamoja. Nyuma ni wafanyakazi wa Mradi wa Core Business Application (CBA).
  Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa na na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, baadhi ya Wakurugenzi na wageni waalikwa, wakiwa katika picha ya pamoja. Nyuma ni washindi wa tuzo mbalimbali wa SSRA.
  Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa na na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, wageni waalikwa, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vya SSRA.
  Mgeni rasmi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akiwa naMkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, wageni waalikwa, wakurugenzi Lightness Mauki (kushoto) na Sarah Kibonde (kulia) wakiwa na Afisa Uhusiano wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji cha SSRA. Gaudiosa Mahundi (nyuma), wakati wa uzinduzi huo.

  Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, akisindikizwa naMkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, mara baada ya kulizindua baraza hilo.


  0 0

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga(mbele aliyesimama) akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano kuhusu ushirikiano wa serikali na vyombo vya Habari katika kuimarisha Mawasiliano Serikalini.Wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Habari na Mawasiliano leo Mkoani Tanga.


  ===========   =============  ============
  Na ASSAH MWAMBENE, Tanga

  Baraza la Habari Tanzania limesema kuna haja ya kujenga miundombinu itakayoboresha ushirikiano kati ya Maafisa Habari na Vyombo vya Habari ili kuboresha utendaji kazi katika tasnia ya habari.

  Akizungumza katika kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kinachoendelea mjini Tanga, Katibu  Mtendaji wa MCT, Bw. Kajubi Mukajanga amesema ili sekta ya habari iweze kuboreka ni lazima kuwe na ushirikiano wa kutosha kati ya Maafisa Habari na Vyombo vya Habari.


  Alisema kimsingi vyombo vya habari vinatakiwa kufanya kazi kwa pomoja kutokana na ukweli kwamba kila upande unamhitaji mwenzake ili kutimiza  majukumu yake.

  “kimsingi tunahukumiwa kufanya kazi kwa pamoja” alisema Bwana Kajubi, akinukuu sehemu ya Hotuba aliyotoa Mhe. Rais Jakaya mrisho Kikwete katika moja ya mikutano ya “open Government uliofanyika London Uingereza.


  Akizungumza kuhusu fikra mgando katika Vyombo vya Habari, alisema kumekuwa na tatizo la baadhi ya wanahabari kugeuka kuwa wanaharakati na kuvaa fikra ya kupambana na serikali kama wanavyofanya wanaharakati.


  unaowaelekeza wadhani kuwa wanahabari wako katika mapambano na serikali.

  “Kama habari nzuri za serikali haziuzi mbona Timu ya Taifa au Mwakilishi wa Taifa kwenye mashindano ya Kimataifa akishinda watu hupenda kusoma” Alisema Bwana Kajubi. Alisema kwa maoni yake kushikilia kuandika matatizo tu kuhusu nchi yetu sio kuisaidia nchi na hakujengi moyo wa wananchi kujiamini na uzalendo.   

  Bw. Kajubi alikuwa akitoa mada kuhusu Ushirikiano wa serikali na Vyombo vya habari katika kuimarisha Mawasiliano Serikalini katika kikao kazi za Maafisa Habari na Mawasiliano. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


  Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano unawahusisha Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Serikali za Mitaa, Mikoa na mashirika ya umma wapatao 130 kutoka nchi nzima.


  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Khamis M. Mgeja akimpa pole Afisa Mtendaji wa kata ya Ubagwe katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu Alphonce John Kimario aliyejeruhiwa kwa kushambuliwa na mapanga na watu aliowataja kuwa ni wafuasi wa CHADEMA, kupitia vurugu zilizotokea juzi saa moja usiku katika kata ya Ubagwe muda mfupi baada ya kumalizika kwa kampeni za kumnadi mgombea wao. 
  Akizungumza na waandishi wa habari Afisa huyo Mtendaji wa kata ya Ubagwe, Alphonce John Kimario amesimulia kuwa sanjari na kuumia vibaya machoni hasa jicho lake la kulia pia analalamika juu ya maumivu makali anayo yasikia mgongoni mara baada ya kupigwa na nondo ambapo kwa hivi sasa upande wa kulia sanjari na bega lake umekufa ganzi. 
  Ndugu Alphonce Kimario (Afisa Mtendaji wa kata ya Ubagwe) ambaye amepigwa nondo, amepigwa mapanga kwenye paji la uso kiasi cha kushonwa nyuzi kadhaa na kutobolewa jicho moja amekimbizwa hospitali ya Rufaa Bugando kutokana na hali yeke kuwa mbaya zaidi.
  Tabitha Shuli ambaye ni Afisa Muuguzi Idara ya Macho Hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza akimhudumia Ndugu Alphonce Kimario.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis M. Mgeja akiongozana na makada wengine wa CCM mkoa wa Mwanza kuelekea ward nyingine kuwaona majeruhi wengine walio lazwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza mara baada ya kushambuliwa kwa mapanga pamoja na kuharibiwa mali zao mara baada ya kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga..
  Dereva wa gali la CCM wilaya ya Kahama Charles Peter akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa mapanga wakati wa kampeni za udiwani wilayani humo.
  Majeruhi wengine  kama Masoud Melimeli (katibu Mwenezi wa Wilaya) amebaki katika uangalizi wa Hospitali ya Wilaya akiwa na majeruhi wengine kama Ramadhani Salum (Umoja wa Vijana) na Mussa Daudi (Katibu Uchumi Kata ya Nyihogo) ambaye alilazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama na mara baada ya kuzidiwa leo asubuhi amepakiwa katika AMBULANCE kuwahishwa Bugando kwa ajili ya matibabu zaidi. Ikitajwa kuwa yeye alipigwa nondo ya kifuani.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Khamis M. Mgeja akimpa pole Sebastian Masonga (Katibu UVCCM Kata ya Majengo) aliyepigwa nondo na hatimaye kuvunjwa mkono wa kushoto, kuliani ni mwenyeji wa msafara huo ulio tembelea hospitali hiyo, Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Mama Joyce Masunga.
  Sebastian Masonga ambaye ni Katibu UVCCM Kata ya Majengo akisimulia juu ya tukio zima la kuvamiwa. 
  Pamoja na kulaani vurugu hizo Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Khamis M. Mgeja,  amesema kuwa jeshi la polisi nchini limeahidi kuweka  ulinzi wa kutosha hivyo amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili kwenye zoezi la kupiga kura ili kuilinda haki yao ya msingi ya kumchagua mtu anaye stahili. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.  0 0


  0 0


  Millions of girls in Tanzania are dis-empowered by the simple biological process of menstruation. Affordable and hygienic sanitary protection is not available to girls in many areas especially rural community. They resort to the use of unhygienic rags and cloths which puts them at the risk of infections.

  Girls in Tanzania suffer from lack of adequate solutions to manage menstruation. Imported pads are prohibitively expensive for low-income families. Research conducted in Tanzania indicates that about 90 percent of the rural girls cannot afford off-the-shelf sanitary pads and instead improvise with materials such as grass, leaves, old papers, and pieces of cloth. These materials have limited absorbency and make it difficult for girls to participate in school during their periods.

  Consequently, these Tanzanian female students are forced to skip classes at least five (5) to seven days (7) in a month (12 weeks a year) depending on an individual period days, this lead to poor performance in their school and different genital diseases.   The failure of Tanzanian female students in primary and secondary schools in rural areas to have access to sanitary pads due to poverty leads them to skip classes for 12 weeks a year, this causes poor performance in their subjects.

  Climb Mount Kilimanjaro for a Cause JOIN Tanzania Aspiration Initiatives - TAI to FUNDRAISE for a Project that will Support girls in Rural Areas on their Menses for Healthy Education in Tanzania and enhance Gender Equality. For More Information please visits www.tai.or.tz or call: +255 712 818 562 

  0 0


  Sasa waweza kutinga Skylight Beach Resort Malimbe kwa njia ya maji.
  Njiani ni full utalii.
  Kwa mbaaaliii kiwanja chaonekana.
  Heee ni paleeee....!!
  Kula upepo muhimu.
  Ukila upepo mwanana Eh bana eeeh... Bustani hii ya kitalii utaimiliki kuanzia Valentine hii.
  Hapa pata badilika zaidi ya unavyo paona vuta subira picha nyingi zitaendelea kumiminika hapa bloguni.
  Another side ya Skylight Beach Resort Malimbe Mwanza.
  Chillin with my broo Nsimbo Jembe.


  "Chekshia paleeee!!
  Thats Y we call it Rock City.
  FULLMOON PARTY at Skylight Beach Resort in Malimbe Mwanza
  VALENTINE'S DAY 14/FEB/2014
  uSIKoSe!!


  0 0

   Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akisoma dua kabla ya kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili kuanza katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaa
   Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa wakiomba dua katika kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili kabla ya kuanza katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
    Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa katika kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili  katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
     Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa katika kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili kuanza katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
     Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa katika kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
     Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya siasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha APPT-Maendeleo, Mhe Peter Mziray akisoma hotuba yake katika  kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili  katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa Barza la Vyama vya Siasa Mhe. Peter Mziray
   Viongozin wakisikiliza hotuba kwa makini
   Viongozi wa vyama vya siasa wakiwa kikaoni hapo
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akiwa na Kamishna Isaya Mungulu Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai DCI wakiwa wageni waalikwa kikaoni hapo
   Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
   Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
   Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
   Viongozi wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete
   Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
   Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete.


   Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
   Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
   Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
   Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
   Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
   Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
   Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
   Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
   Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe na Katibu wake Mhe Wilbroad Slaa wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete kwa makini
   Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe akifuatilia hotuba hiyo

   Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
   Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
   Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
   Viongozi wakimpigia makofi Rais Kikwete
   Viongozi wakiangua kicheko 
   Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akitoa neno la shukurani
   Rais Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariffa Hamad, Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi na viongozi wa vyama na maafisa wa serikali wakitelemka ngazini baada ya kupata chakula cha mcha pamoja
   Rais Kikwete na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariffa Hamad wakiongea
   Sehemu ya wajumbe wa kikao
   Wajumbe wa kikao
   Wajumbe kikaoni
   Wajumbe kikaoni
   Rais Kikwete akiendelea na hotuba
   Wajumbe wakisikiliza kwa makini
   Rais Kikwete akimalizia hotuba yake
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Pokea rasimu ya katiba mheshimiwa...
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
   Rais Kikwete akisalimiana na Mhe Tundu Lissu baada ya kufungua kikao
   Rais Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika picha ya kumbukumbu na wenyeviti wa vyama vya siasa baada ya ufunguzi wa kikao hicho
   Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na Mhe Freeman Mbowe kwa hotuba nzuri
   Picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya siasa
   Picha ya pamoja na makatibu wakuu wa vyama vya siasa
   Picha ya pamoja na wajumbe wa kikao
   Picha ya pamoja na viongozi wa dini na wa vyama vya siasa pamoja na wageni waalikwa
   Rais Kikwete akiongea na Mhe James Mapalala
   Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila
   Mhe William Lukuvi akisalimiana na Mhe Wilbroad Slaa
   Rais Kikwete, Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Francis Mutungi Mhe Peter Mziray na Mhe Freeman Mbowe wakitoka nje ya ukumbi
   Rais Kikwete akiongea na viongozi baada ya kufungua kikao hicho
  Rais Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya siasa Mhe Peter Mziray na viongozi wengine.

  0 0

   Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Ndugu Jamal Malinzi katikati akizungungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo juu ya mafanikio ya uongozi wake kwa siku mia moja toka waingie madarakani, Kulia ni Afisa habari wa TFF Bonifas Wambura na kushoto ni Mshauri wa ufundi Bwana Rutayunga Peregenus
   Pichani ni baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo uliofanyika leo ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Kempisk Hyatt Regence Hotel,jijini Dar.

  0 0

  ·       Mabadiliko yataleta ufanisi kwa huduma ya Airtel money
  ·       Mabadiliko yatawezesha  wateja kufanya mambo mengi na kuongeza watumiaji wa huduma ya Airtel money
  ·       Mabadiliko yataongeza matumizi ya huduma ya Airtel money Tanzania

  Dar es Salam Februri 7 2014:  Airtel Tanzania, kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za kibunifu na zenye ubora nchini iko katika mchakato wa kuboresha mitambo ya huduma ya Airtel money na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi.  Mabadiliko haya yatafanyika mwishoni mwa wiki hii  tarehe 7 hadi 9 februari 2014 ambapo baada ya maboresho hayo wateja wa Airtel Money watafurahia ufanisi bora wa mtambo wa Airtel money  wakati wowote watakapotaka kufanya malipo mbalimbali kwa kupitia huduma za kifedha  za simu za mkononi

   Maboresho hayo ya mitambo ya Airtel money wateja wataweza kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na  kuunganishwa na huduma mbalimbali na kuongeza ufanisi zaidi . Huduma hii itawawezesha wateja kununua muda wa maongezi, kutuma pesa, na kufanya malipo ya huduma mbalimbali, kutoa na kutuma pesa pamoja na kuongeza huduma mbalimbali wanazotakana kuzitumia kupitia Menu/orodha ya mpya ya huduma hiyo ya Airtel Money zikiwemo zile za kuunganishwa na huduma za kibenki

  Akiongea kuhusu mabadiliko hayo ya mitambo, Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “kuboreshwa kwa mitambo yetu ya huduma za kifedha ya Airtel money  ni sehemu ya malengo ya Airtel ya kuwawezesha wateja wetu kufanya miamala ya pesa mahali popote wakati wowote kwa urahisi zaidi. Tunaamini maboresho haya yataleta urahisi zaidi kwa watumiaji wa huduma ya Airtel money nchini”

  Bi Singano aliendelea kusema, “wakati wa kuboresha hatutegemei kuwa na matatizo yoyote wakati wa zoezi hilo la kuborehsha mitambo yetu na tunawaomba wateja wetu wawe wavumilivu kwa usumbufu utakaojitokeza wakati tutakapokuwa tunafanya zoezi hili kuanzia jumamosi saa 3 usiku hadi jumapili asubuhi . 

  tunawahakikishia wateja wetu wa Airtel Money wote kuwa tunafanya mabadiliko yatakayoleta ufanisi zaidi kwa watumiaji wote,  mashirika binafsi, serikali, mabenki na wadau mbalimbali. Huduma yetu kwa wateja inapatikana masaaa 24 siku zote 7 za wiki ili kuweza kutoa huduma iwapo kutakuwa na matatizo yoyote. Pia tutaweza kuwasaidia wateja wetu watakaowasilisha baadhi ya matatizo kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii yaani Facebook and Twitter.”.

  Maboresho ya Airtel Money yenye lengo la kuendelea kutoa huduma Bora zaidi pia yanadhihirisha jitihada za Airtel kuendeleza ubunifu wa hali ya juu  kwa kuleta teknolojia mpya za kisasa zaidi katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, Tumedhamiria kuwaletea wateja wetu huduma bora zaidi inayokwenda sambamba na mahitaji yao ya kila siku. Hii ndio sababu kubwa inayotufanya Airtel kuboresha mtambo wetu wa huduma hii ya Airtel Money kuwa wa kisasa zaidi.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Oman nchini Tanzania, Soud Ali Mohamed Al Ruqaishi, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 7, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Balozi mpya wa Oman nchini Tanzania, Soud Ali Mohamed Al Ruqaishi, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 7.

  ========   ========   =========

  MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA BALOZI WA OMAN NCHINI.

  Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amempokea Balozi mpya wa Oman nchini Tanzania Balozi Soud Ali Mohamed Al Ruqaishi ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam na kisha kufanya naye mazungumzo. Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais amemhakikishia Balozi Ruqaishi kuwa Tanzania na Oman zina uhusiano wa kindugu wa siku nyingi na kwamba uhusiano huo umekuwa ukinufaisha nchi hizi kwa miaka kadhaa. 

  Mheshimiwa Makamu wa Rais aliendelea kufafanua kuwa, Tanzania kwa sasa inashirikiana na Oman kiuchumi na kwamba kuna wawekezaji wengi kutoka Oman ambao wako nchini, sambamba na wengine wanaoonesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali hapa Tanzania.

  Kwa upande wake Balozi Ruqaishi alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, Oman inafurahia uhusiano wake na Tanzania na kwamba jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha kuwa uhusiano huo unadumu na kunufaisha nchi hizi mbili. Pili alifafanua kuwa, atahakikisha katika kipindi chake cha Ubalozi hapa Tanzania anasaidia kutanua fursa za uwekezaji kwa wawekezaji kutoka Oman sambamba na kuwafungulia fursa kama hizo wawekezaji walio na nia ya kuwekeza nchini Tanzania. 

  Oman licha ya kuwa na uhusiano wa karibu na Tanzania na hasa Visiwani Zanzibar, inabakia kuwa ndiyo nchi pekee duniani nje ya Afrika iliyo na wazungumzaji wengi wa lugha ya Kiswahili. Katika siku za hivi karibuni, wawekezaji kutoka Oman wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya Mafuta na Gesi sambamba na kuliimarisha shirika la Ndege Tanzania ili limudu ushindani na kuongeza ufanisi wa shughuli zake katika biashara ya safari za anga.
  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
  Dar es Salaam, Ijumaa Februari 07, 2014

  0 0

  MKUTANO MKUU WA SHIRIKISHO LA WAMILIKI WA SHULE NA VYUO VISIVYO VYA KISERIKALI WAFUNGULIWA LEO MKOANI IRINGA.

  Mkutano mkuu wa shirikisho la wamiliki wa shule na vyuo visivyo vya serikali kanda ya nyanda za juu kusini mkoa wa Ruvuma ,njombe na Iringa, TAMONGSCO umefunguliwa mapema hii leo kwa kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa elimu kutoka maeneo makuu ya muungano wa serikali mbalimbali duniani.
   
  Akitoa hotuba mwenyekiti wa TAMONGSCO  kanda ya nyasa CHELESTINO SIMBAIMILE MOUGA ameiomba serikali kuondoa kodi zote katika elimu ili kuvutia wawekezaji wengi katika sekta hiyo muhimu . Ameiomba serikali itoe ruzuku kwa shule zisizo za serikali ili kuboresha ufundishaji na kupunguza gharama za uendeshaji wa ada za shule kuwa kubwa kwa baadhi ya shule.
   
  Naye mjumbe wa kamati ya kimataifa OGP HADIJA MCHATA MAGGID amesema kuwa serikali pekee yake haiwezi kutoa elimu badala yake inahitaji wadau mbalimbali wa elimu hususani watu binafsi ili kufanikisha sera ya elimu kufanikiwa kwa kasi.
   
  Kwa upande wake mwakilishi wa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya kilolo GERALD GUNINITA amesema kuwa mafanikio hayo ni hatua muhimu ya kujivuniakatika taifa letu kwani inawajibu wa kuelimisha na kuendeleza katika kumkomboa mtanzania kutoka katika umasikini unaotokana na ujinga.
   
  Amesema kuwa wanafunzi wanapaswa kuhimizwa zaidi katika maelekezo ya masomo yao ili waweze kufanikiwa kitaaluma wanapokuwa shuleni na vyuoni pia wakumbuke kuwa kuna gonjwa la ukimwi na kanda yetu inaongoza.
  MWISHO.
   
  SHIRIKA LA CAMFED LATOA MSAADA WA VITABU KWA SHULE ZA SEKONDARI 22 MKOANI IRINGA .

  Katika kuhakikisha kiwango cha elimu nchini kinakua,shirika lisilo la Kiserikali la Campaign for Female Education (CAMFED) chini ya mpango wake kuwasomesha watoto wa kike limetoa misaada ya vitabu 54,935 kwa shule 22 za sekondari zilizoko katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa vyenye thamani ya shilingi milioni 55.
   
  Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Ilula mgeni rasmi Mwenyekiti Huduma za Jamii wa Halmashauri ya wilaya Kilolo, Anna Kulanga amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo kwa kuweza kuwafikia wanafunzi wa shule za Iringa vijijini.
   
   
  Amewataka walimu na wanafunzi wavitumie vitabu  kwa kuvitunza ili viweze kutumika  muda mrefu na kuamini kwamba vitabu vivyo vitaleta ufanisi katika kukuza uelewa wa mwanafunzi katika matumizi sahihi ya lugha ya kiingereza.
   
   
  Aidha amesema vitabu hivyo vitumike kwa wanafunzi wote  wa shule husika na kuwaasa wanafunzi wa shule zilizofaidika na msaada huo kuacha tabia  ya kuuza vitabu na kuwataka walimu wa shule hizo kufatilia kwa makini wanafunzi wote watakaopatiwa vitabu hivyo.
   
  Naye Mwalimu mkuu wa sekondari ya Irole Laurence Maluka akiongea kwa niaba ya wakuu wa sekondari 22 zilizofaidika na msaada huo wa vitabu amesema msaada huo wa vitabu utaweza kuwasaidia wanafunzi kuwa na uweza wa kujisomea zaidi na kuwawezesha kufaulu kwani hapo awali kulikuwa na changamoto kubwa katika shule zetu ambapo uwiano ulikuwa kitabu kimoja wanafunzi 5 lakini kwa sasa ni vitabu 5 kwa mwanafunzi mmoja.
   
   
  Kwa upande wake Afisa Miradi wa CAMFED Tanzania, Christina Kyaruzi amewataka wanafunzi wa sekondari zote wilaya ya Kilolo mkoani Iringa amesema ili kuongeza uwezo wa kujisomea ni lazima vitabu hivyo vitunzwe ili viweze kuwafaidisha wanafunzi wengi huku akiwataka walimu wakuu kuwapatia wanafunzi kila mmoja vitabu vitano na kwenda navyo nyumbani hadi wamalizapo shule ndipo wavirudisha.
   
   
  Amezitaja shule zilizofaidika na msaada huo kuwa ni shule ya sekondari Ilula, Nyalumbu, Mazombe, Irole,Lundamatwe, Selebu, Ngangwe, Uhambingeto, Lukosi, Mlafi, Ndekwa ,Mtitu, Kilolo, Lulanzi,Ukwega, Udzungwa, Dabaga, Kitowo, Mawambala, Masisiwe, Madege na Makwema.

  ==========  =======  ==========

  WANANCHI WA KATA YA NDULI WAOMBWA KUONDOA HOFU KUFUATIA VURUGU ZINAZOTOKEA KWENYE KAMPENI  ZA UCHAGUZI MDOGO.

  Wananchi wa kata ya nduli wameombwa kuondoa  hofu kutokana na vurugu zinazotokea katika kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo wa udiwani.
   
  Akizungumza Mkurugenzi wa manispaa ya Iringa ,BiTheresia Mahongo hii leo, amesema wananchi wa kata ya Nduli wasitishwe na vurugu za wanasiasa ambazo zinatokea katika kampeni wanachotakiwa ni  kufuata sela za wagombea ili kumpata kiongozi atakaye waongoza.
   
  Pia mahongo amewasihi wananchi kujitokeza siku ya uchaguzi kwakuwa ulinzi umeimalishwa na kuwakanya wanachama wa vyama mbalimbali kutovaa sale za vyama vyao na ambao watavaa hawatoruhusiwa kupiga kula.
   
  Vilevile mahongo amesema vifaa vya kupigia kura vimefika katika vituo na amewataka kujitokeza mapema kwani vituo vitafunguliwa saa moja asubuhi.  wakati huo huo amesema kuwa Kutokana na ongezeko la watu katika kata za mtwivila na ruaha,wananchi waishio kata hizo wamependekeza kugawanywa kwa kata hizo.
   
  ameongeza kuwa mapendekezo hayo tayari yameshafikishwa katika serikali kuu hadi itakapo pitishwa na serikali. Aidha amesema mchakato wa ugawaji kata hiyo unaendelea kwa kata zingine kutokana na wingi wa watu na ili kuboresha huduma kwa wananchi hao.

older | 1 | .... | 219 | 220 | (Page 221) | 222 | 223 | .... | 1898 | newer