Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 218 | 219 | (Page 220) | 221 | 222 | .... | 1897 | newer

  0 0

  KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam ipo katika mkakati wa kujenga kiwanda cha kisasa kwa ajili ya kuzalisha bidhaa zinazohusiana na kazi za wasanii.

  Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alex Msama alisema Dar es Salaam juzi kuwa kiwanda hicho kitakapokamilika kitakuwa mkombozi kwa wasanii wa aina mbalimbali ambao wamekuwa wakipata tabu kupata malighafi zinazohusiana na kazi zao. “Badala ya kuhangaika nje ya nchi kupata CD au DVD au mambo mengine yanayohusiana na kazi za wasanii, sisi tutakuwa tunatengeneza hapahapa Tanzania kwa ubora mzuri zaidi.


  “Tumejipanga katika hili na tayari kuna kampuni ya China tumefikia hatua nzuri kwa ajili ya jambo hili na mapema mwezi ujao nitaenda huko kwa hatua za mwisho za mazungumzo ya ujenzi wa kiwanda hicho.

  “Kitakuwa kiwanda cha kisasa ambacho naamini wasanii Watanzania watakifurahia na kitawapunguzia gharama katika kuandaa kazi zao na hilo tunalifanya kwa nia njema kabisa kuhakikisha tunawasaidia wasanii,” alisema Msama ambaye pia Kampuni yake pia inaandaa Tamasha la Pasaka.


  Alisema awali lengo la kuanzisha kampuni yake lilitokana na kugundua kwamba muziki wa Injili bado uko nyuma  na haujapiga hatua nchini kulinganisha na nchi nyingine kama Afrika Kusini. "Niliamua kuanzisha Msama Promotions baada ya kuona muziki wa Injili umesahaulika na unashuka thamani yake, hivyo tukaona ni busara kuuinua ili tuwe kama wenzetu Afrika Kusini ambao wana waimbaji wa nyimbo za Injili wanaotamba kama Rebecca Malope,  Steve Kekane, Vuyo Mokoena na wengine wengi," alisema.


  “Hili la kuuweka katika jamii muziki wa Injili tumefanikiwa sana, hivi sasa nguvu zetu zipo katika kuanzisha kiwanda cha kuzalisha kazi mbalimbali zinazohusiana na kazi za wasanii. Zitakuwa bidhaa nyingi sana sitaweza kuzitaja zote,” alisema Msama.
  0 0


  0 0


  0 0

  Naibu waziri wa maliasili na utalii,Mhe. Mahamud Mgimwa akizungumza katika uzinduzi wa madarasa mawili ykatika shule ya sekondari ya Nkoarisambu wilayani Arumeru.
  Mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi ya taifa TANAPA, Bw. Allan Kijazi akitoa taarifa ya kukabidhi mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule  ya sekondari Nkoarisambu wilayani Arumeru.
  Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira Mh James Lembeli akizindua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule ya sekondari  Nkoarisambu wilayani Arumeru,ujenzi ulifanywa kwa msaada wa shirika la hifadhi ya taifa(TANAPA)na wananchi wa Arumeru.
  Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira Mhe. James Lembeli akizindua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule ya sekondari  Nkoarisambu wilayani Arumeru,ujenzi ulifanywa kwa msaada wa shirika la hifadhi ya taifa(TANAPA)na wananchi wa Arumeru.
  Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Mh Joshua Nassar akizungumza jambo na mwenyekiti wa kamati ya ardhi,maliasili na mazingira Mhe. James Lembeli, kulia kwake ni mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Henry Shekif.
  Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Mhe. Joshua Nassari akizingumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa madarasa mawili ,shule ya sekondari Nkoarisambu wilayani Arumeru,ujenzi ulifanywa kwa msaada wa shirika la hifadhi ya taifa(TANAPA)na wananchi wa Arumeru.

  0 0

  MIKOA sita imeomba kuandaa Tamasha la Pasaka mwaka huu.
  Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka ndani ya Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka kumekuwa na maombi mengi sana ya wadau wanaotaka tamasha hilo.

  Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema kwa sasa wanashughulikia vibali vya tamasha hilo na wala si vinginevyo. “Yapo maombi mengi sana, lakini akili yetu kwa sasa ni suala la kupata kibali cha onesho lenyewe na baada ya hapo mambo mengine yatafuata.

  “Sisi ni watu wa kufuata taratibu za nchi zinasemaje, ndiyo maana unaona hatuhangaiki sana kwa sasa na wanaoomba kuandaa tamasha, ila tukishapata kibali kutoka Basata (Baraza la Sanaa la Taifa), ndiyo mambo yatajipa zaidi,” alisema.

  Kwa mujibu wa Msama, wadau wa muziki wa Injili wa mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Dodoma, Tanga, Dar es Salaam na Shinyanga ndiyo ambao mpaka sasa wameomba kufanyika tamasha hilo mikoani mwao.

  Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Krismasi kila mwaka.

  0 0

  Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.

  Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki  anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.

  Wengine ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa kamanda wa Polisi  Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.

  Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi  Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora .

  Aidha, aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.

  Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Awadh Haji   anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.

  Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe  Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi  (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe,   Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala.  
     
  Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya usalama.

  Imetolewa na:
  Advera Senso-SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika na tayari imeanza mchakato katika kukabiliana na magugu maji katika Ziwa Viktoria sambamba na shughuli nyingine zinazolenga utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na majanga yanayotokana na athari za tabia nchi. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Sola Pawa ndogo maalum kwa kuchajia simu na kusomea baada ya kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikabidhiwa Nembo ya Taasisi hiyo iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam, leo.
  Makamu wa Rais Dkt Bilal akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa ofisi hiyo baada ya kufunguliwa rasmi, eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiagana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, baara ya uzinduzi huo. Picha na OMR 

  0 0

  Kutoka kushoto ni mratibu mwenza wa Tamasha la Jogging, Mashauri, Mratibu wa Jogging, KP, Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Mratibu wa Matukio wa Global, Luqman Maloto na Meneja wa Stamina, Said Ramadhani 'Kabwela'.
  Abdallah Mrisho akisisitiza jambo katika mkutano huo na waandishi wa habari (hawapo pichani)
  Mkutano ukiendelea.
  Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
  Mwanamuziki wa Bendi ya Msoondo Ngoma, Said Mabela akizungumzia maandalizi yao katika bonanza hilo.

  Mambo yameiva! Waratibu wa lile tamasha kubwa la mbio za taratibu (jogging) na huduma ya habari mpya zilizotokea punde ya Global Breaking News chini ya Global Publishers wameahidi kufanya makubwa ndani ya Dar Live Jumapili hii.

  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza ya Afrika-Sana, Dar leo asubuhi, meneja mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ alisema kuwa shughuli itakuwa nzito hivyo watu wafurike kwa wingi kushuhudia burudani ya aina yake.

  “Baada ya jogging, kutakuwa na burudani kubwa ya muziki kutoka kwa wasanii wakubwa, Nay wa Mitego, Stamina, H. Baba na bendi inayopendwa na wengi ya Msondo,” alisema Abby Cool huku akisisitiza kuwa kwa mara ya kwanza Dar Live itaangusha burudani ya nguvu bila kiingilio.

  Kwa upande wake, mratibu wa tamasha hilo la jogging, KP amesema: “Jogging itaanzia pale Uwanja wa Taifa hadi Dar Live. Vikundi zaidi ya 150 vimethibitisha kushiriki. Watu waje kwa wingi kuona mambo matamu bure kabisa kwani hakutakuwa na kiingilio.”

  Naye meneja wa msanii Stamina, Kabwela aliahidi kuwa Stamina amejipanga kufunika vibaya siku hiyo kwani amekuwa kwenye mazoezi ya kufa mtu.

  Mbali na Jogging, Breaking News, pia Global Publishers imetambulisha shindano lake jipya la Global Star Search litakaloanza hivi karibuni kwa lengo la kuibua vipaji na kutengeneza ajira kwa vijana.
  PICHA HABARI NA ERICK EVARIST/GPL

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Bi. Rose Shelukindo akisisitiza umuhimu wa zoezi la Kujiandaa na Maafa yanayofanyika mjini Bagamoyo.
  Baadhi ya Washiriki wa zoezi la Kujiandaa na Maafa wakifuatilia maelezo ya Mpango wa kujiandaa na Maafa yanayofanyika mjini Bagamoyo kutoka kushoto ni John Jordan Mratibu i mradi CDHAM , Mhandisi. Fanuel Kalugendo-Ofisi ya Waziri Mkuu na Faith Cooper Mratibu Mradi CDHAM.
  Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba (wa pili kulia), Mkurugenzi Msaidizi (Operasheni) Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Nyancheghe Nanai (kushoto) na Mkurugenzi wa Masuala ya Afya USAFRICOM wakiwa pamoja mara baada ya Uzinduzi wa zoezi la kujiandaa na maafa.
  Washiriki kutoka Tanzania, Marekani, Kenya, Nigeria,Ghana na Uganda wakiwa pamoja baada ya Uzinduzi wa zoezi la Kujiandaa na Maafa yanayofanyika kuanzia tarehe 3- 7 Februari 2014 Mjini Bagamoyo, Zoezi hilo limeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na USAFRICOM na CDHAM. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

  0 0

   Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akiongea na wafanyabiashara wa jijini Mwanza katika ukumbi wa Benki Kuu alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea mikoa ya Kagera, Mara na Mwanza. Wa kwanza ushoto ni Meneja wa Mashine za Kodi za Kielektroniki (EFDs) nchini Massoud Issangu na wa katikati ni Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato nchini Patrick Kasera.
   Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato nchini Patrick Kasera akiongea na akiongea na wafanyabiashara wa jijini Mwanza katika ukumbi wa Benki Kuu tawi la Mwanza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Fedha  kutembelea mikoa ya Kagera, Mara na Mwanza. Wa kwanza ushoto ni Meneja wa Mashine za Kodi za Kielektroniki (EFDs) nchini Massoud Issangu.


   Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (kulia) akiwa kwenye mkutano na wafanyabiashara wa jijini Mwanza katika ukumbi wa Benki Kuu tawi la Mwanza.alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea mikoa ya Kagera, Mara na Mwanza. Kushoto ni . Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato nchini Patrick Kasera.

   Baadhi ya wajumbe wa mkutanao wa wafanyabiashara wa Mwanza wakiwa kwenye mkutano wao na Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima jijini Mwanza kuhusu masuala ya kibiashara ndani ya mkoa wao    
   Mmoja wa wafanyabiashara wa jijini Mwanza Leopord Kararugira akiuliza swali juu ya matumizi bora ya kibiashara ya mashine za EFD wakati wa mkutano wafanyabiashara hao wa jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Fedha katika ukumbi wa Benki Kuu tawi la Mwanza.

   Mfanyabiashara wa jijini Mwanza Mgesi Marwa akiuliza swali juu ya hofu yao ya bei za mashine za EFD wakati wa mkutano wafanyabiashara hao wa jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Fedha katika ukumbi wa Benki Kuu tawi la Mwanza ambapo kwa mujibu wa Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato nchini Patrick Kasera bei ya chini ya mashine hizo ni sh.600, 000/= na bei ya juu ni sh.690,0000/=

  Naibu Waziri Adam Malima akiwa na baadhi ya viongozi wa TRA na Hazina ndogo mara baada ya mkutano na wafanyabiashara jijini  nje ya  ukumbi wa Benki Kuu tawi la Mwanza. (Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Mwanza)  0 0

   Kijana Bakari Hassan Katumbaku (Kulia) akionyesha Picha zake enzi za utoto kabla ya kupata ajali ya moto kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Vincent Tiganya.(Picha Benjamin Sawe wa Wizara ya Habari)
    Kijana Bakari Hassan Katumbaku (Kulia) akionyesha Picha ya Mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa Waandishi wa Habari hawapo Pichani wakati alipotembelewa kipindi cha matibabu yake katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam  baada ya kupata ajali ya moto, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Vincent Tiganya
  Kijana Bakari Hassan Katumbaku ambaye alipata msaada wa matibabu kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ambapo mpaka sasa anaendelea kupata msaada wa kusoma (kulia) akimshukuru Mheshimiwa Rais mbele ya waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kwa msaada aliopewa,kijana huyo kwa sasa anasoma katika Chuo cha "Tanzania School of Journalism" akichukua fani ya Uhandishi wa Habari ngazi ya Cheti.Bakari alipata ajali ya Moto, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Vincent Tiganya

  0 0  Juma Nkamia –Naibu  Waziri  mpya,Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

  Na Eleuteri Mangi (MAELEZO).

  Ni siku chache tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amuapishe Mheshimiwa Juma Nkamia kuitumika Serikali kama Naibu Waziri katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. 

  Kwa taaluma, Naibu Waziri Nkamia ni mwanahabari ambaye amesomea na kufanya kazi ya habari kwa kipindi kirefu kabla ya kuingia katika Ubunge ambao umemuwezesha kuteuliwa kuwa waziri.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika wizara hiyo,   Nkamia alisema anamshukuru  Rais Kikwete kwa kumteua na kumpa dhamana hiyo na kuahidi kuwa atasaidiana na Waziri wa wizara hiyo kutimiza majuku ya wizara katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya nne. 

  “Kama kiongozi mwenye mamlaka ndani ya wizara hii, nipo tayari kushirikiana na viongozi wenzangu katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara zote zinazounda wizara hiyo”, alisema.

  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inaundwa na idara kuu nne za kisekta ambazo ni Idara ya Habari, Idara ya Vijana, Idara ya Maendeleo ya  Utamaduni na Idara ya Maendeleo ya  Michezo.

  Kwa kuwa tasnia ya habari ni miongoni mwa idara zilizo chini ya wizara hii, Nkamia alisema kuwa yupo tayari kushirikiana na wadau wa habari ikiwemo kusimamia maslahi ya waandishi wa habari nchini.

  “Ukitaka kujua umuhimu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari katika nchi yeyote ile, jaribu kuvifanya  vyombo hivyo kuanzia redio, televisheni na magazeti visifanye kazi hata kwa muda wa saa moja tu uone ni hasara kiasi gani na hatari kiasi gani zitatokea katika nchi ile” alisema Nkamia.

   Alisema anaheshimu na anatambua umuhimu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari nchini na atafanya nao kazi vizuri kwa kipindi chote atakachokuwa wizarani hapo.

  Alisema kuwa anatambua kuwa  waandishi wa habari wanafanya  kazi katika mazingira magumu wakati wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo  tatizo la “ukanjanja” na lugha mbalimbali zinozotolewa juu yao.

  Ameahidi kushirishirikiana na viongozi na wadau wa habari kuhakikisha kinaundwa chombo (bodi) kitakachosimamia maslahi ya waandishi wa habari. 

  Bodi itakayoundwa itasaidia kusimamia tasnia ya habari na kuhakikisha habari zinazoandikwa zitakuwa kwa maendeleo, manufaa na maslahi ya taifa na kuhakikisha inawajengea heshima waandishi wenyewe kwa kazi zao wanazofanya kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na ya nchi.

  Naibu Waziri Nkamia ametoa rai kwa wadau wote wa habari kushirikiana ili kufanikisha uundwaji wa sheria ya habari. Alisema “Sheria hii ikikamilika itasaidia kuboresha baadhi ya changamoto za wanahabari ikiwemo ajira zao na mafao yao ya sasa na uzeeni”. 

  Nkamia amepewa wadhifa huo baada ya Rais Dkt. Kikwete kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri katika kuziba nafasi zilizoachwa na mawaziri wanne waliojiuzulu na mmoja aliyefariki mwanzoni mwa mwezi huu.

  Nkamia ni mkongwe aliyebobea katika taaluma ya uandishi wa habari akiwa amefanya kazi na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi.

  Aliajiriwa kwa mara ya kwanza na  Redio ya Taifa (Radio Tanzania Dar es Salaam) mnamo Oktoba 10, 1994 kama mwandishi msaidizi. Alifanya kazi RTD kwa muda wa miaka tisa hadi 2003  alipojiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

  Akiwa BBC Nkamia alifanya mambo mengi mazuri yaliyomjengea heshima mwenyewe na taifa. Ikizingatiwa kuwa Nkamia  alipenda sana kutangaza habari za michezo, alifanikiwa kutangaza mechi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

  Kama mwandishi wa habari za michezo, Nkamia alikuwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza kutangaza mchezo wa mpira wa miguu wa ligi ya Uingereza kwa lugha ya Kiswahili.

  Kutokana na umahiri wake katika kutangaza habari za michezo, Nkamia aliaminiwa kutangaza mchezo wa fainali ya ligi ya Uingereza mwaka 2006 kati ya Manchester United na Arsenal  na mwaka huo huo, BBC ilimpa tena jukumu la kutangaza mechi ya fainali ya Ligi ya klabu bingwa ya Ulaya kati ya Arsenal na Barcelona.

  Mwaka 2006 Nkamia alirudi nyumbani Tanzania na kujiunga na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo alifanyakazi kama mwandishi na mhariri hadi 2009.

  Mwaka 2009 hadi 2010 Nkamia alifanya kazi ya uandishi katika shirika la utangazaji la Sauti ya Amerika (VOA) inayomilikiwa na Taasisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kazi ambayo aliifanya kwa mwaka mmoja. 

  Mwaka 2010 Nkamia alitambua na kuitikia dhamiri yake ya kuitumikia nchi yake katika mambo ya siasa hivyo aliamua kurudi Tanzania kuomba ridhaa ya wana Kondoa Kusini awe mwakilishi wao bungeni na Kamati Kuu ya chama chake, Chama cha Mapinduzi, ikapitisha jina lake kuwa mgombea ubunge wa chama hicho jimboni humo.

  Nkamia anasema, kwa kuwa alikuwa anafanya kazi na watu, wapo waliomshagaa kuacha kazi ya maslahi zaidi na kurudi nyumbani. Miongoni mwa hao ni Dkt. Shaka Ssali mtangazaji na mmoja wa  wanahabari maarufu duniani aliyeuliza  Nkamia anafanya nini katika karne yenye changamoto ya ajira duniani kuacha kazi yenye mshahara na maslahi makubwa na kwenda kwenye siasa.

  Anasema kwake jibu la swali hilo lilikuwa rahisi kuwa ni Uzalendo wa nchi kwanza ndiyo maana aliamua kurudi  kutoa mchango wake kwa maendeleo ya watu wake wa Kondoa Kusini na nchi kwa ujumla.

  Kwa kuzingatia ukomavu na weledi alionao kwenye taaluma ya habari, ndiyo maana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ameamini na kumpa dhamana ili asaidiane  na Waziri mwenye dhamana katika Wizara hiyo, Fenella Mukangara, kuiongoza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

  Nkamia amechukua nafasi hiyo badala ya Mhe. Amosi Makalla aliyehamishiwa Wizara ya Maji.

  Wengine waliowahi kushika nafasi ya Naibu Waziri katika wizara hiyo ni Dkt. Makongoro Mahanga, N. Nswanzungwanko, Joel Bendera, Dkt. Emmanuel Nchimbi na Dkt.Fenella Mukangara ambaye sasa ni waziri wa wizara hiyo.    

  Juma Nkamia ni mtoto wa tatu kuzaliwa kati ya watoto sita wa familia ya Mzee Selemani Nkamia na Mwanaidi Ndwata. Anatokea eneo la kanda ya Kati katika mkoa wa Dodoma wilayani Kondoa. Ni  baba wa familia mwenye mke mmoja Bi Amina na watoto wawili ambao ni Kassi mwenye umri wa miaka 13 anayesoma kidato cha pili Shule ya Sekondari ya Wavulana Fezza na Hassani mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la pili katika shule hiyo hiyo.

  Kwa sasa Nkamia anaendelea kujiimarisha kielimu akiwa anasoma katika chuo Kikuu cha Dodoma.
  0 0

   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mohammed Said Mohammed amabe ni Mgeni Rasmin katika siku ya Cancer Duniani iliyo adhimishwa jana 04/2/2014 ofisini kwao Mpendae (kulia) Dkt. Msafiri Marijani ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ja maradhi ya Cancer Zanzibar (ZCA).
    Mwenyeki wa Jumuiya ja maradhi ya Cancer Zanzibar (ZCA). Dkt. Msafiri Marijani akitoa maelezo juu ya ukonjwa hatari wa Cancer katika madhimisho ya siku Cancer Duniani iliyoadhimishwa jana Mpendae Zanzibar.


   Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika madhimisho ya siku ya Cancer Duniani iliyoadhimishwa jana Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). 

  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


   OFISI YA RAIS,

   UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI  

   WA MIRADI,

   S L P 9120,

   DAR ES SALAAM.

   

     MFUMO WA MATOKEO MAKUBWA SASA (BRN) UNAFANYAKAZI

  Mabadiliko katika mfumo wa Serikali katika utendaji kazi kupata mafanikio haraka"


  Dar es Salaam, Tarehe 5 Febuari, 2014: Ofisi ya Rais - Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (OR- UUM) imetoa taarifa kwa umma kuwa  utekelezaji wa mfumo wa  – Big Results Now ! (BRN) unaendelea vizuri. Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaweka utaratibu thabiti wa  kufuatilia  na  kutathimini utekelezaji wa miradi  katika maeneo sita ya  kimkakati kitaifa (Kilimo, Elimu, Maji,  Nishati , Uchukuzi na Utafutaji wa Rasilimali). Mfumo wa  BRN unaweka  wazi malengo pamoja na kuainisha  uwajibikaji kwa kila mshiriki mmoja au taasisi katika utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kupata mafanikio haraka.


  Kila Wizara inayotekeleza mfumo huu imeanzisha Kitengo cha Kusimamia  Utekelezaji (Ministerial Delivery Unit (MDU))  ambacho kinafanya kazi kwa karibu sana na OR-UUM.  Majukumu ya MDU ni kufuatilia na kuthamini utekelezaji wa miradi wa kila siku na kuanda taarifa za utekelezaji za kila wiki na mwezi ambazo huwasilishwa OR-UUM. Taarifa za MDU zinajadiliwa kila mwezi kwenye mikutano ya Kamati ya Wizara ya Kusimamia eneo la kimkakati Kitaifa (Steering Committee Meetings) ambayo Mwenyekiti ni Waziri wa Wizara husika pamoja na Baraza la Mageuzi na Ufuatiliaji Utekelezaji ambalo Mwenyekiti ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mikutano hii inalenga  kutatua changamoto au vikwazo vilivyojitokeza.


  Aidha, Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha Vitengo vya Kusimamia Utekelezaji katika ngazi za Mikoa (Regional Delivery Units - RDUs) pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Council Delivery Units - CDUs) ili kuongeza ufanisi wa kutekeleza miradi katika ngazi zote.


  Bwana Omari Issa, Mtendaji Mkuu wa OR- UUM alisema, “Tanzania ina mawazo makubwa na Dira na mipango sahihi ya kuleta maendeleo. kinachokosekana ni mfumo sahihi wa kufuatilia utekelezaji ili kupata matokeo yaliyolengwa. BRN inaondoa dosari hii. Aidha, BRN inaleta mageuzi ya uwajibikaji katika ngazi zote za utumishi wa umma.


  Ili kufanikisha BRN, tunahitaji kupata ushirikiano kutoka  sekta binafsi ambayo italeta teknolojia, utaalum wa menejimenti na mtaji. Ili kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi, BRN imeanza mchakato wa kurazinisha  mfumo  na taratibu za  ubia baina ya Sekta ya Umma na  Sekta Binafsi (PPP) ili tuhakikishe kwamba sekta binfasi inatoa mchango wake  stahiki katika kutekeleza BRN

                                     
                                 


  -       MWISHO  -


  Kuhusu Matokeo Makubwa Sasa (BRN):


  BRN ni usimamizi utendaji unao tafsiri mipango ya miradi ya maendeleo kuwa mipango yenye tija kwa sababu ya malengo yaliyopangwa kufanya watendaji kuelewa wajibu wao vyema na kutambua kirahisi nani na maeneo ambayo hakuna uwajibikaji katika utekelezaji wa mradi.


  Maeneo sita ya kimkakati kitaifa yaliyochaguliwa na kuridhiwa na Baraza la Mawaziri kufuatia mikutano kadhaa maalum ni:


  1.                   Usambazaji wa maji salama vijijini- Wizara ya Maji

  2.                   Ulinzi wa Chakula  – Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

  3.                   Elimu ya msingi na sekondari– Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

  4.                   Kumiarisha usafirishaji wa Bandari, Reli na Barabara katika kanda ya

             kati– Wizara ya Uchukuzi

  5.                   Upatikanaji and Uzalishaji– Wizara ya Nishati na Madini

  6.                   Kuziwezesha kifedha miradi katika mfumo wa MMS– Utafutaji wa

             rasilimali fedha (Fedha)- Wizara ya Fedha


  Kazi ya OR-UUM kusaidia, kuwezesha, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa MMS katika  maeneo sita ya kimakakati kitaifa kwa njia ya mawasiliano na ufumbuzi wa matatizo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


    
  Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari imetolewa na:

  OR- UUM Mawasiliano, tafadhali wasiliana na OR- UUM kwenye:

  (pdbcommunications@gmail.com) or +255 658 870010 kwa maelezo zaidi au ufafanuzi.

  0 0


  Bondia Fabian Gaudence kushoto akipambana na Hussein Mnimbo  wakati wa mashindano ya wazi ya Nelson Mandela  yaliofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam,Gaudence alishinda mpambano huo kwa pointi .
  Bondia Rashidi Samvu kutoka Kigoma  kushoto  akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hafidhi Kassimu wa Ngome
  wakati wa mashindano ya wazi ya Nelson Mandela  yaliofanyika katika Viwanja vya TanganyikaPackers Kawe  jijini Dar es salaam
   
   
  Bondia Part Kimweri kutoka Tanga  kushoto  akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Saidi Jabir wa Ngome Dar wakati wa mashindano ya wazi ya Nelson Mandela  yaliofanyika katika Viwanja vya TanganyikaPackers Kawe  jijini Dar es salaam Kimweri alishinda mpambano huo kwa pointi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com.
  Baadhi ya viongozi wakifatilia mashindano hayo
  Mkeni wa heshima katikati Diwani wa Kata ya Kawe Othumani Kipete akiwa na viongozi wa Shilikisho la mchezo wa ngumi za Ridhaa nchini kulia ni Rais wa shilikisho hilo Mutta Rwakatare  makamu wa rais Lukelo Willilo na 
  Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis

  MAREFARII MABONDIA NA VIONGOZI WAKISUBILI KUFUNGULIWA KWA MASHINDANO HAYO
  mjumbe wa bft antony mwangonda akiwa na makamu wa rais Lukelo Willilo

  Na Mwandishi Wetu
  MASHINDANO ya mchezo wa Ngumi yanayokwenda kwa jina la Nelsoni Mandela Open ChampionShip  yameanza kutimua vumbi katika 
  Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam

  akizungumzia mashindano hayo yalivyo na ubora wa ali ya juu Makamu wa Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa nchini 'BFT' Lukelo Willilo 'amesema mashindano hayo kwa sasa yameboleshwa kwa kufuata taratibu za chama cha ngumi za ridhaa Dunia kwa sasa mabondia awavai kofia ngumu wanakuwa vichwa wazi hivyo wapenzi wa ngumi weje waone mabadiliko makubwa katika ngumi za ridhaa ndio ambazo ni msingi wa maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini;'

  zamani mabondia walikuwa wanavaa kofia lakini kutokana na mabadiliko sasa awavai kofia wanapigana vichwa wazi  ambapo kwa kuanzia tumeamua kuweka mashindano haya kwenye viwanja vya wazi na ni bule tu akuna kingilio ili kila mtu ajionee mabadiliko ya ngumi mashindano hayo yanayo husisha mikoa mbalimbali nchini

  mashindano haya yatakuwa ya siku tano kuanzia jumatano mpaka jumapili na ngumi zinanza kupigwa saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku ngumi ndio zitakuwa zikisha

  Katika ufunguzi huo bondia Patrck Kimweri wa Tanga alishindwa kufurukuta mbele ya Said Jabir wa ngome na Rashidi Samvu wa Kigoma alipigwa kwa pointi na Hafidhi Kassimu wakati Fabian Gaudence  akimsambalatisha Hussein Mnimbo  

  0 0


  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene,Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania Innocent Mungy (mwenyeshati la mistari) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Hermas Mwansoko (katikati) wakimkabidhi  kiroba cha mchele  moja ya Wazee wa Kituo cha Mwanzange Mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali katika kikao kazi kinachoendelea Mkoani humo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Hermas Mwansoko akimkabidhi Afisa Ustawi wa Jamii anayesimamia kituo hicho cha wazee Bi Otilia Daniel fedha za kununulia mahitaji mengine wakati wa ziara ya kutoa msaada katika kituo hicho leo Mkoani Tanga.
   Nyumba za Makao ya Wazee za Mwanzange Mkoani Tanga.
  Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano waliotembelea kituo cha wazee cha Mwenzange Mkoani Tanga
  Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee wa kito cha Mwanzange ambapo walitoa Unga sembe Kilo 200,mchele kilo 300,mafuta ya kupikia dumu 2,mafuta ya kupaka,dawa za meno,chumvi,sukari,maharage,nyama,majani ya chai,kanzu,misuli pamoja na nguo za kinamama.
  (Picha Na Hassan Silayo)

  0 0
 • 02/06/14--00:06: Beach Plot for SALE

 • Plot size 5800 square meters(1.5 Acres=0.58 Hectare)
  Location: Kunduchi Bahari Beach, near silver sand hotel & Bahari Beach Hotel 
  Its a beach front plot.Asking price is 1.2 USD million(TSH 2 Bilion) its negotiable 
  Contacts: Email address.... mwatawalawaladi@yahoo.com
                    Mobile no 0654254645/0713254645

  0 0
 • 02/06/14--00:22: basata yawashauri wasanii
 •  Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Profesa Penina Mlama akikagua nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga jana, kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza.
  Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Profesa Penina Mlama akikagua nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga jana, kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza.
  =======  ======== =======
  Na Peter Mwenda, Mkuranga

  MWENYEKITI wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Profesa Penina Mlama ametoa wito kwa wasanii kuchangamkia kuchangia ujenzi wa nyumba unaoratibiwa na Mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA) ili kujiandalia makazi.

  Akizungumza baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega, wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Profesa Mlama alisema makazi ni sehemu ya maisha ya binadamu hivyo wasidharau mradi huo ni faida kubwa kwao.

  Alisema nyumba ambazo ameziona ni nzuri, imara na zinauzwa bei ya chini ambayo huwezi kuzipata sehemu nyingine yoyote nchini Tanzania na kuongeza kuwa kujenga kwa lengo la kuishi pamoja kunatoa fursa ya wasanii kubuni njia nyingine ya kuanzisha miradi mbalimbali.

  Profesa Mlama alitaka SHIWATA isikate tamaa bali iendelee kuwashawishi wasanii wajiunge na kuchangia ujenzi wa nyumba ili baadaye wasitafute visingizio kuwa hawakupewa fursa hiyo.

  Naye Katibu Mtendaji wa BASATA,Godfrey Mngereza alisifu SHIWATA kubuni njia ya kuwasainia wasanii kupata makazi na kuahidi kuwa baraza hilo litatoa ushirikiano na kutoa ushauri kila unapohitajika.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema mpango wa ujenzi wa nyumba za wasanii utaendelea kote nchini na kuwataka wasanii waungane kufanya kazi zao kwa pamoja.

  Alisema mpaka sasa nyumba 38 zimekabidhiwa kwa wasanii waliochangia ujenzi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga na nyingine 21 zinatarajiwa kukabidhiwa Machi mwaka huu.

  SHIWATA mbali ya kusimamia ujenzi wa nyumba za wasanii inasimamia matamasha ya wasanii wachanga (Underground) kuendesha makongamano ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya na kutoa elimu na maadili kwa wasanii.


  0 0

   Afisa Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (wa pili kushoto) akiongelea umuhimu wa promosheni ya Mimi ni Bingwa muda mfupi baada ya kukabidhi shilingi milioni moja kwa baadhi ya washindi wa promosheni hiyo (waliopo pichani). Kushoto ni Bw. Ramdhani Wefa, Kulia ni Philemon Nathaniel Mgaya akifuatiwa na Bw. Msemwa Makuzi ambaye pia ni mshindi wa tiketi na wote wakiwa wanatokea Dar es salaam.
  Afisa Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia) akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa mmoja kati ya washindi wa milioni moja Bw. Msemwa Makuzi ambaye pia ni mshindi wa tiketi ya kwenda kushuhudia moja kati ya mechi za Manchester United nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old trafford.Mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 150 zimeshatolewa kwenye promosheni hiyo.
  ========  ========  ========
  Washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa waipongeza Airtel

  Wakati Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel ikisubiria kuchezesha droo kubwa ya shilingi Milioni 50 kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa, baadhi ya washindi waliokwishapatikana wamejitokeza wakiisifia kampuni hiyo kwa kuratibu promosheni zenye kulenga maendeleo kwa watanzania walio wengi nchini.

  Washindi hao wameainisha hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa pesa zao mapema wiki hii kwenye ofisi za makao makuu ya Airtel ziilizopo Morocco jijini Dar es salaam.

  Washindi hao wamedai kuwa mara nyingi watu huwa hawaamini promosheni zinazoendeshwa na kampuni ya simu kama Airtel na hivyo kujikuta wakibaki nyuma kwa kuogopa kuthubutu.

  “Mi binafsi sikuwahi kumuambia mke wangu kwamba nashiriki kwenye promosheni ya Mimi ni Bingwa sababu huwa akijua nashiriki ananikasirikia na kusema nina matumizi mabaya ya pesa, lakini leo nimeibuka mshindi wa shilingi milioni moja yeye akishuhudia na vilevile nimeshinda tiketi ya kwenda kushuhudia mechi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford,” alisema mshindi huyo Bw. Msemwa Makuzi mkazi wa Dar es salaam.

  Mshindi huyo aliendelea kwa kusema, kwa hali ya kawaida ilikuwa ni ngumu kuamini kwamba ameshinda shilingi milioni Moja na tiketi ya kwenda nchini Uingereza kushuhudia mechi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.

  “Kweli mimi kama mtu mwingine yeyote wa kawaida iliniwia vigumu kuamini kwamba nimeibuka mshindi wa pesa hizo na tiketi. Na imenichukua muda kuamini mpaka sasa baada ya kukabidhiwa hizi milioni moja ndo naamini kweli mimi ni mshindi,” alimalizia Bw. Makuzi.

  Aidha washindi wengine wamewaasa wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi katika promosheni hiyo kwani ina manufaa makubwa kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa zima.

  “Kwa kweli mi nawaambia watanzania wenzangu wasidhani hivi vitu ni masihara, watu wanashinda kweli na maisha yao yanabadilika kupitia hizi pesa tunazopewa. Mimi hapa naiwinda hiyo milioni 50 kwani nina uhakika nikishinda nitakuwa nimesahau kabisa umasikini,” alisema Ramadhani Wefa ambaye ni mshindi wa milioni moja kutoka Kinondoni jijini Dar es salaam.

  Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema bado Airtel inatambua na itaendelea kutambua umuhimu wa wateja wake hivyo haina budi kuhakikisha inatoa huduma bora na zenye manufaa kwa wananchi wote kiujumla.

  “Airtel inaelewa fika kuwa wateja ndio kiini cha maendeleo ya kampuni hiyo na hivyo inajitahidi kuhakikisha inatoa huduma bora za kuwanufaisha wateja wake na kuleta maendeleo kwa taifa zima kiujumla,” alisema Jane.


  0 0

  OTT solutions provider Visual Unity Global is expanding its vuMobile platform into Africa after signing a new partnership agreement with Tanzanian media conglomerate Clouds Media.
  Tomas Petra (l) of Visual Unity with Joseph Kusaga of Clouds Media.
  Designed to rapidly mobilise mobile businesses and empower partners and resellers, the vuMobile platform will be white labelled, allowing subscribers to create mobile optimised websites in a fast and effective way, under the Clouds Media brand.
  In a country where nearly 80% of all internet access is carried out via a mobile phone, this partnership between Visual Unity Global and Clouds Media will bring significant benefits to the local business community. With the vuMobile platform, local companies will now have access to mobile optimised websites offering a highly intuitive and user friendly experience.
  Tomas Petru, CEO of Visual Unity Global, said: “By collaborating with Clouds Media we are helping to rapidly grow our web services for mobile devices in the Tanzanian market. Together with Mobile Money, vuMobile will complement the m-commerce offering of local SMBs.”
  Using vuMobile, businesses in Tanzania will have access to the latest website building technologies such as HTML 5/CSS 3 and Responsive Design. Moreover, the platform also enables an m-commerce presence, robust media streaming capabilities and QR codes.
  Joseph Kusaga, Managing Director at Clouds Media, said: “This partnership with Visual Unity will allow us to bring the most relevant and latest technologies to Tanzania, so that we can better serve our clients.”
  Gabriel Dusil, Chief Marketing and Corporate Strategy officer at Visual Unity Global, adds: “In Tanzania, as in many parts of Africa, a company’s mobile presence plays a critical role in establishing new revenue streams. vuMobile™ helps businesses to generate new subscribers, retain existing customers, and stand out from competitors.”

older | 1 | .... | 218 | 219 | (Page 220) | 221 | 222 | .... | 1897 | newer