Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 215 | 216 | (Page 217) | 218 | 219 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa wa Mambo ya Nje wa Japan, Norio Mitsuya (kulia kwake) aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 01, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR 

  0 0

  Hey guys. At Miss World, contestants usually need as much support as they can get. I would therefore like to ask for your help in spreading the word to your fellow fans, friends, family, acquaintances etc. about the representative for Tanzania this year;

  Happiness Watimanywa.

  People around the world can help me make an even bigger impact through social media and I would like you to be informed of my journey from as early as now.

  Please follow: @misstanzania2013 on Instagram @misstz2013 on twitter
  And Like Miss World-Tanzania on Facebook Thanks for the support. Happy

  0 0

   Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwapungia Viongozi mbalimbali wa chama,Serikali,na viongozi wa dini na watu mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kumpokea mara baada kuwasili jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe  tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo. 
   Pichani Kati ni Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe jioni ya leo. 
  Pichani kati Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi wa ngaji za juu wa chama hicho,kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana,Makamu Mwenyekiti Taifa,Mh.Phillip Mangulla na shoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh Godfrey Zambi wakiwa kwenye kikao cha wanachana mbalimbali wa chama hicho (hawapo pichani) ndani ya ofisi ya makao makuu jijini Mbeya jioni ya leo mara baada ya kuwasili.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akilakiwa na waendesha boda boda kutoka sehemu mbali mbali,alipowasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa Songwe,jijini Mbeya mapema leo wakati alipokwenda kumpokea Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili jioni ya leo kwa ajili ya kuhserehekea maadhimisho ya miaka 37 ya chama cha CCM yatakayofanyika katika uwanja wa Sokoini mkoani humo.
   Katibu wa Uchumi na Fedha Bi.Zakia Meghji akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum na Mbunge wa jimbo la Rungwe Mashariki,Mh.Prof.Mark Mwandosya walipokutana jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa songwe walipokuwa wakimsubiri Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili leo jioni tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo. 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kushoto akizungumza jambo kwa msisitizo na Waziri wa uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kyela walipokutana jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Songwe walipokuwa wakimsubiri Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili leo jioni tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo. 

  0 0


  Kanal Mstaafu Iddi Kipingu akizungumza wakati wa mkutano wa mabondia,mapromota na wadau mbalimbali wa ngumi za kulipwa nchini kushoto ni promota Mohamed Bawazir na kulia ni Ofisa Michezo kutoka Baraza la michezo la Taifa BMT, Richard Maganga  picha nawww.suprdboxingcoach.blogspot.com

  WADAU WA MCHEZO WA NGUMI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MGENI RASMI kANALI MSTAAFU IDDI KIPINGU  BAADA YA KUMALIZA MKUTANO HUO PICHA NA WWW.SUPERDBOXINGCOACH.BLOGSPOT.COM.
  Baadhi ya viongozi wakiwa meza kuu anae ongea ni Yasin Abdallah  kushoto ni Habibu Kinyogoli anaefati ni mwakilishi wa BMT  Richard Mganga Rais wa IBF Afrika Onesmo Ngoi na Lucas Retwainura.

  Mdau wa mchezo wa ngumi ambaye pia ni Promota wa mchezo huo Mohamed Bawazir akizungumza wakati wa mkutano huo wa wadau wa masumbwi,mapromoto na mabondia.

  WADAU WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA MASUMBWI

  Baadhi ya Mabondia wakifatilia mkutano huo wa kwanza baada ya miaka 15

  Kocha Mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli akitoa moja ya mada zilizotakiwa kuongelewa kuhusiana na mchezo wa ngumi nchini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Rais wa IBF Africa Onesmo Ngowi katikati akiwa na bondia FRansic Cheka na Promota Lucas Rwetainurwa wakati wa mkutano huo wa kujadili mambo mbalimbali yanayousu mchezo wa ngumi

  Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akifatilia kwa makini mkutano wa Mabondia,mapromota na wadau mbalimbali wa mchezo wa masumbwi kulia ni bondia Sadiki Momba na Fabian Limo na mdau Maga kutoka Tegeta

  Bondia Fransic Cheka akifatilia mkutano huo uliokuwa umewakutanisha makocha mabondia mapromota na wadau mbalimbali wa mchezo wa masumbwi nchini

  0 0

   Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa akizungumza na wananchi wa Sirari wa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua vituo vya forodha na kungea na watumishi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika mikoa ya kanda ya Ziwa.

   Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa akizungumza na wananchi wa Sirari wa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua vituo vya forodha na kungea na watumishi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika mikoa ya kanda ya Ziwa.

   Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa akizungumza na wananchi wa Sirari wa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua vituo vya forodha na kungea na watumishi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika mikoa ya kanda ya Ziwa.

   Mkuu wa wilaya ya Tarime Luteni Kanali John Henjewele akimwonesha Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (aliyevaa barghashia) na msafara wake maeneo ya mpaka wa Tanzania na Kenya katika mpaka wa Sirari. 
   Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akikagua jengo la kituo cha pamoja cha huduma za forodha cha Sirari (OSBP) ambapo amemwagiza mkuu wa wilaya ya Tarime Luteni Kanali John Henjewele na timu yake wafanyiwe tathmini ya haraka na ya kina ndani ya wiki moja kwani jingo hilo limejengwa chini ya kiwango na linanyufa nyingi hata kabla halijaanza kutumika kitu ambacho Serikali imekataa kulipokea hadi tathmini ifanyike na kupewa ushauri kulipokea au kutolipokea.

   Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akikagua jengo la kituo cha pamoja cha huduma za forodha cha Sirari (OSBP) ambapo amemwagiza mkuu wa wilaya ya Tarime Luteni Kanali John Henjewele na timu yake wafanyiwe tathmini ya haraka na ya kina ndani ya wiki moja kwani jingo hilo limejengwa chini ya kiwango na linanyufa nyingi hata kabla halijaanza kutumika kitu ambacho Serikali imekataa kulipokea hadi tathmini ifanyike na kupewa ushauri kulipokea au kutolipokea.

  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akikagua jengo la kituo cha pamoja cha huduma za forodha cha Sirari (OSBP) na kujionea ufa mojawapo ndani ya jingo la kituo hicho.(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Mara).


   . Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima akiwasili katika uwanja wa ndege mkoani Mwanza akitokea mkoa wa Kagera kuendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua vituo vya forodha na kungea na watumishi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika mikoa ya kanda ya Ziwa. Kulia ni Meneja wa TRA mkoa wa Mwanza Jeremia Lusana. 

   Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima (wa pili kutoka kushoto) akiongea na viongozi wa TRA mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege jijini Mwanza. Wa kwaza ni Meneja wa TRA mkoa wa Mwanza Jeremia Lusana.  

   Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima akisalimiana na Naibu Kamishna Uhamiaji Deogratius Magoma mara baaada ya kuwasili kituo cha Sirari wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua vituo vya forodha na kungea na watumishi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika mikoa ya kanda ya Ziwa.
   Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Mara Joseph Kalinga akiteta jambo na Meneja wa Forodha mkoa wa Mara Ben Usaje wakati wa mazugumzo na Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima alipotembelea kituo cha forodha cha Sirari.

   Naibu Kamishna Uhamiaji Deogratius Magoma (wa kwanza kulia) akimsikiliza Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na   Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima alipotembelea kituo cha forodha cha Sirari. Wa pili kutoka kushoto ni Mrakimu Mwandamizi wa Polisi OCD Sirari SSP Omari Nassri.

   Naibu Kamishna Uhamiaji Deogratius Magoma (wa kwanza kulia) akimsikiliza Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na   Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima alipotembelea kituo cha forodha cha Sirari. Wa pili kutoka kushoto ni Mrakimu Mwandamizi wa Polisi OCD Sirari SSP Omari Nassri.

   Naibu Kamishna Uhamiaji Deogratius Magoma (wa kwanza kulia) akimsikiliza Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na   Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima alipotembelea kituo cha forodha cha Sirari. Wa pili kutoka kushoto ni Mrakimu Mwandamizi wa Polisi OCD Sirari SSP Omari Nassri.

   Naibu Kamishna Uhamiaji Deogratius Magoma (wa kwanza kulia) akimsikiliza Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na   Naibu wa Waziri wa Fedha Adam Malima alipotembelea kituo cha forodha cha Sirari. Wa pili kutoka kushoto ni Mrakimu Mwandamizi wa Polisi OCD Sirari SSP Omari Nassri.

  0 0

   Mshindi wa promosheni ya WEKA UPEWE  ya NBC Limited Bw. Abib Gervas Ndendya (kushoto) akipokea funguo ya bodaboda kutoka kwa Meneja wa tawi la NBC Njombe bi Dorah Godfrey Lewis (kulia) baada ya kuibuka mshindi katika promosheni hiyo hivi karibuni na baadhi ya wafanyakazi wa tawi hilo wakishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Njombe. Droo kubwa ya promosheni hiyo itafanyika wiki ijayo. 
    Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera Mheshimiwa Elizabeth Batenga akiwa na wafanyakazi wa NBC tawi la Bukoba Bw. Emmanuel Minja (wa pili kulia) na Bw. Jackson Kajuna (kulia) alipokabidhiwa zawadi yake ya bodaboda baada ya kuibuka mshindi katika promosheni ya WEKA UPEWE ambayo droo yake kubwa inatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

  0 0

   
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete  akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi (hawapo pichani),walioshirikia matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo.Rais Kikwete ambaye ndiye mgeni rasmi wa sherehe hizo atahutubia leo  mchana kwenye maadhimisho ya sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Sokoine mkoani humo.
  Rais Kikwete akiongoza  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto akiwa sambamba na baadhi ya watoto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo. 
   Baadhi ya vijana wakereketwa na chama cha CCM wakiwa na mabango yao. 
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete  (pilia kulia) akiwa tayari kuongoza wanachana na Wananchi (hawapo pichani) kushiriki matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Bwa.Phillip Mangula,wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji pamoja na Waziri Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum,Prof Mark Mwandosya wakiwa tayai kuyaanza matembezi hayo.
   Rais Kikwete akizungumza na baadhi ya watoto waliokuwa miongoni mwa watoto waliojitokeza kushiriki  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
   Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakishiriki kuchukua matukio yaliyokuwa yakijiri kwenye matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akipokelewa na viongozi wa chama hicho ngazi za juu,pichani akisalimiana na  Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana na anaeshuhudia pichani kati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Mh.Phillip Mangula,tayari kwa kuongoza matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
   Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifurahi jambo na Waziri Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum,Prof Mark Mwandosya 
   Ndugu Kinana akizunguza jambo na Mwigulu Nchemba kabla ya kuanza matembezi ya mshikamano. 
    Msafara wa Rais ukiwasili sehemu ya kuanza matembezi ya mshikamano. 
   Mambo ya matembezi ya mshikamani yakiwa yameiva
   Rais Kikwete pia aliungana na Watoto katika matembezi hayo. 
   Mwenyekiti wa CCM,Rais Kikwete akiwasili kwenye bustani za uwanja wa Sokoine kufikia kilele cha matembezi ya mshikamano
   Sehemu ya Wananchi na wakereketwa wanachama mbalimbali wa wa CC Mwakiwa wamekusanyika kwa pamoja tayari kumsikiliza Rais Kikwete mara baada ya kumaliza matembezi hayo yalifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
   Baada ya kumaliza matembezi ya mshikamano viongozi wa juu wa CCM,wakisiliza utaratibu wa kuadhimisha sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

  Rais Kikwete akizungumza machache mara baada ya kumaliza matembezi ya mshikamano,Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo zitakazoanza mapema leo mchana ndani ya uwanja wa Sokoine,jijin Mbeya.

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimchagua kwa siri mgombea wa Jimbo la Kiembesamaki, katika uchaguzi mdogo wa Mwakilishi wa Jimbo hilo, uliofanyika leo mjini Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitumbukiza kura yake ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, wakati wa uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo, uliofanyika leo asubuhi mjini Zanzibar. . Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Kituo chake cha kupigia Kura, kwa ajili ya kushiriki kupiga kura ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki katika uchaguzi mdogo, uliofanyika leo mjini Zanzibar leo asubuhi. Kushoto ni Mgombea wa Jimbo hilo, Mahmoud Thabit Kombo. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita 


  Baadhi ya Wananchi wakisoma ubao wa matangazo kutafuta eneo walilopangiwa kupigia kura ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, wakati wa zoezi hilo lililofanyika leo asubuhi mjini Zanzibar. Picha na OMR 

  0 0


  JUMA LESSO
  KOCHA wa timu ya ngumi  Mkoa wa Kigoma Juma Lesso, amesema timu yake ya mkoa imekuja kamili kwa ajili ya mashindano ya wazi yatakayofanyika Feb 5,
  katika viwanja vya Tanganyika Pekazi vilivyopo kawe jijini Dar es salaam

  Ni mara ya kwanza kwa timu ya Mkoa wa Kigoma kushiriki mashindano makubwa kama haya timu hiyo ambayo imeweka kambi yake maeneo ya kawe kabla ya hapo ilikuwa maeneo ya mabibo na sasa kawe kwani mashindano hayo yalikuwa yafanyike Feb mosi mwaka huu na sasa ni feb 5

  Lakini tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  Kanali Mstaafu Issa Machibya kuakikisha tunashiriki katika mashindano haya kwa mara ya kwanza  timu hiyo ambayo imekuja na wachezaji kumi kati ya hawo wanawake watatu na wanaume saba ambao wakekuja kuwakilisha mkoa wa Kigoma tutahakikisha kuwa tunachukuwa ubingwa huo ambao upo wazi

  Lesso ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo huo ambapo amepitia kozi ya kimataifa ya mchezo huo Lesso aliwataja baadhi ya mabondia aliokuja nao kuwa ni Agnes Mushi, Ezira Josefu,Rashidi na Habasi na wengine ambao walikuwa katika kambi ya mkoa huu  wa Kigoma .

  Ambapo tumepewa sapoti kubwa sana na mkuu wa mkoa hivyo tutaakikisha atumwangushi na tunarudi na ubigwa kigoma kwani tumejipanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya juu kabisa kwani sasa ngumi Dar es salaam akuna tunahamishia mkoa wa kigoma ambapo amasa inaendelea hivyo tunawaomba wana Kigoma wote waliopo Dar watupe sapoti ili mambo yawe safi na mchezo wa ngumi uendelee kuwa juu

  0 0

  Mkuu wa kituo cha Kulelea watoto yatima cha Msimbazi Centre Sister. Ehienne(kushoto),akipokea moja ya msaada wa katoni ya pambazi kwaajili ya matumizi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho toka kwa Mkurugenzi Mtendeji wa Benki ya Biashara ya NBC Tanzania,Bi.Mizinga Melu(katikati) Mkurugenzi huyo alikabidhi vitu mbalimbali kama vile mchele ,mafuta na mashine ya kusagia juisi baada ya kuguswa kama mzazi na maisha ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho,kulia ni Katibu Mhitasi wa benki hiyo Jolanda Songoro.
  Mkuu wa kituo cha Kulelea watoto yatima cha Msimbazi Centre Sister. Ehienne(kushoto),akipokea kifaa cha kusagia bidhaa za chakula kwaajili ya matumizi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho toka kwa Mkurugenzi Mtendeji wa Benki ya Biashara ya NBC Tanzania,Bi.Mizinga Melu(katikati) Mkurugenzi huyo alikabidhi vitu mbalimbali kama vile mchele ,mafuta na mashine ya kusagia juisi baada ya kuguswa kama mzazi na maisha ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho,kulia ni Katibu Mhitasi wa benki hiyo Jolanda Songoro.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya biashara ya NBC Tanzania,Bi.Mizinga Melu akiongea na watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Msimbazi Centre jijiini Dar es Salaam, wakati alipofika kituoni hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na mashine ya kusagia juisi, alipoguswa kama mzazi na maisha ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho.
  Mkurugenzi Mtendeji wa benki ya Biashara ya NBC Tanzania,Bi. Mizinga Melu(kulia)akimuongelesha jambo mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam,alipotembelea kituo hicho kama mzazi aliyeguswa na maisha ya watoto hao na kutoa msaada wa vitu mbalimbali,Kushoto ni Katibu Mhitasi wa benki hiyo Jolanda Songoro. 

  0 0

   Kamishna Msaidizi wa Madini -Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Fredy Mahobe kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifafanua namna  ya kuendesha uchimbaji salama wa madini kwa wachimbaji wadogo mara walipotembelea mgodi wa Minerals Access System Tanzania (MAST). Ziara hiyo ni moja ya mafunzo ya vitendo kwa wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo yanayoendelea Tunduru mkoani Ruvuma.

   Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Julius Sarota akielezea jinsi madini ya shaba yanavyoweza kutambuliwa kupitia kipande cha mwamba alichokishika.

   Mmoja wa wachimbaji wadogo ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza swali kwa mwezeshaji Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Julius Sarota (hayupo pichani)

   Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi (aliyevaa shati jeupe) akiwaelezea wachimbaji wadogo namna uchorongaji wa miamba unavyofanyika mara wachimbaji wao walipotembelea mgodi wa Minerals Access System Tanzania (MAST) uliopo Tunduru, Ruvuma.

   Mtaalam wa kampuni ya MAST akionesha namna ya kuchoronga miamba kwa wachimbaji wadogo ( hawapo pichani). 
   Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Jones Mushi akionesha jinsi  uunganishaji wa mlipuko wa baruti unavyofanyika kwa wachimbaji wadogo (hawapo pichani) kwenye machimbo ya mgodi wa MAST uliopo Tunduru, Ruvuma.


   Kazi ya uunganishaji wa mlipuko wa baruti ikiendelea katika mafunzo ya wachimbaji wadogo wa madini wa Tunduru. 
   Wachimbaji wadogo wakiangalia shimo mara baada ya kulipuliwa na baruti.

   Mtaalam kutoka kampuni ya MAST Mhandisi Thomas Kato alielezea wachimbaji wadogo jinsi vifaa vya uchimbaji madini vinavyofanya kazi.

   Mhandisi  Heri Issa kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) akionesha moja ya mashine ya kuponda mawe inavyofanya kazi kwenye machimbo ya kampuni ya MAST. 
  Kamishna Msaidizi wa Madini - Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Fredy Mahobe kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifafanua namna bora ya utunzaji wa mazingira kwenye eneo la kutunzia mawetaka kwenye  machimbo ya kampuni ya MAST yaliyopo Tunduru, Ruvuma. 

  0 0

   "Miaka michache tu wanajigamba, wanapiga kelele, lakini pia kwa kipindi hicho kifupi tayari wameanza mifarakano,Wafanye kazi kubwa kutufikia,"alisema Angellah Kairuki ambaye ni  Mjumbe Baraza la Taifa la Umoja wa Wanawake (UWT), Angellah Kairuki.


  Angellah ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, aliyasema hayo wakati akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 37, ya Chama cha Mapinduzi,  zilizoandaliwa na UWT, kata ya Mabwepande, Kinondoni Dar es Salaam.  Alisifu kwamba hadi kufika hapo, ni kutokana na mshikamano wa wanaCCM, na kuwataka kushikamana zaidi ili kurudisha majimbo yaliyopotea katika uchaguzi mkuu uliopita. "Wakati ni sasa,m mkono kwa mkono, nyumba kwa nyumba turudishe majimbo uliyopoteza..changamoto za kiamendeleo zipo, lakini haziwezi kutatuliwa kwa siku moja.  Cheers na Wanachama.

  "Ndio maana Chama kina ilani kwa ajili ya kutekeleza vizuri mikakati ya maendeleo nchini,"aliongeza. Angellah alisema  kwa muda ambao CCM ipo madarakani, imefanya mambo mengi na mfano ni mji huo mpya wa Mabwepande. 

  Alisema kwa muda mfupi mji huo  umepiga hatua kubwa, na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imejipanga kikamilifu kutekeleza miradi ambayo mingine imeshaanza, ikiwa ni pamoja na mabweni ya wasichana yanayojengwa kwa kushirikiana na  serikali ya Korea, barabara, madaraja, na mfumo wa maji safi na taka.

  Aliwataka wajivunie mafanikio chini ya serikali ya CCM na kuyatangaza, na kutowapa nafasi wapinzaniaambao wamekuwa wakipiga kelele bila kuona mafanikio hayo. Aidha, aliwahamasisha kushiriki vizuri katika mchakato wa kupata katiba mpya, hususan  wakati wa kura za maoni, kutetea misimamo ya Chama.

  Aliwaasa kujipanga vizuri kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kwakuchagua viongozi, wanaokubali kwenye jamii hodari na mchapakazi.

  0 0

   . Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa (kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi za makao makuu ya mkoa wa Mara.

   Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akiongea na wa wafanyabiashara wa mkoa wa Mara juu ya umuhimu wa utumiaji wa mashine za kodi za kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara hao kukusanya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ili Serikali iweze kutoa mahitaji ya kijamii na uchumi kwa wakati
   Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Patrick Kasera akifafanua kwa wafanyabiashara wa mkoani Mara juu ya mashine za EFDs na kusema kuwa mashine hizo kazi yake kuu ni kutunza kumbukumbu za biashara hasa manunuzi na uuzaji na sio mfumo wa kodi kama ilivyopokelewa mwanzoni na wafanyabiashara nchini.

   Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) alipokuwa alipozungumza na wafanyabiashara hao jana mjini Musoma katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo.

   Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) alipokuwa alipozungumza na wafanyabiashara hao jana mjini Musoma katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo.

  Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) alipokuwa alipozungumza na wafanyabiashara hao jana mjini Musoma katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akimweleza kwa kina hali ilivyokuwa baada ya kutokea kwa mafuriko Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq. Nyuma katika picha ni sem trela tano zilizokuwa zimepakia vifaa na vyakula.

  Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiq akimshukuru mmoja wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salaam Rumin Shar kutoka kampuni ya Pan Africa Enterprises Ltd baada ya Kampuni yao kutoa magodoro 200 aina ya Comfy kwa ajiri ya ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita eneo la Dakawa mkoani humo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwaacha mamia bila makazi.

  Mkurugenzi wa Home Shopping Centre Gharib Said Mohammed (GSM) kushoto akitembea na Mku wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiq katika daraja lilosababisha watu wa kutoka Dar kwenda Dodoma kusimama kwa muda. 

   Wathilika wa mafuriko wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq

   Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiq akimshukuru mmoja wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salaam Rumin Shar kutoka kampuni ya Pan Africa Enterprises Ltd baada ya Kampuni yao kutoa magodoro 200 aina ya Comfy kwa ajiri ya ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita eneo la Dakawa mkoani humo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwaacha mamia bila makazi

  0 0

  Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia Wananchi na Wanachama wakereketwa wa chama hicho,mapema leo jioni kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea kilele cha miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo.
   Sehemu ya Umati wa Watu waliofika kwenye shamrashamra hizo leo.
  Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika jembe na nyundo,ikiwa ni alama ya Mkulima na Mfanyakazi mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo. 

  Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo. 

  Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
  Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete  akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji.
   Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakifuatilia yanayojiri hivi sasa ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya juu ya kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
  Mmoja wasanii Mwimbaji na Mwigizaji wa filamu,ajulikanae kwa jina la kisani kama Dokii akiimba mbele ya umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa CCM waliofika kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama cha CCM,ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya
  Kikundi cha TOT Plus kiongozwa na gwiji wa mipasho hapa nchini,Khadija Kopa wakiimba jukwaani.
  JB akizungumza machace kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutamka kuwa wamejiunga na chama cha CCM.
  Wasanii hao wa Filamu wakifurahia jambo jukwaani.
  Nape na wanachama wengine wakiserebuka kwa raha zao.

  Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana akiwapungia wananchi na wanachama wa CCM,waliofika kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya.
   Nape Nnauye akiwa amembeba mtoto ambaye alionesha umahiri wake mkubwa wa kucheza ngoma ya kiasili.
   Vijana wenye umri wa miaka 37 wakirusha njiwa angani kuashiria amani,utulivu na mshikamano wetu tulionayo.
   Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye sherehe hizo jioni ya leo.
   Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akipiga gitaa kabla ya kumzawadia msanii wa muziki maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awilo.
  Vijana wa Halaiki.

  0 0

   Rais Kikwete akihutubia maelfu ya watu waliofika kwenye sherehe hizo.


  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete leo amevunja ukimya na kuzungumzia suala la mawaziri waliotuhumiwa na wananchi kuwa mizigo wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti katika mikoa kadhaa nchini mwishoni mwa mwaka jana.

  "Najua wapo baadhi ya watanzania, walitaka Mawaziri waliotajwa kuwa ni mizigo wafukuzwe kazi, na kwa vile halikufanyika basi suala hilo limegeuzwa kuwa la malumbano,  ni vyema ieleweke kuwa kuitwa kwa Mawaziri hao na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakuna maana ya kuishia kufukuzwa", alisema, Kikwete leo akihutubia maelfu ya watu katika sherehe za kilele cha miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. 

  Alisema Mawaziri hao waliitwa kwa sababu ya kuwepo matatizo yaliyoonekana yanatakiwa yapatiwe ufumbuzi, matatizo hayo yamezungumzwa na maelekezo kutolewa kuhusu nini cha kufanya.

  "Kamati Kuu ya CCM imetimiza wajibu wake uliobaki ni wa serikali.Kamati Kuu itaendelea kufuatilia na kama hakuna maendeleo ndipo inapoweza kuamua kuomba mamlaka ya uteuzi ichukue hatua zipasazo dhidi ya mhusika.Huko hatujafika" alisema Rais Kikwete.

  Rais Kikwete alimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisema, ziara ambazo amekuwa akifanya ni mfano unaopaswa kuigwa na viongozi wengine hasa wa CCM kwa sababu ndio hasa unaotakiwa.

  Alisema ziara za Kinana zinakijenga Chama na kutoa taswira nzuri ya CCM katika jamii kwani zinahuisha uhai wa CCM kwa kuwa Katibu Mkuu huyo katika ziara hizo huenda hadi kwa wanachama waliopo ngazi za chini.

  "Katibu Mkuu Kinana amekuwa anafanya mambo ambayo baadhi ya watu wanadhani kuwa ni mageni, lakini katika kufanya hayo amekuwa pia akionyesha umahiri na ujasiri mkubwa kwa kwenda  maeneo ambayo ni magumu kufikika" alisema Rais Kikwete na kuongeza;

  "Katika ziara hizo  wakati mwingine amekuwa anatumia njia za usafiri zinazoogopesha, amewahi kutumia meli  ya MV Songea kutoka mkoani Ruvuma hadi Mbeya, amepanda milima na mabonde kwa magari katika maeneo ambayo ni hatari, lakini lengo likiwa ni kuhakikisha anawafikia wanachama wa ngazi za chini kabisa".

  Rais Kikwete alisema mambo mengine yalivyomvutia katika ziara za Kinana, ni hatua ya Katibu mkuu huyo kwenda kukaa na  kula na wananchi katika ngazi za chini na kisha kufanya nao kazi za maendeleo  na zaidi kutoa fursa kwa wananchi kueleza matatizo na manung'uniko yanayowasibu.

  Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alisema Katibu mkuu wa Chama amekuwa anashiriki katika kutafuta majawabu na matatizo anayoambiwa hali ambayo imesaidia sana kumaliza baadhi ya matatizo kulekule mikoani.

  "Pale ambapo pamekuwa panahitaji hatua zaidi za serikali hakusita kutoa taarifa kwa Waziri Mkuu, vile vile amekuwa anatoa taarifa ya ziara zake kwenye Kamati Kuu ya CCM" alisema Rais Kikwete.


  0 0

   Ngalawa zikiwa katika mstari kwa ajili ya kuanza mashindano katika pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza. 
  Meneja mauzo wa  ZANTELTanzania  Salum Ngururu, akikamkabidhi zawadi mshindi wa kwanza katika mashindano ya Ngalawa, Juma Mgeni zawadi yake.

    Sehemu ya umati wa wananchi wakifuatilia michuano ya Ngalawa.

  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), kizindua mashindano ya Ngalawa Wilayani Muheza.

  Mashindano ya Ngalawa yafana Tanga

  Na Mwandishi Wetu, Muheza.


  Mashindano ya ngalawa yaliyofanyika jana Wilayani Muheza katika Kijiji cha Kigombe yamefana huku Kampuni ya simu ya ZANTEL  ikifanikisha kwa kutoa zawadi .


  Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau (CUF), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo amewataka vijana washiriki katika michezo badala ya kukaa vijiweni.


  Kauli hiyo aliitoja wakati  akifungua mashindano ya kwanza ya Ngalawa mkoani Tanga yaliyofanyika kwenye Pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.


   Mwidau alisema kupitia michezo vijana wataweza kupata fursa nyingi ikiwemo elimu na ujunzi kutoka kwa wenzao ,burudani pamoja na kujenga afya za kimwili na kiakili.


   “Mahindano haya ya Ngalawa hapo awali yalikuwa yanafanyika ngazi ya kijiji lakini kupitia kwa wadhamini Kampuni ya simu ya ZANTEL tumeweza kuyafanya kimkoa kwa lengo la kuibua fursa za ajira kwa vijana na kwashirikisha watu katika michezo, ”alisema Mwidau.


   Nae Meneja mauzo wa  ZANTELTanzania  Salum Ngururu,  alisema kuwa lengo la kudhamini mashindano hayo ni kurudisha faida wanayopata kwa jamii kutoka na huduma zake na kuendelea kuwatambulisha bidhaa zinazotolewa na kampuni hiyo.


  Alisema ZANTEL itakuwa ikiboresha zawadi za mashindano hayo kila mwaka ili yaweze kuvuta washiriki wengi. Mshindi wa kwanza alijipatia kitita cha Shilingi laki tatu, kikombe cha ushindi pamoja na medali za dhahabu. Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka ambaye aliweza kujinyakuliwa zawadi hiyo.


  Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya Ngalawa thelathini zilizokuwa na washiriki watano ambapo washiriki walitoka katika Wilaya za Tanga, Pangani na Muheza huku Wilaya ya Mkinga ikishindwa kushiriki kutokana na kushindwa kufanya maandalizi mazuri. 

  0 0
 • 02/02/14--21:34: MBUNGE NAMELOK AGAWA MISAADA
 • DSCF2464Mbunge viti maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine akiwasili katika viwanja vya kituo cha huduma ya walemavu cha kanisa katoliki jimbo kuu Arusha,Monduli jana kwa ajili ya kugawa misaada mbalimbali.
   DSCF2485Mbunge wa Viti maalum Namelok  akimjulia hali mtoto mwenye ulemavu wa utindio wa ubongo kituoni hapo.
  DSCF2533
  Namelok akikabidh msaada huo kwa Mratibu wa kituo cha watoto walemavu Monduli,Bi Mireile Kapilima.
  DSCF2517Katibu wa UWT Mkoa wa Arusha Stamili Dendegu akimuendesha mtoto mwenye ulemavu wa miguu kituoni hapo
  DSCF2515Walemavu wakiwa katika baiskeli zao wakimsikiliza Mbunge Namelok

  Na Pamela Mollel,Monduli.
  Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine ameitaka jamii kujitolea kuwasaidia watoto walemavu wanaolelewa katika kituo cha huduma ya walemavu cha kanisa katoliki jimbo kuu Arusha kwa kuwa wazazi wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu
   
  Alisema hayo jana wilayani Monduli wakati akikabidhi misaada mbalimbali huku akiungwa mkono na wanawake wenzake waliomsindikiza kuwaona watoto wenye ulemavu wa viungo na utindio wa ubongo
   
  Namelok alisema kuwa kuna baadhi ya wazazi ambao hawana uwezo wa kumudu kulipa shilingi 1500 kwa siku hivyo ni vyema jamii ikaguswa kuwasaidia watu wenye uhitaji
   
  “Zipo familia zinatumia zaidi ya  shilingi 1500 kwa siku kila mmoja akijitolea itasaidai kwakuwa kwa mwezi ni shilingi elfu 45000 kwa mtoto mmoja”alisema Namelok
   
  Pia mbunge huyo alitoa shukrani zake kwa Mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa kwa kuweza kutoa eneo hilo  na kujengwa kituo chenye uwezo wa wawahudumia watoto 52.
   
  Misaada aliyokabidhi Mbunge huyo ni pamoja na Blanket 50, shuka,unga,mchele,sabuni,sukari na mafuta
   
  Mratibu wa kituo hicho Mineile Kapilima alisema kituo hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali  ikiwemo ukosefu wa ufadhili wa kudumu hivyo mahitaji  ya kituo kuongezeka siku hadi siku kwa kuwa awali kituo kilikuwa kunauwezo wa kulaza wototo 30 lakini kwa sasa wanafika hadi 52
   
   “ukosefu wa chakula,matibabu,nguo,hatuna ufadhili wa kudumu kwa kuwa wazazi wengi hawana hawana uwezo”alisema  Kapilima

  0 0

  DSC_0133

  Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakibeba mwili wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Kinondoni kwa ajili ya ibada maalum.
  DSC_0140
  DSC_0143
  Marafiki wa karibu wa familia ya marehemu wakiwa wamesimama kuupoke mwili wa marehemu Meja Mstaafu Isaac Chekingo ulipowasili nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa Juma.
  DSC_0047
  Mtoto mkubwa wa marehemu (mwenye koti la suti jeusi) akijadiliana jambo na baadhi ya wanakamati wa msiba ulioongozwa na Afande Thomas Ndonde wa JWTZ.
  DSC_0041
  Baadhi ya waombolezaji wakitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo.
  DSC_0190
  Baadhi ya watoto wa marehemu na wake zao wakiwa kwenye majonzi mazito.
  DSC_0069
  Mtoto mkubwa wa marehemu Samson Samwel Chekingo (mwenye miwani) akijadiliana jambo na wadogo zake kabla kuanza kwa misa ya kumwombea marehemu baba yao.


  DSC_0228
  Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.
  DSC_0245
  Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha (katikati) akiwa amejumuika na baadhi ya waombolezaji kwenye msiba wa Marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
  DSC_0086
  Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamefurika nyumbani kwa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
  DSC_0263
  Mchungaji Charles Mzinga kutoka Kanisa la Usharika wa Azania Front akiendesha ibada ya misa ya kumwombea marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa juma.
  DSC_0291
  Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha akijumuika na waombolezaji wengine kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
  DSC_0388
  Waombolezaji wakiendelea kutoa heshima za mwisho.
  DSC_0452
  Pichani juu na chini ni watoto wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo wakitoa heshima za mwisho kabla ya kuelekea makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya mazishi.
  DSC_0457
  DSC_0463
  Vilio na simanzi vilitawala.
  DSC_0485
  Mke wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa mpendwa mume wake.
  DSC_0568
  Pichani juu na chini Familia ya marehemu ikiwa katika makaburi ya Kinondoni tayari kuanza shughuli za mazishi.
  Kwa picha zaidi ingia humu
  DSC_0572
  WASIFU WA MAREHEMU MEJA SAMUEL ISAAC CHEKINGO.
  Marehemu alizaliwa tarehe 06.06.1953, alizaliwa Ng’ang’ange, Dabaga na alikulia Mufindi kibaoni – Mgelukwa.
  Alisoma shule ya msingi Mufindi na shule ya sekondari Kigonsela.
  Baada ya hapo alijiunga na Jeshi la Ulinzi wa Tanzania, na alihudhuria kozi mbalimbali za kijeshi, zaujuzi na uongozi. Pia kozi na kozi ya taaluma ya urubani nchini Canada.
  Marehemu alitunukiwa medali mbalimbali za kijeshi zikiwemo:-
  a) Medali za Ushindi.
  b) MedaliVita ya Kagera.
  c) Medali ya Miaka Miaka Ishirini ya Utumishi.
  d) Utumishi wa Muda Mrefu.
  Marehemu alishikizwa (Seconded) kwenye wakala wa ndege za serikali hadi alipo staafu jeshi akiwa na cheo cha Meja December mwaka 2000.
  Marehemu akiwa Rubani wa ndege alipata nafasi ya kuwarusha viongozi mashuhuri kama:-
  i) Marehemu Mwal. Julius K. Nyerere.
  ii) Marehemu Nelson Mandela.
  iii) Marehemu Pope John Paul II.
  iv) Raisi Mstaafu Alhaji Alhasan Mwinyi
  v) Raisi Mstaafu Benjamin W. Mkapa
  Na viongozi wengine wengi wa kitaifa na wakimataifa.
  Marehemu alipata fursa ya kushikizwa katika kampuni ya Williamson Diamond kama Rubani, pia Kahama Mining na baadae alifanya kazi nje ya nchi Darfur, Sudan na DR Congo.
  Marehemu katika siku zake za mwisho alifanya kazi katika shirika la Air Tanzania hadi mauti yalipo mkuta.
  Marehemu alianza kuugua mwanzoni mwa mwezi Januari, 2014 na alitibiwa katika hospitali mbalimbali hadi mauti yalipo mkuta tarehe January 28 ya mwaka 2014.
  Marehemu ameacha mke na Watoto wa kiume wane na Watoto wa kike wawili.
  SHUKURANI.
  Mahospitali – regency hospital, Madakitari na wauguzi hasa Dr. Alfonsi, Dr. Kisanga, na madakitari wa hospitali ya jeshi Lugalo.
  Uongozi wa ATC
  Uongozi wa Jeshi la wananchi wa Tanzania walioridhia marehem kuzikwa kwa Heshima za kijeshi, maafisa na maaskari walioshiriki katika paredi za Mazishi, ndugu jamaa na marafiki walioshiriki kwa hali na mali kufanikisha katika kumpumzisha baba yetu mpendwa .

older | 1 | .... | 215 | 216 | (Page 217) | 218 | 219 | .... | 1898 | newer