Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 216 | 217 | (Page 218) | 219 | 220 | .... | 1898 | newer

  0 0

  BfT3Y-wCAAAL8iB
  Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) Chief Executive Officer, Mohammed Dewji shares a light moment with the Finland Prime Minister Jyrki Katainen at the Finland Embassy in Dar es Salaam during his three days state visit to Tanzania.

  Mo and Premier Katainen were mentioned as exceptional Young Global Leaders by the World Economic Forum, bold, brave, action-oriented and entrepreneurial.
  The Forum of Young Global Leaders is an integral part of the World Economic Forum and part of the larger New Champions community.

  0 0  0 0

  Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akifungua kikao kwa maombi katika baraza la madiwani lilofanyika mwishoni mwa wiki kushoto ni naibu meya Gervas Ndaki na kulia  Mkurugen Theresia  Mahongo kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa. (picha na Denis Mlowe).
  Juu na chini ni Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiwa katika kikao cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri mwishoni mwa wiki. 
  Habari na picha na Denis Mlowe.

  MIONGONI mwa watu 6003 mkoani hapa waliopima afya zao kwa hiyari katika kipindi cha Oktoba  hadi Disemba mwaka jana, watu 379 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).

  Akizungumza katika kikao cha utekelezaji wa shughuli za ukimwi zilizotekelezwa na Kamati ya Kudhibiti Ukimwi mbele ya baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya pili Oktoba na Disemba mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naibu Meya Gervas Ndaki, alisema kati ya waliojitokeza kupima na kupata ushauri nasaha, wanaume walikuwa 3074 wanawake 2,929.

  Ndaki alisema kati ya watu 379 waliopima kwa hiari na kukutwa na maambukizi,146 ni wanaume na wanawake ni  233. Alisema huduma ya kuzuia maambukizi ya vvu/ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, wajawazito 1,287 walijitokeza na kupata ushauri wa nasaha na kati yao, 84 sawa na asilimia 6.5 walikutwa na maambukizi.

  Ndaki alisema mapambano ya ukimwi yanaambatana  na huduma za tiba sahihi ya magonjwa ya ngono na jumla ya watu 361, wanaume 110 na wanawake 251, walipata tiba sahihi ya magonjwa ya ngono.

  “Maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi yanaendelea kuwepo na tunajitahidi sana kuwahamasisha wananchi kujitambua na kutumia sana kondom na pia tumefanya sana kampeni kwa wananchi wanaotakiwa kwenda tohara kujitokeza kwenda katika hospitali na vituo vya afya vinavyotambulika kutoa huduma ya tohara” alisema Ndaki.

  Aliongoza kuwa huduma ya kitabibu ya tohara kwa wanaume ilitolewa kwa jumla ya wanaume 171 walitahiriwa na kati ya waliopima vvu wanaume 160 na hakuna aliyekutwa na maambukizi.


  Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi aliwataka watendaji kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa kuwasisitiza wananchi kwa kuwapa elimu kuondokana na maambukizi mapya.

  alisema mkoa wa Iringa una nafasi kubwa sana wa kuwa wa mwisho kama kila mmoja atatumia nafasi yake kuelimisha vijana kwa wazee katika mapambano dhidi ya ukimwi.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi inayokarabati na kufanyia marekebisho ukumbi wa bunge mjini Dodoma tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali za majengo ya Bunge jijini Dodoma alikotembea kukagua inayokarabati na kufanyiwa marekebisho tayari tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua sehemu ya kukalia katika Ukumbi wa Bunge  mjini Dodoma alikotembea kukagua maendeleo ya ukarabati na kufanyiwa marekebisho tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Andrew Chale, Zanzibar
  Mgombea wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameibuka Kidedea kwa ushindi alioupata katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo baada ya kukaa wazi kwa muda mrefu kutokana na kutenguliwa kwa aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.

  Masimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki Ndg. Suluhu Rashid , akitangaza matokeo hayo baada ya kumalizika kwa kazi ya uhesabuji wa Kura na kuzijumlisha kura zote zilizopingwa na Wananchi wa Jimbo hilo jana jiioni (Februari 2) kwenye kituo cha Walimu TC Kiembe Samaki.

  Akitangazo matokea hayo ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki  yalioshirikisha Vyama Sita vya Siasa vilivyosimamisha wagombea wake.

  Msimamizi wa Uchaguzi Ndg. Suluhu akitoa matokeo hayo Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameshinda kwa  Kura 1856, sawa na asilimia 75.1 na kutangazwa mshindi wa Uchanguzi huo Mdogo wa jimbo hilo kuchukuwa nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Mansoor Yussuf Himid, aliyevuliwa Uwanachama na CCM na nafasi hiyo kuwa wazi kwa muda hadi kufanyika kwa uchaguzi mdogo leo na kumpata mrithi wa kiti hicho.
  Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mahmoud Thabit Kombo 
  akiongea na wandishi wa habari baada ya kushinda hiyo jana (Februari 2).(Picha kwa hisani ya mtandao wa http://www.zanzinews.com)
  Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mahmoud Thabit Kombo
   akitia sana mara baada ya kushinda hiyo jana (Februari 2). 
  (Picha kwa hisani ya mtandao wa http://www.zanzinews.com)
  Matokeo ya Uchaguzi kweney fomu yaliyototolea na tume ya 
  uchaguzi mdogo.


  WAKATI HUO HUO..!Mgombea wa Chama cha CUF Mhe. Abdulmalik Juma Jecha, amepata kura 445, sawa na asilimia 18.3, Mgombea wa Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid  amepata kura 84, sawa na asilimia 3.5, Chama hichi ni kipya kimeungwa na Viongozi walioondoka CUF, na hii ni mara ya pili kushiriki Uchanguza tangu kuazishwa kilishiriki uchaguzi wa kwanza kisiwani Pemba katika jimbo la Chambani,Pemba.


  Nae Mgombea wa Chama cha  CHADEMA Mhe. Hashim Juma Issa,amepata kura 34 sawa na asilimia 1.5, katika uchaguzi huo mdogo wa jimbo la kiembesamaki.Mgombea wa TADEA Ali Mohammed Ali (Mbongo) amepata kura 6 sawa na asilimia 0.3. Nae Mgombea wa Chama cha SAU Mhe. Ramadhani Simai Mwita amepata kura 1 sawa na asilimia 0.1

  Kwa matokeo hayo Tume ya Uchaguzi Zanzibar imemtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki na anakuwa Mwakilishi halali baada ya ushindi huo.

  Aidha, katika matokeo hayo, mgombea wa CUF, Abdulmalik Juma Jecha aligomea kusaini fomu ya matokeo ambapo aliaga anatoka mara moja na baadae kukimbia bila kurudi kusaini karatasi Kwa upande wa mgombea wa CHADEMA, Hashim Juma Issa hakutokea kabisa kwenye kutangazwa matokeo hayo.

  0 0

   Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Joyce Mwakisyala  (katikati )akipokea maoni ya  Utafiti  kuhusu Tasnia ya Filamu Tanzania kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Wasanii wa Filamu Tanzania (TAFF) Bwana Simon Mwakifwamba wa kwanza kulia, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fissoo 
  Rais wa Shirikikisho la Wasanii wa Filamu Tanzania (TAFF) Bwana Simon Mwakifwamba wa pili kutoka kulia akionyesha maoni ya  Utafiti  kuhusu Tasnia ya Filamu Tanzania wa Kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bi leah 

  0 0

     Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania akiwa na Majaji wenzake wakipokea heshima ya gwaride katika sherehe hizo katka viwanja vya Botanical Ocean road jijini Dar es salaam leo asubuhi.
      Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akiwaongoza Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania katika Maandamano ya kuadhimisha Siku ya Sheria nchini leo asubuhi katika viwanja vipya vya Mahakama vilivyopo Mtaa wa Chimala karibu na Southern Sun Hotel.

     Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika Sherehe za Siku ya Sheria nchini.

        Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Augustine Ramadhan  akiwa pamoja na Viongozi wengine wastaafu wa Mahakama katika sherehe hizo zilizofanyika mapema leo jijini Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla.

       Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman mara alipowasili katika viwanja hivyo kama Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo.   Ukaguzi wa gwaride kuashiria uzinduzi rasmi wa Shughuli za Mahakama kwa mwaka 2014

  0 0

   Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano waliohudhuria kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano kinachoendelea Mkoani Tanga

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano wakati wa Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano unaoendelea mktoani Tanga, ambapo amewataka kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

   Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano wakiwa kimya kwa ajili ya kuwakumbuka baadhi ya wanataaluma ya habari waliotangualia mbele ya haki, wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Leo Mkoani Tanga.
   Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano (hawapo pichani) na kuwataka kuendelea kutumia mitandao ya kijamii katika kuwasiliana na wananchi, wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Leo Mkoani Tanga. kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko

   Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara akiteta jambo na Kaimu Mhariri Mtendaji Mkuu wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel Nderumaki (aliyesimama) wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Leo Mkoani Tanga.Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko na Mwisho ni kulia ni Afisa Mkuu Mawasiliano toka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bw. Peter Millanzi.

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiteta jambo na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara, wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Leo Mkoani Tanga

  Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene na mwisho kushoto ni Afisa Mkuu Mawasiliano toka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bw. Peter Millanzi. Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko akifuatiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari( MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa na mwisho kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bi. Gaudensia Simwanza.PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

  0 0

  Na Ramadhan Ali-Maelezo  ZANZIBAR          03.02.2014
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej amesema  juhudi za Serikali ya  kuwasogezea wananchi  maendeleo  hazitokuwa na tija iwapo wimbi la vijana  wa Zanzibar watatumika  kusafirisha dawa za kulevya na wataendelea kuwa wahanga wa matumizi ya dawa hizo.
  Amesema hatma ya maendeleo ya Taifa itategemea zaidi vijana wenye mwelekeo mzuri wa tabia na waliojiepusha na matumizi ya mihadharati ambayo inahatarisha  afya na akili zao.
  Waziri Fatma Abdulhabib Ferej ameeleza hayo leo Ofisini kwake Migombani alipokuwa akizindua Kamati ya Kitaalamu  ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibi wa dawa za kulevya  yenye wajumbe  kutoka Taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi.
  Amesema kumekuwa na mwamko wa vijana katika kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya kupitia huduma za makaazi za Marekebisho ya tabia (Sober House)  lakini mwamko huo hautakuwa endelevu iwapo harakati za usafirishaji, uingizaji na matumizi ya dawa za kulevya hazitoendelea kupigwa vita.
  “Harakati za uzalishaji, usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya huleta mtikisiko katika mihimili ya dola na zimekuwa zikiandamana na majanga mbali mbali ikiwemo vifo na  kutoweka kwa amani, ”alisema waziri Fatma.
  Amekumbusha kwamba matukio ya miaka ya karibuni ya hapa nchini ya kukamatwa  dawa za kulevya katika viwanja vya ndege unatoa changamoto ya kubuni mikakati imara zaidi  na endelevu ya kukabiliana kikamilifu na tatizo hilo.
  Kutokana na hali hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amesisitiza Kamati ya Kitaalamu kwamba dhima ya kuratibu na kusimamia mapambano dhidi ya dawa za kulevya kuanzia sasa imo mikoni mwao na ameitaka kutekeleza jukumu hilo kikamilifu ili kufikia  kauli mbiu ya “Zanzibar bila ya dawa za kulevya inawezekana”.
  Waziri Fatma Abdulhabib Ferej ameihakikishia Kamati hiyo kwamba Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais itakuwa pamoja nao kwa  kuwapatia msukumo na kila msaada katika kukamilisha jukumu linalowakabili.  
  Mapema akimkaribisha Waziri Fatma kuzindua Kamati hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais Omar Dadi Shajak alimueleza kwamba  wajumbe wake wote ni watu mahiri wenye uelewa mzuri wa madawa ya kulvya.
  Ameeleza matumaini yake kwamba katika kipindi kifupi kijacho kupitia Kamati hiyo Zanzibar inaweza kuona mwanga wa mafanikio.
  Kuundwa kwa Kamati ya Kitaalamu ya Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za kulevya inatokana na mabadiliko ya Sheria ya udhibiti wa wa dawa za kulevya No. 12 ya mwaka 2011 ambapo moja kati ya jukumu lake ni kuishauri Tume katika suala la udhibiti wa matumizi na usafirisha wa dawa za kulveya nchini.
  Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti  wake Kheriyangu Mussa Khamis inawajumbe 11 kutoka Kitengo  cha kuzuia dawa za kulevya cha Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Idara ya Forodha, Mkurugenzi wa Tiba, Sekta binafsi zinazoshughulikia mapambano dhidi ya dawa za kulevya  na wajumbe wawili kutoka  taasisi za dini.
                                        MWISHO
  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR  0 0

   Amour Haji wa timu ya Mtende (kushoto) akijarbu kumtoka Yussuf Mfaume wa Jamhuri jana kwenye uwanja wa Amaan. Mtende Rangers lishinda bao 1 - 0.Mtende Rangers ya Zanzibar, jana iliisambaratisha timu ya Jamhuri kutoka Pemba bao 1 - 0 kwenye uwanja wa Amaan mjini Zanzibar mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Grand malt ya zanzibar. Picha zote na Martin Kabemba.
   Bakari Khamis wa Jamhuri (kushoto) akiwania mpira na Abeid Salumu wa Mtende Rangers. Matokeo Mtende 1 Jamhuri 0
    Mlinzi wa Mtende Rangers, Fauzi Ali akijiandaa kupiga mpira mbele ya Ramadhan Hassan wa Jamhuri (kulia). Mtende 1 jamhuri 0.

  0 0


  Afisa utetezi wa haki za kiuchumi wa OXFAM Mkamiti Mgawe akielezea kwa kina namna ambavyo wanafanya mchujo  wa kumpata mshiriki wa awali wa mama shujaa wa chakula/ Maisha Plus ambapo washiriki wanatarajia kuingia katika kijiji cha Maisha Plus  mwezi wa tatu mwaka huu 2014.
   Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) Akitoa ufafanuzi namna ya mchujo unavyo fanyika ili kuwapata vijana na akina mama watakao ingia katika Maisha Plus/Mama shujaa wa Chakula, Wakati wa kufanya zoezi la kuwachagua wale watakaoingia katika kijiji cha Maisha Plus 2013/2014.

   Majaji wakuu walioteuliwa kwa ajili ya kufanya mchujo wa kuchagua Mama Shujaa wa Chakula 30 na vijana 45 ambao baadae watafanyiwa usahili na kubakiza wanawake 20 pamoja na vijana 30 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
   Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) aliyevaa kofia akipitia kwa umakini Fomu za mchujo za Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus.
  Wanafunzi 17 ambao wana fani mbalimbali na waliojitolea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo kikuu cha Tumaini ambao wanawasaidia majaji kupitia fomu za mchujo ili kuwapata wale watakaofanikiwa kuingia katika Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.   Baadhi ya wanachuo wakiwa wanaendelea kupitia Fomu kwa umakini kuhakikisha wanawatendea haki washiriki wote walioleta Fomu zao.

   Mmoja wa wanachuo akifanya maheesabu kwa makini ili kutoa alama kwa washiriki walioleta fomu kwa ajili ya mchujo ya kuwapata watakaoingia katika usahili wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula
  Baadhi ya Fomu zikiwa zimemalizika kupitiwa na wanafunzi wa Chuo kikuu ili kupelekwa kwa Majaji wakuu.

  ************
   

  SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA/ MAISHA PLUS
  • Fomu zaidi ya 4,000 za Mama Shujaa Maisha Plus zakusanywa
  • Majaji 9 kusimamia zoezi la kuchaguwa wakulima wanawake 20 na vijana 45
   Zoezi la kuchaguwa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus limeanza leo  ambapo zaidi ya fomu 4,000 zimekusanywa kutoka kwa washiriki. 

  Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akiongea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo alisema zoezi la kupitia fomu litachukuwa siku nne kuanzia Jumatatu tarehe 3 hadi Alhamisi tarehe 6 Februari 2014. “Majaji walioteuliwa wana kazi kubwa ya kupitia zaidi ya fomu 4,000 ambazo tumekishwazipokea na nyingine bado zinawasili kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu. Baada ya uchambuzi majaji watachaguwa wakulima wanawake 20 pamoja na vijana 45 ambao watashiriki kwenye shindano la mwaka huu. Majaji watasaidia kuchambuwa fomu na vijana 17 waliojitolea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Jinsia. “

  Jopo la majaji linajumuisha waliobobea kwenye masuala yanayohusu kilimo, ufugaji, usalama wa chakula, sera na utetezi, uchumi, biashara, vyombo vya habari, vijana na maendeleo ya jamii. 

   Majaji ni kama wafuatavyo:
  Rose Tesha Meneja Programu ya Maisha Salama shirika la VSO; Masoud Kipanya mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus; Tatu Abdi Juma mshindi wa tatu shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 ;Francis Bonda Mkurugenzi wa kampuni ya DMB na mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus, Edmund Matotay Mtafiti kutoka shirika la Oxfam; Anna Oloshoromshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula mwaka 2011; Carolyn Kandusi mtaalamu wa jinsia kutoka shirika la PINGOS akitokea Loliondo; Zephaniah Mugittu mshauri wa mnyororo wa thamani wa mboga mboga anafanya kazi na shirika la Oxfam akitokea Lushoto, Tanga pamoja na Bernick Kimiro mshindi wa Maisha Plus 2012. 
  Washiriki  wa Maisha Plus msimu huu ni vijana wa miaka 21-26 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda wanaogombania kitita cha Fedha za kitanzania Milioni 25.


  0 0


  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipokeaa misaada ya vitu mbalimbali kwa ajili ya Waathirika wa Mafuriko Mkoani Morogogoro  yakiwemo Mabati 10,000 ,Mashuka 200, Vyandarua 200, Magodoro 50 na Biskuti Katoni 50 Kutoka kwa Makampuni matatu na Taasisi na Jumuiya mbili za dini . Vyote vikiwa na dhamani ya Shilingi milioni 141,045,000 .Akikabidhi kwa niaba ni Mwanyekiti wa Kampuni ya M.M. Intergrated Steel Mills Subhash Patel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

   
   Wakili  wa Serekali Mfawidhi mkoa wa Dodoma, Angaza Mwaipopo akifafanua jambo wakati wa sherehe ya siku ya sheria mjini Dodoma leo.
  Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Dodoma, Crecensia Makuru akizangumza jambo mbele ya watendaji na wadau wa mahakama wakati sherehe za siku ya Sheria zilizofanyika leo.
   Wakili wa kujitegemea Mary Munissi wa mkoani Dodoma akielezea jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika leo
   Mahakimu, Mawakili na watendaji wengine wa mahakama wakifuatila jambo walipokuwa kwenye maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika leo Dodoma.
   Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dodoma akizungumza jambo na Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Singida, Mh. Pasiseko Konne mara baada ya kumalizika shughuli za maadhimisho ya siku ya sheria leo.


  Na John Banda, Dodoma
  UCHELEWESHWAJI wa kesi nyingi mahakamani katika mahakama ya kanda ya Dodoma kunasababishwa na upungufu mkubwa wa majaji.
  Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Crecencia Makuru leo mjini humo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama kuu.
  Alisema kuna upungufu mkubwa wa majaji ambao haulingani na kesi zilizopo hali inayosabisha kuzolotatesha mienendo ya kesi mbalimbali.

  Crecencia alisema majaji katika kanda ya Dodoma ni wachache kulingana na kesi zilizopo  ambapo hadi kufikia Desemba 31, 2013 kulikuwa na jumla ya mashauri na 1364 na kuna majaji wawili tu.

  Alisema ''idadi ya kesi ni kubwa mno kwa majaji wawili hii inachangia kwa kiwango kikubwa kesi kutosikilizwa na kutolewa maamuzi kwa wakati, upo umuhimu wa kuongeza majaji ili kuwe na uwiano wa masharti yaliyopo'',

  Aidha alisema Mahakimu ni wachache huku mahakama nyingi za wilaya zina hakimu mmoja mmoja licha  ya kuwa na mashauri mengi na tatizo linakuwa kubwa pindi mahakimu hao wanapougua, kuuguliwa au kwenda likizo.

  Aliongeza kuwa mahakama nyingi za mwanzo hazina mahakimu wa kudumu, mahakama hizo hutembelewa na mahakimu kutoka vituo vingine hali ambayo husababisha ucheleweshaji wa haki kwani mahakimu hulazimika kusafiri umbali mrefu na wakati mwingine miundombinu huwa ni mibovu..

  Jaji  huyo alibainisha kuwa sasa posho za washauri wa mahakama zimeboreshwa kutoka Sh.1,500 hadi kufikia 5,000 kwa kila shauri litakalohitimishwa. Alisema licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama  kuna mikakati ya kutatua changamoto hizo ikiwemo kuondoa mashauri, kesi zote zenye umri zaidi ya miaka miwili, kuboresha takwimu za mashauri, kesi zilizopo mahakamani, kuboresha na kusimamia masjala pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara.


  0 0

   Katibu Mkuuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mama Mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, Consolata Mgovano, alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mgimwa, Kijiji cha Magunga, jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, leo jioni. Wengine ni watoto wa marehemu Mgimwa, Stanisla Mgimwa, na Rozalina Mgimwa.
   Kinana akizungumza na familia huyo ya marehemu Mgimwa. Wapili kushoto ni Johakim Mgimwa
   Kinana akimuaga Mama Mgimwa baada ya mazungumzo
   Kinana akiaga
   Mmoja wa wanafamilia akilia Kinana alipotembelea familia hiyo ya Mgimwa
   Nyumbani kwa marehemu Mgimwa
  Kinana akipokea saluti ya Kijana wa CCM, alipowasili Ifunda, Iringa Vijijini kabla ya safari ya kwenda nyumbani kwa marehemu Mgimwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msavatavangu: Picha na theNkoromo Blog

  0 0
 • 02/03/14--10:59: kaaazi kweli kweli


 • 0 0


   Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya TBL, Doris Malulu,

  Alisema ili miradi iwe endelevu na imnufaishe mwananchi aliyekusudiwa ni vema suala la uangalizi likawa shirikishi kwa kila mtu ambapo itakuwa misaada kwa vizazi vijavyo na kwamba kampuni hiyo imelenga kituo cha Afya kwa kuwa ndiyo kimbilio la Watu wengi.


  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mdogo wa Tunduma, na pia ni mkaguzi wa ndani  Helen Kagamizi, aliishukuru Kampuni ya Tbl kwa msaada wa kisima cha maji katika Kituo cha Afya kwa kile alichosema Mji wa Tunduma unatatizo kubwa la uhaba wa maji.
  KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) imezitaka Halmashauri mbali mbali nchini ambako miradi mingi ya kijamii inatekelezwa kutokana na misaada ya Wahisani kutoa uangalizi ili iwe endelevu kwa manufaa ya wananchi ambao ndiyo walengwa.

  Ombi hilo limetolewa na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya TBL, Doris Malulu,wakati akikagua mradi wa uchimbaji wa Kisima cha Maji  uliofadhiliwa na Kampuni hiyo katika kituo cha Afya cha Tunduma kilichopo Wilayani Momba Mkoa wa Mbeya.

  Doris alisema maeneo mengi wanapeleka miradi ambayo Serikali ilitakiwa kuifanya ambapo baada ya kufanikisha miradi hiyo na walifadhili kuondoka miradi hiyo hufa kutokana na kukosekana kwa uangalizi toka Serikalini.

  Alisema ili miradi iwe endelevu na imnufaishe mwananchi aliyekusudiwa ni vema suala la uangalizi likawa shirikishi kwa kila mtu ambapo itakuwa misaada kwa vizazi vijavyo na kwamba kampuni hiyo imelenga kituo cha Afya kwa kuwa ndiyo kimbilio la Watu wengi.

  Aliongeza kuwa msaada wa kisima hicho unagharimu zaidi ya Shilingi Milioni 24, ambapo alisema TBL imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu iliyojiwekea ya kurudisha fadhila kwa jamii kutokana na faida wanayopata kutokana na mauzo ya bidhaa zao.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mdogo wa Tunduma, Helen Kagamizi, aliishukuru Kampuni ya Tbl kwa msaada wa kisima cha maji katika Kituo cha Afya kwa kile alichosema Mji wa Tunduma unatatizo kubwa la uhaba wa maji.

  Alisema mradi huo utakapoanza kufanyakazi utakuwa mkombozi kwa watu wengi hususani wagonjwa ambao ndiyo wahitaji sana wa Maji na kwa mujibu   Mkandarasi anayechimba kisima hicho anasema kinaweza kuzalisha Mililita 5000 kwa saa.

  Naye Mganga wa Kituo hicho Dk. Gibson Mbaza alisema Tbl imetoa msaada mkubwa na muhimu katika sekta ya afya kwa sababu huduma hiyo inahitaji huduma ya maji kwa wingi kutokana na mahitaji ya usafi kwa wagonjwa na mazingira kuhitaji maji mengi.

  Aliongeza kuwa maji hayo watayatunza vizuri ili yaweze kuwasaidia katika shughuli za kila siku za matibabu na wagonjwa kutokana na kukabiliwa na upungufu wa maji safi na salama kwa mji mzima wa Tunduma.

  Mganga wa Kituo hicho Dk. Gbson Mbaza alienyoosha mkono  alisema Tbl imetoa msaada mkubwa na muhimu katika sekta ya afya kwa sababu huduma hiyo inahitaji huduma ya maji kwa wingi kutokana na mahitaji ya usafi kwa wagonjwa na mazingira kuhitaji maji mengi.
   Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya TBL, Doris Malulu, wa pili toka mwisho wakati akikagua mradi wa uchimbaji wa Kisima cha Maji  uliofadhiliwa na Kampuni ya TBL  katika kituo cha Afya cha Tunduma kilichopo Wilayani Momba Mkoa wa Mbeya.


  0 0


  0 0
 • 02/03/14--19:19: Article 17 • 0 0

   Mwenyekiti wa wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya pamoja na ma-bloggers wakubwa wa Tanzania wakati wa kiadhimisha sherehe za miaka 37 za uhai wa CCM uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Picha hii imepigwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana hapo chini...


  0 0
 • 02/04/14--04:28: Beach Plot for SALE

 • Plot size 5800 square metres(2.2 hectares)
  Location: Kunduchi Bahari Beach, near silver sand hotel & Bahari Beach Hotel
  Its a beach front plot
  Asking price is 1.2 USD million(TSH 2 Bilion) its negotiable
  Contacts: Email address.... mwatawalawaladi@yahoo.com
                    Mobile no 0654254645/0713254645

older | 1 | .... | 216 | 217 | (Page 218) | 219 | 220 | .... | 1898 | newer