Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 214 | 215 | (Page 216) | 217 | 218 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0  Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu. Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda umeeleza kusikitishwa na taarifa za blog ya Rwanda “News of Rwanda” ambayo inaunga mkono serikali ya nchi hiyo iliyotolewa mwishoni mwa juma zikimtuhumu rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuunga mkono na kufanya mikutano na wanachama wa makundi ya waasi yanayopingana na serikali ya Rwanda.  Akizungumza na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania Salva Rweyemamu amesema wao wameshangazwa kwa sababu mwaka jana kulikuwa na matatizo na marais wa nchi hizo wameshazungumza vizuri wakakubaliana na kuonyesha kwamba sasa mambo yameisha na kwamba wanaendeleza urafiki wao, udugu wao na ujirani mwema wa miaka mingi kati yao na kuongeza kwamba hilo ni jambo la kusikitisha sana kwa upande wa Tanzania. 

  Ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini humo visaidie kujenga uhusiano mwema na visiwe mwanzo wa choko choko ya kugombanisha watu akiuliza kuwa “Tanzania wakigombana na Rwanda magazeti yatauzwa?” au mkiwa kwenye hali ya vurugu kama ilivyo nchi zingine ambapo watu wanapigana kila siku kuna watu wananunua magazeti pale? Kusikiliza mahojiano ya Salva Rweyemamu na VOA bofya hapa. http://www.voaswahili.com/content/article/1841294.html

  0 0

  Kamishna Msaidizi- Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Fredy Mahobe kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifafanua taratibu za kupata mikopo kwa wachimbaji wadogo.
  Mhandisi Heri Issa kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) akionesha jinsi uchekechaji wa madini unavyofanyika, katika mafunzo ya wachimbaji wadogo yanayoendelea huko Tunduru mkoani Ruvuma.
  Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Julius Sarota akielezea matumizi ya zebaki kwenye uchenjuaji wa madini katika mafunzo ya wachimbaji wadogo yanayoendelea huko Tunduru mkoani Ruvuma.
  Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ( waliokaa mbele) ikiwa ni pamoja na washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa. 

  0 0

  Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora Mh. Abdallah Sallehe Ahmed akifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani).


  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora imefanya ziara ya kikazi katika Makao makuu ya TASAF jijini Dar es Salaam ili kupata taarifa za utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini na zilizo katika Mazingira hatarishi unaotekelezwa chini ya TASAF awamu ya tatu kote nchini.

   Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora Mh. Deogratius Ntukamazina akichukua dondoo muhimu za TASAF awamu ya tatu kama zilivyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani)

   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama pichani) akitoa kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini na zilizo katika Mazingira hatarishi unaotekelezwa chini ya TASAF awamu ya tatu.

   Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora Mh. Abdallah Sallehe Ahmed akifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani)
   Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora Mh. Abdallah Sallehe Ahmed akifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani).


  0 0
 • 01/31/14--03:56: ZE KIBONZO CHA LEO


 • 0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akimsindikiza na kuagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR.

  0 0

   Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akimkaribisha Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen alipkutana na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Kempasi ya Vuga alipofanya ziara ya siku moja Zanzibar.
   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Professa Idrss Ahmad Raia akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen alipotembelea chuo hicho Kempasi ya Vuga alipokuwa na ziara ya siku  Zanzibar.
   Waziri mkuu wa Finland Jyrki Katainen akizungumza na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) alipotembelea chuo hicho katika ziara yake ya siku moja Zanzibar (wa kwanza kulia) ni Waziri wa Miundombinu na Mwasiliano Rashid Seif Suleiman na (kati kati) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Professa Idriss Ahmad Rai. 
   Baadhi ya wahadhiri na viongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen wakati akiwahutubia katika Kempasi ya Vuga wakati wa ziara yake ya siku moja Zanzibar.


  Picha ya pamoja ya Waziri Mkuu wa Finland na baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar na viongozi aliofutana nao kutoka Tanzania Bara. (wa kwanza kushoto) ni Balozi wa Finland nchini Tanzania Sinikka Antila.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

  0 0

   WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika katika masuala ya uwekezaji nchini endapo itatekeleza kikamilifu Mapitio ya Mfumo wa Uwekezaji yaliyowasilishwa na Taasisi ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD).
   
  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Januari 31, 2014), wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kitabu cha Mapitio ya Mfumo wa Uwekezaji kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   
  Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu Pinda  alisema kuwa malengo ya mapitio ya  mfumo huo ni kuboresha hali ya uwekezaji na biashara nchini ambayo matokeo yake yatasaidia kuongeza wawekezaji katika maeneo mengi.
   
  “Kuna maeneo ya uwekezaji yanayopata uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi (Foreign Direct Investment -FDI) ambayo ni umeme, mafuta, gesi, madini, viwanda, ujenzi na huduma za jamii.”
   
  Amesema kuwa matokeo ya jitihada hizi ni makubwa na yameonekana ndani ya miaka miwili tu. Akitoa mfano, alisema: “Kilimo kimeweza kukua kutoka dola za marekani  milioni 304.5 mwaka 2010 hadi dola za marekani milioni 355.4 katika mwaka 2011. Vilevile kwenye sekta ya Umeme na Gesi imekua kutoka dola za kimarekani  milioni 328.6 hadi dola za kimarekani  539.8 mwaka 2011.”
   
  Kutokana na matokeo hayo, Waziri Mkuu ameeleza kuwa Tanzania ina fursa nyingi zikiwemo rasilimali, nafasi yake kijiografia na historia ya siasa safi ambazo zinaifanya iwe kivutio kikubwa cha uwekezaji. Hali hiyo Waziri Mkuu alisema, imesaidia Pato la Taifa kuendelea kukua kwa asilimia sita kwa miaka 10 mfululizo na mwaka jana ilikua kwa asilimia saba na sasa inatarajiwa kufika asilimia 7.2 kwa mwaka huu.
   
  Miongoni mwa maeneo yanayohusishwa na mfumo huu wa mapitio ya Uwekezaji ni yale yaliyoainishwa katika Matokeo makubwa sasa ambayo ni Kilimo, Maji, Uchukuzi, Elimu na Nishati.
   
  “Ili kufanikisha maeneo hayo ni muhimu tukajenga mazingira bora ya uwekezaji, hivyo Serikali inawataka wadau wote kwa kushirikiana na Sekta binafsi kuchambua kwa makini mapendekezo ya mapitio ya mfumo huo ambayo yanatumika pia kuharakisha mafanikio ya Matokeo makubwa sasa”, alisisitiza Waziri Mkuu.
   
  Waziri Mkuu alisema Serikali ya Tanzania inashukuru sana Taasisi ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) kwa kuweka sura maalum kwenye kitabu hicho  inayozungumzia changamoto za uwekezaji kwenye sekta ya kilimo na jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo.
   
  “Ninatumaini kuwa utekelezaji wa mapendekezo haya utaongeza ufanisi wa mchakato huu na kuhakikisha kuwa tunazitumia fursa zilizopo na nyingine zaidi katika kuboresha uwekezaji katika kilimo nchini. Na kwenye kilimo ninamaanisha kilimo mazao, mifugo, uvuvi na nyuki,” aliongeza.
   
  Mapema, Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi ya OECD, Bw.  Rintaro Tamaki, alisema mazingira ya uwekezaji nchini yanabadilika kila mara kutokana na kuvumbuliwa kwa rasilimali mpya kama vile gesi, makaa ya mawe ambazo zinasababisha watu wavutive kuwekeza nchini.
   
  Kutokana na kugunduliwa na sekta hizo, Serikali isizipuuzie sekta za zamani hususan Sekta ya kilimo, cha msingi ni kuboresha sekta hii kwa kuanzisha viwanda ili kuongeza thamani ya mazao yenu”.

  IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI MKUU,S. L. P. 3021,DAR ES SALAAM.IJUMAA, JANUARI 31, 2014

  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia) akikata utepe kuzindua ripoti ya hali ya Uwekezaji nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine ripoti hiyo imegusia sera na na maendeleo ya uwekezaji nchini pamoja na changamoto zinazokwamisha ustawi wa uwekezaji Tanzania.
   Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akionyesha vitabu vya ripoti ya Uwekezaji Tanzania kwa wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ripoti kuhusu hali ya Uwekezaji nchini Tanzania  leo jijini Dar es salaam.
    Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi kitabu cha Ripoti ya hali Uwekezaji nchini Tanzania Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi (kulia) leo jijini Dar es salaam.
    Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na wadau wa uwekezaji mara baada ya kuzindua ripoti kuhusu hali ya uwekezaji nchini Tanzania.
   Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi (kulia) akizungumza jambo na Bi. Marry Hobbs Mwakilishi wa masuala ya Kilimo na Maliasili wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani nchini Tanzania leo wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya hali ya Uwekezaji nchini.
   Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ripoti ya Uwekezaji nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu changamoto na hali ya uwekezaji katika sekta ya Mifugo na uvuvi nchini.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

  0 0

   aji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akizungumza na waandishi wa habari juu ya sherehe ya siku ya sheria Zanzibar ambayo itaadhimishwa tarehe 10 Februari 2014.  Mkutano huo ulifanyika  Ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar.
   Mwandishi wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Ramadhani Ali akimuuliza swali Jaji Mkuu wa Zanzibar (hayupo pichani)  wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
   Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa ufafunuzi wa jambo wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari yaliyofanyika ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
   Baadhi ya watendaji wa Mahakama ya Vuga mjini Zanzibar na waandishi wa habari wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar leo. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

  ========  =====  ======

  Na Miza Othman   Maelezo Zanzibar  31/1/2014
  Jaji Mkuu wa  Zanzibar  Omar Othman  Makungu amesema ucheleweshwaji wa kesi  katika Mahakama za Zanzibar unasababishwa na mambo mengi  ikiwemo kukosekana mashahidi na kutokamilika  kwa upelelezi  na ukosefu wa vitendea kazi.

  Hayo ameyaeleza  leo huko Ofisini kwake  Vuga  wakati alipokuwa akizungumza na waaandishi wa Habari juu ya sherehe ya siku ya sheria Zanzibar ambayo itaadhimishwa tarehe 10 Februari 2014.
  Amesema kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Saidia mahaka kutenda haki “  ikiwa na lengo wadau wote wa mahakama kutoa mchango wao kuiwezesha mahakama kutenda haki.

  “Kesi sio mahakama pekee wadau wengi wanahusika na kila mmoja anapaswa kutekeleza wajibu wake katika utolewaji wa haki  lakini inayolaumiwa zaidi ni Mahakama kwa sababu utoaji wa haki unamalizia hapa” alisema Jaji Mkuu.

  Amesema kesi za jinai mara nyingi huanzia Polisi na baadae kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mshtaka na hatimae kuwasilishwa  mahakamani kwa mashtaka lakini mahakama hushindwa kumaliza kesi  kwa haraka kutokana na  kukosekana mashahidi na  kutokamilika upelelezi.

  Kwa upande wa kesi za madai Jaji Mkuu amesema  zimekuwa na changamoto nyingi baadhi ya wakati mdaiwa hajulikani  alipo  na mdai anashindwa kuwa na mawasiliano naye.

  Jaji mkuu wa Zanzibar ameongeza kuwa baadhi ya wakati bajeti nayo inakuwa ni kikwazo kwani imekuwa haitoshi na haipatikani kwa wakati.
  Amesema siku ya  sheria Zanzibar itatoa nafasi kwa wadau wa mahakama ikiwemo Polisi Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na serikali  kukaa pamoja kutafakari njia zilizobora za kuendesha kesi kwa haraka.

  Akizungumzia malalamiko ya rushwa katika mahakama, amesema suala hilo linachangamoto nyingi kwani rushwa hutolewa kwa njia ya siri lakini amewashauri wananchi wanaoombwa rushwa kutoa  taarifa kwa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa kwa hatua zaidi.

  Hata hivyo amekumbusha kuwa suala la rushwa ni kosa linalowahusu  mtoaji na mpokeaji hivyo amewataka  wananchi kutokuwa tayari wanapoombwa rushwa ili kuepuka kuingia kwenye makosa.
  Jaji Makungu amesema kabla ya kilele cha sherehe hiyo kutakuwa na harakati mbali mbali ikiwemo mdahalo wa wanafunzi utakaozungumzia umuhimu wa heria na vipindi vya Televisheni na Radio ambavyo vitahusu juu ya siku hiyo.

  0 0

  Pichani ni mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kawe,Halima  Mdee wakiwa wameachiwa na jeshi la polisi akisindikizwa kwenda kupanda chopa katika viwanja vya mwembetogwa mara baada ya kudaiwa kuzidisha muda kwenye mkutano wao wa hadhara mkoani Iringa. (picha zote na denis mlowe)
   
  MBOWE ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI IRINGA.

  Na Denis Mlowe,Iringa

  MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa jimbo la Hai na Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee walishikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa, kwa kosa linalosemekana  kuzidisha muda wa mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mgama wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.

  Kwa majibu wa Mbowe alisema jeshi la polisi walimshikilia kwa masaa mawili kwa mahojiano na mkuu wa kituo cha polisi na kisha kumwachia huru.
  Akizungumza na wafuasi wa Chadema kabla ya kupanda Helkopta na kuelekea mkoa wa Pwani akiambatana na Mbunge wa Kawe Halima Mdee aliwataka wananchama wa Chadema kuungana katika kukijenga chama bila hofu na kuwashukuru kwa kuwaunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi.
  Alisema wakati wanajiandaa kuondoka alipata malalamiko kutoka kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya kuwa wamezidisha muda wa kufanya mkutano katika kijiji hicho.
  Mbowe alisema kuwa chanzo kingine ni baadhi ya viongozi wa kijiji kuwadanganya wananchi katika mkutano uliotakiwa kufanyika katika vijiji vya kata ya Ukumbi kuwa watakuwepo  wabunge na mwenyekiti wa chama katika mkutano  kitu kilichosababisha kuwepo na dalili za ugomvi.  “Jeshi la polisi limetuhoji kuhusu mambo hayo na baada ya kuwaeleza walituachia huru na ila wamesema wakituhitaji watatuita lakini makamanda naomba sana mjenge chama na nawashukuru sana kwa kutuunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi” Alisema Mbowe.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Chama cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambap wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo ukumbi wa Mtenda,Soweto jijini Mbeya.

   Waendesha Bodaboda kutoka sehemu mbalimbali jijini Mbeya,wakiwa wamembeba Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kuzungumza nao mapema leo jioni ndani ya ukumbi wa Mtenda,Soweto mkoani Mbeya.
   Waendesha Bodaboda kutoka sehemu mbalimbali jijini Mbeya,wakiwa wamembeba Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kuzungumza nao mapema leo jioni ndani ya ukumbi wa Mtenda,Soweto mkoani Mbeya.
   Baadhi ya Waendesha boda boda wafurahia jambo kwenye mkutano huo
  Waendesha Bodaboda wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye wakati wa mkutano huo.
  Katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akizungumza wakati wa mkutano na Waendesha Bodoboda kutoka sehemu mbalimbali jijini Mbeya leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema ambaye ni Mlezi wa Bodaboda Mkoani Mbeya,kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na Waendesha Bodaboda wa mjini humo,ambapo Wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la Polisi na Polisi Jamii katika kulinda Usalama wa Wananchi,wao wenyewe na mali kwa ujumla ,Changamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na Utulivu.


  0 0

   Malkia wa Taarab nchini Bi. Hadija Kopa akiimba mbele ya umati wa watu kwenye ukumbi maarufu wa City Pub mjni Mbeya.
   Baadhi ya wanamuziki wa TOT Taarab wakiimba kwa hamasa wakati band hiyo ya muziki wa taarab ilipotumbuiza kwenye ukumbi wa City Pub mjini Mbeya.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpongeza bi Hadija Kopa kwa umahiri wake wa kuimba taarab kwenye ukumbi wa City Pub Mbeya.
  Umati wa watu ukiwa umefurika wakati Malkia wa Taaarab Hadija Kopa na Band ya Taarab ikitoa burudani kwa wakazi wa Mbeya mjini.

  0 0  Its final happen in London, Mfalmeeeeee,

  The one and only, Mwinyi Yusuf Mzeee, Akijulikana kama King of Taarabu,

  Anakuja London kwa show moja tu, show yenye hadhi, show ya watu wanaojuwa raha za Pwani na show ambayo hupaswi kukosa kuhudhuria.

  Ni kwa kiingilio cha Twenty Pound Only ndani ya The Ville 640 Ripple Road BARKINGGGG.

  Njoo upandishwe Jahazini, Njoo Tulambe na Njoo unukie marashi huku tukionja raha za Mpenzi Chocklate,

  Yaaaani itakuwa Hatari Bin Dangerrrr,

  0 0  0 0

  My bad, nimesahau kuweka anwani ya mtandaoni ya RADIO MBAO. Ni www.radiombao.com na itakuwa hewani kuanzia Februari Mosi 2014. Sie tunaamini katika #SharingIsCaring , na RADIOMBAO inakuhamasisha nawe ku-share nasi habari yoyote ile . Usihofie kwamba “ah mie sio mwandishi” tutahariri habari yako na itasomwa/kusikika katika nchi 138 duniani. Na wala usikwazwe na “ah mie sijawahi kuandika” kwani kama unaweza kuandika SMS basi kwa hakika unaweza pia kuandika habari. Pia kila jambo lina mwanzo, mtoto hazaliwi akitembea. Kwahiyo yawezekana RADIOMBAO ikaibua kipaji chako…lakini ili hilo liwezekane basi usihofie ku-share nasi habari. Ni Jumamosi Februari 1, 2014, mahali pa kukutana ni www.radiombao.com #SharingIsCaring (at Glasgow)

  RADIO MBAO: Ninaomba kuwafahamisha kuwa mie na mwenzangu @djkvelli mkongwe wa masuala ya entertainment kama dj nchini Marekani na mmiliki wa kituo maarufu cha radio mtandaoni, RADIOMBAO, tumeunganisha nguvu, na kwa pamoja tunawaletea uzinduzi RADIOMBAO katika sura mpya. Licha ya matangazo ya radio, RADIOMBAO sasa inakuletea habari mbalimbali katika namna tofauti (bringing you news not in your traditional way). Uzinduzi rasmi utakuwa LEO  Jumamosi ya Februari 1 mwaka huu 2014.

   Tunataka nawe uwe mshiriki kwa kututumia habari kwa email radiombao@gmail.com nasi tutataja jina lako kama utapenda tufanye hivyo. Hii pia ni fursa adimu kwa wasanii kutangaza kazi zenu DUNIANI kwani RADIOMBAO inasikika katika NCHI 138 DUNIANI. Tutatangaza kazi yako ya sanaa BURE. Kwa kuunganisha uzoefu na ujuzi wa muda mrefu wa @djkvelli katika masuala ya entertainment nchini Marekani, na uzoefu wangu wa takriban miaka 10 katika fani ya habari, tunawaahidi kuwaletea kitu kipya,tofauti na kitakachokidhi mahitaji yako ya habari,mahojiano,burudani na soka, maisha najamii, teknolojia na mengineyo mengi. 

  Ombi letu kwako ni kuwa sehemu ya familia ya RADIOMBAO: Mfahamishe ndugu, jamaa na rafiki yako kuhudu ujio mpya wa RADIOMBAO. Karibuni sana kutembelea tovuti yetu inayopatikana katika anwani hii

  Wasiliana nasi kwa email radiombao@gmail.com

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la Magreth Kalimwa (wapili kulia), katika Kijiji cha Mlimanyoka, Kata ya Nsalanga, wilala ya Mbeya mjini. Kinana alifika kumsaidia mkulima huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, inayofanyika Kitaifa Jumapili hii mjini Mbeya.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Bi.Magreth Kalimwa mara baada ya kuwasili kwenye shamba lake kwa ajili ya kushiriki kupalilia shamba hilo lenye ekari moja na nusu
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi na Wanachama wa CCM,(hawapo pichani) katika kijiji cha Itesi Mashariki,Kata ya Nshalanga,alipokwenda kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya kata ya chama cha CCM,Wilaya ya Mbeya Mjini mkoani Mbeya mapema leo.
  Ujenzi wa jengo la Ofisi ya kata ya chama cha CCM,Wilaya ya Mbeya Mjini mkoani Mbeya mapema leo kama ionekanavyo mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokwenda kufanya ukaguzi
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisaidiana na vijana kuandaa jukwaa litakalotumika wakati wa mapokezi ya matembezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Sokine mjini Mbeya. Matembezi hayo yanaongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
  Vijana wakiwa kwenye mazoezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika Jumapili hii mjini Mbeya. 

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jumuiya ya Istiqaama, uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Feb 01, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Istiqaama, leo Feb 01, 2014.
  Baadhi ya Wanachama wa Jumuiya ya Istiqaama, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akihutubia kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo leo katika Ukumbi wa Karimjee.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, baada ya kufungua rasmi Mkuu wa Jumuiya hiyo leo katika Ukumbi wa Karimjee.
  Picha ya pamoja baada ya kufunguliwa mkutano huo.Picha na OMR. 

  0 0

  Manji awawakia wanaomuandama Seif Magari
  Dar es Salaam. Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewaonya wanachama na mashabiki wa timu hiyo wanaotishia maisha Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya imataifa wa klabu hiyo, Seif “Magari” Ahmed kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.
   
  Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Manji amesema kuwa si suala jema kwa wanachama kumuhusisha Seif na matokeo ya timu hiyo ambayo kwa sasa imeshinda mechi moja na kutoka sare mechi moja katika mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.
   
  Manji amesema kuwa madai kuwa Seif siyo mwanachama halali  wa Yanga hayana msingi wowote na kuyaita madai hayo kuwa ni ya uzushi na yanaenezwa na maadui zao ambao hawaitakii Yanga mema.
   
  Alisema kuwa hivi karibuni kumekuwa na madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu, taarifa za hujuma ndani ya timu ambazo zimewahusisha uongozi na baadhi ya wanachama jambo ambalo si la kweli.
   
  Alifafanua kuwa ni haki kwa kwa nia njema kwa wanachama kuhoji mwenendo wa timu yao pale wanapoona-hairidhishi na ni wajibu wa wanachama kuchanganua mawazo merna na mabaya na siyo kumuhisha mtu kwa moja kwa moja kutokana na mtazamo hasi walionao.
   
  “Ushindi au mwenendo mzuri  wa timu unatokana na viwango vizuri, nidhamu na ushirikiano wa wahusika wote, wachezaji, walimu, viongozi, wanachama na wapenzi kwa ujumla. Uongozi ulikutana na wachezaji, walimu, baadhi ya wanachama na wapenzi na kuyazungumzia na kukubaliana kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa wahusika wote na kuchukua hatua ya kubadilisha benchi la ufundi,” alisema Manji.
   
  Aliongeza kwa kusema kuwa uongozi ulifika mbali zaid kwa kutoa adhabu na onyo kali kwa baadhi ya wachezaji walionyesha utovu wa nidhamu kwa kipindi kilichopita na kusikitishwa kuona kuwa baadhi ya wadau kwa kutumia vyombo vya habari wanachochea na kutengeneza uhasama ambao kwa kweli haupo ama kwa faida zao binafsiau kwa kutumiwa na watu ambao hawana nia njema kwa klabu.
   

  Manji pia aliwaomba wadau wote wanamichezo na hasa wahariri wa michezo kudhibiti matumizi mabaya ya watu au vyombo vya habari yanayochangia sana kuzorotesha michezo nchini.

  0 0

   Waziri Mkuu  Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na Naibu Waziri Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Japan Norio Mitsuya  alipomtembelea ofisini kwake jana.(Picha zote na  Ofisi ya Waziri Mkuu.)

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Japan  Norio Mitsuya alipomtembelea ofisini kwake jana 

older | 1 | .... | 214 | 215 | (Page 216) | 217 | 218 | .... | 1898 | newer