Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 209 | 210 | (Page 211) | 212 | 213 | .... | 1898 | newer

  0 0  WAZIRI MKUU  Mizengo Pinda amesema ameridhishwa na kazi ya ujenzi wa 
  bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na kwamba anaamini kazi

  hiyo itakamilika mwaka huu kama ambavyo wataalamu wameamuahidi.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Januari 24, 2014),
  wakati akiendelea na ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
  bomba hilo la gesi lenye urefu wa kilometa 542.

  Kwa mujibu wa Meneja wa mradi huo, Eng. Kapullya Musomba, kazi hiyo
  ilipangwa kukamilika Juni mwakani, lakini sasa hivi wanatarajia kazi
  hiyo itakamilika Desemba, mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari eneo la Somanga-Fungu wilayani
  Kilwa, mkoani Lindi, Waziri Mkuu alisema jumla ya mabomba ya kutosha
  km. 440 yamekwishawasili nchini. “Hii ni sawa na asilimia 81 ya
  mabomba yanayohitajika kwa ajili ya kazi hii,” alisema.

  Alisema kwamba kazi ya utandikaji wa mambomba hayo imefanyika vizuri
  kiasi kwamba km. 114 kati ya hizo zimekwishachimbwa (trenching)
  zinasubiri mabomba yaanze kutandazwa ardhini.

  “Kwa kweli kazi inayofanywa ni nzuri, mabomba yaliyokwishaunganishwa
  mpaka sasa yanaweza kutosha kutosha km. 263 ambayo ni zaidi ya nusu.
  Nina imani kwamba kazi hii itakamilika mapema kama alivyosema mshauri
  mwelekezi wa mradi huu,” alisema.

  Mapema, akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu kuhusu maendeleo ya mradi huo,
  Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba, Eng. Thomas Baltazar alisema mabomba  hayo yakishatandazwa ardhini yanaweza kudumu kwa miaka 30 lakini  yakifanyiwa matengenezo na kuchekiwa mara kwa mara yanaweza kudumu kwa  miaka 50.


  Naye Mshauri Mwelekezi wa mradi huo, Eng, Peter Erasmus wa kampuni ya
  Worley Parson ya Afrika Kusini alisifu uimara wa mabomba yaliyotumika
  kwenye mradi huo na kumhakikishia Waziri Mkuu kwamba yana ubora wa
  hali ya juu ilikinganishwa na miradi mingine ambayo kampuni yake
  imesimamia katika bara la Afrika.

  Waziri Mkuu alikagua hatua mbalimbali za ujenzi wa bomba hilo kuanzia
  Vikindu na Bungu mkoani Pwani; Somanga Fungu na Kitomanga mkoani Lindi    ambako alionyeshwa uwekaji wa zege nje ya mabomba ili yasielee


  baharini; utandazaji wa mabomba ardhini na baharini na upindaji wa
  mabomba kwa kutumia mashine maalum.

  Pia aliweka jiwe la msingi la Kiwanda cha Saruji cha Meis kilichopo
  eneo la Machole nje kidogo ya mji wa Lindi.  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU.
  IJUMAA, JANUARI 24, 2014

  0 0

  Doreen Noni at Davos

  Doreen Noni at Davos.
  In January 2012, Doreen Noni, Creative Director of Eskado Bird, was one of the 70 carefully selected Global Shapers from 36 countries to attend the first ever Global Shapers delegation in Davos, Switzerland hosted by the World Economic Forum representing her fashion label Eskado Bird.

  This year, Doreen is the only Global Shaper from the Tanzanian hub attending the Annual 2014 World Economic Forum in Davos, Switzerland. She is representing the country well!

  Her presence didn't go unnoticed! She was a panelist during the session titled “Africa’s Next Billion” which was addressing Africa's population rising to 2 billion by 2050 and the actions that are needed now to ensure sustainable and inclusive growth.
  Doreen Noni Conference
  The panel of speakers consisted of very prominent and influential people. Doreen was sitting along side dignitaries such as his Excellency Goodluck Ebele Jonathan; President of Nigera, Aliko Dangote; President & CEO of Dangote Group, and his Excellency, John Dramani Mahama, President of Ghana.
  Her attendance at the Forum shows great progress for women, youth and future entrepreneurs.
  Doreen Noni Quote

  0 0


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako  walikuwa wakihudhuria  Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF.

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako  walikuwa wakihudhuria  Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF.  PICHA NA IKULU

  ========  ========  =========
  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  Telephone:255-22-2114512, 2116898

                press@ikulu.go.tz             

  Fax: 255-22-2113425


  PRESIDENT’S OFFICE,

        THE STATE HOUSE,

                P.O. BOX 9120,  

  DAR ES SALAAM.

  Tanzania.

   
  TAARIFA KWA  UMMA

  Rais Kikwete aalikwa Nigeria na Rais Jonathan


  Rais wa Nigeria Mheshimiwa Goodluck Jonathan amemwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Taasisi ya Uchumi Duniani Afrika (WEF-Africa) unaofanyika katika mji mkuu wa Nigeria wa Abuja mwezi Mei mwaka huu.


  Rais Jonathan ametoa mwaliko huo kwa Rais Kikwete wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo leo, Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako viongozi hao wanahudhuria wa Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF.


  Rais Kikwete amekubali mwaliko huo wa kuhudhuria Mkutano huo uliopangwa kufanyika Mei 7-9 mwaka huu mjini Abuja, Nigeria.

                       

  Mkutano huo kati ya viongozi hao wawili umehudhuriwa na Mawaziri wa Nigeria wa Mambo ya Nje na Fedha na Uchumi.


  Nigeria inakuwa nchi ya nne katika Afrika kuandaa mkutano huo. Kwa miaka mingi, mkutano huo wa WEF-Africa ulikuwa unafanyika Cape Town, Afrika Kusini mpaka Tanzania ilipofanikiwa kuwa nchi ya kwanza ya Afrika nje ya Afrika Kusini kuandaa Mkutano huo mwaka 2010.


  Tokea wakati huo, Ethiopia imeandaa mkutano huo na sasa Nigeria.


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.


  23 January, 2014  0 0

  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Titus Kamani, amesema ili kwenda na kasi ya maboresho ya wizara hiyo, inahitajika dhana ya uwajibikaji na uwazi sambamba na kujitolea kwa nguvu zote katika kufanya kazi.

  Waziri Kamani, ameyasema hayo leo katika mkutano wa kwanza uliowakutanisha wafanyakazi wote wa wizara hiyo, wakiwemo wastaafu wa mwaka jana katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Temeke jijini Dar es Salaam.

  Amesema kama kuna mtu ambaye ni kikwazo katika kukwamisha shughuli za wizara, ni bora akawapisha mapema na kwamba kila mtumishi kwa nafasi yake, anatakiwa kuifanya kazi kwa uwazi na akaitaka wizara kufanya kazi na vyombo vya habari kwani ndio njia pekee ya kuwafanya watanzania wajue wizara inafanya nini.

  “Wewe upo ofisini, halafu unaogopa ogopa vyombo vya habari, kwani unatatizo gani, kuweni wazi mambo yenu yawe hadharani, watanzania wa Mbeya wayajue, Rufiji mpaka Pemba, hakuna kufichaficha jambo katika wizara yangu.” Alisistiza Dk Kamani.


  0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa mbunge wa Chalinze,Mh. Said Bwanamdogo wakati wa mazishi yaliyofanyika kijijini kwake Miono Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani leo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe (CHADEMA) wakati wa mazishi ya mbunge wa Chalinze Marehemu Said Bwanamdogo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika huko Miono Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani leo.
   Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Picha na OMR
   Rais Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo. Picha na OMR
   Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge huyo yamefanyika leo kijijini kwao Miono. Picha na OMR.
   Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri Mkuu Mizengo Pinda na msafara wake wakiangalia eneo utakapochimbwa mtaro wa kupitishia bomba la gesi.

   Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba kabla ya kuyalaza na kuyafukia chini kwenye mitaro.

   Mkuu wa mkoa wa Lindi akiwa na Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili mkoani humo na kuendelea na ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi.

   Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha MEIS Merea Barabuu akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi.

   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi na wafanyakazi wa ujenzi kiwanda cha MEIS faida zitzkazotokana na kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa gasi kijijini hapo kwa njia rahisi baada ya kuunganishwa kutoka bomba kuu la gasi ikiwemo ajira kwa wanachi na upatikanaji wa saruji kwa bei nafuu ili kuboresha makazi yao.

   Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha MEIS kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi.

  Picha ya sura na muonekano wa kiwanda cha MEIS kitakapokamilioka. (Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO-Mtwara).
   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na mafundi wanaojenga bomba la mradi wa gasi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua mradi huo.

   Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akieleza hatua iliyofikiwa katika ujennzi wa bomba la gasi linalojengwa kutoka Mtwara hadi Dar es salaam kwa Waziri Mkuu na msafara wake. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Lu Younqing.

   Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akimsikiliza Waziri wa Nishati na Prof. Madini Sospeter Muhongo akizungumzia ujenzi wa bomba la gasi eneo la Bungu mkoa wa Pwani.


  ========  ========  =========

  Na Eleuteri Mangi-Maelezo Mtwara.

  Waziri Mkuu amewaasa wanachi kutunza miundo mbinu ya mradi wa gasi nchini.


  SERIKALI imewapa jukumu wananchi wanaoishi maeneo linapopita  bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam la kulitunza na kulilinda  kwa manufaa yao na taifa zima.


  Wito huo ulitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda  leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba hilo. Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali inavihakikishia vijiji lilipopita bomba hilo kuwa watapatiwa umeme unaotokana na uzalishaji wa gasi na utakuwa wa gharama nafuu.

  Zaidi ya hayo, gasi itatumika kwa matumizi ya nyumbani kwa kuunganishiwa bomba la gasi na ambao hawatafanikiwa watakuwa na fursa ya kupata mitungi ya gesi ambayo itakuwa ya bei nafuu. Waziri Mkuu ameagiza mashirika ya Shirika la gasi na Petroli Tanzania (TPDC) na Mradi wa Nishati Vijijini (REA) wachukue jukumu la kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo lilipopita bomba hilo katika maeneo ya barabara, shule, kuwapatia maji safi na salama,kuwaboreshea utoaji wa huduma za afya kwa kuboresha zahanati na vituo vya afya kama mchango wao kwa jamii.

  Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa serikali kupitia shirika la TPDC na REA itahakikisha wanachi waishio vjijini wanapata umeme mapema iwezekanavyo.


  Kwa kuthibitisha kauli hiyo Prof. Muhongo alisema serikali kupitia TPDC na REA imetenga sh. Bilioni 20 kwa awamu ya kwanza ambayo itasimamiwa na REA wakati awamu ya pili nayo itatumia bilioni 20 iotkaysimamiwa na TPDC.


  Katika ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na mke wake bi Tunu Pinda, Balozi wa China nchini, Lu Younqing, Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, mbunge wa Mchinga Said Matanda na Fatma Mikidadi mbunge wa viti maalum. Maeneo aliyotembelea Waziri Mkuu ni pamoja na Vikindu, Jopika, Bungu, Ikwiriri, Somanga, Somanga Fungu, Kitomanga na Lindi.


  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu (katikati) akikabidhi pikipiki kwa moja ya vikundi 130 vya Vicoba vilivyo chini ya Taasisi ya PFT katika hafla ya kuviongezea uwezo kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam . Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo. Abbas Mtemvu. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
   Mwenyekiti wa PFT, Abbas Mtemvu akihutubia wakati wa hafla hiyo
   Waziri, Dk Mary Nagu akihutubia katika hafla hiyo, ambapo alimsifia Mtemvu kwa kuanzisha taasisi hiyo ambayo imewasaidia kupunguza umasikini wa wananchi jimboni humo.
   Mtemvu akimpatia Dk. Mary Nagu tuzo kwa ajili ya Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ameisaidia Taasisi hiyo
   DK. Mary Nagu akimkabidhi mmoja wa viongozi wa VICOBA pikipiki ya mkopo
   Waziri Dk. Mary Nagu akimkabidhi gari dogo mmoja wa viongozi wa Vicoba. PFT imetumia sh. mil. 195 kununua magari, pikipiki na Bajaji vilivyotolewa mkopo kwa wanachama.


   Waziri, Dk. Mary Nagu akimkabidhi gari aina ya Toyota Noah mmoja wa viongozi wa VICOBA
   Kikundi cha Msanii Snura (katikati), kikitumbuiza wakati wa hafla hiyo
   Wageni waalikwa wakifurahi wakati Snura  'mama wa Majanga' akitumbuiza katika hafla hiyo
   Sehemu ya wana Vicoba

                                           Snura 'Majanga' akifanya vitu vyake ukumbini

   Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim 'Juma Nature' akitumbuiza wakati wa hafla ya kuviongezea uwezo vikundi vya Kuweka na Kukopa (VICOBA) 130 ambavyo ni wanachama wa Taasisi ya PFT kwenye Ukumbi wa  PTA Sabasaba, Dar es Salaam, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu. Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu. Baadhi ya vikundi hivyo viligawiwa pikipiki, bajaji na magari pamoja na fedha taslimu.
   Wana Vicoba wakishangilia wakati Nature akifanya mambo ukumbini
  Mary Nagu akiondoka huku akisindikizwa na Mtemvu


  TAARIFA FUPI KWA MHE: WAZIRI WA UWEZESHAJI NA UWEKEZAJI MAMA MARY NAGU KUHUSU POVERTY FIGHTING TANZANIA (PFT) TAREHE 24/01/2014 PTA SABA SABA

  Mhe: Mgeni Rasmi Waziri wa Uwezeshaji na uwekezaji Mama Marry Nagu.
  Awali ya yote tunachukua fursa hii Kukushukuru kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika shughuli yetu hii muhimu inayowahusu wajasilia mali wa Vicoba wanaoratibiwa na PFT katika Manispaa ya Temeke na tunakukaribisha karibu sana Temeke na ujisikie upo Nyumbani
  .
  1. UTANGULIZI.
  Poverty Fighting Tanzania (PFT) ni Taasisi isiyo ya kiserikali lililosajiriwa chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) sheria namba 24  kifungu kidogo cha 12 sheria ya mwaka 2002 kwa namba ya usajiri 00NGO/00004071.
  Ofisi za PFT zipo Mtaa wa Kitunda Tandika Wilaya ya Temeke,Mkoa wa Dar-es-salaam.
  2. Muundo wa PFT:
  Mhe: Mgeni Rasmi: PFT inaongozwa na Mkutano mkuu hiki ndio chombo cha juu katika kufanya maamuzi yanayohusina sera,na taratibu za PFT, ikifuatiwa na Bodi ya wakurugenzi  na Menejimenti ambayo inasimamia kazi za siku hadi siku  inayoongozwa na mkurugenzi Mtendaji.
  3. Lengo la PFT:
  Mh: Mgeni Rasmi:
  Lengo la PFT:  Ni kuunganisha Nguvu kazi katika kupambana na Umasikini Tanzania.
  Dira ya PFT:  Kujenga jamii ambayo itakuwa huru kutokana na umasikini na maradhi .
  Dhamira ya PFT:  Kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya jamii kupitia kuanzisha vikundi vilivyoandaliwa na kuwezeshwa kwa ustadi na mitaji ya kutosha.
  Mhe: Mgeni rasmi:  Kutokana na malengo hayo PFT inatekeleza shughuli zifuatazo:
  ·    Kuhamasisha na kuunda vikundi vya Vicoba katika  ngazi chini yaani Grassroots  level
  ·    Kuwajengea uwezo wanachama wa PFT katika maeneo makuu matatu:
  i.    Mfumo wa Vicoba namna unavyofanya kazi
  ii.    Stadi za uongozi wa vikundi na ujasilia mali
  iii.    Kuwaunganisha wanachama wa Vicoba wa PFT na wadau wengine wa maendeleo  kwa lengo la kujenga ubia na kubadilishana uzoefu,taarifa, maarifa na kupanua masoko yao.
  4. Walengwa wa mradi:
  Mhe: Mgeni Rasmi:
  Katika kutekeleza program ya kupunguza umasikini ,walengwa wa mradi huu ni familia zenye kipato cha chini ,jamii iliyoko pembezoni mwa huduma za kifedha na makundi maalumu.
  5. Mafanikio  ya mradi huu:
  Mhe: Mgeni rasmi: Hadi kufikia sasa PFT imefanikiwa  kuunda jumla ya Vikundi 130 venye wanachama 2,228 wanawake wakiwa 1,956 sawa na asilimia 87.8 na wanaume wakiwa 272 sawa na asilimia 12.2  wanachama hao wamewekeza jumla ya Tshs: 833,967,140 kupitia mpango wa ununuzi wa hisa za kila wiki na kuchangia mfuko wao wa jamii, fedha zote hizo zinamilikiwa na wanakikundi wenyewe kupitia akaunti  zao 105 zilizofunguliwa Amana Benki  zinazotumika kuifadhi fedha za  mizunguko yao na marejesho ya mikopo yao wanayokopeshana.
  Jumla ya mikopo 1,240 yenye thamani ya Tshs: 584,729,000 imetolewa na wana vikundi wenyewe kupitia mifuko yao ya hisa.
  Mhe: Mgeni Rasmi  Jumla ya Tshs: 75,779,900 zimegawiwa kwa wanachama hao ikiwa faida itokanayo na mikopo wanayokopeshana kwa kipindi cha miaka 3 sasa.
  Mhe: Mgeni Rasmi  pia tumefanikiwa  kuwaunganisha wanachama wa PFT na Taasisi ya kifedha yaani Amana Benki ambayo imekubali kuwakopesha wanachama hao kupitia  PFT jumla ya Tshs: 300,000,000 kwa kuthaminisha bidhaa wanazohitaji wanachama wa PFT ili waweze kukuza shughuli zao za kiuchumi, miongoni mwa mikopo hiyo ndiyo hii ambayo leo utakabidhi  gari aina ya Suzuki carry  6 ,Bajaj 10, Pikipiki aina ya Boxer 19, toyo la kubebea mizigo 1, vifaa vya selemala  vinavyotumia umeme, mbao,vifaa vya  statiories  na vifaa vya shooting Camera kwa vikundi 19 vinavyoratibiwa na PFT vyote vikiwa na thamani ya Tshs: 192,321,000/=
  6. Changamoto
  Mhe Mgeni Rasmi :
  Pamoja na mafanikio yote hayo bado PFT inakabiliwa na changamoto nyingi katika kutimiza malengo yake baadha ya changamoto hizo ni:
  i.    Ugumu wa upatikanaji wa mikopo ya masharti nafuu, kwani hata huu mkopo tuliyopata amana tumechukua muda mrefu zaidi ya 5 na Dhamana kubwa iliyowekwa ndio tumefanikiwa kupata mkopo huo kwaiyo hiyo changamoto inayowasumbua wajasilia mali wengi wadogo Tanzania.
  ii.    Upungufu wa fursa za kupata elimu ya ujasilia mali zaidi kwa wanachama wetu na kujenga ubia  na wadau wengine wa ndani na je ya nchi kupitia wizara ya uwezeshaji na uwekezaji .
  7. Hitimisho:
  Mhe:  Mgeni Rasmi :
  Mwisho tunaludia tena kukushukuru wewe binafsi na msafara wako mliongozana nao kuja katika shughuli hii  muhimu kwa wajasilia mali wa Temeke, PFT ina imani kubwa na wewe.
  Mhe: Mgeni Rasmi : Sisi tunakujua kuwa  una moyo na upendo  kwa PFT na  hiyo imedhirika tena kwa mara ya pili leo,kwani mara ya kwanza Tulikutana ofisini kwako Dodoma mwezi February 2013  ulikuwa na majukumu mengi na msarafa wetu ulikuwa wa ghafla sana  lakini ulitupokea na kutusaidia kwa kutuunganisha na Viongozi wa Baraza la uwezeshaji la Taifa ahsante Mhe: Waziri.

  Mhe: Mgeni Rasmi: kupitia kwako Menejimenti , Bodi ya Wakurugenzi  na wanachama wote wa PFT  tunampongeza sana mwenyekiti wetu wa bodi Mhe; Abbas  Mtemvu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa usimamizi wake makini wa PFT hadi kufikia mafanikio haya.
  Imani yetu ni kwamba utaendelea kushirikiana nasi na  kutusaidia mara kwa mara kwa kadri ya uwezo wako  ili wajasilia mali hawa wa Temeke waweze kufaidika na fursa zinazotokea katika wizara yako ambazo zinawalenga wao.
  Tunakutakia kila heri na mafanikio katika utendaji wako wa majukumu ya kitaifa,Sisi PFT tutaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha tunatekeleza mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini wa kipato Tanzania (MKUKUTA II)
  Karibu tena Temeke wewe na msarafa wako
  Naomba kuwasilisha:
  VICOBA SILAHA DHIDI YA UMASIKINI
  NI MARUFUKU KUKATA TAMAA

  0 0

   Kiwanda cha ngozi kilichopo manispaa ya Shinyanga ambacho kimekamilika na kazi ya kujaribisha mitambo inaendelea.
   Mkuu wa Mkoa Mhe. Ally N.Rufunga akipata maelezo ya maendeleo ya kiwanda hicho mapema leo alipotembelea ili kuona shughuli zinazoendelea
   Mashine za kuosha na kulainisha ngozi zikijaribiwa, chini ni ngozi zinazosubiri kuwekwa kwenye mashine hizo
   Mkuu wa Mkoa akioneshwa baada ya kazi ngozi laini inavyokuwa na tayari kwa matumizi mbalimbali kama kutengeneza viatu,mabegi,pochi,n.k
   Hizi ni mashine za kutengeneza yuzi katika kiwanda cha nyuzi na nguo kilichopo manispaa ya Shinyanga
   Mkuu wa Mkoa Mhe. Ally N. Rufunga akiona shughuli ya kujaribu mitambo katika kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong leo alipotembelea kiwanda hicho


   Ndani ya kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong ambapo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N. Rufunga amekitembelea mapema leo na kujionea kazi ya kujaribu mitambo
  =========  =========   ===========
  Kiwanda cha kutengeneza Ngozi kwa ajili ya matumizi mbalimbali cha kampuni ya Kichina "Xiu hua"  kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga kimekamilika ambapo mhandisi na msimamizi wa kiwanda hicho "Mr.Way" amesema kwa sasa majaribio yanafanyika kabla ya kuanza uzalishaji wakati wowote.

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga ametembelea kiwanda hicho mapema leo na kujionea majaribio ya mitambo ya kutengeneza ngozi za mbuzi,kondoo na ng'ombe.

  Kiwanda hicho kinachotarajiwa kutengeneza jumla ya ngozi za kondoo na mbuzi Elfu kumi hadi 12 kwa siku na ngozi za ng'ombe 2500, kitaajiri zaidi ya Watanzania 500 ambapo Mr.Way amesema kipaumbele zaidi ni kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga.

  Mkuu wa Mkoa pia ametembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya pamba cha Jielong Holdings, ameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Mr. Jerry Q kuwa wanaendelea kuzifanyia majaribio mashine na wakati wowote kitaanza kazi ya uzalishaji. 
  Mr.Jerry amesema kitaajiri zaidi ya wananchi 180 kitakapoanza uzalishaji na tayari kimeanza kuajiri.

  Aidha,kiwanda cha kutengeneza nyuzi za nguo cha Dahong ambacho  kinatarajiwa kuanza kazi mapema mwezi Machi baada ya kukamilisha kazi ya kufunga mashine mwishoni mwa mwezi Februari.
  Msimamizi wa kiwanda hicho Mr.Saimon amesema kiwanda hicho kitaajiri wananchi zaidi ya 80.

  Mhe.Rufunga amefanya ziara hiyo ili kujua maendeleo ya viwanda hivyo ambavyo vinatarajiwa vitakapokamilika pamoja na viwanda vingine, vitabadili sura ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo kwa kukuza uchumi wa mkoa,kwani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha maisha ya wananchi wa Shinyanga yanabadilika kwa kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vitakavyozalisha ajira nyingi zitakazonufaisha wananchi.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kilichofanyika jana tarehe 25 Januari 2014 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Sumbawanga Mjini. 
  Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza katika kikao hicho ambapo alitilia mkazo juu kuboresha elimu na ufaulu katika halmashauri hiyo ambayo haijafanya vizuri katika siku za karibuni. Alisisitiza pia umuhimu wa upandaji miti hususani katika msimu huu wa masika.
  Mbunge wa Jimbo la Kwela (CCM) Ignas Malocha akishukuru ujio wa Mkuu huyo wa Mkoa katika kikao hicho na maelekezo aliyoyatoa ambayo alisema ni muongozo mzuri na wa kuzingatiwa katika maendeleo ya halmshauri hiyo.
  Mkuu huyo wa Mkoa akizungumza na wajumbe wa kikao hicho kushoto wakiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na kulia wakiwa ni wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.
  Madiwani wa halmashauiri ya wailaya ya Sumbwanga.
  Wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Sumbwanga.
  Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Madiwani na Viongozi wa Chama tawala (CCM) walioalikwa katika kikao hicho.


  NA HAMZA TEMBA - OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
  ........................................................

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya amewaonya watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakiwemo wakuu wa idara wenye tabia ya kuwachonganisha madiwani na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Adam Misana, "watumishi mnaofanya mchezo huo nitawaondoeni" Alisema Manyanya. 

  Manyanya aliyasema hayo jana katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga alipotembelea kutoa salam zake za mwaka mpya kwenye baraza hilo. Alisema kuwa tangu Mkurugenzi huyo ateuliwe kuiongoza Halmashauri hiyo amekuwa akifanya vizuri katika udhibiti wa mapato jambo ambalo limekuwa kero kubwa wakuu wa idara na watumishi wa ofisi hiyo.

  Alieleza kuwa Mkurugenzi aliyekuwepo kabla ya Misana alikua akikaimisha ofisi mara kwa mara kwa watu tofauti jambo ambalo lilizorotesha utendaji na kupelekea mambo kufanyika kienyeji na kwa mazoea bila kujali matumizi sahihi ya mapato ya Halmashauri. Ujio wa Mkurugenzi huyu mpya umerekebisha hali hiyo kwa kiwango kikubwa hususani katika matumizi ya fedha za halmashauri, aliongeza Mkuu huyo wa Mkoa.

  Katika salam zake alilieleza baraza hilo kuwa mpaka sasa toka ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameshatembelea kata 51 sawa na asilimia 80% ya kata zote Mkoani Rukwa. Alisema baadhi ya kata hizo ameshazitembelea zaidi ya mara tano kutokana na umuhimu na matukio yaliyojitokeza.

  Aliwata madiwani, viongozi wa chama na halmashauri pamoja watumishi kwa ujumla kutoa uongozi uliotukuka katika maeneo yao kwa kushirikiana katika kutoa huduma bora kwa wanachi na kuwafikia mara kwa mara pale inapowezekana na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

  Katika hali nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alishangazwa kwa Wilaya ya Sumbwanga kutokuwa na Hospitali yake ya Wilaya na badala yake kutegemea huduma katika Hospitali  Kuu ya Mkoa. Alisema mwaka huu 2014 ni mwaka wa afya na kwamba Halmashauri za Wilaya ya Sumbwanga zijipange kuhakikisha zinakuwa na hospitali yao ya Wilaya ili kuweza  kutoa nafasi kwa hospitali kuu ya Mkoa kuhudumia wagonjwa wa rufaa kuliko ilivyo hivi sasa ambapo ambapo inabebeshwa mzigo mkubwa na Wilaya hiyo.

  Katika salam zake Injinia Manyanya aliwashauri madiwani na viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kujipanga kuhakikisha wanahamia katika Mji mdogo wa Laela uliopo takribani kilomita 100 kutoka mjini Sumbawanga. Alisema zipo faida kubwa za kufanya hivyo ikiwemo ya halmasahuri kuwa na mji wake watakaouendeleza kisasa na kujiwekea mikakati mbalimbali ya kimaendeleo. Aliongeza pia kuwa itakuwa fursa ya kuwasogezea wananchi huduma.

   Akielezea kuhusu jengo kubwa la kisasa la Halmashauri hiyo linaloendelea kujengwa mjini Sumabwanga alisema linaweza kutumika kama kitega uchumi cha Halmashauri ambapo litawapatia fedha nyingi za kujiendesha na kwamba wataomba fedha nyingine TAMISEMI ya kujenga ofisi kubwa kama hiyo Laela kwa lengo la kuwasogezea wananchi huduma.

  Akizungumzia kilimo na ufugaji aliwataka viongozi wa halmashauri wakishirikiana na madiwani kuhakikisha wanajiwekea utaratibu maalumu wa maeneo ya wakulima na wafugaji na kuhakikisha kunakuwepo na idadi maalum ya mifugo inayotakiwa kufugwa katika maeneo yaliyotengwa na kuwekewa alama maalum za utambuzi.

  Kwa upande wa ONYARU - Ondoa Nyasi Rukwa alisema kuwa mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa kwani maeneo mengi wananchi wamehamasika kwa kuondoa nyasi na kuezeka kwa bati nyumba zao. Aliwataka viongozi na wasimamizi wa halmashauri kuendelea na uhamasihaji huo kuhakikisha nyumba za nyasi zinauhama Mkoa wa Rukwa.  

  0 0

  Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki-Januari 26,Dk. Ali Mohamed Shein, atakuwa mgeni rasmi na kumandi Mahomoud Thabit Kombo

  Dk. Ali Shein kumnadi mgombea Kiembesamaki
  Na Andrew Chale, Zanzibar.

  MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi,  Dk. Ali Mohammed Shein  kesho Januari 26, anatrajiwa kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi mdogo unaoendelea kwenye jimbo hilo. Katika tarifa yake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,  Dk Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa nne wa hadhara kwenye kampeni hizo zinazoendelea.

  Na kuongeza kuwa, Dk. Shein atawahutubia wananchi sambamba na kumnadi, Mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo, anayewania nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la Kiembesamaki. 

  Vuai aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi ilikusikiliza sera na ilani za chama hicho katika utekelezaji wake iliwakichague chama cha Mapinduzi kwa misingi imara ya kuwaletea maendeleo. Aidha, kwa upande wake,  Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa jimbo hilo, kumpigia kura hiyo Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye Baraza la Wawakilishi.

  “Nawaomba Wanakiembesamaki, kutumia fursa ya kipekee ya kunichagua ilikuweza kuwawakilisha kwenye BAraza, hakika  chama chetu ni sikivu na daima kipo na wananchi katika kuwatetea na kuwaletea maendeleo” alisema, Mahmoud.

  Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki, zilianza Januari 21, ambapo zinatarajia kumalizika Februari Mosi, mwaka huu huku wananchi wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari mbili.

  0 0


  Bondia Muss Chitepete kushoto akitunishiana misuli na Ramadhani Shauli wakati wa upimaji wa uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumapili ya january 26 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Dar es salaam.
  Bondia Muss Chitepete kushotoakipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauli kulia
  Mabondia Bakari Magona 'Beka Ostadhi' kushoto akitunishiana misuli na Juma Fundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumapili ya january 26 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0

  Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akikata keki maalumu ya kuchangisha fedha zinazowasaidia baadhi ya wanafunzi wanaokubwa na matatizo ambayo familia zao hushindwa kuwasaidia .
  Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akikata keki maalumu ya kuchangisha fedha zinazowasaidia baadhi ya wanafunzi wanaokubwa na matatizo ambayo familia zao hushindwa kuwasaidia Baadhi ya wanafunzi wa kike waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili suleni hapo walizawadiwa katika hafla hiyo. Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi hao. Baadhi ya wanafunzi wa kike waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili suleni hapo walizawadiwa katika hafla hiyo. Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi hao.
  Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo. Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.

  SHULE ya Sekondari ya Loyola ya Jijini Dar es Salaam leo imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike shuleni hapo kwa kutoa semina mbalimbali kwa wanafunzi wa kike juu ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike na namna ya kukabiliana nazo hasa kwa wanafunzi shuleni. Mada anuai zimetolewa kwa wanafunzi juu ya changamoto zinazowakabili hasa katika kipindi hiki ambacho nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto ya utandawazi. Miongoni mwa watoa mada waalikwa katika maadhimisho ya siku hiyo ni Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambao walitoa mada anuai kwa wanafunzi juu ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili hasa kipindi hiki ambacho wanahudhuria masomo yao.


  Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akilishwa keki na mmoja wa washiriki katika maadhimisho hayo. Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akilishwa keki na mmoja wa washiriki katika maadhimisho hayo.Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri (kulia) akilishwa keki na Mkufunzi Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kwenye hafla hiyo. Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri (kulia) akilishwa keki na Mkufunzi Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kwenye hafla hiyoWanafunzi wa Kidato cha Tano Loyola, wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kulishwa keki ya uchangishaji fedha kwenye hafla hiyo. Wanafunzi wa Kidato cha Tano Loyola, wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kulishwa keki ya uchangishaji fedha kwenye hafla hiyo.Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kulia akizungumza na vyombo vya habari kwenye maadhimisho hayo. Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kulia akizungumza na vyombo vya habari kwenye maadhimisho hayoBaadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Profesa Jeffrey Sachs usiku wa juzi, Jumatano, Januari 22, 2014, wakati wa mjadala kuhusu jinsi ya kuongeza kasi ya mafanikio katika kilimo cha Afrika kwenye Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Taasisi ya Kilimo ya Grow Africa mjini Davos, Uswisi, ikiwa ni moja ya shughuli za Mkutano wa Mwaka 2014 wa Taasisi ya Uchumi Duniani (WEF). Katikati ni Waziri wa Kilimo wa Nigeria Mhe Dr. Akinwumi Adesina. Picha na IKULU

  0 0

    Afisa Mipango Wilaya Kusini Unguja Bw. Faida Khamis Ali akifungua mafunzo ya siku tatu  juu ya uelimishaji wa sheria ya uvuvi kwa wakuu wa madiko na wavuvi,katika skuli ya kitogani Kusini Unguja (kulia) Mratibu wa mradi Bw. Omar Muh'd na (kushoto) ni Makamo M/kiti wa Jumuiya maendeleo ya Wavuvi wa Kojani (KOFDO) Ussi Suleiman. 
   Mkufunzi  Muhammed Kassim (alie simama kulia) akitoa elimu yuu sheria ya uvuvi ya Zanzibar katika mafunzo yaliyo fadhiliwa na the Foundation for Civil Society huko Kitogani Kusini Unguja.

   Baadhi ya washiri wa mafunzo ya uelimishaji wa sheria ya uvuvi wakimsikiliza kwa makini Mkufunzi Muhammed Kassim (hayupo pichani) katika mafunzo juu ya sheria ya uvuvi.
  Mshika Fedha wa Jumuiya maendeleo ya Wavuvi wa Kojani (KOFDO) Faki Othman akichangia katika mafunzo ya sheria ya uvuvi huko Kitogani Kusini Unguja.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  0 0


  0 0

  Mabango Mbeya
  Mbunge wa Mbozi Mashariki, Davi Silinde (Chadema), akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe mjini Mbeya jana.
  Slaa kuhutubia Mbeya 1
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, wakiondoka kwa shamrashamra, baada ya kuhutubia mkutano wa hadahara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
  Slaa na mtoto
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwa amembeba mtoto Sheila Shukurani (3), kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara matika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
  Sugu kuhutubia Mbeya
  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya na vitongiji vyake katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe jana.
  Picha na CHADEMA

  0 0

   Mhandisi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi asili kilichopo katika eneo la Madimba kinachosimamiwa na Shirika la Maendeleo na Petroli Tanzania (TPDC) Sultan Pwaga akitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akitembelea maeneo mbalimbali kinapojengwa kiwanda cha kuchakata gesi asili eneo la Madimba mkoani Mtwara wakati wa ziara yake mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa huo Kapteni mstaafu Joseph Simbakalia, kulia ni Mhandisi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi asili  Sultan Pwaga

   Meneja Mkuu Ujenzi kiwanda cha Dangote Tanzania Bhupendra Sharma akimwonesha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda moja ya mashimo ambapo itafungwa mitambo ya kiwanda cha kutegeneza saruji eneo la Msijute mkoani Mtwara.

   . Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akikagua baadhi ya vifaa ambavyo tayari vimeshafika eneo la Msijute mkoani Mtwara kinapojengwa kiwanda cha saruji cha Dangote Tanzania.
   Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya sekondari Mstafa J.Sabodo wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipowatembelea shuleni humo kuwapa pole kwa msimba wa wanafunzi sita baada ya kugongwa na gari wati wa mchakamchaka karibu na eneo la shulke yao.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda na Mke wake Mama Tunu Pinda wakimjulia hali moja ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mstafa J.Sabodo Chistopher Ngalapa (miaka 16 kidato cha pili) aliyelazwa katika Hospitali ya mkoa wa Mtwara Lugora baada ya kupata ajili tarehe Januari 22, 2014.  (Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO Mtwara ).

  0 0

    Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiapishwa rasmi rais wa nchi hiyo mjini Antananarivo kufuatia ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013.
    Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akisani kiapo chake tayari kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa Madagascar mbele ya Jaji Mkuu wan chi hiyo Jean –Michael Rasolonjatovo (kushoto) wakati wa sherehe za kumuapisha rais huyo zilizofanyika mjini Antananarivo.
   Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akizungumza na wananchi wa Madagascar  waliofurika ndani ya uwanja wa Antananarivo mara baada ya kuapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo mjini.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumuapisha rais mpya wa Madagascar akiwa kwenye jukwaa kuu pamoja na viongozi wengine wa nchi za Afrika waliohudhuria sherehe hizo mjini Antananarivo.Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano, Rais wa Zambia Ipikefunye Pohamba na aliyekuwa rais wa Madagascar Andry Raojolina.
  Viongozi mbalimbali na wanachi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina mjini Antananarivo. 
    Gwaride maalum la jeshi la Madagascar wakati wa sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Hery Rajaonarimampianina.
   Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akikagua gwaride la majeshi ya Madagascar baada ya kuapishwa.
  Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiwasili Ikulu ya nchi hiyo mjini Antananarivo. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO. 
  ========  ========  ========

  TANZANIA KUISAIDIA MADAGACAR KUONDOLEWA VIKWAZO ILIVYOWEKEWA NA JUMUIYA ZA KIMATAIFA.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  26/1/2014, Antananarivo, Madagascar.

  Tanzania imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Madagascar katika masuala mbalimbali  na kuhakikisha kuwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo na jumuiya za kimataifa vinaondolewa kufuatia nchi hiyo kurejesha utawala wa kidemokrasia.

  Akizungumza katika mahojiano maalum  mjini Antananarivo, Madagascar, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe amesema kuwa sasa serikali ya Madagascar imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano sio tu na Tanzania bali nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya za kimataifa.

  Waziri Membe ambaye alikuwa amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Madagascar Bw. Hery Rajaonarimampianina zilizofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Antananarivo jana  amesema kuwa Tanzania imefurahishwa na hatua hiyo na kuongeza kuwa huo ni ushindi mkubwa kwa SADC.

  Amesema kuwa mwaka 2009 Madagascar iliingia katika machafuko yaliyosababisha serikali halali iliyokuwepo madarakani ya Rais Mark Ravalomanana kupinduliwa na kufafanua kuwa Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Kitengo cha Amani na Usalama cha nchi za jumuiya ya SADC (TROIKA) imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa amani ya kudumu inapatikana nchini humo.

  “Kiongozi mpya wa Madagascar aliyepatikana na kuapishwa ni ushindi kwa Tanzania kwa sababu Rais Jakaya Kikwete amejihusisha sana na upatikanaji wa kiongozi huyo, kama tunakumbuka rais Kikwete alimuita nchini Tanzania kwa mazungumzo rais aliyekuwa madarakani Bw. Andry Rajoelina mara nne, mazungumzo haya yamezaa matunda tunayoyaona leo” amesema Mh. Membe.

  Amefafanua kuwa yapo mambo makubwa ambayo Tanzania imeyafanya kufanikisha kupatikana kwa amani ya kudumu nchini Madagascar ikiwemo upatikanaji wa katiba  ambayo ilikamilika mwezi wa 8 mwaka 2013 ,kufanikiwa kuwashawishi Andry Rajoelina na Mark Ravalomanana waliokuwa mahasimu kutoshiriki kugombea katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

  Amesema Tanzania imefurahishwa na kitendo cha rais Andry Rajoelina aliyeingia madarakani kwa kufanya mapinduzi kukubali kuachia madaraka na kuachia utawala wa demokrasia utawale nchini humo.

  Ameeleza kuwa Tanzania sasa iko tayari kushirikiana na Madagascar na kama mjumbe wa SADC itahakikisha kuwa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo vinaondolewa pia kuhakikisha kuwa kiongozi huyo mpya anashiriki mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika utakaoanza tarehe 30 mwezi huu.

   “Tulimwahidi rais aliyekuwa madarakani Bw. Andry Rajolina kuwa atakapotekeleza hayo tunayoyataka ikiwemo kuanzisha mchakato wa katiba,  kuruhusu utawala wa demokrasia, na kuruhusu uchaguzi ili kupata rais mpya sisi tutakuwa mstari wa mbele kushawishi nchi za SADC na nchi za AU kuwaruhusu kushiriki mikutano yote ili waweze kuijenga nchi yao na jambo hilo tutalifanya ” amesisitiza Mh.Membe.

  Katika houtuba yake mara baada ya kuapishwa rais Rajaonarimampianina amesema kuwa utawala wake unaanza ukurasa mpya wa kuijenga upya nchi hiyo iliyokuwa imegawanyika kisiasa na kusababisha chumi wake kudorora huku akiueleza umati mkubwa wa watu waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake kuwa ataongeza mapambano dhidi ya rushwa na kuleta amani, utulivu na maridhiano kwa mustakabali wa taifa hilo.

  Madagascar ambayo sasa inaingia katika utawala mpya wa rais Hery Rajaonarimampianina ambaye hapo awali alikuwa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo iliingia katika machafuko yaliyosababisha kuondolewa kwa utawala wa rais Mark Ravalomanana aliyekimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini.

   Hery Rajaonarimampianina  akiungwa mkono na rais aliyepita Andry Rajoulina anakuwa rais wa 4 wa nchi hiyo  kufuatia ushindi  mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013 uliompatia  asilimia 53.3  dhidi ya mpinzani wake Bw. Jean Louis Robinson aliyepata asilimia 46.5.

  0 0

  Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya PSPF TANZANIA BOXING AWARDS wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia wakati wa utoaji wa tuzo.
  Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia akimkabidhi tuzo ya bondia bora wa mwaka 2013 kwa ngumi za kulipwa  Francis Cheka wakati wa utoaji tuzo za PSPF BOXING AWARDS zilizofanyiaka katika ukumbi wa PTS.
  Promota wa masumbwi Mohamed Bawazir akimpatia tuzo ya uandishi bora wa mchezo wa masumbwi Mwali Ibrahimu katikati ni Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis .
  Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia ajkiwa na Zuwena Kipingu ambaye ni Mjumbe wa shirikisho la ngumi za ridhaaa nchini BFT.  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com.
  Meneja Mpango wa Uchangiaij wa hiyari kutoka PSPF ,Mwanjaa Sembe kushoto akimpatia ya upiga picha bora wa mchezo wa masumbwi pamoja na uhamasishaji mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa utoaji wa Tuzo hizo kwa mabondia zilizofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es  salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia akimkabidhi tuzo ya bondia bora wa mwaka 2013 kwa ngumi za ridhaa  Gelvars Rogasian wakati wa utoaji tuzo za PSPF BOXING AWARDS zilizofanyiaka katika ukumbi wa PTS Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


  Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia akiwa na Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia
  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia akiwa na Fransic Cheka
  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Tuzo iliyochukuliwa na Rajabu Mhamila Super d
  Rais wa PST Emanuel Mlundwa kushoto akimpatia tuzo ya Bondia bora wa mwaka Bilali Ngonyani kwa niaba ya Ibrahimu Class King Class Mawe

  Aga Peter akimpatia tuzo Franscis Cheka

  Mdau wa masumbwi Aga Peter akimkabidhi tuzo Fadhili Majia kulia ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Rashidi Matumla akimpatia tuzo Fadhili Majia


  Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia ajkiwa na Zuwena Kipingu ambaye ni Mjumbe wa shilikisho la ngumi za ridhaaa nchini BFT wakipiga picha ya pamoja na hadija Khopa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  kocha wa timu ya Taifa Jonas Mwakipesile akimkabidhi tuzo Selemani Kidunda
  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kushoto akimkabidhi tuzo kocha wa timu ya Taifa Jonas Mwakipesile picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


  0 0   Soulful Vocals,Hypnotic Guitars and the driving Extraordinary rhythm of the "Bongo Dance" from East Africa

   The NGOMA AFRICA BAND; known as the (Golden Voice of East Africa) or " FFU- Field force unit" is one of the few amongst african bands in Germany to have touched hearts and left audience dancing and week in the knees.

   Founded in 1993 and led by Tanzanian musician borned Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja - "King of Anunnaki".

  Every concert is unique, uniting the audience after a few minutes on the dancing floor.
  Bongo Dansi –meaning Dance able east african dance, is the "Extraordinary Rhythm" that describes the NGOMA AFRICA BAND and makes the band the people´s choice.

  Baptized under different names by excited fans – the Annunaki empire, FFU –Field Force Unit. The NGOMA AFRICA BAND has succesfully written and released several hits amongst others the latest "Bongo Tambarare", repertoires mostly in the native Tanzania and east african Kiswahili language.

  Under the leadership and great visionary-Ebrahim Makunja AKA -Kamanda Ras Makunja; the NGOMA AFRICA BAND comprises of africa´s young and most talented musicians, drummers,guitarists bassist,percussionist, dancers amongst others multi-talented  soloist –Christain Bakotessa aka "Chris-B"  Mo Benda,Jessy Ouyah, Flora William, Jonathan Sousa aka "Jo Jo" ,Aj Nbongo making the NGOMA AFRICA BAND a complete travel party of eight vibrant musician and dancers.

  Book The NGOMA AFRICA BAND and experience the extraordinary sensational Bongo dansi from East Africa´s best dancable music, best for indoor and outdoor festival and events of all kinds! Give your audience the best of Africa this season with the NGOMA AFRICA BAND

  Click here for more and listen www.ngoma-africa.com.

older | 1 | .... | 209 | 210 | (Page 211) | 212 | 213 | .... | 1898 | newer