Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 208 | 209 | (Page 210) | 211 | 212 | .... | 1904 | newer

  0 0

   Mkuu Wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(Katikati) akishirikiana na Msimamizi wa Duka jipya la Vodacom Kinondoni Donart Alwatani kukata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa huduma kwenye duka hilo jipya lililopo eneo la Kinondoni Manyanya Dar es salaam. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Duka hilo litakuwa likitoa huduma kwa siku saba za wiki ikiwemo siku za sikukuu.
   Mkuu wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa Vodacom Tanzania,Bi.Upendo Richard (wa pili kushoto) akiwawekea Shampeni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa tatu kushoto) na Msimamizi wa Duka jipya la Vodacom lililopo Kinondoni Manyanaya Jijini Dar es salaam Donard Alwatani  ikiwa ni ishara ya kulitakia mafanikio duka hilo mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Anaeshuhudia ni Meneja Uhusiano kwa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
   Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(katikati) akiwa kwenye furaha baada ya kufungua Shampeni kuashiria kuanza rasmi kwa huduma katika duka jipya la kampuni yake lilipo Kinondoni Manyanya  Dar es salaam. Kutoka  kulia ni Msimamizi wa duka hilo Donart Alwatani, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Mkuu wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa Vodacom Upendo Richard na Meneja katika idara hiyo Elihuruma Ngowi.
   Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (wa kwanza kushoto) akitaniana jambo na Mkuu wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa kampuni hiyo Upendo Richard huku wakiwashuhudia Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Msimamizi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo Kinondoni Manyanya jijini Dar es salaam wanavyogida kinywaji cha Shampeni ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa duka hilo.


  Hili ndilo Duka jipya la Vodacom lililopo Kinondoni Manyanaya Jijini Dar es salaam.

  0 0

   Msanii wa Maigizo Tanzania Steve Mongere aka Steve Nyerere akisalimiana na Mwendesha Kipindi cha The Mboni Show , Mboni Masimba (Wa Kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili ndani ya mjengo ambapo kipindi hiko hurekodiwa Pembeni ni Msanii nguli wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael "Lulu" akifuatiwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa Filamu za Kitanzania Nchini.

  Msanii Nguli na mahiri aliye chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited Elizabeth Michael "Lulu" akisikiliza kwa makini wakati msanii mwenzie Steve Nyerere alipokuwa akiongea katika kipindi cha The Mboni Show
   Mwendeshaji wa Kipindi cha The Mboni Show Mboni Masimba (Wa Kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Muigiza Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu aliye chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited mara baada ya kipindi kumalizika
   Meneja masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Evance Steven akiwa tayari kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Mwendesha Kipindi Cha The Mboni Show, Mboni Masimba wakati wa kurekodi kipindi hiko kitakachorushwa leo Alhamisi
   Muigiza wa filamu za vichekesho Steve Mogere "Nyerere" akieleza mikakati yake na filamu zake mpya alizotoa akiwa chini ya Kampuni ya Utengenezaji, Usambazaji na Uuzaji wa Filamu za Kitanzania ya Proin Promotions Limited wakati wa kipindi cha the Mboni Show kitakachorushwa hewani leo
   Mboni Masimba, mwendeshaji wa Kipindi cha the Mboni Show akimsikiliza Steve Nyerere kwa umakini wakati msanii huyo wa vichekesho alipokuwa akielezea Mikakati yake katika Mwaka huu na juu ya filamu zake alizozitoa akiwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited 
   Mwendeshaji wa kipindi cha the Mboni Show, Mboni Masimba (wa kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni aliowaalika katika kipindi chake cha The Mboni Show kitakachorushwa leo usiku. Kutoka Kulia Ni Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Evance Stephen, Msanii Nguli na Mahiri Elizabeth Michael aka Lulu na Steve Mongere aka Steve Nyerere.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  0 0

  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Isilowaya iliyoko kata ya Ilula wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakiwa wamekaa katika baadhi ya madawati 30 yaliyotolewa na Faidika. (Picha na Denis Mlowe)
  =======  ======  ========
  WAASWA KUACHA KUSUBIRI WAHISANI KUTOA MISAADA

  Na Denis Mlowe,Iringa.


  WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kumaliza matatizo yao ya ndani badala ya kusubiri wahisani kufanya hivyo kama sehemu ya kushiriki moja kwa moja katika juhudi za ujenzi wa Taifa .


  Changamoto hiyo imetolewa Meneja wa mikoa ya Iringa na Njombe wa Taasisi mikopo Faidika, Elisha Mboka wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa madawati 30 yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa shule ya msingi ya Isoliwaya iliyopo kata ya Ilula mkoani Iringa.


  Mboka alisema wakati umefika sasa kwa watanzania kuona umuhimu kusaidia juhudi za kumaliza changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii badala ya kuendelea kuwa tegemezi kwa misaada ya wahisani ambayo siku zote inakuwa na masharti ndani yake.


  "Ndugu zangu sisi kama watanzania na kama sehemu ya jamii hii hatuna budi kutoa mchango wa dhati kwa taifa letu na jamii yetu. hakuna siku mtu kutoka nje ya jamii yetu na taifa letu atawajibika moja kwa moja na matatizo yetu. ni lazima tuwe wazalendo na kuepuka kuwa wanafiki kwa maendeleo yetu wenyewe"


  Aidha aliitaka Serikali na jamii kwa ujumla kuelekeza juhudi zake katika maboresho ya mfumo wa elimu nchini kwani kwa kufanya kutasaidia tanzania kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka zaidi kuliko ilivyo sasa.


  kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Isoliwaya Asifiwe Mwagike alisema kwa muda mrefu shule yake imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa madawati, matundu ya vyoo na nyumba za walimu na kuwashukuru shirika la Faidika kwa msaada huo wa madawati. 

  0 0

  Timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na Taswa Queens siku ya Jumamosi, zitapamba bonanza la muziki la bendi ya Msondo Ngoma kwa kupambana na timu za veterans za Bandari wanaume na wanawake.
  Mchezo huo umepangwa kufanyika kwenye uwanja wa TCC, Chang’ombe kuanzia saa 8.00 mchana na maandalizi yake yamekamilika kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary. Majuto alisema kuwa mechi hizo zinatarajiwa kuwa ngumu na za kusisimua kutokana na rekodi ya timu zote mbili.
  Majuto alisema Taswa FC na Taswa Queens hazijawahi kupoteza mechi yoyote mwaka uliopita na kuweza kutwaa vikombe mara mbili mkoani Arusha na hivi karibuni waliweza kuzichapa timu ya wanamuziki wa Twanga Pepeta, Kombaini ya Leaders Club na shirika la maendeleo ya mafuta (TPDC).
  Alisema kuwa timu zake zitakuwa zinacheza kwa mara ya kwanza mwaka huu kwenye uwanja wa TCC na hivyo mashabiki watarajie kupata burudani safi ya mpira na muziki kutoka kwa bendi ya Msondo Ngoma ambayo itatambulisha nyimbo zake mpya ambazo zitakuwa zinatambulishwa kwa mara ya kwanza.
  “Tutaanza kutoa burudani kwa mashabiki na baadaye kuamia kwa Msondo Ngoma, tunatarajia kuwapa burudani safi ambayo itakuwa ya kwanza mwaka huu, mbali ya mechi yetu, timu ya Mass itapambana na Farion, ambapo timu ya maveterani wa Temeke inayojiita kwa jina la Kamazamani itapambana na timu ya Tall, “ a;isema Majuto.
  Wakati huo huo; bendi ya Msondo ngoma na Twanga Pepeta, jumapili zitatumbuiza jukwaa moja kwenye ukumbi wa CCM Kata 14, Temeke. Burudani hiyo itakuwa ya kwanza mwaka huu kwa wakazi wa Temeke na vitongoji vyake kwa bendi hizo kupiga pamoja. Twanga itaonyesha shoo na nyimbo zake mpya.

  0 0
 • 01/23/14--08:13: KUMEKUCHA MBALAMWEZI


 • 0 0


  Bondia Abuu Abas kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Zugo wakati wa uhamasishaji wa tuzo za PSPF Boxing Award zilizofanyika katika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es salaam tuzo hizo zinafika tamati january 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Zugo alishinda kwa K,o ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Hamisi Mpili kushoto akichuana na Khalfani Jumamane wakati waq mpambano wa uhamasishani wa tuzo za PSPF Tanzania Boxing Awards zinazofika tamati january 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba jumanne alishinda kwa point mpambano huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  MJUMBE WA BFT AISHA MZUNGU AKISALIMIA MASHABIKI WALIOJITOKEZA KATIKA KUANGALIA MIPAMBANO YA MASUMBWI YA KUHAMASISHA TUZO ZA BOXING AWARDS KATIKA VIWANJA VYA zakhem mbagala kushoto ni mjumbe mwingine Zuwena Kibena 'Mama Zugo'

  wajumbe wa shilikisho la ngumi za ridhaa wakifatilia mpambano wa masumbwi kutoka kushoto ni Asisha Mzungu, Zuwena Kipingu 'Mama Zugo' na Antoni Mwangonda

  Rais wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchin Mutta Rwakatale akisalimiana na mjumbe wa shilikisho hilo Zuwena Kipingu

  Rais wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchin Mutta Rwakatale akisalimiana na mjumbe wa shilikisho Aisha Mzungu  WANDISHI WA HABARI WAKIFATILIA MPAMBANO WA MASUMBWI

  BAADHI YA MASHABIKI WALIOJITOKEZA KWENYE VIWANJA VYA ZAKHEM MBAGALA KUANGALIA BURUDANI ZA MASUMBWI

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Massele akifuatilia maelezo toka kwa wajumbe toka Jamhuri ya Czech walipofika ili kuanzisha ushirikiano wa kibiashara katika sekta za nishati na madini  kati ya Tanzania na  Czech. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Jamhuri ya Czech Mhe. Tomas Dub na kushoto kwake ni Kamishna msaidizi wa madini anayeshughulikia leseni Injinia John Nayopa.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akimsikiliza kwa makini Naibu waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Czech Bw. Tomas Dub alipoongoza ujumbe toka nchi yake ili kuja kuanzisha ushirikiano baina ya Tanzania na  Czech hususan katika masuala ya uwekezaji sekta za nishati na Madini. Kushoto kwake ni Kamishna wa Madini anayeshughulikia leseni Injinia John Nayopa.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele katika picha ya pamoja na ujumbe toka jamhuri ya Czech mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na madini.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akiagana na Naibu waziri wa Mambo ya nje wa Jamhuri ya Czech Bw. Tomas Dub mara baada ya kumaliza kikao kifupi kilichofanyika ofisini kwake.  Ugunduzi wa gesi na mafuta wavuta mataifa ya mbali kutafuta fursa za kuwekeza nchini.


  Kutokana na ugunduzi wa gesi asilia na mafuta nchini, Tanzania imeonekana kuwa na thamani kwa nchi mbalimbali duniani na  kuiangalia nchi hii kwa namna tofauti na ilivyokuwa awali kwani sasa imeonekana kuwa na utajiri mkubwa.


  Ugunduzi huu umepelekea Wizara ya Nishati na Madini kupokea wageni wanaowakilisha nchi na watu binafsi wanaofika ili kutafuta fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano ya kibiashara baina ya nchi husika.


  Hivi karibuni wizara ya  Nishati na Madini imetembelewa na ujumbe toka Jamuri ya Czech nchi ndogo miongoni mwa nchi zinazounga umoja wa ulaya waliofika kwa lengo la kutafuta fursa za kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kudumisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.


  Ujumbe huu uliongonzwa na  Bw. Tomas Dub Naibu Waziri wa mambo ya Nje ya Nchi ya Czech aliyeelezea uwezo wa nchi yake katika masuala ya nishati na madini na kusema kwamba awali nchi yao ilijikita katika umeme uliozalishwa kwa maji, gesi  pamoja na nishati jadidifu, na kusema kwamba wana wataalamu wa kutosha katika sekta ya nishati.


  Dub alieleza kuwa maendeleo si tu kutegemea utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia bali inatakiwa nchi ifanye nguvu ya ziada katika kuongeza thamani ya bidhaa hiyo na hilo litawezekana tu kwa kujenga viwanda jambo lililowavuta ili kuja kutafuta fursa hiyo nchini.


  Dub alikamilisha mahojiano hayo kwa kuitaka Wizara  kuelimisha watanzania katika chuo cha madini katika nchi hiyo na kwamba mawasiliano yataendelea kufanyika ili kufikia malengo ya uhusiano huo.


  Kwa upande wake Masele amesema kwamba zipo fursa nyingi  za uwekezaji nchini katika sekta ya madini  na zaidi madini ya viwandani lakini pia sekta ya nishati kwa kufuatia ugunduzi wa gesi na mafuta vitalu vimetangazwa hivyo ni fursa kwa Czech kuomba vitalu hivyo ili kuweza kushiriki katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi.
  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi  ya uboreshaji wa kilimo uliofanyika  Davos Uswisi usiku wa kuamkia leo Januari 23, 2014
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe.  Niuck Clegg walipoikutana na kufanya mazungumzo katika hoteli ya Sheraton  Davos, Uswisi Janaury 23, 2014
    Rais Jakaya Mrisho Kiwete kutana na kufanya mazungumzo na  Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya JETRO ya Japan katika hoteli ta Sheraton Davos,  Uswisi, January 23, 2014
    Rais Jakaya Mrisho Kiwete kutana na kufanya mazungumzo na  Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya JETRO ya Japan katika hoteli ta Sheraton Davos,  Uswisi, January 23, 2014
      Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani (USAID) Mhe Rajiv Shah katika ukumbi wa mikutano wa Davos, Uswisi, January 23, 2014
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani (USAID) Mhe Rajiv Shah katika ukumbi wa mikutano wa Davos, Uswisi, January 23, 2014
   Rais Jakaya Kikwete akishangiliwa baada ya kuhutubia wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi  ya uboreshaji wa kupatikana na kulinda maji nsalama kwa miaka ijayo  katika hoteli ya Derby huku  Davos  Uswisi  Januari 23, 2014. PICHA NA IKULU.

  0 0

        Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo ofisini kwake jijijni Dar es Salaam mara baada ya kurudi kutoka Mkoa wa Morogoro alipokwenda kutembelea wananchi waliokumbwa na mafuriko yaliyotokea jana. Mafuriko yalisababisha wanachi kukosa huduma za jamii ikiwemo usafiri wabarabara kutoka Dodoma kuja Morogoro na Morogoro kwenda Dodoma.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijijni Dar es Salaam juu namana Wilaya za Gairo na Kilosa zilivyoathirika  na mafuriko yaliyotokea mkoani Morogoro ambapo usafiri unatarajiwa kurudi katika hali yake ya kawaida takribani baada ya siku tatu hadi nne. (Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)

  0 0

   Aliyekua Naibu Waziri wa Nishati na Madini akisimamia Nishati,Mhe. George Simbachawene (wa tatu kushoto) akikabidhi majukumu ya ofisi kwa Naibu Waziri Mpya wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga katika hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye Ofisi za Wizara ya Nishani na Madini,jijini Dar es Salaam.wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo.
  Aliyekua Naibu Waziri wa Nishati na Madini akisimamia nishati, Mhe. George Simbachawene akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri Mpya wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga.

  Na Asteria Muhozya

  Aliyekua Naibu Waziri wa Nishati na Madini akisimamia nishati Mhe. George Simbachawene amemkabidhi majukumu ya ofisi Naibu Waziri Mpya wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga ambaye atashughulikia Nishati.

  Wakati akimkabidhi majukumu hayo, amemmtaka Naibu huyo kuhakikisha anasimamia suala la usambazaji wa umeme vijijini kwa kushirikiana na Wakala wa umeme Vijijini (REA) ili kukamilisha ghughuli hiyo kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kukamilisha majukumu mengine ambayo ameyaacha akiwa bado hajayakamilisha.

  “Namwaachia ofisi yangu mtu mzoefu, na anayejua kazi kuliko mimi naamini ataendeleza kile ambacho nimekiacha. Alisema Simbachawene.

  Akizungumzia majukumu yake mapya katika Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi , ameeleza kuwa, anaamini atatekeleza majukumu yake vizuri kutokana na kuwa na elimu na ujuzi wa masuala ya Sheria ya Ardhi na Utawala hivyo anaamini atayasimamia majukumu yake mapya vizuri.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayesimamia madini Mhe. Charles Kitwanga, ameishukuru Wizara kwa mapokezi aliyoyapata Wizarani hapo ikiwa ni pamoja na kukabidhiwa majukumu yake mapya aliyopewa na hivyo, kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kukamilisha yale ambayo amekabidhiwa.

  “Nilipoteuliwa nilistuka kidogo, lakini baada ya kushiriki kongamano la viongozi wa dini lililo jadili masuala ya rasilimali hizi za gesi,mafuta na madini na taarifa mlizonipatia kuhusu nini natakiwa kukisimamia sasa nipo tayari kuanza kazi’’. Alisema Kitwanga.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, amemkaribisha Waziri huyo na kueleza kuwa, wanatarajia ushirikiano mzuri kwa kuwa anaamini anao uzoefu na uwezo mzuri utakaosaidia kukamilisha majukumu yake aliyokabidhiwa ambayo kwa kiasi kikubwa yanagusa masuala ya msingi yanayohusu maendeleo ya Taifa na Watanzania.

   Na Asteria Muhozya

  Aliyekua Naibu Waziri wa Nishati na Madini akisimamia nishati   Mhe. George Simbachawene amemkabidhi majukumu ya ofisi Naibu Waziri Mpya  wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga ambaye atashughulikia Nishati.


  Wakati akimkabidhi majukumu  hayo, amemmtaka Naibu  huyo kuhakikisha anasimamia suala la usambazaji wa umeme vijijini  kwa kushirikiana na  Wakala wa umeme Vijijini (REA)  ili kukamilisha ghughuli hiyo kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kukamilisha majukumu mengine ambayo ameyaacha akiwa bado hajayakamilisha.


  “Namwaachia ofisi yangu mtu mzoefu, na anayejua kazi kuliko mimi naamini ataendeleza kile ambacho nimekiacha. Alisema Simbachawene.


  Akizungumzia   majukumu yake  mapya katika Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi , ameeleza kuwa,  anaamini atatekeleza majukumu yake vizuri kutokana na kuwa na elimu na ujuzi wa masuala ya Sheria ya Ardhi  na Utawala hivyo anaamini atayasimamia majukumu yake mapya vizuri.


  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayesimamia madini Mhe. Charles  Kitwanga, ameishukuru Wizara  kwa mapokezi aliyoyapata Wizarani hapo ikiwa ni  pamoja na kukabidhiwa majukumu yake mapya aliyopewa  na hivyo,  kuahidi  kufanya kazi kwa ushirikiano   ili kukamilisha yale ambayo amekabidhiwa.


  “Nilipoteuliwa nilistuka kidogo, lakini baada ya kushiriki kongamano la viongozi wa dini  lililo jadili masuala ya rasilimali hizi za gesi,mafuta na madini  na taarifa mlizonipatia kuhusu nini natakiwa kukisimamia sasa nipo tayari kuanza kazi’’. Alisema Kitwanga.  Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, amemkaribisha Waziri huyo na kueleza kuwa, wanatarajia ushirikiano mzuri kwa kuwa anaamini anao uzoefu na uwezo mzuri utakaosaidia kukamilisha majukumu yake aliyokabidhiwa ambayo kwa kiasi kikubwa yanagusa masuala ya msingi yanayohusu maendeleo ya Taifa na Watanzania.


  0 0

  MRADI WA FLAVIANA MATATA FOUNDATION WA BACK TO SCHOOL PROJECT ILIOFADHILIWA NA MFUKO WA PENSHENI PSPF ILIYOMALIZIKA WIKI ILIYOPITA IVYOENDA ALIANZIA KISARAWE KATIKA SHULE YA MSINGI YA CHANZIGE B NA KISHA SHULE YA MSINGI YA KIMANZICHANA ILIYOPO WILAYA YA MKURANGA NA SHULE YA MSINGI MSINUNE ILIYOKO WILAYA YA BAGAMOYO.

  SHUKRAN ZA PEKEE KWA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF NA KUUNGANA NA FLAVIANA MATATA FOUNDATION NA KUSAIDIA VIFAA HIVI KWA WANAFUNZI 1000 KWA KUANZIA KUNA VINGINE VITAPELEKWA MIKOANI, TUTAENDELEA KUHABARISHANA HAPAHAPA, NA ZOEZI HILI NI ZOEZI ENDELEFU, NDIO MAANA TUNAKARIBISHA WADAU TUFAUTI TOFAUTI, KUHAKIKISHA WANAFUNZI HAWA WANAFIKIA MALENGO NA KULETA MABADILIKO KATIKA TAIFA Flavian matata foundation-kisarawe (21 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (13 of 152)
  HAPA ILIKUWA KWA AFISA ELIMU WA WILAYA YA KISARAWEFlavian matata foundation-kisarawe (17 of 152)
  HAWA KIKEKE AFISA MAWASILIANO KUTOKA PSPF AKIFAFANUA JAMBOFlavian matata foundation-kisarawe (19 of 152)
  ITIFAKI ILIZINGATIWA KILA ALIKOPITA ILIBIDI ASAINI DAFTARI ILI KUTAMBUA UWEPO WAKE
  Flavian matata foundation-kisarawe (28 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (33 of 152) AHSANTE KWA KUTUPOKEA

  Flavian matata foundation-kisarawe (34 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (39 of 152) MENEJA WA KANDA YA PWANI NAE ALIPATA FURSA YA KUMPA ZAWADI YA MWAKA MPYA Flavian matata foundation-kisarawe (40 of 152)  TUKAFIKA CHANZIGE B SHULE YA MSINGI ILIYOPO WILAYA YA KISARAWE Flavian matata foundation-kisarawe (52 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (53 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (59 of 152)  SAMBAMBA NA MKUU WASHULE YA MSINGI CHANZIGE B ISAAC ELIAH, ALIFURAHISHWA NA UJIO HUU SABABU ANAMTAMBUA NA ANAMFUATILIA FLAVIANA MATATA KATIKA HARAKATI ZAKE ZA UANAMITINDO   Flavian matata foundation-kisarawe (61 of 152) WALIMU WA CHANZIGE BFlavian matata foundation-kisarawe (64 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (72 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (75 of 152)  ALIKARIBISHWA NA JIVING YA NGUVU AKAKUMBUKIA ENZI ZAKEE Flavian matata foundation-kisarawe (86 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (91 of 152) KIKAZI ZAIDI Flavian matata foundation-kisarawe (82 of 152) TEEEPE TEEPPEEE, IYAMBA NA KUSELELAA TEEPE TEPEE SEEELLAAA...ndo nilichokuwa nasikia hapo Midundo makofi na mshindo wa miguu yao Flavian matata foundation-kisarawe (103 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (105 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (110 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (118 of 152) ZOEZI LA UGAWAJI MABEGI YENYE VIFAA VYA SHULE ALILISIMAMIA MWENYEWE FLAVIANA MATATAFlavian matata foundation-kisarawe (119 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (122 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (123 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (125 of 152)    HII NI SHULE YA MSINGI KIMANZICHANA, MBALIA NA KUGAWA SCHOOLKIT ,AMBAYO ILIHUSISHA BEGI LENYE MADAFTARI 12, MKEBE,PEN NA PENSELI, PILA FLAVIANA MATATA FOUNDATION PIA LIMEGUNDUA KUNA UMUHIMU KWA WANAFUNZI HAWA KUPATIWA UNIFORM, SABABU WENGINE HAWANA VIATU, WENGINE SARE ZA SHULE WANAVAA PAPA NA NGURU...HIVYO WADAU NA SEKTA MBALIMBALI MNAWEZA KUTUMIA HII FURSA KUUNGANA NA FLAVIANA MATATA ILI KUWEZA KUPUNGUZA KAMA SI KUTOKOMEZA KABISA HILI TATIZO NA KUFANIKISHA ELIMU BORA KWA WATOTO WETU, HASA HASA WALIO PEMBEZONIFlavian matata foundation-kisarawe (136 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (137 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (138 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (139 of 152)
  MIFUKO MINGI NI YA RAMBO (MIFUKO YA PLASTI Lol ) HIVI HII MIFUKO ILIITWA RAMBO KUTOKANA NA ILE YA ZAMANI KUWA INACHORWA PICHA YA YULE MUIGIZA SINEMA AU NDO JINA LAKE ?
  Flavian matata foundation-kisarawe (140 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (141 of 152)Flavian matata foundation-kisarawe (142 of 152)   
  UNAWEZA ONA WENGINE WAKO PEKU NA WENGINE WAKIWA NA YEBO YEBO NA UNIFORM CHAKAVU.....KUNA UMUHIMU WA KUSAIDIA HILI
  NA SIKU YA JUMATATU TULIMALIZIA WILAYA YA BAGAMOYO KATIKA SHULE YA MSINUNE
  Flavianamatata msinune primaryflavianamatatamsinune
  IMG_0322IMG_0328IMG_0331IMG_0338IMG_0339
  SHUKRAN ZA PEKEE KWA MFUKO WA PENSHEN WA PSPF NA KUUNGANA NA FLAVIANA MATATA FOUNDATION NA KUSAIDIA VIFAA HIVI KWA WANAFUNZI 1000, NA ZOEZI HILI NI ZOEZI ENDELEFU, KUNA AMBAYO YATASAMBAZWA MIKOANI, AMBAYO YAMECHANGIWA NA RUSSEL SIMON MAARUFU KAMA ANCLE RUSH AMBAYO YATAENDA MIKOANI NA ZOEZI HILI LITAENDELEA TENA MWEZI YA JULAI PINDI SHULE ZITAKAPOFUNGULIWA TENA
   


  0 0

  Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (kushoto) akikabidhi masaada wa unga wa sembe kwaajili ya uji wa wanafunzi shule ya msingi Levolosi. Wanao pokea ni Mwenyekiti Kamati ya Shule, Edward Ngomuo (kulia) Mwalimu Mkuu Shule ya Luvolosi, Elisante Kaaya na Mwalimu wa Chakula shuleni hapo, Frida Mallya.
  Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (wapili kushoto) akimuweka katika kiti maalum cha magurudumu, motto mlemavu Hassan Ramadhani (10) mkazi wa Luvolosi mjini Arusha jana. Wanaoshuhudia ni mama mzazi wa motto huyo, Hadija Hassan na Mwalimu Mkuu Elisante Kaaya wa Shule ya Msingi Luvolosi.
  *********
  JAMII imetakiwa kuwa na moyo wa kujitolea na kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii hasa wanawake na watoto ili kujenga taifda lenye matumaini na amani.

  Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation, ya jijini Arusha, Catherine Magige wakati akikabidhi msaada wa unga wa sembe na sukari kwaajili ya kuwapikia uji wanafunzi zaidi ya elfu moja katika shule ya Msingi Levolosi ya mjini hapa kwa muda wa mwezi mmoja.

  Magige ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM) mkoa wa Arusha, amesema kila mtu anapswa kujipima kwenye mizani ya ubinadamu, kujitafakari na pia kujiuliza maswali magumu kwenye nafsi yake, kwamba, katika kipindi kifupi cha uhai wake, ameacha nyuma matunda ya aina gani.

  “Tunapaswa tusambaze mbegu za matunda ya amani na upendo na si mbegu za machafuko…kwani ndio mbegu ambazo sote tunapaswa kuzisambaza na kuzipanda ili kujenga taifa lenye matumaini na amani,”alisema Magige.

  Ni ukweli usio pingika kuwa watoto wetu hawa tusipo wawezesha kupata elimu sasa basi tutakuwa tumejingeneneazea wenyewe taifa la watu mbumbumbu na wasio na ujuzi wa kufanya jambo lolote jema na matokeo yake wataishia katika magenge ya uhalifu na watumiaji wa madawa ya kulevya.

  Magige amesema ili watoto wafanye vizuri darasani wanahitaji kushiba na si familia zote zinamudu kuwapa chakula watoto wao kabla ya kwenda shule hivyo taasisi yake ya Catherine Foundation imeona ichangie kulisha watoto hao kwa mwezi mmoja.

  “Sisi kama wazazi hatuna budi kusaidia wazazi wengine ambao wanania njema na watoto walio wazaa isipokuwa uwezo ndio unawakwamisha katika kutimiza malengo yao ya kuwasaidia watoto wao katika elimu,” alisema Magige.

  Aidha amesema utaratibu wa kuwapa watoto chakula shule utaongeza kiwango cha usikivu wa wanafunzi darasani na kuongeza ufaulu huku ukupunguza tatizo la utoro mashuleni ambalo limekithiri katika shule nyingi nchini.

  “Kufanya hivi situ watoto watakuwa wasikivu darasani bali hata kuchangia kwa kiwango cha ufaulu darasani na ni wazi kuwa hata mahudhurio yataongezeka shuleni hapa,” alisema Magige.

  Pia amewataka wanafunzi wanafunzi kukazania masomo yao darasani, kudumisha nidhami mingoni mwao huku akiwataka walimu kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwapa elimu bora na malezi stahiki watoto hao na maadili mema.

  Mapema katika hotuma yake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Levolosi, Elisante Kaaya alisema shule hiyo ina wanafunzi 1,029 na gharama za kuwalisha kwa mwaka zinakadiriwa kuwa zaidi ya Sh Milioni 10.

  Aidha Mwalimu Kaaya alisema kuwa ili kufanya zoezi hilo la kuwapa uji au chakula wanafunzu linaendelea wameazimia kuwashirikisha wazazi na wadau wengine wa elimu ili uwe endelevu na wenye kuleta tija.  Ofisa wa Catherine Foundation Lucy Bongole akizungumza jambo kabla ya makabidhiano kuanza.
  Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Levolosi, Elisante Kaaya akitoa maelezo ya shule hiyo na mpango wa kuwapa uju wanafunzi wanafunzi 1,029 na gharama za kuwalisha kwa mwaka zinakadiriwa kuwa zaidi ya Sh Milioni 10.
  Juice zikigawiwa kwa wanafunzi.
  Mwenyekiti wa Shule ya Msdingi Levolosi ya jijini Arusha, Edward Ngomuo akisema neno.
  Mwenyekiti wa Catherine Foundation na Mbunge wa viti Maalum Arusha, Catherine Magige akigawa juice kwa wanafunzi.
  Mwenyekiti wa Catherine Foundation na Mbunge wa viti Maalum Arusha, Catherine Magige akizungumza.
  Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (kushoto) akikabidhi masaada wa unga wa sembe kwaajili ya uji wa wanafunzi shule ya msingi Luvolosi ya mjini Arusha jana. Anaeshuhudia ni Mwalimu Mkuu Elisante Kaaya.
  Wazazi na walimu wakipokea unga na sukari
  wanafunzi nao wakipokea
  Wawakilishi wa wazazi wakipokea msaada huo.
  Mwalimu wa Chakula shuleni hapo, Frida Mallya akitoa neno la shukrani kwa taasisi ya Catherine Foundation.
  Mwenyekiti wa Catherine Foundation, Catherine Magige akiagana na wanafunzi.

  0 0
 • 01/24/14--02:13: PONGEZI KWA FLAVIANA MATATA
 • Kwanza kabisa naanza kumpongeza mdogo wangu Flaviana kwa kazi nzuri anayofanya ya kusaidia jamii hasa kupitia mfuko wake wa Flaviana Matata Foundation wa kusaidia watoto ili waweze kuipenda shule zaidi.

  Sasa nilikuwa naomba tena aongeze na jingine hasa nilikuwa na mkubunsha kuikumbuka jamii ya kabira ya Wanyambo wanaopatakana mkoa wa kagera wilaya ya karagwe na Kyerwa kama sikosei ndilo kabila lako. kumekuwa na tabia kukatishwa masomo watoto wa kike hasa wanaosoma sekondari kwa kweli hilo ni tatizo la wilaya zetu.

  Kwa sababu amesema tumuunge mkono naomba na hilo aliweke kwenye program yake ilii mfuko wake uweze kulifanyia kazi. watoto wa kike wamekuwa wakikatishwa masomo kwa kubebwa kwa lazima (yaani mtu anaoa kwa lazima ) naomba kupitia mfuko wako tulipige vita ni tabia ambayo imeishapitwa na wakati.

  mdau
  Elewa
  Karagwe

  0 0

  Na Andrew Chale, Zanzibar
  CHAMA cha Mapinduzi CCM, leo Januari 24, kinatarajia kufanya kampeni yake ya tatu ya mkutano wa hadhara kwenye eneo la Buyu Pwani, katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki,  ambapo mgeni rasmi wa kumnadi Mgombea anatarajiwa kuwa, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Jumuiya ya CCM (UVCCM)  na  (MNEC), Ndugu.  Shaka Hamdu Shaka.

  Akielezea mkutano huo wa tatu wa hadhara, unaotarajiwa kuwa majira ya Saa kumi jioni, eneo hilo la Buyu- Chukwani, Mahmod Thabit Kombo ,  aliwaomba wananchi wa Buyu kujitokeza kwa wingi ilikumsikiliza na kuzijua sera za Chama katika kuwaletea maendeleo.

  “Leo Januari 24, nawaomba  wananchi wa Buyu, kujitokeza  kwa wingi ilikusikiza sera , Ilani na mipango endelevu tuliyojipangia ndani ya chama” alisema Mahmoud Thabit Kombo.

  Aidha, aliwaomba wananchi wa Buyu, ifikapo Februari 2, 2014 siku ya Jumapili, wampigie kura ya NDIYO, ili awe Mwakilishi wao atakayeenda kuwatetea kwenye Baraza la Wawakilishi, sambamba na kumaliza kero zinazowakabiri.

  Baadhi ya mambo, mbalimbali anatarajia kuzungumzia ikiwemo kero za maji, elimu, kuwezesha vijana, akinamama na jamii nzima ya jimbo hilo la Kiembesamaki, pindi watakapomchagua.

  0 0

  Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akiongea na waandishi wa Habari(hawapo pichani) Kuhusu Mpango wa kuendelea kusogeza huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini ili kuchangia ukuaji wa kasi na mabadiliko ya haraka ya sekta ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wakati wa Mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari(MAELEZO) Vincent Tiganya.

  Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote Mhandisi Peter Ulanga akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi Serikali ilivyojipanga kuhakikisha wanafikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara.Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa.


  Na Frank Mvungi
  Serikali kutumia zaidi ya bilioni 17.5 kupeleka mawasiliano katika maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara kote nchini ili kuchochea ukuaji wa haraka katika sekta ya Teknolojia ya Habari na mawasiliano.

  Fedha hizo ambazo ni mkopo toka Benki ya Dunia na Vyanzo mbalimbali vya Serikali ya Tanzania zitatumika kutoa ruzuku kwa watoa huduma wa simu za mkononi. 

  Hayo yamesemwa na waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo  jijini Dar es salaam. 

  Prof. Mbarawa amesema fedha hizo zitatumika kupeleka mawasiliano katika Mikoa 20,Wilaya,Kata 29,vijiji 869 , vyenye jumla ya wakazi 1,617,310.

  Prof.  Mbarawa alifafanua kuwa baada ya Zabuni kukamilika jumla ya kampuni nne (4) za watoa huduma zilikidhi vigezo na masharti na kufanikiwa kushiriki kupeleka mawsiliano kwenye kata 52 ambapo kampuni hizo ni  Vodacom (kata 1) Tigo (19) TTCL (20) na Airtel (12).

  Aliongeza kuwa Kata ya Baray mjini Karatu Mkoani Arusha ni moja ya maeneo yaliyokwisha nufaika na mradi huo na ni matarajio ya Serikali kuwa ifikapo mwezi machi mwaka 2014 kata nyingi kati ya 52 zitakuwa zimeshapelekewa mawasiliano na watoa huduma.

  Aidha Prof. Mbarawa alisema watoa huduma wameridhia kupeleka mawsiliano ya Simu kwenye kata 48 ambazo nazo zimebainika kutokuwa na mvuto wa kibiashara kwa gharama zao wenyewe bila ya kupewa ruzuku yoyote na Serikali.

  Pia Prof.  Mbarawa aliwashukuru  watoa Huduma Kwa kuzingatia mchango walioutoa katika kukuza sekta ya mawasiliano nchini.


  Serikali kupitia Mfuko wa mawsiliano kwa wote inatekeleza mpango wa kupeleka mawasiliano vijijini hasa katika maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara.

  0 0

   Siku ya terehe 1 ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni KUANZIA SAA TATU NA NUSU ,kutakuwepo na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota wote,mabondia na makocha  wa ngumi wote kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa zinapoelekewa,kujuana na kuelimishana sheria za ngumi za kulipwa  zinavyotumika kinyume na sasa ,sheria nyingi zinafungiwa macho na kutumia uzoefu zaidi kuendesha mgumi nchini.  

  Mkutano huo ulioitishwa na Rais wa TPBO bw  Yasin Abdallah akishirikiana  na Ibrahim kamwe na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa  kuwa mkutano wa kwanza  kuwakutanisha mapromota wote pamoja na  mabondia wa ngumi  za kulipwa wa hapa nchini ili kuboresha ngumi na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo ,ambao ndio mchezo unaoliletea mataji na  sifa Tanzania katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini wowote ,mpaka sasa ni mchezo  ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za  wadau wachache wachovu  na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo sana kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni mchezo  ambao una huduma nyingi zinazohitaji nguvu ya wadhamini ili  uendelee kuboreka zaidi.

  Akizungumza na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe , amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe,  makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli, matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa na promota wangumi  ahudhurie bila kukosa mkutano huu muhimu sana kwa wamasumbwi ya nchi  yetu.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa baadhi ya viongozi wa Kenya na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo Ijumaa January 24, 2014. 

  Viongozi haO walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. Rais Kikwete ambaye alitua nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto na balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda Buriani walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo January 24, 2014. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. 

  Rais Kikwete, aliyetua Nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo. PICHA NA IKULU

  0 0

   Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta Binafsi (TPSF)   Bw. Reginald Mengi wa pili kushoto akieleza jambo wakati wa kikao baina ya TPSF na Wizara. Wanaosikiliza ni Mkurugenzi Mtendaji  wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye na (katikati mbele) ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi.

   Sehemu ya wajumbe waliohudhuria kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini na TPSF wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao hicho.

  Baadhi ya Wawakilishi kutoka Sekta Binafsi (TPSF) waliofika katika kikao hicho wakifuatilia kikao hicho.


  0 0
  0 0

  Ligi kuu ya Vodacom sasa itarushwa moja kwa moja kupitia Azam TV ili washabiki wa mpira wa miguu Tanzania waweze kujionea mechi kali za ligi kuu muda wowote na mahali popote zitakapochezwa. Ligi hizi zitaonyeshwa katikati na mwisho wa wiki.

  Ratiba za mwisho wa wiki hii:

  Jumamosi tarehe 25 Januari:
  Ashanti United na Young Africans zitacheza Uwanja wa Taifa (DSM)
  Azam FC na Mtibwa Sugar zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)

  Jumapili tarehe 26 Januari:
  JKT Ruvu na Mgambo JKT zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
  Simba SC na Rhino Ranger zitacheza Uwanja wa Taifa (DSM)

  Ratiba za wiki ijayo:
  Jumatano tarehe 29 Januari:
  Azam FC na Rhino Rangers JKT zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
  Coastal Union na Young Africans zitacheza Uwanja wa Mkwakwani (Tanga)
  Alhamis Tarehe 30 Januari:

  Ruvu Shooting na Mbeya City zitacheza Uwanja wa Mabatini (PWANI)
  Mechi zitaonyeshwa moja kwa moja kuanzia saa kumi kamili jioni. Katika habari nyingine mpya na za kusisimua, mashabiki sasa watakuwa na uwezo wakuangalia dondoo za mechi zote kupitia simu zao za mkononi, ikiwapa fursa ya kuangalia matukio yaliyopita na kujua yatakoyojiri mechi zijazo.

  “Baada ya kupata kibali cha kuonyesha ligi kuu ya Vodacom, moja kati ya malengo makuu ni kuhakikisha kuwa tunafikia kiwango cha juu cha kimataifa. Katika kufanikisha hili, tumewekeza Zaidi kwenye teknolojia ya kisasa ya matangazo ya nje na mafunzo ya wafanyakazi wetu. Na tumedhihirisha hilo kwamba tumejizatiti katika kutoa matangazo yenye ubora wa hali juu tuliporusha Ligi ya kombe la Mapinduzi lililomalizika hivi karibuni” Amesema Rhys Torrington, mkurugenzi mkuu wa Azam Media.

  Azam Media Ltd waliingia mkataba wa miaka mitatu (3) na TFF wa haki za kutangaza na kuonyesha mechi zote za ligi kuu ya Vodacom wenye thamani ya Tshs 5,560,800,000.

  AzamTV tayari inaonyesha chaneli Zaidi ya 50, zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa na za kitaifa na chaneli tatu maalumu kutoka Azam. Chaneli hizo maalum ni:
  ·      Azam One – Burudani motomoto kwako na familia kutoka bara la Afrika, ambazo nyingi ni kwa lugha ya Kiswahili.
  ·      Azam Two – Programu maalum mbalimbali zilizochaguliwa ulimwenguni.
  ·      Sinema Zetu – Chaneli maalumu inayoonyesha filamu za kitanzania masaa 24.

  Kwa ujumla, chaneli hizi zinawapa fursa wateja wetu kuweza kuangalia kiwango cha juu cha michezo mbalimbali, filamu, vipindi vya watoto, tamthilia, maisha na burudani na mengineyo kwa bei nafuu kabisa ya Tshs 12,500/= tu!

  Kwa sasa Azam TV inapatakana Tanzania tu, lakini kwa wiki chache zijazo itaanza kupatikana Uganda na Kenya, kabla ya kuenea Afrika Mashariki kwa ujumla. Kwa ujumla AzamTV inakupa nafasi yawewe na familia yako kupata burudani mbalimbali kwa bei rahisi na nafuu.

  Azam Media itaendelea kuwekeza kwenye utengenezaji wa programu mpya za ndani ya nchi kupitia kampuni tanzu ya Uhai Productions kwa ushirikiano na watengeneza vipindi wa kitaifa.


older | 1 | .... | 208 | 209 | (Page 210) | 211 | 212 | .... | 1904 | newer