Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA UKUMBI WA MIKUTANO WA KANISA LA MTAKATIFU PETER.

0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wakati wa Ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwadhama Cardinali Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuh
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akisalimiana na Mwadhama Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuh.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Kanisa la Mtakatifu Peter Oysterbay, leo asubuhi kwa ajili ya kushiriki katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa hilo. ambapo zaidi ya Sh. milioni 65 zilipatikana kati ya Sh. milioni 600, zinazohitajika hadi ifikapo mwezi Julai. Kati ya hizo Cash ni Sh. milioni 5 na zilizobakia zikiwa ni ahadi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais Mtaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, wakishiriki katika Misa maalum ya Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Jan 26, 2014
Mwadhama Cardinali Polycap Pengo akiongoza ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuh
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais Mtaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, wakishiriki katika Misa maalum ya Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio
 Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
 Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
 Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, wakati wa harambee ya kuchangia ujnenzi wa Ukumbi huo iliyofanyika leo asubuhi 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter, baada ya ibada maalum ya harambee ya kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika leo asubuhi, Jan 26, 2014. Kushoto ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akiongoza na na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kutoka kanisani baada ya ibada hiyo.
 Picha ya pamoja ya kumbukumbu ya siku hii adhimu
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais Mtaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, wakisindikizwa baada ya kushiriki katika Misa maalum ya Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

MWIGULU NCHEMBA AZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA UCHAGUZI WA MADIWANI JIJINI ARUSHA LEO

0
0
Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara Mh;Mwigulu Nchemba ameshawasili Jijini Arusha Mchana huu akitokea Kiteto na Babati kwaajili ya Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani zinazoendelea nchi nzima,Chaguzi hizi ni ndogo kwaajili ya kujaza nafasi za Madiwani waliojiuzulu na wengine kufariki.
 Mh.Mwigulu Nchemba akionesha Kadi ya Chadema baada ya Wanachama 4 wa CHADEMA kurudisha kadi zao na kujiunga na CCM.
Watu ni wengi sana waliojitokeza kwenye Mkutano huu wa hadhara wa Ufunguzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Sombetini
 Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa Hadhara wa Ufunguzi wa kampeni Kata ya sombetini Jijini Arusha.Mh.Mwigulu yupo jukwaani anawahutubia wananchi sera za Chama cha Mapinduzi na namna CCM ilivyotekeleza Ilani yake ndani ya kata ya sombetini na namna Inavyohitaji Diwani wa CCM kuendelea kusimamia Ilani ya Maendeleo ndani ya kata hiyo.
CCM imerejesha Heshima yake Jiji la Arusha,Wananchi hawataki tena CHADEMA kutokana na Vurugu mbalimbali zinazoratibiwa na Chama hicho,Wastani wa Kufanya Vurugu ndani ya Jiji la Arusha chini ya Chadema ni Mkubwa kuliko Wastani wa Kufanya kazi za maendeleo kwa Wananchi wa Arusha. Mh.Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa CCM Mwl.David Mollel mbele ya Umati wa Wananchi/wakazi wa Sombetini
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba akiwaonesha Wananchi namna Kijana mwenzao alivyovamiwa na Vijana wanaosadikika ni Wachadema na Kupigwa hadi kupoteza Fahamu na Kisha kuporwa pikipiki yake pamoja na Bendera ya Chama Cha Mapinduzi.Mwigulu alisisitiza kwa Kusema inasikitisha sana kuona Kuna watu wanakiunga mkono Chadema wakati ni chama kinachoongoza kwa Kuratibu mauaji ya Watanzania wasio na hatia kwa madhumuni ya kupata Fedha kwa Wafadhili wao nje ya Nchi.
 Mkutano umemalizika hapa Sombetini na Naibu Katibu Mkuu anagana na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye Ufunguzi huu wa Kampeni za Udiwani kata ya sombetini.
Sehemu ya Mamia ya Wananchi waliomiminika kwenye uwanja wa Soko  hapa Sombetini wakisikiliza kwa makini Sera za Chama Cha Mapinduzi kutoka kwa Mh.Mwigulu Nchemba.

Naibu Katibu Mkuu CCM Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Mgombea wa Udiwani Kata ya Sombetini WIlaya ya Arusha ndugu David,Hapa akiwa kwenye maandamano kutokea Ofisi za chama hapa Sombetini kuelekea Viwanja vya Mkutano,Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.
Mh:mwigulu Nchemba akipata mapokezi mazito kutoka kwa maelfu ya wananchi waliomiminika Viwanja hivi vya Soko la Mbauda kwaajili ya Mkutano wa hadhara wa kampeni za Udiwani.
 Mapokezi yanaendelea hapa Soko la Mbauda kwaajili ya kuanza mkutano wa hadhara.
Sehemu ya Mamia ya Wananchi wakiwa tayari kusikiliza Mkutano huu wa hadhara kwaajili ya Kampeni za Udiwani kata ya Sombetini jijini Arusha.
 Wananchi wanaendela kumiminika kwenye viwanja hivi vya soko la Mbauda kwenye Mkutano wa Hadhara wa CCM kumnadi mgombea wa CCM kwenye Kinyang'anyiro cha Udiwani.

PICHA ZA MIKUTANO YA CHADEMA SEHEMU MBALIMBALI MIKOANI.

0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh.Freema Mbowe akiwahutubia wakazi wa Ngara waliofika kwenye mkutano wao wa hadhara mapema leo.
 Mchango ukipitishwa kwa ajili ya chama
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA,Mh.Said Issa Mohamed akizungumza kwenye mkutano wa hadhara huko Ngara mapema leo.
 Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Isitu, Chimara mkoani Mbeya, Felix Komba akizungumza katika mkutano wa Operesehni M4C Pamoja Daima mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, baada ya katibu huyo kujiunga na Chadema wakati wa mkutano huo uliofanyika Chimara jana.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Cadema), Dk. Willibrod Slaa akimnadi mgombea udiwani katika Kata ya Njombe Mjini kupitia chama hicho, Agrey Mtamba, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Njombe jana.
 Wananchi wa mji wa Njombe na vitongoji wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika mjini Njombe jana. 
 Wananchi wa mji wa Makmabako wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika jana.

 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwasili katika mji wa Chimara mkoani Mbeya, ambako alifanya mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana. 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Makmabako, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu', akihutubia mkutano wa hadhara ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mji wa Chamara mkoani Mbeya jana.

MWENYEKITI WA CCM ATIKISA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA TUNGI MANISPAA YA MOROGORO

0
0
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent  Kalogeris Akimnadi Mgombea wa Udiwani Kata ya Tungi manispaa ya Morogoro Kupitia CCM Ndugu Mzeru Paulo.
 Mgombea wa Udiwani Kata ya Tungi manispaa ya Morogoro Kupitia CCM Ndugu Mzeru Paulo Akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mogogoro Mh Juliana Mwenda Wakiwa Katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani kata ya Tungi.Kata hiyo inafanya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Baada ya Aliyekuwa Diwani Kata Hiyo Mh Mbao Mbao Kufariki Dunia Mwaka jana mara baada ya kusumbuliwa na Ugonjwa kwa Muda Mrefu.Uzinduzi Huo Umeambatana na Uzinduzi wa Sherehe za Chama cha Mapinduzi za Kutimiza Miaka 37.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris Kulia akiwa na Katibu wa CCMwilaya ya Morogoro Katikati Pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Romuli John leo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Tungi.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Mkoa wa Morogoro Mh Doroth Mwamsiku Aliyevaa Kofia Nyeusi Akiwa Pamoja na Mgombea wa Udiwani Kata ya Tungi manispaa ya Morogoro Kupitia CCM Ndugu Mzeru Paul



 Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Mkoa wa Morogoro na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Morogoro Mh Mariam Kyaman Kushoto Akiwa na Mbunge wa Viti Maalum Kupitia Umoja wa Vijana Mkoa wa Morogoro Mh Sara Msafiri
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh Juma Nondo Kushoto Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Romuli John



Wakazi wa Kata ya Tungi waliojitokeza kwa Wingi 
 Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Romuli John Akizungumza Leo Wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kta ya Tungi manispaa ya Morogoro 
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Abdulaziz Mohamed Abood Akizungumza leo katika kata ya Tungi wakati wa Uzinduzi wa Kmpeni za Uchaguzi Mdogo wa Udiwani kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jaza Akiwa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mh Lucy Nkya wakati wa Uzinduzi wa Kmpeni za Udiwani kata ya Tungi

ASKARI 96 WA TANAPA WAMALIZA MAFUNZO YA AWALI WAAHIDI KUPAMBANA NA MAJANGIRI‏‎

0
0
Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoani katavi ambao hawapo pichani hapo juzi katika chuo cha wanyama pori cha mlele ambapo wahitimu 96 walihitimu mafunzo ya awali ya wahifadhi wa rasilimali za nchi na aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili waweze kupambana na kutokomeza ujangiri na kuvunja mitandao ya majangiri ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
 Askari wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama (TANAPA)  wakiwa wamesimama wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA  ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu. 
 Askari wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamekaa wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ALLAN KIJAZI ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu.
 Picha na Katavi yetu Blog

*********************
Na   Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog.
Mpanda Katavi
 Jumla ya  Askari 96 wa  Shirika  la Hifadhi la Taifa  la Wanyama Pori  (TANAPA) wametimu    mafunzo  ya miezi   mitatu  katika  chuo     kipya   cha wanyama   pori   cha Mlele  kilichopo   Mkoa  wa Katavi  na kutoa  kiapo cha uti  mbele ya Mkurugenzi mkuu  wa TANAPA Allan Kijazi

Askari hao  wa TANAPA walimaliza  mafunzo  hayo  hapo juzi  kwenye chuo  hicho   cha  wanyama Pori  cha Mlele  akiwa ni  mafunzo ya  kwanza  hapa  nchini  kwa TANAPA  kutoa  mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori kupatiwa mafunzo hayo  kabla ya kuanza  kazi

Katika  Risala yao ya  wahitimu wa mafunzo hayo  ya kulinda maliasili  iliyosomwa  na Bruno  Mbunda  walieleza kuwa wamejifundisha  mbinu mbalimbali za kulinda   rasilimali za Taifa  kwa Vitendo   na nadharia

Waliyataja baadhi ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata  waharifu  kumpekua  mharifu  na kutotumia  nguvu  sana  katika kukamata  mharifu    pamoja  na  pia wamejifundisha namna ya kutumia silaha

Walieleza  katika kipindi hicho cha  mafunzo    wahitimi   hao walifanikiwa kukamata  waharifu  hamsini  wakati  wakifanya  doria  katika maeneo mbambali ya Mbuga ya  Katavi  na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa  Lwafi

Wahitimu hao walieleza kuwa  mafunzo hayo yaliwashirikisha  Askari  99  lakini  watatu kati yao wameshindwa  kuhitimu  zikiwemo  sababu  mbambali  kama  utoro na utovu  wa nidhamu   hari ambayo ilfanya wahitimu  waliomaliza kubaki  96 ambapo kati yao mwanamke  ni mmoja  na wanaume ni  95

Kwa upande wake mkuu wamapori ya akiba  ya  Rukwa Lwafi  Joseph Mbung’ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mawasiliano  na  ubovu wa miundo  mbinu ya barabaa  na  upungufu  wa  magari pamoja  idadi ndogo ya washiriki  wa mafunzo kwa wanawake na ufinyu  wa bajeti

Nae  Mkurugenzi  wa Hifadhi  na Ikolojia  Martini  Loibook  alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata yanaumuhimu  sana  hasa kutokana na changamoto  zinazoikabili nchi  yetu  inayokabiliwa na wimbi la ujangili

Pia Mkurugenzi wa  utumishi   na utawalla   wa TANAPA  Witnes Shoo  aliwataka wahitimu hao  kufanya kazi  kwa uaminifu  kwa kujituma  na  wawe na didamu  na  wasiwe na tabia ya kutowa siri za ofisi

Mkurugenzi Mkuu   wa TANAPA  Allan Kijazi  aliwaasa wahitimu hao  wahakikishe wanafanya kazi  zao kwa uaminifu mkubwa  hasa  katika shughuli zao  katika kupambana kukomesha ujangili.

Aliwataka kutojihusisha  na masuala ya ujangiri na badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao ya ujangiri iliyopo ndani ya nchi na nje ya nchi

Alisema wapo baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kueubuniwa na mtu yoyote yule au watu

PROIN GROUP OF COMPANIES YAFANYA SHEREHE YA KUUKARIBISHA MWAKA 2014

0
0
  Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group of Companies Bw Johson Lukaza akiwakaribisha wafanyakazi wa makampuni yaliyo chini ya Proin Group of Companies pamoja na wageni waalikwa katika sherehe ya kuukaribisha mwaka 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Jengo la Kampuni hiyo la Tranic Plaza.
Mshereheshaji wa Sherehe hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere akiongea na wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi waliohudhuria sherehe hiyo ya kuukaribisha mwaka 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Mjengo wa Tranic Plaza


Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya kukaribisha mwaka 2014 iliyoandaliwa na Proin Group Of Companies wakigonga glasi kama ishara ya Upendo na Kuupokea mwaka katika sherehe iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Mjengo wa Tranic Plaza

 Baadhi ya wakurugenzi wa Makampuni yaliyo chini ya Proin Group Of Companies wakikata keki Kama ishara ya kuukaribisha Mwaka 2014 kwenye sherehe ya kuukaribisha mwaka iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Jengo la Tranic Plaza.


 Mkurugenzi wa kampuni ya Infinity Communication Stella Sakia akitoa Maneno ya Ukaribisho kwa Wafanyakazi wote walio chini ya Proin Group of Commpanies na wageni waalikwa wote katika sherehe ya kuukaribisha mwaka iliyofanyika Mwishoni mwa Wiki katika Mjengo wa Tranic Plaza

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini kila tukio lililokuwa likiendelea katika sherehe hiyo
 Raha ya sherehe ni Msosi na Mziki baada ya hapo.........
 Baadhi ya wafanyakazi kutoka Proin Promotions Limited kampuni moja wapo iliyopo chini ya Proin Group Of Companies wakiwa katika pozi la picha
Haya Baada ya Msosi wadau wakiserebuka Kwaito...
Mmiliki wa mtandao wa Lukaza Blog, Bw Josephat Lukaza akiwa katika picha ya pamoja na Meneja masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited mara baada ya kukutana katika Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka 2014 iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Mjengo wa Tranic Plaza.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

MKUU WA POLISI WILAYA (OCD) IRINGA APATA AJALI

0
0
Askari  waliokuwa  wakielekea katika mkutano   wa uzinduzi wa  kampeni  za CCM kata  ya  Nduli Iringa mjini wakitazama gari  ambalo alikuwa akiendesha  OCD Iringa  lililopata  ajali majira ya saa 10 jioni leo (jana)  jumapili japo hakuna  aliyepoteza maisha  ktk ajali hiyo iliyotokea  kona  la Mgongo barabara ya Iringa-Dodoma
wasomi  wa  chuo  kikuu cha Iringa wakitazama  ajali hiyo ambayo dereva  wake OCD Iringa  alinusurika  kifo na  kuumia mkono  wake  kiasi.Picha na Francis Godwin-Iringa

TAARIFA KWA UMMA: SERIKALI YAPUNGUZA GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME

0
0

 
SERIKALI YAPUNGUZA GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME
*Ni kwa wanavijiji wanaoishi jirani na bomba la gesi Mtwara - Dar
 
SERIKALI imeamua kupunguza kwa kiasi kikubwa bei ya kuunganisha umeme majumbani na kufikia sh. 27,000/ kwa wanavijiji wanaoishi kwenye maeneo ambayo bomba la gesi linapita.
 
Hatua hiyo imetangazwa jana (Jumapili, Januari 26, 2014), na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo wakati akizungumza na wanakijiji wa Mangaka wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda azindue mradi wa umeme kwenye wilaya hiyo.
 
“Jana Waziri Mkuu aliagiza tutafute namna ya kuwasaidia wananchi wanaoishi jirani na njia ya bomba la gesi. Nami nilikaa na wasaidizi wangu jana usiku na kufanya hesabu na tukaamua tuweke kiwango hicho kwa ajili ya wakazi hao,” alisema.
 
Alisema katika mikoa mikoa mingine gharama za kuunganisha umeme ni sh. 177,000/- lakini kwa mikoa ya Lindi na Mtwara gharama hizo zilishushwa na kufikia sh.99,000/-. “Lakini sasa hawa wenzetu tumewapa upendeleo zaidi na tumewapunguzia gharama hizo hadi sh. 27,000/-,” alisema huku akishangiliwa.
 
Gharama hizo ni maalum kwa ajili ya wakazi waishio jirani na bomba hilo linaloanzia Mtwara hadi Dar es Salaam kupitia mikoa ya Lindi na Pwani.
 
Akizungumza na mamia ya wakazi wa Mangaka waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema uzinduzi wa mradi huo wa umeme ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha kila wilaya inapata umeme.
 
“Mpango wa kupeleka umeme nchi nzima ni wa miaka mitatu na katika sekta ya Nishati chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN), tumeazimia kwenda kwa awamu ili tuwafikie wananchi wengi zaidi kutoka asilimia 24 ya sasa hadi kufikia asilimia 30 ya watumiaji wa umeme,” alisema Waziri Mkuu.
 
Akitoa taarifa juu ya mradi huo wa umeme wilayani Nanyumbu, Meneja Mwandamizi wa TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara, Eng. Mahende Mugaya alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 5.6/- na unatarajiwa kukamilika Aprili, mwaka huu.
 
Alisema kuzinduliwa kwa mradi huo kunafanya wilaya zote za mkoa wa Mtwara ziwe zimepata umeme wa kuanzia na kwamba kazi itaendelea kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ili kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme kwenye mkoa huo.
 
“Chini ya mfuko wa REA tumetenga sh. bilioni 7.6 ili zitumike kusambaza umeme katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara ambao sasa hivi watumiaji wa umeme wamefikia 15,675 sawa na asilimia nne ya wakazi wote wa mkoa huu.”
 
Alisema katika mwaka 2012-2013 walipata wateja 2,609 tofauti na idadi ya zamani ya wateja 1,300 ambayo ilikuwa imezoeleka. Alisema hivi sasa wamepokea maombi kutoka kwa wateja 2,588 ambao tayari wamekwishalipia gharama za kuunganishiwa umeme.
 
Chini ya mradi wa umeme kupitia REA, jumla ya vijiji 54 katika wilaya za Tandahimba, Masasi na Newala vitanufaika na mradi huo ulioanza kutekelezwa Desemba 2013 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2015.
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.
JUMATATU, JANUARI 27, 2014

Washindi wa Airtel ‘Mimi Ni Bingwa’ wakwea pipa kwenda Old Trafford

0
0
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson  Mmbando akiwakabidhi tiketi za ndege baadhi ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel tayari kwa ajili ya safari yao ya kwenda kushuhudia mechi kati  ya Manchester United na Cardiff City itakayochezwa kesho kwenye uwanja wa Old Trafford.
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson  Mmbando akiwa pamoja na baadhi ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa muda mfupi  kabla ya kuanza safari yao ya kuelekea nchini Uingereza kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City itakayochezwa kesho kwenye uwanja wa Old Trafford.

 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson  Mmbando (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa muda mfupi  kabla ya kuanza safari yao ya kuelekea nchini Uingereza kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City itakayochezwa kesho kwenye uwanja wa Old Trafford.
======== ==============  =================

Washindi wa Airtel ‘Mimi Ni Bingwa’ wakwea pipa kwenda Old Trafford


WASHINDI wa tiketi wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa jana waliondoka nchini kwa safari iliyogharamiwa kila kitu kwenda Old Trafford.

Wakisindikizwa na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando, washindi na wenza wao waliowachagua watakuwa na nafasi ya kuangalia mechi baina ya Manchester United na Cardiff City moja kwa moja ‘live’ itakayochezwa Jumanne saa 12 jioni majira ya Afrika Mashariki.

Awamu ya kwanza inayowajumuisha Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Andrew Muta Temwa mkazi wa Bukoba, Ashraf Mohamed Adam kutoka Tanga na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam na wenza wao, pia watapata nafasi ya kufanya ziara katika uwanja wa Old Trafford na kuzungumza na wachezaji wa Manchester United.

Washindi hawa hawakusita kuelezea furaha yao na hamu ya kukutana na wachezaji maarufu wa kimataifa wa mpira wa miguu pamoja na hari ya kuwa sehemu ya mashabiki katika uwanja huo maarufu duniani wakati wa moja ya mechi za ligi kuu ya Uingereza inayoangaliwa zaidi duniani.

“Hii ni nafasi ambayo sikuwahi kuiota katika maisha yangu. Kutokana na hali yangu ya kiuchumi, sikuwahi kufikiria kuwa siku moja nitasafiri kwenda Uingereza na hususani kuingia katika uwanja wa Old Trafford. Nina furaha sana. Naishukuru Airtel kwa kunipa nafasi hii, ambayo pia imenisaidia kuonyesha upendo kwa mwenza wangu kwa kumpa nayeye nafasi ya kwenda Uingereza,” alisema Lyatuu. 
   
Salma, ambaye ni mshindi kutoka Dar es Salaam alisema, “Hii ni kama ndoto ambayo imekuja kutokea kweli. Nilipotaarifiwa kuwa nimeshinda tiketi mbili kwenda Old Trafford, sikuamini hadi nilipokamata tiketi yangu mkononi. Nataka niwahakikishie wananchi na wateja wa Airtel kuwa promosheni hii ni ya kweli na inaweza kukupa fursa ambayo kamwe hukuwa ukihitarajia.”

Akidokeza kuhusiana na safari hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando, alisema kampuni hiyo ya simu itagharamia safari yote, chakula pamoja na gharama za malazi hadi washindi hao watakaporejeshwa makwao.

“Bado kuna safari nyingi zaidi zinakuja. Mpaka sasa, tunaandaa baadhi ya hati za kusafiria za washindi wengine waliojishindia tiketi za promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa  kwenda Old Trafford na zikiwa tayari, wataondoka mapema. Promosheni bado inaendelea lakini muda umebaki mchache kabla ya kuchezesha droo ya kumpata mshindi wa shilingi milioni 50. Wakati wa kushiriki ndo sasa.

“Mbali na tiketi, bado kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa kila siku na kila wiki, ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 mwishoni mwa droo. Kila mshiriki wa promosheni ya  Airtel Mimi ni Bingwa ana nafasi ya kushinda zawadi hizi. Unachohitaji ni kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BNGWA” kwenda namba 15656, kwa kujibu maswali mengi iwezekanavyo,” alisema.

Bw. Mmbando alisema safari hiyo itachukua siku tano ikiwa ni pamoja na siku za safarini na washindi wanatarajiwa kurudi nchini ifikapo Alhamis ya tarehe 30 mwezi huu.   

Washindi hao watakaoelekea Old Trafford toka promosheni ilipoanza mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana ni pamoja na Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa Kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa mkoani - Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro mkoani Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam.

Kuongezeka kwa kina cha bahari,gesi joto,kupungua kwa barafu hususan katika mlima Kilimanjaro na mabadiliko ya mfumo ya mvua ni changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi nchini

0
0
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi (kushoto) akifungua warsha ya mafunzo ya mfumo wa biashara ya hewa mkaa, na athari za mabadiliko ya tabia nchi,mjini Bagamoyo leo.(kulia ni Injinia. Ladslaus Kyaruzi Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu wa Rais.
Baadhi ya washiriki, wa warsha ya mafunzo ya mfumo wa biashara ya hewa mkaa mjini bagamoyo leo.
Picha ya washirki wa warsha ya mafunzo ya mfumo wa Biashara ya hewa mkaa mjini Bagamoyo leo.

=======  ======== ==========
NA EVELYN MKOKOI

Kuongezeka kwa kina cha bahari, kuongezeka kwa gesi joto, kupungua kwa barafu hususan katika mlima Kilimanjaro na mabadiliko ya mfumo ya mvua, Imeelezwa kuwa ni changamoto kubwa zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi nchini.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi msaidizi kutoka Ofisi ya Makamo wa Rais Mazingira, Bw Richard Muyungi katika ufunguzi wa warsha ya mafunzo wa biashara ya hewa ukaa, mjini Bagamoyo iliyohusisha wataalam wa masuala ya mazingira kutoka katika sekta mtambuka nchini.

Bw. Muyungi ameeleza kuwa, Shughuli za kibinadamu hasa katika nchi zilizoendela kama vile za uzalishaji viwandani zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta athari za mabadiliko ya tabia nchi..na hii inatokana na kuachiwa kwa kiasi kikubwa cha hewa ya ukaa kutoka viwandani kwenda angani, ambapo ongezeko la joto ni kichocheo kikubwa cha athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Bw. Muyungi aliongeza kuwa uzalishaji wa gasijoto katika maeneo mengine, kama misitu, kilimo, joto, usafirishaji, majengo na methane huzalishwa kwa kiasi kikubwa katika nchi zilizoendelea na uleta athari za mabadiliko ya tabia nchi.

”Katika nchi zinazoendelea umaskini ndo unasababisha ukataji ovyo wa misitu na kuiuza kwa bei rahisi, aidha matumizi mabaya ya mbolea katika sekta ya kilimo huchangia pia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa gesi joto.”

Alisisitiza Tanzania ni nchi mojawapo iliyoridhia mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi tangu mwaka 1996 na itifaki ya Kyoto ya mwaka 2002 ukiwa na lengo kubwa la kupunguza uzalishaji wa gesijoto.

COMING SOON.!

0
0

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MNADHIMU MKUU WA MAJESHI

0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi, Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 27, 2014 kwa mazungumzo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi, Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 27, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR 

WAZIRI MKUU PINDA AZINDUA MRADI WA UMEME WILAYANI NANYUMBU.

0
0
Waziri mkuu Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wilaya ya Nanyumbu kulia ni waziri wa nishati na madini Prof Sospeter Muhongo na kutoka kushoto ni Meneja Mwandaminzi wa TANESCO, Kanda ya Dar es salaam na Pwani  inayojumuisha  mikoa ya Lindi na Mtwara Mhandisi  Mahende Mugaya,mkuu wa wilaya ya Nanyumbu, mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanal mstaafu Joseph Simbakalia, Mbuge wa Nanyumbu Dastani Mkapa.

 Waziri mkuu  Mizengo Pinda akiangalia moja  kati ya magari yaliyo chomwa moto nyumbani kwa  Mbuge wa Masasi Mariam Kasembe  wakati wa vurugu mwaka moja uliopita alipotembelea wilaya hiyo.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia Mpira wa Matambara wa kijana Hasani Kasim alipokuwa katika ziara ya kukagua adhari za vurugu mwaka mmoja uliopita katika Wilaya ya Masasi .

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia Mpira wa Matambara wa kijana Hasani Kasim alipokuwa katika ziara ya kukagua adhari za vurugu mwaka mmoja uliopita katika Wilaya ya Masasi .

Sehemu ya jengo la CCM Wilaya ya Masasi ambalo liliteketezwa na moto mwaka jana. (Picha zote na ofisi ya Waziri Mkuu) 


 Waziri mkuu  Mizengo Pinda akikagua nyumba ya Mbuge wa Masasi Mariam Kasembe ambayo ilichomwa moto wakati wa vurugu mwaka moja uliopita alipotembelea wilaya hiyo.Kulia ni Omary Lada mume wa Mbuge

WANAFUNZI 1725 WASHINDWA KURIPOTI SHULENI WILAYA YA KILOLO

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo,Mh.Gerald Guninita akifungua kikao cha DCC katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya,Kushoto ni Mkurugenzi Ruukia Muwango na Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Wilaya,kikao kilichofanyika mwisho mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri hiyo. 
Mkurugenzi wa wilaya ya Kilolo Rukia Muwango akisoma taarifa ya wilaya hiyo mbele ya wajumbe wa kamati ya wilaya katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wilaya mwishoni mwa wiki.
========  =======   =======
WANAFUNZI 1725  WASHINDWA KURIPOTI SHULENI WILAYA YA KILOLO

Na Denis Mlowe,Kilolo

JUMLA ya wanafunzi 1725 waliotakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika shule mbalimbali zilizoko katika Wilaya ya Kilolo wameshindwa kuripoti kutokana na sababu mbalimbali.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri hiyo, Rukia Muwango  alisema wanafunzi wasioripoti kati ya hao wavulana walikuwa 788 na wasichana 937 sawa na asilimia 56.1

Muwango alisema wanafunzi waliochaguliwa kwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ni wanafunzi 3101 wavulana 1442, wasichana 1658 kati ya hao wavulana 10 na wasichana 10 wamechaguliwa katika shule za bweni.

Alisema wanafunzi waliopangwa kwenda katika shule za ufundi walikuwa wavulana 6 na hakuna msichana aliyechaguliwa na wanafunzi 3074 walipangwa katika shule za serikali katika halmashauri ya wilaya ya Kilolo.

Aliongeza kuwa wanafunzi walioripoti hadi Januari 23 mwaka huu walikuwa wanafunzi 1349 wakiwemo wavulana 638 na wasichana 711 sawa na asilimia 43.

Muwango alizitaja shule ambazo zina asilimia ndogo ya wanafunzi walioripoti shuleni kuwa ni shule ya Sekondari Mawambala (5.2%), Mlafu (14%), Lukosi (19.3%),Udekwa (21%) na Mtitu yenye asilimia 29 ya wanafunzi walioripoti.

Aliwataka walimu wa wakuu shule za sekondari wawasilishe majina ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2014 waliojiunga katika shule zao ili halmashauri iweze kujua na kujiridhisha kuwa wanafunzi wote wapo shuleni na kutoa taarifa kwa wanafunzi wanaokwenda shule za zisizo za serikali kupata takwimu sahihi.

Alisema kuwa halmashauri imeandaa mikakati kwa wanafunzi wasioripoti kwa kuwaandikia barua waratibu wote kuwafatilia wanafunzi  hao na kuwahimiza kuhudhuria katika shule walizopangiwa.

 Kwa upande wa ke Mkuu wa Wilaya hiyo Gerald Guninita amewataka watendaji wawasisitize wazazi kuwapeleka watoto shule bila kujali suala la ada na sare za shule.

Aliwataka watendaji kupeleka ripoti ndani ya siku 24 kwa wanafunzi wote ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa katika ofisi ya wilaya na kuwachukulia hatua wazazi wakaidi.

“Haki ya mtoto kupata elimu ni muhimu sana na tusiache wazazi wanaowaficha watoto ndani hivyo wabanwe wazazi wao kwa kuwaficha kuna kitu nataka kuwaambia kumpeleka shule mtoto ni kumwongezea thamani mtoto na mzazi mwenye katika maisha yetu ya kila siku hivyo nawsisitiza sana watendaji wabaneni  sana wazazi wote wasiotaka kuwapeleka watoto wa kike shule” alisema Guninita

MAKONGORO NA RAFIKI ZAKE WASHEREHEKEA MWAKA MPYA KWENYE KITUO CHA KULEA WAZEE.

0
0
Juma Makongoro ambaye Mkuu wa Doria za Uvuvi Kanda ya Mwanza akimkumbatia mama mmoja kati ya wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo yeye pamoja na rafiki zake wakiwemo wengine toka sekta ya uvuvi pamoja na wafanyabiashara walitembelea kituo hicho kwaajili ya kula pamoja na kutoa misaada kama sehemu ya kusherehekea mwaka mpya 2014.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bernard Polycap akizungumza na wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo yeye aliwaasa wazee hao kuunda vikundi  kwa kuzingatia vipaji vyao na kujiorodhesha ili ofisi yake itizame jinsi ya kuwawezesha mitaji midogo midogo itakayo wasaidia kuanzisha miradi ya kujikimu kwa mahitaji binafsi.


Juma Makongoro ambaye Mkuu wa Doria za Uvuvi Kanda ya Mwanza (kulia) akimkabidhi msaada wa nguo Bi.Angelina Jonas katika sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya 2014 iliyofanyika katika Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza. Kushoto ni Mkurugrnzi wa kituo hicho. 
Makabidhiano yakiendelea katika kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza, ambapo zawadi za nguo, mafuta, sabuni, mchele, unga na bidhaa nyinenezo gawiwa kwa mabalozi wa wazee hao ambapo kila balozi anakaa na watu wake kisha wana gawana kwa usawa.
Mratibu wa ziara hafla hiyo Juma Makongoro (kushoto) akiwa na mkurugenzi wa kituo wakisaidiana kugawa vinywaji kwa wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Wazee wengi waliopo kwenye kituo hiki waliathiriwa na ugonjwa wa ukoma, upofu na wengine ni walemavu kutokana na ajali na majanga mbalimbali yaliyowakumba kwenye jamii zao hivyo kuwatembelea imekuwa ni faraja sana kwao. 


Marafiki wa Juma Makongoro kutoka Forum Syd nao waliungana naye kuleta zawadi zao na kujumuika pamoja kwenye sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya.
Juma Makongoro ambaye ni Mkuu wa Doria za Uvuvi Kanda ya Mwanza akizungumza na wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande kilichopo Usagara Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Kusanyiko la wadau ndani ya ukumbi wa sherehe.
Akina mama ambao ni marafiki wa Makongoro wakimtunza fedha mama huyu ambaye kutokana na kupatwa na ugonjwa wa ukoma siku za nyuma (sasa amepona) napata shida sana kujihudumia kwani kwa sasa hana viganja na amekatwa mguu mmoja. 
Wazeee na walemavu wasio jiweza wa Kituo cha kulelea wazee cha Kalwande wakisubiri zamu ya kugawiwa zawadi.
Serikali ambayo ndiyo yenye jukumu la kuwatunza na kuwalea wazee hawa kwa mahitaji ya chakula, mavazi na huduma nyingine muhimu kama umeme na maji ni kama imewatelekeza kwani tangu mwezi wa 5 mwaka jana 2013 serikali  inadaiwa kwani haija peleka msaada wowote wa chakula kukihudumia kituo hadi leo.


Hivyo wazee hao wanaishi maisha katika maisha magumu wakitoroka kambini hapo na kuzama mijini na kugeuka kuwa omba omba.


KITUO NA IDADI YA WATU:-

 Wazee wanaume 60.
Wazee wanawake 96.
Vijana wa kiume 54.
Vijana wa kike 55.
Watoto wa kiume 40.
Watoto wa kike 40.
Pamoja na dhima ya Serikali kukitenga kituo hiki cha Kalwande kuwa mahususi kulea wazee na walemavu wasio jiweza changamoto nyingine inajitokeza hapa, watoto wanazaliwa nao wanakuwa na kufikia umri mkubwa nao wana pata watoto kwa hiyo kituo kinakuwa si cha kuwalea wazee pekee bali kuwalea watoto pia ambao wanakabiliwa na changamoto ya kukosa elimu na malezi sahihi wakidhani maisha ni kuomba omba. 
Kikundi cha ngoma cha Kwaya ya Mt. Cecilia kilitumbuiza na hapa marafiki walijumuika na wazee pamoja na watoto wa kituo hicho kusakata ngoma kama sehemu ya kusherehekea mwaka mpya 2014.
Akiwakilisha Ma-blogger  G. Sengo naye hakusita kuhusika pale kati.
Angelina Jonas ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyekimbilia kituoni hapa kupata hifadhi marabaada ya kupata misukosuko toka kwenye jamii aliyokuwa akiishi yeye ni mfanyabiashara wa maandazi na amekuwa akiifanya shughuli hii kwaajili ya kujipatia fedha za kujikimu na mahitaji madogo madogo, licha ya changamoto nyingi zinazo mzunguka.
Naye mama Maria Petro ana duka lake la kuuza bidhaa mchanganyiko kama kanga, vitenge, unga, mchele na maandazi  hapa akimpatia huduma mteja wake bi. Jetruda Mwidima (kulia) ambaye anatatizo la kuanguka anguka kwenye moto. 
Picha ya pamoja ya kamati ya wadau walio fanikisha sherehe hiyo.

MATOKEO YA UTAFITI WA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA 800 YALIYOFADHILIWA NA TBL YAKABIDHIWA KWA KAMANDA WA KIKOSI CHA POLISI CHA USALAMA BARABARANI, DCP MPINGA

0
0
 Meneja Huduma wa Kliniki ambaye pia alimwakilisha Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Abel Mtungi (kushoto), akimkabidhi Kamanada wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, taarifa ya zoezi la upimaji afya kwa madereva wa mabasi ya abiria na malori iliyofanywa wakati wa Wiki ya Nenda kwa Usalama katika Kituo cha Mizani cha Mikese, mkoani Morogoro mwaka jana. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo. TBL ilifadhili zoezi hilo.
 Mteknolojia Maabara wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani, Johannes Rwenyagila (kushoto) akimkabidhi Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, taarifa ya zoezi la upimaji afya kwa madereva wa mabasi ya abiria na malori lililofanywa wakati wa Wiki ya Nenda kwa Usalama katika Kituo cha Mizani cha Msata, mkoani Pwani mwaka jana. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo.

 Afande Mpinga (wa pili kulia) akiwa na Kilindo wa TBL pamoja na madakari  waliowasilisha utafiti huo. Meneja Huduma wa Kliniki ambaye pia alimwakilisha Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Abel Mtungi  na Mteknolojia Maabara wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani, Johannes Rwenyagila

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kulia) akizungumza baada ya madaktari wa Hospitali za Tumbi na Morogoro (hawapo pichani), kukabidhi matokeo ya upimaji wa afya za madereva 800 mabasi ya abiria na malori wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani, mwaka jana katika vituo vya mizani vya Mikese Morogoro na Msata Pwani. Zoezi hilo lilifadhiliwa na TBL. Aliyepokea taarifa ya matokeo hayo, Dar es Salaam juzi,  ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu na Berther Mturi wa TBL.
Mteknolojia Maabara wa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani, Johannes Rwenyagila  (katikati), akielezea jinsi walivyoendesha zoezi hilo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria. Steve Kilindo pamoja na Afande  Kahatano wa kikosi cha usalama barabarani Makao Makuu.
  Meneja Huduma wa Kliniki ambaye pia alimwakilisha Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Abel Mtungi (kushoto), akielezea jinsi walivyofanya utafiti huo.
 Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga (katikati) akielezea kufurahishwa na matokeo ya utafiti huo.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga (kulia), akionesha moja ya matokeo ya utafiti. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA KUANZA KURINDIMA FEBRUARI 13 MJINI NGOME KONGWE,ZANZIBAR.

0
0
 Picha wa tatu kulia,ni Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara Promotions,Bwa.Simai Mohamed akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun,jijini dar kuhusiana na ujio wa tamasha la muziki la Sauti za Busara   la 11 katika kusherehekea utamaduni na muziki wa Afrika.Bwa.Simai amefafanua kuwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika kuanzia tarehe 13 mpaka februari 16 katika viwanja vya kihistoria vya Ngome Kongwe,Zanzibar.

Jumla ya Vikundi 32 vitafanya maonyesho jukwaani kwa asilimia 100 live.Bwa Simai amesema kuwa vikundi hivyo vimechaguliwa kutokana na maombi zaidi ya 560 na vinawakilisha nchi 19,ameongeza kuwa zaidi ya wasanii 200 watafika Zanzibar kufanya maonyesho ya muziki,wasanii hao wanatoka Afrika Mashariki,Afrika Kusini na Magharibi,maeneo ya mto Nile na pia kutoka Puerto Rico.

Kutoka Tanzania,Wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Jhikoman,Ashimba,Swahili Vibes,Hoko Roro,Seven Survivor,Abantu Mandingo,Segere Original na Kazimoto.
 Pichani ni Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo,aitwaye Jhiko Man pichani akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara,aitwaye Ashimba pichani nae akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
Kwa Tarifa mbalimbali za tamasha hilo tembelea www.busaramusic.org.

NEWS KUTOKA ZANZIBAR LEO. Wananchi watakiwa kufanya mazoezi kuepukana na maradhi yasiyoambukiza pamoja na kuzitunza afya zao.

0
0
Akijibu suala la Mhe Hijja Hassan Hijja mwakilishi wa Jimbo la Kiwani aliyetaka mpango  wa  Wizara kuhamasisha wananchi juu ya kujiepusha na maradhi yasiyoambukiza,  katika Baraza la Wawakilishi Chukwani, Waziri wa Afya Juma Duni Haji amesema ni wajibu wa kila mwananchi kufanya mazoezi  kwa lengo la kujikinga  na maradhi  hayo.

Aidha amefahamisha kuwa wananchi wanaweza kujikinga  na maradhi yasiyoambukiza  kwa kutumia njia mbali mbali za kujituma kabla ya kuathirika  kwa kufanya juhudi kubwa ya kufanya mazoezi  pahali popote. Waziri Duni  amewashauri viongozi kuwahimiza wananchi kufanya mazoezi kutokana na jamii kulemaa na usafiri wa vyombo vya moto na kuacha kutembea kwa miguu.

“Wananchi  wameshalemaa kwa gari, mtu anatoka Mlandege anakwenda Darajani anapanda gari hawana mazoezi ya kwenda kwa miguu tutapata maradhi  kwa sababu hatutaki kujituma”, alifafanua.

“Na nyinyi wawakilishi nakushaurini  lakini pia mna wajibu wa kufanya mazoezi kwa lengo la kujikinga na maradhi hayo “, alieleza waziri wa Afya.

Hata hivyo Waziri  huyo amesema kuwa wananchi wameruhusiwa kuunda vikundi mbali mbali kwa lengo la kufanya mazoezi na kulinda afya zao.
Aidha Mhe. Duni amesema wizara yake inatarajia kuanzisha kitengo maalum cha kuratibu magonjwa hayo ambapo vituo 34 vimeteuliwa kwa lengo la kutoa  huduma hiyo.

Pia ameeleza kuwa wizara yake inatarajia kushirikiana  na Idara ya Michezo pamoja na Idara ya Mazingira kwa lengo la kuwashajihisha wananchi kufanya mazoezi pamoja na kutunza mazingira ili kuepuka na maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza ili kuinusuru jamii.

SMZ KUCHUKUA HATUA ZA KISHERIA KWA WANANCHI WANAOVAMIA NA KUCHIMBA MCHANGA KATIKA ENEO LA MAKABURI YA MWANAKWEREKWE

Serikali ya Mapinduzi  ya imesema itachukua hatua za kisheria kwa wananchi wanaovamia na kuchimba mchanga katika eneo la makaburi ya Mwanakwerekwe.

Hayo yameelezwa leo huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani na Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri alipokuwa akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni aliyetaka kujua hatua  zinazotumika kwa wale wanaoendelea kuchimba mchanga katika eneo la makaburi Mwanakwerekwe.

Amesema sio vizuri wananchi kuendelea kuchimba mchanga katika eneo hilo la makaburi kwani kufanya hivyo ni kitendo cha kikatili  na hatua kali za kisheria zitachukiwa kwa yeyote atakaekamatwa anafanya  hivyo.

“Nawasihi sana wananchi katika kufanya vitendo hivi kuwa jambo hili sio zuri watafakari, kuwafanyia hivyo marehemu ni tendo ovu haistahiki ni kitendo cha kinyama dini zote zinakataza kufanya hivyo”, alieleza. Aidha amesema Serikali inafahamu kuwa wananchi wanachimba mchanga katika eneo hilo hivyo itafanya juhudi kubwa za kuwadhibiti  wale wote wataokamatwa na vitendo hivyo.

Waziri Kheir amefafanua kuwa Wizara yake inaendelea kuwashajihisha wananchi pamoja na kuandaa utaratibu wa kutoa michango ili kuweza kuhifadhi eneo hilo lisiendelee kuvamiwa.

Hata hivyo alisema Serikali imepanga kulitumia eneo la Kama, lililozikiwa watu waliofariki katika ajali ya MV. SPICE ISLANDERS, kuwa ni sehemu mpya ya kuzikia waislamu  ili kuondosha usumbufu. Aidha amefahamisha kuwa eneo la makaburi la Mwanakwerekwe limekuwa dogo kutokana na kubadilika kwa matumizi ya ardhi ambapo eneo hilo lilikuwa na ukubwa wa hekta 80 za mraba na  zimebaki hekta 25 kutokana na matumizi mengine ya ardhi.
.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

SHUKRANI

0
0

Ndugu Max Edmund Kafipa wa Ununio Bahari Beach jijini Dar es Salaam inapenda kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa, marafiki wote na wakazi wa Ununio walioshirikiana nae katika msiba hadi mazishi ya mke wake mpendwa  Sophia Uledi Kafipa (pichani) aliyefariki dunia kwa ajali ya gari tarehe 10/01/2014 na kuzikwa tarehe 13/01/2014 kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

Bwana ametoa Bwana ametwaa jina la Mungu lihimidiwe.

Amen

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATETA NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII NA NAIBU WAKE IKULU DAR

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu na Naibu wake, Mohamed Mgimwa, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 27, 2014. Picha na OMR
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images