Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

MABADILIKO YA TABIANCHI YANA MADHARA YA MALI NA UHAI WA BINADAMU - YUNA

$
0
0
DSC_1209
Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), Dr. Lwidiko Edward, akizungumza na vijana kutoka Asasi mbalimbali hapa nchini juu ya ushiriki wa vijana katika mkutano uliopita wa COP 19 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi UNESCO jijini Dar es Salaam.
.Mvua na mafuriko ni mifano hai katika baadhi ya nchi duniani
.Mapigano ya wakulima na wafugaji ni madhara ya mabadiliko ya tabianchi
Na Damas Makangale, MOblog.

CHAMA CHA UMOJA WA MATAIFA CHA VIJANA (YUNA) kimesema kwamba mvua, mafuriko na mapigano ya wakulima na wafugaji yanasababishwa na mabadiliko ya tabianchi na kuomba nchi wanachama kuja na mpango mkakati wa muda mrefu kukabiliana na majanga hayo. 

Akizungumza na vijana kutoka Asasi mbalimbali za vijana nchini kwenye mkutano wa kujadiliana yaliyojiri katika mkutano wa 19 wa mabadiliko ya tabianchi (COP 19) uliofanyika Warsaw, Poland Afisa Mradi wa Jukwaa la Mabadiliko ya tabianchi, Fazal Issa, amesema kwamba mabadiliko ya tabianchi yamesababisha hasara na vifo kutokana na mvua kubwa zinazosababishwa mabadiliko hayo ya tabianchi.

“kwa mantiki hiyo wanachama kutoka nchi 194 kwenye mkutano wa COP 19 nchini Warsaw, Poland walikubaliana kuja na mkakati wa muda mrefu kushughulikia mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha mvua na mafuriko sehemu nyingi duniani,” amesema.
DSC_1265DSC_1238
Afisa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi, Fazal Issa, akiwasilisha ripoti yao ya ushiriki wa vijana na mambo waliokubaliana na wanachama na Asasi za kiraia katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na umuhimu wa kupunguza hewa ukaa duniani.

Issa amesema kwamba moja ya makubaliano ya mabadiliko ya tabianchi ni kuja na mkakati wa teknolojia na habari ili kuweza kupiga hatua katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia teknolojia zaidi kupunguza hewa ukaa kwenye anga ya duniani.

Amesema pia kwamba katika mkutano huo wajumbe walikubaliana katika kutengeneza mfumo wa kifedha wenye kuwezesha kamati na tume mbalimbali za kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuchangisha fedha kutoka kwa wanachama mbalimbali duniani.

“mpaka sasa kamati ya utendaji wa mabadiliko ya tabianchi imeshakusanya karibu Tsh 33 billioni katika kushughulikia matatizo ya mabadiliko ya tabianchi duniani,” alilisitiza
DSC_1273
Mkuu wa kitengo cha Model UN-YUNA , Adam Anthony, akizugumzia ushiriki wa vijana na Asasi za kiraia katika mkutano wa COP 19 uliofanyika nchini Poland na umuhimu wa wanachama kukubaliana kupunguza hewa ukaa wa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), Dkt. Lwidiko Edward , amesema wamekuja na mkakati wa kutoa taarifa kwa vijana wenzao ya juu ya yaliojiri katika mkutano wa tabianchi na nafasi ya vijana katika kupambana na matatizo ya tabianchi duniani.

Dkt. Edward, aliongeza kuwa katika mkutano wa COP 19 vijana waliweza kushiriki kikamilifu katika kupeleka agenda zenye maslahi mapana kwa vijana na vizazi vijavyo na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa vijana duniani.

“wanachama wa mabadiliko ya tabianchi duniani wamekubaliana kupunguza hewa ukaa ili kupunguza joto duniani kwa kuanzia ni kwenye nchi zenye viwanda vingi,” amesema.
Amesema pia mabadiliko ya tabianchi katika nchi zinazoendelea inaonekana dhahiri kwenye sehemu zenye ukame kwa sasa na mapigano ya wafugaji na wakulima ni mifano hai ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika nchi zinazoendelea.

Dkt. Edward, amesema kwamba kupunguza hewa ukaa duniani ni muhimu hata kama baadhi ya nchi tajiri zinategemea viwanda katika kukuza chumi zao na kuleta maendeleo kwa watu wao.
DSC_1250
Vijana wakiuliza maswali mbalimbali juu ya ukweli kwamba Je sauti ya vijana inasikika katika mikutano ya COP duniani.
DSC_1254
DSC_1295
Allyah Mohammed kutoka YUNA, akizungumza kuhusu swala la jinsia na ushiriki wa Mwanamke katika mabadiliko ya Tabianchi kwa sababu wanawake ndio wanaoathirika zaidi na mabadiliko ya Tabianchi duniani.
DSC_1290
Imman Khatib kutoka YUNA akizugumza kuhusu swala la kupata mafunzo mbalimbali kuhusu mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa vijana na hasa wasichana ili wawe na uelewa kuhusu mambo hayo.
DSC_1278
Sehemu ya vijana walioshiriki mkutano huo ulioandaliwa na YUNA kwa maslahi ya vijana wa Tanzania.
DSC_1227

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA LEO

$
0
0
 Vijana  wa  UVCCM mkoa  wa Iringa na Mbeya  wakiwa  wamelibeba  jeneza  lenye  mwili wa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emanuel Mteming'ombe leo  wakati  wa kuelekea  kanisani kwa ibada kabla ya mazishi yake  yaliyofanyika kijijini Kwake Rujewa Mbarali mkoani Mbeya
Naibu katibu mkuu wa CCM Bara Bw Mwigulu Nchemba wa pili kulia akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu kulia na viongozi  wengine nyumbani kwa marehemu Mteming'ombe Rujewa Mbarali

Mkuu  wa mkoa  wa Mbeya  Abas Kandoro wa pili  kushoto akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma katikati
Familia ya marehemu na ndugu mbali mbali  wakiwa kanisani kanisa la RC Rujewa  leo
Waombolezaji  wakiwa ibadani  leo
Naibu katibu mkuu CCM Bara Bw Mgulu Nchemba akiongoza  waombolezaji  kutoa  heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emanuel Mteming'ombe leo katika kanisa la RC Rujewa Mbarali mkoani Mbeya
Mkuu  wa mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma akitoa  heshima zake
Mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu  akiaga mwili  huo
Waombolezaji  wakikimbia mvua  kubwa iliyonyesha kwa dakika kama 10  hivi mara baada ya  mwili kufika makaburini
Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu  akisoma historia ya marehemu Mteming'ombe huku naibu katibu mkuu  CCM Bara Bw Nchemba akionyesha kufuta machozi
Mjane  wa Mteming'ombe akiweka maua
Mzee Mteming'ombe akiweka shada la maua
Naibu katibu mkuu CCM Bara  Mgulu Nchemba  akiongoza  waombolezaji kuweka shaba la maua  katika kaburi la aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa marehemu Emanuel Mteming'ombe leo katika makaburi ya RC Rujewa Mbarali Mbeya
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu  akiweka shada la maua
mkuu  wa  mkoa wa Iringa Dr Ishengoma  akiweka  shada la maua
Mkuu  wa mkoa  wa Mbeya Abas  Kandoro akiweka shada la maua
Kanali Mjengwa akisalimiana na naibu katibu mkuu CCM Bara Mgulu Nchemba  leo nje ya kanisa la RC Rujewa baada ya  kukutana kwa shughuli za mazishi ya aliyekuwa katibu wa CCM mkoa  wa Iringa Emanuel Mteming'ombe
Na Francis Godwin Blog


MWENYEKITI wa  Chama cha  mapinduzi (CCM) Taifa  Dr  Jakaya  Mrisho  Kikwete  ametuma  salam  za rambirambi kwa  uongozi  wa  CCM mkoa  wa  Iringa na  familia ya aliyekuwa  katibu  wa CCM mkoa  wa  Iringa Emanuel Mteming'ombe aliyefariki  dunia juzi na kuzikwa  leo katika mji  wa  Rujewa Mbarali  mkoani Mbeya.

Salam  hizo  za Rais Dr  Kikwete  zilitolewa  jana   wakati  wa mazishi  ya Mteming'ombe  na naibu  katibu mkuu  CCM Bara  Bw Mwinhulu Nchemba  ambae alikiwakilisha  chama taifa  katika mazishi hayo .

Alisema  kuwa Rais Dr  Kikwete  ambae  yupo  nchini Marekani kwa ziara  za  kiofisi amepokea  kwa masikitiko makubwa  taarifa  ya  kifo  cha katibu  huyo na kuwa alitamani  sana  kuweza kufika Rujewa mkoani Mbeya  kwa ajili ya  kushirikia mazishi  hayo ila ameshindwa .

" Nitoe  salama za aina  tatu  salama ya kwanza  kutoka kwa mheshimiwa Rais Dr  Kikwete akiwa  mwenyekiti  wetu wa Chama taifa  amepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa  hii ya kifo  na wakati anapata  taarifa  hii tayari  alikuwa katika ndege  kuelekea  nchini Marekani .....kama  tunavyojua Rais  wetu  ni mwepesi  kufika katika misiba ila ameshindwa na  kuniagiza  mimi  kutoa  salam zake kwa niaba yake"
Hata  hivyo  alisema  kuwa  salama  za pili ni  kutoka kwa katibu mkuu wa CCM Taifa  ambapo amepokea kwa masikitiko makubwa  zaidi  kutokana na kifo  hicho  kutokana na katibu  huyo marehemu Mteming'ombe  enzi  za uhai  wake  alikuwa msaada mkubwa  sana kwa chama  kutokana na kuwa mwepesi  zaidi.

Alisema kuwa  wao kama  chama   wataendelea  kuwa karibu na familia ya marehemu ikiwa ni pamoja na kuitunza  familia  hiyo.

Kwa  upande  wake  mkuu wa mkoa  wa  Iringa Dr Christine Ishengoma akitoa  salama za  serikali mkoa  wa Iringa  kufuatia  kifo  hicho alisema  kuwa katika  kipindi  hiki cha maombolezo  na  baada ya maombolezo  viongozi wa chama na  serikali mkoa  wa Iringa  hawana budi kuendelea  kufanya kazi kwa  kushirikiana  zaidi kama njia ya  kumuenzi Mteming'ombe.

Huku  mkuu  wa  mkoa  wa Mbeya Abas  Kandoro akisisitiza viongozi  wa umma na chama  kujenga  utamaduni  wa kushirikiana na kuacha  tabia ya kujitenga na jamii.

Wakati  huo  huo waombolezaji  waliofulika makaburini hapo walionyesha  kushindwa  kujizuia kushangilia kwa  furaha  kubwa wakati mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca  Msambatavangu  akisoma mchango wa  waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowasa mchango  wa Tsh milioni 1  alioutuma kwa uongozi  wa CCM mkoa wa Iringa kwa ajili ya shughuli  za mazishi  ya  Kiongozi  huyo.
Katika  tukio  jingine  vijana  wanaosadikika kuwa na wafuasi  wa Chadema  wakiwa na sare za chama hicho wamejikuta  wakichezea  kichapo  kutoka kwa vijana  wa UVCCM baada ya kuwavamia  vijana hao katika kanteni ya  polisi Rujewa ambako  walikuwa  wakijipumzisha kwa uchovu .
Imedaiwa  kuwa  vijana wapatao wanne  walifika eneo hilo na kuanzisha  vurugu hali  iliyopelekea vijana wa UVCCM kutoka mkoa  wa Iringa na Mbeya  kuwafunza adabu na polisi  kuwakamata  vijana  hao wa Chadema na kuwatupa mahabusu.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa  wa Iringa Tumain Msowoya  alisema amezipata habari  hizo japo alisema kuwa hakuna majeraha makubwa yaliyowapata  vijana wa CCM mbali ya wavamizi hao kuwa shambulia kwa chupa .



AWALI AKISOMA WASIFU WA MAREHEMU EMMANUEL MTEMING’OMBE ,MWENYEKITI  WA CCM MKOA WA IRINGA JESCA  MSAMBATAVANGU ALISEMA

Marehemu Emmanuel Mteming’ombe alizaliwa tarehe 25/ 06/ 1956 katika kijiji cha Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.

2.     ELIMU NA MAFUNZO.

Marehemu Emmanuel Mteming’ombe alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Chimala, Mbeya kati ya mwaka 1972 – 1978. Baada ya kumaliza darasa la saba, marehemu alijiunga na masoma ya sekondari katika shule ya sekondari ya wavulana Songea kuanzia mwaka 1979 – 1982.
Kati ya mwaka 1986 -1989 marehemu alijiunga na Chuo cha Uganga Songea akisomea kozi ya Utabibu.

3.     UTUMISHI WA SERIKALI.

Mwaka 1991, marehemu aliajiriwa serikalini kwa cheo cha Medical Assistant (Tabibu), kazi aliyofanya kwa miaka mnne hadi mwaka 1994 alipoamua kuacha kazi na kufungua Duka la Dawa na Zahanati yake binafsi.

4.     UTUMISHI KATIKA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Nyota njema huonekana asubuhi. Marehemu Emmanuel Mteming’ombe akiwa Chuo cha Utabibu Songea kati ya mwaka 1986 – 1989 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa vijana Tawi kwa muda wote aliokuwa Chuoni hapo.

Mara baada ya kumaliza masomo yake ya Utabibu alipata tena nafasi ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM wa kata ya Rujewa, Mbarali kuanzia mwaka 1990 – 1994. Kutokana na uhodari aliouonesha, marehemu mwaka 1994 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Rujewa hadi mwaka 1999.

Mwaka 1998, Marehemu Emmanuel Mteming’ombe alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, nafasi aliyoshika hadi mwaka 2003. Katika uchaguzi Mkuu wa Serikali wa mwaka 2000,Marehemu alichaguliwa kuwa Diwani wa kata ya Rujewa, nafasi aliyoshika hadi octoba, mwaka 2005.

Kutokana na uwezo wake mkubwa wa Uongozi aliouonesha katika nafasi mbalimbali za uongozi, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokutana tarehe  26 – 27/ 03/ 2003 ilimteua kuwa Kaimu Katibu wa CCM wa Wilaya na kupangiwa kwenda kufanya kazi katika wilaya ya Kyela. Baada ya kuonekana anamudu nafasi ya Katibu  wa CCM wa Wilaya, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa iliyokutana tarehe 19 -20/ 03 2004 ilimthibitisha kuwa Katibu wa CCM wa Wilaya.

Marehemu Emmanuel Mteming’ombe, akiwa Katibu wa CCM wa Wilaya alifanya kazi katika Wilaya za Kyela, Ireje, Mbozi ambako alionyesha uwezo mkubwa wa Uongozi na kuwa tegemeo la Chama Cha Mapinduzi.

Marehemu Emmanuel Mteming’ombe aliteuliwa kuwa Kaimu Katibu Wa CCM wa Mkoa wa Mbeya, kuanzia tarehe 29/ 01/ 2008 na baadaye kuwa Katibu wa Mkoa na kumpangia kwenda katika Mkoa wa Ruvuma ambako alifanya kazi hadi tarehe 28/ 05/ 2012 alipohamishiwa Mkoa wa Iringa.
5.     UGONJWA.

Marehemu Emmanuel Mteming’ombe alianza kuumwa tarehe 02/ 12/ 2013 akieleza kuwa baada ya kuonana na Daktari iligundulika kwamba anasumbuliwa na homa ya Matumbo (Typhoid), Athma na Figo yake ya upande wa kushoto ikaonekana kuwa ina matatizo na kupewa dawa ambapo alirejea nyumbani kwake na kuendelea kutumia.

Ilipofika tarehe 17/ 12/ 2013 usiku, Marehemu alizidiwa na kupelekwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Iringa ambapo madaktari walijitahidi kumhudumia, lakini ilipofika saa 8 usiku wa tarehe 19/ 12/ 2012 alifariki Dunia.
Marehemu ameacha Mjane na Watoto Watatu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe
Amen.

KIONGOZI WA BENDI YA THE NGOMA AFRICA BAND YA UJERUMANI AKUTANA NA ANKAL JIJINI DAR

$
0
0
 Ankal akimkabidhi zawadi ya Krismasi  na kadi Kamanda wa FFU Ughaibuni The Ngoma Africa Band ya Ujeruman, Ras Ephraim Makunja, a.k.a Field Marshal wa jamii ya Annunaki walipokutana leo katikati ya jiji la Dar es salaam na kufanya mazungumzo ya faragha ya saa moja katika kiota cha Break Point cha mjini. Katika mazungumzo yao waliongelea mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuendeleza undugu uliopo baina ya Globu ya Jamii na FFU Ughaibuni, na kupanga tarehe ambazo The Ngoma Africa Band itakuwa huru kuja kufanya maonesho kadhaa nchini Tanzania.
 Ras Makunja anarivenji kwa kumkabidhi Ankal zawadi ya moja ta T-Shirt kibao alizomletea zikiwa na logo ya Globu ya Jamii.
 Ankal akimshukuru Ras Makunja kwa zawadi hiyo mwanana
Ras Makunja akiwa na mjomba wake akijiondoa eneo la tukio taratibu huku kakumbatia zawadi yake ya Krismasi na kadi. Meno yote arobaini yako nje kwani hakutegemea kupata heshima hii. Picha kwa hisanio ya mpiga picha wa The Ngoma Africa Band aliyeongozana naye katika ziara hii ya mapumziko jijini Dar es salaam. 

Mara ya mwisho kufika Bongo kwa Ras Makunja ilikuwa miaka sita iliyopita, na ameshangazwa na mabadiliko na maendeleo makubwa aliyotaona kila mahali, kuanzia nyumbani kwake mtaa wa Aggrey ambako mbavu za mbwa yao imeshajengwa bonge la Ghorofa, nusura apotee, na huko kwake Segerea ambako anasema kuna lami mpaka jikoni....

KIMENUKA BUNGENI - RAIS KIKWETE ATENGUA NYADHIFA ZA MAWAZIRI WANNE,YUMO NCHIMBI,NAHODHA,KAGHASHEKI NA MATHAYO.

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi  Kaghasheki amejiuzulu wadhifa wake baada ya mjadala mkali wa Bungeni mjini Dodoma hivi sasa. Habari zaidi kwa kirefu zitakuja baadaye. Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini. 

Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa, kuchomewa nyumba, mifugo kuuawa, kupigwa,kubakwa na uporaji.

Operesheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo wawajibike.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo David, naye pia amegoma kujiuzulu baada ya kutoa utetezi wake mrefu. Amedai pia kuwa ameonewa.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki zichukuliwe. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa ameutaja kuwa ni  muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni busara ushauri wa wabunge utekelezwe. Amebainisha kuwa hata baada ya kuongea na Rais.  mkuu wa nchi ameridhia tume iundwe na kila aliyehusika awajibike. 
 
Amesema Rais ameshauri
 kutengua uteuzi wa mawaziri wote wanne ( Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Wazir wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo, na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki) kama ambavyo wabunge walivyopendekeza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe  James Lembeli (pichani juu) amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya kamati kimsingi yote yamekubalika. 
 
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa  Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.

Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu  waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.

Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha.
Spika amuomba Mwanasheria mkuu kutumia kifungu kuongeza muda. Naye ameomba  kuundwa tume ya kisheria ya mahakama. Spika Mhe. Anne Msekwa ameahirisha Bunge (saa tatu na dakika nne usiku huu) hadi saa tatu kesho asubuhi. 
SOURCE MICHUZI BLOG.
 Juu ni Dkt Emmanuel Nchimbi na chini ni Mhe Shamsa Vuai Nahodha

MAMA REGINA LOWASSA ASHIRIKI CHAKULA CHA MCHANA PAMOJA NA WATOTO WENYE ULEMAVU JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akishiriki kuhudumia chakula watoto wenye ulemavu  katika Kituo cha Huduma ya Walemavu kinachomilikiwa na Jimbo Kuu Katoliki jijini Arusha kilichopo Monduli wakati alipokwenda kushiriki nao Ibada ya X-Mass pamoja na kuzungumza na kula nao chakula cha mchana.

Aowa Wanafunzi Mtu na Dada Yake Wilayani Nkasi

$
0
0

 Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba (kushoto) akipitia kitabu cha orodha ya matukio ya dawati hilo. Kulia ni msaidizi wake.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye
=======  ========  ========
Aowa Wanafunzi Mtu na Dada Yake

JESHI la Polisi Wilaya ya Nkasi kupitia dawati la Jinsia na Watoto, linamshikilia Pius Jacob Mkazi wa Kijiji cha Chala kwa kosa la kuoa mtu na dada yake, ambapo mdogo mtu alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kabwe wilayani Nkasi.

Jacob alikamatwa na Polisi wa Dawati la Jinsia na watoto Kituo cha Nkasi ikiwa ni wiki moja tangu amchukue kwa nguvu binti huyo wa darasa la tano (umri miaka 12) na kuja kuishi naye kama mke na mume huku akiwa tayari amemuoa binti mwingine wa kwanza mwenye umri wa miaka 16 ambaye pia ni dada wa binti wa pili.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba alisema walimfuatilia Jacob na kumkamata baada ya wao kupewa taarifa na mmoja wa majirani wa mtuhumiwa kuwa alikuwa akiishi kinyumba na wanafunzi hao.

“…Tulikuwa katika ziara zetu za kawaida zilizoambatana na siku 16 za kupinga ukatili tukizunguka baadhi ya vijiji vya wilaya yetu, ndipo raia wema walituarifu kuwepo kwa tukio hilo na kuanza kufuatilia hatimaye kumkamata mtuhumiwa,” alisema Kisimba.

Tayari mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desenba 10, 2013 kwa kosa la kumuoa mwanafunzi na kubaka katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa kujibu mashtaka ya tuhuma zake.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye alisema baada ya kufuatilia zaidi wamebaini hata binti (16) aliyemuoa wa kwanza alikuwa ni mwanafunzi haijulikani alitumia mbinu gani za kumpata na kuanza kuishi naye kama mke na mume.

Aidha ameongeza kuwa kwa mujibu wa tarifa ambazo walizipata kutoka kwa majirani inadaiwa binti wa pili alimpata kwa kutumia nguvu na vitisho, kwani alimfuata nyumbani kwao na kudai anakuja kuwasalimia lakini baada ya kufika kwake alimjulisha binti huyo kuanzia sasa wewe ni mke wangu na kuanza kuishi naye.

“…Hadi Polisi na Ofisi ya Ustawi wa Jamii tunafikiwa na taarifa hizo inadaiwa mtuhumiwa huyu alikuwa tayari ameishi na binti huyu wa pili kwa wiki nzima nyumbani kwake, na majirani walijua baada ya binti wa pili (12) kuanza kulalamika kwao kuwa alikuwa amechukuliwa kwa nguvu na kulazimishwa kuolewa,” alisema Mdenye.

Juhudi za kumpata mtuhumiwa kuzungumzia tuhuma zake hazikuweza kuzaa matunda baada ya kuwa mahabusu akisubiri mwenendo wa kesi yake inayomkabili. 

Hata hivyo matukio ya ukatili yanayoripotiwa polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Nkasi yamekuwa yakipungua kutoka mwaka hadi mwaka, kwani kwa mujibu wa takwimu za dawati hilo kwa mwaka 2012 kulikuwa na kesi 224 za ukatili zilizoripotiwa, ilhali kwa mwaka 2013 jumla ya kesi 143 zimeripotiwa wilayani hapo.

*Imeandaliwa na www.thehabari.comkwa ushirikiano na TAMWA.

AIESEC Exchange Program

$
0
0

AIESEC University of Dar es Salaam, is a local branch of AIESEC,  an
international leadership development organization which runs a global
exchange program, entirely driven by students and recent graduates.

AIESEC was established over 60 years ago and is present in over 1700
Universities in over 124 countries across the world.

What's more, since its foundation, AIESEC has been entirely youth-led.
This means every single year, new leadership teams are elected from
the membership at every level of the international association.

This
means we have over 1,000,000 alumni who've been through an 'AIESEC
Experience' many of whom have gone on to do incredible things. Our
alumni include leaders within business, global politicians and even a
Nobel Peace Laureate.

The organization works towards the vision of “peace and fulfillment of
humankind’s potential.” The main channel to do this is by providing
young students the opportunity to experience living and working in a
different culture to understand and appreciate diversity, whilst
developing both personally and professionally.  AIESEC in Tanzania has
sent out more than 300 students in the last 15 years since
establishment.  

These students have worked as volunteers and
professionals in over 124 countries worldwide.  Students who embark on
an exchange with us have a multicultural experience (Global Mindset),
self development (they gain skills and competencies that are useful
for their career life) and become more social responsible.

So, if there are university or college students in Dar es Salaam who
want to experience a 6 week volunteering program abroad, or bachelor
graduates who want to work abroad, please contact us.

ZITTO KABWE APOKELEWA KWA KISHINDO KIGOMA LEO.

$
0
0
Mbunge wa Kigoma kaskani Mh Zitto Kabwe akisalimiana na wakazi wa Kigoma mara baada ya Kuwasili kigoma mapema leo asubuhi, ambapo wakazi wa kigoma wamejitokeza kwa wingi kumpokea Mbunge wao.
 Zitto Kabwe akiwa katika gari la wazi mara baada ya kutua kigoma asubuhii ambapo amepata mapokezi ya kishindo.

MARGARETH SIMALENGA ATUNUKIWA SHAHADA YAKE CHUO KIKUU CHA MZUMBE

$
0
0
IMG-20131221-WA000 
Margareth Simalenga, akipozi kwa picha mara baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika Uongozi wa biashara (usimamizi wa mashirika) yaani Master in Business Administration (Corporate Management) katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Cumpas ya Dar es salaam yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
IMG-20131221-WA001
Akiwa katika pozi la picha huku akiwa ameshilikia maua mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya uongozi wa biashara.
IMG-20131220-WA027

Tishio la kukua kwa taka za elektroniki duniani

$
0
0
Moja ya FAIDA zinazooenakana kuletwa na ndugu, jamaa na marafiki walio nje ya nchi ni pamoja vifaa kama simu, tarakilishi (kompyuta) na vingine vya alektroniki ambavyo kwa wengine ni kigezo cha maendeleo ama kuendana na maisha ya kisasa.

Lakini vifaa hivyo ambavyo vinaanza kuwa tishio la mazingira duniani kutokana na TAKATAKA zinazotokana na vifaa na bidhaa zinazoendana nazo. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa hivi karibuni, masalia ya vifaa hivi vya elektroniki inategemewa kukua kwa asilimia 33 kwa miaka mine ijayo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uzito wa vifaa vya elektroniki pamoja na majokofu inategemewa kuongezeka kutoka tani milioni 48.9 mwaka 2012 mpaka tani milioni 65.4 mwaka 2017.
Uzito huu ni sawa na uzito wa mapiramidi 11 ya Misri

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

SALAM ZA KRISIMASI KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS

UZINDUZI WA RIPOTI YA UWEZO

$
0
0
 Msanii Mrisho Mpoto akielezea kupitia mashairi
 Mama Zaida Mgalla akitoa ufafanuzi kwa ripota wa Uwezo TV Bi. Melania Mhagama
 Mgeni Rasmi akionyesha ripoti baada ya kuzindua.

Wakati ambapo asilimia 100 ya watoto wa Darasa la 3 na kuendelea wanapaswa kuweza kusoma na kufanya hesabu za kiwango fulani, matokeo ya Uwezo yanaonyesha kwamba ni wachache tu ndiyo wanaoweza kufanya hivyo.

Katika Darasa la 3, mmoja kati ya watoto wanne anaweza kusoma Kiswahili kwa kiwango sahihi. Shule za binafsi zinafanya vizuri zaidi kidogo kulinganisha na zile za Serikali, ambapo asilimia 61 ya watoto walio na umri chini ya miaka 9 hawawezi kusoma Kiswahili na kufanya Hesabu za Kuzidisha kulinganisha na asilimia 85 ya wenzao walio katika shule za Serikali.

Matokeo haya yalitangazwa na Twaweza, inayosimamia Tafiti ya Uwezo, katika ripoti yake ya tatu ya Tathmini ya Mwaka ya Ujifunzaji. Matokeo haya yamejikita zaidi kwenye tathmini kubwa kabisa ya mwaka kwa ngazi ya kaya inayopima stadi za kusoma na kufanya hesabu za msingi za watoto.

Tathmini ilifanyika nchi nzima mwaka 2012; ikipima watoto 104,568 wenye umri kati ya miaka 7 hadi 16 katika kaya 55,191, katika maeneo (vijiji) 3,752, kwenye wilaya 126 za Tanzania.


Tathmini ya Uwezo inaonyesha kwamba utendaji uko duni nchini kote. Matokeo muhimu yalikuwa:

Stadi ya kusoma Kiswahili
Matokeo bado ni duni na hayajabadilika sana tangu 2011Mtoto 1 tu kati ya 4 (26%) wa Darasa la 3 anaweza kusoma hadithi ya ngazi ya Darasa la 2.

Kwa Darasa la 7, mtoto 1 kati ya 4 (24%) bado hakuweza kusoma hadithi ya ngazi ya Darasa la 2.

Stadi ya kusoma Kiingereza
Matokeo yalikuwa mabaya zaidi kuliko katika Kiswahili

Katika Darasa la 3, 1 tu kati ya watoto 10 (13%) aliweza kusoma hadithi ya ngazi ya Darasa la 2.

Hata katika Darasa la 7, ni watoto 5 kati ya 10 walioweza kusoma hadithi ya ngazi ya Darasa la 2.
Kufanya hesabu
Matokeo yamepanda zaidi kuliko mwaka 2011 lakini bado ni duni
Katika Darasa la 3, zaidi kidogo ya watoto 4 tu kati ya 10 (44%) walioweza kufanya Hesabu za kuzidisha.

Kufika Darasa la 7, mtoto 1 tu kati ya 10 (11%) aliweza kufanya Hesabu ya ngazi ya Darasa la 2.

Matokeo haya yanaonyesha kwamba kundi kubwa kabisa la watoto halipati ujuzi muhimu katika elimu ya msingi. Hata wanapomaliza elimu ya msingi, watoto bado wanashindwa kufanya zoezi la ngazi ya Darasa la 2.

Kuna tofauti kubwa nchini:
Tathmini ya Uwezo inaonyesha jinsi tofauti ya kimatabaka inavyozidi kukua. Watoto katika maeneo ya mijini wanafanya vizuri zaidi kuliko wenzao wa vijijini katika masuala ya kusoma na kuandika.

Watoto wanaotoka kwenye kaya zenye kipato cha juu vilevile walionekana kufanya vema zaidi katika stadi hizi za msingi, sawa sawa na watoto wanaosoma katika shule za binafsi. Ingawa matokeo ya kujifunza kwa ujumla wake ni duni, tofauti hizi zinazozidi kukua zinaonyesha kuwa mfumo wa elimu unawanufaisha zaidi wale wenye hali bora.

Watoto wote, bila kujali umri, darasa au hadhi ya shule walijaribiwa kwa kutumia ngazi ya kusoma na kufanya hesabu ya Darasa la 2. Matokeo muhimu yalikuwa:

Mahali Katika umri wa miaka 9, ni watoto 3 tu kati ya 10 (32%) wa mijini walio na ujuzi huo wa msingi, kulinganisha na mtoto 1 tu kati ya 10 (11%) wa vijijini.

Utajiri Katika umri wa miaka 9, ni watoto 2 tu kati ya 10 (21%) kutoka katika kaya tajiri zaidi walio na ujuzi huo wa msingi, kulinganisha na chini ya mtoto 1 kati ya 10 (6%) kutoka kaya maskini.

Aina ya Shule Katika umri wa miaka 9, ni zaidi kidogo tu ya mtoto 1 kati ya 10 (15%) katika shule za umma aliyefaulu majaribio hayo wakati ambapo ni watoto 4 kati ya 10 (39%) kutoka shule binafsi walioweza kufanya hivyo.

 “Kuna habari kuu mbili katika elimu ya Tanzania leo,” alisema Zaida Mgalla, Mratibu wa Nchi wa Uwezo Tanzania “Kwanza, watoto walio wengi hawajifunzi kitu. Pili, sisi ni jamii ya matabaka mawili – lile lenye utajiri zaidi au la mjini au linaloweza kumudu gharama za shule za binafsi na hivyo watoto wao kufanya vizuri zaidi shuleni kuliko watoto wengine.

Linapokuja suala la elimu, Tanzania si nchi moja.” Tathmini ya Uwezo ya mwaka 2012 iliendeshwa na wananchi waliojitolea 7,560, ambao walisimamiwa na washirika katika wilaya 126 nchini (Wilaya za Mtwara hazikujumuishwa kwa sababu viongozi wa Mkoa hawakuruhusu utafiti kuendeshwa mwaka 2012). Lengo lilikuwa ni kuwashirikisha wananchi katika mchakato wa kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuhakikisha watoto wetu wanajifunza.

Mkuu wa Twaweza, Rakesh Rajani, alisema “Kuinua ubora wa elimu ni jukumu la msingi la Serikali; hata hivyo jukumu hili inatuhusu sote. Hatua zichukuliwe katika ngazi zote, na kila mmoja – kuanzia wazazi hadi watunga sera, kuanzia walimu hadi maofisa wa wilaya – kila mmoja ana mchango wa kipekee katika kuhakikisha watoto wetu wanajifunza.”
Mgeni Rasmi Salum Mjagila, Mkurugenzi, Elimu ya Watu Wazima MOEVT, akikabidhi ripoti kwa mwakilishi wa wanafunzi ambae pia ni ripota wa Uwezo TV, Bi. Fatma Bakari
Rakesh Rajani, John Ulanga, Zaida Mgalla na waalikwa wakifurahia jambo

HOTUBA YA MH ZITTO Z. KABWE ALIOZUNGUMZA LEO - KIGOMA

$
0
0

HOTUBA YA MH ZITTO Z. KABWE - KIGOMA – 21 DESEMBA 2013

Leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji. Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama Mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la Ujiji.
 

Tuna mengi ya kujivunia kama taifa lakini Ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika historia. Watu wa Ujiji mlipokea harakati za kudai uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya uhuru yalipoanza. Watu wa Ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Na Jimbo la Kigoma Mjini ilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa kutoa mbunge wa CHADEMA mwaka 1995.

 Kabla ya hapo mlitoa madiwani wengi mwaka 1994. Wakati Watanzania wengine wakiwa wanajiuliza mara mbili mbili kuhusu kujiunga na vyama vipya vilivyoanzishwa, watu wa Ujiji, watu wa Kigoma hamkusita kupokea mabadiliko. Wengi wamepoteza maisha yao, wengine kazi zao na wengine hata ndoa zao katika kupata mbegu ya mabadiliko katika nchi yetu. Nawataka msichoke. Wekeni nguvu mpya katika kusimika mabadiliko kwani bado kazi ya kuimarisha demokrasia katika nchi yetu haijaisha na inahitaji uvumilivu, kusameheana na kuaminiana.
 
Na nchi yetu Tanzania ni nchi inayoonyesha uwezo mkubwa katika kupendana, kuaminiana, kuvumiliana na hata kusameheana. Na haya si maneno tu ambayo ninayazungumza kama mwanasiasa. Hii ni hali halisi na maisha niliyoyaishi kwa mifano nilipokuwa ninakua na kusoma katika shule ya Msingi Kigoma na baadaye Shule ya Sekondari Kigoma. Malezi yangu yalikuwa yanaongozwa na jamii nzima ya Kigoma.

 Nimekuwa nikiwaeleza rafiki zangu niliokutana nao kwenye masomo na kwenye siasa kwamba nimeanza kuvaa viatu kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la tatu. Viatu hivyo viliitwa 'asante Salim' vilivyokuwa vinatengenezwa na Kampuni ya Bora Shoes. Vililinunuliwa na mama Coretha Furugunya ambaye tulikuwa tunakaa mtaa mmoja wa Kisangani Mwanga.

Mama Coretha hakuninunulia viatu kwa sababu alikuwa ana uwezo mkubwa, la hasha! Alifurahishwa na matokeo yangu ya mitihani ya darasa la pili kwenda la tatu. Ninaamini kitendo cha mama huyu ni ushahidi wa uungwana, upendo na hata uwajibikaji ambao tunao sisi watanzania. Uwajibikaji kwani alichukua jukumu kunilea ingawa hakuwa mzazi wangu, lakini aliona kuwa kama mwanajamii ana nafasi kubwa katika kuwaendeleza watoto wote. 

Jamii hii ya watu wa Kigoma ilinifunza kuwa nikijitahidi na kukazana kwa bidii kwenye masomo na majukumu, nitafanikiwa. Siwezi kusahau somo hili katika maisha yangu na ni somo hili ndilo limenifanya nijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuwatumikia kwa uadilifu na mafanikio ya hali ya juu sana.
 
Nikiwa nimejaa matumaini haya kuhusu wananchi wenzangu, leo nataka niwakumbushe kwa nini kama jamii tulichagua kufuata njia ya demokrasia. Demokrasia ina maana pale ambapo inatumika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wananchi. Maisha yanayotakiwa ni yale yanayomwezesha mwananchi kupata huduma zake stahili kama Elimu, Afya, Maji na miundombinu. Demokrasia haina maana pale wananchi wanakufa njaa kwa kukosa ajira na kukuza umasikini. 

Demokrasia inahusu maendeleo. Tumejitahidi kwa upande wetu kuondoa mkoa wa Kigoma kutoka mikoa isiyo na miundombinu kabisa ya maendeleo mpaka kuwa mkoa unaotumika kama mfano kwa miradi mingi ya Maendeleo ikiwemo Daraja la Malagarasi, Uwanja wa ndege wa Gombe-Mahale, barabara za lami na upanuzi wa Bandari, ujenzi wa bandari ndogo mpya na ujenzi wa kituo cha Usafirishaji Mwandiga. 

Asije mtu akasema yeye ndio kafanya haya. Haya ni matunda ya nyinyi watu wa Kigoma kupokea demokrasia na bila woga kuchagua viongozi wenu bila kujali vyama bali kwa kuangalia uwezo. Haya ni matunda ya viongozi wenu kupaza sauti yenu kwenye baraza la Taifa, Bunge. Haya ni matunda ya uvumilivu wenu na uamuzi wenu wa kutaka maendeleo. Juhudi hizi lazima ziendelezwe kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa nafasi ya mkoa wa Kigoma katika uchumi wa Tanzania inaonekana dhahiri na hivyo kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa kituo cha biashara katika nchi za maziwa makuu.
 
Lakini tukumbuke pia kuwa Demokrasia ni Uwajibikaji. Katika kipindi cha utumishi wangu kwenu,kutokana na malezi niliyoyapata kutoka kwenu,nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Serikali inawajibika kwa Wananchi. Nakumbuka wakati napambana kuhusu sheria mbovu ya madini kuna watu hapa nyumbani walisema 'sasa huyu kawa mbunge wa Taifa' lakini watu wengi zaidi wakasema tumemtuma Dodoma kusemea Watanzania wote na sio Kigoma tu. Tuliweza ndani ya miaka mitano kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye sera ya Madini na sheria ya madini ambapo baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayafikiriki sasa yametungiwa sheria ikiwemo Serikali kuwa na hisa kwenye migodi, Tanzanite kumilikiwa na Watanzania sio chini ya asilimia 50 na kuzuia kabisa wageni kuchimba vito vya thamani. Uwajibikaji ulipelekea kumshinikiza Rais kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri kwa kuwafukuza mawaziri wanane mwaka jana. 

Hii ilitokana sio tu na hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu bali pia ushiriki mkubwa wa wananchi kupitia simu na mitandao ya kijamii ambapo wabunge walishinikizwa kuweka saini kwenye karatasi za kumtoa Waziri Mkuu. Toka wakati huo kumekuwa na utaratibu sasa ambapo wabunge hawaoni taabu kutaka uwajibikaji waziwazi ili kuzuia ubadhirifu wa fedha za Umma. Ni hivi jana tumeshuhudia mawaziri wanne wamejiuzulu na kufukuzwa kazi kutokana na kashfa ya operesheni Tokomeza ujangili iliyoibuliwa na ripoti ya kamati ya bunge. Mabadiliko haya ni hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia yetu. Pamoja na matunda haya mengi mazuri lakini bado kuna changamoto katika juhudi zetu.
 
Changamoto kubwa tuliyonayo wananchi ni kukosekana kwa imani katika demokrasia yetu.
Kutoaminiana. Ni dhahiri kuwa kutoaminiana katika nchi yetu kumekuwa kwa kiasi kikubwa. Taarifa za kitafiti zinaonyesha kuwa katika kila Watanzania kumi, wanane hawaaminiani. Ni changamoto kubwa sana. Wananchi wameacha kutuamini wanasiasa na wanasiasa wameacha kuaminiana wenyewe kwa wenyewe. Hivi sasa uongo umegeuzwa kuwa ukweli na ukweli umekuwa ni uongo. Hivi sasa ukitaka kuwa mwanasiasa maarufu inabidi ujue kudanganya na ukitaka kuitwa mwanasiasa msaliti inabidi uwe msema kweli. Kukosekana kwa uaminifu na kuaminiana imekuwa ni kansa katika siasa zetu. 

Itachukua muda mrefu sana kujenga demokrasia imara katika nchi yetu kama hatutapata jibu la changamoto hii ya kutoaminiana na kugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Hivi sasa ukweli umekuwa unatengenezwa badala ya kutafutwa. Ni majanga! Juzi bungeni Mwanasheria Mkuu wa Serikali alielekeza shutuma kwangu kwamba sikushirikiana na kamati maalum iliyoundwa na Bunge kufuatilia mabilioni ya uswisi na kwamba chini ya kiapo nilisema sina majina ya watu wenye akaunti huko Uswisi. Huu ulikuwa ni uongo. Ni uongo kwa sababu niliitika wito wa kamati hata nilipokuwa katika mafunzo ya mgambo huko Tanga na nilikutana nao mara nne. Ni uongo kwa sababu niliwapa wajumbe wa Kamati Maalaum maelezo na taarifa nyingi sana kuhusu utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na umiliki wa mali nje ya nchi kinyumecha sheria. 

Ni uongo kwa sababu mimi kutotaja majina haya haina maana sina majina, bali ni kwamba ninaheshimu utaratibu na nimeachia vyombo husika vikamilishe uchunguzi. Kwani mimi kama mtu binafsi nikianza kuchukua majukumu ya taasisi ninaweza kutia dosari harakati hizi muhimu na hata kupelekea mchakato mzima kuvurugika. Sitaingia mtego huu! Lakini hatua hii ya Mwanasheria Mkuu imenipelekea kujiuliza maswali mengi kwa mfano uongo kama huu ulifanywa kwa malengo gani? Na ninajikuta hata mimi ninaingia katika hali ninayoilalamikia ya KUTOAMINIANA
 
Lakini mtambue pia kuwa kutoaminiana kunaleta kutovumiliana. Hivi sasa kuwa na mawazo tofauti katika vyama vya siasa au hata asasi za kijamii ni uhaini. Lakini bila kuenzi tofauti za mawazo hatuwezi kujenga vyama imara wala Taifa imara. Demokrasia imara ni zao la tofauti za mawazo na uhuru wa mawazo. Kama hatuwezi kujenga vyama vinavyorutubisha uhuru wa mawazo na tofauti za mawazo, tutajenga Taifa lenye watu wenye kuogopa na waliojaa woga. Wanachama wanapoogopa uongozi ni udikteta, lakini uongozi unapoogopa wanachama ni demokrasia. Bila demokrasia ya uwazi na kuvumiliana tutakuwa Taifa la kidikteta. Lazima vyama vya siasa, viongozwe kwa namna ile ile ambayo Taifa litaongozwa.
 
Demokrasia bila kuaminiana, demokrasia bila kuvumiliana sio demokrasia ya kweli.
Juzi nilipoingia Bungeni kwa mara ya kwanza baada ya matukio kadhaa yanayoendelea ndani ya chama chetu nilikaa pamoja na mbunge Tundu Lissu. Wabunge wengine walidhani tutarushiana ngumi na badala yake ikawa ni vicheko na mazungumzo. Hii ni kwa sababu sina chuki na mtu yeyote yule. Mmenifunza kutojenga chuki na watu na badala yake kuchukua kila tukio kama changamoto ya maisha. Siasa ni kupambanisha mawazo tofauti na hatimaye kutafuta suluhu ya pamoja. Na siasa ina misingi yake ambayo sisi wanasiasa huwa tunasahau kwa maksudi. Msingi wa siasa ni kuwa inapaswa kuleta unafuu wa maisha ya wananchi na sio malumbano tu ya kurushiana maneno na kuzushiana ili kujijengea umaarufu wa kisiasa. Siasa si kuwekeana chuki na kuonyeshana ubabe.

Na hapo ni muhimu muelewa wanaKigoma mnapoambiwa kuwa eti ninapofuatilia mabilioni ya Uswisi ninatafuta umaarufu, ni uongo! Mnaposikia eti kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki na kujitafutia umaarufu, ni uongo! Kinachonisukuma kufanya vyote hivi ni ninyi. Ninasukuwa kila ninapowaona watoto bado wanatembea bila viatu;kila ninapoona akina mama wanapoteza maisha yao katika uzazi;kila ninapoona vijana ambao hawana uhakika wa kupata hata mlo moja kwa siku kwa kukosa kazi; ninapoona wazee wa Kigoma kukosa hata shilingi mia moja kununua chai asubuhi. Ninawaona si wanaKigoma bali mamilioni ya watanzania wakiishi katika hali hii. Alafu nalinganisha na taarifa tunazozipata kuhusu ufujaji na utoroshwaji wa pesa zetu. 

Hebu sasa linganisheni na ukweli kuwa ripoti ya kimataifa iliyotolewa hivi karibuni imeonyesha kuwa mwaka 2010 pekee, jumla ya dola za kimarekani milioni 1315 (bilioni 1.3), yaani shilingi trilioni  2,113,930,000,000 (sh trilioni 2.1) zilitoroshwa kutoka nchini Tanzania. Mwaka 2011 kiasi cha dola za kimarekani milioni 817 yani shilingi za kitanzania zipatazo trilioni 1,315,370,000,000 (trilioni 1.3) zilitoroshwa. Ripoti hiyo inaeleza kuwa jumla ya fedha za Watanzania zilizotoroshwa nje ya nchi katika miaka kumi iliyopita zilifikia dola za kimarekani milioni 4526 (bilioni 4.5) sawa na shilingi za kitanzania trilioni 7,286,860,000,000 (trilioni 7.3).  

Nimewatajia hapa namba chungu nzima na matrilioni na mabilioni hayaleti maana. Lakini hii ina maana kwamba kiasi cha pesa zilizotoroshwa katika miaka 10 pesa - robo yake tuingeweza kujenga barabara ya lami ya kiwango cha juu kabisa kutoka Kigoma mpaka Dar-es-salaam! Pesa hizi zingeweza kuajiri na kuwalipa vizuri walimu, madaktari na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha tunapata huduma bora na kutengeneza ajira bora kwa vijana wetu. Pesa hizi zingeweza kununua madawa muhimu na kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama tunaowapoteza kila mwaka wakati wa uzazi. Pesa hizi zingeweza kuwanunulia watanzania wote si watoto tu angalau pea 10 ya viatu. Sasa nikitafakari haya siwezi kuchapa usingizi mnono na kufumbia macho utoroshwaji wa fedha au matumizi mabaya ya fedha za umma kwa njia ya sisi wabunge kujilipia posho! Hapana! Nafsi yangu hainiruhusu kukaa kimya kwa kuogopa kuitwa mbinafsi au msaliti!
 
Lakini naomba niwasihi kuwa katika nyakati kama hizi za changamoto za kisiasa jambo la msingi kuliko yote ni kutulia maana hakuna linalotokea bila sababu. Licha ya kwamba kuna watu wengi wanapaza sauti zao katika mambo haya lakini pia kuna wengi zaidi ambao wapo kimya lakini wana mawazo yao, ndani na nje ya chama chetu;ndani na nje ya Serikali na ndani nanje ya nchi yetu. Ndio maana lazima kuibadili nchi yetu ili kuweza kuhakikisha kila raia anakuwa na fursa ya kutoa mawazo na fikra zake zinakuwa huru.
 
Maisha ni mabadiliko; mabadiliko hayana ukomo; mabadiliko hayazuiliki kwa sababu bila mabadiliko hakuna ukuaji, bila mabadiliko hakuna maendeleo. Mabadiliko ni kiu kikubwa cha Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya Tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania. Mungu ibariki Tanzania.

NAPE:ARIDHISHWA MAWAZIRI KUWAJISHWA

$
0
0
*Asema ni fundisho kwa watakaolala
*Ataka hatua zaidi zichukuliwe
*ziara za Kinana zimesaidia sana kutatua kero
*Bado moto wa ziara hizo haujapamba

*2015 CCM kurejesha viti  vya ubunge, Udiwani vilivyoko upinzani
NAPE NNAUYE

NA BASHIR NKOROMO.



KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amesema amepokea kwa faraja kubwa, hatua ya mawaziri wanne kuenguliwa nyadhifa zao kwa ridhaa ya Rais Jakaya Kikwete.

"Najisikia vizuri, maana kwa kitendo cha mawaziri hao wanne kuchuliwa hatua, ninaamini kitasaidia wale wengine waliolala nao waamke. Bila shaka sasa hakuna atakayelala na akilala anajua itakula kwake.", alisema Nape akijibu swali la mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Emmanuel Buhohela, kwenye kipindi cha 'mahijiano' cha televisheni hiyo, mjini Dar es Salaam, leo asubuhi.

Mtangazaji huyo alitaka kujua, Nape kama kiongozi wa ngazi ya juu CCM,  amejisikia au kupokeaje hatua ya Bunge 

kumuomba Rais kuwawajibisha mawaziri hao wanne na kisha Rais kuridhia ombi hilo kwa kutengua uteuzi wake wa nafasi za mawaziri hao jana.

Mawaziri waliofutiwa uteuzi wao na Rais na nafasi walizotoka zikiwa kwenye mabano ni, Dk. Emmanuel Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai (Waziri wa Ulinzi), Mathayo David Mathayo ( Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Khams Kagasheki (Maliasili na Utalii) ambaye ndiye pekee pamoja na uteuzi wake kutenguliwa na Rais lakini alitangaza kujiuzulu akiwa Bungeni, jana.



Kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao kulitangazwa rasmi Bungeni jana jioni, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hatua inayoaminika kuwa imetokana na shinikizo la bunge, baada ya Kamati yake ya Kudumu ya  Ardhi, Maliasili na Mazingira kubaini 'uozo' katika operesheni iliyofanyika hivi karibuni ya tokomeza ujangili.

Chini ya Mwenyekiti wake, James Lembeli, Kamati hiyo ilieleza kwamba pamoja na mambo kadhaa iliyoyaeleza kuwa ya hovyo yaliyojitokeza kwenye operesheni hiyo, vitendo vingi ikiwemo ubakaji na udhalilishaji vilifanyika ambapo ni kinyume na utu na haki za binadamu.

Kufuatia kadhia hiyo, Kamati hiyo kupitia kwa Lembeli, iliwataka mawaziri wanaohusika kutazama kama wanafaa kuendelea na nyadhifa zao au wajiuzulu, na pia Kamati hiyo ikaenda mbali zaidi kwa kumuomba Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua ya kuwawajibisha.

Akizungumzia zaidi hatua hiyo, Nape alisema, pamoja na mawaziri hao kuwajibika, lakini ipo haja ya kwenda mbali zaidi kwa kutazama mifumo na sheria zilizopo sasa kwa kuwa inaonekana navyo ni miongoni mwa vyanzo vya vikwazo katika utekelezaji wa utawala bora.

"Kwa mfano leo hii, mawaziri wameng'oka, sawa ni jambo jema, sitetei, lakini inawezekana kabisa kuna mifumo na sheria ambazo zilimkwaza Waziri huyu kutimiza wajibu wake. Mfano, alihitaji kumfukuza mtu kazi kwa kuzembea jambo fulani, lakini malmaka ya kufukuza kazi mtumishi yapo kwa Katibu Mkuu wa Wizara, hapa atafanyaje!", alisema Nape na kuongeza;

"La msingi hapa ni lazima sasa hatua hizi ziende mpaka chini huku kwa watendaji, ili isiwe mawaziri wanawajibishwa tu kwa sababu ya dhamana zao za kusimamia kisiasa, huku watendaji wanazidi kuvuta shuka bila hofu wakati baadhi yao ni sehemu ya matatizo".

Akijibu swali kuhusu ziara za Katibu Mkuu na sekretarieti ya CCM mikoani, Nape alisema, ziara hizo ndiyo kwanza zimeanza, na mado moto wake mkubwa zaidi unakuja hasa itakapokaribia uchaguzi mkuu wa 2015. Nape alisema, ziara hizo, zimeonyesha matunda makubwa sana, klwa kuwa zimesaidia kupunguza kero nhyingi katika maeneo zilikofanyika.

Alitoa mfano wa ziara hiyo ilivyoweza kuondoa msongamano wa malori wilayani Tunduma mkoani Mbeya, akisema kwamba wakati Kinana na msafara wake wanaingia tunduma walikuta msongamano ni mkubwa sana kutokana na wafanyakazi wanaohudumia malori hayo kufanya kazi kwa mda mfupi.

"Baada ya kuiagiza serikali isimamie wafanyakazi wa eneo hilo wafanya kazi kwa saa 24, kwa zamu, siku ya pili yake ya agizo hilo, msongamano ulionekana kupungua sana na kuleta nafuu kwa madereva na wafanya biashara kwa jumla pale Tunduma", alisema Nape.

Nape alisema, pia kutokana na ziara hizo, mgogoro uliokuwa mkubwa baina ya wananchi na wenye mgodi wa machimbo Nyamongo, umepungua kwa asilimia 90 sasa, na hali imekuwa ya kuridgisha sana.

Akizungumzia wabunge wanaodaiwa kulipwa posho bila kuzifanyia kazi, Nape alisema, kurudisha fedha pekee hakutatosha, kwa upande wa CCM ambayo ndiyo yeneye wabunge wengi itabidi ichukue hatua zaidi dhizi ya waliohusika na kadhia hiyo bila kuoneka mtu.

Kuhusu ajira kwa vijana, Nape alaisema ili kutimiza hilo, ni lazima viwanda vifufuliwe kwa dhati kabisha, ikiwa ni kuchukua hatua za kuwanyang'anya wawekezaji waliochukua viwanda mbalimbali kwa lengo la kuviendeleza lakini baadhi yao majengo ya viwanda hivyo wakayafanyia shughuli zingine tofauti ikiwemo kuyageuza maghala.

Nape aliitaka pia serikali kupunguza au kuondoa kabisa urasimu katika kupokea wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini akisema, kwamba, kwa sasa vikwazo na urasimu bado ni vingi sana kiasi kwamba wawekezaji waanakwazika na hivyo kupunguza kasi ya uwekezaji ambao wakiongezeka haraka ajira kwa vijana nazo zitakua haraka.

Alisema, hatua ya sasa inayofanywa na CCM kusimamia serikali ni ya kawaida kabisa kwa kuwa kazi hiyo haipaswi kufanya na wapinzani kwa kuwa sera inayotekelezwa siyo yao, na wahaijui.

Nape aliahidi kwamba katika uchaguzi zijazo CCM itakomba viti vyote vya ubunge na udiwani vililivyopo sasa chini ya wapinzani, akisema, kwamba, baada ya wapinzani kujaribiwa wameshindwa kuonyesha matunda yoyote ya kusaidia wananchi na hivyo kutokuwa mbadala wa CCM.

SIMBA YAIKWARUZA YANGA 3-1 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR JIONI YA LEO.

$
0
0
Mmoja wa mashabiki wa timu ya Yanga akiwa amebebwa kwenye machela,kama aonekanyo pichani na Watoa huduma ya kwanza uwanjani hapo Reds Cross,mara baada kuzimia kufuatia timu yake ya ushabiki ya Yanga kufungwa goli 3-1 dhidi ya timu ya Simba.Yanga na Simba wamemenyana leo kwenye mchezo wao wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jioni ya leo.Mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Tambwe mawili na Ramadhan Singano huku la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi.
Golikipa Machachari wa Timu ya Simba,Ivo Mapunda akiruka juu kkudaka mpira uliokuwa unaelekea langoni kwake.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Mwalimu shule msingi amtia mimba mwanafunzi wake

$
0
0
Ofisa Elimu Msingi, Wilaya ya Nkasi, Bw. Misana Kwangura akizungumza na Thehabari.com 
========  ========  ========
Mwalimu shule msingi amtia mimba mwanafunzi wake

Na Thehabari.com, Namanyere-Nkasi

MWALIMU mmoja wa Shule ya Msingi Sintali (jina tunalo) anatuhumiwa kwa kuwatia mimba wanafunzi wawili mmoja akiwa wa shule anayofundisha yeye na mwingine wa Shule ya Sekondari Sintali hali iliowafanya wanafunzi hao kukatisha masomo.

Tukio hilo limetokea Katika Kijiji cha Sintali, Wilaya ya Nkasi na baada ya taarifa kuenea kijijini hapo mwalimu huyo alitoroka kituo chake cha kazi na kukimbilia pasipo julikana. Akizungumzia tukio hilo Ofisa Elimu Msingi, Wilaya ya Nkasi, Bw. Misana Kwangura alisema mwalimu huyo anadaiwa kufanya kosa hilo tangu mwezi Agosti, 2013 na baada ya kuanza kufuatiliwa alikimbia kituo chake cha kazi.

Alisema baada ya kutoroka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ulilazimika kusitisha mshahara wake jambo ambalo lilimlazimu ajilete mwenyewe ndipo alipokamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kosa linalomkabili.

Hata hivyo Kwangura alisema wanafunzi hao mmoja wa darasa la saba na mwingine wa kidato cha pili wamekana mwalimu huyo kuwatia mimba na kudai wametiwa mimba na watu wasiojulikana ambao walikuja kijijini hapo kununua mazao. Mwalimu huyo amekana kuhusika na kitendo hicho.

Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limemuachia mwalimu huyo baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani.

“…Uongozi wa Kijiji pamoja na wa shule wanaamini kuwa yeye (mwalimu huyo) ndiye aliyewatia mimba lakini wao wanakataa, sisi tunaamini wanamtetea ili asichukuliwe hatua za kisheria lakini sisi hatujakubali tunasubiri wanafunzi hao wajifungue kasha tutatumia DNA kupima tujue ukweli…tayari mmoja amejifungua tunamsubiri mwingine,” alisema Ofisa Elimu, Kwangura.

Alisema vipimo vitapelekwa kwa Mkemia wa Serikali ili hatuhakikishie bila utata. Alisema tayari wamemkamata mwalimu mwingine wa Shule ya Msingi Itindi ambaye naye amemtia mimba mwanafunzi wa darasa la saba wa shule anayofundisha tangu mwezi wa nane mwaka huu.

Huyu naye baada ya kumtia mimba alipotea lakini baada ya kusitisha mshahara amejileta mwenyewe na tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi Nkasi kwa kosa alilolifanya. tuajabu huyo alikutoroka. Akizungumzia kwa ujumla matukio ya wanafunzi wa Shule ya Msingi kutiwa ujauzito, Ofisa Elimu huyo alisema matukio ya mimba kwa wanafunzi shule za msingi yanapungua kwa sasa kwani tangu Januari hadi Novemba 2013 jumla ya wanafunzi 9 wametiwa ujauzito na kukatizwa masomo yao, idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo wanafunzi 11 walitiwa mimba.

Aidha aliongeza kuwa kwa mwaka 2011 jumla ya wanafunzi 16 wa shule za msingi walitiwa mimba na kukatizwa masomo yao. “…Kimsingi naweza kusema matukio haya kwa sasa yanapungua ukilinganisha na hapo nyuma, na hii inatokana na elimu ambayo tunaitoa kwa kuzunguka kwenye shule mbalimbali kwa kutumia ofisi ya Ofisa Elimu Sayansi Kimu,” alisema Kwangura.

BENKI YA KCB TANZANIA YAMWAGA MISAADA JIJINI

$
0
0
 Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye akimkabidhi  Mwishehe Saidi ambaye ni mlemavu msaada wa mifuko ya  Saruji 28,Mabati 18   vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 2.hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mwishehe Tabata  jijijini Dar es Salaam.Msaada huo utamsaidia kwa ajiri ya ukarabati wa nyumba yake.
 Mkuu wa Masoko na Mahusiano  wa benki ya KCB Tanzania,akisoma hutuba kwa wakazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam, wakati  wafanyakazi wa benki  hiyo walipofika kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 5 katika Zahanati ya NJia  Health Centre.Anayeshuhudia (kushoto)ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Moezz Mir.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Moezz Mir(wapili toka kulia)akimkabidhi msaada wa Mashine ya kupasha moto vifaa vya hospitali kabla ya matumizi na baada ya matumizi  kwa mgonjwa(Sterilizer) Mkurugenzi wa Zahanati ya Njia Heath Centre ya Kiwalani jijini Dar es Salaam,Bw.Stephen Mosha(wapili toka kushoto .Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali vyote vyenye thamani ya  shilingi Milioni 5,wengine wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Utawala wa kituo hicho Bi,Hellen Olengailuva na kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya hiyo  Christina Manyenye.
 Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye ,akimkabidhi  Mwishehe Saidi ambaye ni mlemavu msaada wa mabati na saruji  vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 2.hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mwishehe Tabata  jijijini Dar es Salaam.Msaada huo utamsaidia kwa ajili ya ukarabati wa nyumba yake.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Moezz Mir akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Njia  Health Centre,Bw. Stephen Mosha wakati walipofika katika kituo hicho kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam,kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya shilingi Milioni 5.Katikati ni Mkuu wa Utawala wa kituo hicho Bi,Hellen Olengailuva. 


Mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Njia Heath Centre kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam,Bw Stephen Mosha ,akiongea na waandishi wa habari wakati  Uongozi wa Benki ya KCB Tanzania,walipofika Hospitalini hapo kutoa  msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya shilingi Milioni 5.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki  hiyo Bw.Moezz Mir na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Christina Manyenye.

LOWASSA ASHIRIKI TAMASHA LA WAENDESHA BODABODA JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa alikuwa ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofana sana.
 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza machache kwenye Tamasha hilo kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Tamasha hilo,Mh. Edward Lowassa (kulia).Katikati ni Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga akizungumza akitoa hotuba yake mbele ya Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe akisoma Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Risala ya Chama cha Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Benki ya FNB kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Mfuko wa PSPF kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Zawadi Kutoka kwa Mwenyekiti wa Muda wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Said Magamba.
Salamu kwa waendesha Bodaboda.
Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya wanaounda kundi la KIBEGA,wakitoa Burudani mbele ya Waendesha Bodaboda hao.

Sehemu ya Waendesha Bodaboda hao wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi.
Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo mapema leo.
Mgeni Rasmi katika Tamasha la Waendesha Bodaboda Mkowa wa Dar es Salaam,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka viwanjani hapo huku Vijana Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsindikiza kwa shangwe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwaaga Vijana wa Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiondoka viwanjani hapo huku shangwe zikitawala viwanjani hapo.
Vijana wa Bodaboda wakilisukuma gari la Mh. Lowassa ikiwa ni sehemu ya Furaha waliokuwa nayo.

LOWASSA ALIPOZUNGUMZA KWENYE TAMASHA LA WAENDESHA BODA BODA LEO VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR

KASEBA AMCHAKAZA ALIBABA KWA K,O RAUNDI YA 4

$
0
0
Bondia Japhert Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Alibaba Ramadhani wakati wa kugombania ubingwa wa Taifa uliofanyika Manzese Dar es salaam Kaseba alishinda kwa KO ya raundi ya nne ya mpambano huo .
Kanda kabongo akimuhudumia Japhet Kaseba
Bondia Omari Nampekecha 'peche boy' kushoto akipambana na hasani Kiware wakati wa mpambano huo nampekecha alishinda kwa pointi.
Kaseba akiwa na familia yake pamoja na mashabiki baada ya kushinda mchezo wake
Bondia Pendo Njau kushoto akiwa na bondia Llulu Kayage wakati wa mpambano huo
mashabiki wakiangalia mpambano
Wapiganaji wa mpambano wa Kick Boxing kareem kutch kushoto akipambana na Hassani Juma 'Tata Boy' wakati wa mpambano huo kutch alishinda kwa point picha nasuperdboxingcoach.blogspot.com
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images