Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 191 | 192 | (Page 193) | 194 | 195 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkurugezi mtendaji wa Vizion One Inc Bw,Abdallah Kitwara Amewapongeza Wafanyakazi na Wahisani wa kampuni hiyo kwa jitihada yao ya kufanya kazi kwa bidii ili kutoa huduma bora kwa Wagonjwa na wateja wao.
  C.E.O Vizion One Home Health Services Bwana. Abdallah Kitwara  akizungumza na wafanyakazi wa kampuni yake na wageni mbali mbali waliohudhuria, pembeni yake ni Mkewe Bi.Vanessa Kitwara.
  Pongezi hizo alitoa wakati wa hafla maalum ya mwisho wa mwaka iliyoandaliwa na kampuni hiyo Siku ya Ijumaa Dec 20, katika Ukumbi wa Lanham hapa Washington D.C

  Amesema kampuni yake ya Vizion One Home Health Services hivi sasa Mbali ya kutoa huduma yake Mjini Washington D.C,  Pia imesambaza huduma zake katika majimbo mengine hapa marekani ikiwemo Pennsylvania, Massachusetts, Kentucky na Kansas Missouri.

  Aidha  amewashukuru , wafanyakazi na washirika mbali mbali waliojitolea kutoa msukumo mkubwa wa kupelekea kampuni yake ya Vizion One Inc kutoa huduma bora zaid.

  Sherehe hizo zinazofanyika kila mwisho wa mwaka kampuni ya Vizion One Inc iliweza kuwatunuku cheki wafanyakazi wake kama tunzo la ufanyakazi bora na kuongeza bidi za kazi kwa mwaka unaofuata lakini pia katika hotuba yake meneja wa kampuni hiyo Abdallah Kitwara aliweza kizunguimzia historia yake kwa kifupi baada ya pongezi na shukurani kwa wafanyakazi wake.
  Kwa taswira zaidi click read more.


  0 0

    
  Karibu katika sehemu ya pili ya kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.Katika kipindi hiki, tunaendeleza mjadala juu KWANINI WANANDOA HUTEMBEA NJE YA NDOA?Wachangiaji studio walikuwa ni Elizabeth Cherehani, Denzel Musumba na Mubelwa Bandio
  KARIBU UUNGANE NASI.


  0 0

   Exim Bank Tanzania Assistant Project Manager Donald Mlaki (right) inspects an on-going construction of a 10 holes latrine at Kilakala Primary School in Temeke District Dar es Salaam, which is fully funded by the bank. The lavatory facility is part of several projects funded by Exim Bank Tanzania, which adopted the school two years back. Left is the school Head Teacher Mr Abdul Kutarasa.

  Exim Bank Supports Kilakala School lavatory project 

  Exim Bank Tanzania is in the final stages of completing the construction of a modern lavatory facility at Kilakala Primary School in Temeke District, Dar es Salaam. The construction of a 10 holes latrine and a good water system is part of several development projects implemented and fully funded by Exim bank Tanzania at Kilakala School.       

  Speaking at the construction site, Exim Bank Tanzania Assistant Project Manager Donald Mlaki, who went to inspect the construction progress, said his bank saw the need of supporting the school by adding the number of latrines the school had based on the importance of hygiene in schools. “The school had a latrine with only eight (8) holes against 2739 pupils. Now that the bank has added another 10 holes, we are sure that this will be a relief to both teachers and pupils at this school,” he said. He mentioned that Exim Bank has been gradually transforming the school since it adopted Kilakala Primary early 2012.

  Mentioning some of the recent projects funded by the bank, Mlaki said the school now enjoys the use of a state of the art library, all pupils sit on desks donated by the bank, the school  has a good clean water system, just to mention a few.
   Exim Bank Tanzania Assistant Project Manager Donald Mlaki (center) inspects an on-going construction of a 10 holes latrine at Kilakala Primary School in Temeke District Dar es Salaam, which is fully funded by the bank. The lavatory facility is part of several projects funded by Exim Bank Tanzania, which adopted the school two years back. Looking on are artisans at the site.
   Exim Bank Tanzania Assistant Project Manager Donald Mlaki (center) speaks to artisans at the construction site where he went to inspects an on-going construction of a 10 holes latrine at Kilakala Primary School in Temeke District Dar es Salaam, which is fully funded by the bank. The lavatory facility is part of several projects funded by Exim Bank Tanzania, which adopted the school two years back. On the far left is school Head Teacher Mr Abdul Kutarasa.
   Exim Bank Tanzania Assistant Project Manager Donald Mlaki (right) inspects an on-going construction of a 10 holes latrine at Kilakala Primary School in Temeke District Dar es Salaam, which is fully funded by the bank. The lavatory facility is part of several projects funded by Exim Bank Tanzania, which adopted the school two years back. Left is the school Head Teacher Mr Abdul Kutarasa.

  Exim Bank Tanzania Assistant Project Manager Donald Mlaki (left) is shown a sample of a sink to be used in the newly constructed 10 holes latrine at Kilakala Primary School in Temeke District Dar es Salaam when he went to inspect the on-going construction at the school which is fully funded by the bank. The lavatory facility is part of several projects funded by Exim Bank Tanzania, which adopted the school two years back. Right is the school Head Teacher Mr Abdul Kutarasa.

  0 0

   MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krismasi,Bwa.Alex Msama akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar wakati alipokuwa akielezea maandalizi ya lala salama ya tamasha hilo,linalotarajiwa kufanyika siku ya sikukuu ya Krisimasi,kwenye Uwanja wa Taifa.

  Tamasha hilo litakalojumisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za kiroho wa hapa nyumbani sambamba na kutoka nje ya nchi ikiwemo nchini Afrika Kusini na Ruanda.Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu na Liliani Kabaganza kutoka nchini Ruanda wanatarajiwa kuwasili jijini Dar leo tayari kwa ushiri wa tamasha hilo linalowakutanisha watazamaji lukuki.
  MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krismasi,Bwa.Alex Msama akiwataja baadhi ya Waimbaji watakatumbuiza kwenye tamasha hilo la Krisimas,kuwa ni Rose Muhando,Solomon Mukubwa,Upendo Nkone,Upendo Kilahiro,Anastazia Mukabwa,John Lissu,Boni Mwaitege,Ephrahim Sekeleti,Glorious Warship Team,The Voice Acapella,New Life Band na wengineo kibao.Msama alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekwishakamilika na kinachosubiriwa mashambulizi tu yatakayoanzia jijini Dar,Morogoro,Tanga,Arusha na kumalizia mkoani Dodoma

  0 0

   MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Mabibo, wilaya ya Kinondoni, Zakaria Kimemeneki (kulia), akikabidhi zawadi ya picha ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwa Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage, wakati wa kufungwa semina ya Baraza la UVCCM kata hiyo, jana. Picha hiyo imetolewa na UVCCM Mambibo, ili akabidhiwe Nape kutokana na kutambua mchango wake katika kuijenga CCM. Zaidi ya Vijana Wajumbe 30 walishiriki semina hiyo.
   Kisha Mwenyekiti huyo akakabidhi picha ya Kamanda wa UVCCM Kata ya Mabibo, Dk. Fenella Mkandara ili nayo imfikie kwa kushukuru mchango wake kwa uilea jumuia hiyo ya Chama usiku na mchana
   Kisha Mwenyekiti huyo wa UVCCM akamvalisha Cholage kofia maalum ambayo UVCCM hao wanasema, walimuona kwa mara ya Kwanza katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ameivaa ya aina hiyo baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo mjini Dodoma
   Cholage akitoa kitabu cha Kanuni za UVCCM kwa mmoja wa washiriki wa semina hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mabibo, Bononi Mlowe.
   Wanasemina wakimsikiliza mgeni rasmi
  Mgeni rasmi akivishwa skafu Cjolage,  baada ya kuwasili kwenye ukumbi. Alisema hii ilikuwa mara yake ya kwanza kuvishwa skafu!!

  0 0

   NA BASHIR NKOROMO

  UMOJA wa Vijana wa CCM, Kata ya Mabibo, Kinondoni jijini Dar es Salaam, umempongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwa kuwavua uongozi mawaziri wanne mwishoni mwa wiki.

  Mawaziri waliovuliwa uongozi kufuatia Rais Kikwete kutengua teuzi wao ni, Dk. Emmanuel Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai (Waziri wa Ulinzi), Mathayo David Mathayo ( Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Khams Kagasheki (Maliasili na Utalii) ambaye ndiye pekee pamoja na uteuzi wake kutenguliwa na Rais lakini alitangaza kujiuzulu akiwa Bungeni.

  Kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao kulitangazwa rasmi Bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hatua iyotokana na mapendekezo ya bunge, baada ya Kamati yake ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kubaini 'uozo' katika operesheni iliyofanyika hivi karibuni ya tokomeza ujangili.

  Pongezi hizo ya UVCCM Mabobibo, ni miongozi mwa mazimio waliyofikia wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM kata hiyo, baada ya semina yao iliyomalizika jana kwa kufunguwa na Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage.

  Katika maazimio hayo, Vijana hao, Wamepongeza ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambazo amefanya hivi karibuni na sekretarieti yake, na kumuomba Kinana kuendeleza ziara hizo, kwa maelezo kwamba zimeonyesha manufaa makubwa kwa Chama.

  Katika ziara iliyomalizika hivi karibuni Kinana alifanya ziara katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe akiambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ambaye sasa pia ni Mbunge kufuatia kuteuliwa na Rais Kikwete.

  Pamaoja na kupongeza ziara hizo, UVCCM Mabibo pia wameazimia kuhakikisha mitaa mitatu iliyopo chini ya chama cha CUF, kati ya sita ya kata hiyo ya Mabibo inarejeshwa kwenye himaya ya CCM baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika mwakani.

  Akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo, Cholage aliunga mkono maazimio hayo, akiyaeleza kwamba ni ya msingi.

  "Kwa kweli naunga mkono maazimio. Siyo kwamba tunafurahi mawaziri hawa kukosa kazi, la hasha, lazikini kinachotufurahisha zaidi ni kuona kwamba Mwenyekiti wa Chama Rais Kikwete amesimamia inavyostahili misingi ya uwajibikaji", alisema Cholage na kuongeza;

  "Pia hii kazi inayofanywa na Mzee wetu Kinana na kina Nape, ni ya kupigiwa mfano ambayo sisi kama vijana, lazima kuiunga mkono kwa dhati ya mioyo yetu yote, lakini si kwa maneno tu bali kwa vitendo".

  Cholage aliwahimiza vijana, kuwania nafasi za uongozi wa mitaa, uchaguzi utakapowadia, lakini akawataka kufanya hivyo kwa kujipima kwanza kama anatosha kila atakayekuwa anadhamira ya kugombea.

  Aliwataka UVCCM kuwa imara katika kukilinda Chama akiwakumbusha kuwa wao ndiyo askari wa mstari wa mbele katika kazi hiyo.

  Cholage aliwataka vijana wa CCM na vijana wote kwa jumla, kujiepusha na tabia ya kulalamika waliyonayo baadhi yao, badala yake wawe mstari wa mbele kukosoa katika njia zinazostahili na kisha kuonyesha njia wanazoona zinafaa kutumika katika utatuzi wa changamoto wanazoziona.

  0 0

  WAWANAKE mkoani Iringa wametakiwa kuzitambua haki zao sambamba na sheria za utawala bora ndani ya jamii katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika masuala ya utawala na mifumo ya maisha ihusuyo tamaduni mbalimbali zinachochangia kuchochea vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia dhidi yao.
   
  Hayo amesema Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha(RUCO) Dk. Cephas Mgimwa wakati wa mafunzo ya juu ya haki za wanawake yaliyoandaliwa na Kitengo cha Haki za Binadamu na Utawala bora wa chuo hicho kwa wanawake wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa yaliyofanyika katika ukumbi mdogo wa chuoni hapo.
   
  Amesema kuwa wanamke anapaswa kupewa nafasi za kutoa michango yao katika maamuzi mbalimbali ndani ya jamii ikiwemo masuala ya ndoa, umiliki wa mali na masuala ya mirathi.
   
  Amesema mafunzo hayo ya utawala bora yamelenga kuwajengea uwezo wanawake kufikia mifumo mbalimbali ya mahakama ili kupata msaada wa kisheria kwa lengo la kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake zikiwemo kupigwa, kubakwa, kuachika (talaka) na kunyimwa mirathi kutokana na baadhi ya mila potofu katika baadhi ya makabila.
   
  Mgimwa amesema kumekuwa na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii nyingi za Kitanzania hasa watoto na wanawake walioko ndani ya ndoa na nje ya ndoa na kwa kukosa ufahamu wa sheria na haki za binadamu wengi wao wameshindwa kupeleka malalamiko yao sehemu husika.
    
  Kwa upande wake Mhadhiri na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa chuo hicho Dk. Mary Livera amesema binadamu wote ni sawa na hakuna tofauti ya mwanamke na mwanaume katika kupata haki za msingi za binadamu kila mmoja anastahili kupata haki katika huduma za mifumo ya sheria katika mahakama.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt.Christina Ishengoma amewapongeza wananchi wa mkoa huo kwa ushirikiano wao katika shughuli za kujiletea  maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dkt.Christina Ishengoma amesema katika kipindi cha mwaka 2013 wananchi wa mkoa wa Iringa wamekuwa wakifanyakazi kwa kujituma na kwa ushirikiano mkubwa.
   
  Kwa upande mwingine  ishengoma amewataka wananchi wote wa mkoa wa iringa  kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa  kupanda mazao yanayovumilia ukame ambayo ni Mtama, Muhogo, Viazi vitamu na Ulezi kwa na kila familia ihakikishe inapanda chini ya hekari mbili.
   
  Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutawahakikishia uhakika wa chakula hasa maeneo ambayo hupata mvua chache. Hata hivyo mkuu wa mkoa huyo amewaasa wananchi kutumia mbegu bora za kilimo,mbolea ya kundia na kukuzia hasa kwa mazao ya mahindi na mpunga ili kupata mazao bora.
   
  Aidha Ishengoma amewatakia heri ya krismasi na mwaka mpya huku akiwahakikishia kuimalishwa kwa ulinzi katika kipindi hiki cha sikukuu.

  0 0
 • 12/23/13--00:55: X-MAS REGGAE BEACH PARTY

 • ....it's X-MAS REGGAE BEACH  PARTY..at One LOVE Lounge-ngonda BEACH-kigamboni....live REGGAE  performance by JHIKO MAN & afrikabisa band..also non stop reggae mixing by top REGGAE DJs..lot's of beach games & kids program...ALL on Christmas day-25 -DEC.. ALL from morning till late night....never miss dis...

  0 0

   Marehemu Jacob Arid kwa jina maarufu Oming'o enzi za uhai wake
  Familia ya Marehemu Oming'o ikiwa uwanjani wakati wa bonanza lililopewa jina la OMING'O SOCCER BONANZA kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu Jacob Arid kwa jina maarufu Oming'o   lililofanyika kwenye kiwanja cha Segerea siku ya jumapili December 22, 2013 . Marehemu ameacha mjane na watoto wanne.
   Msemaji wa Timu ya Segerea Veterans Sports Club akizungumza jambo wakati wa bonanza lililofanyika kwa ajili ya kumkumbuka mchezaji mwenzao aliyefariki akiichezea timu hiyo katika uwanja wa Segerea ulioko Tabata jijini Dar es Salaam
   Timu kapteni wa Segerea Veterans Sports Club akizungumza na vyombo vya habari wakati wa bonanza la OMING'O SOCCER BONANZA lililofanyika jana kwenye kiwanja cha Segerea, Tabata jijini Dar es Salaam hapo jana.
   Mechi zikiendelea wakati wa bonanza la kumkumbuka mchezaji mwenzao aliyefariki uwanjani akiichezea timu yake ya Segerea Veterans Sports Club
   Mchezaji wa timu ya Kigamboni akiwa ameumia wakati wa nusu fainali ya kwanza
   Ilikuwa ni furaha baada ya timu ya Kigamboni kuingia Fainali
   Ubishi katika mechi kama hizi huwa haukosekani lakina refa ndo ana maamuzi yote
   Wachezaji wa timu ya Segerea Veterans Sports Club wakishangilia baada ya kushida ubingwa wa bonanza la OMING'O SOCCER BONANZA lililofanyika kwenye kiwanja cha Segerea kwa ajili ya kumkumbuka mchezaji mwenzao Oming'o aliyefariki akiichezea timu hiyo ya Segerea Veterans Sports Club
   Wachezaji wa timu ya Segerea Veterans Sports Club baada ya kushinda fainali hiyo walielekea meza kuu ilipokuwa picha ya mchezaji mwenzao marehemu Jacob Arid kwa jina maarufu Oming'o na kumwombea mungu ampumzishe mahali pema.
   Hapa ni furaha  kwa timu ya Segerea Veterans Sports Club baada ya kuchukua ubingwa
  Mmoja wa mashabiki wa timu ya Segerea Veterans Sports Club akiwa amebeba picha ya marehemu Jacob Arid kwa jina maarufu Oming'o baada ya kumalizika kwa bonanza hilo


  0 0

   Mfanyakazi wa TBL Mwanza ambaye jina halikufahamika mra moja akimimina bia kabla ya shindano la kuonja bia kwa waandishi wa habari kuanza..
   Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuendesha zoezi la kuonja bia katika Kiwanda cha Bia cha TBL Mwanza juzi.
   Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima,Sitta Tumma akionja bia kwenye shindano la kuonja bia lililoandaliwa katika Kiwanda cha Bia cha TBL Mwanza juzi.


   Meneja Ubora wa TBL Jeremiah Kamambi, akitoa elimu kuhusu utengenezaji wa bia katika shindano la kuonja bia lililoendeshwa kwa waandishi wa habari na kampuni hiyo.
   Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Jijini Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TBL muda mfupi baada ya kumalizika kwa shindano la kuonja bia lililofanyika kiwandani hapo juzi
   Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Mwanza, Richmond Raymond, akimkabidhi zawadi  Mwandishi wa habari wa gazeti la Majira, Wilhelm Mulinda (kulia) ,baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la kuonja bia, jijini Mwanza juzi..

   Mshindi wa pili katika shindano la kuonja bia Miguel Suleman akipokea zawadi zake kutoka kwa Meneja wa TBL Mwanza, Raymond Richmond

  0 0

  · Watanzania waaswa kutumia huduma ya 
  bure ya Airtel Money kutuma na kutoa pesa Dar es Salaam

  Kampuni ya mitandao wa simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendeleza ushirikiano wake na Baraza la Taifa la Usalama barabarani katika juhudi za kuelimisha uma kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani hususani msimu huu wa sikukuu. 
  Airtel imekuwa ikishirikiana kwa karibu na kikosi cha Usalama Barabarani katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kudhamini kampeni mbalimbali.
  Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kulia) akisisitiza juu ya umuhimu wa wananchi kujikinga na ajali za barabarani kwenye msimu huu wa sikukuu leo wakati wa kikao na waandishi wa habari kilichofanyika makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam.  Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga akifuatiwa na Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi.Hawa Bayumi alisema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wananchi wanapaswa kuwa waangalifu zaidi ili kujikinga na ajali za barabarani.
  “Hiki ni kipindi ambacho wananchi wanapaswa kuwa makini sana katika kuhakikisha wanajilinda na wimbi la ajali za barabarani ambazo husababisha asara kubwa kwa taifa, na pia madereva wajitaidi sana kuepuka ulevi wa kupindukia,” alisema Hawa.

  Aliongeza kwa kusema pia katika msimu huu wateja wa Airtel wanaweza kutumia huduma ya Airtel money kutuma na kupokea pesa bure mahali popote nchi nzima kuepuka kutembea na viwango vikubwa vya pesa.
   Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu ya umuhimu wa kujikinga na ajali za barabarani  katika msimu huu wa sikukuu pia kuepuka kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha badala yake wananchi watumie huduma ya Airtel money. Kushoto kwake ni Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi pamoja na Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi.

   Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam leoDCP Mohammed Mpinga alisema Lengo la kampeni hizi ni kupunguza ongezeko la ajali za barabarani pamoja na madhara yake kwa kipindi cha sikukuu za mwaka huu 2013/2014 na wanajitaidi kuhakikisha elimu inatolewa ipasavyo. 
  “Tunashukuru Airtel kwa kuungana nasi katika kujali usalama wa watanzania, kazi ya  kuelimisha watumiaji wa barabara ni kubwa na hivyo tunaendelea kutoa wito kwa wadau wengine kutuunga mkono ili kusaidia kufikisha ujumbe. Lengo hili litatimia kwa kushirikiana na wadau katika kufanya operasheni mbalimbali pamoja na kutoa elimu.” Alisema DCP Mpinga.

  Mpinga alitumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania wote kote nchini kuepuka kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha badala yake watumie huduma ya Airtel Money kutuma, kuweka na kutoa pesa.
  Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi akizungumzia athari zinazotokana na ajali za barabarani na kuwaasa wananchi waziepuke hususani katika msimu huu wa sikukuu. Bw. Athumani Hamisi alisema Kuelekea mwisho wa mwaka, matukio ya ajali za barabarani yamekuwa yakiongezeka kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani hivyo wananchi wanatakiwa kujitahidi kutokiuka taratibu hizo.
  “Ukiukwaji wa sheria husababisha sana ajali za barabarani, wananchi wanapaswa kuhakikisha wanafuata sheria za barabarani ili kuepusha ongezeko la ajali hizo ambazo hutokea mara kwa mara haswa katika msimu huu wa sikukuu.” Alisema Athmani.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya nne katika maeneo yanayohusu Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji,wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) Dkt. Omar Issa.
  Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara wakitia saini mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ya GS1Tanzania Bi. Fatma Kange (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza wakitia saini Mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ya GS1Tanzania Bi. Fatma Kange (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza wakibadilishana hati ya  mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara wakibadilishana hati ya Mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza akieleza malengo ya Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania ikiwa ni kuanzisha na kuendeleza ufugaji kisasa wa nyuki unaojali mazingira, unaozalisha bidhaa bora za ufugaji nyuki zitakazomwingizia mfugaji kipato cha kutosha na kumwezesha kuchangia kikamilifu pato la Taifa. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara.
  Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ya GS1Tanzania Bi. Fatma Kange akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya mipango iliyowekwa katika kuhakikisha sekta ya ufugaji wa nyuki na uzalishaji asali inaendelea kukua, wakati wa hafla ya utiaji saini kwa ajili ya programu endelevu ya ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali katika kanda ya mashariki,kati na magharibi mwa Tanzania.kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza.
  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi serikali ya awamu ya nne inavyoendelea kusaidia mpango wa ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali ili kuhahakikisha ukuaji katika sekta hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.kushoto ni katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza


  (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)  Na Hassan Silayo-MAELEZO

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuhamasisha na kuvutia miradi ya uwekezaji nchini kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu wakati wa hafla ya utiani saini wa hati ya mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo.

  Dkt. Nagu alisema kuwa serikali itaendelea kuhamasisha uwekezaji nchini kwa kuboresha na kutekeleza sera na sheria zitakazovutia uwekezaji kwani inasaidia kuongeza pato la taifa na kuongeza fursa za ajira kwa watanzania. 

  “kutokana na jitihada za serikali za kuweka mazingira wezeshi na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, idadi na thamani ya miradi iliyoidhinishwa na kituo cha uwekezaji Tanzania imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na hii inasaidia kuongeza pato la taifa na kuongeza fursa za ajira kwa watanzania”Alisema Dkt.Nagu.

  Dkt. Nagu aliongeza kuwa ili kuendelea kuboresha Sera na Sheria za uwekezaji ili ziendane na mazingira na mahitaji ya uwekezaji serikali imeshakamilisha maandalizi ya Taarifa ya Mapitia ya Sera zinazohusu uwekezaji yaliyofanyika kwa kutumia mfumo wa kutathmini Sera za Uwekezaji unaotumiwa na shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo(OECD).

  Katika ushiriki wa Serikali katika utoaji elimu ya ujasiriamali Dkt. Nagu alisema kuwa serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika utoaji wa elimu na mafunzo ya ujasiriamali nchini hasa wale wa vijijini.


  Serikali imetekeleza Mpango wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Kuongeza Ajira ambapo tathmini iliyofanyika inaonesha mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 50.03 imetolewa kwa utaratibu wa serikali kutoa Dhamana ya mikopo kwenye benki za CRD NA NMB, mpango ulionufaisha wajasiriamali 74,70

  0 0

   Kituo cha Polisi cha Oysterbay, pamoja na nyumba za Polisi wanaoishi katika Kambi hiyo, vitabomolewa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa maduka ya kisasa mfano wa Mlimani City ujenzi unaotarajia kuanza mwakani.

   Tayari baadhi ya askari waliokuwa wakiishi katika Kambi hiyo wameshapewa 'Notis' ili kuhama katika nyumba zao na wengine kubomoa wenyewe majengo waliyokuwa wamejengwa kwa mabati katikati ya kambi hiyo ambayo walikuwa wakiishi, ambapo wengi wao waliokuwa wakiisha katika nyumba za mabati wamekwishabomoa nyumba zao na kuhama, huku baadhi wakiwa wamesalia wakisubiri awamu ya pili. Askari hao wameelekezwa kuhamia katika nyumba mpya zinazojengwa eneo la Kunduchi.

  Baadhi ya askari wamelalamikia utaratibu huo wa kuhamishwa katika eneo hilo, hali ya kuwa pamoja na kubomolewa nyumba zao na Kituo cha Polisi, lakini imeelezwa kuwa kitajengwa Kituo kipya kikubwa katika eneo hilo ambacho kitajengea upande wa pili barabara ya Ubalozi wa Marekani.

  Kinachowafanya baadhi ya askari kulalamikia utaratibu huo ni kutokana na kujengwa tena kituo kikubwa katika eneo hilo, lakini nyumba za askari zikiondolewa na kutotakiwa kuwepo tena, ambapo askari wote watapewa nyumba Kunduchi na kila atakayekuwa zamu atalazimika kusafiri ili kufika kazini, jambo ambalo limeonekana ni usumbufu na hasa pale itakapotokea dharula za kikazi.

  Kamera ya Sufianimafoto, ilibahatika kukatiza katikati ya kambi hiyo na kushuhudia nyumba nyingi zikiwa tayari askari wameshahama huku zile za mabati zikiwa zimebolewa na askari wakiwa tayari wamehama huku wengine wakiendelea na zoezi la ubomoaji na kuhamisha mizigo yao kwa awamu.

  HABARI ZAIDI BOFYA  http://www.sufianimafoto.com

  0 0


  WINGA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Edibily Lunyamila leo hii asubuhi amekimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kusumbuliwa na kifua na sasa anapumua kwa msaada wa mashine. 


  Mtandao huu ulifanikiwa kufika hospitalini hapo muda mfupi baada ya winga huyo kukimbizwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa tangu jana usiku akiwa nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam.   Shaffihdauda.com imemshuhudia Lunyamila akiwa amelala kitandani katika wodi ya wanaume namba 5 kitanda namba 16 katika hospitali hiyo ya rufaa ya Kinondoni.
  Daktari Madirisha Pascal anayemuhudumia winga huyo wa zamani, Lunyamila anasumbuliwa na tatizo la kifua ambalo linamfanya ashindwe kupumua vizuri.   “Kama mnavyomuona anapumua kwa msaada wa mashine na bado tunaendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini nini kinachomsumbua zaidi,” alisema Pascal.   Mmoja wa ndugu wa Lunyamila, Lameck John alisema kwamba, mchezaji huyo wa zamani alianza kujisikia vibaya jana Jumapili na leo asubuhi hali yake ilibadilika ndipo walipomkimbiza hospitali.    Lunyamila alivyokuwa enzi anaichezea Yanga..

  “Alianza kulalamika hawezi kupumua na kifua kinamsumbua pia mbavu zilikuwa zikimuuma, baada ya majibu ya vipimo tutajua kinachomsumbua zaidi,” alisema Lameck. 


  Kutokana na hali iliyoonekana hospitalini hapo, Lunyamila anahitaji huduma ya haraka ili kuweza kuokoa uhai wake kwani anapumulia mashine akiwa katika sehemu yenye joto kali hivyo anapambana na vitu vingi kwa wakati mmoja.Taarifa za kiuchunguzi zilizofanywa na mwandishi wetu zimebaini Lunyamila anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.


  ''Nilikuja jana hospitali ya mwananyaala ikagundulika moyo wangu umekuwa mkubwa,hivi sasa naenda muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi nikifika na kukutana na daktari nitakujulisha ''ilipofika mchana wa leo mwandishi alipokea simu kutoka kwa Lunyamila akimwambia ameambiwa arejee tena hospitali ya Mwananyamala.

  HABARI HII NI KWA HISANI YA MTANDAO WA SHAFFIH DAUDA BLOG.

  0 0


   Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa wa ngumi za Ridhaa pamoja na wadau wengine wa mchezo huo katika Picha ya pamoja, wakati wa hafra hiyo
   Aliyesimama kushoto ni mkurugenzi wa Afrika Mashariki kupitia kinywaji cha Battery Bwana Tony Misokia akiwa anaongea na wananchi walioshiriki katika Hafra hiyo.
   
   Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF) Bwana. Lukelo  Anderson akiwa sambamba na Afisa habari wa Ngumi za ridhaa Tanzania  Bwana Salum Viduka wakati wa Hafra hiyo.

   Hawa ni Baadhi ya wachezaji wa  Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF)

   Wa kwanza kulia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi za ridhaa Tanzania bwana Nassari Mafuru
   Kutoka kushoto aliyevaa shati jeupe ni Bwana Anthon Mwang'onda ambaye ni mjumbe wa mashindano na vifaa wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF) akiwa na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Bwana Hassan Mzonge

  *******

  Shirikisho la ngumi za ridhaa Tanzania  limefanya hafra fupi iliyo jumiisha wachezaji wa ndondi , makocha wadau na Vyombo vya habari kwaajiri ya kuendeleza kuweka mshikamano wa kuweza kuwainua vijana ambao bado hawajaweza kupata ajira  kuweza kujiunga na shilikisho la ngumi za ridhaa Tanzania

  Shilikisho hilo ambalo limeanzisha mashindano ambayo yanatambulika kwa jina la  PSPF  Boxing Award sambamba na waandaaji wa Hafla hiyo wakiwa ni wadhamini wa mashindano hayo  iliyofanyika katika eneo la   (CnG) ambapo waliweza kudhamini kwa kuandaa chakula cha usiku kwaajili ya kuendelea kuweka mahusiano baina ya washiriki wote wanao shiriki katika kuendeleza mchezo wa ngumi Tanzania

  Akizungumzia lengo la kuweka hafra  hiyo Afisa habari wa shirikisho la ngumi Tanzania Bw.Salum Kuhowa Viduka amesema "Tunawaomba wanajamii kuweza kutupa ushirikiano kwa muda wote ambao mashindano haya yanapo kuwa yana wasili katika miji,wilaya,manispaa,na nk kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuona jinsi fursa kwa vijana zinavyo patikana kupitia mchezo wa ngumi za Ridhaa"

  Mwisho Makamu Rais  Bw.Lukelo Andason aliweza kufunga hafla hiyo kwa kuwapongeza watu wote walio weza kufika na kujumuika pamoja ili kuendeleza kujenga umoja wa ngumi Tanzania.

  0 0

  Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa, tarehe 25 Desemba 2013 atajumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole Orphanage kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro.
   
  Mrembo huo ataungana na warembo wengine watatu, akiwemo Miss Tanzania mshindi wa pili Latifa Mohamed, Miss Tanzania mshindi wa tano Elizabeth Perrty, na Sabra Islam Miss Morogoro 2013 ambaye ndie atakae kuwa mwenyeji wao wakati wote wakiwa mkoani hapo.
   
  Ni kawaida kwa Mrembo wa Taifa, Miss Tanzania kila mwishoni mwa mwaka kula X Mass na Watoto Yatima, wasiojiweza pamoja na wale waishio katika mazingira magumu.
   
  Baada ya shughuli hiyo Miss Tanzania Happiness Watimanywa atajumuika pia na watoto wa aina hiyo jijini D’salaam siku ya Mwaka mpya tarehe 1 January 2014 katika vituo vingine atakavyopangiwa na  Kamati ya Miss Tanzania.
   
  Pamoja na shughuli hiyo, Mrembo Happiness Watimanywa pia anakusudia  kusaidia jamii wenye matatizo ya Maji kwa kuwachimbia visima vya maji safi katika mikoa ya Dodoma na Singida.
   
  Miss Tanzania Happiness Watimanywa ambaye pia ni Miss Dodoma na Miss Kanda ya Kati 2013, ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu  nchini Scotland ameahirisha masomo yake kwa muda wa mwaka mmoja hadi hapo atakapovua Taji la Mrembo wa Taifa mwishoni mwa mwaka ujao 2014.
   

  HIDAN .O. RICCO.
  PUBLIC RELATIONS OFFICER
  LINO INTERNATIONAL AGENCY
   

  0 0

  kurugenzi wa Msama Promotions,Inayoandaa tamasha la Krismasi,Bwa.Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya kwa msimamizi wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi,Haruna Mtandika.

  Hafla hiyo ilifanyika hapo jana kwenye ofisi za kampuni hiyo jijini dar,vituo vitano vilinufaika na msaada huo ambavyo ni onorata Temeke,Mwandaliwa Boko,Malaika Kinondoni,Yatima Group Truts Fund ya Chamazi na Mahabusu ya Watoto Upanga,vyote vya jijini Dar.Makabidhiano yao yamefanyika jana kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizopo Kinondoni jijini Dar.
   Baadhi ya Wanahabari mbalimbali waliofika kwenye tukio la Msama Promotions Ltd,ilipokuwa ikikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuuu za Krisimasi na Mwaka mpya kwa vituo vitano vya Watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu,jijini dar jana. 
  Mkurugenzi wa Msama Promotions,Inayoandaa tamasha la Krismasi linalotarajiwa kufanyika kesho Duniani kote,Bwa.Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha Mwandaliwa-Boko jijini Dar,Bi.Halima Mpeta.

  Mwenyekiti wa Tamasha hilo,Msama amesema kuwa kama ilivyo ada ya kampuni yake,imeamua kutoa kiasi fulani cha mapato yake ya tamasha hilo na kununua vyakula kwa ajili ya kuwapa zawadi watoto yatima na wasiojiweza ili na wao washerehekee sikukuu kwa furaha kama wenzao.

  Vituo vilivyopata zawadi hizo ni Honorata Temeke,Mwandaliwa Boko,Malaika Kinondoni,Yatima Group Truts Fund ya Chamazi na Mahabusu ya Watoto Upanga,vyote vya jijini Dar.Makabidhiano yao yamefanyika jana kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizopo Kinondoni jijini Dar.

  0 0
 • 12/23/13--20:23: UMEME BEI JUU JANUARI MOSI
 •  Taarifa ya EWURA YA bei mpya za umeme zitakazoanza kutumika Januari, Mosi,2013


  Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.

  Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.

  Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa 
  kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.

  Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011. 

  Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).


  USHIRIKISHWAJI WA WADAU

  Kulingana na Kifungu Na. 19(2) (h) cha Sheria ya EWURA, Mamlaka ilifanya Taftishi ili kupata maoni juu ya ombi la kurekebisha bei za umeme. Ukusanyaji wa maoni ulihusisha pia mikutano minne (4) iliyofanyika Iringa na Shinyanga tarehe 15 Novemba 2013, Bagamoyo tarehe 20 Novemba na kuhitimishwa Dar es Salaam tarehe 22 Novemba 2013. Aidha, tarehe 6 Desemba 2013, EWURA iliitisha mkutano wa mwisho wa wadau wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini(MEM), TANESCO, Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO), Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania, Baraza la Watumiaji na Baraza la Ushauri la Serikali, Umoja wa Wazalishaji wa Saruji wa Afrika Mashariki, na kiwanda cha ALAF. Katika mkutano huo EWURA iliwasilisha mwelekeo wa maamuzi kuhusu maombi ya TANESCO na namna zilivyokokotolewa. Wadau walipewa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu mwelekeo wa bei na maoni yao yamezingatiwa katika kufikia maamuzi ya mwisho.

  UCHAMBUZI NA UAMUZI

  Kwa kufuata sheria na kanuni zinazoelekeza kuhusu uchambuzi wa bei ya umeme, EWURA ilifanya uchambuzi wa kifedha na kiufundi ili kubaini uwezo wa TANESCO katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Uchambuzi uliangalia utendaji wa Shirika la TANESCO katika miaka iliyopita na pia iliangalia majukumu yanayoikabili TANESCO katika miaka mitatu ijayo. EWURA imebaini kwamba hali ya kifedha ya Shirika la Umeme sio nzuri. Shirika limeendelea kupata hasara, ambayo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 47.3 katika mwaka 2010 na kufikia shilingi bilioni 223.4 mwishoni mwa mwaka 2012. Pamoja na mapungufu ya kiufanisi, sababu kubwa ya ongezeko la hasara ni kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa umeme ambao TANESCO inanunua kutoka kwa wazalishaji binafsi. Hali hii imelifanya shirika kushindwa kulipa madeni yake ya muda mfupi na ya muda mrefu, ambayo yamelibikizwa na kufikia TZS 456.8 bilioni tarehe 22 Novemba 2013, hali ambayo inatishia uendelevu wa huduma ya umeme hapa nchini.

  Mamlaka imetumia Kanuni ya Ukokotoaji wa Bei kama ilivyopendekezwa na AF-MERCADOS wakati wa kukokotoa mahitaji ya mapato ya TANESCO. Kanuni hiyo inawezesha kukokotoa bei zinazolandana na gharama halisi kwenye mfumo wa umeme na kuzigawa kwenye makundi ya watumiaji umeme, kadiri kila kundi linavyosababisha gharama kwenye mfumo wa umeme kwa mujibu wa mahitaji ya Sheria ya Umeme ya 2008 Kifungu cha 23(2)(f).

  EWURA imejiridhisha kwamba, ufumbuzi wa matatizo ya kifedha ya TANESCO, unahitaji njia/mikakati miwili itekelezwe kwa pamoja:
  kuongeza bei ya umeme ili kufikia bei inayokidhi gharama halisi (Cost Reflective Tariff); na
  TANESCO kupata mkopo wa gharama nafuu ama ruzuku kutoka Serikalini ili kulipa limbikizo la madeni ya Shirika.

  Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, katika kikao chake cha tarehe 10 Desemba 2013 pamoja na mambo mengine, ilitoa maamuzi ya ongezeko la bei za umeme kwa viwango mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya wateja, kama ifuatavyo:

  Kundi D1: Hili ni kundi la wateja wadogo wa majumbani, hasa vijijini, ambao hutumia wastani usiozidi wa Uniti 75 kwa mwezi. EWURA imeongeza wigo wa mahitaji ya umeme na kufikia uniti 75 kwa mwezi, lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wateja wa TANESCO wanaoweza kulipa kidogo kwa matumizi ya umeme kwa kiwango hicho, na pia kuwahamasisha kutumie zaidi umeme. Awali kundi hili lilikuwa linatunia wastani wa matumizi ya uniti 50 kwa mwezi. Bei mpya ni shilingi 100 kwa uniti moja, kutoka shilingi 60 za sasa, sawa na ongezeko la shilingi 40.

  Kundi T1: Hili ni kundi la watumiaji wakubwa wa umeme majumbani, biashara ndogondogo, mashine za kukoboa na kusaga nafaka, taa za barabarani, mabango n.k. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 306 kwa uniti moja, ikiwa ni ongezeko la Shilingi 85 ya bei ya sasa. TANESCO ilipendekeza ongezeko la shilingi 131.

  Kundi T2: Hili ni kundi la watumiaji umeme wa kawaida ambao hupimwa katika msongo wa volti 400, na ambao matumizi yao ya wastani kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500 wateja wafanyabiashara kubwa, viwanda vya kati. Bei ya nishati iliyoridhiwa ni shilingi 205 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 73 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 145 ya bei ya sasa.

  Kundi T3-MV: Hili ni kundi la wateja wakubwa kama viwanda vikubwa waliounganishwa katika msongo wa kati (Medium Voltage). EWURA imeidhinisha bei ya nishati kwa kiwango cha shilingi 166 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 45 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 148 kwa uniti moja.

  Kundi T3-HV: Hili ni kundi la wateja wakubwa waliounganishwa katika msongo wa juu (High Voltage – Voti 66,000 na zaidi) ikiwa ni pamoja na ZECO, Bulyanhulu, na Twiga Cement. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 159 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 53 la bei ya sasa. TANESCO waliomba ongezeko la shilingi 80 kwa uniti moja.

  Bei ya umeme itakuwa inarekebishwa kila baada ya miezi mitatu kulingana na mabadiliko ya kiwango na bei za mafuta; mfumuko wa bei, mabadiliko ya thamani ya fedha, na upatikanaji wa ruzuku toka Serikalini.

  Vilevile, TANESCO inatakiwa kutekeleza miradi ya uwekezaji iliyoainishwa kwa kutumia fedha zitakazokusanywa kutokana na bei zilizoidhinishwa. EWURA inaweza kurekebisha bei ya umeme ya TANESCO kila mwisho wa mwaka 2014 na/au mwaka 2015 endapo TANESCO itashindwa kutekeleza miradi iliyotajwa katika Jedwali husika. Marekebisho hayo yatatokana na makadirio ya gharama za miradi ambayo haikutekelezwa.

  Kutokana na matazamio ya kuwa na mabadiliko makubwa katika uzalishaji wa umeme (generation mix) katika mwaka 2015 na kuendelea, kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa kwa upatikanaji wa gesi asilia, EWURA itafanya utafiti kubaini gharama halisi (Cost of Service Study) ya huduma ya umeme kwa wakati huo. Hivyo, bei zilizoidhinishwa zitatumika mpaka mwaka 2016, kama utafiti unaotazamiwa kufanywa hautakamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015.

  EWURA ililinganisha bei za umeme kwa kila Uniti, katika nchi za Afrika ya Mashariki, na kuona kuwa bado bei za umeme za Tanzania zipo chini ukilinganisha na bei za katika nchi jirani kama inavyoonyeshwa hapa chini, kwa makundi mbalimbali ya watumiaji umeme.

  Pamoja na maamuzi hayo, Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, pia iliagiza TANESCO kutekeleza yafuatayo:
  • kuzalisha umeme kwa kutumia mitambo yenye gharama nafuu ("least cost merit order") na kuwasilisha ripoti kwa Mamlaka katika kila mwezi ikionyesha uzalishaji halisi na mpango wa uzalishaji kama ilivyoidhinishwa na EWURA;

  • kuhakikisha kuwa zabuni za miradi ya uzalishaji umeme zinatolewa kulingana na mahitaji kama ilivyoidhinishwa kwenye Mpango wa Umeme wa Taifa (Power System Master Plan). Miradi yote mipya lazima ipatikane kwa njia ya ushindani kwa kufuata Sheria ya Umeme, "Public Private Partnership Act", Sheria ya Manunuzi ya Umma na Kanuni husika;

  • kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kuhusu viashiria vya takwimu za ubora na uhakika wa umeme (supply and reliability) katika misongo ya 11kV, 33 kV, 66 kV, 132 kV, na 220 kV kwa kila mkoa kwa ajili ya uhakiki. Takwimu husika zinatakiwa kuonyesha jumla ya masaa mteja aliyokosa umeme kwa kila njia ya umeme ("feeder"), kukosekana kwa umeme kulikopangwa (planned outages), na ambao haukupangwa (unplanned outages), idadi ya matukio ya kukosa umeme katika kila "feeder", idadi ya wateja wanaohudumiwa na kila "feeder", idadi ya wateja walioathirika na katizo la umeme katika kila "feeder" na kiasi cha umeme kilichokosekana kutokana na katizo hilo (total unserved energy in kWh);

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, katika kipindi cha miezi mitatu baada kuanza kwa Agizo hilo la Mamlaka, mpango wa utekelezaji wa "Demand Side Management Programme" ili uidhinishwe;

  • kupunguza kiwango cha upotevu wa umeme (technical and non-technical losses) katika mtandao wa usambazaji kutoka asilimia 19 ya mwaka 2012 hadi asilimia 15.1 ifikapo mwisho wa mwaka 2015;

  • kubuni mikakati ya kupambana wizi wa umeme utokanao na uunganishaji umeme usio halali, na kuondoa ucheleweshaji usio wa lazima katika kutunganisha wateja wapya;

  • kuhamisha wateja walio katika kundi la D1 kwenda T1 endapo matumizi yao ya mwezi yatazidi uniti 75 kwa miezi mitatu mfululizo;

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi, 2014, Mpango wa kuwawekea wateja wake mita za LUKU na AMR ili kupunguza wateja wanaotumia mita za zamani (conventional meters);

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, kila baada ya miezi mitatu, taarifa/ripoti ya ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wateja wake ili kuongeza mapato ya Shirika;

  • kutoa elimu kwa wateja wake kuhusu haki na wajibu wa wateja kwa mujibu wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja na kushughulikia kero za wateja kama inavyoelekezwa katika Mkataba husika na Kanuni za Umeme;

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, maombi ya marekebisho ya bei yatokanayo na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na ubadilikaji wa thamani ya fedha; Ukokotoaji wa marekebisho hayo utakuwa kama ulivyoainishwa katika Kanuni za Kupanga Bei za Umeme za mwaka 2013 (Electricity (Tariff Setting) Rules, 2013);

  • kuendelea kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu hali ya kifedha na kiundeshaji. Taarifa hizi zitatumiwa na Mamlaka katika kutathmini utendaji wa TANESCO ikilinganishwa na mashirika mengine ya umeme katika nchi jirani ili kuboresha utendaji wake. Tathmini hii pia itatumiwa na Mamlaka katika kubaini uhalali wa maombi ya baadae ya kurekebisha bei;

  • kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi 2014, mpango wa utekelezaji wa kila sharti katika Agizo la EWURA.

  Bei mpya za umeme zitaanza kutumika tarehe 1 Januari 2014. Ni matarajio ya EWURA kwamba TANESCO watatumia fursa hii kutoa huduma bora zaidi za umeme na kuhakikisha kuwa wanashughulikia malalamiko ya wateja kila yanapojitokeza ili kurejesha imani kwa Shirika la Umeme la TANESCO.

  0 0older | 1 | .... | 191 | 192 | (Page 193) | 194 | 195 | .... | 1897 | newer