Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

BONDIA FRANSICI MIYEYUSHO AJIFUA KWA AJILI YA KUMTWANGA DAVID CHALANGA WA KENYA DESEMBA 31

$
0
0
Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akielekezwa jinsi ya kutupa makonde kwa mpangilio na Doi Miyeyusho wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika GYM ya lazima ukae iliyopo kinondoni Dar es salaam. Miyeyusho anajiandaa na mpambano wake wa kimataifa wa kufunga mwaka na David Chalanga wa Kenya mpambano utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani klabu.

Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akielekezwa jinsi ya kutupa makonde kwa mpangilio na Doi Miyeyusho wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika GYM ya lazima ukae iliyopo kinondoni Dar es salaam Miyeyusho anajiandaa na mpambano wake wa kimataifa wa kufunga mwaka na David Chalanga wa Kenya mpambano utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani klabu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

WAZAZI WAMALIZA SEMINA MOROGORO

$
0
0
 KATIBU wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abilah Mihewa, akizungumza na washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, mwishoni mwa semina hiyo, Des 18, 2013. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Kinondoni, Charles Mgonja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Salum Madenge.
 Washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, wakiwa katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, Des 18, 2013, wakati wa semina hiyo.
 Katibu Mwenezi wa CCM, mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba akizungumza na washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, mwishoni mwa semina hiyo, Des 18, 2013. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Kinondoni, Charles Mgonja, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Salum Madenge na Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abilah Mihewa. Kushoto ni Katibu wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage.
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abilah Mihewa (kulia) akiingia ukumbini kujumuika na  washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, Des 18, 2013.
 Washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, wakila kiapo cha kuyashika mafunzo, walipokuwa kwenye semina hiyo, katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, Des 18, 2013
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akimshukuru Katibu wa Itikadi na Uenezi, CCM mkoa wa Morogoro Dorothy Mwamsiku baada ya Katibu huyo kufungua semina ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Wilaya ya Kinondoni, katika ukumbi wa Road View mkoani Morogoro, Des 17, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).

MAASKOFU ,WACHUNGAJI WABARIKI TAMASHA LA KRISMASI LA MUZIKI WA INJILI CCM KIRUMBA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste mkoani Mwanza Alexanda Mwakisumbwa (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo. wengine katika picha ni Mwenyekiti msaidizi Zenobius Isaya ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Filadelfia Church (kushoto) na Mwenyekiti wa Makanisa ya Kiprotestant Askofu Charles Sekelwa (kulia).
MAASKOFU ,WACHUNGANJI WABARIKI TAMASHA LA KRISMASI LA MUZIKI WA INJILI CCM KIRUMBA 

MAASKOFU na Wachungaji wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Jijini Mwanza,wameunga mkono Tamasha la Muziki wa Injili, baada ya kuridhia Kwaya ya Makanisa yao kushiriki tamasha hilo.

Tamasha hilo la Krismasi la  Muziki wa Injili, litafanyika Desemba 25 mwaka huu,majira ya saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti kwenye kikao cha pamoja kati yao na waandaaji wa tamasha hilo, The Great Lake  Zone Entertainment,kilichofanyika Vizano hoteli, Maaskofu hao walisema, mbali na kutangaza neno la Mungu na utukufu wake, litasaidaia kuutangaza muziki wa injili wa kwaya za Makanisa hayo ya Jijini hapa.

“Ni maono mazuri kwa waandaaji wa tamasha hilo,na sisi Maaskofu tunapaswa kuwaunga mkono badala ya kuwakatisha tamaa.Haiwezekani tukatafute waimbaji kuoka Dar es salaam badala ya kutumia hawa tulionao hapa,”alisema 

Askofu wa Kanisa la Menonite Tanzania (KMT) Nyakato,Albert Randa, alisema teknolojia imepanuka tofauti na zamani ambapo nyimbo nyingi na nzuri za kwaya hazikupata fursa ya kurekodiwa.Kwamba ukanda wa Ziwa hasa Mwanza na Mara kuna waimbaji wazuri wenye vipaji.

Askofu Charles Sekelwa,alisema jambo hilo (tamasha) likienda vizuri, ni heshima kwa waandaaji na akawataka Maaskofu wasiwe sehemu ya ubaya bali uzuri ili sifa na utukufu zimwendee Mungu ikiwa ni pamoja na kuwahamsisha waumini wao kuja kushiriki tamasha hilo ili kuwaepusha na starehe zinazomchukiza Mungu. 

Hata hivyo Askofu Sekelwa ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja huo wa Makanisa ya Kikristo Mwanza,  alionya tamasha hilo lisiwe la kisiasa ndani yake, ili kuepusha maaskofu kuchafuliwa kutokana na kuunga kwao mkono na ushiriki wao.

Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo Fabian Fanuel,mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, na kutakuwa na chakula cha usiku katika hoteli ya Malaika baada ya tamasha hilo. 

Tamasha hilo la muziki wa Injili litafanyika uwanja wa CCM Kirumba kuadhimisha kuzaliwa kwa Masiha (Yesu) kiingilio kitakuwa shilingi 2000 kwa watu wazima ambapo watoto watalipa shilingi 1000.

Tayari wasanii na waimbaji maarufu, Martha Mwaipaja ,Nesta Sanga, Neema Nga’sha,Daniel Safari na mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS) Pascal Cassian,watanogesha tamasha hilo kwa vibao vyao vilivyotamba na vinavyotamba kwa sasa katika muziki wa Injili,wamethibitisha kushiriki.

Wengine watakaopaza sauti zao siku hiyo ni Seiri Andrew (Nzega Tabora), Joseph Vedasto (Geita), Dan Sanga na Mary Msigwa (Iringa), Pendo Kanyumi, Christine Victor, Betty Lucas, Excellence Band, Revival Mission Band na kwaya mbalimbali kutoka Mwanza.

PATA GAZETI LAKO LA PATA HABARI KWA SH 500 TU

MAMA SALMA KIKWETE APOKEA TUZO KUTOKA KITUO CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA UONGOZI (CELD)

$
0
0
IMG_1583Wake wa Marais kutoka Barani Afrika waliotunukiwa Tuzo na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi wakionyesha tuzo,nishani na hati walizokabidhiwa kwa washiriki wa mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia na wageni wengine waliohudhuria sherehe ya utoaji tuzo hizo huko Dubai tarehe 18.12.2013. IMG_1628Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na watu aliofuatana nao kwenye sherehe ya kupokea Tuzo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia uliomalizika tarehe 18.12.2013 huko Dubai, Umoja wa Falme Aza Kiarabu .
IMG_1301 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na  Mama Denise Nkurunziza, Mke wa Rais wa Burundi (kushoto) pamoja na Mke wa Rais wa Namibia Mama Penehupifo Pohamba muda mfupi kabla ya kuhudhuria sherehe za kukabidhiwa tuzo  za Uongozi Uliotukuka  mwiswhoni mwa kikao cha siku tatu cha wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia kilichofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis The Palm iliyoko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (URA) kuanzia tarehe 16 hadi 18, Desemba 2013.IMG_1416Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake  na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Uongozi Uliotukuka kimataifa (Global Inspirational Leadership Award 2013) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Maendeleo ya  Kiuchumi na Uongozi Mheshimiwa Bibi Furo Giami, mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia.  Mkutano huo ulioandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi  (CELD), wakishirikiana na CEO Clubs Network na African Leadership Magazine uliofanyika katika hoteli ya Atlantis The Palm, huko Dubai , Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE.) Tuzo hiyo imetolewa tarehe 18.12.2013.IMG_1457Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya kushukuru mara tu baada ya kupokea Tuzo hiyo huko Dubai tarehe 18.12.2013.IMG_1555Dr. Angela Moore, Balozi wa Hisani kutoka kutoka Jimbo la Georgia, nchini Marekani akiwavisha nishani washindi wa Tuzo . 
IMG_1599Baadhi ya wajumbe na washiriki waliofuatana na msafara wa Mama Salma Kikwete kwenye mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia wakisherehekea na kumpongeza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, wakiongozwa na  Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu Mheshimiwa Mbarouk Mbarouk, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Uongozi Uliotukuka kwenye ukumbi wa Atlantis The Palm hotel tarehe 18.12.2013. 
PICHA NA JOHN   LUKUWI

KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA AFARIKI DUNIA

$
0
0

Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Bw. Emanuel Mteming'ombe. Bw. Mteming'ombe enzi za uhai wake.

KATIBU  wa  chama cha mapinduzi  (CCM) mkoa  wa  Iringa Bw Emanuel Mteming'ombe amefariki  dunia katika hospital  ya  mkoa  wa  Iringa.

Katibu   huyo  alikuwa amelazwa  katika Hospital  ya  mkoa  wa  Iringa kwa  zaidi  ya siku moja akisumbuliwa  kwa ugonjwa Athma na  leo amefariki  dunia.

Mwenyekiti  wa  CCM  mkoa wa  Iringa Jesca Msambatavangu  amethibitisha   juu ya taarifa  hiyo  na  kuwa  taratibu  za mazishi  zinafanywa .

DAR LIVE KURINDIMA KWA BURUDANI MSIMU HUU WA SIKUKUU

DK. FENELLA AFUNGA SEMINA YA WAZAZI MOROGORO.

$
0
0
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Waziri wa Habari, VIjana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Kata ya Kawe, Benjamin Joseph, alipotoa vyeti kwa wahitimu wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi Kata zote za Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, mwishoni mwa semina hiyo, leo Desemba 19, 2013, katika ukumbi wa Hioteli ya Road View, nje kidogo ya mji wa Morogoro. Wengine kutoka wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Kinondoni Salum Madenge na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi wilaya hiyo, Charles Mgonja. Jumla ya wahitimu 31 walitunukiwa vyeti baada ya kuhitimu semina hiyo. (Picha na Bashir Nkoromo).

MDAU GREYSON MWASE ALAMBA NONDOZ YA MASTERS OF ARTS IN CORPORATE COMMUNICATIONS AND PUBLIC RELATIONS KATIKA CHUO KIKUU CHA LEEDS KILICHOPO NCHINI UINGEREZA

$
0
0
 Bw. Greyson Mwase ambaye ni Afisa Mawasiliano katika Wizara ya Nishati na Madini ametunukiwa leo tarehe 19 Desemba, 2013  Masters Degree of Arts in Corporate Communications and Public Relations katika chuo kikuu cha Leeds kilichopo nchini Uingereza.
 Bw. Greyson  Mwase ambaye ni Afisa Mawasiliano katika  Wizara ya Nishati na Madini akiwa ameshikilia shahada  yake ( M. A. in Corporate  Communications and Public  Relations) mara baada ya kutunukiwa kwenye ukumbi maarufu wa mahafali ujulikanao kama Great Hall  uliopo katika chuo kikuu cha Leeds kilichopo nchini Uingereza.
 Bw. Greyson Mwase akiwa pamoja na wahitimu wenzake  wanaowakilisha nchi za Nigeria, Ghana na Kenya.
 Greyson Mwase akiwa  na wahitimu wenzake katika ukumbi maarufu wa Great Hall kabla ya kutunikiwa  shahada

 Bw. Greyson Mwase akiwa pamoja na wahitimu wenzake wanaowakilisha bara la Asia kabla ya kuanza kwa sherehe za kukabidhiwa shahada zao.

KUMEKUCHA TAMASHA LA KRISMASSI.

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI CHAFANYIKA MKOANI TANGA L EO.

$
0
0
 katikati waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Mh Ddkt Terezya Huvisa kulia ni katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula na kushoto ni katibu mpya wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Isaya Kisiri,katika kikao cha Baraza la wafanyakazi la ofisi hiyo mjini Tanga leo.
Waliokaa, katikaTi ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza jipya la wafanyakazi la Ofisi hiyo jijini Tanga leo...Picha na Evelyn Mkokoi.
 Wajumbe wa baraza jipya la wafanyakazi kutoka ofisi ya makamu wa rais katika kikao cha baraza hilo mjini tanga leo.

CHIBOKO YA SIMBA,OKWI ATUA JIJINI DAR JIONI HII,UWANJA WA NDEGE PALIKUWA HAPATOSHI KWA SHANGWE ZA MASHABIKI WA SOKA

$
0
0
Okwi akilakiwa kwa shangwe na mashabiki waliofika kumpokea mapema leo jioni.
 Okwi akiwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Yanga waliofika uwanja wa ndege kumpokea mapema leo jioni,jijini dar
 Okwi akionesha namba yake ya mashambulizi siku ya jumamosi

HATIMAYE mshambuliaji raia wa Uganda Emanuel Okwi ametua nchini leo majira ya saa tisa na nusu alasiri  na kupokelewa na viongozi wa Yanga katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Okwi  ambaye amesajiliwa Yanga kwa miaka miwili na nusu kwa jumla ya dola 60,000 alitua nchini na ndege ya  shirika la Rwanda mbali na viongozi hao wa Yanga ambao ni Abdallah Binkleb, Musa Katabalo na Seif Ahmed  'Magari' pia alilakiwa na wanachama wachache ambao walijitokeza uwanjani hapo kwa lengo la kushuhudia ujio  wake.

Akizungumza mara baada ya kutua uwanjani hapo Okwi ambaye amezaliwa  Desemba 25, mwaka 1992  alisajiliwa Simba akitokea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa kinda wa miaka 17, akisajiliwa kwa dau la  dola za Kimarekani 40,000 alisema "Mimi ni mchezaji na mpira ni kazi yangu, nimekuja kuichezea Yanga na  nitaitumikia kwa mapenzi yangu yote, nimekuja kufanya kazi na si kuiangalia Simba, mkataba wangu na Simba  ulishaishaga.

Akizungumzia mechi ya Yanga na Simba itakayofanyika Jumamosi ijayo alisema "Mimi nipo fiti, nipo tayari  kucheza mechi ya Simba, nimejiandaa kikamilifu, ila mwenye maamuzi ya mwisho ya mimi kucheza au  kutocheza ni kocha, kama atanipanga nitafurahi zaidi."alisema Okwi ambaye amejiunga kambini na wenzake jana  jioni kwenye hotel ya Protea iliyopo Oyesterbay jijjini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya  Nani Mtani Jembe Jumamosi.

Kuhusu utata wa usajili wake Yanga, Okwi alisema "Mimi hayo mambo siyajui, nimeyaacha mikononi mwa  viongozi wa Yanga ndio watakaomaliza hilo suala."alisema Okwi ambaye baada ya mkataba wake na Simba  kuisha Desemba mwaka jana aliongezewa mkataba wa miaka miwili na Simba kabla hajaanza kuutumikia  akahamia Etoile du Sahel ya Tunisia ambako aliuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 fedha ambazo Simba  wanazisotea  mpaka leo kwa kile walichoeleza kuwa Etoile haijawalipa.

Kufuatia hali hiyo, Simba walipeleka malalamiko yao Fifa kuishtaki Etoile ambayo nayo ilipeleka malalamiko  ya Okwi kuwa ametoroka kwenye klabu hiyo, ambayo hata hivyo alidai alikalishwa benchi miezi mitatu bila  kuchezeshwa wala kulipwa mshahara wake kitu ambacho kilimfanya atimkia nchini kwao Uganda miezi  michache iliyopita na Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), lilimuombea kibali mchezaji huyo Fifa ili ajiunge  na klabu ya Sports Clab Villa ili kulinda kiwango chake na Fifa ilimuidhinisha kuichezea klabu hiyo kwa muda   wa miezi sita suala lake likiwa linashugulikiwa na tayari ameichezea klabu hiyo kwa  miezi miwili.

Tayari Fufa wameiandikia Fifa barua kutaka ufafanuzi  wa usajili wa mchezaji huyo Yanga kwa vile alizuiwa  kucheza michuano ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kwa vile  hajamaliza matatizo yake na Etoile du Sahel.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb alisema "Baada ya mechi ya Jumamosi  tutatoa ufafanuzi zaizi kuhusu usajili wa Okwi, sisi hatujakurupuka, tumemsajili kwa ajili aweze kutusaidia  kwenye mechi zetu za kimataifa, tunaenda kupeperusha bendera ya Tanzania hivyo Simba wawe wazalendo,  kumsajili Okwi ni kama kunogesha 'ice' kwenye keki, tunalenga kuhakikisha michuano ya klabu bingwa 
mwakani tunafika mbali.

Kauli ya Binkleb imekuja kukiwa kwa mahasimu wao Simba kunawaka moto kwa wanachama kumshinikiza  mwenyekiti wao Ismail Aden Rage kujiuzulu huku wakimtuhumu kutafuna dola laki tatu za mauzo ya Okwi kitu  ambacho Rage anakipinga vikali kwa kusema hajatafuna fedha hizo na kuweka ngumu kujiuzulu.

WATOTO YATIMA KITUO CHA MOYO KWA MOYO KUFANYIWA HARAMBEE

$
0
0
 
Mratibu wa Harambee Meneja wa miradi wa kituo cha Moyo kwa Moyo, Renatus Mpiluka akizungumza kuhusu harambee katika ofisi za kituo hicho mjini Iringa.
Consolata Sanga meneja wa fedha wa CPEC kushoto , Renatus Mpiluka meneja mradi na Destory Wikedzi  Mkurugenzi wa CPEC wakiwa katika picha ya pamoja katika ofisi hizo (Picha zote na Denis Mlowe)
=========  ==========   ==========
WATOTO YATIMA KITUO CHA MOYO KWA MOYO KUFANYIWA HARAMBEE

Na Denis Mlowe,Iringa

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Creating Partnerships to Empower Communities (CPEC) la Iringa kwa kushirikiana na kituo cha radio cha Nuru Fm wameandaa harambee ya kukichangia kituo cha watoto yatima cha Moyo kwa Moyo kilichoko Matanana wilayani Mufindi.

Akizungumza na Tanzania Daima mratibu wa Harambee hiyo na Meneja wa Miradi wa kituo hicho Renatus Mpiluka alisema lengo la harambee hiyo ni kutunisha mfuko wa kituo hicho ili kuboresha huduma kwa yatima wapatao 300 wanaohudumiwa na kituo hicho.

Mpiluka alisema wameamua kufanya harambee hiyo kwa kuwa waliokuwa wafadhili wa kituo hicho kutoka Sweden wamepunguza misaada zaidi ya asilimia 70 kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani.

Alisema watoto yatima wanamahitaji makubwa ya ada za shule kwa wanafunzi wanaenda shule za sekondari, mavazi, chakula hivyo inawawia vigumu kituo kumudu gharama za uendeshaji wa kituo hicho.

“Kituo kinakumbana na changamoto nyingi sana tangu wafadhili kupunguza msaada hivyo tumeamua kufanya harambee ili tuweze kujiendesha na kuwasaidia watoto hao yatima ambao kwa kweli ni wengi na ni jukumu letu kuweza kuwasaidia kwa hali na mali katika kufanikisha ndoto zao za miasha” alisema Mpiluka

Mpiluka alisema changamoto hizo za mahitaji makubwa ya watoto yatima zimepelekea kituo cha Moyo kwa Moyo  kushirikisha wadau mbalimbali katika kuchangia na kujitolea misaada mbalimbali kwa kituo hicho.

Alisema kituo kimefanikiwa kuwapatia mafunzo ya ufundi watoto yatima na kuwawezesha kusoma masomo ya komputa na hivyo wafikishapo miaka 18 waweze kujitegemea na kuwapatia huduma ya chakula watoto walioko katika shule za msingi za Mufindi.

Katika harambee hiyo itakayofanyika siku ya Krismasi,Mgeni rasmi anatarajia kuwa Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Jackson Kiswaga na kusindikizwa na bendi ya Whispers  ya jijini Dar es salaam.

Kwa yoyote anayetaka kuchangia katika harambee hiyo anaombwa atume kwa tigo pesa 0655161678 na M-pesa 0756 56 56 03 au kwa kiingilio cha shilingi 20,000 kwa VIP na wakubwa 5000, watoto 2000. Kumbuka Kutoa ni moyo usambe si utajiri

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATUNUKU SHAHADA ZA UZAMILI WAHITIMU KATIKA TAASISI YA NELSON MANDELA ARUSHA

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha, akimtunuku Clarence Msafiri mhitimu wa shahada ya uzamili kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.
 Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha akimkabidhi zawadi maalum Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambae pia ni Mkuu wa Taasisi hiyo kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha, akihutubia kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha, akiwa  kwenye maandamano ya wahitimu wa shahada ya uzamili kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa shahada ya Uzamili kwenye Mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Disemba 19-2013.Picha na OMR)
 


WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS IKULU NA UTAWALA BORA ZANZIBAR AWEKA JIWE LA MSINGI LA KITENGO KIPYA CHA UTIBABU WA UTI WA MGONGO NA UBONGO

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mhe. Mwinyi Haji Makame akifungu pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo katika sherehe zilizofanyi Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Jengo jipya la kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo linalojengwa kwa mashirikiano ya Serekali ya Spen na ya Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mhe. Mwinyi Haji Makame akiwahutubia wageni mbalimbali katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la kitengo cha matibabu ya Uti wa mgongo na Ubongo huko Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
 Wageni mbalimbali kutoka tasisi za Serikali na madaktari wakimsikiliza mgeni rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mhe. Mwinyi Haji Makame (hayupo pichani) alipokua akitoa nasaha mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika sherehe zilizofanyi Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.

OPALACH & MAISHA MANO-A-MANO AT THE WEIGH-IN CEREMONY AND PROMISED FIREWORKS IN THEIR DUEL TOMORROW

$
0
0
ACCRA, GHANA, DEC. 19, 2013: Boxers Premyslaw Opalach 13(12)-2-0of Poland and Maisha Samson 8(4)-4(2)-2
of Tanzania
weigh - in today in a much fanfare atmosphere at the Accra Sports Stadium's auditorium before a battery of sports journalists from all the media houses in Ghana. The meeting of the two young Turks who landed in the capital city of Ghana ready for their much awaited duel, as like a hide and seek game.

Opalach weighed 167 lbs. while Samson weighed 165 and were both declared on weight by the IBF Africa & Mideast President Onesmo Alfred McBride Ngowi who will be at the ringside tomorrow to supervise the exciting rumble.

The ground started to shake when both boxers were asked to face each other and pose for the photo opportunity and it was the President of GBA who intervened to save the situation from generating to a fist fight as the two marauding young Turks aimed their arsenals at each other.

Asked how he would approach the fight tomorrow, Maisha promised fireworks and asked fans from all parts of Ghana to come in thousands to see his style of boxing as he teaches the Polish gunner a lesson or two. Speaking in Kiswahili language which was interpreted by his accompanied Kenyan boxing agent Thomas Mutua, he said that he flew all the way from Tanzania to win the title and not as a mere participant.

Opalach was more excited when he was asked how he perceived the game tomorrow. Speaking in Polish language with a Ghanaian interpreter, he said that he appreciated Maisha's talents as a good boxer and promised to give Ghanaians a good entertainment come tomorrow.

The IBF International Super Middleweight Title was declared vacant after its immediate champion and Germany based Serbian Beard Ajetovic relinquished it for the much superior title, the IBF Inter Continental Super Middleweight Title respectively.

The tournament will take place tomorrow at the Accra Sports Stadium and promoted by Box Office Promotion Limited of Ghana and sanctioned by International Boxing Federation (IBF).

Ring officials for the tomorrow's rumble will be lead by the President of IBF Africa & Mideast Onesmo Alfred McBride Ngowi as a supervisor while Freddy Ghartey from Ghana will be the third man in the ring (referee). Judges will be Michael Neequeye, Emanuel Brenya and Clément Ashong all from Ghana.

Congratulations Ghana. Africa & Middle East is proud of you.
They Call itAFRICA &MIDDLE EAST.....! We Call it HOME

IDDY MNYEKE AMPANIA COSMAS CHEKA DESEMBA 31

$
0
0

Bondia Iddy Mnyeke  akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala  Amana CCM Dar es salaam mabondia hawo watapanda ulingoni kuwakabili wapinzani wao, ambapo Mnyeke atacheza na Cosmas Cheka na King class mawe atazidunda na Mohamed Kashinde desemba 31 katika ukumbi wa msasani klabu.  kulia ni kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli 'Masta' Picha na BLOG YA SUPER D

 
========= =========  ==========
 
BONDIA Iddy Mnyeke  yupo katika mazoezi mazito akijiandaa na mpambano wake na Cosmas Cheka utakaofanyika desemba 31 katika ukumbi wa msasani klabu jijini ar es salaam 

akizungumzia mpambano huo Mnyeke amesema Ccheka ni mtoto mdogo sana,anadhani anaweza kusafiria nyota ya kaka yake, ajue ameingia anga nyingine hivyo atakiona cha mtema kuni kuwa  mimi sio kama mabondia aliewahi kuwashinda

Mnyeke ambaye anafanya mazoezi katika kambi ya Ilala jijini Dar es salaam,ameongeza  kusema siku hiyo watu waje kwa wingi wangalie anavyo mchakaza na kuongeza kuwa waje yeye na kaka yake ili apate msaada wakati atakapo mwangusha chini kwa ngumi kali misri ya nondo ambazo zitakazo msambalatisha raundi za awari kwani yeye ni cha mtoto kwake  


Katika mchezo huo kutakuwa na michezo mingine ambapo  bondia  Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  ataoneshana ubabe na Mohamed Kashinde,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha katika mchezo mwingine ni kati ya Fransic Miyeyusho wa Tanzania akizichapa na David Chalanga kutoka Kenya


LEO NI LEO MZALENDO PUB MILLENNIUM TOWERS KIJITONYAMA

KAA TAYARI,TAMASHA LA KRISIMASI LAJA.

WATAKIWA KUACHA KULIMA KANDO MWA HIFADHI

$
0
0
Na Denis Mlowe.Aliyekuwa Arusha
WANANCHI  wa wanaozunguka   hifadhi   ya  Taifa ya Ziwa Manyara iliyoko mkoani Arusha wametakiwa kulinda hifadhi hiyo kwa kuachana na kulima katika vyanzo vya maji na maeneo yanayoizunguka hifadhi hiyo.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa TANAPA Dk.Ezekiel Dembe hivi karibuni wakati akizungumza na  wanahabari mkoa wa Iringa ambao  walikuwa katika ziara ya mafunzo ya kutangaza utalii katika  Hifadhi za Kaskazini.
Alisema kuna hatari kubwa ya  Ziwa Manyara kukauka zaidi kutokana na wananchi kuendelea kulima na kupelekea ziwa kujaa tope kutokana na kilimo hicho cha pembezoni.

Dk.Dembe alisema kutokana na kisichozingatia uhifadhi wa Ziwa Manyara baadhi ya ofisi za hifadhi  hiyo zimeharibika vibaya kutokana na mafuliko hivyo Tanapa wana mpango wa kutafuta  eneo  jingine ili kujenga ofisi  hizo.
Akizungumzia ubovu  wa  miundo  mbinu katika hifadhi za Taifa alisema kuwa  TANAPA  wapo katika mkakati kuboresha miundo mbinu  hiyo ili kuvutia  zaidi watalii wanaofika katika  hifadhi  hizo kuendelea kupitika kwa urahisi kwa mwaka

Akielezea kuhusu hifadhi ya Taifa Ruaha iliyoko Iringa kutangazwa kama ilivyo hifadhi za Kaskazini Dk. Dembe, alisema kuwa hivi  sasa mkakati umewekwa wa kuelekeza nguvu ya kuitangaza hifadhi hiyo  ili kuvutia watalii  zaidi  japo alisema  changamoto  kubwa ni upatikanaji wa mafuta  ya Ndege ambazo zinaleta  watalii ambao  hulazimika kujaza mafuta Dodoma .
“Hata  hivyotumeanza mkakati wa kuhakikisha hifadhi ya Katavi na Ruaha katika viwanja wa ndege  vilivyopo  huko kunakuwa na mafuta ya ndege  kupunguza gharama ambazo watalii wanatumia kwa sasa” alisema Dk. Dembe 
Alisema TANAPA wako katika mchakato wa kutafuta  wawekezaji wa kujenga  Hotel za kisasa katika hifadhi ya Ruaha ili kuvutia  watalii wengi zaidi.
Kuhusu  usalama wa watalii alisema kuwa  TANAPA wamejipanga  kuweka usalama mzuri wa watalii ili ni pamoja na kuanzisha ulinzi wa askari  watakaofanya kazi ya kulinda  watalii pekee.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images