Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Washindi promosheni ya Tigo Wakala Kinara Kitaifa na kikanda wazawadiwa

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Promosheni ya kishindo cha Funga Mwaka na Tigo , Mara baada ya kukabidhiwa hundi zao mapema leo.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari . katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa promosheni ya Kishindo cha Funga Mwaka na Tigo.
“Tunapenda kuwashukuru sana wateja wetu wote ambao walishiriki kwenye promosheni hii lakini kwa leo tumeweza kuwapata washindi watatu ambao wanahitimisha promosheni hii ambayo ilifanyika nchi nzima na tulikuwa na washidi zaidi ya 331 ambao wameshinda milioni 500,” Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Mapema leo
“Mimi nimfanya biashara wa vifaa vya umeme hapa Dar es Salaam na mtaji wangu ni wa kawaida tu lakini kupitia ushindi huu naamini kabisa malengo yangu ya kumiliki biashara kubwa zaidi yatatimia.Nawashukuru sana Tigo kwa kuanzisha promosheni hii kwani ushindi huu utabadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa,”Mshindi wa kwanza Salum Biwi mkazi wa Manzese baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh20 milioni leo Januari 3, 2019.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akimkabidhi mfano Hundi Hamidu Mtabiage kutoka mkoani Lindi aliyeshinda Sh15 milioni alisema “Naishukuru sana Tigo Pesa kwasababu mimi ni mfanyabiashara mdogo wa vifaa vya pikipiki na kwa kushinda pesa hizi zitaniwezesha kukuza mtaji wangu kutoka kuuza vifaa hadi kuuza pikipiki kwani hii ni ndoto yangu ya muda mrefu.
Anna Mkongwa kutoka Dodoma ndiye mshindi wa tatu wa promosheni ya KishindoChaFungaMwaka aliweka pesa kwenye Tigo pesa ili ashinde pesa.

 Huenda changamoto za Januari zikawa historia kwa baadhi ya washindi ambao wamejipatia fedha kupitia promosheni ya Kishindo cha Funga mwaka kutoka Kampuni ya Tigo (Tigo Pesa) jambo linalowaweka katika nafasi nzuri ya kukabiliana na mambo mbalimbali yanayojitokeza hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka.

“Nilipigiwa simu Jumatano iliyopita nikataarifiwa kwamba ni mshindi wa shillingi milioni 20m, kwa kweli sikuamini mpaka nilipoona jina langu katika mitandao ndio nikaamini. Nimshukuru Mungu kwani nilikuwa nina shiriki katika promosheni hii,kwa matarajio ya kwamba na mimi nitaibuka mshindi wa million hata moja,ili niweze kuongeza mtaji,kwa bahati nzuri nimeibuka mshindi wa kwanza wa shilling million 20” ndivyo alivosema Salum Biwi mkazi wa Manzese baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh20 milioni leo Januari 3, 2019.

Biwi ambaye ni mshidi wa kwanza wa Kampeni hiyo alisema ushindi huo ni mkubwa kwake na kwamba amejipanga kutumia fedha hizo kuongeza mtaji kwenye biashara yake ya sasa.

“Mimi nimfanya biashara wa vifaa vya umeme hapa Dar es Salaam na mtaji wangu ni wa kawaida tu lakini kupitia ushindi huu naamini kabisa malengo yangu ya kumiliki biashara kubwa zaidi yatatimia.Nawashukuru sana Tigo kwa kuanzisha promosheni hii kwani ushindi huu utabadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa,” alisema Biwi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema promosheni hiyo ilifanyika mwezi Desemba kwa lengo la kuwashukuru wateja kwa kutumia huduma ya Tigo Pesa kwa kipindi chote cha mwaka 2019.

“Tunapenda kuwashukuru sana wateja wetu wote ambao walishiriki kwenye promosheni hii lakini kwa leo tumeweza kuwapata washindi watatu ambao wanahitimisha promosheni hii ambayo ilifanyika nchi nzima na tulikuwa na washidi zaidi ya 331 ambao wameshinda milioni 500,” alisema Pesha.

Kwa upande wake Hamidu Mtabiage kutoka mkoani Lindi aliyeshinda Sh15 milioni alisema “Naishukuru sana Tigo Pesa kwasababu mimi ni mfanyabiashara mdogo wa vifaa vya pikipiki na kwa kushinda pesa hizi zitaniwezesha kukuza mtaji wangu kutoka kuuza vifaa hadi kuuza pikipiki kwani hii ni ndoto yangu ya muda mrefu.” 

Naye, Anna Mkongwa aliyeshinda Sh10 milioni, alisema pamoja na kuwa yeye ni mtumishi wa Umma, fedha alizozipata zitamsaidia kutimiza malengo mbalimbali hasa mwanzo huu wa mwaka.

“Kiukweli pesa hizi ni nyingi na sikutegemea kama ningeshinda hivyo kwa sasa nitakachokifanya ni kuweka malengo vizuri na pesa hii itanisaidia kuyatimiza,” alisema Mkongwa mkazi wa Dodoma.

Mbali na washindi hao, Kampeni hiyo ilikuwa ikitoa zawadi kwa washindi 8 wa Sh1 milioni kila siku na washindi 8 wa Sh5 Milioni kila wiki na tayari wamekwisha pokea zawadi zao.

NBC yawaasa watanzania kutumia malengo akaunti kama suluhisho ya changamoto zao

$
0
0
 Meneja wa Kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Mtenya Cheya  ( kushoto), akizungumza na mmoja washindi aliyeshinda zawadi ya bodaboda katika droo ya tatu ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza wa NBC,  Dorothea Mabonye, Meneja Chapa na Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond na Wakaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga na Abdallah Hemedi.
 Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC, David Raymond (wa tatu kushoto),  akizungumza waandishi wa habari katika droo ya tatu ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni; Meneja wa kampeni hiyo, Mtenya Cheya,  Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza wa NBC,  Dorothea Mabonye, na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga. 
 Maofisa wa NBC na kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, wakichezesha droo ya tatu ya kqampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo ambapo wateja watano walijishindia pikipiki mpya aina ya Yamaha. 
 Meneja wa Kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Mtenya Cheya  (kushoto), akizungumza na mmoja washindi aliyeshinda zawadi ya bodaboda, huku Meneja Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye (kushoto kwake) akishangilia  katika droo ya tatu ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto kwa Dorothea ni; Meneja Chapa na Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond , Wakaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga  na  Abdallah Hemedi pamoja na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imewahamasisha watanzania kutumia akaunti ya malengo ya benki hiyo kama suluhisho ya changamoto mbalimbali za kifedha hivyo kuwawezesha kutimiza malengo ya ndoto zao. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo kwenye droo ya tatu ya kampeni ya Ibuka kidedea na NBC Malengo, Meneja Chapa na Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond alisema kwamba wateja wa benki hiyo waendelee kutumia benki hiyo ili kutatua changamoto zao za kila siku. 

“Huu ni mwanzo wa mwaka na watanzania wengi wanakabiliwa na majukumu kadhaa kama vile ada za shule, kodi za nyumba na bima za gari na nyumba, ni muhimu kwao kuendelea kuwa karibu na benki hii na kwa wale ambao bado hawajafungua akaunti ya malengo ni vyema wakufungua ili waweze kunufaika na zawadi,” alisema Raymond. 

Meneja huyo wa Chapa na Mawasiliano alisema kwamba droo hiyo ni ya tatu ambayo ilianza mwezi wa Oktoba mwaka jana na washindi kadhaa wa bodaboda na safari za kutalii mbuga za wanyama Serengeti na Visiwani shelisheli walikwenda na kurudi salama kwa usimamizi na ufadhili wa benki hiyo kupitia kampeni ya malengo akaunti. 

Kwenye droo hiyo ya jana washindi watano waliibuka kidedea kwa kujishindia pikipiki aina ya Yamaha, washindi hao ni; Luka Haule Baraka wa Dodoma, Juma Halfani kutoka Songea, Rebeka Ndosh anayeishi Mwanza, Rosemary Kibodya wa Dar es Salaam na Restituta Mbuya wa Morogoro. 

Kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo itashuhudia washindi watatu wakiibuka kidedea na kujishindia zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo katika droo kubwa inayotarajiwa kufanyika Mwezi Machi mwaka huu. 

NEWZ ALERT: Matokeo ya Kidato cha Nne, Kidato cha Pili na QT yatangazwa, Yatazame hapa

Baraza la wafanyakazi ni ‘bunge’ la taasisi, litumieni vizuri

$
0
0
 Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Pontian Kitorobombo akiongea katika mkutano wa baraza la Wafanyakazi la THBUB.

 Mgeni rasmi (Mwenyekiti wa THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akifungua   mkutano wa baraza la Wafanyakazi wa kumi na nane (18) uliofanyika jijini Dodoma Januari 10, 2020.

 Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB, Hajjat Fatuma Muya akiongea katika Mkutano huo. Kushoto kwake ni Mgeni rasmi, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu.

 Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi  wakifuatilia kwa karibu mkutano huo.



Na Mbaraka Kambona, 

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wametakiwa kutumia vizuri mikutano ya baraza kujadili kwa hekima na kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya watumishi wote ili kuleta tija kazini. 

Wito huo ulitolewa na Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (Mgeni rasmi) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, katika mkutano wa kumi na nane (18) uliofanyika jijini Dodoma Januari 10, 2020. 

Wakati akifungua Mkutano huo, Jaji Mwaimu aliwaeleza wajumbe kuwa baraza hilo ni kama bunge la taasisi kwa kuwa linaundwa na wawakilishi wa wafanyakazi waliochaguliwa kidemokrasia. 

“Baraza hili ni chombo muhimu kilichoundwa kisheria kwa madhumuni ya kuwashirikisha watumishi katika kujadili na kufanya maamuzi yanayohusu maslahi ya ajira kwa lengo la kuleta tija mahala pa kazi”, alisema Jaji Mwaimu 

Jaji Mwaimu aliendelea kueleza kuwa wajibu wa mabaraza kama vyombo vya ushauri na usimamizi ni kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao na wanazingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo makubwa ya utendaji kazi yenye tija. 

“Baraza la wafanyakazi wajibu wake ni kuhakikisha kunakuwepo na ushirikiano wa kutosha baina ya watumishi na mwajiri ili kuweza kutekeleza ipasavyo majukumu ya taasisi na kufikia malengo yaliyokusudiwa”, aliongeza 

Aliendelea kuwataka wajumbe kushiriki kikamilifu katika kujadili utendaji wa kazi wa kila siku ili kuuboresha kwani tija na maslahi lazima viwe na uwiano ili kuwe na matokeo bora ya utendaji kazi unaolenga kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi wanaowatumikia. 

Aidha, Jaji Mwaimu alitoa rai kwa wajumbe hao kuwa majadiliano yao yatawaliwe na hekima, busara, uwazi na maelewano ili uwakilishi wao uwe na maana iliyokusudiwa, na yale yote watakayoyajadili wayapeleke na kuwaeleza watumishi wenzao ili kujenga uelewa wa pamoja. 

RAIS DKT MAGUFULI AWASILI ZANZIBAR KUSHIRIKI SHEREHE ZA MIAKA 56 ZA MAPINDUZI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (aliyeketi) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdallah Juma
Sadallah 'Mabodi' mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume mjini Unguja  tayari kushiriki katika Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitazofikia kilele
siku ya Jumapili Januari 12, 2020 .PICHA NA IKULU.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume mjini Unguja  tayari kushiriki katika Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitazofikia kilele siku ya Jumapili Januari 12, 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume mjini Unguja
tayari kushiriki katika Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitazofikia kilele siku ya Jumapili Januari 12, 2020

RAIS MAGUFULI AZINDUA HOTEL VERDE – AZAM LUXURY RESORT AND SPA ILIYOPO MTONI ZANZIBAR. JANUARI 11, 2020

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa na Makamu wa Rais wa Jamhuri Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa group Mzee Said Salim Bakhresa pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mapinduzi  kuashiria uzinduzi wa Hotel Verde – Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa group Mzee Said Salim Bakhresa mara baada ya kuzindua Hotel Verde ya Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na Makamu wa Rais wa Jamhuri Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa group Mzee Said Salim Bakhresa pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mapinduzi  kuashiria uzinduzi wa Hotel Verde – Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa group Mzee Said Salim Bakhresa pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mapinduzi  wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Vyakula wa Bakhresa Salim Aziz Salim huku wakitazama maeneo mbalimbali ya Hotel Verde – Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar wakati wa sherehe za uzinduzi wa hoteli hiyo Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijaribu vifaa vya mazoezi alipoambatana na Viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mapinduzi kutazama maeneo mbalimbali ya Hotel Verde – Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar  wakati wa sherehe za uzinduzi wa hoteli hiyo Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa group Mzee Said Salim Bakhresa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Vyakula wa Bakhresa Salim Aziz Salim huku alipokuwa akigagua moja ya chumba  cha Hotel Verde – Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar wakati wa sherehe za uzinduzi wa hoteli hiyo Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa group Mzee Said Salim Bakhresa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Vyakula wa Bakhresa Salim Aziz Salim akikagua moja maeneo mbalimbali ya Hotel Verde – Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar  wakati wa sherehe za uzinduzi wa hoteli hiyo Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hotel Verde – Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hotel Verde – Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa group Mzee Said Salim Bakhresa alipowasili kabla ya kuzindua Hotel Verde – Azam Luxury and Spa iliyopo Mtoni Zanzibar Januari 11,2020 kuelekea sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofanyika Januari 12, 2020 Visiwani Zanzibar.
PICHA NA IKULU

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AHUTUBIA KILELE CHA MIAKA 56 YA MAPINDUZI ZANZIBAR.

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride Maalum la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza vla Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar
 Mgeni rasmi,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Sheinakisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya sita Dk. Amani Abeid Karume alipowasili jukwaa kuu,katika Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.Pichani kati anaeshuhudia ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

VIJANA wa Maandamano Maalum ya kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa na Picha za Waasisi wa Mapinduzi, wakati wa hafla hiy0 iliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Vijana wa Chama cha mapinduzi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi ikiwa ni Ishara ya kutoa heshima katika maandamano ya maadhimisho ya ya Miaka 56 ya Mapinduzi yaliofanyika Aman mjini Zanzibar. 
WANACHAMA wa Chama cha CUF wakishiriki katika Maandamano ya kuadhimisha sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar
VIJANA wa payunia wakitowa salamu ya heshima kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein wakati wa maandamano ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vikosi vya Jeshi la Ulinzi na Usalama Vikipita mbele ya Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi yaliofanyika Aman mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya kilele cha  Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi yaliofanyika Aman mjini Zanzibar.PICHA NA IKULU PAMOJA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA KILELE CHA SHEREHE ZA MIAKA 56 ZA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR MJINI UNGUJA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea salamu ya heshima kutoka katika paredi maalum ya vyombo vya ulinzi na usalama wakati wa sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ally Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bi. Mwanamwema Shein mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ally Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ally Mohamed Shein wakati maandamano yakipita mbele  katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ally Mohamed Shein wakati paredi ikipita mbele kwa heshima  katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma kitabu cha hotuba wakati  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ally Mohamed Shein akihotubia katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ally Mohamed Shein baada ya kumalizika kwa sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa baada ya kumalizika kwa sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bi. Fatuma Karume mke wa muasisi na Rais wa kwanza  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Abeid Karume mara baada ya kuwasili katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020
Makomandoo wa jeshi la JWTZ wakionyesha mazoezi ya ukakamavu  mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ally Mohamed Shein wakati wa sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Amani Unguja. Januari 12, 2020
 PICHA NA IKULU

TICTS YAFANYA BONANZA LA MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WAKE KUIMARISHA AFYA

$
0
0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia shehena ya kontena bandarini (TICTS), mwishoni mwa wiki walikusanyika kwa pamoja kufanya mazoezi ya kuimarisha afya zao, mazoezi yanayofanyika kila mwanzo wa mwaka kwa Wafanyakazi hao kufanya shughuli mbalimbali za michezo ili kuimarisha afya zao mahala pa kazi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa Bonanza hilo, Mkurugenzi wa Shirika na Maendeleo wa Kampuni hiyo, Donald Talawa amesema wafanyakazi hao wamekusanyika kwa pamoja kufanya shughuli hizo za michezo ili kuimarisha afya zao na kuleta tija wawapo kazini.

“Wafanyakazi wamefanya riadha ya KM 5 na 21, Mpira wa Miguu, kuvuta kamba na michezo mbalimbali, tunaamini hii italeta tija na ufanisi mahala pa kazi kwa kufanya hivi mara kwa mara”, amesema Talawa.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wafanyakazi hao, Getrude Lamu amesema wamefanyakazi wamefurahi sana kufanya mazoezi katika michezo mbalimbali katika bonanza hilo, amesema wamehamasisha michezo hiyo mahali pa kazi kwa kufanya mazoezi mara kwa mara.

“Wafanyakazi wa TICTS katika bonanza la leo wamefika kwa wingi na wamefurahi sana kufanya bonanza hili, mwezi huu ni mwezi wa mazoezi, tunashughuru utawala wa Kampuni yetu kuleta kitu hiki kwa Wafanyakazi wetu”, amesema Getrude Lamu. Endelea kuangalia picha mbalimbali za michezo hiyo hapo chini.
























WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, AZINDUA JENGO LA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU) WILAYANI RUANGWA.)

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati alipozindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikata utepe, wakati alipozindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, wakati alipozindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, wakati alipozindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya ruangwa, wakati wa uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), lililopo katika Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya ruangwa, wakati wa uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), lililopo katika Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipanda mti, baada ya kuzindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


KATIBU MKUU HAZINA AHIMIZA WATUMISHI WA TRA KUONGEZA BIDII UKUSANYAJI MAPATO

$
0
0
Veronica Kazimoto na Rachel Mkundai,Arusha

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, amewahimiza watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, na kwa kuzingata misingi wa Sheria za kodi ili kuhakikisha kuwa TRA inaendelea kuvunja rekodi ya makusanyo ya mapato kama ilivyokuwa katika mwezi Septemba na Desemba, 2019.

Pia, amewapongeza watumishi wote wa Mamlaka hiyo kwa kujituma na kupelekea Serikali kukusanya mapato kiasi cha Sh. trilioni 9.341 sawa na ufanisi wa asilimia 47.67 ya lengo la kukusanya sh. trilioni 19.595 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2019/2020 yaani kuanzia Julai hadi Desemba 2019.

Akizungumza wakati wa mkutano wa mapitio na tathmini ya utendaji kazi wa nusu mwaka 2019/20 wa Mamlaka hiyo uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha, Bw. James alieleza kuwa, mapato makubwa yanayotegemewa na Serikali ni makusanyo ya kodi ambapo aliwaasa watumishi wa TRA kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuongeza mapato na hatimaye Serikali iweze kutekeleza mipango yake iliyojipangia ya kuwaletea wananchi wake maendeleo.

“Ukiangalia mchanganuo wa makusanyo yote ya Serikali, sehemu kubwa sana ni kodi inayokusanywa na TRA. Kwa msingi huu, TRA inapofanikiwa kukusanya kodi kwa ufanisi mkubwa ndiyo mafanikio ya Serikali katika kutekeleza bajeti inayokuwa imepangwa kwa kipindi hicho,” alisema Katibu Mkuu huyo.

Aidha, aliwashukuru wananchi na walipakodi wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati ambapo makusanyo ya mwezi Septemba na Desemba, 2019 ni ishara kwamba, walipakodi kwa ujumla wao, wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuongeza mapato ya ndani na pia wameendelea kutambua umuhimu wa kulipa kodi baada ya kuona utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini inayofanywa na Serikali yao.

“Tunawashukuru sana walipakodi wa nchi hii kwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kuisadia Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania kukusanya kodi hiyo kubwa tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo. Kitendo hiki kiendelee na ikiwezekana iwe zaidi ya hapo”, alieleza Bw. James.

Akizungumzia suala la mifumo ya kieletroniki ya ukusanyaji mapato, ukiwemo mfumo wa mnada wa forodha kwa njia ya mtandao, Katibu Mkuu huyo, ameipongeza TRA kwa kuendelea kuboresha mifumo hiyo ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato ya Serikali.

“Mfumo wa mnada wa forodha kwa njia ya mtandao ni mfumo mmojawapo kati ya mifumo mingi inayotumiwa na TRA katika kukusanya mapato. Mfumo huu, ambao umejengwa na Watalaam wetu wa TRA, umeonesha mafanikio makubwa kwa sababu unashirikisha watu wengi na kuleta ushindani wa haki kwa wote.

“Ni matarajio yetu kuwa, Serikali itapata mapato yake stahiki kutokana na kuuzwa kwa bidhaa zilizokaa muda mrefu bandarini tofauti na matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 na ni matumaini yetu kwamba, kuuzwa kwa wakati kwa bidhaa hizo kupitia mfumo huu, kutapunguza mrundikano wa bidhaa bandari na hivyo kuongeza ufanisi wa bandari zetu na vituo vingine vya forodha”, alieleza.

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James amewaagiza viongozi wa TRA kufanya maboresho ya mifumo ndani ya Mamlaka hiyo mara moja pale watakapobaini mapungufu yoyote ambayo yanaweza kukwamisha utendaji kazi wa mfumo husika.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Edwin Mhede, alisema kwamba, mkutano huo wa mapitio na tathmini ya nusu mwaka ulilenga kufanya maboresho katika utendaji kazi ili kuhakikisha kuwa malengo waliyopangiwa na Serikali yanafikiwa.

Dkt. Mhede aliongeza kuwa, TRA imepewa agizo na Serikali la kukusanya kiasi cha sh. trilioni 19.5 katika mwaka huu wa fedha 2019/20 ambapo pamoja na kufanya vizuri katika miezi ya Septemba na Desemba, 2019, alikiri kuwa bado Mamlaka hiyo haijafikia malengo ya makusanyo kwa asilimia 100. Hivyo, mkutano huo ulilenga kufanya marejeo na maboresho ya mikakati ya utendaji kazi itakayowezesha kufikia malengo hayo kwa asilimia 100.

“Kupitia Sheria ya Bajeti, SURA 439, TRA tumepewa agizo na Serikali la kukusanya mapato kiasi cha sh. trilioni 19.595 hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2020 na wakati tukitekeleza robo ya kwanza na ya pili ya mwaka wa fedha 2019/2020, hatukufanikiwa kufikisha asilimia 100 ya makusanyo ya robo hizo. Hii ndiyo moja ya sababu tumeona tukutane ili tubaini maeneo yenye mapungufu na kisha tufanye marejeo shirikishi ili tujisahihishe na kuweka mikakati itakayotuwezesha kufikia lengo”, alisema Dkt. Mhede.

Mkutano wa mapitio na tathmini ya utendaji kazi wa nusu mwaka 2019/20 wa TRA ulihudhuriwa na jumla ya washiriki 361 ukihusisha Menejimenti nzima ya Mamlaka, Mameneja wote wa Mikoa na Wilaya kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo.

Washiriki wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na wawakilishi kutoka baadhi ya Asasi za Serikali kama vile Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Ofisi ya Rais - Tume ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Mganga Mkuu - Mkoa wa Arusha, na Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAeSA) iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi na Ajira) ambapo kwa siku ya kwanza wawakilishi wa Asasi hizo walitoa maada kuhusu masuala mbalimbali ya kuisaidia TRA kuongeza makusanyo ya Serikali. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mara baada ya Mkutano wa Mapitio ya Utendaji kazi wa Nusu Mwaka wa Fedha wa 2019/2020 uliofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akizungumza na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa Mkutano wa Mapitio ya Utendaji kazi wa Nusu Mwaka wa Fedha wa 2019/2020 uliofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akizungumza na baadhi ya watendaji wa TRA mara baada ya Mkutano wa Mapitio ya Utendaji kazi wa Nusu Mwaka wa Fedha wa 2019/2020 uliofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.

MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA AANAYEMALIZA MUDA WAKE BI.BELLA BIRD APONGEZA TASAF KWA MAFANIKIO YA KUPUNGUZA UMASKINI NCHINI.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga  (picha ya juu na chini ) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake nchini Bi. Bella Bird katika hafla ya kuagana naye .
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuagana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia aliyemaliza muda wake, Bi. Bella Bird alipofika kwenye ofisi ndogo za Mfuko huo jijini Dar es Salaam kuagana na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (hayupo pichani ) wakati alipofika katika taasisi hiyo kuagana nao baada ya kumaliza muda wake nchini.


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bw.Ladislaus Mwamanga (aliyevaa tai) akimwongoza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake bi. Bella Bird kuingia katika ukumbi wa mikutano wa TASAF katika ofisi ndogo jijini Dar es Salaam.


Na Estom Sanga- TASAF- DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake Bi.Bella Bird amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF- kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kukabiliana na umaskini nchini.

Bi.Bella Bird amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa katika azma ya kuwaondolea wananchi wake kero ya umaskini jambo ambalo amesema limeijengea heshima kubwa serikali na hivyo kufanya mataifa mengine hususani ya bara la Afrika kuwavutiwa nayo.

Mkurugenzi Mkazi huyo wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake ameyasema hayo alipokutana na Wafanyakazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- katika Ofisi ndogo ya Mfuko huo jijini Dar es salaam ambako alikwenda kuagana nao baada ya kumaliza kipindi chake cha takribani CHA utumishi wa miaka minne hapa nchini.

‘’ mataifa mengine ya Afrika yamekuwa yakija Tanzania kujifunza namna TASAF ilivyofanikiwa kuwafikia watu maskini kabisa kupitia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Maskini’’ amesisitiza Bi. Bella Bird.

Amesema tafiti huru za ndani na nje ya nchini zilizofanywa zinaonyesha kuwa umaskini nchini Tanzania umepungua katika kipindi cha utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kuwa kinachotakiwa sasa ni kuhakikisha kuwa mafanikio hayo yanalindwa, kuboreshwa na kuendelezwa.

Bi.Bella Bird amesisitiza kuwa Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza kuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia TASAF ni miongoni mwa miradi hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira yaliyosaidia Benki ya Dunia kukubali kufadhili shughuli za Mpango was Kunusuru Kaya Maskini.

Bwana Mwamanga amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ya sehemu ya kwanza yamewezesha Serikali kukubali kutekeleza sehemu ya pili ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli baadaye mwezi ujao.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ameahidi kuwa taasisi hiyo imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa sehemu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali huku Mkazo ukiwekwa katika kuwashirikisha Walengwa katika kutekeleza miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira kama sehemu ya kuwaongezea kipato .

Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ulianzishwa na Serikali kwa lengo la kusaidia wananchi kupitia utaratibu wa Kaya Maskini sana ili ziweze kujikimu kwa kupata mahitaji muhimu yakiwemo lishe, elimu na afya huku mkazo ukiwekwa katika kuziwezesha kaya za Walengwa kutumia sehemu ya ruzuku kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji mali ili kuinua kipato chao na kuboresha maisha yao.

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI NA KUWAAPISHA MABALOZI WATEULE 4 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM. JANUARI 14, 2020

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu  jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Balozi mteule Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini. Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini. Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Balozi mteule Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Namibia. Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo ya Mhe. Balozi Dkt. Modestus Francis Kipilimba baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Namibia. Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Balozi mteule Prof. Emmanuel David Mwaluko Mbennah kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Mhe. Balozi Prof. Emmanuel David Mwaluko Mbennah mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Balozi mteule Dkt. Benson Alfred Bana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria. Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshuhudia Mhe. Balozi Dkt. Benson Alfred Bana akitia sahihi hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria. Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Mabalozi wapya  wakila kiapo cha maadili kwa watumishi wa Umma  mbele ya Kamshna wa Maadili Jaji Mstaafu Haroid Nsekela huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani)  akishuhudia mara baada ya kuwa apisha kuwaikilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa . Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mabalozi wapya  wakila kiapo cha maadili kwa watumishi wa Umma  mbele ya Kamshna wa Maadili Jaji Mstaafu Haroid Nsekela mara baada ya kuwa apisha kuwaikilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa . Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kuwaapisha Mabalozi wapya  wanne walioteuliwa kuwaikilisha Tanzania katika nchi mbalimbali walizopangiwa . Hafla iliyofanyika Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na  Mabalozi wapya wanne walioteuliwa kuwaikilisha Tanzania katika nchi mbalimbali walizopangiwa mara baada ya kuwaapisha Ikulu  Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya  wanne walioteuliwa kuwaikilisha Tanzania katika nchi mbalimbali walizopangiwa  mara baada ya kuwaapisha Ikulu Jijini Dar es salaam. Januari 14, 2020
Picha na Ikulu

MBEZI BEACH SEKONDARI: BADO TUPO KATIKA KIWANGO BORA CHA UFUNDISHAJI

$
0
0

Na Mwandishi Wetu

Uongozi wa Shule ya Mbezi Beach Secondary, Dar es Salaam, umesema hatua ya shule hiyo kupata alama mbili tu za daraja ziro (0), wakati zikiwa zipo shule nyingine ambazo zimepata hadi ziro 75, katika matokeo ya Mitihani ya Kidato cha nne ya mwaka huu, ni ishara kwamba shule hiyo bado ipo kwenye kiwango bora cha ufundishaji.


Akizungumza na baadhi ya wazazi wa wanafunzi, Meneja wa shule hiyo Dk. Prosper Kiramuu Mbowe, amesema, licha ya kuwa katika matokeo hayo shule imepata wanafunzi wawili wa daraja 0 lakini inajivuna kwamba imeweza kupata ufaulu wa wanafunzi kumi katika daraja la kwanza na kupata 49 daraja la pili, 68 daraja la tatu na 81 wa daraja la nne.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania, miongoni mwa shule zilizopata daraja ziro nyingi ni pamoja na Jitegemee iliyopata ziro 75, Azania ambayo imepata ziro 26, Green Acres ziro 18, Africana ziro nane, Makongo ziro saba, Jordan ziro 9 na Kawe Ukwamani ziro 39.


Akitangaza matokeo ya upimaji kitaifa darasa la nne, kidato cha pili na cha nne ya mitihani iliyofanyika Novemba 2019. Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Dk. Charles Msonde, alisema kwa upande wa matokeo ya kidato cha nne ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.4 kutoka ule wa mwaka 2018, lakini karibu nusu au asilimia 48.6 ya watahiniwa wote wa mwaka 2019 wamepata daraja la nne. 

"Ni kweli mitihani ya mwaka 2019 ilikuwa na ushindani mkubwa, lakini kutokana na shule yetu kuwa na walimu hodari tumeweza kupata ufaulu wa kuridhisha, tukijilinganisha na shule kadhaa ambazo wakati sisi tuna divisheni ziro mbili wenzetu wamefika hadi ziro 75",

Sisi lengo letu ni kuhakikisha shule yetu inatoa kiwango bora cha elimu kwa watoto na uwezo wa kufanya hivyo tunao, jambo la msingi ni kwa ninyi wazazi na wananchi wengine kwa jumla kuendelea kutuamini na kutuunga mkono ili tuweze kutumiza azma hii ambayo pia ni muhimu kwa Taifa la Tanzania", alisema Dk. Prosper.

"Kama mnavyojua pamoja na kwamba lengo letu ni kutoa mchango wetu kwa taifa katika sekta ya elimu, lakini wapo watu ambao kwa kuhofu ushindani wakati mwingine hujaribu kutumia mbinu ovu hata kueneza uongo katika jamii kwa lengo la kuchafua na kushusha hadhi ya shule yetu, maana mkumbuke hizi shule zetu binafsi licha ya kwamba lengo kuu ni kutoa huduma lakini pia ni biashara", alisema Dk. Prosper.

Aliwaomba wazazi kuepuka kusikiliza maneno yanayoweza kutolewa na watu wasioitakia mema shule hiyo badala yake, wawe wanajipa muda wa kufuatilia kwa karibu kila jambo linalohusiana na shule hiyo kwa kuwa uongozi wa shule upo tayari wakati wote kutoa taarifa sahihi hasa kwa watu sahihi.

MAKAMU ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KIFO CHA MFALME WA OMAN

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo Katika Ofisi ya Ubalozi wa Oman Mikocheni Jijini Dar Es Salaam leo Januari 16,2020 kufuatia kifo cha Mfalme Qaboos bin Said wa Oman.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumfariji Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Ali Almahroqi alipofika kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Oman Mikocheni Jijini Dar Es alaam leo Januari 16,2020 kwa ajili ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Mfalme Qaboos bin Said.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Ali Almahroqi kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Oman Mikocheni Jijini Dar Es Salaam leo Januari 16,2020 baada ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Mfalme Qaboos bin Said.

TCRA yakabidhi Vifaa vya Tehama katika Shule za Sekondari Kilakala na Mzumbe

$
0
0
NaChalila Kibuda,Globu ya Jamii Morogoro

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa vifaa vya Teknolojia ya Habari Mawasiliano (Tehama) na komputa 20 kwa shule za Sekondari Mzumbe pamoja na Kilakala zilizopo Mkoa wa Morogoro.

Vifaa hivyo wamefunga pamoja na mashine ya kuchapia karatasi , Internet pamoja na Komputa 10 kwa kila shule hizo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Komputa na Vifaa vya Tehama katika shule hizo Mwakilishi wa Katibu wa Tawala Mkoa wa Morogoro Afisa Elimu wa Mkoa wa Morogoro Tullo Fundi amesema kuwa vifaa vilivyotolewa lazima vitunzwe na kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi kujua Tehama.

Amesema kuwa TCRA imetambua umuhimu wa Tehama na kuamua kutoa Komputa ambapo kwa Dunia ya sasa Tehama haipukiki.

Fundi amesema kuwa shule za sekondari Mzumbe na Kilakala zimepata vifaa hivyo kutokana na kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne kitaifa hivyo juhudi zinahitajika kuendelea kufanya vizuri.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ,Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema amesema Mamlaka imekuwa na utaratibu wa kutoa vifaa vya Tehama kwa shule zinazofanya vizuri kitaifa kwa matokeo ya kidato cha nne ambapo kwa Kanda ya Mashariki shule hizo ziko tano.

Mhandisi Odiero amesema vifaa hivyo wamevitoa ni pamoja na matumizi salama ya mtandao."Ninaamini vifaa hivi mtatumia na kusaidia maendeleo ya shule kuendelea kufanya vizuri zaidi ikiwa ni kupata wataalam wa Tehama kutokana na kuwekewa msingi ya huduma hiyo"amesema Odiero .

Nae Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala mkoani Morogoro Mildreda Selula amesema watatuza vifaa hivyo na kuongeza ufanisi katika somo la Komputa.

Amesema kuwa wataendelea kuongeza juhudi zaidi katika usimamizi wa kuendelea kufanya vizuri.Makamu Mkuu Shule ya Sekondari Mzumbe Edwin Matenga amesema TCRA imeongeza nguvu kwa kuwapa vifaa vya Tehama na kuandaa wataalam katika sekta hiyo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kilakala wakiwa katika chumba cha Tehama

 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero  (mwenye miwani )akimkabidhi  moja ya Komputa 10 na Vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilakala  Mkoani wa Morogoro , Mildreda Selula katika hafla uliofanyika Shule ya hiyo
 Picha ya Pamoja kati ya TCRA na Watendaji wa Mkoa wa Morogoro na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mzumbe
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero  (mwenye miwani )akimkamkabidhi  moja ya Komputa 10 na Vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro ,Afisa Taaluma wa Mkoa Huo Tullo Fundi katika hafla uliofanyika Shule ya Sekondari Kilakala mkoani Morogoro katikati anayeshuhudia mwenye suti ni Makamu Mkuu wa Wa Shule hiyo Mildreda Selula (katikati)
 Picha ya Pamoja Watendaji wa TCRA na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kilakala na Watendaji wa Mkoa wa Morogoro. 
 Afisa Mwandamizi wa Tehama wa TCRA Thuwayba Hussein akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kilakala Fatuma Jadi mara baada ya kujibu changamsha bongo wakati TCRA ilipokwenda kukabidhi Vifaa vya Tehama katika Shule hiyo.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero  (mwenye miwani )akimkamkabidhi  moja ya Komputa 10 na Vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro ,Afisa Taaluma wa Mkoa Huo Tullo Fundi katika hafla uliofanyika Shule ya Sekondari Mzumbe katikati anayeshuhudia mwenye suti ni Makamu Mkuu wa Wa Shule hiyo Edwin Matenga.

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA 'CHANJA, LIPA, SEPA' NA TEMBOCARDVISA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif akifanya malipo kwa kutumia  huduma ya “Chanja, Lipa, Sepa” ya Benki ya CRDB kwa kutumia TemboCardVisa, baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika leo kwenye Duka la Miniso, Mlimani City, jijini Dar es salaam. Benki ya CRDB imezindua rasmi huduma ya “Chanja, Lipa, Sepa” kwa maduka yote yanayokubali malipo ya kadi, ambapo wateja watakao fanya malipo kwa TemboCardVisa na  SimBankingVisa wataweza kufurahia punguzo la bei hadi asilimia 60 kwa manunuzi ya kuanzia shilingi 30,000 katika maduka na migahawa mbalimbali hapa nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ijulikanayo kama “Chanja, Lipa, Sepa” uliofanyika leo kwenye maduka ya GSM na Miniso, yaliyopo Mlimani City, jijini Dar es salaam.
Meneja wa Mahusiano na Huduma za Uwakala wa Benki ya CRDB, Fadhil Mollel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ijulikanayo kama “Chanja, Lipa, Sepa” uliofanyika leo kwenye maduka ya GSM na Miniso, yaliyopo Mlimani City, jijini Dar es salaam.

UFAFANUZI KUHUSU KINYWAJI CHA UKWAJU KINACHODAIWA KUWA NA KEMIKALI YA BENZENE

SAYONA DRINKS LIMITED YAINGIZA KINYWAJI CHA ‘ TWIST’ SOKONI

$
0
0

Balozi wa Kinywaji cha SayonaTwist, Rajabu Abdul Kahali almaarufu, Harmonize akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji cha Sayona Twist uliofanyika Januari 15,2020 jijini Dar es salaam. Pamoja nae kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Motisun Group, Subhash Patel na wengine ni viongozi kutoka Sayona Group.
Balozi wa Kinywaji cha Sayona Twist, Rajabu Abdul Kahali almaarufu, Harmonize akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji cha Sayona Twist uliofanyika  Januari 15,2020 jijini Dar es salaam. Pamoja nae kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Motisun Group Veer Patel, Mwenyekiti wa bodi ya Motisun Group, Subhash Patel, Mkurugenzi Mtendaji wa Sayona Drinks Limited, Pawan Patel, Mkurugenzi Mkuu wa Sayona Group, Nitin Menon na Meneja wa Harmonize, Sebastian Ndege maarufu kama Jembe ni Jembe.

Mwenyekiti wa bodi ya Motisun Group, Suhbash Patel (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji cha Sayona Twist uliofanyika jijini Dar es salaam  Januari 15,2020. Pamoja nae kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Motisun Group Veer Patel na Balozi wa Kinywaji cha SayonaTwist, Rajabu Abdul Kahali almaarufu, Harmonize.
Balozi wa Kinywaji cha Sayona Twist, Rajabu Abdul Kahali almaarufu, Harmonize akinywa kinywaji kipya cha Sayona Twist wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanyika Januari 15,2020 jijini Dar es salaam. Pamoja nae kushoto ni viongozi kutoka Motisun Group.
 
Wateja wa vinywaji vya Sayona, sasa watakuwa na fahari ya kuchagua zaidi baada ya kampuni inayotengeneza vinywaji baridi ambayo inakuwa kwa kasi jijini Dar es salaam, Sayona Drinks Limited kuboresha na kuzindua upya kinywaji kinachofahamika kwa jina la TWIST.

Kampuni ya Sayona imedhamiria kuwapa machaguo mengi zaidi wateja wake ili kukidhi hitaji za ladha mbalimbali zinazopendwa na wateja.

Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa bidhaa hiyo, Pawan Patel, Mkurugenzi Mtendaji wa Sayona Drinks Limited alisema, “Twist ni kiburudisho chenye ladha nzuri, kinachokupa thamani ya pesa yako. Twist inakuja na ladha saba za kipekee ikiwemo ya pasheni, chungwa, limao, embe, nanasi, tangawizi na ladha ya Cola,”

Pia amebainisha kuwa Kampuni itatangaza ujio wa ladha nyingine za kipekee katika siku za usoni. Aliongeza kuwa, Sayona, imedhamiria kukidhi hitaji la wateja wake ndiyo maana wameendelea kuwa wabunifu na kila mwaka wamekuwa wakitambulisha bidhaa mpya sokoni.

“Tunaamini kupitia Twist, tunayo bidhaa bora ambayo ina utofauti na bidhaa nyingine zilizopo sokoni, kuwapa wateja wetu kiburudisho chenye ladha nzuri na ya kipekee,"alisema.

Kwa upande wake, Nitin Menon, Mkurugenzi Mkuu wa Sayona Drinks Ltd Group yeye alizungumzia juu ya utoaji wao huduma kwa wateja na gharama za bidhaa hii mpya.

Menon alisema, hatua ya kuizindua Twist ni matokeo ya kazi kubwa inayofanyika ya kuimarisha ukuaji wa kampuni kupitia mkakati kabambe ambao unaenda sambamba na badiliko la ladha kwa watumiaji na tabia katika ununuzi.

“Bidhaa yetu mpya ya Twist inakuja kwa ujazo wa milimita 300 na 400 katika chupa ya plastiki. Bidhaa itauzwa kwa bei ya rejareja ya shilingi 500 na itapatikana nchi nzima,” aliongeza.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuutangazia umma kuwa, wameingia makubaliano na staa wa bongo fleva, Rajabu Abdul Kahali (Harmonize) kuwa balozi wa heshima wa bidhaa za Sayona, ambaye pia alishiriki katika uzinduzi huo.

“Tunajisika fahari kuwa na Harmonize kama balozi wa heshima wa bidhaa yetu. Ni miongoni mwa vijana wapambanaji, mwenye msaada kwa watanzania wengi, anayefanya kazi kwa bidii, lakini pia amekuwa na chachu ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbali zaidi. Hili ni Jambo ambalo linaunga mkono malengo na maono yetu ya kuwa kinara katika biashara ya vinywaji baridi barani Afrika,” alisema Menon.

“Tuna imani kwamba ushirikiano huu utawezesha vinywaji vya Sayona kuwa miongoni mwa bidhaa zenye nguvu zaidi Tanzania. Harmonize atatusaidia kuwafikia walengwa wetu nchini Tanzania na sisi kufanya naye kazi kama balozi, ni miongoni mwa hatua muhimu ya yeye kushiriki katika miradi yetu mingi inayokuja.”

Kwa upande wa Harmonize, alisema ni jambo la faraja kufanya kazi na Sayona Drinks Limited na huu ni mwanzo wa ushirikiano mzuri zaidi baina yake na kampuni.

Akizungumzia juu ya uzinduzi wa bidhaa hiyo, Harmonize amesema, “Twist ni kinywaji kizuri chenye ladha za kipekee. Nimekuwa nikikitumia mara kwa mara na nimekuwa sehemu ya ubunifu huu mpya wa bidhaa hii, nina hakika kuwa Watanzania watafurahia bidhaa hii na matumizi yake yatafika nje ya Tanzania. Pia ninajisikia fahari sana kujumuishwa ndani ya Sayona Group ambao wamekuwa na sifa kubwa ya ubora wa bidhaa zao,” alimalizia.

OPEC YARIDHISHWA NA MIRADI YA TASAF KATIKA KUKABILIANA NA UMASKINI NCHINI.

$
0
0
 
 Picha ya juu na chini ni baadhi ya majengo yaliyojengwa na serikali kupitia TASAF kwa ufadhili  wa OPEC katika kijiji cha Oldonyowas mkoani Arusha.
 Na hapa sasa ni zawadi kutoka kwa wenyeji wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (kushoto ) akiangalia zawadi iliyotolewa na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha kwa Ofisa Mwandamizi wa OPEC Bwana Shams (katikati) baada ya kukagua miradi inayotekelezwa kwa ufadhili wa OPEC katika halmashauri hiyo.

 Majengo yaliyojengwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC kupitia mradi wa kupunguza umaskini katika kijiji cha Oldonyowas Mkoani Arusha.
 Afisa Mwandamizi kutoka OPEC (aliyevaa t-shirt)  Bw.Sharagim Shams akiwa na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha na maafisa kutoka wizara ya fedha na TASAF katika picha ya pamoja mbele ya mojawapo ya majengo yaliyojengwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC katika kijiji cha Oldonyowas mkoani Arusha.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari katika kijiji cha Oldonyowas mkoani Arusha wakiwa mbele ya majengo yaliyojengwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC. Chini ni viongozi wa TASAF, halmashauri ya wilaya ya Arusha wakimsikiliza Afisa Mwanadamizi kutoka OPEC wakati wa ukaguzi wa majengo yaliyojengwa kwa ufadhili wa opec.


NA Estom Sanga- Arusha

Utekelezaji wa miradi ya kuondoa umaskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF-unaofadhiliwa na Umoja wa nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi Duniani- OPEC umepunguza kwa kiwango kikubwa adha ya watoto kwenda umbali mrefu kufuata huduma ya elimu katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Arusha.

Wakitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa ujumbe wa Wataalamu kutoka OPEC, Wizara ya Fedha na TASAF, wakazi wa kijiji cha Oldonyowas ambao wamenufaika na miradi hiyo, wamesema ujenzi wa miradi hiyo umeleta hamasa ya kupambana na umaskin na kuhamasisha wananchi kuwapeleka watoto wao shule.

Kupitia utaratibu wa ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa kuwashirikisha wananchi , Serikali kupitia TASAF kwa ufadhili wa OPEC imeweza kutatua tatizo lililokuwa linawakabili wakazi wa kijiji cha Oldonyowas la uhaba wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, mabweni ya wanafunzi na matundu ya vyoo katika shule ya sekondari kijijini hapo.

Mafanikio hayo yameelezwa na uongozi wa kijiji hicho kuwa yameleta mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu ambayo kabla ya ujenzi wake haikuwa rahisi kwa watoto wa maeneo hayo kupata elimu ya sekondari kutokana na umbali wa kupatikana kwa huduma hiyo.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF pia umewezesha kupatikana kwa samani kwenye shule hiyo yakiwemo madawati, viti na meza na hivyo kusaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la uhaba wa vifaa shuleni hapo na hivyo kuongeza ari ya walimu na wanafunzi katika masomo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amepongeza namna wananchi wa maeneo hayo walivyoitikia mwito wa serikali wa kushiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo jambo ambalo amesema limesaidia kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na ufanisi mkubwa.

Bwana Mwamanga pia ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuruhusu utekelezaji wa sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF, hatua ambayo amesema italeta mchango muhimu katika mapambano dhidi ya umaskini kama ambavyo ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 inavyoelekeza.

Kwa upande wake, mmoja wa maafisi waandamizi wa OPEC, Bwana Sharagim Shams amesema utekelezaji wa miradi ya TASAF ni ya kiwango kizuri hali iliyosababisha Umoja huo kukubali kuendelea kufadhili miradi ya kupunguza umaskini na kuboresha miundombinu hususani ya elimu nchini.

‘’nimevutiwa sana na namna ubora wa miradi tunayoifadhili ulivyo, tutaendelea kufanyakazi na serikali ya Tanzania kupitia TASAF’’ amesisitiza Bwana Sharagim Shams.

Amewashauri Walengwa wa TASAF na wananchi wengine kutumia vizuri fursa hiyo hususani kwa kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata elimu kwenye shule zinazojengwa na TASAF kwa ufadhili wa OPEC ili kujenga raslimali watu iliyoelimika kwa siku zijazo. 


Miradi inayofadhiliwa na OPEC kupitia TASAF inatekelezwa katika mikoa ya Njombe na Arusha . Miradi kama hiyo imekwishatekelezwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara nakiwa na lengo kuuu la kusaidia jitihada za wananchi na serikali kutatua changamoto za maendeleo ya wananchi na miradi ambayo huibuliwa na wananchi wenyewe.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live


Latest Images