Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ZANZIBAR

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikata utepe, wakati akizindua huduma ya afya ya kijiji, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kusini, Kizimkazi Dimbani, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu Zanzibar. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe kuzindua huduma ya (ULTRA SOUND), baada ya kuzindua huduma ya afya ya kijiji, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kusini, Kizimkazi Dimbani, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu Zanzibar. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia mashine ya kupimia uzito, kwenye kituo cha afya cha Kizimkazi Dimbani, baada ya kuzindua huduma ya afya ya kijiji, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kusini, Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Watumishi, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib, Unguja, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu Zanzibar. Januari 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  

VIFURUSHI VYA BIMA YA AFYA VITABORESHA HUDUMA NHIF

0
0

 
MKURUGENZI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga akizungumza wakati wa kikao cha Mfuko huo na Waandishi wa Habari mkoani Tanga
 
Meneja wa Masoko na Huduma Kwa Wateja (NHIF) Hipoliti Lello akiwasilisha mada kuhusu mkakati wa kupanua wigo wa wanachama wa NHIF wakati wa kikao hicho
 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga Ally Mwakababu kushoto akisistiza jambo katikati ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Anjela Mziray na anayefuatilia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini Benard Konga

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga Ally Mwakababu kushoto akiwa na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Anjela Mziray

 
Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini Benard Konga akisisitiza jambo kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama Christopher Mapunda kushoto ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Anjela Mziray na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
 
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Mkoani Arusha Isaya Shekifu

Dinna Mlwilo wa NHIF Tanga akifuatilia matukio mbalimbali kwenye kikao hicho

Maafisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiwa kwenye kikao hicho

Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye kikao hicho katika aliyevaa suti ni Dege Masoli wa Nipashe
 
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Mkoani Tanga Amina Omari akiuliza swali kwenye kikao hicho

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (Tanga Press Club) Hassani Hashim akiuliza swali kwenye kikao hicho

Mwandishi wa Gazeti la Majira mkoani Tanga Mashaka Mhando akiulizwa swali katika kikao hicho

Mwandishi wa Gazeti la Majira wilayani Korogwe Yusuph Mussa akizungumza wakati wa kikao hicho



MKURUGENZI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) Benard Konga amesema kwamba mfumo wa vifurushi vya bima ya afya hautakwenda kuua mfuko huo bali utakuwa ndio chanzo kingine cha mapato hatua itakayowasaidia kuboresha huduma zao kwa wanachama.

Konga aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Waandishi wa Habari mkoani Tanga kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo alisema kwamba vitakuwa na manufaa makubwa kwa watanzania.

Alisema kwamba mfumo wa bima ya Afya ni muhimu sana kwa watanzania kwa ajili ya kupata matibabu wakati wanapougua hivyo ni muhimu kuhakikisha wanajiunga na mpango wa vifurushi ambayo vitakuwa msaada mkubwa sana kwao na jamii zinazowazunguka.

Kauli hiyo ya Mkurugenzi huyo inatokana na swali aliloulizwa na Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Mkoani Tanga Mashaka Mhando ambaye alieleza kwamba mfumo huo wa vifurushi utakwenda kuua mfumo huo.

Akijibu swali hilo Mkurugenzi huyo aliwatoa hofu watanzania na kueleza kwamba uwepo wa mfumo huo wa vifurusi utakuwa chachu kubwa ndani ya mfuko huo kwa sababu unakwenda kuongeza chanzo kingine cha mapato na hivyo kusaidia kuboresha huduma wanazozitoa kwa wanachama wao.

“Ninaamini kwamba mfumo huo wa vifuriushi utaleta wanachama wengi wanakaoleta michango itakayowezesha mfuko kutekeleza majukumu yake vizuri ikiwemo kuwahudumia wanachama hao hivyo una faida kubwa sana “Alisema Mkurugenzi huyo.

Hata hivyo alisema kwamba kuhusu watanzania kumudu gharama mfuko huo alieleza wameangalia mazingira halisi ya kipato cha mtanzania na kubaini wanaweza kumudu gharama hizo kutokana utafiti walioufanya.

“Lakini niulize kwamba wana habari hapa simu mnazomiliki hapa ukiangalia ni za bei juu sana na tunachangia masherehe tutoke huko tutambue kwamba uwekezaji kwenye afya zetu kwa manufaa yetu sisi wenyewe na Mwenyekitk wangu amekuwa akisema suala hilo sio siasa hivyo tuweke siasa pembeni tujiunge na mfuko huo”Alisema Mkurugenzi huyo.

Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Meneja wa Masoko na Huduma Kwa Wateja (NHIF) Hipoliti Lello alisema kwamba licha ya kuongeza magonjwa ya yasiyoambukiza na matatibu yake kuwa ya juu lakini bado wananchi wengi hawajapata mwamko wa kujiunga na Bima ya Afya.

“Akitolea mfano wastani wa matibabu ya mgonjwa mmoja wa Kansa kwa mwaka mmoja anatumia zaidi ya milioni 69 kwa ajili ya matibabu na kwa upande wa mgonjwa wa figo anatumia milioni 35 kwa mwaka huku mgonjwa wa moyo akitumia zaidi ya milioni 12.5 kwa mwaka kulingana na gharama hizo ifike wakati watanzania waone umuhimu wa kujiunga na bima ya Afya waweze kupata uhakika wa matibabu”Alisema 

Alisema kuwa ili kujihakikisha huduma bora za matibabu ni muhimu watanzania wakaama na kujiunga na mfuko huo kwani kutokana na maboresho ya sekta ya afya kwa sasa matibabu lazima yatakuwa na gharama.

Awali akizungumza katika kikao hicho Mweka hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Tanga (Tanga Press Club) Gift Kika aliushukuru mfuko kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu kwa wana habari kwani wanadhamana kubwa ya kuelimisha wananchi umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.

TANZANIA YATANGAZA UTALII UHOLANZI

0
0
Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi na wadau wengine; Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) pamoja na makampuni binafsi kama vile, Sea-Cliff Resort & Spa Ltd, Natures Land Safari’s & Rentals na Mbalageti Safari wanashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Utalii (Holiday Fair 2020) yanayofanyika katika mji wa Utretch, Uholanzi kuanzia tarehe 16 hadi 19 Januari 2020. 

Hii ni fursa nyingine muhimu kwa Tanzania kujitangaza na kuzidi kuvutia wadau zaidi katika Sekta ya Utalii, kuja kutembelea na kufanya biashara na Tanzania. Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene F. M. Kasyanju tayari amekutana na wadau wote waliofika Uholanzi, kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika ipasavyo na maonesho hayo.

Maonesho hayo ambayo kwa lugha ya kidachi yanajulikana kama “Vakantiebeurs 2020” hufanyika mwezi Januari kila mwaka na yanahudhuriwa na mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kutangaza na kuuza vivutio vya Utalii na Burudani 
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wawakilishi wa taasisi za Tanzania wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Utalii nchini Uholanzi. Kutoka kushoto ni Bw. Michael Christian Makombe kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bibi Alistidia Karaze kutoka Bodi ya Utalii Tanzania na Bw. Gerald Mono kutoka TANAPA. 
Balozi Irene Kasyanju ( wa pili kulia) akiwa na wawakilishi wa TTB na Kampuni ya MAKASA Safaris kutoka Moshi, Kilimanjaro. 
Balozi Irene Kasyanju akipokea zawadi ya Kalenda za 2020 kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Maonesho hayo, Bibi Alistidia Karaze ambaye ni Afisa Mkuu wa Utafiti na Maendeleo kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). 
Balozi Kasyanju akiwa na wawakilishi kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, TTB, TANAPA; pamoja na Kampuni binafsi yaani, Nature’s Land Safaris & Rentals; na Mbalageti Safari zote kutoka Mwanza, Tanzania na Sea-cliff ya Dar es Salaam. 

Benki Ya Exim Yatoa Msaada Wa Taulo Za Kike Kwa Wanafunzi WaSekondari Mkoani Iringa

0
0
Meneja wa Benki ya Exim tawi la mkoa wa Iringa, Bw Michael Richard (Katikati) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa Mlezi wa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Ruaha iliyopo mkoani humo Bi. Fatuma Tembo (kushoto kwake) ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares. Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Meneja wa Benki ya Exim tawi la mkoa wa Iringa, Bw Michael Richard (Katikati) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa Mlezi wa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Ruaha iliyopo mkoani humo Bi. Fatuma Tembo (kushoto kwake) ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares. Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo pamoja na muwakilishi wa wanafunzi wa shule hiyo.
Maofisa wa Benki ya Exim tawi la mkoa wa Iringa, wakiongozwa na Meneja wa Tawi la benki hiyo mkoani humo Bw Michael Richard (Katikati) wakifurahi pamoja na wanafunzi Shule ya Sekondari ya Ruaha iliyopo mkoani humo baada ya kukabidhi msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi hao ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares.
Maofisa wa Benki ya Exim tawi la mkoa wa Iringa, wakiongozwa na Meneja wa Tawi la benki hiyo mkoani humo Bw Michael Richard (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi Shule ya Sekondari ya Ruaha iliyopo mkoani humo baada ya kukabidhi msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi hao ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares.

Vodacom Tanzania Plc yamzawadia shilingi Milioni 150 mshindi shindano la TUSUA MAPENE

0
0
 Mkurugenzi wa kitengo cha dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania Plc, Nguvu Kamanda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye  thamani ya shilingi 150,000,000/- mshindi wa shindano la TUSUA MAPENE na Vodacom , Eveneth Rutiyomba ambaye ni fundi cherehani  mkazi wa Kimara Bucha , hafla ya makabidhiano ilifanyika Kimara jijini Dar Es Salaam jana. Pichani katikati ni Afisa wa Huduma za Ziada Vodacom, Paulina Bisheko.
 Mkurugenzi wa kitengo cha dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania Plc, Nguvu Kamanda (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa shindano la TUSUA MAPENE, Eveneth Rutiyomba (kulia) pamoja na wazazi wake, John Ndebisa na Fasness Ndebisa


DCC TABORA YAPITISHA MAPENDEKEZO YA BAJETI YA BILIONI 52 YA MWAKA UJAO

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala ( wa pili kutoka kushoto) akisisitiza jambo jana wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Manispaa ya Tabora (DCC) cha kupitia makisio ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya shilingi bilioni 52 kwa ajili ya mwaka wa fedha ujao wa fedha. 
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Manispaa ya Tabora (DCC) wakiwa katika kikao cha kupitia makisio ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya shilingi bilioni 52 kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha. 
Picha na Tiganya Vincent 


NA TIGANYA VINCENT 

WAJUMBE wa Kamati ya Ushauri ya Manispaa ya Tabora (DCC) wamepitisha makisio ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya shilingi bilioni 52 kwa ajili ya mwaka wa fedha ujao wa fedha. 

Wajumbe hao walipitisha mapendekezo hayo jana baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru kuwasilisha wakati wa kikao kupitia mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2020/21. 

Alisema katika mapendekezo hayo wanatarajiwa kukusanya shilingi bilioni 4.7 kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ikiwa ni ongezeko la asilimia moja ukilinganisha na masikio ya mwaka 2019/20 ya kukusanya bilioni 4.6. 

Ndunguru alisema kwa upande wa Serikali Kuu na kwa wahisani wanatarajia kupata jumla shilingi bilioni 48 ikiwa ni ongezeko la asilimia 25 ukilinganisha na bilioni 38.2 ya mwaka 2019/20. 

Alivitaja vipaumbele vya bajeti ijayo kuwa ni uendelezaji wa jengo la utawala ambalo limetengewa milioni 200, kutenga fedha milioni 70 kwa ajili ya ununuzi wa ardhi ekari 140 za uwekezaji. 

Nduguru aliongeza kuwa vipaumbele vingine ni kutenga milioni 50 kwa ajili ya fidia kwa wananchi ili kutatua migogoro, milioni 84 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari na ununuzi wa taulo kwa ajili ya wanafunzi wa kike na milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mbili za Kidato cha Tano na Sita. 

Aliongeza kuwa kiasi cha milioni 445 kinatarajiwa kutolewa kama mikopo ya vikundi vya vijana , wanawake na walemavu na milioni 117 zimetengwa kwa ajili ya shughuli za lishe. 

Ndunguru alisema kwa upande wa miradi wamependekeza shilingi milioni 580 zitumike katika miradi ya maendeleo kwenye Kata 29 za Manispaa ya Tabora na bilioni 1 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Halmashauri hiyo

Benki Ya Exim Na Matawi Yake Nje Ya Nchi Yashinda Tuzo Muhimu Za Kimataifa

0
0
Benki ya Exim imekamilisha mwaka 2019 kwa kishindo! Ikiwa ni benki ya tano kwa ukubwa wa mali nchini Tanzania, Benki ya Exim imefanikiwa kutwaa idadi kubwa ya tuzo za kiufanisi katika sekta ya benki kutoka taasisi na mashirika mbalimbali ya kimataifa.

Wakati benki hiyo ikifanikiwa kutwaa tuzo ya 'Benki ya Bora ya Uwekezaji' nchini Tanzania kwa mwaka wa nne mfululizo kupitia tuzo za Global Banking and Finance Awards, pia huko nchini Djibouti benki hiyo kupitia tawi lake Benki ya Exim Djibouti ilifanikiwa kutwaa tuzo ya "Benki Bora ya Mwaka" kwa miaka mitatu mfululizo huku pia tawi la benki hiyo nchini Comoros, Benki ya Exim Comoros ikitwaa tuzo ya ‘Benki Bora ya Ubunifu’ kwa mwaka 2019.

Akizungumzia tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bwana Jaffari Matundu alisema, "Benki ya Exim inafurahi kutambuliwa kupitia tuzo hizi muhimu katika mwaka uliopita wa 2019. Lengo letu ni kuendesha ukuaji wa bara la Afrika huku tukitoa huduma za kifedha zenye suluhisho sahihi. Utambuzi huu unaadhihirisha namna ambavyo tumejitoa kuwa zaidi ya watoa huduma za kifedha. Sisi ni kichocheo cha mabadiliko ya uchumi katika nchi zote ambazo tunaendesha huduma zetu kwa kufanya biashara sahihi kwa njia sahihi.” alisema.

"Suala la ubunifu ndio kipaumbele cha benki yetu na tuzo hizi ni ushahidi tosha wa namna tunavyojizatiti katika kutafuta njia bora za kutoa majawabu ya huduma za kifedha mataifa yote tunayotoa huduma zetu,’’

Bwana Matundu alihitimisha kwa kubainisha kuwa mbali na kuhisi ufahari, tuzo hizo zimeongeza chachu kwa benki hiyo iweze kwenda mbele zaidi huku akiwaahidi wateja wa benki hiyo watarajie huduma bora zaidi kutoka benki ya Exim.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma atembelea duka la Vodacom kujionea zoezi la usajili wa laini kwa alama za vidole

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ,Patrobas Katambi (kulia) akijadiliana jambo na Meneja mauzo mwandamizi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati, Andrew Temu (kushoto) na Meneja wa masoko Vodacom Kanda ya kati ,Baraka Siwa alipotembelea Ofisi za Vodacom Kanda ya Kati zilizopo eneo la Kilimani Jijini Dodoma mwisho wa wiki, kuangalia zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole linavyoendelea
Meneja mauzo mwandamizi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati, Andrew Temu (kushoto) akimpa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (wapili toka kushoto) wakati alipotembelea duka la Kampuni hiyo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki kuangalia zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole linavyoendelea ambapo Serikali ilitangaza mwisho wa zoezi hilo ni tarehe 20 ya mwezi huu.

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KWA WALEMAVU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU UJAO

0
0
Shirika la Under The Same Sun kwa kushirikiana na mashirika wenza GNRC NA CEFA wamezindua mradi wa “HAKI YETU” awamu ya pili, ambao umelenga kupunguza ama kutokomeza kabisa matukio ya kikatili ambayo wamekuwa wakifanyiwa watu wenye ualbino.
Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo Januari 19, 2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na viongozi wa dini, ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimwakilisha mkuu wa mkoa Zainab Telack. 
Mboneko amesema Serikali inaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili mradi huo ufanikiwe kwa asilimia 100, pamoja na kutoa elimu ya kupinga matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino, kuwaimarishia ulinzi na usalama, kuwapatia hifadhi na elimu katika shule ya Buhangija Jumuishi, pamoja na kufanya msako kwa wale wote wanaotekeleza mauaji na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
 Amesema bado kuna maeneo mengi katika jamii hayajafikiwa na elimu juu ya uelewa kwa watu wenye ulbino, kwa kutambua hao ni sawa na binadamu wengine, ambacho kinachowatofautisha ni rangi, huku akiahidi Serikali pamoja na wadau watashirikiana kwa pamoja kusambaza elimu hiyo ambayo itapunguza ama kutokomeza matukio ya ukatili na ubaguzi kwa watu wenye ualbino.
 “Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutoa elimu ya kupinga ukatili wa mauaji ya watu wenye ualbino, kuimarisha ulinzi na usalama, kuwapa hifadhi, kufanya msako kwa wale wote wanaotekeleza mauaji dhidi yao ama kupanga njama, pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria,”amesema Mboneko. 
“Kutokana na jitihada hizi za kupinga matukio ya ukatili kwa watu wenye ualbino, katika mkoa wetu kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni hakuna tukio lolote lililotolewa taarifa linalohusu mauaji ya watu wenye ualbino, hivyo natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga wasiwafanye ukatili watu hawa pamoja na kuwabagua, “Natoa rai pia kwa wazazi na walezi kutowaficha watoto wenye ualbino, bali wawa patie haki zao kama walivyo watoto wengine, ikiwamo kuwapeleka shule, pamoja na kuwapenda,” ameeleza. 
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ameziagiza halmashauri zote sita za mkoa wa Shinyanga kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa mahitaji maalum ya watu wenye ualbino, pamoja na maofisa maendeleo kuwapatia elimu ya ujasiriamali na kuwaunga kwenye vikundi na kuwapa mikopo, ili wapate kufanya shughuli za kuwaingizia kipato.
 Naye meneja mradi wa ‘HAKI YETU’ kutoka Shirika la Under The Same Sun Wakyo Musongo, amesema mradi huo unatekelezwa katika mikoa mitano kwa kushirikiana na mashirika matatu ambayo ni Under The Same Sun, GNRC NA CEFA, mikoa ambayo ni Simiyu, Kigoma, Mwanza, Geita pamoja na Shinyanga.
 Amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Oktoba mwaka 2019, na sasa wameuzindua katika awamu ya pili mkoani Shinyanga ambapo utakoma Juni mwaka 2021, na utatekelezwa katika halmashauri ya Ushetu pamoja na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo watakuwa wakitoa elimu ya kupinga matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino. 
Aidha amesema katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya pili kupitia warsha, maonyesho ya sanaa sehemu za wazi, semina, na vyombo mbalimbali vya habari, wanatarajia kufikia watendaji wa serikali 450, viongozi wa dini 400, wanafunzi 30,000, walimu 500, wenye ualbino 250, wananchi 26,000 pamoja na kupitia vyombo vya habari matarajio yao ni kufikia watu 4,000,000. 
  


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Haki Yetu unaotekelezwa na shirika la "Under the same sun" kwa kushirikiana na mashirika ya GNRC na CEFA hapo jana katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa shirika la "Under the same sun" Bi. Berthasia Ladislaus na wengine ni wafanyakazi wa shirika hilo, kulia ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Afya Dkt. Rashid Mfaume na timu kutoka shirika hilo.Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akitoa neno la uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack Mkurugenzi wa shirika la Under the same sun Bi. Berthasia Ladislaus akitoa neno la shukrani kwa Mkoa wa Shinyanga mara baada ya uzinduzi wa mradi wa Haki YetuMeneja mradi wa Haki Yetu Bi. Wakyo Musong'o akitoa taarifa ya malengo ya mradi kabla ya uzinduzi wa mradi huo Baadhi ya washiriki wa uzinduzi huo wakifuatilia matukio yanayoendelea, chini ni watoto kutoka shule ya msingi Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga.(Picha zote na Marco Maduhu - Shinyanga)

KILIMANJARO MARATHON 2020 LAUNCHED IN KILIMANJARO

0
0
 The 18th edition of the prestigious Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2020 was launched at the Kibo Palace Homes, in Moshi, Kilimanjaro region, barely one and half months away. Speaking during the launching of the Marathon, the Kilimanjaro Regional Commissioner Anna Mgwira praised the sponsors and organisers led by the main sponsors of the event, Kilimanjaro Premium Lager-42 km,

 Tigo-21km Grand Malt-5km Fun Run and other water table sponsors for their contributions in uplifting Kilimanjaro Region through the yearly event that has gained popularity inside and outside the country. She praised Kilimanjaro Premium Lager for sponsoring the event for 18 years now and for among other things offering an additional Tsh. 5 million to encourage Tanzanians to do better, 

whereby the first Tanzanian male and female will receive an extra Tsh. 1.5 million each. She said that the regional administration would support the sponsors and organizers of the event with the intention of maintain the status of Kilimanjaro region as one of the leading tourists centres through the annual event.

 “May I take this opportunity to urge the ministry of natural resources and tourism to come and join forces with us in this event because it adds new tourists in the region and the country in general every year”, she said. She called upon business persons in the region to make good use of the event as a business opportunity because it attracts many potential buyers from different countries of the world and that this year is expected to draw participants from more than 50 countries worldwide.

 “Hotel owners and other business persons should start thinking of coming up with different business types of business packages which would attract tourists including those who will want to visit various tourists attractions a move which will generate more income”, she added. Speaking during the event, the Kilimanjaro Premium Lager Brand Manager, Pamela Kikuli, whose brand sponsors the 42 km race expressed her expectations that this year’s event would be better due to the excitement and awareness shown by different people concerning the event.

 “Tanzanians taking part in the full marathon should train harder so that most of the prizes can remain home,” she said, adding, the total prize money is Tsh. 23 million with the first male and female receiving Tsh. 4 million each while there is an additional Tsh 3 million to encourage Tanzanians to perform better. “There would be an extra Tsh. 1.5 million to both Tanzanian men and women who will finish first in the full marathon category”, she noted. 

 On his part, the Northern Zone Tigo Acting Zonal Director, Aidan Komba said they were proud to be the sponsors of the 21km race popularly known as the Tigo Half Marathon which will be part of the Kilimanjaro Marathon. 

 “We are excited to once again be part of this iconic road race that brings together elite athletes alongside people from all walks of life under the umbrella of celebrations through sports, fun, culture, tourism and healthy living,” he said. 

 "I urge participants to register and pay via Tigo Pesa services by dialing *149*20# in order to participate in the world-renowned 21km Tigo Half Marathon,” said Komba, adding, Tigo is partnering with other organizations to support the landmark event, which not only plays a huge part in promoting Tanzania’s tourism attractions to the worldwide community, but also brings together families and friends from all nations to create unforgettable memories. 

 Grand Malt Brand Manager, David Tarimo, said they were gearing towards a bigger 5km Fun Run and appealed to participants to register on time, whereby he assured the participants of Grand Malt drinks which he said would be available in the newly-launched 330 ml can.

 Other sponsors include Kilimanjaro Water, Barclays Bank, Simba Cement, TPC Sugar, Precision Air, Kibo Palace Hotel, Unilever, GardaWorld Security, Keys Hotel and CMC Automobiles.

 According to the Kili Marathon Local Race Director, John Bayo, registration was still going on through the race’s website he mentioned as www.kilimanjaromarathon .com as well as through Tigo Pesa services by dialing *149*20#, whereby he said the registration processes were expected to end on February 16, this year. 

 The Tanzania Revenue Authority (TRA) in Kilimanjaro region have expressed its intention in co-operating with the organizers of the Kilimanjaro Marathon event with the intention of ensuring its success.

 "We understand very well that apart from been a sports competition and entertainment, the event also plays a big role in improving the economy of the region through its participants who come inside and outside the country, that's why we have decided to be part of this event whereby this year, some of our members of staff have already registered as participants in different categories of the race", said Khaleed Mchumwa who is the Assistant TRA Regional Manager in Kilimanjaro region. 

 The Chairman of the Kilimanjaro Hotel Owners Jacob Tarimo, hailed the organizers of the event, which he said has been very valuable to their hotel businesses as well to other businesses within the region and the neighbouring Arusha region.

 “May I take this opportunity to urge the regional administration and other development stakeholders to look on ways to add two or three other annual or seasonal events a move which would help advertise and improve the economic wellbeing of Kilimanjaro region”, he said. 
 The Kilimanjaro Regional Commissioner Anna Mghwira(centre) cuts teh ribbon to officially launch the Kilimanjaro PPremium Lager Marathon 2020 in Moshi as sponsors and other invited guests look on.(1)
 The Kilimanjaro Regional Commissioner shaking hands with the Tigo acting Northern Zone Director, Aidan Komba(2)
 The Kilimanjaro Regional Commissioner Anna Mghwira shaking hands with the Kilimanjaro Premium Lager Brand Manager Pamela Kikuli
The Kilimanjaro Regional Commissioner shaking hands with the Grand Malt Brand Manager David Tarimo

Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha yaipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

0
0

Na Kassim Nyaki-NCAA

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Mhe. Zelothe Stephen Zelothe imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho katika hifadhi ya Ngorongoro.

Mwenyekiti wa CCM mkoani Arusha Mhe. Zelothe Stephen aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mrisho Gambo pamoja na wajumbe wa kamati hiyo mkoani Arusha ameeleza kuwa ziara hiyo imelenga kutembelea na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo hasa miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani na nje ya Hifadhi hiyo.

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro Dkt Freddy Manongi ameieleza kamati hiyo kuwa pamoja na utekelezaji wa malengo makuu matatu ya Uhifadhi, Utalii na maendeleo ya jamii, Mamlaka hiyo imeendelea pia kutoa msaada wa fedha kwa jamii katika miradi ya afya, elimu, maji, mifugo na chakula kwa wakazi wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo.

Dkt Manongi ameongeza kuwa katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli, katika mwaka wa fedha 2018//2019 Mamlaka hiyo imetoa kiasi cha shilingi milioni 500 ili kusaidia ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karatu, pia imetoa shilingi milioni 400 za ujenzi wa Hospitali ya Samunge iliyoko Loliondo, vilevile imechangia kiasi cha shilingi milioni 100 katika ujenzi wa kituo cha afya Arash kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongro.

Kamishna Manongi pia amebainisha kuwa takribani asilimia 47 ya mapato ya NCAA kwa kila mwaka zinaelekezwa kwenye shughuli nyingine za Kiserikali ikiwemo kutoa gawio Serikalini na kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo hasa ujenzi wa miundombinu na huduma za kijamii kama maji, elimu, ujenzi wa vituo vya afya, majosho, chanjo za mifugo na kusaidia vikundi vya ushirika vya wananchi ndani ya hifadhi hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuunga mkono juhudi kazi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ameileza kamati ya siasa mkoa wa Arusha kuwa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwa mdau mkubwa katika kuunga mkono juhudi za Serikali hasa katika kuchangia shughuli za maendeleo na kuupongeza uongozi wa mamlaka hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya.

 Kamishna wa Uhifadhi kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt Freddy Manongi (aliyesimama) akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Arusha.
 Kamati ya siasa mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mhe. Zelothe Stephen (kulia) wakisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.



 

MAFUNDI SIMU WATAKIWA KUULIZA HISTORIA YA SIMU KABLA YA KUTENGENEZA

0
0
 Mkuu wa Kanda ya mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na mafundi simu mkoa Morogoro kuhusina na umuhimu wa mafundi simu kuwa leseni.
 Afisa Mwandamizi wa Huduma za Leseni Mhandisi Kadaya Balyhye akitoa maelezo kuhusiana utaratibu wa leseni kwa mafundi zinazotolewa na mamlaka hiyo. 
 Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Simu Mkoa wa Morogoro Ipyana Haraba akitoa maelezo kuhusiana na mafundi siku kuwa leseni katika mkutano. 
Baadhi ya mafundi Simu wa mkoa wa Morogoro wakiwa katika mkutano uliohudhuriwa na Watendaji wa TCRA na Manispaa Morogoro. 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa Mafundi simu wote wanatakiwa kuwa leseni kutoka mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na weledi wa kazi wanazozifanya. 

Akizungumza na mafundi simu wa Manispaa ya Morogoro Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania , Mkuu wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa mafundi simu ni kazi nyeti hivyo lazima wawe na leseni kazi hiyo na kuendelea kutengeneza simu bila leseni ni kosa la jinai. 

Amesema kuwa mafundi simu hao wanatakiwa kupata leseni ikiwa ni kupatiwa mafunzo kwa TCRA kushirikiana na wadau ambao na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam. 

Odiero amesema mafundi simu wakiwa na mafunzo watakuwa ni watu kulinda usalama wa mawasiliano ikiwa ni kuweka utaratibu wa kuwa na vitabu vya kusajili simu na kuuliza simu historia ya kabla ya kutengeneza kwa wateja wao simu walikozitoa ili kuondoa wizi wa simu. 

“Hakuna sababu ya fundi simu kutengeneza simu ambayo mwisho wa siku taarifa za simu hazieleweki ndipo hapo mtu anaingia katika tatizo lisilomhusu lililotokana na kushindwa kuwa kutokuwa na taarifa za simu ya mteja”amesema Mhandisi Odiero. 

Aidha amesema kuwa kwa mafundi simu kuwa na umoja kutarahisisha TCRA kufanya mawasiliano kwa mafunzo ambayo yatakuwa yameandaliwa ya kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kuzingatia matumizi ya simu kutoka kwa wateja. 

Nae Afisa Mwandamizi wa Huduma za Leseni Ipyana Haraba amesema kuwa mafundi simu ni watenda kazi hivyo ushirikiano unahitajika kutambua wanaofanya nje ya utaratibu na sheria itashika mkondo wake. 

Mhandisi Baluhye amesema kuwa mafundi simu nchini wakisajiliwa ni fursa ambapo serikali iko katika uchumi wa viwanda hivyo kunaweza kutokea kiwanda cha simu au kuunganisha simu mafundi wataotumika ni wa ndani. 

Mwenyekiti wa Mafundi Simu Mkoa wa Morogoro Ipyana Haraba amesema wameweka mkakati wa wa mafundi simu wote wawe wamejisajili katika umoja huu kurahisisha utoaji huduma na mafunzo ya weledi yatakyotolewa na TCRA. 


Haraba amesema kuwa safari imeanza kwa mafundi simu kuweka utaratibu wa mazingira ya kufanya kazi na vyombo vingine ikiwemo jeshi la polisi kushiriana katika kubaini wezi wa simu. 

Vodacom kuwarejeshea huduma Wateja wake baada ya kujisajili

0
0

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania leo imetangaza kufunga huduma kwa Wateja wake 157,000 ambao wameshindwa kujisajili kwa kutumia alama za vidole.
Hatua hii inafuatia agizo la Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuyaagiza makampuni yote ya Simu nchini kuwafungia wateja ambao wameshindwa kusajili kwa kutumia alama za vidole (biometria) ifikapo Januari 20, 2020.

Akitangaza uamuzi huo leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC Hisham Hendi, amewaomba Wateja wote waliofungiwa laini zao kutembelea vituo vya huduma au mawakala wa kampuni hiyo zaidi ya 35,000 nchini kusaijili laini zao ili kuendelea kufurahia huduma za kampuni hiyo.

“Baadhi ya maduka yetu kwenye miji mikubwa yatakuwa wazi masaa 24  siku saba za wiki, ili kuhakikisha kwamba wateja wetu wote ambao wana vitambulisho vya Taifa wanasajiliwa na hivyo kuendelea kupata huduma za kampuni yetu ikiwa ni pamoja na huduma za M-Pesa,” alisema Hendi.

Aliongeza kwamba Wateja walioathiriwa na zoezi hili ni wale tu waliopokea namba za vitambulisho vya Taifa kutoka mamlaka ya vitambulisho hivyo (NIDA), lakini wameshindwa kujisajili kwa sababu moja au nyingine, “kwa kuwa zoezi hili ni endelevu, wateja wetu wote ambao hawajapata namba za utambulisho kutoka NIDA, waendelee na mchakato wa kupata namba hizo au vitambulisho  vitakavyowawezesha kujisajili kwa kutumia alama za vidole na kuepuka usumbufu wa kufungiwa huduma.”

 “Tukiwa ni kampuni iliyo orodheshwa kwenye soko la hisa nchini, tuna jukumu la kufuata sheria na taratibu zote zilizowekwa na serikali pamoja na vyombo vilivyo chini yake,” alisema Mkurugenzi.

Hendi aliongeza kwamba zoezi la usajili kwa alama za vidole litasaidia kupunguza idadi ya matapeli wanaosumbua wateja, “kusajili kwa biometria unatuhakikishia kwamba kila mmoja aliyesajili anajulikana kwa kutumia alama hizo, hii itarahisisha vyombo vya usalama kupambana na matukio hayo ya kitapeli,” alifafanua Hendi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Bi Harriet Lwakatare alisema “Wateja wanaweza kubofya namba *152*00# au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15096 ili kupata namba za vitambulisho vyao ambazo watazitumia kujisajili kwa alama za vidole. Kwa wale walioathiriwa na zoezi hili la kufungiwa wasiwe na wasiwasi kwa vile taarifa zao zitatunzwa kwa muda wa miezi sita ambapo wanatarajiwa wawe wamejisajili kwa alama za vidole.” 

“Wateja wote waliofungiwa wanaweza kupata huduma zetu za kidijitali  kupitia mitandao ya kijamii kupata taarifa za namna ya kuendelea au kukamilisha usajili,” alimalizia Bi Lwakatare.

Mwanzoni mwa mwaka jana, serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano nchini ilitoa maelekezo kwamba wamiliki wote wa laini za simu wasajiliwe upya kwa kutumia biometria (biometric registration), usajili kwa alama za vidole unatumiwa kama namna ya "kumjua mteja wako" [Know Your Customer (KYC)] na kudhibiti matapeli wanaotumia mitandao ya simu kutapeli watumiaji wa huduma za mawasiliano.



RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA MABALOZI WANAOWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI KATIKA SHEREHE ZA MWAKA MPYA 2020 (DILPOMATIC SHERRY PARTY) LEO IKULU JIJINI DAR

0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Waakilishi wa Mashirika ya kimataifa katika Sherehe za Mwaka mpya 2020 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakimsikiliza Rais Dkt John Pombe Magufuli katika Sherehe za Mwaka mpya 2020 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifuatlia jambo wakati wa sherehe za Mwaka mpya 2020 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kabla ya chakula cha jioni alichowaandalia Mabalozi hao katika Sherehe za Mwaka mpya 2020 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

T-MARC TANZANIA YATOA MSAADA WA DIAPERS ZA SMILEY HOSPITALI YA MWANANYAMALA, DAR ES SALAAM

0
0
Mmoja wa wanawake waliojifungua katika hospitali ya Mwananyamala, Rebecca Nelson akifurahia Diapers mpya za Smiley baada ya kukabidhiwa na balozi wa bidhaa hizo za T-MARC Tanzania, Dinah Marrios (kushoto),wengine pichani ni watumishi waandamizi wa hospitali hiyo na kutoka taasisi yak T-MARC.
Mkurugenzi wa bidhaa za kijamii wa T-MARC Tanzania , Flavian Ngole, (kulia) akikabidhi msaada wa diapers mpya za Smiley zilizozinduliwa katika soko nchini karibuni na T-MARC, kwa mzazi, Rebecca Nelson, katika wodi ya wazazi ya hospitali ya Mwananyamala jijiji Dar es Salaam, wakati wa hafla ya taasisi hiyo kukabidhi msaada wa bidhaa hizo hospitalini hapo , (katikati) ni Balozi wa Smiley , Dinah Marrios, wengine (kutoka kushoto) ni Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo , Dk.Mussa Wambura na Muuguzi Rosa Moses.
Wauguzi Waandamizi wa hospitali ya Mwananyamala wakipokea msaada wa Diapers za Smiley zlizozinduliwa hivi karibuni kutoka kwa Mkurugenzi wa bidhaa za kijamii wa T-MARC Tanzania, Flavian Ngole (kushoto) na balozi wa bidhaa hizo, Dinah Marrios.

TCAA YAWAJENGEA UWEZO KUPENDA SEKTA YA ANGA ZAIDI YA WANAFUNZI 600 WA SHULE ZA SEKONDARI MJINI TABORA

0
0
Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kituo cha Tabora Bw. Daniel Nyimbo akielezea jambo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo. Zaidi ya wanafunzi 600 kutoka shule ya sekondari Mirambo, Tabora Boys na Tabora Girls wameshiriki Warsha hiyo. Sehemu ya wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo wakisikiliza maelekezo kutoka kwa wataalamu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania. Mkufunzi Mkuu Kitengo cha huduma za viwanja vya ndege kutoka Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) kilichopo Dar es Salaam Bi.Thamarat Abeid akitoa ufafanuzi wa fursa za kimasomo katika chuo hicho pamoja na sifa za ujumla zinazohitajika ili kujiunga na masomo ya usafiri wa Anga kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo. Picha ya pamoja baada ya warsha. Wanafunzi wa shule ya sekondari Milambo wakijiandaa kushiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo. Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kituo cha Tabora Bw.Daniel Nyimbo akielezea jambo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Milambo walioshiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo. Mkufunzi Mkuu Kitengo cha huduma za viwanja vya ndege kutoka Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) kilichopo Dar es Salaam Bi.Thamarat Abeid akitoa ufafanuzi wa fursa za kimasomo katika chuo hicho pamoja na sifa za ujumla zinazohitajika ili kujiunga na masomo ya usafiri wa Anga kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo. Picha ya pamoja baada ya warsha. 

BALOZI IBUGE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI MBALIMBALI,WAKUU WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA YALIPO NCHINI

0
0


Naibu Rais wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Bw. James Gitau, akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge.  Mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akimfafanulia Naibu Rais wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Bw. James Gitau wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Comoro nchini Tanzania Mhe. Balozi Ahamada Elbadaour Mohamed akiongea na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika 22 Januari 2020 katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akimfafanulia jambo Balozi wa Comoro nchini Tanzania Mhe. Balozi Ahamada Elbadaour Mohamed wakati wa mazungumzo yaliyofanyika 22 Januari 2020 katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Balozi Frederic Clavie akiongea na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akimfafanulia jambo Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Balozi Frederic Clavie wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akiongea na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Aga Khan (AKDN) Bw. Amin Kurji.
Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Balozi Yonas Yosef Sanbe akiongea na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibugea kiongea na Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Balozi Yonas Yosef Sanbe
Balozi wa Iran nchini, Mhe. Balozi Mousa Farhang akimsikiliza Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Denmark nchini Mhe. Balozi Mette Norgaard akimsikiliza Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Italia nchini Meh. Balozi Roberto Mengoni akimsikiliza Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
……………
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa tarehe 22 na 23 Januari 2020 katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi hizo na mashirika hayo.

 Mabalozi hao ni Balozi wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Balozi Ahamada Elbadaour Mohamed, Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Balozi Frederic Clavie, Balozi wa Denmark nchini Mhe. Balozi Mette Norgaard na Balozi wa Iran nchini, Mhe. Balozi Mousa Farhang, Balozi wa Ethipia nchini, Mhe. Balozi Yonas Yosef Sanbe, pamoja na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Balozi Roberto Mengoni. 


Mbali na mabalozi, Mkuu wa Itifaki, Balozi Kanali Ibuge amekutana na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa ambao ni Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Bw. James Gitau na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Aga Khan (AKDN) Bw. Amin Kurji. 

AFISA MTENDAJI MKUU BRELA AANZA KAZI RASMI

0
0
Na Robertha Makinda - BRELA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa amewasili rasmi katika kituo chake kipya cha kazi leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili katika BRELA Ofisi Kuu Bw. Nyaisa amepata wasaa kukaa kikao kifupi na Menejimenti, kutambulishwa kwa wafanyakazi pia kukutana na baadhi ya wadau wa BRELA waliokua wakipata huduma kwa siku ya leo.

Katika maneno yake ya utambulisho kwa wafanyakazi wa BRELA amewataka wampe ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii.

“Wafanyakazi wanzangu naomba kwa kipindi hiki tushirikiane ili tuweze kufanya kazi za serikali ni matumaini yangu kila mmoja atasimama katika nafasi yake na kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha azma ya Tanzania ya Viwanda na kuwa nchi ya uchumi wa kati”, alisema Bw. Nyaisa.

Aidha alipokua akizungumza na wadau wa BRELA waliokuwa wakipata huduma siku ya leo, amewaomba waweze kuwa wavumilivu kwa kwa kipindi hiki wakati BRELA inajipanga kutoa huduma bora na kuondoa malalamiko yaliyopo, alibainisha Bw. Nyaisa.

Bw. Nyaisa aliteuliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA tarehe 19 Januari, 2020 akichukua nafasi ya Bi. Loy Muhando aliekuwa akikaimu nafasi hiyo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana wadau wa BRELA alipokua akitembelea Ofisi za Idara na Vitengo mbalimbali baada ya kuwasili leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Leseni BRELA Bw. Andrew Mkapa mara baada ya kuwasili leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji Bw. Bakari Mketo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa akifafanua jambo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa (Mbele) Akizungumza na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo Mbalimbali BRELA mara baada ya kuwasili leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.


Wateja wa Tigo kupiga simu mitandao yote, ya kwanza Tanzania.

0
0

Mkuu wa Kitengo cha Masoko, William Mpinga akifafanua Jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa kampeni mpya iitwayo Ujanja Ni, wateja kuwa na Uwezo wa kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu kupitia huduma zilizoboreshwa zaidi. Pembeni yeke ni Kaimu Mkuu Afisa Mkuu wa biashara, David Umoh
Kaimu Mkuu Afisa Mkuu wa biashara, David Umoh akizindua kampeni mpya iitwayo Ujanja Ni, wateja kuwa na Uwezo wa kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu kupitia huduma zilizoboreshwa zaidi.pembeni yake ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko, William Mpinga. 
Kaimu Mkuu Afisa Mkuu wa biashara, David Umoh akizindua kampeni mpya iitwayo Ujanja Ni, wateja kuwa na Uwezo wa kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu kupitia huduma zilizoboreshwa zaidi.pembeni yake ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko, William Mpinga


 Kwa mara ya kwanza Tanzania, Tigo imezindua kampeni ijulikanayo kama ‘Ujanja Ni’ ikiwa na lengo la kuwapa wateja thamani ya pesa zao kila wanapotumia bidhaa za Tigo. 

Kampeni hii itawapa wateja uwezo wa kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu kupitia huduma zilizoboreshwa zaidi. Vifurushi vyote vya sauti vinampa mteja uhuru wa kupiga simu mitandao yote kwa bei ile ile.

Huduma hii ni ya kwanza katika soko la simu na ni suluhisho kwa wateja wa Tigo kwasababu itaweza kubadili namna ambavyo watu wanatumia huduma za mawasiliano hapa nchini.

“Huduma hizi zinampa mteja uhuru wa kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa gharama ileile na wateja wanaweza kununua kifurushi chochote cha dakika, intaneti au vifurushi mchanganyiko na kufurahia faida zote muhimu kwa gharama nafuu zaidi,” alisema Kaimu Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, David Umoh wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

Aidha, vifurushi vyote vimeboreshwa kwa kuongezewa muda wa maongezi, SMS pamoja na intaneti.Pia, huduma hizi zinakuja pamoja na vifurushi vya wiki na mwezi ili kumpa mteja uwezo wa kuwasiliana zaidi, kuperuzi na kupata thamani ya pesa yake katika kila matumizi anayoyafanya.

Uzinduzi wa kampeni hii unaendana na jitihada za Serikali za kuhakikisha huduma za kupiga simu kwenda mitandao yote zinakuwa nafuu na huduma hii inampa mteja uwezo wa kufurahia mtandao mkubwa zaidi wa 4G+ hapa nchini.

“Kama kampuni ya kidigitali tunaamini kuwa huduma hii itasaidia kuongeza uhuru wa mawasiliano na kuwaunganisha wateja wetu na wapendwa wao bila mipaka kutoka Tigo kwenda mitandao mingine.Tunaanzisha huduma hii chini ya kampeni iitwayo ‘Ujanja ni’ ikiwa na maana kwamba ujanja ni kutumia fursa hii ya kupiga simu kwenda mitandao yote ukiwa na Tigo,” alisema Umoh

Pia huduma hii inawapa wateja uhuru zaidi kupitia vifurushi vya wiki pamoja na mwezi vya sauti na intaneti ambavyo vina thamani zaidi sokoni.Vifurushi hivi vinadumu kwa muda mrefu huku vikimpa mteja nafasi ya kuokoa pesa kwani vinapatikana kwa bei nafuu.

“Kwa mara ya kwanza, zaidi ya wateja 12 milioni hawatakuwa na wasiwasi tena pale wanapotaka kuwasiliana na watu waliopo kwenye mitandao mingine hapa nchini. Hii inadhihirisha jitihada zetu za kuwa mtandao ambao unampa mteja thamani zaidi kupitia huduma za kibunifu,” alisema Umoh.

Ili kupata huduma hii mteja wa Tigo anaweza kupiga *147*00# na kuchagua vifurushi vya wiki na vya mwezi kupitia menyu iliyorahisishwa.Huduma hii inapatikana pia kupitiaTigo Pesa App kwa kupiga *150*01# , au kwa kupitia tovuti ya Tigo au kwa kupiga namba ya huduma kwa wateja 100.

KAMPUNI YA MADINI YA TWIGA YAUNDWA KULINDA RASILIMALI ZA WATANZANIA

0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.
Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akikidhiana mikataba na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow iliyosainiwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.

Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akiwa na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow wakionyesha Mikataba iliyosainiwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.
Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow akizungumza mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020

Wageni waalikwa wakipiga makofi mara baada yay a hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020. PICHA NA IKULU


 
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo Januari 24, mwaka huu wa 2020 ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold Corporation, makubaliano ambayo yameunda Kampuni ya Twiga Minerals Cooperation Limited.

Mazungumzo hayo yaliyoanza tangu mwaka 2017 hatimaye yamefika mwafaka ambapo imeundwa Kampuni ya Madini ya Twiga kwa Serikali ya Tanzania kuwa na hisa asilimia 16 na kwamba faida itakayopatikana katika kampuni hiyo, zitagawanywa asilimia 50 kwa 50 kwa manufaa ya Kampuni husika ya Twiga.

Akizungumza baada ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Rais Magufuli amesema kuwa hiyo ni hatua kubwa kwa Watanzania baada ya mazungumzo hayo kufika mwafaka kuundwa Kampuni hiyo ya Twiga itakayokuwa na manufaa kwa Wananchi wa Tanzania katika rasilimali zao.

Rais Magufuli amesema huo ni ushindi mkubwa kwa Watanzania kutokana na hapo awali kudanganywa kuhsusu Madini hayo, "Barrick ni Kampuni kubwa duniani kufanya nao mazungumzo sio jambo dogo mwanzo Madini yalipokuwa yanachukuliwa Watanzania tuliamini ni mchanga, tunajiuliza swali kama ni mchanga kwa nini usafirishwe hadi nje ya nchi? baadae tulielewa kwamba ule haukuwa mchanga", amesema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameruhusu makontena yaliyokamatwa katika Bandari ya Tanzania, amesema watafutwe Wabia yauzwe kwa faida ya Kampuni ya Twiga, Rais Magufuli amesema kama kuna mnunuzi anatakakununua Makontena hayo, ajitokeze kwa faida ya Kampuni hiyo.

Pia Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Madini kuhakikisha inasimamia kuwapata Watanzania watakaowakilisha Taifa katika Kampuni hiyo (Twiga) wasiende kununuliwa, na kuangalia maslahi yao binafsi, badala yake waiwakilishe nchi kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla. 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu na Rais wa Barrick Gold, Mark Bristow amesema wamefurahi kuwepo nchini Tanzania, amesema mchakato huo haukuwa rahisi ulianza tangu 2017, ameeleza kwa sasa wamefikia mwisho na safari ya maisha bado inaendelea.

Bristow amesema Kampuni hiyo ya Twiga itawaruhusu Watanzania kuwa na maamuzi yatakayofanyika ndani ya Kampuni, amesema wanajukumu kubwa, kwa kufanya hivyo kwani sio faida yao peke yao bali faida ya wadau husuka kwa faida ya nchi husika.

Amesema Watanzania wa sasa na vizazi vijavyo wanahaki kushiriki katika taifa hili katika Migodi hiyo kwa Jamii zinazunguka kuwashirikisha zaidi katika maendeleo ya Uchumi wa Taifa.




Mikataba 9 iliyosaini mbele ya Rais kuhusu umiliki wa Hisa katika Kampuni ya Twiga mbele yako Rais Magufuli ni Mkataba wa Msingi wa Makubaliano, Mkabata wa Menejimenti na Utoaji Huduma, Mkataba wa Wanahisa wa Kampuni ya Twiga, Mkataba Wanahisa wa Kampuni ya North Mara, Mkataba wa Wanahisa wa Bulyanhulu, Mkataba wa Wanahisa wa Kampuni ya Pangea Buzwagi, Mkataba wa Maendeleo wa North Mara, Mkataba wa Maendeleo wa Bulyanhulu na Mkataba wa Maendeleo wa Pangea.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images