Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

RAIS MAGUFULI ASAJILI LAINI YAKE YA SIMU NA KUTOA POLE KWA FAMILIA YA ATANASI MNAKU

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka alama ya kidole gumba alipokwenda kusajili Laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole katika kampuni ya simu ya Airtel Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.Kushoto ni Msajili wa laini za Simu wa Airtel tawi la Chato Michael Martin.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitambulisho chake cha Taifa Msajili wa laini za Simu wa kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin aliokwenda kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Msajili wa laini za Simu wa kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin baada ya kusajili Laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha simu yakeambayo ametoka kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kisha kuzungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote ambapo ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza naWananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza naMjasiliamali wa Chipsi Joseph Wandwi wa Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza naWanafamilia pamoja na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu Mzee Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki Dunia Desemba 25, 2019 Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa kwa kuondokewa na Mpendwa wao leo Disemba 27, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali na Wanafamilia pamoja na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu Mzee Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki Dunia Desemba 25, 2019 Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa kwa kuondokewa na Mpendwa wao leo Desemba 27, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu chamaombolezo nyumbani kwa marehemu Mzee Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki Dunia Desemba 25, 2019 Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa kwa kuondokewa na Mpendwa wao leo Desemba 27, 2019. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita Desemba 27,2019.
PICHA NA IKULU

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA SH. BILIONI 4.2 KUTOKAJAPAN KWA AJILI YA KUFUFUA SHIRIKA LA TAFICO Inbox x

$
0
0

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Tanzania imepokea msaada wa Yen za Japan milioni 200 sawa na Shilingi Bilioni 4.2 kutoka Serikali ya Japan kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

Mkataba wa msaada huo umesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Katsutoshi Takeda, kwa niaba ya Serikali ya Japan.

Katibu Mkuu, Bw. Doto James, alisema kuwa msaada huo utatumika kununua Meli ya Uvuvi yenye vifaa vya kisasa, mashine ya kutengeneza barafu, ghala la baridi la kuhifadhia samaki, Vifaa mbalimbali vya kuvulia samaki na vya karakana, gari lenye mitambo maalum ya barafu na Gari kwa ajili ya kusambazia samaki.

Alisema kuwa utekelezaji wa Mradi huu utachangia kwa kiasi kikubwa katika kufikia malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Awamu ya Pili (FYDP II), ambayo pamoja na mengine unalenga kuboresha Sekta ya Uvuvi na hatimaye kuvutia Watanzania zaidi kujihusisha katika Sekta ya Uvuvi kama shughuli kuu ya kujipatia kipato.

“Mradi huu utaongeza uuzaji wa samaki nje ya nchi, kuongeza uhakika wa chakula nchini, na pia utaboresha usindikaji wa samaki, kuongeza thamani na masoko na kupunguza upotevu wa mazao ya samaki baada ya kuvua”, alieleza Bw. James.

Alisema kuwa Kiwango cha ukuaji kwa shughuli ndogo za kiuchumi za uvuvi kilifikia asilimia 9.2 mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 8.4 mwaka 2017 ambapo kiwango kikubwa cha ukuaji kilitokana na utunzaji mzuri wa mazalia ya samaki yakiwemo mabwawa ya watu binafsi sambamba na kuongezeka kwa mahitaji katika soko la ndani na nje.

Bw. James alisema kuwa, shughuli za uvuvi zilichangia asilimia 1.7 katika Pato la Taifa mwaka 2018, ambayo inadhihirisha umuhimu wa uvuvi katika uchumi, hivyo msaada uliotolewa utachangia jitihada za Serikali katika kufikia Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, Malengo Endelevu ya mwaka 2030 na Agenda ya Maendeleo ya Afrika ya mwaka 2063.

Alisema kuwa Serikali ya Japan imekuwa ikiisaidia Tanzania kupitia misaada na mikopo nafuu katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Miundombinu ya barabara, Maji, Nishati Utawala Bora na Uwajibikaji ambapo mpaka sasa Jumla ya Sh. Trilioni 1. 3 zimetolewa na Serikali hiyo tangu mwaka 2012.

Misaada na mikopo hiyo inadhihirisha kuwa kuna uhusiano mzuri wa kirafiki kati ya Tanzania na Serikali ya Japan, hivyo matumaini ni kuwa urafiki huo utaendelea kuimarishwa na Serikali zote mbili kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizo.

Kwa upande wake Naibu na Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Katsutoshi Takeda, kwa niaba ya Serikali ya Japan amesema nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na ushirikiano mzuri kati ya nchi hizo mbili lakini pia kuchangia jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini wa wananchi wake.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamahtamah ameishukuru Serikali ya Japan kwa msaada huo utakaosaidia kufufua Shirika hilo la Uvuvi.

Alisema kuwa Serikali itapeleka mswaada Bungeni mwezi Januari mwakani, ili kuliwezesha TAFICO kuanza kazi zake rasmi na kwa kishindo ili Shirika hilo liweze kuchangia katika uchumi wa Taifa kwa kiwango kikubwa.

Alisema kuwa pamoja na msaada huo, Serikali imechukua hatua za kuchambua mali zilizokuwa zikimilikiwa kinyemela na baadhi ya taasisi na watu ambapo mpaka sasa mali zenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 118 zimerejeshwa Serikalini na kazi ya kurejesha mali nyingine zinaendelea kwa kushirikiana na Msajili wa Hazina.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Bw. Katsutoshi Takeda, wakisaini mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Bw. Katsutoshi Takeda, wakibadilishana mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ambapo TAFICO itaweza itaweza kuwa na Meli ya Uvuvi, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Bw. Katsutoshi Takeda, wakiwa wamenyenyua Mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Maafisa waandamizi (mbele) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakishuhudia kusainiwa kwa mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati) akieleza kuhusu misaada na mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na Japan, wakati wa hafla ya kusainiwa kwa Mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Bw. Katsutoshi Takeda na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa upande wa Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa upande wa Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah, akielezea jitihada za Serikali za kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia), na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Bw. Katsutoshi Takeda (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Japani baada ya hafla ya kusainiwa kwa mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Jijini Dar es Salaam.(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

UHAKIKA WA MAJI UNATOKANA NA UHIFADHI WA VYANZO VYA MAJI BONDE LA WAMI/RUVU

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Amani, Tanga

Katika kuendelea kuwepo kwa maji ya uhakika na yenye usalama hakuna budi jamii kuhifadhi vyanzo vya maji wanavyozunguka kwa kuendesha shughuli za kilimo zisizo na madhara katika vyanzo hivyo.

Vyanzo ya maji vikihifadhiwa kwa katika sekta ya kilimo kwa kupanda mazao ambayo hayana madhara katika utiririshaji maji mamlaka husika kupunguza gharama za kutibu maji wakati wa usambazaji wa maji hayo kwa wananchi.

Mkoa wa Tanga kwa wananchi wanaozunguka vyanzo vya maji wameunda Umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira Kihuhwizigi (Uwamasiki) ambao wamekuwa wakihifadhi vyanzo vya maji na kufanya mamlaka ya Maji Safi na Mazingira jiji la Tanga Tanga Uwasa) kuunga mkono jitithada za umoja huo.

Kutokana na Mamlaka ya Tanga kuwa umoja wenye nguvu katika uhifadhi vyanzo vya maji Bonde la Wami/Ruvu imepeleka jumuiya za Watumia Maji katika vyanzo vya bonde hilo kujifanza katika umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira (Uwamasiki) ili kuleta chachu kuongeza mbinu katika uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Akizungumza wakati wa ziara ya Jumuiya ya Watumia Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii na Mahusiano wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Horold Kayoza amesema kuwa wamepeleka jumuiya hizo kwenda Tanga kwenda kujifunza namna Umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira (Kihuhwi) inavyolinda vyanzo vya maji kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika vyanzo hivyo ikiwemo kilimo.

Kayoza amesema baada ya kutoka Tanga nia ni kuona jumuiya ya watumia maji wanakwenda na kasi ya kuweka mikakati ya kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kushirikisha wadau wote kwa kutumia elimu walioipata katika ziara ya Mkoa wa Tanga.

Aidha amesema kuwa mazingira ya vynzo vya maji katika mkoa wa Tanga havina tofauti na Mikoa ya Morogoro na Pwani hivyo wanajumuiya ya watumiaji katika Bonde la Wami/Ruvu watatumia mbinu mbalimbali walizozipata katika ziara ya Tanga.

Nae Afisa Udhibiti Ubora wa Huduma na Mratibu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira jiji la Tanga (Tanga-Uwasa) Ramadhan Nyambuka amesema kuwa kutokana na Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira (KIHUHWIZIGI) kuhifadhi vyanzo vya maji kumeleta matokeo chanya kwa mamlaka kupunguza gharama za kutibu maji.

Amesema kuwa wakati umoja huo ukiwa haujaanzishwa walikuwa wanatumia gharama kubwa ya kutibu maji lakini kuanzishwa kwa umoja huo Tanga-Uwasa limeendelea kupunguza gharama hizo ikiwa ni kuunga mkono kwa ufadhili wa miradi kwenye umoja ili waendelee kutunza vyanzo vya maji.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI , Twaha Mbaruku amesema kuwa umoja umesimama vizuri kutokana na kila mmoja kujua umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji. 
Amesema wakati wanaanza umoja huo kuna vyanzo vingine vilikuwa vimekufa lakini sasa vyanzo vyote vinatiririsha maji wakati wote huku shughuli za kiuchumi zikiendelea bila kuathiri vyanzo hivyo.
 Maji yakitiririka msimu mzima wa mwaka  katika Msitu wa Amani wilayani Muheza.
 Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo  ya Jamii na Mahusiano  wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu  Horold Kayoza akizungumza na wanajumuiya watumia maji wa Bonde la Wami/Ruvu pamoja na Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira (KIHUHWIZIGI) wakati wa ziara wa Jumuiya ya Bonde la Wami/Ruvu kutembelea namna ya utunzji wa vyanzo vya maji katika msitu wa Amani wilayani Muheza mkoani Tanga.
 Afisa Udhibiti  Ubora wa Huduma  na Mratibu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira jiji la Tanga (Tanga-Uwasa) Ramadhan Nyambuka akitoa maelezo kuhusiana na namna walivyonufaika Mamlaka hiyo  kutokana na jamiI kuwa na uthubutu wa kuhifadhi vyanzo vya maji.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI , Twaha Mbaruku akizungumza kuhusiana na umoja huo walivyopokea utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja kuinuka kiuchumi wakati wa ziara ya Jumuiya ya Watumia maji wa Bonde la Wami/Ruvu.
 Mwenyekiti wa Makinga Maji Mkazi wa Kijiji cha Mbomole  Michael Simon akieleza kwa waandishi wa  habari namna ya makinga maji yanavyosaidia katika kuhifadhi vyanzo vya maji pasipo kuwepo kwa udongo wa kutiririka ka vyanzo vya maji.

 .Wanaumoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI wakicheza ngoma za uhamasishaji wa Uhifadhi wa wa vyanzo vya maji wakati wanajumuiya watumiaji maji wa bonde la Wami/Ruvu walipofanya ziara katika  umoja huo namna wanavyohifadhi vyanzo vya maji katika msitu wa Amani wilayani Muheza mkoani Tanga.
 Mmoja wa wenye viti wa Watumia Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Basley Matangaru akieleza namna walivyopata elimu  ya utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji  katika umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI.
 Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI wamejenga sehemu mahsusi kwa ajili ya kuonyeshea pikipiki ili wasiweze kutiririsha uchafu katika vyanzo vya maji.
 Mradi wa ufugaji samaki wa kikundi cha hamasa ambacho kinasaidia kutojihusisha na shughuli za kilimo chenye madhara katika vyanzo vya maji.
 Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo  ya Jamii na Mahusiano  wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu  Horold Kayoza akimkabidhi fedha taslimu sh.100,000 kwa Katibu Msaidizi wa Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI Willium Masonda kwa ajili ya uhamasishaji wa uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kikundi cha hamasa vhs umoja huo.

NBC YAWAPONGEZA NA KUWAAGA WASHINDI WAKE WA KAMPENI YA “IBUKA KIDEDEA” .

$
0
0
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa tatu kushoto) akimkabidhi tiketi ya ndege, mwenza wa mshindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Kijakazi Mohamed aliyejishindia safari ya kwenda Sychelles wakati wa hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond na Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo. NBC inalipia gharama za safari ya mwenza huyo pamoja na mshindi mwenyewe Ramadhani Saidi (hayupo pichani).


Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (katikati) akimkabidhi tiketi ya ndege mmoja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Jocelyne Rwechungura aliyejishindia safari ya kwenda Sychelles wakati wa hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo. NBC inalipia gharama za safari ya mshindi huyo pamoja na mwenza wake aliyemchagua.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke akimkabidhi tiketi ya ndege, mmoja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Prof. Lettice Rutashobya (kulia), aliyejishindia safari ya kwenda Sychelles wakati wa hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka Kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond na Meneja Masoko wa Benki hiyo, Alina Maria Kimaryo. NBC inalipia gharama za safari ya mshindi huyo pamoja na mwenza wake aliyemchagua.
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na maofsa wa NBC katika hafla hiyo.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond akizungumza katika hafla hiyo ambapo alitoa hamasa kwa wateja na wasio wateja kuitumia kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC ili kutimiza malengo yao.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke akizungumza katika hafla ya kuwapongeza na kuwaaga washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo walioshinda safari za kwenda Sychelles na katika mbuga za wanyama za Serengeti. 
Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo akizungumza kuhusu kampeni hiyo akisema Ibuka Kidedea imekuwa ikitoa zawadi kila mwezi na hadi sasa jumla ya pikipiki tano zimeshatolewa tangu mwezi Oktoba ilipozinduliwa.



Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imefanya hafla maalumu ya kuwapongeza na kuwaaga wateja walioibuka washindi katika Kampeni yake ya Ibuka Kidedea na akaunti ya NBC Malengo. Washindi hao wamejishindia safari za kitalii ambapo baadhi watazulu Mbuga ya Wanyama ya Serengeti na wengine visiwa wa Sychelles. 

Kampeni ya Ibuka Kidedea ilizinduliwa mwezi Okotoba mwaka huu ikiwa na lengo kuu la kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba kwa wateja ambapo zawadi mbalimbali zikiwemo zikiwemo bodaboda zimekuwa zikitolewa kwa washindi walioingia kwenye droo maalum inayosimamiwa na Bodi ya michezo ya kubahatisha nichini. 

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton (zamani New Africa), jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke aliwashukuru wateja wote waliojitokeza kushiriki kampeni hii tangu kuzinduliwa kwake . 

“Ibuka Kidedea imefanyika kwa mafanikio makubwa, tumeshuhudia idadi kubwa ya wateja wetu wakishiriki katika kampeni hii, lakini pia wateja wanashuhudia kuongezeka kwa amana zao kutokana na faida za kila mwezi. 

"Natoa pongezi kwa washidi wetu wote na tunaamini mtaendelea kuwa mabalozi wetu wakati mkifurahia safari hizi katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka”, kampeni hii bado inaendelea hivyo tunatoa wito kwa wateja wengine kushiriki katika kampeni hii kwa kuendelea kuweka akiba ili kupata nafasi ya kushinda zawadi”, aliongeza Bwana Masuke. 

Naye Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond alisema ni matumani ya NBC kuwa kampeni hii inatoa hamasa kwa watanzania kuwa na utamaduni endelevu wa kujiwekea akiba ili kutimiza mahitaji yao ya kifedha lakini zaidi ni kuwa na uhuru wa kifedha. 

"Tunahamasisha wateja wetu na wasio wateja kuitumia akaunti ya Malengo ya NBC ili kutimiza malengo yao, iwe ni nyumba, gari nzuri, pikipiki, kwenda mapumzikoni, ada za shule na mengineyo. 

"Tunajua kila mtu ana ndoto yake, jiunge na NBC Malengo na tutafurahi kukusaidia kutimiza ndoto zako", aliongeza. 

Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo, Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo alisema Ibuka Kidedea imekuwa ikitoa zawadi kila mwezi na hadi sasa jumla ya pikipiki tano zimeshatolewa tangu mwezi Oktoba. 

Ili kujishindia pikipiki (bodaboda) mteja anachotakiwa kufanya ni kuweka akiba kwa kiwango kinachoanzia shs 100,000 katika akaunti yake ya Malengo, na kwa safari ya Serengeti kiwanngo kinaanzia shs 1,000,000 na kiwango kinachoanzia 50,000,000 kwa safatri ya Sychelles. 

"Pamoja na zawadi hizi katika kampeni hii, wateja watakaoweka akiba katika akaunti zao za Malengo kwa kiwango kinachoanzia shs 1,000,000 wanapata nafasi ya kujishindia pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo katika droo kubwa ambayo jumla ya pikipiki za kubebea mizigo (Toyo) tatu zitatolewa”, alisema. 

Mmoja wa washindi aliyejishindia bodaboda, Daudi Patrick Majani, mstaafu na mfanyabiashara anayeishi Tabata Segerea jijini Dar es Salaam alisema atatumia bodaboda yake kumuingizia kipato na kuitumia kwa usafiri utakaosaidia kuiwezesha biashara yake. 

Washindi walioshinda safari ya Serengeti ni, Christopher Mgote kutoka Nzega, Makongoro Makongoro kutoka Arusha, Bi. Jocelyine Rwechengura na Bi. Esther Ndunguru wote kutoka Dar es Salaam. 

Washindi walioshinda safari ya Sychelles ni, Wambura John Wambura kutoka Tarime mkoani Mara, Ramadhan Saidi, Lettice Rutashobya na Sylevester Ambokile wote wa jijini Dar es Salaam. 

SERIKALI YAVUNJA MKATABA NA KAMPUNI YA NICOL KUENDESHA MACHINJIO YA DODOMA

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imevunja mkataba wake na Kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOL) ambayo kupitia kampuni ya TMCL ilikua ikiendesha kiwanda cha nyama jijini Dodoma.

Uamuzi huo umefikiwa hii leo baada ya Serikali kugundua kuwepo kwa udanganyifu kwenye mkataba wao ambao umeisababishia hasara Taifa ya Shilingi Bilioni 9.7.

Akizungumza leo jijini Dodoma na wafanyakazi wa kiwanda hicho na wadau wa nyama, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina amesema tangu waikabidhi kampuni ya NICOL uendeshaji wa kiwanda hiko hakuna faida yoyote ambayo Serikali imeipata zaidi ya hasara.

Waziri Mpina amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua za kisheria watendaji wote wa NICOL, TMCL na viongozi wa Ranchi ya Taifa (NARCO) ambao wameisababishia serikali hasara hiyo tangu mwaka 2008.

Pia ameipa siku 60 NARCO kujiondoa kwenye ubia na kampuni hiyo ya TMCL kwani ni jambo la aibu kwa kampuni ya Umma kuendelea kushirikiana na watu ambao wamekua wakiipa hasara serikali.

" Hatuwezi kuvumilia hii hali, kuna harufu kubwa ya ufisadi hapa na ndio maana nimevitaka vyombo vyetu vya ulinzi kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote waliokula fedha hapa. Rais Magufuli alishasema ni heri ukala sumu kuliko kula hela ya wananchi wanyonge.

Ni jambo lisiloingia akilini kwamba walikua wakiendesha machinjio haya kwa hasara. Kuna fedha nyingi zinaonekana kampuni iliingiza, mfano kuna fedha Bilioni 1.2 lakini hawakuingiza kwenye mapato. Kuna Bilioni tano iliingia lakini pia haikwenda Benki jambo ambalo ni kinyume na sheria. Lazima tuchukue hatua," Amesem Mhe Mpina.

Akijibu malalamiko ya baadhi ya wafanyakazi waliowahi kusimamishwa na ambao wako kazini, Waziri Mpina pia ameitaka NICOL kuwalipa watumishi wote ambao wamekua wakidai stahiki zao, pamoja na madeni yote zaidi ya Bilioni tano ambayo kampuni ya TMCL ilikua ikidaiwa.

Mhe Mpina amesema baada ya kuvunja mkataba baina yao na NICOL kwa sasa huduma ndani ya kiwanda hicho zitaendelea kama kawaida zikiwa chini ya serikali.

" Serikali itaendesha kiwanda hichi kwa mpito wakati huu ambao tunatafuta mwekezaji ambaye ataweza kuendana na Sera zetu, mahitaji ya sasa, kutafuta masoko nje na ambaye atakua tayari kutoa ajira bila ubabaishaji wa mishahara.

Na kwa kuanzia nimemteua ndugu Victor Mwita kuwa Kaimu Meneja wa kiwanda hiki na uteuzi wake umeanza mara moja baada ya kufanyika kwa makabidhiano chini ya Katibu Mkuu wa Wizara, Prof Elisante Ole Gabriel, " Amesem Mhe Mpina.

Waziri Mpina amesema kwa kipindi chote ambapo machinjio hayo yalikua chini ya kampeni hiyo wameua masoko yote ya kuuza nyama katika Nchi za Kiarabu ambao kwa muda mrefu wamekua wakichukua nyama nchini jambo ambalo limesababisha serikali kukosa mapato ya fedha za kigeni.

Amesema kutokana na uongozi dhaifu wa kiwanda hicho kumesababisha pia wafanyakazi wengi kupoteza ajira kwa makosa yasiyoeleweka lakini pia kushindwa kulipa mishahara wafanyakazi walioko kazini.

Mhe Waziri amewataka wafanyakazi wote wanaodai fedha zao kuwa na subira katika kipindi hiki ambacho serikali inatafuta njia bora za kuhakikisha wanapata stahiki zao na baada ya siku 60 atatoa taarifa rasmi ambayo itakua yenye matumaini kwa wale wote ambao wamekua wakidai kwa muda mrefu.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina akizungumza na wafanyakazi wa machinjio ya Dodoma leo ambapo ameagiza machinjio hiyo kurudi mikononi mwa Serikali.
 Kaimu Meneja wa Machinjio ya Dodoma akizungumza na wafanyakazi wa machinjio hayo baada ya kuteuliwa leo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina ikiwa ni baada ya Serikali kuyachukua machinjio hayo kutoka mikononi mwa Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa, NICOL.

 Mmoja wa wafanyakazi ambao wanadai mishahara yao kutoka kiwanda cha nyama cha TMCL, Bw Charles Hema akitoa malalamiko yake kwa niaba ya wenzake mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina (hayupo pichani) alipofika katika kiwanda hicho leo jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa kiwanda cha nyama Dodoma wakimsiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina alipofika katika machinjio hayo leo.

RAIS MAGUFULI AWASILISHA FOMU ZAKE ZA TAMKO LA MALI NA MADENI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amewasilisha tamko linalohusu Mapato,Rasilimali na Madeni ya viongozi katika Ofisi ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria na kikatiba.

Tamko hilo limewasilishwa katika ofisi hizo kanda maalumu ya Dar es salaam na katibu wa Rais,  Bwana Ngusa Samike ambaye ametumwa na Mhe Rais akiwa mapumzikoni Chato na limepokelewa na Kamishna wa Sektretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Jaji mstaafu Harold Nsekela.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea tamko hilo Jaji mstaafu Nsekela amesema kitendo alichokifanya Mhe.Rais kimetekeleza takwa la kikatiba Ibara ya 132 (5) (D) linalowataka viongozi kuwasilisha taarifa za tamko la mapato, Rasilimali na madeni mara kwa mara lakini pia ametekeleza sheria no 13 ya mwaka 1995 kingu cha 9.

Jaji mstaafu Nsekela akatumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wengine kutumia siku 2 zilizobaki kufanya hivyo kabla ya tarehe 31 Desemba katika kutekeleza takwa hilo la kisheria na kikatiba






Wateja wa Vodacom M-Pesa wavuna Sh. bilioni 9

$
0
0
Ikiwa miezi mitatu imepita tangu Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc kutoa gawio la Sh. bilioni 50.4 kwa wanahisa wake, Kampuni hiyo leo inatangaza kutoa riba ya ziada kwa watumiaji wake wa huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi. Zaidi ya wateja milioni 8.3 wa Vodacom M-Pesa watapata sehemu yao ya faida ya bilioni 9 iliyokusanywa kwenye akaunti ya M-Pesa Trust kama faida ya kutumia huduma hiyo kwa kipindi cha mwezi Aprili hadi Septemba. 

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania M-Commerce, Epimack Mbeteni, alisema kuwa, faida hiyo italipwa kwa wateja wote ikiwamo wakala wa rejareja na washirika wengine wa M-Pesa ambapo faida yao italipwa kulingana na jinsi walivyofanya miamala ya malipo kupitia M-Pesa. 

“Huduma yetu ya pesa kupitia simu ya mkononi kwa maana ya M-Pesa, inaendelea kuleta simulizi zenye mafanikio, ikitoa dhamana muhimu za kijamii na thamani ya kifedha kwa watanzania wote. Tumeshuhudia ukuaji katika jukwaa la watumiaji wa M-Pesa, ambapo zaidi ya wateja, mawakala, wafanyabiashara wakubwa na taasisi watapata gawio hili. Tunafurahia kuona ongezeko hilo kwa wateja wetu wanaotumia huduma ya M-Pesa,” alisema 

Kwa mujibu wa Takwimu za hivi karibuni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Vodacom Tanzania PLC, kampuni inayoongoza kwa mawasiliano ya simu nchini ina wateja zaidi ya milioni 10 kwenye jukwaa lake la M-Pesa ikiwa ni asilimia 41 katika mgawanyiko wa umiliki wa soko. Hadi sasa Vodacom Tanzania PLC imekwishalipa riba ya zaidi ya shilingi bilioni 130 kwa wateja wake wa M-Pesa. 

Epimack aliongeza kwa kusema kuwa, sehemu ya faida kwa wateja huhesabiwa kulingana na mwongozo wa Benki Kuu ya Tanzania na itategemea kiwango cha shughuli za M-Pesa zilizofanywa kwa kipindi husika. 

“Mgao huo ulianza tangu wiki ya kwanza ya sikukuu ambapo mteja anatuma ujumbe mfupi wa neno AMOUNT kwenda 15300 ili kufahamu kiasi cha faida ya riba atakachopokea. Baada ya kupokea kiasi hicho kilichotolewa, wateja wa M-Pesa wanaweza kutoa riba zao kupitia pesa taslimu, muda wa maongezi au vifurushi, na kulipa bili au kulipia bidhaa mbalimbali ” alisema. 

Jukwaa la Vodacom M-Pesa linaongoza kwa kutoa fursa kwenye soko ambapo limeongeza kasi katika ujumuishaji wa kifedha na kuchochea shughuli za uchumi nchini Tanzania. 

“Kwa kipindi cha miaka 11 iliyopita tumejitahidi kuwekeza zaidi kwenye uvumbuzi ambapo kupitia ushirikiano wetu wa kimkakati na benki pamoja na wavumbuzi wengine, tumeenda mbali zaidi ya kufanya miamala kwa kuanzisha bidhaa nyingine kama M-Koba, M-Pawa, Halal Pesa, Songesha, M-Pesa MasterCard na nyinginezo nyingi. Tunaendelea kuhakikisha tunakuza ujumuishaji wa kifedha na kukuza uchumi wa kidijitali nchini Tanzania,” Alielezea Mbeteni. 

Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wapaa

$
0
0
 Washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakifungua shampeni muda mfupi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo wakielekea Seychelles. Kupitia kampeni hiyo inayoendelea, kila mwezi washindi wanajishindia safari za kitalii kwenda Seychelles, mbuga za wanyama za Serengeti, bodaboda na pikipiki za miguu mitatu (Toyo). 
 Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza wa Benki ya NBC, Dorothea Mabonye (kushoto), pamoja na Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), wakiagana na mmoja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Ramdhani Saidi (kulia) muda mfupi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo akielekea Seychelles pamoja na mwenza wake. Kupitia kampeni hiyo inayoendelea, washindi wanajishindia safari za kitalii kwenda Seychelles, mbuga za wanyama za Serengeti, bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu (Toyo).

 Meneja Masoko wa benki ya NBC,  Alina Maria Kimaryo (kulia), akikabidhi tiketi ya ndege ya kwa moja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Esther  Ndunguru muda mfupi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo akielekea Arusha kufanya utalii katika Mbuga za Wanyama za Serengeti akiwa na mwenza wake. Kupitia kampeni hiyo inayoendelea, washindi wanajishindia safari za kitalii kwenda Seychelles, mbuga za wanyama za Serengeti, bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu (Toyo).
 Mshindi wa safari ya kwenda Mbuga za Wanyama za Serengeti wa Ibuka kidedea na NBC Malengo, Esther Ndunguru (kushoto) akikaguliwa tiketi yake kabla ya kupanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo. Safari hiyo paamoja na mwenza wake inalipiwa na NBC. Washindi wanne wameibuka kidedea na kushinda safari ya kwenda Serengeti pamoja nma wenza wao huku gharama zote zikilipiwa na NBC.    
 Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakitakiwa heri ya safari yao na wawakilishi wa NBC waliowasindikiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kabla hawajaondoka.

 Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakipozi kwa picha pamoja na  wawakilishi wa NBC waliowasindikiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kabla hawajaondoka huku wakiwa wameshika glasi zenye shampeni ikiwa ni ishara ya kuwatakia safari njema.
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakiwa katika hatua ya mwisho ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 

Rais Magufuli awatakia Watanzania heri ya mwaka Mpya 2020

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia Watanzania wote heri ya Mwaka mpya wa 2020 na kuwaomba waendelee kudumisha amani na upendo ili uwe mwaka wa maendeleo na ustawi kwa Taifa.


Mhe. Rais Magufuli ametoa salamu hizo leo tarehe 31 Desemba, 2019 wakati akiagana na Maafisa na Askari Wanyamapori na Hifadhi ya Misitu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ambako ametembelea na kujionea vivutio vya utalii pamoja na wananchi wa Nyabugera na Muganza aliowasalimu wakati akiwa njiani kurejea nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.


Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amepokea salamu za heri ya Mwaka Mpya wa 2020 kutoka kwa wananchi, viongozi mbalimbali wakiwemo Marais Wastaafu, Maaskofu na Masheikh ambao wamempongeza kwa kazi nzuri ya kuongoza nchi kwa mafanikio makubwa na wamemuelezea matarajio yao ya kufanikiwa zaidi katika mwaka ujao.


“Mhe. Rais wangu, Dkt. Magufuli, Bwana Yesu Asifiwe. Ninakupa hongera sana kwa wajibu mzito ulionao. Kwa neema ya Mungu tumejaaliwa kufikia siku ya mwisho kwa mwaka huu wa 2019. Mimi nakupongeza kwa jitihada zako nyingi za kuleta maendeleo kwa nchi yetu. Ninakuombea na kukutakia Mwaka Mpya 2020 wa heri na mafanikio makubwa. Uso wa Bwana uende nawe popote utakapokuwa”amesema Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Frederick Shoo.


Kabla ya kuondoka katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi, Maafisa na Askari wote wa hifadhi hiyo kwa mapokezi mazuri na juhudi kubwa zilizowezesha hifadhi hiyo kuvutia na amewahakikishia kuwa pamoja na kutoa shilingi Bilioni 2 za ujenzi wa kivuko cha kwenda hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo, Serikali itatoa shilingi Milioni 200 za kuboresha barabara za hifadhi hiyo.


Baada ya kuvuka ziwa Victoria kwa kivuko cha MV Chato, Mhe. Rais Magufuli amekutana na wananchi wa Kasenda na kuelezea kutoridhishwa kwake na ukusanyaji wa mapato ya soko la dagaa na samaki la Kasenda baada ya kuelezwa kuwa makusanyo ya mapato ya soko hilo ni shilingi laki 5 kwa siku licha kuwa soko kubwa namba 2 kwa kuuza dagaa katika ukanda wa Ziwa Victoria.


Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Chato, kufuatilia ukusanyaji wa mapato katika soko hili na kuchukua hatua za kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato itakayobainika ili Halmashauri ya Wilaya ya Chato iweze kupata fedha zitakazosaidia kutatua kero za wananchi ikiwemo kuboresha mazingira ya soko hilo na ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyabugera ambayo amechangia shilingi Milioni 5.


Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Bw. Eliud Mwaiteleke kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya Kasenda - Muganza yenye urefu wa kilometa 2.2 ili ijengwe kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi, na kwamba Serikali itatoa fedha za ujenzi wa barabara hiyo.


Mhe. Rais Magufuli pia amewasalimu wananchi wa Muganza, ambapo amewapongeza kwa maendeleo yaliyopatikana katika eneo hilo na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma ili iendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi.


“Nchi hii ilikuwa inaliwa sana na majizi na mpaka sasa bado wapo, namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kunipa uhai ili katika mwaka 2020 niendelee kuwatumbua majizi wote na fedha tutakazopata tuzipeleke kwenye miradi ya maendeleo kama ambavyo tumenunua ndege 11, tunajenga reli (standard gauge), tunatoa elimu bure na mengine mengi” amesema Mhe. Rais Magufuli.


Mhe. Rais Magufuli pia amemuonya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Bw. Eliud Mwaiteleke kwa matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na halmashauri hiyo na ametaka dosari hizo zirekebishwe mara moja. “Nataka ujirekebishe, wananchi hawa wanateseka sana”amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.



Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chato

31 Desemba, 2019


Rais Magufuli atoa siku 5 kwa Waziri Kigwangalla na Katibu Mkuu Mkenda kuelewana

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akipanda Kivuko kuelekea  Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo leo
Jumanne Desemba 31, 2019




RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO WILAYANI CHATO MKOA WA GEITA

$
0
0








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) pamoja na maafisa na askari wa Jeshi Usu la Mamlakahiyo wakati alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo leo Jumanne Desemba 31, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) pamoja na maafisa na askari wa Jeshi Usu la Mamlaka hiyo wakati alipotembeleaHifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo leo Jumanne Desemba 31, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakielezwea jambo kuhusu sehemu ya Ziwa Victoria na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA Dkt. Allan Kijazialipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo leo Jumanne Desemba 31, 2019
Sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo kama inavyoonekana kutoka angani leo Jumanne Desemba 31, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipanda Kivuko kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo leo Jumanne Desemba 31, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono boti lililobeba watalii wakati wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ambako yeye pia alitembelea leo JumanneDesemba 31, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli akiwa na familia ya watalii ya klutoka Ufaransa ya Bw. Arnaudde Vanssay aliokutana nao wakati akitembelea Hifadhi ya Taifa yaKisiwa cha Rubondo leo Jumanne Desemba 31, 2019

Mkazi wa Manzese ashinda mil.20 ya Kishindo cha Funga mwaka

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa-Tigo Pesa, James Sumari akiongea na waandishi wa habari alipokuwa akizindua kampeni iitwayo kishindo cha funga mwaka, kwaajili ya wateja wanao tumia Tigo Pesa. kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum-Tigo Pesa, Mary Rutta. (Picha kutoka Maktaba) 


Salum Biwi (32) mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam ameibuka mshindi wa kwanza wa Kampeni ya Kishindo cha Funga mwaka inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo na kujishindia kiasi cha Sh20 Milioni.

Promosheni hiyo pia imeshuhudia washindi wengine wawili akiwamo Hamidu Mtabiage (32) mkazi wa Lindi akiibuka na Sh15 milioni na Anna Mkongwa (32) kutoka Mkoani Dodoma ambaye ameshinda Sh10 milioni kama sehemu ya washindi watatu wa jumla.

Akizungumza mara baada ya kupigiwa simu ili kumfahamisha kuhusu ushindi huo, Biwi alisema amepokea kwa furaha ushindi huo huku akiishukuru Tigo kwa kuja na promosheni hiyo ambayo imemfanya kufunga mwaka kwa kishindo zaidi.

“Nimekuwa nikiweka pesa na kupokea pesa kwenye namba yangu ya Tigo Pesa na sikutegemea kama ningeshinda kiasi hiki cha fedha, nawashukuru sana Tigo kwa kampeni yao hii ambayo imenifanya nimalize mwaka vizuri zaidi,” alisema Biwi ambaye ni mtaalamu wa masoko.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema Kampeni hiyo iliyodumu kwa mwezi mmoja ilikuwa na lengo la kuwawezesha wateja wanaoweka au kupokea pesa kwa njia ya Tigo Pesa ili waweze kufunga mwaka kwa kishindo.

“Kampeni hii ilitenga jumla ya Sh500 milioni kwaajili ya wateja zaidi ya 331 wanaoweka na kupokea pesa kwa njia ya Tigo Pesa na hatimaye leo imeweza kufikia kikomo kwa kuwapata washindi watatu wa jumla,” alisema.

Mbali na washindi hao, Kampeni hiyo ilikuwa ikitoa zawadi kwa washindi 8 wa Sh1 milioni kila siku na washindi 8 wa Sh5 Milioni kila wiki na tayari wamekwisha pokea zawadi zao.

“Wateja walitakiwa kuweka na kupokea pesa kwenye akaunti ya Tigo Pesa kutoka kwa wakala wa Tigo Pesa, benki au mitandao mingine na moja kwa moja unakuwa kwenye nafasi ya kushinda.Tunawashukuru wateja wetu kwa kushiriki kwenye kampeni hii na tunawapongeza washindi wote,” alisema.


Anna Mkongwa ambaye ameshinda Sh10 milioni alisema “Kwakweli siamini kama nimeshinda, nawashukuru sana Tigo kwa kuleta kampeni hii. “

TRA YAVUNJA REKODI NYINGINE KWA KUKUSANYA TRILIONI 1.987 DESEMBA 2019

$
0
0
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati akitangaza makusanyo ya kodi ya kipindi cha Robo ya Pili ya mwaka 2019/20 ambapo amesema kwa mara nyingine, TRA imevunja rekodi kwa kukusanya jumla ya kiasi cha sh. trilioni 1.987 kwa mwezi Desemba 2019 sawa na ufanisi wa asilimia 100.20 kutoka katika lengo la kukusanya kiasi cha sh. trilioni 1.983 kwa mwezi huo. Kulia kwake ni Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati akitangaza makusanyo ya kodi ya kipindi cha Robo ya Pili ya mwaka 2019/20 ambapo amesema kwa mara nyingine, TRA imevunja rekodi kwa kukusanya jumla ya kiasi cha sh. trilioni 1.987 kwa mwezi Desemba 2019 sawa na ufanisi wa asilimia 100.20 kutoka katika lengo la kukusanya kiasi cha sh. trilioni 1.983 kwa mwezi huo. Kulia kwake ni Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo na kushoto kwake ni Kamishna wa Idara ya Walipakodi Wakubwa Bw. Alfred Mregi.
******************************
Na Veronica Kazimoto
Dar es Salaam.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa mara nyingine, imevunja rekodi kwa kukusanya jumla ya kiasi cha sh. trilioni 1.987 kwa mwezi Desemba 2019 ambayo ni rekodi ya kwanza kufikiwa tangu kuanzishwa kwake ikilinganishwa na rekodi ya mwezi Septemba, 2019 iliyokuwa sh. trilioni 1.767.  

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa, makusanyo hayo ya mwezi Desemba 2019 ni sawa na ufanisi wa asilimia 100.20 kutoka katika lengo la kukusanya kiasi cha sh. trilioni 1.983 kwa mwezi huo.

“Ni kweli kwamba, kitaalam, miezi tofauti hailinganishiki moja kwa moja. Hata hivyo, kwa makusanyo haya ya sh. trilioni 1.987 kwa mwezi Desemba 2019, TRA imevunja rekodi yake yenyewe iliyoiandika mwezi Septemba 2019 ambapo ilikusanya jumla ya sh. trilioni 1.767 ikiwa ni sawa na asilimia 97.20 ya lengo la kukusanya sh. trilioni 1.817 katika kipindi hicho,” alisema Dkt. Mhede.

Akizungumzia makusanyo ya kipindi cha Robo ya Pili ya mwaka 2019/20 inayohusisha mwezi Oktoba, Novemba, na Desemba yenyewe, Kamishna Mkuu Mhede amesema kuwa, TRA imefanikiwa kukusanya jumla ya sh. trilioni 4.972 sawa na ufanisi wa asilimia 97.49 ya lengo la kukusanya jumla ya sh. trilioni 5.100.

“Makusanyo haya ya robo ya pili ya mwaka 2019/20 ni sawa na ukuaji wa asilimia 19.78 ikilinganishwa na kipindi kama hiki cha Robo ya Pili ya mwaka 2018/19 ambapo Mamlaka ilikusanya sh. trilioni 4.151 ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 87.59 kutokana na lengo la kukusanya mapato kiasi cha sh. trilioni 4.739 katika kipindi hicho,” alifanunua Kamishna Mkuu Mhede.

Ameeleza kuwa, kwa upande wa makusanyo ya mapato ya Serikali kwa mwezi Oktoba 2019, TRA ilikusanya kiasi cha sh. trilioni 1.484 na Novemba 2019, Mamlaka ilikusanya sh. trilioni 1.501 sawa na ufanisi wa asilimia 93.98 na asilimia 97.59 kutoka katika malengo ya kukusanya sh. trilioni 1.579 na sh. trilioni 1.538 kwa mwezi Oktoba na Novemba 2019.

Kamishna Mkuu Mhede ameongeza kuwa, makusanyo hayo ni muendelezo wa kiashiria cha wazi kwamba Walipakodi na Watanzania walio wengi wameendelea kuelewa, kukubali, na kuitikia wito wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kuongeza mapato ya ndani kwa ajili ya maendeleo ya Taifa zima. 

“Kwa kuwa Walipakodi wengi wameitikia wito wa kulipa kodi kwa mujibu wa Sheria, ni rai yangu kwamba asiwepo mlipakodi hata mmoja ambaye atathubutu kubaki nyuma. Ni busara wafanyabiashara wote wakaungana na kundi kubwa la Washindi, yaani, kundi kubwa la wanaolipa kodi kwa hiari, kwa ukamilifu, na kwa wakati, alisisitiza Dkt. Mhede.

Pia, amewashukuru walipakodi waliolipa kodi kwa wakati na hivyo kupelekea kuongezeka kwa makusanyo ambayo yatapelekea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.

“Kwa namna ya kipekee, napenda kuwashukuru Walipakodi wote waliolipa kodi ya Serikali na kupelekea Mamlaka kufikia makusanyo haya ya kihistoria kwa mwezi Desemba 2019. Pia, tunaishukuru sana Serikali ikiwa ni pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bodi ya Wakurugenzi ya TRA, Taasisi za Maendeleo, na Sekta Binafsi kwa kuendelea kuipatia TRA ushirikiano stahiki katika kutekeleza majukumu yake ya kukadiria, kukusanya, na kuhasibu mapato ya Serikali,” Alisema Kamishna Mkuu Mhede.

Aidha, ametoa wito kwa wamiliki wote wa majengo nchini kujitokeza kulipia kodi za majengo ili kuepuka usumbufu wa kulipa mwishoni mwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo amesema kuwa, kwa sasa viwango ni rafiki na vinalipika kwa urahisi.


Amevitaja viwango hivyo kwa mwaka kuwa ni sh. 10,000 kwa nyumba ya kawaida, sh. 50,000 kwa kila sakafu ya nyumba ya ghorofa katika Majiji, Manispaa, na Halmashauri za Miji, na sh. 20,000 kwa jengo la ghorofa katika maeneo ya Halmashauri za Wilaya.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MNADA WA FORODHA KWA NJIA YA MTANDAO

BRELA YAONGEZA MUDA WA KUHUISHA TAARIFA ZA MAKAMPUNI NA MAJINA YA BIASHARA


Washindi Promosheni ya Kishindo cha Funga Mwaka ya Tigo wakabidhiwa zawadi zao

$
0
0

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari . katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa promosheni ya Kishindo cha Funga Mwaka na Tigo.
“Tunapenda kuwashukuru sana wateja wetu wote ambao walishiriki kwenye promosheni hii lakini kwa leo tumeweza kuwapata washindi watatu ambao wanahitimisha promosheni hii ambayo ilifanyika nchi nzima na tulikuwa na washidi zaidi ya 331 ambao wameshinda milioni 500,” Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Mapema leo
“Mimi nimfanya biashara wa vifaa vya umeme hapa Dar es Salaam na mtaji wangu ni wa kawaida tu lakini kupitia ushindi huu naamini kabisa malengo yangu ya kumiliki biashara kubwa zaidi yatatimia.Nawashukuru sana Tigo kwa kuanzisha promosheni hii kwani ushindi huu utabadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa,”Mshindi wa kwanza Salum Biwi mkazi wa Manzese baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh20 milioni leo Januari 3, 2019.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akimkabidhi mfano Hundi Hamidu Mtabiage kutoka mkoani Lindi aliyeshinda Sh15 milioni alisema “Naishukuru sana Tigo Pesa kwasababu mimi ni mfanyabiashara mdogo wa vifaa vya pikipiki na kwa kushinda pesa hizi zitaniwezesha kukuza mtaji wangu kutoka kuuza vifaa hadi kuuza pikipiki kwani hii ni ndoto yangu ya muda mrefu.

Anna Mkongwa kutoka Dodoma ndiye mshindi wa tatu wa promosheni ya #KishindoChaFungaMwaka aliweka pesa kwenye Tigo pesa ili ashinde pesa.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Promosheni ya kishindo cha Funga Mwaka na Tigo , Mara baada ya kukabidhiwa hundi zao mapema leo.


Dar es Salaam. Huenda changamoto za Januari zikawa historia kwa baadhi ya washindi ambao wamejipatia fedha kupitia promosheni ya Kishindo cha Funga mwaka kutoka Kampuni ya Tigo (Tigo Pesa) jambo linalowaweka katika nafasi nzuri ya kukabiliana na mambo mbalimbali yanayojitokeza hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka.

“Nilipigiwa simu Jumatano iliyopita nikataarifiwa kwamba ni mshindi wa shillingi milioni 20m, kwa kweli sikuamini mpaka nilipoona jina langu katika mitandao ndio nikaamini. Nimshukuru Mungu kwani nilikuwa nina shiriki katika promosheni hii,kwa matarajio ya kwamba na mimi nitaibuka mshindi wa million hata moja,ili niweze kuongeza mtaji,kwa bahati nzuri nimeibuka mshindi wa kwanza wa shilling million 20” ndivyo alivosema Salum Biwi mkazi wa Manzese baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh20 milioni leo Januari 3, 2019.


Biwi ambaye ni mshidi wa kwanza wa Kampeni hiyo alisema ushindi huo ni mkubwa kwake na kwamba amejipanga kutumia fedha hizo kuongeza mtaji kwenye biashara yake ya sasa.

“Mimi nimfanya biashara wa vifaa vya umeme hapa Dar es Salaam na mtaji wangu ni wa kawaida tu lakini kupitia ushindi huu naamini kabisa malengo yangu ya kumiliki biashara kubwa zaidi yatatimia.Nawashukuru sana Tigo kwa kuanzisha promosheni hii kwani ushindi huu utabadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa,” alisema Biwi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema promosheni hiyo ilifanyika mwezi Desemba kwa lengo la kuwashukuru wateja kwa kutumia huduma ya Tigo Pesa kwa kipindi chote cha mwaka 2019.

“Tunapenda kuwashukuru sana wateja wetu wote ambao walishiriki kwenye promosheni hii lakini kwa leo tumeweza kuwapata washindi watatu ambao wanahitimisha promosheni hii ambayo ilifanyika nchi nzima na tulikuwa na washidi zaidi ya 331 ambao wameshinda milioni 500,” alisema Pesha.

Kwa upande wake Hamidu Mtabiage kutoka mkoani Lindi aliyeshinda Sh15 milioni alisema “Naishukuru sana Tigo Pesa kwasababu mimi ni mfanyabiashara mdogo wa vifaa vya pikipiki na kwa kushinda pesa hizi zitaniwezesha kukuza mtaji wangu kutoka kuuza vifaa hadi kuuza pikipiki kwani hii ni ndoto yangu ya muda mrefu.”

Naye, Anna Mkongwa aliyeshinda Sh10 milioni, alisema pamoja na kuwa yeye ni mtumishi wa Umma, fedha alizozipata zitamsaidia kutimiza malengo mbalimbali hasa mwanzo huu wa mwaka.
“Kiukweli pesa hizi ni nyingi na sikutegemea kama ningeshinda hivyo kwa sasa nitakachokifanya ni kuweka malengo vizuri na pesa hii itanisaidia kuyatimiza,” alisema Mkongwa mkazi wa Dodoma.

Mbali na washindi hao, Kampeni hiyo ilikuwa ikitoa zawadi kwa washindi 8 wa Sh1 milioni kila siku na washindi 8 wa Sh5 Milioni kila wiki na tayari wamekwisha pokea zawadi zao.

Vodacom Tanzania Plc yaendelea kusaidia wanafunzi kujisomea bila gharama kwa kutumia mfumo wa Instant schools

$
0
0

 Mratibu wa mradi wa Instant Schools Christine Lucas (Kulia) akimkabidhi zawadi mwanafunzi Zakati Athumani wa kidato cha tatu, shule ya Sekondari Kinyerezi baada ya kuwaelekeza kuhusu mfumo huo unavyosaidia wanafunzi kujisomea mahali popote bila gharama yeyote. Mfumo huo unatolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC kupitia Vodacom Tanzania Foundation.

DKT MPANGO AFUNGUA KIKAO KAZI CHA WAHASIBU WA SERIKALI NA KUZINDUA MFUMO MPYA WA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA ZA MAJUMUISHO LEO JIJINI DAR

$
0
0
Na Avila Kakingo, Michuzi Globu.

SERIKALI ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli imesema dhamira yake kubwa ni kuboresha mifumo  Bora ya Kielektroniki  ya ukusanyaji mapato na kuongeza uchumi kupitia mifumo ya Kielektroniki inayokidhi viwango vya kimataifa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mipango wakati akifungua Kikao kazi Cha wahasibu wa Serikali Cha siku tatu pamoja na kuzindua mfumo mpya wa Uandaaji wa taarifa za fedha za majumuisho,Kikao hicho kimewakutanisha wahasibu kutoka taasisi zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali.

Waziri mpango amesema mfumo huo utapunguza gharama kwa Serikali pamoja na kuongeza usahihi wa taarifa kwa majumuisho ya Fedha za Serikali.

"Mifumo mingi madhubuti ya ukusanyaji mapato na matumizi ya serikali imeanzishwa ikiwa ni pamoja na mifimo uabuhasibu na rasilimali za umma zenye kukidhi biwango vya kimataifa. "

"Niseme tuu kwamba hii ndio Tanzania ambayo Rais Magufuli anatamanikuifikia yaani nchi yetu iwe ya kwanza katika kila jambotunalolifanya".

Aidha amewapongeza wataaalamu walioweza kutengeneza mfumo huo ambao utaokoa Fedha nyingi, huku akitoa rai kwa vijana na wataalam wa mifumo hiyo walioajiriwa  kuwajengea zaidi maadili ya kiwahasibu lengo ikiwa ni kuboresha mifumo mingine Bora zaidi,huku akitoa onyo kwa wahasibu wote watakaokiuka maadili kwa kujihusisha na Rushwa watachukuliwa hatua za kusheria .

Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Fransis Mwakapalila alibainisha majukumu ya Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali  ambayo ni kuandaa taarifa za Fedha za majumuisho za Serikali na kuziwasilisha kwa mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya ukaguzi Kama ilivyo matakwa ya sheria ya fedha hivyo mfumo huo utasaidia kwa kiasi kukubwa

Aidha amesema kuwa  hatua ya kuandaa Hesabu za majumuisho kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki unafanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutayarisha Hesabu za Majumuisho kwa kutumia mfumo ulioandaliwa na wataalam wake wa ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango

Awali akimkaribisha Waziri Mpango Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Marry Maganga alisema kuwa siku zote wamekuwa wakiwasisitiza wahasibu kufanya kazi kwa uzalendo, ubunifu na kuachana na kufanya Mambo kwa mazoea hivyo kikao kazi hicho kitaleta mabadiliko makubwa.

Hata hivyo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango, amewapongeza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha na wote walioshiriki kufanikisha shughuli nzima ya mkutano huo.

Dkt Mpango ametoa rai kwa wahasibu wote nchini."Napenda nitoe rai kwenu kwamba, hakikisheni mafanikio haya tuliyoyapata yanakuwa endelevu. Pia, Hakikisheni kuwa usalama katika Mifumo yetu ya Fedha unakuwa madhubuti ili kuondoa uwezekano wa mifumo yetu kudukuliwa na kuleta hasara kubwa kwa Serikali na Wananchi".

Aidha amewakumbusha Wahasibu wote katika Utumishi wa umma kudumisha uadilifu na Uzalendo kwa nchi yetu.

Kikao kazi cha wahasibu wa Serikali kitadumu kwa muda wa siku tatu kikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa uwezo wa kutumia mfumo mpya wa kuandaa Taarifa za fedha za Majumuisho za Serikali (Government Accounting Consolidation System - GACS) ambao umetengenezwa na watalaam wa ndani.

 Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt  Philip Mpango akizungumza wakati akifungua Kikao kazi Cha wahasibu wa Serikali Cha siku tatu kilichowakutanisha wahasibu kutoka taasis zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali,leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmmi,Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango kufungua Kikao kazi  cha Wahasibu wa Serikali cha siku tatu kilichowakutanisha wahasibu kutoka taasis zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali,leo jijini Dar es Salaam.
  Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Fransis Mwakapalila akizungumza mbele ya Mgeni Rasmi ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Wageni waalikwa mbalimbali katika Kikao kazi Cha wahasibu wa Serikali cha siku tatu kilichowakutanisha wahasibu kutoka taasis zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali,leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahasibu kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani)
Sehemu ya wahasibu kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza,leo wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha Wahasibu wa Serikali cha siku tatu kilichowakutanisha wahasibu kutoka taasis zote za Serikali Kuu ,Halmashauri,Mashirika na taasisi nyingine za Serikali,leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ,jijini Dar es Salaam.

DCB yamahasisha watanzania kuifanya DCB Skonga suluhisho la elimu ya watoto wao.

$
0
0

  Balozi wa akaunti maalumu ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Hadija Kimaro (kushoto), akizungumza na wanafunzi waliofika katika banda la benki hiyo katika maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam hivi karibuni uhusu faida ya akaunti hiyo inayompa mteja uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu hata atakapopata majanga yatakayosababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.  
Balozi wa akaunti maalumu ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Neema Mziray (kulia), akizungumza na baadhi ya watu waliofika katika banda la benki hiyo katika  maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam hivi karibuni kuhusu faida na jinsi ya kujiunga na akaunti hiyo inayomhakikishia mteja uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi kufika chuo kikuu hata yanapotokea majanga yatakayosabisha ulemavu wa kudumu ama kifo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja wa kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance, Dk. Maria Janja na Mfanyabiashara wa Vyakula, Happy Lyimo.
 Balozi wa akaunti maalumu  ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Angel Joachim (wa tatu kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja waliofika maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam hivi karibuni kuhusu faida za akaunti hiyo inayompa mteja uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu hata itakapotokea majanga yatakayosababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.
 Balozi wa akaunti maalumu ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Irene William (kulia), akizungumza na wateja waliofika katika banda la benki hiyo katika maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam hivi karibuni  kuhusu faida za akaunti hiyo inayompa  mteja uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu hata atakapopata ulemavu wa kudumu au kifo. 

SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA SH. BILIONI 8.7 KUTOKA KWA MASHIRIKA NA TAASISI ZA UMMA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) (wapili kulia) akipokea gawio kutoka Kampuni ya Star Media ambayo imetoa gawio kwa mara ya kwanza tangu imeanza kufanyakazi nchini miaka kumi iliyopita, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Msajili wa Hazina, Bw. Athuman Mbuttuka na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji nchini, Dkt. Ayoub Rioba.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) (wapili kulia) akipokea gawio kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji mstaafu Damian Lubuva, katika hafla ya kupokea gawio kutoka kwa Mashirika, Kampuni na Taasisi za Umma 13, jijini Dodoma, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) akifafanua jambo wakati wa hafla ya kupokea gawio kutoka kwa Mashirika, Kampuni na Taasisi za Umma 13, jijini Dodoma, ambapo aliwahakikishia watanzania kuwa fedha hizo zitatumika kuboresha maisha ya wananchi wa hali ya chini.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akielezea kuwa ongezeko la maduhuli na michango kwa asilimia 552 kuwa ni ishara kuwa Tanzania imeamua kusimamia vema rasilimali zake, wakati wa kupokea gawio kutoka kwa Mashirika, Kampuni na Taasisi za Umma 13, jijini Dodoma.
 


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) (katikati), Naibu wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wapili kushoto), Manaibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Mary Maganga na Bw. Adolf Ndunguru (kushoto) pamoja na Msajili wa Hazina, Bw. Athuman Mbuttuka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Mashirika, Kampuni na Taasisi za Umma zilizotoa gawio la jumla ya Sh. Bilioni 8.7, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) na Naibu wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) wakifurahia jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jaji mstaafu Damian Lubuva, muda mfupi baada ya kupokea gawio kutoka kwa Mashirika, Kampuni na Taasisi za Umma 13, jijini Dodoma.



(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM)

………………

Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali imepokea gawio na michango ya Sh. bilioni 8.7 kutoka kwa baadhi ya Mashirika, Kampuni na Taasisi za Umma, ikiwa zimebaki siku 15 kati ya siku 60 zilizotolewa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, za kuzitaka Taasisi, Kampuni na Mashirika hayo kutoa gawio kwa Serikali.

Gawio hilo limepokelewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango katika hafla iliyowakutanisha Wakuu wa Mashirika, Kampuni na Taasisi za Umma 13, jijini Dodoma.

Dkt. Mpango amewaagiza, Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi, Kampuni na Mashirika ya Umma ambao hawatatoa gawio ifikapo Januari, 23 saa sita usiku kujiondoa katika nafasi zao na wasisubiri barua.

Alisema kuwa ni vema kuhakikisha watu waliopewa dhamana katika Taasisi na Mashirika ya Umma wanatumia rasilimali zilizopo katika kuiwezesha Serikali kujitegemea kuliko kutegemea wafadhili ambao kwa sasa wanapeleka nguvu kubwa katika nchi zao.

“Nawahakikishia kuwa fedha hizi zilizopokelewa katika Mfuko Mkuu wa Hazina zitatumika kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi masikini kwa kuwa Taasisi za umma zilianzishwa ili uwekezaji wake uwanufaishe wananchi na Taifa kwa ujumla”, alieleza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango amezishukuru Taasisi, Kampuni na Mashirika ya Umma kwa kutii agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Novemba 24, 2019 lililozitaka taasisi hizo kutoa gawio ndani ya siku 60.

Alisema kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) liliingia ubia na Kampuni ya Star Media ya China kwa kipindi cha miaka kumi na kwa mara ya kwanza Kampuni hiyo imetoa gawio kwa Serikali la kiasi cha Sh. milioni 500, jambo ambalo linapaswa kusifiwa hasa kwa uongozi wa TBC ulio saidia kufanikisha jambo hilo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alisema kuwa ongezeko la maduhuli na michango kutoka kwenye Taasisi za umma kwa zaidi ya asilimia 552, sio jambo dogo na inatoa tafsiri kwa ulimwengu kuwa Tanzania sio masikini na sasa imeamua kusimamia rasilimali zake.

Alisema kuwa ni muda wa kuwaambia wananchi kuwa ni wakati wa kufaidika na fedha zao za ndani ambazo Serikali yao iliwekeza kwa kuwa Rais ameamua kutumia rasilimali za Taifa kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.

Naye Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka, alisema kuwa kati ya Taasisi 187 ambazo hazikutoa gawio na michango kabla ya agizo la Rais la Novemba 24 mwaka jana, tayari Taasisi 151 zimetoa gawio na michango hiyo hadi kufikia Januari 7, 2020.

Alisema kuwa mpaka sasa jumla ya Sh. bilioni 20.8 zimepokelewa katika Mfuko Mkuu wa Hazina, ambapo awamu ya kwanza katika kipindi cha kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 11, zilipokelewa Sh. bilioni 12.1 na awamu ya pili kuanzia Disemba 12 mwaka jana hadi Januari 7 mwaka huu zimepokelewa Sh. bilioni 8.7.

Bw. Mbuttuka, alisema kuwa taasisi ambazo bado hazijatoa gawio na michango ni 36, hivyo kuzitaka kuhakikisha zinatekeleza agizo la Rais la kutoa gawio hilo kwa kuwa ifikapo Januari, 23, 2020 saa sita usiku Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Taasisi, Kampuni na Mashirika ya Umma wasiotekeleza hawatakiwi kuingia ofisini.

Miongoni mwa Taasisi zilizowasilisha gawio na michango ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Chuo cha Ushirika Moshi, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Star Media, Bodi ya Utalii, Shirika la Maendeleo la Taifa na Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB).

Zaidi ya Sh. trillion 1.2 zimekusanywa kutoka katika Taasisi, Kampuni na Mashirika ya Umma 230 ikiwa ni gawio na michango mbalimbali kuanzia Novemba 24 mwaka jana hadi Januari 7, mwaka huu.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images