Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

Benki ya Exim Yaibuka Kinara Tuzo ya Mwajili Bora 2019.

$
0
0
Benki ya Exim Tanzania imeendelea kuwa kinara kwenye Tuzo za Mwajili Bora (EYA) za mwaka 2019 baada ya kutwaa Tuzo ya mshindi wa jumla ya Mwajili Bora kutoka ndani ya nchini ya mwaka 2019 zilizoandaliwa na kutolewa na Chama cha Waajili Tanzania (ATE) katikati ya wiki hii.

Mbali na tuzo hiyo ilishuhudiwa pia benki hiyo ikiibuka kinara kwenye Tuzo ya mshindi wa jumla ya Ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi ya mwaka 2019 sambamba na kutangazwa kuwa miongoni mwa waajili kumi bora hapa nchini kati ya waajili 800 walioshiriki kuwania tuzo hiyo.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika jijini Dar es Salaam ikipambwa na uwepo wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Mkuu wa Idara wa Rasimali watu wa benki hiyo Bw Frederick Kanga alisema tuzo hiyo ni kiashiria tosha mbele ya jamii kuhusiana na namna ambavyo benki hiyo imewekeza kwenye rasilimali watu, hatua ambayo ina umuhimu mkubwa katika kufanikisha malengo ya benki hiyo.

“Tuzo zote hizo tatu ni heshima kubwa kwetu na ni matokeo ya uwekezaji wa muda mrefu ambao tumekuwa tukiufanya kwa rasilimali watu kwenye taasisi yetu katika kuwasaidia waweze kutoa mchango wao kiutendaji katika ubora tunaoutarajia na ikibidi zaidi ya matarajio’’ alibainisha Bw Kanga.

Aliongeza kuwa moja ya vipaumbele vya benki hiyo ni pamoja na kuwaandaa watendaji wake kwa kuwaongezea ujuzi unaowawezesha kuwa mbele ya wakati katika utendaji wao ili kuleta matokeo bora na yenye ubunifu mpya kwa wateja.

“Lengo ni kuifanya taasisi yetu iwe sehemu ambayo mfanyakazi anakuwa bora zaidi, mwenye mabadiliko na mwenye utofauti,’’ alisisitiza.

Katika tuzo za hizo kwa mwaka huu zaidi ya waajili 800 kote nchini walishiriki kuwania tuzo mbalimbali ikilinganishwa na idadi ya waajili 150 tu walioshiriki mwaka jana.

Kwa mujibu wa Bw Kanga benki hiyo imedhamilia kuandaa wafanyakazi wenye ushirikiano katika kuunda timu imara ya pamoja kwa kuandaa mazingira ambayo wafanyakazi hao watajihisi kuwa wanathaminiwa, wanashirikishwa sambamba na kupewa fursa ya kukua na kujiendeleza kitaaluma.
Muonekano wa Tuzo Ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi ya mwaka 2019 ambayo ilikabidhiwa kwa Benki ya Exim Tanzania wakati wa hafla hiyo.


Mkuu wa Idara wa Rasimali watu wa benki ya Exim Tanzania, Bw Frederick Kanga (wa pili kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo wakifurahia baada ya kutwaa Tuzo ya mshindi wa jumla ya Mwajili Bora kutoka ndani ya nchini ya mwaka 2019 pamoja na Tuzo ya mshindi wa jumla ya Ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi ya mwaka 2019 zilizoandaliwa na kutolewa na Chama cha Waajili Tanzania (ATE) jijini Dar es Salaam katikati ya wiki hii.

MKOA WA MOROGORO KUPATA CHANZO CHA MAJI CHA UHAKIKA –NAIBU WAZIRI WA MAJI AWESO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Milima ya Ulugulu ,Morogoro

MKOA wa Morogoro hivi karibuni itaondokana na tatizo la maji kutokana na kupata chanzo cha uhakika kutoka milima ya Ulugulu katika eneo la Hululu ambapo bwawa la Mindu litatumika kama ziada ya Maji.

Chanzo cha maji hicho kimefikiwa na Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso wakati alipokwenda kuangalia chanzo hizo na Watendaji wa Bonde la Wami/Ruvu pamoja na Mamlaka ya Safi na Mazingira (Moruwasa).

Katika ziara ya Naibu Waziri Aweso aliwaagiza na Watendaji wa Bonde la Wami/Ruvu pamoja na Mamlaka ya Safi na Mazingira (Moruwasa) kuandika andiko kwa kina ili kuwekeza miundombinu katika chanzo cha maji cha milima Ulugulu katika eneo la Hululu.

Viongozi wa eneo la chanzo cha maji walieleza kuwa Naibu wa Waziri huyo ni kiongozi wa kwanza kufika eneo la chanzo cha maji tangu dunia iiumbwe na kudai kuwa serikali ya awamu ya Tano ina udhubutu wa viongozi katika utendaji wa kuhakikisa wananchi wa Mkoa wa Morogoro wanaondokana na tatizo la maji.

Naibu Waziri Aweso amesema kuwa kutokana na chanzo cha maji hayo kuwepo kwa muda wote kulikuwa hakuna sababu ya kutumia Bwawa kwani mabwawa huwekwa sehemu ambayo ni kame hivyo mkoa wa Morogoro si Kame kwa kuwa na chanzo cha maji kinachotegemea bwawa.

Amesema kuwa chanzo hicho cha maji katika milima ya Ulugulu ni kufikisha Morogoro ni jirani ukilinganisha na mradi wa maji wa Ziwa Victoria kutolewa mwanza na kwenda katika mikoa mbalimbali ambayo ilikuwa na ukame wa maji na hawakujua watapata katika chanzo kipi.

Nae Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani alimweleza kuwa chanzo hicho kinatokana na utunzwaji wa mazingira na kutaka wananchi waendelee kulinda vyanzo vya maji.

Ngonyani amesema kuwa kuna miradi mbalimbali ya miundombinu katika Mkoa wa Morogoro lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji na kwenda kwa kasi katika ujenzi wa viwanda ambavyo kuendelea kwake kunatokana na upatikanaji wa maji.

Mhandisi Ngonyani amesema kuwa wanapokea maagizo ya Naibu Waziri Juma Aweso na kuahidi watafanyia kazi kwa kuandika andiko la mradi kwa kushirikiana na Moruwasa ikiwa chanzo hicho kuanza kufanyiwa kazi.

“Ninaamini chanzo hiki kitakuwa mkombozi kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro na kuwa historia kutegemea bwawa kwa mkoa wenye vyanzo vya maji Lukuki hivyo bonde litaendelea kuhakikisga vyanzo vya maji vinalindwa vizazi kwa vizazi”amesma Ngonyani.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mwalimu Mohamed Utaly amesema kuwa chanzo cha maji hicho kwa Mkoa wa Morogoro kwa serikali ya awamu chanzo cha maji kitajengwa.


Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akipumzika na viongozi mbalimbali wakati kupanda mlima wa kufikia chanzo cha maji katika eneo Hululu.

Sehemu ya chanzo ambapo mtambo utajengwa kwa ajili ya maji katika mkoa wa Morogoro.

Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kuangalia chanzo cha maji cha Milima ya Ulugulu katika eneo la Hululu ambapo mitambo itajengwa kwa ajili ya kusambaza maji katika mkoa wa Morogoro.


Mhandisi wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza kuhusiana na umuhimu chanzo cha maji cha uhakika kwa mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso ya kwenda kuangalia chanzo hicho cha maji. 

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mwalimu Mohamed Utaly akizungumza na wananchi wa kata ya Bunduki kuhusiana na umuhumu wa utunzaji wa vyanzo vya maji wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso ya kwenda kuangalia chanzo hicho cha maji.
Watendaji wa Bonde la Wami/Ruvu na Mamlaka ya Maji Safi na Mazingori mkoa wa Morogoro wakwapungia wananchi wa kata ya bunduki wakati mkutano uliolenga utunzaji wa vyanzo vya maji kuzuka maeneo yao.
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akiteta jambo na watendaji na viongozi wa kata

Legendary Expeditions kuvutia watalii maarufu duniani ,Kambi tatu za watalii maarufu kujengwa

$
0
0





Mwandishi wetu.Serengeti

Arusha.Sekta ya Utalii nchini, inatarajiwa kuimarika zaidi kutokana na uwekezaji wa zaidi ya sh 6 bilioni katika ujenzi wa hoteli za kitalii na kambi tatu za kitalii za wageni maarufu eneo la Serengeti na pori la akiba la Maswa ili kukuza sekta ya utalii nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwiba Holdings na Friedkin Group,Jean Claude, akizungmza katika uzinduzi kambi ya kitalii ya Mila,ambayo inatarajiwa kuanza kupokea watalii katika eneo la serengeti na kupunguza tatizo la vitanda kwa watalii amesema ni faraja kubwa kwao kuendelea kutoa mchango mkubwa katika sekta ya utalii nchini .

Amesema uzinduzi wa kambi hiyo, utafatiwa na kambi nyingine mbili za kitalii ambazo zitakuwa katika maeneo ya Kaskazini mwa Serengeti pia na pori la akiba la Maswa ambapo, kampuni hiyo imewekeza.

Claude alisema Mwiba holdings hadi sasa imewekeza kiasi cha dola 3 na tayari imetoa ajira kwa watu 120 katika maeneo iliyowekeza kaskazini mwa hifadhi ya Serengeti na eneo la pori la akiba la Maswa.

Alisema kuanzishwa kambi hizo za kitalii,ikiwa pia ni mkakati wa kuendeleza uhifadhi na utalii endelevu wa taasisi ya friedkin Conservation Fund(FCF) katika eneo la ikolojia ya serengeti na maeneo mengine nchini.

amesema ujenzi wa kambi, kutaongeza vitanda 50 vya watalii lakini pia mchango wa kampuni hizo katika sekta ya Utalii utaongezeka zaidi.

Amesema ujenzi wa kambi hizi kutaongeza vivutio vya watalii hasa kutokana na huduma nyingine ambazo zimekuwa zikitolewa kutalii kwa kutumia chopa kuona wanyama mbali mbali katika ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania.

Alisema uwekezaji wa kampuni zilizochini ya friedkin utaendelea kuwa na faida na manufaa makubwa kwa watanzania wote kwa kuzingatia uadilifu na hivyo kiunua sekta ya utalii nchini.

Kampuni za Friedkin zimewekeza maeneo mbali mbali nchini, katika utalii wa picha, uwindaji wa kitalii na masuala ya uhifadhi wa mazingira,wanyamapori na kutoa misaada mbali mbali za kijamii.

ELIMU YA KUJIKINGA, KUUTAMBUA UGONJWA WA EBOLA YATOLEWA KWA VIONGOZI KUTOKA KADA MBALIMBALI JIJINI DAR

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imeamua kuandaa mafunzo maalumu yanayohusu namna ya kutambua na kujikinga na ugonjwa wa ebola kwa makundi ya kada mbalimbali ikiwemo ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala, viongozi wa dini na wasanii.

Lengo na kutolewa mafunzo hayo kwa makundi hayo ni kuhakikisha yanajengewa uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huo ili wawe mabalozi ambao watakuwa na jukumu la kutoa elimu hiy kwa jamii ya Watanzania kama hatua muhimu za kukabiliana na ugonjwa huo hatari waebola ambao kimsingi haujaingia nchini lakini baadhi ya nchi jirani ikiwemo ya Jamhuri ya Democrasia ya Congo ugonjwa huo upo na umesababisha watu kupoteza maisha.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Mratibu wa utoaji elimu ya ugonjwa wa Ebola ambaye pia ni Mratibu wa elimu ya Afya katika Shule za Mkoa wa Dar es Salaam Dk.Ndeniria Swai amesema sababu za kukutana na viongozi hao wa makundi hayo ni kuendelea kuoa elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola, ambao bado haujaingia nchini Tanzania lakini nchi za jirani na tanzania zimekuwa zikiripotiwa kuwa na wagonjwa wengi wa ebola hususani nchi ya Congo.

"Nchi ya Congo ambayo imekuwa na wagonjwa wa Ebela imekuwa na muingilia mkubwa na nchi ya Tanzania na hiyo inatokana na raia wengi wa nchi ya Congo wamekuwa wakija jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kununua bidhaa.Watanzania nao wanatoka Dar es Salaam na kwenda Congo kufanya biashara.

"Wapo wengine ambao wanakwenda kwa ajili ya kupeleka magari ya mafuta na wengine wamekuwa wakipeleka vyombo vya moto na wakati huo huo wapo raia wa Congo ambao wanakuja nchini Tanzania kwa ajili ya mikutano mbalimbali na Watanzania nao wanakwedna huko kwenye mikutano, hivyo muingiliano ni mkubwa na hivyo nchi yetu kuwa hatarini kupatwa na ugonjwa huo,"amesema Dk.Swai.

Amesema hivyo Wizara ya Afya, imeona kuna kila sababu sasa Watanzania wote wakapewa elimu kuhusu ugonjwa Ebola na kuongeza wizara hiyo inapenda kila mtanzania mwenye uwezo wa kuelewa afahamu kuhusu ugonjwa wa ebela, afahamu dalili na kubwa zaidi afahamu namna ya kujikinga ili kuepuka maambukizi.

"Hivyo leo hii tumeita viongozi mbalimbali wakiwamo wakurugenzi , wakuu wa wilaya, makatibu tawala , tumeita viongozi wa afya ngazi ya halmashauri , viongozi wa dini, wanamichezo , wasanii, wakurugenzi wa taasisi wanaosimamia usafiri wa anga, majini nchi kavu, mameneja wanaosimamia vituo vya mabasi ubungo na wadau wengine.Tunapenda kila mmoja kupata nafasi hiyo ili wawe mabolozi ambao watatoa elimu sahihi kuhusu ugonjwa wa Ebola.

"Elimu hiyo itahusu kuwa na uelewa kuhusu nini maana ya ebola nini, inapatikana vipi, namna gani ya kutoa taarifa ya ugonjwa huo katika sehemu sahihi na jinsi gani mgonjwa wa ebola anaweza kusaidiwa.Hivyo viongozi wa Serikali watapeleka ujumbe, viongozi wa dini nao watapeleka ujumbe, tunataka wasanii nao wawe sehemu ya kutao elimu hiyo kwa kutunga nyumba,"amesema.

Ameongeza kuwa mlipuko wa kumi tangu ugonjwa umeanza lakini nchi yetu ina kila sababu ya kuchukua hatua ili kujikinga ebola isiingie nchini na hiyo itawezekana kwa kuhakikisha elimu sahihi kuhusu ugonjwa huo inafika kwa jamii ikiwa sahihi.

Kwa upande wake Oscar Kapela ambaye anatoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Kitengo cha elimu ya afya kwa umma ambacho kipo chini ya idara ya kinga amesema lengo na mafunzo hayo ni kuhusu elimu ya ebola, lakini ni mafunzo ambayo yanalenga kushirikisha jamii ili iweze kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo.

"Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa mpana kuhusu ugonjwa wa ebola , jinsi gani ya kujikinga,tunafahamu kuwa kinga ni bora kuliko tiba. Elimu imezidi kutolewa kwa njia mbalimbali, na waandishi wamekuwa wakifikisha elimu hiyo, elimu tunataka ifike nyumba kwa nyumba,"amesema.

Wakati huo huo Simon Kadogosa ambaye anatoka Taasisi ya Tanzania Red Cross amesema wameungana na Serikali katika kampeni hiyo ya kutoa elimu ya uelewa kuhusu namna ya kujikinga na ugonjwa ebola kwa kuanza na viongozi 

"Red cross tuko pamoja na Serikali kwa kila hatua kuhakikisha lengo linafikiwa na ukweli baadhi ya nchi jirani zinakabiliwa na ugonjwa huo , hivyo lazima jamii ya watanzania wajue na wafahamu namna ya kujikinga kwa kuchukua tahadhari,"amesema na kuongeza ugonjwa huo upo nchi za Congo, sudan, sera lioni pamoja na baadhi ya nchi ambazo zimeendelea kupata shida ya Ebola.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Tegeta Wazo Hili jijini Dar es Salaam Richard Hananja amesema mafundisho kuhusu ugonjwa wa ebola ni muhimu kwao ili nao kutoa elimu hiyo kwa waumini wao.

Amesema katika Tanzania ya viwanda, yeye kama kiongozi wa dini, kiwanda chake ni waumini ambao anawaongoza Kanisani na hivyo lazima waumini hao wawe wenye afya iliyobora na hivyo elimu ambayo wameipata watahakikisha inafika kwa jamii wanayoingoza.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni kiongozi wa dini kutoka Kigamboni Seif Muyenga amesema kwa kweli mafunzo hayo ni muhimu katika maisha ya mwanadamu na wao kama viongozi wa dini na wajumbe wa kamati ya amani ni lazima wayapokee mafunzo hayo kwa mikono miwili na kufanyia kazi.

"Kama mwili hauna amani maana yake hata amani kwenye jamii haitapatkana. Mwili ukiumwa akili nayo haitafanya kazi na hivyo amani haitakuwepo.Hivyo baada ya kupata mafunzo hayo tutakwenda kuyafikisha kwa waumini na jamii kwa ujumla .Kwa kweli ugonjwa huo ni mkubwa na tishio kwa ulimwengu, hivyo kinga ni bora kuliko tiba.

"Na moja ya kinga ni mafunzo ambayo yametolewa ambayo yatasaidia jamii kujikinga, gharama za kutibu ugonjwa huo ni kubwa, hivyo nitoe pongezi kwa walioandaa mafunzo haya kwetu kwan wamefanya jambo lenye tija kubwa , nasi tutaenda kuisambaza elimu hii kwa wengine na nitoe ombi tunaomba mafunzo hayo yatolewe kwa makundi mengine ambayo kwa leo hawakuwpo hapa,"amesema.
 Mratibu wa utoaji elimu ya ugonjwa wa Ebola ambaye pia ni Mratibu wa elimu ya Afya katika Shule za Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Ndeniria Swai akielezea namna Ugonjwa wa Ebola unavyoambukizwa kwa binadamu na njia za kujikinga na ugonjwa huo hatari
  Mratibu wa utoaji elimu ya ugonjwa wa Ebola ambaye pia ni Mratibu wa elimu ya Afya katika Shule za Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Ndeniria Swai akielezea namna mgonjwa aliyekumbwa na Ugonjwa wa Ebola anavyokuwa baada ya kuathiriwa na ugonjwa huo na hatua za kuchukua kuhakikisha ugonjwa huo hausambai kwa mtu mwingine.
 Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam,Bi Spora Liana akizungumza jambo huku akiwashukuru viongozi mbalimbali wa Dini na kada nyinginezo waliofika kwenye Mafunzo maalumu yanayohusu namna ya kutambua na kujikinga na ugonjwa wa Ebola . 

Viongozi kutoka Kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini wakimsikiliza kwa makini  Oscar Kapela ambaye ni mratibu Kitengo cha elimu ya afya kwa umma ambacho kipo chini ya idara ya kinga katika Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mratibu Kitengo cha elimu ya afya kwa umma ambacho kipo chini ya idara ya kinga katika Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Oscar Kapela akifafanua jambo kwenye mkutano huo uliondaliwa makhususi kwa mafunzo maalumu yanayohusu namna ya kutambua na kujikinga na ugonjwa wa ebola kwa makundi ya kada mbalimbali ikiwemo ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala, viongozi wa dini na wasanii. 

 Viongozi kutoka Kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo muhimu katika kutoa Mafunzo maalumu yanayohusu namna ya kutambua na kujikinga na ugonjwa wa ebola kwa makundi ya kada mbalimbali ikiwemo ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala, viongozi wa dini na wasanii. 


NBC YAZINDUA KAMPENI YA BIMA YA MAGARI KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU KWA KUSHIRIKIANA NA SANLAM.

$
0
0

Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Mauzo wa Total, Marieme Sow (kushoto kwake), wakionyesha kadi ya kuwekea mafuta ya Total wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayofanyika kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka, Meneja Masoko wa Sanlam, Marco Yambi, Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total, Marsha Msuya na Meneja Mahusiano Kitengo cha Bima cha NBC, Kuruthum Mwaluwinga.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (kushoto), akikabidhi kadi ya kujazia mafuta ya Total kwa  mteja wa kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Danford Robert Buguru wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoangalia ni wawakilishi kutoka NBC, Sanlam na Total.
Mkuu wa Kitengo cha Bima cha Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kushoto), akikabidhi zawadi mbaimbali kwa  mteja wa kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Robert Danford Buguru, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoangalia ni wawakilishi kutoka NBC, Sanlam na Total.
 Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (katikati), akisaidia kuweka mafuta ya ofa katika gari la mteja wa kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Robert Danford Buguru (kulia), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Nyuma yake ni Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka.

Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni iliyozinduliwa na NBC kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka, Meneja Masoko wa Sanlam, Marco Yambi na Mkurugenzi wa Mauzo wa Total, Marieme Sow.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC, David Raymond (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ambapo NBC ilizindua kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana.  

KAMPENI YA MASTABODA YAZIDI KUNOGA,WASHINDI NANE WAIBUKA NA ZAWADI ZA KISIMUJANJA

$
0
0
 MENEJA Mwandamizi wa Idara ya Kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala, akimkabidhi zawadi ya simu mpya aina ya Tecno Pop 2 dereva wa Bodaboda kituo cha Buguruni Rozana, Mohamed Abdallah, baada ya kuibuka mshindi wa kufanya miamala ya kibenki zaidi ya 200 kwa mwezi kulipwa nauli na abiria wake kwa kutumia huduma mpya ya Master Boda QR, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi za washindi iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa Idara ya Bidhaa za Kadi, Lupia Matta na Mwenyekiti wa    Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dar es Salaam, Michael Massawe. 

KAMPENI ya MastaBoda imezidi kushika kasi kwa kungia hatua ya pili ya utoaji wa zawadi za Simujanja kwa washindi nane wa awamu ya kwanza kujishindia Simujanja 'smartphone'.

MastaBoda ni kampeni  inayoendeshwa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuwaunganisha waendesha Bodaboda katika mfumo wa kibenki wa kupokea malipo kwa Mastercard QR kutoka  kwa wateja wa Benki ya NMB, Benki zilizounganishwa na Mastacard QR pamoja na mitandao ya simu iliyounganishwa na huduma ya Mastercard QR.

Zoezi hilo la utoaji wa zawadi limeendeshwa jana Makao Makuu ya NMB na Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa za Kadi, Lupia Matta.

Matta amesema NMB imejipanga kuwafikia waendesha Bodaboda elfu 75 Tanzania nzima, kwa lengo la kulasimisha biashara ya usafiri wa Bodaboda.

"Tunaenda kufanya kundi la waendesha Bodaboda kuwa kundi maalum linaloheshimika katika nyanja ya usafirishaji."Kupitia MastaBoda waendesha Bodaboda wanaenda kunufaika na mifumo ya kifedha inayotolewa na benki yetu. " amesema Matta.

Aidha Matta amebainisha kuwa wataendelea kutoa zawadi za Simujanja kwa wshindi wanaofikisha miamala zaidi ya 200 kwa mwezi mmoja na wale wanaofikisha miamala 50 kwa wiki wataendelea kujishindia elfu 50, huku zawadi kubwa ya Bodaboda aina ya Boxer zikitarajiwa kutolewa kuanzia Januari 2020 kwa washindi watakao fikisha miamala 600.

Washindi nane walioibuka na Simujanja ni John Haonga (Mabibo), Abdallah Maulid (Morroco),  Florian Calestine (Rozana), Twalha Ally (Rozana),  Mohammed Abdallah (Rozana),  Ebenezer Elisha (Mwenge), Ladislaus Abel (Ubungo) na Adam Gunza (Mlimani).

Kishindo cha Funga mwaka’ ya Tigo yaendelea kutoa Zawadi

$
0
0

Mshindi wa 5m/- wa promosheni ya Kishindo cha Funga mwaka Emmanuel Mwaijumba akipokea mfano wa hundi kutoka kwa balozi wa kampeni hiyo Meena Ally jijini Dar es Salaam. 

Dar es Salaam. Emmanuel Mwaijumba, ambaye ni mkazi wa Mikocheni, Dar es Salaam amejinyakulia zawadi ya Sh Milioni 5 kupitia kampeni ya ‘Kishindo cha Funga Mwaka’ inayofanywa na Kampuni ya Mawasiliano Tigo. 

Kwa kupitia kampeni hiyo, mkuu wa kitengo cha bidhaa cha Tigo Pesa, James Sumari amesema kampuni yao imetenga zawadi zenye thamani ya Sh Milioni 500 kwa wateja 331 nchi nzima wanaoweka na kupokea pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa. 

Ili kushiriki alisema, mteja wa tigo pesa anatakiwa kuweka miamala inayoanzia Sh 10,000 kwenye akaunti yake ya Tigo Pesa kupitia kampeni hiyo maalumu kwa ajili ya msimu huu wa kufunga mwaka itakayodumu kwa mwezi mmoja. 

“Wateja wanatakiwa kuweka pesa kwa Wakala au kupokea pesa kwenye akaunti zao za Tigo, Pesa kutoka benki, mitandao mingine au vyanzo vingine mbalimbali na moja kwa moja watakuwa kwenye nafasi ya kushinda,” alisema. 

Alisema kwa kupitia kampeni hiyo kutakuwa na washindi watatu wa mwezi watakaoibuka na zawadi ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wa kwanza, Sh Milioni 15 wa pili na Sh Milioni 10 wa tatu huku kila wiki ikitoa washindi nane wa Sh Milioni 5 kila mmoja na wengine nane wa Sh Milioni moja kila siku. 

Akishuruku kwa zawadi hiyo, Mwaijumba ambaye ni mfanyabiashara alisema atatumia kiasi hicho cha kukuza biashara yake ili kipato atakachopata kutokana na mauzo atakayokuwa akiyafanya kisaidie kuchangia kipato cha familia na kulipia ada za shule 

Mpaka sasa promosheni imeshawazawadia washindi zaidi ya 20 wa wiki, na zaidi ya 120 wa kila siku. 


Vijana waaswa kwenda kwa kasi na Tehama-Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

$
0
0
*TCRA yawapongeza Wanafunzi wa walioshiriki Shindano la Usalama wa mitandao

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ni Teknolojia ambayo inabadilika kila siku hivyo kunahitaji mafunzo katika usalama wa mitandao.
Hayo ameyasema Mwakilishi wa Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Richard Mgema wakati kufunga Shindano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini la Usalama wa Mitandao lililoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Kushirikiana na Kampuni ya Nchini Kenya lilofanyika Jijini Dodoma.

Mgema amesema kuwa Dunia iko katika mabadiliko ya Tehama kila siku ambapo Tanzania hatuwezi kuwa kisiwa cha kutoendana na Teknolojia hiyo.
Amesema Wanafunzi walioshiriki Shindano hilo wamekwenda katika mchujo mbalimbali hivyo washindi watakwenda kushindana na nchi nyingine katika suala la ulinzi katika mitandao.

Aidha amesema kuwa kama nchi kumekuwa na mabadiliko ya huduma za fedha kwenda katika mitandao hivyo vijana wengi wanahitajika kuhusiana na kujua mifumo ya ulinzi wa mitandao ili Fedha za Wananchi ziwe salama.
Amesema Tehama ukuaji wake ni kasi kutokana na mifumo ya kiteknolojia kubuniwa hivyo lazima kuwapo kwa Rasilmali Watu ya kwenda kwa kasi katika Teknolojia hizo.

Nae Mkuu wa Kanda ya Kati wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Antonio Manyanda amesema kuwa wakati wa usajili wa Shindano la Usalama wa Mitandao Wanafunzi wa Vyuo Vikuu walikuwa 1056 baada ya mchujo wa Kwanza walipatikana Wanafunzi 600 na mchujo wa Tatu walipatikana Wanafunzi 50 katika Vyuo Vikuu Nane.

Manyanda amesema kuwa Wanafunzi hao waliokuwa wanashiriki Shindano hilo walikuwa ni wale wanaosoma Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT) na umri wao kati ya Miaka 18 hadi 24.

Amesema walioshiriki wote ni washindi kwani wamepita katika Makundi mbalimbali hadi kufika hatua ya mwisho ya kupatikana kwa washindi wawili.Mkurugenzi wa Tehama wa TCRA Connie Francis amesema kuwa katika Shindano hilo amegundua wasichana hawako nyuma kwani wanashiriki Shindano hilo.

Amesema kuwa dunia haijabagua wanawake kuwa kuna vitu vya kufanya wanaume tu.Amesema walioshiriki waendelee kusoma kwa bidii kwa kuleta mabadiliko katika Tehama kwa dunia ndio iliko huko.

Washindi wa Shindano hilo wa Kwanza ni Godwin Mpapalika na Mshindi wa Pili Karim Muya.
 Mshauri wa Maendeleo ya Biashara wa Silensec wa nchini Kenya Kapere Ndege akitoa mafunzo kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu walioshiriki Shindano la Usalama wa Mitandao.
 Mgeni rasmi wa kufunga Shindano la Usalama wa mitandao wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Richard Mgema akimkabidhi cheti cha  Mshindi wa Kwanza katika Shindano la Usalama wa mitandao kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Godwin Mpapalika lililofungwa Mjini Dodoma.
 Mgeni Rasmi wa Mafunzo ya Usalama wa Mitandao wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Richard Mgema akimkabidhi cheti cha mafunzo katika Shindano la Usalama wa Mitandao Nasra Mohamed lililoandaliwa na TCRA .
 Mkurugenzi wa Tehama wa TCRA Connie Francis akiwa na washiliki wasichana wa Shindano la Usalama wa mitandao   Vyuo vikuu
 Mkuu wa Kanda ya Kati wa TCRA  Antonio Manyanda akizungumza kuhusiana na utaratibu uliotumika kupata washiriki wa Shindano la Usalama wa mitandao kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu lililifungwa mjini Dodoma.
Washiliki wa Mafunzo ya Shindano la Usalama wa mitandao kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu.

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA BANDARI YA KASANGA,KASI UJENZI WA MIUNDOMBINU YASHIKA KASI

$
0
0
 Shughuli za ujenzi wa miundombinu ukiendelea katika Bandari ya Kasanga mkoani Rukwa.Bandari hiyo ni ya pili kwa ukubwa katika bandari zilizopo ndani ya Ziwa Tanganyika ambapo TPA imeamua kuboresha miundombinu yake.

 Sehemu ya upanuzi wa gati ya bandari ya Kasanga ukiendelea kwa kuwekwa mawe ya kokoto na nondo 

 Baadhi ya mafundi wakiwa wamebaba mawe kwa ajili ya kwenda kuweka eneo ambalo ujenzi wa gati ya bandari ya Kasanga unaendelea katika eneo hilo.
 Mafundi wakisuka nondo kwa ajili ya kutengeza nguzo ambazo zitatumika kubeba gati ya bandari ya Kasanga iliyopo Ziwa Tanganyika mkoani Rukwa.

 Moja ya meli ya Mizigo kutoka nchini Burunfi ikiwa katika bandari ya Kasanga ikipakia mifuko ya saruji inayotoka kiwanda cha Mbeya Cement 
Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama akizungumza kuhusu ujenzi wa miundombinu unaondelea katika bandari ya Kasanga mkoano Rukwa.


*Kukamilika barabara ya lami Sumbawanga kwenda Kasanga yaongeza idadi ya malori yanayopeleka mizigo bandarini


Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Rukwa


MENEJA wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama amesema bandari ya Kasanga ni ya pili kwa ukubwa kwenye ziwa hilo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari  Tanzania(TPA) imeamua kufanya mradi mkubwa wa Sh.bilioni 4.764 ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wanaotumia bandari hiyo kusafirisha mizigo kutoka nchini Tanzania kwenda nchi jirani.


Amesema kwa sasa katika bandari hiyo nyumba za wafanyakazi zinajengwa na kwamba tayari wameanza kuongeza gati ya sasa kutoka mita 20 mpaka mita 120 kwa  lengo ni kuruhusu meli zaidi ya moja kutia nanga kwa wakati mmoja kwa sababu meli kama Mv. Liemba ina ruti ndefu kwenye Ziwa Tanganyika ina urefu wa mita 71.4, hivyo maana yake katika gati hiyo gati ya sasa ya mita 20 tafsiri yake meli nyingine hawezi kukaa. 


Salama ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini waliopo katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA).


Ambapo mbali ya ujenzi wa miundombinu ya bandari hiyo, waandishi wameshuhudia barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Sumbawanga mjini hadi Bandari ya Kasanga ikiwa ni mkakati wa Serikali kuhakikisha bandari hiyo inafika kwa urahisi ikilinganishwa na awali kabla ya kutengenezwa.


Akizungumza zaidi kuhusu bandari hiyo Salama amesema baada ya kuona gati ya eneo hilo ni dogo, kiasi cha kusababisha meli zisirubiane na kusababisha kukaa muda mrefu bandarini. TPA imeliona haja ya kuongeza urefu wa gati hilo na sasa urefu utakuwa mita 120."Tafsiri yake sasa itakuwa na uwezo wa kuweka meli mbili mpaka tatu kwa wakati mmoja kulingana na urefu wa meli, kutakuwa hakuna tena kusubiriana.Huu ni uboreshaji mkubwa kupata kutokea. 


"Pia tunaweka sakafu ngumu pale eneo bandari kuhakikisha kontena zinaweza kukaa bila tatizo , kwani tunamatarajio na tumeanza kuzungumza na mfanyabiashara mmoja ameonesha nia ya kutaka kushusha kontena kwenye Bandari ya Kasanga, likifanikiwa na huu uwekezaji ambao unaofanyika maana yake kwamba azma ile ya uwekezaji na matokeo ya uwekezaji yatakuwa yamefikiwa,"amesema Salama.


. Ameongeza katika ujenzi huo wa miundombinu TPA inajenga nyumba za wafanyakazi wa bandari ambazo ziko mbili na hivyo wafanyakazi na familia zao watakaa katika nyumba hizo, hivyo hawatakuwa na shida kwenda mahali pengine na kwamba wanaishukuru  Serikali kwa kipekee kwa kuwezesha kuboresha barabara ambayo ilikuwa imebaki kama kilometa kama 50 hivi ambayo sasa imewekwa lami kutoka Sumbawanga mpaka Kasanga. 


"Kwa hiyo ile barabara ya kilometa 90 ambayo mwanzo ilikuwa changamoto kubwa ni amini sasa hivi tu nazungumzia barabara ile kukamilika kufikia mwishoni mwa Desemba au kama ikichelewa sana Januari itakuwa imekamilika yote kabisa.Inaleta matokeo makubwa sana, sasa Bandari  ya Kasanga ya sasa ukiiangalia mwaka jana ilikuwa inachangia karibu asilimia 19 ya mapato. 


"Unapozungumzia zile Shilingi bilioni 4.148 tulizopata mwaka jana kwenye mwaka wa fedha 2018/19 kama gawio kwa Serikali, Bandari ya Kasanga ilichangia asilimia 19 ya mapato lakini ukiiangalia kwenye mwaka huu wa fedha tulianza nao 2019/19 mpaka sasa miezi mitano hii kuanzia mwezi wa 7 mpaka 11 tayari bandari hii imeishatuingizia karibu Sh.milioni 490 , hivyo mchango wake umeongezeka kutoka asilimia 19 za mwaka jana kwenda mpaka asilimia 29,:amesema.


Salama amesema katika mapato Bandari ya Kasanga ya Sh.million 288 unaona karibu Sh.milioni 100 zimechangiwa na Kasanga, uwekezaji ule ambao Serikali inaufanya Kasanga kupitia TPA ni muhimu na una tija kwa Taifa kwani umeshaanza kuonesha kupandisha huduma na kuvutia wateja hasa wenye meli kutumia bandari ya Kasanga, hivyo ni uwekezaji sahihi. 

Maduka ya Vodacom yaongeza muda wa kazi kufanikisha usajili wa alama za vidole

$
0
0
Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC imeongeza muda wa kufanya kazi katika maduka zaidi ya 400 ya Vodashop na madawati ya huduma kwa Mteja (Customer Service Desk) nchini kote ili kukidhi mahitaji ya wateja wake ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole kabla ya kufikia ukomo Desemba 31 mwaka huu. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC – Hisham Hendi alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa wateja wote wa Vodacom wanatekeleza matakwa ya kusajili laini zao za simu kwa kutumia alama za vidole ili kuendelea kupata huduma ya mawasiliano. 

“Tumeongeza saa zetu za kazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili usiku. Hivyo wateja wetu wenye vitambulisho vya Taifa au namba ya kitambulisho cha Taifa watembelee maduka yetu katika kila kona ya nchi ili kusajili laini zao za simu. 

Hii itawawezesha kuendana na matakwa ya Serikali na kuwaondolea usumbufu wa kukosa mawasiliano, hasa katika msimu huu wa sikukuu ambapo kila mtu anahitaji kuwasiliana na ndugu, jamaa, marafiki na watu wake muhimu. Pia tunawashauri wateja ambao hawajaomba kitambulisho cha Taifa wafanye hivyo haraka ili kukamilisha mchakato wa usajili wa laini zao,” alisema Hendi. 

Aliongeza kuwa mawakala wa Vodacom wenye vitambulisho na mavazi maalumu watapita katika maeneo mbalimbali ya makazi, ofisi na biashara kuwezesha wateja kusajili laini zao za simu.Usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole unalenga kupunguza matumizi mabaya ya simu za kiganjani na kuongeza usalama. 

Watanzania wanatakiwa kuwa na kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho hicho ili kukidhi mahitaji ya usajili huo. Kwa mujibu wa agizo la Serikali, laini zote za simu ambazo hazitasajiliwa kufikia Desemba 31 mwaka huu zitafungiwa. 

“Sio lazima kuwa na kitambulisho cha taifa. Kama mtu anaweza kukumbuka nambari yake ya kitambulisho cha taifa (NIN) tunamsajili,” alifafanua Hisham. 

Mapema mwaka huu, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa agizo kwamba laini zote za simu nchini zinatakiwa kusajiliwa katika mfumo wa alama za vidole. Mfumo wa utambuzi kwa kutumia alama za mwili (Biometrics) unatumika zaidi kama njia mojawapo ya kuwafahamu wateja (know your customer – KYC) ili kuzuia utapeli miongoni mwa wateja, hasa wale wa mitandao ya simu.

RAIS MAGUFULI ASALI IBADA YA MISA TAKATIFU DOMINIKA YA NNE YA MAJILIO KANISA LA BIKIRA MARIA PAROKIA YA CHATO,ATOA SALAMU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2020

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kupokea Sakramenti Takatifu, alipoungana na waumini wengine wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita katika Misa Takatifu ya Dominika ya nne ya Majilio iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Henry Mulinganisa, ambapo Mhe. Rais amewatakia heri ya Krismas na Mwaka mpya Watanzania wote. Disemba 22,
2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amejumuika pamoja na waumini wengine wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita katika Misa Takatifu ya Dominika ya nne ya Majilio iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Henry Mulinganisa, ambapo Mhe. Rais amewatakia heri ya Krismas na Mwaka mpya Watanzania wote. Disemba 22, 2019.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya nne ya Majilio iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Henry Mulinganisa, ambapo Mhe. Rais amewatakia heri ya Krismas na Mwaka mpya Watanzania wote . Disemba 22, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Padre Henry Mulinganisa Paroko wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita alipozungumza na Waumini wa Kanisa wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya nne ya Majilio iliyoongozwa na Paroko huyo, ambapo Mhe. Rais amewatakia heri ya Krismas na Mwaka mpya Watanzania wote . Disemba 22, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia mtoto Zioni nje ya kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita mara baada ya kushiriki Misa Takatifu ya Dominika ya nne ya Majilio iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Henry Mulinganisa, ambapo Mhe. Rais amewatakia heri ya Krismas na Mwaka mpya Watanzania wote. Disemba 22, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Waumini nje ya kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita mara baada ya kushiriki Misa Takatifu ya Dominika ya nne ya Majilio iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Henry Mulinganisa, ambapo Mhe. Rais amewatakia heri ya Krismas na Mwaka mpya Watanzania wote. Disemba 22, 2019.PICHA NA IKULU

NAIBU WAZIRI MABULA AAGIZA WADAIWA NHC KUCHUKULIWA HATUA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC Margreth Ezekiel (Kulia) na Mhandisi Mburuga Matamwe wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu wa NHC Margreth Ezekiel wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti mwishoni mwa wiki. Wa Kwanza kushoto ni Mhandisi kutoka NHC Mburuga Matamwe.


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipokutana kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Shirika hilo. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dkt Maulid Banyani.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) alipokutana nayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kujadili uboreshaji wa Shirika hilo. Kulia aliyekaa ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dkt Maulid Banyani .(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI) 

******************************** 

Na Munir Shemweta WANMM 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekutana na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa saa nne na kulitaka shirika hilo kuhakikisha kufikia Januari 2020 inawachukulia hatua wapangaji wote wa Shirika hilo wanaodaiwa kodi inayofikia bilioni 8.23. 

Dkt Mabula alikutana na Menejiment ya Shirika hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam ikiwa ni mkakati wake wa kulifanya Shirika la Nyumba la Taifa kuimarika kimapato pamoja na kufanya kazi zake kwa ufanisi. 

Alisema, katika kuifanya NHC inaimarika kimapato ni lazima madeni kutoka kwa wapangaji wake yanakusanywa kwa kuanzisha opreresheni maalum inatakayowezesha kutambuliwa wadaiwa wote wa kodi ili waweze kulipa kwa wakati. 

‘’Ukiacha zile taasisi za serikali, wote wanaodaiwa ikifika januari 2020 wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na zile taasisi za serikali mkamuone Katibu Mkuu HAZINA ili taasisi hizo zikatwe fedha moja kwa moja’’ alisema Dkt Mabula 

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wakati wa zoezi la kufanya opresheni ya kukusanya madeni sheria lazima ifuatwe ikiwemo kutoa hati za wito wa madai kwa wadaiwa wote kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umiliki na Uendelezaji wa Shirika la Nyumba la Taifa Greyson Godfrey alimueleza Dkt Mabula kuwa, pamoja na NHC kuimarika katika makusanyo lakini liko kwenye mikakati maalum wa kukusanya madeni kutoka kwa wadaiwa wake na moja ya jitihada zake ni kuingia makubaliano maalum ya namna wadaiwa watakavyolipa madeni. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani alisema Shirika lake limekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha linaimarika kimapato ikiwemo kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya vizuri katika mikoa itakayofikia lengo la makusanyo na kutokuwa na malimbikizo ya madeni kutoka kwa wadaiwa wa kodi. 

‘’Tumekuwa tukitoa motisha kwa watumishi wanaofanya vizuri na sasa tunaangalia ile mikao ambayo haina malimbikizo ya madeni kwa wapangaji wake kwa asilimia mia moja tuone namna tutakavyotoa motisha ili kuhamasisha mikoa kutokuwa na madeni’’ alisema Dkt Banyani 

Aidha, Dkt Banyani alisema, kwa sasa NHC imeanza kufanya uhakiki kwa wapangaji wake ili kubaini wapangaji waliopangisha watu wengine ambapo eneo la Ubungo limetumika kama eneo la majaribio na tayari wapangaji sita washaondolewa na kusisitiza kuwa zoezi hilo litakuwa ni la nchi nzima. 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mabula aliagiza kupatiwa orodha ya nyumba zote za NHC zilizouzwa, zisizouzwa, zilizopangishwa na zisizozopangishwa, viwanja vya Shirika hilo visivyoendelezwa pamoja na Nyumba zilizokuwa za Msajili wa Majumba zilizohamishiwa NHC hilo ili kujua hali ya shirika na mkakati wake katika kuleta ufanisi. 

Pia Dkt Mabula alitembelea maendeleo ya ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo ambao uko katika hatua za mwisho za kukamilika.

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA AWASILI WILAYANI SERENGETI

$
0
0
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TYanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adama Malima alipowa Uwanja wa Ndege wa Seronera Wilaya ya Serengeti leo Disemba 22, 2019 kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na  Mamlaka ya Hifadhi ya NGORONGORO (NCAA) yanayotarajiwa kufanyika kesho katika Hifadhi ya Ikoma Serengeti Mkoani Mara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TYanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.  Hamis Kigwangala Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adama Malima alipowa Uwanja wa Ndege wa Seronera Wilaya ya Serengeti leo Disemba 22, 2019 kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na  Mamlaka ya Hifadhi ya NGORONGORO (NCAA) yanayotarajiwa kufanyika kesho katika Hifadhi ya Ikoma Serengeti Mkoani Mara.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Mama lishe ajishindia bodaboda kupitia promosheni ya ‘TUNZA, UTUNZWE na M-PAWA’

$
0
0
 Meneja wa Huduma ya M-Pawa kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu (kushoto) akimpongeza mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.

 Meneja wa Huduma ya M-PAWA kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu (kushoto) akimpongeza mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 Meneja wa Huduma ya M-Pawa kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu (kushoto) akimpongeza mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko wa CBA Bw. Solomon Kawiche. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 Meneja Masoko wa CBA Bw. Solomon Kawiche (kulia) akimpongeza mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.

 Mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (26) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam akionesha kadi ya pikipiki wakati wa makabidhiano ya zawadi yake hiyo. Kushoto ni Meneja wa Huduma ya M-Pawa kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu akionesha funguo za pikipiki. Akishuhudia kulia ni Meneja Masoko wa CBA Bw. Solomon Kawiche. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 . Meneja wa Huduma ya M-PAWA kutoka Benki ya CBA Bi. Gloria Njiu (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (hayupo pichani) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yalifanya uwanja wa Sahara, Mabibo. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.
 . Meneja Masoko wa CBA Bw. Solomon Kawiche (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana (hayupo pichani) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yalifanya uwanja wa Sahara, Mabibo. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania

Mshindi wa bodaboda ‘Boxer BM125’ wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ Bi. Leticia Yohana mwenye miaka 26 (kushoto) ambaye ni mama lishe kutoka Mabibo makutano, Dar es Salaam akisindikizwa na wapambe kwenda kukabidhiwa zawadi yake. Promosheni hii itatoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa Watanzania.


Benki ya CBA na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom jana imemkabidhi mshindi mmoja wa promosheni ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ pikipiki mpya aina ya ‘Boxer BM125’ yenye thamani ya shilingi milioni tatu baada ya kuibuka kidedea katika droo ya wiki ya kwanza ya shindano hilo. 

Mshindi huyo, Bi. Leticia Yohana (26) mkazi wa Mabibo makutano jijini Dar es Salaam anayejishughulisha na kazi ya upishi ‘mama lishe’ alionekana mwenye furaha na bashasha alivyokabidhiwa pikipiki hiyo mpya katika hafla ya makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya Sahara, Mabibo.

“Kwa kweli haikuwa rahisi kuamini kwamba nimeshinda. Ninafuraha sana kuwa mshindi wa pikipiki hii leo. Nimekuwa mtumiaji wa huduma ya M-Pawa kwa muda mrefu, kwa kuweka pamoja na kukopa kwa ajili ya biashara yangu ya chakula,” alisema Bi. Yohana.

“Nitatumia pikipiki hii kama fursa ya kuendelea kujikwamua kiuchumi kwa kuitumia kwa matumizi ya kubeba abiria, yaani bodaboda. Napenda kuchukua fursa hii pia kuwashawishi Watanzania wenzagu watumie M-Pawa ili nao waweze kupata nafasi ya kushinda,” aliongeza mshindi huyo.

Akimpongeza mshindi huyo, Meneja wa Huduma ya Kibenki ya M-Pawa kutoka CBA, Bi. Gloria Njiu alisema benki ya CBA inajivunia kubadilisha maisha ya watanzania kwa kupitia promosheni hii ya ‘Tunza, Utunzwe na M-Pawa’ inayotoa zawadi kedekede ikiwemo zaidi ya pesa taslimu shilingi milioni 150 na bodaboda 18 kwa wateja wao. 

“Promosheni hii ya wiki sita inawapa fursa Watanzania kushinda mara mbili ya akiba yao katika akaunti zao za M-Pawa, kushinda bodaboda kila wiki, na mshindi mmoja kuondoka na donge nono la fedha taslimu ya shilingi milioni 10,” alisema Bi. Njiu.

Akielezea zaidi kuhusu promosheni hii, Bi. Njiu alisema “Promosheni hii imelenga kuwazawadia watumiaji wazuri wa huduma ya M-Pawa zawadi mbali mbali. Mpaka sasa tumeshafanya droo mbili na kupata washindi 120 walioshinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 4, huku washindi 7 wakishinda pikipiki zenye thamani ya shilingi milioni 21 hadi sasa.”

“Mshindi mkubwa wa promosheni hii atazawadiwa shilingi milioni 10 kwenye droo ya mwisho hivyo tunaendelea kuwasisitiza watumiaji wa M-Pawa na wengine ambao hawajajiunga bado kujiunga na kuweka akiba na kurejesha mikopo mapema ili waweze kupata nafasi ya kushinda,” alieleza Bi. Njiu.

Kujiunga na M-Pawa, piga *150*00# kisha chagua M-Pawa. 

TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA YASHIRIKISHA WADAU MABORESHO YA SERA

$
0
0


Mkurugenzi wa Mipango, Tathmini na Ufuatiliaji wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bw. Buji Bampebuye akifungua kikao cha wadau wa Ushirika katika kikao kazi cha kukusanya maoni ya maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika mkoani Dar es salaam, kulia ni Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Abdillahi Mutabazi
Wadau wa Ushirika wakijadiliana kuhusu masuala ya kufanyiwa maboresho katika Sera ya Maendeleo ya Ushirika, mkoani Dar es salaam hivi karibuni
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Mtwara akifungua kikao kazi cha mjadiliano na kupokea maoni ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika Mkoani Mtwara
Wadau Mkoani Mtwara wakijadiliana maboresho ya kufanyika katika Sera ya Maendeleo ya Ushirika



Mkurugenzi wa Mipango, Tathmini na Ufuatiliaji wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bw. Buji Bampebuye ametoa wito kwa wadau wa Sekta ya Ushirika kutoa maoni yatakayotumika katika kuboresha na kupitia upya Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002.

Wito huo umetolewa wakati wa ukusanyaji wa maoni hayo katika kikao kazi kilichofanyika Dar es salam hivi karibuni, Tume ilipokutana na viongozi wa Vyama vya Ushirika pamoja na wanaushirika waliokuwa wakijadili masuala mbalimbali ya namna bora ya kuboresha utendaji na uendeshaji wa Sekta ya Ushirika nchini.

“Wanaushirika tujadiliane kwa kina changamoto zilizopo katika Sekta tutoe mapendekezo nini kifanyike na namna gani kifanyike ili kuimarisha na kuondokana na changamoto pamoja na vikwazo vilivyopo katika Sekta ya Ushirika inayochangia Uchumi wa nchi na kutoa fursa za ajira nchini. Ushirika ni wa wanaushirika wenyewe kwa hiyo tumieni fursa hizi vizuri kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa Taifa letu,” alisema Bw. Bampebuye

Sambamba na kikao kazi hicho Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Mtwara Bw. Juma Mokili akifungua kikao cha wadau katika ukusanyaji wa maoni mkoani Mtwara alisema Sera inatoa Dira ya uendeshaji wa Sekta ya Ushirika. Hivyo, wadau wana mchango muhimu katika kuujenga Ushirika watumie fursa hiyo kutoa maoni yao kwa uwazi na uhuru ili kuweka msingi wa Sera bora itakayotumika kuendelea kuunda Sheria, Miongozo pamoja na Kanuni zitakazotumika kwa maslahi ya wanaushirika na Taifa kwa ujumla.

Pamoja na mambo mambo mengine wadau walijadili masuala mbalimbali ikiwemo muundo wa Ushirika, fedha, Uwekezaji katika Vyama, Usimamizi na Uendeshaji wa miradi ya Pamoja, mali za Ushirika, ubunifu na Ujasiriamali katika Ushirika, masoko ya bidhaa, huduma za Ushirika, utawala, usimamizi, utafiti, elimu pamoja na mafunzo ya Ushirika.

Kwa upande wake Mjumbe wa kikao kazi Mkoani Mtwara Bw.Issa Mangochi kutoka Chama Kikuu cha Ushirika Masasi na Mtwara (MAMCU) amepongeza utaratibu huo shirikishi ambao umetoa fursa kwa wadau kutoa maoni na mapendekezo yao yatakayosaidia kutengeneza Sera bora zaidi itakayo hudumia wanaushirika wengi zaidi na utendaji wenye tija na maendeleo kwa wananchi. Aliongeza kwa kuwaomba watendaji katika Sekta ya Ushirika kufanya kazi zao kwa weledi, uadilifu na kwa kuzingatia taratibu za kazi.

Vikao kazi hivyo vimehusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vyama vya Msingi (AMCOS), Vyama vikuu, Taasisi za Vyuo vikuu, Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo, Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO). Tume tayari imeshapokea maoni kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikiwemo Kilimanjaro, Kanda ya Juu Kusini mkoani Mbeya pamoja na Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

TAWLA YAWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA DINI KUHUSU NDOA ZA UTOTONI NA MIMBA ZA UTOTONI

$
0
0
Mwezeshaji wa semina hiyo Mwanasheria Jones John akiwasilisha mada na taarifa ya tafiti mbalimbali barani Afrika zinazoonyesha matukio ya ndoa za utotoni na mimba za utotoni ambapo nchi kama Tunisia imepiga hatua katika kuzuia ndoa za utotoni na mimba za utotoni ukilinganisha na mataifa mengine kama Niger ambayo ina kiwango kikubwa cha matukio hayo.
Mwezeshaji wa semina hiyo Mwanasheria Jones John akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada na taarifa ya tafiti mbalimbali barani Afrika zinazoonyesha matukio ya ndoa za utotoni na mimba za utotoni.
Mwanasheria Kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Adv. Barnabas Kaniki akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa juu ya mbinu za ulizni wa watoto hasa kwenye ndoa za utotoni na mimba za utotoni.Lengo likiwa ni kuangalia namna gani asasi za kiraia zinaweza kufanya kazi kwa pamoja na viongozi wa dini kutokomeza ndoa za utotoni na mimba za utotoni, Semina hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Makumbusho Posta jijini Dar es salaam.
Mwanasheria Kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Adv. Barnabas Kaniki akifurahia jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada kwenye semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa juu ya mbinu za ulizni wa watoto hasa kwenye ndoa za utotoni na mimba za utotoni.
Baadhi ya viongozi wa dini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Viongozi wa dini wanawake pia walihusishwa katika semina hiyo Mwanamke anachukuliwa kama nguzo muhimu katika kujenga familia iliyobora na inaweza kuleta manufaa katika taifa lolote lile.
Mwanasheria Kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Adv. Barnabas Kaniki katikati akijadiliana jambo na mmoja wa wanasheria wa TAWLA Bi Subira wakati semina hiyo ikiendelea.

Shabiki wa Man United, Simba ashinda mili 124.1 za M-Bet

$
0
0
 Shabiki wa timu ya Simba na Manchester United na mkazi wa mkoa wa mkoa wa Dodoma, Fredrick Kimario ameshinda Sh 124,150,810 baada ya kubashiriki kwa usahihi jumla ya mechi 12 katika za mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.


Kimario ambaye ameajiliwa katika kazi za kuuza duka anaifanya M-Bet kutumia zaidi ya Sh billion 3 kuzawadia washindi mbalimbali tokea kuanza kwa mwaka huu.

Meneja Masoko wa M-Bet, Allen Mushi amesema kampuni yao inazidi kupata washindi na Kimario anaaga mwaka kwa kishindo kwa kutwaa kitita hichi cha fedha.Mushi alisema kuwa kampuni yao inazidi kuwabadili maisha Watanzania na Kimario anakuwa mshindi wa 19 tokea kuanza kwa mwaka huu.

“M-Bet inazidi kuchanja mbuga na kuinua vipato vya Watanzania na kuchangia maendeleo ya nchi chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli. Nawaomba Watanzania kucheza ili kushinda zawadi za fedha na kubadili maisha yao, ” alisema Mushi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Kimario alisema kuwa alianza kubeti muda mrefu kabla ya kupata ushindi huo mnono.

Kimario alisena kuwa amekuwa akishinda fedha kiasi kisichopungua Sh400,000 na ushindi huu umemfanya kuanza kufikiria mambo makubwa zaidi kibiashara kwani kwa sasa ameajiliwa.

“Sikukata tamaa na kuendelea kubeti, niliamini kuwa siku moja nitapata bahati ya kushinda, nashukuru Mungu kupata kiasi hiki cha fedha na nitakaa na ndugu zangu kupanga jinsi ya kuanzisha biashara zangu,” alisema Kimario.

Alisema kuwa ndoto zake za kuwa mfanyabiashara zimetimia na anaahidi kuwa mfano wa kuigwa kwa washindi M-BET.
Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kulia) akimzawadia mfano hundi, Fredrick Kimario aliyeshinda Sh124, 150,810 kwa kubashiri kiusahihi zaidi mechi 12 za mchezo wa Perfect 12.

 

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MAADHIMISHO MIAKA 60 YA TANAPA NA NCAA MKOANI MARA

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunuku Tunzo kwa Deogratius Chami kwa niaba ya Makundi ya watu wenye Mahitaji Maalum kwa kutambua Mchango wao Mkubwa katika kutunza na kutangaza Hifadhi za Taifa kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yaliyofanyika leo Disemba 23,2019 katika Uwanja wa Eneo la Fort  Ikoma Serengeti  Mkoani  Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi na Wananchi kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yaliyofanyika leo Disemba 23,2019 katika Uwanja wa Eneo la Fort  Ikoma Serengeti  Mkoani  Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata Utepe kuzindua Minara Miwili ya kumbukumbu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yaliyofanyika leo Disemba 23,2019 katika Uwanja wa Eneo la Fort  Ikoma Serengeti  Mkoani  Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Kasha la Wakati la kuhifadhia kumbukumbu za nyaraka za Hifadhi za Taifa wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yaliyofanyika leo Disemba 23,2019 katika Uwanja wa Eneo la Fort  Ikoma Serengeti  Mkoani  Mara.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Saluti ya heshima kutoka kwa Jeshi Usu la Maliasili wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yaliyofanyika leo Disemba 23,2019 katika Uwanja wa Eneo la Fort  Ikoma Serengeti  Mkoani  Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Rasmi la Jeshi Usu la Maliasili kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yaliyofanyika leo Disemba 23,20
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunuku Tunzo kwa Pro. Adolfo Mascarenhas kwa kutambua Mchango wake Mkubwa katika kutunza na kutangaza Hifadhi za Taifa kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yaliyofanyika leo Disemba 23,2019 katika Uwanja wa Eneo la Fort  Ikoma Serengeti  Mkoani  Mara.

RAIS MSTAAFU KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MAMA WA MWENYEKITI WA CCM MKOA MOROGORO

$
0
0
Mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya zake, wanachama na wakereketwa wa CCM, wanachama wa vyama mbali vya siasa, viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo 24 Disemba 2019 wamehudhuria na kushiriki mazishi ya *Mama mzazi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris

Mama Theodora Vasos Kalogeris amefariki dunia Jumapili 22 Disemba 2019 Hospital ya Chuo cha Kilimo (SUA) Morogoro na kuzikwa leo alasiri makaburi ya Kola Hill Morogoro Mjini.

Mapema viongozi na wanachama walipata kuaga mwili kisha kufanyiwa ibada fupi nyumbani kwake Mji mpya na baadae kufuatiwa na Ibada ya mazishi kanisa la Kuu St Patrick.

Viongozi wengine walishiriki Mazishi hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Katibu Mkuu wa UWT, Wabunge kutoka mkoa wa Morogoro na Mbunge wa jimbo la Korogwe Marry Chatanda, Wakuu wa Wilaya zote za mkoa huo, IGP mstaafu Mahita, Mwenyeviti wa Chama wa Wilaya zote wakiongoza kamati za siasa za Wilaya zao, wakuu wa vyombo vya ulinzi na ulinzi na Usalama mkoa huo, wakuu wa taasisi za umma pamoja na ndugu jamaa na marafiki.

Mwendo Umeutimiza, Pumzika kwa Amani
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo na Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro , Shaka Hamdu Shaka na pichani kati ni MKuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loatha Sanare wakati wa mazishi ya Mama mzazi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris

WAZIRI LUKUVI AMFYATUA MKURUGENZI NHC KWA UZEMBE, AKAGUA UJENZI WA MRADI WA MACHINJIO VINGUNGUTI

$
0
0
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akitoa maagizo ya kumsimamisha kazi Grarson Godfrey Mkurugenzi wa Miliki Shirika la Nyumba (NHC) baada ya kugundua uzembe kazini kuhusu upangishaji wa nyumba ya NHC iliyopo Muhimbili jijini Dar es salaam.

................................................

Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemsimamisha kazi Grarson Godfrey Mkurugenzi wa Miliki Shirika la Nyumba (NHC) baada ya kugundua uzembe kazini na kusababisha upotevu wa fedha za serikali kutokana na moja ya nyumba iliypopo Muhimbili jijini Dar es salaam kupangishwa kinyume cha utaratibu wa shirika hilo.

Akizungumza katika eneo la tukio Waziri Lukuvi leo amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo Dk.Maulid Banyani kumuondoa katika nafasi hiyo na kuangalia wote waliohusika au kushiriki kwa upotevu wa fedha hizo kuchukuliwe hatua za kinidhamu.

Mtu mmoja ambaye hakutajwa jina lake amewapangisha wafanyabiashara mbalimbali katika jengo hilo wakimlipa kiasi cha shilingi laki moja 100,000 kila mmoja kwa mwezi huku yeye akililipa shirika la nyumba (NHC) kiasi cha shilingi elfu ishirini na Nne 24,000 kwa mwezi.

Wapangaji hao wamepanga katika jengo hilo kwa muda wa miaka 13 na wamekuwa wakimlipa mtu huyo kiasi hicho kila mwezi jambo ambalo linalikosesha mapato shirika la nyumba pia Mamlaka ya Mapato TRA haikusanyi kodi ya serikali kutokana na udanganyifu huo uliofanyika kwa muda mrefu na kusababisha upotevu wa fedha nyingi za serikali.

Waziri Lukuvu ameongeza kuwa kama Mkurugenzi huyu wa Miliki katika shirika la nyumba (NHC) ameshindwa kuchukua hatua kwa ubadhirifu uliopo kwenye nyumba ya hapa Muhimbili tu. ataweza kugunda na kuchukua hatua katika majengo yaliyopo nchi nzima maana yake ni fedha nyingi zinapotea kwa uzembe huu.

"Huyu ameshindwa kwenda na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. DK. John Pombe Magufuli ambaye anataka kila fedha ya serikali ikusanywe na kuleta maendeleo kwa watanzania wanyonge".

Wakati huohuo Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk. Maulid Banyani kumpa taarifa ya kiufundi na kitaalamu itakayokuwa imejitosheleza kuhusu sababu za kuchelewa kumalizika kwa ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti ambayo Rais. Dk. John Pombe Magufuli aliagiza ujenzi ukamilike Disemba 31 2019 wakati alipotembelea mradi huo. 

Ameongeza kwamba sababu hizo zielezwe wazi na ziwe ni za msingi ili baada ya hapo yeye amtaarifu Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kuhusu ucheleweshwaji huo kabla mwezi januari mwaka ujao.

Lazima nijiridhishe nione sababu zenyewe kama ni za msingi, Kitaalam na Kiufundi ili nami nimtaarifu Ras kuhusu kuchelewa kukamilika kwa mradi huu.

Hata Hivyo Waziri Lukuvi amelipongeza shirika hilo kwa utekelezaji wa mradi huo wa machinjio ya Vingunguti kwa kasi na viwango vizuri ambao ni wa 35 kati ya miradi yote ambayo Shirika la hilo linatekeleza nchi nzima ambapo amesema mradi huo unaendelea vizuri.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiangalia leseni za wajasiriamali hao ambao wamepangishwa katika nyumba ya NHC kinyume cha utaratibu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo Dk.Maulid Banyoni na katikati ni Said Seif Mketo mmoja wa wapangaji.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani na katikati ni Said Seif Mketo mmoja wa wapangaji.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimsikiliza mmoja wa wapamgaji katika nyumba hiyo Said Seif Mketo alipokuwa akimuelezea jinsi ambavyo wamekuwa wakinyanyaswa na mtu aliyewapangisha kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la machinjio ya nyama Vingunguti ambalo linajengwa na NHC.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akzungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi huo kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa machinjio hayo Vingunguti.
Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Saguya kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la nyumba NHC Dk.Maulid Banyani
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images