Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

BOOK TO MAKE AFRICA WORLD’S ECONOMIC POWERHOUSE LAUNCHED IN JANUARY

$
0
0
By Staff Reporter, Dar es Salaam

Dar es Salaam, 15 December, 2019: A Book that inspires Africa to think of implementing generational reforms to becoming world’s largest economy is expected to hit African book stores from January 2020.

Speaking during the interview with Tanzania’s ITV Channel over the weekend, Derek Murusuri, author of the much awaited book, said his 21-year researched book, is a game changer for Africa’s future.

“This book is for Africa. It brings back to African minds, the forgotten concept of liberation.

It breaths a fresh air in the struggle for Africa’s economic liberation in the World’s richest continent yet poor, a paradox indeed” the author said.

“The young men and women of Africa must now rise to the new helm, as the roads rise to meet them, to rejuvenate the possibilities embalmed in their dreams which will raise new values, norms and beliefs to lead the continent to economic triumphs,” he said.

The author who once lived and worked in the UK, said his book assures black people on earth to know and believe that they were never created to be followers, neither were they predestined underdogs.

He told ITV’s Kumekucha host, Abdallah Mwaipaya, that the book hits the African book stores on 15 January, 2020 after a grand launch in Tanzania’s business capital of Dar es Salaam.

Mr. Murusuri said he shares the ideas on solutions to end Africa’s centuries of economic bondage and hopelessness in his much awaited book. He did not reveal much contents neither did he reveal the presider.

The post-independence African leaders who came to power in recent years, exhibit the zeal to transform and change the continent, making it increasingly competitive.

What the book says and whether the continent will truly gamble to skip the hurdles and navigate through becoming the World’s leading economy, is a matter of weeks, when political scientists, academicians, politicians and other analysts will scan the book, review and implement the author’s ideas. 

In November, Tanzania’s third President, Dr. Benjamin Mkapa, had his memoirs titled “My Life, my Purpose,” inaugurated by Tanzania’s President Dr. John Pombe Magufuli.

Book readership in this East African country, is slowly rising as the country prides the largest University in East and Central Africa.







K-Finance yaandaa maonyesho kwa wanawake wajasiriamali maarufu kama Women in Balance Business

$
0
0
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya K-Finance, Judith Minzi ametaja sababu za biashara nyingi zinazoanzishwa nchini zimeshindwa kuendelea kuwa ni pamoja na kutokujua namna ya kutafuta masoko, kunakili biashara ambayo anafanya mtu bila kujua wazo lake namna lilivyoanzishwa.

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji aliiagiza Benki Kuu ya Tanzania(BOT) kushirikiana na Mfuko wa Udhamini wa Sekta ya Fedha(FSDT) kufanya utafiti kujua sababu ya biashara nyingi hasa zinazoanzishwa na wanawake zinashindwa kufikisha miaka mitatu.

Ashatu alitoa maagizo hayo katika mdahalo wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuhusu sekta ya fedha, akiwataka watafute sababu zinazosababisha asilimia 51 ya biashara zinazoanzishwa na wanawake nchini hufa kabla ya kufikisha miaka mitatu.

Akizungumza katika maonesho ya Biashara ya Wanawake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Judith alisema elimu ya biashara kwa wafanyabiashara wengi ni tatizo hivyo kushindwa kujiendesha.

Alisema changamoto nyingine ni uelewa mdogo wa wafanyakazi wanaomsaidia mfanyabiashara kuuza bidhaa hiyo kama wanaijua na wanajua maono ya mwanzilishi.

“Ni muhimu kwa wafanyabiashara kutafuta elimu ya biashara kupitia njia mbalimbali ikiwamo mafunzo yanayotolewa na taasisi nyingi hapa nchini,” alisema Judith.

Aliishauri serikali kuanzisha somo la ujasiriamali kwa shule za msingi ili kuwajengea uwezo wanafunzi waweze kukua wakijua namna ya kufanyabiashara.

“Tuendelee kushawishi wanafunzi wapende kusoma somo la hesabu kwani linasaidia katika uanzishaji na usimamizi wa biashara,” alisema Judith.

Alisema kwa kuliona hilo taasisi ya K-Finance imeandaa mafunzo kwa wajasiriamali yatakayofanyika Januari 18, 2020 pale Hekima Garden, Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa kufundisha jinsi ya kutumia vipaji vyako kufikia uhuru wa kiuchumi.

Judith alisema katika uchunguzi walioufanya wamebaini kuwa watu wengi wanaoanzisha biashara wanashindwa kufikia malengo kutokana na kutokuwa na elimu hiyo.

Alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwapa uelewa wa biashara wanazofanya na watakazoanzisha ili kuziwezesha kuwa imara na kudumu kwa muda mrefu.“Tutawakutanisha wafanyabiashara waliofanikiwa na ambao ndio wanaanza ili kubadilishana uzoefu na changamoto zinazopatikana katika ufanyaji biashara,” alisema Judith.

Alisema wafanyabiashara wengi waliofanikiwa wamepitia changamoto mbalimbali ambazo wakibadilishana na wanaoanzisha biashara zitawasaidia kujua namna ya kuzitatua watakapokumbana nazo.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yaitwayo ‘Ignite Business Clinic’ yataongozwa na Mchumi Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BOT) kwa Zaidi ya miaka 20, na ndiye Mkurugenzi Mwanzilishi wa K-Finance, Bi. Devotha Minzi pamoja na uwepo wa mgeni rasmi aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo na sasa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb)






Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya K-FINANCE inayotoa Mikopo na Ushauri wa Kibiashara kwa wafanyabiashara na watu binafsi Judith Minzi (aliyesimama), akipewa maelezo na moja ya washiriki wa maonyesho ya wanawake wajasiriamali maarufu kama Women in Business Balance ambayo yalifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni. K-Finance ilidhamini maonyesho hayo kuongea na washiriki juu ya uhuru wa kiuchumi na vile vile kuhamasisha semina maarufu kama Ignite Business Clinic (IBC) Msimu wa pili ambao utafanyika Januari 18 2020 kwenye ukumbi wa Hekima jijini Dar es Salaam. (Picha na mpigapicha wetu).

MFK AUTOMOBILE YAZINDUA MAGARI YA KISASA AINA YA HONGYAN

$
0
0
 Wafanyabiashara wa sekta ya usafirishaji waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa magari ya kisasa ya mizigo aina ya Hongyan wakishuhudia moja kati ya magari hayo, kampuni ya MFK Automobile Tanzania kushirikiana na Hongyan kutoka China walizindua magari hayo jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa MFK Automobile Tanzania, Mehboob Karmali (kushoto) akikabidhiwa funguo na Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, Winnie Xiong kuashiria uzinduzi wa magari ya mizigo ya kisasa aina ya Hongyan yenye uwezo wa hali ya juu na ya kwanza kutumia katika nchi za Afrika Mashariki kwenye  hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam.

 Mkurugenzi Mtendaji wa MFK Automobile Tanzania, Ali Jawad Karmali akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan

 Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, Winnie Xiong akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan

 Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina Ngalula akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan

 Picha ya pamoja kati ya  Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina Ngalula (wa nne kulia) na viongozi wa MFK Automobile Tanzania na SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China kwenye hafla ya uzinduzi wa Hongyan.


 Kampuni ya MFK Automobile ambayo inajihusisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa magari ya mizigo nchini, imezindua magari ya kisasa yenye uwezo wa hali ya juu na ya kwanza kutumia katika nchi za Afrika Mashariki. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa MFK Automobile Tanzania, Ali Jawad Karmali alisema shukrani za pekee kwenu kwa kuitikia wito wetu wa mualiko wa uzinduzi wa vifaa vipya vya kampuni ya MFK, Gari ambazo kwa mara ya kwanza kuingia Afrika Mashariki aina ya HONGYAN. 

MFK ni kampuni mpya ambayo inajishughulisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa magari mbalimbali aina ya Tiper na Tracto head, tumekuja kuunga jitihada za serikali za kuelekea uchumi wa viwanda ambapo utawezesha fursa mbalimbali katika kukuza uchumi, tutatengeneza fursa kwa wasafiri na wasafirishaji na ndio sababu kuu iliyotufanya kuleta magari yenye teknolojia ya ulaya na umadhubuti wa China alisema Karmali 

Katika magari haya ya Hongyan, MFK Automobile inawapa Watanzania bidhaa yenye ubora kwa mtumiaji na mmiliki,bila usumbufu wowote na kiufundi wa gari hizi za HONGYAN, zina manufaa mengi kwa mmiliki kwa kumuwezesha kuhimili barabara zozote nchini, matumizi madogo ya mafuta na zina chumba cha kupumzika kwa dereva aliendelea kusema Karmali. 

Pia tumeona fursa katika sekta ya usafiri na usafirishaji, hivyo tumejipanga katika kuleta vifaa vyenye ubora ambavyo vitahakikisha Tanzania inakuwa kituo kikuu katika sekta hii kwenye ukanda huu wa Afrika ya mashariki na kati. 

“Lengo kuu la kampuni yetu ni kufanya Tanzania ipate bidhaa zenye ubora na za bei nafuu zinazoendana na kasi ya uchumi wa viwanda ambayo ni moja ya sera ya serikali ya awamu ya tano ili kufikia uchumi huo wa kati ifikapo mwaka 2025, MFK tunasimamia hilo”, alimalizia kusema Karmali. 

Tunajisikia fahari kufanya kazi na kampuni hii ya utengenezaji wa magari,katika ushirikiano huu wa IVECO GROUP NA WASHIRIKA WAO WA CHINA HONGYAN. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina Ngalula alisema “sekta ya usafirishaji imetoka mbali sana nakumbuka tulianza tukiwa na malori aina ya Scania 682 hadi kufikia sasa tunatumia magari ya kisasa zaidi, tunawashukuru MFK kwa mpango huu wa kuleta magari haya ya kisasa, pia yatatufanya sisi wafanya biashara kuyanunua kwa umoja wetu tuuweze kufanya sekta hii ya usafirisahji kuwa pana zaidi ukanda huu,. Pia nawaomba mabenki yaweze kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa sekta hii kwani haina ubabaishaji kurudisha mikopo hiyo. alisema Ngalula. 

Aliongezea kusema Ngalula “tuna bidhaa nyingi sana zinahitaji usafirishaji kama vile mazao, shaba, madini mbalimbali, hii itasaidia kuweka vituo vya kufanyia huduma(service) za magari na kuuza vipuri mikoani ili kuepusha wizi unaotokana na madereva wasio waaminifu”. 

Hata standard gauge SGR itahitaji zaidi kushirikiana na sekta hii ya usafirishaji ili kuwafikishia mizigo kwa urahisi zaidi, huwezi kuwa na Treni bila kuwa na magari ya mizigo, ukizingatia usafirishaji wa kutumia barabara unahitajika kwa asilimia 75 . alimalizia kusema Ngalula. 



Nae Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, -MS Winnie Xiong alisema hii ni fursa ya kipekee kwa kampuni yetu kuleta magari haya nchini Tanzania, hasa ukizingatia Tanzania na china zimeweka mahusiano ya kidiplomasia miaka 55 hadi sasa tokea mwezi Aprili 26, 1964, nchi hizi mbili zimejenga uhusiano imara na kushirikiana bega kwa bega. Leo nawaahidi kuwa Hongyan itazalisha magari bora ya mizigo kwa soko la Tanzania kwa kupitia washirika wetu MFK na kuwawezesha wateja wetu kugharamia huduma na vipuri vya magari haya kwa bei nafuu. alimaliza kusema Xiong.



MASHAMBA DARASA YANAVYOWANOA WATAALAMU WA KILIMO

$
0
0

Washiriki wa Mafunzo ya Msasa ya kuhusu Uwezeshaji Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wiakiwa katika mafunzo kwa vitend
o.

Sehemu kubwa ya Watanzania hutegemea shughuli za kilimo kwa ajili ya chakula na biashara na hivyo ni mchango mmojawapo wa uchumi wa Taifa. 

Pia Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wakulima wananufaika nma shughuli hizo za kilimo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kwa kilimo cha mazao tofauti tofauti 

Hata hivyo pamoja na juhudi hizo za Serikali bado wakulima wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli zao za kilimo na hivyo kupata wakati mgumu. 

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na changamoto ya uharibifu wa ardhi ambayo inayoleta athari kwa kilimo hali inayochangia uzalishaji duni wa chakula. 

Hali hiyo hutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanyika zikiwemo zikiwemo kuharibu vyanzo vya maji na ukataji miti kwa ajili ya kuni au uchomaji wa mkaa hali inayochangia uharibifu wa mazingira. 

Kutokana na changamoto hizo, Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ina dhamana ya usimamizi wa mazingira inaratibu na kutekeleza Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula (LDFS) hapa nchini. 

Mojawapo ya malengo ya mradi huo ni kuboresha mifumo ya ikolojia ya kilimo ambayo itawezesha kuongeza uzalishaji wa chakula na kuchangia kuboresha mazingira katika wilaya husika. 

Miongoni mwa wilaya ambazo mradi huo unatekelewa ni nne za Tanzania Bara ambazo mikoa yake iko kwenye mabano ni pamoja na Kondoa (Dodoma), Mkalama (Singida), Nzega (Tabora) na Magu (Mwanza). Pia unatekelezwa katika wilaya moja kwa upande wa Tanzania Zanzibar ambayo ni Micheweni (Pemba). 

Hivi karibuni Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa mafunzo msasa ya uwezeshaji kuhusu mashamba darasa kwa maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi huo. 

Mfunzo hayo yatakuwa msaada mkubwa kwa maafisa hao ambao wataitumia elimu waliyoipata katika kufanikisha uanzishaji wa mashamba darasa katika maeneo ya mradi. 

Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamekuwa wakitekeleza miradi inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kwa kusogeza karibu teknolojia kwa wakulima, lengo likiwa ni kuongeza usalama wa chakula na kuongeza kipato cha jamii. 

Hizi ni juhudi za Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inahusisha uingizaji na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea, mbegu zenye ubora, uboreshaji wa nyanda za malisho na utoaji wa huduma za ugani na mafunzo kupitia shamba darasa. 

Hivyo kutokana na mukhtadha huu juhudi hizi zote zina lengo la urejesha ardhi iliyoharibika ili iweze kuendelea kuzalisha mazao ya kilimo, mifugo na misitu hapa nchini. 

Mratibu wa mradi kutoka Ofisi hiyo, Joseph Kihaule anasema kuwa mradi huo unajumuisha uanzishwaji wa mashamba darasa 100 katika wilaya hizo Tanzania Bara na Zanzibar. 

Wawezeshaji wa mradi huo ni Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Wakala wa Taifa wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA) huku washiriki wa mafunzo wakitoka taasisi mbalimbali za Serikali. 

Miongoni mwa taasisi hizo ni pamoja na Wizara za Kilimo, Maliasili na Utalii, Maji, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Idara ya Mazingira, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar. 

Wengine ni kutoka katika Halmashauri zinazotekeleza mradi huo huku mikoa ikiwa kwenye mabano ni Mkalama (Singida), Micheweni (Pemba), Magu (Mwanza), Nzega (Tabora) na Kondoa (Dodoma). 

Mradi huu umenufaisha Watanzania kwa kupanga mipango ya matumizi bora ya ardhi iliyoandaliwa ambayo itawasaidia kuwa na usimamizi bora wa maliasili, matumzi endelevu ya ardhi na kupungua kwa migogoro ya matumzi ya ardhi na maliasili. 

Aidha, mradi huu umewezesha wananchi kupatiwa mikopo kwenye taasisi za fedha, kuandaa mafunzo kuhusu upangaji wa matumizi ya ardhi yamewajengea uwezo wa upangaji na usimamizi wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao. 

Pamoja na hayo pia mradi umesaidia katika uboreshaji wa hali za maisha ya wananchi kwa matumizi ya taarifa za awali za utafiti lakini pia wataalamu wamejengewa uwezo wa uanzishaji na uendeshaji wa mashamba darasa. 

Kazi zilizofanyika hadi sasa katika utekelezaji wa mradi Miongoni mwa kazi zilizofanyika ni kuundwa kwa Kamati za usimamizi wa Maliasili na Mazingira, Kamati za Mipango Bora ya Matumizi ya Ardhi za vijjiji katika vijiji vyote vya mradi isipokuwa wilaya ya Micheweni ambako Kamati za Mipango Bora ya Matumizi ya Ardhi za shehia hazijaundwa. 

Pia yameendeshwa mafunzo ya upangaji wa matumizi ya ardhi kwa maafisa wa ngazi ya wilaya na vijiji, wajumbe wa Kamati za Mipango ya Matumizi ya Ardhi za vijjiji, Halmashauri za Vijiji na baadhi ya wananchi na jumla ya maafisa na wanavijiji 821 wamepata mafunzo hayo. 

Kufanya Tathmini ya utambuzi wa vyanzo vya maji na teknolojia zitakazotumika kupata maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu, kilimo na mifugo katika vijiji vyote vya mradi katika wilaya za Mkalama, Nzega, Magu na Kondoa. 

Kuandaa Mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 15 kwenye wilaya za Mkalama (vijiji vitano), Nzega (Vijiji vitano), Kondoa (vijiji viwili) na Magu (vijiji vitatu). Uainishaji wa Vipaumbele vya maeneo na makundi ya watumiaji raslimali kwa ajili ya urejeshwaji wa uoto wa asili na hifadhi ya bioanuai umefanyika na kukubalika na wadau katika vijiji vyote vilivyoandaa mipango ya matumizi ya ardhi. 

Muda wa kutekeleza mradi huu ni kwa kipindi cha miaka mitano (2017-2022) na gharama ya mradi ni Dola za Marekani millioni 7.156. Mfadhili mkuu ni Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) kupitia Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).

Benki ya NMB yatambuliwa kuwa mwajiri aliyeidhinishwa na Chama cha Wahasibu ulimwenguni (ACCA)

$
0
0

Benki ya NMB imepokea kibali cha ithibati kuwa mwajiri aliyeidhinishwa na Chama cha Wahasibu cha Kimataifa Association of Chartered Certified Accountants (ACCA) katika kutoa maendeleo stahiki ya taaluma kwa wafanyakazi. 

Utambuzi huu unamaanisha kwamba Benki ya NMB ina kiwango cha kimataifa cha kutoa fursa za wafanyakazi kujiendeleza kitaaluma na kuamini kuwa mafunzo hayo husaidia wanachama wa ACCA kwenye benki na taaluma nyingine kukidhi mahitaji yao ya uzoefu wa vitendo makazini. 

NMB walipokea utambuzi huo kutoka ACCA mwishoni wa mwaka huu, ambapo NMB inakuwa miongoni mwa taasisi 13 nchini na taasisi za kimataifa zisizopungua 7,000 duniani zinazotambuliwa na ACCA. 

NMB na ACCA zitaendelea kuhakikisha wafanyakazi wanakuzwa kwa viwango vya juu zaidi. Ambapo NMB itaendeleza kuweka mazingira mazuri na rafikii ya kufanya kazi ili kusaidia wanachama na wanafunzi wa mafunzo ya ACCA kupata mafunzo stahiki. 

Akizungumza katika mahojiano maalumu, Meneja mwandamizi Idara ya Ukaguzi wa ndani NMB, Gaudence Nganyagwa, amesema ni wakati sasa wa Tanzania na Ulimwengu kufahamu jinsi gani NMB inathamini wafanyakazi wake kwa kuwajengea uwezo ili kuwa wenye ushindani katika kutoa huduma bora yenye weledi wa kimataifa. 

“Tunaamini kuwa ni wakati wa kuifanya Tanzania na Ulimwengu ujue ni kwa kiasi gani NMB tunathamini maendeleo ya wafanyakazi wetu. Kwa miaka mingi, benki imekuwa ikiwekeza katika mafunzo na kuwaendeleza wafanyakazi ili kuzalisha kilicho bora sokoni. 

“Tunaamini kwamba kwa ACCA kutupatia tuzo hii, imethamini na kutambua juhudi zetu za kujitolea katika kuwajengea uwezo wafanyakazi. Tunaamini kuwa kama viongozi katika tasnia ya huduma za kifedha, ni jukumu letu kuhamasisha taasisi zingine kuwekeza katika stadi za watu.”amesema Nganyagwa. 

Nae Mkaguzi wa Ndani wa NMB Sulemani Manyiwa amesema faida kubwa kwa NMB kuwa mwanachama wa ACCA ni kuifanya NMB kuwa na mwonekano wa kimataifa. 

“Kuwa mwajiri aliyeidhinishwa wa ACCA kunaboresha mwonekano wa benki kimataifa. Ni rahisi kwa NMB kuajiri na kuendeleza vipaji bora katika soko. NMB sasa inaweza kutangaza nafasi mbalimbali kimataifa kupitia tovuti za kazi za ACCA na kushiriki katika maonesho ya kazi kimataifa. 

“Hii pia itafungua milango hata kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi au wageni wanaotaka kuendeleza kazi zao na mwajiri aliyejitolea nchini Tanzania. Tafiti zetu na dodoso sasa zitashughulikiwa na ACCA ili kuongeza ufahamu wa kitaalam kwa mustakabali wa tasnia. Pia tutapigwa msasa wa mara kwa mara na mwelekeo wa tasnia na kufanya tafiti na matukio ya pamoja na ACCA.”amesema. 

Akithibitisha kuwa nafasi ya kujiendeleza kielimu na kitaaluma kwa wafanyakazi wa NMB ni ajenda nyeti na ya kimkakati, Kaimu Ofisa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu, Emmanuel Akonaay aliongeza kuwa uwekezaji wa benki katika kuendeleza wafanyakazi ni uwekezaji makini ambao utahakikisha benki ya NMB inaendelea kuwa benki bora katika kuvutia vipaji na kuviendeleza. 

“Benki pia itapata huduma bora zaidi na za haraka kutoka kwa ofisi ya ACCA ya Tanzania kuhusu suala lolote. Wanachama waliohitimu mafunzo ya ACCA ambao ni wafanyakazi wa NMB watakuwa na uhakika wa kutunza uanachama wao, na wataweza kujiendeleza na fursa mbalimbali za ACCA katika gharama ndogo zaidi” amesema. 

ACCA inafanya kazi katika nchi 179 ikiwa na dhamira ya kuwa kiongozi wa ulimwengu katika kuunda na kuimarisha uwezo na utendaji wa uhasibu kote ulimwenguni. 

Wataalam wajengewa uwezo kupunguza vifo kwa watoto wanaozaliwa utumbo nje

$
0
0
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto nchini Uingereza, Dkt. Naomi Wright akielekeza namna ya kumhudumia mtoto aliyezaliwa matumbo yakiwa nje.

 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Zaituni Bokhari akielezea kwa vitendo namna ya kutumia mfuko safi wa plastiki ili kuzuia upotevu wa maji maji na joto la mwili kwa mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje kabla ya kumpeleka katika hospitali yenye wataalam bobezi.

 Wataalam wa Afya wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa hospitalini hapa leo.

 Daktari wa Watoto MNH, Dkt. Neema Bayyo akionyesha jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje.

 Dkt. Zaituni Bokhari akishirikiana na Dkt. Neema kuhifadhi matumbo yaliyotoka nje kwa kutumia mfuko maalum (Silo bag).

Dkt. Bokhari na Dkt. Wright wakielekeza namna mama anavyotakiwa kumbeba mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje mara baada ya kupatiwa huduma ya kwanza.





Wataalam wa Afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo wamejengewa uwezo ili kuwasaidia kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa nje.


Ambapo takwimu za Hospitali ya Taifa  Muhimbili zinaonyesha kuwa asilimia 100 ya watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa nje hupoteza maisha kutokana na ukosefu wa elimu kwa watoa huduma za afya ya namna wanavyoweza kutoa huduma ya kwanza kabla ya kumfikisha mtoto katika hospitali zenye wataalam bobezi.


Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Zaituni Bokhari wakati wakutoa mafunzo hayo kwa njia ya vitendo yanayolenga kuwafikia watoa huduma za afya katika hospitali mbalimbali za rufaa ndani na nje ya Dar es Salaam.



“Tunatumaini kuwa mafunzo haya yatasaidia kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa utumbo ukiwa nje ambapo hadi sasa tayari madaktari na wauguzi wa MNH-Upanga na Mloganzila wamekwisha kupatiwa mafunzo na kuanzia kesho tutaanza kuzifikia hospitali mbalimbali za rufaa ndani na nje ya Dar es Salaam ili kuwapatia mafunzo haya,” amesema Dkt. Bokhari.



Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto nchini Uingereza, Dkt. Naomi Wright ametaja nchi nne ambazo zimechaguliwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa watoto hao kuwa ni Tanzania, Ghana, Zambia na Malawi.



“Sababu hasa ya Tanzania kupatiwa mafunzo haya ni kutokana na ongezeko la vifo vya watoto wanaozaliwa matumbo yakiwa nje ambapo kwa nchi zilizoko kusini wa jangwa la Sahara ni zaidi ya asilimia 98%,” amesema Dkt. Wright.


Baadhi ya mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na jinsi ya kumhudumia mtoto aliyezaliwa utumbo ukiwa nje, njia sahihi za kutoa huduma kwa mtoto huyo kwa kutumia mifuko safi ya plastiki na hatua za kufuata wakati wa kujiandaa kumtoa mtoto katika hospitali aliyopokelewa hadi kumfikisha katika hospitali yenye wataalam bobezi.



T-PESA WAINGIA MAKUBALIANO KIBIASHARA NA HALOPESA

$
0
0


Mkuu wa Kitengo cha T-PESA, Lulu Mkudde (kulia) akibadilishana nakala ya hati ya makubaliano ya ushirikiano kibiashara na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Halopesa, Bw. Magesa Wandwi (kushoto) mara baada ya kusaini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam. Kwa makubaliano hayo hivi sasa wateja wa T-Pesa wataweza kutuma pesa kwenda mtandao wa Halopesa na vile vile wa Halopesa kutuma kwenda T-Pesa.
Mkuu wa Kitengo cha T-PESA, Lulu Mkudde (kulia) akisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano kibiashara na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Halopesa, Bw. Magesa Wandwi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Kwa makubaliano hayo hivi sasa wateja wa T-Pesa wataweza kutuma pesa kwenda mtandao wa Halopesa na vile vile wa Halopesa kutuma kwenda T-Pesa.

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kupitia kampuni yake tanzu ya T-PESA imeingia makubaliano ya kibiashara na HaloPesa, ambapo kwa sasa wateja wa T-PESA wanaweza kutuma pesa kwenda Halopesa na vile vile wa Halopesa kutuma pesa kwenda T-Pesa.

Makubaliano hayo ya kibiashara yamesainiwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo Mkuu wa Kitengo cha T-PESA, Bi. Lulu Mkudde ameiwakilisha T-PESA huku HaloPesa ikiwakilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Bw. Magesa Wandwi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bi. Mkudde alisema kupitia wakubaliano hayo kwa sasa mteja wa T-PESA ataweza kununua vifurushi, muda wa maongezi, kulipia bili na kufanya miamala mbalimbali kwenda taasisi zingine.

"Huduma hizi ni kwa wateja wote ambao wanatumia mtandao wa simu wa TTCL na pia kwa mtandao wa simu wa Halotel. Napenda kutumia fursa hii pia kuwapongeza ndugu zetu wa kampuni ya Halotel kwa kuunganisha taasisi kadhaa za umma kote nchini kwa kupitia 'Optical Fiber' na kuunganisha vijiji zaidi ya 1000 kwenye gridi ya mawasiliano ya simu ambayo hapo awali haikuhudumiwa," alisema Bi. Mkudde.

Aidha aliongeza kuwa T-PESA ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) inazidi kuboresha huduma zake kwa wateja wake siku hadi siku nchi nzima.

Hata hivyo alibainisha uboreshaji huduma za T-Pesa umeleta ufanisi na kuongeza kwa matumizi ya miamala ya kieletronikia ambayo ni pamoja na uuzaji na ununuzi wa bidhaa na utoaji wa huduma kwa njia za ki-elektroniki huku wakizingatia usalama na unafuu wa huduma.

T-PESA nikampuni ambayo imedhamiria na inatekeleza adhma ya kuwafikishia wananchi huduma za kifedha kwa njia za simu mahali walipo ili kuokoa muda wao ambao wanautumia kuzalisha na kukuza uchumi. T-PESA imekuwa kiungo muhimu cha kurahisisha shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na biashara na pia ufikishaji wa huduma kwa wananchi zaidi ya milioni mbili walokuwa mjini na vijijini.

Mkuu wa Kitengo cha T-PESA, Lulu Mkudde (kulia) akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Halopesa, Bw. Magesa Wandwi.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Halopesa, Bw. Magesa Wandwi (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha T-PESA, Lulu Mkudde.

WorldRemit yazindua huduma ya gharama nafuu ya utumaji wa pesa kwenda akaunti ya M-Pesa nchini Tanzania

$
0
0

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (wapili kulia) akimkabidhi bango Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui kuashiria uzinduzi wa huduma ya World Remit itakayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 50 ulimwenguni. Wengine kushoto ni Meneja Mkazi wa World Remit Tanzania, Cynthia Ponera na Meneja Maendeleo ya Biashara M-Pesa, Ruth Moshi.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya World  Remit itakayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 50 ulimwenguni. Wengine ni Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui na Meneja Mkazi wa World Remit Tanzania, Cynthia Ponera.
Meneja Mkazi wa World Remit Tanzania, Cynthia Ponera (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya World Remit na Vodacom M-Pesa. Wengine ni Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni na Meneja Maendeleo ya Biashara M-Pesa, Ruth Moshi.
Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya World Remit itakayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 50 ulimwenguni. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni  na Meneja Maendeleo ya Biashara M-Pesa, Ruth Moshi.
**************************************
Desemba 17, 2019, Dar es salaam. Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na vinara wa kutoa huduma ya kutuma pesa kwa njia ya mtandao WorldRemit , watawawezesha zaidi ya watumiaji wa M-Pesa Zaidi ya milioni 10 kupokea pesa moja kwa moja katika akaunti zao kutoka kwa marafiki na familia wanaosafiri na kufanya kazi nje ya nchi.

Huduma hiyo mpya inaongeza urahisi wa wapokeaji wa uhamishaji wa pesa mijini na vijijini kwani wanaweza kupokea pesa kutoka kwa jamaa na marafiki nje ya nchi moja kwa moja kwenye simu zao, bila kuhitaji kuwa na akaunti ya benki au kuunganishwa katika mtandao.

WorldRemit ni mojawapo ya vinara ulimwenguni katika utoaji wa huduma ya uhamishaji pesa kupitia akaunti za simu ya mkononi, ambapo wameunganishwa na akaunti zaidi ya milioni 160 katika nchi 29. Mbali na huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi, kampuni hiyo pia inatoa huduma za uhamishaji wa kibenki,huduma ya kuchukua pesa papo hapo na kuongeza muda wa maongezi nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa M-Pesa Ltd Epimack Mbeteni alisema, “Ushirikiano huu mpya na WorldRemit utatuwezesha kutambua malipo yanayofanyika kuja nchini Tanzania kila mwaka, utaongeza urahisi na uwezo kwa familia na marafiki nchini Tanzania kupokea pesa kupitia M-Pesa kutoka ulimwenguni kote na kufaidika na huduma za mawakala wetu zaidi ya 106,000 wa M-Pesa kote nchini, pamoja na mfumo wetu wa kibenki, unaowaunganisha na M-Pesa. Hii ni njia mojawapo ya kuboresha maisha ya wateja wetu “. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mwaka 2017 Wahamiaji wa kiafrika walituma dola bilioni 38 kurudi nyumbani ambapo mwaka huu inakadiriwa kufikia bilioni 39.6. Pesa inayotumwa kwa familia hutumika kuleta maendeleo na kufanya shughuli mbalimbaliza kiuchumi.

Malipo katika kiwango cha kidunia kwa Tanzania mara nyingi yanafanyika kupitia katika benki, ambapo bado kuna changamoto za gharama za kutuma, utaratibu wa utambulisho na muda unaotumika hadi kupata pesa.

“Ushirikiano huu utatoa suluhisho mbadala kwa kuwepo na wepesi na gharama nafuu katika kupokea pesa kutoka nje ya nchi kwa maana ya familia kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao za M–Pesa na wanaweza kuzitumia kwaajili ya kuleta maendeleo na katika shughuli nyingine za kiuchumi kama akiba na mikopo, huduma ya kutoa pesa zaidi,malipo ya kieletroniki na nyingine nyingi kutoka Vodacom,” aliongeza Epimack.

Kwa kutumia WorldRemit Watanzania wanaoishi katika nchi zaidi ya 50, ambazo ni pamoja na Amerika, Uingereza na Canada huokoa muda wao mwingi na pesa kwani hawahitaji kusafiri kwenda kwa wakala wa kuhamisha pesa na kulipa ada ya kutuma C2: VODACOMGENERAL pesa nyumbani. Badala yake wanaweza kutuma pesa kwa njia ya mtandao wakati wowote kwa kutumia zana (app) au tovuti ya WorldRemit.

WorldRemit hailazimiki kulipa gharama zinazohusiana na mawakala wa maeneo katika nchi zinazohusika kutuma pesa, kampuni inapeleka akiba hizi moja kwa moja kwa wateja.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, gharama ya wastani ya kutuma £120 (~ $ 155) kutoka Uingereza kuja Tanzania ni karibu 9.5% Gharama ya WorldRemit kwa kiasi kama hicho inaanzia chini ya 2%. Kampuni hiyo pia kwa sasa imeondoa gharama katika miamala mitatu ya kwanza endapo watatumia namba ya utambulisho 3 FREE wanapofanya malipo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa World Remit ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Sharon Kinyanjui alisema kwamba ushirikiano huu utapunguza ada za kutuma fedha, “uzinduzi huu utapunguza ada ambazo wateja wamekuwa wakilipa, hii ni kwa sababu kila kitu kinafanyika kidijitali,” aliongeza.

Meneja wa WorldRemit Tanzania, Cynthia Ponera, alisema, “Huduma yetu ya kuhamisha pesa kwa Tanzania inakua kwa zaidi ya asilimia 100, mwaka hadi mwaka, na huduma ya pesa kwa njia ya simu ya mkononi ndiyo njia yetu kuu tunayoitumia kutuma pesa nchini.

Tunafurahi kushirikiana na Vodacom kupanua mtandao wetu zaidi na kuwaunganisha wateja zaidi ya milioni 12 wa M-Pesa kwenye huduma yetu ya kuhamisha pesa. Ushirikiano wetu utapunguza gharama ya kutuma pesa nchini na kuunga mkono mipango ya ujumuishaji wa kifedha kwa kuwapa fursa wapokeaji walioko vijijini katika kupata huduma hii rasmi ya uhamishaji pesa huko walipo”, alihitimisha bi. Ponera.

NMB yaahidi kushirikiana na Serikali kukuza utalii

$
0
0
BENKI ya NMB imeahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia harakati za Serikali kukuza Utalii nchini, ili kuinyanyua zaidi sekta hiyo ambayo inaongoza katika kuchangia pato la taifa na kuingiza fedha nyingi za kigeni ukilinganisha na sekta nyingine.

Ahadi hiyo ilitolewa na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa NMB-Filbert Mponzi, wakati wa Chakula cha Usiku, kilichoandaliwa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO) na kufadhiliwa na NMB, kikihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda.

Katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Arusha, Mponzi alibainisha kuwa, NMB imeshaanza kutoa mikopo ya magari kwa Waongoza Watalii ‘Tour Operators Vehicle Finance,’ lengo likiwa ni kuwawezesha waongozaji kurahisisha majukumu yao na kuvutia watalii zaidi na kukuza pato la taifa.

“Ni mikopo inayolenga kuwawezesha Waongoza Watalii kufanya biashara ya utalii bila kikwazo na kujiingizia kipato, ikiwa ni pamoja na kulinufaisha taifa kutokana na shughuli za utalii. NMB tumewekeza kwenye Sekta ya Utalii na imedhamiria kutoa rasirimali muhimu za kuwezesha ukuaji wa sekta hii.

Aliongeza kuwa, NMB wanashirikiana na Kampuni ya Hanspaul na RSA, huku akizitaja baadhi ya huduma walizojikita kuzitoa katika Sekta ya Utalii kuwa ni pamoja na ‘Asset Financing,’ Internet Banking, Makusanyo na Mapato ya TANAPA na NCAA na kurahisisha malipo kupitia Visa na Mastercard.

Kwa upande wake, Profesa Mkenda alikiri kuwa NMB ni wadau muhimu wenye mchango mkubwa katika ukuaji wa Sekta ya Utalii, ambayo inakua kwa kasi zaidi, hivyo akaipongeza benki hiyo kwa kushirikiana vyema na Serikali katika kukuza sekta hiyo.

Alifafanua kuwa, NMB imejipanga vya kutosha kuendeleza ushirikiano na Serikali pamoja na wadau katika kukuza Utalii nchini kwa kuwekeza zaidi kwenye sekta hiyo, ambayo ni kinara wa uchangiaji wa pato la taifa na kuingiza fedha nyingi za kigeni.

Mkenda aliwataja Benki ya NMB pamoja na TATO kuwa ni kati ya wabia muhimu katika maendeleo ya sekta hiyo na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana vyema na wabia hao ili kuibakisha Sekta ya Utalii kuwa vinara wa uchangiaji wa pato la taifa.

"Napenda kuwashukuru sana NMB kwa kuwezesha kufanikisha jambo hili, pia tumefurahi mnaiunga mkono Serikali, kwani nimesikia katika risala yenu kuwa mtaenda kule ambapo Serikali inaenda," alisema Profesa Mkenda.

Awali Mwenyekiti wa TATO-Willy Chambulo, alisema kuwa chama hicho kitaendelea kushirikiana na Benki ya NMB katika kukuza utalii na kuwawezesha waongoza watalii kutekeleza majukumu yao vema kwa ustawi wa sekta hiyo na ukuaji wa pato la taifa.
 Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa Benki ya NMB-Filbert Mponzi akizungumza na wanachama wa chama cha waongoza watalii Tanzania (TATO) chenye lengo la kuihimiza ushirikiano kati yao.
 Mponzi akibadilishana mawazo   na baadhi  ya wageni Waalikwa
Mponzi akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa.
 Sehemu ya wageni waalikwa
 

Benki ya DCB yaziasa familia kushiriki mazoezi ya viungo

$
0
0
  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya  DCB, pampja na wakimbiaji wengine wakipasha viungo wakati wa mashindano ya Familia Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach jijini Dar es Salaam hivi karibuni. DCB ilidhamini tukio hilo. 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB walioshiriki mbio za Familia Marathon wakionyesha medali zao mara baada ya mbio hizo katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hilo lilidhaminiwa na DCB. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB walioshiriki mbio za Familia Marathon pamoja na wakimbiaji wengine wakishangilia mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach, Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hilo lilidhaminiwa na DCB.

BENKI ya Biashara ya DCB imezihamasisha familia kujenga tabia ya kushikiri mazoezi ya viungo ili kuweza kuwa na taifa lenye watu wenye afya bora jambo muhimu katika shughuli za uzalishaji mali za kila siku.

Akizungumza na washiriki wa mbio zilizopewa jina la Familia Marathon katika viwanja vya chumvi, Bahari Beach, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa DCB, Rahma Ngassa alisema ni muhimu kufanya mazoezi ili kuupa mwili afya na nguvu na kuzalisha mali. 

“Ni ukweli usiopingika kuwa magonjwa mengi yasiyo ya kuambukiza huchangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya maisha tunayoishi na uzito mkubwa, mazoezi ya mwili yanasaidia sana kupambana na hali hizo”, alisema.

Bi Rahma aliongeza kuwa ili tuweze kuendelea na pia kutimiza azma ya serikali yetu ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda, tunahitaji sana kuwa na rasilimali watu wenye nguvu na afya bora ya kuweza kuzalisha mali kwa wingi.

Mkuu huyo wa mawasiliano alisema ndio maana DCB ilipopata maombi ya kudhamini Familia Marathon walipokea maombi hayo kwa mikono miwili kwani kutokana na umuhimu wa mazoezi kwa afya za wateja wao na watanzania kwa ujumla.

“Wateja wetu wakiwa na afya bora wataongeza kasi ya uzalishaji mali hivyo hata nasi benki tutanufaika kutokana na kuwa kwa wateja wetu wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara kwani biashara zao zikikua na benki inakuwa.

“Endapo tukiwa na watanzania wenye afya bora, tutapunguza mzigo wa ghara za matibabu kutoka ngazi ya familia hadi kwa serikali, natoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na kuwa na utamaduni wa kushiriki mazoezi ya mwili ili kujenga afya bora ya miili yao”, aliongeza Bi Rahma.

Sambamba za hayo Bi Rahma alisema licha ya kujali afya ya wateja wao na watanzania kwa ujumla, DCB imeendelea kutoa fursa na bidhaa mbalimbali kwa wateja zinazolenga kutoa suluhisho la mahitaji ya kifedha kwa wateja wao. “Bidhaa hizi zinawalenga wateja wetu wote wakubwa kwa wadogo, wafanyabishara wakubwa na wadogo, wakulima pamoja na wateja katia makundi mengine”,alisema.

Alizitaja bidhaa hizo kama DCB Sokoni inayolenga kumkomboa mkulima na mfanyabiashara wa kilimo katika mnyororo wake wa thamani, DCB Skonga, ikilenga kuwasaidia wazazi katika suala zima la ada za watoto wao, DCB Lamba Kwanza ambayo mteja huanza hupata riba nzuri mara anapoamua kuwekeza, DCB kibubu ambayo mteja hujiwekea akiba mwenyewe kidogo kidogo huku ikianzisha huduma ya DCB Digital ambayo pamoja na mambo mengine humuwezesha mteja kufungua kaunti mahali alipo na kweza kupata huduma nyingi za kibenki za DCB kwa njia ya kidigitali.

WAZIRI KAIRUKI AIPONGEZA TIRDO KUSAIDIA WAWEKEZAJI WADOGO

$
0
0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kariuki akionja bidhaa ya nyama iliyochakatwa na kuwa soseji soseji inayozalishwa na Kiwanda cha ORI Meat Product Ltd kilichopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019) na kujionea uzalishaji. Kushoto ni Mfanyakazi wa Kiwanda hicho, Martha Gwali na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Goodluck Hussein.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki (kushoto) akitazama bidhaa ya nyama inavyochakatwa na kuwa soseji inayozalishwa na Kiwanda cha ORI Meat Product Ltd kilichopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019) na kujionea uzalishaji. Katikati ni Meneja Uzalishaji wa ORI Meat Product Ltd, Mitesh Dhokie.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki (kushoto) akitazama bidhaa ya nyama inavyochakatwa na kuwa soseji inayozalishwa na Kiwanda cha ORI Meat Product Ltd kilichopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019) na kujionea uzalishaji. Katikati ni Meneja Uzalishaji wa ORI Meat Product Ltd, Mitesh Dhokie.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kariuki akizungumza jambo na Viongozi wa Kiwanda cha ORI Meta Product Ltd kinachochakata bidhaa ya nyama na kuwa soseji wakati alipofanya ziara yake katika Kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019). Kushoto ni Meneja Uzalishaji wa Kiwanda hicho, Mitesh Dhokie na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji, Goodluck Hussein.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akitazama bidhaa ya nyama iliyochakatwa na kuwa soseji inayozalishwa na Kiwanda cha ORI Meat Product Ltd kilichopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019) na kujionea uzalishaji. Kushoto ni Mfanyakazi wa Kiwanda hicho, Martha Gwali.  (PICHA NA MAELEZO)

*******************************

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki amelipongeza Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) kwa kuweka msukumo na mkakati endelevu wa kuwaendeleza na kuwasaidia wafanyabiashara na wawekezaji wadogo nchini.

Akizungumza na Uongozi na Wafanyakazi wa Kiwanda cha kuchakata nyama cha ORI Meat Product Ltd leo Jumatano (Desemba 18, 2019), Waziri Kairuki alisema TIRDO imeendelea kutekeleza vyema majukumu kupitia shabaha iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika ujenzi wa viwanda unaochochea katika kukuza mnyororo wa thamani na kuleta tija iliyokusudiwa.

Aliongeza kuwa msukumo uliowekwa na Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) ni kuhakikisha kuwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wanakuwa na fursa kuwa katika kukuza uchumi kwa kuwawezesha kujenga viwanda vidogo vidogo na kuchakata bidhaa zenye ubora.

‘’Niwapongeze TIRDO kwa kutambua wajibu wenu katika masuala ya utafiti na viwanda lakini pia kutoa eneo lenu lenye ukubwa square (mraba) mita 600-700 na ghorofa moja na kukodisha kwa kiwanda cha ORI na kwa msukumo huu tutaweza kuwasaidia wajasiriamali, wafanyabiashara na wenye viwanda vidogo kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa’’ alisema Waziri Kairuki.

Aidha Waziri Kairuki aliitaka TIRDO kuhakikisha kuwa mpango huo unakuwa endelevu ili kuwafanya wafanyabiashara, wawekezaji na wajasiriamali wadogo wanaendelea kupata maeneo makubwa zaidi kupitia miradi yake hatua itakayowawezesha kuweza kuongeza mnyororo wa thamani ya uzalishaji na hivyo kuleta tija kwa taifa.

Waziri Kairuki pia aliipongeza Kampuni ya ORI Meat Product Ltd kutokana na juhudi na ubunifu mkubwa walioufanya katika kuchakata bidhaa za nyama kupitia soseji za ng’ombe na kuku, na kuongeza kuwa Ofisi yake itawasiliana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuona namna bora mauzo na uzalishaji wa bidhaa za kampuni hiyo.

‘’Ndani ya muda mfupi wa kipindi cha mwaka mmoja vijana hawa wa Kitanzania wameweza kuwekeza mtaji wa Tsh Bilioni 1.1, walianza na wafanyakazi 50 lakini sasa wapo 64 lakini pia wameweza kuongeza mnyororo wa thamani kupitia label (alama), vifungashio vya plastiki, wazalishaji wa kuku ambapo wajasiriamali wanaweza kuuza kuku katika kiwanda hiki’’ alisema Waziri Kairuki.

Akifafanua zaidi Waziri Kairuki aliitaka Kampuni hiyo kuendelea kupanua shughuli zake ikiwemo kuimarisha mtandao wa masoko ya ndani na nje ya nchi, ikiwemo soko la Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na kuzalisha bidhaa zenye viwango na ubora unaostahiki.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO, Humphery Ndossi Ofisi yake imeendelea kufanya kazi na wawekezaji wa ndani kwa kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara zao, na miongoni mwao ni Kiwanda cha ORI Meat ambapo wamekuwa wakitoa msaada mbalimbali ikiwemo upimaji wa ubora wa bidhaa za kiwanda hicho.

Aliongeza kuwa TIRDO imeendelea kusimamia wajibu wa msingi wa majukumu yake kwa kuwasisitiza wafanyabiashara kuzingatia ubora wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini ili kuweza kuliepusha taifa na mlundikano wa bidhaa bandia na zisizo na ubora na kuzuia matumizi yake ili kulinda afya za wananchi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ORI Meat Product Ltd, Goodluck Hussein alisema Ofisi yake imeendelea kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Serikali na imeweza kuuza pakiti 1200-1500 kwa mwaka, jambo ambalo lilikuwa gumu kwa miaka ya nyuma kutokana na uwepo wa bidhaa nyingi za nyama kutoka nje ya nchi.

TTCL yafurahisha wapenzi wa filamu, sasa ni movies bila intaneti

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi wa huduma ya 'T-Burudani' toka TTCL inayomwezesha mteja kupakua, kuhifadhi pamoja na kuangalia filamu aipendayo bila ya kuwa na mtandao wa intaneti. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Puyo Nzalayaimisi pamoja na Meneja Mauzo na Usambazaji wa TTCL, Bw. Hamis Mruta (kushoto). 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizinduwa huduma ya 'T-Burudani' toka TTCL inayomwezesha mteja kupakua, kuhifadhi pamoja na kuangalia filamu aipendayo bila ya kuwa na mtandao wa intaneti. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi wa huduma ya 'T-Burudani' toka TTCL inayomwezesha mteja kupakua, kuhifadhi pamoja na kuangalia filamu aipendayo bila ya kuwa na mtandao wa intaneti. Kushoto ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa TTCL, Bw. Hamis Mruta. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (wa kwanza kulia) akiangalia ratiba ya kampeni ya Mtaa kwa Mtaa ya TTCL kuanza kuwazungukia wateja wake maeneo mbalimbali. 


WATANZANIA hususan wapenzi wa filamu nchini sasa watanufaika na huduma ya 'T-Burudani' toka TTCL itakayomwezesha mteja kupakua, kuhifadhi pamoja na kuangalia filamu aipendayo bila ya kuwa na mtandao wa intaneti

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, kutambulisha huduma hiyo ambayo kwa sasa inatolewa bure, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba alisema kampuni hiyo imeamua kutoa zawadi ya T-Burudani kwa wateja wake hasa wapenzi wa filamu.

"T-BURUDANI ni huduma itolewayo na TTCL itakayomuwezesha mteja kupakua filamu bila kutumia kifurushi cha intaneti, mteja ataweza kuangalia filamu zote za ndani ya nchi pamoja na kimataifa. Huduma hii mteja ataweza kupakua kupitia simu janja ya mkononi pamoja na kompyuta ya kiganjani 'Tablet'," alisema Bw. Kindamba.

Akifafanua zaidi Kindamba alisema TTCL katika huduma hiyo imeweka mfumo rahisi utakaomuwezesha, mteja kupakua filamu aitakayo kutokana na maudhui toka kote duniani pamoja na Hollywood, Nollywood, Bollywood, HBO, hata Bongo movies.Aidha aliongeza kuwa mteja ataweza kuangalia kwa kipindi atakachohitaji lakini vile vile ataweza kupakua na kuhifadhi kwa gharama nafuu kupitia 'App'. Sanjari na huduma hiyo alibainisha TTCL imeamua kuwafuata wateja wake maeneo yao kwa kuwatakia heri na sikukuu kupita kampeni yake ijulikanayo kama MTAA KWA MTAA, pia kuwahudumia zaidi.

"Zawadi hii ni kwa wateja wetu wa TTCL ni kwa gharama nafuu sana ambapo kuna kifurushi kwa shilingi elfu moja kwa siku,elfu tatu kwa siku saba na shilingi elfu tano kwa mwezi mzima. Hakika hii ni burudani tosha kwa watanzania. Mteja ataweza kupata huduma hii kwa kupitia T-Burudani App ambayo inapatikana katika 'playstore' na 'App store'. Aidha nitangaze rasmi kwa sasa bidhaa hii ni bure kabisa pasipo na malipo yoyote mpaka tarehe 31 Desemba," alisema.

"Nichukue fursa hii kuwatangazia rasmi wateja wetu bidhaa hii ni bure kwa muda maalumu hasa katika kuwashukuru wateja wetu kwa kuwa nasi kwa kipindi cha mwaka mzima. T-Burudani ndio zawadi pekee na nono katika msimu huu wa sikukuu kulinganisha na watoa huduma wengine wa mawasiliamo. Tuendelee kufurahia kurudi Nyumbani kumezidi kunoga na T-Burudani."

Hata hivyo alisema zawadi hiyo kwa wateja, inaenda sanjari na kampeni ya MTAA KWA MTAA inayolenga kuwatembelea Mawakala wao pamoja na wateja wa TTCL

NSSF YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU MIRADI YA NYUMBA KIGAMBONI

$
0
0


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisistiza kwa menejimenti ya NSSF, umuhimu wa miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya  kukagua uboreshaji wa miundombinu wa  nyumba hizo leo tarehe 18, Desemba, 2019. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisistiza kwa menejimenti ya NSSF, umuhimu wa miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya  kukagua uboreshaji wa miundombinu wa  nyumba hizo leo tarehe 18, Desemba, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akikagua shughuli za uboreshaji miundombinu katika  miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18, Desemba, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na vijana wa SUMA JKT wanahusika na uboreshaji wa miundo mbinu miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya  kukagua uboreshaji wa miundombinu hiyo  leo tarehe 18, Desemba, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akikagua shughuli za uboreshaji miundombinu katika  miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18, Desemba, 2019.
*************************************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameridhishwa na utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu Majaliwa aliyoyatoa mwishoni mwa mwezi Novemba, mwaka huu baada ya  kukagua miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es Salaam.

Akiongea mara baada ya kukagua miradi ya nyumba za NSSF leo Desemba 18, 2019 baada ya kukagua miradi ya nyumba za NSSF zilizopo wilayani Kigamboni, Jijini Dar es salaam, Mhe. Mhagama amesema kuwa Mhe. Waziri Mkuu alielekeza menejimenti ya NSSF Kuharakisha kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo ili ziweze kutumiwa na watanzania.

Waziri Mkuu alielekeza menejimenti ya NSSF kuwasiliana na vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu na elimu ya kati, Taasisi za Umma ili kuangalia uwezekano wa wanafunzi wa  elimu ya juu na watumishi wa umma pamoja na watanzania wenye nia ya kutaka kupanga nyumba hizo waweze waweze kupangishwa kwenye nyumba za hizo 161 zilizoko  Tuangoma, 720 zilizoko Mtoni Kijichi.

“Nimefurahishwa katika taarifa yenu kuwa mmewasiliana na vyuo kadhaa ikiwemo DUCE ambao wameonesha nia ya kuomba nafasi za wanafunzi 3000, lakini pia DIT wanahitaji nafasi za wanafunzi 300, tunawasubiri IFM na taasisi nyingine za elimu ya juu na Umma,kwa kuwa kwa Mradi wa Kijichi unazo nyumba 720 ambazo zinaweza kupangishwa na wananfunzi 7,200 kwa mantiki hii inaonesha tunao uwezo wa kukidhi mahitaji ya vyuo vikuu ” Amesema Mhe.Mhagama.

Mhe. Mhagama, ameongeza kuwa katika kuhakikisha nyumba hizo zinakuwa mkombozi wa malazi kwa wanafunzi wa vyuo, hivyo ameishauri menejimenti ya NSSF kuwapa kipaumbele wanafunzi wa kike kwa kuzingatia kuwa takwimu za hivi karibuni zimebainisha kuwa maabukizi mapya ya virusi vya UKIMWI asilimia 40 ni kwenda kwa vijana ambapo asilimia 80 ya vijana ni watoto wa kike wa vyuo vikuu, amabapo mojawapo ya kichocheo cha maabukizi hayo ni  kutokana na kutokuwa na malazi salama.

Waziri Mkuu, alielekeza TARURA kuhakiksha wannatengeneza  miundombinu ya barabara katika miradi ya nyumba za NSSF, ambapo tayari wamekamilisha taratibu za  awali za ujenzi wa barabara hizo na wataalamu wa NSSF tayari wamehakiki gharama za ujenzi wa barabara hizo ili kuona kama zinaendana na uhalisia wa ujenzi utakaofanyika kupitia SUMA JKT. Zahanati

“Katika kuboresha barabara za mitaa za hizi nyumba nimeonakazi inayoendelea  na wameniambia DIT wanafanya kazi yao ya kuweka  taa za sola kwenye barabara za mitaa yote ya nyumba hizi na watafanya kazi kwa wakati kama tulivyokubaliana” amesema Mhagama.

Aidha, agizo jingine kwa menejimenti ya NSSF ilikuwa ni kuboresha miundo mbinu ya Umeme, maji taka na maji safi, ambapo tayari taasisi zinazohusika na miundo mbinu hiyo ikiwemo TANESCO na DAWASA wamekamilisha taratibu za awali za utekelezaji na wameahidi kukamilisha shughuli zake kwa wakati ili nyumba ziweze kutumika.

Waziri Mhagama amefafanua kuwa agizo lingine ambalo NSSF wamelitekeleza ni  Mthamini Mkuu wa Serikali kutathimini nyumba hizo na kutoa   bei halisi ya soko kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma kununua na kupanga katika nyumba hizo.
“Nimefurahishwa na taarifa mliyonipatia kuwa mthamini mkuu wa serikali atakabidhi ripoti yake leo kwa NSSF na naamini sasa watu wengi ambao wameonesha nia ya kupanga au kununua tutawapatia huduma kwa kuwa tunalo kundi la wanafunzi, watumishi wa umma na watu binafsi wenye uwezo wa kununua nyumba hizo”, Amesisitiza Mhagama.

Pia, Waziri Mkuu aliagiza  Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kupewa kipaumbele kwa nyumba 439 za Nungu ambapo Mkuu wa wilaya  na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni walielekezwa kuwasaidia watumishi wa wilaya na Halmashauri hiyo  kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha watumishi  hao kupewa kipaumbele katika kununua au kupanga kwenye nyumba hizo mara ukarabati utakapo kamilika.

“Nimeridhishwa na utekelezaji wa shughuli za miundo mbinu kwa hapa Nungu na hivyo menejimenti ya NSSF wasilianane na Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kuwa uboreshaji wa majengo unaenda vizuri ili watumishi tunaowalenga waweze kutumia nyumba hizo, ” Amesema Mhagama.

Pia Mheshimiwa Mhagama amefurahishwa  na hatua ya LATRA kuanza kutekeleza agizo la kuanzisha njia za mabasi ya daladala   kupitia kwenye nyumba za NSSF Mtoni Kijichi na Dungu ili kuwezesha wapangaji na wananchi watakaonunua na kupanga  nyumba hizo kupata usafiri wa umma, kama ilivyokuwa imeelekezwa na Mhe. Waziri Mkuu.

Aidha, Mhe. Waziri pamoja na kuwapongeza NSSF kuanza kutekeleza maagizo hayo, pia amewataka wazingatie muda uliowekwa wa kukamilisha kazi hiyo, hivyo amewataka kufanya kazi usiku na mchana kwa kuzingatia ubora wa kazi.

“Zingatieni uhalisia wa gharama zinazotumika katika ujenzi wa mradi huu ili fedha za wanachama zitumike vyema kwa kuonekana fedha zimewekezwa kwenye miradi yenye tija ” Amesema Mhe. mhagama
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio, amesema NSSF imeyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri Mhagama  na kwamba watafanya kwa weledi na ubora ili kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa au kupangishwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF, Balozi Ali Idd Siwa amemhakikishia Mhe. Waziri Kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha kuwa maagizo aliyoyatoa yanatekelezwa kwa wakati ili kuhakikisha nyumba hizo zinawanufaisha watanzania.

 Miradi ya nyumba za NSSF, wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam, ipo katika maeneo ya Tuangoma   jumla ya nyumba 161, Dungu nyumba 439 na Mtoni Kijichi   jumla ya nyumba 720.

RAIS MAGUFULI AFUNGUA MRADI WA VISIMA VIREFU PAMOJA NA UJENZI WA MADARASA SHULE YA MSINGI CHATO A-B MKOANI GEITA

$
0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akifungua moja ya mradi wa Kisima kirefu kilichojengwa katika Shule ya Msingi Chato A-B kwa ufadhili wa Emirates Red Crescent-UAE kwa usimamizi na Utekelezaji wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Chato A-B Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waChato katika sherehe za Ufunguzi wa Madarasa yaliyojengwa kwa mchango wake Mhe. Rais Dkt. Magufuli pamoja na mradi wa Visima virefu vya Maji vilivyojengwa na Emirates Red Crescent-UAE kwa usimamizi na Utekelezaji wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini
Tanzania zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Chato A-B Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Msingi Chato A-B mara baada ya kufungua Madarasa pamoja na Ofisi zilizojengwa kwa Mchango wake mwenyewe katika shule hiyo ambayo alisoma elimu yake ya Msingi.
Sehemu ya Madarasa ya Shule ya Msingi Chato A-Bkama yanavyoonekana mara baada ya ujenzi wake kukamilika. PICHA NA IKULU

RC MAKONDA ATOA POLE KWA WANANCHI WALIOATHIRIWA NA MVUA,ASEMA SERIKALI ITAKARABATI MARA MOJA MIUNDOMBINU ILIYOHARIBIWA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Disemba 18  ametembelea na kukagua miundombinu iliyoharibiwa na Mvua ambapo amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali ipo katika hatua ya kukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na Mvua ili irudi katika hali ya kawaida na kuwaondolea wananchi kero.

RC Makonda amesema Serikali imejitaidi kwa kiasi kikubwa Kujenga miundombinu ya kupitisha maji ya Mvua ikiwemo upanuzi wa Mito, Madaraja na Mifereji lakini kinachotokea ni tabia chafu ya baadhi ya Wananchi kutupa taka kwenye miundombinu hiyo jambo linalosababisha maji kushindwa kupita kwenye njia yake na kusababisha mafuriko.

Aidha RC Makonda amewataka wananchi waliojenga na wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhakikisha wanahama kwakuwa Mvua bado zitaendelea kunyesha kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Hata hivyo RC Makonda amesema Serikali kwa sasa inaendelea kutekeleza miradi mikubwa Ujenzi wa Mito na Mifereji kwa lengo la kupunguza kero mafuriko kwa wawananchi ambapo kwa Wilaya ya Ilala kuna ujenzi wa Mito yenye urefu wa Km 16, Temeke Km 14 na Kinondoni Km 8  ili maji yaende moja kwa moja Baharini.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi na Upanuzi wa Mto Ng'ombe, Mto Msimbazi, Ujenzi wa Daraja la Juu eneo la Jangwani pamoja na Maboresho ya eneo hilo ili liweze kutumika kwa shughuli za utalii wa Boti.
 Moja ya nyumba iliothiriwa na mvua ilionyesha jana maeneo kadhaa jijini Dar
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Paul Makonda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mh.Daniel Chongolo sambamba na kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wakikagua maeno mbalimbali yaliothiriwa na mvua ya jana 

 Maeneo yaliothiriwa na mvua ya jana  


KAMPENI YA NMB MastaBoda yafungwa rasmi Kisarawe,DC aishukuru na kuipongeza.

$
0
0
KAMPENI ya MastaBoda inayoendeshwa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuwaunganisha waendesha Bodaboda katika mfumo wa kibenki wa kupokea malipo kwa Mastercard QR kutoka kwa wateja wa Benki ya NMB, Benki zilizounganishwa na Mastacard QR pamoja na mitandao ya simu iliyounganishwa na huduma ya Mastercard QR sasa imevuka boda hadi Kisarawe Mkoani Pwani. 

Akizindua kampeni hiyo na kufunga mafunzo ya siku sita yaliyotolewa na NMB kwa waendesha Bodaboda Wilayani humo, Mkuu wa Wilaya Jokate Mwegelo amesema kampeni hiyo imefika muda muafaka katika Wilaya yake. 

Jokate amesema, kama Wilaya na Serikali wamejipanga kuipokea kampeni hiyo kwa waendesha bodaboda 150 waliyozitokeza katika mafunzo hayo. 

Amesema kupitia kampeni hiyo wanataka vijana wawe mstari wa mbele katika kujenga uchumi wa nchi na maendeleo ya jamii zao. Pia amewataka vijana kuishi kwa malengo kwani sasa wamepata mfumo ambao unaipa ulinzi fedha wanayoipata katika kazi zao za kila siku. 

Aidha Jokate ameimwagia kongole Benki ya NMB kwa kuipa heshima Kisarawe kuwa sehemu ya pili kufikiwa na MastaBoda baada ya kuzinduliwa Dar es Salaam miezi miwili iliyopita. 

"Nashukuru sana NMB kwa kunipa heshima hii kwa Wilaya yangu ya Kisarawe, naamini hamkupanga kuanzia hapa baaada ya Dar es Salaam, ila mmeona jitihada zangu asanteni sana. Hakuna mafanikio bila nidhamu, NMB mmetuletea nidhamu ya pesa pamoja na usalama kwa vijana wetu maana sasa hawatakuwa wanatembea na pesa mfukoni."amesema Jokate. 

Nae Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo amesema NMB imejipanga kuyafikia makundi mbalimbali ya wajasiriamali ili kuwaongeze thamani katika kukuza uchumi wa nchi. 

Amesema MastaBoda ni kampeni ambayo inalengo la kuwafikia waendesha bodaboda zaidi ya Milioni 2 nchi nzima, ila kufikia 2020 watakuwa wamewafikia elfu 75.
Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa Benki ya NMB- Philbert Casmir, akizungumza wakati akifunga rasmi mafunzo ya matumizi ya huduma mpya ya MastaBoda kwa waendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kisarawe na vitongoji vyake. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB-Vicky Bishubo. 
Mmoja wa waendesha Bodaboda akifungua akaunti ya NMB.
Waendesha Bodaboda katika picha ya pamoja baada ya semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Wilaya ya Kisarawe. 
Waendesha Bodaboda wakifurahia jambo wakati wakiendelea na mafunzo ya matumizi ya huduma mpya ya MastaBoda.

DCB YAZINDUA MKOPO WA ADA YA SHULE

$
0
0
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, James Ngaluko (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa DCB Skonga, Zamaradi Mketema, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Fortunata Benedict.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB, Fortunata Benedict (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko. 
Balozi wa bidhaa ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Zamaradi Mketema (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa, Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Fortunata Benedict.

=====  =======  ======  ========  ========
 BENKI ya Biashara ya DCB imezindua huduma ya mkopo maalumu wa Ada ya Shule ikiwa ni fursa nyingine tena itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kulipa ada za watoto wao kwa wakati na uhakika.

Mkopo wa ada wa DCB ni mwendelezo wa mkakati wa benki kubuni huduma na bidhaa bora zinazowanufaisha wateja. Benki imekuja na bidhaa hii ya mkopo wa ada katika harakati ya kuwaondolea hofu wazazi linapokuja suala zima la elimu kwa watoto wao hii ni sambamba na akaunti ya DCB Skonga inayomuwezesha mtoto kusomeshwa pindi mzazi anapopata ulemavu wa kudumu ama kifo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi wa mkopo huu, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bi Rahma Ngassa alisema ‘’DCB inaendelea kuleta kwenye soko bidhaa zinazo kidhi maisha ya watanzania, benki hii ni ya watanzania hivo ni lazima kuja na fursa inayowawezesha wateja wetu kunufaika na benki yao.

Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Bwana James Ngaluko aliongeza ‘’mkopo huu ni wa dharura na ni suluhisho kubwa kwa wateja wetu, siku hazilingani na kama Benki tunataka watoto wetu wasome, elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo tunampa mzazi fursa ya kupata mkopo wa dharura ndani ya masaa 48 kwa ajili ya ada ya mtoto pindi amekwama.

Alisema wakati tunaendelea kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kukaribisha mwaka 2020, Benki tumeona tuwazawadie zawadi ya kipekee kabisa wateja wetu kwani ni jambo lililo dhahiri kuwa suala la ada ni moja ya changamoto kubwa inayowakabili wazazi wengi kila ifikapo mwanzoni mwa mwaka. Mkopo wa Ada wa DCB una riba ya chini sana na utalipwa moja kwa moja kwenye shule ya mtoto. Mkopo huu unakupa fursa ya kukopa hadi shilingi milioni tano ndani ya masaa 48 na muda wa marejesho unachagua mwenyewe hadi miezi sita.

Nae Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi Bi Fortunata Benedict alisema ‘’Wazazi wengi kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao wamejikuta wakihangaika kutafuta fedha za ada kwa njia zozote hivyo kujikuta kuingia katika matatizo. Mzazi sasa huna haja ya kupata stress za kulipa ada, acha DCB ikufikirie masuala ya elimu ya mtoto wako hii ni suluhisho la uhakika la kifedha. 


Ikumbukwe kua mwaka wa 2019 DCB imetoa fursa mbalimbali kwa wateja ikiwemo

· DCB imewapa maelfu ya watanzania fursa ya kuwekeza kwa kununua Hisa na kua wamiliki halali wa benki hii kupitia mfumo wa hisa za upendeleo

· DCB kibubu inampa fursa mteja kuweka akiba mwenyewe kidogo kidogo kupitia simu ya mkononi (DCB Digital) na kuhakikisha watanzania wengi wanafikiwa na huduma za kibenki.

· DCB ilizindua DCB Sokoni inayolenga kumkomboa mkulima na mfanyabiashara wa kilimo katika mnyororo wa thamani

· DCB Lamba kwanza inayomuwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14% papo hapo na kila mwanzo wa mwezi.

· DCB Skonga, ikilenga kuwasaidia wazazi katika suala zima la elimu ya watoto wao pindi watakapopata majanga ya ulemavu wa kudumu au kifo.

WAJASIRIAMALI MOROGORO WATAKIWA KUFAHAMU KANUNI ZINAZOWEZA KUATHIRI BIASHARA ZAO.

$
0
0
KITUO cha ujasiriamali cha CEED Tanzania, kimetoa mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kwa wajasiriamali mkoani Morogoro yenye lengo la kuwawezesha namna ya kusimamia biashara zao, kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto za kibiashara pamoja na fursa mbalimbali mkoani humo.

Akizungumza na wajasiriamali wa mkoani Morogoro, Bw Atiba Amalile ambaye ni Mkurugenzi wa CEED Tanzania, amewakumbusha wajasiriamali hao kuwa haitakuwa biashara kama kawaida ikiwa Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati miaka ijayo.

Naye Bwana Baptist Mnyalape ,mshauri wa masuala ya kodi na mwakilishi wa CEED Tanzania jijini Dodoma amewahimiza wajasiriamali wa Morogoro kuhakikisha wanafahamu kanuni zinazoweza kuathiri biashara zao moja kwa moja.

‘’ Niwakumbushe tu ndugu zangu wajasiriamali kuhusu kuzingatia masuala mazima ya kodi, tuhakikishe tunafahamu kanuni na sheria ambazo zinaweza kuingilia na kuathiri biashara zetu moja kwa moja, ukishindwa kuzingatia haya itagharimu muda wako pamoja na pesa zako," Amesema Mnyalape.

Kwa upande wa mwakilishi kutoka Benki ya CRDB, Dennis Kayanda amewasisitizia wajasiriamali hao juu ya umuhimu wa kufuata sheria ya matumizi ya ushuru wa ardhi na kusema ni hatari zaidi kwa kutafuta mikopo kutoka benki za biashara na kuwekeza katika biashara ambazo zinaweza kuwa hazifanyi kazi katika eneo hilo na hivyo kuathiri biashara.

Naye Bwana Victor Mfinanga mnufaikaji wa mafunzo hayo na Mkurugenzi Mtendaji wa Maziwa Shambani Milk mkoani Morogoro amefurahia kupata nafasi tena kwani mafunzo haya yamemuwezesha kufahamu namna ya kuendesha biashara yake.

‘‘Nimekuwa nikihudhuria mara kwa mara mafunzo ya CEED, mfano mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam na CEED Tanzania yamenisaida kujua habari za biashara bora, namna ambavyo mtu unawezakutumia teknolojia kujifunza namna ya kuendesha biashara yako," Amesema Mfinanga.

Mafunzo hayo yameudhuriwa na wajasiriamali mbalimbali wa mkoani Morogoro na wawakilishi kutoka benki za CRDB, NMB NBC, Azania, pamoja na Benki ya Afrika ambazo kwa pamoja zimewapa elimu wajasiriamali jinsi ya kupata mikopo bila shida na namna ya kutumia mikopo hiyo kukuza biashara zao.
 Mmoja wa wanachama wa CEED Tanzania na Mkurugenzi wa Shambani Milk, Victor Mfinanga akielezea namna ambavyo amenufaika na elimu za ujasiriamali na kutoa wito kwa wafanyabiashara wadogo kuwa na utaratibu wa kujifunza
 Balozi wa CEED Tanzania, Dennis Kayanda akiwafundisha wajasiriamali mkoani Morogoro njia bora za ufanyaji wa biashara
Washiriki mbalimbali wa mafunzo ya ujasiriamali wakifuatilia mafunzo hayo kutoka kwa wawezeshaji. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wajasiriamali mkoani Morogoro.

Athari za mapinduzi ya teknolojia katika soko la ajira zinakabilika

$
0
0
Katika mkutano wa Shirika la kazi Dunia (ILO) uliofanyika mwezi Julai 2019 ilielezwa kuwa ulimwengu wa ajira unapitia mabadiliko makubwa ambayo yanatokana na ubunifu wa kiteknolojia, mabadiliko ya demographia, tabia ya nchi na utandawazi.

Kutokana na mabadiliko hayo Shirika hilo liliamua kuwa na azimio la miaka mia moja ijayo ya ulimwengu wa (kazi) huku likiwataka nchi wanachama kuhakikisha kuwa watu wao wananufaika na mabadiliko hayo.

Kadhalika nchi wanachama zilitakiwa kuendeleza mahusiano ya kazi yaliyopo, ulinzi wa wafanyakazi, kuwezesha ukuaji wa uchumi jumuishi na kuhakikisha kunakuwa na kazi kwa watu wake, ajira za kudumu na kazi za staha.

Katika kutekeleza hilo ILO ilizitaka nchi hizo kuwekeza zaidi katika kuwajengea uwezo watu wake ili waweze kuendana na fursa nyingi zinazojitokeza kwa ajili ya ustawi wao.

Pia ILO ilizitaka nchi wanachama kuimarisha taasisi za kazi ili kudhibiti mikataba ya ajira, kupunguza umasikini, na kulinda ajira za baadaye kwa utu, usawa na kulinda uchumi.

Kadhalika kuwekeza katika maendeleo ya kazi endelevu na za staha na katika hili ILO ilisisitiza kuwa mabadiliko yanayoendelea yanaweza kuathiri uchumi na kazi hivyo mataifa yanapaswa kutoa kipaumbele kwa uwekezaji endelevu na wa muda mrefu ambao unatoa kipaumbele kwa binadamu na kulinda dunia.

Mbali na ILO kulimulika hilo suala mabadiliko hayo limekuwa ni tishio kwa ajira za wengi, wapo wanaodhani kuwa kwa siku zinavyozidi kwenda soko la ajira litazidi kuwa gumu kuliko sasa.

Jumanne Mtambalike ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Kampuni ya teknolojia iitwayo Sahara Ventures , yeye kwa taaluma ni mhandisi wa programu za Compyuta na sasa anasema teknolojia ndiyo kila kitu.
Anasema katika kada yake mtu apaswa kujifunza kila siku ili kuenza kuendana na kinachotokea ulimwenguni kwa kuwa teknolojia inabadilika kwa kasi naye anatakiwa kubadilika hivyo ni lazima atenge muda wa kujifunza.

Jambo zuri ni kwamba mambo mengine anaweza kuyapata mtandaoni na huko unaweza kujifunza vitu vipya kwakuwa kozi nyingi zisizo za kulipia lakini unaweza kujifunza vitu muhimu.

Anasema kutokana na mwenendo wa dunia hakuna budi kuwapa vijana ujuzi zaidi ya maarifa wanayoyapata shuleni, wanapaswa kuwa na fikra tunduizi na kuelewa namna ya kuchambua vitu sanjari na kufahamu namna ya kuwasiliana na kuchangamana na watu.

“Watu sasa wanapaswa kuwa na ujuzi wa vile vitu ambavyo kompyuta haiwezi kufanya, vitu ambavyo mashine haziwezi kufanya, hilo ndilo litakalowafanya waendelee kuonekana ni watu wa muhimu,” alisema.

Anasema miaka ijayo kazi nyingi zitachukuliwa na mapinduzi ya teknolojia lakini pia nyingine zinaweza kutengenezwa kupitia mapinduzi hayo suala la muhimu ni maandalizi ya kizazi ili kuweza kupata kazi hizo.

“Ukienda katika mtandao wa instagram sasa maelfu ya wanawake wanatumia jukwaa hilo kuendesha biashara zao, nafikiri sasa kinachohitajika sio ujuzi kwani kwa sasa kompyuta inaweza kufanya karibia kila kitu nadhani tunapaswa kufundisha zaidi ya mtalaa,” anasema Mtambalike

Mwingine ni Tulalana Bohela, mwanzilishi mwenza wa kampuni ya simulizi na teknolojia iitwayo Onastories anasema huwa anawaambia wanafunzi na wafanyakazi wenzangu kuwa google ni rafiki.

Anasema hatma ya kazi inakwenda kasi kwenye sekta tofauti akitolea mfano sekta ya uzalishaji ambayo ina nafasi kubwa katika kukuza uchumi lakini kuna kuhama kuelekea matumizi zaidi ya mashine kuliko watu na mashine zinajifunza na kufanya kazi kwa haraka, kuendana na mazingira kuliko mtu.

“Kwa kazi yangu mimi nafikiri mashine haiwezi kufanya kwa sababu inahusu zaidi mtu na roboti sidhani kama inaweza kufanya labda ipandikiziwe binadamu, tunapaswa kubuni shughuli ambazo haziathiriwi na mabadiliko hayo,” anasema.

Anaongeza kuwa kwa ujumla Tanzania bado ipo nyuma katika mapinduzi ya viwanda awamu ya nne na kuna wakati alizungumza na wanafunzi tofauti wakamwambia kuwa wanadhani kuwa mambo wanayojifunza shuleni ni mambo ya awamu ya pili ya mapinduzi ya viwanda.

“Nafikiri wanafunzi wanapaswa kuwa wanafundishwa namna mazingira yanavyobadilika, unaweza kufundisha mtu ujuzi wa ubunifu wa kutatua changamoto katika jamii, uwezo wa kujieleza, kujiamini, kupanga mikakati na sio kwa ajili ya waajiri wao bali wao wenyewe,”

Alisema hilo linapaswa kutiliwa mkazo zaidi kwa vijana ili wajua thamani yao ni kile wanachokizalisha kwa minajili ujuzi, fikra na ubunifu.
Aidha Utafiti mmoja uliofanyika nchini India mwaka huu na kuchapishwa na taasisi ya McKinsey Global unaonyesha kuwa mpaka ifikapo mwaka 2025 ajira milioni 45 zitakuwa zimepotea kutokana na mapinduzi ya teknolojia, hata hivyo utafiti huo unaonyesha kuwa zaidi ya ajira milioni 65 zitatengenezwa na mapinduzi hayo.

Vilevile ripoti ya jukwa la kimataifa la uchumi (WEF) ya mwaka 2018 unaonyesha kuwa kukuwa kwa teknolojia kutaondoa kazi zaidi ya milioni 75 hadi kufikia mwaka 2022 hata hivyo teknolojia itatengeneza kazi mpya milioni 133 katika kipindi kama hicho.

Ripoti hiyo iliyotokana na utafiti uliofanywa katika makampuni makubwa 313 duniani yanayotoa huduma tofauti inasema jambo hilo litatokana na namna ambavyo teknolojia itabadilisha namna ya ufanyaji wa kazi tofauti na ilivyokuwa awali.

“Takribani asilimia 50 ya kampuni zinatarajia mifumo ya teknolojia katika uzalishaji itapunguza nguvu kazi kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 22, mwaka 2018 asilimia 71 ya masaa ya kazi yanafanywa na binadamu huku asilimia zilizosalia zikifanywa na mashine. kufikia 2022 muda wa nguvu kazi utapungua hadi asilimia 58,” ilieleza ripoti hiyo.

Hata hivyo lengo la mabadiliko ya teknolojia ni kurahisisha shughuli mbalimbali na sio kuua ajira za watu na mpaka sasa tu teknolojia umeongeza kasi na ufanisi wa kufanya shughuli Fulani kwa kutumia mifumo ya kompyuta.

Mambo mengi hivi sasa yamerahisishwa mtu akiwa na simu ya mkononi ama kompyuta anaweza kufanya mambo mengi kwa urahisi akiwa sehemu moja kwa kubonyeza tu katika simu yake.Mfano huduma nyingi kama kuitisha usafiri, kufanya malipo ya miamala mbalimbali sasa inaweza kufanyika kwa kutumia simu ya mkononi kupitia huduma za kifedha zinazotolewa na kampuni za simu na taasisi za kifedha.

John Manase ambaye ni muhitimu wa shahada ya manunuzi na usambazaji anasema hofu ya ajira kutokana na teknolojia ni kubwa lakini kuna matumaini mapya kwani teknolojia hiyo imefungua fursa nyingine lukuki.

Bodi ya Makandarasi yajipanga kufanya ukaguzi miradi ya ujenzi

$
0
0
BODI ya Makandarasi nchini(CRB), inatarajia kuanza kufanya ukaguzi katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na kampuni za nje ili kubaini kama kuna ushirishikishwaji wa kampuni za wakandarasi za ndani katika miradi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bodi hiyo kubaini  uwepo wa baadhi ya kampuni zinazotekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mikubwa kutoshirikisha kampuni za ndani kama  sheria na taratibu zinavyotaka na hivyo kuiathiri sekta hiyo hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ziara iliyofanywa na  Bodi hiyo leo Desemba 19, mwaka huu kukagua miradi mbalimbali jijini  Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi Consolata Ngimba, alisema hatua hiyo imelenga kuwalinda na kuziinua kampuni za kizalendo zilizopo nchini.

Alisema ili kuleta tija katika kampuni hizo hususani kushiriki katika miradi mikubwa ya ujenzi inayofanaywa na kampuni za kigeni, CRB itafanya ukaguzi huo nchi nzima ili kubaini kama kampuni hizo zinatekeleza matakwa  ya kisheria ya kuzishirikisha kampuni za wazawa katika miradi hiyo.

“Ukaguzi wetu  umebaini kwa kiasi kikubwa kampuni za kigeni zimekuwa hazishirikishi kampuni za hapa ndani na hivyo kuathiri uwezo wa kampuni hizo, hivyo kwa kufanya hivyo tunaamini kuwa kutazisaidia kushiriki katika miradi hiyo” alisema Consolata.

Pia Mwenyekiti huyo wa Bodi ya CRB alizitaka kampuni hizo za kigeni kuhakikisha inatoa nafasi za ushiriki wa miradi mbalimbali inayoitekeleza ili kuepuka kukiuka taratibu za kisheria ambapo kwa kufanya hivyo kunaweza kuwaingiza matatani ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kufanya kazi katika miradi mingine hapa nchini.

Pia alizitaka kampuni zinazohusika na masuala ya ukandarasi hapa nchini kujenga ushirikiano wa  pamoja ili kuwa na nguvu ambazo licha ya kuzisaidia kupata mitaji mikubwa pia itaziwezesha kufanya kazi kwa kipindi kifupi na ufanisi utakaoleta matokeo chanya katika miradi husika.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi(CRB) Mhandisi Consolata Ngimba akiwa na wajumbe  wengine wa bodi hiyo wakimsikiliza Mhandisi wa Ujenzi kutoka kampuni ya 'China Hobour Engeneering Company' inayotekeleza ujenzi wa Upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Bodi hiyo

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images