Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI

$
0
0
Action Music Tanzania (AMTZ) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza desemba 19 mwaka huu, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge karibu na magorofa ya jeshi ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828 au barua pepe, actionmusictz@yahoo.com, Like Facebook Page au tembelea www.amtz.org
 Mwalimu Abeid Mussa akitoa maelekezo ya wakati wa mazoezi ya kufanya onyesho la muziki
 Mwalimu wa Kinanda Prosper Shirima (katikati) akifundisha
Mwalimu wa Gita, Ashimba (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kupiga chombo hicho

BIFU LA MLELA NA HEMED LIVE!

$
0
0
Hemed (kushoto) akimtishia bastola Mlela
Hemed na Mlela wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya kuumizana huku mama yao akiwaangalia kwa huzuni
Kasha la filamu mpya ya bifu la kina Mlela na PHD inayotarajiwa kuingia mtaani keshokutwa Jumatano.

LILE bifu lililowahi kufukuta kwa kasi mithiri ya moto wa kifuu baina ya ‘tozi’ wawili ndani ya tasnia ya filamu, Hemed Suleiman ‘PhD’ na Yusuf Godfrey Willard Mlela ‘Mlela’ linadaiwa kuibuka upya na kuzidisha uhasama baina ya wasanii hao.


Aidha, alisema bifu hilo lilidhihirika hivi karibuni wakati wawili hao walipokutanishwa kuigiza filamu moja, kwani mara kwa mara walijikuta wakifanya kweli kwenye baadhi ya vipande vya ugomvi na mapigano jambo lililompa wakati mgumu muongozaji wa filamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni kuanzia Desemba 18 mwaka huu iliyopewa jina la I Know You.



“Walikuwa na muda mrefu sana bila kukutana, tukadhani bifu lao halipo tena, lakini hivi karibuni walikutana kwenye filamu iliyoandaliwa na Mtitu Game 1st Quality, wakawa wanafanya kweli kwenye baadhi ya sehemu za majibizano na mapigano huku wakifanyiana fujo mbalimbali huku kupigana vijembe vya wazi,” alisema rafiki huyo.



“Ni kweli tulikuwa na utofauti, ule mvutano wa zamani bado ulikuwepo, kila mmoja hakutaka kuwa dhaifu kwa mwenzake, utaona baadhi ya vipande tulivyofanya kweli,” alisema Mlela ambapo simu ya Hemed iliita bila kupokelewa licha ya mwandishi wetu kuipiga mara kwa mara.



Naye Meneja matayarishi wa Kampuni ya Game st Quality Ltd, Noel Amani ‘Futo’ alisema filamu ya I know You iliwapa wakati mgumu sana kutokana na bifu la wasanii hao kuonekana waziwazi.
“Walitumbua sana, kuna wakati walifokeana kweli, kukunjiana ngumi hata hivyo kuna baadhi ya vipande walivyofanya kweli tumelazimika kuviacha ili kuleta uhalisia zaidi. Kila mmoja anaamini yuko juu ya mwenzake,” alisema Futo.

TASWIRA ZA KIJIJI CHA QUNU ALIKOZIKWA MZEE NELSO MANDELA JUMAPILI DESEMBA 15, 201

$
0
0
Mandhari ya Qunu
Mandhari ya Qunu
Ni kijiji chenye mandhari nzuri. Wakati wa majira ya baridi barafu huanguka hapa
Qunu

Qunu ni kijiji kidogo katika jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini, kilomita 32 Kusini-Magharibi ya mji wa Mthatha, katika barabara ya Butterworth na Mthata. 

Kijiji cha Mvezo, pembezoni mwa mto Mbashe, ni jirani ya mahali ambapo Mzee Nelson Mandela alizaliwa. Hapo Qunu ndipo alipokulia na aliweka nadhiri ya kurejea. 

Kijiji cha Qunu ndipo baba yake Mandela alipohamia baada ya kuvuliwa Uchifu wa Mvezo. Katika kitabu chake cha ‘Long Walk to Freedom’ Mzee Mandela amekitaja kijiji hicho kuwa ndipo alipoishi maisha ya furaha wakati wa utotoni. 

Jumapili ya Desemba 15, 2013 Mzee Mandela alizikwa kijijini Qunu katika mazishi ya Kitaifa yaliyoshuhudiwa dunia nzima. Alizikwa kwa heshima zote za kiongozi wa Taifa katika sehemu aliyochagua mwenyewe kuwa nyumba yake ya milele.


 Daraja la waendao kwa miguu likipita juu ya barabara mpya ya lami inayojengwa kuelekea kijijini Qunu.
Siku ya mazishi barabara ya kuelekea Qunu ilifungwa na ni magari yaliyokuwa na kibali tu ndiyo yaliyoruhusiwa kupita
Ulinzi ulikuwa mkali kila sehemu kijijini Qunu
Wageni wakiwa katika geti kuu la nyumba ya Mzee Mandela hapo Qunu
Nyumba ya Mzee Mandela
Nyumbani kwa Madiba kijijini Qunu
Hema maalumu zilikofanyika shuguli zote za mazishi. Kaburi lake liko nje ya hema upande wa kushoto
Hali ilivyokuwa saa kumi na moja alfajiri siku ya Jumapili
Nyumbani kwa Madiba kumejaa magari hata kabla ya jua kupanda angani
Sehemu ya kijiji cha Qunu. Mahema mbele ya nyumba ni ya wanahabari wa kimataifa waliopiga kambi hapo
Kila engo Qunu inapendeza
Kijiji cha Qunu
Bango linalotangaza kijiji cha Qunu kuwa cha urithi
Ulinzi ulikuwa si wa kawaida siku ya mazishi
Foleni ilikuwa ya kufa mtu
Wana Afrika Kusini toka kila kona walitembea umbali mrefu kwa miguu kuhudhuria mazishi
Nyimbo na ngoma vilitawala
Mdau aklipoza koo baada ya kutembea kwa muda mrefu
Sehemu ya mji wa Mthatha, kilomita kama 32 kutoka Qunu
Magari yalizuiwa kwa muda wakati mwili wa Mzee Madiba uliopowasili uwanja wa Mthatha na kupelekwa Qunu
Sehemu ya foleni ya magari ikikaribia mji wa Mthatha na hapa wakisubiri msafara wa mwili wa Mzee Mandela upite

Rais Kikwete afungua mkutano wa TNBC jijini Dar es Salaam leo

$
0
0
 Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Dr.Reginald Mengi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa TNBC uliofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Chini akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya Tanzania National Business Council muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa TNBC uliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo

WAZAZI KINONDONI WAENDA MOROGORO KUJINOA

$
0
0
 Baadhi ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi Kata za wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, wakiwa kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Kinondoni wakati wakisubiri kuanza safari ya kwenda Morogoro leo kwa ajili ya semina yao ya mafunzo itakayoanza kesho
 Wakisubiru usafiri ofisi ya CCM wilaya ya Kinondoni
 Wawakilishi kutoka Kata ya Kawe wakiwa ofisi ya CCM Kinondoni kabla ya safari
 Baadhi ya viongozi wa Jumuia hiyo wakiwa Oofisi ya CCM Kinondoni
 Baadhi wakitaniana kabla ya safari
 Mwenyekiti wa Jumuia aya Wazazi Kata ya Tandale, Yahya Akilimali aka Mzee wa Yanga, akifurahia jambo na Katibu wa Jumuia hiyo Kata ya Goba, Rehema Ngulume, kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Kinondoni kabla ya safari hiyo
 Wakiondoka kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Kinondoni kwenda kupanda basi lililowafuata kwenye ofisi hiyo
 Wakipanda basi
Wakiwa katika basi wakati safari ikiendelea kwenda Moro

MATUKIO YA MICHEZO YA BANDARI ‘INTER-PORTS’

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Dowuta Taifa, Bw. Jonathan Msoma akizungumza na Wanamichezo wa Bandari, katika siku ya kufunga michezo iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Sigara Chang’ombe. Kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadhi Massawe na Mganga Mkuu wa Mamlaka, Dkt. Mkunde Mlay.
Katibu Mkuu wa Dowuta Taifa, Bw. Jonathan Msoma akisaini mprira kama kumbukumbu ya kufunga michezo ya Bandari iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Sigara Chang’ombe. Kushoto ni mwamuzi wa Kimataifa, Othaman Kazi na katikati ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadhi Massawe.
 Timu ya mpira wa soka ya Makao Makuu ikiwa katika picha ya pamoja.
Mganga Mkuu wa Mamlaka, Dkt. Mkunde Mlay akisalimiana na wachezaji kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu.
 Mashabiki wa timu ya Bandari ya Dar es Salaam wakishangilia.
Mstahiki Meya wa wilaya ya Temeke, Maabad Hoja akisoma hotuba yake wakati wa kufungua michezo ya Bandari iliyofanyika katika viwanja vya Sigara hivi karibuni.
Mashabiki wa timu ya Makao Makuu wakishangilia.
Shabiki wa timu ya Makao Makuu, Saidi Janguo.

KUMEKUCHA USIKU WA WAKONGWE WA MUZIKI WA DANSI IJUMAA HII NDANI YA MZALENDO KIJITONYAMA

SEMINA YA WAZAZI MORO

$
0
0
  Katibu wa Itikadi na Uenezi mkoa wa Morogoro, Dorothy Mwamsiku, akifungua semina ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Kinondoni, leo Des 17, 2013, katika hoteli ya Road View, nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro. Wengine ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Salum Madenge na Mwenyekiti wa Wazazi Kinondoni, Charles Mgonja.(Picha na Latifa Ganzel)
Baadhi ya Wajumbe wakiwa ukumbini kwenyesemina ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Kinondoni, leo Des 17, 2013, katika hoteli ya Road View, nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro

MKUTANO MAALUM WA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA WAFANYIKA

$
0
0
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (kati kati) akifuatilia mada katika Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma, kulia kwake ni Katibu wa baraza Bw. Mathias Kabunduguru na kushoto ni Msaidizi wa Katibu Bi.M. Koka. Bw. Yambesi pia ni mwenyekiti wa baraza hilo.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi  (Kati kati) akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma 
 Kaimu Katibu wa Chama cha Walimu Bw.Ezekiel Oluoch akitoa mchango wake mkutano huoKatibu wa TUGHE Bw. Ally Kiwenge akitoa maoni yake katika mkutano .

 
 Katibu wa Sekretariati ya Ajira bw. Xavier Daudi akitoa mchango wake katika mkutano
 Katibu wa Bodi ya Mishahara Bi. Tamika Mwakahesya akitoa mchango wake katika mkutano
 Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome akijitambulisha kwa wajumbe wa mkutano ika mkutano
9272 Moja kati ya mada zilizowasilishwa katika mkutano kuhusu muundo wa utumishi wa walimu unaotumika hivi sasa

MKUTANO MAALUM WA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA  WAFANYIKA

 

Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma imeitisha Mkutano maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma ili kupata mrejesho kuhusu masuala yanayowagusa watumishi.



Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi akifungua mkutano huo mjini Dodoma amesema mkutano huo maalum unafuatia maagizo yaliyotolewa katika mkutano uliopita.



“Kati ya yale yaliyosisitizwa na kukubalika ni kuitisha Mkutano Maalum wa Baraza kwa ajili ya kujadili Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa Walimu na masuala mengine muhimu yanayohitaji ushauri wa Baraza” Bw. Yambesi alisema.



Bw. Yambesi, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo alisema baraza limeundwa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha sheria ya Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa Umma, Na. 19 ya mwaka 2003, ambapo jukumu lake kubwa ni kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wa watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na utumishi wao. Utumishi wa Umma unasimamiwa na sheria, Kanuni na Taratibu mbalimbali. Hivyo, Baraza linao wajibu wa kushauri kuhusu miongozo mbalimbali inayosimamia Utumishi wa Umma.



Katibu Mkuu Bw. Yambesi alisema serikali inapenda kupata maoni ya wajumbe wa baraza kuhusu Tathmini ya utekelezaji wa Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 1 wa mwaka 2000 unaohusu watumishi wa umma kujiunga na Siasa.



Alifafanua kuwa kwa sababu tunatarajia kuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na huenda baadhi ya watumishi wa Umma wakapenda kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa ambapo utaratibu uliopo sasa uliandaliwa miaka kumi na tatu (13) iliyopita, hivyo kuwepo umuhimu wa kupima kama bado unakidhi matarajio.



Pamoja na wajumbe wa baraza, katika mkutano huo maalum ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Taasisi mbalimbali ndani ya Utumishi wa Umma.



USAID YAAHIDI KUENDELEA KUISAIDIA TFDA KATIKA UDHIBITI WA USALAMA NA UBORA WA BIDHAA ZA CHAKULA, DAWA, VIPODOZI NA VIFAA TIBA TANZANIA.

$
0
0
Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Sharon L. Cromer ameahidi kuendelea kushirikiana na TFDA katika kuhakikisha afya ya wananchi inalindwa kwa kuisaidia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika kuijengea uwezo kwenye masuala ya udhibiti wa usalama na ubora wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini. 

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17/12/2013 katika ziara ya ujumbe wa USAID iliyofanyika Makao Makuu ya TFDA kwa lengo la kujionea ufanisi wa utendaji wa Mamlaka kufuatia misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na Shirika hilo la kimaendeleo kwa TFDA kuanzia mwaka 2011 hadi sasa.

USAID imekuwa ikiisaidia TFDA katika kuwajengea uwezo watumishi wake hususan udhamini wa mafunzo kwa wakaguzi wa dawa, mafunzo kwa watumishi kuhusu mifumo bora ya utendaji kazi na utoaji huduma pamoja na manunuzi ya vifaa vya maabara ya Mikrobiolojia kwa lengo la kuendelea kukidhi vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo, alikabidhi tuzo maalum kwa shirika la USAID ikiwa ni alama ya kutambua mchango wa USAID katika mafanikio yaliyofikiwa na Mamlaka kwa kipindi cha miaka 10 (2003-2013). 


Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo akikabidhi tozo maalum kwa Mkurugenzi wa USAID Bi. Sharon L. Cromer katika hafla iliyofanyika TFDA makao Makuu.
Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya TFDA na ujumbe wa USAID wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara hiyo.
 
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo akiuonesha ujumbe wa USAID moja ya vitabu rejea vya viwango vinavyotumika katika maabara ya TFDA.

MKAZI WA MOSHI AKABIDHIWA JENERETA YAKE YA WEKA UPEWE YA NBC

$
0
0
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Moshi, Ally Janja (wa tatu kushoto) akikabidhi funguo ya jenereta la umeme kwa mshindi wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Michael Charles Kipingu katika hafla iliyofanyika katika tawi hilo mjini Moshi hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Shedafa Omari Shedafa mmoja wa mashuhuda katika tukio hilo, Mhasibu wa Tawi, Rose Ntwale, Lazaro Mollel, teller na Digna Sawalla Meneja Huduma kwa Wateja na Mauzo katika tawi hilo.
Mshindi wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Michael Charles Kipingu (kushoto) akijaribu kuwasha jenereta yake mara baada ya kukabidhiwa na Meneja wa NBC Tawi la Moshi, Ally Janja (mwenye suti). Hafla hiyo ilifanyika mjini Moshi.
Mshindi wa promosheni ya Weka Upewe ya NBC, Michael Charles Kipingu (aliyechuchumaa karibu ya jenereta) akipiga picha ya kumbukumbu pamoja na wafanyakazi wa Benki ya NBC Tawi la Moshi katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi huyo iliyofanyika katika tawi hilo hivi karibuni.

WAZIRI WA ARDHI, MAKAZI NA NISHATI MHE. RAMADHAN SHAABAN AFUNGUA JENGO LA OFISI YA KITENGO SHIRIKISHI CHA AFYA YA MAMA NA WATOTO ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Mhe. Ramadhan Shaaban akikata utepe wakati akifungu Jengo la Ofisi ya Kitengo Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto kiliopo Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Mdhamini wa kitengo Shirikishi Afya ya Mzazi na Mtoto Dkt. Ali Omar Ali akimfahamisha kitu Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Mhe. Ramadhan Shaaban alipokua akikagua jengo hilo mara baada ya kulifungua huko Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Baadhi ya wageni walikwa waliohururia katika ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Kitengo Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto huko Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Waziri wa Afya Juma Duni Haji akimkaribisha mgeni rasmin Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Mhe. Ramadhan Shaaban azungumze na wageni waalikwa katika sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Kitengo Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto huko Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Mhe. Ramadhan Shaaban akiwahutubia wageni walikwa katika ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Kitengo Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto liliopo Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

Air Tanzania yarudisha safari za ndege za kwenda Burundi

$
0
0
 Meneja Rasilimali watu kutoka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Eliezer Mwasele, akishuka kutoka ndani ya ndege mara baada ya ndege ya Air Tanzania kutua wakati wa uzinduzi wa safari za kwenda Bujumbura- Burundi. Nyuma yake ni aliekuwa Balozi wa Tanzania Burundi, Francis Mndolwa.
 Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi (kushoto) akiwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa (wa pili kushoto) mara baada ya kupokea ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, Air Tanzania, iliyoanza sarai za kwenda Bujumbura mwishoni mwa wiki. Wengine mbele ni baadhi ya mawaziri wa serikali ya Burundi.

 Baadhi ya abiria wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania –Air Tanzania- kabla ya kuanza safari ya kuelekea Bujumbura –Burundi, wakati wa uzinduzi wa safari hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya viongozi wakisindikiza abiria walioshuka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania –Air Tanzania- mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bujumbura- Burundi kama ishara ya uzinduzi rasmi wa safari hizo. Kutoka kushoto ni Waziri wa Burundi wa Afrika Mashariki, Bi Nziyemana Leontine akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa
 ========   ========   ==========
Air Tanzania yarudisha safari za ndege za kwenda Burundi
·       Waanza safari za kwenda Mbeya
·       Warejesha safari za Mwanza

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) limezindua rasmi huduma za usafiri wa anga kutoka Dar es Salaam kuelekea Bujumbura, Burundi kwa kupitia mkoani Kigoma, safari hizo zitafanyika mara tatu kwa wiki yaani Jumatano, Ijumaa na Jumapili.

Hatua hiyo imekuja baada ya hali ya amani kutengamaa katika nchi hiyo ya Burundi ambayo ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuilazimu Tanzania kusitisha huduma hizo kwa muda wa miaka 20.

Wakati huo huo, ATCL pia imeanza safari za Dar es Salaam kwenda Mbeya, safari hizo zitafanyika mara nne kwa wiki yaani Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili. imerejesha safari za Dar es Salaam – Mwanza kila siku, safari  zilizoanza rasmi Jumapili iliyopita. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Bujumbura Burundi katika uzinduzi wa huduma hizo juzi, Meneja Rasilimali watu wa Shirika hilo la ndege, Ndugu Eliezer Mwasele, alisema uzinduzi wa safari hizo utakuwa ni njia mojawapo ya kuchochea maendeleo ya uchumi kwa nchi zote mbili.

Alisema kutokana na hali hiyo Watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika nchi hiyo ya Burundi, kwani asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa nchi za Kongo na Burundi wanatarajiwa kuanza kutumia usafiri huo kwa wingi.

Akizungumzia hatua hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi, alisema kuanza kwa safari hizo ilikuwa ni ndoto ya siku nyingi ambayo aliipigania na kutamani kuona wananchi wa pande zote mbili wananufaika kwa pamoja.

“Tumefurahi sana kwa kutimiza ndoto hii leo (juzi), kwa sababu sasa uhusiano kati ya nchi hizi mbili unazidi kuimarika hasa ukizingatia tunategemena kibiashara kulingana na fursa zilizopo.

Kwa upande wake, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa, alisema kwa kuwa ATCL imefunga mkanda na kuanzisha tena safari hizo, ni vyema ikazingatia muda na kuhakikisha huduma stahiki zinatolewa ili kukuza shirika hilo.

Naye Waziri wa Burundi katika Bunge la Afrika Mashariki, Nziyemana Leontine alisema, “kuanzishwa kwa Air Tanzania kuja Burundi, kutasaidia wananchi wa Burundi, hususani wafanyabiashara kwani walikuwa wanaunganisha ndege kupitia nchi nyingine, lakini sasa hivi wananchi watakuja moja kwa moja. Tunashukuru sana,” alisema.

Naye mmoja wa abiria kutoka Burundi waliopanda ndege hiyo, Dk. Owera Kodime, alisema, kuanzishwa kwa safari hizo kutawapunguzia sana gharama za usafiri wananchi wa Burundi, kwa sababu Tanzania imepunguza gharama kuliko mashirika mengine.

“Tulikuwa tukitumia muda mrefu sana kuzunguka lakini sasa tutaweza kuja moja kwa moja Dar es Salaam, ni hatua nzuri ambayo imetuletea faraja sana Warundi,” alisema.

Kwa upande wa abiria kutoka Tanzania, Joseph Kisaro, alisema, “ Muda mrefu sana kulikuwa hakuna huduma, tangu mwaka 1993 huduma zilikatatika, lakini uongozi wa Tanzania umefanya juhudi baada ya mapigano kuisha. “Tunashukuru ubalozi ulioteuliwa mwaka 2003 kwani ulianza harakati haraka za kurudisha huduma hizi ambazo sasa tumefanikiwa.

“Tunaomba uongozi wa ATCL uangalie pia kuwa na safari za kuelekea Kongo mashariki kwa sababu kuna abiria wengi sana ambao ni wafanyabiashara wanaokuja Tanzania,” alisema

Jokate azindua Kidoti Club

$
0
0

 Pichani kulia ni aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006,Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali mapema leo Mikocheni jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa klabu yake iliyojulikana kwa jina la KIDOTI CLUB,Shoto ni mmoja waratibu,Mtangazaji wa East Africa Radio aitwaye Bhoke.
 Mmoja wa Mashuhuda akitoa ushuhuda wake mara baada ya kujiunga kwenye klabu ya KIDOTI CLUB,kwa njia ya simu kwa kutuma neno KIDOTI  kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.
 Baadhi ya wanahabari waliofika kwenye uzinduzi huo uliofanyika Mikocheni,jijini Dar.

=========  ========  ========

Baada ya kutamba na mitindo ya nywele na nguo aina ya Kidoti brand, msichana mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la Kidoti Club.

Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo  jana, Jokate alisema kuwa Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine kwani katika ujio wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali katika jamii hususani masuala ya urembo na mitindo. Jokate pia alizindua aina mpya ya nywele zake za kisasa katika mtindo wa kidoti Brand.

Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbali mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti. Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na anaamini watu wengi watajiunga naye.

Kwa mujibu wa Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa kutuma neno  kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.

 “Huu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii,Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake, mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbali mbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi. Alisema kuwa pia ataendesha mashindano mbali mbali kwa wanachama wake na kutoa zawadi kwa washindi.

 “Kama unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji chake kwa watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu name kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu yoyote, natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na masuala mbali mbali ya maisha,” alisema.

WATU MILIONI 2 HUFARIKI DUNIA KWA POMBE

$
0
0
 Mwakilishi kutoks IOGT-NTO, Gunnar Lundstom akiwasilisha mada katika kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini Iringa.
 Mganga wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Iringa na Mratibu wa madhara ya pombe afya mkoa,Dk. Ally Ngala akizungumza katika kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini Iringa.
  Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini Iringa.
 
========  ======  ======== 

WATU MILIONI 2 HUFARIKI DUNIA KWA POMBE

Na Denis Mlowe na Pauline Kuye, Iringa

UTAFITI uliofanywa na serikali kupitia Wizara ya Afya imebainika kuwa watu milioni mbili hufariki kila mwaka duniani kutokana na matumizi ya pombe.

Hayo yameelezwa na Mganga wa Hospitali ya Rufaa ya 
Mkoa wa Iringa Dk. Ally Ngala wakati akizungumza  katika kongamano juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe kwa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth Disabled and Childen Care (IDYDC) na kufanyika katika ukumbi wa Valentine mjini hapa.

Dk.Ngala alisema asilimia 4 ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa husababishwa na matumizi mabaya ya pombe kupita kiasi na kusababisha madhara mengi zaidi kwa watumiaji wa pombe ikiwemo mama wajawazito kuzaa mtoto kabla ya miezi tisa (njiti).

Alisema utafiti huo ulifanywa Februari na Octoba 2012 ulibainisha asilimia 26.8 mpaka 31.9 sawa na watu milioni 15 nchini Tanzania wanatumia pombe, na kati ya hao asilimia 27.4 ya wanaume wanywaji wa pombe ni  walevi kupindukia na  huku  wanawake ikiwa ni asilimia 13.4.

Aidha Ngala alisema  hunywaji wa pombe una hasara nyingi na  kubwa sana kuliko faida zake na alibainisha kuwa hasara mbaya za pombe kwa mtumiaji  ni upande wa kiafya.

“Pombe ina hasara kubwa sana kwa binadamu kiuchumi kwa kusababisha umaskini kifamilia lakini kwa upande wa afya ndio zaidi hii inatokana na kuwa na mchango mkubwa katika kuleta magonjwa, ingawa sio kila ugonjwa husababishwa na pombe pekee” alisema Dk. Ngala

Ngala alisema madhara mengine ya unywaji wa pombe kupita kiasi ni kusababisha  ugonjwa wa Ini kwa  kufa kwa seli za ini hivyo baadaye ini linapoteza uwezo kabisa kwa kushindwa kufanya kazi hivyo kusababisha vifo vingi kwa ugonjwa huo.

Alibainisha pombe husababisha kansa za tumbo na kansa ya kongosho na mtumiaji wa pombe kwa kiasi kikubwa watoto huzaliwa katika hali ya utegemezi wa pombe(Fotal alcoholic syndrome) ambayo huweza kumpotezea maisha mtoto ndani ya mwezi wa kwanza au utaahira wa kudumu(matatizo ya akili).

Alisema  pombe huathiri kiasi kikubwa watumiaji  mfumo mzima wa uzazi na hata kupelekea mtumiaji kupoteza uwezo wa kuzaa kabisa, na huanzia  kupoteza siku za hedhi kwa mwanamke.

Aliongeza madhara mengine ya unywaji wa pombe kupita kiasi ni chanzo kikubwa cha ajali za barabarani na kusababisha hasara kubwa kwa taifa kwa ujumla.

Airtel yatoa somo kwa wanafunzi kutumia vyema maendeleo ya Teknolojia

$
0
0
Wanafunzi wa shule za sekondari kote nchini wameaswa kutumia vizuri maendeleo ya teknolojia yanayotokea kwa sasa ili kuongeza kiwango cha ufaulu nchini.

Madai hayo yalitolewa na Meneja Biashara wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya ziwa Raphael Daudi wakati akikabidhi kompyuta kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kalangalala iliyopo mkoani Geita.

Meneja huyo alisema kumekuwa na wimbi la wanafunzi ambao hutumia kompyuta kwa matumizi ambayo ni kinyume na maadili na kusababisha jamii kuelekea kwenye mkondo tofauti na uliokusudiwa.

“Baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakibatilisha matumizi ya kompyuta kwa kujifunza mambo yasiyofaa badala ya kuitumia kupanua uelewa wao wa masomo. Wanasahau kuwa kufanya hivyo maadili humomonyoka kwa kiasi kikubwa katika jamii yetu,” alisema Daudi.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Kalangala, Deusdedith Omchamba alisema mpango wa kuleta mapinduzi katika sekta ya elimu kwa kusababisha matokeo makubwa kwa wanafunzi unaofahamika kama “Big results now” utafanikiwa katika shule hiyo kwa kutumia teknolojia ya kompyuta kujifunzia.

“Teknolojia ya kompyuta ni muhimu sana kwa maendeleo ya wanafunzi kwa sasa kwani wanafunzi wanaweza kutumia kompyuta kusomea na hata kutafuta habari mbalimbali zinazoshabihiana na masomo yao,” alisisitiza Mwalimu Omchamba.

Aliongeza kwa kusema kuwa ni jukumu la wanafunzi kutambua umuhimu wa teknolojia hiyo na kuitumia vyema kwa kujiendeleza katika suala la elimu zaidi kuliko mambo mengine ambayo hayana kipaumbele kwa jamii yetu ya Tanzania.

Baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo walielezea  hisia zao na kusema kuwa wanafurahia sana kuwa na somo la kompyuta shuleni hapo na pia watajitahidi kutilia maanani ushauri uliotolewa na Meneja biashara wa Airtel kuhusu matumizi yanayofaa.

Pamoja na kutoa vitabu kwa shule za sekondari nchini Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imekuwa ikisaidiana na serikali kuhakikisha kiwango cha elimu kinaimarika na kuleta mapinduzi katikla sekta hiyo kwani elimu ndio ufunguo wa maisha.

Muumin Mwinjuma ndani ya mkasi

POSHO KWA WAWAKILISHI WA WANANCHI NI KIKWAZO CHA MAENDELEO YA TAIFA

$
0
0
Picha_no_2
Na.Mhariri wa MOblog
Ingawaje Tanzania inaitwa nchi masikini pamoja na kwamba wahisani na wadau wa maendeleo wanasema ni nchi inayoendelea lakini kwa ujumla na kwa yeyote anayeijua nchi yetu kwa maana ya hali ya maisha ya wananchi wake, ni jambo la hatari kwa kikundi kidogo cha watu waliokalia ofisi za umma na kujipangia utaratibu fulani wa kujinufaisha.

Kikundi hiki kidogo tena kilichochaguliwa na wananchi kama wawakilishi wao (wabunge) na ndio watunga sheria kujinufaisha kwa jasho la walipa kodi kwa kisingizio cha sheria ambazo wametunga wao wenyewe kwa kujipendelea. Ni aibu zaidi kusikia kwamba wabunge wengi na hata baadhi ya mawaziri kukejeli juhudi binafsi za baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wenye kuogopa kodi za wananchi na kutaka mabilioni hayo kuelekezwa katika miradi ya maendeleo ya wananchi kwa maslahi mapana ya taifa.

Tumeamua kusema hayo bila kuficha kwamba ni muhimu kwa Serikali pamoja na Bunge kufikiri upya mtindo huu wa kifisadi wa kulipana posho ya kukaa (Sitting Allowance) wakati wana mishahara mikubwa kuzidi wafanyakazi wenye kufanya kazi usiku na mchana kama vile madaktari wanaosubiri kulipwa posho ya (overtime) ya shilingi elfu kumi ambayo hukaa hadi miezi mitatu mpaka sita haijalipwa.

Tunasema na kusisitiza kuwa ujira wa vikao ambavyo ni kazi halali za ubunge ni mshahara na si posho! Posho ni wizi wa fedha za umma mchana kweupe kwa sababu kazi ya Mbunge ni uwakilishi na pale anapokaa kwenye vikao vya bunge na kamati mbalimbali anatimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi iweje alipwe Posho?
Mwaka juzi kwenda mwaka jana 2011/2012 Serikali ililiomba Bunge kupitisha sh bilioni 987 kwa ajili ya psoho mbalimbali za watumishi wa Serikali wakiwamo wabunge. Hii ni hatari kwa mustakabali wa taifa changa kama Tanzania.

Huu ni kweli kwamba mabilioni ya shilingi zikiwa ni kodi za wananchi kila mwaka wa fedha yanatengwa kwa ajili ya posho tu, na hata mwaka jana Benki ya Dunia na wahisani wa maendeleo walihoji uwepo wa posho za kukaa kwa watumishi wa serikali na wabunge lakini bado tatizo hili la kuzoea posho linaitafuna nchi yetu bila huruma.

Serikali kupitia wizara ya fedha mwaka 2011/2012 iliahidi kwamba posho ambazo hazina tija zitaondolewa kauli iliyoonekana kama mwanzo wa mageuzi ya kweli, lakini leo asubuhi niliposikia kipindi cha tuongee magazeti juu ya Wabunge kutafuna posho ovyo wote wa chama tawala na upinzani ni ishara kwamba serikali ilitaka kauli ile ieleweke kinyume nyume.

Gazeti la kila wiki la Raia Mwema limeongoza leo na habari za wabunge kutafuna posho hovyo hovyo na Mbunge kijana Joshua Nasari amekiri kwamba alichukua posho ya kwenda safari Malaysia lakini ikatokea dharula ya Harambee jimboni kwake akaona ni busara kujumuika na wananchi wake bravo kwake.

Bila kutafuna maneno Tanzania ni nchi maskini, kwani kipato cha mwaka cha mwananchi wa kawaida ni Sh 770,463 hivi, wastani wa kama Sh 2,140 kwa siku, kwa mantiki hiyo Mtanzania wa kawaida kuishi katika maisha ya leo kwa kipato hiko ni kwa kudra za mwenyezi mungu kama si rushwa dogo dogo zinazomwezesha kumaliza mwaka. 

Lakini wakati wananchi walio wengi wakiishi katika umaskini wa kutupa, wapo watu waliaomua kusaka nafasi za uongozi katika nchi hii si kwa nia ya kusaidiana na wananchi kutokomeza umaskini ulioelemea taifa hili, ila kujitenga nao kwa kutengeneza utaratibu mbaya na kandamizi wa kujilipa mafao manono kama hizi zinazoitwa posho za vikao za wabunge.

Kwa maelezo yoyote yale, posho hizi si halali hasa zinapolipwa na taifa maskini kama Tanzania ambalo haliwezi hata kujitegemea kwa kuwa na bajeti yake walau kwa mwaka mmoja tu bila kutembeza bakuli kwa wafadhili ili kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa mtanzania yeyote makini atakubaliana nasi kwamba walioweka utaratibu huu ama walipotea njia kwa ama walitanguliza mbele maslahi binafsi lakini wananchi wameamka na wanajua kinachoendelea na wanawasubiri 2015 kwenye uchaguzi watawaita wabunge wa posho na vitambi vya posho kama si mchemsho na kiti moto na bia kaeni chonjo uchaguzi unakuja!

Na kuna taarifa za kutisha kwamba siku hizi hata kazi ambazo ni wajibu wa watumishi wa umma kuzifanya watu hawafanyi mpaka kuwepo na posho (Bahasha) yaani ofisa wa serikali kukaa kwenye kikao cha kazi ambayo ni wajibu wake, anadai mshiko tumekwisha!

Kwa utaratibu huu watanzania itatuchukua muda mrefu mpaka kuja kupata maendeleo ya kweli na hakuna jambo lolote linalokwamisha uwezo wa serikali kutimiza wajibu wake zaidi ya maposho yasiyo kuwa na kichwa wala miguu ndugu zangu tukafanye kazi tuliotumwa na wananchi tuache rongo rongo za posho zisizo kuwa na tija kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Mafundi Viyoyozi na Majokofu jijini Mbeya wapigwa msasa

$
0
0
Washiriki wa Warsha ya mafunzo kwa mafundi wa kuhudumia majokofu na viyoyozi kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Bi. Magdalena Mtenga Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Waliokaa - kwanza kushoto). Mafunzo haya yanafanyika katika Hotel ya Mbeya Paradise Inn, Jijini Mbeya. 
Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Japhet Kanizius, Akimkaribisha Mgeni Rasmi Bi. Magdalena Mtenga, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kufungua rasmi warsha ya mafunzo kwa mafundi wa kuhudumia majokofu na viyoyozi kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa. Mafunzo haya yanafanyika katika Hotel ya Mbeya Paradise Inn, Jijini Mbeya.
Sehemu ya washiriki kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mgeni Rasmi, Bi. Magdalena Mtenga, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

Homa ya mpambano wa Msondo, Sikinde yazidi kupanda

$
0
0
Na Badru Kimwaga

HOMA ya pambano la watani wa jadi katika muziki wa dansi nchini kati ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' na Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' litakalofanyika siku ya Krismasi imeanza kupanda kwa bendi hizo kujificha kambini na huku wakipigana vijembe.


Bendi hizo kongwe nchini zinatarajiwa kuonyeshana kazi katika onyesho litakalofanyika kwenye viwanja wa TCC Club Chang'ombe, Temeke Dar es Salaam katika kunogesha sikukuu hiyo ya Krismasi.


Katika kuonyesha wamelipania pambano hilo bendi ya Sikinde tayari imeiendea Msondo wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuweka kambi yao na wamewatahadharisha 'mahasimu' wao hao wasije wakatoa visingizio baada ya kugaragazwa kwenye onyesho hilo.

"Sisi tumeamua kuweka kambi yetu mjini Bagamoyo ambako tutatua viwanja vya TCC kutokea huko ili kuisambaratisha Msondo, na tunataka wajipange sawasawa ili wasije wakatoa visingizio tena kwa maana kama vyombo vipya bendi zote imepewa na Konyagi," Katibu wa Sikinde, Hamis Milambo alisema.

Milambo alisema mashabiki wa dansi wajitokeze kwa wingi kushuhudia namna gani wanavyowachachafya wapinzani wao hao, ikizingatiwa hawajakutana kwa muda tangu mwaka jana.

Upande wa Msondo kupitia Meneja wao, Said Kibiriti, alisema hawana haja ya kutaja mahali kambi yao ilipo isipokuwa wamejiandaa kuwatoa nishai wapinzani wao siku ya onyesho hilo litakaloanza saa nane mchana.


"Sisi hatuna mchecheto wowote na mpambano huo, tunaendelea kujifua kimya kimya mahali ambapo siwezi kupataja kwa sasa," alisema Kibiriti.


Naye muimbaji anayekuja juu wa bendi hiyo ya Msondo alitokea Sikinde, Athuman Kambi, alisema amejipanga kuonyesha umahiri wake katika mpambano huo baada ya kufanya hivyo wakati akiwa Sikinde dhidi ya Msondo kwenye ukumbi wa Diamond na kuwawehusha mashabiki wa muziki wa dansi nchini.

"Najua watu watataka kuona nafanya kitu gani dhidi ya bendi yangu ya zamani iliyonitangaza vyema, wasiwe na hofu waje Desemba 25 waone nini nitakachofanya TCC Club Chang'ombe," alisema Kambi.

Mpambano huo wa Sikinde na Msondo umeandaliwa na kampuni ya Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, gazeti la NIPASHE, Integrated Communications, CXC Africa na Salute5.
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images