Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA NELSON MANDELA, AONGEA KIJIJINI QUNU AFRIKA KUSINI

$
0
0


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Dkt Dlamini Zuma kwa hotuba ya kusisimua aliyoitoa wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda. Rais Kikwete alialikwa kuzungumzia sifa za mapambano ya ukombozi aliyoongoza Mzee Madiba ambapo Tanzania ndiyo ilikuwa ni nchi yake ya kwanza kusaidia mapambano yote ya ukombozi kusini mwa Afrika kwa kuwahifadhi na kuwapa misaada ya hali na mali wapigania ukombozi wake.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wageni wengine akitoka katika hema maalumu lililotumika kwa shughuli za mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Wa tatu kulia ni Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Uingereza Prince Charles. PICHA NA IKULU

DAKIKA 90 ZA DUNIA: Papa Francis atwaa tuzo ya PERSON OF THE YEAR 2013

$
0
0
Jumatano wiki hii, jarida maarufu na kongwe duniani la TIME, lilimtangaza kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, kuwa mtu aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwa mwaka huu wa 2013.
Tuzo hiyo, ijulikanayo kama PERSON OF THE YEAR, hutolewa kwa mtu ambaye ametawala vyombo vya habari kwa mwaka husika, iwe ni kwa mambo mema ama mabaya.

Mwaka jana, Rais Barak Obama alishinda tuzo hiyo kwa kutetea kiti chake cha urais nchini Marekani.
Na katika fainali ya tuzo za mwaka huu, walikuwemo pia Rais wa Syria Bashar al Assad ambaye amekuwa akituhumiwa kutumia gesi ya sumu kuua raia wake, pia mwanasayansi aliyevujisha siri za serikali ya Marekani Edward Snownden, Rais Obama na wengine sita.
Hii ilikuwa ripoti ya Disemba 14, 2013


Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC

Ujangili wapungua hifadhi ya Saadani

$
0
0
Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa Saadani, Ismail Omar, akizungumza na waandishi wa habari wa Chama cha Habari za Sayansi Tanzania (TASJA), wakati walipotembelea hifadhi hiyo, mkoani Pwani, wakiwa katika ziara ya kujifunza kuhusu mazingira na viumbe hai.

Na Mwandishi Wetu, TASJA.

VITENDO vya ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani vimeendelea kupungua siku hadi siku kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wananchi wa kijiji wa Kijiji cha Saadan.

Kauli hiyo imetolewa na Mhifadhi ya hifadhi hiyo idara ya ulinzi Ismail Omary alipokuwa akitoa taarifa kwa wanachama wa Chama cha waandishi wa habari za sayansi(TASJA) waliotembelea hifadhi hiyo kujifunza masuala mbalimbali.

Alisema ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, kwa sasa vitendo vya ujangili hifadhini hapo ikiwemo ya uharibifu wa misitu na uwindaji haramu wa wanyama, vimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na wananchi kutambua umuhimu wa hifadhi hiyo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1100.

Katika ziara hiyo ya mafunzo iliyowezeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO)waandishi hao walijifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na umuhimu wa hifadhi za Taifa, kuzitunza na kuziendeleza.


Kutokana na kufanisha mafunzo hayo Mwenyekiti wa TASJA Greyson Mutembei, aliishukuru UNESCO kwa niaba ya wananchi kwa kuhakikisha wanajenga wigo mpana kwa wanahabari kuhusu taarifa za mazingira hasa za wanyama na vioumbe hai.

WAZIRI MAGHEMBE AKABIDHI VISIMA 20 VILIVYOKARABATIWA NA TBL WILAYANI MISUNGWI

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL) wa mikoa ya Simiyu, Mwanza  na Mara, Josephat Changwe, akimwongoza Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe (kulia) kuzindua moja ya visima 20 vya maji salama ya kunywa vilivyokarabatiwa na kampuni hiyo kwa gharama ya sh.49.5 milioni, wilayani Misungwi,Mwanza juzi.Anayepiga makofi (kushoto) ni Mbunge wa jimbo la Misungwi, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Charles Kitwanga.
 Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe (kulia), Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (wa tatu kulia) na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL) wa mikoa ya Simiyu, Mwanza  na Mara, Josephat Changwe wakisaidia kumtwisha dumu la maji mmoja wa wanawake wa Kijiji cha Mapilinga, Wilaya ya Misungwi, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa moja kati ya visima 20 vilivyokarabatiwa na TBL wilayani humo, kwa sh. mil 49.5.
 Mama akiondoka na maji huku viongozi wakipiga makofi kwa furaha
 Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (kulia), akipampu maji huku Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe (pili kulia),  na Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo wakionja maji wakati wa hafla ya kukabidhi visima vya maji 20 vilivyokarabatiwa na TBL wilayani Misungwi, Mwanza, kwa sh. mil 49.5, juzi.
  Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Bia (TBL),Stephen Kilindo,wa kwanza kulia akitoa taarifa fupi ya ukaratabati wa visima 20 Wilayani Misungwi kwa Waziri wa Maji ,Profesa Jumanne Maghembe wa pili kutoka kushoto.wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mariam Lugaila na wa Kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mapilinga,Benard Busangu juzi
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, akizungumza na mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mapilinga Misungwi,baada ya kuzindua kisima cha maji kati ya visima 20 vilivyoakaratbatiwa na Kampuni ya Bia (TBL) kwa sh.49.5 milioni.wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TBL , Stephen Kilindo na Naibu Waziri Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga.
Charles Kitwanga (kushoto) akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo muhimu. PICHA ZOTE NA MDAU BALTAZAR MASHAKA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

PATA NAKALA YAKO YA DIRA YA MTANZANIA KWA SH 500 TU

TIMU YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAIADHIBU ISTIQAAMA MABAO 2-1 KWAO

$
0
0
 Kikosi timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais
 Kikosi cha timu ya Istiqaama
 Meza kuu ya mgeni rasmi, Balozi msaidizi wa Urusi, Vicent Kalchenko wa tatu (kulia) na baadhi ya viongozi. 
 Katibu wa Timu ya VPO, Neemia Mandia, akisalimiana na mgeni rasmi Balozi msaidizi wa Urusi, Vicent Kalchenko kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
 Mtanange ukiendelea, (kulia) ni Sufiani Mafoto na (kushoto) ni Lucas, wakiwadhibiti wachezaji wa Istiqaama. Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Dar es Salaam Zoo Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar, timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda mabao 2-1, yaliyofungwa na Kifaru katika kipindi cha kwanza.


 Mtanange ukiendelea...
 Nahodha wa Istiqaama, Saleh Omar (katikati) akichuana kuwania mpira na beki wa VPO.
 Nahodha wa Istiqaama, Saleh Omar, akijaribu kumiliki mpira huku akizongwa na beki wa VPO.
 Neemia Mandia, akijaribu kuwatoka mabeki wa Istiqaama.
 Chenga ya mwili....
 Mandia akitimua vumbi na kumuacha beki wa Istiqaama, chini..
 Beki wa Istiqaama Amadi (kushoto) akiondosha mpira mbele ya mshambuliaji wa VPO, Sufiani Mafoto.
 Kiungo wa VPO, Kombo (kulia) akimzungusha beki wa Istiqaama, Amadi.
 Hapa hupiti......
 Wachezaji wakipongezana baada ya mtanange huo
 Chenga ya mwili.....

Kwanini Hotuba Ya JK Kumuaga Mandela Qunu Ilikuwa Bora?

$
0
0

Ndugu zangu, 

NOTHING can come from NOTHING. Wamesema hili Wanafalsafa wa Uyunani ya Kale .

Nimemwona na kumsikiliza Rais wetu Jakaya Kikwete akizungumza kwenye siku muhimu ya kumuaga kwa mara ya mwisho Mzee wetu Nelson Mandela. 

Muda wote wa hotuba yake, JK alibaki kwenye mstari kwa namna ile ile ya kuweka bayana kwa ulimwengu, kuwa ' msione vinaelea'. 

Hakika alichofanya JK jana ndicho haswa alipaswa kukifanya, na amekifanya kwa kutumia weledi wake kwenye diplomasia na kuchanganya uzoefu wake kwenye uongozi wa kisiasa na dola kwa ujumla.

Ni kuitumia fursa ile ambapo macho na masikio ya dunia yalielekezwa Qunu, kwa yeye rais kuiambia dunia, na si kuisubiri CNN au vyombo vya habari vya Kimagharibi kuifanya kazi hiyo, juu ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo mchango wa Tanzania kumfanya Mandela na viongozi wengine wa Kiafrika kuonekana kama walivyoonekana kwenye macho ya dunia. 

Hakika, JK anastahili pongezi kwa kazi njema aliyoifanya leo ya kuiweka tena Tanzania katika ramani ya dunia, si tu kama nchi ile ya mbuga za wanyama na Mlima Kilimanjaro, bali ' Taifa Kubwa' lililochangia kushiriki mikakati ya ukombozi ikiwemo kutoa misaada ya silaha, mafunzo na hata makazi kwa wapigania ukombozi wa Afrika.

JK aliipitia historia ya mchango wa Tanzania ambayo wengi waliokuwa wakimsikiliza, ama waliisahau au hawakuijua kabisa.

Lakini, tujiulize pia kama Watanzania, katika aliyoyasema JK kule Quni, ni Watanzania wangapi wanayajua? Inahusu umuhimu wa kuipitia historia yetu ili, kama Watanzana, tuweze kumiliki ' K3'- Kujitambua, Kujiamini na kuthubutu. Imefika mahali tunaionea aibu hata historia yetu.

Na nyongeza katika yale aliyoyasema JK leo ni kumbukumbu ya kihistoria ambayo haitajwi pia, kuwa Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, ndiye aliyempa hifadhi Tanzania, Rais wa Pili wa Afrika Kusini huru. Ni Thabo Mbeki. Baada ya kutoroka Afrika Kusini. Baadae Thabo Mbeki akaenda kusoma Uingereza.

Jambo hilo linathibitishwa katika kitabu alichoandika msomi mahiri wa Afrika Kusini, William Gumede. Anasema;

" In 1962, Thabo slipped out of the country to which he would not return for twenty -eight years, travelling through Botswana to Rhodesia, where he was arrested and held in a Bulawayo prison for several weeks. The white Rhodesian authorities intended to deport him back to South Africa and waiting for security police, but British Labour MP, Barbara Castle intervened after being lobbied by the ANC, and Mbeki was granted asylum in Tanzania by President Julius Nyerere." ( William Gumede, Thabo Mbeki and The Search For Soul of The ANC, pg 36)

Naam, ni wakati sasa wa viongozi wengine, bila kujali itikadi zao, wanapokuwa kwenye majukwaa ya kimataifa, kuzitafuta fursa za kuonyesha yale ambayo huko nyuma tumekuwa na uwezo nayo, na bado, kama nchi, tunaweza kuaminika katika kutoa mchango wa uzoefu wetu kwenye masuala mbali mbali ya Kimataifa. 

Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...Kwanini wanandoa hutembea nje ya ndoa zao?

$
0
0
  
Karibu katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production. Katika kipindi cha wiki hii, mjadala ulikuwa KWANINI WANANDOA HUTEMBEA NJE YA NDOA?

Mbali na washiriki waliokuwa studio, pia tuliweza kusoma maoni toka kwa wasikilizaji wetu wanaoacha katika kurasa zetu za FACEBOOK
Karibu uungane nasi.


Ukiwa na maoni, maswali ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia jamiiproduction@gmail.com

RAIS KIKWETE ALIPOZUNGUMZA WAKATI WA SAFARI YA MWISHO YA MZEE NELSON MANDELA KIJIJINI KWAO QUNU

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR AFUNGUA CHUO CHA UTALII MARUHUBI ZANZIBAR

$
0
0
 Picha ya pamoja ya Mgeni rasmin Mukamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad Mawaziri mbalimbali na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

 Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar ikiwa pia ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi huko Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad (hayupo pichani) katika sherehe za ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad (hayupo pichani) katika sherehe za ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar liliopo Maruhubi lililofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad leo Dec 15 2013.


==========   ==========   ============
 Na Maryam Fumu  Maelezo Zanzibar 15/12/2013.
Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad  amesema serikali imekuwa na muelekeo mkubwa wa kuimarisha  sekta ya Utalii  na kuleta mafanikio makubwa  yanayoweza kuingiza watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.

Alisema Zanzibar inaimarika mwaka hadi mwaka katika sekta hiyo ambapo hivi sasa imekuwa ikichangia wastani wa asilimia 80 ya fedha za kigeni katika kukuza uchumi wa Zanzibar.

Alieleza hayo katika ufunguzi wa jengo la ofisi, Madarasa na Lebrary ya chuo cha maendeleo ya Utalii Maruhubi ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema  kuwa serikali ina malengo makubwa  ya kuiendeleza sekta hiyo  kwa lengo la kuwanufaisha Wazanzibar na kufikia dhana ya utalii  kwa   wote kupitia katika ngazi zote za wilaya za Unguja na Pemba.

Hata hivyo Maalim Seif amewataka viongozi kufanya juhudi kwa kukiimarisha na kuletea maendeleo Chuo hicho kwa  kuweka msimamizi mzuri wa historia ya  utamaduni, mila na silka za Wazanzibar ili zienendelee kuchafuliwa. 

Pia makamo wa kwanza wa Rais aliahidi kulichukulia hatua barabara liliopo chuoni hapo ili liweze kupatiwa ufumbuzi.
Nae mkurugenzi wa chuo hicho Bi Zuleikha Kombo Khamis amewaomba viongozi kushirikiana na  sekta Utalii katika kukijenga chuo hicho katika sehemu ilioharibika ili iweze kuwa na mazingira mazuri.
   
Aidha Mkurugenzi   huyo alisema kuwa changamoto  zinazokikabili chuo hicho ikiwemo ukosefu wa barabara pamoja na mmongonyoko wa ardhi  sehemu ya nyuma ya chuo hicho linapelekea kuharibu maendeleo ya chuo.
Hata hivyo Bi Zulekha ameshukuru serikali ya awamu ya saba kwa kuwajengea Jengo la Ghorofa mbili  jambo ambalo linawapa faraja katika kuleta maendeleo chuoni hapo.

Dar wahakikishiwa usalama Tamasha la Krisimasi

$
0
0
Na Samia Mussa

IKIWA zimesalia siku 13 kufanyika kwa Tamasha la Kimataifa la Krisimasi, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Temeke limewahakikishia ulinzi wa uhakika Watanzania  wote watakaohudhuria tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 

Kutokana na hali halisi ya kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakijitokeza katika matamasha ya kila mwaka yanayoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions, Dira ya Mtanzania lilitaka kujua kuhusiana na Jeshi la Polisi lilivyojipanga kuimarisha usalama siku ya Krimasi ambako Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo anasema kuwa kawaida Jeshi hilo limekuwa likijipanga vilivyo katika mikusanyiko ya namna hiyo hasa katika matamasha ya muziki wa Injili.

Kiondo anasema kuwa Jeshi la Polisi ni wajibu wake kuhakikisha hali ya usalama inapatikana katika kila mkusanyiko mkubwa wa watu hasa katika matamasha kama itakavyokuwa katika siku ya Krisimasi katika Uwanja wa Taifa. Anasema kuwa kawaida katika matukio makubwa kama Tamasha la Krismasi ambalo litakwenda kukusanya umati wa watanzanzia kwa nia ya kusikiliza neno la Mungu kupitia nyimbo za injili wataweka ulinzi wa hali ya juu kulingana na hali halisi ya kiusalama ilivyo ulimwenguni.

“Ni wajibu wetu kulinda usalama na kwamba tamasha linafanyika katika Uwanja wa Taifa, unawekwa ulinzi wa hali ya juu na wataalam wa mabomu pamoja na Mbwa wanakuwepo pale siku tatu kabla ya tamasha kwa ajili ya kufanya ukaguzi kila mahali eneo la uwanja,’’ anasema Kiondo.

Anasema mbali ya kufanya ukaguzi huo pia kuna  wingi wa maaskari watakao eneo kila upande kwa ajili ya kuimarisha ulinzi baada ya kujiridhisha na hali ya usalama wa kutokuwepo kwa hatari ya mabomu.
Kiondo anaeleza kuwa pamoja na kuwa hali si nzuri ya kiusalama kutokana na matishio ya ugaidi, Jeshi la polisi limejipanga vya kutosha ambapo alisisitiza kuwa wakazi wa Temeke na Watanzania kwa ujumla wasiwe na wasiwasi kwa kuwa hali ya usalama imeimarishwa hasa katika mikusanyiko.

“Katika kipindi cha Krisimasi tunalazimika kufanya kazi ya ziada, kutokana na hali ilivyo hivi sasa, tunapenda kuwahakikishia watanzania kwamba kila atakayekwenda kwenye Tamasha ajihakikishie kwamba yupo salama kabisa,” anasema Kiondo.

Anasema kila kamanda anawajibika katika eneo lake na endapo linatokea tatizo anawajibika moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kuulizwa na rais Jakaya Kikwete kwamba alikuwa wapi wakati tatizo linatokea jambo ambalo Kiondo amesema halitatokea kwake ndio maana amejipanga vilivyo kuhakikisha hakuna hatari yoyote itakayotokea wakati wa Tamasha hilo la kimataifa.

Ni mara ya kwanza kufanyika kwa tamasha la Krismasi ambako kampuni ya Msama imekuwa ikiandaa pia Tamasha la Pasaka ikiwa ni miaka 13 sasa kwa nia ya kusaidia jamii ikiwa pamoja na kusomesha watoto waliopo katika mazingiza magumu katika ngazi ya shule ya msingi, Sekondari na Vyuo, vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wanawake wajane. 

Lengo la Tamasha hilo ni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kutolea misaada (Center)  pamoja na kiwanda cha kisasa cha kuzalishia kazi za wasanii  kwa manufaa ya Taifa na watu wake, kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imesaidia Watanzania wengi wenye ndoto ya kuwa wasanii wakubwa nchini.

Tamasha la Kimataifa la Krismasi linatarajia kuanzia kufanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Desemba 25, Morogoro Desemba 26, ambako pia linatarajia kuwafikia wakazi wa  Tanga Desemba 28, Arusha Desemba 29 na Dodoma  Januari 1 mwaka 2014.

Tamasha la Handeni lafana chini ya udhamini wa NSSF

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akimtunza Mmoja wa
wasanii wa Jeshi la JKT Mgambo, waliokuwa wakitoa burudani katika la
Utamaduni Handeni.picha na mpiga picha wetu.
 Wasanii wa ngoma za asili kutoka JKT Mgambo, wakitumbuiza Mamia ya
Wananchi waliofika katika Tamasha la Utamaduni Handeni, sherehe hizo
zilifanyika Juzi katika Uwaja wa Azimio, wilayani Handeni, Mkoani
Kikundi cha Sarakasi kutoka JKT Mgambo wakionesha uwezo wao katika
Tamasha la Utamaduni Handeni, Tamasha hilo lilifanyika juzi, katika
uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, Mkoani Tanga.
=======  ========  =========
Tamasha la Handeni lafana chini ya udhamini wa NSSF

Na Mwandishi Wetu, Handeni.

MSIMU wa kwanza wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, (Handeni Kwetu 2013), lililokuwa likisubiriwa kwa hamu hatimaye lilifanyika Juzi, wilayani hapa ambapo Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilijitokeza na kudhamini, hivyo kulifanikisha kwa kiasi kikubwa mno.

Shirika hilo, likiwa limejitokeza dakika za mwisho katoa udhamini wake katika tamasha hilo kubwa na la kwanza kuwahi kufanyika katika Ardhi ya wilaya ya Handeni linalojumuisha vijiji zaidi ya kumi, lilichangia fedha taslimu shilingi milioni mbili, fedha ambazo kwa kiasi kikubwa ukiacha mchango wa wahisani wengine zilichangia  kufanikiwa kwa Tamasha hilo.

Akizungumza wakati wa kutambulisha wadhamini na wahisani mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo, mratibu wa Tamasha la utamaduni Handeni 2013, Kambi Mbwana alisema udhamini wa NSSF ulikuwa mkombozi mkubwa kwao.

“Awali ya yote napenda kutanguliza shukrani zangu zote kwa wahisani
wa tamasha hili, hasa ndugu zetu wa NSSF maana hakika wameonyesha moyo wa uungwana katika kuhakikisha kuwa Handeni Kwetu inazaliwa kwa mafanikio, ukizingatia kuwa tamasha hili limekusanya watu wa aina mbalimbali.

Awali akizungumza baada ya kuzindua Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kuwakutanisha watu wa Handeni kusherekea utamaduni wao pamoja na kukumbusha umuhimu wa kujenga Handeni, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kwa kuwa na Matamasha kama hayo jamii inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kupata Maendeleo wanayoyataka.

Muhingo alisema ili mafanikio yapatikane katika kila jambo ni lazima watu wa eneo fulani wawe na utayari wa kukutana na kujadili mambo yao kwa sauti kama waratibu wa tamasha hilo walivyofanya.

“Tunajivunia kuwa na vijana wenye mawazo mapana kama haya, naambiwa tamasha hili ni matokeo ya mawazo ya kimaendeleo ya vijana wetu, hongereni sana,” alisema Rweyemamu.

Kwa upande wake, Meneja wa NSSF, mkoani Tanga, Frank Maduga alisema shirika hilo limedhamiria kuendelea kushirikiana na waaandaaji wa tamasha hilo kwa lengo la kuhakikisha Utamaduni wa Mtanzania unatumika kulitangaza Taifa, pamoja na kutumia fursa hiyo kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa kutoa elimu ya huduma zao wilayani Handeni na Tanzania kwa ujumla.

"NSSF ni shirika la Watanzania na tumedhamiria kuwapatia huduma bora Watanzania wote, hivyo kila mtu ana haki ya kujiunga na mfuko huu kwa ajili ya kujiwekea mazingira mazuri katika wakati wote wa maisha yake," alisema Maduga.


Katika tamasha hilo,kulikuwa na vionjo mbalimbali vya Utamaduni wa Wanahandeni, ikiwa ni Pamoja na Ngoma za asili kutoka katika Vijiji vya wilaya ya Handeni kama vile, Kweingoma, Kwamatukutu, Kwediamba, Kwachaga pamoja na vikundi vingine vya Handeni Mjini.

Burudani kali na ya kuvutia iliyoonesha asili kamili ya Mtanzania ilitoka kwa Kundi la Sanaa la Jeshi la JKT Mgambo, Azimio Jazz band bila kusahau msanii wa kundi la Fataki, Machenja ambaye alipiga onesho la kukata kiu akiwa na wana okalandima.

Tamasha la Utamaduni Handeni ambalo linafanyika kwa mara ya Kwanza lilidhaminiwa na NSSF, Clouds FM, Vodacom, Plan B, gazeti la Mwananchi, Kajunason Blog, Chichi Local Wear, Katomu Solar specialist, Dullah Tiles and Construction, Anesa Company Limited, Country Business
directory, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.

NEWS NOW LATEST KUTOKA IRINGA

$
0
0
 TATIZO SUGU LA MAJI MKOANI IRINGA.

Kutokana na tatizo la maji kukatika mara kwa mara katika baadhi ya maeneo mkoani IRINGA, kaimu msaidizi wa  mamlaka ya maji mkoa wa Iringa (IRUWASA) SHABANI ALLY  amesema  kuwa tatizo hilo linatokana na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara hivyo kupelekea baadhi ya maeneo kukosa maji kwasababu mitambo katika vyanzo vya maji vinategemea  nishati ya umeme ili kuweza kufanya kazi katika kiwango kinacho hitajika
  
Suala lingine amezungumzia kutoka kwa maji machafu ambapo amesema  kuwa sababu  inasababishwa na kupasuka kwa mabomba yanayotumika kusambaza maji kutokana  na  shughuli mbalimbali  za kijamii katika makazi Ikiwemo ujenzi wa barabara na uchimbaji wa visima.
 
Ameongeza kuwa wananchi  wasisite kutoa taarifa endapo matatizo kama hayo yanapojitokezaka kwenye maeneo yao ili waweze kupatiwa huduma  haraka kabla tatizo kuwa kubwa na kuwataka wananchi kuwa makini wanapofanya shughuli za kimaendeleo ili kuzuia usumbufu wa maji kutokea.
  
Aidha  ameongeza kwa kusema kuwa pamoja na IRUWASA kutoa maji safi na salama amewataka wananchi wa manispaa ya Iringa kuchemsha maji kabla ya matumizi ya nyumbani ili kuepukana na magonjwa mbalimbali ikiwemo homa za matumbo.
 
==========  ========  ========

WAZAZI MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUWAENDELEZA WATOTO WAO KITAALUMA.

Wazazi Mkoani Njombe Wametakiwa Kuwaendeleza Watoto Wao Kitaaluma Ikiwa ni Pamoja na Kuwapatia Mafunzo ya Fani  Mbalimbali  Zinazotolewa na Taasisi za vyuo Vilivyopo Mkoani Njombe, Jambo Ambalo litasaidia Kupunguza Tatizo la Ajira Miongoni Mwa Vijana Mkoani Njombe.

Akizungumza Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Benki ya NJOCOBA  Wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Cha Utalii na Uandishi wa Habari Cha  Eckros Njombe,Mwakilishi wa Mkurugenzi Bw Mfikwa Amesema Kuwa Vijana Wanaweza Kuondokana na Tatizo la Ajira Endapo Wataendelezwa Kitaaluma na Hivyo Kuwataka Wazazi Kutokata Tamaa Dhidi ya Vijana Hao.

Amesema Pamoja na Mambo Mengine Uongozi wa Chuo Unatakiwa Kutatua Baadhi ya Changamoto Zinazokikabili Chuo Hicho Ili Kuhakikisha Inaboresha Hali ya Taaluma na Kiwango Cha Elimu Inayotolewa Chuoni Hapo Jambo Litakalosaidia Kuwa na Wahitimu Wenye Uwezo Kitaaluma na Kufanya Kazi Kwa Ubora.

Awali Akisoma Risala Kwa Niaba ya Wahitimu Mmoja wa Wahitimu Katika Fani ya Uandishi wa Habari  Ester Pascal Ameuomba Uongozi wa Chuo Kutatua Baadhi ya Changamoto Zinazokikabili Chuo Hicho Ikiwemo Upungufu wa Vifa Hasa Kwa Fani za Uandishi wa Habari na Ufundi Mitambo.

Katika Mahafali Hayo Jumla ya Wahitimu 72 Wametunukiwa Vyeti Vya Kuhitimu  Fani Mbalimbali Ikiwemo Utalii,Uhudumu wa Hoteli,Katibu Muhtasi,Ufundi Mitambo na Uandishi wa Habari.

=========  ======  ========

 WANANCHI WA IRINGA WASHAURIWA KULIMA MAZAO YANAYOHIMILI UKAME.

Wananchi mkoani Iringa wameshauriwa kulima mazao yanayohimili ukame kutokana na kutokuwepo kwa mvua za kutosha katika baadhi ya maeneo. Hayo yamesemwa na Afisa kilimo mkoa ROSE KASOLE na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kulima mazao kama mtama,viazi vitamu,ulezi na  alizeti.
  
Pia ametoa ushauri kwa wakulima kutumia kilimo cha matuta ili kusaidia udongo usiende na maji kutokana na maji yanayotililika kutoka milimani kwa kuwa ndicho kilimo kinachofaa katika sehemu za miinuko. Katika hatua nyingine KASOLE amesema kuwa mwaka huu wa kilimo wametoa vocha na pembejeo mbalimbali kwa lengo la kuinua kipato cha mazao kwa wakulima na kusisitiza kuwa wakulima wanapaswa kupewa vocha kwa usawa na wasisite kutoa taarifa katika ofisi husika endapo kuna matatizo ya ugawaji wa vocha.
  
ameongeza kuwa mwaka huu wametoa mikopo kwa wakulima kupitia sacos mbalimbali ambazo zimeweza kuwafikia wakulima ili waweze kulima kilimo kilicho bora.

Airtel yapiga tafu timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17

$
0
0
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala jerry Slaa(kushoto) akimuongoza mchezaji wa zamani wa Manchester United Andy Cole kwenda kuwafunda vijana wa  timu ya Taifa chini ya miaka 17. Shughuli hiyo ilifanyika jana Dar es Salaam katika viwanja vya karume mara baada ya mchezaji huyo kuzuru/kutembelea ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania.  

 Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) akiwasalimia vijana chini ya miaka 17 kabla ya kukutana na timu ya vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa. 
 Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) akiwasalimia vijana chini ya miaka 17 kabla ya kukutana na timu ya vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa.  
 Mchezaji wa zamanai wa Manchester United Andy cole(wa pili kulia) akisisitiza jambo kabla ya kujumuika na vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 jana - Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania. 
 Meya wa manispaa ya Ilala(wa pili kushoto) akikabidhi mipira iliyotolewa na Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bwana Jamali Malinzi (kushoto) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni mchezaji wa zamani wa klabu Manchester UnitedAndy Cole na Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Sunil Colaso(kulia). 
 Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester united(Kulia) akionyesha ufundi wa kuchezea mpira mbele ya timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 jana jijini Dar es Salaam. Anayeangalia ni Meya wa Manispaa ya Ilila Jerry Slaa.
Meya wa Manispaa wa Ilala Jerry Slaa akipiga mpira katika hafla iliyoandaliwa na Airtel jana kukabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17. Anayeangalia(kushoto) ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bwana Jamal Malinzi.  


=========  =======  ==========
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza michezo nchini ili kuleta ufanisi katika sekta ya michezo.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso alisema uwekezaji katika michezo ni mhimu hasa katika kipindi hiki amabacho Tanzania inajipanga kushiriki katika mashindano ya kikanda na kimataifa.

 “Airtel Tanzania tunakabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 kama sehemu ya juhudi zetu kusaidia maendeleo ya michezo.
 “Tutaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha nchi inapata mabalozi wa kutuwakilisha vizuri katika mashindano ya kimataifa” alisema.

Colaso alisema mwaka 2011 kampuni yake kwa makusudi ilianzisha Airtel Rising Stars ikiwa ni mpango wa kuvumubua na kuendeleza vipaji kwa vijana wadogo kutoka ngazi ya chini ili kuwapeleka ngazi za kimataifa.

Wakati wa hafla hiyo, mkongwe wa klabu ya Manchester United Andy Cole aliwaasa vijana hao chini ya miaka 17 kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao za kucheza kwenye timu kubwa duniani.

 “Nimeona vipaji vingi Tanzania. Wachezaji wanaweza kabisa kuchezea klabu kubwa kama wataongeza bidii katika mazoezi yao. Naomba nichukue nafasi kuwakumbusha wachezaji chini ya miaka 17 kuwa na nidhamu si ndani tu ya uwanja bali na nje ya uwanja kwani hiyo ndio nguzo ya mafanikio” Alisema.

Nae Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa aliwashukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa juhudi zake endelevu kusaidia michezo na kutoa wito kwa makapuni mengine kuiga mfano wa Airtel katika kusaidia michezo.

 “Tunahitaji nguvu za pamoja kati ya sekta binafsi na umma kama kweli tunataka maendeleo katika michezo. Nawashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika michezo, niwaombe makampuni mengine waige mfano huu katika kusaidia juhudi za Serikali kuendeleza michezo

Rais mstaafu wa zanzibar,Abeid karume asisitiza utengenezaji wa miundo mbinu katika suala zima la kuinua uchumi wa nchi

$
0
0
Na Ali Issa Maelezo -Zanzibar .

Rais mstaafu  wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume amesema utengenezaji wamiundo mbinu ya Barabara ndio njia moja wapo ya kuinua Uchumi wa Nchi na kupelekea wananchi wake kua na kipato kizuri na  kujikwamua na hali ngumu ya kimaisha. 


Hayo ameyasema leo huko  Zanzibar Beach Resort Mzizini Mjini Unguja katika kongamano la sherehe za kutimiza miaka kumi wa mfuko wa barabara, sambamba na  uzinduzi wa kitabu cha mfuko huo hotellini hapo.


Amesema nchi nyingi duniani zimepigahatua kubwa za kimaendeleo na kuinua uchumi wa nchi zao kulitokana na njia  na ujenzi mkubwa wa kujenga Barabara. Amsema halihiyo ni ili zifanya nchi kusonga mbele ,hivyo  mfuko huo nao hakuna budi kulifikia ipasavyo.  Amesema iwapo na Zanzibar itafikia huko uchumi wake utakuwa kwa ubora jambo ambalo lina paswa kuigwa.

Nae katibu mkuu wizara ya fedha Hamis MUssa alisema barabara ni nafasi maalumu ya kuunganisha uchumi kwani wananchi hupata frusa ya kuweza kusafirisha malizao kwa urahisina kuyafikia mahitaji kwa haraka.


Aidha alisema kua mfuko wa barabara uliazishwa kwa malengo malumu ikiwa ni pamoja wa kuangalia ubora wa barabara ,kutafutamapato ya ujenzi wa barabara ,na kuangalia matumizi bora ya matumizi ya fedha zinazo tolewa na wahisani na walipakodi wa nchihii.


Kongamano hilo la siku moja litajadili changamota zinazo ikumba mfuko huo na mafanikio yalio patikana kwamiaka kumi na kutafuta njia za utatuzi wa changamoto unao ikumba mfuko huo.


Kongamano hilo limewasrikisha wajumbembali mbali kutoka Tanzania bara na Zanzibar wakiwemo mawaziri makatibu wakuu na wajumbe wa Baraza la wakilishi.   

KUTOKA KWA WATANI WETU WA JADI:President Jakaya Kikwete’s speech at Mandela Funeral SHAMED Kenyatta Regime

$
0
0
Tanzania’s President Jakaya Mrisho Kikwete was accorded a stunning ovation in his tribute to the late Nelson Mandela.
President Kikwete’s speech made shame of Jomo Kenyatta regime that failed to help ANC set base in Kenya. Kikwete highlighted the support given by Mwalimu Julius Nyerere to the struggle against apartheid in South Africa.
Kikwete named TANU, ANC, ZANU PF, FRELIMO and SWAPO as comrades, KANU was left OUT!
“Tanzania under Julius Nyerere helped Black people struggle for emancipation in SA. Kenya under Jomo Kenyatta helped Boers/Whites to oppress and subjugate Black people in SA. Today, Jakaya Kiwete was global platform to pay tribute to global icon” George Nyongesa posted in his Facebook Page.

AZAM TV YAANZA RASMI KUTOA HUDUMA ZAKE OFISI KUU JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Jengo la Ofisi za huduma kwa wateja za Azam TV, zilizopo kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, Tazara jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa akizungumza na vyombo mbali mbali vya habari vilivyokuwepo kwenye ufunguzi huo wa Jengo la Ofisi za huduma kwa wateja za Azam TV, zilizopo kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, Tazara jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa akizungumza.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington akisisitiza jambo mbele ya waandishu wa habari (hawapo pichani) juu ya huduma mbali mbali wazitoazo kama Azam TV.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa akisalimiana na baadhi ya waigizaji wa Filamu nchini kutoka kundi la (Bongo Movie) waliokuwepo kwenye Ufunguzi huo uliofanyika leo jijini Dar.
Burudani ya ngoma za asili pia zilikuwepo kwenye Uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Yusuf Bakhresa (kushoto) akizungumza jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media wa Kampuni ya Azam Media Ltd,Rhys Torrington mara baada ya Ufunguzi wa Jengo la Ofisi za Azam TV jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja Uzalishaji na Ufundi wa Kampuni hiyo,Mehboob Aladdad.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa kwenye picha ya pamoja.

AzamTV leo imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Huduma za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa Desemba 6, 2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi kuangalia bure hadi hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada ya shilingi 12,500 kwa mwezi.

Kwa kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za Azam ambazo ni:

·         Azam One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo itakuwa kwa lugha ya Kiswahili.

·         Azam Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia

·         SinemaZetu – Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.

Kwa pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya michezo, tamthilia, watoto na maisha.

Ofisi ilifunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd.

“Ofisi hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni kielelezo cha nia thabiti ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika shughuli ya utangazaji hapa Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa familia kwa bei nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika. Hili ni jambo ambalo kila mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema Bakhresa

Rhys Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema: “Naona faraja kubwa kwamba leo hii AzamTV  ipo sokoni kwa ajili ya kila mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote tutaburudusha watu kote nchini. Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – situ katika ofisi hizi lakini pia kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala 50 katika kila mkoa. AzamTV ni ya kudumu”

Azam Media pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia kampuni yake tanzu, Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa vipindi wa hapa Tanzania.

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA SIDO

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone:255-22-2114512, 2116898

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

              P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Eng. Omari Jumanne Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO).


Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Desemba 04, mwaka huu, 2013. Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtafiti Mwandamizi katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam.

Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtanzania mwenye elimu, weledi na uzoefu ambao umemfanya Mheshimiwa Rais aamini kuwa atakapoongoza SIDO, atasaidia kukidhi matarajio ya taifa kwa kueneza ujasiriamali, uwekezaji,uzalishaji na kutoa nafasi za ajira katika ngazi ya viwanda vidogo na vya kati kama msingi imara wa uchumi wa Tanzania, ikiwemo kwa kuingiza sayansi, teknolojia na ubunifu katika viwanda vidogo vidogo.

         “Mwisho”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

DAR ES SALAAM.


16 Desemba, 2013

UNIC YAFANYA MAFUNZO YENYE TIJA YA UJASIRIMALI PEMBA

$
0
0
DSC_0181
Mshehereshaji Bw. Salum Msellem kutoka Istiqama Radio akitambulisha meza kuu kwa washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya siku moja kwa Vijana Visiwani Pemba yaliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Madungu.
DSC_0240
Mratibu wa YUNA kisiwani Pemba, Bw. Mohammed Ali, akisoma taarifa ya maendeleo ya vilabu vya Umoja wa Mataifa visiwani humo na changamoto zinazowakabili kwa walezi wa vilabu hivyo.

.Vijana waaswa kujikita katika ujasirimali ili kuondokana na umaskini

Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), kilifanya mafunzo yenye tija ya ujasirimali kwa vijana katika Mji wa Pemba visiwani, Zanzibar na kupata washiriki wenye kiu ya kutaka kujiajiri na kuondokana na umasikini hapa nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa mafunzo hayo ya siku moja ya ujasirimali kwa vijana hivi karibuni Mjini Pemba, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2000 walizindua malengo ya milenia ili kusaidia nchi zinazoendelea kuondokana na umaskini.

“malengo manane ya milenia ni pamoja na Afya ya Uzazi kwa kinamama, Elimu, kuondoa umaskini na mambo ya mazingira vile vile kusaidia mikakati mbalimbali ya nchi hizo katika utekelezaji wake mpaka kufikia mwaka 2015,” amesema Bi. Ledama.
DSC_0265
Afisa Vijana - Mshauri kutoka WIZARA ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Bi. Stara Salim akizungumzia jitihadi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuwawezesha Vijana kupata mikopo kupitia asasi mbalimbali za fedha ili waweze kujikwamua kimaisha na kuondokana na lindi la umaskini visiwani Pemba.


Amesema kwamba kazi kuu ya Umoja wa Mataifa na taasisi zake ni kusaidia Serikali mbalimbali katika nchi zinazoendelea kufanikisha mikakati na utekelezeji wa malengo ya milenia ikiwemo dhana ya kupunguza umaskini.
Bi.Ledama alilisitiza kwamba katika utekelezaji huo Umoja wa Mataifa inasaidia mikakati hiyo ya kuondoa umaskini kwa kuandaa program mablimbali na kufanya mafunzo ya ujasirimali kwa vijana ili waweze kujiajiri na kuondokana na umasikini.

“Serikali pekee haiwezi kutoa ajira kwa watu wote kwa sababu nafasi ni chache na mahitaji ni makubwa kwa hiyo ndugu zangu kujiajiri na kuajiri wengine katika sekta binafsi kupitia ujasirimali ni nafasi pekee ya kuondokana na umaskini,” aliongeza.

Amesema kwamba asilimia 43 ya wakaazi wa Zanzibar ni vijana kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa kwa Umoja wa Mataifa na sekta binafsi kuhamasisha ujasirimali kama njia pekee ya kujiajiri na kuondokana na umaskini wa kipato na wa jumla.
DSC_0278
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumzia lengo la kuendesha mafunzo ya Ujasiriamali kwa watu walio nje ya shule ikiwa ni moja ya agenda ya kutekeleza malengo ya milenia ya kupunguza umaskini kwa nchi zinazoendelea.

Bi. Ledama amesema sekta binafsi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaweza kupunguza tatizo la ajira kwa kusisitiza ujasirimali zaidi katika maeneo mbalimbali ya Bara na Visiwani.

“Haya ni mafunzo ya pili kufanyika bara na visiwani yenye kutoa mafunzo yenye tija juu ya ujasirimali na faida zake katika kupunguza na kupambana umasikini kwenye nchi zinazoendelea,” aliongeza.

Amesema kwamba Shirika la Kazi Duniani (ILO) wana kitengo maalum cha mambo kujenga uwezo kwa vijana na mafunzo ya ujasirimali yenye lengo la kuondoa umasikini miongoni mwa vijana nchini Tanzania.
DSC_0377
Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali kupitia Program ya kazi Nje nje inayolenga kuelemisha Vijana stadi za Ujasiriamali iliyoasisiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bi. Mwanapili Hamad akitoa mada kuhusu dhana nzima ya uongozi katika biashara (Business Management) kwa wajasiriamali Vijana visiwani Pemba ili waweze kuboresha kipato chao.
DSC_0220
Picha juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya siku moja yaliyoratibiwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
DSC_0354
DSC_0228
DSC_0466
Mjasiriamali mwenye kipaji cha kuchora ramani za majengo, kutengeneza sampuli za nyumba kwa kutumia maboksi Bw.Steven Timothy Mihale kutoka Temeke Youth Development Network (TEYODEN) akionyesha moja ya kazi zake kwa wajasiriamali wenzake ambayo inampatia kipato na kuweza kuendesha maisha yake.
Bw. Steven Mihale aliwapa moyo wajasiriamali wenzake na kuwataka kuwa na uthubutu na kutokata tamaa mapema.
DSC_0486
Vijana wajasiriamali wakiangalia kazi ya Mjasiriali mwenzao.
DSC_0388
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akiuliza swali kwa wakufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali yaliyoratibiwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
DSC_0498
Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali Bi. Mgeni Salum akitoa somo la namna ya kuhifadhi hesabu za mauzo na kujua kama biashara ina faida au hasara sanjari na kupata mikopo kupitia taasisi za kifedha.
DSC_0391
Mratibu wa YUNA kisiwani Pemba, Bw. Mohammed Ali akiteta jambo Mkutubi wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha (katikati) wakati wa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vijana visiwani Pemba yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Madungu.
DSC_0524
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akifunga mafunzo ya siku moja ya wajasiriamali Visiwani Pemba yaliyoratibiwa na kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).

SERIKALI YA TANZANIA NA UJERUMANI ZATITLIANA SAINI MSAADA WA BILIONI 121.89 KUBORESHA UMEME, MAJI NA HIFADHI YA TANAPA

$
0
0

1 (2)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile akibadilishana mikataba ya makubaliano na Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam.
2 (1)Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile akizungumza na waandishi wa habari9hawapo pichani) baada ya kusaini mikataba ya makubaliano na Serikali ya Ujerumani.Katikati ni Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel.
3Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikataba iliyosainiwa kati ya Serikali yake na Serikali ya Tazania. Kushoto ni Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher.
5Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumzia jinsi mikataba hiyo itakavyonufaisha Hifadhi ya Serengeti huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel, wakimsikiliza.
6Picha ya pamoja kutoka kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel, atibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile(mwenye suti ya kaki), Mkuregenzi Mkazi wa KfW Ofisi ya Dar es Salaam Wolfgang Solzbacher (mwenye tai nyekundu), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Modestus Lilungulu na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.


Picha na Hussein Makame, MAELEZO
Hussein Makame, MAELEZO
SERIKALI ya Tanzania na ile ya Shirikisho la Ujerumani zimesaini makubaliano ya msada wa Fedha za Ulaya EURO Milioni 55.5 sawa na Shilingi Bilioni 121.89 za Kitanzania kusaidia sekta ya Maji, Umeme na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Akizungumza baada ya utiaji saini huo uliofanyika Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dk. Servacius Likwelile alisema katika makubalianao ya kwanza Serikali ya Ujerumani itatoa EURO Milioni 20.5 sawa na Shilingi Bilioni 45.059.
Alisema fedha hizo zitatumika kusaidia Kuhifadhi wa Hifadhi ya Serengeti katika Kuendeleza na Kutunza maliasili ya hifadhi hiyo, kuboresha miundombinu ya kijamii na kujenga barabara katika wilaya za Loliondo na Srengeti.
 “Mkataba wa makubaliano wa pili utawezesha Serikali ya Ujerumani kutoa mchango wa EURO Miloni  20 sawa na Shilingi Bilioni 43.96 kusaidia kusambaza umeme Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania “ alisema Dk. Likwelile.
Alisema msaada huo utasaidia kuunganisha wananchi wa vijijini 32,500 katika maeneo hayo kupata umeme na kuunganisha Gridi ya Taifa hadi kwenye Mtambo wa Kuzalisha Umeme wa maji wa Rusumo na kuuza umeme nchini Rwanda na Burundi.
Dk. Likwelile aliongeza kuwa mkataba wa makubaliano wa tatu utaiwezesha Serikali ya Ujerumani kutoa msaada wa EURO Milioni 15 sawa na Shilingi Bilioni 32.97 kusaidia Sekta ya Maji kupitia Programu ya Maendeleo awamu ya pili.
Alifafanua kuwa kupitia programu hiyo msaada huo utafabikisha utekelezaji wa Usimamizi wa Rasilimali ya Maji, Usambazaji wa maji Vijijini na Mijini na Kuimarisha Taasisi na Kujengea Uwezo Sekta ya Maji.
Aliihakikishia Serikali ya Ujerumani kuwa fedha hizo zitatumika vizuri na kuwanufaisha wananchi wa maeneo husika na aliwaomba wanachi husika wathamini msaada huo kwa kutunze miradi ya maendeleo katika maeneo hayo.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Hans Koeppel msaada huo unathibitisha kuwa Serikali yake imedhamiria kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo ili kuchangia kuboresha ustawi na utajiri wa wananchi wa Tanzania.  
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Modestus Lilungulu alisema msaada huo utasaidia kutekeleza Mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa ambao lengo lake ni kufikisha huduma ya maji vijijini kwa asilimia 74 na mijini asilimia 90 ifikapo mwaka 2015.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi alisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muwafaka kutokana na changamoto ya ongezeko la idaidi ya watu lililosababisha kuongezeka kwa huduma kwa binadamu kuongezeka.
Kwa zaidi ya miongo mitano iliyopita Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Ujerumani umefanikisha misaada yenye thamani ya Fedha za Ulaya EURO Bilioni 2.03 huku Serikali ya Ujerumani ikisaidia sekta za Umeme, maji, mazingira na Afya.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images