Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

TAMASHA LA 38 LA SANAA BAGAMOYO,KUANZA KURINDIMA KESHO VIWANJA VYA CHUO

$
0
0
Wasanii zaidi ya 100 kushiriki, wamo Mwana FA, Juma Nature, Dullah Makabila, Gigy Money, Vitalis Maembe,Pia wapo Mashauzi Classic, Malkia Khadija Kopa, Msondo Ngoma, Sisi Tambala, Sinaubi Zawose

TAMASHA la 38 la Sanaa Bagamoyo linaanza rasmi kesho Oktoba 19-26 katika mji wa kihistoria Bagamoyo mkoani Pwani litatemesha mji wa Bagamoyo na mkoa wa Pwani kwa ujumla.

Mwaka huu tamasha hilo litaanza kwa mtindo wa tofauti na ilivyozoeleka, litaanza kwa kuzunguka mitaa mbalimbali ya wilaya hiyo, lengo likiwa ni hamasa kwa tukio hilo muhimu.

Wasanii wa kazi mbalimbali watazunguka mji huo kwa ngoma mbalimbali ili kuwachochea wadau kujitokeza katika ukumbi ulioko chuoni hapo.

Zoezi hilo la kuzunguka maeneo ya Bagamoyo, litaanza asubuhi likishirikisha wadau mbalimbali.

Bagamoyo ni mojawapo ya maeneo yenye urithi na utajiri mkubwa wa kiutamaduni Ulimwenguni, ambako Tamasha hilo la kimataifa, kwa mara nyingine tena litawakutanisha wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ambao wataonesha kazi zao za sanaa na utamaduni.

Dk. Hebert Makoye, ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), ambao ni waandaaji wa tamasha hilo linalozidi kujizolea umaarufu kila mwaka, anasema lengo ni kuendeleza na kudumisha Utamaduni wa Mtanzania, kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa mataifa mengine kupitia warsha, kongamano na maonyesho mbalimbali.

Dk. Makoye, anasema tamasha la 38 linatarajiwa kushirikisha wasanii zaidi ya 100 ya hapa nchini na nje, likiwa na dhamira ya kubadilishana uzoefu katika sanaa, hivyo ni nafasi ya wadau mbalimbali wa sanaa kujitokeza na kushuhudia elimu kutoka kwa wasanii watakaopanda jukwaani.

Anasema, tamasha la mwaka huu litashirikisha vijana wa shule za Msingi na Sekondari kutoka Bagamoyo, Vyuo na Vyuo Vikuu.

“Mwaka huu, tamasha linatarajiwa kuhudhuriwa na jumla ya watazamaji 60,000 kutoka maeneo ya Bagamoyo, Dar es Salaam na sehemu zingine za Tanzania pamoja na nje ya nchi,” anasema Dk. Makoye na kuongeza.

Kusudi la Tamasha hili ni kutoa fursa kwa wasanii wa ndani na nje ya nchi, pamoja na watazamaji kukutana na kuuenzi utajiri wa utamaduni wao unaowatofautisha na mataifa mengine, ambao unaonyesha utofauti wao katika muktadha wa maadili na mshikamano, pamoja na ubunifu.

Malengo maalum ya Tamasha

Dk. Makoye, anasema ni jukwaa kwa wanafunzi wa TaSUBa na wa kutoka taasisi zingine za mafunzo, kuonesha kazi zao na stadi walizopata katika mafunzo yao ya sanaa na utamaduni.

Anasema, pia ni kukuza na kubadilishana tamaduni kati ya wasanii wa ndani na wa kimataifa, ni jukwaa la wasanii wachanga kuonesha vipaji na ustadi wao kwenye sanaa na utamaduni, kuongeza uhamasishaji miongoni mwa vijana na wasanii juu ya masuala yanayohusu sanaa, michezo na utamaduni wa Kitanzania.

Dk. Makoye, anasema Kauli mbiu ya Tamasha la mwaka huu ni ‘Sanaa na Utamaduni Ajira Yangu’.Aidha, anasema katika tamasha la mwaka huu, kutakuwa na maonesho ya bidhaa mbalimbali za sanaa na za kiutamaduni, vyakula mbalimbali kama vile nyama choma, samaki, pamoja na vyakula vya baharini.Pia, anasema wageni watapata fursa ya kutembelea mji wa kihistoria wa Bagamoyo.

TaSUBa, Clouds Plus kuboresha tamasha

Mapema mwaka huu, TaSUBa imeingia makubaliano na Kampuni ya Clouds Plus Production yenye lengo la kushirikiana katika kusaka rasilimali za uendeshaji wa Tamasha hilo la Kimataifa la 38.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano iliyofanyika ukumbi mkubwa wa maonesho wa TaSUBa, Dk. Makoye, anasema lengo kuu la makubaliano hayo ni kutafuta rasilimali zitazowezesha kuendesha tamasha hilo lenye lengo la kuenzi, kudumisha na kutunza utamaduni wa Mtanzania.

Anasema tangu kuanzishwa kwake mwaka 1982, tamasha limekuwa likifanyika kila mwaka bila kukosa mbali na kukumbwa na uhaba wa fedha, lakini anaamini kwa kushirikiana na kampuni kubwa ya biashara ya Clouds Plus Production, tamasha linaweza kuvutia wawekezaji mbalimbali.

Naye Mkurugenzi Uendeshaji wa Clouds Plus Production, Ramadhani Bukini, anasema kampuni yake inayomiliki runinga na redio, itatumia mbinu mbalimbali kulitangaza tamasha hilo Duniani ili kufanya lifikie malengo yake ya kuenzi na kudumisha utamaduni wa Mtanzania na pia kuvutia wawekezaji wengi.

Ratiba mahsusi

Dk. Makoye, anasema katika wiki ya tamasha zipo siku zitakuwa maalum kwa ajili ya ratiba mahsusi, ambako Jumatatu itakuwa ni ‘Usiku wa Filamu’, Jumatano ‘Usiku wa Muziki wa Dansi’ na Jumapili ‘Usiku wa Taarabu’.

Wasanii wanaotarajiwa kupanda jukwaani

Wasanii wanaotarajiwa kupanda jukwaani mwaka huu ni Khamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, Juma Kassim ‘Juma Nature’, Barnaba Elias ‘Barnaba’, Dullah Makabila, Gigy Money na Vitalis Maembe.

Wengine ni Mashauzi Classic, Malkia Khadija Kopa, Thabit Abdul, Bendi ya Msondo Ngoma, John Kitime na bendi yake, Sisi Tambala, Sinaubi Zawose, Shada Acrobatics na Baldreda kutoka Marekani.

Dk. Makoye, anabainisha kuwa pia makundi ya hapa nchini yatashiriki, ambapo Bagamoyo itatoa 37, Dar es Salaam 28, Zanzibar mawili huku mikoa  ya Mwanza, Ruvuma, Morogoro, Kilimanjaro, Njombe yatatoa kundi moja moja, Arusha mawili na Dodoma 10.

Makundi kutoka nje ya Tanzania, Marekani yatakuwa mawili, Botswana, Korea Kusini, Zimbabwe, Uganda, Zambia na Finland kundi moja moja huku kutoka Kenya yakiwa nane.


Mgeni rasmi ufunguzi/ufungaji

Dk. Makoye, anaweka wazi mgeni rasmi wakati wa ufunguzi katika tamasha la mwaka huu, anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe huku wakati wa kufunga atakuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juliana Shonza.
 Kikundi cha Sanaa cha Kisonge cha TPS-Moshi kikitoa burudani ya aina yake katika tamasha hilo
 Kundi la walimu wa Taasisi hiyo wakionesha umahiri katika tamasha la mwaka jana
 mojawapo ya makundi kutoka nje yaliyoshiriki tamasha la mwaka jana
 Watazamaji waliofika katika ukumbi wa taasisi hiyo
 Waziri Mwakye akijaribu fulana katika tamasha la mwaka jana huku Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Dk Herbert Makoye akifurahia hatua hiyo
 Waziri Mwakyembe alipowasili kwenye viwanja vya TaSUBa mwaka jana
Waziri Mwakyembe katika tamasha la mwaka jana 
Waziri Shonza akiangalia mojawapo ya sanaa za ufundi katika tamasha la mwaka jana

Tigo yatoa msaada wa Sh110 Milioni Hospitali ya CCBRT kusaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya mguu kifundo (clubfoot).

$
0
0

Mkurugenzi mtendaji (Tigo) Bw. Simon Karikari akimkabidhi mfano wa hundi ya Mil 110/- Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi.Hafla ya makabidhiano yalifanyika katika wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hospitali ya CCBRT

  Kampuni ya mawasiliano ya Tigo leo imetoa msaada wa Sh110 milioni kwa Hospitali ya CCBRT kwa lengo la kusaidia uboreshaji wa huduma za afya hasa kwa wagonjwa wenye matatizo ya mguu kifundo (clubfoot) utakaowanufaisha wagonjwa zaidi ya 400 hapa nchini. Msaada huu unatolewa ikiwa ni njia ya kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa ufuatiliaji wa mara kwa mara wa matibabu ili kuwawezesha wagonjwa kupatiwa matibabu stahiki na ya wakati ili kuhakiksha ugonjwa huo unatokomezwa hapa nchini.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hospitali ya CCBRT, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema “Upatikanaji wa huduma za afya kwa wagonjwa wenye ugonjwa wa mguu kifundo hasa watoto imekuwa ni changamoto kubwa hivyo tatizo hili linatakiwa kupewa kipaumbele na kwa kuona hilo Tigo tunahakikisha tunabadili historia,” alisema. Karikari alisema pia msada huo utaongeza ushiriki wa jamii na utayari wa wadau katika kuhakiksiha matibabu ya uhakika kwa watoto wenye tatizo hilo yanapatikana ili kutoa fursa kwa wao kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Aidha, Karikari alitoa wito kwa wadau wengine kuungana na Tigo katika kuboresha maisha ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa miguu kifundo kwakuwa ugonjwa huo unaweza kutibika. “Kupitia mchango huu tunaendelea kudhihirisha dhamira yetu ya kusaidia kujenga Taifa la watu wenye afya ambao wataweza kuchangia katika shughuli za kimaendeleo na pia nitoe wito kwa wadau wengine kuungana na CCBRT ili kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii yetu,” alisema. Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi aliishukuru Tigo kuwa sehemu ya maendeleo ya hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha ya wagonjwa hasa watoto. 
 
“Tigo imeonyesha mfano wa kazi ya sekta binafsi katika kutoa suluhuhisho kwa matatizo yanayozikumba jamii zetu.Kwa miaka kadhaa, CCBRT imefanikiwa kutatua changamoto ya matibabu ya ugonjwa huu wa miguu kifundo kwa kuhakikisha wagonjwa wanapatiwa huduma endelevu pamoja na ufuatiliaji wa mara kwa mara,” alisema Msangi. 
 
Aliongeza “Kupitia Tigo tumeweza kuja na mfumo wa kuwakumbusha wateja wao kwa njia ya SMS juu ya ufuatiliaji wa matibabu kwa wagonjwa ili kuhakikisha wanamaliza matibabu kikamilifu, hivyo napenda kutoa wito kwa taasisi nyingine kuunga mkono hatua hii.
 
” Kwa kutambua umuhimu wa teknolojia ya meseji (SMS) katika kurahisisha mawasiliano kwa wagonjwa wake, CCBRT imeungana na Tigo na kuanzisha mfumo wa kuwakumbusha wagonjwa kufuatilia matibabu mara kwa mara. Mfumo huo ambao ulizinduliwa mwaka 2013, ni hatua muhimu katika kuhakikisha wagonjwa wanafuatilia matibabu kwa wakati hadi pale wanapopona kikamilifu.Mgonjwa anaweza kutumiwa ujumbe wa kumkumbusha ndani ya siku nne na siku moja kabla ya siku ya kuonana na daktari. 
 
 Tangu ulipoanza kutumiwa na CCBRT, mfumo huo umeweza kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokatisha matibabu kabla ya wakati ambapo zaidi ya watoto 1,500 wameshanufaika na njia ya matibabu ya Ponseti (bila upasuaji) ya kutibu mguu kifundo. Aidha, zaidi ya wagonjwa 400 wamepata matibabu ya upasuaji kwa miaka minne iliyopita na ikitegemea kuongeza idadi hiyo mara mbili baada ya Tigo kutoa fedha hizo. //Mwisho//

SHIRIKA LA RELI TANZANIA LAMSHUKURU RAIS DKT MAGUFULI KWA KUDUMISHA MAWAZO YA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Shirika la Reli Tanzania – TRC pamoja na ‘Clouds Media Group’ (CMG) wameadhimisha miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya safari ya kihistoria kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kwa kutumia treni ya Deluxe kwa lengo la kuenzi mawazo ya Baba wa taifa ya kuhamasisha watanzania kuhamia makao makuu ya nchi jijini Dodoma kwa kutumia usafiri wa treni hivi karibuni, Oktoba 2019.

Katika safari hiyo Menejimenti ya Shirika la Reli Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa  iliungana na timu kutoka ‘Cloud Media Group’, timu ya Tigo Fiesta pamoja na wasanii zaidi ya 200 kuelekea Dodoma kuadhimisha miaka 20 ya Baba wa Taifa lakini pia kutoa burudani na hamasa kwa  wananchi wa mkoa wa Dodoma.

Licha ya kujionea Vivutio kibao vya nchi yetu ikiwemo maajabu ya mto Ruvu kwenye Safari ya kihistoria kati ya CMG na TRC, timu ya Tigo Fiesta 2019 imefanikiwa kujionea utendaji kazi wa wakandarasi waliopewa dhamana na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kujenga Reli ya Kisasa – SGR kuanzia Dar e Salaam hadi Makutupora mkoani Singida ambapo wasanii walitembelea Kilosa katika eneo ambalo handaki refu zaidi nchini linajengwa.

Katika safari hii ya kuadhimisha miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere, TRC na  CMG walihakikisha uwepo wa Mwl. Nyerere ndani ya treni ambapo vitu kadhaa ambavyo vilipendwa na Baba wa Taifa vilienziwa ikiwemo mchezo wa Bao ambao alikuwa akiupenda, hotuba zake pamoja na vyakula pendwa vya Mwl. Nyerere navyo vilipikwa katika safari hiyo.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli alionekana akifurahia mchezo wa Bao na baadhi ya wafanyakazi wa CMG, naye ACP S.K Kulyamo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Reli pia ni moja kati ya watu ambao siku ya leo alikuwa kwenye safari ya treni kutoka Dar mpaka Dodoma kuhakikisha usalama wa wasafiri, kubwa ni kuweza kuandika historia kwa kumuenzi Baba wa taifa na kuweza kukumbuka kifo cha Baba wa Taifa ndani ya treni ikiwa ni miaka 20 toka atangulie mbele za haki.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amelipongeza Shirika la Reli Tanzania kwa mapinduzi makubwa yaliyofanyika katika kipindi kifupi pia amefurahi kuona wasanii wengi wameingia Dodoma kwa kutumia usafiri wa treni na anaamini kwamba wasanii wamefurahi, wamejifunza mengi na watakuwa mabalozi wazuri kuhusu usafiri wa reli pamoja na Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa kwa niaba ya Shirika amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kudumisha mawazo ya Mwalimu kwa kuhamisha serikali mjini Dodoma na kuboresha miundombinu ya reli ambayo ndio msingi mkuu wa usafirishaji nchini, pia amewashukuru Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi, timu ya CMG na wasanii kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 20 ya Baba wa Taifa na amesema kuwa ana imani kwamba safari hiyo iimesaidia kutunza historia kuhusu maisha ya Baba wa taifa. 

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI VIONGOZI MBALIMBALI

VODACOM YAZINDUA HUDUMA YA LIPA KWA SIMU JIJINI DODOMA

$
0
0


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (kulia), akimsikiliza mhudumu wa Vodacom katika kampuni ya mabasi ya Shabiby jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo. Kushoto ni ni Meneja wa Lipa, Luis Maro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (kulia), akimsikiliza mhudumu wa Vodacom katika kampuni ya mabasi ya Shabiby jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo. Kushoto ni ni Meneja wa LIpa, Luis Maro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, akimsikiliza mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby, Mohammed Shabiby (kushoto) jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (kushoto), akionyeshwa namna meseji ya “Lipa kwa simu yako” inayoingia kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby, Mohammed Shabiby (kushoto) baada ya mteja kulipa kupitia huduma hiyo wakati wa uzinduzi katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo.
Ofisa Masoko wa Vodacom, Robert Massinda, akimuelekeza mteja wa Vodacom, Fatma Haji wakati akilipia tiketi yake kwa “Lipa Kwa Simu Yako” kwenye kampuni ya mabasi ya Shabiby wakati wa uzinduzi wa huduma wa huduma hiyo Dodoma leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (kulia), akimsikiliza mfanyakazi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (katikati), akimsikiliza mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby, Mohammed Shabiby (kushoto) jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo. Kushoto ni Meneja wa Lipa, Luis Maro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto (katikati), akimsikiliza mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Shabiby, Mohammed Shabiby (kushoto) jinsi wanavyopokea wateja wanaolipa kupitia huduma ya Vodacom ya Lipa Kwa Simu Yako wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika ofisi za Shabiby jijini Dodoma leo. Kushoto ni Meneja wa Lipa, Luis Maro.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Bazi Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerald Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshugulikia Elimu katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ali Sakila Bujiku kuwa Balozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.


Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.


Viongozi mbalimbali walioapishwa kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakisaini Hati ya kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mathias Bazi Kabunduguru wapili kutoka (kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Godfrey Mweli wa kwanza (kushoto), pamoja na Balozi Ali Sakila Bujiku wakwanza (kulia) mara baada ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa sambusa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

TANZANIA KUNUFAIKANA MIKOPO YA KUENDELEZA MIRADI YA MIUNDOMBINU KUTOKA BENKI YA ‘ASIANINFRASTRUCTURE INVESTMENT’.

$
0
0
Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrustructure Investment Bank’ Bw. Danny Alexander jijini Washington DC. Katika mazungumzo na Benki hiyo wamekubaliana kusaidia katika miardi endelevu ya Miundombinu kama Barabara na Reli.

Mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Mohammed Abdiwawa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt.Yamungu Kayandabila yalikuwa na lengo la kuangalia fursa ambazo Tanzania inaweza kunufaika kutoka katika Benki hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa na Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ Katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb) akiwa katika mazungumzo na Bw. Danny Alexander Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’  yaliyofayika katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC. Kushoto kwa Mhe.Waziri ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana, Dkt.Yamungu Kayandabila.
Makamu wa Rais wa ‘Asian Infrastructure Investment Bank’ akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) kulia, na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Mohammed Abdiwawa. Kulia kwa Mhe. Mpango ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Mashimba Ndaki na kushoto kwa Mhe.Abdiwawa ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga.


Tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako ilivyokonga mashabiki Jijini Dodoma

$
0
0

MKALI wa nyimbo za injili Godluck Gozbert akilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako katika tamasha lililofanyika juzi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma 

NYOTA wa muziki wa bongo fleva Heri Samir 'Mr Blue' akiimba katika tamasha la Tigo Fiesta 2019


Mwanadada Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ akifanya vitu vyake kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako, lililofanyika juzi Uwanja wa Jamhuru mjini Dodoma
Msanii wa Bongofleva Abdul Chande ‘Dogo Janja’ akifanya vitu vyake kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako lililofanyika juzi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
MKALI wa bongo fleva Nurdin Billal 'Shetta' akilishambulia jukwaa kwenye tamasha hilo jana


Na MWANDISHI WETU, Dodoma

ZAIDI ya wasanii 16 juzi walitingisha baada ya kutoa burudani ya aina yake katika tamasha la Tigo Fiesta Saizi Yako, lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Juzi ilikuwa zamu ya Jiji la Dodoma na maeneo jirani kupata burudani hiyo ya aina yake baada ya kufanyika mikoa mingine mitatu tangu tamasha hilo lililopozinduliwa msimu huu.

Katika tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako mjini Dodoma, walihudhuria viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mawaziri na wabunge pamoja na mashabiki kutoka katika kila kona ya mkoa huo.

Kabla ya kuanza tamasha la Tigo Fiesta 2019, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Paul Kunambi, aliwatambulisha baadhi ya wabunge na mawaziri ambao walihudhuria kwenye tamasha hilo.Kunambi alisema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu limetoa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukuza biashara za wajasiriamali kutokana na kuongeza mitaji.

Alisema kuwa kumekuwa na ajira za muda mfupi ambazo zinachangiwa na tamasha hilo ikiwa ni sehemu ya kukuza kipato kwa vijana.Alisema anaishukuru Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo kutokana na kuonyesha ubunifu wa hali ya juu na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako.

“Tunaishukuru Tigo kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na ubunifu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuendeleza vijana kupitia muziki wa bongo fleva,” alisema.Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini, Idan Komba, alisema wanaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli kwa kuhakikisha wanakamilisha usajili kwa alama za vidole kwa wateja wote wa Tigo nchini.

“Tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usajili wa alama za vidole unafanyika na kuwafikia wateja wote wa simu za Tigo nchini,” alisema.Tamasha hilo lilianza kwa wasanii chipukizi kupanda jukwaani na baadaye alipanda mkali wa bongo fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Badest na kuimba kibao chake cha Nikagongee kilichowainua mashabiki na kuanza kumshangilia kwa kupiga kelele.

Baadaye alipanda jukwaani Heri Samir ‘Mr Blue’, na kuonyesha makali yake ikiwa ni pamoja na kuporomosha vibao vya zamani na vile vinavyotamba kwa sasa katika vituo mbalimbali vya redio nchini.Mr Blue alianza na wimbo wa Tabasamu ambao aliimba live pamoja na bendi, baadaye akapiga wimbo wa Mbwa Koko, na kumalizia na Mboga Saba iliyowafanya mashabiki kuimba naye mwanzo hadi mwisho wa wimbo huo.

Hata hivyo Mr Blue alionyesha ukomavu wa hali ya juu kwenye onyesho la Tigo Fiesta Saizi Yako baada ya kumpandisha Nurdin Bilal ‘Shetta’, na kushirikiana naye kuimba wimbo wa Hatufanani.Baadaye Shetta alibaki mwenyewe jukwaani na kutoa burudani kabambe ikiwa ni pamoja na kuimba nyimbo kama Shikorobo ilioonekana kuwavutia sana mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako.

Msanii wa bongo fleva, Abdul Chande ‘Dogo Janja’alipanda jukwaani na kutoa burudani murua ambapo aliimba nyimbo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ngarenaro, Kilele na Yente.Nyota wa muziki wa injili, Godluck Gozbert alipewa nafasi kubwa na mashabiki kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako baada ya kupanda jukwaani na kuimba nyimbo mbalimbali zinazofanya vyema kwa sasa.

Staili aliyoingia nayo msanii huyo ilikuwa ya kipekee na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa kiasi kikubwa baada ya kuimba nyimbo za Shukrani, Nibadilishe na Hauwezi Kushindana.Mwanadada Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ alipanda jukwaani na kuonyesha manjonjo akiwa na wanenguaji wake.

Msanii huyo anayefanya vizuri kwenye muziki wa bongo fleva, alitawala vilivyo jukwaa kutokana na kuimba nyimbo zilizoteka hisia za mashabiki wake.Msanii huyo aliimba wimbo wa Kodo, Polepole pamoja na Muwa na kuwafanya mashabiki kumshangilia vilivyo.

Wasanii wengine waliopanda jukwani kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako, ni pamoja na Barnaba Elias, Marioo, Juma Jux na Weusi.

TCRA YASHIRIKI KUTOA ELIMU YA MAWASILIANO MAONESHO YA VIWANDA

$
0
0

Afisa Mwandamizi wa Mitambo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki Kenneth Chitemo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TCRA katika maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani yanayofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
MKUU wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akimkabidhi kitabu cha mongozo wa mawasiliano kwa mwananchi aliyetembelea maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa pwani yanayofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa.
Wakuu wa Taasisi wakiwa katika Kongamano la wiki ya viwanda mkoa wa Pwani yanayofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akiwa picha pamoja na wadhamini wa maonesho ya viwanda.

*****************

Na Mwandishi WETU

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imeshiriki maonesho ya wiki ya viwanda mkoa wa Pwani katika utoaji wa elimu ya mawasiliano pamoja na usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Akizungumza katika maonesho hayo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa katika maonesho hayo wananchi watembelee banda la TCRA kuweza kupata elimu namna ya kutumia l simu katika kupata maendeleo ya Taifa.

Mhandisi Odiero amesema kuwa uchumi wa viwanda unakwenda na mawasiliano ya simu na kutaka wadau kutumia simu katika biashara zao kwa kutangaza biasha kwa kutumia simu hizo.

Aidha amesema TCRA iko katika kampeni ya kuhamasisha wananchi kujisajili kwa laini za simu kwa lama za vidole kwa muda uliopangwa na usajili huo utafungwa Desemba 31 mwaka huu.

“Tunataka wananchi wajisajili simu zao kwa alama za vidole kwa muda uliopangwa na wasije wakapata usumbufu wakati zoezi hilo likiwa limefungwa kwa laini za simu kutopata mawasiliano.amsesema Mhandisi Odiero.

Mhandisi Odiero amesema kuwa Kanda ya Mashariki ya TCRA itapita Wilaya zote zilizo katika kanda hiyo katika kutoa elimu ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole pamoja na huduma nyinginezo za bidhaa za mawasiliano.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi waepuke kufanya maawsiliano na watu wasiowajua kwa kuwaomaba fedha ni mpaka pale watakapojiridhisha na katika mawasiliano kwani baadhi yao wanafanya utapeli.

Vodacom yatoa msaada wa kompyuta zilizounganishwa na intaneti kwa shule 14 wilayani Urambo, kukuza elimu ya kidigitali

$
0
0

· Yaonyesha njia katika maendeleo ya teknolojia ya Kidijitali kupitia mfumo wa e-learning

· Zaidi ya wanafunzi 7,000 kunufaika na msaada huo.

Oktoba 19, 2019 Urambo. Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania Plc, kupitia taasisi yake ya Vodacom Tanzania Foundation leo imetoa msaada wa kompyuta na Kipanga njia (Router) vilivyounganishwa katika intaneti kwa shule 14 za Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora. Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi 67,634,000 ni sehemu ya mpango endelevu wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu katika sekta ya elimu.

Hii ni sehemu ya ushirikiano wa Vodacom na mfuko wa pamoja wa huduma za Mawasiliano (UCSAF) wa kutoa elimu shuleni kwa kutumia miundombinu bora ya teknolojia ya mawasiliano ya Vodacom kote nchini . Kupitia ushirikiano huo, jumla ya shule 300 na hasa zilizoko vijijini zitapata kompyuta zilizounganishwa katika intaneti bure.

Akipokea msaada huo, katika shule ya Sekondari Urambo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe, alisema msaada huo wa kompyuta ni hatua muhimu kuelekea mchakato wa maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya kidijitali.

“Maendeleo ya kuelekea kwenye matumizi ya dijitali yanaonesha kuwapo mafanikio kutokana na uwepo wa kompyuta kama hizi katika shule zetu sambamba na kasi ya matumizi ya simu za mkononi nchini,” alisema Waziri Kamwelwe.

“Shule ni mahala pazuri pa kuanzia kufundisha matumizi ya kompyuta katika maisha ya kila siku. Kompyuta zikiwa shuleni hazitatumika kwa wanafunzi pekee kujifunza matumizi yake, lakini pia walimu kutumia kompyuta hizi kupata ujuzi zaidi na kuboresha uwezo wao wa kufundisha. Walimu pia watatumia muda huo kuboresha ujuzi wao ili kwenda sambamba na ulimwengu wa kidijitali na kupata maarifa Zaidi,” aliongeza Mh Kamwelwe.

“Tunaamini kwamba kompyuta hizi ni hatua nyingine katika mchakato wa mabadiliko ya kidijitali. Tunawashukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa msaada wao mzuri,” alisema Kamwelwe.

Mkurugenzi wa Vodacom Foundation, bi Rosalynn Mworia, alisema msaada huo ni sehemu ya ajenda ya Vodacom Foundation yenye lengo la kusaidia sekta ya elimu ili kutoa elimu bora na kuhakikisha wanafikia malengo ya millenia na ajenda ya kitaifa kama sehemu ya mradi wa shughuli za kijamii.

“Fursa za kidijitali ni nishati muhimu katika uchumi unaokua, zina matokeo ya haraka katika uchumi na jamii kwa ujumla. Kwa pamoja zinachangia ukuaji wa uchumi, kuongeza mianya ya ajira pia ina mchango mkubwa katika kupunguza umasikini, huku ikitoa mwanya katika kuchochea ukuaji wa sekta muhimu kama vile elimu na afya,” alisema bi Mworia.

“Vodacom imeamua kuweka nguvu katika maendeleo kidigitali Tanzania. Ndiyo maana tunajivunia kutoa msaada huu leo ambao unajumuisha kompyuta, rota vyote vikiunganishwa katika mtandao vikiwa na thamani za zaidi ya shilingi milioni 67 katika shule 14 wilayani Urambo ambayo inategemea kuwafikia zaidi ya wanafunzi 7,000,” alisema Mworia.

“Vodacom imejikita zaidi katika kukuza maendeleo ya kidijitali, mawasiliano na ubunifu nchini. Tunataka kuwasaidia wanafunzi ili waende sambamba na zama hizi za kidijitali tulizomo kwa sasa na kuwashawishi zaidi kutokuwa watumiaji tu, bali kushiriki kikamilifu katika fursa za kidijitali. Tukio la leo ni mwendelezo wa utoaji wa Kompyuta chini ya ushirikiano wa Vodacom Tanzania Foundation na UCSAF kwa shule za Tanzania Bara na Visiwani,” alisema Mworia

Wiki iliyopita, Vodacom ilitoa kompyuta na router zilizounganishwa na intaneti yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 48 kwa shule 10 Mkoani Simiyu.

Kompyuta hizi zitawezesha shule hizo kupata taarifa mbalimbali za elimu kutoka katika mfumo wa kidijitali kupitia katika muundo wa foundation yetu na hivyo kuhamasisha usomaji wa kidijitali.

Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono maendeleo ya teknolojia shuleni kupitia mpango wa Instant Schools, ambapo imetoa kompyuta mpakato na za kawaida 75 katika wa shule za sekondari za Kambangwa, Makumbusho, Mtakuja na Kinyerezi.
 
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia akimuelekeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe jinsi mfumo wa Instant Schools  unavyofanya kazi, Vodacom Tanzania Foundation imekabidhi kompyuta mpakato, router na kuunganisha intaneti yenye tahamani ya Shilingi 67m kwa shule 24 wilayani Urambo.
 

Wakenya wang'ara Rock City Marathon 2019

$
0
0
Wakati msimu wa kumi wa mbio za Rock City Marathon ukihitimishwa kwa kushirikisha mamia ya wanariadha kutoka ndani ya nje ya nchi, Serikali imesema ipo haja ya kufanya tathmini ili kupima mchango wa mbio za aina hiyo katika kuinua sekta ya utalii hapa nchini ili iweze kuwekeza nguvu zaidi katika kuziboresha.

Akizungumza wakati wa kilele cha mbio hizo zilizofanyika kwenye viunga vya jengo la Biashara la Rock City Mall ambapo ilishuhudiwa wakimbiaji kutoka nchini Kenya wakiendelea kutamba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. HamisI Kingwalla alisema wingi wa wawashiriki kutoka ndani na nje ya nchini ni kiashilio tosha kuwa mbio hizo zikitumika vizuri kutangaza utalii zitachochea ukuaji wa sekta hiyo muhimu kiuchumi.

“Nimeshuhudia mamia ya washiriki kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wamekuja kushiriki mbio hizi,tayari hiyo ni sehemu ya utalii wa ndani. Zaidi imeshuhudiwa ushiriki wa wenzetu kutoka nje ya nchini ikiwemo Kenya,Rwanda na wengine nje ya bara la Africa nao wamekuja.’’

“Ili kupata mchango hasa wa mbio kama hizi kwenye sekta ya Utalii na ukuaji wa uchumi naagiza ufanyike utafiti wa kisayansi ili Serikali tujue namna ya kuziunga mkono ziendelee kufanya vizuri zaidi,’’ aliagiza Dr Kigwangalla ambae pia alishiriki kukimbia mbio za Km 21.

Tangu kuanzishwa kwa mbio miaka 10 iliyopita zimekuwa zikivutia zaidi washiriki kutoka mataifa ya Kenya na Rwanda ambapo ilishuhudiwa Mwanariadha Kutoka Kenya Ibrahimu Too akiibuka mshindi wa mbio za km 42 upande wa wanaume baada ya kutumia muda wa 2:18:34 akifuatiwa na Wakenya wenzake Willium Koskei na John Muthui waliotumia muda wa 2:19:06 na 2:21:30 kila mmoja.Mtanzania pekee kwenye kumi bora wanaume alikuwa Hamis Athumani aliefanikiwa kushika nafasi ya nne huku akitumia muda wa 2:21:36

Kwa upande wa wanawake katika mbio hizo za km 42 ilishuhudiwa mwanariadha Elilither Tamui kutoka Kenya akiibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 2:42:50 akifutiwa na wakenya wenzake Joan Rotich (2:46:07) na Lydia Wafula (2:48:57) ambapo Watanzania Fabiola John na Zainabu Hamis walifanikiwa kushika nafasi ya 6 na nafasi ya 10.

Katika mbio za Km 21 mshindi wa kwanza upande wa wanaume ni Bernard Musau kutoka Kenya alietumia muda wa 01:11:26 akifuatiwa na Ochieng Julius kutoka Uganda alitumia muda wa 01:11:36 huku mshindi wa tatu akiwa ni Alex Nizemana kutoka Rwanda alitumia muda wa01:12: 21

Kwa upande wanawake katika mbio hizo za km 21 mshindi wa kwanza hadi wa nne wote ni kutoka Kenya ambao ni Ester Kakuri alietumia muda wa 1:21:44 , Vane Nyaboke (1:22:13), Ronah Nyabochoa (1:23:10) na Martha Njoroge(1:23:17) huku mshindi wa tano ni Grace Jackson kutoka Tanzania alietumia muda wa 1:24:23

Akizungumzia matokeo hayo Mshauri wa Masuala ya Ufundi wa Mbio hizo Bw John Bayo pamoja na kuwapongeza wanariadha kutoka Kenya kwa kufanya vizuri alisema kuwa Tanzania haikupata ushiriki wa wanariadha wakubwa kutokana na wengi wao kushiriki kwenye mbio za kimataifa na hivyo kutoa mwanya kwa wanariadha hususani wa Kenya kuweza kutamba kwenye mbio hizo.

Mbio hizo zilipambwa kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili na maonesho ya waadau mbalimbali wa utalii pamoja na wadhamini wa mbio hizo ikiwemo Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) sambamba na wadhamini wa mbio hizo ambao ni pamoja na kampuni za TIPER na Pepsi.

Wadhamini wengine ni pamoja na, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Metro FM, Mwanza Water, Pigeon Hotel, The Cask and Grill, SDN na Kampuni ya Ulinzi ya Garda World.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. HamisI Kingwalla (katikati) akimpatia zawadi ya fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 4/- mshindi wa mbio za Rock City Marathon Km 42 kwa upande wa wanawake Bi Elilither Tamui kutoka Kenya alieibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 2:42:50. Wengine ni pamoja na Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya TIPER, Bw Emmanuel Kondi (kulia) ambao ni moja ya wadhamini wakubwa wa mbio hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall jijini Mwanza.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya TIPER, Bw Emmanuel Kondi (katikati) akimpatia zawadi ya fedha taslimu mmoja wa washindi wa mbio za Rock City Marathon Km 21.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. HamisI Kingwalla (wa pili kulia) akishiriki mbio za km 21 za RockCity Marathon sambamba na mamia ya washiriki wengine wa mbio hizo.
Baadhi ya matukio yaliyopamba mbio za Rock City Marathon msimu wa 10 jijini Mwanza.














WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI URUSI KUMWAKILISHA JPM MKUTANO BAINA YA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AFRIKA NA URUSI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa mkate na chumvi  ikiwa ni utamaduni wa kukaribisha wageni wa Warusi wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sicho nchini humo Oktoba 21, 2019 ambako  anamwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, Asha Mkuja wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Demodedovo uliopo Moscow akiwa njiani kwenda Sicho nchini Urusi kumwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya viongozi wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi, Oktoba 21, 2019. Kushoto  ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Marco Mumwi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Marco Mumwi (kushoto) na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, Asha Mkuja wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Demodedovo uliopo Moscow akiwa njiani kwenda Sicho nchini Urusi kumwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya Viongozi wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi, Oktoba 21, 209.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Benki ya DCB yashinda tuzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kushoto), akikabidhi tuzo ya  mshindi wa tatu katika kitengo cha makampuni bora ya mwaka katika eneo la uwekezaji katika sekta za  kibenki  kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria wa Benki ya Biashara ya DCB, Regina Mduma wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanachama wa DSE jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  Wengine pichani kutoka kushoto ni;  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es salaam, Moremi Marwa,  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama na Ofisa katika kitengo cha Sheria wa DCB, Grace Ringo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akishikana mikono  Mkurugenzi wa Kitengo Cha Sheria was Benki ya DCB, Regina Mduma, baada ya kumkabidhi iliyoshinda benki hiyo ya  mshindi wa tatu katika kitengo cha makampuni bora ya mwaka katika eneo la uwekezaji katika sekta za  kibenki  wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanachama wa DSE jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Ofisa katika kitengo cha Sheria wa DCB, Grace Ringo.
Mkurugenzi katika Kitengo cha Sheria wa Benki ya DCB, Regina Mduma (kulia), na Ofisa wa Kitengo hicho Grace Ringo wakionesha tuzo hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha

Wateja wa Tigo Pesa wataweza kutoa pesa kupitia ATM zaidi ya 350 za UmojaSwicth

$
0
0











Kaimu Mkuu wa kitengo cha huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akizingumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM, pembeni yake ni Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi, uzinduzi huu umefanyika leo Dar es salaam.
Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi, akifafanua Jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM .Uzinduzi hum umefanyika katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es salaam.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akifanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati akizindua huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM, pembeni yake ni Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi, uzinduzi huu umefanyika leo Dar es salaam

Kaimu Mkuu wa kitengo cha huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akizindua huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM, pembeni yake ni Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi, uzinduzi huu umefanyika leo Dar es salaam


 Tigo kupitia kitengo cha Tigo Pesa imeingia ubia na taasisi ya UmojaSwitch (BCX) kuzindua huduma ya kutoa fedha kwa njia ya ATM ambayo ni rahisi na ya uhakika kwa wateja wa Tigo.

Ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ni hatua muhimu katika kuchochea agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwani inaifanya huduma ya Tigo Pesa kuwa zaidi ya huduma ya kifedha kwa njia ya simu na kuwa huduma ya kibenki.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Kaimu Mkuu wa kitengo cha huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema huduma hiyo mpya ni utekelezaji wa mkakati wa Tigo wa kutoa huduma za kidigitali zenye ubora ili kukidhi mahitaji ya wateja.

“Tuna furaha kuzindua huduma hii mpya ya kibenki ambayo itawapa wateja wetu uhuru wa kifedha kwakuwa ni njia rahisi na ya haraka ya kupata pesa mahali popote kupita ATM za UmojaSwitch zilizopo maeneo mbalimbali ya nchi,” alisema Pesha.

Pesha alisema huduma hiyo mpya itarahisisha utumaji na kupokeaji wa pesa kwa kutumia ATM za UmojaSwitch zaidi ya 350 zilizopo hapa nchini hivyo kuchochea ustawi wa kiuchumi kwa wateja wa Tigo.

“Ni matumaini yetu kuwa huduma hii itachochea utekelezaji wa lengo letu la kuwafikia wananchi kila kona ya nchi na zaidi kuchangia agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi.Kwa ushirikiano huu Tigo inakuza mtandao wake kwa kuwapa wateja njia mbadala ya kutoa fedha zilizoko kwenye akaunti ya Tigo Pesa kupitia ATM za UmojaSwitch.Hii inasaidiwa zaidi na mawakala zaidi ya 100,000 waliopo nchini,” alisema.

Mteja wa Tigo atatakiwa kufuata hatua zifuatazo kwa ajili ya kuweza kutoa fedha kutoka katika ATM za benki ya UmojaSwitch, ata Piga *150*01, Chagua 7. Huduma za Kifedha, Chagua 5. Kutoa pesa ATM,Chagua Benki, alafu ataandika Kiasi cha fedha anachotaka kutoa kisha namba yake ya siri.Katika ATM, mteja atabonyeza kitufe cha TigoPesa alafu ataingiza namba ya simu, kisha OTP(namba ya siri ya kutumika mara moja tu), halafu atapata fedha zake kutoka kwenye ATM.

Pia, huduma hiyo mbali na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa pesa pia itasaidia katika ukuzaji wa sekta ya fedha pamoja na kurahisisha ufanyaji wa miamala muda wowote.

Naye, Afisa Mkuu Mtendaji wa UmojaSwitch,Company Ltd, Danford Mbilinyi alisema “ushirikiano huu utachochea ukuaji wa sekta ya fedha huku ukirahisisha upatikanaji wa huduma kwa watu wote kila mahali,” alisema.

Alisema UmojaSwitch ina farijika kushirikiana na Tigo ili kuwapatia wateja uhuru wa kifedha muda wote na zaidi kuokoa muda na gharama kwani ATM za UmojaSwitch zipo maeneo mengi ya nchi.

TCRA YAKUTANA NA WATU WENYE ULEMAVU WA KUSIKIA KUTOA ELIMU YA HUDUMA YA MAWASILIANO

$
0
0

 Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Walter Marick, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Dorice Mhimbira, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), mwenye shati jeupe Sohela Mabeyo, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
 Mmoja kati ya washiriki wa semina hiyo Yusuph Mloli, akiuliza swali kwa kutumia lugha ya vitendo kwa maafisa wa TCRA hawapo pichani, namna bora ya kutumia huduma ya mawasiliano wakati semina iliyofanyika jijini Dodoma.
Mmoja kati ya washiriki wa semina hiyo David Chamila, akiuliza swali kwa kutumia lugha ya vitendo kwa maafisa wa TCRA hawapo pichani, namna bora ya kutumia huduma ya mawasiliano wakati wa semina iliyofanyika jijini Dodoma.
Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Dorice Mhimbira, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
 Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Walter Marick, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), mwenye shati jeupe Sohela Mabeyo, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
 Mmoja kati ya washiriki wa semina hiyo Yusuph Mloli, akiuliza swali kwa kutumia lugha ya vitendo kwa maafisa wa TCRA hawapo pichani, namna bora ya kutumia huduma ya mawasiliano wakati semina iliyofanyika jijini Dodoma.
Mmoja kati ya washiriki wa semina hiyo David Chamila, akiuliza swali kwa kutumia lugha ya vitendo kwa maafisa wa TCRA hawapo pichani, namna bora ya kutumia huduma ya mawasiliano wakati wa semina iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa semina walipokuwa wakiwasikiliza maafisa wa TCRA wakati wa semina ya kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia, namna bora ya kutumia huduma za mawasiliano, semina iliyofanyika jijini Dodoma.


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania TCRA imekutana na kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa kutokusikia katika mkoa wa Dodoma kwa lengo la kutoa elimu kuhusu utumiaji wa huduma za mawasiliano na namna ya kukabiliana na changamoto katika kutumia huduma za mawasiliano.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Walter Marick,amesema ni utaratibu wa mamlaka hiyo kutoa elimu ya mawasiliano kwa watumiaji, lakini watu hao wametoa maombi maalamu .

Kwa ajili ya kupatiwa mafunzo hayo kwa lengo la kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika kutumia bidhaa za mawasiliano, kwani watu hao wamekuwa wahanga katika kutumia mawasiliano kutokana na ulemavu walionao.

“Ni utaratibu kila wakati kutoa elimu kuhusu elimu ya kukabiliana na changamoto katika mawasiliano, lakini tumepewa ombi maalamu kwa ajili ya kutoa elimu kwa watu hawa wenye ulemavu wa kutokusikia, na elimu hii ni mahususi kwa sababu hawa ndio wahanga katika uhalifu wa mtandaoni”amesema Marick.

Amesema kundi hilo kama wadau wao wamekuwa na changamoto nyingi katika kutumia bidhaa za wasiliano, kwani baadhi yao hawana uelewa katika suala la changamoto za mawasiliano, hali inayopelekea kuathrika na vitendo vya wizi wa mitandaoni.

“Tumetoa tahadhari ya changamoto zilizopo katika mawasiliano ambazo wengi wamekuwa wakikutana nazo hasa katika utapeli, njia mojawapo wa kupunguza ni kumsaidia mtumiaji, mfano kapokea ujumbe wa kutakiwa kutuma fedha kwa namba usiyoifahamu usitekeleze kwanza na nini cha kufanya” amesema.

Aidha amesema na wao kama mamlaka wamesikia changamoto ambazo wanakutana nazo katika kutumia mawasiliano, na wengi hawana uelewa katika kukabiliana na vitendo vya wizi mitandaoni na uhalifu mwingine mitandaoni, hasa katika kutunza siri zao za mawasiliano kuepuka na na vitendo hivyo.

“Ametolea mfano baadhi yao wanaweza kuwa amejiunga kifurushi na kabla hajakitumia wakakata, na yeye bila kuelewa kuwa anahaki ya kujua, lakini ana amua kununua vocha na kujiunga tena bila kujua kwanini, na tumewaelekeza kuwa anapokutana na kitu kama hicho, anatakiwa kuhoji na tumewaelekeza mamlaka ilipo kwa ajili ya msaada zaidi anapokuwa hajaridhika na majibu ya mtoa huduma” amesema.

Pia amesema kila kanda kuna mamlaka za mawasiliano na wanajukumu la kuhakikisha wanatoa elimu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano ili kila mtumiaji atambue haki yake katika kutumia huduma ya mawasiliano na namna ya kuepuka uhalifu wa mitandaoni.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwamo Yusuph Mloli na David Chamela, wenye ulemavu wa kusikia wameshukuru kupewa mafunzo hayo kwani yamekuwa msaada mkubwa kwao, na yametusaidia katika kuwafungua na kupata uelewa juu ya huduma za mawasiliano na mamna ya kukabiliana nazo.

“Niwashukuru sana TCRA kwa sababu hapo mwanzo sikuwa na uelewa na kunavitu nilikuwa na fanyiwa na mitandao ya simu lakini sikujua kama sitendewi haki lakini kwa sasa nimeelewa vizuri, na ukizingatia sisi walemavu wa macho ndio waathirika katika vitendo vya wizi mitandaoni” amesema Chamela.
Baadhi ya washiriki wa semina walipokuwa wakiwasikiliza maafisa wa TCRA wakati wa semina ya kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia, namna bora ya kutumia huduma za mawasiliano, semina iliyofanyika jijini Dodoma.


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania TCRA imekutana na kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa kutokusikia katika mkoa wa Dodoma kwa lengo la kutoa elimu kuhusu utumiaji wa huduma za mawasiliano na namna ya kukabiliana na changamoto katika kutumia huduma za mawasiliano.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Walter Marick,amesema ni utaratibu wa mamlaka hiyo kutoa elimu ya mawasiliano kwa watumiaji, lakini watu hao wametoa maombi maalamu .

Kwa ajili ya kupatiwa mafunzo hayo kwa lengo la kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika kutumia bidhaa za mawasiliano, kwani watu hao wamekuwa wahanga katika kutumia mawasiliano kutokana na ulemavu walionao.

“Ni utaratibu kila wakati kutoa elimu kuhusu elimu ya kukabiliana na changamoto katika mawasiliano, lakini tumepewa ombi maalamu kwa ajili ya kutoa elimu kwa watu hawa wenye ulemavu wa kutokusikia, na elimu hii ni mahususi kwa sababu hawa ndio wahanga katika uhalifu wa mtandaoni”amesema Marick.

Amesema kundi hilo kama wadau wao wamekuwa na changamoto nyingi katika kutumia bidhaa za wasiliano, kwani baadhi yao hawana uelewa katika suala la changamoto za mawasiliano, hali inayopelekea kuathrika na vitendo vya wizi wa mitandaoni.

“Tumetoa tahadhari ya changamoto zilizopo katika mawasiliano ambazo wengi wamekuwa wakikutana nazo hasa katika utapeli, njia mojawapo wa kupunguza ni kumsaidia mtumiaji, mfano kapokea ujumbe wa kutakiwa kutuma fedha kwa namba usiyoifahamu usitekeleze kwanza na nini cha kufanya” amesema.

Aidha amesema na wao kama mamlaka wamesikia changamoto ambazo wanakutana nazo katika kutumia mawasiliano, na wengi hawana uelewa katika kukabiliana na vitendo vya wizi mitandaoni na uhalifu mwingine mitandaoni, hasa katika kutunza siri zao za mawasiliano kuepuka na na vitendo hivyo.

“Ametolea mfano baadhi yao wanaweza kuwa amejiunga kifurushi na kabla hajakitumia wakakata, na yeye bila kuelewa kuwa anahaki ya kujua, lakini ana amua kununua vocha na kujiunga tena bila kujua kwanini, na tumewaelekeza kuwa anapokutana na kitu kama hicho, anatakiwa kuhoji na tumewaelekeza mamlaka ilipo kwa ajili ya msaada zaidi anapokuwa hajaridhika na majibu ya mtoa huduma” amesema.

Pia amesema kila kanda kuna mamlaka za mawasiliano na wanajukumu la kuhakikisha wanatoa elimu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano ili kila mtumiaji atambue haki yake katika kutumia huduma ya mawasiliano na namna ya kuepuka uhalifu wa mitandaoni.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwamo Yusuph Mloli na David Chamela, wenye ulemavu wa kusikia wameshukuru kupewa mafunzo hayo kwani yamekuwa msaada mkubwa kwao, na yametusaidia katika kuwafungua na kupata uelewa juu ya huduma za mawasiliano na mamna ya kukabiliana nazo.

“Niwashukuru sana TCRA kwa sababu hapo mwanzo sikuwa na uelewa na kunavitu nilikuwa na fanyiwa na mitandao ya simu lakini sikujua kama sitendewi haki lakini kwa sasa nimeelewa vizuri, na ukizingatia sisi walemavu wa macho ndio waathirika katika vitendo vya wizi mitandaoni” amesema Chamela.

USAFIRI WA RELI KUIMARISHWA KATIKA MAJIJI- MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP , Alexsey Pankov (kushoto) na Ignat Dydyshko baada ya mazungumzo kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP, Alexsey Pankov (kushoto) na Ignat Dydyshko baada ya mazungumzo kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP, Alexsey Pankov (kuatikati) na Ignat Dydyshko kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Russian Railways, Alexander Misharin kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya ya Zarubezhnefe, Bw. Sergey Kundryashov kwenye hoteli ya Marriot iliyopo Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya ya Zarubezhnefe, Bw. Sergey Kundryashov kwenye hoteli ya Marriot iliyopo Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwakilishi wa Kampuni ya Sinara Transport Machinary kwenye hoteli ya Marriot, Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

………………………

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Russian Railways, Bw. Alexander Misharin na kumweleza kuwa Tanzania inahitaji sana kuimarisha usafiri wa ndani wa reli hasa katika Majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga.

Amesema kampuni hiyo yenye uwezo mkubwa wa kujenga reli mpya, kukarabati reli, kutengeneza injini za treni na mabehewa pamoja na ukarabati wake inahitajika sana nchini ili kufanikisha mpango wa Serikali wa kuimarisha reli za zamani za TAZARA, Reli ya Kati na kufugua reli ya Kaskazini inayounganisha mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Waziri Mkuu alizungumza na Mkurugenzi huo jana (Oktoba 22, 2019) kwenye hoteli ya Marriot iliyopo Sochi nchini Urusi, ambapo alitumia fursa hiyo kuikaribisha kampuni ya Russian Railways kuwekeza nchini hususani katika sekta ya ujenzi, ufundi na mafunzo ikishirikiana na makampuni ya Watanzania.

Waziri Mkuu yuko nchini Urusi kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na Urusi (Russia-Africa Summit), unaotarajiwa kuanza leo Oktoba 23 hadi 24, 2019 katika jiji la Sochi. Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

“Katika kipindi hiki ambacho Tanzania inajenga reli ya kiwango cha kimataifa ya SGR pamoja na kufufua reli ya Kaskazini, inaikaribisha Kampuni ya Russian Railways kwa mikono miwili ije ifanye mazungumzo rasmi na Wizara husika. Pia Serikali inao mkakati wa kujenga reli mpya katika ukanda wa Kusini kutoka Mtwara hadi Ruvuma ili kuiunganisha bandari ya Mtwara na mikoa ya Kusini pamoja na nchi jirani za Malawi na Zambia.”

Alisema Tanzania kwa sasa inahitaji sana kuimarisha usafiri wa ndani wa reli hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga hivyo endapo mazungumzo kati ya Wizara husika na kampuni hiyo yataonekana kuwa na tija na yana maslahi kwa Watanzania, kampuniyo itapewa fursa ya kuwekeza nchini.

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wafanyabiashara wa Tanzania, wito wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuwataka watumie fursa lukuki zilizopo nchini kuanzisha makapuni ya pamoja na makampuni ya nje ili kuunganisha nguvu kwa kuendesha kwa pamoja makampuni yatakayoanzishwa.

Alisema utaratibu wa makampuni ya Tanzania kuanzisha makampuni ya pamoja na makampuni ya nje utawapa Watanzania fursa ya kujipatia kipato pia wataweza kulinda maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kapuni ya Russia Railways, Bw. Misharin alimuhakikishia Waziri Mkuu kuwa kampuni yake iko tayari kushirikiana na wafanyabiashara wa Kitanzania katika kuanzisha makapuni ya pamoja ili kuipatia Tanzania tekinolojia ya masuala ya reli na kubadilisha ujuzi. 

Awali, Waziri Mkuu alizungumza na Wakurugenzi wa Kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP, Bw. Alexsey Punkov na Bw. Ignat Dydyshkoa ambaye alisema kuwa kampuni yake inakusudia kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya kilimo kwa kuleta nchini mashine mbalimbali kama vile matrekta na mitambo ya ujenzi wa barabara. 

Viongozi wote wa makampuni ya Urusi waliozungumza na Waziri Mkuu waliahidi kuja Tanzania mwaka huu ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji na kufanya mazungumzo yenye lengo la kushirikiana na wafanyabiashara wa Kitanzania katika uwekezaji wao wanaokusudia kuufanya nchini.

Mheshimiwa Majaliwa pia alizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Zarubezhnefe, Bw. Sergey Kundryashov ambaye pia alionyesha nia ya kutaka kuwekeza nchini Tanzania.

Katika safari hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), James Matarajio.

Exim Bank Launches Nyumba Yangu Loan Campaign

$
0
0
Exim Bank Tanzania has recently launched a three-month long home loan campaign at an attractive low-interest rate to make home ownership more accessible, affordable and within reach of many Tanzanians.

The product named “Nyumba Yangu Loan’’ offers a fantastic interest rate of 15% per annum to all new applications for new house loans for the next 90 days, according to Exim Bank Head, Retail and SME Assets Mr. Charles Kapufi.

Speaking during the campaign launch held in Dar es Salaam on Monday, Mr. Kapufi, said through the product customers will be rewarded with the right loan at the right cost.

“Buying a house could be a single most important investment decision for many first-time homebuyers but could mean something different to those buying their next homes. That is why our approach to home purchases loans and equity release by refinancing a self-owned house is not that of one-size-fits-all.’’ He said.

He said the product, will further assist current homeowners who have existing mortgage loans  elsewhere  replacing their high-interest payment with low rates and favorable loan tenor.

“And the story does not just end there, for those whose houses have increased in value because of price appreciation or quality improvements done on the property, we are better placed to help them convert the value in their houses into cash through a cash-out mortgage loan. Upon which they can use the monies advanced to buy the next home, upgrade the property with the landscape, new paint, new roof, set up an additional saving or put the money towards long-term investment.’’ He said.

As part of a development ecosystem, the bank is committed to taking a front seat in providing a valuable opportunity to potential and existing homeowners, the right change and growth in their livelihoods by providing them with affordable loan terms, according to Mr. Kapufi.

“It’ is our belief that, this will surely be achieved by advising and serving our customers as part of our family, as we help them in every stage of the loan application process, in friendly easy steps.A perfect home needs a perfect financial partner, welcome and let’s prosper together through Nyumba Yangu Loan’’. He proudly said.

Vodacom yanyakua Tuzo ya DSE 2019

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji(wa pili kulia) akikabidhi tuzo ya Kampuni Bora DSE kwa mwaka 2019 katika sekta isiyo ya Viwanda, kwa
Mkuu wa Uhusiano wa Uwekezaji na Miradi Maalumu wa Vodacom Plc, Robin Kimambo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Usalama wa Mitaji, Nicodemus Mkama. Hafla hii ilifanyika juzi jijini Dar Es Salaam.



Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania, Vodacom imeshinda tuzo ya soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika juzi jijini Dar es Salaam, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Mazingira, Jamii na Utawala Endelevu’ Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu K. Kijaji.

Lengo kuu la tuzo hizi ni kukuza ubora wa biashara katika nyanja ya Utunzaji wa Mazingira, Utawala Bora wa Kampuni, Kuongeza Uwajibikaji katika shughuli za Kijamii na kuhakikisha kuwa DSE inaendelea kutimiza wajibu wake kwa wanachama.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkuu wa Uhusiano wa Uwekezaji na Miradi Maalumu wa Vodacom Plc, Robin Kimambo, alisema tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa kampuni hiyo ambayo kwa sasa inaongoza kwa uvumbuzi kwenye teknolojia ya mawasiliano nchini.

“Jambo la msingi ni kuwaahidi watanzania kuwa, tutaendelea kuwa wabunifu na wavumbuzi ili kuendelea kutoa huduma ambapo kwa sasa tuna takriban wateja zaidi ya milioni 14 nchi nzima,” alisema.

Washiriki wa tuzo hizo ni kampuni zilizoorodheshwa DSE ambazo ni pamoja na Madalali au Wafanyabiashara, Washauri waliopendekezwa pamoja na vyombo vya habari vya kidigitali na magazeti.

Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc iliorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam Agosti 15, 2017.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA AALCO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA – IKULU JIJINI DSM

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi wa
Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika
(AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa
nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49
na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam.
Oktoba 23, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa
Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad
Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina) mara baada ya mazungumzo na
Viongozi hao wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia
na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika
hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama
49 na mashirika mbalimbali ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Bi. Wang Liyu
Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria wa China mara baada ya
mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa
Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58
unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka
nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu
jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti
cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou, ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba
23, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti
cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou aliyeambatana na Katibu Mkuu wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa na Balozi wa
China hapa nchini Mhe. Wang pamoja na Kanali Ngamela Lubinga Katibu
wa NEC siasa na Uhusiano wa Kimatifa wa Ccm ikulu jijini Dar es
Salaam. Oktoba 23, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais
wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh
(Waziri wa Sheria wa Palestina) mara baada ya mazungumzo na Viongozi
hao wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika
(AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa
nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49
na mashirika mbalimbali ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja
na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama
cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou aliyeambatana na
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally
Kakurwa na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang na Kanali Ngamela Lubinga Katibu wa NEC siasa na Uhusiano wa Kimatifa wa Ccm mara baada ya mazungumzo yao ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Amon Mpanju
Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria (Tanzania) mara baada ya
mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa
Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58
unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka
nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu
jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Waziri wa Sheria na Katiba, Tanzania), Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina), Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Kennedy Gastorn (Tanzania) na Naibu Makatibu Wakuu wa AALCO
watatu ambao ni Bw. Yukihiro Takeya (Japan), Bi. Wang Liyu (China) na
Dr. Ali Garshasbi (Iran) pamoja na Amon Mpanju Naibu katibu mkuu
Wizara ya Katiba na Sheria (Tanzania), ambao wanahudhuria mkutano
wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe
kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea
ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akigana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa (Wakwanza kulia) na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang (wakwanza kushoto) mara baada ya Mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019

PICHA NA IKULU

Tigo Pesa yakuza uchumi wa mawakala nchini

$
0
0
  Baadhi ya mawakala wa Tigo Pesa hapa nchini wameeleza namna ambavyo wamekuza vipato vyao kupitia utoaji wa huduma ya Tigo Pesa huku wakiwataka watu kuchangamkia fursa hiyo. Mbali na huduma ya kutuma na kupokea pesa, huduma ya Tigo Pesa imekuwa huduma kamili ya kifedha ikitoa mikopo, bima, kuweka akiba pamoja na kupokea pesa kutoka nje ya nchi jambo linaloifanya kuongeza wigo wa fursa kwa mawakala wake.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti, Mawakala hao ambao wana uzoefu wa kati ya miaka mitano na saba kwenye huduma hiyo wamesema bado kuna fursa kupitia huduma hiyo inayokua kwa kasi hapa nchini. Suleiman Hussein kutoka visiwani Zanzibar ambaye amefanya kazi ya uwakala kwa kipindi cha miaka saba anasema kuwa kupitia Tigo Pesa ameweza kuimarisha kipato chake kwa kiasi kikubwa ikiwamo kumuwezesha kununua gari mbali na kuendesha familia yake. 

 “Nashukuru Mungu kupitia Tigo Pesa kipato changu kimekua na nimeweza kununua gari langu pamoja na kuendesha familia yangu.Naona kuna fursa kubwa sana kwenye huduma hii ya Tigo Pesa na ndio maana naendelea kukuza mtaji wangu, kuhudumia wateja wengi zaidi kwasababu ni huduma inayohitajika kila siku,” alisema Hussein.

 Hussein anawahimiza mawakala kuboresha zaidi utoaji wa huduma ili kuweza kuvutia wateja.Pia, aliwataka wateja kutumia zaidi huduma za Tigo Pesa katika shughuli zao za kila siku. Naye, Vicky Ibrahim wakala wa Tigo Pesa katika maeneo ya Kariakoo – Msimbazi anasema tangu ameanza kazi hiyo ya uwakala miaka mitano iliyopita ameona mabadiliko makubwa kiuchumi licha ya kuanza na mtaji kiduchu.

 “Nilianza na mtaji mdogo sana wa laki sita (600,000/-) ila kwa sasa namshukuru Mungu umezidi kukua siku hadi siku.Kuna mafanikio mengi sana nimezidi kuyapata katika kazi zangu kwanza familia yangu imezidi kunufaika kwa kiasi kikubwa.” Anasema siri kubwa ya ukuaji huo ni utoaji wa huduma zenye kuzingatia uaminifu na ubora kwa wateja jambo ambalo linawafanya kuzidi kufika katika ofisi yake. “Wale ambao wanatarajia au wanataka kuwa mawakala nawakaribisha kwa mikono miwili kwani mimi nilianza na msingi mdogo sana lakini saizi nimepata mafanikio makubwa kupitia hii kazi ya uwakala wa Tigo Pesa,’ alisema. 

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha anasema kuna fursa nyingi zinazopatikana kupitia uwakala wa Tigo Pesa kwakuwa kwa sasa huduma hiyo imekuwa huduma kamili ya kifedha. “Tigo Pesa ilianza kama huduma ya kutuma na kutoa pesa ila kwa sasa ni huduma kamili ya kifedha tunatoa mikopo,tunatoa bima ya matibabu kwa mtu na familia na pia tunawawezesha wateja wetu kuweka akiba.Pia, tunawezesha makampuni kufanya malipo mbalimbali kwa urahisi na usalama zaidi,” anasema Pesha. 

Pia, huduma ya Tigo Pesa imeingia katika huduma za fedha kidigitali kupitia App ya Tigo Pesa ambayo inampa mteja uwezo wa kutuma na kupokea pesa na pia kurudisha muamala uliokosewa kwa urahisi zaidi. “Napenda kuwahamasisha mawakala wetu kuendelea kufanya kazi na Tigo kwani fursa bado ni nyingi na pia tunaendelea kutafuta mawakala na kwa wateja wetu waendelee kufanya miamala na Tigo kwani Tigo Pesa ni zaidi ya Pesa,” alisema Pesha. Mwisho.
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images