Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1885 | 1886 | (Page 1887) | 1888 | 1889 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard(wa tatu kutoka kulia) akiwakabidhi mfano wa tiketi wafanyabiashara kumi waliodhaminiwa na benki ya NMB kwenda nchini China kwa ajili ya kushiriki maonyesho ya biashara nchini humo kyanayotarajia kuanza wiki ijayo


  Mkuu wa Kitengo cha biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard akikabidhi mfano wa tiketi ya kwenda china Mfanyabiashara kutoka Musoma mkoani Mara, Oliver Kisamba (wa pili kutoka kushoto) wakati wa hafla ya kuwakabidhi tiketi wafanyabiashara kumi kwa ajili ya kwenda nchini China kwa ajili ya kushiriki maonyesho ya 125 ya biashara yakayofanyika chini humo. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa benki ya NMB Idara ya biashara, Theresia Mayanie na wa kwanza kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha wafanyabiashara wadogo,
  Beatrice Mwambije

  Mkuu wa Kitengo cha biashara wa NMB, Donatus Richard akizungumza na wafanyabiashara kati ya kumi waliofadhiliwa na benki ya NMB kwenda nchini China kwa ajili ya kwenda kushiriki maonyesho ya biashara yanayaotarajia kuanza wiki hii nchini humo wakati wa hafla ya kuwakabidhi tiketi jijini Dar es Salaam


  WAFANYABIASHARA 10 wanachama wa Klabu za Biashara za Benki ya NMB (NMB Business Club), wameondoka nchini jana kwenda China, kushiriki Maonesho ya 125 ya Canton Fair 2019, yanayofanyika wiki hii mjini Guangzhou, ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kibiashara ya siku 10.

  Tiketi za safari ya wafanyabiashara hao (kwenda na kurudi), malazi, chakula na kila kitu, vimegharamiwa Benki ya NMB, ambayo iliwataka kuitumia fursa hiyo vema kwa kwenda kujifunza namna ya kuboresha biashara, kukuza mitaji na kuchangia uchumi wa taifa.

  Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wafanyabiashara hao kutoka Kanda mbalimbali za klabu zao nchini, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Donatus Richard, (Head of Business Banking) aliwataka kuwa mabalozi wema NMB wakiwa China na kutumia vema elimu watakayopata kupitia maonesho watakayoshiriki.

  “Ni matumaini yetu kwamba mtaitumia vizuri safari hii kujifunza fursa mbalimbali za kibiashara zikiwemo za uwekezaji wa viwanda ili kuendana na kasi ya Tanzania ya Viwanda inayochakatwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

  “Kufanya hivyo kutawasaidia kuongeza mbinu katika nyanja mbalimbali, ikiwemo kujua kwa namna gani mnaweza ushirikiana kufanya biashara kimataifa, hatua ambayo itawanyanyua kiuchumi,” alisema Richard huku akiwataka kurejea wakiwa bora zaidi kimbinu katika kukuza mitaji yao.

  Kwa niaba ya NMB, Donatus akawasistiza wafanyabiashara hao kuwa, furaha yao kama taasisi kinara ya fedha nchini itakuwa ni kushuhudia mapinduzi chanya ya kimaendeleo kupitia elimu watakayopata kupitia ziara na maonesho watakayoshiriki China.

  Akitaja vigezo vilivyotumika kupata wafanyabiashara hao 10 kutoka miongoni mwa wanachama zaidi ya 200,000 kote nchini, Richard alisema ni pamoja na rekodi nzuri za marejesho ya mikopo na nguvu ya ushawishi ya mwanachama kuongeza wanachama/wateja wapya katika NMB.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa NMB Business Club wilaya ya Ilala, Award Mpandilah, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kamuni ya Mpandilah General Supplies Ltd, aliishukuru NMB kwa fursa waliyowapa, ambayo ana uhakika inaenda kubadili mifumo yao kibiashara.

  Alibainisha ya kwamba, ziara ya siku 10, inayoambatana na ushiriki wa Maonesho ya Canton Fair 2019, vitawaongezea elimu na kuwatia chachu ya mafanikio kibiashara na kwamba watarejea wakiwa wamejenga chaneli za ushirikiano na wafanyabishara wa nchi hiyo.

  “Ni fursa ambayo inatamaniwa na kila mtu aliye na kiu ya maendeleo. Tunaishukuru NMB kwa nafasi waliyotupatia na tunaahidi kuitumia vema kuhakikisha tunapiga hatua za haraka kimaendeleo ya mfanyabiashara mmoja mmoja, benki inayotuhudumia na taifa kwa ujumla,” alisema Mpandilah.

  0 0


  Afisa Mauzo wa Kampuni ya Kansai Plascon (T) Ltd, FloraMapunda,akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi, Robson Majura, mshindi wa Promosheni ya Nunua na ushinde Rangi za Plascon .Mshindi alikabidhiwa fedha tasilimu kiasi cha shilingi,!1,000,000,(milioni moja) jana katika Ofisi za Kampuni hiyo Barabara ya Nyerere Jijini Dares Salaam.
  Muwakilishi kutoka kampuni ya Plascon Mkoani Mwanza Subodh Issar akimkabidhi Frank Silver mshindi wa Promosheni ya Nunua na ushinde Rangi za Plascon .Mshindi alikabidhiwa fedha tasilimu kiasi cha shilingi 1000,000,(milioni moja) jana katika Ofisi za Kampuni Jijini Mwanza.


  Washindi kujishindia zawadi za pesa taslimu 

  Dar es Salaam: Promosheni ya Paka Rangi ya Plascon na Ushinde imerejea, na sasa inakuja na toleo maalumu la rangi, maarufu kama Rangi ya Pesa kwa nia njema ili kuwanifaisha wateja wake. Mwaka huu washindi watajishindia na zawadi za pesa taslimu.

  Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Hussein Jamal, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo kipya cha mauzo ya rangi ya Plascon, jijini Dar es Salaam.

  Jamal alisema, “Kibiashara tunafurahi kuwa na kampeni kama hii ambapo kupitia katika promosheni yetu , tuna uhakika kwamba, kuwapo na ushindi wa pesa taslimu kutaleta nyuso za furaha kwa washindi katika kipindi chote cha msimu wa kampeni hii.

  Promosheni ya Paka Rangi na Ushinde inatupatia fursa, siyo tu kuwazadia wateja wetu muhimu, watumiaji wa rangi na wauzaji, lakini pia kujenga msingi wa mafanikio ambayo tumeyapata kupitia bidhaa yetu ya hii ya Plascon, tangu tulipoizindua mwaka 2017,”

  Kadhalika, Jamal alifafanua kuwa, promosheni hiyo ni ushahidi tosha wa kuonesha jinsi ambavyo Plascon imeamua kutoa huduma kwa watanzania na namna biashara yake inavyolenga kuongeza thamani katika uzalishaji wa rangi bora, zenye viwango, utafiti na wenye lengo la kukidhi haja ya mahitaji ya rangi na kutoa ushauri bora kwa watanzania na watumiaji wa rangi kwa ujumla.

  Promosheni iliyopewa jina la ‘Colour of Money’ itaendeshwa kuanzia Otoba 7 hadi Desemba 14, 2019, na inatarajia kushirikisha mamia na maelfu huku kila mshiriki akiwa na uhakika wa kutotoka mikono mitupu .

  Meneja Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Tyron Immelmann, alisema kuwa, mwaka huu , Plascon itatoa zawadi za pesa taslimu shilingi milioni tano kila wiki, ambapo kila siku kutakuwa na mshindi wa Sh 1,000,000 taslimu.

  Washiriki watatakiwa kununua lita 20 za rangi ya Plascon, na kupewa kadi ambayo mteja ataisugua na na kutuma namba zake za bahati kwenda 15054, baada ya hapo atakuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi.

  Matangazo ya Msimu huu wa Promosheni ya Paka Rangi Ushinde na Rangi ya Pesa, yatatangazwa kupitia vipeperushi kutoka kwa wauzaji, halikadhalika kupitia katika radio na televisheni.

  0 0

  Katibu tawala wa wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma Mh Zahara Muhidin Michuzi zao la uvccm ,amekua kivutio kikubwa Kwa vijana katika kongamano la kumuenzi Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere ambalo limefanyika tarehe 12 /10/2019  Katika wilaya ya Tabora mjini.

  Das Zahara katika mada na hotuba yake Katika kumuenzi Muasisi wa Taifa letu aliwataka vijana kuenzi Maisha ya Nyerere kitabia na mienendo ya Mwl kwa kuchagua viongozi bora ,,waadilifu ,wenye uthubutu ,wachapakazi ,wabunifu ,waadilifu na wenye uzalendo kwa Jamii wanayoiongoza na Taifa kwa Ujumla ,,
  Das Zahara alisisitiza kwa kuchagua viongozi wa aina hii tutakua tunaliweka Taifa katika mikono salama , Kwani viongozi hawa watakua sehemu ya urithi wa mwalimu katika kutoa uongozi huru na wa haki usimamiao misingi ya haki na usawa kwa watu na utakua chachu ya maendeleo kwa Taifa ,

  Das Zahara pia alisisitiza kwamba hatuwezi kufikia Lengo la kuwachagua viongozi bora endapo Kama wananchi hawatojitokeza kujiandikisha Katika daftari la mpiga kura ili kuweza kukidhi kigezo cha kushiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa,Akatoa wito kwa vijana kujiandikisha kwa wingi na kuhimiza wengine kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ,

  Katika kumjenga mtoto wa kike Das Zahara aliwaambia washiriki wa kongamano kwamba Vijana wa kike wana nafasi Sawa na vijana wa kiume akatoa wito kwa wao kuzichangamkia fursa pale zinapojitokeza zikiwemo za uongozi ili kuendelea kuuthibitishia uma juu ya uwezo wa uwajibikaji wa mwanamke katika nyanja mbalimbali na akawataka wathubutu kwa Kila jambo Jema ili waweza kufikia Malengo makubwa .

  Katika kumjenga Kijana kiuchumi Das, Zahara aliwataka vijana kuchangamkia fedha zitolewazo na serikali katika kuwawezesha vijana wajasiliamali kujikwamua kiuchumi fedha Ambazo hazina riba ,,alisisitiza vijana kujiunga kwenye vikundi na kuvisajili kisha kuanzisha shughuli ya pamoja ili vigezo vya kukopesheka vitimie,Pamoja na Mambo mengine Das Zahara aliwataka vijana kuendelea kumuunga mkono kwa vitendo Rais John Pombe Magufuli, Rais ambaye amefata fikra sahihi za Hayati Baba wa Taifa katika kuijenga Tanzania yenye haki na usawa kwa watu wote 

  #UVCCM TABORA MJINI #
  Tunakushukuru sana Mh Zahara Michuzi kwanza kwa kufika katika kongamano na kutoa mada Nzuri iliosheheni mafunzo kwa vijana wenzio, lakini pia Hamasa za kutimiza ndoto na Malengo Hasa kwa mtoto wa kike

  0 0  Msanii wa Bongofleva Barnaba akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana mjini Sumbawanga
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Joriii akiitawala jukwaa la Tigo Fiesta 2019 Mjini Sumbawanga usiku wa kuamkia laeo
  Msanii wa Bongofleva Barnaba akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana mjini Sumbawanga

   

  Msanii wa bongoflava Jay Melody akiwa jukwaani katika tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo mjini Sumbawanga
  Msanii Badest akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta sumbawanga jana
  Mtangazaji wa kipindi cha Double XXL kinachorushwa na radio ya crouds fm ambaye alikuwa moja washereheshaji katika tamasha la Tigo Fiesta Sumbawanga akiwa na wapenzi wa kipndi hicho kutoka Sumbawanga
  Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dr Alfani Haule akiburudika na mziki katika jukwaa la Tigo Fiesta.
  Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dr Alfani Haule akiwa na mtangazaji wa Double XXL katika jukwaa la Tigo Fiesta mwisho wa wiki .
  Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akimtambulisha mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini mh Aeshi Hilaly na kuchemza muziki jukwaani usiku wa kuamkia leo Sumbawanga
  Mbunge wa Sumbawanga mjini akiongea na wananchi walio hudhulia kwenye tamasha la Tigo Fiesta jana Sumbawanga.
  Msanii Marioo akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo Fiesta jana Sumbawanga
  Msanii wa muziki wa injili Goodluck Gozbeth akitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta jana Sumbawanga
  Msanii wa bongo fleva Joh Makini akiwa jukwaani akitumbuiza kwenye Tigo Fiest 2019 sumbawanga usiku wa kuamkia leo
  Msanii Mr Blue akitumbuIza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo Sumbawanga
  Maelfu ya wapenda burudani wa mkoa wa Rukwa na Mikoa ya karibu wakifurahia burudani mbali mbali zinazotolewa katika jukwaa la Tigo Fiesta saizi yako Mjini Sumbawanga

  0 0

  Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wameilazimisha suluhu  ya 0-0 timu ya Taifa ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo Nchini Rwanda.

  Mchezo huo wa Kirafiki wa Kalenda ya FIFA ulizikutanisha timu hizo Ambapo kila mmoja kushindwa kuona lango la mwenzake.Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa, timu zote mbili zikisaka ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya viwango vya FIFA.

  Rwanda waliokuwa nyumbani, walionesha uhai mkubwa katika kulisakama lango la Tanzania ila umahiri wa golikipa Metacha Mnata uliweza kuhakikisha lango lake linakuwa salama.

  Uwepo wa wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika safu ya ushambuliaji ya Rwanda ulikua ni mwiba mkali, ila mpaka dakika tisini zimekamilika kwa timu zote kutoka sare ya 0-0.

  Wachezaji hao Meddie Kagere, Patrick Sibomana na Haruna Niyonzima ambaye kwa sasa anacheza As Kigali ambapo kabla ya kwenda huko alicheza timu ya Yanga na Simba.Kocha msaidizi wa Stars, Seleman Matola amesema kuwa wachezaji walipambana kupata matokeo ila bahati haikuwa yao.

  Matola amesema wachezaji wake walicheza vizuri katika dakika zote 90 wameonesha kiwango kizuri, ila mpira una matokeo matatu kupata sare sio jambo baya ila kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya mchezo wa Sudan wa kufuzu kwenda CHAN.

  Stars watashuka tena dimbani kucheza dhidi ya Sudan mchezo unaotarajiwa kuwa wa kufa na kupona ambapo Tanzania wanatakiwa wapate ushindi wa goli 2-0 ugenini baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kupoteza kwa goli 1-0.

  0 0

  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo (mwenye suti) ambaye alikuwa mgeni maalum akiungana na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) kuonyesha katiba ya umoja wao mara baada ya kufanya uzinduzi  wa umoja huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia pembeni ni wanachama wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi. Frida Kundy (wa pili toka kushoto). Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo (wa kwanza kulia) ambaye alikuwa mgeni maalum akisoma katiba kabla ya kukata utepe ikiwa ishara ya kuzindua Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia pembeni ni wanachama wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi. Frida Kundy (wa pili toka kwa mgeni maalum).
  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo (wa kwanza kulia) ambaye alikuwa mgeni maalum akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia pembeni ni wanachama wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi. Frida Kundy (wa pili toka kwa mgeni maalum).
  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) wakati wa hafla ya kuzindua Umoja huo iliofanyika katika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa UWAMITA Bi. Frida Kundy na kutoka kushoto ni Bi. Lilian Patrick na Mama mstaafu Bi. Gladness Mkamba.
  Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) wakimsikiliza mgeni maalum wakati wa hafla ya kuzindua Umoja huo iliofanyika katika jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akionyesha katiba ya Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) mara baada ya kuzindua umoja huo, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa UWAMITA Bi. Frida Kundy na kushoto ni Mama mstaafu Bi. Gladness Mkamba.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) Bi. Frida Kundy akizungumza na wanachama wa Umoja huo wakati wa sherehe ya uzinduzi iliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Akina mama wastaafu waliokuwa wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakipiga makofi ambapo mbali na uzinduzi huo, akina mama hao waliagwa rasmi.
  Mama mstaafu Bi. Gladness Mkamba akitoa nasaha zake.
  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akigongeana glasi (Cheers) na viongozi wa UWAMITA na akinamama waliostaafu ikiwa ishara ya upendo hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akiongoza zoezi la ukataji keki na viongozi wa UWAMITA na akinamama waliostaafu ikiwa ishara ya upendo hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akilishwa keki na mmoja akinamama waliostaafu ikiwa ishara ya upendo hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo ambaye alikuwa mgeni maalum akiwagawia keshi akinamama waliostaafu ikiwa ishara ya upendo hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) Bi. Frida Kundy akicheza muziki na akinamama waliostaafu wakati wa sherehe ya uzinduzi iliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo akiburudika na akina mama ambao ni wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (UWAMITA) mara baada ya umoja huo kuzinduliwa. Kamishna Mhifadhi Misitu Prof. Dos Santos Silayo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa UWAMITA pamoja na akina mama waliostaafu wakati wa sherehe ya uzinduzi iliofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanachama wa UWAMITA wakifurahi katika picha ya pamoja.
  Wanachama wa UWAMITA na viongozi wao wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

  0 0

  BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imetoa wito kwa wazazi kote nchini kufungua akaunti maalumu ya watoto ya Chanua pamoja na bima ya elimu ya Educare za benki hiyo ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao pindi wawapo hai ama wasipokuwepo.

  Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo,  Benjamin Nkaka katika hafla waliyoiandaa kwa ajili ya watoto wa wateja wao ikiwa ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha Mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC.

  Mkurugenzi huyo alisema akaunti ya watoto ya Chanua ya NBC pamoja na bima ya elimu ya educare vitamuwezesha mzazi kuanza kuwekeza kidogodogo kwa ajili ya mtoto wake hivyo kuondoa hofu ya watoto kupata elimu  bora pindi  mzazi  anapoondoka duniani.

  “Akaunti ya Chanua na bima ya Educare za NBC ni suluhisho la uhakika kwa elimu ya watoto, wakati mzazi awapo duniani,asipokuwepo au atakapotapa ulemavu wa kudumu, nawashauri wazazi kuwafungulia watoto wenu akaunti hii na kuanza kuwekeza pamoja na bima ya educare zote kutoka NBC,” alisema.

  Kuhusu hafla hiyo Bwana Nkaka alisema NBC imekuwa na desturi ya kukutana na wateja wao mara kwa mara ikiwa ni moja ya azma yao ya kusogeza huduma zao karibu na wateja wao hivyo licha ya kuwaeleza watoto  walioambata na wazazi wao bidhaa mbalimbali zinazotolewa na benki hususan zinazowalenga watoto, lakini pia watoto walishiriki burudani za aina mbalimbali jambo ambalo ni muhimu katika malezi ya watoto.

  “NBC imekuwa ikibadilika siku hadi siku tukitumia njia mbalimbali katika kuwafikia wateja wetu, licha ya kuwa na mtandao mpana wa matawi lakini pia tumeanzisha NBC Kiganjani inayomuwezesha mteja kupata huduma mbalimbali za kibenki kwa kupitia simu yake ya mkononi.

  “Lakini hii haitoshi NBC inao mtandao mkubwa wa mawakala wake wakitoa huduma mbalimbali za kibenki nchini kote, lakini hivi karibuni tumeingia ushirika na Shirika la Posta ambapo wateja wetu wanaweza kupata huduma zetu za kibenki katika ofisi zote za shirika hilo mahali kote nchini,” aliongeza mkurugenzi hiuyo.

   Ofisa Malipo ya Ndani wa NBC, Suzyo Gwebe Nyirenda akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
   Meneja Huduma Bora wa NBC, Jane Dogani akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
   Baadhi ya watoto waliohudhuria katika hafla hiyo wakichorwa picha ikiwa ni sehemu ya shamra shamra zilizokuwepo katika kuadhimisha moja ya matukio ya mwezi wa huduma kwa wateja ambapo NBC iliandaa sherehe hiyo kwa watoto wa wateja wao.
   Baadhi ya watoto walihudhuria hafla hiyo wakifurahia burudani mbalimbali zilizokuwepo katika siku hiyo ikiwa ni moja ya matukio ya NBC kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja.
    Meneja Huduma Bora wa NBC, Jane Dogani akiwawekea chakula baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
   Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki ya NBC, Benjamin Nkaka akizungumza na watoto wa wateja wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi kuhusu umuhimu wa wazazi kuwafungulioa watoto wao akaunti ya Chanua na pia bima ya elimu ya educare ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao wakati wawapo hai ama wasipokuwepo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.


  0 0


  Baadhi ya watumishi wa Idara ya uhamiaji ,Wahifadhi pamoja na watumishi wa Mega Group wakiwa kwenye eneo la hifadhi ya Tarangire wakati walipotembelea hifadhi hiyo kuhamasisha utalii wa ndani


  Na Vero Ignatus,Arusha.

  Katika kuhamasisha utalii wa ndani nchini Idara ya Uhamiaji mkoa wa Arusha imeshiriki kutembelea hifadhi hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambapo wamejionea vivutio mbalimbali ikiwemo makundi makubwa ya tembo,twiga,pundamilia na vivutio vingine.

  Naibu Kamishna Abdallah Towo ni Afisa wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, amesema kuwa wameamua kutembelea hifadhi ikiwa ni moja kati ya njia za kuhamasisha Taasisi nyingine za serikali kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi wakiwa na wafanyakazi wao lengo ikiwa ni kuhimiza ufanisi kazini na kujenga mahusiano bora kazini.

  Issa Mlweta ni Mrakibu wa Uhamiaji amesema kuwa Uhamiaji ni wadau wakubwa wa utalii kwani wanawakaribisha watalii wanapoingia na kutoka katika mipaka ikiwa ni pamoja na kuhamasisha utalii na kutangaza vivutio muhimu tulivyonavyo.

  Harieli Msaki ni Mhifadhi Mwandamizi Ujirani Mwema hifadhi ya Tarangire ,amesema kuwa hifadhi hiyo inatembelewa na watalii laki moja kila mwaka kutoka nchi za nje huku utalii wa ndani ukiwa chini hivyo ameipongeza uhamiaji na kuzitaka Taasisi nyingine ziige mfano wake.

  Hikloch Ogola ni Mkurugenzi wa tafiti na Maendeleo kutoka Mega Media Group ,ambao ni waandaaji wa ziara hiyo amesema kuwa wameanzisha program maalumu ya kuhamasisha taasisi za umma na binafsi kutembelea vivutio vya utalii ili kuinua mapato ya utalii wa ndani na vile vile kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii..

  Utalii ni moja kati ya sekta ambazo zinaongoza kwa kuliingizia taifa fedha za geni na kuchangia kiasi cha asilimia 17% katika pato la taifa hivyo juhudi endelevu zinahitajika katika kuhamasisha utalii wa ndani.

  0 0


  Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akipata maelezo ya Ntambo Mahinya mtaalamu wa kupika chakula cha asili kutoka Mbeya alipotembelea banda la vyakula hivyo kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Singida.


  Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa kilimo alipotembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Singida.

  Dkt. Tulia akipata maelezo jinsi mashine ya kuchakata viazi lishe inavyofanya kazi katika banda la TARI. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Pasacas Muragiri.
  Afisa Kilimo Robert Dimoso Idara ya Usalama wa Chakula Wizara ya Kilimo akimuelezea Dkt.Tulia shughuli zinazofanywa na Idara hiyo.
  Mratibu wa Mradi wa Tanipac Wizara ya Kilimo, Clepin Josephat akimurleza Dkt.Tulia Ackson shughuli wanazozifanya.
  Dkt. Tulia akipata maelezo ya kilimo cha mapapai.


  Afisa Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mary Yongolo akimpatia zawadi ya maziwa Dkt.Tulia Ackson baada ya kutembelea banda la wizara hiyo.
  Afisa Lishe Mkoa wa Singida, Teda Sinde akimuelekeza Dkt.Tulia Ackson jinsi ya kupika vyakula vya asili ambavyi ni muhimu katika kuboresha lishe. Kushoto ni Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Federick Ndahani.
  Dkt.Tulia akipakua chakula cha asili alipotembelea banda la vyakula hivyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi akila chakula cha asili kilichotengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)

  0 0

  BENKI ya NBC imeendelea kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja kwa kufanya matukio sehemu mbalimbali nchini na hapo jijini Dar es Salaam ikitoa elimu kuhusu umuhimu wa bima na pia ikiwaleleza wateja aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na benki hiyo.

  Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Kitengo cha Bima wa NBC, Benjamin Nkaka alisema watanzania wanapaswa kuwa utamaduni wa kujiwekea bima wao pamoja na watoto wao dhidi ya matukio na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza wakati wowote.

  Akitoa mfano wa bima hizo ni bima ya elimu ya Educare itolewayo na inayomuwezesha mzazi kuweka akiba kidogokidogo kwa ajili ya elimu ya mtoto wake pindi yatokeapo majanga yanayoweza kusababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.

  “Tumekwishakuwa na huduma hii, tunachotaka sasa ni kwa wateja kuweza kuielewa vivuri, na ndio maana tumendaa hafla kama hii ili kuwafahamisha wateja wetu na wananchi kwa ujumla huduma ya bima ya elimu ya NBC inavyoweza kumkomboa mteja,” alisema.

  Alisema kwa kupitia huduma hii mteja humwekea akiba mtoto wake kidogokidogo kwa kiasi atakachopanga kwa mkataba wa muda kuanzia miaka saba hadi 18 ili kugharamia elimu ya mtoto wake.

  “Bima hii ya elimu ni mpango ambao mzazi huweka akiba kila mwezi hivyo kuleta faraja moyoni kwamba endapo chochote kitatokea iwe ulemavu wa kudumu ama kifo kabla ya muda huo basi bia itagharamia elimu ya mtoto wako.

  “Kiwango cha chini ni miaka saba hadi 18 na kiwango cha chini cha kuwekeza katika mpango huu kwa mwezi ni shs 7,500/- hakuna kiwango cha mwisho cha juu. Uwekezeji katika elimu ya mtoto ni jambo pekee katika kuhakikisha malengo ya kielimu ya mtoto yanatimia ,” aliongeza Bwana Nkaka.
   Ofisa wa Bima wa Benki ya NBC, Catherine Ngowi (kulia) akitoa elimu ya masuala ya bima n aina mbalimbali ya huduma za  bima zitolewazo na  NBC kwa ammoja wa wateja wa benki hiyo,  Miryam Mjema ikiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bima wa benki hiyo, Benjamin Nkaka na ofisa mwingine wa NBC,  Batuli Kassim. 
   Ofisa wa Bima wa benki ya NBC, Emarynziana Mtega (kulia), akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kujiwekea bima na aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na NBC kwa mmoja wa wateja  wa benki hiyo kutoka Kampuni ya Mogas Tanzania Ltd, Grayson Kazeni kiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam hivi karibuni.
   Maofisa wa benki ya NBC, wakizungumza na wateja wakati wakitoa elimu kuhusu masuala ya bima kwa wateja ikiwa ni moja ya matukio ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
  Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo. Wafanyakazi hao walitoa elimu ya bima ikiwa ni pamoja na bidhaa mbalimbali za bima zitolewazo na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC.  0 0

  Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini-Lilian Mwalongo Akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo iliyofanyika jana viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.Pembeni yake ni Mtaalamu wa huduma za Kidigitali wa Tigo,Fabian Felician.
  Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo akifungua mlango wa gari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Tigo Fiesta 2019 Chemsha bongo iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma jana. 
  Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini , Lilian Mwalongo akijaribu kuwasha gari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo iliyofanyika jana viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.   Wateja kushinda zawadi mbalimbali pamoja na gari aina ya Renault Kwid yenye thamani ya Sh23 milioni. 


  Dodoma.Oktoba 15 2019. Kampuni inayolenga kuleta mageuzi ya kidigitali katika maisha ya watanzania, Tigo, leo imetangaza promosheni kabambe ijulikanayo kama Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo jijini Dodoma.Promosheni hiyo inaenda sambamba na msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako ambayo ilizinduliwa jijini Mwanza na itamalizika jijini Dar es Salaam. 

  Wateja wa Tigo wanaoshiriki katika promosheni ya Tigo Fiesta 2019 Chemsha Bongo kwa mara ya kwanza wana nafasi ya kushinda hadi Sh1 milioni kila wiki huku mshindi wa jumla ataweza kujinyakulia gari mpya aina ya Renault Kwid yenye thamani ya Sh23 milioni. 

  Washindi wa promosheni hiyo hutangazwa kila wiki na ili kushiriki kwenye promosheni hiyo, wateja wanatakiwa kujisajili kwa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kwakutembelea tovuti www.tigomusic.co.tz nakuchagua neno ‘Trivia’. 

  Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Lilian Mwalongo alisema “Shindano hili ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kujumuika na kuungana na wateja wetu kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wa aina zote hapa nchini.” 

  Aidha, Mwalongo aliwajulisha wateja wa Tigo watakaoshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako jijini Dodoma kwamba wanaweza kulipia tiketi kwa njia ya Tigo Pesa kwa Sh5,000/= au pesa taslimu kwa Sh7,000. 

  “Kama kampuni inayolenga kuchochea matumizi ya digitali, tumejizatiti kutoa huduma zenye kukidhi mahitaji ya wateja kila siku.Ili kununua tiketi kupitia Tigo Pesa mteja anatakiwa kufuata hatua za kawaida za kutuma pesa na kutuma Sh 8,000/= kwenda namba 0678 888 888 na watapokea ujumbe wa kuthibitisha malipo ya tiketi,” alisema. 

  Pia, aliwahimiza wateja wa Tigo walioko Dodoma kusajili upya namba zao za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole hasa wakati wa msimu huu wa Tigo Fiesta kabla ya mwezi Desemba. 

  Zoezi la kusajili namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole linalenga kudhibiti matumizi mabaya ya huduma za mawasilaino na pia kuwawezesha wateja kutambulika ili kupata hudma zenye usalama zaidi ikiwamo huduma za kifedha pamoja na malipo ya huduma kama maji, umeme pamoja na televisheni.

  0 0

  0 0
  0 0


  BENKI ya NMB imezindua malipo ya kimtandao kwa huduma za bodaboda ambapo mfumo huo wa malipo ni wa aina yake na wa kwanza nchini Tanzania ambao unawawezesha abiria na wateja wa bodaboda kulipa nauli zao kwa kutumia simu zao za mkononi na fedha hizo kwenda moja kwa moja kwenye akaunti ya NMB ya dereva husika.

  Kwa mujibu wa benki hiyo huduma hiyo iliyozinduliwa jana ni mwendelezo wa juhudi za kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanatumia huduma za benki sambamba na kuhamasisha utunzaji fedha kwa njia salama na za uhakika.

  Akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema kuwa huduma hiyo inaweka msingi wa kurasimisha sekta ndogo ya usafiri wa bodaboda.

  "Mnachokifanya leo kina baraka zote za Serikali. Hiki kitawasaidia vijana kuongeza umakini kwenye shughuli zao na kuchangia uchumi wa Taifa," amesema Mhagama.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema huduma hiyo inatoa fursa kwa maelfu ya madereva wa bodaboda nchini kutumia huduma za benki hatua ambayo itaimarisha usalama wa fedha zao pamoja na wao wenyewe.

  “Hii ni namna bora zaidi ya kurudisha uwajibikaji kwa shughuli za madereva wa bodaboda ambao mchango wao kwenye uchumi wa Taifa unatambulika,"amesema na  kuongeza huduma hiyo itaanza kwa Jiji la  Dar es Salaam kisha itaenda Mwanza, Arusha, Ruvuma, Dodoma na Mbeya wiki chache zijazo.

   Zaipuna ameongeza kuwa mfumo huo wa malipo utawasaidia madereva bodaboda kukuza biashara zao kwa kuwapunguzia adha ya kuhifadhi fedha taslimu na kuwapa fursa ya kuepuka matumizi yasiyokuwa na mpangilio.

  “Kwa kutumia MasterCard QR, tunatoa huduma ya uhakika wa malipo kwa madereva bodaboda kutoka kwa watoa huduma wote na benki za biashara wanaotumia huduma hii.

  " Malipo yatafanywa kwa kutumia simu ya mkononi yenye programu ya MasterCard QR na kupunguza hatari za kumiliki fedha taslimu. Huduma hii kwa bodaboda ni sehemu ya mkakati wa benki kufikisha huduma zake kwa watu wengi zaidi,” amesema Zaipuna .

  Wakati huo huo Mwakilishi wa MasterCard Tanzania  Frank Molla amesema mfumo huo wa malipo ya kidijiti unakusudia kuwapa uhuru dereva na abiria wake wakati wote wa safari huku ukimuepushia dereva uwezekano wa kuporwa au kupoteza fedha zake.

  “MasterCard inakusudia kuhamasisha na kuwezesha malipo ya kidijiti hapa nchini. Benki ya NMB inayo dira inayofanana nasi katika ujenzi wa miundombinu itakayoiwezesha jamii kufurahia ulimwengu wa malipo ya kimtandao kwa kutumia teknolojia ya kisasa,” amesema.

  Tayari Benki ya NMB imewajengea uwezo zaidi ya madereva 1,000 wa jinsi ya kutumia QR kufanikisha malipo kwa kutumia simu za mkononi. Mfumo huo unatarajiwa kuongeza usalama wa malipo ya kimtandao kwa sekta hiyo ndogo ya watoa huduma.

  Kumlipa bodaboda, abiria anatakiwa kwenda kwenye simu yako – NMB Mkononi, piga *150*66# kupata menu na kuchagua kufanya malipo halafu ‘Scan to Pay.’ Pia ukiwa na simu janja nenda kwenye programu (App) ya NMB Mkonini ambako atachagua ‘Scan to Pay’ na kuendelea na maelekezo.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiwa kwenye boda boda baada ya kuzindua Mastaboda ambao ni mpango maalum wa benki ya NMB kwa kushirikiana na Mastercard ambao utawawezesha waendesha boda boda kukopa piki piki ,wengine ni kaimu Mkurugenzi mtendaji wa NMB Ruth Zaipuna,Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma makao Makuu ya Usalama Barabarani ,Mrakibu wa Polisi Abel Swai.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiwa kwenye boda boda baada ya kuzindua Mastaboda ambao ni mpango maalum wa benki ya NMB kwa kushirikiana na Mastercard ambao utawawezesha waendesha boda boda kukopa piki piki ,wengine ni kaimu Mkurugenzi mtendaji wa NMB Ruth Zaipuna,Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma makao Makuu ya Usalama Barabarani ,Mrakibu wa Polisi Abel Swai.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza mbele ya wageni waalikwa na Waendesha piki piki kutoka sehemu mbalimbali ndani ya jiji la Dar,kabla ya kuzindua huduma ya Mastaboda,jana jijini Dar.Huduma hiyo ni maalum kwa  waendesha boda boda.
  Mgeni rasmi (wanne kushoto) ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akiongoza uzinduzi wa huduma hiyo ya Mastaboda,jana jijini Dar.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna  akimshukuru Mgeni rasmi ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama  mara baada ya tukio la uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna akifafanua jambo mbele ya Waendesha piki piki (hawapo pichani),kuhusu huduma ya Mastaboda,alisema kuwa huduma hiyo inatoa fursa kwa maelfu ya madereva wa bodaboda nchini kutumia huduma za benki, hatua ambayo itaimarisha usalama wa fedha zao pamoja na wao wenyewe.
  Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa hudma hiyo ya Mastaoda.

  0 0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James na Kaimu Balozi Bw. Jorg Herrera Wakionesha nakala za Mikataba ya Msaada baada ya kutia saini .Hafla hiyo fupi ilifanyika jana katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akisaini Mkataba wa Msaada wa Shilingi Bilioni 20 Kati yake na Kaimu Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bw.Jorg Herrera, Hafla hiyo fupi ilifanyika jana katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James na akimpa mkono wa shukurani Kaimu Balozi Bw. Jorg Herrera mara baada ya kutia saini mikataba hiyo,hafla hiyo fupi ilifanyika jana katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam. Wakifurahi kwa pamoja mara baada ya shughuli hiyo kuisha


  ………………………….

  Na.Mwandishi Wetu –MAELEZO.

  Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani limetoa msaada wa Euro milioni 8 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 20 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwaajili ya kuboresha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mfuko wa Bima ya Afya nchini NHIF.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini wa msaada huo, Kaimu Balozi wa Ujerumani nchini Bw.Jorg Herrera amesema msaada huo ni kwaajili ya kuimarisha mfuko wa Bima ya Afya ili uweze kuwahudumia watanzania wengi zaidi hasa wale wa vijijini.

  Amesema lengo la Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani ni kuisaidia Serikali ya Tanzania katika azma yake ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama wa mfuko wa Bima ya Afya ili hatimaye kufikia lengo la kutoa huduma ya Afya kwa wote .

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Doto James amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya Awamu ya Tano inajitahidi kuboresha huduma za Afya kwa wananchi wake ili waweze kufanya kazi kwaajili ya kuelekea Tanzania ya Viwanda.

  “Msaada huu ni wa masharti nafuu kabisa na hatulazimiki kulipa fedha yoyote, na sisi kama Serikali tumeupitia na kujiridhisha kwamba hauna chembe yoyote ya masharti ndio maana leo hii tumetoka hadharani kusaini ” Alisema.

  Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Fedha alisema msaada wowote ambao serikali inapatiwa hupitiwa na wataalam makini ambao wanahakikisha hakuna masharti ambayo yatakuja kusumbua baadaye na pia ni kwa kuzingatia Sheria na Katiba ya nchi.Pia amesema kwa upande wa Ujerumani wamekuwa marafiki wazuri sana ambao mara kwa mara wameendelea kuisidia Serikali katika masuala mbalimbali ya maendeleo.

  Aidha Bw. James amesema uimarishaji wa mfumo wa TEHAMA katika mfuko wa Bima ya Afya una manufaa makubwa ikiwemo,kuongeza usajili wa wanachama wa bima ya Afya ikiwajumuisha walioko kwenye sekta isiyo rasmi pia kuboresha namna ya kuwatambua ,kuwasajili na kuwalipa watoa huduma.

  Faida nyingine ni kuboresha utendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa kuongeza matumizi ya TEHAMA katika shughuli zake za kila siku pamoja na kuwajengea uwezo wa watumishi wa mfuko wa Bima ya Afya.

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeazimia kutoa huduma za Afya kwa wote na ili kufikia lengo hili, kuna mpango wa kuwa na mfuko mmoja wa Bima ya Afya utakaojulikana kama “Single Health Insurance Fund” (SNHIF) ambapo itakuwa ni lazima kila mtanzania kujiunga.

  Serikali ya ujerumani siyo mara ya kwanza kuisaidia Tanzania, kwani imekuwa ikisaidia katika sekta za Maji, Nishati,Uhifadhi wa maliasili,Usimamizi wa fedha za umma pamoja na kuijengea uwezo Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

  Hivi karibuni Serikali ya Tanzania imeshuhudia mashirika ya kimataifa nchi mbalimbali pamoja na wahisani wakiendelea kumimina misaada kwaajili ya shughuli za maendeleo kutokana na uongozi wa Rais Dkt.John Magufuli , ambao umejitahidi kupambana na ufisadi na kusimamia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wengi.

  0 0

  Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil Richard Fielden-Watkinson akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyojipanga kuwahudumia watoto wataojiunga kwenye kozi za taasisi hiyo wakati wa Taasisi hiyo ilipokuwa inatangaza siku ya kuanzisha kozi ya lugha ya kingereza kwa watoto na kuwajengea uwezo na kujiamini iliyofanyika katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja na Mauzowa British Council, Benard Mosha.
   Meneja wa Huduma kwa wateja na Mauzowa British Council, Benard Mosha akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kuwaondoa wananchi hofu kuhusu malipo ya kozi zitolewazo na Shirika hilo wakati wa kutangaza siku ya uzinduzi wa mafunzo ya kiingereza kw watoto kuanzia miaka 6 hadi 11. Wa kwanza kushoto ni  Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil Richard Fielden-Watkinson  na katikati ni  Mkuu wa kitengo cha Ufundishaji cha British Council Tanzania, Doris Ndewa Likwelile.
  Mkuu wa kitengo cha Ufundishaji cha taasisi ya kimataifa ya British Council , Doris Likwelile akizungumza na waandhi wa habari kuhusu taasisi hiyo kuanzisha kozi ya lugha ya kingereza kwa watoto na kuwajengea uwezo na kujiamini iliyofanyika katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil Richard Fielden-Watkinson.

  KATIKA kukabiliana na changamoto ya watu wengi kutokuwa na ujasiri wa kujieleza mbele za watu taasisi ya kimataifa ya British Council imeanzisha kozi ya lugha ya kingereza kwa watoto na kuwajengea uwezo na kujiamini.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha ufundishaji wa taasisi ya kimataifa ya British Council, Doris Likwelile jijini Dar Es Slaam leo, amesema kuwa programu kwaajili ya watoto itazinduliwa Jumamosi ya Oktoba 19,2019.

  "Kwa mara ya kwanza  kabisa tunaanza kuwa na kozi za kingereza kwa watoto lakini hii kozi itakuwa zaidi kwa mtoto kujifunza kingereza". Amesema Doris

  Amesema kuwa ni jambo nzuri kuanzisha kozi hiyo kwa watoto wa kuanzia miaka sita hadi 11 kwani kwa mara ya kwanza itaanza kutolewa hapa nchini ikiwa  taasisi hiyo ilishaenea kwenye nchi zaidi ya 65 duniani kote.

  "Mtoto zaidi ya kujifunza Kingereza  mtoto ataongezewa ujuzi ambao unahitajika kwa karne hii ya sasa ya 21 kwa kufanya mawasiliano pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano na kuwa na mawazo mapana,na kuwawezesha kuwa na ujasiri na kuwa wabunifu". Amesema Doris


  Nae Meneja wa Huduma ya wateja na mauzo wa Taasisi ya kimataifa ya British Council, Bernard Mosha, amesema kuwa kozi hiyo kwa watoto itakuwa gharama nafuu na mtihani kwaajili ya kiwango utafanyika bila gharama yoyote yaani ni bure kabisa.

  "Naomba niwaondoe wasiwasi wazazi kuhusiana na bei zetu kwani wanawezakufikiri kuwa bei zetu zinaweza kuwa za kimataifa hii ni hapana bei zetu zitakuwa za kawaida kwani tumefanya utafiti na kugundua kuwa wazazi kiwango cha uchumi cha wastani kwahiyo gharaama za kozi hii kwa mtoto itakuwa ni nafuu.

  Pia amewaomba mzazi au mlezi kumpele mwanaye katika taasisi hiyo ili mtoto aweze kufanya mtihani wa kiwango kwaajili ya kuweza kujua kiwango chake na kuangalia namna ambavyo wanaweza kumfundish kwa ufasaha zaidi.

  Kwa Upande wa Usalama wa watoto Mosha amewaondoa wasiswasi wazazi kwani ni sehemu salama kwa watoto.

  Hata hivyo Meneja taaluma wa Taasisi ya British Cancil,Richard Watkinson amesema kuwa wazazi wawapeleke watoto wakafundishwe lugha ya Kingereza na waingereza wenyewe.
  Amesema kuzi hiyo itakuwa na awamu tatu ambapo mtoto atasoma wakati yupo likizo.

  0 0


  Wananchi wakisoma vitabu vya muongozo wa TCRA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nyehunge Sengerema.
  Mhandisi Francis Mihayo akizungumza na wananchi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika katika Viwanja vya Nyehunge Sengerema.

  Wananchi wakipata huduma ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa katika Viwanja Nyahunge.

  0 0

  Mgeni rasmi mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Tabora, Katibu Tawala msaidizi anayeshughulikia Utawala, Hamisi Mkunga akizungumza na wananchi katika hafla ya uzinduzi wa duka la Vodacom mjini Tabora.
  Mgeni rasmi mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Tabora, Katibu Tawala msaidizi anayeshughulikia Utawala, Hamisi Mkunga akipata maelezo toka kwa wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom ndani ya duka
  Baadhi ya wateja wa kampuni ya Vodacom wakiendelea kupata huduma ndani ya duka jipya lililoko mjini Tabora
  Baadhi ya watumishi wa duka la Vodacom lililopo mjini Tabora wakifungua champagne wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
  Baadhi ya Watumishi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wakiwa katika maandamano ya amani wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom mjini Tabora

  0 0

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na wazazi waliofika kwenye uzinduzi wa chanjo iliyofanyika kwenye viwanja vya jamhuri mkoani morogoro
  Muuguzi Tumaini Majoji.kutoka kituo cha afya Uhuru akimpatia chanjo mmoja wa mtoto aliyepelekwa kwenye uzinduzi huo ambapo chanjo hiyo itatolewa kwa siku tano kwa watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miaka mitano 
  .Waziri Ummy Mwalimu akihutubia wakazi wa Morogogo(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa kampeni shirikishi ya chanjo 
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Lowata Olesanare akiongea na wananchi walofika kiwanjani hapo 
  Waziri.Ummy Mwalimu akiongea na mmoja wa mzazi ambaye alipeleka watoto wake mapacha kupatiwa chanjo kwenye uzinduzi huoMwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) nchini Tanzania Dkt.Tigest Mengestu akizungumza kwenye uzinduzi huo.
  Muuguzi Tumaini Majoji akichanganya dawa wakati wa zoezi hilo


  *******************

  Na. Catherine Sungura-Morogoro


  Inakadiriwa watoto wapatao 8,028,838 wenye umri wa miezi tisa hadi umri wa chini ya miaka mitano (miezi 59) wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Surua-Rubella kwenye kampeni shirikishi ya chanjo itakayotolewa nchi nzima.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoro Ummy Mwalimu wakati akizindua kampeni hiyo iliyofanyika kitaifa mkoani hapa.

  “Kampeni hii inaanza leo na itamalizika tarehe 21 mwezi huu na itatolewa bila malipo tanzania bara na itaendeshwa katika vituo vya kutolea huduma za afya na vituo maalam vitakavyoundwa na kubainishwa na halmashauri katika kipindi hiki ili kusogeza huduma karibu na walengwa”. Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

  Aidha, kwa upande wa kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na nusu, Waziri huyo alisema inakadiriwa kuwa watoto 4,041,934 watapata chanjo hiyo.

  “Lengo kuu ni kushiriki katika mkakati wa kitaifa wa kutokomeza ugonjwa wa surua na rubella ili kuchangia katika kupunguza vifo vya watoto hapa nchi,Zoezi hili la kampeni linatarajiwa kugharimu takribani shilingi za kitanzania billion 11.9 sawa na dola za kimarekani milioni 4.59”.

  Hata hivyo alisema kuwa chanjo hupunguza gharama kubwa ambazo familia na taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu magonjwa yanayozuilika kwa chanjo“kuna faida kubwa katika uchumi wa taifa tunapowekeza kwenye chanjo,kwani imethibitishwa kwamba kila dola moja unawekeza kwenye chanjo unapata faida ya dola kumi na sita”.

  Naye Mwakili Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Mengestu alisema kuwa Tanzania inatoa chanjo hii kwa asilimia 95 na hivyo kampeni hii inasaidia kuimarisha afya za watoto nchini na kuwakinga na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

  0 0

  Na Eva Valerian na Ramadhani Kissimba, Washington DC

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kupata dola za Marekani Milioni 150 kutoka Benki ya Dunia-WB zitakazotumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya kukuza Utalii na kustawisha miji katika visiwa hivyo.

  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Khamis Omar alisema Jijini Washington DC kuwa Benki ya Dunia imekuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na misaada mbalimbali wanayoitoa katika kutekeleza miradi yao ya maendeleo.

  Bw. Omar alisema Benki hiyo imesaidia kufadhili ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara zinazoingia mijini, Uwanja wa Ndege wa Zanzibar pamoja na bandari. 

  Aidha, alisema Benki hiyo imesaidia zaidi katika ujenzi wa Uwanja wa ndege, kwa kujenga sehemu ya maegesho ya ndege, njia ya kutua na kurukia ndege na njia ambazo ndege zinapita kabla ya kuingia kwenye sehemu ya kurukia (runway). 

  “Pia Benki hii imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya Elimu Visiwani Zanzibar ukiwemo mradi wa kukuza matokeo na kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika shule za Zanzibar” alisema Bw. Omar

  Alieleza kuwa kwa sasa wanatekeleza mradi mkubwa wa ustawishaji wa huduma za mijini ambao unafadhaliwa na Benki ya Dunia, na mradi huo utasaidia kuboresha huduma muhimu katika Miji ya Zanzabar ikiwa ni pamoja na kuongeza vivutio vya utalii. 

  “Mradi huu umekamilika katika awamu ya kwanza,na awamu ya pili itatekelezwa baada ya Benki hiyo kuridhia na kutoa idhini ya utekelezaji wa mradi huo ambapo idhini hiyo inatarajiwa kutolewa mwezi Aprili, 2020” alisisitiza Bw. Omar 

  Katibu Mkuu -Wizara ya Fedha na Mipango ameishukuru Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa kwa ushikiano mzuri wanaouonyesha katika kusukuma maendeleo ya Visiwani Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla. 

  Awali Waziri wa Fedha na Mipango, wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Mohamed Abdiwawa alisema lengo la kushiriki katika Mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia-WB na Shirika la Fedha la Kimataifa -IMF ni kujadiliana na vyombo hivyo vya fedha duniani kuhusu miradi inayotekelezwa kwa sasa na kuangalia mustakabali wa utekelezaji wa miradi ambayo inategemewa kutekelezwa kwa siku zijazo.
   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Khamis Omar akielezea jambo katika Mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kundi la Afrika Bi. Anne Kabagambe uliofanyika katika Ofisi za Benki ya Dunia zilizopo Washington DC. Kushoto kwa Katibu Mkuu ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mohamed Abdiwawa.
   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Khamis Omar akifafanua jambo kwa Mawaziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Mhe. Mohamed Abdiwawa wakati wa Mkutano na Viongozi wa Benki ya Dunia Jijini Washington DC.
   Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania wa Bara na Visiwani Zanzibar wakifuatilia majadiliano katika Mkutano na Viongozi kutoka Benki ya Dunia (hawapo pichani) uliofanyika Jijini Washington DC. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi na anayefuatia kulia kwa Mhe. Balozi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kundi la Afrika(Katikati) Bi. Anne Namara Kabagambe akiongea na ujumbe wa Tanzania uliohudhuria mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia -WB na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF inayofanyika Jijini Washington DC nchini Marekani.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM Washington DC)

older | 1 | .... | 1885 | 1886 | (Page 1887) | 1888 | 1889 | .... | 1897 | newer