Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

MASHINDANO YA “HASUNGA CUP 2019” YAFIKA UKOMO, WAZIRI HASUNGA APANIA SEKTA YA MICHEZO

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akimkabidhi vifaa vya michezo nahodha wa timu ya Hasamba Fc Ndg Waziri Nzunda wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisalimiana na waamuzi kadhalika wachezaji wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisalimiana na mashabiki wa mpira wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019.
Moja ya mshambuliaji wa timu ya Hasamba Fc akiwatoka wachezaji wa timu ya Ihanda Fc wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na wachezaji kabla ya mchezo wa fainali wakati wa kilele cha Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" yaliyofanyika katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe leo tarehe 29 Septemba 2019.


Na Mathias Canal, Songwe

Mashindano ya "HASUNGA CUP 2019" Leo tarehe 29 Septemba 2019 yamefika ukomo Wilayani Mbozi Mkoani Songwe ambapo timu ya Hasamba Fc ndiyo iliyoibuka kidedea na kunyakua zawadi kwa kuibamiza bila huruma timu ya Ihanda Fc kwa jumla ya Penati 7 kwa 6

Timu hiyo ya Hasamba Fc imeambulia ushindi huo wa goli 7 kwa 6 mara baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu magoli yaliyofungwa na mshambuliaji Asili Mnkondya wa timu ya Ihanda mnamo dakika ya 20 huku Beny Mgonde akiisawazishia timu yake mnamo dakika ya 72 ya mchezo huo.

Michuano hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Vwawa na kuendeshwa kwa umahiri mkubwa, ilizinduliwa mwezi Machi 2019 katika uwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe huku ikizikutanisha timu 18 zilizotokana na muunganiko wa timu za vijiji katika kata hizo 18 katika Jimbo la vwawa.

Akizungumza katika kilele cha Mashindano hayo kilichofikia ukomo katika katika viwanja wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe, Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa mashindano hayo yalianzishwa kwa lengo mahususi kwa ajili ya kubaini vipaji vya vijana kwa ajili ya kuunda timu itakayoshiriki ligi daraja la nne na hatimaye ligi kuu Tanzania bara.

Amesema kuwa mashindano hayo pia yamekuwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali ambayo yamewaimarisha vijana hususani katika kuonyesha vipaji vyao.

Katika mashindano hayo Mshindi wa kwanza ambayo ni timu ya Hasamba Fc amekabidhiwa zawadi ya Seti moja ya jezi, Seti moja ya soksi na kitita cha Shilingi laki tatu.

Mshindi wa pili timu ya Ihanda Fc imepewa zawadi seti moja ya jezi, seti moja ya soksi na kitita cha shilingi 200,000, Mshindi wa tatu yeye amekabidhiwa seti moja ya jezi na kitita cha Shilingi 100,000 huku mshindi wan ne akijinyakulia seti moja ya jezi pekee.

Katika hotuba yake Mbunge huyo wa Jimbo la Vwawa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga aliwapongeza viongozi wote na timu zote zilizoshiriki ligi hiyo kwani bila wao kusingekuwa na mafanikio yenye tija.

Mhe Hasunga aliwahakikishia wananchi kuwa mashindano hayo yatakuwa endelevu ili kutekeleza mpango mkakati wa uimarishaji na uboreshaji wa michezo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ibara ya 161.

MWISHO.

Wakulima Sikonge wanufaika na kilimo cha umwagiliaji

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Sikonge Tabora 

UBORESHAJI wa miundombnu ya umwagiliaji katika Halmashauri ya Siikonge Mkoani Tabora umeongeza uzalishaji wa zao la mpunga, hivyo kuinua kipato cha wakulima wilayani humo. 

Akizungumza na waandishi wa habari na Maafisa toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Katibu wa Chama Cha Wamwagiliaji cha Skimu ya Ulyanyama wilayani Sikonge Bw. Simon Kalosa amesema kuwa baada ya serkali kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na kutoa mafunzo ya uendeshaji na utunzaji wa skimu, uzalishaji wa mpunga umeongezeka tofauti na ilivyokuwa awali. 

Bw. Kalosa amesema kuwa wastani wa uzalishaji wa mpunga kwa sasa katika skimu ya Ulyanyama ni tani 8 kwa hecta wakati kabla ya uboreshaji wa miundombinu uzalishaji ulikuwa ni magunia sita hadi nane kwa ekari. 

Kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa mpunga katika skimu ya ulyanyama Kalosa amesema hali za maisha ya wananchi wengi zimekuwa bora na wengi wameweza kujenga nyumba za kisasa na kusomesha watoto wao. 

Kalosa amesema kuwa skimu ya ulyanyama ina jumla ya wakulima 306 ambao hujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji na wengi wao wamefaidika na uwekezaji uliofanywa na serikali katika kuboresha miundombinu ya umwagiliaji katika skimu hiyo. 

Akizungumza awali mkulima wa kilimo cha Umwagiliaji Bi. Happiness Mpunda amesema kilimo cha umwagiliaji kimebadilisha maisha yake na familia kwa ujumla kwani sasa anajitosheleza kwa chakula na kuinua kipato cha familia. 

Bi.Mpunda amesema katika msimu wa 2018/2019 ameweza kuvuna magunia 35 kwa ekari ambapo kabla ya kupata mafunzo ya matunzo bora ya mashamba alikuwa akipata gunia sita tu kwa ekari. 

” Kuna tofauti kubwa sana ya uzalishaji kabla na baada ya mafunzo ya uendelshaji na matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji, tulipokuwa tunatumia mbinu za kienyeji tulitumia nguvu nyingi sana uzalishaji kidogo wakati kwa sasa ni kinyume chake”Alisema Bi. Mpunda. 

Amesema kutokana na kilimo cha umwagiliaji ameweza kusomesha watoto watano na amenunua usafiri ambao umeweza kurahisisha mizungo ya kutafuta masoko ya mazao yake. 

Naye mwenyekiti wa Chama Cha Wamwagiliaji cha Ulyanyama Bwn. Dikson Simbila amesema kuwa ijapokuwa masoko ya mpunga wanaolima lipo ndani nan je ya Halmashauri ya Sikonge bado bei ziko chini kinyume na matarajiao yao. 

Bw. Simbila amesema ili kuongeza thamani ya mpunga wao, chama kilinunua kinu cha kukobolea mpunga ambao pia huweza kupanga madaraja mbalimbali ya mpunga tayari kwa kuuza. Kwenye masoko mbalimbali. 

Amesema kutokana na bei kuwa chini inawalazimu kusubiri hadi mwezi Disemba ili walau wapate bei nzuri ya mpunga ambapo hii huchelewesha maandalizi ya mashamba kwa ajili ya msimu unaofuatia. 

Akizungumza mapema, Mhandisi wa unwagiliaji wa mkoa wa Tabora Bwana Bahati Bulekele amesema kuwa a wake eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hecta 38,000 ambapo hekta 5,352 zimeshaendelezwa . 

Mhandisi Bulekele amesema Mkoa wa Tabora una jumla ya skimu za umwagiliaji 58 katika halmashauri mbalimbali na kati ya hizo 16 ndio zinazofanya kazi kwa kiwango cha juu. 

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ina mamlaka ya kuratibu, kuendeleza na kusimamia maendeleo ya sekta ya Umwagiliaji nchini ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali katika utekelezaji na kufanya mapitio ya sera ya Taifa ya umwagiliaji, mkakati wa maendeleo ya umwagiliaji. 

Tume pia inaratibu shughuli zote za umwagiliaji katika sekta ya umwagiliaji zinazotekelezwa na wadau wengine wa maendeleo, kuuhamasisha na kudumisha ushirikiano na taasisi za kimataifa zenye kutekeleza majukumu yanayofanana na Tume.

Bi Happiness Mpunda mkulima katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Uliyanyama akiongea kuhusu faida alizozopata kutokana na kilimo cha Umwagiliaji. 
Pichani ni ghala la kuhifadhia nafaka lililojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora. 
Katika Picha ni kinu cha kuchakata zao la mpunga kinachotumiwa na wakulima wa umoja wa wakulima wa umwagiliaji Uliyanyama Wilayani Sikonge Mkoani Tabora, ili kuweza kuongeza thamani ya mazao yao.

ZANA ZA UVUVI HARAMU ZENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.150 ZATEKETEZWA KWA MOTO

$
0
0




Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na wavuvi leo 29/9/2019 katika bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Zana zinazo tumika katika shughuli za Uvuvi Haramu zenye Thamani ya zaidi ya million 150, ikiwemo vyavu aina kokoro 56, kwa lengo la kupiga Vita Uvuvi haramu zikiteketezwa kwa Moto leo katika bwawa la Nymba ya Mungu Kilimanjaro.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akisisitiza jambo kwa wavuvi pamoja na wananchi waliojitokeza kumsikiliza leo katika eneo la Bwawa la nyumba ya Mungu Mwanga Kilimanjaro.


NA:Vero Ignatus,Mwanga Kilimanjaro.


Serikali imeteketeza kwa Moto zana zinazo tumika katika shughuli za Uvuvi Haramu zenye Thamani ya zaidi ya million 150, ikiwemo vyavu aina kokoro 56, kwa lengo la kupiga Vita Uvuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Akiwa katika Oparesheni maalumu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali itaendelea kupiga Vita Uvuvi haramu kwa ajili ya kunusuru mazalia ya viumbe hai wa majini kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

Waziri Mpina amewataka wale wote wanaojishughulisha na uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ambapo uvuvi haramu umeshamiri kuacha mara moja ambapo zoezi hilo la kuwasaka wavuvi haramu liakuwa la nchi nzima

''Hivi sasa tunachoma nyavu hapa za ni safari tuliyoianza ya kuchoma nyavu na kukamata wavuvi haramu, na wale wote wanaojishughulisha na uvuvi haramu nchi nzima ,kwahiyo tunaanza safari hapa mwanga ambapo safari hii itakuwa ni ya nchi nzima "Alisema Mpina

Katika Hatua nyengine Waziri Mpina ametoa miezi mitatu kwa halmashauri ya wilaya ya mwanga kuhakikisha Ujenzi wa choo Bora kwa ajili ya wavuvi na Wafanyakazi Biashara wa eneo hilo vinginevyo Marufuku halmashauri kukusanya ushuru katika eneo Hilo.

"Halmashauri inaendelea kukusanya mapatao kila uchao na wala hawachoki hawana likizo wala jumapili,lakini choo tu wakati mwingine hata milioni mbili hakifiki,kimeshindikana kujengwa,ifikapo tarehe 30/12/2019nitarudi hapa kuja kukagua,nikikuta hakuna mwalo,nikikuta hakuna vyoo,nitaifungia halmashauri ya mwanga kukusanya chochote"akisema Mpina

Samuel Kifoyo ni Mkazi wa mwanga ambae imeelezwa amekuwa akitafutwa na Baadhi ya watu wakiwemo Baadhi ya Askari kwa tuhuma mbalimbali ambapo baada ya kupata taarifa za ujio wa waziri wa uvuvi anajitokeza adharani akiwa katika mavazi ya kike kuhofia kupigwa na mahasimu wake Katika kata ya Lang'ata Kama anavyo anabainisha.

"Nimekuja hapa leo ili unilinde ,mama yangu ni mjane kazi yake anakata kuni nimeteseka nimekaa muda mrefu,watu wametoa pesa ili nikamatwe niuliwe na dada huyo yupo hapa,na leo alikuwa aseme kama alivyosema mwanga ndiyo maana nikaona bora mimi nikaona niwahi,nilikuwa nimejificha kwenye mapori nikivizia msafara wako mheshimiwa".Alisema Samweli Mkazi wa Mwanga.

Joachim Haule na Juma Waziri ni Baadhi ya wakazi wa kata hiyo wanasema eneo Hilo bado Hali ya usalama si shwari na hapa wakaeleza changamoto wanazo kabiliana nazo katika Oparesheni zinazo fanywa eneo Hilo.

Kwa mujibu wa wizara ya mifugo na uvuvi kwa sasa tanzania inasamaki wakutosha bila kuagiza nchi nyengine lakini bado suala la Uvuvi haramu limeshamiri katika Baadhi ya maeneo Kwenye maziwa na baharini, huku Oparesheni zilizo kuwa zikiendelea miaka iliyo pita zikianza upya kwa Kasi kubwa maeneo yote ya uvuvi na mifugo.

WEUSI, FID Q WAFUNIKA,OMMY DIMPOZ AMWAGA MACHOZI JUKWAA LA TIGO FIESTA 2019 _SAIZI YAKO MWANZA

$
0
0

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya Sanaa(THT) wakiwa wamebeba picha ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Ruge Mutahaba kwenye jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako Katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wakati wakimkumbuka na kumtakia alale mahali pema peponi. 


Msanii wa muziki wa kizazi kipya na Injili Goodluck Gozbert akishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Barnaba Classic akishambulia jukwaa la TTigo Fiesta 2019 _Saizi yako k katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpozi akifuta machozi wakati akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Mkali wa HipHop Fareed Kubanda ''Fid Q'' akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Maua Sama akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Weusi wakishambulia jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lulu Diva akitawala jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Marioo akishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rich Mvoko akitawala jukwaa laTigo Fiesta 2019 _Saizi yako k katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya TID '' Mnyama'' akipagawisha jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Badman Mkali wa Ngoma ya "NIKagongee " akipagawisha jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Bilnass akipagawisha jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy ;;African Princess'' akishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza






TAMASHA la Muziki, Msimu wa Tigo Fiesta 2019 limezinduliwa jana kwa kishindo jijini Mwanza huku kundi la Weusi likifunika kwa kuwapagawisha washabiki luluki waliojitokeza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Mbali na wasanii hao kukonga vilivyo nyoyo za washabiki wa muziki wa kizazi kipya msanii mwingine machachari Farid Kubanda ‘Fid Q’ hakuwa nyuma kuwarusha wapenzi huku Omar maarufu kama Ommy Dimpoz akimwaga kukwaani.

Washabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba walishindwa kujizuia kutokana na makamuzi ya nguvu yaliyowaacha hoi yaliyofanywa na kundi la Weusi wakiongozwa na JOH Makini,Nikki wa pili na G Nako baada ya kupanda jukwaani na kutoa burudani tosha.

Aidha, katika tamasha hilo la Tigo Fiesta 2019 msanii Fid Q alipanda jukwaani akiwa kwenye Wheel Chair (kiti cha magurudumu mawili) kabla ya kuwazodoa waliomzushia kifo na kwamba hataweza kuimba kutokana na kuugua maradhi kwenye koo kasha kumwaga machozi mithili ya mtoto.

Tamasha hilo limefanyika Mwanza kwa mara ya kwanza kuasisiwa kwake lilikuwa na mvuto na msisimko mkubwa ambapo washabiki kutoka viunga vya jiji hilo la milima ya miamba ya mawe walisuuzika nyoyo na mara kadhaa walishiriki kuimba nyimbo za wasanii mbalimbali hasa kundi la Weusi na Fid Q.

Mbali na kundi la weusi lililopagawisha vilivyo, wengine ni Barnaba, TID, Mavoko na Diva ambapo wasanii wa jiji la Mwanza nao hawakubaki nyuma.

Akizindua tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela alisema waandaaji wa Tigo Fiesta 2019 kwa ubunifu na uamuzi wao wa kuzindua tamasha hilo hawakukosea ikizingatiwa jiji hilo ni kitovu cha biashara kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati.

“Mwanza ni kisima cha burudani kutoka na kuwa na wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya hivyo niwapongeze Clouds na Tigo kwa ubunifu wao wa kuandaa na kuzindua tamasha lao hapa.Sisi kama mkoa tutaendelea kuwaunga mkono.Pia tamasha hili mbali na kutoa burudani lina umuhimu kiuchumi, linatoa ajira za muda mfupi,linaongeza kipato cha wananchi wetu na waandaaji nao wananufaika,”alisema Mongela.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Clouds Media Entertainment, Joseph Kusaga, alisema wana mapenzi nakubwa na Mkoa wa Mwanza na ndiyo sababu msimu huu wamezindua tamasha la Tigo Fiesta 2019 kwa kutambua mchango wa mkoa huo.

Naye Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati, kampuni hiyo ya mawasiliano itaendelea kushirikiana na kuiunga mkono Clouds ili kuhakikisha wanawapatia Watanzania burudani yenye vionjo na ladha tofauti tofauti.


Hata hivyo washabiki na wapenzi Tigo Fiesta 2019 waligubikwa na huzuni na simanzi ya muda mfupi wakati kundi la wasanii wa Tanzania House of Talent (THT) likitoa burudani huku wakionyesha picha za aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds, marehemu Ruge Mutahaba ikiwa ishara ya kumbukumbu yake.

Ikumbukwe marehemu Ruge kabla ya kufikwa na mauti alikuwa mhimili na muasisi wa tamasha hilo zamani likiitwa Fiesta kabla ya kubadilishwa na kuitwa Tigo Fiesta.

Tamasha hilo baada ya kuzinduliwa mashambulizi yataelekezwa mkoani Kagera katika Wilaya ya Muleba na hivyo wapenzi wa huko wakae mkao wa kula kwa nafasi

NMB yaboresha mfumo wa ulipaji kwa kutumia kadi

$
0
0
UONGOZI wa Benki ya NMB umesema kuwa unazidi kuboresha mifumo ya huduma zao za kadi ili kuhamasisha watalii pamoja wananchi wa kawaida kutumia kadi kwenye malipo na ununuzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir wakati akizungumza kwenye maonesho ya Utalii visiwani Zanzibar, ambapo benki hiyo ni moja wapo ya mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyofika tamati siku ya Jumamosi.
Alisema kutokana na ukuaji wa Teknologia Duniani, ndivyo wanavyo buni mbinu zitakazo wawezesha wateja wao kupata huduma bora na za kimataifa. Vilevile, mifumo ya Kidigitali na matumizi ya kadi za MasterCard ambazo zinatumika kitaifa na kimataifa  zimekua zikiondoa usumbufu kwani huduma hizo zinaweza kutumikaa ndani na nje ya nchi.
Benki ya NMB benki hivi sasa ipo karibu na wananchi mjini na vijijiNI  hivyo kuingia katika masauala ya utalii, kwa kiasi kikubwa itasaidia kuzidi kujitangaza na kuvutia wateja wengi zaidi pamoja na wageni wanaofika nchini. 
Naye Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar- Balozi Seif Ali Iddi ameomba mashirikiano na taasisi nyingine katika kutangaza utalii wa Zanzibar ili kuongeza idadi kubwa ya watalii Zanzibar.
Alisema wananchi wa Zanzibar wananufaika na utalii kupitia sera ya Utalii kwa wote na kubainisha kuwa sera hiyo ipo wazi  kuweza kunufanisha wananchi hasa kwa kuwa na usalama wa nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale- Mahamoud Thabiti Kombo alisema kuwa maonyesho hayo ni agizo la Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, ambapo lengo ni kuitanganza Zanzibar kiutalii baada ya mafanikio makubwa ya waka jana.
Alisema kuwa maonesho ya kila mwaka yanawasadia wajasiriamali wadogo wadogo kujitangza kupitia utalii ili waweze kunufanika na matunda ya utalii kwa kuuza bidhaa na kukuza biashara zao.
Kwa upande wake Meneja wa NMB tawi la Zanzibar - Abdalla Duchi, amewataka wananchi wa Zanzibar kuchangamkia fursa za utalii zinazopatika  nchini ili kujikwamua na umaskini .
Amewataka wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati  kutumia fursa zinazotolewa na Benki hiyo katika maeneo mbalimbali kwa kujisajili kuwa mawakala, ambapo itafungua fursa za ajira sambamba na kutoa huduma kwa wananchi wa kawaida ikiwemo watalii wanaokuja kutembea Zanzibar.
Aliongeza kuwa benki ya NMB ina wateja zaidi ya milioni tatu huku ikiongoza kwa matawi mengi - 229 nchini, yakiwemo NMB Zanzibar, NMB Mwanakwerekwe na NMB Chakechake- Pemba, huku ikiwa na jumla ya mawakala 84 Zanzibar kwa jumla ya idadi ya  mawakala 6000 nchi nzima.
  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (mwenye miwani) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya pili ya 'Zanzibar Tourism Show' Visiwania Zanzibar.
 Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mheshimiwa  Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Maofisa wa Benki ya NMB alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya pili ya 'Zanzibar Tourism Show'  Visiwani Zanzibar.
  Maofisa wa Benki ya NMB wakifurahi pamoja na Waziri wa Habari, Utalii, Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mheshimiwa  Mahmoud Thabit Kombo baada ya kukabidhiwa cheti cha shukrani kwa udhamini wao.

NAIBU WAZIRI MGUMBA AWATAKA WALIMU NCHINI WAACHE KUTUMIA KILIMO KAMA ADHABU YA KUWAPA WANAFUNZI

$
0
0

NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba akizungumza na watumishi wa Halamashauri ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kulia akimueleza jambo Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba wakati wa ziara yake wialayani humo
MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange 
 NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisalimiana na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Seif
 NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisialimiana na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalim Hassani Nyange wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo
 NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisalimiana na Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba kushoto akisalimiana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi 
NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari waache kutumia kilimo kama adhabu ya kuwapa wanafunzi wakati wanapokosea kwani inawajengea tafsiri mbaya kwa jamii na baadae wanapokuwa wanachukia kilimo.

Mgumba alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake wilayani Pangani ambapo alisema kwamba kuna tabia ambayo imejengeka kwa walimu hao kwamba mtoto anapokosea anaambiwa leo utakwenda kilima siku nzima, utakwenda kumwagilia hali ambayo inapelekea baadae wakikua wanakuwa hawahitaji kilimo kwa sababu awali waliona kama adhabu.

Alisema kwamba hapana suala hilo sio jema na ndio maana wao wanasema kilimo ni ute wa mgongo lakini watafungamanisha kilimo na elimu ili watoto tokea anakuwa ajue kwamba nchi hii uchumi wake unategemea kilimo.

“Hivyo ninapoambiwa niwe na tuta la mchicha sio adhabu bali ni sehemu ya kuniandaa kielimu nije kujitegemea au nije kuajiri wengine kwenye mashamba yao kwani bila kufanya hivyo tutakuwa tunaimba kitu kingine wakati uchumi wetu unategemea kilimo”Alisema Naibu Waziri huyo.

Naibu Waziri huyo alisema kwamba mkakati wa serikali ni kuimarisha kilimo hivyo wataendelea kufungamanisha elimu yao na kilimo chao.

Akizungumzia Kilimo cha Minazi wilayani humo Naibu Waziri huyo alisema kwamba kilimo cha minazi ni kweli mpaka sasa hawaapata ufumbuzi wa magonjwa yake kwa miaka zaidi ya 30 mpaka leo ambayo yanasababsihwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Alisema pia hilo linatokana na kukubali kuletewe mbegu ya kisasa ambayo haiendani na mazingira ya nchi hivyo kama Taifa  wameendelea kuimarisha vituo vyao vya utafiti hasa cha utafiti wa minazi mikocheni lengo ni kuanza kurudi kwenye kuzalisha miche kutumia minazi ya asili inayokabiliana na hali ya hewa na ikolojia ya ya nchi yetu .

“Na sasa tumeanza kuzalisha kitalu cha miche asili Bagamoyo na itasambazwa nchi nzima kwa lengo la kupanda na hatimaye kuweza kurejesha minazi hiyo”Alisema

Akizungumzia udogo wa bei ya nazi nchini Naibu Waziri huyo alisema kwamba nazi zinauzwa bei ndogo na imeendelea kuwa ndogo ni kutokana na ushindani uliopo kwenye soko la ndani, kanda na kimataifa kwa sababu ya bidhaa mbadala.

 “Hivyo kila nazi ikipanda bei watu wanakwenda kutumia mafuta lakini kila tunapoacha kutumia nazi na kutumia mafuta na kwenda kwenye chukuchuku wanapunguza mahitaji ya nazi”Alisema.

Hata hivyo alisema kwamba wanakuja na mkakati wa kuanzisha viwanda ambavyo vitaongeza thamani bidhaa hiyo ili kupanua soko la nazi hapa nchini na mbegu za nazi ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi huku akieleza kwamba wakienda kuongeza thamai tatizo hilo litakwisha.

Katika hatua nyengine Naibu Waziri huyo aliwataka watanzania tuendelee kutumia nazi kwani wanapoendelea kuitumia zaidi wanatongeza mahitaji na soko la nazi litakuwa kubwa huku akisistiza kwamba watakaendelea kutumia mafuta bei ya nazi itashuka.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso alisema kwambazao la nazi limeathiriwa namaradhi kwa muda mrefu mpaka yamepatikana bado tiba yake haijapatikana miaka 30.

Alimwambia Naibu Waziri Mgumba kwamba ugonjwa huo umekuwa haupati ufumbuzi kama lilivyokuwa gonjwa la ukimwi hiyo walimuomba watafiti na watalamu wafanye utafiti ambao utafika mwisho na wenye manufaa na kuweza kurudisha uchumi wake.

“Kwa sababu nazi zinakazi nyingi unaweza kusingwa na machicha yake ukabaki hapa Pangani….lakini pia inaleta heshima kwenye ndoa na hivyo kuweza kurejesha furaha”Alisema.

Mwisho

NMB yatoa msaada wa madawati, vifaa tiba Mikoa Morogoro, Simiyu, Manyara.

$
0
0

Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya kati wakiangalia mashuka na wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya zaidi ya milioni tano hospitalini hapo.
Baadhi ya Wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya Chief Sarwat ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara wakibeba viti na meza muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa msaada huo na Benki ya NMB wenye thamani ya shilingi milioni tano shuleni hapo. 


Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 215 katika shule za sekondari Mahenge, Vigoi na Isongo zilizoko Wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro na Ng’hoboko iliyoko Wilayani Meatu Mkoani Simiyu.

Mbali na hilo benki hiyo pia imetoa msaada wa vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto vyenya thamani ya shilingi milioni tano ambapo vifaa hivyo vilivyotolewa ni pamoja na vitanda na mashuka na magodoro.

Msaada huo wa madawati umegharimu kiasi cha sh. Milioni 20, ambapo katika shule za Wlaya ya ulanga benki hiyo imetoa madawati 165 yaliyogharimu Milioni 15 huku katika shule ya Ng’hoboko imetoa madawati 50 ambayo yamegharimu Milioni 5.

Vifaa hivyo pamoja na madawati vimetolewa kwa nyakati tofauti ndani ya wiki hii, ambapo vinaifanya benki hiyo kuchangia katika shughuli za maendeleo jumla ya shilingi Milioni 675 hadi sasa kwa mwaka huu tu.

Meneja wa benki hiyo kanda ya Magharibi Sospeter Magesse akiongea katika hafla ya kukabidhi madawati shule ya Ng’hoboko alisema kuwa msaada huo umetolewa ili kuwawezesha wanafunzi wasome vizuri.

Alisemakuwa benki hiyo imekuwa ikitenga kiasi cha sh. Bilioni moja kila mwaka kwa ajili ya kurejesha kwa wananchi, pesa ambayo imekuwa ikitumika kuboresha huduma za elimu, na afya.

“ NMB kama benki ya watanzania itaendelea kusaidiana na serikali pamoja na watanzania katika kuboresha huduma za afya na elimu, tuna imani kwa msaada huu wanafunzi watajisomea vizuri,” alisema Magesse.

Naye Nsolo Mlozi Meneja wa benki hiyo kanda ya kati akikabidhi vifaa tiba katika hospiali hiyo alisema kuwa NMB inatoa msaada huo kama njia ya kurudisha faida kwa wananchi ambao ndiyo wateja wao wakubwa.

“ Ingawa Serikali inafanya makubwa, Benki hiyo inao wajibu wa kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo kwa kusaidia jamii kwani kupitia jamii hii hii, ndio imeifanya benki NMB kuwa hapa ilipo na kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini,” Alisema Mlozi.

“ Vifaa hivi vya tiba na afya tunavyokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata,” aliongeza Mlozi.

Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Ngolo Malenya akipokea madawati ameishukuru benki ya NMB kwa kutoa madawati 165 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari za mahenge ,vigoi na isongo

Ametoa wito kwa wanafunzi hao kuwa mabalozi kwa wazazi wao kwa kuwaeleza mambo mazuri yanayofanywa na benki hiyo ili pia wazazi hao waiunge mkono benki hiyo kwa kufungua account mbalimbali ili NMB izidi kurudisha faida wanazopata kwa jamii kwa kuleta maendeleo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Meatu Dkt Joseph Chilongani aliishukuru benki ya NMB huku akitaka wanafunzi wa shule hiyo na walimu kuhakikisha madawati hayo yanatunzwa ili kudumu kwa muda mrefu.

“ Kuna haja ya kuweka adhabu kidogo kwa wale ambao watahusika kuaribu haya madawati, akiaribu mwanafunzi yeye au mzazi wake wahusike katika kutengeneza, tunataka haya madawati yatumiwe na wadogo zetu ili waone umuhimu wa NMB,” Alisema Chilongani.

TAMASHA KUBWA LA KUMKUMBUKA MWALIMU JULIUS NYERERE KUFANYIKA BUTIAMA KUANZIA OKTOBA 8 HADI OKTOBA 14, JAJI WARIOBA MGENI RASMI

$
0
0

Na Said Mwishehe, Michuzi Blog

KAMPUNI ya Miranda Investment kwa kushirikiana na Serengeti Media Centre, Chuo cha Utalii Serengereti na Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu ya Wazanaki imeandaa tamasha kubwa la Kumbukumbu ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambalo linatajia kufanyika kuanzia Oktoba 8 hadi Oktoba 14 Butiama Musoma mkoani Mara ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa kwanza wa Rais Joseph Warioba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi utamaduni wa Wazanaki Mashaka Mgeta amesema kuna umuhimu mkubwa wa kufanyika kwa tamasha hilo na kwamba ni miaka 20 tangu Mwalimu Julius Nyerere, hivyo wao kampuni hiyo wameona kuna umuhimu wa kufanya tamasha hilo ambalo pamoja na mambo mengine litawaleta Watanzania pamoja.

Amesema tamasha hilo ambalo limebeba kauli mbiu ya Uadilifu na Uchapakazi ni dira ya kuufikia uchumi wa viwanda na kwamba Mwalimu Nyerere alipambana sana katika ukombozi wa Taifa la Tanzania. Mgeta ameongeza wakati taifa linamkumbuka Mwalimu Nyerere, kupitia tamasha hilo wananchi kutoka Mkoa wa Mara na mikoa jirani watapata burudani za kila aina kupitia michezo mbalimbali ambayo imeandaliwa kwa mwaka huu.

Kwa upande wake Mtaribu wa Tamasha hilo Kulwa Karedia amesisitiza kama Watanzania wanavyotambua kila ifikapo Oktoba 14 ya kila mwaka nchi yetu huadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa ,Hayati Mwalimu Julius Nyerere na kwa mwaka huu maadhimisho hayo ni ya 20.

Amesema kuwa maadhimisho haya huambatana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali, vikundi na watu binafsi, lengo kubwa ni kumkumbuka mwasisi wa taifa letu kutokana na kujitoa kwa kila namna dhidi ya utawala dhalimu wa kikoloni na hatimaye kuleta uhuru ambao tunajivunia kwa kuupata bila kumwaga damu.

"Tunatambua mwalimu Nyerere alilifanyia taifa hili mambo ambayo hayawezi kufutika kamwe machoni mwa Watanzania. Kutokana na msingi huo, tuliopo tunapaswa kumuenzi kwa kuyaendeleza yote mazuri aliyoyafanya. Kwa kutambua uzito wa hili, Miranda Investment, Serengeti Media, Chuo cha Utalii Serengeti na Kituo cha Kuendeleza Utamaduni wa Wazanaki, tumeandaa tamasha na kongamano la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambalo litaanza kuunguruma Oktoba 8- 14 kijijini Butiama mkoani Mara,"amesema Karedia.

Pamoja na Serikali kuwa na siku ya kitaifa ambayo inaadhimishwa mwaka huu mkoani Lindi kwa shughuli mbalimbali, zikiwamo sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru ambao Mwalimu Nyerere aliuasisi, tumeona ni jambo jema na la msingi tuungane na wakazi wa kijiji cha Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla kukumbuka siku hiyo muhimu kwa kufanya tamasha la burudani kwa michezo mbalimbali.

Pamoja na mambo mengine amesema kubwa ni kuwapo kwa mashindano ya riadha yaliyopewa jina la Mwalimu Nyerere Historical Marathon yakiwakilisha wanariadha kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara na nje ya mkoa huo."Tamasha hili tutashirikisha pia wananchi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mara, Tarime, Bunda, Musoma, Butiama na Serengeti na mikoa ya jirani kama Mwanza, Simiyu na Arusha,"amesema.

Kuhusu matukio yatakayofanyika katika tamasha hilo Karedia amesema ni riadha, Mbio za Kilomita 10, Mbio za Kilomita Tano kwa vijana kati ya miaka 13 - 18.Pia kutakuwa na mbio za kilomita mbili na nusu , mbio za kujifurahisha
Karedia amesema mbio zote zitaanzia Uwanja wa Mwenge Butiama kupitia Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kuelekea Barabara ya Kiabakari ambayo Mwalimu Nyerere aliitumia wakati wa kuunga mkono matembezi ya Azimio la Arusha mwaka 1967.Pia kutakuwa na mbio za baiskeli, bonanza la mpira wa miguu na kuongeza kuwa timu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mara zimealikwa kushiriki, wakiwamo mabingwa watetezi Butiama Stars 

Pia kutakuwa na mpira wa pete ambapo Karedia amesema kwa mwaka huu wameboresha zaidi mashindano hayo kwa kuongeza mchezo wa mpira wa pete, maana wanaamini mwalimu alikuwa mpenzi wa kila kundi. Tunagetemea timu kutoka wilaya zote zitafika Butiama.

Amefafanua kuwa mchezo wa bao nao utakuwapo kwenye tamasha hilo hasa kwa kuzingatia Baba wa Taifa, alikuwa mchezaji hodari wa mchezo huu, kutokana na hali hiyo, tumealika timu zaidi ya sita kutoka Sengereti, Musoma, Tarime na Butiama. Hapa tunagemewa kivumbi kutimka kwa sababu kuna wazee waliobebea, wataonyeshana umwaba hapa.

Wakati huo huo kutakuwa na ngoma na kwaya ambapo vikundi vya ngoma za asili na kwaya vitashiriki. "Tunagetegea kuwa na wageni mbalimbali wa kitaifa na kitamaifa. Nasema hivi kwa sababu tumefanya mawasiliano na balozi kadhaa kama ule wa Marekani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda, Msumbiji,Afrika Kusini na China,"amesema Karedia .

Wakati huo huo amesema washiriki zaidi ya 1,000 kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Mara na maeneo jirani wanatarajiwa kushiriki tamasha hili Tunamshukuru Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Mara, Profesa Sospter Muhongo kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha mno wana Mara kujitokeza.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais Jaji Joseph Warioba. Pia wanatarajia uwapo wa wakuu wa wilaya, wabunge na viongozi wengine kutoka mikoa ya jirani.

Karedia ametoa mwito kwa kuwaomba wakazi wa Mkoa wa Mara na mikoa ya jirani wajitokeze kwa wingi kushiriki tamasha hili ili kumuenzi Mwalimu Nyerere wa vitendo, tukiongozwa nakauli mbiu ya mwaka huu katika tamasha hilo inasema hivi: Uadilifu na uchapakazi ni dira ya kufikia Tanzania ya Viwanda

 Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi  Kumbukumbu ya Utamaduni wa Zanaki Mashaka Mgeta akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  kuhusu tamasha la kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere linalotarajia kufanyika Butiama wilayani Musoma mkoani Mara .Kulia ni Mratibu wa tamasha hilo Kulwa Karedia.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu ya utamaduni wa Wazaki Mashaka Mgeta(kushoto) akiwa na Mratibu wa tamasha la kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo linalotarajia kufanyika Butiama mkoani Mara
 Mratibu wa Tamasha la Kumbukumbu ya miaka ya 20 ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Julius Nyerere, Kulwa Karedia(kulia) akizungumzia ratiba ya  shughuli zitazofanyika wakati wa tamasha hilo linalotarajia kuanza Oktoba 8 hadi Oktoba 14 mwaka huu Butiama mkoani Mara .Kushoto Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu ya utamaduni wa Wazanaki Mashaka Mgeta.
 


Mchango wa Kampuni ya Tigo katika uenezaji wa huduma ya intaneti/mtandao Tanzania.

$
0
0

Kampuni ya Tigo ambayo kwa sasa ni namba mbili kwa ukubwa hapa nchini.Kwa mujibu wa takwimu za TCRA Tigo ina wateja wapatao 11.6 Milioni.

Kampuni hiyo ni moja ya waanzilishi wa teknolojia ya intaneti yenye viwango vya kimataifa kupitia mtandao wa 2G na 3G.Aidha, imekuwa ya kwanza kuanzisha intaneti yenye kasi ya 4G-LTE na kuiboresha kwenda 4G+, jambo ambalo limedhihirisha utayari wake katika kuleta mapinduzi ya kidigitali hapa nchini.

Kwa mujibu wa Afisa Biashara Mkuu wa Tigo, Bw.Tarik Boudiaf, safari ya Tigo katika kuleta suluhu kidigitali kwa wateja wake ilianza baada ya Kampuni hiyo kufanya mageuzi ya kiuendeshaji na kuifanya kuwa kampuni ya kidigitali ikitoa bidhaa mbalimbali pamoja na intaneti ya kasi mbali na huduma za kawaida za kupiga simu, kutuma meseji na huduma za kifedha.

Kupitia dhamira yake ya kuleta mapinduzi ya kidigitali nchini, Tigo inakuwa mmoja wa kampuni za juu zenye kuchochea ueneaji na matumizi ya intaneti kwa wateja wake.

Aidha, kupitia mkakati maalumu, Tigo imeanzisha jitihada mbalimbali ambazo zimebadilisha mwenendo wa soko huku ikichangia katika agenda ya ujumuishwaji wa watu kidigitali nchini.

“Mkakati wetu ni kuendelea kuleta ujumuishwaji wa kidigitali na kuboresha mfumo wa maisha Tanzania.Tigo ni kampuni ya kwanza kuanzisha intaneti ya 4G na hivi karibuni imeleta teknolojia ya 4G+ iliyozinduliwa chini ya kampeni ya “Always a step ahead”. Hii inadhihirisha nia yetu ya dhati ya kuwaunganisha watanzania na intaneti ya kasi na ya uhakika huku tukiwajengea uelewa juu ya faida za huduma hii ya mtandao,” anasema Boudiaf.

Anaongeza “Tunatambua kwamba wateja wetu wanahitaji huduma ya uhakika na yenye ufanisi ambayo inahusisha teknolojia yenye miundombinu ya hali ya juu, vifurushi mahsusi pamoja na simu janja (smartphones) za kisasa pamoja na kuwapa maudhui yenye uhaisia”.

Ili kufanikisha malengo hayo, Afisa huyo anaeleza mikakati mbalimbali ya kuwezesha ueneaji wa intaneti ikiwamo uwekezaji mkubwa uliofanywa na Tigo kwenye ujenzi wa miundombinu ya teknolojia ya intaneti ya 4G ambayo imeboreshwa na kuwa 4G+ na hatimaye kukidhi mahitaji ya huduma za mtandao.

Aidha hatua hii sit u imeboresha huduma za kampuni hiyo bali imewezesha kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Takwimu za Taasisi ya Kimataifa ya GSMA kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ya mwaka 2019, inaonyesha kuwa matumizi ya simu janja yataongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2025 huku ukanda wa Afrika Mashariki ukitajwa kushuhudia ongezeko kubwa Zaidi.Ripoti inazitaja nchi za Rwanda na Tanzania kuongoza kwenye ukuaji huo.

Kadhalika,kutokana na ukweli kuwa matumizi ya mtandao hufanyika hasa kupitia simu za mkononi hivyo upatikanaji wa simu za bei nafuu ni chachu katika kuchochea ueneaji wa intaneti nchini. Katika hili, Boudiaf anasema “Tigo imetengeneza mkakati madhubuti wa kuchochea matumizi ya smartphones kwa watu nchini.Tunaamini kuwa kupitia kuingia ubia na wazalishaji wa simu za mkononi kama Kampuni ya Samsung, Tecno, Nokia, Infinix na Itel imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za simu na kuzifanya zipatikane kwa urahisi hadi kwa watu wenye kipato cha chini.”

Sambamba na hilo, Tigo imekuwa ikiendesha kampeni mbalimbali zenye lengo la kutoa simu kwa wateja ikiwamo ile ya Wagiftishe na hivi karibuni imekuja na kampeni ya Lamba Dume ambapo mbali na kutoa simu, zinatoa fursa ya kupata intaneti ya bure inayodumu kwa takribani mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, ijapokuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye tozo ndogo za intaneti kwenye ukanda huo, suala la kutengeneza vifurushi nafuu vya intaneti ni jambo la msingi. Mfano; Kifurushi cha Saizi Yako ni moja ya vifurushi ambavyo vinavyolenga kumpa mteja huduma ya intaneti bila mipaka ambapo mteja anaweza kujipatia intaneti kulingana na mahitaji yake.

Vilevile, upatikanaji wa maudhui ya ndani ni moja ya sababu za kuongeza matumizi ya intaneti.Tigo inatoa vifurushi mbalimbali ambavyo vinaruhusu wateja kujipatia maudhui yenye kukidhi mahitaji ambapo kupitia mtandao wa You Tube, StarTimes na DSTV wateja wanaweza kuunganishwa na chaneli hizo na kufurahia maudhui yenye uhalisia wa ndani.

Kuhusu suala la uridhishwaji wa huduma za mtandao zinazotolewa na Kampuni hiyo, Boudiaf anasema “Kupitia kufanya vumbuzi mbalimbali, Tigo inalenga kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora na zenye viwango kupitia bidhaa na huduma za kisasa kila wanapokutana na nembo yetu.Uwekezaji wa Tigo kwenye intaneti ya 4G umehakikisha kupatikana kwa intaneti ya uhakika na yenye viwango stahiki, nia hii ya Tigo inaiweka sekta ya mawasiliano kwenye viwango vya juu na kuleta mageuzi ya kidigitali,” .

Tigo Tanzania inajinasibu kwa kuongoza soko katika kuchochea maendeleo ya digitali na zaidi katika kuleta huduma zenye kukidhi mahitaji ya wateja na hii imesabisha kutengeneza huduma na bidhaa zenye kukidhi mahitaji ya soko soko la Tanzania.

Wateja wa Tigo wanafikiwa kote nchini kupitia njia mbalimbali ikiwamo maduka ya Tigo,dawati la huduma kwa wateja pamoja na mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook, Twitter, WhatsApp na Instagram ambayo inampa fursa mteja kushiriki katika uboreshaji wa huduma kwa kutoa maoni juu ya huduma zitolewazo na kampuni hiyo.

Hatahivyo, fursa ya kuwaunganisha watanzania na huduma ya intaneti ya uhakika bado inatakiwa kupewa kipaumbele kutokana na ukweli kuwa bado idadi kubwa ya watu wanakaa nje ya mtandao (offline).

WAFANYAKAZI TISA NSSF WAFIKISHWA KORTIN WAKIKABILIWA NA KESHI YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0


WAFANYAKAZI tisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Jamila Vulu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka matano yakiwemo ya kughushi na kutakatisha fedha wa zaidi ya Sh. bilioni mbili.

Mbali na Vulu, washitakiwa wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Tikyeba Alphonce, Mwandishi wa hundi, Abdulrahaman Njozi, Meneja Uhakiki, Amir Kapera, Mhasibu anayehusika na maridhiano, James Oigo, Hellen Peter Mhasibu Mkuu, Ivonne Kimaro Mhasibu Mwandamizi anayeshughulikia matumizi, Restiana Lukwaro Mhasibu dawati la Uchunguzi na Dominic Mbwete Mhasibu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 15, mwaka huu kwa
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa kati ya Julai Mosi, 2016 na Septemba 4,2017 maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kughushi na utakatishaji fedha haramu.

Imedaiwa, kati ya Julai Mosi 2016 na Septemba 4,2017 katika Ofisi za NSSF Makao Makuu zilizopo katika Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, washtakiwa Njozi na Kapera kwa nia ya kulaghai walighushi hundi 47 za benki ya CRDB Kwa jina la NSSF yenye fedha Sh 2,130,211,437 huku wakionesha kuwa hundi hizo ni halali na zimetolewa na bodi ya wadhamini ya shirika hilo.

Imeendelea kudaiwa kuwa, siku na mahali hapo washitakiwa wakiwa watumishi wa umma na waajiliwa kwa vyeo hivyo, waliiba Sh 2,130,211,437 mali ya bodi ya wadhamini ya NSSF

Aidha katika shtaka la nne la kusababisha hasara, inadaiwa washitakiwa wote hao wakiwa watumishi wa umma na waajiriwa wa NSSF, walisababishia shirika hilo hasara ya Sh 2,130,211,437 kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Kati ya Julai Mosi 2016 na Septemba 4, 2017 katika Ofisi za NSSF Makao Makuu wilayani Ilala, Dar es Salaam, washtakiwa wote walijihusisha na miamala mbalimbali huku wakijua fedha hizo ni mazalia ya makosa tangulizi ya kughushi na wizi.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika

Wakili wa utetezi, Alex Mushumbuzi aliuomba upande wa mashitaka kuhakikisha wanaongeza spidi katika upelelezi kwa sababu mpaka washitakiwa wanaletwa mahakamani wanaamini kuna mchakato ulianza kufanyika.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 15, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.




WAFANYAKAZI tisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Jamila Vulu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka matano yakiwemo ya kughushi na kutakatisha fedha wa zaidi ya Sh. bilioni mbili.

Vodacom ilivyonogesha Utalii Zanzibar

$
0
0
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi akizungumza na wageni waalikwa kwenye tafrija ya Utalii wa Zanzibar mwishoni mwa wiki. Vodacom walidhamini tafrija hiyo iliyofanyika  6 Degrees Hotel mjini Zanzibar.
Msanii Ali Kiba akitoa burudani kwenye tafrija ya Utalii wa Zanzibar mwishoni mwa wiki. Vodacom walidhamini tafrija hiyo iliyofanyika 6 Degrees Hotel mjini Zanzibar.
Wageni waalikwa wakipata burudani toka kwa Msanii Ali Kiba.



VIVUKO VYA BILIONI 7.3 KUKAMILIKA FEBRUARI MWAKANI

$
0
0
Muonekano wa Kivuko kipya cha Kayenze Bezi ambacho ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu, kivuko hicho kimegharimu jumla ya shilingi Bilioni 2.7 za Kitanzania na kitatoa huduma kati ya Kayenze na Bezi Wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akitoa taarifa fupi wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TEMESA Profesa Idriss Mshoro kulia ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko viwili vipya vya Chato Mharamba na Bugorola Ukara vinavyogharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3 za Kitanzania. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella.



Meneja wa Kampuni ya Songoro Major Songoro (wa pili kushoto) akimpa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella katikati wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko viwili vipya vya Chato Mharamba na Bugorola Ukara vinavyogharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle na Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TEMESA Profesa Idrissa Mshoro.



Meneja wa Kampuni ya Songoro Major Songoro kulia akimpa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko viwili vipya vya Chato Mharamba na Bugorola Ukara vinavyogharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3 za Kitanzania.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

……………………

NA ALFRED MGWENO- TEMESA MWANZA

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inatarajiwa kukamilisha ujenzi wa vivuko viwili vipya vinavyogharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3 ifikapo mwezi Februari mwaka 2020.

Hayo yamebainishwa leo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Profesa Idrissa B. Mshoro alipotembelea yadi ya Songoro Ilemela jijini Mwanza kukagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko hivyo unaoendelea katika karakana hiyo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alialikwa kushuhudia ukaguzi huo.

Mhandisi Maselle alisema mkataba kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha Bugorola Ukara ulisainiwa Tarehe 8 mwezi Februari mwaka huu wakati ule wa Chato Mharamba ulisainiwa Tarehe 15 mwezi Aprili na ujenzi wa vivuko vyote unafanywa na kampuni hiyo ya kizalendo ya Songoro Marine.

‘’Ujenzi wa kivuko cha Bugorola una gharama ya shilingi za Kitanzania bilioni 4.2 wakati ule wa Chato Nkome ni wa shilingi bilioni 3.1 bila VAT na fedha zote hizi zinatolewa na serikali ya Tanzania.’’ Alisema Mtendaji Mkuu.

Aliongeza kuwa Wakala unaendelea na ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV. Sengerema kwa gharama ya shilingi milioni 689.4 na utakamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu huku ule wa kivuko cha Kayenze Bezi unaogharimu bilioni 2.7 ukitara
jiwa kukamilika ifikapo mwezi Novemba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala huo Profesa Idrissa B. Mshoro akizungumza katika ziara hiyo alisema ununuzi wa vivuko hivyo ni jitihada za serikali katika kuboresha huduma kwa wananchi na kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanafikika kirahisi ili kuinua uchumi wa nchi hasa katika kulenga kufikia malengo ya nchi ya uchumi wa kati kufikia 2025.

‘’Naomba niishukuru serikali tena kwa kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vivuko hivi ambavyo vitakuwa ni mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo kwani vitawaondolea adha ya usafiri waliyonayo kwa sasa hasa wananchi wenye kipato cha chini na mimi na bodi yangu tutahakikisha tunaisimamia vizuri TEMESA ili kutimiza malengo hayo.’’ Alisema Profesa Mshoro.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza katika ziara hiyo aliishukuru serikali kwa kuendelea kurahisisha usafiri wa vivuko katika mkoa huo ambapo vivuko vyote vikikamilika vitafanya idadi ya vivuko katika mkoa huo kutoka 11 na kufikia 14 ikiwemo boti moja ya uokozi ya (SAR II).

‘’Nichukue fursa hii kuwapongeza TEMESA kwa usimamizi mzuri na kazi nzuri wanayoifanya katika kuboresha miundombinu ya vivuko kote nchini.’’ Alisema Mhe. Mongella.

Kukamilika kwa miradi hii mipya ya vivuko kutaifanya TEMESA kutoka kuwa na vivuko 30 na kufikia kuwa na jumla ya vivuko 34 nchi nzima.

Rais Magufuli awaapisha Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Balozi

$
0
0
Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 01 Oktoba, 2019 amemuapisha Dkt. Wilson Mahera Charles kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Balozi.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage.

Akizungumza baada ya kuwaapisha, Mhe. Rais Magufuli amewatakia heri viongozi walioapishwa na kuwataka wafanye kazi kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu na kwa maslahi ya Taifa.
  
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
01 Oktoba, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Wilson Mahera Charles kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Balozi ambaye ameteuliwa leo kuwa Mkuu wa Itifaki Chief of Protocol wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Kanali Wilbert Augustine Ibuge akila Kiapo cha  kuwa Balozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Wilson Mahera Charles wa kwanza kushoto na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Wilbert Augustine Ibuge. Wengine katika picha ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC ) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage. PICHA NA IKULU

KAMISHNA JENERALI ANDENGENYE WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI APANDA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ( CGF) Thobias Andengenye (aliyeshika bendera) akiongoza msafara wa askari 11 wa jeshi hilo kupanda mlima Kilimanjaro.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (kulia) akiongoza msafara wa askari 11 wa jeshi hilo kupanda mlima Kilimanjaro.

**************************
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye amewaongoza maofisa 11 wa jeshi hilo kupanda mlima Kilimanjaro kwa kuitaka jamii kuwa wazalendo kwa kupenda utalii wa ndani na kutembelea hifadhi za Taifa. 

Akizungumza jana kamishna Jenerali Andengenye alisema watanzania wanapaswa kupenda vivutio vya utalii wa ndani. 

Alisema askari watapanda mlima Kilimanjaro kujionea ufahari uliopo ili kukuza uchumi wa nchi wakiwawakilisha askari wa zimamoto wengine hapa nchini.
Alisema wenyewe wanahusika na dharura zote za uokoaji isipokuwa za jinai ndiyo sababu wakaonelea wapande juu ya Afrika kupitia mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kwenye bara hilo. 

“Sisi tunapaswa tutumie karama tuliyopewa na Mungu kwa kutembelea na kujionea ili kukuza uchumi wetu kwa watanzania wenyewe kuchangia pindi tukitembelea hifadhi zetu,” alisema Andengenye. 

Mkaguzi msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji, Bilhah Chaila akizungumza wakati wakijiandaa kupanda mlima Kilimanjaro aliwahamasisha wanawake wa ndani na nje ya nchi kushiriki kwa wingi kwenye vivutio vya utalii. 

Chaila alisema kuwa wanawake wanauwezo mkubwa kama wanawake hivyo wanapaswa kushiriki kuchangia pato la Taifa kwa kutembelea hifadhi za Taifa zilizopo sehemu mbalimbali hapa nchini. 

Kamishna Jenerali Andengenye na maofisa hao 11 wanatarajia kupanda mlima Kilimanjaro na kurejea ijumaa ijayo Octoba 4 mwaka huu. Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu zaidi barani Afrika una urefu wa karibia mita 6,000 sawa na zaidi ya futi 20,000.

WANANCHI MIKOA YA KASKAZINI WAASWA KUFUATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imewaasa wananchi wa mikoa ya Kaskazini, Kilimanjaro Arusha na Manyara  kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kila siku na mamlaka hiyo  ili kuweza kuepuka majanga yanayoweza kujitokeza.

Katika Taarifa iliyotolewa na Meneja wa kituo Kikuu cha  utabiri TMA, Samwel Mbuya leo Oktoba Mosi, 2019 imesema leo majira ya mchana katika baadhi ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara kulitokea na upepo mkali uliotokana na mkusanyiko wa mawingu ya radi katika eneo dogo na kutengeneza mkondo wa mawingu.

"Mawingu hayo yalisababisha dhoruba ya upepo uliokuwa na kasi ya kilomita 50 kwa saa hali ambayo  ilidumu kwa takribani dk.30 katika eneo husika kabla ya hali hiyo kurejea kawaida.

Taarifa hiyo imesema, mkondo huo wa mawingu ulianzia kusini mwa Kenya na kujielekeza katika baadhi ya mikoa hiyo na kufuatiwa na vipindi vya mvua na ngurumo kutokana na mawingu hayo.

Amesema,  matukio hayo ni hali inayoweza kujitokeza panapotokea mawingu hayo mazito kujikusanya katika mkondo, hivyo amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku na kuzingatia kufuatilia hali ya hewa.

WADAU WAKUTANA KUKAMILISHA MWONGOZO WA UPANGAJI MATUMIZI YA ARDHI

$
0
0
Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kwa kushirikiana na Mashirika ya TNC pamoja na PELUM-Tanzania imekutana na wadau wa uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini kwa ajili ya kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini (Guideline for participatory village land use planning, administration and management in Tanzania) 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kazi hiyo, M kurugenzi Mkuu wa Tume Dkt. Stephen Nindi amewataka wadau hao kuhakikisha Mwongozo huo unakuja na majibu ya kisayansi katika uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia na mabadiliko ya tabianchi kwa malengo ya kuwasaidia wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akifungua kikao cha kikao kazi kuhusu kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini, Morogoro, Octoba 2, 2019
Bw. Peter Lorri, Meneja Uhifadhi nchi kavu kutoka Asasi ya kiraia ya The Nature Conservancy (TNC), akieleza ushiriki wao katika uwezeshaji wa upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini. 
Bw. Angolile Rayson Afisa Programu kutoka PELUM Tanzania akielezea ushiriki wao katika Mwongozo wa mpango wa matumizi ya ardhi na namna walivyoshiriki katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja uandaaji wa matumizi ya ardhi katika baadhi ya vijiji nchini Tanzania
Bw. Joseph Osena Kaimu Mkurugenzi, mipango ya matumizi ya ardhi, usimamizi na uratibu akiwapitisha wana kikosi kazi aina 14 za ramani ambazo zinatakiwa kuandaliwa wakati wa upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji ambazo zitaifanya mipango hiyo kuwa ya kisayansi zaidi
Bw. Paulo Tarimo Mkurugenzi wa Mipango ya ya Matumizi ya ardhi Wizara ya Kilimo, akichangia jambo wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
Bw. Zakaria Faustin Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la TNRF akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
Bi. Albina Burra kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) akijibu na kutoa ufafanuzi katika baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wadau katika mjadala wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
Kikao kazi cha kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini, kikiendelea.

TUSIRUHUSU MFUMO MPYA UNUNUZI WA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake waliokuwa wakibangua korosho wakati alipotembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin cha Mtwara, Oktoba 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake waliokuwa wakibangua korosho wakati alipotembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin kilichopo Mtwara, Oktoba 2, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



WAZIRI MKUU amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote inayolima korosho nchini wahakikishe wanasimamia vizuri zao hilo na wasiruhusu kuingizwa kwa mfumo mpya wa ununuzi ambao haujaeleweka kwa wadau na wanunuzi.

“Mabadiliko ya mifumo yalitolewa na baadhi ya viongozi ambao sio waaminifu, Serikali iko macho itawachukulia hatua viongozi wa vyama vya ushirika wasiokuwa waaminifu. Tunataka mfumo wenye manufaa ndio utumike.”

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 2, 2019) wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Mtwara baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo, wilayani Mtwara.

Waziri Mkuu amesema msimu wa korosho kwa mwaka huu unatarajiwa kutangazwa hivi karibuni, hivyo ni lazima kwa wakuu wa mikoa inayolima korosho wakajiandaa vizuri ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

Waziri Mkuu ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara kutojihusisha na ununuzi wa korosho kwa njia ya kangomba.”Kangomba imepigwa marufuku, watakaojihusisha moto utawawakia huko huko . Tunataka wakulima wenyewe ndio wanufaike”

Pia, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wakulima wa zao la korosho kuendelea kujiimarisha na wahakikishe wanajiwekea akiba kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo kwa sababu. “Serikali itaendelea kusimamia zao hili ili wakulima wapate tija.”

Mapema, Waziri Mkuu ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini na kukagua kazi ujenzi inayoendelea hospitalini hapo, ambapo amesema itakapomalizika itawapunguzia wananchi safari ya kwenda Muhimbili kufuata huduma.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imejikita katika kuboresha huduma mbalimbali za wananchi zikiwemo za afya, hivyo wananchi wa Kanda ya Kusini watapata matibabu ya kibingwa karibu na maeneo yao.

“Hakuna mashaka wala wasiwasi wa kupata huduma bora za afya kuanzia sasa na kuendelea kwa sababu Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuwezesha utaratibu mzuri wa kupata huduma za afya nchini.”

Ujenzi wa hospitali hiyo ya Rufaa ya Kanda ya Kusini unatarajiwa kukamilika Agosti 2020 na kwa sasa inajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa gharama ya zaidi ya sh. bilioni 15 na tayari Serikali imeshatoa zaidi y ash. bilioni sita.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali imetenga zaidi ya sh. Bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya

Alisema historia ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa Mkoani Mtwara ilianzia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi cha Mkoa cha tarehe 16 Januari 1979. Halmashauri Kuu ilijadili na kuazimia kuishawishi Serikali kujenga hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini itakayohudumia Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Waziri Ummy aliongeza kuwa hospitali hiyo inajengwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza ilianza mwaka wa fedha 2005/2006 kwa kazi ya upimaji wa mipaka na mwinuko wa ardhi kupitia kampuni ya Beacon Consult Ltd kwa gharama ya sh. 26,000,000 na ilikamilika ndani ya siku 30 za mkataba. Kwa sasa ujenzi huo upo katika awamu ya nne.

Awali,Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin kilichopo katika eneo la Msijute mkoani Mtwara na kukagua kazi ya ubanguaji pamoja na kuzungumza na watumishi wa kiwanda hicho ambao waliishukuru Serikali kwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda.

Benki Ya Exim Yazindua Akaunti Mpya za Akiba

$
0
0
Katika kuboresha huduma zake kwa wateja, Benki ya Exim Tanzania leo imezindua huduma mpya zinazolenga kuhamasisha wateja wake na jamii kwa ujumla kuhusu uwepo wa akaunti zake mpya tatu zinazofahamika kama Akaunti ya ‘Haba na Haba', Akaunti ya ‘Haba na Haba Plus’ pamoja na Akaunti ya ‘Mzalendo’ zote zikilenga kuwawezesha wateja hao kuhifadhi fedha bila makato ya mwezi kwa matumizi ya kuweka akiba na kwa shughuli za kila siku.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja jijini Dar es salaam mapema leo, Mkuu wa Idara ya Amana wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Agnes Kaganda alisema kuwa huduma hizo zinalenga wateja wote  ikiwemo wenye kipato cha chini, kati na kipato kikubwa.

"Akaunti hizi za Haba na Haba zinalenga kukidhi mahitaji ya wateja ambao wanahitaji kuhifadhi fedha zao kwa matumizi ya siku zijazo. Huduma zote zimelenga kutatua changamoto ya ukosefu wa namna iliyo bora ya kuhifadhi fedha miongoni mwa watanzania walio wengi bila kuwa na akiba isiyopungua pitia makato ya kila mwezi,’’ alisema.

Aidha, akifafanua kuhusu akaunti ya Haba na Haba, Bi Agnes Kaganda alisema inawalenga watu wenye nia ya kuweka akiba kwa ajili ya malengo ya baadae huku akitaja faida zinazombatana na ufunguaji wa akaunti hiyo kuwa ni pamoja na kunufaika na kiwango cha juu cha riba, hakuna makato ya mwezi na huduma ya haraka katika matawi yote ya benki hiyo,

“Pia inatoa fursa ya kuweka kiwango chochote cha akiba kwa wateja aidha kila mwezi au kwa muda wowote ambao wateja wataona ina manufaa kwao katika kutimiza malengo yao, Wateja wataweza dunduliza akiba zao kupitia simu za mikononi kutoka Mpesa/Tigopesa/Airtel money/Zantel kwenda kwenye akaunti ya Haba na Haba.’’ alitaja


Ili kufungua akaunti hiyo Bi Agnes Kaganda alisema mteja anapaswa kuwa na picha mbili sampuli ya hati ya kusafiria (passport size), nakala moja ya kitambulisho ambacho kinaweza kuwa hati ya kusafiria, kitambulisho cha kitaifa, au leseni ya udereva, Uthibitisho wa makazi au kibali cha makazi kwa raia wa kigeni na barua kutoka kwa serikali ya mtaa pamoja na fedha kiasi cha Tsh 50,000 kama kiasi cha kuanzia.

Akizungumza kuhusiana na akaunti ya Haba na Haba Plus, Bi Agnes Kaganda alisema inawalenga watu wenye kipato cha juu ambao pia kupitia akaunti hiyo wataweza kunufaika na viwango vikubwa vya riba.

 “ Akaunti hii pia inalenga kukidhi mahitaji ya wateja ambao wanahitaji kuhifadhi fedha zao kwa matumizi ya siku zijazo.’’ Alisema huku akitaja faida zitokanazo na ufunguaji wa akaunti hizo kuwa ni pamoja na kunufaika na kiwango cha juu cha riba na huduma ya haraka katika matawi yote ya benki hiyo.
“Pia inatoa fursa ya kuweka kiwango chochote cha akiba kwa wateja aidha kila mwezi au kwa muda wowote ambao wateja wataona ina manufaa kwao katika kutimiza malengo yao, Kunufaika na riba kubwa jinsi akiba yako inavoongezeka ikiwa sambamba na huduma zilizoongezwa thamani kutoka kwa Mameneja wanaohusika na mahusiano ya wateja. Wateja wataweza dunduliza akiba zao kupitia simu za mikononi kutoka Mpesa/Tigopesa/Airtel money/Zantel kwenda kwenye akaunti ya Haba na Haba.’’ alitaja
“Pia ili kufungua akaunti hii mteja anapaswa kuwa na picha mbili sampuli ya hati ya kusafiria (passport size), nakala moja ya kitambulisho ambacho kinaweza kuwa hati ya kusafiria, kitambulisho cha kitaifa, au leseni ya udereva, Uthibitisho wa makazi au kibali cha makazi kwa raia wa kigeni na barua kutoka kwa serikali ya mtaa pamoja na fedha kiasi cha Tsh 10,000,000 kama kiasi cha kuanzia.,’’ alitaja

Alitaja akaunti ya tatu kuwa ni Mzalendo akaunti ambayo itawawezesha wateja kupata huduma ya kufanya mihamala ya kila siku kupitia benki hiyo masaa 24 na siku saba za wiki bila kukatwa malipo ya kila mwezi  na pamoja na kupatiwa ATM kadi ya malipo bure.

Bi Agnes Kaganda alizitaja faida za akaunti hiyo kuwa ni pamoja na kutoa fursa kwa mmiliki wake kuweza kuindesha bila kuwekewa kiwango cha chini cha salio, haina ada ya uendeshaji,kupatiwa kadi ya malipo bure pamoja na manunuzi kwenye maduka yote yenye huduma ya POS (merchant Point of Sale) bila gharama yoyote.

‘Pia ili kufungua akaunti hii mteja anapaswa kuwa na picha mbili sampuli ya hati ya kusafiria (passport size), nakala moja ya kitambulisho ambacho kinaweza kuwa hati ya kusafiria, kitambulisho cha kitaifa, au leseni ya udereva, Uthibitisho wa makazi au kibali cha makazi kwa raia wa kigeni na barua kutoka kwa serikali ya mtaa’’ alisema.

SERIKALI YATAJA MAENEO YANAYOASHIRIA KUVUMBULIWA RASILIMALI YA MAFUTA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akifungua Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.  Kongamano hilo linawakutanisha wadau zaidi ya 592 kutoka Mataifa mbali mbali ikiwemo Austaralia, Brazili, Canada, China, Visiwa Vya Comoro, Ghana. Mengine ni Itali, India, Japani, Kenya, Msumbiji, Netherand, Nigeria, Afrika Kusini, Oman, Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Waziri wa Nishati na Madini Meldard Kalemani akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. Serikali ya Tanzania ametaja maeneo manne yanayoashiria matumaini ya ugunduzi wa rasilimali ya Mafuta nchini kwa siku za usoni kupitia shughuli za utafiti zinazoendelea. 

 Maeneo aliyoyataja ni pamoja na ya ukanda wa Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika na Kitalu cha Eyasi Wembere chenye ukubwa wa kilometa za mraba 19. 2. Kitalu hicho kinapita katika mikoa ya Arusha, Manyara, Simiyu, Shinyanga na Tabora. 

 Dk Kalemali ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 2, 2019 Jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Mafuta na Gesi. “Kuanzia eneo la Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, maeneo ya Pwani ya Tanga pamoja na Kitalu cha Eyasi Wembere, tunashukuru timu ya wataalamu ya Uganda inayosaidiana na Shirika letu la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kusaidia ushauri,” amesema Waziri Kalemani. 

 Akifungua Mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wanaokuja katika sekya ya Mafuta na Gesi. "Tunawakaribisha wawekezaji zaidi wajitokeze katika sekta hii ili kuweza kukuza uchumi wa nchi na kuzidi kutoa ajira wa jamii," amesema. Meza kuu: Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Angellah Kairuki akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Makamu mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim, Waziri wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib na Bi. Irene Batete aliyemwakilisha waziri wa Nishati Nchini Uganda. Waziri wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. Bi. Irene Batete aliyemwakilisha Waziri wa Nishati Nchini Uganda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Makamu mwenyekiti wa Chama Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdulsamad Abdurahim ambao ndiyo waandaaji akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. 
Wageni waalikwa toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019. 
Wageni waalikwa toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Wageni na viongozi wawakilishi Mabalozi toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.
Wageni na viongozi wawakilishi Mabalozi toka Mataifa mbali mbali waliohudhuria Kongamano la Tatu la Mafuta na Gesi Tanzania linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2-3, 2019.

Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA yawafikia wakazi wa Chalinze, TCRA yatoa Elimu ya Usajili wa laini kwa alama za vidole

$
0
0





Picha mbali za matukio katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja vya Bwilingu Chalinze mkoani Pwani.
 Mwananchi akiweka taarifa za usajili katika Mnada wa Chalinze wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA ikiwa imepita kwa ajili ya kutoa Elimu ya usajili wa laini kwa alama za vidole.
 Afisa wa TCRA akitoa elimu kwa Wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja  vya Bwilingu , Chalinze mkoani Pwani.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja. Vya Bwilingu Chalinze mkoani Pwani.

WAKAZI wa Chalinze  na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu ianzishwe imeenda katika Mikoa 15 lengo kuu ni nchi nzima kufiwa na Kampeni hiyo.

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA  Mhandisi Lawi Odiero amesema ni fursa kwa wananchi wa Chalinze na vyunga brake   katika Uwanja wa Bwilingu wajitokeze ya kujisajili laini za simu kwa alama za vidole na  huduma nyinginezo  kutokana  na kuwepo kwa mnyororo   wadau wa  mawasiliano. 

Mhandisi Odiero amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Amesema muda uliopo ni miezi mitatu hivyo Wananchi wakamilishe taarifa zinazohitajika katika kujisajili laini za simu  kwa alama  za vidole.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika mawasiliano ya simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Odiero  amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Hata hivyo Kanda ya Mashariki itapita katika wilaya zote katika mikoa mitano ya kanda hiyo ambayo Morogoro,Pwani Dar es Salaam, Lindi pamoja  Mtwara.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Mhandisi Odiero amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Kavishe.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

Ameongeza kuwa watahakikisha kila mwananchi anajisajili kwa alama za vidole kwani Watu wana haki ya kuwa na mawasiliano ya simu.
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images