Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1882 | 1883 | (Page 1884) | 1885 | 1886 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka kuwa mgeni rasmi, akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Duka maalum la huduma za Vodacom (Vodacom Shop) mjini Bariadi – Simiyu, jana.
  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Bw. Festo Kiswaga aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw. Antony Mtaka akiongea na wananchi katika uzinduzi wa Duka la VODACOM SHOP mjini Bariadi.
   
  Mgeni rasmi mkuu wa wilaya Bariadi Festo Kiswaga akimlisha keki Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo kanda ya Ziwa – Vodacom, Bw. Ayubu Kalufya mara baada ya uzinduzi rasmi wa Vodacom Shop mjini Bariadi.
  Meneja wa Vodacom Mkoa wa Simiyu, Chanila akimimina kinywaji cha Champagne kwa Mgeni rasmi na kiongozi mkuu kanda ya ziwa kampuni ya Vodacom ikiwa ni ishara ya kufurahia uzinduzi wa duka jipya
  Meneja wa Vodacom Mkoa wa Simiyu, Chanila akimimina kinywaji cha Champagne kwa Mgeni rasmi na kiongozi mkuu kanda ya ziwa kampuni ya Vodacom ikiwa ni ishara ya kufurahia uzinduzi wa duka jipya 


  Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Festo Kiswaga ambaye ndiye alikuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo na wadau mbali mbali wa Vodacom wakitoa zawadi kwa wasanii maarufu kutoka mjini Bariadi.

  Baadhi ya wananchi wilayani Bariadi wakisubiri kushuhudia uzinduzi wa duka maalum la Vodacom.
  Baadhi ya watumishi na wadau wa kampuni ya Vodacom wakiwa katika maandamano ya furaha ya uzinduzi wa Duka maalum la Vodacom mjini Bariadi mkoani Simiyu. 
   

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah wakimsikiliza Mama wa mtoto Aidan Mfunya mkazi wa Kigoma ambaye mtoto wake anasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo ambaye wadau wake mbalimbali walimchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Hadi sasa jumla ya Watoto 50 wameshafanyiwa upasuaji kwa ufadhili wa Mhe. Makonda na wadau wake na hali zao zinaendelea vizuri.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wazazi ambao watoto wao wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto ambao wametibiwa kwa ufadhili wa wadau waliomchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah ambaye kampuni yake imechangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.
   
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah wakimjulia hali mtoto Jasin Ally mkazi wa Arusha ambaye anasubiri kufanyiwa upasuaji katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo ambaye wadau wake walimchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kampuni ya PUMA Energy imemuunga mkono kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah wakimjulia hali mtoto Doreen Likweri ambaye anasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ambaye wadau wake walimchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania imemuunga mkono mkuu wa mkoa huyo kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiwaeleza  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dominic Dhanah huduma zinazotolewa katika chumba cha wagonjwa watoto walioko katika uangalizi maalum (JKCI) wakati ugeni huo ulipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto waliotibiwa kwa ufadhili wa wadau waliomchangia fedha mkuu wa mkoa huyo kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Hadi sasa jumla ya Watoto 50 wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimfundisha jinsi ya kupiga picha mtoto Jovin Muniko ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo na wadau wake kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Dominic Dhanah ambaye kampuni yake imemuunga mkono Mhe. Makonda na kuchangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Dominic Dhanah wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), wazazi na Watoto ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo mara baada ya kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania kukabidhi mfano wa hundi ya shilinngi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.

  Zainabu Mundera mkazi wa Kyela mkoani Mbeya akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda kwa kumfadhili mtoto wake kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Hadi sasa jumla ya Watoto 50 wameshafanyiwa upasuaji kwa ufadhili wa Mhe. Makonda pamoja na wadau wake na hali zao zinaendelea vizuri.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na baadhi wa wafanyakazi wa chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) na upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto ambao wamefanyiwa na wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo pamoja na wadau wake.Picha na JKCI
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimfundisha jinsi ya kupiga picha mtoto Jovin Muniko ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo kwa ufadhili wa mkuu wa mkoa huyo na wadau wake kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Dominic Dhanah ambaye kampuni yake imemuunga mkono Mhe. Makonda na kuchangia kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 20.

  0 0


  Wachezaji chipikizi wa mpira wa miguu kutoka Afrika waliodhaminiwa na QNET wahadhithia mambo waliyoyaona Manchester City Watoto wamewakilishwa na mwandishi wa habari na Meneja wa PR wa QNET bwana Akoua Maxime.
  Wachezaji chipikizi wa mpira wa miguu kutoka Afrika waliodhaminiwa na QNET wahadhithia mambo waliyoyaona Manchester City Mkurugenzi wa Masoko wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Ivory Coast, Mashabiki 3 wa mpira wa miguu waliodhaminiwa na QNET, Meneja wa PR wa QNET – SSA na Meneger wa Mambo ya Sheria wa QNET – SSA.

  ………..

  Wachezaji wa mpira wa miguu chipukizi wa Afrika waliochaguliwa kutoka nchi za Ghana, Ivory Coast na Cameroun tarehe 31 August 2019, wameeleza fursa hiyo ya pekee na yenye kuhamasisha wakati wa mahojiano na vyombo vya habari jijini Abidjan, mji mkuu wa Ivory Coast. QNET iliwaalika waandishi wa habari katika mechi ya kupeana uzoefu kati ya Manchester City FC na Brighton & Hove Albion; Waandishi hao walitazama ligi ya mabingwa na kuzungumza na wachezaji chipukizi kutoka Afrika. 

  QNET kampuni ya biashara ya mtandao inayoongoza ulimwenguni, kama sehemu ya jitihada zake za kuendeleza vipaji na kama namna ya kurudisha fadhila kwa jamii ambako inafanyia kazi, imedhamini wachezaji watatu vijana wa kiafrika kwenda kuhudhuria programu ya Lugha na Mpira wa Miguu ya kipindi cha msimu wa joto katika shule ya mpira wa miguu cha Manchester City jijini Manchester. Programu hii ilikua ya wiki mbili yenye lengo la kuhamasisha na kufundisha mpira wa miguu na kozi ya Lugha ya Kiingereza kwa wachezaji chipukizi wenye umri kati ya miaka 12-17. Programu hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 28 Julai mpaka tarehe 12 Agosti, 2019 katikati ya viwanja vya mafunzo vya timu ya Manchester City katika shule ya Mpira wa Miguu ya klabu ya City. 

  Kwa mujibu wa Hamza Gaveh, wachezaji chipukizi kutoka Ghana walisema: “Ilikuwa ni moja kati ya wakati mzuri sana katika maisha yangu. Nimepata fursa ya kupata mafunzo pamoja na klabu bora zaidi ya mpira wa miguu katika mashindano ya ligi za uingereza. Nimejifunza mengi kutoka katika vipindi vya mpira na kutoka katika vipindi vya Lugha ya Kiingereza. Nilikuwa kinara katika darasa langu la lugha ya kiingereza na katika michezo, nimejifunza zaidi kuhusu kufanya kazi kwa pamoja katika timu na mikakati ya kijihami. Nimepata marafiki wapya kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Urusi na katika nchi za Sacandinavia.”

  Baba Ndiaye kutoka Ivory Cost amesema: “Japo kuwa nimesafiri sehemu kadhaa kucheza mpira wa miguu, Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester City ni sehemu bora zaidi kati ya zote nilizowahi kwenda. Baada ya vipindi vya kuhamasisha tulivyovipata, sasa ninajihisi kwa kiasi kikubwa kwamba siku moja nataka kuchezea klabu ya manchester City. Ninafanya vizuri sana darasani na natumaini kufanya vizuri katika mpira wa miguu na kuchezea Ligi ya Maibingwa uingereza. 

  Na Yvan Noh Nafeng kutoka Cameroun kwa furaha kubwa alisimulia: “Sikuwahi kusafiri kwa ndege hapo awali na ilikuwa ni mara ya kwanza kupata hati ya kusafiria ya kimataifa. Tukio zima hili lilikuwa ni kitu kikubwa sana ambacho hakijawahi kutokea maishani mwangu. Nawafahamu wachezaji wengi chipukizi kutoka katika klabu yangu ya mpira wa miguu nchini Cameroun wanaotaka kuwa kama mimi, nimepanga kubakia na tabia njema na kuwa makini. Vile vile ninapanga kuwafundisha wenzangu baadhi ya masomo ya mpira wa miguu niliyojifunza”.

  Akiongea katika sherehe, Bwana Rajesh Rao, Mkurugenzi wa Mkuu wa QNET wa Mahusiano ya Kimataifa, alisema. “Programu hii ni sehemu ya jitihada za QNET za kuendeleza vipaji, kurudisha kwa jamii ambako tunaendesha shughuli zetu pamoja na jamii kwa ujumla. Tunaamini kwamba fursa waliyopata kutoka Klabu ya Manchester City FC imewahamasisha vijana hawa kutafuta viwango vya juu katika maisha yao”.

  Akiongea kuhusu ushirikiano kati ya Manchester City, QNET na programu ya mpira wa miguu, Bwana Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET kanda ya Afrika, amesema “QNET ni biashara ambayo inaamini na kudumisha uendelevu. Tunaamini katika kuendeleza na kukuza vipaji katika ngazi zote. Udhamini wa Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City kama mshirika wa mauzo ya moja kwa moja na mdhamini wa lebo za mikononi (Sleeve Sponsor) ni moja kati ya jitihada zetu katika mpira wa miguu pamoja na hamasa ambayo mpira huo unaambatana nao duniani kote. Kupitia Ushirikiano huu, tumepata fursa ya kupeleka watoto wanaotokea katika familia zenye kipato cha chini Afrika kwenda katika klabu za mpira wa miguu na shule ya lugha ya kiingereza jijini Manchester; jambo hili kweli limebadilisha maisha ya watoto hawa, Watoto tunaowasherehekea leo ni matunda ya ushirikiano huu. Tunatumaini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutafuta njia mpya za kibunifu za kushirikiana na kuwafikia wadau wetu wote.”

  QNET inaendelea kupanua uwepo wake katika sehemu mbalimbali katika bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambako inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kuwasaidia kubadilisha maisha yao kuwa bora zaidi. Mbali na ushirika katika michezo, QNET vile vile ni kampuni ambayo imewekeza katika kuwajibika kwa jamii, kurudisha na kutoa kwaajili ya manufaa ya jamii na jambo hili linafanyika katika maeneo yote ambako QNET inaendesha shughuli zake. Katika mwezi Novemba mwaka 2018, Kampuni ya QNET ilitunukiwa tuzo ya e-Commerce CSR Company kuwa ni kampuni bora ya biashara ya mtando kwa mwaka huo, ambayo ilitolewa na Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirka kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa.)

  0 0


  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kitengo cha forodha Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya kupitia Idara ya Afya, Usafi wa mazingira na Udhibiti wa taka ngumu, imeteketeza bidhaa zilizoingizwa kwa njia ya magendo zenye thamani ya sh. milioni 25.

  Akizungumza wakati wa uteketezaji huo ,katika dampo la Sanzale lililopo Kata ya Magomeni ,Ofisa Mwandamizi wa Forodha Bagamoyo Noel Makere alisema bidhaa hizo zilikamatwa katika doria zinayofanywa na ofisi hiyo.

  Alitaja bdhaa hizo ni pamoja na betri dazeni 12, matairi ya magari na pikipiki yaliyotumika (Used Tyres) 400, Nguo za mitumba balo 9 na vilainishi ‘lubricants’ lita 960.Bidhaa nyingine ni mafuta ya taa lita 300, Friji 2, kompresa za friji 12 na sabuni za unga Kilo 30 .“Serikali imepiga marufuku bidhaa hizi kuingizwa nchini kwani hazifai kwa matumizi ya binadamu na hazina ubora”

  “Matairi haya 400 tunayoteketeza yamekatazwa kabisa kuingizwa na kutumika nchini, bidhaa kama friji na mitumba ni bidhaa zilizozuiwa kuingizwa nchini,”alisema Makere.

  Makere alibainisha , bidhaa zote hizo zilizoteketezwa zimethibishwa na shirika la viwango nchini (TBS) kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.
  Alitoa onyo kwa wafanyabishara kuwa wazalendo na kufuata sheria na taratibu za uingizaji bidhaa nchini hususani ulipaji wa kodi ili kuepuka usumbufu na hasara zisizo za lazima.

  Nae ofisa Afya wa Wilaya ya Bagamoyo Mohamed Farah aliwaasa ,wafanyabiashara kutii sheria bila shuruti na kuhakikisha bidhaa wanazoingiza kupitia bandari ya Bagamoyo, hazina madhara kwa watumiaji ili kuepuka madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na matumizi ya bidhaa zilizokosa ubora na zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.
   

  0 0

   
  Meneja wa benki ya NMB Tawi la Mirerani Allan Kombe (katikati) na wadau na watumishi wa benki hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye tafrija ya wiki ya huduma kwa wateja.
  Watumishi wa benki ya NMB Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
  Meneja wa benki ya NMB Tawi la Mirerani, Allan Kombe (kushoto) akiwa na wadau na watumishi wa benki hiyo kwenye tafrija ya wiki ya huduma kwa wateja.

  *******************************
  Na mwandishi wetu, Mirerani .

  Wafanyakazi wa benki ya NMB Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamezindua wiki ya huduma kwa wateja kwa kutangaza mpango mpya wa mikopo ya ‘Afya Loan’. 

  Meneja wa NMB Tawi la Mirerani, Allan Kombe akizungumza na wadau na wafanyakazi wa benki hiyo kwenye tafrija ya wiki hiyo alisema Afya Loan ni huduma mpya maalum ya mikopo kwa watu au taasisi binafsi. 

  Kombe alisema Afya Loan ina lengo la kuwakopesha wadau binafsi wenye maduka ya dawa, maabara, zahanati na vituo vya afya vya watu binafsi. 

  Alisema lengo la kuanzishwa kwa mikopo hiyo ya ‘Afya Loan’ ni kwa ajili ya kuimarisha huduma hizo za afya zinazotolewa na watu binafsi au taasisi binafsi.
  “Mpango huo wa ‘Afya Loan’ utakuwa endelevu na wiki hii ya huduma kwa wateja itaendelea kwa mud wote wa mwezi huu wa Octoba,” alisema Kombe. 

  Ofisa Tarafa ya Moipo, Joseph Mtataiko aliwapongeza wafanyakazi wa benki ya NMB Tawi la Mirerani kwa kutoa huduma zao ipasavyo kwa wateja wanapofika kupata huduma za kibenki. 

  Mtataiko alisema watumishi wa serikali, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, wachimbaji madini na watu wa kada zote za Mirerani wanaopata huduma kwenye benki hiyo wanapongeza huduma nzuri zinazotolewa na benki hiyo. 

  Meneja wa huduma kwa wateja wa benki ya NMB Tawi la Mirerani, Bahati Nelson aliwakaribisha wadau wote wa benki hiyo kufika ofisini kwao ili wapatiwe huduma. 

  Bahati alisema benki ya NMB Tawi la Mirerani ipo pembeni ya barabara kuu ya Mirerani-Okresumet mbele kidogo ya kituo cha polisi Mirerani.

  0 0

  Naibu Kamishina (Operesheni) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. Albert Kingu akimkabidhi Mhe. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ‘Road map’ na makubaliano ya malengo waliyojiwekea Mamlaka hiyo na Mameneja wa Mikoa katika kuhakikisha wanafikia malengo ya ukusanyaji mapato katika Mikoa yao.
  Kaimu Meneja wa Mkoa wa Kodi wa Ilala, Bw. Steven Kuzeni akieleza taarifa ya utekelezaji wa Ofisi yake kwa Mhe. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea Ofisi hiyo jijini Dar es Salaam.
  *******************************

  Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar es Salaam

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuweka mifumo imara ambayo itamtambua kila mfanyabiashara na bidhaa anayouza ili kuweza kukusanya kodi stahiki na kupunguza mianya ya ukwepaji kodi. 

  Mhe. Kijaji aliyasema hayo kwa viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa Mikoa ya Kodi ya Ilala na Kariakoo, wakati wa ziara yake ya kutembelea Ofisi za Mamlaka hiyo inayoendelea Jijini Dar es Salaam. 

  Dkt. Kijaji alisisitiza kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ina jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba inavuka lengo la makusanyo iliyojiwekea ili kuweza kumsaidia Mhe. Rais DKt. John Pombe Magufuli, atekeleze majukumu yake kwa ufanisi na kulifikisha Taifa pale alipodhamiria.

  “Naiagiza Mamlaka kuanza zoezi la kukagua watumiaji wote wa mashine za utoaji risiti za kieletroniki (EFD) hasa kwa wafanyabiashara wa Kariakoo ili kuhakikisha kila anayeuza anatoa risiti na anayenunua anadai risiti na kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza makusanyo na kupelekea Taifa letu kujiendesha kupitia fedha zetu wenyewe kwa kuwa hakuna Taifa huru bila mapato’’ alisisitiza Dkt. Kijaji 

  Aliwataka Maafisa wa TRA kutokaa ofisini badala yake wawatembelea wafanyabiashara ili kuhakiki matumizi ya mashine za utoaji wa risiti za kieletroniki (EFD).

  Awali Meneja wa Ofisi ya Mkoa wa Kodi wa Kariakoo, Bw. Alex Katundu alimueleza Mhe. Kijaji kuwa Mkoa wake wa kikodi una jumla ya wafanyabiashara waliosajiliwa na Mamlaka hiyo 22,279 na kati ya hao wafanyabiashara 16,068 wanatumia mashine za EFD. 

  Alisema Mkoa wa kodi wa Kariakoo kwa mwaka 2018/19 walidhamiria kukusanya shilingi bilioni 138.66 lakini walifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 109 ambayo ni sawa na asilimia 79 ya malengo waliyojiwekea. 

  Katika Mkoa wa kikodi wa Ilala, Kaimu Meneja Bw. Steven Kuzeni amesema katika kuhakikisha Mkoa wake unakusanya ipasavyo kodi ya Majengo, wamedhamiria kusajili majengo yote yanayozunguka Mkoa huo wa kikodi na hadi sasa wameshasajili majengo katika kata 26 kati ya kata 32 zilizopo katika eneo lake. 

  “Ofisi yangu kwa mwaka 2019/20 ina mkakati kabambe wa kuhakikisha inaongeza idadi ya walipa kodi ya mapato na wale wa ongezeko la thamani (VAT)” Aliongeza Bw. Kuzeni.

  Katika hatua nyingine Kijaji amewapongeza watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuvuka lengo la makusanyo kwa mwezi Septemba ambapo imekusanya sh. trilioni 1.76, kiasi ambacho hakijawahi kukusanywa tangu nchi ipate uhuru na kuwahimiza kukaa pamoja na Taasisi zote zinazofanya kazi kwa karibu na Mamlaka hiyo ili kuona ni kipi kinaweza kuboreshwa zaidi ili kuwapa fursa Watanzania kulipa kodi bila Serikali kuwalazimisha.

  0 0

   TMDA imechangia taulo za kike pakiti 2,448 kwa wanafunzi wa kidato cha nne walio kambi ya kitaaluma ili kuunga mkono jitihada za Mkoa wa Simiyu katika kukuza elimu ili kumuunga mkono Mkuu wa mkoa huo Bw. Anthony Mtaka.

  Pichani ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) akimkabidhi Taulo za kike Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso aliyekuwa Mgeni rasmi wa hafla hiyo katika hafla hiyo Katikati ni Mkuu wa mkoa huo Anthony Mtaka.
  Bi. Gaudensia Simwanza Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ummaakiwa pamoja na wanafunzi wa kike walioweka kambi ya kitaaluma mkoani Simiyu wakionesha taulo hizo.

  Wanafunzi wakishangilia mara baada ya kupokea taulo hizo.

  0 0

    Mratibu wa Mbio za Rock City Marathon, Bw. Kasara Naftal akionyesha medali ambayo washiriki wote watakaomaliza mbio hizo watapatiwa.
    Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano ya mbio za Rock City Marathon, Bw. Samwel Gisayi (Wa pili kushoto) akizungumzia usajili wa washiriki wa mbio hizo, mapema leo katika mkutano na waandishi wa Habari.
  Muwakilishi wa washiriki wa mbio za Rock City Marathon, Bw. Frank R. Mtweve akionyesha medali tofauti watakazopatiwa washindi wa mbio hizo.


  Ikiwa zimebaki wiki mbili kabla ya kufanyika kwa mbio za Rock City Marathon jijini Mwanza, wadau mbalimbali wanaotarajia kushiriki katika mbio hizo wameonyesha kufurahishwa na zawadi zitakazotolewa kwa washindi na washiriki ikiwemo medali na fedha taslimu zaidi ya Sh Mil 30.

  Mbio hizo zilizojinyakulia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi zinatarajiwa kufanyika Octoba 20 mwaka huu kwenye Viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall huku wadau mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi serikalini akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella wakitarajia kushiriki katika mbio hizo. 

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Kasara Naftal amesema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi na tano nao pia wakiibuka na zawadi za medali na pesa taslimu. 

  Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, Bw Kasara alisema pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 2/- kila mmoja, sh. Mil 1/- kwa washindi wa pili na sh. Laki 7/- kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi na tano wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja. 

  “Kuhusu mbio za kilomita tano ambazo zitahusisha washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporates) tunatarajia kwamba zitaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk Philis Nyimbi sambamba na washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani albino ambapo zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa washindi watatu wenye ualbino pekee.” Alisema. 

  Bw Kasara aliongeza kuwa kwa washindi wa mbio za kilomita mbili na nusu zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 watapatiwa fedha taslimu. 

  Mbio hizo zilizoanzishwa miaka kumi iliyopita zinatarajiwa kupambwa naburudani mbalimbali ikiwemo ngoma za asili sambamba na maonesho ya waadau mbalimbali wakiwemo wadhamini wa mbio hizo ambao ni pamoja na kampuni za TIPER, Pepsi, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). 

  Wadhamini wengine ni pamoja na kampuni ya uwakili ya Lis Law Chambers & Consultants, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Metro FM, Mwanza Water, Pigeon Hotel, Cask Bar, Kampuni ya Usafi ya SDN na Kampuni ya Ulinzi ya Garda World. 

  Akizungumzia usajili wa mbio hizo Bw. Samwel Gisayi kutoka idara ya mahusiano ya mbio hizo alitoa wito kwa washiriki kuendelea kujisajili kupitia vituo na mawakala wa mbio hizo katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Dodoma, Pwani na Arusha 

  ‘’Kwasasa usajili wa mbio hizo unaendelea kupitia vituo mbalimbali katika mikoa ya Mwanza (Rock City Mall, Pasiansi Afro Twist Gym), Dodoma (Shabiby Bus Terminal), Dar es Salaam (Shamo Tower, Imalaseko Super Market (Posta), Heleana Fashion – Dar Free Market), Arusha pamoja na Bagamoyo mkoani Pwani.’’ 

  “Pia usajili unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia website yetu ya Rock City Marathon ambayo ni www.rockcitymarathon.co.tz’’ 

  Naye muwakilishi wa washiriki Bw. Frank R. Mtweve alielezea kufurahishwa kwake na zawadi zinazotolewa na waandaaji wa Rock City Marathon. 

  “Rock City Marathon ndio mbio pekee hapa nchini ambazo zinatoa zawadi kubwa kuliko na washiriki wake wote watakaomaliza mbio kupata medali. Na pia ndizo pekee ambazo zinashirikisha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism).” Alisema

  0 0  Kaimu Mkurugenzi wa PCI, Jennifer Waugaman akiwa na Mratibu wa PCI ncuini, John Lafa(kulia) wakipewa zawadi baada ya kuzindua mradi huo.  Mwandishi wetu,Monduli

  Wafugaji wa wilayani tatu za mkoa wa Arusha,watakuwa wakifikia malisho na maji ya mifugo yao kwa kutuma ujumbe wa simu kuulizia eneo lenye maji na malisho na kujulishwa.

  Mradi huu umezinduliwa jana na shirika la kimataifa la PCI ,l, katika kijiji cha Arkaria wilayani Monduli na utatekelezwa pia wilaya za Longido na Ngorongoro ambazo zina idadi kubwa ya mifugo.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais wa PCI, Carrie Hetessler-Radelet alisema, wafugaji kupitia simu zao za mkononi, baada yakupakuwa application ya Afriscout watatuma bure ujumbe kwenda15054 kuuliza malisho na maji.

  Hetessler –Radalet amesema baada ya kuuliza,mtandao huo utaonesha ramani za sehemu ya maji na malisho ambayo imepigwa angani.

  Amesema mradi huo, utawezesha wafugaji kuacha kusafiri muda mrefu kusaka malisho, kuharibu mazingira lakini pia utapunguza vifo vya mifugo na adha ya wafugaji kushindwa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.

  Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, Jennifer Waungaman amesema mradi huo ambao unatarajiwa kuwanufaisha sana wafugaji.“tunawaomba wafugaji kutumia huduma hii ambayo pia itawasaidia kusimamia vizuri nyanda za malisho yao”alisena

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu mkurugenzi endeshji wa malisho na vyakula vya mifugo,Dk Asimwe Rwiguza alisema mradi ho una manufaa makubwa kwa wafugaji na amelitaka shirika hilo kupanua huduma hiyo nchi nzima.

  Mfugaji John Laizer amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwao na itaondoa tatizo la mifugo kufariki wakati wa kiangazi na migogoro na wakulima.Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Monduli,Joseph Rutabingwa alisema halmashauri ya Monduli itaupa ushirikiano mradi huo ili wafugaji wanufaike zaidi.

  Mradi huu pia unatekelezwa katika nchi tatu barani ambazo ni Tanzania, Kenya na Ethiopia na shirika hilo linafanya kazi katika nchi 16 Duniani.

  0 0

  Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Equity, Dk. James Mwangi, akiwaonesha Logo mpya ya Benki ya Equity, Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo Uganda, Apollo Makubuya (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Logo hiyo iliyozinduliwa Makao Makuu ya benki hiyo Upperhill, Nairobi nchini Kenya Oktoba 2 mwaka huu. 
  ************************************

  NAIROBI, Kenya

  BENKI ya Equity imezindua muonekano mpya wa logo ya benki hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuboresha utendaji kazi wa benki hiyo katika huduma na uboreshaji wa maisha ya watu ikidhamiria kuwa benki ya mfano Barani Afrika.

  Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Equity, Dk. James Mwangi, zilisema kuwa muonekano mpya utaleta ufanisi katika huduma za kifedha, hasa kwenye uwanja wa utoaji wa huduma kielektroniki.

  Alisema logo hiyo ni ya kipekee na imekuja wakati mwafaka katika kuleta mapinduzi kwa wateja wao, baada ya kupata ujuzi kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mjini hapa, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu, Dk. James Mwangi alisema, 

  “Muonekano wetu mpya una akisi mtazamo mpya wa kibiashara, wateja na kuleta matokeo bora kwenye benki kuelekea katika mafanikio ya baadae pasipo na kusahau tulikoanzia”.

  Alisema Benki ya Equity imedhamiria kuwa na ubora wake kwa kuzingatia malengo na dhamira ya kuwahudumia wateja kwa kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kupitia huduma zenye ubunifu na za kisasa. Uimarishaji wa huduma za kielektroniki pia utasawadia wateja wa Equity Bank kufungua fursa mpya za kibenki katika mfumo wa kielektroniki kwa kuangazia kuleta ufanisi katika ugunduzi wa huduma zake za kibiashara.

  Equity Bank iliyoanza kutoa huduma miaka 35 iliopita na hadi sasa inatoa huduma za kimkakati katika nchi 9 za Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, South Sudan, Rwanda, Democratic Republic of Congo (DRC), Zambia, Msumbiji na Ethiopia.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Makampuni ya Equity, Mhandisi. Raymond Mbilinyi (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti (katikati) na Mkurugenzi asiyekuwa na majukumu, Dino Stengel wakifurahia jambo wakati wakipiga picha ya pamoja mbele ya bango lenye Kogo mpya ya Benki hiyo ya Equity wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Oktoba 2, mwaka huu Makao Makuu ya benki hiyo, Upperhill, Nairobi nchini Kenya.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Menejmenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira katika kikao cha kazi ikiwemo Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Mazingira, kikao hicho kimefanyika leo Octoba 05,2019 katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba Jijini Dodoma.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda mti pamoja na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kufungua Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Nakonde Zambia . PICHA NA IKULU

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kufungua Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Nakonde Zambia

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika eneo hilo la Tunduma mkoani Songwe.

   Wafanyakazi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania na Zambia wakiwa tayari kwa kutoa huduma katika eneo hilo la mpakani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kuwasili katika eneo la Nakonde Zambia.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakisalimia wananchi mara baada ya kuwasili katika Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania. 
   Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu akifurahia hotuba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakisalimia wananchi mara baada ya kuwasili katika Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

   Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kuwasili Tunduma mkoani Songwe kwa ajili ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.


  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mbegu za pamba katika kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mandewa, katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Dkt. Riyaz Haider. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimpa zawadi ya cheti, fedha,na baiskeli, mkulima wa zao la pamba kutoka Ikungi, Juma Shabani, wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, kilichopo Mandewa, katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mtego wa molasis, wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, kilichopo Mandewa katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Dkt. Riyaz Haider. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, Dkt. Riyaz Haider, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mandewa, katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia pamba katika kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mandewa, katika Manispaa ya Singida, Oktoba 6.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU AKASIRISHWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NDAGO WILAYANI IRAMBA

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya cha Ndago, wilayani Iramba mkoani Singida kwa sababu uko chini ya kiwango.

  Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Oktoba 6, 2019), wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ndago mara baada ya kukagua majengo ya kituo hicho.

  “Nimepita kote nchini kukagua vituo hivi lakini hapa wamenikasirisha. Wamenileta kwenye jengo nilikaguem nikajua ni jipya kumbe ni la zamani. Lazima nikiri kwamba fedha yetu hapa haijakamilika, jengo la mama na mtoto halijakamilika. Nilipouliza linakamilika lini, wananijibu tuko kwenye final touches (tuko hatua za mwisho),” amesema.

  “Jengo lile halivutii kabisa, wanaotoa maelezo hakuna kinachoeleweka. Sijaridhishwa kabisa na hali hii. Jengo la upasuaji nalo pia nimeona ni la zamani. Hii ina maana hamjajenga jengo jipya. Mimi nataka nione jengo jipya hapa,” amesisitiza.

  Alipomuuliza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw, Leno Mwageni amebakiza kiasi gani cha fedha katika sh. milioni 400 ambazo zililetwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo, Mkurugenzi huyo alijibu kwamba hakuna kiasi cha fedha kilichobakia.

  Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao kwamba Mheshimiwa Rais John Magufuli anatambua wao hawana uwezo, na tena wanaugua na kuna watu ambao wanapoteza maisha kwa sababu hawawezi kufika kwenye tiba kwa wakati.

  “Vituo vya afya vinajengwa kila mahali nchini ili wewe mwananchi usilipe nauli kwenda Iramba mjini au Singida mjini kutafuta tiba, bali upate vipimo vyote hapa hapa ulipo. Vipimo vya magonjwa yote vinapatikana hapa hapa.”

  “Fedha hizi zikiletwa zinataka pajengwe maabara, chumba cha upasuaji mdogo na mkubwa, chumba cha huduma ya mama na mtoto, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mkuu wa kituo, lakini hapa Ndago fedha yetu imeharibika,” amesema.

  Alipoenda kukagua chumba cha kuhifadhia maiti, Waziri Mkuu alikuta limewekwa mlango wa mbele tu na vyumba vingine vyote havina milango wala mabomba na masinki hayajakamilika tofauti na taarifa aliyopewa kwamba jengo hilo liko tayari.

  “Mkurugenzi nimekuta wagonjwa wamelazwa katika baadhi ya vyumba na kazi haijakamilika. Huwezi kupanga vifaa wakati ujenzi unaoendelea ili kumdanganya Waziri Mkuu. Na wala hunidanganyi mimi bali unawadanganya wananchi.”

  “Ninazo taarifa kwamba jana mlikesha kupanga vitu ndani. Nenda kaondoe vifaa vyote hadi ujenzi utakapokamilika ndipo madaktari warudi kuendelea na kazi. Serikali hii haiwezi kuvumilia vitu vya hovyo. Hatua kali zitachukuliwa,” alisisitiza.

  Mapema, Mbunge wa jimbo hilo, Bw. Mwigulu Nchemba alimweleza Waziri Mkuu kwamba alichangia mifuko 400 ya saruji na wananchi wa kata hiyo walichangia mawe na ujenzi wa msingi.

  Alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa vituo vya afya. “Tunashukuru kwa sababu fedha hizi zimekuja kamili, na siyo kwa mafungu. Wananchi wamechangia nguvu zao na mimi mwenyewe nilitoa mifuko 400 ya saruji,” alisema.

  Alitumia fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu awasaidie wananchi wa kata ya Ndago wapate barabara ya lami ya kutoka Singida-Sepuka-Ndago-Kizaga yenye urefu wa kilometa 76. “Hii ni tarafa kubwa kuliko zote na huku ndiko uzalishaji mkubwa uliko. Hii barabara imeshafanyiwa upembuzi yakinifu, kilio na furaha ya wana-Ndago ni barabara hii kuwekwa lami,” alisema.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia aliyeshika utepe, viongozi wa mkoa wa Rukwa, Mawaziri, viongozi wa Dini pamoja na Chama, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Ufunguzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale mara baada ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 223.21 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Laela mkoani Rukwa.
   Sehemu ya Barabara ya Tunduma –Sumbawanga km 223.21 iliyofunguliwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Laela mkoani Rukwa.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Laela mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Chiwanda Tunduma mkoani Songwe mara baada ya kusimama wakati akielekea Sumbawanga mkoani Rukwa.
   Wananchi wa Ikana wakisangilia mara baada ya kumuona  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye eneo hilo wakati akielekea Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na maaskari wa Jeshi la Polisi wakati akielekea kukagua kituo cha polisi cha Laela mkoani Rukwa mara baada ya kufungua barabara ya Tunduma-Sumbawanga. PICHA NA IKULU

  0 0


  Wasanii wa Bongo fleva Bill Nas na Nandy wakitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.
  Msanii wa Bongo fleva Whozu, akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.
  Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja, akitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.
  Mashabiki wa burudani wakionyesha shangwe la levels za Saizi Yako kwenye tamasha la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.   Msanii wa Bongo fleva Maua Sama, akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.

  Wasanii wa Bongo fleva Saida Karoli na Chege Chigunda, wakitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta mjini Muleba mkoani Kagera.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na watu wenye mahitaji maalumu,kuilia kwake ni Philipo Meli Mwenyekiti wa watu wasioona mkoa wa Arusha ,kushoto kwake ni Mhandisi Imelda Salum Mkuu wa kanda ya ya kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA na wa kwanza mulia ni Katibu wa chama cha Viziwi Tanzania tawi la Arusha .Picha na Vero Ignatus.
  MHANDISI Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona
  Julius Felix Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini kanda ya Kaskazini TCRA ,wengine ni washiriki wa semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo kwaajili ya kuwajengea uelewa juu ya usajili wa laini za simu kwa kutumia mfumo wa alama za vidole.
  Jan Kaaya ni Mhandisi Mwanadamizi wa Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA).Picha na Vero Ignatus
  Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus
  MHANDISI Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini (TCRA akizungumza na watu wenye mahitaji maalum Viziwi na watu walemavu wasioona katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus.
  Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus.
  Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Arusha.Picha na Vero Ignatus.
  Mhandisi Imelda Salum Mkuu wa kanda ya kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA akizungumza katika uzinduzi wa semina hiyo ya siku moja ya wadau wa mawasiliano ,kutoka makundi mawili Viziwi na walemavu wa kutoona.Picha na Vero Ignatus.
  Mmmoja wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wa siku moja ulioandaliwa na TCRA Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus.
  Mmmoja wawakalmani wa lugha ya alama wakiwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kuelewa kile kinachoendelea katika mkutano huo wasiku moja ulioandaliwa na TCRA Mkoani Arusha.Pcha na Vero Ignatus
  Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini (TCRA)Viziwi na walemavu wasioona .Picha na Vero Ignatus.
  Mmoja wa wakalimani wa lugha ya aklama akisaidia ujumbe ufike kwa waandaaji wa semina ya watu wenye mahitaji maalum (TCRA).Picha na Vero Ignatus


  Na.Vero Ignatus,Arusha .
  Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kanda ya kaskazini imefanya mkutano wa siku moja na wadau wa mawasiliano wenyenye mahitaji maalumu, wakiwa katika makundi mawili Viziwi na walemavu wa kutokuona.


  Lengo haswa la mkutano huo ni kutoa uelewa kwa watu wenye mahitaji maalum, kuhusu zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya mfumo wa alama za vidole ,pia kuangalia changamoto mbalimbali walizonazo katika huduma za Mawasiliano


   Gabriel Daqqaro ni mkuu wa wilaya ya Arusha amesema kuwa semina hiyo itasaidia ,ukizingatia kwasasa kuna changamoto nyingi za mitandao japo kuwa  zipo faida zake kama vile kupashana habari,kuelimisha,kuburudisha na kukataza yale mambo mabaya katika jamii katika maendeleo yanayokwenda kwa kasi.


  Amesema kuna makosa ya uhalifu wa kimtandao ,watu wasiowaaminifu wanaotuma jumbe za kulaghai wa wananchi,kwasababu hiyo serikali imeelekeza  laini zote za simu zisajiliwe kwa alama za vidole ,hivyo ameipongeza TCRA kwa kuona watu wenye ulemavu kuwa ni sehemu ya jamii.


  “Watu hawa wenye mahitaji maalumu wananchwa mara nyingine kutokana na baadhi ya watu kudhania kwa mawazo yao hasi kwamba ulemavu ni hasara,niseme hujafa huijaumbika,nisisitize hebu tubebane tonane tupo sawa.


  Daqqaro amesema serikali ya awamu ya tano imeona hilo, ndipo ikaona watu wenye mahitaji maalum ,walikuwa hawajajumuishwa katika kunufaika na zile 10% za mapato ya ndani ,kuanzia mwaka 2018 imetoa maelekezo kwamba na wenyewe ni miongoni mwa kundi linalotakiwa kunufaika ,ambapo  halmashauri zote zimeelekezwa hivyo .


  Amesema ni muhimu kusajili line za simu ili kuepusha makosa ya uhalifu wa kimtandao, matapeli wanao tuma jumbne

   Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo mkuu wa wilaya ya Arusha amesema serikali serikali iliagiza kuwa 10%za mapato nao watu wenye ulemavu wanufaikike na mapato ya ndani iliagiza laini zote za simu zisajiliwe kwa mfumo wa alama za vidole hivyo watu wenye uhitaji maalumu nao ni sehemu ya jamii.


  MHANDISI Imelda Salum ni Mkuu wa kanda ya kaskazini(TCRA) amesema kuwa Mamlaka hiyo imeamua kwasababu wao nao ni sehemu ya jamii ,na pia wanatumia huduma ya mawasiliano hivyo .wanahaki ya kupata taarifa mbalimbali,mafunzo.


  “Tunafahamu kwa namna walivyo wenzetu wana changamoto mbalimbali yumkini kuna wengine hawawezi kupata taarifa kwa wakati ,lakini kwa wenzetu wa kwa wasiosikia taarifa kwa taarifa zinazopelekwa kwa jamii kwa njia ya  radio,televisheni,asiyeona hawezi kuona kwenye televisheni,halikadhalika asiyesikia vileviel


  TCRA imesema kwa kuona umuhimu wa kundi hilo wameamua kuwashirikisha Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA)ili waweze kutoa huduma kwa watu hao wenye mahitaji maalum


  Mkuu huyo wa  kanda ya amesema Swala la usiri na faragha kwa watu wasioona bado limekuwa ni tatizo ,mawasiliano yao yanaweza kutatuliwa tu endapo kuna vifaa maalumu ambavyo wanaweza kuvitumia zikiwemo simu za mkononi ,pale mtu anaposoma ujumbe aweze kusikia sauti ujumbe unasemaje.


  ''Ila mamlaka ya mawasiliano tunajitahidi kuona ni kwa namna gani tunaweza kuwasaidia ,kwa wenzetu wasioona tunawapa taarifa mbalimbali kupitia vitabu ambavyo vimechapiushwa kwa zile alama zao maalum.''


  Ameainisha kuwa kila mmoja aone umuhimu wa kujisajili ni kwani watakaposajili kutumia alama za vidole taarifa zao zinafahamika ,sambamba na kuimarusha usalama wanapotumia mawasiliano.


  Ametoa wito kwa jamii kulitilia uzito swala hili la kusajili laini,na kwa wale ambao hawajapata kitambulisho cha NIDA,Mamlaka husika itawasaidia kupata namba zao,sambamba na wale ambao hawajajiandikisha NIDA wapo tayari kwaajili ya kuwasaidi ili wajiandikishe wapate kitambuluisho cha taifa.  Philipo Meli ni mwenyekiti wa wasioona mkoani Arusha amesema wanaishukuru TCRA kwa kuwathamini na kuwapatia semina hiyo ya kuwajengea utaalamu na kuwapatia vitabu vya nykta nundu kwaajili ya kujisomea na kupata uelewa kuhusiana na mamlaka hiyo ya mawasiliano.

  Amesema katika mawasiliano watu wasioona changamoto kubwa ni mtu wa kuwasomea ujumbe lazima awepo,hakuna usiri,tunaomba serikali itusaidie uwepo wa simu ,ambazo tunaweza kusoma ujumbe kwa kusikia sauti ,na iwe katika lugha ya kiswahili ambapo itaweza kuondoa utegemezi kwa kiwango kikubwa.

  "Changamoto kubwa mtu anakutumia ujumbe hata kama unataka uwe wa siri,inashindikana mpaka utafute mtu mwaninifu aweze kukusomea ujumbe wako,hiyo ndiyo changamoto inayotupata sisi watu tusioona.''Alisema Philipo.  0 0

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa
  maelekezo kwa Mhandisi wa Vodacom, Benedict Mara (wa kwanza kulia) kuhakikisha mawasiliano yanapatikana muda wote Kata ya Ilolangulu wakati wa zaiara yake ya kukagua upatikanaji wa hudumaza mawasiliano wilayani Mbogwe, Geita.
  Mkuu wa uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) kuhusu mnara wa Ilolangulu wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano Mbogwe mkoani Geita.
  Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Agostino Masele akimuonesha Naibu Waziri wa
  Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye vijiji ambavyo havina
  mawasiliano ya uhakika wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano wilayani Mbogwe mkoani Geita.
  Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi akitoa taarifa ya hali ya mawasiliano kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake wilayani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano.

  **********************************

  Prisca Ulomi, Geita

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye yuko ziarani mkoani Geita kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchikusajili laini za simu kwa njia ya alama ya vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa chaNIDA na kufuatilia utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi mkoanihumo.

  Wakati akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Mbogwe, Nditiye amesema kuwamalengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanawasiliana, huduma zamawasiliano zinakuwa zenye ubora unaotakiwa, za uhakika na kunakuwa na usikivumzuri wa mawasiliano kwa kuwa Serikali inataka wananchi wawasiliane.

  “Serikali tunataka wananchi wawasiliane kwa kuwa wakiwasiliana tunapata mapatoambayo yanaendesha shughuli mbali mbali za kuhudumia wananchi,” amesema Nditiye.Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi amemweleza Nditiye kuwa wanashida yamawasiliano kwenye wilaya yao na mara nyingine wanakwama kukusanya mapato yaSerikali hivyo inawapa changamoto katika kuwatumikia wananchi na utekelezaji wamajukumu ya kila siku ya Serikali.

  “tunashida ya mawasiliano kwenye wilaya yetu na mara nyingine tunakwama hata kukusanya mapato na kupeana taarifa za ulinzi na usalama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi,” amefafanua Mkupasi.

  Nditiye amemweleza kuwa amekagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano wilayani humo na amegundua kuwa Wilaya ya Mbogwe inapata mawasiliano kwa kiwango cha asilimia 90 na ina mitandao mingine ya mawasiliano ila wananchi wanaonekana wanapenda mtandao wa Vodacom.

  Naye Mbunge wa Mbogwe, Agostino Maselle amekiri kuwa wanapata huduma za
  mawasiliano za mitandao mingine ya TTCL, tigo, halotel, airtel na yote iko vizuri ila mtandao wa Vodacom unasumbua na huduma za m-pesa kwenye kata ya Ilolangulu, Itobe na Isesya.

  Akizungumza kwa niaba ya wananchi wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kata ya Ilolangulu, mkazi wa kata hiyo Daniel Mishigitu amemweleza Nditiye kuwa wanapata kero ya mawasiliano ya Vodacom na wakitumiwa hela inakaa muda mrefu kwenye mtandao. Naye Vedastus Rwechungura amemshukuru Nditiye kwa kufika na kusikiliza shida ya mtandao huo na mzunguko wanaoupata wakitaka kutoa pesa ambapo mara nyingine wanalazimika kusafiri kwenda Ushirombo.

  Akijibu malalamiko ya wananchi, Nditiye amewaeleza kuwa amegundua kuwa kuna mzunguko wa hela kwenye kata hiyo na uchumi wa wananchi uko vizuri, hivyo ameielekeza kampuni ya Vodacom kuwa ndani ya muda wa miezi sita mnara uwepo ili wananchi waweze kuwasiliana, kutuma na kupokea pesa kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanawasiliana na wakiwasiliana inapata mapato.

  Nditiye amefanunua kuwa sehemu inapokuwa na mawasiliano ya kampuni moja
  inatosha na sio lazima kuwa na mitandao yote ila kwa kuzingatia kuwa wananchi wamehitaji mtandao huo hivyo UCSAF kwa kushirikiana na Vodacom ihakikishe kuwa mnara huo unajengwa na TCRA wafuatilie na kusimamia jambo hilo.

  Katika ziara hiyo, Nditiye ameambatana na wataalam kutoka wizarani kwake Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na watoa huduma wa kampuni ya Vodacom

  0 0

  Charles James, Michuzi TV

  SERIKALI imewaonya walimu na maafisa elimu kuacha tabia ya kuvujisha mitihani na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote wakataojaribu kuvujisha mitihani.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha wakati akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi kwenye mahafali ya kidato cha nne kwenye Shule ya Sekondari ya Kwamtoro iliyopo Wilayani Chemba mkoani Dodoma.

  Ole Nasha amesema kumekuepo na tabia ya baadhi ya walimu na viongozi wanaohusika na elimu kuvujisha mitihani hasa ile ya ngazi ya Taifa jambo ambalo linaharibu taswira ya elimu nchini.

  Amewataka wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne kutodanganyika kununua mitihani kutoka kwa watu wanaowalaghai kutaka kuwauzia na badala yake watoe taarifa kwenye vyombo vya sheria.

  " Niwapongeze wanafunzi wote ambao leo mnaagwa, hatua hii ni kubwa sana kwenye maisha yenu. Tunajivunia nyinyi kwa kuwa ndio zao la kwanza la Elimu bure toka Mhe Rais alivyotangaza kufuta ada mashuleni mwaka 2016 ambapo nyie ndio mlikua mnaanza kidato cha kwanza.

  Niwasihi msidanganyike eti mkauziwa mitihani. Hasara zake ni kubwa na zitawaponza. Tumieni elimu na maarifa ambayo walimu wenu wamewafundisha kuweza kufanya vizuri mitihani yenu, lengo ni kuona nyinyi nyote mnaogwa leo mnafaulu na kuendelea na kidato cha tano," Amesema Ole Nasha.

  Amesema Wilaya ya Chemba mwaka jana ilikutwa na kashfa ya kuvujisha mitihani hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo na watakaobainika sheria kali itachukuliwa dhidi yao.

  Ole Nasha ameahidi pia kumaliza changamoto ya nyumba za walimu katika shule hiyo ambapo amesema atatoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara yake ili Shule ya Kwamtoro iweze kupatiwa fedha za ujenzi wa nyumba hizo.

  Aidha ameitaka Bodi ya Shule kuhakikisha inaharakisha ujenzi wa bweni la wasichana ili likamilike haraka ili waweze kupatiwa fedha zingine kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bweni lingine la wavulana.

  " Nimefika hapa na nimekagua maendeleo ya ujenzi wa bweni la wasichana, sijaridhishwa nalo ndio maana mlivyoomba niwapatie fedha za ujenzi wa bweni la wavulana nimekataa. Hakikisheni mnamaliza hilo la kwanza ndio mje tuwapatie fedha za ujenzi wa bweni la pili.

  Mhe Rais amefanya Mapinduzi makubwa kwenye sekta ya elimu zaidi ya Bilioni 945 zimetumika kwenye sera hii ya elimu bure. Ni jukumu lenu sasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili kumpa moyo Rais wetu kwa kazi kubwa anayofanya ya kutuletea maendeleo wananchi tulio wanyonge," Amesema Mhe Ole Nasha.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amemshukuru Mhe Naibu Waziri kwa kukubalj kuhudhuria mwaliko huo na kumuahidi kuongeza usimamizi katika sekta hiyo muhimu kwenye maendeleo ya Nchi na hasa katika kudhibiti vitendo vya uvujishaji mitihani.

  Nae Mbunge wa Jimbo la Chemba, Juma Nkamia amishukuru Wizara ya Elimu kwa namna ambavyo imekua ikitoa fedha katika kuhakikisha miradi ya elimu ndani ya Jimbo lake inatekelezwa.

  " Mhe Naibu Waziri nakushukuru sana kwa kukubali mwaliko wetu wa kuwa mgeni rasmi. Tunakupongeza wewe na wizara unayoiongoza kwa jinsi ambavyo mmekua mstari wa mbele kutuletea maendeleo wananchi wa Chemba," Amesema Nkamia.

  Awali Mhe Ole Nasha aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa matundu ya vyoo kwenye Shule hiyo ambapo kiasi cha Shilingi Milioni mbili zilipatikana na kuzikabidhi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ili kukamilisha ujenzi huo na kumaliza changamoto hiyo.
   Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha akikagua ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya Kwamtoro wakati alipofika kwenye mahafali ya kidato cha nne.
   Mbunge wa Jimbo la Chemba, Juma Nkamia akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kwamtoro ambapo yeye ndie mlezi wa Shule hiyo.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kwamtoro wilayani Chemba, Dodoma.
   Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Chemba, walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kwamtoro wilayani humo wakati wa mahafali ya kidato cha nne ambapo Mhe Ole Nasha alikua mgeni rasmi.

  0 0

  Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi ussu wakipita mbele ya Waziri wa utalii na maliasili katika sherehe hizo.
  Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya awali ya jeshi ussu akipita juu ya kamba katika moja ya maonesho yaliyofanyika mbele ya waziri wa utalii na maliasili Mhe.Khamis Kigwangaka katika sherehe ya kuhitimisha mafunzo hayo

  Na Jusline Marco-Arusha

  Waziri wa maliasili na utalii Dkt.Khamis Kigwangala ametoa siku 14 kwa manaibu katibu wakuu na katibu mkuu wa wizara hiyo kuwasilisha mchakato wa mswada wa sheria ya uundwaji Jeshi Ussu ofisini kwake ili iweze kuwasilisha bungeni.

  Ametoa agizo hilo katika sherehe za kuhitimisha mafunzo ya Awali ya Jeshi Ussu katika kituo cha mafunzo cha Mbulu-mbulu kilichopo katika kata ya Kambi ya simba,Wilayani Karatu Mkoani Arusha.

  Dkt.Kigwangala amesema kuwa kutokukamilika kwa mswada huo ni mapungufu ya wizara kwani amekuwa akielekeza mara kadhaa mswada huo ukamilike na umekuwa haukamilishwi.

  "Katika maagizo niliyopewa na Mhe.Rais sikusudii kujiona nikitumbuliwa kwasababu ya kuchelewa kutimiza wajibu wangu,"Alisema Dkt.Kigwangala huku akiongeza kuwa kama ni madokezo ameandika mara kadhaa lakini wamekuwa wakijivuta.

  Ameongeza kuwa kwa  zaidi ya miaka kumi tangu ilipoelekezwa na sheria ya uhifadhi ya wanyamapori haijawahi kuanza ila kwasasa taasisi mbalimbali za uhifadhi wa wanyamapori zimeanza kuonyesha bidii katika kuwapatia mafunzo wafanyakazi wao kwenye eneo la Jeshi Ussu.

  Vilevile ametoa jukumu kwa bodi ya mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori Ngorongoro kupeleka ushauri wa mapendekezo yaliyotolewa ya kufanya kiwtuo hicho kuwa kamili kwa kuangalia vigezo vyote vitakavyowezesha kufanya kituo hicho kuwa kituo cha kudumu.

  Awali akitoa risala yake kwa mgeni rasmi  mkuu wa kutuo hicho Kanali Martin kilugha  amesema kuwa jumla ya wahitimu wa mafunzo hayo ni 112 ambapo katika mafunzo hayo wakufunzi wa ndani wametumika,wakufunzi wa hifadhi pamoja na wakufunzi wa muda kutoka katika jeshi la JWTZ kwa ajili ya kuimarisha Jeshi Ussu.

  Amesema kuwa wahitimu hao wamefundishwa mafunzo mbalimbali ya uhifadhi ikiwemo utimamu wa mwili,na ulinzi wa nadharia na vitendo na kufaulu kwa madaraja mbalimbali.

  Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amesema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya ujangili ya kuuawa kwa wanyama hivyo wahitimu wa mafunzo hayo wanapaswa kufahamu kuwa wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanalinda rasilimali za nchi.

  "Niwaomba wahitimu walio chini ya uongozi wako Mhe.Waziri wakapambane na ujangili ili kukomesha mchezo huo na rasilimali za nchi ziweze kuwa salama kwa faida ya wananchi kwani huo ndio msimamo wa Rais wetu ndiyo maana ameridhia tuende kwenye mfumo wa kijeshi kama sehemu yake ya kuonyesha dhamira ya kupambana na ujangili na kulinda rasilimali zetu".Amesema  Mkuu huyo.

older | 1 | .... | 1882 | 1883 | (Page 1884) | 1885 | 1886 | .... | 1898 | newer