Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1880 | 1881 | (Page 1882) | 1883 | 1884 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kampuni ya Engen Petroleum (T) Limited, imezidundua kituo kipya cha mafuta jijini Dodoma,ikiwa ni sehemu ya kujitanua  na kuongeza wigo wa kibiashara kwa kuwafikia Wateja wake walioko katika maeneo mbalimbali nchini,
  Akizungumza jana katika uzinduzi rasmi wa kituo hicho kilichopo barabara ya Meliwa (zamani Kilimo kwanza),Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Paul Muhato aliuhakikishia umma kuhusu upatikanaji wa soko la bidhaa za Kampuni hiyo,ikiwa ni sehemu ya uchangiaji wa kukuza uchumi jijini Dodoma na miji mingine nchini Tanzania ambako kampuni hiyo imekuwa ikijitanua .
  Alisema Kampuni ya Engen Petroleum (T) Limited ni kampuni yenye mafanikiyo, iliyojidhatiti vilivyo na yenye ubunifu  mkubwa,hasa katika utoaji wa huduma na bidhaa zake bora za mafuta,pamoja na maduka yanayorahisisha upatikanaji wa bidhaa bora za kampuni hiyo.

  "ENGEN imekuwa mshirika katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa zaidi ya miaka 20 sasa,hivyo kama sehemu ya kuendeleza mkakati wake wa kujitanua kibiashara,nauhakikishia  umma kuhusu uwepo wa soko  la bidhaa za kampuni ya Engen zipo za kutosha,zilizo na kiwango cha ubora wa Kimataifa na usiotia shaka kabisa'',alisema Muhato.

  Amesema upanuzi wa vituo katika maeno mbalimbali ni hatua ya asili katika mpango wa ukuaji wa kampuni kwa sasa,na pia wanaendelea kuangalia maeneo ya kimkakati nchini kote kwa ajili ya maendeleo na ununuzi wa vituo vya rejareja ili kutumikia vyema soko la Tanzania.
   
  "Hivi sasa tuna vituo 10 vinavyopatikana katika mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Tanga, Moshi, Arusha na Mwanza - lakini idadi hii itaongezeka katika kipindi cha miaka michache ijayo,

  Tukiwa tunakusudia kuweka mteja kama kipaumbele cha kwanza, tunatarajia angalau vituo vinne  zaidi katika maeneo ya kimkakati mwishoni mwa mwaka,huku tukisisitiza umuhimu wa kuwa na mafuta bora  kwa wateja wetu poote pale'',
  alisema  Muhato .
  Amesema katika suala la utoaji huduma,Wana  wahudumu Waliofundishwa vizuri kawahudimia wateja kwa saa 24 kila siku, lakini pia upatikaji wa malipo ya bidhaa zao,unaweza kutumia njia nyingi ikiwemo ya kwa njia ya kadi  ya Mafuta ya Engen.

  "Wateja pia watafurahia huduma zingine kadhaa kama vile maduka, migahawa ya hali ya juu, Sehemu ya matengenezo ya magari, mahali pa kuosha gari na huduma zingine, zote zikiwa chini ya paa moja. "alimaliza kusema Muhato. 


  Muoenekano wa Kituo kipya cha mafuta Engen kilichopo barabara ya Meliwa (zamani Kilimo kwanza)jijin Dodoma mjini
  Madereva wa pikipiki wakisubiri kupata ofa ya kujaziwa mafuta kila mmoja waliohudhuria katika siku ya uzinduzi wa kituo cha  mafuta  cha Engen jijini Dodoma.

  0 0

  Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 imezinduliwa rasmi leo Septemba 27,2019 wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.


  Ilani hiyo inayojumuisha sauti za wanawake kutoka sauti za wanawake kutoka makundi mbalimbali chini ya Uongozi wa TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Taasisi ya Women Fund Tanzania na Mtandao wa Wanawake na Katiba,Uchaguzi na Uongozi imezinduliwa na Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro.

  Awali akizungumza,Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba,Ruth Meena alisema ilani hiyo imebeba masuala muhimu yanayohusu wanawake kwenye uchaguzi.

  “Ilani hii imebeba ajenda ya mwanamke,turufu ya ushindi 2019/2020 imewalenga wanawake,serikali,vyama vya siasa,wagombea nafasi za uongozi,vyombo vya habari na wapiga kura”,alisema Muro.

  Alisema ilani hiyo inaendeleza madai ya wanawake watetezi wa haki za ushiriki katika uongozi wa kisiasa tangu taifa lipate uhuru mpaka leo.

  “Hii ni ilani ya tano iliyobeba madai ya wanawake tukiwa wadau na washiriki wakuu katika michakato mbalimbali ya uchaguzi.Ilani ya kwanza ilikuwa ya mwaka 2000 ikijulikana kama ilani ya wapiga kura,ilani ya pili ni ya mwaka 2005,ya tatu ni ya mwaka 2015 na ya nne ni ilani ya mwaka 2015”,alieleza Muro.

  “Sisi wanawake wapiga kura tunatambua ni wadau muhimu kwenye shughuli zote za kisiasa na maendeleo ya jamii.Tunatambua na kudai haki za kushiriki katika uchaguzi kama wapiga kura na wanaowania nafasi za uongozi,walioteuliwa na kugombea hatimaye kushinda nafasi za uongozi kupitia uchaguzi”,aliongeza.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi alisema madai yaliyomo kwenye ilani ya uchaguzi ya wanawake yanahusu masuala ya wanawake wote nchini Tanzania.
  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba,Ruth Meena akielezea kuhusu Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 ambayo imezinduliwa rasmi leo Septemba 27,2019 wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.
  Kulia ni Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 
  Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 
  Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020
  Wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakionesha mabango yenye ujumbe wa ‘Uongozi sio misuli ni hekima na busara kila mtu anao’.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 .
  Mwenyekiti wa TGNP Mtandao Asseny Muro akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020,Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi.
  Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 ukiendelea.
  Wanaharakati wakisherehekea wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
  Wanaharakati wakisherehekea wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
  Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.
  Mkurungezi wa Jinsia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Julius Mbilinyi akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.
  Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

  0 0

  Kikundi cha Ngoma na Sarakasi cha Safi kutoka nchini Tanzania kikitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019. 
  Mmoja ya kijana wa kikundi cha ngoma na sarakasi cha Safi kutoka Tanzania akionyesha umahili wake wa kucheza kwa kutumia shingo na mikono katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Vijana wa Kikundi cha ngoma na sarakasi cha Safi wakionyesha umahili wao katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Wakiwaaga wanajumuiya wa Afrika Mashariki waliohudhuria katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Wasanii wa Kenya wakionyesha umahili wao wa kuigiza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Kikundi cha ngoma toka Zanzibar, Tanzania wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Kikundi cha ngoma ya Kisukuma kutoka Wilaya ya Buchosa, Sengerema - Mwanza wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Akina mama wa Kigogo wanaweza, wakionyesha umahili wao wa kupiga ngoma na kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Ngoma ya kigogo toka Dodoma wakionyesha umahili wao wa kucheza katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Kikundi cha Ngoma kutoka nchini Kenya kikionyesha umahili wake wa kuimba na kucheza.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshugulikia maswala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (wa pili toka kushoto) akishuhudia ngoma za mataifa toka Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kuhudhuria katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
  Naibu Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia Wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akiangalia bidhaa za nguo katika moja ya banda la mjasiriamali anayeshiriki Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST linaloendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
  Mambo ni moto!

  0 0


  Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv,

  IKIWA ni siku ya tano tangu Rais John Magufuli atoe ruhusa kwa mahabusu wa kesi za uhujumu uchumi kukiri makosa yao na kulipa vigogo Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms Limited, akiwemo Wakili maarufu Dk Ringo Tenga, wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) yenye maombi mbalimbali kuhusu kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  Mbali na Tenga, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni wa hiyo, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.

  Mapema, wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori alidai jmbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo leo Septemba 27, limekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba katika ahirisho lililopita, upande wa utetezi uliomba kujadiliana na wateja wao.

  Wakili wa Utetezi, Bryson Shayo amedai mahakamani hapo kuwa, wameshauriana na wateja wao na katika mashauriano hayo washitakiwa wameandika barua kwa DPP kuzingatia agizo hilo la Rais John Magufuli la Septemba 22, mwaka huu.

  Amedai Septemba 26, mwaka huu washitakiwa hao waliandika barua kwenda kwa DPP yenye maombi mbalimbali kuhusu shauri hilo hivyo, aliomba ahirisho la siku 14 ili barua iweze kujibiwa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayowakabili hayana dhamana kisheria.

  Septemba 24 mwaka huu upande wa utetezi uliomba mahakama kuitisha shauri hilo leo (jana) kwa sababu ya mazingira ya kesi yenyewe wanaomba wazungumze na wateja wao.Dk Tenga na wenzake wanadai kuwa, kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 Dar es Salaam, walitoza maalipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango USD 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.

  Pia katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa USD 3,282,741.12 kwa TCRA, kama malipo ya mapato.

  Pia wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kulipa ada za udhibiti USD 466,010.07 kwa TCRA.

  Vile vile ,washitakiwa hao wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara USD 3,748,751.22 sawa na Sh bilioni nane .


  0 0

  Florah Mgonja Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini ,akiwa katika ofisi za Utamaduni Jijini Arusha

  Na.Vero Ignatus,Arusha.


  Baraza la sanaa nchini lipo mkoani Arusha kwaajili ya kuratibu shughuli zote za sanaa ,kwa maana ya usajili na uratibu wa wadau kwa ujumla wakiwemo wamiliki wa kumbi,bendi ,studio ,washehereshaji,DJ,waandaaji wa matamasha pamoja na matukio mbalimbali ya sanaa kanda ya kaskazini.  Florah Mgonja ni Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini amesema   baraza hilo limeanzishwa kwa mujibu wa sheria no 23 ya mwaka 1984 ,na kanuni zake za mwezi February 2018, zinawatambua wasanii pamoja na kazi zao ,pia zinamtambua Afisa utamaduni kanuni ya mwaka 2018 kipengele cha 22,kinamtanbua Afisa huyo kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa.  Amewataka wasanii kwenda kujisajili ili waweze kuhudumiwa sambamba na kauli mbiu ya Basata inavyosema kuwa sanaa ni kazi na  kama zilivyo kazi nyingine hivyo ni vyema wakajisajili ili watambulike .  Mgonja amesema wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanasajiliwa na hawaoni faida,watambue kuwa faida zipo nyingi kwani Basata lipo dawati ambalo msanii hupewa fursa mbalimbali, na kazi zao namna zinaweza kulindwa kisheria.  “Vipo vinandaumiza vingi ambavyo vinachukua kazi nyingi za wasanii,kama umesajiliwa serikali ipo kwaajili ya kuangalia haki ya msingi ya msanii na tunaishughulikia kwa namna gani ili msanii aweze kusonga mbele”alisema Flora.  Mratibu huyo wa kazi za sanaa kanda ya kaskazini, amesema kuwa kwa sasa wapo wanatoa elimu kwa wasanii na vikundi mbalimbali,ila wakati unakuja kwa wasanii ambao hawatajisajili sheria itachukua mkondo wake .  Aidha amesema Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia  kupitisha Sheria amabayo itawabana wasanii ili kuwasaidia kiuchumi badala ile ya Mwanzo ya mwaka 1984 sheria No 23 kuwa na mapungufu.  Florah Mgonja ni Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini ,akisisitiza jambo kwa waandishi wanhabari (hawapo pichani)katika ofisi Utamaduni Jijini Arusha.
  Aidha amesema kulikuwa na malalamiko juu ya COSOTA,BODI YA FILAMU,BASATA kutokana na utendaji kazi wake kwani msanii alikuwa kote anatozwa kwa sasa serikali imaangalia namna gani hizi Taasisi tatu zinakuwa mamlaka ya usimamizi wa kazi za sanaa ambapo michakato tayari imeshaanza na inaratibiwa na TCRA.  Amesema kwa wale wote a,mbao wanafanya kazi bila kusajiliwa sheria itafuata mkondo wake kwasababu kwa sasa Basata ipo katika kuelimisha ,itafika mahali tukishaeka mambo sawa ikiwemo sheria na hizi mamlaka kuwa pamoja ,tutahakikisha kuwa kila anayejihusisha na shughuli za sanaa anasajiliwa.  Amesema zipo faida nyingi za msanii kujisajili ikiwemo sheria,kazi zao kutunzwa kupata fursa mbalimbali huku akiwataka wale ambao wameshajisajili kuhuhisha vibali vyao ,kwa msanii binafsi ni shilingi 45,000 kwa vikundi 85,000 ikiwa imejumlishiwa na fomu.  Amebainisha kuwa kwa sasa msanii hawezi kwenda nje ya kwa kupitia viwanja vya ndege  nchi kama hajasajiliwa Basata,hivyo umuhimu wa kujisajili ni mkubwa, kwani hata msanii akipata shida akiwa nje ya nchi ni rahisi kusaidika kama amesajiliwa.  Amesema Basata ipo kwaajili ya kushughulikia usajili kwa wasanii sambamba na ushauri wa namna ambavyo wanavyoweza kuendesha shughuli zao za sanaa kwani fursa zipo nyingi sana.  Aidha Basata ilianza usajili kwa mwaka wa fedha 2018-2019 na usajili ulikuwa mzuri na wasanii waliitikia kwa wingi,hivyo kwa mwaka huu wengi wanahuisha vibalivyao kwa wale waliokwisha sajiliwa tayari ambapo wamekuwa mabalozi kwa wengine .  Ameeleza kuwa kwasasa Basata imewarahisishia kazi wasanii,badala ya kwenda Jijini Dar es salaam imewafuata hadi mkoa husika kwaajili ya kuwafanyia kushughulikia usajili wao .  Hata hivyo ameeleza kuwa msanii anapojisajili 25% ya makusanyo katika usajili huu unarudi halmashauri kama sehemu ya uendelezaji wa shughuli za sanaa.

  0 0  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya SGA Security, Eric Sambu (kushoto) akizungumza jijini Dar Es Salaam leo wakati wa kuadhimisha miaka 35 ya kutoa huduma za ulinzi nchini. Kulia ni Meneja wa Wateja na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Aikande Makere.  Kampuni ya ulinzi, SGA Security, imetoa mafunzo ya bure ya usalama kama sehemu ya utoaji wa huduma kwa jamii na kuwazawadia watumishi wake wa muda mrefu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 35 ya kuwepo nchini Tanzania.

  Wiki iliyopita kampuni hiyo ilitoa mafunzo kwa wateja wake wakubwa juu ya mbinu mbalimbali za kisasa za kupambana na changamoto za kiusalama.

  Semina hiyo kwa wateja wake ilifanyika Ijumaa Septemba 27 jijini Dar es Salaam na mafunzo yaliongozwa na wataalam waliobobea kwenye masuala ya usalama ambapo zaidi ya mameneja 80 wa usalama wa makampuni makubwa na mabenki nchini walihudhuria.

  Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa SGA, Eric Sambu, alisema kwamba kampuni hiyo ya ulinzi imeamua kutoa huduma kwa jamii kama sehemu ya kusheherekea mafanikio yake nchini.

  SGA pia imetoa mafunzo ya usalama kwenye shule 12 za msingi mkoani Dar es Salaam ambapo wanafunzi zaidi ya 2,000 walinufaika. Mafunzo hayo yalikua juu ya majanga ya moto, huduma ya kwanza, mazingira, afya na usalama kwa ujumla.


  Ikiwa ina watamushi zaidi ya 5,800, nchini Tanzania, SGA kwa sasa ndio kampuni kubwa ya ulinzi nchini.Katika shughuli za kuadhimisha miaka 35 nchini, kampuni pia imeanzisha ‘Club 20’ ambao wanachama wake ni watumishi walioitumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20.

  SGA aliwatuza watumishi 16 waliotumikia kampuni kwa muda mrefu ambao pia wamefikia muda wa kustaafu.Wakati huo huo, mwakilishi kutoka jeshi la polisi nchini ameipongeza SGA kwa kujali maslahi ya watumishi wake na kuongoza kwa mfano, akisema kwamba kampuni nyingi binafsi za ulinzi hazifuati miongozo iliyotolewa kuhusiana na mafunzo, usimamizi, ukaguzi na mishahara.


  Amezitaka kampuni nyingine za ulinzi kuiga mfoano wa SGA.

  Ikiwa ina waajiriwa zaidi ya 80 waliotumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20 kwenya biashara ya faida kubwa, SGA ina kila sababu ya kusherehekea, amesema Sambu. SGA pia ina watumishi takribani 2,200 walioajiriwa kwa zaidi ya miaka 10.

  “SGA ni kampuni ya kwanza binafsi ya ulinzi kuingia Tanzania na imedhihirisha kwamba kuwajali watumishi wake ni muhimu kwa mafanikio ya kampuni,” Sambu amesema.
  Watumishi wa SGA wakishiriki kwenye Siku ya Usafi Duniani kama sehemu ya kuadhimisha miaka 35 ya kuwepo nchini Tanzania  “Kampuni mama ina watumishi za ya 18,000 na suala la muhimu kwetu ni watu. Tumewekeza sana katika utoaji wa mafunzo na tunahakikisha kwamba mishahara yetu inaongoza kwenye soko kama sehemu ya kuwapa motisha watumishi wetu,” aliongeza.

  Amesema kwamba kampuni anaadhimisha miaka 35 ya utoaji huduma nchini Tanzania huku ikiwa inakua siku hadi siku, hususan katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

  Ameeleza zaidi kwamba mafanikio ya kampuni yameletwa na watumishi wake ambapo amesema ni waaminifu, waadilifuna wachapa kazi kwa bidii.Matukio ya hivi karibuni kwenye mazingira ya kibiashara nchini yamekuwa kama fursa ya kujifunza na kuwawezesha wafanyakazi wetu kwenda sambamba na matakwa ya wateja,” ameongeza.

  “Kila mara tunajipanga upya katika utendaji wetu, huku tukiwekeza kwenye teknolojia na watumishi wetu kuhakikisha kwamba hakuna jambo linaloharibika,” amesema Sambu.SGA ni kampuni kongwe binafsi ya ulinzi Tanzania, ikiwa imeanza kazi mwaka 1984 kama Group Four Security. Inatoa huduma mbalimbali zikiwemo za walinzi, usalama wa kielektroniki, huduma za dharura na usafirishaji wa fedha.

  “Tuna magari 224 na vituo 12 mikoani na watumishi wanaojituma, tuna miundombinu ya kutosha kuwahudumia wateja popote pale nchini,” Sambu amesema.enaja Rasilimali Watu wa SGA, Ebenezer Kaale, alisema kwenye tukio hilo kwamba watumishi wengi walioajiriwa kwa miaka mingi wanafanyakazi kwenye idara ya kusafirisha fedha, idara nyeti inayohitaji uadilifu na nidhamu ya hali ya juu.

  Ikiwa ina mafanikio makubwa kwenye huduma za fedha, ambapo kampuni imehodhi asilimia 90 ya soko, watumishi kwenye idara wanastahili pongezi kwa mafanikio hayo.

  Meneja wa Mahusiano ya Wateja, Aikande Makere, amesema kwamba kazi za SGA zitarahisishwa ikiwa wateja wanaenda na wakati kwa kufahamu mbinu za kisasa za kupambana na changamoto za kiusalama.

  0 0


  Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Nelson Olotu likiwa kanisani tayari kwa Ibada ya Maziko.
  Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika ibada ya mazishi katika kanisa la KKKT Usharika wa Sasi mtaa wa Ilmeshorori,Dayosisi ya Kaskazini Kati

  Umati wawatu waliojitokeza wakiwa nje ya kanisa baada kumalizika kwa Ibada
  Gari lioilobeba mwili wa Nelson likiondoka eneo la kanisa kuelekea makaburini kwaajili ya maziko.


  Na.Vero Ignatus,Arusha

  ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Dk.Solomon Masangwa jana ameongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Urubani Nelson Olotu (25) aliyefariki kwa ajali ya ndege Septemba 23 mwaka huu, huko Seronera Serengeti Mkoani Mara.

  Aidha katika ajali hiyo pia mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Nelson Mabeyo ambaye alikuwa rubani wa ndege namba 5H-AAM ya kampuni ya Auric air alipoteza maisha.

  Akizungumza katika ibada hiyo jana iliyofanyika katika Usharika wa Sasi mtaa wa Ilmeshorori, Dayosisi ya Kaskazini Kati,Dk.Masangwa aliwapa pole wazazi na ndugu wote walioguswa na msiba huo na kuwataka kuwa na utulivu katika kipindi hicho cha majonzi.

  "Binadamu siku zetu za kuishi hapa duniani fupi na zimejaa dhiki,hivyo hakuna ambaye ajuaye siku wala saa ya kifo kitakapompata, kutokana na fumbo hili inatupasa kila mmoja kukesha tukiomba,"alisema

  Alisema ajali za ndege zinasababishwa na mambo mbalimbali kuanzia inaporuka,ikiwa angani na inapotua hivyo ni suala la kumwachia mungu.

  "Baadhi ya sababu hizo ni makosa ya rubani,matatizo ya kiufundi,hali ya hewa,vyuma,wakati wa ndege kupaa na wakati wa kutua,huweza kusababisha ajali katika hili hakuna wa kulaumiwa,"alisema

  Aidha alisema katika mazingira hayo huwezi kumlaumu mtu yoyote sababu hata rubani akijitahidi kukwepa ajali lakini bado mazingira ya ajali yanaweza kuwepo.
  Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa salamu za pole kwa niaba ya serikali na kusema kazi ya mungu haina makosa.

  "Huyu Nelson angemaliza safari ya masomo yake angetusaidia sana Serikali na taifa,lakini makusudi ya mungu lazima yatumike na tumwachie yeye,"alisema

  Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya,ametoa pole na kusema hakuna mwenye jibu kwanini mtu mwenye umri mdogo kama walivyo vijana hao waliofariki katika ajali hiyo na katika kipindi hiki ambacho wazazi wao walikuwa wakiwahitaji kuliko kipindi chochote.

  "Mahali salama na pekee ni kujikabidhi mikononi mwa mungu,"alisemaKatibu wa Chama cha Marubani nchini,Khalid Lqbal amesema marehemu alikuwa mpole,mnyenyekevu, msikivu ba mwenye kupanga kujifunza zaidi.

  "Hivyo tumepoteza kijana mdogo ambaye angekuja kuwa msaada hapo baadaye,"alisemaPia amesema vifo vya vijana hao Nelson Olotu na Nelson Mabeyo ni pigo kubwa kwa taifa na sekta ya masuala ya anga.


  Kwa upande wa kaka wa marehemu aliyesoma histori fupi ya marehemu,Calvin Olotu alisema marehemu alisoma shule ya Msingi Trust St.Patrick mwaka 1998 na kumaliza 2009 na Sekondari ya Duluti ambayo alimaliza mwaka 2013.

  Baada ya hapo alijiunga shule ya Urubani mwaka 2014 katika Chuo cha Aviation College Dar esalaam na kuhitimu mwaka 2015 kisha alikwenda kujiunga na Chuo cha urubani Nairobi nchini Kenya cha PRO-ACTIVE AVIATION COLLEGE na kuendelea na ground School na Flight mpaka mwaka 2019.

  Calvin alisema marehemu alikuwa mtoto wa tatu katika familiya ya mzee Wilberd Phillemon Olotu na mauti yalipomkuta akiwa safarini katika Hifadhi ya Serengeti na amezikwa nyumbani kwa wazazi wake Kambi ya Chupa Wilaya ya Arusha.


  0 0  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Kwanza TV kwa kipindi cha miezi sita ili waweze kujirekebisha katika uendeshaji luninga katika mitandao.

  Kwanza TV walikutwa na kosa la kuchapisha habari iliyokuwa inamuhusu Dkt.Gwajima kupata ajali ya gari ambapo katika utetezi wao walidai kuwa taratibu za kihabari zilifuatwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Joseph Mapunda amesema kuwa Kwanza Tv walikutwa na makosa ya habari ya ajali ya Dkt.Gwajima ambayo haikufafanunua ni Gwajima yupi ambapo ni kosa katika uandishi.

  Amesema Kamati hiyo ilisema kuwa ajali hiyo ilikuwa inamhusu Katibu Mkuu wa Tamisemi Afya Dkt.Doroth Gwajima hivyo kulifanya watu wengine kushindwa kujua ni Dkt.Gwajima gani kutokana na kutokwepo kwa majina yote.

  Aidha Kamati hiyo imetoa faini ya sh.milioni tano kwa Ayo na Watetezi TV kwa kila mmoja kulipa fedha hiyo kwenye mamlaka hiyo kutokana na kushindwa kuchapicha Sera ya maudhui na miongozo katika luninga zao na kuweza kuona watazamaji. Mapunda amesema vyombo vya habari vifuate taratibu , kanuni na sheria katika kutangaza au kuhabarisha umma kwa kuzingatia misingi ya uandishi.

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Joseph Mapunda akitoa hukumu kwa vyombo vya habari viliyokiuka maudhui ya utangazaji leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Iringa, Septemba 27, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga
  Baadhi ya watumishi wa wilaya ya Kilolo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao, Septemba 27, 2019.

  \Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
  …………….


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi afuatilie utendaji kazi kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo kufuatia watumishi 14 wa ofisi hiyo wakiwemo madereva 10 kuhamishwa baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Asia Abdallah kudai kuwa hawafanyi kazi ipasavyo.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema ni mhuimu kwa viongozi wakatambua dhamana zao katika utekelezaji wa shughuli zao pamoja na kuwatambua, kuwajali na kuwathamini watumishi wa kada zote wakiwemo madereva, hivyo ni vizuri wawaandae kwa kuwapa maelekezo kwa wakati kwa kuwa nao ni binadamu na wanafamilia.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 27, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Kilolo, Halmashauri ya wilaya ya Kilolo pamoja na Madiwani wa Halmashauri hiyo akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Iringa. Amesisitiza umuhimu wa watumishi hao kushirikiana.

  Waziri Mkuu amesema pamoja na shughuli za maendeleo wanazofanya katika wilaya hiyo lakini hawana mshikamano, hivyo amemtaka Mkuu wa Wilaya ahakikishe anashirikiana vizuri na wenzake kwa sababu watumishi wengi wamehamishwa tangu aingie katika ofisi hiyo na hata wanaoletwa wanalalamika na wanaomba wahamishwe.

  Amesema watumishi wengi katika ofisi hiyo anawaona hawana uwezo wakiwemo wasaidizi wake kama madereva, watunza kumbukumbu na makatibu muhtasi. “Hata aliyekuwa Katibu Tawala wa wilaya hii alihamishwa kwa sababu na kutoelewana na DC, na hata huyu Katibu Tawala wa Wilaya aliyepo sasa hana raha anataka kuhama kwa sababu hizo hizo.”

  “Lazima tuwatambue wasaidizi wetu na majukumu yao. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya haiwezekani ikawa hivi, lazima kuna shida kuwaondoa watumishi wote, Mkuu wa Mkoa fuatilia hii ni mpya. Hapa tujue mbovu ni nani Mkuu wa Mkoa tunataka tujue DC wako anataka dereva wa aina gani, tangu amefika hapa madereva 10 wote hawafai?

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa “ili mfanye kazi vizuri mnatakiwa mshikamane mfanye kazi kama timu moja kwani pamoja na shughuli mnazofanya hamna ushirikiano. DC (mkuu wa wilaya) sasa utabaki peke yako utakuwa unaandika mwenyewe, unaendesha gari mwenyewe maana wote hawafai. Mkuu Mkoa nakukabidhi majina ya watumishi hao ushughulikie suala hili. Na Katibu Tawala wa Mkoa usilete watumishi wengine hapa mpaka suala hili litakapopatiwa ufumbuzi”

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza halmashauri zote nchini zihakikishe zinatenga kiasi cha fedha katika makusanyo yao ya ndani kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati kwenye maeneo yao kama ujenzi wa vituo vya afya, barabara za halmashauri na masoko badala ya kutegemea fedha kutoka Serikali Kuu pekee.

  Amesema wilaya ya Kilolo ambayo haina kituo cha mabasi inatakiwa itenge fedha kutoka kwenye makusanyo yao na kuanzisha mradi wa kituo hicho ambao utekelezaji wake utaboresha huduma kwa wananchi pia, mradi huo utasaidia katika kuongeza mapato ya halmashauri. Halmashauri ya wilaya ya Kilolo inakusanya sh. bilioni nne kwa mwaka.

  Waziri Mkuu amesema watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwani wananchi wanahitaji waone matokeo ya uwepo wao kutokana na dhamana waliyotewa na Serikali katika wilaya hiyo. “Madiwani nanyi simamieni halmashauri yenu vizuri kwa sababu nyie ndiyo wenye dhamana ya kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri.”

  Awali, Mbunge wa jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya yao ikiwemo ya umeme, ambapo kati ya vijiji 94 vilivyoko vijiji 54 vimeunganishiwa huduma hiyo na vilivyosalia vitakuwa viunganishiwa umeme ifikapo Desemba mwaka huu.

  Akizungumzia kuhusu miradi ya maji mbunge huyo alisema kati ya vijiji 94 vya wilaya hiyo vijiji 15 tu ndio bado havina maji ya uhakika lakini wanaendelea na mchakato wa ufuatiliaji ili kuhakikisha navyo vipata maji safi na salama.”Kuhusu sekta ya elimu tatizo tulilonalo ni madai ya walimu waliohama na waliopandishwa madaraja.” Waziri Mkuu amesema suala hilo linafanyiwa kazi.

  Mapema, Waziri Mkuu alikagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kupokea taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo ambapo alisema ameridhishwa na ujenzi huo uliogharimu sh. bilioni nne na alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa wilaya hiyo akiwemo Mkurugenzi pamoja na mkandarasi anayenga.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi wa mionzi, Frank Mwamakula, ambaye ni mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Mafunzo hayo yametolewa leo na Tume hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala, akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uchunguzi wa mionzi kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanza(Na Mpiga Picha Wetu).

  Washiriki wa mafunzo hayo.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
  0 0


  BENKI ya NMB, imewahakikishia askari wa Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa Serikali nchini, huduma bora, rafiki na sahihi za kibenki, zitakazokuza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, ili kuendana na kasi ya maendeleo kuelekea Uchumi wa Kati.

  Ahadi hiyo imetolewa na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi na Kati wa NMB, Ally Ngingite, katika siku ya pili ya Kikao Kazi cha Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

  Kikao Kazi hicho kiliozinduliwa Septemba 24 na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, kimefika ukomo jana Ijumaa Septemba 27, 2019 ambapo kwa siku nne maofisa hao wamejadili juu ya mafanikio, changamoto na
  mikakati ya Kamisheni katika Kuzuia, Kupambana na Kutanzua Uhalifu.

  Kupitia Kikao Kazi hicho kinachofanyika chini ya Kaulimbiu: Umoja Wetu Ndiyo Nguvu Yetu, Tudumishe Usalama Katika Uchumi wa Viwanda, wadau wa Jeshi la Polisi wamealikwa kushiriki, ikiwemo NMB iliyotoa ahadi ya
  ushirikiano wa kudumu, sambamba na huduma bora kwa askari polisi nchini.

  Ngingite aliwataka maofisa na makamanda hao kuwa mabalozi wema wa benki hiyo kwa askari walio chini yao kote nchini na kwamba wanapaswa kuifanya NMB kama mshirika wa kweli katika kujikweza kiuchumi kupitia mikopo na aina nyingine za uwezeshaji kutoka katika benki hiyo.

  “Makamanda na maofisa wote mlioshiriki Kikao Kazi hiki, mkitoka hapa huku mnafikiria namna sahihi ya kuboresha maisha yenu ya sasa na baadaye, kukuza pato lenu kuelekea Uchumi wa Kati, maana yake ni kuwa askari wote nchini walioko chini yenu watafikia kufanya hivyo pia.

  “Unafuu wa huduma zetu kwa Askari wa Jeshi la Polisi, majeshi mengine na Wafanyakazi wa Serikali, unatokana na ukweli kwamba tunatambua, kuthamini na kujali mchango wenu kwetu kama taasisi ya kifedha,” alisema Ngingite,
  ambaye alipokea maoni mbalimbali kutoka kwa makamanda hao.

  Aliwaomba askari hao wanapoamua kukopa, kuhakikisha wanaitumia mikopo hiyo kwa usahihi, na kwamba siri ya mafanikio iko katika kufikiria kabla ya kukopa, kufanya uwekezaji mdogo baada ya kukopa ili kutanua pato lao na hatimaye kupunguza makali ya marejesho.

  Akizindua Kikao Kazi hicho juzi, IGP Sirro aliwataka askari hao kuhakikisha wanajitoa kadri wawezavyo katika kulitumikia taifa na kwamba yeye anatamani kumaliza nafasi yake Jeshi likiwa na heshima, ambayo itapatikana kwa kila mmoja kuacha unafiki, kwani likichafuka, watachafuka wote.

  0 0


  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike akitoa hotuba ya
  ufunguzi wa Kikao Maalum cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza leo 28
  Septemba, 2019 Mkoani Morogoro.
  Meneja wa SACCOS ya Magereza(TPS SACCOS), Kamishna Msaidizi wa
  Magereza, Abdallah Missanga akitoa ufafanuzi wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Chama hicho cha Ushirika cha Jeshi la Magereza mbele ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.
  Kamishna wa Huduma za Urekebishaji na Urekebu, Tusekile Mwaisabila
  akitoa utambulisho mfupi wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya
  kumkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza kufungua rasmi kikao kazi hicho.
  Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
  Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa
  Magereza, Phaustine Kasike (hayupo pichani).
  Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Magereza,
  Josephine Mbogo(kushoto), Mkuu wa Magereza Mkoani Geita, Kamishna Msaidizi
  wa Magereza, Edith Mbogo(katikati) na Mkuu wa Magereza Mkoani Pwani,
  Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rehema Ezekiel kwa pamoja wakiteta jambo mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambacho kimefanyika kwa siku moja leo 28 Septemba, 2019 Mkoani Morogoro.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike, akisalimiana na
  Naibu Kamishna wa Magereza, Afwilile Mwakijungu mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Nanenane, Mkoani Mororogoro tayari kwa Kikao Maalum cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja leo 28 Septemba, 2019 Mkoani Morogoro.

  0 0


  · Maelfu wahudhuria gulio la Vodacom M-pesa jijini Dar es salaam. 

  · Wateja na Umma kwa ujumla kunufaika na huduma za M-pesa zinazoruhusu malipo kwenda mitandao na mabenki yote. 

  Kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza Tanzania, Vodacom Tanzania PLC leo imezindua huduma yake ya LIPA KWA SIMU katika gulio la M-pesa lililofanyika Mlimani City Mall jijini Dar es salaam. Gulio hilo lina lengo la kuongeza ufahamu wa upana wa huduma za kifedha zinazotolewa na mfumo wake mpya wa malipo. 

  Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa M-Pesa Epimack Mbeteni alisema kwamba Vodacom Tanzania iliona hitaji la kupanua mfumo wa LIPA kwa M-Pesa kutoka katika mfumo wa M-Pesa, na kuanza kupokea malipo kutoka mitandao na benki zote na kufikia katika kuwezesha malipo ya kidijitali katika mifumo ya rejareja na manunuzi mitandaoni. 

  Amesema kwamba Vodacom imezindua huduma ya "Lipa Kwa Simu" kuhamasisha matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali kama njia kuu ya malipo nchini, na kuhama kutoka katika utegemezi mkubwa wa fedha taslimu uliopo sasa. 

  "Lipa kwa Simu ni hatua ya kimapinduzi iliyochukuliwa na kampuni ya Vodacom kuelekea katika kujenga jamii isiyotumia fedha taslimu kwa kusaidia ushirikiano wa malipo katika mitandao na benki zote. Kwa kutumia huduma ya Lipa kwa Simu, wafanyabiashara na wamiliki wa biashara wanaweza kupokea malipo kutoka katika mitandao na benki zote na kuongeza ufanisi na usalama katika biashara zao. Na kwa upande wa wateja, bila kujali unatumia mtandao gani, sasa unaweza kufanya malipo kupitia mfumo wa LIPA kwa kutumia gharama za kawaida za kuhamisha fedha. Jambo ambalo linaondoa mahitaji ya kutembea na kiasi kikubwa cha fedha taslimu," alisema Mbeteni. 

  Vodacom imewezesha LIPA kwa Simu kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara wa sekta zote kama Baa, Hoteli, migahawa, Supamaketi, Vituo vya mafuta, kumbi za sinema, maduka ya dawa, Maduka ya vifaa vya ujenzi na kadhalika kwahivyo inapatikana kote. 

  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo ameipongeza huduma hii inayotolewa na M-Pesa na kusema kwamba imerahisisha na kuleta ufanisi katika mifumo ya malipo ya Umma kwa sababu sasa wateja wanaweza kulipia bili, tozo na huduma nyingi za kijamii kupitia mfumo huu wakiwa sehemu yeyote ile, iwe nyumbani au maeneo yao ya kazi. 

  "Serikali inajivunia kuwa mshirika katika huduma ya fedha kupitia simu za mkononi, kwa sababu watu wanaweza kufanya malipo kwetu. Iwe katika mifumo ya mahakama za manispaa, polisi au huduma za afya na nyinginezo. Jambo hili limeongeza uwazi na hali ya kukidhi taratibu za malipo kwa jamii," aliongeza Kayombo. 

  Gulio la M-Pesa lililofanywa na kampuni ya Vodacom lilivutia maelfu ya wateja, wafanyabishara na jamii kwa ujumla ambao walikuja kujifunza na kuona jinsi ambavyo mfumo mpya wa Lipa kwa Simu umerahisisha huduma ya malipo nchini. 

  Kwa upande wake, Bi Mwajuma Hamisi amesherehekea mfumo wa Lipa kwa Simu akisema kwamba ni mfumo ambao utaleta mabadiliko kwa kuwa hakutakuwa na haja tena ya kutembea na kiasi kikubwa cha fedha au kulipia gharama za miamala za kuhamisha fedha kutoka benki kwenda katika simu za mkononi. 

  "Nimenunua vipodozi na vitu vingine kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali hapa katika gulio na nilichofanya ni kuscan msimbo wa majibu ya haraka (QR Code) katika tili ya Lipa kwa Simu na niliweza kulipa moja kwa moja kutoka katika benki yangu. Hii ina maanisha kwamba ninaweza sasa kufuatilia malipo yangu yote kadri yatakavyokuwa yanafanyika kutoka benki," aliongeza bi Mwajuma.
  Msemaji Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji, Mrakibu Mwandamizi Al-Hajj Ally Mtanda akitoa maelezo kuhusiana na huduma za idara ya Uhamiaji kwa Mkurugenzi wa M-pesa Vodacom Tanzania PLC, Epimack Mbeteni leo jijini Dar Es Salaam, kwenye gulio la M-Pesa (M-Pesa Expo).

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Iringa Mjini na Iringa Vijijini pamoja na vionzi wa Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa, Septemba 28, 2019.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Iringa Mini na Iringa Vijijini pamoja na vionzi wa Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa, Septemba 28, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa muda wa saa nne kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Himid Njovu awe ameandika barua ya kusitisha ujenzi wa ukumbi wa mikutano na sherehe katika eneo la shule ya msingi Gangilonga.

  Amesema maeneo yote ya taasisi za elimu nchini hayaruhusiwi kujengwa miradi ambayo haihusiani na masuala ya elimu, hivyo amtaka mkurugenzi huyo kusitisha mkataba na mtu aliyemkodisha eneo hilo na kisha alizungushie uzio kwa matumizi ya shule.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Septemba 28, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Madiwani wa Halmashauri hizo akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.

  “Mkurugenzi kafute mikata yote ya ujenzi wa miradi katika eneo la shule ya Gangilonga pamoja na shule ya Wilolesi kwa sababu maeneo hayo hayaruhusiwi kujengwa miradi isiyohusiana na elimu. Eneo hilo lisafishwe na ujengwe uzio.”

  Kwa upande wake, Mwanasheria wa Manispaa ya Iringa Nocholous Mwasungura amesema aliandaa mkataba wa kupangisha eneo kwa maelekezo ya Kamati ya Fedha, ambapo Waziri Mkuu alimuuliza kwa nini hakuwashauri kuhusu suala hilo kwa sababu tayari Serikali ilishatoa waraka wa kuzuia jambo hilo.

  Pia, Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi ofisi ya ardhi ya Manispaa ya Iringa kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka wananchi juu ya Afisa Ardhi ambaye anadaiwa kujigawia viwanja vingi pamoja na kugawa kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja.

  Awali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi aliwaonya watumishi hao kutojihusisha na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kuacha chuki, ubinafsi na roho mbaya na badala yake washikamane na wafanye kazi wa bidii.

  Naye,Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesera aliiomba Serikali izisaidie halmashauri za wilaya hiyo vyombo vya usafiri kwa sababu magari mengi ni chakavu hali inayosababisha Mkurugenzi wa Manispaa awe anaomba lifti kwake. Waziri Mkuu amewataka waombe kibali cha ununuzi wa magari na watumie fedha zao za ndani.

  0 0

  Tanga, Septemba 27, 2019-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni inayolenga kutoa elimu kwa umma juu ya unywaji wa kistaarabu, ikiwa ni moja ya hatua muhimu inayochukuliwa na kampuni hiyo kuzuia ajali nyingi zinazosababishwa na madereva wanaoendesha wakiwa wametumia vilevi 

  Kampeni hiyo inayobeba ujumbe wa, “Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ imezinduliwa jijini Tanga leo katika Stendi ya mabasi na kuwakutanisha pamoja wadau mbalimbali ikiwamo Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, madereva, abiria, na wadau wengine katika sekta ya usafirishaji 

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) Tanga, Solomon Mwangamilo, amesema kwa kulishirikisha jeshi la Polisi kampuni ya SBL imeiunga mkono serikali katika kuelimisha umma juu ya unywaji wa kistaarabu na kusisitiza umuhimu wa kutatua tatizo hilo. 

  RTO amesema baadhi ya watu na haswa madereva hunywa kiasi kikubwa cha pombe pasipo kujali madhara yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho na kuonya kuwa vitendo vya aina hiyo vinaweza kusababisha ajali mbaya barabarani. 

  “Sote tunafahamu kuwa matumizi ya vileo yana uhusiano mkubwa na uendeshaji mmbovu ambao unaweza husababisha ajali mbaya za barabarani zenye athari kubwa kwa jamii zetu. Athari zake siyo tu zinawagusa watumiaji wa vilevi bali hata maisha ya wengine na kusababisha upotevu wa maisha na ulemavu kwa watu ambao wangeweza kuchangia uchumi wa nchi,” amesema. 

  RTO ameongeza kusema kuwa pamoja na kusababisha vifo visivyotarajiwa na majeraha, unywaji usiokuwa wa kistaarabu una maadhara makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha kinatumika kwa ajili ya huduma, madawa na vifaa tiba kwa waathirika wa ajali za barabarani na hivyo kuwa ni mzigo kwa Serikali. 

  Akizungumzia namna kampeni hiyo itakavyoisadia jamii, mkuu huyo wa usalama barabarani amesema, “sote kwa pamoja ikiwamo askari, madereva, jamii na wadau wengine tuna jumuku la kutafuta suluhisho la kumaliza tatizo la kutumia vilevi na kuendesha vyombo vya moto. Ninayo furaha kuona SBL pamoja na kwamba biashara yao ni kuuza vilevi, wameona wanawajibu wa kuhimiza unywaji wa kistarabu”. 

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyancha amesema kampeni ya unywaji wea kistaarabu inalenga kuielimisha jamii kuwa wanywaji wanapaswa kunywa kwa kiasi na kuhakikisha unywaji wao hauna madhara kwao na kwa watu wanaowazunguka. 

  “SBL imedhamiria kuungana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa jamii na haswa madereva ambao wanakunywa na kuendesha vyombo vya moto wanaelimishwa juu ya madhara ya vitendo hivyo na kutakiwa kubadilisha tabia,” amesema Wanyancha. 

  Kampeni hii ambayo imekuwa ikifanyika katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania, inalenga kuwafikia vijana na watu wengine kwa kuwaeliisha juu ya madhara ya unywaji usiokuwa wa kistaarabu huku ikiwataka kubadili tabia kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla

  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tanga, Solomon Mwangamilo, akimvalisha reflector mmoja wa madereva wa pikipiki (bodaboda) katika tukio la uzinduzi wa kampeni ya ‘Don’t Drink and Drive’ inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti ikiwa na lengo la kutokomeza ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva walevi.

  0 0

   Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza akipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
  Wanamitindo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (kulia) akipita mwanamitindo kuonyesha mavazi. 
  Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu akipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019), Bi. Joyce Fisoo akipita kuonyesha mavazi.
  Mbunge wa Viti maalumu (CCM), Halima Bulembo akipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
  Mwanamitindo akipita kuonyesha vazi la ubunifu wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe afuatilia maonyesho ya mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika Dar es Salaam, Tanzania.
   Mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali akizungumza wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika usiku wa leo jijini Dar es Salaam, Tanzania.
   Mshereheshaji Taji Liundi akiunguruma katika maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
  Wanamitindo wenye mahitaji maalum wakionyesha mavazi katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika usiku wa leo jijini Dar es Salaam, Tanzania.
   Mbunifu wa mavazi Khadija Mwanamboka akipita katika wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
  Wanamitindo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa maonyesho ya mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akimvalisha tuzo maalum ya mavazi ya Vazi la JAMAFEST 2019 kwa Mwanamitindo Whitney yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akipewa zawadi ya kofia na Mbunifu wa Mavazi kutoka nchini Burundi.
  Burudani ya ngoma ikiendelea.
  Wanamitindo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

  0 0  Msanii bongofleva kutoka kundi la Weusi Gnako akisajili laini yeke kwa mfumo wa alama za vidole katika duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza Anayeshuhudia pembeni yake ni Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019 Jijini Mwanza.


  Msanii bongofleva Billnass akiangalia simu zinazouzwa katika duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza pembeni yake ni Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019 Jijini Mwanza.
  Wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako Jijini Mwanza wakifurahi jambo mara baada ya kutembelea na kusajili laini kwa alama za vidole na kuona huduma mbalmbali zinazotolewa na duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019 Jijini Mwanza.


  Wasanii watakaotumbuiza katika tamaha la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako Jijini Mwanza wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kutembelea na kusajili laini kwa alama za vidole na kuona huduma mali mbali duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019 Jijini Mwanza.


  Msanii bongofleva Billnass akisajili laini yake kwa mfumo wa alama za vidole alipotembelea duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019_Saizi yako Jijini Mwanza.
  Msanii wa Nyimbo za Injili Goodluck Gozbert akiwa Pamoja na msanii chipukizi wa Bongofleva Badest walipofika kusajili laini zao kwa alama za vidole na kuona huduma mali mbali duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019_Saizi Yako Jijini Mwanza.

  0 0

  Watanzania wametakiwa kuyafanya majukumu ya kitaifa wanayopewa na viongozi wa serikali kwa uzalendo usiotiliwa mashaka,uamini na ufanisi kama walivyoelekezwa wakati wa kukabidhiwa majukumu hayo kwa faida ya Nchi.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akitoa Kongole kwa Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim kufuatia kitendo cha kukabidhiwa Nishani ya Juu ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China nishani ambayo inamfanya Dkt. Salim kuwa mwafrika wa kwanza kupewa heshima na tuzo hiyo ya juu katika historia ya China.

  Prof. Kabudi ameongeza kuwa nishani aliyokabidhiwa Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim imeliletea heshima kubwa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nay eye mwenyewe kutokana na utendaji wake usiotiliwa mashaka baada ya kuaminiwa na kukabidhwa majukumu hayo na Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuwataka Watanzania wote hususani vijana kuiga mfano huo.

  Amesema Dkt Salim Ahmed Salim ni Mtumishi mwaminifu na mzalendo kwa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameitumikia nchi katika nafasi mbalimbali kuanzia na ukurugenzi katika wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki balozi katika nchi za Misri,India,China na Umoja wa Matifa lakini pia ,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Waziri wa Mambo ya Nje,Naibu waziri Mkuu kisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadae Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

  Nishani hiyo iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping ilipokelewa na Bi. Maryam Salim, Binti ya Dk. Salim Ahmed Salim ambaye pia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Albania kwa niaba ya Baba yake kutokana na kushindwa kuhudhuria kwa sababu za kiafya.

  Katika tukio hilo, Serikali ya Tanzania iliwakilisha na Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki.

  Hafla hiyo kubwa ya kitaifa ya kukabidhi nishani ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Chama na Serikali ya China akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Wang Qishan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang, Spika wa Bunge Mheshimiwa Li Zhanshu na Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Taifa.

  Nishani ya Juu ya Urafiki ya Taifa la China imetolewa kwa Dkt. Salim kutokana na mchango wake wa kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kuwa Mwanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1971 alipokuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

  Aidha, mchango wa Dk. Salim katika kuimarisha mahusiano kati ya China na Tanzania wakati aliposhikilia nyadhifa mbalimbali umetajwa kama sababu ya kutunukiwa Nishani hiyo. Vilevile, mchango wa Dk.Salim katika kujenga mahusiano kati ya China na Afrika akiwa na nafasi ya Katibu Mkuu wa OAU umetajwa kuwa sababu nyingine ya kutunukiwa Nishani.

  Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini China Balozi Mbelwa Kairuki amesema mamilioni ya Wachina hususani vijana wamepata fursa ya kufahamu nafasi na mchango wa Tanzania na Bara la Afrika katika historia ya taifa lao.

  Aidha, tukio la leo limeifanya Tanzania kufahamika kwa watu wengi zaidi nchini China kupitia tukio mara moja. Hatua hiyo itaamsha udadisi na hamasa miongoni mwa Wachina wengi wa kizazi kipya kutaka kuifahamu zaidi Tanzania. Hali hii yaweza kujitafsiri katika fursa kubwa ya kukua kwa utalii, biashara na wawekezaji ikizingatiwa kuwa wananchi wa China hutoa mwitikio mkubwa kwa nchi ambazo husemwa vizuri na kuthaminiwa na Serikali yao.

  Ni kwasababu hiyo, katika maadhimisho ya miaka 70 ya Taifa la China, Jumuiya ya Urafiki wa watu wa China na Tanzania ni miongoni mwa Jumuiya za mataifa 17 yenye urafiki wa majira yote na China walioalikwa kushiriki kwenye maadhimisho hayo na tarehe 1 Oktoba 2019 watakuwa na gwaride lao maalum. Katika jumuiya hizo 17, Kutoka Barani Afrika ni Tanzania na Zambia ndio watahudhuria.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akiuliza swali kwa Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile (wa kwanza kushoto mwenye kofia) wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula wakisalimiana na uongozi wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha (CSTC) walipotembelea kiwandani hapo kwa lengo la kukagua mazingira ya kiwanda hicho, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake mkoani Lindi ili kusikiliza na kutatucha changamoto za wawekezaji. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula akijibu hoja za masuala ya ardhi kwa watendaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha (CSTC) kilichopo Wilaya ya Lindi Vijijini alipotembea mwishoni mwa wiki. Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kuchakata mihogo katika kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki (kushoto kake) pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (kulia kwake) kilichopo Lindi alipotembelea kiwandani hapo. Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kuchakata mihogo inayotumika katika kiwanda cha CSTC kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula kilichopo Lindi Vijijini alipotembelea kiwandani hapo.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (mwenye kofia) wakiangalia moja ya mfuko wa unga wa muhogo uliotengenezwa na kiwanda hicho.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (mwenye kofia) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Shaibu Ndemanga (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi na watumishi wa kiuwanda cha kutengeneza unga wa muhogo kilichopo Lindi.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Tuzo ya Shukurani, Mkurugenzi Mkuu wa Makmpuni ya ASAS, Salim Abri kutokana na mchango wake mkubwa katika huduma mbalimbali za jamii mkoani Iringa. Tuzo hiyo imetolewa na Halmashauri ya Mji wa Iringa. Wa pili kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Mizengo Pinda, wa pili kulia ni Naibu Waziri Ofis ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipowasili kwenye uwanja wa Kichangni Kihesa mjini Iringa kuzindua Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Walemavu, Septemba 29, 2019. Wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozindua Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapngia wazee wakati alipozindua Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wazee wakati alipozindua Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na wazee waliojitokeza kupata huduma za tiba na vipimo wakati Waziri Mkuu alipozindua Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

older | 1 | .... | 1880 | 1881 | (Page 1882) | 1883 | 1884 | .... | 1897 | newer