Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

KWETU FASHION YAPAGAWISHA CALIFORNIA SHEREHE ZA UHURU!

$
0
0
  Nuthing Makes a Woman more beautiful than the Belief that She is Beautiful..Trust Kwetu Fashion Design to Compliment your Beauty
            Juu na chini Kwetu fashion ilivyo pepea California.....Ndiyo habari ya mujini
            PICHA ZAIDI BOFYA WWW.SWAHILITV.BLOGSPOT.COM



Rais Kikwete aongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akingoza kikao cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika katika makao makuu ya CCM Mjini Dodoma mchana huu.Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein na kulia ni katibu Mkuu wa CCM Bwana Abdulrahman Kinana. 
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akutana na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia Kujadiliana Kuhusu Masuala ya Gesi Nchini

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiongoza kikao kati yake na Ujumbe  kutoka Benki ya Dunia pamoja na Watendaji wa Wizara. Kikao hicho kimejadiliana kuhusu suala zima la Gesi nchini na hatua mbalimbali zilizofikiwa hadi sasa.


Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuzungumzia Masuala ya Gasi nchini. Miongoni mwa Masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni kuhusu hatua mbalimbali ambazo zimefikiwa hadi sasa na Serikali kuhusu Sekta hiyo. Aidha, kikao hicho pia kimewashirikisha Watendaji kutoka Wizara hiyo wanaosimamia masuala ya Gesi Asilia na Nishati.
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiongoza kikao kati yake na Ujumbe  kutoka Benki ya Dunia pamoja na Watendaji wa Wizara. Kikao hicho kimejadiliana kuhusu suala zima la Gesi nchini na hatua mbalimbali zilizofikiwa hadi sasa.

 Kamishna Msaidizi anayesimamia Masuala ya Gesi Asilia Engineer. Bw. Nobert Kahyoza akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.

 Kamishna Msaidizi anayesimamia Maendeleo ya Nishati Bw. James Andilile  akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho baina ya Wizara na Ujumbe toka benki ya Dunia.

MCHEZAJI WA ZAMANI WA KLABU YA MANCHESTER UNITED ANDY COLE ATUA JIJINI DAR

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimkaribisha Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) mara tu baada ya kuwasili nchini kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kati kati ni Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole akikabidhiwa maua mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania .
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kushoto) akimuongoza Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (katikati) kuelekea sehemu ya VIP kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)mara tu baada ya kuwasili nchini jana usiku.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) pamoja na Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (kulia) wakikamilisha taratibu zakupata hati ya kuingia nchini kwenye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania .
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimuelekeza jambo Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (katika) mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kushoto ni Picha na Mpiga picha wetu. Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (mbele) akitoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwelekea hotelini alipofikia mara bada ya kuwasili nchini jana usiku. Nyuma yake ni mwenyeji waka ambaye ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando . 

KILA LAKHERI MZEE WETU GURUMO.

YALIYOJIRI KWENYE MAHAFALI YA 19 YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI DAR ES SALAAM (DSJ)‏‎

$
0
0
Mahafali ya 19 ya chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) yamefanyika ijumaa ya desemba 13 mwaka huu ambapo wahitimu katika ngazi za stashahada na cheti kwenye fani ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma, na mahuasiano ya umma wamehitimu.

Tazama picha za baadhi ya matukio wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
 Mgeni  rasmi akiwa katika meza kuu  na Mkuu wa chuo , pamoja na viongozi wengine wa chuo na viongozi wa Serikali ya wanafunzi 

 Kutoka kushoto ni Fabian, Dotto Mandolin Kahindi, Abushehe Nondo, Benjamin Mwangoka
  Wahitimu wakiwa katika mahafali hayo 

Rais Mstaafu wa DASJOSO Alfred Ochali akisoma risala
 Mkuu wa Chuo cha DSJ, Joachim Rupepo akitoa hotuba yake na kumkaribisha mgeni rasmi kutoa nasaha zake
Mgeni Rasmi Bi. Jimhada malembeka akitoa nasaha  kwa niaba ya Meya wa manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa

 Wahitimu wakiwa wanasikiliza kwa umakini hotuba kutoka kwa mgeni rasmi
Kutoka kushoto ni  Anifa, Grace, Zourha na Cartace ambao pia walikuwa wahitimu katika mahafali hayo
Wahitimu wakiwa wanatunukiwa
Wahitimu wakiwa wanatoa mkono wa Shukurani baada ya kutunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali

Wahitimu wakiwa katika pozi baada ya kumaliza mahafali
Baadhi ya wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu zao
Kutoka kushoto ni Elizabeth Lazaro akiwa na Jackline  Marandu ambao pia ni wahitimu.
 Wageni waalikwa wakiwa wanafuatilia kwa makini kinacho endelea katika mahafali hayo 
 Kwaito time

VIJANA WATAKIWA KUSHIKAMANA NA KUJIKUZA KWENYE UKWELI.

$
0
0
Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Hassan Othman Ngwali akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Al-Madrasat Amir iliyopo Bweleo Wilaya ya Magharibi Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
 Jengo jipya la Al-Madrasat Amir lililofunguliwa leo na naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar katika kijiji cha Bweleo Wilaya ya Magharibi Unguja. 
 Mkuu wa Madrasa za Unguja na Pemba Shekh. Khamis Abdulhamid akitoa nasaha kwa wanafunzi kabla ya ufunguzi wa Al-Madrasat Amir katika kijiji cha Bweleo Wilaya ya Magharibi Unguja.

==========   ===========

Na Miza Kona  Maelezo Zanzibar 
Vijana wametakiwa kushikamana na kujikuza kwenye ukweli ili wapate kuongoka katika maisha yao ya dunia na akhera .

Hayo yameelezwa leo na Naibu Kadhi Mkuu Shekhe Hassan Othman Ngwali wakati alipokuwa akifungua madrasa Amir ya Bweleo. Amesema kuwa ukweli na uaminifu ndio unaomkuza mja kuongoka katika misngi iliyomema na kuachana na tabia mbaya inapelekea kujiingiza katika vikundi viovu.

Aidha amesema vijana wakijitahidi kujifunza katika misingi ya dini na kishirikiana katika ukweli na uaminifu na kuyafanyia kazi wataweza kuepukana na vishawishi vibaya na kuogopa kufanya maovu.  Aidha amewasitiza vijana kusoma kwa bidii na kuacha kufanya mchezo katika kutafuta elimu ili wasije kuijutia baabae.

Hata hivyo amewataka vijana hao kufufuata mwenendo wa Mtume SAW ili kuweza kuendeleza mbele dini ya kiislam. Aidha amewahimiza wazazi kuwakuza watoto wao katika misingi ya kiislamu kwa kuitafuta elimu hiyo kwani vijana ndio taifa la kesho na kupata viongzi wazuri wa baadae.
  
Aidha ameuomba uongozi wa madrasa hiyo kuwa na umoja,  imani na kujiepusha na  makundi kwa kuwa na maamuzi ya pamoja  ili ipate kuendelea vizuri na kuongeza watoto wenye misingi ya dini na imani.
Zaidi ya shilingi milioni 20 zimetumika hadi kukamilika ujenzi wa madrasa hiyo ambayo yenye madarasa manne


MAWAZIRI WAHENYA NA MAFAILI KUHOJIWA NA KAMATI KUU YA CCM MJINI DODOMA

$
0
0

NA BASHIR NKOROMO

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kikao chake kilichofanyika jana mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete imeibuka na masuala mazito kadhaa, ambayo leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (pichani) ameyaeleza wakati akizungumza na waandishi wa Habari, Katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijini Dar es Salaam.

Moja ya mambo ambayo Nape amezungumzia, ni kuhusu Kamati Kuu hiyo kuwahoji Mawaziri saba, kujibu kero au mambo kadhaa ambayo yaliibuliwa wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana iliyomalizika hivi karibuni katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe.

Nape  alisema, Kamati Kuu iliwahoji mmoja baada ya mwingine, kuanzia saa tano asubuhi hadi jioni, baada ya kila mmoja kufika akiwa ameandaa majibu ya tuhuma au hoja alizokuwa ametakiwa kujibu mbele ya Kamati Kuu hiyo.

"Kwa kuwa mawaziri hao tulikuwa tumeshawapelekea hoja zinazowahusu ambazo tulizipisha kwa kiranja wao Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wengi wao walifika wakiwa na mafaili yenye majibu, ambapo waliingia na kujieleza mmoja baada ya mwingine, na baada ya maelezo ya kila mmoja wajumbe walitoa mapendekezo kwa Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete", alisema Nape.

Hata hivyo Nape alisema, si vema kueleza kwenye vyombo vya habari kuhusu mapendekezo ambayo Kamati Kuu ilimshauri Mwenyekiti kuchukua, akisema kufanya hivyo itakuwa sawa na kumshinikiza kiongozi huyo kutekeleza mapendekezo yao kwa lazima na hivyo kuharibu maana nzima ya ushauri.

"Sisi tulichofanya ni kumpa mapendekezo, naye kwa mujibu na namna atakavyoona inafaa, atachukua hatua, ambavyo si lazima kumfukuza Waziri Kama wengi wanavyotaka iwe, bali anaweza kuchukua hatua yoyote ili mradi yeye mwenyewe kwa mamlaka aliyo nayo ataona ina manufaa yatakayotoa majibu ya kero zilizosaababisha kila mmoja wa mawaziri hao kuitwa mbele ya Kamati Kuu", alisema Nape.

IFUATAYO NI TAARIFA YOTE KAMA ALIVYOITOA NAPE LEO.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana mjini Dodoma kwa kikao chake cha kawaida tarehe 13/12/2013. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete.

Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ilipokea taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti kwenye baadhi ya mikoa nchini.
Kamati Kuu imepongeza ziara hizo kwa kuwa na mafanikio makubwa na kwa jinsi zilivyoongeza uhai wa Chama na zilivyojishughulisha na mambo na mahitaji ya wanachi.

Aidha Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye maeneo yote ambayo Katibu Mkuu ametembea. Maeneo yaliyopongezwa ni pamoja na Miundombinu hasa barabara, hatua kubwa kwenye fursa na ubora wa elimu, maeneo ya afya na umeme vijijini.

Kamati Kuu iliwaita mawaziri saba kuja kutoa maelezo ya mambo mbalimbali yaliyoibuliwa kwenye ziara hizo za Katibu Mkuu wa CCM. Mawaziri hao ni;-

i). Ndg. Christopher Chiza- Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
ii). Ndg. Shukuru Kawambwa- Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
iii). Ndg. Celina Kombani - Waziri wa Utumishi
iv). Ndg. Hawa Ghasia -Waziri wa TAMISEMI
v). Ndg. Abdallah Kigoda- Waziri wa Viwanda na Biashara
vi). Ndg. Mathayo David Mathayo- Waziri wa Mifugo na Uvuvi
vii). Ndg. Saada Mkuya- Naibu Waziri wa Fedha( kwa niaba ya Waziri wa Fedha).
Baada ya maelezo ya kutosha kutoka kwa mawaziri husika, Kamati Kuu iliagiza yafuatayo kwa Serikali;-

1.Kuhusu wakulima wa Pamba
(i). Serikali iangalie upya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa Pamba nchini.
(ii). Uwepo wa mbegu bora ni muhimu lakini ni vizuri pakawa na ushindani unaozingatia ubora ili kuondoa ukiritimba wa mtengenezaji mmoja, hivyo kusaidia bei kuwa nzuri kwa wakulima. Hata hivyo Chama kimeiagiza serikali kutowalazimisha wakulima kutumia mbegu ya Quiton badala yake elimu itumike zaidi badala ya nguvu. Serikali imetakiwa kuangalia upya utaratibu wa kutoza bei ya mbegu ya Quiton kwa dola za kimarekani badala ya pesa ya kitanzania,wakizingatia mbegu hiyo inazalishwa nchini.
(iii).Kamati Kuu imepongeza juhudi za Serikali kuvutia wawekezaji kwenye viwanda vya pamba mjini Shinyanga, hata hivyo imeitaka Serikali kuangalia upya urasimu katika uwekezaji wa viwanda nchini hasa vinavyoongeza thamani ya mazao na kutoa ajira nyingi nchini.

(iv). Kuhusu kilimo cha mkataba kwa wakulima wa Pamba, Serikali imetakiwa kuratibu utaratibu wa kilimo hicho cha mkataba ili kuhakikisha kunakuwa na sheria na kanuni zinazosimamia mfumo huo, ili kuwe na haki kwa pande zote mbili. Aidha wakulima wasilazimishwe kufanya kilimo cha mkataba bali waingie kwa hiari yao wenyewe.

2. Kuhusu wakulima wa Korosho.
(i). Pamoja na kuridhishwa na hatua za muda mfupi kwa msimu wa korosho kwa mwaka 2013/2014 ambazo zimesaidia bei na soko kuwa afadhali, bado Kamati Kuu imesisitiza Serikali kujipanga kutatua tatizo la korosho kwa suluhisho la kudumu kwa kuhakikisha korosho ina banguliwa nchini.

(ii). Serikali imetakiwa kuangalia upya orodha ndefu ya makato wanayokatwa wakulima hasa wa korosho na vyama vya msingi au mamlaka zinginezo ili kuondoa makato yasiyo ya lazima ili kuongeza kipato cha mkulima.

(iii). Serikali pia imetakiwa kuangalia upya mfumo wa uendeshaji wa vyama vya ushirika nchini ili uwe ni ule wenye tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla badala ya huu wa sasa unaotoa mwanya kwa walaji kujipenyeza.

3. Kuhusu pembejeo za ruzuku
(i). Kamati Kuu imepokea taarifa ya malalamiko ya wakulima juu ya ufanyaji kazi wa mbolea ya Minjingu na kuagiza kuwa pamoja na kuendelea na utafiti wa nini kinachotokea kwenye mbolea hiyo ya Minjingu kiasi cha kuleta malalamiko yote hayo, wananchi wawe huru kutumia mbolea wanayoitaka badala ya kulazimishwa kutumia mbolea wanayoilalamikia ya Minjingu.

(ii). Serikali iangalie utaratibu bora wa kuratibu swala zima la pembejeo za ruzuku ili lifaidishe zaidi wakulima walio wengi badala ya utaratibu wa sasa ambao licha ya kulalamikiwa na wakulima unaotoa mwanya kwa watu wachache kutumia vibaya utaratibu huo kuiibia serikali na wakulima.

4. Kuhusu wakulima wa mahindi.
(i). Pamoja na Serikali kuanza kulipa madai ya wakulima wa mahindi kwa mikoa ya Ruvuma baada ya ziara ya Katibu Mkuu kwenye maeneo hayo, bado serikali imetakiwa kumalizia malipo yaliyobaki na kuhakikisha wanakomesha utaratibu wa kuwakopa wananchi mazao yao bila kuwalipa.

(ii). Utaratibu uwekwe wa kufanya tathimini mapema ya mahitaji na uwezo wa kununua  mahindi wa Serikali ili kuepusha utaratibu wa kuchukua mahindi ya wakulima bila kuwalipa.

5. Kuhusu madai mbalimbali ya waalimu.
(i). Kamati Kuu imesisitiza kupandishwa vyeo na kulipwa stahiki  zao waalimu ni haki yao ya msingi hivyo lazima itekelezwe bila kuwa na visingizio na ifanyike kwa haki.

(ii). Kamati Kuu imeiagiza Serikali kukamilisha haraka uhakiki wa madai ya waalimu na kuwalipa haki zao zote mapema iwezekanavyo. Lakini Kamati Kuu imeitaka Serikali kuhakikisha madeni haya hayazaliwi tena kwa kuweka mfumo utakao zuia madeni haya kuzaliwa.

(iii). Kuhusu wakuu wa idara mbalimbali wasiotenda haki kwa waalimu, na wale wanaotumia lugha mbaya na za kejeli kwa waalimu wakibainika wachukuliwe hatua mara moja.

(iv). Pamoja na kuwa Serikali inaangalia utaratibu bora wa kuboresha mawasiliano kati ya wizara zinazohusika na kusimamia waalimu, Kamati Kuu imeitaka Serikali jambo hili lifanyike mapema ili kupunguza malalamiko ya waalimu.

6. Kuhusu ubadhirifu kwenye Halmashauri.
(i). Kamati Kuu imekemea watendaji wachache wanaojihusisha na ubadhirifu kwenye Halmashauri mbalimbali nchini. Imewataka madiwani wa CCM kuwa wakali na wasiamamie vizuri halmashauri zao kuhakikisha fedha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kupata thamani ya fedha.
(ii). Aidha Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali na kwa haraka kwa wote wanaobainika kufanya ubadhirifu, ili iwe fundisho kwa wengine.

(iii). Serikali imeshauriwa kuangalia upya sheria kama zinakidhi mahitaji ya wakati na mazingira ya sasa ili kuongeza uwezo wa udhibiti na kuokoa pesa za walipakodi zinazopotea kwa walafi wachache kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.

7. Kuhusu tatizo la Maji nchini.
Kamati Kuu ilipokea taarifa ya tatizo kubwa la maji nchini, ambalo lilijitokeza kila sehemu aliyotembelea Katibu Mkuu. Chama kimeishauri Serikali kuchukua juhudi na mkakati wa makusudi na dharura kulitafutia ufumbuzi wa haraka na wakudumu tatizo la upatikanaji wa maji nchini.

8. Kuhusu migogoro ya Aridhi, Wafugaji na Wakulima.
Pamoja na kupokea taarifa juu ya migogoro mbalimbali ya wakulima ,wafugaji na wakulima nchini, kamati kuu imepongeza uamuzi wa bunge kuunda Kamati teule ya bunge na uamuzi wa kuiagiza kamati ya kudumu ya bunge ya aridhi, maliasili na mazingira kuchunguza migogoro hii na kutoa mapendekezo juu ya namna bora ya kuimaliza kabisa migogoro hii.

Aidha kamati kuu imeitaka Serikali na wabunge wa CCM kuzijadili kwa makini ripoti hizo na kufikia hitimisho la migogoro hii nchini. Hata hivyo Kamati Kuu imeitaka Serikali kuangalia upya utaratibu uliotumika kuwamilikisha watu wachache maeneo makubwa ya aridhi, ambao wameshindwa kuyaendeleza badala yake wanayatumia kuwakodishia wakulima wadogo.

Aidha maagizo yote haya yatatolewa taarifa kwenye Chama mara kwa mara, ili kuwezesha Chama kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010/2015.

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
14/12/2013

magari yakwama tandala Makete leo

$
0
0
 Fuso ikiwa imekwama.
Jamaa akichimba ili aweze kupita 
 
 Lori likiwa limebeba nguzo za umeme likiwa limekwana eneo la Lwamadovela wilayani Makete
 Basi la kampuni ya Mwafrika likipenya kwa tabu pembezoni lilipokwama lori lililobebe nguzo za umeme
Basi la kampuni ya Japanese nalo likivutwa kunasuka kwenye tope zito wakati likitafuta upenyo wa kupita.Picha zote na Edwin Moshi, makete

TAMASHA LA AFTER SKUL BUSH LAFANA NDANI YA MBALAMWEZI BEACH LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Mashabiki kibao wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri jukwaani jioni ya leo. 
 Baadhi ya wasanii chipukizi kutoka anga ya muziki wa Bongofleva pia walipewa nafasi ya kuonesha umahiri wao wa kulishambulia jukwaa vilivyo.
 Watangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu na Dj Fetty wakijadiliana jambo nyuma ya jukwaa.

 Mashabiki wakifurahi burudani iliyokuwa ikitolewa juu ya steji
 DJ Mahiri kutoka Clouds FM akifanya makamuzi ya nguvu ndani ya Mbalamwezi Beach,wakati wa tamasha la After Skull Bash likiendelea,Tamasha hilo limewakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali jioni ya leo.
 Msanii Nguli wa muziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda a.k.a Mtoto wa Mama Said akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar. 
 Mmoja wa watangazaji mahiri wa Clouds FM,Hamis Mandi a.k.a B Dozen akitoa utaratibu mzima wa tamasha hilo utakavyofanyika.Tamasha hilo limeratibiwa na Clouds FM kwa kushirikiana na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd.
 Msanii wa muziki wa Kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga ya muziki wa bongofleva,Rich Mavoko akikamua vilivyo jioni ya leo kwenye tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.
Mashabiki waliofika kwenye tamasha hilo wakifuatilia kwa makini

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA KIBADA,KIGAMBONI, DAR

$
0
0
 Kaimu Mhandisi wa Maji Manispaa ya Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Meckiline Haule (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa gharama ya sh. mil. 35 katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Isabela Ipopo (kushoto),Mwakilishi wa Mauzo wa TBL, Allen Mwebuga (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane
 Kaimu Mhandisi wa Maji Manispaa ya Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Meckiline Haule (katikati) akipokea ufunguo kutoka kwa Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Allen Mwebuga (wa pili kushoto) tayari kuzindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 35 katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Zahanati hiyo, Nassoro Sande (kulia) na Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Isabela Ipopo.
 Mwebuga wa TBL (kushoto) na Bakilane wakifujaza maji kwenye ndoo wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
 Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane  akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kijiji cha Kibada, Diana Salvatory baada ya kampuni hiyo kukabidhi kisima cha maji katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho chenye uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo 1,600 kwa saa uchimbaji umegharimu sh. mil 35 zilizotolewa msaada na TBL.

 Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Allen Mwebuga akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kijiji cha Kibada, Hidaya Mshindo baada ya kampuni hiyo kukabidhi kisima cha maji cha msaada katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho chenye uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo 1600 kwa saa uchimbaji umegharimu sh. mil 35 zilizotolewa msaada na TBL.
 Wakifurahi baada ya kuzindua kisima hicho

 Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Ipopo akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwasidia kisima hicho, hivyo kupunguza kwa asilimia kubwa tatizo la maji katika zahanati hiyo.
 Mkazi wa Kijiji cha Kibada akitoa shukrani wa TBL kwa msaada huo.
 Wakazi wa Kibada wakiangalia kisima hicho
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya TBL kusaidia miradi ya maji nchini ambapo kwa mwaka wafedha wa TBL tayari imetenga sh. mil. 450 kwa kazi hiyo.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

SALIM ABRI ASASI AWAPA SOMO UVCCM IRINGA

$
0
0

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa na kamanda wa vijana ccm Iringa Salim Abri Asas Abri akiwa katika moja ya matukio ya kuwahudumia wananchi  kulia ni RTO  SP Panfil Honono
==========  ========  =========
SALIM ABRI ASASI AWAPA SOMO UVCCM IRINGA

Na Denis Mlowe, Iringa

KAMANDA wa umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Iringa, Salim Asas ameunga mkono wito wa Mwenyekiti wa UVCCM mkoani humo, Tumaini Msowoya la kutaka vijana wa jumuiya hiyo wasikubali kugawanywa kwenye mambo ya siasa na watu wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ubunge,udiwani  ili kulinda heshima ya jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.

Akifunga mkutano wa uchaguzi wa Chipukizi wa mkoa huo, Abri alisema heshima ya jumuiya hiyo ni vijana kufanya kazi kwa mujibu wa kanuni na taratibu na sio mapenzi ya mtu bali ni sera ya chama ndio wanayotakiwa kuifuata na kuepuka ushawishi kutoka kwa watu wenye nia ya kuwagawanya.

Alisema ni jukumu ya UVCCM mkoa wa  Iringa ni kuhakikisha vijana hawafanyi kazi kwa maslahi ya watu wanaotaka uongozi mwaka 2015, jambo ambalo likiachwa liendelee linaweza kuimega na kuidhoofisha jumuiya yao inayojitegemea katika maamuzi kwa upande wa vijana.

Awali, akimkaribisha Kamanda huyo, Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Iringa, Tumani Msowoya alitoa wito kwa CCM na wanachama wanachama wake kuhakikisha kuwa, wanaiacha jumuiya yao ifanye kazi kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizopo kwa manufaa ya chama hicho na sio mtu au watu wenye nia ya kujinufaisha kupitia umoja wao.

Aliwaagiza viongozi wa UVCCM kwa ngazi zote kutoa taarifa ya kuwepo kwa baadhi ya watu wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi, ambao wanataka kuitumia jumuiya yao kama njia ya mafanikio yao kiuongozi.

“UVCCM ya sasa haitakubali kuyumbishwa wala kugawanywa na mtu yeyote mwenye nia ya kuomba madaraka, itafanya kazi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa na katiba ya chama hicho kwa upande wa vijana” alisema Msowoya.

Msowoya aliwataka vijana kufanya kazi kwa juhudi zote kwa lengo lakujiongezea kipato ikiwepo kujiunga kwenye vikundi vidogo vidogo kuweza kupatiwa mikopo ya riba nafuu kuliko kuwa mmoja mmoja na kushindwa kupata mikopo katika taasisi zinazohusika katika kutoa mikopo.

“Vijana wenzangu tuepuke kuchagua kazi kwa maisha ya sasa ebu jiulieze kama tutachagua kazi, tutaendelea kugawanywa kwani watatupatia fedha ili tulinde maslahi yao, nawaomba sana tusikubali kuwatetemekea wenye fedha wanaotaka madaraka kwa njia ya kuhonga badala yake kila mmoja afanye kazi kwa bidii ili kuwa na uhakika wa kipato anachokipata kwa kazi halali kuliko fedha ya muda mfupi majuto baadaye,”alisema Msowoya

Akizungumzia uchaguzi wa chipukizi mkoani humo, Katibu wa UVCCM mkoani humo Alawi Haidar alisema umefanyika kwa amani na utulivu na kwamba, watoto hao wameweza kuwapata viongozi bora walioona wanawafaa.

Akitangaza matokeo hayo, Haidar alisema Mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoani humo, Enock Luhala alifanikiwa kushindwa kwa kura 18 kati ya 33 zilizopigwa na kuwashinda wenzake, Ashraf Mpogole aliyepata kura 12 na Magreth Lusingo kura nne.

Katika nafasi ya mkutano mkuu wa chipukizi taifa, Junior Mlelwa alishinda kwa kura 26 na kuwabwaga wenzake, Halid Aziz na Christopher Dalu.

Wengine walioshinda ni Tausi Mgambo, Rukia Kimweli na Amina Kimweli kuwa wajumbe wa kamati ya uendeshaji mkoa.

Rais Kikwete atunuku Kamisheni Maofisa wa Jeshi la Wananchini,pia ampa pole Mh. Lowassa kwa kunusurika kwenye ajali ya ndege

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Luteni usu Evarist Mawalla wakati alipowatunuku Kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi Tanzania baada ya kuhitimu mafunzo yao katika Chuo Cha Jeshi Monduli Juu mjini Arusha jana.Luteni Usu Mawalla aliibuka mwanafunzi bora katika mafunzo hayo yaliyochukua takribani mwaka mmoja ambapo wanafunzi kutoka nchi za kigeni pia walishiriki.
Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Luteni Usu Immaculata Leodgar Mapunda baada ya kuibuka mwanafunzi bora wa kike katika kozi ya maafiseshi la Wananchi wa Tanzania iliyofanyika Chuo Cha Jeshi Monduli mjini Arusha jana.Katika mafunzo hayo yaliyochukua takriban mwaka mmoja baadhi ya wanafunzi kutoka nchi za kigeni nao walishiriki mafunzo hayo.
Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku Kamisheni Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania iliyofanyika Chuo Cha Jeshi Monduli mjini Arusha jana.Katika mafunzo hayo yaliyochukua takriban mwaka mmoja baadhi ya wanafunzi kutoka nchi za kigeni nao walishiriki mafunzo hayo.(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole na kumrekebisha tai mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa ambaye juzi alinusurika katika ajali ya ndege baada ya ndege aliyokuwa akisafiria inayomilikiwa na Shirika la Ndege ya Precision kupasuka matairi yote ya nyuma wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa mjini Arusha. Rais Kikwete alikuwa Monduli Mkoani Arusha kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania katika chuo cha jeshi Monduli. 

TAZAMA MAZISHI YA MZEE NELSON MANDELA LIVE KIJIJINI KWAO QUNU AMBAKO MAZISHI YAKE YANAFANYIKA LEO

Maelfu wamzika Mzee Nelson Mandela kijijini kwao Qunu leo

$
0
0
  Mazishi ya Nelson Mandela yanaendelea katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa wa Afrika,Nelson Mandela.
Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.
Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa. Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo wa Mandela wa Thembu.
Viongozi wa Afrika, familia na marafiki wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati Nelson Mandela katika mazishi yake ya kitaifa katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Cape Mashariki. Mandela alikuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa wakati safari ndefu ya Mandela kuelekea uhuru imekwisha, raia wa Afrika Kusini wana jukumu la kuendeleza sera zake na urithi wake.

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MWANZA AUWAWA.

$
0
0

Marehemu Clement Mabina enzi za uhai wake.

MWENYEKITI wa zamani wa chama cha mapinduzi(ccm) mkoa wa Mwanza Clement Mabina ambaye pia ni diwani wa kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza ameuawa na wananchi wenye hasira katika ugomvi wa mashamba.

Tukio la kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa Ccm Mkoa wa Mwanza ambaye alishindwa katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mwanza mwaka jana na Waziri wa zamani na Mbunge wa zamani wa Ilemela Dk Antony Diallo lilitokea leo asubuhi katika eneo la kijiji cha Kanyama wilayani Magu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa polisi wa wilaya(OCD) ya Magu ODC Mkapa pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga zimeeleza kuwa tukio limetokea majira ya saa mbili asubuhi.

ODC Mkapa alikiri kutokea kwa tukio la kupigwa na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm Mkoa na Mwenyekiti wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu baada ya kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi wa eneo la kijiji cha Kanyama alikokuwa na shamba lake alikokuwa amekwenda kupanda miti.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga alisema kuwa amepokea taarifa za kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kutokana na ugomvi wa mashamba na kuelezwa kuwa amesikitishwa sana na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu.

Taarifa zaidi toka eneo la tukio la Kanyama kulikotokea mauaji hayo zimeeleza kuwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm alifika katika eneo hilo majira ya asubuhi kwa ajili ya kupanda miti katika eneo la milima ya Kanyama ambalo analimiliki ambavyo hata hivyo linadaiwa kuwa na mgogoro baina yake na wananchi.

Baada ya kufika katika eneo hilo,wananchi nao walifika katika eneo hilo na kumhoji sababu za kupanda miti katika eneo hilo ambalo bado lina mgogoro wa umiliki na kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi.

Baada ya majibishano ya muda mrefu na kuona wananchi wameanza kumzingira Mabina aliamua kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao ambapo kwa bahati mbaya mojawapo ya risasi hizo zilimpiga mtoto aliyekuwa katika eneo hilo na kupoteza maisha.

Taarifa hizo toka katika eneo hilo la tukio zimeeleza kuwa kutokana na tukio hilo wananchi walimzingira Mabina na kuanza kumpiga kwa silaha mbalimbali za jadi kama vile mapanga, fimbo, mawe, mikuki na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kabla ya kurejea chama cha mapinduzi(ccm) na kufanikiwa kuwa diwani wa Kata ya Kisesa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mabina aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi na aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo mwaka 1995 na kushindwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Malaki Lupondije.Habari kwa hisani ya Gsengo Mwanza.

UVCCM WAMKATAA MKUU WA WILAYA YA IRINGA

$
0
0

 Mwenyekiti wa Uvccm wa Wilaya ya Iringa Benitho Kayugwa akizungumza na uvccm baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku 5 kuhusu ujasiliamali, kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika katika kambi ya vijana ya Ihemi hivi karibuni. 
 baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
mwenyekiti wa Uvccm wa Wilaya hiyo Benitho Kayugwa akimkabidhi cheti ya utambulisho wa mafunzo hayo Newton (Picha zote na Denis Mlowe Iringa)
==========  =======  =========

Na Denis Mlowe

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa wamemkataa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dk. Leticia Warioba na kumuomba, Rais Jakaya Kikwete aweze kumuondoa katika Wilaya hiyo na kumpangia Wilaya nyingine ya kufanyia kazi baada ya kushindwa kuwajibika ipasavyo katika majuku yake na kutokuwa na ushirikiano kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza  wakati wa kufunga mafunzo ya Itikadi, Siasa,Utendaji na Ujasiliamali yaliyofanyika katika Chuo cha Vijana Ihemi kwa siku tano mwenyekiti wa Uvccm wa Wilaya hiyo Benitho Kayugwa, alisema Warioba hana ushirikiano katika kuwajibika na kutoa agizo ndani ya siku 60 serikali inayoongozwa na Jakaya Kikwete kuweza kumwondoa katika wilaya hiyo na kuwaletea mkuu wa wilaya anayejua wajibu wake katika kazi.

Kayugwa alisema wameamua kwa kauli moja kutokumtaka mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwa hana ushirikiano katika majukumu yake kulalamikiwa na wananchi pamoja na baadhi ya viongozi kwa kushindwa kuzingatia ushirikiano na kuendelea kukumbatiwa.

“Sisi Vijana wote tumeamua kwa pamoja tunataka kupata majibu ndani ya siku 60 kuweza kuondolewa kwa mkuu huyu wa wilaya ambaye anaonyesha kabisa kazi yake hawezi kuifanya na tutamgomea katibu yoyote atakayeletwa hapa wilayani hadi katibu aliyekuwa likizo ya miaka 3 apewe fedha zake kwenda kusoma, aidha kiongozi yoyote aliyechaguliwa na wananchi na hayuko tayari kuwajibika tuko tayari kumshughulikia ." alisema Kayugwa 

Kayugwa aliitaka serikali kuwawajibisha watumishi wote wa vituo vya afya wanaokiuka maadili ya kazi kwa kuuza madawa ya serikali yanayotakiwa kupelekwa katika vituo vya afya na kushindwa kuyafikisha sehemu husika na kusababisha wananchi wasiwe na imani na serikali.

Aidha aliitaka serikali kuweza kuwajibisha viongozi wote wa ngazi tofauti ambao wanakiuka kuweka wazi matumizi na mapato ya kijiji kwa wananchi kwa kuwachukulia hatua kali kwa kuwa wanasababisha wananchi kuichukia serikali yao kutokana na uzembe wa watu wachache.

Aliongeza kwa kuiomba Serikali kuwahamisha watumishi waliokaa sehemu moja kwa muda mrefu kuwea kuleta mabadiliko chanya kutokana na baadhi ya watumishi kufanya kazi kwa mazoea na kufanya kazi pasipo weledi kwa kuzoea mazingira.

MITIKISIKO YA PWANI YACHENGUA MASHABIKI DAR LIVE KWA KISHINDO

$
0
0

 Mwimbaji wa bendi ya Super Shine, Queen Salma akifungua pazia la burudani.
 
Nuru Moshi wa Super Shine akitoa burudani.
 Waimbaji wa Super Shine wakiimba.
 Khadija Omar Kopa wa TOT akitoa burudani.
 …Akiviringisha kiuno chake.
 Mashabiki waliojitokeza kushuhudia onyesho hilo.
 Khadija Kopa akicheza na baadhi ya waimbaji wake.
 
Ally J wa kundi la Five Star akipagawisha mashabiki.
 ...Akiwapa 5 mashabiki.


 
Maua Tego wa Five Star akiimba.
 
Hashim Saidi wa Mashauzi akiwapagawisha mashabiki.
 Waimbaji wa Mashauzi wakiserebuka.
 
Fatma Machupa wa Jahazi akiimba.
                                                          Fatma Mahamud wa Jahazi naye akiimba.
 Khadija Kopa akiwa amepozi akisubiri kupanda jukwaani.
MC wa tamasha hilo, Khadija Shaibu ‘Dida’ (kushoto) akipozi na wenzake. Kulia ni msanii wa maigizo, Monalisa.
 Monalisa akiwa na shabiki wake.
 
MC Dida akisherehesha.
 Mabaunsa wakilinda usalama wa mali na mashabiki.
 
Dida (kushoto) akikabidhiwa keki na shabiki wake.
 Mtangazaji wa Times FM, Cliford Ndimbo, akiwa na mkewe.
 
Dida akipozi na mumewe.
Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live usiku wa kuamkia leo ulitikisika kutokana na kufurika mashabiki ambao walijitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho la Mitikisiko ya Pwani lililoandaliwa na Redio TIMES  FM kwa udhamini wa Vodacom.
Katika onyesho hilo, bendi tano za miondoko ya taarab zilidondosha burudani ya nguvu ambayo iliwafanya mashabiki wa miondoko hiyo washindwe kutulia katika viti vyao.
Pazia la burudani hiyo lilifunguliwa na kundi la Super Shine ambao waliingia na staili ya ngoma ya Kimwera ambayo ilisababisha mashabiki kuwashangilia kwa nguvu.
                                                     (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/ GPL)  


ASAA SIMBA,MOHAMED BAWAZIR WAONGEA NA WANA CCM KATA YA JANGWANI KUIMARISHA CHAMA

$
0
0


Mwenyekiti wa CCM  Kata ya Jangwani Mohamed Bawazir katikati akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kujadili kelo mbalimbali zinazowakabili katika kata hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Ilala Asaa Simba ambaye pia ni Diwani wa Vingunguti na kulia  ni katibu wa kata ya jangwani, Majala Balawa
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Asaa Simba kushoto akizungumza naMwenyekiti wa CCM  Kata ya Jangwani Mohamed Bawazir
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Asaa Simba kushoto akizungumza naMwenyekiti wa CCM  Kata ya Jangwani Mohamed Bawazir wakingia katika ukumbi wa mkutano
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Asaa Simba kushoto akiongea na baadhi ya wanachama wa CCM wa kata ya Jangwani wakati alipotembelea kwa ajili ya kujadili kelo mbalimbali zinazo ikabili kata hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Chama Hicho Kata ya Jangwani Mohamed Bawazir

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Asaa Simba kushoto akiongea na baadhi ya wanachama wa CCM wa kata ya Jangwani wakati alipotembelea kwa ajili ya kujadili kelo mbalimbali zinazo ikabili kata hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Chama Hicho Kata ya Jangwani Mohamed Bawazir
Baadhi ya wanachama wa CCM wakisikiliza mada mbalimbali katika mkutano huo

Wataalamu wa pamba waondoa hofu juu ya mbegu zilizotolewa manyoya

$
0
0

Wataalam wa pamba kutoka sehemu mbalimbali za wilaya nchini sasa wameondoa hofu juu ya ukuaji wa mbegu za pamba zilizothibitishwa na kusambazwa kwa ajili ya kupanda msimu huu.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Ibrahim Msigwa, ambaye ni mtaalamu wa pamba, Ihanamilo, Geita alisema kuwa mbegu hizo za pamba huota kwa kutegemea hali ya hali ya hewa na chache kati ya mbegu hizo hupata matatizo kwenye ukuaji kwasababu ya kupanda bila ya kufuata utaratibu sahihi wa upandaji.

“Mwaka huu tumetoa mbegu zinazotoa manyoya ambapo wengi wao wameanza kupanda. Kwa mkulima mwenye mwamko baada ya kupata mafunzo juu ya utunzaji na upandaji mbegu, hawana tatizo na matokeo yao ni mazuri kabisa,” alisema Bw. Msigwa.

Wachache ambao hawakufuatilia maelekezo yanayotolewa na wataalamu ndio wanaokabiliwa na matatizo. Mbegu zenyewe hazina tatizo lolote, "aliongeza.

Kwa mujibu wa mkaguzi wa pamba (cotton inspector) kutoka Pandagichiza, Shinyanga, Dayton Chelahani, alisema kuwa wakulima 60 wa pamba chini yake wamefanikiwa kuanza kuotesha mbegu zenye manyoya na kupanda mbegu hizo za pamba kwa kufuata utaratibu wa upandaji usio na matatizo yoyote.

"Ninatarajia wakulima hao kuvuna pamba yenye kiwango cha juu zaidi msimu huu kutokana na kutumia mbegu zenye manyoya. Mara ya kwanza walipinga kwa kiasi kikubwa sana kutokana na kukosa mafunzo sahihi juu ya mbegu hizo na baadhi ya wakulima walikuwa wakipanda mbegu hizo katika kina kirefu ardhinikitu ambacho kilisababisha mbegu hizo kuota kidogo lakini baada ya maelekezo matokeo yamekuwa mazuri sana, "aliongeza.

“Hapa Chato, wakulima 52 kati ya 90 walikusanya mbegu zenye manyoya na hawana tatizo lolote katika uotaji wa mbegu hizo, alisema mtaalamu mwingine wa pamba kutoka Chato, Charles Ndebalema.

Kilimo cha mkataba hivi karibuni kilipata sapoti baada ya serikali kutoa tamko kupitia Waziri wa Kilimo , Chakula na Ushirika , Mhandisi Christopher Chiza kutangaza kutoa ruzuku ya shilingi bilioni 4.8 ambayo itawezesha wakulima kununua mbegu bora za pamba kwa shilingi 600 kwa kilo badala ya shilingi 1,200.

Wakaguzi wa pamba , hata hivyo walitoa mfano wa jinsi wakulima walivyokuwa wakipanda mbegu mbali sana kati ya mche na mche kama ilivyopendekezwa, juu ya kuzingatia kina au upandaji wa mbegu nyingi katika kila shimo, ambapo husababisha kuvuna chini ya kiwango kwa baadhi ya wakulima . 

“Hata hivyo, maelekezo ya ufungaji yanaweza kuwa na utata kwa wakulima ambao wanatumia mbegu zilizothibitishwa kwa mara ya kwanza,” mtaalam huyo anasema.

Kukabiliana na hali hii, tumeanzisha mfano wa kitalu kueleza wakulima hatua za kuchukua kwa wakulima juu ya mchakato wa kupanda mbegu zenye manyoya na kuwa na kuweza kupata mrejesho mzuri kutoka kwa wakulima.


Wataalamu hao waliyasema hayo wiki moja baada ya madiwani kutoka kata mbalimbali za Sengerema kutoa malalamiko yao kwa mamlaka za wilaya juu ya uoteshaji wa mbegu mbaya na kutishia kumpeleka mahakamani, Waziri wa Kilimo , Chakula na Ushirika , Mhandisi Christopher Chiza , ambaye alipigia debe kilimo cha mkataba.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Gabriel Mwalo , amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima na kwamba juhudi za haraka zinachukuliwa ili kukabiliana na masuala hayo, ikiwa ni pamoja na kusambaza mbegu mbadala, elimu kwa wakulima na upimaji maeneo yao.

“Toka Jumamosi iliyopita, timu ya wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Ukiriguru, na kampuni ya Quton Tanzania Limited sambamba na Bodi ya Pamba (TCB) imekuwa katika upimaji wa maeneo mbalimbali yanayoonekana kuwa na matatizo na kupata chanzo cha sababu za kweli ," alisema Bw Mwalo.

Pia alisema kuwa timu yake itafuatilia kwa ukaribu juu ya kama wakulima wana elimu ya kutosha kuhusu utunzaji na upandaji mbegu. Kwa mujibu wa Bw. Mwalo, timu ya wataalamu wengine watapelekwa kwa wakulima ili kuwapa elimu juu ya utunzaji na upandaji mbegu zenye manyoya.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa kampuni ya Quton Ltd, Tariro Sithole, alisema kuwa sampuli na upimaji hufanyika wakati wa usindikaji mbegu kwa kutumia mfumo wa random, ambao kuhakikisha upatikanaji wa sampuli ya mbegu yenye ubora wa juu mbegu unapatikana kwa kila kundi. Hii ina maana kwamba kabla ya kupeleka kwa wakulima ubora wake unakuwa wenye kiwango cha juu.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images