Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

NBC YAMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA UPEWE

$
0
0
 Mkuu wa Huduma za Rejereja za Kibenki wa Benki ya NBC Tanzania, Mussa Jallo (wa pili kushoto) akizungumza katika  hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyo ambayo washindi wanne walikabidhiwa pikipiki mpya aina ya Honda. Hafla hiyo ilifanyika pamoja na uchezeshwaji wa droo ya pili katika Tawi la NBC Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe, Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Chiku Saleh. 
 Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya NBC Weka Upewe, Festo Mukerebe (kulia) akionyesha ufunguo wa pikipiki aina ya Honda, mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Kanda wa NBC, Rachel Mwalukasa (kushoto) katika hafla hiyo iliyofanyika katika Tawi la Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Huduma za Rejereja za Kibenki wa Benki ya NBC Tanzania, Mussa Jallo (kulia) akikabidhi zawadi ya pikipiki mpya aina ya Honda kwa Dk. Isaya Mpelumbe aliyopokea kwa niaba ya mtoto wake, Edna Ndumbaro aliyeshinda katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo.
 Meneja wa NBC Tawi la Ubungo, David Nsimba (kushoto) akikabidhi funguo ya pikipiki mpya aina ya Honda kwa Hassan Khamis aliyepokea kwa niaba ya Prof. Peter Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye naye aliibuka kidedea katika droo ya kwanza ya promosheni ya NBC Weka Upewe.
Mmoja wa washindi wa promosheni ya Weka Upewe ya benki ya NBC, Festo Mukerebe akitoa shukrani zake kwa benki ya NBC mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya pikipiki mpya aina ya Honda. Kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na kushoto kwa Alina ni mke wa Festo, Alphoncena Mukerebe. 

BASI LA BURUDANI LAPATA AJALI MBAYA LIKITOKEA KOROGWE KUELEKEA JIJINI DAR,WATU ZAIDI YA 12 WAHOFIWA KUFARIKI NA MAJERUHI ZAIDI YA 50.

$
0
0
Basi la Burudani baada ya ajali leo Wilaya ya Handeni, Tanga.
Basi la Burudani leo limepata ajali kijiji cha Taula Wilaya ya Handeni, Imeripotiwa mpaka sasa watu zaidi ya 12 wamefariki na majeruhi zaidi ya 55. Watu 4 wamepelekwa MOI na KCMC. Tuwaombee majeruhi.
Hospitali ya wilaya ya Korogwe.
Majeruhi wakipatiwa matibabu.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo ( kushoto) akiangalia mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu.
Manesi wakiendelea na matibabu kwa majeruhi.
Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa kwenye benchi.
Wananchi wakiwa eneo la Hospitali.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA MKUU WA WILAYA YA KOROGWE, MRISHO GAMBO.

Rais Kikwete ahudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Kenya leo

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete(kulia) wakihudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Kenya zilizofanyika katika uwanja wa Michezo wa Kasarani mjini Nairobi leo.Kushoto ni Mwenyeji Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta.Watatu kushoto ni Naibu Rais Wa Kenya William Ruto,Watano Kushoto ni Waziri Mkuu wa Ethiopia Haile Mariam Desalegn, na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na mkewe.(picha na Freddy Maro)

Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima yajidhatiti kuboresha elimu ya watu wazima Nchini.

$
0
0

Mkuu wa Idara ya Elimu Masafa toka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima(TEWW) Bw. Baraka Kionywala akiwaonesha waandishi wa habari(Hawapo pichani) kijitabu cha sera ya Elimu ya Watu Wazima,wakati wa Mkitano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).Kushoto ni Kaimu naibu Mkurugenzi Taaluma, Tafiti na Ushauri toka Taasisi hiyo Dkt. Meena.

Mkuu wa Idara ya Elimu Masafa toka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima(TEWW) Bw. Baraka Kionywala akieleza kwa waandishi wa habari(Hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa kuvifungia vituo vinavyotoa elimu katika mfumo usio rasmi,wakati wa Mkitano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).Kushoto ni Kaimu naibu Mkurugenzi Taaluma, Tafiti na Ushauri toka Taasisi hiyo Dkt. Meena.

Serikali yatumia zaidi ya shilingi Bilioni 16 kujenga Kampasi mpya ya Makao Makuu ya Chuo cha Taifa cha Utalii.

$
0
0

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Bi. Rosada Msoma akieleza kwa waandishi wa Kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Chuo hicho tangu kuanzishwa kwake, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkufunzi na Msimamizi wa Usajili wa Chuo hicho Bi. Ishika Perpetua.

Mkufunzi na Msimamizi wa Usajili wa Chuo cha Taifa cha Utalii Bi. Ishika Perpetua akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu vigezo vinavyotumika kudahili wanafunzi katika chuo hicho.kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Bi. Rosada Msoma.

Meneja wa Kampasi ya Temeke ya chuo cha Taifa cha Utalii Bw. Steven Madenge akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu namana ambavyo chuo hicho kinaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha wanatoa elimu bora katika sekta ya utalii,wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Bi. Rosada Msoma.

(Picha na Hassan Silayo)


Na Frank Mvungi

Serikali yatumia zaidi ya shilingi Bilioni 16 kujenga Kampasi mpya ya Makao Makuu ya Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Rosada Msoma wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

Rosada aliongeza kuwa kampasi hiyo imejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa ili kupanua wigo wa utoaji wa huduma bora katika sekta ya utalii.

Akifafanua zaidi alisema kuanzishwa kwa chuo hicho ni matokeo ya Kukua kwa Sekta ya Utalii nchini ambako kumepelekea kuongezeka kwa uhitaji wa watumishi wenye weledi katika fani za Ukarimu na Utalii.

“Tunaishukuru serikali ya Ufaransa kwa kuona umuhimu wa kuchangia kukuza sekta ya utalii nchini kwa kuchangia katika ujenzi wa chuo chetu katika kampasi ya Bustani,ambayo ni makao makuu ya chuo chetu”alisema Rosada.

Aliongeza kuwa kwa mwaka 2012 jumla ya watalii 1,077,058 walitembelea Tanzania ukilinganisha na na wastani wa watalii 501,669 waliotembelea nchi yetu katika kipindi cha mwaka 2000.

Rosada alibainisha kuwa jukumu kuu la Wakala ni kutoa mafunzo bora katika fani za ukarimu na Utalii hapa nchini hali ambayo imechangia kukuza utalii nchini.

Naye Meneja wa Chuo hicho kampasi ya Temeke bw. Steven Madenge alisema kuwa chuo hicho kinaendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa wahitimu wanaomaliza katika chuo hicho wanakidhi viwango vya kimataifa.


Chuo cha Taifa cha Utalii ni wakala pekee wa Serikali ulioanzishwa mwaka2003 kwa sheria ya wakala no. 30 ya mwaka 1997 kwa lengo la kutoa mafunzo ya Utalii na Ukarimu hapa nchini.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA TAIFA HUDUMA ZA FEDHA NCHINI.

$
0
0
Gavana wa  Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Prof. Benno Ndulu, akisaini mfano wa cheti cha Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la kusimamia  na kutafuta  ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Wanaoshuhudia nyuma (katikati) ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kulia kwake ni Malkia Maxima wa Uholanzi (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha Sada Mkuya Salumu. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha, wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam 
 Malkia Maxima wa Uholanzi, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa Changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Mohammed Gharib Bilal imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, leo
 Malikia Maxima wa Uholanzi, akibofya kitufe kama ishara ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha. Hafla hiyo  imefanyika jijini Dar es Salaam, leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Malkia Maxima wa Uholanzi na Naibu Waziri wa Fedha, Sada Mkuya Salumu, wakiwa wameshikilia Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha baada ya kuzinduliwa leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania.
 Baadhi ya wadau wa Sekta za Fedha waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia, wakati wa uzinduzi.

TAWI LA CCM-MOSCOW URUSI WAADHIMISHA MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA KWA MAONYESHO MBALIMBALI

$
0
0
                                KATIBU WA TAWI NDG HASSAN KAPILIMA
Mgeni rasmi katika maonyesho hayo alikuwa mwenyekiti wa tawi Ndg Salim Mfungahema, mwenyekiti alifurahishwa na maonyesho hayo ambayo yaliudhuriwa na watanzania na wasio watanzania, katika taarifa yake fupi alipendekeza kuwepo na utaratibu wa kutangaza nchi na utamaduni wetu mara kwa mara katika maazimisho mbalimbali kama kuzaliwa kwa CCM, sherehe za muungano, mapinduzi ya Zanzabar na sherehe za mwaka mpya, Mgeni rasmi ndg Mfungahema alisema kwa kufanya hivyo tutapata watalii wengi nchini na kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni na kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza wakati wa maonyesho hayo katibu wa tawi ndg Hassan Kapilima alisema umefika wakati kila mtanzania, taasisi na vyama mbalimbali vya siasa kutangaza utamaduni wa Tanzania ili kuweka kumbukumbu sahihi na taswila ya mtanzania ndani na nje ya nchi.
Mwanautamaduni maarufu Moscow Bi Neema Mwambi akimpokea mwenyekiti wa tawi kwa furaha, mwenyekiti wa tawi Ndg mfungahema Salim alialikwa kuhudhuria maonyesho hayo.
Mwenyekiti wa tawi Ndg Salim Mfungahema (wa tatu kutoka kushoto mwenye shati la kijani)akiwa kwenye picha ya pamoja na watanzania na wasio watanzania kwenye maonyesho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika jijini Moscow-Urusi. 

Taarifa kwa umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini-mashariki, ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na magharibi mwa nchi.


Corruption undermining the Growth of Natural Resources in Africa-UNESCO

$
0
0
AA
Ministry of Natural Resources and Tourism, Deputy Permanent Secretary, Mr Selestine Gesimba gives his opening speech at the two days workshop on World Heritage Communication Strategy for UNESCO African Field Offices in Dar es Salaam. Centre is UNESCO, Officer in Charge, Abdoul Wahab.
B
UNESCO, Nairobi, Programme Specialist Culture, Mr. Marc Party present his paper on information sharing at the two days workshop of the world heritage site in Dar es Salaam today.
D
UNESCO, Consultant for Culture and Development, Ms Nicole Bolomey present a paper on Culture and Development in the World Heritage context at Coral Beach Hotel in Dar es Salaam .
E
Some of the participants from Burundi, Ghana, Congo Brazzaville, Congo Kinshasa and other countries listening attentively session in Dar es Salaam.
By Damas Makangale, MOblog

High level of corruption in developing countries is undermining and suppresses economic growth management of the environment as well natural resources in Africa. Moblog can report.
Presenting a paper during the two days workshop of the World Heritage Communication Strategy for United Nations Educational, Cultural and Scientific Organization (UNESCO) African Field Offices, UNESCO, Consultant for Culture and Development, Ms Nicole Bolomey said that corruption in both private and public sector suppresses the growth natural resources including cultural tourism and heritage sites in most of African countries.

She said that governments in the region should found ways to curb rampant corruption in all importance sector including natural resources and tourism as path to foster economic and social development.

Bolomey added that cultural tourism is a driver of world heritage sites in most countries in the world, deserve proper attention from all stakeholders in the private and public sector.
She further said that the convention of 1972 set up a defense system against any destruction and disappearance of heritage sites while it’s reduce heavily the impacts of climate change.

Early in his opening speech the Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Natural Resources and Tourism, Mr Selestine Gesimba told participants that the government of Tanzania is one of the earliest signatories to the World Heritage Convention, with first sites listed already in 1979.

“Through the ministry of natural resources and tourism, we have been working very closely with UNESCO over the past 4 decades to promote the implementation of the 1972 World Heritage Convention,’.

“We are actively participating in the debates during the annual sessions of the World Heritage Committee, and our experts take active part in a number of thematic working groups,’ he said. On his part UNESCO, Officer in Charge, Abdoul Wahab said that most of the challenges in the World Heritage Sites in the developing countries are fueled by conflicts between conservation and development goals.

“Despite the great success of this convention in other regions of the world, it seems that the African continent is still not totally convinced of its value,” he underscored.

DR.ASHA-ROSE MIGIRO ALA KIAPO

$
0
0

TASAF yafungua Warsha ya siku mbili ya kujenga uelewa wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini kwa wahariri na waandishi wa habari.

$
0
0
  Washiriki wa Warsha ya siku mbili ya kujenga uelewa wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini kwa wahariri na waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TASAF Ladislaus Mwamanga (wa tatu toka kushoto waliyokaa).
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akifungua Warsha ya siku mbili ya kujenga uelewa wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini kwa wahariri na waandishi wa habari (hawapo pichani) inayofanyika katika Hoteli ya Oceanic Bay & Resort mjini Bagamoyo.
 Mkurugenzi wa Programu wa TASAF Bw. Amadeus Kamagenge akielezea juu ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya Masikini katika warsha ya wahariri na waandishi wa habari (hawapo pichani).

 Kaimu Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo Bw. Fariji Mishael akitoa maelezo juu ya lengo la warsha kwa wahariri na waandishi wa habari. 

 Mtaalam wa mazingira wa TASAF Bw. Barnabas Jachi akielezea juu ya miradi ya Ujenzi, kanuni zake, utekelezwaji wake na manufaa yake.
Mwenyekiti wa siku ya kwanza ya warsha ya kujenga uelewa wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini kwa wahariri na waandishi wa habari ambaye ni Mhariri wa Channel Ten Ester Zelamula (katikati aliyeshika mic) akifafanua jambo kwa washirki (hawapo pichani), wa kwanza kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TASAF Ladislaus Mwamanga na wengine ni wakurugenzi wa idara mbalimbali wa TASAF.
 Afisa program wa uhawilishaji fedha wa TASAF Edith Mackenzie akitoa mada juu ya uhawilishaji fedha kwa walengwa.

 Mhariri wa Habari Leo Shadrack Sagati akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa Mkurugenzi Mkuu wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) mara baada ya kufungua warsha. 
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa uratibu Bw. Alphonce Kyariga, Mkurugenzi wa Ukaguzi Christopher Sanga na Kaimu Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo Fariji Mishael wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada katika warsha ya kuwajengea ufahamu wanahabari.

 Baadhi ya washiriki wa Warsha ya siku mbili ya kujenga uelewa wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini kwa wahariri na waandishi wa habari wakifuatilia uwasilishwaji wa mada mbali mbali katika hoteli ya Oceanic Bay & Resort Mjini Bagamoyo.

MASTAA WA SIKINDE KUSHUKA NA NYIMBO 5 TAMASHA LA GURUMO JUMAMOSI TCC CLUB.

$
0
0
 Muhidin Maalim Gurumo akiwatembelea vijana wake mazoezini
 Abdalla Gama (shoto) na Miraji Shakashia wakila tizi la nguvu
 Wakongwe wa kupuliza midomo ya bata Kinga Maluu (shoto) na Yahaya wakiwa mazoezini
 Hafsa Kazinja, Edo Sanga, Juma katundu na Hussen Jumbe wakila tizi.
Kwa picha zaidi na Saidi Mdoe BOFYA HAPA..

WANAMUZIKI nyota waliowahi kutamba na bendi ya DDC Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” watapiga bonge la show kwenye tamasha la Gurumo Jumamosi hii ndani ya TCC Club Chang’ombe jijini Dar es salaam. Wakali hao ambao kwa sasa hawako na Sikinde, jana walihitimisha mazoezi  ya nyimbo tano watakazopiga katika tamasha hilo.

 Mazoezi hayo makali yalifanyika Amana Club Ilala ambako kwa wiki nzima  wanamuziki watakaoshiriki tamasha hilo wamekuwa wakikutana hapo na kupiga mazoezi ya kufa mtu. Baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na “Celina” utunzi wake Gurumo kwa kushirikiana na marehemu Joseph Mulenga, “Barua kutoka kwa Mama” uliotungwa na Cosmas Chidumule na “Gama” (Tshimanga Kalala Assossa). 

Mratibu wa mazoezi hayo, Mzee Kassim Mapili alisema nyimbo mbili zingine za Sikinde zitajulikana siku ya onyesho lakini akafichua kuwa zitakuwa ni kati ya “Neema” (Chidumule), “Supu umeitia nazi” (Karama Legesu), “Nachechemea” na “Isaya” (Hussein Jumbe). 

Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. 

Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachala, Tshimanga Kalala Assossa, Shaaban Lendi na Ibrahim Mwinchande. Katika maendeleo mengine, Komandoo Hamza Kalala naye kwa kushirikiana na wakongwe hao, amekamilisha mazoezi ya nyimbo mbili “Vicky” na “Tumezaliwa wote Kijiji kimoja” ambazo zitapigwa Jumamosi kusindikiza tamasha hilo. 

Mkongwe Mzee Makassy nae katika tamasha hilo atashuka na wimbo wake uliowahi kutamba sana “Anifa”. Tamasha la Gurumo 53 ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha miaka 53 ya utumishi uliotukuka katika muziki wa dansi kwa Muhidin Maalim Gurumo ambaye ametangaza rasmi kustaafu muziki. Wasanii wengine wanaoshiriki mazoezi hayo ni Miraji Shakashia, Hafsa Kazinja, Juma Katundu, Edo Sanga Majengo na King Maluu. Burudani zingine zitakazokuwepo siku hiyo ni pamoja na bendi za Msondo Ngoma Music Band, Talent Band, na Twanga Pepeta.

Hafsa Kazinja anatarajiwa kumwaga kibao cha 'Nimuokoe nani' alichokipiga upya kumuenzi Gurumo na sasa kinatamba katika redio nchi nzima. Yeye ni mwanamuziki pekee wa kizazi kipya anayeshiriki katika hafla hii ya kihistoria.

MTEMVU AZIDI KUWAPATIA WATANZANIA KAZI DUBAI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Mkazi wa Bagamoyo, Asha Vitalis tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa jili ya safari ya kwenda kufanya kazi Dubai, aliyotafutiwa kazi na kampuni hiyo. Hafla hiyo ya kukabidhi tiketi kwa Watanzania wawili walioondoka  kwenda kufanya kazi Dubai, ilifanyika Dar es Salaam juzi. Mpaka sasa kampuni hiyo imewatafutia kazi ughaibuni zaidi ya Watanzania 100.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Mkazi wa Kinondoni, Neema Ndunguru tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa ajili ya safari ya kwenda kufanya kazi Dubai, aliyotafutiwa na kampuni hiyo. Hafla hiyo ya kukabidhi tiketi kwa Watanzania wawili akiwemo Asha Vitalis (aliyekaa kushoto) walioondoka  jana kwenda kufanya kazi Dubai, ilifanyika Dar es Salaam juzi. Mpaka sasa kampuni hiyo imewatafutia kazi ughaibuni zaidi ya Watanzania 100.
 Mtemvu akiwasihi Asha na Neema kulinda maadili na heshima ya Tanzania wakiwa kazini
 Asha na Neema wakisikiliza kwa makini wakati Mtemvu alipokuwa akizungumza nao kuhusu ajira yao hiyo
 Mtemvu akiwa na Asha, Neema pamoja na baadhi ya wadhamini wao na baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Bravo.
Mtemvu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, akiwa katika picha ya pamoja na Asha (kushoto) na Neema baada ya kuwakabidhi tiketi. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

Magesa arudisha fomu za kuomba uongozi TBF

$
0
0
Makamu wa Rais (TBF) Phares Magesa kushoto akirudisha fomu za kugombea uongozi wa TBF leo katika ofisi za baraza la michezo la Taifa (BMT), anayepokea fomu ni afisa mwandamizi wa michezo wa BMT, Ndg. Magesa anagombea nafasi ya Rais wa shirikisho la mpira wa Kikapu (TBF).

IN MEMORIAM OF MWL.RUTH MOLLEL BIDUGA

$
0
0

      IN MEMORIAM  
  MWL.RUTH MOLLEL BIDUGA


              01-06-1946 to 13-12-2012
Today the 13th of December 2013 is exactly a year since you departed without a word of farewell.  You are sadly and deeply remembered by your family, relatives and friends.



MAY THE ALMIGHTY GOD REST YOUR SOUL IN ETERNAL PEACE.
                     AMEN.

B –PESA ROLLED OUT IN TANZANIA MARKET

$
0
0
 The Managing Director of Smart Banking Solutions Limited (SBS) Gustavo Vermaas (second right) holds a blind fold shortly after unveiling a prepaid bank grade closed loop card of its kind in Tanzania market named B-PESA at a ceremony held in Dar es Salaam evening. Left is Judges Association Chairman, Justice Thomas Mihayo and Right is SBS Chairman Edmund Mdolwa.
The Managing Director of Smart Banking Solutions Limited (SBS) Gustavo Vermaas (right), Judges Association Chairman Justice Thomas Mihayo (second right), Elibariki Lukumay Head of business development (third right) and SBS Chairman Edmund Mdolwa holds a knife to cut a cake in form of a newly launched prepaid bank grade closed loop card named B-PESA which was rolled out in Tanzania market at a ceremony held in Dar es Salaam on Wednesday evening.
============  ======================= 
B –PESA ROLLED OUT IN TANZANIA MARKET

By Correspondent

SMART Banking Solutions Limited (SBS) has introduced the first prepaid bank grade closed loop card of its kind in Tanzania market named B-PESA.

Speaking shortly before unveiling the B-PESA card at a ceremony held in Dar es Salaam Wednesday evening, SBS Managing Director Mr.Gustav  Vermaas said the card allows a customer to transact at any B-PESA branded merchants, member banks and B-Pesa branded ATM’s.

“This card allows you to have the flexibility of card to card transfers, withdraw cash, deposit cash, paybills and payment of purchases at B-PESA branded merchants. The B-PESA card is not a credit card as it does not provide a line of credit, and it is not a debit card either as it is not linked to a bank account, however, it is managed through its own electronic financial wallet that is sponsored by member banks.

“B-PESA is secure as the card utilizes the latest in chip and pin security methods to protect against unauthorized transactions. It increases safety as it reduces the requirement to carry large sums of cash, and is convenient as there is a large network of B-PESA branded merchants and member banks. The consumer will have convenient access to the B-PESA card, as it will be issued instantly off the shelf through the same B-Pesa branded network.

Mr. Vermaas said the introduction of the B-PESA card will help by reducing circulation of cash in the Tanzanian market and transform the country into a cash-lite society once fully implemented.

He mentioned some examples of the B-PESA cards being rolled out into the market, being the generic B-PESA card for general use, the MAFUTA card for fuel consumers and the ADA Card for all school fees and school related expenses.

“We also have the B-Pesa Salary Card and the Mafao Card coming soon. With the Mafaocard pensioners can receive their pension payments directly into their card wherever they are and then spend at B-Pesa branded merchants and ATM’s.

Speaking at the same event, SBS Board Member; DrEdmund Mndolwa, said the B-Pesa product is both a card and a mobile wallet, which caters for the entire supply chain ecosystem, starting from the consumer to the retailer to the distributor and finally to the manufacture.

“You can access your card from your mobile phone as well as from the internet. B-Pesa is a community and loyalty driven product which focuses on specific payment opportunities in a specific demographic group,” he said.
He mentioned that the B-Pesa value proposition is about creating a solution for every layer of the value chain, thus, creating an environment of sustainability, security and convenience.

Dr. Mdolwa said the introduction of this payment system will create substantial benefit to Tanzanian traders as they will not need to look for foreign currency when buying goods abroad, because B-PESA will soon be accepted at all UnionPay  International points worldwide, after B-PESA and UnionPay signed an agreement of cooperation during the event.    

Many banks have expressed interest in partnering with SBS to start issuing B-PESA cards to their customers, where both Commercial Bank of Africa (Tanzania) Limited Managing Director Mr. Yohane Kaduma and The People Bank of Zanzibar Mr. Ame Makame   who is the deputy Managing Director expressed their excitement about the product and its attributes and indicated their desire to swiftly launch the product in their environment.

SHIRIKA LA MAENDELEO CIDA KUPITIA MRADI WA WAZAZI NA MWANA (THE MnW PROJECT) LAKABIDHI SIMU SITINI MKOANI RUKWA KURAHISISHA MAWASILIANO VITUO VYA AFYA

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipokea boksi la simu kutoka kwa Bi Safia Telatela ambae ni Mratibu wa Mradi wa Wazazi na Mwana nchini (The WnM Project) kwa ajili ya kusaidia mawasiliano kwa vituo vya afya Mkoani Rukwa katika kupambana na vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga. Jumla ya simu sitini aina ya Nokia zimetolewa katika maeneo ya mradi huo Mkoani Rukwa ambayo ni Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Kalambo na Nkasi. Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Tawala Mkoa hu amelishukuru shirika la maendeleo CIDA kwa kufadhili mradi huo utakaosaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto kwa kurahisisha mawasiliano na sehemu zenye huduma sahihi za afya.
Afisa Tawala wa Mradi huo wa Wazazi na Mwana (MnW) Bwana Mashauri Ndebile akionyesha moja ya simu hizo aina ya Nokia kwa waandishi wa habari waliohudhuria katika hafla hiyo ya makabidhiano. Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo CIDA na kutekelezwa na Miradi Mitatu ya Plan, Africare, Jhpiego kwa kushirikiana na MOHSW. Mradi huo unatekelezwa katika Mikoa miwili nchini ambayo ni Mwanza kwa Wilaya za Ilemela na Sengerema na Rukwa kwa Wilaya za Kalambo, Nkasi na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizindua simu hizo kwa kupiga simu moja ya majaribio. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga Boksi moja lenye simu ishirini kwa ajili ya vituo vya afya katika halmashauri hiyo. 
Bi Safia Telatela ambae ni Mratibu wa Mradi wa Wazazi na Mwana nchini (The WnM Project) akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema lengo kubwa la mradi huo ni kuona vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga vinapungua na hatimae kuisha kabisa, alisema hilo litawezekana pale jamii, taasisi binafsi, mashirika ya maendeleo na Serikali zitakaposhirikiana katika kuleta ustawi katika eneo hilo.
Picha ya Pamoja
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Kuzinduwa Tamasha la Vipaji

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi na Fadhil Nandonde kutoka UCA-Tz, kulia ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma. Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi na Fadhil Nandonde kutoka UCA-Tz, kulia ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma.Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwakilishi wake wa UCA, na kuzungumzia tamasha kwa ujumla.Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy alipozungumza nao juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA THEHABARI.COM Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy alipozungumza nao juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA THEHABARI.COM


KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la vipaji vya sanaa na muziki lililoandaliwa na asasi ya ukuzaji vipaji (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz). 
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo, Emmanuel Mushy alisema tamasha hilo la pekee litakalofanyika Uwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam linatarajia kushirikisha vijana zaidi ya 500 kutoka maeneo anuai ya jiji. 
 Akifafanua zaidi juu ya tamasha hilo, Mushy alisema UCA-Tz ni program yenye dhumuni la kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji vya muziki na sanaa ili vijana hao waweze kukua katika vipaji vyao. “…Neno ‘unscripted’ linamaanisha kitu ambacho kipo lakini hakijaandikwa, yaani kwa maana nyingine ni kitu kilichopo nyuma ya pazia.
 UCA-Tz baada ya utafiti imebaini kuwa kuna vijana wengi ambao wanajihusisha na muziki pamoja na sanaa lakini hawapati ile nafasi (platform) ya kuendeleza vipaji vyao, hivyo ni kama vijana hawa wapo nyuma ya pazia,” alisema Mushy. 
 Aliongeza kuwa UCA Tz kwa kutambua umuhimu wa vipaji vya vijana vinavyopotea imeona umuhimu wa kutengeneza njia kwa vipaji hivyo ili vitoke nyuma ya pazia kukua na hatimaye kujionesha kwa jamii. Aidha alisema moja ya njia ambazo UCA-Tz inazifanya ni kuandaa matamasha ya vipaji kwa kila mwaka kuwashirikisha vijana na kwa mara ya kwanza inazindua Tamasha la vipaji nchini Tanzania, ambalo litashirikiza vijana zaidi 500 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. 
 “…Tamasha hili la vipaji linatarajia kufanyika kesho, Jumamosi ya tarehe 14th December pale Uwanja wa Kinondoni Biafra, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 za jioni. Katika tamasha hilo vijana wenye vipaji vya kuimba, ku-rap, kucheza, kuchora na ubunifu (ku-design) watawasilisha kazi zao kwa umati utakao jitokeza na vijana wenzao,” alisema Mushy. 
 Alisema ili kuleta radha na hamasa zaidi asasi hiyo imealika wawakilishi vijana kutoka nchi mbalimbali za Africa kama Kenya, Uganda na Ghana ambao nao watashiriki. “…Kutakua na outside performances kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao wameshapiga hatua kwenye tasnia za muziki na sanaa nao watashiriki kwa pamoja. 
 Naye Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi ambao ni moja wa makampuni yaliofanikisha tamasha hilo, akizungumza alisema kampuni yao itaendelea kuunga mkono shughuli anuai za kuwawezesha vijana ikiwa ni sehemu ya kurudisha mchango wa wateja wao wanaotumia mtandao wao. 
 Kampuni nyingine zilizounga mkono kiushirikiano (supporters/sponsers) kufanikisha tamasha hilo ni pamoja na kampuni ya Coca Cola, Maezeki, Arise Media, LGBY Media na mtandao wa kijamii wa habari-Thehabari.com (www.thehabari.com) na mitandao mingine ya kijamii nchini.

WIVU WA MAPENZI NA UKATILI WA KIJINSIA: MAMA MMOJA AMWAGIWA MAJI YA MOTO MWILI MZIMA

$
0
0
Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

 TAHADHARI: PICHA ZINAZOFUATA  CHINI YA UZI HUU SI NZURI SANA KUZITAZAMA.



Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA UTAKAZOZIONA
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA UTAKAZOZIONA

 Na Gadiola Emanuel -Arusha
Mwanamke mmoja mkazi wa Mbuguni Arusha,Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kisa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. 

Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.


Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru alikolazwa,Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma lililopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka afike nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kumwagia maji ya moto.


Neema Teti-Majeruhi
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la madaktari hospitalini hapo. 


Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru Hospitali Bi.Neema Bayo amesema matukio kama hayo yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali
nchini,bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini.



Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha Maria Maswa akizungumza wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika hospitali ya mount Meru,amesema yanapotokea matukio hayo,walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo hayo.


Maria Maswa-Afisa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa. 

Picha zote na Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog.

Ufungaji Mradi wa Matumizi salama ya Bioteknolojia ya Kisasa

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula akisoma hotuba ya ufunguzi katika warsha ya kufunga mradi wa matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa katika Chuo ChaTaifa cha Utalii jijini Dar es Salaam 
 Sehemu ya Washiriki wa warsha ya matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo pichani). Warsha hiyo ya kufunga mradi imefanyika leo katika Chuo cha Taifa cha Utalii jijini Dares Salaam.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (kulia) akisaini mkataba wa Makubaliano wa uanzishwaji wa Kituo cha ushauri wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa (biosafety Center of excellency) kushoto ni Bi Epiphania E. Kimaro, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu - Tanzania (Tanzania Pesticides Research Institute)
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (kushoto) akikabidhi kifaa maalumu kwa Bw Haji Saleh, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo - Zanzibar. Kifaa hicho ni kwa ajili ya kufanya tathmini na usimamizi angalifu wa bidhaa za mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images