Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1872 | 1873 | (Page 1874) | 1875 | 1876 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya jiji wakichagua mahitaji yao mbalimbali katika eneo la maegesho ya magari Tandika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo kama wanavyo onekana pichani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)


  Wajasiriamali maarufu kama machinga katika eneo la maegesho ya magari Tandika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam wakiwahudumia wateja wao kama wanavyo onekana pichani.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika Kikao na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje Ikulu jijini Dar es Salaam
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika Kikao na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje Ikulu jijini Dar es Salaam
   ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje mara baada ya kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi watano kutoka (kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Damas Ndumbaro watano kutoka (kulia) pamoja na Mabalozi Wanawake wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU  0 0


   Pichani wa pili kulia  ni  Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB Filbert Mponzi  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 21 kwa Nahodha wa Gofu kutoka Lugalo Kapten Japhet Masai,leo jijini Dar kwa ajili ya Udhamini wa mashindano ya Gofu yanayotarajiwa kufanyika Septemba 7 na Septemba 8 mwaka huu,ambapo zaidi wachezji 10o wanatarajiwa kushiriki  WACHEZAJI wa mchezo wa Gofu zaidi ya 100 wanatarajia kushiriki mashindano ya mchezo huo yanayotarajiwa kufanyika Septemba 7 na Septemba 8 mwaka huu huku Benki ya NMB ikiahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo kila mwaka.
  Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo huwa ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Majeshi ya Wananchi wa Tanzania ambayo hufanyika Septemba 1 ya kila mwaka huu lakini kutokana na ufinyu wa ratiba mashindano hayo yatafanyika Septemba 7 na Septemba 8 ambayo itakuwa Jumamosi na Jumapili.

  Akizungumza jana Agosti 22, 2019 jijini Dar es Saalam kuhusu mashindano hayo Nahodha wa Gofu kutoka Lugalo Kapten Japhet Masai amesema mashindano hayo hufahamika kwa jina la CDF NMB 2019 ambao ndio wadhamini wakuu.
  "Siku ya Septemba 1 ya kila mwaka huwa ni Maadhimisho ya Siku ya Majeshi ya Wananchi Tanzania.Kutokana na ufinyu wa ratiba yatafanyika Septemba 7 na Septemba 8,"amesema.

  Kapten Masai amesema wanatoa shukrani kwa Chama cha Gofu Tanzania kwa kukubali mashindano hayo yawe chini ya usimamizi wa Chama cha Gofu Tanzania na kuongeza zamani yalikuwa ni mashindano ya ndani lakini safari hii yatakuwa mashindano ya wazi.

  Amesema mashindano hayo yatashirikisha wachezaji wa gofu kutoka wa ndani na nje ya Tanzania."Pia litajumuisha wachezaji wa kulipwa na wachezaji wa ridhaa.Kutakuwa na wachezaji chini ya miaka 18 na wachezaji kuanzia umri wa miaka 55 na kuendelea,"amesema Kapten Masai.

  Ameongeza mwitikio wa mashindano haya ni mkubwa na kusisitiza wachezaji zaidi ya 100 wamethibitisha kushiriki kutoka vilabu mbalimbali vya nchini Tanzania.

  "Tunatoa mwito kwa wachezaji wengine watambue mashindano hayo yatafanyika tarehe hiyo na hivyo muda bado upo wa kushiriki,"amesema Kapten Masai.
  Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB Filbert Mponziamesema huu ni mwaka wa nne sasa benki hiyo imekuwa ikidhamini mashindano hayo na wataendelea kudhamini mwaka hadi mwaka.

  "Benki ya NMB imekuwa ikidhamini kwa zaidi ya miaka minne sasa na tukaona tuendelee kusapoti na tutaendelea kwani benki yetu ni wadau wakubwa wa majeshi yetu.


  "Katika mashindano ya mwaka tumetoa Sh.milioni 21 kwa ajili ya kuyadhamini na hatujaishia hapo kwani kwa kutambua umuhimu wa michezo.
  "Pia tumedhamini mashindano ya majeshi yanayoendelea Nairobi nchini Kenya kwa kutoa Sh.milioni 15 ambazo zimetumika kununua vifaa ya wachezaji wetu,"amesema.

  Amefafanua hiyo yote inaonesha ushirikiano mkubwa kati ya NMB na majeshi ya Tanzania na wajisikia faraja kuendelea kushirikiana na majeshi yetu.

   Pichani wa tatu kulia ni  Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB Filbert Mponzi  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 21 kwa Nahodha wa Gofu kutoka Lugalo Kapten Japhet Masai,leo jijini Dar kwa ajili ya Udhamini wa mashindano ya Gofu yanayotarajiwa kufanyika Septemba 7 na Septemba 8 mwaka huu,ambapo zaidi wachezji 10o wanatarajiwa kushiriki

  0 0

  Na Estom Sanga -TASAF 

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi.Anne Kabagambe amepongeza mafanikio ya Serikali ya Tanzania Kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kuboresha maisha ya Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

  Bi. Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya Kikazi , ametoa pongezi hizo baada ya kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF,na kujionea bidhaa wanazozalisha katika Mtaa wa Keko Machungwa ,Wilaya Temeke, mkoani Dar es salaam. 

  Amesema kutokana na ubora wa Utekelezaji wa Miradi ya TASAF, Benki ya Dunia imekubaliana na Serikali ya Tanzania kuidhinisha kiasi cha Shilingi Trilioni Moja kwa ajili ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Sehemu ya Pili , fedha ambazo amesema zitasaidia zaidi juhudi za Serikali katika kuwahudumia Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

  ‘’Tumejiridhisha pasi na mashaka kuwa utekelezaji wa Shughuli za TASAF katika awamu zote tatu umekuwa wa mafanikio makubwa hivyo Benki ya Dunia imeamua kuendelea kusaidia juhudi hizi’’ amesisitiza Bi.Kabagambe. 

  Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika amesema kiasi hicho cha fedha kitatolewa mwezi Ujao wa Septemba na kuwataka Walengwa na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuendelea kuboresha miradi ya kiuchumi ili kuongeza tija na hatimaye waweze kuboresha zaidi maisha na kuondokana na umaskini wa kipato. 

  Kwa Upande wao Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameishukuru Serikali kupitia TASAF kwa jitihada za kuwaondolea kero ya umaskini wa kipato na kuomba juhudi zaidi zielekezwe katika kuwapatia elimu ya Ujasiliamali ili waweze kuboresha shughuli za uzalishaji mali na kukuza kipato chao. 

  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF umekuwa ukitekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unahudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja Kote Tanzania Bara,Unguja na Pemba na hivi sasa uko katika maandalizi ya utekelezaji wa Sehemu ya Pili ya Mpango inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya taratibu muhimu kukamilika.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (aliyeshika mkoba) akilakiwa na Mmoja waMaafisa wa TASAF, Bi. Tatu Mwaruka wakati wa ziara ya kukutana na Walengwa wa TASAF katika Mtaa wa Keko Machungwa wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. 


  Bi. Anne Kabagambe (picha ya juu na chini) akiwa katika mkutano na walengwa wa TASAF katika mtaa wa Keko Machungwa ,wilaya ya Temeke, jijini Dar es salaam. 

  Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakiwa na bidhaa walizozitengeneza baada ya kupata ruzuku kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-PSSN. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe akikagua bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa TASAF mtaa wa Keko Machungwa,Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DuniaBi. Anne Kabagambe katika picha na Walengwa wa TASAF baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato kkupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa Kata ya Rutamba, akiwa mkoani Lindi katika ziara ya kikazi ya siku mbili, Agosti 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutibia wananchi wa Kata ya Rutamba, kwenye mkutano wa hadhara, akiwa mkoani Lindi katika ziara ya kikazi ya siku mbili, Agosti 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Samwel Gunza, kuhakikisha maji yanatoka katika Kata ya Rutamba, mkoani Lindi, Agosti 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni, kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu Shetta kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu jamii kuachana na Mila na tamaduni zisizofaa zinazochangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika mkutano huo uliolenga kuhabarisha umma kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni,kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu Shetta
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu kwa jina la Shetta akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa Taasisi yake ya Shetta Against Women Abuse (SAWA) katika Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Elias Barnaba akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu ushirki wa wasanii katika kuunga mkono Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

  Na Mwandishi Wetu

  Kampeni ya Twende Pamoja Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi inatarajiwa kuzinduliwa kesho jijini Dar es Salaam katika Wilaya ya Kigamboni inayolenga kushirikisha wanaume na wanawake kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kupitia mbinu anwai.kwa lengo la kuunganisha nguvu pamoja katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Maendeleo ya Jinsia kutoka Wazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi wakati wa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu uzinduzi wa Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja. 

  Aidha Bw. Mbilinyi amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi mojawapo kati ya nchi zinazoripotiwa kuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia na asilimia 67 ya kesi zinazoripotiwa za ukatili hutokea kwa wanawake na 33 kwa wanaume.

  Ameongeza kuwa Serikali imeliona tatizo hilo na kwa kushirikiana na wadau wengine imeandaa kampeni hiyo itakayosaidia kutoa kwa elimu nchini na kubadilisha fikra hasa kwa wanaume na kwa kiasi kikubwa itapunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mimba na ndoa za utotoni.

  Bw. Mbilinyi ameongeza kuwa kwa asilimia kubwa umasikini unachangia kutokea kwa vitendo vya kikatili kwa wnawake na watoto ingawa pia hata kwa wenye vipato vikubwa na vya kati wanakabiliwa na vitendo vya kikatili.

  Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza amesema kuwa tamaduni na mila zenye madhara zimekuwa ni sababu kubwa kwa jamii kuendeleza vitendo vya kikatili kwa kutolea mfano wa mkoa wa Shinyanga katika miaka ya nyuma vitendo vya mauaji ya wazee wenye macho mekundu vilishamiri ikiushishwa na imani za kishirikina.

  Kwa upande wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya na Mwenyekiti wa Taasisi ya SAWA Bw. Nurdin Bilal (Shetta) amesema kuwa wao wasanii wameguswa na vitendo vya kukatili kuzidi kuongezeka na wameamua kutumia sanaa yao katika kufikisha ujumbe kwa jamii kuachana na vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.

  0 0

  Wataalam wa Masula ya film wa kampuni ya Baidu kutoka China wakiwasili
  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III, kwa ajili yakutembelea maeneo ya vivutio vya utalii Tanzania lengo likiwa ni kujionea na baadayekuzalisha film na picha ya vivutio hivyo kwa ajili ya mtandao wa Baidu.
  Wataalam wa Masula ya film wa kampuni ya Baidu kutoka China wakipata
  maelezo kutoka kwa kiongozi wao Prof.Li Kunruonan, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III, wataalam hao wako nchini kwa siki 11 kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii Tanzania lengo likiwa ni kujionea na baadaye kuzalisha film na picha ya vivutio hivyo kwa ajili ya mtandao wa Baidu.
  Baadhi ya Wataalam kutuka kampuni ya Baidu kutoka China wakicheza
  ngoma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.
  Wacheza ngoma wa Kikundi cha Nimujo wakitoa burudani kwa wageni wa
  kampuni ya Baidu (hawapo pichani), mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.
  Mpiga ngoma wa Kikundi cha Nimujo akipiga ngoma kwa wageni wa kampuniya Baidu (hawapo pichani), mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege waKimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.

  ********************

  Na. Paschal Dotto-MAELEZO
  22-08-2019

  Katika Jitihada za kukuza utalii nchini Taasisi iliyopewa jukumu hilo yaani Bodi yaUtalii Tanzania(TTB) ikishirikiana na Ubalozi wa Tanzania Nchini China, wamewezesha kampuni ya Beijing Pseacher Business na Baidu kuja nchini kutembelea na badaye kufanya kazi ya uzalishaji wa picha mjongeo(Film) na picha zitakazowekwa kwenye mtando wao wenye wafuasi takribani 700 kwa lengo la kutangaza utalii wa Tanzania.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Bodi ya Utalii, Geofrey Tengeneza alisema kuwa ujio wa wageni kutoka China ni neema kwa sekta ya utalii, kwani utawezesha kuwepo kwa mradi mkubwa wa kupiga picha na kutengeneza Film ya vivutio vya utalii Tanzania ambavyo vitatangazwa kwenye mtandao wa Baidu na kuwezesha watalii kutoka China kuja kutalii nchini.

  “Tumefanya kazi kubwa kwa kushirikiano na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini China, ambapo tumepata kampuni hii waliowasili leo kutembelea na baadae kuja kufanya mradi wa kupiga picha, kutengeneza makala ya vivutio vyetu, vyakula vyetu vya asili, lakini pia watapata fursa ya kutembelea Serengeti, Bonde la Mamlaka ya Ngorongoro, Zanzibar na bagamoyo na badae watafanya mradi huo ambao utaisaidia Tanzania kuliteka soko la utalii la China”, Geofrey Tengeneza.

  Tengeneza alisema kuwa wataalam hao 12 kutoka Baidu wamekuja kwa lengo la kuona jinsi gani watafanya mradi huo mkubwa ili kuwezesha uzalishwaji Film, picha za kawaida na kuziweka kwenye mtandao wao ambao unawafuasi wengi na hii itasaidia kukuza soko la utalii wa Tanzania kwa upande wa soko la China.

  Aliongeza kuwa leongo la TTB ni kuiwezesha sekta ya utalii kupata watalii wengi kutoka china na kuongeza idadi ya watalii wa kigeni wanakuja kuitembelea Tanzania kutokana na kuona vivutio vitakavyochukuliwa kwenye mradi huo wa kampuni ya Baidu.

  Kwa upande wake kiongozi wa kundi hilo, Prof. Li Kunrounan alisema kuwa wamekuja Tanzania ili kuona jinsi gani wataweza kutekeleza mradi huo wa uzalishaji wa film kubwa ya vivutio vya utalii Tanzania na kuiweka kwenye mtandao huo mkubwa ili kukuza ushirikiano wa Tanzania na China kwenye Sekta ya Utalii.

  “tumekuja kujionea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini Tanzania na baada ya hapo tutakuja sasa kufanya film na picha ambazo tutaziweka kwenye mtandao wetu unafuatiliwa na watu zaidi ya milioni 700 nchini China”; alisema Prof. Li Kunrounan.

  Prof. Li Kunrounan alieleza kuwa Tanzania ina vivutio vingi sana ikiwemo wanyama, mabonde pamoja na fukwe mbaliambali hayo ni moja ya maeneo ambayo yanahitaji kuitangazwa, lakini pia watu wake ni wakarimu sana

  0 0  Profesa Lazaro Busagala ni Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini akizungumza na washiriki wa wa mafunzo ya namna ya kujikinga na mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo kwa kutumia mashine ya X-Ray.Picha zote na habari na Vero Ignatus,Michuzi Blog.
  Dkt.Remugius Kawala mtafiti mwanadamizi na Mratibu wa tafiti wa mafunzo ya TAEC.


  Washiriki wa Mafunzo yaliyoendeshwa na TAEC kuhusiana namna ya kuepuka madhara yatokanayo mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo,Watumishi 8 kutoka TRA na mmoja kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )
  Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Nchini Profesa Lazaro Busagala akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi 8 kutoka TRA na mmoja kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tano ya namna ya kuepuka madhara yatokanayo mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo,

  Washiriki wa Mafunzo yaliyoendeshwa na TAEC kuhusiana namna ya kuepuka madhara yatokanayo mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo,Watumishi 8kutoka TRA na mmoja kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )katikati ni mwanadada pekee aliyeshiriki katika mafunzo hayo Devotha Mwenda kutoka TRA Makao makuu Dar es salaam.
  Mkurugenzi mkuu wa TAEC Nchini Profesa Busagala akimkabidhi cheti cha mafunzo hayo Afisa Usalama Mwandamizi Idara ya mambo ya ndani TRA kutoka makao makuu Jijini Dar es salaamMmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo kutoka TRA Majid Lema akipokea cheti cha mafunzo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini Profesa Lazaro Busagala.


  Albert Mwangila Afisa mkuu wa Idara ya mambo ya ndani kutoka TRA makao makuu Dar es salaam akitoa neno la shukrani mara baada ya mafunzo hayo kukamilika.  Na.Vero Ignatus,Arusha.

  Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini imeendesha mafunzo ya siku tano kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato nchini lengo likiwa ni kujua namna ya kujilinda na mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo ,kwa kutumi a mashine za X-RAY .

  Profesa Lazaro Busagala ni Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini,amesema lengo la nguvu za Atomiki Tanzania ni kuendesha mafunzo ya aina hiyo mara kwa mara, kwani ni muhimu ili kuweza kuhakikisha kwamba wananchi kwa ujumla wao wanakuwa salama kutokana na madhara yanayoweza kujitokeza kwasababu ya mionzi au Teknolojia ya Nyuklia .

  Profesa Busagala amesema kuwa hata katika viwango vya Kimataifa ,Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani International Atomic Energy Agency ( IAEA) linatumia kuwa ni kigezo kimoja wapo kuiweka nchi katika kundi la kuwa salama ikiwa kuuna mafunzo ,amesema kama hakuna mafunzo ni kwamba watu hawana uelewa wa kutosha na mambo yanakwenda bora yaende na watu wanatumia visivyo.

  “Kwasababuhiyo pia tunabadilisha kanuni zinazowalinda wananchi kutokana na madhara ya mionzi tayari katika hatua za ndani ya Tume ya nguvu za Atomiki nchini Tanzania tumeshapitisha na tumeshapeleka kwa serikalini,na serikali sasa inaendelea kutumia kwa muda kuzipitia na mwanasheria mkuu wa serikali anazipitia,na zikishwa pitishwa tuweze kuweka mambo vizuri zaidi “Alisema Profesa.

  Dkt.Remugius Kawala ni mtafiti mwanadamizi na mratibu wa tafiti wa mafunzo ya TAEC amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kwa wale wanaoratibu mashine hizo,pamoja na uelewa wa jamii,na kuripoti namna ya watu wanaokwenda mipakani na Bandarini kutumia hizo mashine na kuwasaidia wadhibiti kuwa na watu ambao wanauelewa wakutumia hizo mashine.

  “Mzigo unapoingia nchini kwa mara ya kwanza lazima ukaguliwe kwa mashine,kwahiyo ukiangalia tunamaeneo mengi sana ya hizo check point,bandari,mamlaka mbalimbali nchini,viwanja vya ndege,mahoteli makubwa,ila kwa sasa tumeanza na Mamlaka ya Mapato nchini TRA na baadae tutaendelea na Mamlaka nyingine Nchini”Alisema Dkt.Kawala.

  Dkt Kawala amesema kuwa wanashauri wakati mashine ya Scan ikiwa haijazimwa hawaruhusu mtu kuingiza mkono kwani mionzi inayotoka katika mashine hiyo husababisha baadhi ya seli za mwili kufa japo kuwa hawajui ni kwa kiwango gani kwa wakati huo ,amesema ikiwa inajirudia mara kwa mara kuna uwezekano wa kusababisha madhara mengine kama ya kansa.

  “Mashine ikishamulika ule mzigo unatakiwa uache utoke kabisa kwenye mkanda uje uupokelee nje kabisa hata Yule operetta ukimuangalia kwa umakini utaona hawai kukimbilia lile begi,kwasababu kunavidhibiti vinaitwa leedsheets”alisema Dkt.Kawala.

  Albert Mwangila ni Afisa mkuu wa Idara ya mambo ya ndani kutoka TRA makao makuu Dar es salaam amesema kuwa mafunzo yalikuwa yakilenga namna ya kutumia mashine bila ya kuleta madhara kwa mtumiaji ,wakati huohuo kuweza kuwalinda wateja pamoja nawageniwanaotembelea ofisi za Mamlaka hiyo .

  “ Mashine hizo tulizopatiwa elimu ni kwaajili ya ukaguzi,mashine zinazotoa mionzi ambazo ni X-Ray,na mashine ya kuskani mizigo “Alisema Mwangila.

  amesema kuwa wanaishukuru TAEC kwa kuwapatia mafunzo hayo sambamba na mambo mengi ambayo Taasisi hiyo imeyafanya kwaajili yao wakati wa mafunzo,wamekuwa na wataalam tofauti kwa nyakati mbalimbali na wote walikuwa wamebobea katika maeneo yao.

  Hata hivyo mafunzo hayo yamefungwa leo huku idadi ya wahitimu wakiwa ni watumishi nane kutoka mamlaka ya mapato nchini TRA , na mmoja M

  eneja usalama kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )

  0 0

  Waziri Selemani Jafo,akizungumza kwenye ufunguzi wa Teachers day mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na benki ya NMB
  Baadhi ya walimu Mkoa wa Dodoma wakishiriki Mkutano uliyoandaliwa na benki ya NMB

  Waziri Selemani Jafo akikaribishwa na Meneja wa Kanda ya Kati NMB,Nsolo Mlozi.
  Waziri Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja  ………………….

  Serikali imeitaja benki ya NMB kuwa miongoni mwa taasisi zilizofanikisha makusanyo ya fedha kwa mwaka 2018/19 kwa kuwa benki hiyo haina tofauti na Wizara ya Tamisemi kwa kufika maeneo yote nchini.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) Seleman Jafo, wakati akizungumza na walimu zaidi ya 300 kutoka halmashauri za wilaya mkoani Dodoma katika siku ya mwalimu ambao walikutanishwa na benki ya NMB.

  Waziri Jafo alisema uamuzi wa benki hiyo kwenda nchi nzima na kufungua matawi, mawakala pamoja na kuongeza ATM, ulisaidia kwa watu kuzifikia kwa urahisi huduma za kibenki pamoja na halmashauri kuitumia kwa makusanyo yake.

  Hivi karibuni Jafo alitangaza mapato ya serikali kutoka katika halmashauri yakipanda kutoka asilimia 73 ya mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 81 mwaka 2018, juzi kwenye za mapato katika mmalaka ya serikali za mitaa tumekusanya takriban billioni 664 sawa na asilimia 91 kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa. Ninyi NMB mmetusaidia kwa hili,” alisema Waziri Jafo.

  Kuhusu benki ya NMB alisema ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri hapa nchini ikiwa na wateja zaidi ya 3.5 milioni pamoja na matawi 229 ambayo ni zaidi ya halmashauri zilizopo ingawa aliwataka waongeze wateja na kuagiza kitengo cha utafiti kufanya kazi yake vizuri.

  Kuhusu mikopo alisema kuna kilio kutoka kwa watumishi kuhusu riba kubwa ya mikopo kwenye mabenki yote nchini kwani wanatoza kiwango ambacho si rafiki kwa wafanyakazi jambo linalopekea malalamiko na wengine kujutia uamuzi wa kukopa.

  “Naomba suala la riba mliangalie, haiwezekani riba ya mfanyakazi ikawa sawa na anayefanya biashara, ndiyo maana mnasababisha walimu kuingia madeni kwenye visaccos vingine hadi wanaacha kadi zao huko mwisho wa siku wengine wanataka kujinyonga, tafakarini ikibidi mfike hata kwenye single digit,” alisema Jafo.

  Katika hatua nyingine aliwataka walimu kutumia mishahara yao kwa utaratibu na kuacha maisha ya kuiga kwani ndiyo yanayowapelekea kwenye madeni makubwa.

  Meneja wa NMB Kanda ya kati Solo Mlozi alisema benki hiyo imejipanga kuwafikia Watanzania mahali walipo kwa kutumia mawakala wake na kuendelea kuboresha huduma zao kwa kadri iwezekanavyo.

  Mlozi alimwomba Waziri kufikisha ujumbe wao serikalini ili waendelee kuiamini benki hiyo na kufanya nayo kazi kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 31 ndani yake hivyo na mambo yaliyozungumzwa watashauriana ili kuwapunguzia mzigo Watanzania.

  Awali Meneja Mwandamizi wa wateja wadogo Ally Ngingite alisema benki hiyo imeweka utaratibu kuwafikia walimu kama sehemu ya wateja na kusikiliza changamoto zao.

  Ngingite alisema mpango huo ulianzia Jijini Dar es Salaam,Pwani na jana Dodoma kabla ya kwenda mikoa mingine ikiwemo Zanzibar huku akitaja benki kusogeza huduma zaidi kw akutumia simu za mkononi.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu,Zanzibar

  NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna kila sababu ya kuendelea kutolewa elimu ya usalama barabarani na matumizi sahihi ya barabara zetu ili kupunguza ajali zinazosababisha ulemavu na vifo kwa watu wasio na hatia nchini.

  Pia amesema kwa sasa Wizara hiyo ipo kwenye mchakato wa kuangalia upya sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuziongezea ukali sheria hizo ili kukabiliana na watumiaji wa vyombo vya moto na hasa bodaboda ambao wengi wao wamekuwa wakivunja sheria mara kwa mara na kusababisha ajali ambazo zinaweza kuepukika.

  Mhandisi Masauni ameyasema hayo wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi na shule za msingi ambazo zimeshinda michoro yenye ujumbe wa usalama barabarani visiwani humo kwa mwaka 2019, ambapo Shule ya Msingi Mkunazini imepata kitita cha Sh.milioni nne kutoka kwa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania baada ya kuibuka mshindi wa kwanza.

  Mafunzo hayo ya elimu ya usalama barabarani yamefadhiliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania ndio mara ya kwanza kutolewa visiwani humo.

  "Kuna umuhimu mkubwa wa jamii yetu ya Watanzania kwa upande wa Bara na Visiwani kuendelea kupatiwa elimu inayohusu uslama barabarani pamoja na matumizi sahihi ya barabara zetu.


  "Hivyo nitumie nafasi hii kuipongeza Kampuni ya Puma Tanzania kwa uamuzi wake wa kutoa elimu hii ambapo kwa hapa Zanzibar shule tano za msingi zimepata elimu hiyo na tunaamini itasaidia kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika,"amesema Mhandisi Masauni.

  Ameongeza kuwa kutolewa kwa elimu ya usalama barabarani kwa wafunzi kutasaidia kuokoa maisha yao na kuwapusha na ajali kwani watakuwa na uelewa mzuri wa kutumia barabara zetu.

  Ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mikakati ya Serikali katika kuendelea kukabiliana na ajali za barabarani nchini na moja ya mkakati ni pamoja na kusimamia sheria zilizopo na kuongeza wanaendelea na mchakato wa kupitia upya sheria za usalama barabarani ili ziwe kali zaidi.

  "Ajali za barabarani zimeendelea kupungua siku hadi siku, lakini bado kunachangamoto ya baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto na hasa waendesha bodaboda wanavunja sana sheria za barabarani.

  "Tumeamua atakeyakamatwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani awekwe mahabusu na kisha apelekwe mahakamani ili sheria ichukua nafasi yake.Wanavunja sheria kwa kuamini sheria sio kali sana, sasa tumeamua na tutawadhibiti ipasavyo kwa watakaoendelea kutoheshimu sheria zilizopo,"amesema.

  Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Ltd Dominic Dhanan amesema kuwa elimu ya usalama barabarani imetolewa kwa shule tano za msingi za Zanzibar.

  "Tumekutana hapa kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la michoro ya Usalama barabarani kwa mwaka 2019 kisiwani Zanzibar. 

  "Tukio hili la utoaji zawadi linahitismisha prgramu iliofanywa na kampuni ya Puma kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali la AMEND kupitia New vision Consortium trainers ya Zanzibar wa kutoa elimu ya usalama barabarani,"amesema.

  Amefafanua programu hiyo ilihusisha mafunzo kuhusu usalama barabarani katika shule za Msingi Mwembeshauri, Kisiwandui, Shule ya Msingi Jang’ombe, Shule ya Msingi Nyerere na Shule ya Msingi Mkunazini.

  "Wanafunzi wasiopungua 6500 wamapeta elimu hiyo ambayo imekwenda sambamba na uchoraji wa michoro inayohamasisha matumizi sahihi ya barabarani na kufuata sheria zilizopo,"amesema.

  Ameongeza programu hiyo ya usalama barabarani ni mwendelezo wa kampeni ambayo ilizinduliwa rasmi mwaka 2013 ambapo zaidi ya shule 80 zimefikiwa na jumla ya wanafunzi 106,500 wamepata mafunzo katika mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Ruvuma, Dodoma na sasa visiwani Zanzibar. 

  Ametumia nafasi hiyo kueleza Kampuni ya Puma ya Tanzania imeamua kufika visiwani Zanzibar kwa sababu ya ukuaji wa shughuli za utalii na za kiajamii ambazo zimesababisha ongezeko la watu na magari ambayo yanahatarisha usalama wa watoto wanapokwenda shule na kurudi nyumbani. 

  "Lengo kubwa la mpango huu ni kuwafanya watoto hawa kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara wakiwa bado wadogo.Kwa kufanya hivyo tunawaongezea uelewa kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa waTanzania wengi zaidi,"amesema Dhanah.

  Kwa upande wake Mwanafunzi wa shule ya Msingi Mkunazini ambaye ameibuka ushindi wa kwanza kwa mwaka 2019 kwa kuchora mchoro bora wenye ujumbe wa usalama barabarani Raya Zuberi Hemed ambaye amejinyakulia Sh.500,000 ameishuku kampuni ya Puma kwa kutoa elimu hiyo na kuahidi atakuwa balozi wa kueleza matumizi sahihi ya alama za barabarani.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma, Dominic Dhanah (watatu kushoto) na Mrajisi wa Jumuiya sisizo za Kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdullah (watatu kulia) wakikabidhi mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni Nne kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Mkunazini baada ya mwanafunzi Raya Zubeir Hemed(kulia), kuibuka mshindi wa kwanza kwenye Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani kwenye hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni, akimpa zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mkunazini, Saidat Jumbe zawadi baada ya kujibu swali lililohusiana na Kanuni za Uvukaji wa Barabara ili kuepuka ajali.Hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni, akimkabidhi kikombe mshindi wa kwanza wa Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani mwanafunzi wa Shuke ya Msingi Mkunazini Rayah Zubeir Hemed.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma,Dominic Dhanah.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma,Dominic Dhanah, akimkabidhi zawadi Mshindi wa Pili Salum Ali Khatib baada ya kushika nafasi hiyo katika Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani lililodhaminiwa na kampuni hiyo.Hafla hiyo imefanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Mrajisi wa Jumuiya sisizo za Kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdullah akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kisiwandui,Salma Ali Seif baada ya kujibu swali lililohusiana na usalama barabarani, wakati wa Hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Agosti 25, 2019 ameondoka nchini kwenda Japan kwa ziara ya kikazi ya siku saba. Pichani, Mhe. Majaliwa akizungumza na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Avemaria Semakafu (wapili kushoto) kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Nahodha wa timu ya Dar es Salaam Corridor akinyanyua kombe juu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Charteredb Bank Ajmair Riaz mara baada ya kukabidhiwa na Rais wa TFF Bw. Wallace Karia kushoto kwenye michuano ya fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 katika viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019
  Rais wa TFF Wallace Karia akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Dar es Salaam Corridor (katikati) ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank Ajmair Riaz.


  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Charteredb Bank Ajmair Riaz akinyanyua kombe na nahodha wa timu ya Dar es Salaam Corridor mara baada ya kukabidhiwa.
  Wachezaji wa timu ya wa timu ya Dar es Salaam Corridor mara baada ya kukabidhiwa nishani zao kabla ya kukabidhiwa kombe.
  Wachezaji wa timu ya wa timu ya Dar es Salaam Corridor wakiwa na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa.
  Timu ya Coca Cola jezi nyekundu ikichuana na timu ya Dar es Salaam Corridor katika michuano ya fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019
  Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki hiyo, Juanita Mramba akizungumza na wanahabari kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019 kuhusu michuano ya fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 .
  Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akijadilia jambo na waratibu wa michuano hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019.
  Timu ya Coca Cola na Airtel zikichuana kwenye pambanpo la awali la fainali hizo.Coca Cola ilishinda mabao 2-0.
  Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz akiwa na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia pamoja na Ali Mayayi Mchezaji wa Zamani na Mchambuzi wa soka katika fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2019.  Baadhi ya watu waliohudhuria katika michuano hiyo kutoka makampuni mbalimbali ambao ni wateja wa benki ya Tandard Chatered jijini Dar es salaam.
  Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz akiwa na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba wakizungumza na baadhi ya waratibu wa michuano hiyo.
  Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akizungumza jambo na MC wa michuano hiyo.
  Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz akiwa na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba wakikagua timu ya Dar es salaam Coridor kabla ya fainali za michuzno hiyo.
  Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz akiwa na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Bw. Wallace Karia na wadau wengine.
  Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akisalimiana na wachezaji wa timu ya Dar es salaam Coridor.

  ................................................................

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Ajmair Riaz amesema kombe la Standard Chartered ni michuano inayokwenda sambamba na ushirikiano wao na timu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) Liverpool ambapo benki hiyo imekuwa ni mfadhili wa timu hii tangu mwaka 2010.

  Ajmair Riaz amesema wamekuwa wakifanya miradi mbalimbali ya michezo wakishirikiana na timu ya Liverpool, na kombe la Standard Chartered ni mojawapo ya michuano ambayo imekuwa ikifanyika katika nchi mbalimbali ambapo biashara ya benki hiyo ipo katika mabara ya Asia, Africa na Mashariki ya Kati.

  Bw. Ajmair Riaz ameyasema hayo wakati wa fainali za kombe la Standard Chartered Bank Cup 2019 zilizofanyika kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya Agosti 24, 2019.

  "Wengi wenu mtakumbuka michuano ya mwaka juzi, 2017, ambapo timu ya Tanzania ya Azania – Mikoani Traders iliibuka na ushindi na kwenda kwenye mashindano ya fainali pale Anfield Uingereza ambako pia walicheza vizuri na kuiinua bendera ya Tanzania vyema! Hii ilikuwa ni baada ya kuzishinda timu washindi za Kenya na Uganda katika michuano ya mabingwa wa Afrika Mashariki" Amesema Ajmay Riaz.

  Amesema mwaka jana walitangaza mfumo mpya wa michuano hii ambapo walianzisha mashindano ya kitaifa tu. Mfumo huu hauhusishi tena mashindano ya kanda ya Afrika Mashariki ya kuwania safari ya kwenda Anfield Uingereza kwa kupambana na washindi wa nchi za Kenya na Uganda!

  Ameongeza kuwa mwaka huu wanaendelea na mfumo huu na timu itakayoshinda michuano hii ya kitaifa, , itakuwa imejishindia safari ya kwenda Anfield Uingereza moja kwa moja! badala ya kuchuana na nchi za Afrika Mashariki tena.

  Alitangaza kuwa timu ambayo itaibuka kuwa mshindi katika mashindano hiyo moja kwa moja itakwenda nchini Uingereza, Anfield, kuangalia mchezo mkali wa ligi kuu ya Uingereza kati ya timu ya Liverpool na timu ya Watford, utakaofanyika tarehe 14 Disemba mwaka huu.

  "Benki ya Standard Chartered itagharamia safari za wachezaji saba wa timu hiyo, yaani tiketi za ndege, na malazi yao kwa siku tatu. Pia wakiwa kule Uingereza watakuwa na ratiba nzuri kabisa itakayohusisha matembezi katika uwanja wa Anfield, na pia watakutana na magwiji mbalimbali wa timu ya Liverpool.

  "Ninafurahi kuwajulisha kuwa tiketi za mechi hii kwa ajili ya washindi wetu wa siku ya leo tayari zimeshaandaliwa" alisema, Ajmay Riaz.

  Aliwashukuruwageni waliofika katika viwanja vya JK Park kwa ajili ya michuano hiyo na washiriki wote wa awamu ya nne ya michuano ya kombe la Standard Chartered ambapo historia nyingine itawekwa .

  0 0  Meneja wa Vodacom Tanzania Plc wilaya ya Kinondoni, Suleiman Amri akimsajili Mama Maria Nyerere kwa njia ya alama za vidole nyumbani kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc inaendelea kuunga mkono zoezi hilo lililoainishwa na serikali na kuhamasisha watu wote kujisajili kwa njia ya alama za vidole ambayo ni ya haraka na haina gharama yeyote

  0 0

   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Tulia Akson akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali alipowasili katika viwanja vya Majengo mjini Moshi kwa ajili ya Kongamano la Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) lililofanyika mjini Moshi mwishoni mwa wiki. 


   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Tulia Akson akipokelewa katika uwanja wa Majengo mjini Moshi na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro pamoja na serikali wakati wa Kongamano la Wanawake lililofanyika mkoani Kilimanjaro akimwakilisha Spika Job Ndugai.

   Naibu Spika wa JAmhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Tulia Akson akizungumza katika Kongamano hilo. 

   Baadhi ya Wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotoklewa katika kongamano hilo. 

   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza katika kongamano hilo. 

   Baadhi ya Wanawake katika kongamano hilo.


   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira ambaye alikuwa mwenyeji wa kongamano hilo akieleza juu ya miradio mbalimbali iliyotekelezwa katika mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020. 


   Baadhi ya Viongozi wa Taasisi mbalimbali za serikali wakiwa katika Konagamano hilo. 

   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro ,Patrick Boisafi akizungumza katika kongamano hilo. 


   Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kilimanjaro Zuhura Chikira akizungumza katika Kongamano hilo. 


   Naibu Waziri wa Nishati ,Mh Subila Mgalu akiwaeleza washiriki wa Kongamano hilo namna ambavyo utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ulivyofanyika katika sekta ya Nishati. 

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa akiwaeleza washiriki wa Kongamano hilo namna ambavyo njia ya Treni ya kutoka Tanga kuja Kilimanjaro ilivyofanyiwa marekebisho ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na mipango ya baadae ya shirika hilo. 

   Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa ,Esther Mmasi akizungumza katika Kongamano hilo. 

   Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akizungumza katika Konagamano hilo.

   Burudani ya muziki kutoka Bendi ya Chuo cha Polisi iliwakusanya wanawake hao kucheza muziki katika ya uwanja.
  Na Dixon Busagaga,Moshi 
  Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametaja mambo 15 aliyofanya Rais John Magufuli kwa kipindi cha miaka minne alichokaa madarakani na kuwataka watanzania kumuunga Mkono.


  Ndugai ameyataja mjini Moshi, wakati wa kongamano la kumpongeza Rais lililoandaliwa na Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT).


  Hotuba ya Ndugai ilisomwa kwa niaba yake na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson , katika uwanja wa Majengo na kuhudhuriwa na wanachama wa UWT na wanawake wa mkoa huo.


  Ndugai alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, imetekelezwa kwa kiwango kikubwa,na kwamba miongoni mwa mambo ambayo ametekeleza Rais ni kurejesha nidhamu kwa watumishi.


  Alisema lingine ni kushughulikia tatizo sugu la Rushwa ndani ya serikali,na ndani ya chama cha mapinduzi hali ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa rushwa ya uchaguzi katika Chaguzi zijazo.


  Akizungumza mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudensia Kabaka, alisema kongamano hilo lililenga kumpongeza Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka minne na kwamba mambo makubwa yamefanyika katika kipindi hicho.  0 0  · Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City imeongeza muda wa ushirikiano na mshirika rasmi wa mauzo ya moja kwa moja, QNET 

  · Muhula huu mpya utasherehekea miaka kumi ya ushirikiano 

  Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City imeongeza muda wa ushirikiano wake na kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ya Asia, QNET. Hii itadumisha ushirikiano huu kufikia miaka kumi. Ushirikiano huu wa muda mrefu utaifanya kampuni ya QNET kuendelea kuwa Muuzaji rasmi wa moja kwa moja wa timu ya wanawake na wanaume ya Manchester city. 

  Ushirikiano huu unaashiria hatua kubwa sana katika mwezi Mei mwaka 2018 wakati klabu ya Manchester city ilipoikaribisha kampuni ya QNET kama mshirika wa kwanza wa lebo za mikononi (sleeves) katika Ligi ya Wanawake ya Super League. Katika kipindi chote kijacho cha ushirikiano huu kampuni ya QNET itaendelea kutoa kliniki za mpira wa miguu zinazosimamiwa na klabu ya mpira a miguu ya Manchester city kwa jamii duniani kote, pamoja na kujihusisha na watumiaji na wasambazaji kupitia uhusiano huu na klabu ya City. 

  Kusherehekea tangazo hili QNET imezindua toleo dogo la saa za mkononi inayojulikana kama 'QNETCity Champions' zinazoundwa na kuzalishwa na mafundi mashuhuri wa nchini Switzerland. 

  Makamu wa Raisi Mwandamizi wa ushirikiano wa City Football Group, bwana Damian Willoughby, alitoa maoni yake na kusema "Tunafuraha kutangaza kwamba QNET imekuwa mshirika wa hivi karibuni kuongeza muda wa ushirikiano na Manchester City katika makubaliano ya muda mrefu ambayo yatashuhudia tukisherehekea miaka kumi ya kufanya kazi kwa pamoja. Ushirikiano huu uliweka historia pale QNET ilipokuwa mshirika wa kwanza wa lebo za mikononi (sleeve) katika ligi ya wanawake ya Super League na tunafuraha kuingia katika ukurasa mwingine kwa pamoja". 

  Mkurugenzi Mkuu wa QNET Bwana, Malou Caluza alisema: “Huu ni ushirikiano unaothaminiwa sana kwa QNET na Manchester City kwa sababu utendaji bora ni msingi wa chapa zote mbili. 

   Sote tunamsukumo kuelekea katika mafanikio kwa kufanya kazi kwa bidii, ari na kujitolea. Kupitia ushirikiano huu, tumeweza kuwa na fursa ya kuwapeleka watoto kutoka katika familia zenye kipato kidogo kutoka maeneo mbalimbali duniani kwenda manchester kwaajili ya kambi ya mafunzo ya mpira wa miguu na kozi ya lugha ya kiingereza, ambayo kweli imekuwa ni fursa nzuri sana ya kubadilisha maisha kwa watoto walio wengi. 

  Tunatumaini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutafuta njia mpya za kibunifu za kushirikiana na kuwafikia mashabiki wetu."

  0 0

  BENKI YA I&M YAZINDUA HUDUMA YA USIMAMIZI WA DHAMANA NA UWEKEZAJI
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama, akibonyeza kitufe wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji ya Benki ya I&MBank  jijini Dar es Salaam Agosti 26.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&MBank  Baseer Mohammed (kulia) akiteta jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&MBank , Baseer Mohammed (kulia) akiteta jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama.

  Mkuu wa Idara ya Wateja wa RejaReja Benki ya I&MBank  Lilian Mtali.

  Meza Kuu.

  Baadhi ya maofisa wa Benki ya I&MBank

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&MBank , Baseer Mohammed, akizungumza katika uzinduzi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji.

  Baadhi ya wageni waalikwa.

  Meneja Msaidizi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji Benki ya I&M , Frank Bunuma, akizungumza kuhusu Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji iliyozinduliwa na benki hiyo.  OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) Nicodemus Mkama ametoa mwito kwa benki za biashara kuanzisha huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji katika masoko ya mitaji kwani hatua hiyo ni muhimu na itazisaidia benki hizo kuongeza idadi ya wawekezaji na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

  Aidha amezishauri benki zote hapa nchini kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ikiwemo kuuza dhamana kwa umma na hatimaye kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam ili kuongeza mitaji yao.

  Mkama amesema hayo leo Agosti 26 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji wa Benki ya I&M ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza hiyo ni uthibitisho sekta ya fedha ina wadau wengi wanaounga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano.

  Amesema hatua hiyo itasaidia utekelezaji wa agizo la Serikali kwa benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi kutimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha ili kuweza kujiendesha kibiashara. Aidha,ametoa mwito kwa kampuni za bima kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ili kuongeza mitaji yao.

  Amesisitiza hiyo itaziwezesha kampuni za bima hapa nchini kuwa na uwezo wa kushindana na kampuni za nje zinazotoa huduma ya bima (underwriting risks) hapa nchini. Vile vile, natoa wito kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na taasisi za fedha kuunga mkono malengo na azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda kupitia masoko ya mitaji nchini.

  Akizungumzia Benki ya I&M,Mkama amesema kuwa benki hiyo amesema imefanikiwa kupata leseni kutoka kwa Mamlaka hiyo ya kutoa huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji kwa mujibu wa kanuni za masoko ya mitaji na dhamana za mwaka 2006.

  Amesema kuwa hiyo ni hatua muhimu katika maendeleo ya masoko ya mitaji nchini, kwani benki ya I&M inakuwa ni benki ya saba kati ya benki za bishara 40 zinazofanya shughuli zake hapa nchini, kupata idhini ya kutoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji katika masoko ya mitaji na dhamana hapa nchini.

  Ametumia nafasi hiyo kutumia fursa hiyo kuipongeza bodi ya wakurugenzi na uongozi wa Benki ya I&M pamoja na taasisi na wadau wote waliohusika katika kufanikisha hatua hiyo muhimu na kwamba masoko ya mitaji ni sehemu muhimu katika sekta ya fedha nchini. Sekta hii inasaidia upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo.

  Amefafanua masoko ya mitaji hujumuisha uuzaji wa hisa za kampuni (shares), hatifungani za kampuni (Corporate Bonds), hatifungani za Serikali Kuu (Government Bonds), hatifungani za Serikali za Mitaa (Municipal Bonds), na vipande katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Collective Investment Schemes).

  Mkama amesema hivyo masoko ya mitaji husaidia pia kurekebisha kiwango cha ukwasi na mfumuko wa bei katika uchumi. Aidha, sheria na taratibu za masoko ya mitaji zinazitaka kampuni zilizopo katika masoko ya mitaji kujiendesha kwa uwazi wa hali ya juu na kwa kufuata kanuni za utawala bora. Matokeo ya masharti haya ni kwamba mara nyingi kampuni hizo hufanya kazi kwa ufanisi na kwa kuwa taarifa zao za fedha ziko wazi ni rahisi kwa serikali kukusanya kodi stahiki.

  Amesema huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji ni huduma inayotolewa na benki za biashara na ili kutoa huduma hii ni lazima kupata leseni kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na kwamba wanaopata leseni hiyo hutoa huduma hiyo kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

  Pia amesema Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji hutoa huduma za utunzaji wa dhamana: akaunti za dhamana za wawekezaji huifadhiwa na kusimamiwa kwa umakini na benki za biashara (custodians) ikiwa ni pamoja na kukusanya taarifa za siku kwa siku kuhusu thamani halisi ya dhamana hizo.

  Mkama ametaja nyingine ni utunzaji wa mapato ambapoo wawekezaji hupatiwa taarifa kuhusu faida za uwekezaji wao ikiwa ni pamoja na kuwekewa gawio au riba kwenye akaunti zao pale uwekezaji wao unapokuwa umepata faida. Ukamilishaji wa miamala ya dhamana kwa kuhakikisha miamala ya dhamana inakamilika vizuri, kwa uhakika na kwa wakati kulingana na maelekezo ya mwekezaji na matakwa ya sharia, kanuni na taratibu zote.

  Pia Utoaji wa taarifa kwa maana ya kutengeneza taarifa mbalimbali kuhusu uwekezaji husika kama vile muhtasari, salio la akaunti na taarifa za siku. Pia kutengeneza taarifa atakazohitaji mwekezaji kuhusu uwekezaji wake na utunzaji wa fedha ili kuwezesha uwekezaji zaidi, utunzaji wa fedha ni muhimu. Utunzaji wa fedha unahusisha kuwa na taarifa moja ya fedha kutokana na vyanzo vyote vya mwekezaji, kusaidia uamuzi wa uwekezaji na dhamana husika, kufanya uwekezaji, kuratibu fedha kutokana na uwekezaji na kuratibu mtiririko wa fedha

  “Kwa huduma hii wawekezaji huwakilishwa katika mikutano mikuu ya mwaka ya kampuni walizowekeza dhamana zao, na hivyo kupata fursa ya kushiriki katika maamuzi yote ya kampuni hizo. Kwa ujumla, huduma hii ni muhimu kwani inarahisisha uwekezaji katika masoko ya mitaji na hivyo kuchangia kupanuka kwa uwekezaji unaoleta ongezeko la ajira.

  “Aidha huduma hii inachangia kuongezeka kwa idadi ya wawekezaji wa kigeni na hivyo kuchangia kuongezeka kwa akiba hapa nchini; kuongezeka kwa mapato kwa njia ya kodi kwa Serikali; na kuinua kipato cha watanzania kwa ujumla. Ni matumaini yangu kuwa, ninyi mliohudhuria hafla hii, na hasa waandishi wa habari mtaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) katika kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji”,

  Amesema kuwa kadiri Taifa letu linavyosonga mbele katika utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Viwanda, mahitaji ya fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo hususani miundombinu yanaongezeka. Serikali na kampuni binafsi zinaweza kujipatia fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa njia ya kuuza hisa, hatifungani na bidhaa zingine za masoko ya mitaji. Ili kufanikisha azma hiyo kunahitajika kuwepo kwa benki nyingi za biashara zinazotoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji.

  Amoengeza hatua hiyo ni muhimu kwani inachangia kuongezeka kwa uwekezaji na hivyo kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Viwanda hapa nchini. Hivyo anao ujasiri wa kueleza benki ya I&M imekuja katika wakati muafaka. Pia leseni hiyo ya benki ya I&M kwa ajili ya kutoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji ni mojawapo wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuifanya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati. Benki I&M Hongereni Sana.

  Pia amesema huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji inawezesha na kurahisisha biashara kwa wawekezaji wa kigeni katika soko la hisa. Itakumbukwa kwamba katika mwaka wa fedha 2014/1015, Kanuni za Masoko ya Mitaji na Dhamana (Wawekezaji wa Kigeni) za 2003 zilirekebishwa ili kuruhusu ushiriki wa bila kikomo wa wawekezaji wa kigeni katika soko la hisa.

  Hivyo watoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji ndio wanaoweza kuingia mikataba na wageni kwa ajili ya kutoa huduma hiyo. Kwa sababu hiyo, inatarajiwa kuwa kuongezeka kwa huduma hiyo kutaongeza biashara katika soko la hisa inayohusisha wawekezaji wa nje ya nchi.

  Pia amesema benki ya I&M ina uhusiano mzuri na benki washirika katika nchi mbalimbali kama vile Kenya ambao wanatoa huduma kama hii. Pia inao uzoefu wa zaidi ya miaka kumi katika masoko ya mitaji na hivyo kutawezesha wawekezaji wa Afrika ya Mashariki na kwingineko kuweza kuingia Tanzania kirahisi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi wakati alipowasili kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan Agosti 26, 2019, ambako anatarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa TICAD 7 na kufanya ziara ya kikazi nchini humo. Kulia ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Japan, John Kambona.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi wakati alipowasili kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan Agosti 26, 2019, ambako anatarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa TICAD 7 na kufanya ziara ya kikazi nchini humo. Kulia ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Japan, John Kambona.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya maofisa wa serikali ya Tanzania wakati alipowasili kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan Agosti 26, 2019, amabako anatarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa TICAD 7 na kufanya ziara ya kikazi nchini humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akitoa maelekezo kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Tokyo,Japan Bw. John Kambona akiwa na Afisa Ubalozi Bi. Edda Magembe. August 26,2019.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasili katika Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo,Japan. Katikati ni Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Japan Bw. John Kambona akifuatiwa na Bi. Edda Magembe Afisa Ubalozi. August 26,2019. 

  Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Japan Bw. John Kambona (katikati) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) mara baada ya kuwasili katika Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo,Japna anayefuatia ni  Bi. Edda Magembe Afisa Ubalozi. August 26,2019.  
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anaingia katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo,Japan. August 26,2019.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika moja ya Maktaba ya vitabu iliyopo katika Ubalozi wa Tanzania - Tokyo,Japan. August 26,2019.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akikagua aina  ya vitabu vilivyopo katika Maktaba ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Japan. August,26,2019.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika ofisi ya Balozi wa Tanzania Nchini Japan. August 26,2019.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongoza kikao kazi cha ujumbe wa Tanzania uliopo Yakohama Nchini Japan kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika 2019 (TICAD7 YOKOHAMA 2019). August 26,2019.

  Kaimu Balozi wa Tokyo - Japan Bw. John Kambona akiwa anatoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na baadhi ya ujumbe uliopo Yakohama, Japan kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika 2019 (TICAD7 YOKOHAMA 2019). August 26,2019.

  Baadhi ya wajumbe waliopo Yakohama-Japan kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika 2019 (TICAD7 YOKOHAMA 2019) wakiwa katika kikao kazi cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(hayupo Pichani). August 26,2019.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amewasili jijini Yokohama, Japan tarehe 26 Agosti kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 7 wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development-TICAD 7) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019.

  Mkutano huu wa Saba utatanguliwa na kikao cha Maafisa Waandamizi wakiwemo Makatibu Wakuu na Mabalozi tarehe 25 na 26 Agosti 2019 ukifuatiwa na kikao cha Mawaziri tarehe 27 Agosti, 2019 na utahitimiswa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019. Kauli mbiu ya Mkutano huu ni “Kuendeleza Maendeleo ya Afrika kupitia Watu, Teknolojia na Uvumbuzi”.

  Mkutano wa Saba pamoja na mambo mengine unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano na agenda za kimaendeleo zitakazotelezwa kati ya Japan na Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.

  Agenda za mkutano wa mwaka huu zinalenga kujadili mageuzi ya kiuchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kukuza sekta na uvumbuzi. Pia kuimarisha usalama na ustahimilivu endelevu kwenye jamii pamoja na kuendeleza jitihada za kuimarisha amani na usalama barani Afrika. Agenda za Mkutano wa Saba zinaenda sambamba na agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na maazimio mengine ya kimataifa kama Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

  Kutokana na mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya kiuchumi barani Afrika, Mkutano wa TICAD 7 umeandaa ratiba maalum itakayozishirikisha taasisi binafsi na za umma kwenye majadiliano ya kibiashara yatakayofanyika tarehe 29 Agosti 2019. Lengo la majadiliano hayo ni kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Serikali wamiliki wa Kampuni, wafanyabiashara na wawekezaji ili kujadili kwa pamoja masuala mbalimbali ya kukuza baishara, uwekezaji na utalii kati ya Japan na Afrika.

  Kadhalika  wakati wa mkutano wa saba nchi zote za Afrika zimepatiwa nafasi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali kwa lengo la kutangaza fursa za biashara, uwekezaji na vivutio vya utalii za nchi husika. Tanzania kupitia Bodi ya Utalii (TTB) imejipanga kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini wakati wa mkutano huo.

  Mkutano wa Saba wa TICAD utahitimishwa kwa Wakuu wa Nchi kupitisha Azimio la Yokohama na Mpango Kazi wa utekelezaji wa Azimio hilo. Serikali ya Japan ilianzisha jukwaa la majadiliano kati yake na nchi za Afrika mwaka 1993 kwa ajili ya kujadili maendeleo na nchi hizo.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Yokohama, Japan.
  26 Agosti 2019


  0 0


   Afisa wa Idara ya Uhamiaji akitoa huduma kwa mwananchi wakati alipotembelea banda la Uhamiaji katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
   Wananchi wakipata huduma ya usajili wa katika banda la vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
   Afisa wa TCRA akimuhudumia mwananchi wakati alipotembelea banda la TCRA katika Mnada wa Tangamano jijini Tanga.
   Mwananchi akiweka alama za kidole kwa ajili ya usajili wa laini ya simu katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
   Wananchi wakipata huduma za Mawasiliano katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
  Wananchi wakipata huduma za Mawasiliano katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

  WAKAZI wa jijini Tanga   na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

  Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA  Mhandisi Emelda Salum amesema ni fursa kwa wananchi wa wa Tanga kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 
  Amesema Mnada kwa Mnada utadumu kwa siku tatu katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga ambapo itatoa fursa kwa wananchi wengi kufika kupata huduma za Mawasiliano na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

  Salum kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

  Salum amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
  Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
  Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

  Amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

  Salum amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

  "TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Salum

  0 0

  Diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani akiongea na mwandishi wa habari wa blog hii ofisini kwake

  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ametakiwa kutimiza ahadi ya kukarabati shule ya msingi Kihesa kama alivyowaahidi wakazi wa kata ya kisheza wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika katika shule hiyo.


  Akizungumza na blog diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani amemuomba mbunge huyo kutimiza ahadi aliyoitoa kwa lengo la kuhakikisha wanaboresha sekta ya elimu katika kata hiyo.


  “Naomba nimpongeze bwana Jose Mgongolwa kwa kusaidia kukarabati baadhi ya majengo ya madarasa kwa msaada wake wa kukarabati madarasa hayo katika shule ya msingi Kihesa” alisema Sawani


  Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati amesema kuwa atatimiza ahadi hiyo mwezi wa tisa akitoka bungeni na kila kitu kipo sawa.


  “Utaratibu wa sasa ukiomba pesa kwa wadau unatakiwa kutoa account ya Halmashuri ili kila kitu kinapitia kwenye ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hivyo tayari wadau tayari wameshazitoa na zipo halmashuri” alisema Kabati


  Aidha Kabati amesema anamifuko ya saruji zaidi ya mia saba kwa lengo la kukamilisha ahadi zote alizoahidi katika shule mbalimbali mkoani Iringa.


  Mwezi wa tisa naanza kutekeleza ahdi zote kwa kuwa pesa ninazo hivyo ni jukumi la mkurugenzi kuninunulia mifuko hiyo ya sariji ili nianze kutimiza ahadi zote.older | 1 | .... | 1872 | 1873 | (Page 1874) | 1875 | 1876 | .... | 1904 | newer