Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1871 | 1872 | (Page 1873) | 1874 | 1875 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakibadilishana hati za mikataba ya mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) akizungumza jambo mbele ya waandishi wa wahabari (hawapo pichani) baada ya kusaini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi. Kulia kwake ni Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila (pili kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi siku ya nyumba,kwanza kulia Mkuu wa wilaya ya Mbeya Paul William Ntinika na kwanza kushoto Kaimu Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na wa kati Ally Ngingite,na pili kulia Meneja na bank ya Nmb kanda ya Manda za juu kusini Straton Chilongola wakati wa hafla uzinduzi siku ya nyumba NMB Mwanjelwa jijini Mbeya Agosti 16 mwaka huu .
  Baadhi ya wananchi na wateja wa Benki ya NMB Mwanjelwa ,wakifatilia hatoba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila hayupo katika picha wakati hafla ya uzinduzi wa siku ha nyumba iliyoandaliwa na benki ya NMB Katika eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya Agosti 16 mwaka huu
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akizugumza na wateja wa benki ya NMB katika uzinduzi wa siku ya nyumba iliyoandaliwa na Benki ya NMB eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya Agosti 16 mwaka.


  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila katikati walioketi akiwa na wafanyakazi wa Bank ya NMB wakati wa uzinduzi wa siku ya nyumba iliyoandaliwa na benki ya NMB,hafla ambayo imefanyika katika Viwanja vya benki hiyo Mwanjelwa Jijini Mbeya Agosti 16,2019.

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila (wa pili kulia) akimsikiliza kwa Makini Kaimu Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na wa kati kutoka Bank ya NMB Ally Ngingite (wa pili kushoto),wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonyesho ya nyumba katika viwanja ya Benki ya NMB Tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika wa kwanza kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akipewa ufafanuzi kuhusiana na masuala ya nyumba na Steven Mohamed (katikati) amabaye ni Msanifu majengo Kampuni ya Malk Consultants(T) Ltd wakati wa hafla ya uzinduzi siku ya Nyumba iliyoandaliwa na benki ya NMB hafla ambayo imefanyika katika eneo la benki hiyo Mwanjelwa Jijini Mbeya.
   

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia),akimkabidhi Cheti Mtumishi wa Wizara hiyo kutoka Tanzania Bara, Bi. Patricia Mlowe,wakati wa hafla ya kuagwa rasmi kwa ajili ya safari ya kwenda masomoni Uingerezakwa udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), hafla iliyofanyika jijini Dares Salaam, wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Shaaban.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia),akimkabidhi Cheti Mtumishi wa Wizara hiyo kutoka Zanzibar, Bw. Hamad Said, wakati wa hafla ya kuagwa rasmi kwa ajili ya safari ya kwenda masomoni Uingereza kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Shaaban.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akimpongeza mtumishi wa Wizara hiyo, Bi. Diana Ulomi, aliyepata fursa ya udhamini wa masomo katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID)
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Amina Shaaban (wa tatu kushoto) Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Bi. Beth Arthy (wa tatu kulia) na wajumbe wengine kutoka Tanzania na British Council-Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wa watumishi waliopata fursa ya kwenda kusoma Uinnereza kwa udhamini wa DFID.

  **************

  Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka Watumishi wa Wizara hiyo waliopatiwa ufadhili wa masomo na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo (DFID) katika vyuo vikuu vya nchi hiyo kusoma kwa bidii ili kuja kulitumikia taifa kwa umahili zaidi katika nyanja za uchumi na uchambuzi wa masuala ya fedha.

  Hayo yameelezwa na Waziri huyo wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi watumishi watano wa Wizara hiyo waliopata udhamini huo, iliyofanyika katika Ofisi za British Council- Tanzania, jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Mpango alisema kuwa, miaka miwili iliyopita aliiomba Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID), wasaidie kusomesha watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Vyuo vikuu vya Uingereza, kwa kuwa Wizara ya Fedha katika nchi yeyote ndio nguvu ya fikra katika Serikali, hivyo bila watumishi wenye ujuzi kutakua na wizara dhaifu.

  “Ninawasisitiza sana vijana waliopata fursa ya kwenda kusoma Uingereza, wajue dhamana wanayokwenda nayo, watanzania takribani milioni 50 wanaimani nao, wanamatarajio kwamba watakapokwenda huko watazingatia kusoma kwa bidii, ili wakirudi wawe wataalam waliobobea katika masuala ya uchumi na uchambuzi wa masuala yote ya fedha ndani ya Wizara”, alieleza Dkt. Mpango.

  Dkt. Mpango alisema kuwa, pamoja na kuiomba Serikali ya Uingereza kutoa mafunzo kwa vijana hao aliwaomba pia iwapatie mafunzo kwa vitendo katika taasisi zinazojihusisha na masuala ya uchumi na fedha nchini humo ili wapate udhoefu.

  Alisema anaishukuru Serikali ya Uingereza kwa kukubali ombi hilo na sasa ni timu ya tatu kupelekwa masomoni, awamu ya kwanza na ya pili walipelekwa jumla ya vijana kumi, na sasa tumewaaga rasmi watumishi watano ambao wataenda mwezi ujao na kufikisha idadi ya watumishi 15.

  Amewataka watumishi hao wakaitangaze vizuri Tanzania na wakirudi waje kuitumikia Tanzania ili taifa lipate maendeleo yanayotarajiwa baada ya hatua hiyo muhimu ya kuwekeza kwa vijana watanzania katika kupata ujuzi.

  Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa Uingereza (DFID), Bi Beth Arthy, alisema kuwa tangu mpango huo uanze Serikali yake imekwisha wasomesha wanafunzi kumi katika fani za uchumi na uchambuzi wa masuala ya fedha na idadi ya watumishi watano watakao kwenda kusoma nchini humo itafikisha idadi ya watumishi 15.

  Alisema kuwa lengo la hatua hiyo ni kuisaidia Serikali kuimarisha utawala wa fedha, masuala ya usimamizi wa kodi na mifumo ya kifedha.

  Aidha amewapongeza waliofanikiwa kufuzu mitihani mbalimbali iliyowawezesha kupata nafasi hizo kwa watumishi wa Wizara hiyo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na kuwataka kufanya bidii kwa kuzingatia masomo ili watakapomaliza masomo yao warudi kulitumikia Taifa la Tanzania.

  Watumishi waliopata ufadhili wa masomo kupitia Shirika la DFID ni pamoja na Patricia Mlowe, Diana Ulomi, Alex Mwakisu, Martha Luanda na Hamad Bakar Said.

  Kwa upande wa wanufaika kupitia wawakilishi wao, Bi. Diana Ulomi na Hamad Said waliishukuru Serikali ya Uingereza na Wizara ya Fedha na Mipango kwa jitihada za kufanikisha kuwapatia masomo kwa ngazi ya Uzamili ili kuongeza ujuzi wa kulitumikia taifa katika masuala ya uchumi hasa kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati uliojikita katika Viwanda na wameahidi kusoma kwa bidii ili kufikia malengo hayo.

  0 0

  Mabalozi wakisiliza maelezo kuhusu ujenzi wa uwanja mpya wa ndege Zanzibar (Tereminal 3), kutoka kwa Mratibu wa Mradi huo Bw. Yasiri Costa. 
  Mabalozi wakiwasili eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya Kitope hadi Mkokotoni katika kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 31. Barabara hiyo hadi kukamilika kwake itagharimu jumla ya shilingi za Bilioni 58.6. 
  Mabalozi wakiwa Wameambatana na watumishi wa Wizara wakitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa barabara 
  Ujenzi wa daraja ukiendelea katika barabara ya Kitope-Mkokotoni 
  Mabalozi wakiwa eneo la ujenzi wa bandari ya mafuta iliyopo Mnangapwani walipotembele eneo la mradi huo Agosti 19, 2019. 
  Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, (katikati; ambaye pia aliongoza ujumbe wa mabalozi katika ziara) akitoa maelezo kwa Mabalozi waliopotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la makazi na biashara (Shopping mall) unaotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

  Jumla ya mabalozi 42 wanaoiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani wapo nchini, ambapo pamoja na mambo mengine wametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

  Wakiwa Zanzibar Mambalozi wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la biashara na makazi (shopping mall), uwanja mpya wa ndege (terminal 3), ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi Fumba, ujenzi wa mradi wa barabara ya kilomita 31 (Kitope hadi Mkokotoni) na ujenzi wa bandari ya mafuta iliyopo eneo la Mnangapwani.

  Mabalozi wamendelea kuridhishwa na kufahishwa na namna Serikali zote mbili (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano) zilivyo jidhatiti kutekeleza miradi mikubwa ambayo itachagiza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. 
  Mabalozi wakisikiliza maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la makazi na biashara (Shopping mall) lililopo eneo la Mapinduzi square, Michenzani kutoka kwa mtaalam na msimamizi wa mradi huo
  Mabalozi wakitembelea maeneo mbalimbali yanayouzunguka maradi kuona shughuli zinazondelea katika eneo hilo
  Mabalozi wakiwasili katika jengo la Makubusho ya Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar lililopo eneo la Michenzani, ambapo walipata fursa ya kufahamu kwa undani historia na taarifa mbalimbali kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar
  Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Jengo la Makumbusho ya Kumbukumbu ya Mapinduzi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipotembelea jengo hilo Agosti 19, 2019. 
  Balozi Ramadhani Mwinyi Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa Zanzibar, alipoongoza ujumbe wa mabalozi katika ziara ya mradi huo Agosti 19, 2019.

  0 0

  Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu akitoa neno la utangulizi katika mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
  Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
  Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akitoa taarifa katika mkutano wa tathimini ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) mara baada ya kufungua mkutano wao wa siku tatu, Agosti 19, 2019 ambao unafanyika kwa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
  Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini Agosti 19, 2019 ambao unafanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
  Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Agosti 19, 2019 ambao unafanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
  Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini Agosti 19, 2019 ambao unafanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu..  ……………………..

  Na Stella Kalinga, Simiyu RS

  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa (MSD) Laurean Bwanakunu amesema Bohari ya dawa inatarajia kuanza ujenzi wa kituo cha mauzo na usambazaji dawa mkoani Simiyu ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.  Bwanakunu ameyasema hayo Agosti 19,2019 katika ufunguzi wa mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa menejimenti na mameneja wa kanda wa bohari ya dawa nchini.

  lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu.

  Bwanakunu amesema wameamua kufanyia mkutano wa tathimini mkoani Simiyu ili kuweza kujionea eneo la ujenzi wa kituo cha mauzo ya dawa ikiwa ni moja ya kuongeza wigo mpana wa utoaji huduma.

  “Tutakuwa na mkutano wa siku tatu hapa Simiyu kwa ajili kufanya tathmini ya utendaji kazi ulivyokuwa kwa mwaka mzima, tutawafanyia tathmini wakurugenzi wote na wenyewe watamfanyia Mkurugenzi Mkuu; lakini pia tutatumia fursa hii kutembelea mahali tulipoamua kujenga bohari kwa kuwa tunatarajia kujenga bohari hapa Simiyu”alisema Bwanakunu.

  Akifungua mkutano huu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema maboresho ya usambazaji wa dawa yaliyofanywa na Bohari ya Dawa (MSD) yameongeza upatikanaji wa dawa mkoani Simiyu ambapo kwa sasa upatikananji wa dawa ni zaidi ya asilimi 88.

  Aidha, Sagini ametoa wito kwa Taasisi zote za Umma zinazohitaji maeneo kwa ajili ya kujenga Ofisi zao kufika mkoani Simiyu, ambapo amewahakikishia upatikanaji wa maeneo lengo likiwa ni kuendelea kusogeza huduma mbalimbali karibu na wananchi.

  Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Bibi. Victoria Elangwa amesema uwepo wa kituo cha kusambaza dawa Simiyu kutapunguza umbali kwa Mkoa wa Simiyu na mikoa ya Mara na Shinyanga kupata huduma za Bohari ambazo kwa sasa zinapatikana Mwanza.

  Ameongeza kuwa ujenzi wa Kituo hicho unatarajia kuanza mara moja kwa kuwa tayari wataalam wameshaanza kushughulikia masuala ya ukamilifu wa mazingira na baada kukamilisha kazi hiyo atatafutwa mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi.

  0 0

  Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) Kanda ya Mashariki umewashukuru wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani kwa namna walivyojitokeza kuchangiaji damu kwa ajili kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji ikiwemo majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 90 wameripotiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.

  Sambamba na shukrani hizo Mpango huo umeendelea kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kuchangia damu huku ukiwahimiza kuendelea kuchangia damu zaidi ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu waliopo kwenye vituo mbalimbali vya afya hapa nchini.

  Akizungumza wakati wa hitimisho la zoezi la uchangiaji damu lililofanyika kwa siku tatu mfululizo kwenye viunga vya stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam ili kusaidia majeruhi hao, Muhamasishaji Jamii kutoka NBTS, Bi Mariamu Juma alisema shukrani hizo zinafuatia mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa zoezi hilo muhimu lililoandaliwa na NBTS kwa kushirikiana na benki ya Exim Tanzania.

  “Kwa kweli muitikio ulikuwa wa kuridhisha na tumefanikiwa kukusanya chupa takribani 155 kulingana na malengo yetu hivyo tunawashukuru sana wakazi wa Mbagala na vile vile tunawashukuru sana Benki ya Exim Tanzania ambao ni washirika wetu wakubwa kwa kujitoa kwao kwa hali na mali hadi kufanikisha zoezi hili pamoja na wakazi wa Dar es Salaam kwa ujumla wanaoendelea kuchangia damu kwenye vituo vingine ikiwemo ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili.’’ Alisema.

  Tangu kutokea kwa ajali hiyo ya moto mkoani Morogoro imeshuhudiwa idadi kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam na kwinginepo nchini wakiguswa na kuitikia wito wa kuchangia damu kwa majeruhi hao ambapo imearifiwa kuwa bado kuna uhitaji wa damu huku jamii ikiendelea kuhamasishwa kujitolea zaidi ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji.

  “Watanzania wasisubiri kuuguliwa na ndugu ndio wakumbuke kuchangia damu na mazao ya damu wanatakiwa kuwa na tabia ya kuchangia damu mara kwa mara ili itumike kuwatibu wagonjwa na si tu majeruhi wa ajali bali pia kuna makundi mengine yenye uhitaji mkubwa wa damu ambayo ni pamoja na wagonjwa wa saratani, watoto, kina mama wajawazito na wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji’’ alisema.
  Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye viunga vya Stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakifuata taratibu ili kuchangia damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa. Zoezi hilo la siku tatu lilikamilika mwishoni mwa wiki, kwa uratibu wa benki ya Exim Tanzania kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS).

  0 0
  Waziri Kabudi afungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje kuongeza jitihada katika kuhamasisha wawekezaji, wafanyabiashara na watalii kuja nchini ikiwa ni utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.


  Waziri Kabudi ameyasema hayo leo tarehe 20 Agosti 2019 wakati akifungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere kuanzia tarehe 20 hadi 23 Agosti 2019.


  Mhe. Waziri Kabudi alisema kuwa, Mabalozi ambao wana jukumu kubwa la kusimamia maslahi ya nchi kwenye nchi mbalimbali duniani, wameendelea kufanya kazi nzuri katika katika kuhakikisha dhana ya diplomasia ya uchumi inafikiwa na kwamaba matokeo ya jitihada hizo ni pamoja na kuongezeka kwa watalii, wawekezaji na wafanyabiashara nchini. P.ia kuongezeka kwa fursa za ufadhili wa masomo na ajira kwa Watanzania kwenye nchi mbalimbali


  “Hii ni mara yangu ya kwanza kukutana nanyi Waheshimiwa Mabalozi tangu niteuliwe na Mhe. Rais kwenye wadhifa huu. Nazipongeza jitihada zenu katika utekeelzaji wa diplomasia ya uchumi kwani matokeo tunayaona kwa biashara kuongezeka hapa nchini watalii na hata wawekezaji. Hivyo nataka mwongeze jitihada Zaidi ili nchi yetu ifikie azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025” alisema Mhe. Kabudi”.


  Aidha, Mhe. Waziri Kabudi alitoa rai kwa Mabalozi kuendelea kuwahamasisha Watanzania waishio nje (Diaspora) kujiandikisha na kuanzisha jumuiya zao ili kwa namna moja au nyingine na wao washiriki kuchangia maendeleo hapa nchini.


  Akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili Mabalozi hao ikiwa ni pamoja na uchakavu wa baadhi ya majengo ya balozi, Mhe. Kabudi alieleza kuwa Wizara inaendelea kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo.


  Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi, Kiongozi wa Mabalozi hao, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Mabalozi walipata fursa ya kuitembelea. Alisema kuwa, miradi hiyo ni chachu ya maendeleo katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.


  Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati. Tumepata fursa ya kujionea miradi hiyo ikiwemo ile ya ujenzi wa barabara, reli na umeme. Kimsingi miradi hii inalenga kumwondolea umaskini Mtanzania kwa vile itarahisha usafirishaji na kumwezessha mkulima kusafirisha kwa urahisi mazao yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia miundombinu hiyo.


  Pia aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kufanikisha Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanyika nchini kwa mafaniko makubwa.


  Imetolewa na:


  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,


  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,


  Dar es Salaam


  20 Agosti


  2019

  Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani. Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Agosti 20,2019oLengo la kikao hicho ni kujadili masula mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

  Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizumgumza kwenye kikao na Mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani.


  Mabalozi na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyo kuwa ikitolewa na Waziri Mhe. Prof Kabudi (Hayupo pichani).  Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia kikao


  Waziri Kabudi afungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje kuongeza jitihada katika kuhamasisha wawekezaji, wafanyabiashara na watalii kuja nchini ikiwa ni utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.

  Waziri Kabudi ameyasema hayo leo tarehe 20 Agosti 2019 wakati akifungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere kuanzia tarehe 20 hadi 23 Agosti 2019.

  Mhe. Waziri Kabudi alisema kuwa, Mabalozi ambao wana jukumu kubwa la kusimamia maslahi ya nchi kwenye nchi mbalimbali duniani, wameendelea kufanya kazi nzuri katika katika kuhakikisha dhana ya diplomasia ya uchumi inafikiwa na kwamaba matokeo ya jitihada hizo ni pamoja na kuongezeka kwa watalii, wawekezaji na wafanyabiashara nchini. P.ia kuongezeka kwa fursa za ufadhili wa masomo na ajira kwa Watanzania kwenye nchi mbalimbali

  “Hii ni mara yangu ya kwanza kukutana nanyi Waheshimiwa Mabalozi tangu niteuliwe na Mhe. Rais kwenye wadhifa huu. Nazipongeza jitihada zenu katika utekeelzaji wa diplomasia ya uchumi kwani matokeo tunayaona kwa biashara kuongezeka hapa nchini watalii na hata wawekezaji. Hivyo nataka mwongeze jitihada Zaidi ili nchi yetu ifikie azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025” alisema Mhe. Kabudi”.

  Aidha, Mhe. Waziri Kabudi alitoa rai kwa Mabalozi kuendelea kuwahamasisha Watanzania waishio nje (Diaspora) kujiandikisha na kuanzisha jumuiya zao ili kwa namna moja au nyingine na wao washiriki kuchangia maendeleo hapa nchini.

  Akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili Mabalozi hao ikiwa ni pamoja na uchakavu wa baadhi ya majengo ya balozi, Mhe. Kabudi alieleza kuwa Wizara inaendelea kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo.

  Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi, Kiongozi wa Mabalozi hao, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Mabalozi walipata fursa ya kuitembelea. Alisema kuwa, miradi hiyo ni chachu ya maendeleo katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati. Tumepata fursa ya kujionea miradi hiyo ikiwemo ile ya ujenzi wa barabara, reli na umeme. Kimsingi miradi hii inalenga kumwondolea umaskini Mtanzania kwa vile itarahisha usafirishaji na kumwezessha mkulima kusafirisha kwa urahisi mazao yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia miundombinu hiyo.

  Pia aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kufanikisha Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanyika nchini kwa mafaniko makubwa.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dar es Salaam
  20 Agosti 2019
  Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani. Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Agosti 20,2019oLengo la kikao hicho ni kujadili masula mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.
  Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizumgumza kwenye kikao na Mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani.
  Mabalozi na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyo kuwa ikitolewa na Waziri Mhe. Prof Kabudi (Hayupo pichani).
  Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia kikao

  Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Wizara mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi
  Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake
  Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki mara baada ya ufunguzi wa Kikao.
  Mhe. Nahimu Azizi Balozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Kikoa kazi cha Mabalozi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Wizara mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi
  Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake
  Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki mara baada ya ufunguzi wa Kikao.
  Mhe. Nahimu Azizi Balozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Kikoa kazi cha Mabalozi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

  MKURUGENZI wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) Basila Mwanukuzi Shayo amesema fainali za mashindano hayo yatahitimishwa rasmi Ijumaa ya Agosti 23 mwaka 2019, ukumbi wa Millenium Tower LAPF uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwanukuzi amesema washiriki wapatao 20 kutoka mikoa mbalimbali nchini wapo kambini tangu Agosti 12 mwaka huu wakijiandaa na kinyang'anyiro cha kuwania taji hilo.

  "Kufanyika kwa fainali hizi ni hitimisho ya mashindano ya Mikoa ambayo yalifanyika kuanzia mwezi April mwaka huu" ameeleza.

  Amesema kwa kipindi walichokuwa kambini washiriki wameshiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutembelea, kuwafariji na kucheza michezo mbalimbali na watoto katika kituo cha watoto yatima kilichopo Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam na kufanya shughuli nyingine za kijamii.

  "Washiriki wakiwa kambini wamepata pia nafasi ya kufanya mashindano madogo madogo kwa mujibu wa mashindano ya dunia ambapo walifanya mashindano ya kumtafuta mrembo mwenye kipaji.

  "Mrembo mwenye mvuto katika picha, mrembo mwanamitindo, mrembo mwanamichezo na mrembo chaguo la watu, na washindi watatangazwa siku ya tukio" ameeleza Mwanukuzi.

  Mashindano hayo yanategemewa kuwa ya aina yake ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kujipatia tiketi zao ili kumshuhudia mlimbwende atakayeliwakilisha Taifa katika mashindano ya urembo ya dunia.
   Washiriki wa shindano la Miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania nchini, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akiwa na baadhi ya wadhamini wa shindano hilo pamoja na warembo hao (waliosimama) leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano ya urembo ya Miss Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii, ambapo ameeleza kuwa maandalizi yapo tayari na mashindano yatakuwa ya aina take, leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Meneja wa Kitengo cha Sayansi Jinai, Biolojia na Vinasaba Bi. Hadija Saidi Mwema alipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wagonjjwa na wafanyakazi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wakati akitembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa kukagua sehemu mbali mbali za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam alipotembekea leo Agosti 20, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Bw. Kagera Zacharia Ng’weshemi juu ya uendeshaji wa mashine ya kisasa ya kuchambulia na kugundua vinasaba vya aina mbalimbali ikiwemo dawa za kulevya alipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019. Mashine hiyo za aina hiyo katika Afrika zipo Tanzania, Afrika Kusini na Madagascar pekee.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam alipotembelea leo Agosti 20, 2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason na kulia ni MKEMIA Mkuu wa erikali, Dkt. Fidelice Mafumiko.
  Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukiondoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam ambako Mhe Rais alitembelea leo Agosti 20, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli akiongea na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam alipotembelea leo Agosti 20, 2019.
  Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukiondoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam ambako Mhe Rais alitembelea leo Agosti 20, 2019.
  Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza kwa kazi nzuri viongozi wa vyombo vya ulinzi na Usalama wa Mkowa wa Dar es salaam wakati wa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi za SADC wakati akiwa anaondoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam alikotembelea leo Agosti 20, 2019.

  0 0

   Awali Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa madarasa, Bweni na Matundu ya vyoo katika shule ya Sekondari Ulowa. 
   Serikali mkoani Shinyanga imewatoa wasiwasi wakulima wa zao la Tumbaku katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama juu ya uuzaji wa tumbaku kilo milioni mbili ambayo imebaki na kusema kwamba wanunuzi wapo na itanunuliwa yote.

  Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo Agosti 20.2019 katika viwanja vya shule ya Msingi Kangeme kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wakati wa ziara ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga.

   Telack amesema serikali inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha kwamba wakulima hao wa tumbaku wanapata mnunuzi na tayari kampuni ya British American imekwishapatiwa kibali na itaanza kununua tumbaku hiyo hivi karibuni. "Kutokana na changamoto iliyojitokeza hapo awali ya ununuzi wa zao la Tumbaku kutokana kampuni ya TLTC kusitisha ununuzi wa zao hili, serikali sikivu iliendelea kutafuta wanunuzi na tayari kampuni ya Alliance itanunua asilimia 10 ya tumbaku hiyo pamoja na kampuni ya British American ambapo yenyewe itanunua tumbaku yote itakayobaki",amesema Telack. 

  "Naagiza pia acheni kukata miti hovyo kwa ajili ya kuchomea tumbaku zenu ,nilishasema muwe mnakata matawi na siyo miti kama mnavyofanya hivi sasa na mkiendelea na hali hii nitasitisha ulimaji wa zao la tumbaku kwa sababu hatutaki tuishi kwenye hali ya jangwa,"ameongeza. 

  Aidha amewataka wakulima hao wa tumbaku kutumia vyema pesa ambazo watazipata kutokana na mauzo ya tumbaku, kwa kuzifanyia shughuli za maendeleo ikiwemo kujenga nyumba za kisasa na kusomesha watoto wao. Kwa upande wake, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga, amesema serikali ya Tanzania itawasaidia wakulima wa tumbaku ili kuhakikisha tumbaku yao inanunuliwa.

  Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesema kuwa shauku kubwa ya wakulima wa tumbaku wa kata ya Ulowa, ni kujua hatma ya uuzaji wa tumbaku yao iliyobaki yenye kiasi cha kilo milioni mbili na kumuomba mkuu wa Mkoa awapatie ufafanuzi wakulima hao juu ya suala hilo  Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga akiwatoa wasiwasi wakulima wa zao la tumbaku katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu kuwa serikali yao itahakikisha inawasaidia wakulima na kuhakikisha tumbaku yao inanunuliwa yote. Picha zote na Annastazia Paul,Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na wananchi wa kata ya Ulowa halmshauri ya Ushetu wilayani Kahama ambao ni wakulima wa zao la tumbaku na kuwatoa wasiwasi kuwa tumbaku yao iliyosalia kilo Milioni 2 itanunuliwa yote.  Awali Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, alimuomba mkuu wa mkoa Zainab Telack kuwatoa wasiwasi wakulima wa zao la Tumbaku juu ya hatma ya ununuzi wake mara baada ya kampuni ya awali iliyokuwa ikinunua zao hilo kusitisha ununuzi.  Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Jimbo la Ushetu kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo Elias Kwandikwa,ambapo alisema asilimia kubwa ya miradi ya maendeleo imetekelezwa ikiwamo ya huduma za afya , ujenzi wa zahanati, kituo cha afya , hospitali ya wilaya pamoja na unuaji wa vifaa tiba.  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Iddi, akiwataka wananchi wa kata ya Ulowa kuwa wawe wanachangia shughuli mbalimbali za maendeleo na siyo kutegemea kila kitu wafanyiwe na serikali, huku akitoa Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya ununuzi wa saruji mifuko 50 ili kukamilisha ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari Ulowa.  Wananchi wa Kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.  Wananchi wa Kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.  Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kangeme Kata ya Ulowa- Ushetu wilayani Kahama. 
   Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsalimia mmoja wa wanafunzi katika shule ya Sekondari Ulowa Leticia Tungu (15) ambaye anasoma kidato cha kwanza.  Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya sekondari Ulowa kusoma kwa bidii hasa masomo ya Sayansi ili waje kuwa tegemeo katika familia zao pamoja na taifa kwa ujumla kwa kupata watalaamu ambao watailetea maendeleo nchi.  Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini,Mhe. Jumanne Kishimba akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Jimbo hilo, kuwa changamoto kubwa ambayo wanakabiliana nayo ni ubovu wa miundombinu ya barabara hasa za mjini.  Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba akikabidhi Taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Kwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.  Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akiwaapisha wanachama wapya watano wa Chama cha Mapinduzi CCM, ambao wamekihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Picha zote na Annastazia Paul,Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

  0 0  0 0

  Kampuni ya TBL chini ya kampuni ya Kimataifa ya ABInBev,imekabidhi masada wa vipuri vya kukarabati magari ya kituo cha polisi cha Ilala akiwa ni mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za Serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuimarisha usalama kupitia kuboresha usafiri katika Jeshi hilo. 
   
  Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Ilala, Calvin Martin na ulipokelewa naMkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma,ambaye alishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia taasisi za Serikali sambamba na kufanya nazo kazi kwa kariibu katika kufanikisha kampeni mbalimbali zenye kunufaisha jamii. 
   
  Meneja wa kiwanda cha Ilala,Calvin Martin, alisema kuwa TBL, itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali kama ambavyo imetoa vipuri (Shock Absorber) kwa ajili ya kufanikisha kutengeneza magari ya kituo cha Polisi cha Ilala, kwa ajili ya kuboresha usafiri wa askari wakati wa kutekeleza majukumu yake ya ulinzi na huduma mbalimbali katika jamii. 
   
  Aliongeza kusema kwa muda mrefu kampuni ya TBL imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Jeshi la Polisi katika kufanikisha kampeni zake mbalimbali za kijamii hususani zinazohusu usalama barabarani,kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia na kampeni ya kuhamasisha matumizi yenye vinywaji vyenye kilevi kistaarabu.


  Meneja wa kiwanda cha TBL ilala jijini Dar es Salaam, Calvin Martin, akiwa na wafanyanyakazi wa kiwanda hicho wakikabidhi masada wa vipuri kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma,kwa ajili ya kuboresha usafiri wa Jeshi hilo.
  Meneja wa masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi na Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma, wakisaini nyaraka za makabidhiano ya vipuri hivyo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Ilala, wakishuhudia makabidhiano hayo katika hafla iliyofanyika katika kiwandani.
  Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma, akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Ilala jijini Dar es Salaam Wakati wa hafla hiyo

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimina na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakati Bw. Alvaro alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 21,2019 kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa nchini. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakati Bw. Alvaro alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 21,2019 kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa nchini .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

  =========
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono mageuzi ya mfumo wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa kwenye maeneo mbalimbali yaliyoafikiwa. 


  Amesema Tanzania itaendelea na mpango wa pili wa Maendeleo wa Msada wa Umoja wa mataifa ambao unatekelezwa sambamba na Dira ya Zanzibar ya 2020 pamoja na awamu ya pili ya mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Taifa (F2016,2021 FYDP2) wenye lengo la kuisaidia Tanzania kufikia Uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025. 

  Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Agost 21, 2019 Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kufanya Mazungumzo na Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa ayefika Ofisini kwake kwa ajili ya kumuaga Baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa Nchini. 

  Aidha Makamu wa Rais amemshukuru Bw. Alvaro kwa Ushirikiano na Uhusiano Mzuri alioujenga baina ya Tanzani na Umoja wa Mataifa katika kipindi chake chote alichokuwepo hapa Nchini kwa kusukuma Agenda za Nchi na kuiletea mafaniko katika Sekta mbalimbali na kumtakia kila la heri na kazi njema katika kituo chake kipya cha kazi, ambapo Bw. Alvaro ameteuliwa kuwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Uturuki. 

  Wakati huo huo Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bw. Alvaro ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwasilisha Taarifa za mapitio ya Hiyari (VNR) ya Utekelezaji wa Maelengo ya Maendeleo Endelevu ya Mwezi Julai 2019 kwa kuwainisha Mafanikio, Changamoto na mbinu bora za kukabiliana nazo pamoja na kujifunza.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimkabidhi zawadi ya picha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, baada ya mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimkabidhi zawadi ya picha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, baada ya mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), wakifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, aliye katika ziara ya kikazi hapa nchini, Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), walipokutana Jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Benki na Serikali ya Tanzania.
  Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (kulia) na Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara hiyo, Bw. Shogholo Msangi, wakifuatilia mazungumzo kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), walipokutana Jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Benki hiyo na Serikali ya Tanzania
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kulia), akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, aliye katika ziara ya kikazi hapa nchini, Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagamba (wa pili kushoto), akieleza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kulia), Jijini Dar es Salaam. (Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)


  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam


  Uhusiano wa Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania umeimarika baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia nchi 22 zilizoko Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango kuwa Benki hiyo iko tayari kutoa kwa Tanzania fedha zote za mkopo wa masharti nafuu kiasi cha dola za marekani bilioni 1.7 zilizobaki katika mgao wa 18 wa IDA.

  Bi. Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi amesema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.

  Alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kutolewa kabla ya kuanza mgao mpya wa 19 wa IDA utakaoanza Julai 2020, baada ya kukamilisha taratibu zote za upatikanaji wa fedha hizo.

  ”Fedha hizi zitaelekezwa katika kutekeleza miradi kadhaa muhimu ikiwemo ya Elimu, Afya, Mradi wa kusaidia Kaya Masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF, Awamu ya Pili na Uendelezaji wa Miji na Masuala ya Uchumi Jumuishi Visiwani Zanzibar” alisema Bi. Kabagambe

  Aidha, alipongeza hatua kubwa zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli, katika kupiga vita rushwa na ufisadi nchini pamoja na kutekeleza miradi ya jamii kwa umahili mkubwa ikiwemo miradi ya kimkakati ya reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa pamoja na mradi wa kufua umeme wa maporomoko ya maji katika mto Rufiji wa Julius Nyerere.

  Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameiomba Benki hiyo kuisaidia Serikali kwa kuipatia fedha za kufanikisha ujenzi wa miundombinu hiyo ya umeme, reli, maji safi na salama, kuimarisha sekta ya kilimo, viwanda, bandari, rasilimali watu na masuala ya teknolojia ya habari na Mawasiliano-TEHAMA.

  Alibainisha kuwa miradi hiyo itachochea zaidi ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini wa wananchi kwa kuwa nishati ya umeme itachochea ukuaji wa sekta ya viwanda hivyo na kukuza ajira, wakati reli imara na ya kisasa itaimarisha mtandao wa reli na kuwa uti wa mgongo wa maendeleo ya Tanzania na nchi za Ukanda wa Afrika kwa ujumla.

  Amepongeza pia uamuzi wa Benki hiyo wa kuruhusu upatikanaji wa fedha kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.7 na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika sekta ya elimu, kusaidia kaya maskini kupitia TASAF, kuendeleza masuala ya uchumi jumuishi Visiwani Zanzibar, masuala ya ardhi na miundombinu ya barabara ili kuboresha shughuli za kiuchumi katika jamii.

  Akitoa majumuisho ya mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na Mgeni wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban, alisema kuwa Serikali inapongeza uamuzi wa Benki wa kuendelea kuipatia fedha serikali ya Tanzania kwa manufaa ya wananchi.

  Mpaka sasa, Benki ya Dunia imefadhili miradi 28 ya Maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.0 sawa na takriban sh. trilioni 11.5, ambapo miradi 20 ni ya kitaifa yenye thamani ya dola 4.065 bilioni na miradi 8 ni ya kikanda yenye jumla ya dola za Marekani 938 milioni.

  0 0

  Charles James, Michuzi TV

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe Edward Mpogolo amepongezwa kwa namna ambavyo ameweza kusimamia miradi ya maendeleo ndani ya muda mfupi tangu ateuliwe kwenye nafasi hiyo.

  Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally wakati Mwenge wa Uhuru ulivyofika kukagua miradi ya maendeleo wilayani Ikungi.

  Miradi mitano ya Maendeleo iliyokaguliwa na kuzinduliwa ni pamoja na vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Darajani, Mradi wa Maji uliopo Kijiji cha Ighuka, Mnara wa Mwenge wa Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na Ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi ambapo miradi yote hiyo imegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.162.

  Akizungumza Wilayani hapo Kiongozi huyo amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi kufanya kazi kwa uzalendo ili kuwafanya Watanzania waendelee kuiamini Serikali yao chini ya Rais Dk John Magufuli.

  " Niwapongeze sana Wananchi wa Ikungi kwa namna ambavyo mmeendelea kumuamini Rais wetu Dk Magufuli, kipekee nikupongeze DC Mpogolo kwa uzalendo wako unaouonesha toka uteuliwe na Mhe Rais kuwa Mkuu wa Wilaya hii, nikuombe uendelee kuwatumikia wananchi wetu kwa kasi hii hii uliyoanza nayo.

  " Niwaombe pia ndugu zangu wa Ikungi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na muende kuwachagua viongozi ambao ni waadilifu na wenye kuichukia rushwa, msichague viongozi mafisadi, chagueni watu safi watakaoweza kuwatumikia bila kujali itikadi zenu," amesema Mzee Mtongea.

  Kwa upande wake DC Mpogolo ameahidi kuendelea kusimamia miradi ya Serikali kwa uadilifu pamoja na kuwatumikia wananchi hawa ambao walimuamini Rais Dk Magufuli na kumpa kura.

  DC Mpogolo amesema atahakikisha wananchi wa Ikungi wananufaika na miradi ambayo imezinduliwa ndani ya Wilaya hiyo ili waweze kuona kazi kubwa ambayo Serikali inaifanya katika kuwahudumia.

  " Miradi hii imegharimu Fedha nyingi upo ujenzi wa madarasa mawili ambayo yanaakisi Sera ya Elimu bure inayosimamiwa na Rais wetu kipenzi, mradi wa Maji kama sehemu ya kampeni yetu ya kumtua Mama ndoo kichwani, yote hiyo ni katika kuwatumikia nyinyi wananchi wetu na zaidi kutimiza ahadi ya Rais aliyoitoa kwenu mwaka 2015.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally (wa mbele) akikagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Darajani Wilayani Ikungi ambapo aliridhishwa na ujenzi huo na kuuzindua.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Edward Mpogolo (katikati) akizungumza mbele ya wakimbiza Mwenge Kitaifa wakati Mwenge ulipofika kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya yake
  Sehemu ya wananchi wa Eneo la Puma wilayani Ikungi waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru uliofika Wilayani hapo kukagua miradi ya maendeleo

  0 0  Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Alex Ntanguligwa (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL alipokuwa akifungua mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo.
  Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo ukiendelea katika Hotel ya Landmark.
  Meneja Maendeleo wa Mtandao wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Enocent Msasi akichangia mada katika Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA).
  Katibu Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA), Eng. Jacob Munodawafa (kushoto) akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

  Katibu Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA), Eng. Jacob Munodawafa akiwasilisha mada katika mkutano huo.

  Katibu Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA), Eng. Jacob Munodawafa akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano huo (hawapo pichani).
  Sehemu ya wajumbe wa Mkutano Maalum wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) wakifuatilia mada anuai katika Hotel ya Landmark.
  Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo ukiendelea katika Hotel ya Landmark.
  Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Alex Ntanguligwa akiwaonesha wajumbe picha ya Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli iliyokuwa katika ukumbi wa mkutano kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
  Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo ukiendelea katika Hotel ya Landmark.
  Baadhi ya wajumbe wa Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo kwenye Hotel ya Landmark.

  0 0

  Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario akiongoza ya misa takatifu ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kesyy iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Yohani Mtume ,Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.
  Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia alikuwa miongoni mwa waumini walioshiriki Ibada hiyo ,ambapo Padri Thomas Kessy ni kaka yake mkubwa .
  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika Ibada ya Misa ya takatifu ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Kessy .
  Padri Thomas Kessy akizungumza wakati wa ibada hiyo.
  Baadhi ya ndugu wa Padri Thomas Kessy wakishiriki ibada hiyo.
  Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa hotuba yake wakati wa ibada ya Misa takatifu ya Jubilei ya fedha ya kaka yake Padri Thomas Kessy .
  Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario akimkabidhi Padri Thomas Kessy sululu na vitu vingine vilivyotolewa kanisani hapo kama kumuunga mkono.
  Baada ya kumalizika kwa misa hiyo ,shughuli ilihamia nyumbani kwa familia hiyo eneo la Kirua Vunjo wilaya ya Moshi.
  Padri Thomas Kessy akiwaongoza ndugu zake kufungua Champegne wakati wa hafala fupi ya pongezi kwa Padri Thomas Kessy kufikisha miaka 25 ya utume.
  Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akiwawekea wageni waalikwa kinywaji cha Champegne wakati wa hafla hiyo
  Padri Thams Kessy akikata ndafu katika hafla hiyo.
  Padri Thomas Kessy akimlisha kipande cha ndafu  Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario.
  Baadhi ya wageni wakiwa katika hafla hiyo.
  Wageni wakicheza muziki na Padri Thomas Kessy katika hafla hiyo hiy iliyofanyika nyumbani kwa familia ya Mbatia.

  Na Dixon Busagaga .


  MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewapa neno wakuu wa nchi 16 zinazounda Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), katika mkutano ujao kufikiria kuja na ajenda ya pamoja ya sera moja ya elimu inayofanana.

  Mbatia amesema kuwa kama itakuwapo dhamira ya pamoja ya kuwa na sera hiyo ya elimu kwa wanachama wa SADC, kunaweza kubadili sura ya Afrika na mageuzi makubwa yakaonekana kwa miaka 20 yakisadifu mfumo wa elimu wa nchi za Ulaya.

  Mbatia ametoa kauli hiyo mara  baada ya kumalizika kwa ibada ya misa takatifu ya Jubilee ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kessy, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Yohani Mtume, Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo, mkoani Kilimanjaro.

  Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Mhashamu Rogathe Kimario, akisaidiwa na Msimamizi wa Jimbo Katoliki la Moshi na Wakili wa Askofu, Deogratius Matiika.


  “Kwa mfano, majuzi nilisikia na kusoma baadhi ya maandiko kwamba watu wa Namibia wao wanasema mfano mwanafunzi anayetoka Tanzania na amemaliza kidato cha sita na akienda kwao, kupata Chuo Kikuu kule ni shida, kwa sababu Namibia wao mfumo wao ni mgumu, wao elimu zao wanamalizia kidato cha nne. Unajiuliza hivi silabasi zetu zimeundwa namna gani, nawashauri wakuu wa nchi wanachama ni vizuri tukawa na sera moja ya SADC katika masuala ya elimu,”alisema

  Mwaka huu, Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa SADC ikiwa imepita miaka 16, tangu mkutano kama huo kufanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2003 chini ya utawala wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

  Kuhusu Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, kuweka mikakati ya kuziwezesha nchi wanachama kufikia malengo ya kuelekea kwenye ukuaji wa uchumi wa kati utakaokuwa maendeleo ya viwanda, Mbatia alisema:

  “Mimi nina ushauri kwa SADC, pamoja na mambo ya viwanda na mambo mengine yote ambayo ni muhimu, wakuu wa nchi 16 wajitahidi sana kuhakikisha nguvu kazi ya SADC ambayo ni vijana, wanapata elimu ambayo ni ujuzi na wanaweza kuzalisha kwenye viwanda, wanaweza kuondoa masuala ya umasikini, njaa, watu wakawa na afya njema lakini penda tusipende ni lazima tuangalie je mifumo yetu ya elimu ikoje,”alieleza

  Alisema malengo hayo yanatekelezeka, lakini sharti nchi wanachama wawe wamejiandaa vizuri na kwa utafiti alioufanya, bado kuna kazi kubwa mbele ya safari, na akashauri zaidi kuwa malengo hayo yasiwe ya maneno, yaende kwenye vitendo zaidi

  0 0


  Baadhi ya Watanzania 64 wakiwa uwanja wa Kimataifa wa ambao tayari kwa safari kuelekea nchini Israel kwaajili ya safari ya Kidini pamoja na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Teknolojia.
  Baadhi ya Watanzania 64 ambao wameshaanza safari kuelekea nchini Israel kwaajili ya safari ya Kidini pamoja na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Teknolojia.

  Mratibu wa Safari hiyo Padre Melodis Mlowe wa Jimbo Katoliki la Njombe  Haryson Chanjo kutoka kamapuni ya Exellence Guide ni miongoni mwa waratibu wa safari ya kidini ya utalii kuelekea ISRAEL


  Mmoja wa wasafiri akiwa tayari uwanja wa Kimataifa KIA akiwa ameambatana na binti yake
  Baadhi ya Watanzania 64 amabao wameshaanza safari kuelekea nchini Israel kwaajili ya safari ya Kidini pamoja na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Teknolojia.


  Na.Vero Ignatus,Arusha.

  Zaidi ya Watanzania 64 kutoka Mikoa yote nchini wameondoka kwenda nchini Israel kwaajili ya safari ya kidini pamoja na kujifunza mambo mbalimbali yaTeknolojia pamoja nakutangaza utalii na vivutio mbalimbali vilivyo Nchini.

  Akizunguza Mratibu wa Safari hiyo Padre Melodis Mlowe wa Jimbo Katoliki la Njombe amesema kuwa mafanikio ya safari hiyo yanatokana na Balozi wa Tanzania nchini Israel kuwataka watanzania kutumia fursa ya ndege inayowaleta watalii nchini,ili waweze kuitumia kwenda Israel kujifunza kwani bei yake ni nafuu ukilinganisha na bei za ndege nyingine.

  \\Kupitia fursa gharama ambayo ilikuwa inasomeka mil 8-9 kwa mashirika na makampuni mengine kupitia program hii gharama ni pungufu sana kwasababu dola wanayolipa ni 1390 kwa tikati ya ndege malazi chakkula na na safari nzima kwenda na kurudi kwa siku saba ni gharama pungufu kuliko gahrama yeyote ile.

  Padre Mlowa amesema lengo kuu ya safari hiyo ni watanzania kwenda nje ya nchi kujifunza,yakiwemo mambo mengi ambayo wanatakiwa kujifunza ikiwemo ujasiri,teknolojia na maendeleo,amesema Israel ndiyo nchi sahihi kwani uoto wa nchi hiyo ni mawe mchanga pamoja na jangwa ila ndiyo nchi yenye mafanikio makubwa.

  Akizungumza wakati wakianza safari Padre amesema katika matatizo ya uoto wa nchi hiyo ya Israel, wameigeuza kama fursa kwao hivyo wao kama watanzania wanakwenda siyo kwaajili ya kutalii peke yake bali kujifunza fursa mbalimbali na kutangaza Utalii wa Tanzania.

  Hakuna haja ya Nchi ya Tanzania kuendelea kuwa maskini wakati tunazo fursa nyingi ukitofautisha na Israel,wao changamoto kubwa waliyonayo ni ardhi yao kubwa ni mawe,mchanga na jangwa ila sisi tunakwenda kujifunza wamewezaje kufanikiwa alisema padre Mlowa.Amewataka watanzania kutoka kwaajili ya kujifunza katika nchi mbalimbali kwaajili ya kupata mtazamo chanya kwaajili ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

  Haryson Chanjo kutoka kamapuni ya Exellence Guide ni miongoni mwa waratibu wa safari ya kidini ya utalii kuelekea ISRAEL amesema kuwa wameitumia fursa hiyo ya ndege inayoleta watalii kutoka Israel kuja kutembelea mbuga za wanyama nchini ambayo wanafanya mabadilishano ya wao kuja na watanzania kwenda kujifunza mambo mbalimbali kwani wao wanapata biashara na Tanzania vilevile.

  Amesema safari kama hizo lengo kubwa ni kutangaza utalii wa taifa katika masoko mapya kwani zipo nchi nyingi duniani zinahitaji kujua Tanzania kuna vivutio mbalimbali ,ikiwemo mlima Kilimanjaro,hifadhi na vivutio vingi vya asili.

  \\Novemba 12 mwaka huu tutakuwa na ndege nyingine inaondoka kuelekea Israel, safari nyingine Mwezi wa kumi na moja mwakani tutaanza mara tu baada ya pasaka tutakuwa na mtiririko wa safari kwani mwitiko mkubwa sana kwa watanzania ila changamoto kubwa ni muda wa maandalizi umekuwa mdogo sana na vithibitisho vyote vinavyohusisha nyaraka paspoti na na viza //Alisema Hurryson

  Amesema kuwaamefurahi kuona Tanzania ina balozi nchini Israel kwani imekuwa rahisi kwa watanzania kupata nafasi ya kwenda Israel vilevile wanaomba Israel iweze kufungua ofisi ya ubalozi nchini ili iwe rahisi kwa watanzania kupata viza kirahisi ilikuepusha watanzania kwenda kutafuta viza nchini Kenya.

  Kuna gharama ya watanzania kwenda Kenya kutafuta viza na kurudi Tanzania tena kampuni ya Exellent Guide watoe huduma hiyo kwa wingi zaidi ili watanzania wengi waweze kunufaika na huduma hiyo sambamba na kutangaza utalii katika masoko mapya kama Asia,Amerika na nchi nyingine ambazo zinahitaji kuifahamu Tanzania.

  Aidha Watanzania waliosafiri kwenda nchini Israel wametoka katika mikia ya Mwanza Dar es salaam,Iringa Njombe,Musoma Dodoma,
  jombe,Kilimanjaro,Arusha,Tanga,ambapo safari hizo zitakuwa endelevu.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru (aliyevaa shati jeupe) akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mh. Tae-ick-Cho ambaye leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.
  Balozi Tae-ick-Cho akizungumza jambo wakati wa kikao hicho mapema hii leo katika Hospitali ya Mloganzila.
  Baadhi ya viongozi wa MNH-Mloganzila pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa Korea nchini , wakimsikiliza kwa makini Balozi Tae-ick-Cho ambaye ameahidi kushirikiana na Hospitali ya Mloganzila katika kutatua changamoto zilizopo.
  Balozi Tae-ick-Cho (wa kwanza kulia) akiwa na ujumbe wake, wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumalizika kwa kikao, wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.
  Balozi Tae-ick-Cho (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru (kushoto), kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.

  Na Neema Wilson Mwangomo

  Balozi wa Jamhuri ya Korea Tae-ick-Cho leo amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kuahidi ushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali kwa lengo la kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

  Pamoja na mambo mengine katika mazungumzo hayo, Balozi Tae-ick-Cho pia amezungumzia jinsi ya kuboresha mfumo wa TEHAMA uliokuwepo katika kusimamia utoaji wa huduma za afya hospitalini.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema watanzania wanapenda kuona hospitali hii ikifanya kazi iliyokusudiwa ya kutoa huduma, elimu na utafiti na kusisitiza kuwa hilo ndio kusudio kubwa la Rais John Magufuli.

  “Lengo letu ni kuhakikisha hospitali hii inafanya kazi kama inavyotakiwa hasa ukizingatia ni hospitali kubwa na ya kisasa hivyo tutaendelea kuboresha huduma zetu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa” amesema Prof. Museru.Balozi Tae-ick- Cho mapema hii leo amefika MNH-Mloganzila kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza na uongozi wa hospitali.

  0 0


  Meneja Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Magdalena Lyimo akiwasilisha mada ya hali ya upatikanaji wa damu salama nchini kwenye kikao.kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri unaondelea jijini Dodoma.
  Mkurugenzi Idara ya TIba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiongea kwenye kikao.kazi hicho.
  Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia uwasilishaji wa mada unaoendelea kwenye ukumbi wa CCM

  ……………………

  Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

  Mpango wa damu salama umefanikiwa kukusanya chupa 51819 sawa na asilimia ishirini zaidi ya malengo waliyojiwekea kwa mwaka 2018/2019.

  Hayo yameelezwa leo na meneja mpango wa taifa wa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo wakati akiwasilisha mada ya upatikanaji wa damu kwenye kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri kinachoendelea jijini hapa.

  Dkt. Lyimo amesema kwamba kwa mwaka 2018/2019
  wizara ya afya kupitia mpango huo uliweka malengo ya kukusanya kiasi cha chupa 309376 nchi nzima ikilinganishwa na chupa 257557 zilizokusanywa mwaka 2017/2018.

  Hata hivyo Dkt. Lyimo alisema kuwa wameweza kukusanya chupa 309,376 sawa na,asilimia sitini ya mahitaji ya nchi kulingana na idadi ya wananchi waliopo “tumeweza kufanikiwa kuvuka lengo la kukusanya chupa za damu zaidi na hii ni kutokana na uelewa mkubwa wa wananchi wa kuelewa umuhimu wa kuchangia damu katika kuokoa maisha hususani akina mama wajawazito na wahitaji wengine wa damu”.Alisema.

  Aidha, Dkt. Lyimo alitaja makundi ya wachangia damu kuwa wanawake ni asilimia 14 pekee huku idadi ya wanaume ikiwa ni asilimia 86 hapa nchini.

  Hata hivyo alisema hali ya maambukizi ya magonjwa kwa damu zinazobainika katika ukusanyaji huo ameeleza kuwa ugonjwa wa homa ya Ini ndio inayoongoza kwa asilimia 5.9 ikifuatiwa HIV kwa asilimia 2.8.

  Dkt. Lyimo amewashukuru wananchi wanaoendelea kuchangia damu ikiwemo vijana watumishi wa umma, taasisi na mashirika mbalimbali kwa moyo wa kutekeleza zoezi hilo ili kufikia malengo yanayotarajiwa.

older | 1 | .... | 1871 | 1872 | (Page 1873) | 1874 | 1875 | .... | 1904 | newer