Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1873 | 1874 | (Page 1875) | 1876 | 1877 | .... | 1904 | newer

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bibi Ririko Tanabe kuhusu historia ya kampuni ya Toshiba ya Japan wakati alipotembelea makumbusho ya Sayansi ya kampuni hiyo, Agosti 27, 2019.
   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipata maelezo kutoka kwa  Bibi Ririko Tanabe   kuhusu redio ya kwanza  ilitengenezwa na kampuni ya Toshiba kwenye miaka ya 1930, wakati alipotembelea Makumbusho ya Sayansi ya Kampuni ya Toshiba nchini Japan, Agosti 27, 2019. (
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Bibi Ririko Tanabe   kuhusu redio ya kwanza ya kucheza santuri iliyotengenezwa na kampuni ya Toshiba kwenye miaka ya 1930, wakati alipotembelea Makumbusho ya Sayansi ya kampuni ya Toshiba nchini Japan, Agosti 27, 2019.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Makumbusho ya Sayansi ya Kampuni ya kampuni ya Toshiba nchini Japan baada ya kutembelea makumbusho hiyo, Agosti 27, 2019. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa kiwanda cha kutengeneza mitambo ya  kuzalisha umeme cha Tsurumi kinachomilikiwa na kampuni ya Toshiba nchini Japan wakati alipotembelea kiwanda hicho, Agosti 27, 2019. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Japan, John Kambona.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme cha Tsurumi kinachomilikiwa na kampuni ya Toshiba nchini Japan baada ya kutembelea kiwanda hicho, Agosti 27, 2019. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chombo muhimu kinachounda  mitambo ya kuzalisha umeme wa maji na gesi (turbine) wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme cha Tsurumi kinachomilikiwa na Kampuni ya  Toshiba nchini Japan, Agosti 27, 2019. Wapili kulia ni Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Shinya Fujitsuka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  WAZIRI MKUU AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA TOSHIBA


  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Toshiba nchini Japani, ambapo amewashawishi waje nchini na wafungue ofisi kubwa na waanzishe viwanda vya bidhaa za elektroniki watakavyoona vinafaa hapa nchini.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Agosti 27, 2019) baada ya kutembelea Makumbusho ya Sayansi ya Kampuni ya Toshiba na kiwanda cha kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme cha Tsurumi kinachomilikiwa na Kampuni hiyo.

  Akizungumza na viongozi wa kampuni ya Toshiba, Waziri Mkuu amewashawishi waje nchini na wafungue viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali za kielektroniki kama vile redio, televisheni, pasi na viwanda vingine watakavyoona wao vinafaa kujengwa nchini.

  Waziri Mkuu amewahakikisha viongozi hao kwamba hawatojuta kuwekeza nchini Tanzania kutokana na sera nzuri na mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara pamoja na soko la uhakika wa bidhaa zitakazozalishwa kwa kuwa Tanzania imezungukwa na nchi nyingi.

  “Wawekezaji wote wanaokuja kuwekeza Tanzania wakiwemo na wa kutoka Japan pamoja na kampuni ya Toshiba, watambue kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imeboresha mazingira ya uwekezaji na kuyafanya yawe rafiki, nina uhakika wawekezaji watakaoamua kuwekeza Tanzania hawatajutia uamuzi wao huo”.

  Waziri Mkuu amesema ujio wa kampuni kubwa kutoka nchini Japan utawapa Watanzania fursa ya kujifunza tekinolojia mpya na namna bora ya uendeshaji wa biahsara unaozingatia viwango vya Kimataifa.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Sayansi ya Toshiba, Takano Lwakiri amemwambia Waziri Mkuu kuwa Kampuni yake iko tayari kupanua ofisi yake ya Tanzania na kufungua biashara, ambapo ameomba yafanyike mazungumzo yatakayotoa dira sahihi ya kufanikisha jambo hilo.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development (TICAD 7) utakaoanza kesho Yokohama, nchini Japan, amesema anaamini kuwa utakuwa na mafanikio makubwa kutokana na ajenda zilizoandaliwa.

  Waziri Mkuu amesema miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na kuhusu namna ya kuunganisha kibiashara shughuli za Serikali na sekta binafsi.

  Amesema kwa kutumia mkutano huo wa TICAD 7 wafanyabiashara wa Tanzania wanayo fursa ya kunufaika kwa kuunganisha nguvu zao na makampuni makubwa ya nchini Japan kama Toshiba ili kupata uzoefu na teknolojia muafaka. 

  Hivyo, Waziri Mkuu amewasihi wafanyabiashara kutoka Tanzania ambao watashiriki mkutano huo wafanye mazungumzo na wenzao wa Japan, wawashawishi ili waweze kushirikiana nao kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali.

  Waziri Mkuu yuko nchini Japan akimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano wa TICAD 7 utakaoanza kesho, ambapo ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Paramagamba Kabudi na viongozi wengene wa Serikali na Taasisi za Umma.


  0 0

  Muonekano wa hatua ya ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50 kwa kiwango cha lami. Ujenzi wa barabara hiyo umefikia zaidi ya asilimia 50 na utagharamu zaidi ya shilingi bilioni 89.
  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, walipokuwa wakikagua moja ya ujenzi wa barabara ya kimkakati ya Mtwara-Mnivata yenye urefu wa KM 50, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo, Mkoani Mtwara.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mjini Dodoma.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani Kakoso, akitoa maelekezo na ushauri kwa Viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Watendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mara baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Wakala huo, mjini Dodoma.
  ……………………………..

  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeupongeza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kwa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madaraja makubwa na barabara ya kuunganisha mkoa kwa mkoa kupitia mtandao wa barabara nchini.

  Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji ya Wakala huo ilyowasilishwa kwa Wajumbe wa Kamati jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Selemani Kakoso, amesema kuwa kupitia utaratibu huo hata barabara zilizosahaulika nchini zinaweza kunufaika kwa kuwa na maendeleo ya kiuchumi kutokana na uwepo wa miradi hiyo.

  “Naipongeza Serikali kupitia TANROADS kwa kufikiria kuunganisha mikoa kupitia barabara hususan katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Kigoma na Kagera. Mikoa hii ilionekana kama imesahaulika lakini sasa inaonekana kupata maendeleo kutokana na uwepo wa miradi ya barabara ambayo inatekelezwa”, amesema Mhe. Kakoso.

  Aidha, Ameutaka Wakala huo kuendelea kuziangalia na kuzipa kipaumbele barabara za kimkakati ambazo zina maslahi mapana katika maendeleo na ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Ametaja miradi hiyo kama barabara ya Mtwara- Mnivata, Katavi- Kigoma na Kasulu – Kagera ambayo kwa pamoja ikikamilika itaunganisha mikoa hiyo na mikoa jirani na hatimaye kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi. 

  Mwenyekiti Kakoso, ameusisitiza Wakala huo kuendelea na uboreshaji wa viwanja vya ndege hususan katika ujenzi wa majengo ya abiria ambayo yanaendana na wingi wa abiria pamoja na kujenga uzio katika viwanja vya ndege ambavyo havina uzio lengo likiwa ni kuweka usalama katika viwanja hivyo.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza ujenzi na ukarabati wa barabara, madaraja na mizani.

  Amefafanua kuwa hadi kufikia Juni, 2019 Wakala umefanikiwa kujenga kituo cha mizani cha Kurasini ambacho kimejengwa kwa ajili ya kuhakiki uzito wa magari yanayotoka bandarini na kuweka CCTV Kamera katika mzani huo.

  Kwandikwa, ameongeza kuwa Wakala umeendelea na kazi za ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya viwanja vya ndege ambapo hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwa baadhi ya miradi zinaridhisha. 

  Amesema kuwa hadi kufikia Juni, 2019 ujenzi wa Jengo la abiria katika Kiwanja cha ndege wa Songwe umefika asilimia 77 na ukarabati na ujenzi wa Jengo la kuongozea ndege na mizigo katika Kiwanja cha Ndege cha Mwanza umefika asilimia 93. 

  “Sisi kama Serikali tutaendelea kuboresha viwanja vingine vya ndege, tunajua wananchi wanahitaji maendeleo kupitia sekta ya anga, hivyo hatuna budi kuboresha viwanja hivi, amesisitiza Kwandikwa.

  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepokea taarifa ya TANROADS ambayo imeainisha majukumu ya Wakala huo kwa mwaka wa Fedha 2018/19 na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi na ukarabati wa barabara kuu, barabara za mikoa, madaraja na viwanja vya ndege.

  0 0

  Mhandisi Akaniwa Msengi (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kuhusu mtambo wa liquid oxygen.
  Mhandisi Msengi akiwaelezea wataalam wa Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar jinsi mtambo wa oxygen mbadala unavyofanya kazi. Ujumbe wa wataalam hao umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kujifunza matumizi ya oxygen kwa wagonjwa.

  Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Timothy Wonanji (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila mara baada ya kutembelea hospitalini hapo.
  Mhandisi wa Hospitali ya Mloganzila, Happymark John (wa kwanza kushoto) akielezea jinsi tanki la kuhifadhi maji linavyofanya kazi.
  ……………………….

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imesema itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila katika kuhakikisha inatatua changamoto zilizopo ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za fya.

  Kauli hiyo nimetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Timothy Wonanji mara baada ya kutembelea Hospitali ya Mloganzila ili kuangalia utoaji wa huduma, miundominu na changamoto zilizopo.

  “Nawapongeza kwa utendaji wenu wa kazi nahidi tutaendelea kushirikiana katika kuhakikisha Hospitali ya Mloganzila inafikia malengo yake na wananchi wanaendelea kupata huduma bora’’amesema Dkt. Wonanji.

  Katika hatua nyingine, Ujumbe wa wataalam kutoka Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kujifunza matumizi ya oxygen kwa wagonjwa.

  Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar, Haji Nyonje Tandu amesema ujumbe huo umehusisha viongozi wa ngazi mbalimbali kwa lengo kujifunza jinsi oxygen inavyopatikana, matumizi yake kwa wagonjwa na kuona namna mitambo inavyozalisha na kusambaza.

  “Tumekuja kujifunza kwenu ili tuendelee kuboresha utoaji huduma za afya kwa wananchi kwani hospitali yetu ina matumizi makubwa ya oxygen ikiwa ni wastani wa mitungi 45 kwa siku, hivyo inatupasa kuendelea kujifunza zaidi’’amesema Bw. Haji Nyonje Tandu.

  0 0

   
   Tigo Tanzania ni kampuni inayoongoza katika kubuni, na kuleta huduma na bidhaa bora zinakata kiu ya watanzania, sasa kutana na Innocent Rwetabura mtanzania wa kwanza kuwa Afisa Mkuu wa Fedha


  Historia ya bwana Rwetabura inajieleza yenyewe. Alijiunga na kampuni ya Tigo akiwa na uzoefu mkubwa unaotokana na kutumikia katika nyadhifa mbalimbali za juu katika makampuni mengine katika sekta ya mawasiliano.

  Kwa mujibu wa maelezo yake, uhasibu upo katika damu yake. Ndio ni ukweli kwamba uhasibu unaambatana na donge nono, lakini hamasa yake haitokani na malipo au mafao yatokanayo na taaluma hiyo, bali hamasa na msukumo wa kuwa mhasibu mahiri unatokana na ukweli kwamba kazi hii inasisimua kitaaluma.

  Safari yake katika sekta ya uhasibu na fedha ilianza pale alipochukuliwa kwenda kufanya kazi mara baada ya kuhitimu kutoka katika chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1998.

  Kwa mara ya kwanza kabisa aliingia katika sekta ya ajira kama mhasibu msaidizi wa benki, Citibank. Akiwa na miezi michache tu tangu kuajiriwa, Price water house Coopers (PwC) walimpigia simu ya kutaka kufanya naye kazi na akachukua fursa hiyo. “Japokuwa mazingira na mafao yalikuwa mazuri sana pale Citibank lakini matarajio aliyokuwa nayo kwa kufanyakazi PwC yalikuwa bora zaidi. Nilihitaji kuwa pale ambapo utendaji upo. PwC ilikuwa ni njia yangu ya kuelekea kuwa mhasibu mahiri katika mazingira ambayo yanatoa kiwango cha juu cha utaalamu wa uhasibu,” alisema bwana Rwetabura.

  Ni wazi kabisa kwamba bwana Rwetabura ni mtu mwenye malengo makubwa. Ametumikia makampuni mbalimbali akiwa katika nyadhifa mbalimbali kwa miaka mingi. Amefanya kazi na PwC kwa takribani miaka miwili. Baada ya hapo alihamia katika kampuni ya Celtel (ambayo kwa sasa ni Airtel) kama Meneja wa Fedha akitokea kuwa Mkaguzi wa Mahesabu. Alipoanza kazi kama Meneja wa Fedha, kampuni ya Celtel ilikuwa ni ndogo. Kadri ambavyo kampuni hiyo ilivyokuwa inakua, nafasi yake ilipandishwa hadi kufikia kuwa Mdhibiti wa Fedha.

  Baada ya mwaka mmoja na nusu, alihamishiwa nchini Sierra Leone akitumikia kampuni hiyo hiyo na katika wadhifa huo huo wa Mdhibiti wa Fedha. Alifanikiwa kupanda vyeo mbalimbali na kufikia ngazi ya Mdhibiti wa Fedha baada ya mwaka mmoja.

  Mafanikio yake haya hajayapata pasipokuwa na gharama yoyote. “Sierra Leone ni nchi ambayo ilitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kutokana na mtazamo mbaya uliokuwa unasambazwa wakati huo katika vyombo vya habari wakati huo, ilikuwa ni changamoto kwa mke wangu na familia kufwatana na mimi japo kuwa alikuwa akinitembelea mara kwa mara,” Alisema bwana Rwetabura.

  Baada ya miaka mitatu, mwaka 2010, bwana Rwetabura aliona kwamba ni wakati mwafaka wa kurudi Tanzania.

  Alipowasili, alijiunga na kampuni ya Zantel kama Mkurugenzi wa Fedha. Alishikilia wadhifa huu kwa karibia miaka miwili kabla ya kuhamia katika kampuni ya ulinzi ya G4S. Sababu zilizopelekea kuhama ni kwamba aliahidiwa kuchukua nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji, nafasi ambayo hakupewa.


  Baada ya hapo aliachana na kampuni ya ulinzi na kujiunga na kampuni ya Helios Towers japo katika ngazi za chini. Baada ya muda, kampuni hiyo iliamua kuunganisha vitengo vya idara ya fedha na hivyo nafasi yake iliondolewa.


  Bwana Rwetabura alipewa muda wa miezi sita kuweka sawa mambo yake. Wakati bado anapangilia hatua inayofwata, kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania ilimpigia simu na ilipofika mwaka 2015 safari yake yenye mafanikio na kampuni ya simu ya Tigo Tanzania ilianza rasmi.


  Maisha yake katika kampuni ya Tigo


  Awali kabisa bwana Rwetabura alishikilia wadhifa wa Mdhibiti wa Fedha katika kampuni ya Tigo. Mwenendo wake binafsi pamoja na taaluma yake ulichangia kwa kiasi kikubwa katika kumteua bwana Rwetabura kushika nafasi ya Afisa Mkuu wa Fedha (CFO). Amekuwa na mafanikio makubwa tangu alipojiunga na kampuni ya Tigo ikiwemo kuongeza ufanisi kwenye matumizi (Operating Expenditure (OPEX) kwa kiwango ambacho kilikuza faida ya kampuni. Timu anayoiongoza ya idara ya Fedha, iliunganisha kwa wakati mifumo ya Tigo na mfumo wa serikali wa ukusanyaji mapato (ERCS), hatua ambayo imesaidia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi na ushuru wa bidhaa kielektroniki.

  “Kazi kubwa ya CFO ni kulinda na kusimamia rasilimali za wanahisa na kuhakikisha maslahi yao yanalindwa na kufwatwa. Jukumu hili linajumuisha kiwango kikubwa cha uwekaji wa mikakati, utekelezaji, usimamizi na uendeshaji wa shughuli zote za kifedha za kampuni ikiwepo kuandaa bajeti na kusimamia utekelezaji wake,” alisema bwana Rwetabura

  “Wakati mwingine CFO anajiona kama mpinzani wa Mkurugenzi Mtendaji na wakati huo huo, mshirika muhimu. CEO na timu yake ya biashara wanaweza kuja na wazo, Ili wazo hilo litekelezwa CFO anakiwa kukubaliana nalo au kuja na wazo mbadala ambalo ni bora zaidi. Kwa muda mrefu CFO wameokuwa wakionekana kama wapinzani. Lakini kwa sasa CFO wameanza kubadilika na kushirikiana na mfumo mzima kwa lengo la kuleta matokeo chanya kwa manufaa ya kampuni na wanahisa,” Aliongeza.

  Ni dhahiri kuwa, mazingira ya usimamizi wa fedha yanabadilika sana na ni muhimu kukidhi viwango vilivyowekwa duniani. Matumizi ya teknolojia za kisasa ni muhimu katika kuongeza ufanisi na kubaini viashiria vya hatari kwa wakati.

  “Tunapaswa kuendana na kasi hii ya mabadiliko kama tunataka kusonga mbele. Kwa mfano, taarifa zetu za fedha zinapaswa kukidhi viwango vya utoaji wa taarifa za kifedha vya kimataifa. (International Reporting Standards)Kwa hiyo, kuwa na timu yenye weledi sio tu katika idara ya fedha lakini pia katika kampuni nzima ni jambo la muhimu.” alisema

  0 0
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo katika Mkutano wake na Wasanii wa Sanaa mbalimbali kujadili mabadiliko ya Tasnia hiyo nchini, mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wanachama wa Chama wa Washereheshaji (SAA) wakifuatilia Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, kuhusu mabadiliko mbalimbali Tasnia hiyo nchini, ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
  Msanii wa Bongo Movie Nchini, Muhogo Mchungu akifuatilia, Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, kuhusu mabadiliko mbalimbali Tasnia hiyo nchini, ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa Bongo Movie Nchini, Simoni Mwapagata akifuatilia, Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, kuhusu mabadiliko mbalimbali Tasnia hiyo nchini, ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Wasanii wa Bongo Movie, Shemsa Ford (kulia) na Jackline Wolper (kushoto) wakiteta jambo kabla ya Mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, na Wasanii wa Sanaa zote nchini kuanza katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, akiandika mapendekezo anayoyasikia kuhusu mabadiliko ya Taasisi za Sanaa nchini katika Mkutano wake na Wasanii wa Sanaa mbalimbali kujadili mabadiliko ya Tasnia hiyo nchini, mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

  (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

  …………..

  Na Dianarose Shirima-MAELEZO

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amekutana na wadau wa Sanaa mbalimbali nchini katika kujadili maendeleo ya tasnia hiyo, zikiwepo haki za wasanii na jinsi ya kuboresha tasnia ya Sanaa na muziki ili wasanii waweze kufaidika kwa kile wanachokifanya

  Akizungumza katika Mkutano huo Waziri Mwakyembe amesema kuwa Serikali ipo tayari kupokea mapendekezo ya wasanii kuhusu kuunganisha nguvu katika vyombo vya wasanii ambavyo ni COSOTA, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) NA Bodi ya Filamu Tanzania ili waweze kuhudumia wasanii kwa maendeleo ya kazi zao.

  “Sisi tunawaletea mawazo tu, si Sheria, si Mswada ni mawazo ambayo yatamilikiwa na ninyi baada ya kuyapitisha”, na ninyi kama wadau wa Sanaa na muziki waliohudhuria kwenye mkutano huu mnatakia kutoa mawazo yenu ili Tasnia hii iweze kufikia katika muafaka mzuri ambao utaboresha kazi za wasanii na kutetea maslahi ya kazi zao, Alisema Dkt.Mwakyembe.

  Dkt. Mwakyembe alisema kuwa Tasnia ya Sanaa na Mziki imekuwepo muda mrefu na imekuwa kimbilio kwa vijana wengi, lakini imekuwa ikitajirisha baadhi ya watu na wengine kuachwa nyuma kimaendeleo, kwa hiyo mabadiliko katika Tasnia hiyo hayana budi kutokea ili kuleta ufanisi zaidi

  Aliongeza kuwa mabadiliko hayo hayalengi kuvunja au kuingilia Mamlaka ya vyombo hivyo, bali lengo lake ni kusogeza huduma karibu kwa ajili ya kurahisisha kazi kwa wasanii na wadau wote wa Sanaa nchini.

  Aidha Dkt.Mwakyembe alisema kuwa mabadiliko hayo yatafanya vyombo hivyo kuwa na lugha moja ili kuepuka wasanii kukamatwa au kufungiwa pale wanapokuwa wanafanya kazi zao kutokana na utofauti wa kanuni na Sheria zilizopo.

  “Kipindi cha mabadiliko kimefika, watanzania tusiogope kufikiri katika tasnia hii, kwa muda mrefu imekuwa ikisaidia sana lakini haiwezi kuwafaidisha wachache na wengine wabaki masikini, haiwezekani ni lazima tufikirie njia itakayo tusaidia wote”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Tanzania, William Frank Chitanda, alisema kuwa Mabadiliko ya kuiunganisha Basata na Bodi ya Filamu ziungane na COSOTA ihamishiwe Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Utafiti kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
  (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akiwaeleza wafanyakazi wa Taasisi hiyo (hawapo
  pichani) kuhusu tafiti saba za magonjwa ya moyo zilizofanywa na Taasisi
  hiyo ambazo zitawasilishwa katika mkutano wa kimataifa wa magonjwa
  yasiyo ya kuambukiza utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia.
  Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Happiness Swai
  akiwaeleza wafanyakazi wa Taasisi hiyo (hawapo pichani) kuhusu utafiti wa
  shinikizo la damu na tatizo la kisukari uliofanywa na Taasisi hiyo ambao ni
  moja ya tafiti saba za magonjwa ya moyo ambazo zitawasilishwa katika
  mkutano wa kimataifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza utakaofanyika
  wiki ijayo nchini Zambia.
  Wataalamu wa Afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
  ambao walifanya tafiti saba za magonjwa ya moyo ambazo zitawasilishwa
  katika mkutano wa kimataifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza
  utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia wakiwa katika picha ya pamoja mara
  baada ya kuzielezea tafiti hizo kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo leo jijini Dar
  es Salaam.Picha na JKCI

  *****************

  Na Ales Mbilinyi – JKCI

  28/08/2019 Tafiti saba za magonjwa ya moyo zilizofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zinatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa wanasayansi, madaktari bingwa na wahudumu wa afya wanaotoka katika nchi za ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia.

  Tafiti hizo ambazo zimefanyika mwaka jana na mwaka huu ni kuhusu mwenendo wa mapigo ya moyo kwa mgonjwa, wagonjwa wenye moyo ambao uwezo wake wa kufanya kazi umepungua jinsi wanavyozingatia matibabu kama walivyoshauriwa na madaktari, shinikizo la damu na tatizo la kisukari.

  Tafiti nyingine zitakazowasilishwa ni upungufu wa nguvu za kiume katika jamii, uelewa wa sababu hatarishi za magonjwa ya moyo katika jamii, magonjwa matatu kwa pamoja yaani moyo na figo kushindwa kufanya kazi na upungufu wa damu mwilini.

  Akizungumza kuhusu tafiti hizo Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo alisema tafiti hizo zimefanyika katika mkoa wa Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka miwili na na kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

  “Tumekuwa tukifanya tafiti mbalimbali kuhusu magonjwa ya moyo ambazo zinatusaidia kufahamu wagonjwa wetu pamoja na wananchi wanaotuzunguka wanakabiliwa na matatizo gani katika afya za moyo na hii inatusaidia kuweza kuboresha huduma zetu”,.

  Akizungumza kuhusu mkutano huo wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dkt. Pedro alisema kwa upande wa magonjwa ya moyo utawasaidia kubadilishana matokeo ya huduma za matibabu wanazozitoa hasa tafiti zinazofanywa katika nchi mbalimbali ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa wagonjwa.

  Kwa upande wake Afisa uuguzi wa JKCI Jalack Milinga ambaye alishiriki katika kufanya tafiti hizo alisema kwake ni mara ya kwanza kuhudhuria mkutano huo ambao utamsaidia kuongeza ujuzi katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa moyo lakini pia kubadilishana uzoefu na wauguzi wenzake watakaoshiriki katika mkutano huo.

  “Utafiti wangu uliangalia jinsi ya uzingatiaji wa unywaji wa dawa za moyo kwa wagonjwa ambao mioyo yao haifanyi kazi vizuri. Hivyo naamini ushiriki wangu katika mkutano huu utaniwezesha kupata mbinu mpya za kusimamia jukumu la kuwasaidia wagonjwa wetu kuzingatia matibabu ili kupata matokeo bora ya tiba”, alisema Jalack.

  Naye daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa JKCI Smita Bhalia alisema ushiriki wa wataalamu kutoka Tanzania umelenga kutoa matokeo ya utafiti uliofanywa hapa nchini na kuonesha baadhi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza jinsi yanavyoweza kusababisha magonjwa ya moyo ama magonjwa ya moyo yanavyoweza kupelekea mtu kupata magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza.

  Malengo ya mkutano huo ni kwa nchi washiriki kutoka ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika kuona jinsi ya kushirikiana katika kufanya tafiti za ndani, kuwa na njia bora na za kisasa za matibabu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuwa na mbinu mpya za kuweza kuzia magonjwa hayo.

  Mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka unatarajia kufayika mjini Living stone nchini Zambia kuanzia tarehe tano hadi saba mwezi ujao ambapo mwaka jana mkutano kama huo ulifanyika jijini Nairobi nchini Kenya.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo kushoto akipeana mkono wa pongezi na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo mara baada ya halfa ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho amabcho kimejengwa katika kijiji cha Mgenge kata ya Beta Wilayani Mkuranga,(PICHA NA VICTOR MASANGU).
  Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kushoto Ramadhani Maneno akimshika mkono Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ikiwa ni moja ya ishara ya kumpongeza katika juhudi zake za kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa viwanda(PICHA NA VICTOR MASANGU).
  Mmoja wa viongozi wa kiwanda hicho cha kuchakata zao la muhogo kulia Leonard Jambeli akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho pembeni yake kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho(PICHA NA VITCOR MASANGU
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani kushoto Mhandisi Evarist Ndikilo akipata maelekezo kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha kuchakata muhogo wakati alipofanya ziaara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho,(PICHA NA VICTOR MASANGU).

  *****************

  VICTOR MASANGU, MKURANGA

  KILIO cha muda mrefu ambao kilkuwa kinawakabili wakulima wa zao la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani hatimaye hivi karibuni wanatarajia kuondokana na changamoto sugu ya upatikanaji wa soko la uhakika kufuatia kuanza kwa ujenzi wa mradi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata zao hilo ambacho kitagharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.5

  Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakulima hao wakati wa Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa halfa ya uwekeaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho ambacho kimejengwa na mwekezaji kutoka nchini China katika kijiji cha Mkenge kata ya Beta Wilayani Mkuranga ambapo wamedai hapo awali walikuwa na tatizo la kuuza mihogo yao kwa bei ya hasara.

  “Sisi kama wakulima wa zao hili la muhogo katika Wilayah ii ya mkuranga tumefarijika sana kwa ujio wa mradi w akiwanda hiki ambacho kimejengwa na marafiki zetu wa kutoka nchini chini, na tunashukuru kwa jitihada ambazo zinafanywa na Mkuu wetu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Rais wetu Dk. John Pombe Magfuli kwa kuwaleta wawekezaji hawa ambao watatusaidia kuondokana na tatizo la kupata soko la uhakika,”walisema wakulima hao.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka maafisa kilimo wote kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwasimamia vema wakulima wa zao hilo la muhogo kutonyonywa na walanguzi na kupata haki zao stahiki na kuahidi kuwaondoa kazini wale wote ambao watabainika kukwamisha juhudi za serikali katika uwekezaji sekta ya viwanda.

  Aidha Ndikilo alisema kuwa lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawasaidia kwa hali na mali wananchi wake katika kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili ikiwemo ukosefu wa masoko ya ukakiha, ajaira hivyo aatahakikisha zao hilo la muhogo linapata soko kupitia viwanda ambavyo vinajengwa na waekezaji katika maeneo mbali mbali na kuwahimiza wasikate tama na badala yake waendelee zaidi kulima mazao ya biashar ikiwemo ufuta,muhogo na korosho.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amesema kuwa kipindi cha nyuma wakulima wengine walikuwa tayari wameshakata tamaa katika kilimo cha zao la muhogo,hivyo kumamilika kwa kiwanda hicho kitaweza kuleta mabadili chanya kwa kuwapa fursa wananchi kuwa na soko la uhakika .

  “Kwa kweli wananchi wangu hasa kwa wakulima wa zao hili la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga baadhi yao walikuwa tayari wameanza kukata tama kabisa na kujikitza zaidi na kilimo cha zo la muhogo nah ii hali ni kutokana na mfumo ambao ulikuwepo wanauza mazao yao kwa bei ya hasara kweli lakini kwa sasa kiwanda hiki kinakamilika mwaka huu hivyo wataondokana kabisa na changamoto ya soko,”alismema Sanga.

  Awali akisoma Risala ya ujenzi wa mradi huo mmoja wa vongozi wa kiwanda Leonard Jambeli kwa niaba ya Mkurugenzi amebainisha kwamba waanategemea kutoa fursa za ajira za moja kwa moja kwa wazawa zaidi ya mia moja pindi uzalishaji utakapoanza kufanyika rasmi.

  KUKAMILIKA kwa mradi huo wa ujenzi wa kiwanda mwishoni mwa mwaka huu kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakulima wa zao hilo katika halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ambao kwa miaka mingi walikuwa wanapata hasara kutokana na kunyonywa na walanguzi kununua zao hilo kwa bei ndogo.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar kabla ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. Wote wawili wako Japan kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development -TICAD 7

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar kwenye ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. Wate wawili wanahudhuria Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa – TICAD 7.


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar kwenye ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. Wate wawili wanahudhuria Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa – TICAD 7. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakati alipotembelea banda la maonyesho la Tanzania kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019.


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na maofisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakati alipotembelea banda la maonyesho la Tanzania kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  …………………..

  WAZIRI MKUU AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA MAURITIUS


  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Mauritius waje washirikiane na Watanzania katika uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo ya utalii, viwanda vya sukari, nguo na bidhaa za uvuvi. 

  Ametoa kauli hiyo leo, (Jumatano, Agosti 28, 2019) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar katika Ukumbi wa Monyesho wa Pasfico Yokohama nchini Japan.

  Waziri Mkuu amesema nchi ya Mauritius ina uwezo mkubwa sana katika uzalishaji wa sukari na wanayo nafasi kubwa ya kushirikiana na Watanzania katika kilimo cha miwa na ujenzi wa viwanda vya sukari na Tanzania ina ardhi nzuri na kubwa inayofaa kwa kilimo hicho pamoja na soko kubwa ndani na nje ya nchi.

  Amesema uwekezaji katika sekta ya sukari utasaidia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli za kuhakikisha inamaliza tatizo la upungufu wa sukari nchini.

  Akizungumzia kuhusu sekta ya utalii, Waziri Mkuu amesema Mauritius imefanya vizuri sana katika utalii na hasa ule wa kutumia fukwe za bahari. “Kwa vile Tanzania inazo fukwe za bahari na maziwa naamini ushirkiano katika eneo hilo utatuletea tija.”

  Kuhusu usafiri wa anga, Waziri Mkuu amesema kuwa wakati umefika sasa kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuanza safari za kwenda Mauritius ili kuvutia watalii wengi wanaokwenda Mauritius kufanya utalii wa fukweni waje pia nchini.

  Kuhusu viwanda vya nguo, Waziri Mkuu amewahamasisha wafanyabiashara wa Mauritius kuwekeza nchini hasa katika viwanda vya nyuzi za pamba na nguo kwani Tanzania hivi sasa inazalisha pamba nyingi na yenye ubora wa juu. 

  “Watanzania wengi wameishia kuwekeza kwenye viwanda vya kuchambua pamba hivyo wanalazimika kuuza pamba yao nje ya nchi na wenzetu Mauritius wameenda mbali zaidi kwani wana viwanda vya nguo na viwanda vya nyuzi. Kwa sasa Serikali ya Tanzania imeweka mkakati wa kujenda viwanda vya nguo ili kuongeza tija.”

  Amesema kwa sasa wamekuabaliana na Waziri wa Mkuu huyo wa Mauritius kuwakutanisha Mawaziri wa viwanda na Biashara wa Mauritius na Tanzania wakae pamoja kwa ajili ya kufanya mazungumzo yenye lengo la kuwashawishi wafanyabiashara wa Mauritius waje wawekeze katika viwanda vya nguo na nyuzi nchini.

  Kadhalika,Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu sekta ya Uvuvi, ambapo amesema Tanzania ina eneo kubwa la bahari na maziwa linalofaa kwa uvuvi wa kibiahara na lina samaki wengi lakini wanavuliwa kwa kiwango kidogo sana kutokana na uwekezaji duni katika sekta hiyo.

  Amesema ingawa Serikali ya Awamu ya Tano inaandaa mazingira ya kufufa kampuni za uvuvi nchini, bado nafasi ipo kwa wawekezaji kutoka nje ya nchi hasa nchini Mauritius kuja Tanzania kuwekeza kwenye uvuvi.

  Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa nchi yake iko tayari kufanya mazungumzo na Wizara na Taasisi zinazohusika na masuala ya uwekezaji nchini ili kupata taarifa za kutosha zitakazomwezesha kuwashawishi wafanyabiashara wa nchi yake waje wawekeze nchini.

  Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Paramagamba Kabudi na viongozi kutoka Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua katika kata ya Masengwa na Samuye zilizopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwaonya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikwamisha wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.Mboneko amefanya ziara hiyo leo Agosti 28, 2019 kwa akianzia wenye Kata ya Masengwa ambapo mkutano wake wa hadhara ameufanyia kwenye kijiji cha Bubale, huku kata ya Samuye akifanyia kwenye kijiji cha Ibingo. 
   
  Akizungumza kwenye mikutano hiyo, Mboneko aliwataka wananchi washiriki na kuchangia shughuli za maendeleo, na kuwapuuza watu ambao hupinga maendeleo. Alisema Serikali itaendelea kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo zinawakabili likiwamo suala la maji, huduma za afya, umeme, kilimo, miundombinu ya barabara pamoja na elimu. “Licha ya serikali kuendelea kutatua kero mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi, pia tunawaomba na nyie wananchi muwe mnashiriki kuchangia shughuli za maendeleo ili kuunga juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo, na muwapuuze wale ambao hupenda kupinga maendeleo,”alisema Mboneko. 
   
  “Naomba pia viongozi wa maeneo haya husika, pamoja na Diwani mtusaidie kutuletea majina ya watu ambao hupenda kupinga maendeleo na kukwamisha wananchi wasishiriki kuchangia shughuli za maendeleo ili tushughulike nao,” aliongeza. Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao utafanyika Novemba 24 mwaka huu,Mboneko aliwataka wananchi wasichague viongozi wasiopenda maendeleo, bali wachague wale ambao ni wapigania maslahi ya wananchi ili wapate kutatuliwa matatizo yao.
   
   Katika hatua nyingine amewataka maofisa ugani kuwatembelea wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo cha kisasa, ili pale watakapoanza kulima walime kilimo chenye tija, ambacho kitawapatia mavuno mengi na hatimaye kuinuka kiuchumi. Nao baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye mikutano hiyo ya hadhara ya mkuu huyo wa wilaya, wamepongeza kwa kusikilizwa kero zao pamoja na kutatuliwa, yakiwemo masuala ya umeme, maji, barabara, elimu, pamoja na kilimo hasa kwenye ununuzi wa pamba. 
   
  TAZAMA PICHA HAPA CHINI Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi wa kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwataka washiriki kuchangia kwenye shughuli za maendeleo, licha ya serikali kuwatatulia matatizo yao ambapo nao wanatakiwa waunge juhudi hizo za serikali. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akionya watu ambao wamekuwa wakipinga maendeleo pamoja na kuwashawishi wananchi wasishiriki kuchangia shughuli hizo za maendeleo kuwa serikali itawachukulia hatua kali. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akiwataka wananchi kuendelea kuiamini serikali yao ambayo ni sikivu ambapo itaendelea kutatua changamoto zao zote ambazo zinawakabili. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko akizungumza pia na wananchi wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwataka washiriki kuchangia kwenye shughuli za maendeleo, licha ya Serikali kuwatatulia kero hivyo nao wanatakiwa waunge juhudi hizo za Serikali. Diwani wa Kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simoni, akiwahakikishia wapiga kura wake kuwa changamoto zao zote zitatatuliwa ikiwa serikali ya awamu ya awamu ya Tano ipo kwa ajili ya wananchi. Diwani wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga John Ngegeshi akiomba serikali kuongeza msukumo wa ukamilishaji wa mradi wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria pamoja na kasi ya usambazaji wa umeme wa REA. Mtendaji wa Kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Husein Majaliwa akisoma taarifa ya kata hiyo na kueleza changamoto ambazo zinawakabili wananchi, ikiwemo uhakika wa masoko ya mazao yao ambayo hulima likiwemo zao la pamba.
   
    Mtendaji wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Damiani Ndassa, akisoma taarifa ya kata hiyo na kuelezea changamoto ambayo ipo ni wananchi kugoma kuchangia shughuli za maendeleo mara baada ya serikali ya Kijiji cha Ibingo kufanya ufujaji wa fedha. Awali Mwananchi Jumanne Makanga mkazi wa kata ya Masengwa akiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.  
   
  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bubale kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Eliakimu Methew akiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. Mwananchi Ndeshema Nshimbi mkazi wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
   
  Kaimu Meneja wakala wa maji mijini na vijijini (RUWASA) Emaeli Nkopi, akijibu maswali ya ukamilishwaji wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya Jasinta Mboneko wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwenye Kata ya Masengwa na Samuye. Msimamizi wa umeme wa REA Hally Twaha akimwakilisha Meneja wa Tanesco mkoa wa Shinyanga, akijibu maswali ya umeme kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.  
   
  Meneja wa TARURA halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Eng. Salvatory Yambi, akijibu maswali ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. DR Joseph Ngowi akimwakilisha Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Amosi Mwenda, akijibu maswali ya sekta ya afya yaliyoulizwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi Afisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akijibu maswali ya Pamba yaliyoulizwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwenye Kata zote za Masengwa na Samuye. Wananchi wa Kata ya Masengwa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Masengwa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Masengwa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

  0 0


  MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akipokea mabati 160 kutoka kwa Bw. Bill Ndilla Mkurugenzi wa Makampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD kama msaada wake katika ujenzi wa madarasa 4 katika shule ya Msingi Mbezi Ndumbwi Kata ya Bezi Juu wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
  MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akikabidhi mabati 160 kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule Judith Senkoro Kilimo baada ya kupokea mabati hayo kutoka kwa Bw. Bill Ndilla Mkurugenzi wa Makampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD kama msaada wake katika ujenzi wa madarasa 4 katika shule ya Msingi Mbezi Ndumbwi Kata ya Bezi Juu wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
  MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akiwasili katika shule ya msingi Mbezi Ndumbwi kata ya Mbezi juu kwa ajili ya kupokea vifaa vya ujenzi kutoka kwa wadau wa maendeleo Makampuni ya kampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD.
  Baadhi ya maofiza walioongozana na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo katika shule hiyo.
  Bw. Bill Ndilla Mkurugenzi wa Makampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTDakizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 4 kwenye shule ya Mbezi Ndumbwi jijini Dar es salaam.
  MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya ujenzi katika shule ya msingi Mbezi Ndumbwi kata ya Mbezi vilivyotolewa na wadau wa maendeleo Makampuni ya kampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD.

  Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika hafla ya makabidhiano shuleni hapo.
  Kwaya ya wanafunzi wa shule ya msingi Mbezi Ndumbwi wakiimba mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo.
  Baadhi ya watendaji wa kata madiwani na walimu wa shule ya msingi Mbezi Ndumbwi wakiwa katika hafla hiyo.
  MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akitoa maagizo kwa watendaji alipokagua ujenzi wa maradasa wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya ujenzi katika shule ya msingi Mbezi Ndumbwi kata ya Mbezi Juu vilivyotolewa na wadau wa maendeleo Makampuni ya kampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD.
  Afisa Elimu Wilaya ya Kinondoni Bw. Kiduma Mgeni akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo wakati alipokagua ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mbezi Ndumbwi kata ya Mbezi Juu wilaya ya Kiondoni jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Judith Kilimo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbezi Ndumbwi wakati alipkagua ujenzi wa madarasa shuleni hapo.
  MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akifuatana na Bw. Bill Ndilla Mkurugenzi wa Makampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD kabla ya kupokea msaada wa mabati 160 kutoka kwa mkurugenzi huyo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 4 katika shule ya Msingi Mbezi Ndumbwi Kata ya Bezi Juu wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo.

  0 0

   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, alipowasili kuhutubia Mkutano wa sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali Olusegun baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wastaafu katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Taasisi ya Uongozi baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Somalia Mhe. Hassan Mohamed alipowasili kuhutubia Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019. Wanaofuatia kulia kwake ni Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali Olusegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mhe. Thabo Mbeki na Mfanyabiashara mashuhuri wa Tanzania Bw. Ally Mufuruki

   
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na viongozi wastaafu kukiliza majadiliano wakati wa Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikaribisha chakula cha mchana na viongozi wastaafu na na wageni wengine wakati wa mapumziko ya mchana katika Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019 PICHA NA IKULU

  0 0

  Mhe. Prof. Kabudi akimwonesha Mhe. Uchiya jarida linaloonesha vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini 
  Mhe. Prof. Kabudi akiagana na Mhe. Shigeharu Uchiya mara baada ya kumaliza mazungumzo kati yao 
  Mhe. Prof. Kabudi akisalimiana na mmoja wa raia wa Japan aliyewahi kufanya kazi za kujitoleak kwenye sekta ya afya nchini Tanzania miaka ya 1960.


   


  Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Meya wa Jiji la Nagai nchini Japan 

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ameishukuru Serikali ya Japan kwa kuishirikisha Tanzania kikamilifu kwenye maandalizi ya Michezo ya Olympic inayotarajiwa kufanyika jijini Tokyo mwaka 2020 ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wanamichezo wanawake kutoka Tanzania.

  Mhe.Prof. Kabudi ametoa shukrani hizo wakati wa mkutano wake na Meya wa Jiji la Nagai, Mhe. Shigeharu Uchiya uliofanyika leo tarehe 29 Agosti 2019 jijini Yokohama pembezoni mwa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Ushirikiano na Afrika (TICAD 7).

  Mhe. Prof. Kabudi alisema kuwa, anaishukuru Japan kwa kuwa imeonesha nia ya dhati ya kuifanya Tanzania ishiriki kwenye Michezo hiyo muhimu ya Olympic ambayo itafanyika nchini humo mwaka 2020 na kuzishirikisha nchi zote duniani. Mhe. Waziri alifafanua kuwa tayari Serikali hiyo imesaini Hati ya Makubaliano na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwezi Julai 2019 kuhusu ushiriki wa Tanzania kwenye michezo hiyo pamoja na kufanikisha ziara ya Timu ya wanariadha kutoka nchini wakiongozwa na mkimbiaji wa mbio za marathon mstaafu, Bw. Juma Ikangaa iliyofanyika mwezi Oktoba 2018. Pia Japan imeahidi kutoa mafunzo kwa wanamichezo wanawake yatakayotolewa jijini Nagai. 

  “Ushikiano wa kirafiki kati ya Japan na Tanzania ni wa miaka mingi hususan kwenye medani za siasa, uchumi na diplomasia. Umefika wakati sasa nchi hizi mbili zishirikiane katika masuala ya kijamii na utamaduni ili kuwaunganisha mtu mmoja mmoja na kwamba ushirikiano huo ndio muhimu kwa ukuaji wa Taifa lolote” alisema Prof. Kabudi.

  Aidha, alieleza kufurahishwa na ahadi kuwa Japan itatoa mafunzo kwa wanamichezo wanawake ili kuwajengea uwezo kwenye michezo mbalimbali ikiwemo ile ya Olympic itakayofanyika Tokyo mwaka 2020. “Tumepokea kwa furaha taarifa kwamba Nagai itatoa mafunzo kwa wanamichezo wetu wanawake. Hii itawajengea uwezo mkubwa wanamichezo hao wakati wakijiandaa na mashindano ya Olympic” alisisitiza Prof. Kabudi.

  Kadhalika, Mhe. Prof. Kabudi alitumia fursa hiyo kumweleza Mhe. Uchiya kuwa Serikali ya Tanzania imehamishia shughuli zake jijini Dodoma ambako ni Makao Makuu ya nchi na kwamba ipo tayari kuanzisha ushirikiano wa kidada kati ya Jiji la Dodoma na Jiji la Nagai.

  Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Nagai, Mhe. Shigeharu Uchiya alisema kwamba jiji hilo litaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania na tayari limeanzisha program ya kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya michezo ambapo Mtanzania, Bw. Bahati Rogers ni miongoni mwa vijana wanaoshiriki program hiyo jijini humo. Pia alisema kuwa aliongoza ujumbe wa watu ishirini kutembelea Tanzania mwaka 2017 kwa ajili ya kubadilisha uzoefu kuhusu michezo.

  Serikali ya Japan ambayo imeanza maandalizi ya Michezo ya Kimataifa ya Olympic itakayofanyika jijini Tokyo mwaka 2020, imetenga Jiji la Nagai kuwa kituo cha Wanamichezo wote wa Tanzania kitakachotumika kuwaadaa kabla ya kuanza kushiriki michezo hiyo rasmi. Maandalizi hayo ni pamoja na kuwawezesha wanamichezo kuzoea hali ya hewa, tamaduni, chakula na masuala mengine muhimu kuhusu Japan kabla ya ushiriki wao rasmi wa michezo hiyo.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasil
  iano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Yokohama, Japan
  29 Agosti 2019

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akipokea zawadi kutoka kwa  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil Mohamed Ahmed, ambaye yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, ziara ambayo imelenga kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Sudani.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil Mohamed Ahmed, akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambayo imelenga kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Sudani.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil Mohamed Ahmed, wakati akitoa hotuba mbele ya Makamishna na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi hilo (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili ambayo imelenga kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Sudani.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil Mohamed Ahmed, wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishna na Maofisa Wakuu Waandamizi baada ya kumaliza kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo leo Jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi Nchini.

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa akiwa katika mzungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi. Mazungumzo hayo yamefanyika kando na mkutano wa TICAD7 Yokohoma,Japan.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi(hayupo pichani) Yokohama, Japan.
  Mazungumzo kati ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi kuhusu wakimbizi waliopo Tanzania yakiendelea. Yokohama, Japan.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa akiagana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao kuhusu wakimbizi waliopo Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika Yokohama, Japan.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandimara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu mhe. Kassim M. Majaliwa. Yokohama, Japan.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiteta jambo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi mara baada ya kumalizika mazungumzo ya Waziri Mkuu mhe. Kassim M. Majaliwa. Yokohama, Japan.


  SERIKALI ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) katika kutatua changamoto zinazotokana na uwepo wa wakimbizi nchini pamoja na kutafuta suluhu ya kudumu kwenye nchi zao ili wakimbizi hao waweze kurejea makwao kuendelea na shughuli za maendeleo.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo (Ijumaa, Agosti 30, 2019) katika mazungumzo yake na Kamishna Mkuu wa UNHCR, Bw. Filippo Grandikwenye Kituo cha Maonyesho cha Yokohama nchini Japan baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development – TICAD 7).

  Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa UNHCR kuisaidia mikoa inayokaliwa na wakambizi kutokana na kuharibiwa kwa mazingira. “Hata hivyo Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na UNHCR kuimarisha ulinzi wa maeneo ya wakimbizi ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kuishi kwa amani na utulivu.”

  Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Bw. Filippo Grandi amesema amefurahishwa na utayari wa Serikali ya Tanzania katika kupokea wakimbizi na usikivu wa Rais Dkt. John Magufuli katika kushughulikia changamoto za wakimbizi. 

  Waziri Mkuu yupo nchini Japan akimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano wa Kilele wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development – TICAD 7) ambao umehitimishwa leo.

  Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza katika kikao cha Maafisa Uhamiaji Waandamizi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Trita, Mjini Moshi, leo. Lugola aliwataka maafisa hao kufanya kazi kwa weledi kwa kuepuka rushwa na kuwasimamia wageni mbalimbali hasa wawekezaji bila kuwanyanyasa.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akizungumza katika kikao cha Maafisa Uhamiaji Waandamizi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Trita, Mjini Moshi, leo. Dkt Makakala aliwataka maafisa hao wawe waadilifu katika utendaji wao wa kazi. Kikao hicho kilifunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola (kulia), na katika hotuba yake aliwataka maafisa hao kufanya kazi kwa weledi kwa kuepuka rushwa na kuwasimamia wageni mbalimbali hasa wawekezaji bila kuwanyanyasa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza katika kikao cha Maafisa Uhamiaji Waandamizi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Trita, Mjini Moshi, leo. Lugola aliwataka maafisa hao kufanya kazi kwa weledi kwa kuepuka rushwa na kuwasimamia wageni mbalimbali hasa wawekezaji bila kuwanyanyasa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala, walipokuwa katika kikao cha Maafisa Uhamiaji Waandamizi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Trita, Mjini Moshi, leo. Lugola alikifungua kikao hicho na aliwataka maafisa wa Idara ya Uhamiaji nchini, kufanya kazi kwa weledi kwa kuepuka rushwa na kuwasimamia wageni mbalimbali hasa wawekezaji bila kuwanyanyasa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  …………..

  Na Felix Mwagara, Moshi (MOHA).

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka Maafisa Uhamiaji nchini, kuepuka rushwa na kutokuwanyanyasa wageni na hasa wawekezaji nchini.

  Akizungumza katika kikao cha Maafisa Uhamiaji Waandamizi kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Uhamiaji (Trita), Mjini Moshi, leo, Lugola alisema wawekezaji ni watu muhimu katika maendeleo ya nchi, hivyo wanaposumbuliwa kwa kunyanyaswa bila sababu za msingi ni kuvunja misingi ya uadalifu.

  Pia Waziri Lugola aliwataka maafisa hao waache kutoa PI (tangazo la kuondolewa mtu asiye raia nchini) zenye utata kwa maslahi binafsi bila kuzingatia athari ambazo nchi inazipata.

  “Yapo malalamiko kwamba kuna wageni wanaingia nchini na kuwekeza kwa ubia na Watanzania, biashara inapokuwa inaendelea Watanzania huwazunguka wageni na kuwatengeneza mazingira ya kuwafukuza ili wapate fursa ya kumiliki hizo biashara na hapo ndipo Idara ya Uhamiaji hutumika, acheni hayo mambo kwa kuwa yanatuchafua kama taifa letu,” alisema Lugola.

  Aliongeza kuwa, Rais John Magufuli anatafuta wawekezaji kwa nguvu na kuwahakikishia usalama wao na biashara zao lakini baadhi ya watumishi wa umma badala ya kusaidia jitihada hizi wao wanatumika kuwafukuza kwa dhuluma.

  Alisema wageni hao wakishafukuzwa na wanaacha uwekezaji wao nchini ambao wanadhulumiwa huko waliko wanaisema nchi vibaya na kwa uzoefu huo wageni wengine hawawezi kuja nchini.

  “Tujitathimini, tuzingatie sheria, kanuni, taratibu na miongozo yetu kwa kuzingatia maslahi ya taifa, pia nawasihi sana mumsaidie mheshimiwa Rais kutimiza ahadi zake kwa Watanzania ambazo amezitoa kupitia Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na ahadi zake nyingine mbalimbali ambazo amekuwa akiahidi na kuzitekeleza,” alisema Lugola.

  Aidha, Waziri Lugola kabla ya kukifungua kikao hicho kilichojumuisha Maafisa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, alisema kikao hicho kitakuwa chachu ya kudumisha maadili ya kazi, nidhamu, utii, na ushirikiano katika maeneo yao ya kazi ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Idara hiyo ya Upendo, Mshikamano, Uwajibikaji na Kukataa Rushwa.

  “Ni imani yangu kuwa, mtaendelea kutekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma katika utoaji wa huduma bora kwa Wananchi,” alisema Lugola.

  Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, alisema kikao hicho zitatolewa mada mbalimbali zitakazowasilishwa kuhusu rushwa na Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018 ambazo ndio mwongozo wa utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji.

  “Kwa kuwa Idara yetu ya Uhamiaji inatoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo pasipoti, vibali vya ukaazi, pasi pamoja na viza, hivyo kupitia kikao hiki tutazingatia kikamilifu mada hizo kwa kuwa zitatusaidia katika kutoa huduma bora kwa maslahi ya Idara yetu, Wizara na taifa kwa ujumla,” alisema Dkt. Makakala.


  0 0

  Heshima na hadhi ya Tanzania Kimataifa imeendelea kupanda kutokana na nia njema na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo (Agosti 31, 2019) Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali kwa mwezi Agosti 2019.

  Dkt. Abaasi anasema: “kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa Julai 12, 2019 kwa pamoja kati ya Transparency International na Afro-Barometer, Tanzania imeongoza katika nchi 35 kwa kuonesha juhudi za wazi katika kupambana na rushwa”.

  “Mafanikio haya yanatokana na msimamo thabiti wa Mhe. Rais Magufuli na Serikali yake katika kuimarisha taasisi muhimu kama vile TAKUKURU, Kuanzisha Mahakama ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi, mfumo wa udhibiti wa rushwa katika manunuzi kupitia PPRA”, ameongeza Dkt. Abbasi.

  Akitolea mfano, amesema kuwa TAKUKURU imeokoa jumla ya shilingi bilioni 86 zilizotokana na mishahara hewa na ukwepaji kodi.

  Aidha, Dkt Abbasi ameabainisha kuwa jumla ya shilingi bilioni 25.5 zimerejeshwa Serikalini kwa mchanganuo ufuatao; bilioni 14.6 ikiwa ni urejeshwaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu na bilioni 10.9 zilizotokana na thamani ya mali zilizotaifishwa yakiwemo magari, vituo vya mafuta, nyumba nane, magari nane na Bilioni 20 ambazo ni mali zilizozuiwa kesi zikiendelea.

  Amesema kuwa kwa upande wa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imeokoa takribani shilingi bilioni 46.9 zilizokuwa zipotee kutokana na kutofuatwa taratibu za ununuzi, malipo ya zaidi ya mkataba kwa wakandarasi au baadhi kutorudisha fedha walizopewa kama dhamana na uzembe na rushwa.

  Akizungumzia utekelezaji katika sekta ya uchukuzi, Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali imeanza zabuni ya kuagiza vichwa 22 (vitano vya mafuta yaani Diesel Locomotive na 17 vya umeme yaani Electrical Locomotive) na mabehewa ya abiria 60 na 1430 ya mizigo.

  Aidha ameongeza kuwa, Serikali imeanza zabuni ya treni tano (5) zilizokamilika (Electrical Multiple Unit) za abiria zenye mabehewa nane (8) kila moja na vichwa viwili kwa ajili ya uendeshaji wa treni za abiria kwa kipande cha Dar es salaam hadi Morogoro na kisha Dodoma.

  Mbali na hayo, ameeleza kuwa, Serikali imetenga fedha za ndani shilingi Bilioni 71.4 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja jipya la Mto Wami lenye urefu wa Mita 513.5 litakalojumuisha ujenzi wa barabara za KM 4.3 kwa kila upande ambapo kazi ya ujenzi huo imeshaanza.

  Pia, Serikali imesaini mkataba wa shilingi bilioni 699.9 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja refu zaidi Afrika Mashariki na Kati la Kilometa 3.2 kuunganisha mikoa ya Mwanza na Geita kwenye eneo la Kigongo-Busisi katika Ziwa Victoria.

  Katika Sekta ya Afya, Dkt Abbasi amesema kuwa, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa (RHH) na sehemu nyingi ujenzi umekamilika. Mikoa husika ni; Mwanza, Simiyu, Njombe, Songwe, Katavi, Geita na Dar es Salaam (Mwananyamala) na kuna Bilioni 3 imetolewa Kujenga Hospitali ya Kanda ya Wazazi Mbeya na shilingi bilioni 6.32 kujenga Hospitali ya Kanda Mtwara.

  Vilevile, katika kuwekeza katika maisha ya watu ngazi ya Wilaya, Serikali mapema mwaka huu ilitoa shilingi Bilioni 105 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67 ambapo katika miaka zaidi ya 50 ya Uhuru tumekuwa na Hospitali katika Wilaya 77 tu; ndani ya mwaka huu mmoja zinajengwa 67 ambapo ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.

  “Niwathibitishie Watanzania kuwa azma yetu ya kuiendeleza nchi kwa kasi chini ya Jemedari Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kushika kasi na katika hili hakuna mwanadamu wa kutuzuia wala kuturudisha nyuma” Amesisitiza Dkt Abbasi.

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo kwa mmoja wa washiriki
  Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akiwahutubia washiriki wa mafunzo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS yaliyofanyika jijini Arusha
  Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo kwa vitendo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS .


  Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imetoa wito kwa Taasisi nunuzi kuwaruhusu watumishi wa vitengo vya usimamizi wa manunuzi pamoja na mifumo ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kushiriki kwenye mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa njia ya Mtandao ili ziweze kuunganishwa na kufanya manunuzi yake kwa kutumia mfumo huo. 

  Wito huo umetolewa jijini Arusha na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo, alipokuwa akifunga mafunzo ya siku sita kuhusu matumizi ya Mfumo huo unaojulikana kwa jina TANePS (Tanzania National e-Procurement System) kwa maafisa 110 wa vitengo vya usimamizi wa manunuzi na Tehama kutoka Taasisi 44. 

  Mhandisi Kapongo amezisisitiza Taasisi nunuzi kuhakikisha zinaunganishwa na kisha kufanya manunuzi yake kwa kutumia mfumo huo wa TANePS ili kukidhi matakwa ya sheria ya manunuzi ya umma pamoja na uamuzi wa Serikali kutaka taasisi zote za umma kuunganishwa na TANePS ili ziweze kufanya manunuzi yote kupitia mfumo huo kwa lengo la kurahisisha michakato ya manunuzi kufanyika kwa ufanisi na tija zaidi na kuhakikisha upatikanaji wa thamani halisi ya fedha. 

  Amezitaja baadhi ya faida za mfumo wa TANePS unaosimamiwa na PPRA kuwa ni kupunguza gharama na muda kwenye michakato ya manunuzi serikalini pamoja na kuongeza uwazi, ushindani na usawa kwa wazabuni na watoa huduma wanaoshindania zabuni mbalimbali zinazotangazwa na Taasisi za Umma. 

  “TANePS inawezesha mchakato wote wa manunuzi serikalini kufanyika kielektroniki ambapo hakutakuwa na sababu ya wazabuni kutumia muda mwingi kutembelea ofisi za Taasisi za Umma pale wanapotaka kushindania zabuni, pia hawawezi kukutana ana kwa ana na watumishi wa taasisi za umma kwa kuwa kila kitu kinafanyika mtandaoni,”alisema Mhandisi Kapongo. 

  Aidha, Mhandisi Kapongo ametoa wito kwa wafanyabiashara, wazabuni na watoa huduma kuhakikisha wanajisajili kwenye mfumo huo ili waweze kushiriki au kushindania zabuni mbalimbali zinazotangazwa na taasisi za umma. 

  Tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2019, wataalamu kutoka PPRA wamepiga kambi jijini Arusha kwa ajili ya kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya TANePS kwa awamu tofauti, programu inayotarajiwa kuwa endelevu ili kutoa fursa kwa wataalamu wa manunuzi kwenye taasisi zote za umma kupata fursa ya mafunzo hayo. Tangu kuanza kwa programu hii kabambe jumla ya watumishi 204 kutoka taasisi za umma 75 wameshapatiwa mafunzo hayo, ambapo wahusika wanapaswa kutembelea tovuti ya mfumo (www.taneps.go.tz) au tovuti ya PPRA (www.ppra.go.tz) ili kupata zaidi maelezo ya namna kujisajili kushiriki. 

  Mafunzo haya yanagharamiwa na Serikali pamoja na ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali  katika Misa Takatifu Dominika ya 22 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Dkt. Alista Makubi, Septemba 01,2019.  PICHA NA IKULU


  0 0


  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

  “ADHABU mnazopewa shuleni ni adhabu za upendo, zinalenga kuwarekebisha ili akili ziweze kupokea maarifa mnayopewa na walimu na hatimaye muwe raia wema wenye uwezo wa kuztumikia taifa na jamii, tofauti na adhabu mtakazopewa baada ya kumaliza elimu, huko mitaani mtakutana na adhabu za chuki zinazotokana na maarifa kidogo mliyonayo.” Hayo ni maneno yaliyosemwa na Padri Jiso kutoka Mtakatifu Vincent wakati wa mahafali ya saba ya darasa la saba shule ya Carmel Convent iliyoko Vikindu, Wilayani Mkuranga

  Padri Jiso ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo ambayo ni ya saba kufanyika katika shule hiyo, aliwaasa wanafunzi kuendeleza yale mema waliyojifunza katika kipindi cha miama saba waliyokuwa shuleni.

  Alisema binadamu wametunukiwa zawadi kubwa na Mwenyezimungu ya kutumia maarifa na akili katika kuyatawala mazingira, licha ya kwamba sayansi inaonyesha miaka mingi ya nyuma binadamu ambaye yuko katika kundi la wanayama, na kama walivyo wanayama wengine aliishi porini.

  “Lakini kutokana na upendo wa Mungu, alituongezea maarifa na vipaji mbalimbali vilivyotuwezesha kutawala mazingira kwa manufaa yetu na viumbe vingine ndio maana leo hii binadamu licha ya kutokuwa na maguvu kama walivyo wanyama wengine Tembo na Simba tumeweza kujenga majumba kuishi kwenye mazingira mazuri na yakliyo bora, kupata huduma za afya na elimu.” Alifafanua na kuongeza Tembo na mahguvu yake, Simba na magubvu yake wao bado wako pori ni na hawajabadilika kwa miaka yote hiyo.

  Alitoa mfano wa ndege aitwaye Tai (Eagle) ambaye ana nguvu nyingi, kucha kali zenye uwezo wa kuchakura na kupokonya, mdomo wenye chongo kali na anakadiriwa kuishi hadi miaka 50, lakini watafiti wengi wanase kabla ya kufikisha miaka hiyo 50 Tai ama Eagle hufa kabla ya kufikisha umri huo kutokana na viungo vyake vinavyomuwezesha kupata chakula, kutishiwa nguvu hizo, kwani nkucha hupinda na hivyo hushindwa kupokonya na kuchakura vyakula, mdomo nao hupinda na hivyo uwezo wake wa kudonoa nao hupungua na hatimaye hufa kwa sababu hawezi tena kujitafutia chakula.

  “Hii ndiyo tofauti ya wanyama wengine na binadamu kwani sisi tumejengewa maarifa kwa hivyo tunatumia maarifa hayo kutatua kero mbalimbali na hivyo kishi kwa furaha.” Alisema Padri Jiso.

  Kwa kutumia mfano huo Padri Jiso alisema ndio maana watoto hujengewa msingi mzuri wa maarifa kwa kupatiwa elimu ili hatimaye baadaye waweze kutawala mazingira wanayoishi kwa kuwa wananachi wazuri na wenye faida kwa taifa na jamii kwa ujumla.

  Padri huyo aliwaonya wanafunzi hao kuwa lazima watambue, adhabu walizokuwa wanapata wakiwa shuleni ni adhabu za upendo zilizolenga kuwarekebisha ili kujaza maarifa kwenye vichwa vyao kwa faida ya baadaye na kwamba nje ya mazingira ya shule adhabu wataakazopata ni za “chuki” na hazina upendo wowote zaidi ya kuwuadhibi ili kuleta majuto.

  Katika mahafali hayo pamoja na mambo mengine, wanafunzi walikabidhiwa vyeti (Living certificates) na kushuhudia burudani mbalimbali zilizoporomoshwa na wanafunzi wenzao.Mtihani wa taifa wa darasa la saba unatarajiwa kufanyika nchini kote kuanzia Septemba 11, 2019.
  Mlulu Khalfan Said (kulia), akipokea cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (Darasa la VII) kutoka kwa Padri Jiso kutoka Mtakatifu Vincent wakati wa sherehe za Mahafali ya Saba Shule ya Carmel Convent iliyoko Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani Agosti 31, 2019.

older | 1 | .... | 1873 | 1874 | (Page 1875) | 1876 | 1877 | .... | 1904 | newer