Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

4% YA WANANCHI WAAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI

$
0
0
Na WAMJW-DOM

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa miongoni mwa Watanzania wenye umri kati ya miaka 15-49 wameabukizwa Virusi vya Homa ya Ini aina ya B, hii ni kutokana na Takwimu za Ofisi ya Taifa wa Takwimu 206-2017.

Dkt. Alphonce Chandika amesema hayo leo wakati wa Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo, yenye kauli mbiu ya “Wekeza katika mapambano ya Homa ya Ini “ maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma katika Hospitali ya Benjamini Mkapa.

“kati ya wachangiaji damu 307,835 takribani watu 13,613 sawa na asilimia 4.4 walikuwa na maambukizi ya homa ya ini kwa mujibu wa takwimu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS)” alisema Dkt. Alphonce Chandika.

Dkt. Alphonce Chandika aliendelea kusema kuwa Mwaka 2017, kati ya wachangiaji damu 233,953 takribani watu 11,417 sawa na asilimia 4.9 walikuwa na maambukizi, aidha asilimia 0.5 ya wachangiaji damu walikuwa na maambukizi ya homa ya ini aina ya C kwa mwaka 2017 na asilimia 0.3 kwa mwaka 2018.

Aidha, Dkt. Alphonce Chandika alisisitiza juu ya kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi juu ya athari za ugonjwa wa Homa ya Ini katika jamii na kwa nchi kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa Serikali itaokoa kiasi kikubwa cha fedha kama itawekeza nguvu kwenye kinga, ambacho kinachotumika kwenye matibabu dhidi ya ugonjwa huu wa homa ya ini.

Nae, Mkurugenzi msaidizi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba amesema kuwa huduma hii ya chanjo ya homa ya Ini imeanza kutolewa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa za Sokoture Mwanza,Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi Kilimanjaro, Hospitali ya Rufaa ya Geita, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Temeke, Hospitali ya Mwananyamala, Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Hospitali ya Muimbili, Moi, Ocean Road na vituo vyote vya mipakani.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, kushoto ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba, na Kulia ni mwakilishi wa WHO anaitwa Dr. Christine Chakanyuka Musanhu .
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akitembelea moja ya banda la kufanyia uchunguzi wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba. 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akiwajulia hali baadhi ya watu waliojitokeza kufanya uchunguzi homa ya ini, katika maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba. 
Wadau mbali mbali wa Afya wakifuatilia kwa makini taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akiteta jambo na mwakilishi wa WHO Dkt. Christine Chakanyuka Musanhu wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika katika picha ya pamoja na Wadau pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya, wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA YASHIRIKI KONGAMANO LA CORPORATE UNWIND JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akizungumza wakati wa kongamano la Corporate Unwind lililoandaliwa na Smart Codes katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Vodacom Tanzania ni kampuni ya mtandao wa simu inayoongoza Tanzania iliyojikita katika kuisaidia Tanzania kufikia uchumi wa kidigitali kwa kuvumbua mifumo suluhishi ya kidigijitali kwa kutumia teknolojia ya simu. Kongamano hilo lilikutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya biashara na uvumbuzi pamoja na wafanyabiashara, taasisi na makampuni mashuhuri nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akieleza jambo kwa baadhi ya washiriki wa kongamano la Corporate Unwind lililoandaliwa na Smart Codes katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Vodacom Tanzania ni kampuni ya mtandao wa simu inayoongoza Tanzania iliyojikita katika kuisaidia Tanzania kufikia uchumi wa kidigitali kwa kuvumbua mifumo suluhishi ya kidijitali kwa kutumia teknolojia ya simu. Kongamano hilo lilikutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya biashara na uvumbuzi pamoja na wafanyabiashara, taasisi na makampuni mashuhuri nchini Tanzania.

Makonda apiga marufu Wasiooga ,kufua nguo,kunyosha nguo kuja mjini

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, leo Julai 29 amezindua kampeni ya tano ya usafi yenye lengo la kuendeleza kufanya usafi wa jiji Dar es Salaam ikiwa ni hatua za maandalizi ya kupokea ugeni wa viongozi wa Umoja wa Nchi zilizo Kusini Mwa Afrika (SADC).

Akizungumza na waandishi wa Habari Julai 29/2019 katika uzinduzi Kampeni ya Usafi katika Uwanja wa Ndege Terminal I,Makonda amesema lengo kubwa ni kuweka Jiji Safi huku akizitaka Taasisi zote za Serikali kuhakikisha kwamba zinakuwa na watu wao wa usafi katika maeneo yao ya kazi.

Makonda amesema pamoja na kuweka Jiji la Dar es Salaam kuwa safi ni kuonyesha ubora wa wananchi wa jiji hilo na mikoa mingine ifanye hivyo na wakija wajifunze vitu vingine ikiwemo usafi kutokana na kuwepo Marais 16 katika mkutano wa SADC. 

Amesema kuwa Mkoa wa Dar Es Salaam unachangamoto ya usafi hivyo ni vyema wakajenga utamaduni wa kufanya usafi Mara kwa Mara.

Aidha amesema wananchi wote wanaoingia barabarani kutumia Kanuni za Mazingira katika kuweka Jiji safi, amezitahadharisha kampuni za uzoaji taka kwamba zitapoteza tenda zao endapo watakuwa wakichota mchanga na kuweka katikati ya barabara. 

"Nataka kuwaambia tu kwamba nimemsikia Mratibu wa kila Taasisi ya Serikali katika mkoa wangu iwe na watu wa usafi" Amesema RC Makonda.Amesema ugeni wa SADC ni heshima kwa Rais Dkt John Magufuli na Mkoa wa Dar Es Salaam kwa ujumla hivyo lazima Jiji liwe safi wakati wa kuwapokea wageni pia usafi huo uwe endelevu.

Katika hotuba yake Makonda amewataka wakazi wa Dar Es Salaam, kuzingatia usafi na kupiga marufuku mtu yoyote kufika mjini kama hajafanya usafi wa mwili wake ikiwemo kuoga, kufua na kupiga pasi nguo zake.

“Tabia ya kuja mjini hujafua, hujaoga usitutie aibu kama umezoea kuja mjini hujaoga wala kufua nguo baki nyumbani walau huu mwezi wa nane uishe, tunataka sio usafi tu wa mazingira, usafi pia wa wananchi wetu, watu wamejaa chawa tu hapa”. Amesema.

“Ule utaratibu wetu wa Lugalo tunauanza rasmi leo haiwezekani wawe na nidhamu kwenye kile kipande cha kukaribia mita 200, 300 kwahiyo ule utaratibu wa mtu kwenye gari kutupa taka hovyo mshusheni akikataa chukueni namba yake ya gari tutamkamata ili aje apige deki” Amesema Makonda.

Pia amesema ifikapo Agosti 5 Jiji la Dar Es salaam liwe safi kwa ajili ya mapokezi ya wageni na amewataka Maafisa Mazingira kuhakikisha miti yote inayopandwa inaota kwani Serikali imekuwa ikitenga bajeti kubwa na pesa hizo hazioneshi matunda na Mazingira chanya kama inavyokusudiwa.

Makonda amewataka Vijana wa usafishaji kuhakikisha kwamba Dereva wa gari akitupa taka taka hovyo apigishwe deki kwa kupewa kipande cha bara bara badala ya kuwapiga faini za pesa na watendaji wa mitaa husika kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi la sivyo watapoteza ajira zao.

Katika hatua nyingine amewataka Wananchi na Tanzania kwa ujumla wajitokeze kwa wingi katika uzinduzi wa Uwanja mpya wa ndege wa Kisasa wa Mwalimu Nyerere Terminal 3 wenye uwezo wa kubeba Abiria Milioni 6 utakaotarajiwa kuzinduliwa na Rais Dkt John Magufuli Agosti 4/2019 asubuhi.

NMB YATOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KUKUZA ELIMU RUANGWA MKOANI LINDI

$
0
0
Meneja wa Tawi la Ruangwa Abrahamu Eliakimu akimueleza Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kuhusu vifaa mbalimbali vilivyokabidhiwa na Benki ya NMB, NMB imetoa msaada wa thamani ya TZS 25 milioni
Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali Vicky Bishubo akikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo kompyuta, madaftari, na madirisha ya aluminum kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kwenye shughuli iliyofanyika zahanati ya Nandangala wilayani Rukwa
………………………
Benki ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi, kompyuta, na Madaftari vyenye thamani ya Tsh. Milioni 25 kwa ajili ya kukuza sekta ya elimu na afya katika halmashauri ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambae pia ni Mbunge wa jimbo hilo katika Zahanati ya Nandagala iliyopo katika Kijiji cha Nandagala Wilayani humo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali Bi, Vicky Bishubo alisema Vifaa hivyo vilivyotolewa ni pamoja na Madilisha ya Aluminium kwa ajili ya Zahanati ya Nandagala yenye thamani ya Tsh. milioni 15, mabati 56 zikiwa na Mbao zake za kupaulia vyenye thamani ya Tsh. Milioni 3.3, Kompyuta 10 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kasimu Majaliwa pamoja na Madaftali yenye thamani ya Tsh. Milioni 5 kwa ajili ya Shule mbali mbali katika Wilaya hiyo ya Ruangwa.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali Bi, Vicky Bishubo kwa niaba Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Benki hiyo Albert Jonkergouw alisema kuwa kwa NMB changamoto za sekta ya Afya na Elimu hapa Tanzania ni jambo la kipaumbele kutokana na umuhimu wa sekta hizo kuwa ndio nguzo kuu ya maendeleo kwa Taifa.

“Sisi kama NMB tumekuwa msitari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii, ambapo kwa zaidi ya miaka saba mfululizo tumeweza kuchangia 1% ya faida yetu kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayotuzunguka” alisema Bishubo

Hata hivyo Bishubo aliongeza kuwa kwa mwaka 2019 Benki yao imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia sekta ya Elimu na Afya ambapo mpaka sasa tayari imeshatoa msaada wa zaidi ya Tsh. Milioni 600.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliishukuru Benki ya NMB kwa kutoa msaada huo ikiwa ni moja ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano

Majaliwa alisema kama Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Benki hivyo katika shughuli mbali mbali za maendeleo pamoja na majanga yanapotokea.

Rais Magufuli amteua Dkt. Elirehema Joshua Doriye kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIC

KAMPUNI ya Jatu PLC yaendesha mafunzo kwa vijana 100,yawaasa kuacha kutegemea kuajiriwa

$
0
0
KAMPUNI I ya Jenga Afya Tokomeza Umaskini (Jatu PLC), imeendesha mafunzo kwa vijana 100 lengo likiwa ni kutokomeza umaskini kupitia rasilimali watu.

Meneja mkuu wa Jatu, Mohamed Simbano akizungumza wakati wa mafunzo hayo alisema mkakati wa taasisi yao ni kusaidia kuondoa kutu vichwani mwa vijana kwa kuacha kutegemea kuajiriwa na badala yake waangalie fursa zilizopo na kuweza kujiajiri.

“ Tukiwa hapa kwenye mafunzo, una diploma, degree weka pembeni kwa sababu hazina maana sana kama huna uwezo wa kubuni wazo na kutengeneza pesa,” alisema Simbano na kuongeza

“Aliyejaribu na akashindwa, anafaida kubwa kuliko asiyejaribu, kufeli haina maana umeshindwa bali utatafuta namna nyingine ya kujaribu.” Alisema

Akimnukuu mwanafalsafa Joseph Chilton Pearce aliyeelezea thamani ya ubunifu aliyosema, ‘to live a creative life we must lose our fear of being wrong’ kwa tafsiri isiyo rasmi alimanisha kuishi maisha ya ubunifu kunahitaji kuondoa hofu ya kukosea.

Simbano alisema elimu ambayo wanawapatia vijana hao itawaondoa katika dhana ya kusaka ajira au kubweteka majumbani na badala yake watachukua hatua na kujiikingiza kwenye ujasiriamali wa kilimo na masoko.Alisema mafunzo hayo ni bure kwa kila kijana mwenye ndoto za kujikwamua kiuchumi,bila kujali elimu.

Alisema mara baada ya mafunzo hayo watatoa nafasi kwa vijana katika masoko kwa kuwaajiri na kuimarisha kitengo chao cha masoko, hadi kufikia mwaka 2022 kila anayetumia soko bidhaa za Jatu aweze kupata manufaa na kwamba chakula kinacholiwa kiwe suluhisho la masoko.

“Mafunzo haya ni endelevu, vijana 100 tutakaowapa ajira ni fursa pekee kwao kwa kuimarisha kitengo cha masoko cha Jatu, na kazi yao kubwa ni kuhakikisha kila mwanachama wa jatu aweze kutumia bidhaa.” Alisema

Alisema mafunzo hayo yanaenda sambamba na mpango mkakati na kufikia malengo, waliojiwekea ikiwemo kutokomezaz umaskini kupitia rasilimali watu, kilimo na viwanda, ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye soko la hisa (DSE) mwezi Septemba.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 30,2019

TCRA KUHAKIKISHA HUDUMA BORA NA ZA UHAKIKA ZA MAWASILIANO KWENYE UJENZI MRADI WA UMEME MTO RUFIJI

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Rufiji

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeagiza kuwepo kwa huduma bora za Mawasiliano katika eneo la Mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa maji Mto Rufiji Mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa ziara ya Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, kwenye eneo la Mradi huo Julai 28, 2019, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James M. Kilaba alisema, Mradi huo mkubwa ni mradi wa kimkakati na TCRA kama msimamizi wa sekta ya Mawasiliano hapa nchini inaamini hakuna uwekezaji unaotendeka bila ya uwepo wa mawasiliano, jamii na watu watakaokuwa wanatekeleza ujenzi wa mradi huo wanapaswa kuwa na mawasiliano ya uhakika wakati wote wakiendelea na kazi ya ujenzi.

Ujenzi wa Mradi huo wenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Trilioni 6.5 fedha za Serikali, ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli juzi Ijumaa Julai 26, 2019 na utakamilika mwaka 2022 ambapo utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 2115.

Akieleza zaidi Mhandisi Kilaba alisema, Shirika la TTCL kama Shirika la Serikali pamoja na watoa huduma wengine ya mawasiliano wanaowajibu wa kuhakikisha mawasiliano yapo na TCRA wajibu wake ni kuhakikisha watoa huduma wanafanya yale wanayopaswa kufanywa.

“Hapa umesema zaidi ya wafanyakazi 6,000 watakuwa kwenye eneo hili, lakini pia hata watakaokuwa wanakuja kufanya utalii kwenye National Park ya Nyerere ni lazima wawe na mawasiliano na mawasiliano ya sasa ni Data, kwahiyo tunachoweza kuagiza hususan TTCL ni kuhakikisha wanaenda kwa kasi kubwa kuweka mawasiliano katika eneo hili na mawasiliano tunayotaka sisi kama wadhibiti ni 4G as Minimum.” Alifafanua Mhandisi Kilaba na kuongeza

“Kwa hiyo 4G siyo isubiri mpaka turbines (mitambo ya kufua umeme)zianze kuzunguka, la hasha, ujumbe tunaowapa kwakweli mwisho wa mwezi wa Nane (Agosti) mwaka huu, watu waanze kupata huduma za 4G katika maeneo haya.” Alisisitiza.

Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt. Jones Killimbe alisema Mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa nchi na kwamba TCRA imekuwa ikitembelea miradi mikubwa (Flagship Project), kama vile ujenzi wa SGR, Jengo la tatu la abiria la kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere Terminal III na leo tumekuja hapa kutembelea mradi huu mkubwa wa kimakakati wa bwawa kubwa la kufua umeme wa maji ambao utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi, alifafanua Dkt. Kilimbe.

Alimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi kubwa anazofanya kuhakikisha nchi inaelekea kwenye uchumi wa viwanda kwa uhakika zaidi kwa kuimarisha miundombonu wezeshi kama vile nishati ya Umeme wa uhakika na wa bei nafuu.

Nae Mhandsi Mkazi wa ujenzi wa bwawa hilo, Eng.Mushubila Kamuhambwa kutoka kampuni ya TECU, ambayo ni kampuni tanzu ya TANROADS, alisema bwawa hilo litakuwa ni miongoni mwa mabwawa makubwa yaliyotengenzwa na binadamu na litakuwa na urefu wa kilomita 100.

Akieleza faida za bwawa hilo licha ya kuzalisha umeme, pia shughuli za uvuvi wa samaki katika maeneo yatakayoainishwa, ongezeko la Mamba na Viboko ambao wanapatikana kwenye mto Rufiji lakin I pia kuwa kivutio cha utalii.

Hata hivyo alieleza changamoto za mawasiliano ya simu inayowakabili eneo la mradi na kuomba TCRA kuyahimiza makampuni ya simu kuboresha huduma zao."Umbi letu, tunaomba muwasukume hawa wanaotoa huduma za mawasiliano ya simu, kwakweli mawasiliano ni changamoto kubwa sana kwenye eneo hili." Alisisitiza Mhandisi Kamuhambwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba (wapili kushoto) na mmoja wa wajumbe wa bodi, wakiwa kwenye eneo la Mto Rufiji ambako kunajengwa bwawa la kufua umeme wa maji Megawati 2115.
Baadhi ya wajumbe wa bodi na menejiment ya TCRA wakiwa kandokando ya Mto Rufiji Julai 28, 2019 wakati wa ziara ya kutembeela ujenzi wa Mradi wa umeme wa Mto Rufiji. 
Mwenyekiti wa Bodi, TCRA, Dkt. Jones Killimbe akifafanua jambo.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi Jmes M. Kilaba, akizungumza mwanzoni mwa ziara hiyo.
Msafara wa TCRA ukipatiwa maelezo ya utekelezaji wa Mradi.
Msafara wa TCRA ukiwa eneo la mradi

WAZIRI MKUU AKAGUA UJEZI WA OFISI ZA HALMASHAURI NA HOSPITALI YA WILAYA RUANGWA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa kwenye eneo la Nachingwea , Julai 29, 2019. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea jengo la wazazi wakati alipokagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa, Julai 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Andrew Chezue, wakati alipowasili kwenye eneo la Nachingwea kukagua ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Ruangwa, Julai 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa na yuko jimboni kwake kwa mapumziko mafupi, alikagua ujenzi huo jana jioni (Jumatatu, Julai 29, 2019). Jengo hilo linalojengwa na SUMA JKT, linahitaji sh. bilioni 3.77 hadi kukamilika kwake.

Akiwa kwenye eneo la ofisi hizo, Waziri Mkuu alielezwa kwamba Halmashauri hiyo imepokea shilingi milioni 500 kutoka Serikali Kuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi mpya ya Halmashauri hiyo.

Ujenzi wa ofisi hiyo ambayo ikikamilika itakuwa na ghorofa moja, ulianza Juni mosi, 2019 na unatarajiwa kukamilika Julai, mwakani. Jengo litakuwa na ofisi 33 za chini, ofisi 26 za ghorofa ya kwanza na kumbi mbili za mikutano.

Kazi ambazo zimeshafanyika hadi sasa ni usafishaji wa eneo kwa ajili ya ujenzi; upimaji wa sampuli ya udongo (Geotech Survey); uingizaji wa maji eneo la ujenzi;uchimbaji wa kisima kikubwa cha kuhifadhia maji na uvutaji wa umeme eneo la ujenzi.

Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ufyatuaji wa tofali ambapo hadi sasa jumla ya matofali 10,000 yamekwishafyatuliwa ambayo ni sawa na asilimia 50 ya mahitaji ya matofali yote. Pia ukusanyaji wa vifaa vya ujenzi eneo la ujenzi unaendelea.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu jana alikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo na kukiri kwamba ameridhishwa na kazi iliyokwishafanyika hadi sasa.

Akiwa hospitalini hapo, Waziri Mkuu alielezwa na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Mahela Njile kwamba hadi kukamilika kwake, hospitali hiyo itakuwa na majengo 22 yanayokisiwa kugharimu jumla ya sh. bilioni 7.5 kulingana na maksio ya OR-TAMISEMI.

Dkt. Njile alisema katika awamu ya kwanza Serikali imetoa sh. bilioni 1.5 na kuelekeza yajengwe majengo saba ya kipaumbele ambayo ni jengo la uzazi, la wagonjwa wa nje (OPD), maabara, la X-ray, la utoaji dawa, la kufulia nguo na la utawala.

“Serikali imeelekeza ujenzi huu ufanyike kwa kutumia njia ya manunuzi inayoitwa ‘Force Account’ ambapo Halmashauri inanunua vifaa vya ujenzi na kuajiri mafundi wa kujenga majengo yaliyoelekezwa wakisimamiwa na wataalam wa halmashauri na kamati mbalimbali,” alisema.

Akizungumza na wakazi waliojitokeza kumsikiliza hospitalini hapo, Waziri Mkuu aliwapongeza viongozi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia vizuri ujenzi na kwa kuamua kutumia force account ambayo alisema inapunguza sana gharama za manunuzi.

Aliitaka Halmashauri hiyo isisubiri hadi kazi ya ujenzi ikamilike, na badala yake wahusika wajipange na kuanza kufanya usafi wa eneo linalozunguka hospitali hiyo.“Halmashauri tusikae tu kusubiri ujenzi uishe. Tufanye usafi kuzunguka eneo lote, tupande miti na maua ili mandhari ianze kupendeza,” alisema.

Kuhusu muda wa kukamilisha kazi hiyo, Waziri Mkuu aliwashauri mafundi wazidishiwe muda wa kufanya kazi. “Badala ya kufanya kazi mchana peke yake, bora waongezewe muda wafanye hadi usiku ili kufidia muda uliopotea, na uliobakia ni mfupi mno,” alisema.

Alisema anaamini kazi hiyo itakamilika ndani ya muda mfupi ili huduma zianze kutolewa hapohapo Ruangwa na kuwapunguzia wananchi adha ya kwenda hadi hospitali ya Ndanda.

MAKAMU WA RAIS AONYA MATUSI NA VITENDO VYA UDAHALILISHAJI MASOKONI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Bango Juu kama ishara ya Uzindua rasmi Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko pamoja na ugawaji wa Pikipiki 14 kwa Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dodoma kwa ajili ya kuongeza kurahisisha Usafiri katika kufanikisha kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji kwa Wanawake na watoto . Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Katikati Mwenyekiti wa ALAT Taifa na Meya wa Manispa ya Shinyanga Mhe. Gulamhafeez Z. Mukadam na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Funguo ya Pikipiki Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith S. Mahenge Baada ya kuzindua rasmi Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko kwa ajili ya kuongeza Chachu ya kurahisisha Usafiri katika kufanikisha zoezi hilo, Jumla ya Pikipiki 14 zilitolewa kwa Mkoa wa Dodoma . Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Wajasiriamali Wanawake katika Mkoa wa Dodoma alipotembelea Mabanda ya Maonesho kwenye Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Masokoni Wanawake na Wanancho wa Dodoma, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akihutubia kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodriquez walipokutana kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake (UN WOMEN) Bibi. Hadon Addou walipokutana kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
Mwenyekiti wa ALAT Mhe Gulamhafeez Mukadam,akizungumza na Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata Utepe kuzindua rasmi Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko pamoja na ugawaji wa Pikipiki 14 kwa Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dodoma kwa ajili ya kuongeza kurahisisha Usafiri katika kufanikisha kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji kwa Wanawake na watoto . Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema watu wanatumia matusi ni watu waliokosa malezi kwa namna tofauti tangu wakiwa wadogo hivyo kuitaka Jamii ya Watanzania kutumia nguvu nyingi katika malezi ya watoto ili kuepukana na athari za ukosefu wa malezi ukubwani. 

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo jijini Dodoma katika hotuba yake ya uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya masoko na zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa waataalam wa maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma. 

Aidha Makamu wa Rais amekemea wanaume wanaotumia lugha ya matumisi katika maeneo ya masoko kuwa yanasabababisha wakina mama wafanya biashara Sokoni kukosa uhuru na hata kushindwa kuleta watoto wao sokoni kwa ajili ya kuwasaidia kwa kutopenda vijana wao kusikia lugha isiyokuwa na maadili. 

“Mnawazalilisha wanawake kwa kuwatukana matusi kwa kutumia viungo vyao, kuwashika au kuwapapasa bila idhini yao kwanini nyie wanaume msishikane wenyewe vitendo vya kuwazalilisha wanawake havikubaliki kabisa’’. Alisisitiza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. 

Katika hotuba yake hiyo Makamu wa Rais wa Tanzania amesema vitendo hivyo vya ukatili havikubaliki na ndio maana ya ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ibala ya 168 c inasema wanawake wanayo haki ya kulindwa dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote ile hivyo hatua za kukomesha vitendo vya ukatili dhidi yao ni utekelezaji wa ilani hiyo. 

Pamoja na kukemea vitendo hivyo Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wanaume wanaonyanyaswa Kijinsia wasione aibu bali watoe taarifa kwenye dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ili Serikali iweze kupata takwimu sahihi ili iweze kufanyia kazi chanagamoto hiyo. 

Aidha Makamu wa Rais amehoji wanawake walio katika Kamati ya Soko kwanini wanafumbia macho vitendo vya ukatili ili hali wao ni viongozi watoa maamuzi sokoni hapo na kuonya kuwa uenda na wao wanachangia kuendelea kuwepo kwa ukatili katika maeneo ya sokoni. 

Makamu wa Rais amewataka viongozi wa masoko nchini kuhakikisha wanafanyia kazi tabia ya watoto wadogo kufanya biashara sokoni kwa lengo la kusaidia familia na kuutaka uongozi wa soko kuwahoji na kuwarudisha shuleni ili kusaidia kukata mnyororo wa umasikini wa familia kwani mtoto akipata elimu inamsaidia kutumia elimu yake kupambana na umasikini. 

Kwa upande wake Waziri wa Afya, MAendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemwomba Makamu wa Rais kuagiza Halmashauri zote nchini kuacha kutoa kiwango kidogo cha mikopo kwa akina na mama na waongeze kiwango cha fedha ili wakinamama wapate miradi ya maana ya biashara kupitia makato ya 4% ya mapato ya kwa Halmashauri. 

“Unakuta kikundi cha akina mama watano wapewa mkopo wa laki tano nakugawana fedha kidogo hii ni pesa gani ndio maana wakina mama wanaishia kuila na kushindwa kufanya marejesho kwa kuwa fedha hii inakuwa haitoshi kufanya chochote’’ Aliongeza Waziri Mwalimu. 

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau wataendelea kutafuta na kugawa Pikipiki kwa Mikoa mingine baada ya Mkoa wa Dodoma ili kuwawezesha Maafisa Maendeleo nchini kutoa elimu kwa jamii kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto. 

Dkt. Jingu amesema kuwa Wizara imetoa pikipiki 25 kwa mkoa wa Dodoma na mapema mwezi ujao itatoa pikipiki kumi na tano kama hizo kwa Mkoa wa Rukwa ili kuwawezesha Maafisa Maendeleo Mkoani humo kutumia usafiri huo kuelimisha wananchi kuhusu ukatili na unyanyasaji dhidi ya Wanawake na Watoto. 

Naye Beatrice Siame ambaye ni Mwakilishi wanawake Soko la Majengo ameiomba Serikali kusimamia usawa wa kijinsia katika maeneo ya kazi ili wanawake waweze kunufaika na kuwezeshwa kiuchumi lakini pia akibainisha kuwa changamoto ya soko ya bidhaa zao ni kikwazo katika kumwendeleza mwanamke kiuchumi. 

Uzinduzi wa Mradi wa kupinga unyanyasaji na udhalilishaji wanawake kijinsia katika Masoko ni hatua muhimu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto unaolenga kutokomeza vitendo vya ukatili Nchini kwa 50% ifikapo 2022.

TTCL na TOSCI washirikiana kusaidia wakulima kubaini mbegu 'feki'

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi (kulia) wakibadilishana nyaraka za makubaliano mara baada ya kusaini makubaliano hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi (wa pili kulia) wakionesha nyaraka za mikataba ya ushirikiano mara baada ya kuingia makubaliano hayo, ambapo TTCL imetengeneza mfumo ujulikanao kama TTCL HAKIKI utakaofanya kazi ya kuhakiki mbegu kwa kutumia simu ya mkulima. Pembeni yao ni wanasheria wa taasisi zote mbili wakishuhudia. 





Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi (kulia) wakisaini makubaliano ambapo TTCL imetengeneza mfumo ujulikanao kama TTCL HAKIKI utakaofanya kazi ya kuhakiki mbegu kwa kutumia simu ya mkulima.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi (kulia) wakisaini makubaliano ambapo TTCL imetengeneza mfumo ujulikanao kama TTCL HAKIKI utakaofanya kazi ya kuhakiki mbegu kwa kutumia simu ya mkulima. Nyuma yao ni wanasheria wa taasisi hizo wakishuhudia. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye hafla hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi.






SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeingia makubaliano na Taasisi ya Udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), ambapo TTCL imetengeneza mfumo ujulikanao kama 'TTCL HAKIKI' utakaofanya kazi ya kuhakiki mbegu kwa kutumia simu ya mkulima. Mfumo huo utamwezesha mkulima na watumiaji wengine kuthibitisha ubora wa pembejeo za mbegu na vifaa vya kilimo kupitia simu za mkononi na tovuti.

Akizungumza katika hafla hiyo leo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema shirika hilo linatambua umuhimu wa sekta ya kilimo nchini katika kuchania maendeleo kiuchumi hivyo imefarijika kushirikiana na TOSCI kuwasaidia wakulima kubaini pembejeo zisizo na ubora.

"...Sote tunatambua kuwa nchini Tanzania, sekta ya kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chaanzo cha chakula pamoja na utoaji fursa za ajira zaidi ya 75% ya Watanzania,"

"Kwa kutambua ukweli huo na kwa kusukumwa na nia ya dhati ya kutaka kuboresha maisha ya Wananchi wetu, TTCL na TOSCI tunaunganisha nguvu ili kuwapatia wakulima mbegu zilizozingatia viwango vya ubora wa mbegu ambazo ni chanzo kikuu cha mavuno mazuri yatakayompatia mkulima faida zinazoendana na juhudi na uwekezaji wake katika shughulihiyo," alisema Bw. Waziri Kindamba.

Huduma hiyo ya kuhakiki pembejeo kwa kutumia 'TTCL HAKIKI' itakuwa ni bure na kwa simu isiokuwa na mtandao wa internet mkulima atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wenye code kwenda namba 15035 zilizopo kwenye kifungashio cha mbegu na mteja wa simu janja atatakiwa kupakua app ya TTCL HAKIKI kutoka play store au kuingia www.ttclhakiki.co.tz .

Katika hafla hiyo ya kuingia makubaliano hayo, Taasisi ya Udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Patrick Ngwediagi ambaye alikiri kuwa mfumo huo utawasaidia wakulima na kupunguza mtawanyiko wa mbegu zisizo na ubora.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 31,2019

WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI TERMINAL III

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wilson Kantambula (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Damas Ndumbaro (kushoto) wakati alipokagua maadalizi ya mapokezi ya wajumbe wa mkutano wa SADC kwenye jengo la pili na la tatu katika kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Julai 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wakati alipokagua maandalizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC kwenye Jengo la pili na la tatu la abaria katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Julai 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maandalizi ya mapokezi ya wajumbe wa mkutano wa SADC kwenye jengo la pili na la tatu la abaria katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

***********

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua jengo la tatu la abiria kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere ili kuona maandilizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC.

Akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na Kamati ya maandalizi uwanjani hapo leo jioni (Jumatano, Julai 31, 2019), Waziri Mkuu amesema maandalizi ni mazuri isipokuwa kwa kasoro chache zilizobakia.

“Nimepita VIP hakuna shida. Pale terminal 2, sehemu ya Uhamiaji iko vizuri, uchunguzi wa afya nayo iko vizuri, lakini vyoo inabidi vibadilishwe haraka sana. Vile vyoo pale nje vimechoka, vibadilishwe mara moja, siyo tu kwa ajili ya ugeni, bali ni kwa faida yetu pia,” amesema huku akimwagiza meneja wa uwanja huo, Bw. Paul Lugasha aharakishe zoezi hilo.

Katika jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo, Waziri Mkuu amekagua eneo ambalo viongozi wakuu wa nchi watashukia, watakagua gwaride la heshima na kuangalia vikundi vya ngoma. Pia amekagua vyumba ambavyo watapumzikia kabla ya kuelekea mjini.

Amesisitiza kuwa usafi wa barabarani bado hauridhishi sababu kuna mawe, udongo na michanga kwenye barabara kuu ya kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. “Tulikubaliana kuwa zile bustani ziboreshwe, vyuma vya barabarani vitengenezwe lakini hata leo nimepita kwenye fly-over, bado kuna mawe na michanga, hata sijui vinatokea wapi,” alisema.

Amewataka wahusika waweke banners za kutosha za aina mbalimbali na picha za wanyama kutani, uwanjani hapo ili kuonesha kwamba kuna mkutano mkubwa unafanyika hapa nchini.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya uwepo wa mkutano huo mkubwa kuendesha biashara zao na ujasiriamali.

“Ziko fursa nyingi za uwepo wa mkutano huu. Kila mmoja atumie nafasi hii kuweza kuongeza na kuboresha kazi yake inayomletea uchumi,” amesema.

Barabara ya Njombe-Makete km 107,4 kukamilika mwakani.

$
0
0
Muonekano wa barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Njombe.
Mkandarasi China Railway Seventh Group Co. Ltd (CRSG), akiendelea na kazi ya kuweka lami katika barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 
Mkandarasi China Railway Seventh Group Co. Ltd (CRSG), akiendelea na kazi ya kuweka lami katika barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusufu Mazana akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Moronga- Makete km 53.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami.


Muonekano wa box calvat linalojengwa katika barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Bw, Ali Kassinge akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua ujenzi wa barabara ya Moronga - Makete km 53.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Muonekano wa nyumba ya Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Wilayani Makete zinazojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoani Njombe
Muonekano wa bweni la wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Wilayani Makete linalojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoani Njombe. 

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Julai 31,2019.

MAGAZETI YA LEO AGOSTI 1/2019


RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA 21st CENTURY FOOD AND PACKAGING LTD JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwana Mkewe Mama Janeth Magufuli wapili kutoka kushoto,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Mohamed Dewji, Waziri waViwanda Innocent Bashungwa, akikata utepe kuashiriaufunguzi wa Kiwanda cha 21 st Century Food andPackaging kilichopo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuliakizungumza na Mkurugenzi wa Kiwanda cha 21 st CenturyFood and Packaging Mohamed Dewji mara baada yauzinduzi wa kiwanda hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuliakisikiliza maelezo ya kutoka kwa Mkurugenzi waKiwanda cha 21 st Century Food and Packaging MohamedDewji kuhusu ubora wa bidhaa mbalimbali za kiwandahicho jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuliakizungumza na wananchi mara baada ya kufunguakiwanda hicho jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA KILIMO KIZIMBANI ZANZIBAR LEO.

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifurahia wakati akivuna mboga aina ya spinachi katika kitalu cha maoneshi ya JKU , kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Alim Iddi.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwanafunzu wa Chuo cha Kilimo Kizimbani Ndg. Faki Ali Faki na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiponyeza kitufe kuashiria kuyafungua Maonesho ya Kilimo Zanzibar katika viwanja vya Kizimbani Wilaya Magharibi “A” Unguja kulia Kaimu Waziri wa Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvivi Waziri wa Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano,Mhe. Dkt Sira Ubwa Mwamboya.*(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika moja ya Trekta lililotolewa Mkopo na Benki ya TAD kwa Vikundi vya Ushirika Zanzibar, wakati wa hafla ya maonesho hayo yaliofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi”A” Unguja leo.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabihi Ufungo wa Treka Mwenyekiti wa Ushirika wa Kilimo Mkombozi cha Mkokotoni Ndg. Haji Mashaka Omar,wakati wa hafla ya Maonesho ya Kilimo yaliofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi”A” Unguja.(Picha na Ikulu)

Rais Magufuli afungua Jengo la 3 la JNIA leo jijini Dar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe akishuhudiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na viongozi wengine kuashiria ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 201
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakifurahia baada ya kuingia kwenye ndege ya ATCL aina ya Dreamliner iliyotua kutokea Mumbai wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Wapiga picha wakifurahia kupigwa picha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ndani ya ndege ya Dreamliner ya AITCL iliyowasili kutoka Mumbai wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakipigwa picha na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiwa ndani ya ndege ye ATCL ya Dreamliner iliyotua kutoka Mumbai wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry bin Ally wakitembezwa sehemu mbalimbali wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea kwa furaha na wafanyakazi wa Tawi la Benki ya NMB lililoko ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuufungua rasmi leo Alhamisi Agosti 1, 201
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na marubani wa ndege ye ATCL ya Dreamliner waliotua kutoka Mumbai wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiondoka baada yakuhitimisha sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifawa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga Push Up na wasanii wa Tanzania One Theatre (TOT) wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri ya kutumbuiza msanii wa Tanzania One Theatre (TOT) Plus Khadija Omar Kopa wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakifunua pazia kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi kwa furaha akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry bin Ally na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wakielekea kukata utepe wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019.


WIZARA YA KILIMO YAJA NA MKAKATI WA TAIFA WA MIAKA 10 WA USIMAMIZI WA MAZAO BAADA YA KUVUNWA – MHE HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan, kuhutubia wananchi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Wakulima, Nane Nane, yaliyoanza tarehe 1-8 Julai 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Mkakati wa Taifa wa miaka 10 wa Usimamizi wa Mazao baada ya Kuvunwa wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Wakulima, Nane Nane, yaliyoanza tarehe 1-8 Julai 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akitoa maelezo kuhusu Tume ya Maendeleo ya Ushirika mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Wakulima, Nane Nane, yaliyoanza tarehe 1-8 Julai 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Wakulima, Nane Nane, yaliyoanza tarehe 1-8 Julai 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisalimiana na Bi Vumilia Zikankuba mara baada ya kutembelea banda la Maonesho ya kilimo la Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili-ASDP II wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Wakulima, Nane Nane, yaliyoanza tarehe 1-8 Julai 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu

Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo, mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia kupungua kwa uzalishaji na tija ya mazao, uhaba wa malisho ya mifugo na rasilimali maji, teknolojia duni za kuhifadhi mazao baada ya mavuno, uelewa mdogo wa wadau katika kukabiliana na upotevu wa mazao na uhaba wa miundombinu ya masoko. 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Wakulima, Nane Nane, yameanza leo tarehe 1-8 Julai 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. 

Mhe Hasunga amesema kuwa wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo watapata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya bidhaa za kilimo ili kuona hali halisi ya Maadhimisho pamoja na teknolojia za uzalishaji, uongezaji thamani wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, zilivyoandaliwa. Waoneshaji wengine wako njiani na tunatarajia uwanja huu wa Nyakabindi utafurika kwa maonesho.

Alisema kuwa ili kuweza kukabiliana na baadhi ya changamoto hizo za upotevu wa mazao baada ya kuvuna, Wizara ya Kilimo imetayarisha Mkakati wa Taifa wa miaka 10 wa Usimamizi wa Mazao baada ya Kuvunwa. 

Alisema kuwa Mkakati huo umeandaliwa ili kuendana na malengo endelevu ya dunia ya kutokomeza njaa ifikapo 2030, kuhakikisha usalama wa chakula na lishe na kukuza kilimo endelevu kama lengo la pili la Umoja wa Mataifa kati ya Malengo 17.

“Katika utafiti uliofanyika inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 watu watakuwa bilioni tisa (9) na hivyo mahitaji ya chakula yatakuwa asilimia 60 zaidi ya mahitaji ya sasa. Hivyo basi mkazo utakuwa kuzalisha chakula kati ya asilimia 50 – 70 zaidi ya sasa. Hivyo, udhibiti wa upotevu wa mazao ya chakula ni suala muhimu na la kipekee” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

Mkakati huo utakuwa Mwongozo kwa Sekta za Umma na Binafsi katika kukabiliana na changamoto ya upotevu wa Mazao baada ya mavuno. Aidha, Mkakati huo umezingatia mabadiliko yanayoendelea ya Kitaasisi na Kisera.

Alisema, suala la udhibiti wa upotevu wa mazao ya chakula ni suala muhimu na la kipeee, linalopaswa kupewa kipaumbele na kila Mdau katika mnyororo wa thamani na shabaha yetu ni kupunguza upotevu kwa asilimia 50 ya mazao ya chakula ifikapo 2025. 

Waziri Hasunga ametaja Mkakati huo kuwa una malengo makuu tisa ambayo ni Kujenga uelewa kuhusu usimamizi wa mazao baada ya kuvuna ili kuboresha ufanisi na kupunguza upotevu wa mazao katika mnyororo wa thamani; Kuhamasisha upatikanaji, ufikiaji, unafuu na utumiaji wa teknolojia na mbinu zilizothibitishwa kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna; Kuwezesha mifumo ya masoko ya kilimo, ili kuboresha upatikanaji wa soko na kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna; na Kuhamasisha tatifi na uvumbuzi wa teknolojia mpya inayoendana na mazingira yetu pamoja na mbinu za kupunguza upotevu wa mazao.

Mikakati mingine ni Kupitia na kuweka sheria mpya ili kuhakikisha kuwa viwango vya ubora vinazingatiwa kwa mujibu wa sheria ili kupunguza upotevu baada ya kuvuna; Kuimarisha uwezo wa taasisi, uratibu, ushirikiano, ubia na ushiriki wa Wadau wa usimamizi wa upotevu baada ya kuvuna katika kuimarisha utekelezaji malengo ya kimkakati; Kutengeneza mifumo ya usimamizi wa mazao baada ya kuvuna ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi; Kukabiliana na upungufu wa fedha katika kugharamia usimamizi wa mazao baada ya kuvuna; na Kuwa na mbinu za kiwango kinachokubalika za kukusanya taarifa za upotevu wa mazao baada ya kuvuna nchini.

Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wengine wameandaa mpango wa kutekeleza Mkakati huo. Ili kutekeleza mpango na malengo hayo kwa ufanisi ni vema kushirikikana Wadau wote kwenye mnyororo wa thamani. 


BENKI YA CRDB NA KAULI MBIU YA “KILIMO CHETU, VIWANDA VYETU, UCHUMI WETU” MAONYESHO YA NANE NANE SIMIYU

$
0
0

Benki ya CRDB imeendelea kudhihirisha kuwa Benki kinarakatika kuwezesha sekta mbalimbali za maendeleo nchiniambapo katika maonesho ya mwaka huu ya nane naneambayo kitaifa yanaadhimishwa mkoani Simiyu Benki hiyo
imekuja na kauli mbiu ya “Kilimo chetu, Viwanda vyetu, Uchumi
wetu”.

Akizungumza katika maonesho hayo ambayo yamezinduliwarasmi leo hii na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Boma Raballaalisema Benki ya CRDB inaamini kuwa uwezeshaji wa sekta yakilimo utasaidia kuongeza malighafi katika viwanda nchini na
hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

“Tukiwa Benki ya kizalendo nchini tupo tayari kushirikiana naSerikali yetu kujenga uchumi wa kati unaoshamirishwa naviwanda. Ambavyo kwa uhalisia vinategemea sana mazao yakilimo kama malighafi zake,” alisema ndugu Boma Raballa.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliipongeza Benki yaCRDB kwa kuwa mstari wa mbele kuwezesha sekta ya kilimokupitia huduma na bidhaa mbalimbali inazozitoa Benki hiyokwa ajili ya kilimo ikiwamo mikopo ya pembejeo za kilimo.

“Nimefurahishwa sana na kauli mbiu yenu ya ‘Kilimo Chetu,Viwanda Vyetu, Uchumi wetu’ hii inaonyesha ni jinsi gani Benkihii imejipanga vilivyo kuboresha sekta hii muhimu ambayo nikichocheo kikubwa katika kufikia uchumi wa kati wa viwanda”,alisema Hussein Bashe.Akimueleza Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe juu yamchango wa Benki ya CRDB katika maendeleo kilimo nchini
ndugu Boma Raballa alisema Benki ya CRDB inatoa zaidi yaasilimia 40% ya mikopo yote itolewayo kwa ajili ya kilimo nchini.

Ambapo kwa kipindi cha mwaka 2018/2019, zaidi ya shilingibilioni 650 zimeshatolewa. Katika hizo, shilingi bilioni 150 yaaniasilimia 23% , zimeelekezwa katika kilimo cha mazao yabiashara na malighafi za viwanda, utengenezaji wa pembejeo,usindikaji na usambazaji.

Raballa alisema pia Benki ya CRDB imekuwaikishirikiana na kwa karibu wadau wadau mbalimbali wa sektaya kilimo nchini ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania, Benki yaMaendeleo ya Kilimo (TADB), Shirika la Uwezeshaji wa Kilimo(PASS), Mfuko wa Afrika Gurantee (AGF), Shirika laUwezeshaji Kifedha la Kimataifa (IFC), Benki ya MaendeleoAfrika (AFDB), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO),Ushirikiano wa Maendeleo ya Viwanda (IDC) na Kampuni ya
ETC Agro katika kuwawezesha wakulima nchini kupitiamafunzo mbalimbali juu ya ufahamu wa masuala ya fedha,uwekezaji , utafutaji masoko na mikopo ya kilimo.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballa wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019),yaliyofunguliwa rasmi leo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akisaini kitabu cha wageni
wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), yaliyofunguliwa rasmi leo na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu. Katikati ni Mkurugenzi wa Wateja wa Kati na Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akisalimiana na Afisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Nassib Kalamba wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akizungumza na Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB, Felix Kisenha wakati alipokuwa akipatiwa huduma za kibenki katika Tawi la Benki ya CRDB linalotembea, katika maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Afisa wa Benki ya CRDB, Maregesi Shaaban akieleza jambo kuhusu huduma ya Malkia Akauti kwa baadhi ya wateja wa Benki hiyo waliotembelea banda lao, wakati wa maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.











Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images