Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live

NMB yauza Hati Fungani za Bil.83.3/-

$
0
0





Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati Benki ya NMB – Filbert Mponzi akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza matokeo ya hati fungani ya Benki hiyo katika ofisi za NMB jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna.


Afisa Mkuu wa Fedha, Ruth Zaipuna akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza matokeo ya hati fungani ya Benki hiyo katika ofisi za NMB jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkuu wateja wadogo na wakati (Chief Retail Banking), Filbert Mponzi na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha (Head, Global Markets Treasury department), Gladness Deogratius.

***********

BENKI ya NMB, imetangaza matokeo ya mauzo ya toleo la tatu laprogramu ya hati fungani ya benki hiyo, ambako imekusanya Sh. Bilioni83.3 sawa na asilimia 333 ya mauzo yaliyotarajiwa awali ya Sh. Bilioni 25.Mauzo ya toleo la tatu la hati fungani ya NMB yalifunguliwa Juni 10 na kufungwa Julai 8, mwaka huu, ambako kipindi hicho cha miezi miwili,kilikuja baada ya Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA),kutoa idhini ya mauzo hayo.

Akizungumza katika hafla ya kutangaza matokeo hayo, iliyofanyika jijiniDar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Fedha , Ruth Zaipuna, alisema waokama benki wanajivunia kiwango hicho cha mauzo, kinachothibitishaimani ya wananchi na jamii kwa benki yake.

Zaipuna alibainisha kuwa, tayari NMB imeyapokea na kuyakubali maombiyote na kwamba waombaji wote wa manunuzi ya hati funganiwametaarifiwa na kwamba leo Agosti 2, wanaorodhesha hati funganizote, kabla ya wanunuzi kukabidhiwa vyeti mwezi mmoja ujao.

Alifafanua ya kwamba, mauzo hayo ya kiwango cha juu kulikowalivyotarajia, yanaiongezea benki nguvu ya kiuchumi katika kufanikishautoaji wa mikopo kwa wateja wao na kwamba mchakato mzimaumeshirikisha zaidi ya matawi 200 kote nchini.

“NMB inatoa shukrani za dhati kwa taasisi zote zilizofanikisha uuzwaji watoleo la tatu la hati fungani ya NMB, ikiwemo CMSA, Soko la Hisa la Dar esSalaam (DSE), Mshauri Kiongozi wa NMB, Stanbic Bank Tanzania Ltd naDalali Mfadhili wa NMB, Orbit Securities Company Ltd,” alisema Zaipuna.

Hati fungani ni aina ya uwekezaji, ambao unamuwezesha mteja kuwekezapesa katika taasisi (hasa shirika la kibiashara au Serikali), kwa kuikopeshafedha kwa muda maalum na kwa riba isiyobadilika. Riba ya hati funganiza NMB kwa mwaka ni asilimia 10.

Mteja anaponunua Hati Fungani ya NMB, anakuwa ameikopesha benkifedha zake, ambako NMB inaahidi kurejesha fedha zake (msingi) katika kipindi maalum cha ukomavu. Kuanzia muda uliowekeza hadi muda waukomavu ambao unakuwa miaka mitatu.

MISS UTALII KUCHELE, NCHI ZAIDI YA 100 KUIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KWA KUTANGAZA UTALII

$
0
0
*BASATA yaibariki bodi mpya na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

BODI maalumu itakayosimamia mashindano ya urembo, utalii na utamaduni maarufu kama Miss Toursim Tanzania imezinduliwa rasmi jana  jijini Dar es Salaam na hiyo ni kufuatia kushindwa kwa usimamizi wa mashindano hayo kupitia taasisi iliyokuwa inasimamia mashindano hayo hali iliyopelekea kurekebishwa kwa mfumo wa mashindano hayo kwa kuimarisha usimamizi wa mashindano pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji.

Akizungumza mara baada ya kuizindua bodi hiyo Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa baraza la sanaa la taifa (BASATA) Vivian Shalua amepongeza uamuzi wa kuanzishwa kwa bodi maalumu itakayosimamia mashindano hayo tofauti na ilivyokuwa awali huku akiwataka wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu na kuipepereshusha vyema bendera ya Tanzania.

Shalua amesema kuwa mwaka 2013 baraza hilo ilitoa muda wa wasimamizi wa mashindano hayo kujichunguza na kuboresha mashindano na wanaamini bodi hiyo itafanyavizuri zaidi kwa kuwa wamekuwa wakishirikisha baraza la sanaa kwa kila hatua na katika vikao vyao wamedhamiria kutangaza vivutio vya nchi kitaifa na kimataifa na kuwaomba wadhamini kujitokeza ili kuweza kudhamini mashindano hayo.

Kwa upande wake Rais na mwenyekiti wa bodi hiyo Gideon Chipungahelo amesema kwamba baada ya kutathimini na kupanga mikakati kuhusiana na mashindano hayo wamekuja na nguvu mpya kwa kuandaa shindano la kitaifa la miss utalii Tanzania kwa kuhusisha zaidi ya nchi 100 duniani pamoja na washiriki watakaowakilisha Tanzania kupitia kanda maalumu za ushiriki.

Chipungahelo amesema kuwa bodi inayosimamia mashindano hayo ipo imara na yataendeshwa kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu kwa malengo ya kulitangaza taifa kupitia utalii, utamaduni pamoja na mila za kitanzania.

Vilevile amewashauri wasanii na wadau wa Sanaa kuwatumia wataalamu kutoka BASATA ili waweze kufahamu namna bora za uendeshaji wa shughuli za sanaa kote nchini.

Mchakato wa mashindano hayo ya urembo unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti na utahusisha kanda nane katika Mikoa yote nchini na kubeba kauli mbiu ya, "Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa- Utalii mi Maisha, Utamaduni ni Uhai wa Taifa-"
Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo (kulia) akimshukuru Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua mara baada ya kumaliza kikao chao na kupatikana kwa bodi mpya ya shindano hilo na kuitangaza rasmi mbele ya Waandishi wa Habari,jana jijini Dar.Picha na Michuzi Jr-Michuzi Media

Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo (kulia) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mikakati mipya ya shindano hilo,mara baada ya kutangazwa bodi mpya ya shindano hilo,huku wakishirikiana bega kwa bega na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA)

Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),mara baada ya kuizindua bodi mpya ya Miss Tourism Tanzania,ambapo pia alipongeza uamuzi wa kuanzishwa kwa bodi maalumu itakayosimamia mashindano hayo tofauti na ilivyokuwa awali huku akiwataka wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu na kuipepereshusha vyema bendera ya Tanzania.
Bodi mpya ya Miss Tourism Tanzania ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa BASATA katika meza kuu,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari.


Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) muonekano mpya wa shindano hilo mara baada ya kuzinduliwa upya na Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua

Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo akiwashukuru wanahabari (hawapo pichani) na Wadau mbalimbali waliojitokeza kushuhudia tukio hilo adhimu,kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua

Bodi mpya ya Miss Tourism Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa BASATA

ZANZIBAR WAENDELEA KUFAIDI MBEGU YA MPUNGA AINA YA SUPA BC ILIYOBORESHWA KWA MIONZI

$
0
0
Wananchi wa Tanzania upande wa Zanzibar wameendelea kufaidika na mchele unaotokana na mbegu ya mpunga aina ya SUPA BC iliyoboreshwa kwa Teknolojia ya Nyuklia kwa kutumia Mionzi aina ya gamma iliyotumika kununurisha bengu hizo . 

Mradi huo ulifadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) na kuratibiwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI) ili kuhakikisha mbegu hiyo inaboreshwa na kuwa yenye ubora wa hali ya juu. 

Akizungumza katika maonesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Nyakabindi, Wilayani Bariadi, Mkoani Simiyu, Mtafiti Msaidizi wa mazao ya kilimo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar Bwana Hamza Hamid Hamza amesema kuwa mbegu hiyo ina ubora na huzalisha mpunga kwa wingi na kwa sasa ni chaguo la wakulima na wananchi wengi Kisiwani Zanzibar. 

Amesema mbegu aina ya SUPA BC, ina uwezo wa kuzalisha mpunga hadi kufikia tani 7 kwa hekta moja ambapo huchukua muda wa siku 130 mpaka kuvunwa kwake hali ambayo kwa sasa imewahamasisha wakulima wengi kulima aina hiyo ya mpunga visiwani humo. 

“Mchele unaotokana na mpunga wa mbegu ya SUPA BC ni mzuri, wenye harufu nzuri na wenye ladha tamu kwa walaji na wakulima wengi wanashawishika kupanda mbegu hiyo kwa wingi” alisema Hamza Hamid. 

Kwa mujibu wa Hamza amesema kuwa mpunga huo una sifa nyingi ikiwemo urahisi katika kufikicha tofauti na mbegu nyingine nyingi za mpunga zilizozoeleka na kuwa mmea wake una urefu wa wastani na usioweza kuanguka baada ya kubeba mpunga ukiwa shambani hivyo hupelekea kubaki na mazao yote hadi wakati wa kuvuna pamoja na uwezo wa kutoa machipukizi mengi wakati wa ukuaji wake. 

Mbegu hiyo ilizinduliwa rasmi na Wizara ya Kilimo na Mifugo ya Zanzibar mwaka 2011 ambapo mpaka sasa inaendelea kulimwa kwa wingi visiwani humo. 

Mtaalamu huyo amesema kuwa teknolojia hii ya nyuklia kwa kutumia mionzi ya Gamma ikiendelea kutumika inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo hasa katika kutafiti wa mbegu mbali mbali za mazao hapa nchini. 

Bw. Hamza pia ameshauri kwamba kwa sasa kutokana na mbegu hiyo ya mpunga kutumika visiwani Zanzibar pekee , ni wakati muafaka sasa mbegu hiyo ikaanza pia kutumika pia katika eneo la Tanzania Bara. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga , Bi Zainab Terak akiwa ameshika mpunga uliotokana na mbegu ya aina ya Supa BC iliyoboreshwa kwa Teknolojia ya Nyuklia kwa kutumia mionzi aina ya gamma iliyotumika kununurisha mbegu hizo mradi ulioofadhiliwa na Shirika la nguvu za Atomiki la kimatifa (IAEA) kwa kuratibiwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Kilimo (SUA) na Taasisi ya Utafiti wa kilimo Zanzibar (ZARI) .


NMB Kuwawezesha wakulima kisasa, Yadhamini Maonesho Ya Kitaifa Ya Nanenane Kwa Milioni 30

$
0
0
BENKI ya NMB imesema kuwa itahakikisha inaendeleza jitihada zake kwa wakulima za kuwawezesha kadri wanavyohitaji kulingana na mazao yao ili kuifanya sekta ya kilimo nchini kubeba uchumi wa nchi.

Mbali na hilo benki hiyo imesema kuwa kwa muda mrefu imekuwa ikitangaza sekta ya wakulima na kuwasaidia wakulima kama ajenda yake kuu, kutokana na asilimia kubwa ya watanzania kutegemea sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Meneja wa benki hiyo Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse wakati akikabidhi kiasi cha sh. Milioni 30 na tisheti 300 kwa katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini kama udhamini wa benki hiyo kwenye maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) kitaifa yanayofanyikia Mkoani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magese. Fedha hizo zitatumika kwenye maonesho ya NaneNane ya kitaifa. NMB ni wadhamini wa Maonyesho hayo ya kitaifa yanayolenga kutoa fursa kwa wakulima na Wafugaji



Magesse alisema kuwa benki hiyo imekuwa haifanyi kazi ya kutunza fedha za wateja wake tu, bali hata kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali za Kilimo, Ufugaji, Elimu, Afya na Biashara.

Alisema kuwa katika maonesho hayo benki ya NMB imejipanga kuhakikisha inatoa elimu kwa wakulima, wafugaji, jinsi ya kulima kisasa na kitaalamu ikiwa pamoja na kuwaeleza jinsi gani benki hiyo inaweza kushiriki kwenye kilimo kwa kuwapatia mikopo.

“Kwenye maonesho ya mwaka huu ambayo yatakuwa bora zaidi, ushiriki wetu kama benki utakuwa mkubwa zaidi, na umelenga kuwasaida wakulima, tutakuwa na bidhaa za wafugaji wa ng’ombe, na wakulima wa mazao ya pamba, tumbaku na kahawa lakini hata Matrekta tutakuwa nayo,” alisema Magesse.

Aliwataka wakulima kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo hasa kwenye banda la NMB ili waweze kupata elimu itakayowafanya walime kisasa kwa kutumia teknoloJia na kuzalisha kwa tija.

Akiongea mara baada ya kupokea mchango huo Katibu Tawala huyo ameishukuru benki hiyo kwa mchango wake, ambapo alisema utawezesha kuboresha zaidi eneo la Nyakabindi ambako sherehe hizo zinafanyikia.

Sagini ameeleza kuwa Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kusaidia mambo mbalimbali katika mkoa wa Simiyu ikiwemo Elimu na Afya, huku akibainisha kuwa mchango huo utawezesha maonesho hayo kuwa bora zaidi.

“Kwa mchango huu NMB watakuwa kwenye wachangiaji wale wa pili kwa ukubwa, tunawashukuru sana kwa mchango wao na tuombe mahusiano yetu na wao yaendelee kuwa mazuri zaidi ya hapa,” alisema Sagini.


Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (wa pili kushoto) akitazama bidhaa za mfanyabiashara Raphael Buja (Buja Pure Honey) kwenye Banda la NMB wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Biashara na Kilimo wa NMB John Machunda na Mkuu wa Idara wa Biashara kwa Serikali NMB Vicky Bishubo
Wananchi wakipata huduma mbalimbali kwenye banda la NMB, wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu walipotembelea banda hilo. NMB ni mmoja ya wadhamini wakuu wa maonesho hayo .

TCRA YAENDELEA KUTOA ELIMU MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI MKOANI MOROGORO

$
0
0
*Yahamasisha usajili laini za simu kwa alama za vidole

Na Chalila Kibuda, MICHUZI TV

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzani Kanda ya Mashariki (TCRA) imesema kuwa wananchi wa Kanda ya Mashariki watumie maonesho ya Nane Nane kupata elimu ya Mawasiliano pamoja uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Hayo ameyasema Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro, amesema maonesho ya Nane Nane yatumike kwa wananchi kusajili laini za simu alama za vidole kwa huduma zote za kufanya usajili zipo ndani za maonesho hayo.

Mhandisi Odiero amesema muda uliokuwepo wananchi kusajili laini za simu kwa alma za vidole kwani mwisho wa usajili huo ni Desemba 31 mwaka huu.

Amesema kuwa muda uliopangwa lazima utumike kikamilifu kupunguza kujazana kwa watoa huduma katika tarehe za mwisho za Desemba na kufanya watu wengine kuona muda uliopangwa ulikuwa hautoshi.

“Muda uliowekwa ni mkubwa kwa wananchi kupata kitambulisho cha Taifa na kusajili laini zao za simu na walio na vitambulisho vya Taifa kusajili laini zao za simu kuondokana na usumbufu wa kufungiwa mawasiliano simu hizo. 

Aidha amesema kuwa TCRA iko bega kwa bega katika kutoa elimu kwa wananchi kwa huduma mbalilbali za amawasiliano ili wasitumie mawasiliano kinyume cha sheria.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (wane kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa timu ya TCRA katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (wane kutoka kushoto) akiwa katimu picha ya pamoja na timu ya TCRA katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Christopher John akizungumza na mwananchi wakati alipotembelea banda la TCRA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Mwananchi akisaini kitabu wakati alipotembelea banda la TCRA kanda ya Mashariki katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Wananchi wakipata huduma katika banda la NIDA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Baadhi ya watoa huduma za Simu katika Banda la TCRA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.

DSTV YAWATOA HOFU WATEJA WAKE MSIMU MPYA WA LIGI KUU

$
0
0
Na.Khadija seif, Michuzi tv 

KAMPUNI ya Multi Choice Tanzania kupitia King'amuzi Cha dstv wamewahakikishia mashabiki wa soka kuendelea kuwapatia mechi ya ligi kuu maarufu duniani kwa msimu mpya.

Ligi ambazo zitarushwa mubashara kwa lugha ya kiswahili ni Ligi kuu ya Uingereza(EPL), Italia (Serie A), Hispania (La Liga), Liga ya mapingwa Ulaya(UEFA) pamoja na makombe mengine maarufu.

Akizungumza na waandishi wahabari Mkuu wa Masoko wa Kampuni hiyo Ronald Shelukindo amesema pazia la msimu mpya litafunguliwa Agosti 2 kwa mtanange wa ngao ya jamii.

"Msimu huu tutaanza na Ligi ya ngao ya jamii Kati ya Liverpool na kigogo wa Ligi ya Uingereza Manchester City huu utakua mubashara kwa lugha ya nyumbani kiswahili," alisema Shelukindo

Akaongeza kuwa watangazaji wa msimu huu ni Salama Jabir, Edo Kumwembe, Maulid Kitenge, Ibrahim Madoud, Abduli Liongo na Oscar Oscar pia kingamuzi cha DStv unaweza kuunganisha vifaa mbalimbali kama vile Simu, Tablet na Laptop.

Aidha uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadua wa soka, wachezaji wastaafu Sekolojo Chambua, Mohmed Hussein na Fikiri Magoso na wasanii mbalimbali Pierre Liquid, Romeo Jonsoni' Dj RJ' na Quickracka.
Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo, Kauli Mbiu ya Msimu huu ni SOKA MWANZO MWISHO’
Afisa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Bi. Shumbana Walwa akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dar es salaam.
MMoja wa wachezaji wa zamani Sekilojo Chambua akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso na Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo pamoja na wafanyakazi wengine wakiwa meza kuu wakifurahia jambo katika hafla hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Bw. Jonson Mshana akiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka.
Mmoja wa wachambuzi wa soka Ole Mjengwa akizungumza wakati hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka.

Benki ya CRDB yazindua kwa kishindo zao jipya la SAFARI CAR LOAN jijini Arusha

$
0
0
Katika kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza sekta ya utalii nchini benki ya CRDB imezindua zao jipya la kibiashara liitwalo “SAFARI CAR LOAN”zao ambalo lina lengo la kuwawezesha  wajasiriamali waliopo katika sekta hiyo kufanya biashara yao kwa ufanisi kwa kuwapatia mikopo ya magari  mapya ya utalii kwa  riba nafuu 
Mkopo huo wenye riba ya asilimia 10 unatolewa na benki ya CRDB ambayo imeingia mkataba na kampuni ya utengenezaji magari maalum ya utalii ya Hanspaul ya jijini Arusha ambayo gari jipya hugharimu kiasi cha dola elfu sabini na tano hadi laki moja ambayo mkopaji atarejesha mkopo ndani ya miaka mitano.
Afisa  biashara Mkuu wa Benki ya CRDB ,Dakta Joseph Witts akizungumza hafla maalum ya uzinduzi wa zao hilo  la Safari Car Loan jijini Arusha iliyoenda sambamba na kongamano la utalii liloshirikisha a wafanyabiashara kutoka Hongkong China ,Tanzania na taasisi za serikali zinazojihusisha na uwekezaji dakta Witts alisema lengo la kuanzisha zao hilo ni kutatua changamoto ya usafiri usafiri katika sekta hiyo.
“CRDB tumekuja kutatua changamoto kubwa ambayo wafanyabiashara wamekuwa wakikumbana nayo kutokana na ukosefu wa mitaji ya kuweza kununua magari ya kusafirishia watalii tukijua kwamba utalii unachangia sehemu kubwa katika pato la taifa”alisema Witts.
Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda aliipongeza benki ya  CRDB kwa uvumbuzi  wa zao jipya la kibenki ambalo litasaidia wajasiriamali kuweza kujipatia magari ya kusafirisha watalii kwa uhakika Zaidi.
“Uvumbuzi huu wa zao jipya la biashara la kibenk linasaidia wajasiriamali kuweza kujipatia magari ya kubeba watalii, huu ni ubunifu mzuri utasaidia vijana wetu ambao hawana mitaji mingi kuweza kujiingiza kwenye shughuli hizi hususani wakati huu ambao serikali ikiiendelea kuongeza vivutio vya utalii nchi”alisema Mkenda
Kwa pande wao baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo bi Fransisca Masika mkurugenzi wa  kampuni ya Nature Rensiposible Safari na S.M. Mwanonga mkurugenzi wa kampuni ya SAMLESS Adventures wameishukuru CRDB kwa mkopo huo ambao walisema utaboresha biashara yao.
 Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda (kulia) akipata maelezokatika halfa ya uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB jijni Arusha. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania jaji mstaafu Thomas  Mihayo 
 Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda (kulia) akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB jijni Arusha
 Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda (kulia) akiwa katika moja ya gari katika halfa ya uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB jijni Arusha
Moja ya gari katika halfa ya uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB jijni Arusha
  Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania jaji mstaafu Thomas  Mihayo akimkabidhi ufunguo wa gari jipya mmoja wa wadau aliyenufaika na mkopo wa benk ya CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
 Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii profesa Adolf Mkenda akimkabidhi ufunguo wa gari mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Samless adventures Sam Manonga baada ya kupata mkopo kutoka benki ya CRDB katika halfa ya uzinduzi wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN unaotolewa na benki ya CRDB.
 Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania jaji mstaafu Thomas  Mihayo akimkabidhi ufunguo wa gari jipya mkurugenzi wa kampuni ya Nature responsible safari  Bi Francisca Masika ambae ni mwanamke pekee aliyenufaika na mkopo wa benk ya CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
 Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania jaji mstaafu Thomas  Mihayo akimkabidhi ufunguo wa gari jipya mkurugenzi wa kampuni ya Nature responsible safari  Bi Francisca Masika ambae ni mwanamke pekee aliyenufaika na mkopo wa benk ya CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
 Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Profesa Adolf Mkenda akimkabidhi ufunguo wa gari jipya mkurugenzi wa kampuni ya Excelent guides Diason baada ya kupata mkopo wa  CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Profesa Adolf Mkenda akimkabidhi ufunguo wa gari jipya mkurugenzi wa kampuni ya Excelent guides Diason baada ya kupata mkopo wa  CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.

  Mmoja wa wadau akipongezwa kwa mkopo wa benk ya CRDB wa zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.
 Wafanyakazi wa benk ya CRDB wakifurahia mapokeo ya  zao jipya la SAFARI CAR LOAN uliozinduliwa jana jijini Arusha.

TAASISI YA PASS YAMVUTIA MKUU WA MKOA KILIMANJARO KWENYE MAONESHO YA NANENANE ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa taasisi ya kuwezesha sekta binafsi kuwaunganisha wakulima na taasisi za kifedha nchini PASS,Hellen Wakuganda alipotembelea banda hilo kwenye uwanja wa Taso Njiro jijini Arusha. 
Wafanyakazi wa PASS walio katika viwanja vua Taso Njiro jijini Arusha kuwahudumia wakulima kuongeza tija katika shughuli zao.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Mbulu mkoa wa Manyara,Celestine Mofuga wakimsikiliza Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa taasisi inayounganisha wakulima na taasisi za kifedha nchini PASS,Hellen Wakuganda alipotembelea banda hilo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Nanenane (Kilimo, Mifugo na Uvuvi) kwenye uwanja wa Taso Njiro jijini Arusha. 

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira(kulia) akizungumza jambo alipotembelea banda la taasisi inayowaunganisha wakulima na taasisi za kifedha nchini PASS wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Nanenane (Kilimo, Mifugo na Uvuvi) kwenye uwanja wa Taso Njiro jijini Arusha. 



Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira ameipongeza taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) chini ya Programu ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini kwa juhudi inazofanya kuwasaidia wakulima kuongeza tija katika shughuli zao.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonesho ya 26 ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi maarufu Nanenane katika Kanda ya Kaskazini kwenye viwanja vya Taso Njiro jijini Arusha yanayohudhuriwa na wananchi kutoka mikoa ya Kilimanjaro,Manyara na Arusha.

Amesema utendaji kazi wa taasisi ya PASS hautiliwi shaka kutokana na kupenya maeneo mengi ya vijijini kutoa elimu kwenye vikundi na kuwaunganisha wakulima wa ngazi mbalimbali na taasisi za kifedha huku PASS ikitoa dhamana.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa PASS ,Nicomed Bohay amesema taasisi hiyo inafanya kazi kama kiungo kati ya sekta ya kilimo na sekta za fedha lengo likiwa kuwawezesha kuwawezesha upatikanaji wa huduma za kifedha na kibiashara kwa wajasiriamali binafsi wa biashara za kilimo katika mnyororo mzima wa thamani.

Bohay amesema kuwa walengwa na wakulima binafsi,vyama vya ushirika,makundi ya wakulima wadogo na makampuni yanayojihusisha na kilimo.

Ameongeza kuwa hadi sasa PASS inafanya kazi na jumla ya benki 15 nchini zinazotoa mikopo kwa wakulima na makampuni yanahusiana na kilimo huku jumla ya wajasiriamali 929,172 wamenufaika na mikopo iliyodhaminiwa na taasisi hiyo inayofikia Sh 712 bilioni


“SERIKALI KUPITIA TASAF YAANDAA UTARATIBU MPYA WA KUWAPATA WALENGWA WA TASAF WENYE UFANISI ZAIDI” - DKT. MWANJELWA

$
0
0
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Burugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ambako yuko kwenye ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kukutana na Watumishi wa Umma kuhimiza uwajibikaji.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi  na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  katika kijiji cha Burugo (hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.
 Baadhi ya Wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika katika kijiji cha Lukindo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani).
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akiwa nyumbani kwa mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Burugo Bi. Justa Migini (kulia kwa Naibu Waziri),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Miradi ya Ajira za Muda TASAF Bw. Paul Kijazi  wakishuhudia nyumba iliyojengwa na mlengwa huyo kwa kutumia ruzuku ya TASAF.
 Mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa  kijiji cha  Burugo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Bi. Agnes Kemilembe akitoa ushuhuda wa namna alivyotumia ruzuku kuboresha makazi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb). Picha ya chini ni mlengwa huyo akimuonesha naibu waziri shamba lake analoliendeleza kwa kutumia ruzuku ya TASAF. 


NA ESTOM SANGA---KAGERA 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa amesema Serikali kupitia TASAF imeandaa utaratibu utakaowezesha kuorodheshwa kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini watakaokidhi vigezo vya umaskini. 

Akiwahutubia Wananchi na Walengwa wa TASAF katika vijiji vya Lukindo na Burugo katika halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Dkt. Mwanjelwa amesema utaratibu huo mpya wa kuzitambua na kuziorodhesha kaya za walengwa kwenye Mpango utahusisha matumizi ya kielektroniki na kupiga picha kwa wahusika ili kuondoa uwezekano wa kuorodhesha kaya zisizostahiki. 

Aidha Naibu Waziri huyo amesema serikali kupitia TASAF inaendelea kukamilisha maandalizi ya uzinduzi wa sehemu ya pili ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao amesema haitawapa mwanya wananchi wenye uwezo kujumuishwa kwenye Mpango huo. 

Amesema Walengwa wa Mpango huo wenye uwezo wa kufanya kazi watawekewa utaratibu wa kutekeleza miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yao watakayoibua na kisha kulipwa ujira kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 

Katika hatua nyingine Dkt. Mwanjelwa amewaagiza wataalamu wa sekta mbalimbali katika halmashauri za wilaya kutenga muda wa kuwatembelea Walengwa wa TASAF na kuona namna wanavyotekeleza miradi yao na kuwashauri namna bora zaidi ya kutekeleza miradi hiyo ili waweze kupata matokeo bora na yenye tija. 

Wakati huo huo ameonyesha kuridhishwa kwake na mafanikio waliyoanza kupata Walengwa wa TASAF katika Nyanja mbalimbali jambo linaloonyesha kuwa mkakati wa Serikali katika kupambana na umaskini unatekelezeka. 

Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipotembelea vijiji vya Lukindo, na Burugo katika halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera na kukutana na Walengwa ambako amekagua shughuli wanazozifanya kwa kutumia ruzuku wanayoipata kutoka TASAF. 

Naibu Waziri huyo amesema Walengwa hao wa TASAF wameweza kubadilisha maisha yao kwa kutumia ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa kuboresha maisha yao hususani katika Nyanja za makazi, uchumi huku wengine wakifanikiwa kujenga nyumba zao bora ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kupata ruzuku hiyo.

KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA AWATAKA WATAFITI NA WADADISI KUZINGATIA VIWANGO UKUSANYAJI WA TAKWIMU

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kulia) akizungumza
jambo na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ofisi ya Dar es Salaam Ms Preet Arora(kushoto) muda mfupi baada ya kufungua mafunzo kwa wadadisi na wasimamiziwa utafiti wa sekta isiyo rasmi leo Jumapili (Agosti 4, 2019). Katikati niMtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi-Idara ya Ajira na Ukuzaji ujuzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu. 
Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ofisi ya Dar es Salaam, Ms Preet Arora
akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Doto
James, muda mfupi baada ya baada ya uzinduzi wa mafunzo kwa wadadisi nawasimamizi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi leo Jumapili (Agosti 4, 2019).
Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa pamoja na
Mkurugenzi Msaidizi- Idara ya Ajira na Ukuzaji ujuzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu.(PICHA NA MAELEZO) 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (katikati waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na waddisi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi nchinimara baada ya kufungua mafunzo yao leo Jumapili (Agosti 4, 2019) Jijini Dar esSalaam. Kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa na kulia kwaMgeni rasmi ni Mkurugennzi Msaidizi- idara ya Ajira na Ukuzaji Ajira, Ofisi yaWaziri Mkuu, Bw. Ahmed Makbel. 
************* 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James amewataka wadadisi na wasimamizi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi nchini kuzingatia viwango vya ubora katika ukusanyaji wa taarifa ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi zenye kubaini mahitaji na changamoto za sekta hiyo nchini. 

Akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Sekta isiyo rasmi Nchini leo Jumapili (Agosti 4, 2019) Jijini Dar es Salaam, Bw. James alisema matokeo ya utafiti huo yataisaidia Serikali kufahamu mchango halisi wa sekta isiyo rasmi katika Pato la taifa ikijumuisha ulipaji kodi. 

Aliongeza kuwa ni ukweli ulio dhahiri kuwa sekta isiyo rasmi imekuwa nguzo muhimu katika pato la taifa kwani kulingana na utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi uliofanyika mwaka 2014 ilibainika kuwa, asilimia 21.7 ya watu waliokuwa na ajira walikuwa katika sekta isiyo rasmi, na hivyo kuleta kiashiria kuwa sekta hiyo ina mchango muhimu katika pato la taifa. 

Bw.James alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejiwekea malengo mbalimbali katika kuinua uchumi wa wananchi wake ikiwemo kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta isiyo rasmi ikiwemo hali ya upatikanaji wa masoko, fursa za mikopo, ujuzi unaohitajika pamoja na matumizi ya teknolojia kwa nia ya kuongeza tija kwenye uzalishaji. 

“Sina shaka na ubora wa takwimu zitakazokusanywa kwa kuwa mnaendelea kufanya kazi hii kwa karibu sana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Benki ya Dunia (WB), tumieni uzoefu wenu ili na sisi Watanzania tunufaike kuifahamu zaidi sekta hii katika kukuza uchumi wa Tanzania” alisema Bw. James. 

Kwa mujibu wa Bw. James alisema utafiti wa kwanza wa kitaifa katika sekta isiyo rasmi ilifanyika nchini mwaka 1991 na kufuatiwa na utafiti kama huo katika Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1995, hivyo ni kipindi kirefu kimepita na kufanya kuwepo na mahitaji makubwa ya takwimu zinazoakisi hali halisi ya sasa ya sekta hiyo nchini. 

Kwa upande wake, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa alisema hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano kufanya utafiti huo ni uthubutu mkubwa kwa Tanzania kwa kuwa ni nchi chache za Bara la Afrika zimeweza kufanya utafiti huo kwa ajili ya kupima sekta yenyewe na upatikanaji wa rasilimali fedha sambamba na kubaini fursa za ajira kwa wananchi wengi wakiwemo wananchi maskini. 

“Kama mnayofahamu Serikali kwa sasa inatekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21 ambao unahitaji takwimu katika ngazi za chini za utekezaji, ili kuongeza wigo wa hifadhi ya jamii kwa lengo la kufikia lengo la angalau asilimia 40 ya watu wenye ajira ifikapo mwaka 2020” alisema Dkt. Chuwa. 

Aidha Dkt. Chuwa alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imeshakamilisha maandalizi yote ya kufanyika kwa utafiti huo, unaotarajia kuanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam Mwezi Agosti hadi Novemba mwaka huu. 

Dkt. Chuwa alisema muundo wa utafiti huo umegawanyika katika ngazi kuu mbili, ikiwemo ngazi ya ukusanyaji wa taarifa katika ngazi ya kaya na ngazi ya pili ni ngazi ya biashara (uchumi), ambapo katika ngazi ya kaya, utafiti huo umejikita katika maeneo ya taarifa za kidemokrasia, elimu, hali ya ulemavu, ajira, ukosefu wa ajira. 

Akifafanua zaidi, Dkt. Chuwa alisema sampuli ya utafiti huo katika ngazi ya kaya pia utahusisha maeneo ya kuhesabia yapatayo 200 yaliyo mkoani Dar es Salaam na kaya zilizochaguliwa zaidi ya 2,400 pamoja na ukusanyaji wa taarifa kutoka kwenye biashara zaidi ya 4,000 na matokeo ya utafiti huo yatawezesha upatikanaji wa taarifa za kitakwimu ambazo ni wakilishi katika ngazi za Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

MKUTANO MKUU WA SADC WAIVA, WANAWAKE NA VIJANA FURSA NJE KUONESHA GUNDUZI ZAO

$
0
0



*Mwito watolewa kwa wafanyabiashara kujitokeza na kutangaza bidhaa zao


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IKIWA zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa jumuiya ya maendeleo wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC) ambao utatanguliwa na wiki ya viwanda itakayoanza kesho kwa kuzinduliwa rasmi na Rais Dkt. John Joseph Magufuli katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kutengeneza masoko na kupata oda kutoka nchi 16 zinazoshiriki mkutano huo.

Akizungumza katika kilele cha siku ya wanahabari leo jijini humo Naibu Waziri wa viwanda na biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa mkutano huo ni fursa kwa watanzania hasa wafanyabiashara katika kutangaza bidhaa zao, kupata ujuzi mpya na kutafuta masoko.

"Niwaombe wananchi watumie fursa hii adhimu katika kutangaza bidhaa zao, kupokea oda, kubadilishana na kupokea ujuzi kutoka kwa wageni pamoja na kujenga ushirikiano wa hali ya juu na wageni wetu, na mmeona hata uzito uliopewa na viongozi wetu Rais Magufuli atazindua wiki ya viwanda kesho na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein atafunga wiki ya viwanda Agosti 8 hivyo tuwaunge mkono" ameeleza Mhandisi Manyanya.

Kuhusiana na idadi ya wananchi waliojiandikisha kushiriki katika maonesho hayo Mhandisi Manyanya ameeleza kuwa zaidi ya watu 2000 wamejiandikisha huku wengi wakiwa wazawa hali inayoashiria watanzania wamekubali mabadikiko na kasi ya maendeleo yanayoongozwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

"Hadi kufikia jana idadi ya washiriki waliojiandikisha ilifikia 2000, huku wazawa wakiwa zaidi ya 700 na watakaoonesha bidhaa mbalimbali wakifikia zaidi ya 900. Kwa hali hii tunategemea matokeo chanja na maendeleo kupitia mkutano wa 39 wa SADC" Ameeleza.

Aidha Mhandisi Manyanya amewataka watanzania kuendeleza desturi ya ukarimu na uzalendo katika kipindi chote Cha mkutano ili kuweza kuendelea kupeperusha vyema bendera ya amani ya nchi yetu.

Vilevile kaimu Mkurugenzi wa mipango wa sekta ya viwanda na ushindani Dkt. barani Afrika Dkt. Johansein Rutaihwa amesema kuwa malengo ya wiki ya viwanda ni pamoja na kutoa elimu ya uelewa kuhusu mpango wa maendeleo hasa maendeleo ya viwanda uliogawanya katika vipindi vitatu ambavyo ni ule wa mwaka 2015/2020, 2021/2050 na ule 2051/2063 mikataba ambayo iliidhinishwa mwezi Machi mwaka 2015.

Amesema kuwa wiki ya viwanda imelenga kuleta ushirikiano pamoja na kutengeneza mnyororo katika ngazi mbalimbali za kitaifa na kimataifa na kubwa kuliko nikuwashirikisha wanawake na vijana katika sekta ya viwanda kwa kuwapa fursa za kuonesha gunduzi zao.

Mkutano huo wa Jumuiya ya Maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ulifanyika nchini mwaka 2003 ambapo Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa alihudumu nafasi ya uenyekiti kwa mwaka 2003/2004 na mwaka huu Rais Magufuli atapokea kijiti hicho kutoka kwa Rais wa Namibia Hage Geingob na atahudumu nafasi ya uenyekiti kwa muhula mmoja na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za kikanda na mikutano ya kisekta ikiwemo afya na elimu.

Utapeli kwa kutumia simu za mkononi waendelea kudhibitiwa.

$
0
0
Matapeli wanaojitambulisha kama wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kwa makosa ya kudukua taarifa za wateja wa huduma ya kifedha ya Tigo Pesa inayotolewa na kampuni hiyo ambapo wamekuwa wakiwatapeli wateja wa kampuni ya Tigo kwa kujitambulisha kama wafanyakazi halali wa Tigo wakati kiukweli sio waajiriwa wa Tigo.

 Matapeli hao utumia mbinu hiyo kujipatia taarifa za siri za wateja hao ambazo baadae wamezitumia kuiba kiasi cha fedha zipatazo shilingi milioni 26 kutoka kwa wateja mbalimbali wa mtandao huo kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Hawa watu wana mbinu mbalimbali, tukitolea mfano, kuna ambao watakupigia wakisema aidha wamekutumia hela kimakosa, au anakupigia kutoka makao makuu ya kampuni ya simu husika na angependa utatue tatizo ambalo mteja amelalamikia.

Tulipata nafasi ya kumuhoji wakala mmoja, kwa jina la Amos Chirwa kutoka Kijichi, ambae alisema, " kwa kweli matapeli ni wengi, na kila siku wanabuni njia tofauti tofauti ili waweze kutuibia sisi mawakala au wateja".

"Mimi kama wakala, ambae nina uzoefu wa miaka 6 sasa, ningependa kuwashauri watanzania kwa ujumla, kwamba usimpe mtu namba yako ya siri, au taarifa binafsi hata kama amejitambulisha kama mfanyakazi wa kampuni za simu kama Vodacom, Airtel, Tigo au Zantel". Alimalizia kwa kusema.

Mtandao huu ungependa pia kuwaasa watanzania kutojishirikisha na masuala ya kiuhalifu hususan katika masuala ya simu za mkononi kwani serikali ina mkono mrefu.

Bashe: Tutaweka Mazingira Rafiki Kwa Ushiriki wa Benki Katika Kilimo

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, akizungumza na wafanyakazi wa NMB kwenye banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (wa pili kushoto) akitazama Bidhaa za mfanyabiashiara Raphael Buja (Buja Pure Honey) kwenye banda la NMB, wakati wa uzinduzi wa maonesho ya nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu, kushoto ni Meneja Mwandamizi Biashara na Kilimo wa NMB John Mchunda, Mkuu wa Idara ya biashara kwa Serikali kutoka NMB Vicky Bishubo (aliyevaa skafu).


Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa wakati serikali ikijiandaa kufanya marekebisho makubwa ya sera ya kilimo, taasisi za kifedha nchini zitajumuishwa katika kutoa maoni jinsi gani zinaweza kushiriki kikamilifu kwenye kilimo. 

Alisema kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo imepanga kuweka mazingira rafiki kwa taasisi za kifedha ili ziwekeze kwenye sekta hiyo, ikiwa pamoja na kuangalia mfumo gani sahihi wa utolewaji mikopo kwa wakulima. 

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo jana wakati alipotembelea banda la Benki ya NMB kwenye maonyesho ya sikuu ya wakulima kitaifa (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 

Alisema kuwa kumekuwepo na tatizo la pembejeo hasa kwenye kilimo cha pamba, ambapo serikali kupitia bodi ya pamba imekuwa ikitumia fedha nyingi kuziagiza na kupelekwa kwa wakulima lakini matokeo yamekuwa hayaonekani. 

“Nitakutana na taasisi zote za fedha tufanye majadiliano kwenye sera mpya wa kilimo wao wanaweza vipi kushiriki moja kwa moja mpaka kwa wakulima, wanaweza vipi kuweka mfumo mzuri na rahisi wa kutoa mikopo kwa wakulima wa chini,” alisema Bashe. 

“ Tunahitaji benki zihusike katika kubadilisha mfumo wa kuagiza pembe nje, tuache kutumia mawakala na baadala yake twende moja kwa moja viwandani kwa kutumia fedha zao na zitarejeshwa na wakulima mara baada ya kuvuna,” aliongeza Bashe. 

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Biashara za serikali Vicky Bishubo kutoka NMB alisema kuwa taasisi za kifedha kujumuishwa kwenye marekebisho ya sera hiyo ni suala muhimu. 

Alisema NMB kupitia kilimo biashara (Agri-business) utakuwa wakati sahihi katika kuhakikisha wakulima na wajasliamali nchini wanawezeshwa zaidi kupitia vikundi vyao ili waweze kuongeza tija katika uzalishaji. 

Aliongeza kuwa NMB inatambua kuwa inalo jukumu kubwa la kuhakikisha wakulima na wananchi wote maeneo ya vijini, wanajumuishwa katika mfumo rasmi wa fedha kupitia kupewa elimu na mafunzo. 

Naye Meneja Mwandamizi katika mahusiano ya biashara ya kilimo kutoka NMB, John Mchunda alisema kuwa benki hiyo ilitenga kiasi cha sh. Bilioni 500 kwenye kilimo- biashara kwa muda wa miaka mitano toka mwaka 2015 kwa ajili ya kusaidia mnyororo wa thamani kwenye sekta ya kilimo na wakulima wenyewe. Na baada ya fedha hizo kuisha mwaka jana, NMB imeongeza bilioni 500 nyingine kusaidia kukuza mnyororo wa thamani (Agricultural value Chain) kwa wakulima, Wafugaji na wavuvi na biashara zao.

Azania Benki yatangaza washindi wa promosheni ya ‘AMSHA NDOTO’

$
0
0
Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Jackson Lohay (katikati) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Amsha Ndoto’ katika droo iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Jumla ya Sh. 8,000,000/- ilitolewa kwa washindi watatu walioshiriki katika promosheni hiyo.
Benki ya Azania (ABL) leo imewatangaza washindi wa promosheni yake ya ‘Amsha Ndoto’ ambayo ina lengo la kuwahamasisha wateja wake na umma wawatanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba itakayowasaidia kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.

Promosheni hii ambayo ni ya mizezi mitatu ilianza rasmi tarehe 27/06/2019 na inatarajia kufikiatamati tarehe 27/09/2019 huku ikihusisha wateja wa Azania Benki wa zamani na wale wapya naimejikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti pamoja naWatoto Akaunti.

Akitangaza washindi kwenye droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mauzo ya RejaReja wa Benki ya Azania, Jackson Lohay, amesema benki imetimiza ahadi ya kuwapatia zawadiwashindi walioshoriki kwenye promosheni na kwamba zawadi wanazopewa zitawasaidiakutimiza ndoto zao.

Kwa mujibu wa Lohay, washindi wa mwezi Julai wa promosheni hii ambao wamepatikana baadaya droo kufanyika ni;

1. Barakaeli Mmari amejishindia kiasi cha TZS 2,000,000/- (Arusha)
2. Rose Anaeli amejishindia kiasi cha TZS 3,000,000/- (Dar es Salaam)
3. Ketus Isack Malekamo amejishindia kiasi cha TZS 3,000,000/- (Tunduma)

Lohay ameongeza kuwa ili mtu aweze kushiriki kwenye promosheni ya Amsha Ndoto ni lazimakwanza awe mteja wa Azania Benki mwenye akiba ya kiasi kisichopungua TZS 1,000,000 ambayeanapewa tokeni zinazomwezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho inayowapata washindi.

Wanaobahatika kushinda watafurahia riba ya 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwakamzima.Akitoa pongezi kwa washindi wa promosheni, Lohay amewahasa wateja wa ABL kushiriki kwawingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata hukuwakijahakikishia kuwa na akiba ya kutosha kwenye akaunti zao kwa ajili ya matumizi yao ya sikuza usoni.

“Tunawahamasisha wazazi wote na walezi kuwafungulia Watoto wao ‘Watoto Akaunti’ ili kuwana uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafutanamna gani ya kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye kwani akaunti hii inaweka msingiwa kuwaandaa watoto kujifunza namna ya kuweka akiba kuanzia kwenye umri mdogo”,amesema Lohay.

Promosheni hii, yenye kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde Tumuwezeshe ada ya shule’,inawasilishwa kupitia mitandao ya kijamii na tovuti za ndani za benki. Benki pia imetengenezatovuti ndogo, maalumu kwa wateja wapya kujiunga na inaweza kupatikana kupitiaamshandoto.com

WCF MBIONI KUANZISHA MFUMO WA WAAJIRI NA WAFANYAKAZI KUWASILISHA MADAI YA FIDIA KIMTANDAO

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), hivi karibuni uko mbioni, kuanzisha mfumo wa waajiri na wafanyakazi kuwasilisha madai ya Fidia kwa njia ya mtandao, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anselim Peter ameyasema hayo jana kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Bw.Peter alisema lengo la kuanzisha mfumo huo ni kusogeza karibu huduma za Mfuko kwa wateja wadau wake na hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi unashiriki katika maonesho ya Nanenane kwa lengo la kupata fursa ya kuwaelimisha waajiri na wafanyakazi kuhusu shughuli za Mfuko ambazo ni kulipa Fidia, utaratibu gani wa kufuata ili kuwasilisha madai kabla ya kulipwa Fidia.
"Pia katika banda la WCF hapa Nyakabindi, wataalamu wetu watatoa elimu kuhusu Mfuko, kusajiliwa, kuwafahamisha taratibu za michango, kuwafahamisha taratibu za madai ya fidia na pia kupokea maoni ya wadau kuhusu Mfuko. Lakini pia tunatoa huduma kwa vitendo jinsi wanavyoweza kufanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wafanyakazi wake kwenye orodha iliyoko WCF, kuprinti cheti, na pia kulipa michango ofisini kwako.” Alifafanua Bw. Peter.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka, ameupongeza Mfuko huo kutokana na ushiriki wake katika mpango wa Mkoa kujenga kiwanda cha kutengenza vifaa tiba Huu ni utekelezaji kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuanzisha na kuimarisha viwanda ambavyo vitaipeleka nchi kafika uchumi wa Kati.
"Nishukuru na kutambua mchango mkubwa wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba na WCF kwa ujumla kwa sababu ni partner (Mshirika) Mkubwa kwenye mipango yetu ya ujenzi wa kiwanda cha Vifaa tiba." Alisema Mhe. Mtaka.
Alisema uongozi wa Mkoa walishirikiana na WCF katika hatua mbalimbali za kushirikiana katika ujenzi wa kiwanda hicho ambapo tayari site clearance imeshafanyika na kwamba hivi sasa wizara iko katika nafasi nzuri ya kutangaza zabuni ili kumpata mkandarasi atakayejenga kiwanda hicho.
"Kwetu sisi kama mkoa WCF imetoa ushirikiano mkubwa katika mipango yetu ya kushiriki katika uchumi wa viwanda wametoa ushirikiano mkubwa." Alisema Mkuu wa Mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (watatu kushoto), akizungumza jambo mbele ya Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter (katikati) na Mussa Mwambujule, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko, wakati alipotembelea banda la WCF kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Simiyu 
 Afisa Uhusiano Mwandamizi WCF, Bw. Sebera Fulgence (kulia) akitoa elimu ya Fidia kwa wafanyakazi
 Mussa Mwambujule, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akitoa elimu hiyo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akisalimiana na mama huyu aliyefika banda la WCF kupata elimu ya Fidia kwa wafanyakazi


RAIS MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA TANZANIA, AWAPA UJUMBE KUHUSU GAWIO

$
0
0
*Puma nao wampongeza Rais kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji

 Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania imemueleza Rais Dk.John Magufuli kuwa mazingira mazuri ya uwekezaji nchini yameifanya kampuni hiyo kuendelea kutengeneza faida mwaka hadi mwaka na hivyo imesababisha kuongezeka kwa gawio kwa Serikali.

Rais Magufuli alifika kwenye banda la Puma Energy Tanzania wakati anatembelea mabanda katika Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) yanayoendelea Ukumbi wa  Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda la Puma Energy Tanzania, Rais Magufuli pamoja na mambo mengine aliuliza maofisa wa kampuni hiyo mwaka huu wamejipanga kutoa gawio la shilingi ngaoi kwa Serikali, ambapo alijibiwa watatoa Sh.bilioni 22 ambapo  Sh.bilioni 11 zitakwenda kwa Serikali.

 "Mwaka jana mlitoa gawio kiasi gani?(Akajibiwa) basi mwaka huu uongezeni  ongezeni kidogo,"alisema Rais Magufuli ambapo maofisa wa Puma nao  wakamhakikishia Rais kuwa watajitajihidi kuongeza huku wakipongeza mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yamesababisha wao kuendelea kufanya vema siku hadi siku.

Akizungumza mbele ya Rais Meneja Operesheni wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Lamecky Hiliyai amemwambia Rais kuwa kampuni hiyo kutokana na mazingira mazuri yaliyopo nchini katika uwekezaji wamekuwa wakiendelea kufanya biashara ya mafuta na kupata faida.

"Mheshmiwa Rais tunashukuru kwani kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji katika nchi yetu, nasi Kampuni ya Puma tumeendelea kufanya biashara, hivyo tumeendelea kupata faida na tunaahidi hata gawio kwa Serikali nalo tutaendelea kuongeza mwaka hadi mwaka,"alisema Hiliyai.

Kwa upande wake Meneja wa Sheria na Mahusiano ya kampuni hiyo, Godluck  Shirima amewaambia waandishi wa habari Kampuni yao inajivunia kufanya 

biashara katika nchi 13 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).Kampuni hiyo ambayo inamilikiwa kwa ubia na Serikali ya Tanzania imesema  mbali na kudhamini maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC pia imekuwa ikisaidia  jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Shirima, alisema wamekuwa wakijiendesha kwa faida tangu walipoanza shughuli  zao mwaka 2011/12. Kwa mujibu wa Shirima mwaka 2011/12 walitoa gawio la Sh bilioni 3.5 kwa wanahisa wake na kati ya fedha gizo Serikali ilipata Sh bilioni 1.25.

Alisema mwaka 2018/19 wanatarajia kutoa gawio la Sh bilioni 22 na Serikali  itapata Sh bilioni 11. "Sisi ni wadau wakubwa wa SADC ndio maana tumedhamini maonesho haya na shughuli zingine za mikutano na tuko hapa kuonesha bidhaa  na huduma zetu kwa nchi wanachama," alisema Shirima.

Ameongeza hata katika uwekezaji unaofanywa na Serikali hasa katika ujenzi wa miundombinu wa kuwezesha usafirishaji wa malighafi na rasilimali za viwanda  umeiwezesha kampuni hiyo kuendelea kunufaika.

"Tumekuwa tukisambaza mafuta katika miradi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa 
(SGR), Daraja la Salenda na tumejenga mfumo wa usafirishaji mafuta katika 
jengo la tatu la abiria Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,"amesema Shirima.
Rais Dk.John Magufuli akipata maelezo katika Banda la Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania akipata maelezo kutoka kwa Meneja Opereheni Lamecky Hiliyai kuhusu namna  ambavyo wanaonesha shughuli zao.Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kuwataka Puma kuendelea kuongeza gawio kwa Serikali ambapo maofisa wa Puma wamemhakikishia kutekeleza maagizo yake.Wa kwanza kushoto ni Meneja Sheria na Mahusiano wa kampuni hiyo Godluck Shirima.

UJENZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM WAENDELEA VYEMA

$
0
0

Maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Dar es Salaam yanakwenda vizuri ambapo ujenzi wa magati 2 kati ya 7 yaliyopo umekamilika na kuanza kupokea meli kubwa za mizigo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema mradi wa ujenzi wa magati hayo utakaogharimu takribani shilingi Trilioni moja utaiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kuongeza ufanisi kwa kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa mizigo na kupokea meli yoyote duniani zikiwemo meli kubwa za kizazi cha saba (7th Generation).

Mhandisi Kakoko amefafanua kuwa kazi inayoendelea imewezesha kukamilika kwa ujenzi katika gati namba 1 na gati namba 2 ambazo zimeongezwa kina kutoka mita 8 hadi kufikia kati ya mita 15 na 19, kina ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na kina kinahitajika kwa meli kubwa zaidi ambacho ni mita 12.

Aidha, Mhandisi Kakoko amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutilia mkazo ujenzi wa Bandari ya Dar es Salaam na kuamua kujenga gati nyingine ya magari iitwayo RORO ambayo itaiwezesha bandari hiyo kupokea meli hata 2 kwa mpigo zenyewe uwezo wa kuchukua magari 10,000 ikilinganishwa na uwezo wa kuchukua magari 200 kabla ya mradi huo.

“Sasa maana yake nini, magari ni kati ya shehena inayoingiza tozo zaidi, kwa magari pekee yake tunaweza kukusanya tozo mara 2 au mara 3 ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, ndio maana tunamshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutuongezea hiyo gati ya RORO.

Kwa hiyo faida ya kwanza tunaipata katika kuongeza kina kwa maana meli kubwa zitaingia kwa mara moja, na kuna watu wamekuwa wakiona kuna Kijiji cha meli zinazosubiri kuingia bandari kushusha mizigo, hiyo haiwezi kuwepo tena” amesema Mhandisi Kakoko.

Mhandisi Kakoko amesema juhudi hizo zinakwenda sambamba na uboreshaji eneo la nyaraka (clearing) kupitia serikali mtandao ili kuondoa mianya ya udanganyifu ambao husababisha upotevu wa mapato.

“Sasa tutaweza kupata moja kwa moja Bill of Lading na hivyo kuondokana na baadhi ya wafanyabiashara au waagizaji mizigo ambao hudai makontena yana mitumba wakati ndani mna magari” amesema Mhandisi Kakoko na kubainisha kuwa uwekaji wa mfumo wa nyaraka unakwenda sambamba na uwekaji wa mitambo ya ukaguzi (scanner).

Amesema baada ya kukamilika kwa gati namba 1 na gati namba 2, ujenzi kwa sasa unaendelea katika gati namba 4 ambayo inakaribia kukabidhiwa TPA na gati namba 5 ambayo uchorongaji unaendelea.

Ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa gati namba 3 na gati namba 4, ujenzi huo utaendelea kwa gati namba 5,6 na 7 na baada ya hapo kazi itaendelea kwa magati ambayo yapo chini ya Kampuni ya Kimataifa ya Huduma za Makontena Bandarini (TICTS) ambayo tayari Serikali ya Awamu ya Tano imeshafanya mazungumzo ya kurekebisha mkataba na sasa mrabaha unaolipwa ni mara 2 ikilinganishwa na zamani.

Mhandisi Kakoko amesema pamoja na kujenga gati hizo, Serikali pia inanunua mitambo mikubwa ya kupakulia na kupakia mizigo na hivyo kuongeza kasi na ufanisi zaidi wa bandari.

Kufuatia juhudi hizo amesema sasa bandari ya Dar es Salaam itakuwa na uwezo wa kutumia vizuri faida yake ya kijiografia kukabiliana na ushindani wa bandari zote zilizopo katika ukanda wa bandari ya Hindi na kuwa lango bora na muhimu kwa nchi za Afrika.

Mhandisi Kakoko amesema kazi hii ya uboreshaji wa Bandari a Dar es Salaam iliyopaswa kufanyika miaka 30 iliyopita imesababisha Tanzania kupoteza kiasi kikubwa cha mapato na kwamba kutokana na uboreshaji huu na hatua ambazo Serikali ya Awamu ya Tano imechukua, TPA itaendelea kuongoza katika utoaji wa gawio.

Ameahidi kuwa mwaka huu TPA inatarajia kutoa gawio la kati ya shilingi Bilioni 150 na shilingi Bilioni 200 na kwamba miaka michache ijayo TPA kwa kushirikiana na wadau wengine wa bandari watakuwa na uwezo wa kuzalisha fedha za kugharamia bajeti nzima ya Serikali ambayo ni takribani shilingi Trilioni 30 kwa mwaka.

Halikadhalika Mhandisi Kakoko amesema kazi ya ujenzi wa bandari pia inaendelea katika Bandari ya Mtwara na ujenzi katika Bandari ya Tanga utaanza mwezi huu (Agosti 2019)

TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa) YANG’ARISHA USIKU WA SADC

$
0
0
Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kutoa burudani kwa wageni mbalimbali walioalikwa katika chakula cha jioni. Hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya ukaribisho wa wageni wa Mkutano wa SADC hususan wa wale wa Wizara ya Viawanda na Biashara.
Mgeni Rasmi katika hafla hio alikua Mheshimiwa Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kikitoa burudani kwa wageni katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City. Ngoma hii inaitwa Druming Ensemble ambayo ni mchanganyo wa upigaji wa ngoma mbalimbali za kitanzania kwa kundi.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali (aliyevaa miwani) alikua mmoja wa wageni waliohudhururia hafla hio na kuonyesha kufurahia uchezaji wa ngoma uliyofanywa na kikundi cha ngoma kutoka TaSUBa.
Waimbaji wa Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wakiimba kwa kupokezana katika ngoma ya Nsimba ambayo inabebwa na uimbaji wa majibishano. 
Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kikicheza kwa madaha ngoma ya Nsimba ambayo huchezwa kwa kutumia ala ya vyungu ambayo asili yake huchezwa na wanawake wa kabila la kifipa.

WAZIRI MKUU: MAONESHO YA SADC NI FURSA PEKEE KWA WATANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa George Lous Chuwa kuhusu bidhaa mbalimbali wakati alipotembelea banda la Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa Habari wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) , Jamila Mbarouk (kulia) na Ben Mwanantala wakati alipotembelea banda la TRC katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Wickled Msian ambaye ni Meneja wa Kudhibiti Ubora wa Bidhaa wa Kampuni ya Ital shoe (wa pili kulia) wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Dkt William Mugisha wakati alipotembelea banda la Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dr es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha yake iliyochorwa kwa kutumia shanga na Bw. Aman Greon (kulia) wakati alipotembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema wiki ya maonesho ya nne ya viwanda ya nchi za SADC ni fursa pekee ya kutangaza bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Agosti 6, 2019) wakati akizungumza na waandishi wa habari mara ya kukagua mabanda kwenye maonesho hayo yanayoendelea kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo ambayo yalifunguliwa jana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, yanafanyika katika maeneo matatu ambayo ni ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, viwanja wa Gymkhana na viwanja vya Karimjee.

“Nimekuja kufanya ufuatiliaji wa maandalizi ya mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za SADC, nimekuta yanaendelea vizuri. Nimekuja kuangalia mwitikio wa wajasiriamali wa pande zote mbili za Muungano pamoja na wajasiriamali kutoka nchi wanachama wa SADC, na pia mwitikio wa wananchi wetu ukoje,” amesema.

Waziri Mkuu amesema fursa hiyo ni muhimu kwa Watanzania kuonesha bidhaa za ndani ili wageni wanaokuja wajue kuna bidhaa zipi zinazozalishwa nchini. “Tumetoa fursa kwa nchi za SADC zote nao pia waoneshe bidhaa zao. Maonesho haya ni ya wazi, Watanzania wanayo nafasi ya kuja kuona na kujifunza,” amesema.

Amesema mbali ya fursa ya masoko, Tanzania inayo pia fursa ya kupata teknolojia mpya na za Kisasa ikiwa ni pamoja na wawekezaji wa viwanda vya usindikaji bidhaa mbalimbali. “Tumeona utaalamu unaotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali, hii maana yake ni kwamba tunajifunza na teknolojia zinazotumika,” amesema.

“Tunayo fursa ya kukaribisha viwanda kutoka nje ya nchi, wote hapa wameleta bidhaa zao. Pia tunawakaribisha waje waanzishe viwanda kwa ubia na Watanzania. Sisi tunayo ardhi, tunazalisha mazao mengi tu, kwa hiyo mbia wa nje anaweza kuunganisha mtaji na Mtanzania na wakajenga kiwanda hapa nchini,” amesema.

Mbali ya fursa za kiuchumi kwao binafsi, Waziri Mkuu amewataka washiriki wa maonesho hayo, watangaze vivutio vya utalii vilivyopo nchini ambavyo vitasaidia kuwafanya wageni wanaoshiriki mkutano huo watamani kubaki nchini na kuvitembelea.

“Watanzania tutumie nafasi hii kutangaza vivutio vingine tulivyonavyo. Mbuga za wanyama tunazo nyingi, tunao Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika na huwezi kuupanda kutokea popote. Ili uupande, ni lazima uje Tanzania,” amesema.

“Pia tuna eneo maarufu la Olduvai Gorge ambalo ni chimbuko la binadamu wa kwanza duniani, na hili liko eneo liko Ngorongoro. Tuna fukwe nzuri, zenye mchanga mzuri ambazo ukikaa wala huwezi kuchafuka, zina urefu wa zaidi ya km. 1,400 kutokea Tanga hadi Mtwara,” ameongeza.

Mapema, Waziri Mkuu alifanya kikao na Mawaziri wa Mambo ya Nje, Utumishi na Utawala Bora, Viwanda na Biashara wa SMT, Viwanda, Biashara, Wazee na wa Zanzibar (SMZ), Naibu Mawaziri wa TAMISEMI, Mambo ya Nje na Mifugo na Uvuvina kuwapa maelekezo ya kuboresha maandalizi hayo. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makatibu Wakuu wa wizara hizo

Bodi ya Utalii yaahidi 'kuibeba' Rock City Marathon

$
0
0

Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw Geofrey Tengeneza (wa pili kushoto) akionyesha fulana maalumu ya mbio za Rock City Marathon msimu mwa mwaka 2019 kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio, Bw Clement Mshana (wa pili kulia) Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw Kasara Naftali (wa kwanza kulia) Pamoja na muwakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bi Ombeni Zavara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio, Bw Clement Mshana (Kulia) akizungumza kuhusiana na maandalizi ya mbio hizo. Wengine ni pamoja na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw Geofrey Tengeneza (Kulia kwake), muwakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bi Ombeni Zavara (wa pili kushoto) pamoja Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (Kushoto)

Waratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw Kasara Naftali (kushoto) na Bi. Irine Lyimo wakionyesha muonekano wa T-shirts na medali maalumu kwa ajili ya msimu wa mwaka 2019 wa mbio za Rock City marathon.
Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (kushoto) sambamba na mmoja wa raratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bi Irine Lyimo wakionyesha muonekano wa T-shirts maalumu kwa ajili ya msimu wa mwaka 2019 wa mbio za Rock City marathon.
Mojawapo ya medali zitakazotelewa kwa washiriki wa mbio za Rock City Marathon msimu wa mwaka 2019
Baadhi ya wakiambiaji (joggers) kutoka klabu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wakifurahia muonekano wa Tshirts pamoja na medali maalumu kwa ajili ya mbio za Rock City Marathon msimu wa mwaka 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.



Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeahidi kushirikiana na waandaaji wa mbio za Rock City Marathon ili kuhakikisha kuwa mbio hizo zinatumika vema kuutangaza utalii wa ndani hapa nchini.

Akizungumza hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa unzinduzi wa msimu wa kumi (10) wa mbio hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi Devota Mdachi, Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TTB,Bw Geofrey Tengeneza alisema adhma hiyo inasukumwa na malengo ya mbio hizo ambayo ni kutumia mchezo wa riadha katika kutangaza utalii hususani katika Ukanda wa Ziwa.

Hafla hiyo iliyofanyika kwenye viunga vya ofisi za TTB jijini Dar es Salaam ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wadhamini mbalimbali wa mbio hizo.

"Kwa kuzingatia uzito wa malengo ya mbio hizi nitamke bayana kuwa TTB tupo tayari kushirikiana na waandaaji wa mbio hizi kuhakikisha kwamba mwaka huu mbio hizi zinafana na zinavutia washiriki wengi zaidi hususani wa kimataifa,'' alisema Bw Tengeneza.

Zaidi, Bw. Tengeneza pia alithibitisha ushiriki wake Pamoja na viongozi waandamizi wa bodi hiyo kwenye mbio hizo zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jingo la kibishara la Rock City Mall, jijini Mwanza ambapo washiriki wa mbio hizo watapita katika barabara mbalimbali za jiji hilo kabla hazijamalizikia katika viunga hivyo.

Mbali na ushiriki huo, Bw Tengeneza pia alitoa pongezo kwa mashirika mbalimbali yenye dhamana ya utalii hapa nchini ikiwemo la Hifadhi za Taifa(TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)kwa kuwa sehemu ya wadau wakubwa wa mbio hizo hizo.

"Ukanda wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo sisi kama kama chombo chenye dhamana ya utalii lazima tuendelee kuvitangaza kwa nguvu na kwa njia tofauti ikiwemo michezo,'' alisema Bw Tengeneza huku akivitaja baadhi ya vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Kisiwa cha Saanane, Makumbusho ya kabila la Wasukuma pamoja na tamaduni za makabila ya wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Mbio za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka kumi iliyopita zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, Pepsi, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Wadhamini wengine ni pamoja na kampuni ya uwakili ya Lis Law Chambers & Consultants, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Mwanza Water, Isamilo Lodge, Pigeon Hotel, Real PR Solutions Limited na Afrimax Strategic Partnerships Limited.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International waandaaji wa mbio hizo, Bw Clement Mshana alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 3000.

Alisema mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuhusisha washiriki wengi zaidi kutoka kila kona ya dunia ikiwemo Afrika, Ulaya, China, Mashariki ya Kati hususani Israel na Marekani huku akitoa wito kwa washiriki wa ndani kujisajili kwa wingi ili kuthibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo alisema maandalizo ya mbio hizo kwasasa yamekamilika kwa asilimia 60 huku akitumia uzinduzi huo kuonyesha Tshirts na medali za zitakazotimika katika msimu wa mbio hizo kwa mwaka huu.
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live




Latest Images