Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI WAMWITA KAIMU BALOZI WA MAREKANI WIZARANI

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akimsikiliza Mwakilishi wa Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini Bi Janine S. Youngalipomwita Wizarani kutoa ufafanuzi kuhusu angalizo la kiusalama lilitolewa na ubalozi huo kupitia tovuti ya Ubalozi wa Marekani hapa Nchini. June 20,2019.

Tarehe 19 June 2019, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania ulitoa taarifa katika mitandao ya kijamii “Twitter” kuhusu angalizo la kiusalama “security alert”. Angalizo hilo la kiusalama lilitokana na uvumi unaodaiwa na ubalozi huo kusambaa kuhusu uwezekano wa kutokea kwa shambulio katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulimwita wizarani Kaimu Balozi wa Marekani ili kutoa ufafanuzi wa “twitter” yao. Ubalozi wa Marekani ulimtuma Mwakilishi wa Kaimu Balozi wa Marekani Bi Janine S. Young kuonana na uongozi wa Wizara.

Bi Janine S. Young ameutambua na kukiri kuwa ujumbe huo umetumwa na ubalozi wa Marekani hapa nchini. Katika ufafanuzi wake amekiri kuwa Ubalozi umefanya makosa ya kutoa tetesi ambazo hazikuwalenga raia wa Marekani pekee bali raia wote wakitambua kuwa Ubalozi hauna mamlaka ya kufanya hivyo jambo lililosababisha taharuki kwa wananchi na wageni wanaotarajia kuitembelea Tanzania.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeukumbusha Ubalozi wa Marekani umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi na taratibu za kidiplomasia zinazokubalika duniani kote katika utoaji wa taarifa za aina hii.

Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe amewataka wananchi na Jumuiya za Kimataifa pamoja na wageni mbalimbali waliopo nchini na wanaotarajia kuitembelea Tanzania kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyothibitishwa ya kuwepo kwa tishio la aina hiyo hapa nchini na kwamba Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejizatiti kukabiliana na matishio yeyote.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam.
20 Juni 2019

Tumepokea Maombi Mapya ya kuuza Mahindi Tani Milioni Moja kwenda Kenya – Naibu Waziri Mgumba

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba akipata amelezo ya ujenzi wa vihenge vya kisasa kwa upande wa ndani kutoka kwa Mhandisi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makao Makuu Bwana Iman Nzobonaliba kulia kwake na wengine ni Mkurugenzi wa Uhifadhi Bwana Mikalu Mapunda na kushoto kwake ni Mhandisi Mgole Chambili Msimamizi kutoka Kampuni ya Feruum 
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba akipata amelezo ya ujenzi wa vihenge vya kisasa kutoka Mhandisi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makao Makuu Bwana Iman Nzobonaliba kulia kwake na wengine ni Mtendaji Mkuu wa NFRA Bwana Milton Lupa 
Mafunsi wa Kampuni ya Feruum wakiendelea na kazi ya kuunganisha vyuma vya ujenzi wa vihenge vya kisasa eneo la Kizota Jijini Dodoma wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba alasiri ya leo 
………………………… 
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba amesema Serikali ya Tanzania imepokea maombi mapya ya kuuza mahindi kwenda nchini Kenya yenye jumla ya Tani milioni 1. 

Mhe. Mgumba ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya gafla kwenye Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA – Makao Makuu) Jijini, Dodoma alipotembelea leo alasiri ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula katika eneo la Kizota, Jijini Dodoma. 

Naibu Waziri Mgumba amesema wakati Serikali ikiwa kwenye hatua ya kuiuzia Zimbabwe kiasi cha mahindi Tani laki saba (700,000) na tani laki moja (100,000) kwa mazao mengine ya nafaka, Serikali ya Kenya imewasilisha ombi rasmi la kununua kiasi hicho kutoka Tanzania. 

Naibu Waziri Mgumba amesema huu ni wakati muhafaka kwa Wakulima wa Tanzania kuchangamkia fursa ya kuuza chakula cha ziada nje ya nchi na kwa bei nzuri ambayo italeta tija na maendeleo na uchumi wao. 

Aidha Mhe. Mgumba alidokeza kuwa amefanya ziara hiyo lengo lake likiwa ni kujionea maendeleo ya ujenzi wa vihenge vya kisasa (Silos) vya kuhifadhia mazao kwa lengo la kuongeza akiba ya taifa ya chakula kwa Kanda ya Kati yenye kuhudumia mikoa ya Dodoma, Singida kutoka uwezo wake wa sasa wa kuhifadhi, tani elfu thelasini na tisa (39,000) hadi kufikia tani elfu hamsini na tisa (59,000). 

Mradi wa ujenzi wa vihenge hivyo vya kisasa, ulizinduliwa rasmi tarehe 24 Aprili, 2018 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na ulianza rasmi Mwezi Juni 2018 huku Kampuni ya Feruum kutoka nchini Poland ndiyo iliyoshinda zabuni ya ujenzi huo. 

Akijibu swali la Mhe. Mgumba, Mhandisi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bwana Iman Nzobonaliba amesema Mradi unataraji kuisha kwa wakati mnamo Mwezi Disemba 2019. 

Akijibu swali la Naibu Waziri Mgumba ambaye alitaka kufaham namna Wakala ilivyojianda kununua mazao ya Wakulima katika msimu wa kilimo wa 2019/2020 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bwana Milton Lupa amemwambia Naibu Waziri Mgumba kuwa NFRA imeanza zoezi la kununua chakula cha ziada kutoka kwa Wakulima tangu tarehe 17 Juni 2019 katika Kanda ya Makambako na Sumbawanga na kwamba kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kitatumika kwa sasa. 

Bwana Lupa amesema NFRA imejipanga kutumia bajeti ya kiasi cha bilioni 15 pamoja na kuomba mkopo kutoka Benki ya Kilimo wenye riba nafuu na kuongeza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 62.6 zitatumika kwa ununuzi wa nafaka kwa msimu wa kilimo wa 2019/2020. 

Akizungumzia bei ya kununulia mahindi kwa kilo, Mtendaji Mkuu amesema bei ya ununuzi itakuwa ikitofautiana kutoka eneo moja na eneo linguine. 

“Niseme tu kuwa tutaanza na bei ya shilingi 400 hadi 500 kwa kila kilo moja ya mahindi lakini bei hii pia itakuwa ikibadilika kutokana na sababu mbalimbali” Amekaririwa Bwana Milton Lupa. 

Naibu Waziri Mgumba ameongeza kuwa NFRA ni Taasisi ya Serikali na imeaminiwa kusimamia jukumu la uhifadhi wa chakula na kuwa Taifa linatarajia makubwa katika kuhakikisha Taifa linakuwa na akiba ya chakula ya kutosha. 

“Sisi kama Viongozi wenu, hatuna shaka na uzoefu wenu na umahiri wenu katika nyanja ya uhifadhi wa chakula hususan nafaka kama mahindi, endeleeni mbele na sisi tutahakikisha mnapata mahitaji yenu, nawahakiki kuwa fedha za ununuzi mtazipata kwa kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imetuahidi kuwa zitakuja mapema kama mlivyopanga” Amekaririwa Mhe. Mgumba

Songas yawekeza kuwawezesha wakazi wa fukwe

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songas Tanzania, Nigel Whitaker (Watatu kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 108 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sea Sense, Joana Trindade (watatu kulia), kwa ajili ya wa kuchangia TZS 108 milioni kudhamini programu ya mafunzo ya mwaka mmoja kuwawezesha wananchi katika kisiwa cha Kilwa kupata elimu ya utunzaji wa fukwe na uvuaji salama mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Songas imetoa msaada wa shilingi huo kama jitihada za kudumisha viumbe hai na kuchochea ukuwaji wa sekta ya uvuvi nchini. Wa mwisho upande wa kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara na ufuatiliaji, Sebastian Kastuli na Mshauri wa masuala ya kiufundi, Bi. Lindsey West. (wamwisho kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songas Tanzania, Nigel Whitaker (wapili kushoto aliekaa) akisaini mkataba na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sea Sense, Joana Trindade (wa kati aliekaa), kwa ajili ya wa kuchangia TZS 108 milioni kudhamini programu ya mafunzo ya mwaka mmoja kuwawezesha wananchi katika kisiwa cha Kilwa kupata elimu ya utunzaji wa fukwe na uvuaji salama mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Songas imetoa msaada wa shilingi huo kama jitihada za kudumisha viumbe hai na kuchochea ukuwaji wa sekta ya uvuvi nchini. Wa mwisho upande wa kushoto alieketi ni Afisa Mkuu wa Biashara na  ufuatiliaji, Sebastian Kastuli na Mshauri wa masuala ya kiufundi, Bi. Lindsey West (wapili kulia), wengineo ni wafanyakazi wa kampuni ya songas .

MAANDALIZI YA TAIFA STARS-MISRI

$
0
0
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars,inaendelea vizuri na matayarisho yake kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa michuano ya Mataifa Afrika dhidi ya Senegal,Juni 23 mwaka huu katika Uwanja wa 3o June Cairo.

Kutokana na maandalizi yanayoendelea hadi sasa katika kikosi hicho,benchi la ufundi lina imani kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa ufunguzi na michezo mingine dhidi ya Kenya na Algeria.

Pamoja na wachezaji hao kufanya mazoezi ya uwanjani,pia wamekuwa wanafundishwa mbinu mbalimbali nje ya uwanja kwa kutumia mikanda mbalimbali ya video kuwasoma wapinzani wao,kabla ya kuanza kutupa karata yake rasmi katika mashindano hayo.

Kwa upande wa majeruhi,hadi sasa mchezaji ambaye hatoweza kushiriki mashindano hayo ni Aggrey Morris,ambaye nafasi yake imechukuliwa na David Mwantika,ambaye tayari ashawasili ndani ya kambi tayari kwa ajili ya mashindano.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Emmamuel Amuneke,kimeweka kambi nchini Misri tangu Juni 7,kwa ajili ya kuweza kupata nafasi ya kufanya maandalizi ya kina kabla ya kuanza kwa mashindano hayo

TanFootball




TAWA YAJIPANGA KULIPANDISHA HADHI ENEO LA ZIWA NATRON

$
0
0

 Wajumbe wa Bodi ya TAWA wakiangalia baadhi ya viumbe na Samaki aina ya Alcolapia wanaopatikana Ziwa Natron RAMSAR SITE lilipo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.
Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk. James Wakibara akijambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jeneral Mstaafu Hamis Semfuko, Bodi hiyo ilitembelea eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba. 
 Mkuu wa wilaya ya Longido mkoani Arusha Frank Mwaisumbe mwenye (Kaunda suti) akiwa na Wajumbe wa Bodi ya TAWA wakiongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko kulia. Bodi hiyo ilitembelea eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.

 Muikolojia wa eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE John Sule akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko kushoto, wajumbe wa bodi hiyo wametembelea eneo hilo linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori Tengefu ili kuliongezea thamani ya kiutalii. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko akiruka maji kwenye eneo chepechep la Ziwa Natron RAMSAR SITE lilipo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori Tengefu.

Na Ripota Wetu, ARUSHA

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imejipanga kulipandisha hadhi eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE kutoka aneo la ardhi owevu na kuwa eneo maalumu la Uhifadhi.

Hatua hiyo imelenga kunusuru hatari ya kutoweka kwa ndege maarufu duniani aina ya flamingo kutokana na shughuli mbalimbali za kibinaadamu zinazoendelea kufanywa pembezoni mwa Ziwa hilo. 

Bodi ya TAWA ikiongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko imetembelea eneo hilo na kujionea hali halisi ya mazingira na maisha ya viumbe hai wanaopatikana eneo hilo maarufu duniani.

Eneo hilo ni maarufu duniani kwa kuwa na makazi Heroe wadogo kwa asilimia 100 wanaopatikana Afrika Mashariki na mazalia ya asilimia 80 ya Heroe wadogo wanaopatikana eneo hilo pamoja na aina tatu ya za Samaki aina ya Alcolapia.

Aidha eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE pia limekuwa muhimu kwa utalii wa ndege aina ya Heroe Afrika Mashariki.



BENKI YA MAENDELEO TIB YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUINGIA MKATABA WA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (katikati) akimkabishi mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Charles Singili (kulia) mara baada ya kuuzindua mkataba huo. Uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya TIB.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto) akimkabidhi nakala ya mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) Bw.Joseph Kidaha (katikati) mwakilishi wa wateja waliohudhuria uzinduzi rasmi wa Mkataba huo. 
 Mkurugenzi, Mkakati na Mahusiano ya Kibiashara, Bw. Patrick Mongella (kulia) akipokea nakala za Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Charles Singili (katikati) akionesha mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) mara ya kukakidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto). Anayeshuhudia ni mmoja wa wateja wa benki hiyo, Bw.Joseph Kidaha (kulia).
 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakifuatilia uzinduzi Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter).
Baadhi ya wateja wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (katikati waliokaa) pamoja na menejimenti ya benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Charles Singili (wapili kulia waliokaa).

Na Mwandishi wetu
Benki ya Maendeleo TIB (TIB Development Bank) imeadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza kuadhimishwa tarehe 16 Juni, 2019 kwa kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customers’ Service Charter) ili kuendeleza kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wateja wake.
Akizungumza wakati wa unzinduzi wa Mkataba huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Dkt. Mary Mashingo amesema kuwa malengo ya Mkataba huo ni kuendeleza kutoa huduma bora bila ya upendeleo, kwa heshima na kwa haraka.
“Huu ni Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unaakisi dhamira ya dhati ya Benki ya kuwahudumia wateja bila ya upendeleo, kwa heshima na kwa haraka. Mkataba huu una ahadi za huduma mahsusi na za hiari.
Aliongeza kuwa Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unatambua wateja wetu wana haki ya kuelewa kiwango cha huduma kinachotolewa na Benki yao kwa wakati wote.
Kwa mujibu wa Dkt. Mashingoo, Benki iko tayari kupokea maoni ya namna ya kurekebisha na kuboresha zaidi huduma zake.
“Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo TIB, tumejipanga kusimamia kwa dhati utekelezaji wa mkataba huu katika kutekeleza dhamira  ya Mheshimiwa  Rais ya  kuwa  na  taasisi za umma zinazowahudumia  wadau wake. Watumishi  wa  Benki mnatakiwa kufanya kazi  kwa weledi,  juhudi,  maarifa  na uadilifu  mkubwa.  Pamoja na utoaji wa huduma bora, kwa haraka na kwa staha ili kuwaondolea wananchi usumbufu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Charles Singili alisema kuwa TIB imejidhatiti katika kuimarisha mahusiano nawateja wake, hivyo kuzinduliwa kwa Mkataba huu kutachochea utendaji kazi wake ikizingatiwa kuwa benki hiyo muhimili muhimu katika kuunganisha Serikali na Sekta Binafsi.
“Zipo Benki za biashara lakini hii ya TIB ni tofauti kabisa kwa kuwa yenyewe imejikita katika kuleta maendeleo kwa wateja na watanzania kwa ujumla. Hivyo, mkataba huu utaimarisha mahusiano na wateja wetu,” amesema.
Ameongeza kuwa TIB ni benki kiunganishi muhimu kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kwa kuchagiza uchangiaji kwa kiasi kikubwa katika masuala ya uwekezaji.
Akizungumzia kaulimbiu ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019, isemayo “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi.” Bw. Singili ametoa wito kwa vijana kutumia uwepo wa taasisi wezeshi ili waweze kujikwamua katika kuinua vipato vyao na taifa kwa ujumla.
“TIB tumejikita katika kuwasidia vijana waweze kusimamia misingi ya utawala bora lakini pia kuangalia kwa namna ambavyo wanaweza kuzalisha mazao mbalimbali hali inayoweza kuwasaida kutimia malengo yao binafsi na ya serikali kwa ujumla hasa kupitia mkakati wa Tanzania ya viwanda,’’ alifafanua.
Kwa upande wa wateja wa benki hiyo waliowakilishwa na Bwa. Joseph Kidaha amesema kuwa, mkataba huo una maana kubwa kwa wateja wa benki hiyo huku akisisitiza kuwa,  ukisimamiwa vizuri utaleta manufaa makubwa kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
“Ni jambo zuri kuona mahusiano mazuri yanatengenezwa kati ya benki na wateja wake, hiyo itaamsha ari kwa watu katika kuitafuta hudumu ya benki hii na tulio wengi kutimiza matarajio tuliyojiwekea ,’’ alisema.
Bwana Kidaha aliwataka wadau kuja kukopa katika benki ya TIB na kufanya marejesho kwa muda unaostahili ili kuwafanya watanzania wengi waendelee kunufaika na mikopo ya benki ya maendeleo (TIB)

BODI YA TCRA, MENEJIMENT NA KAMATI YA MAUDHUI WATEMBELEA MAKTABA MPYA YA KISASA UDSM NA JENGO JIPYA LA KIWANJA CHA NDEGE CHA JULIU NYERERE TERMINAL 3 TBIII

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

BODI ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), pamoja na Menejimenti ya Mamlaka hiyo, zimemefanya ziara kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere ili kujionea jengo jipya la kiwanja hicho, Terminal III (TBIII), pamoja na Maktaba mpya na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.

Ziara hiyo iliyofanyika Ijumaa Juni 21, 2019 pia iliwahusisha wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA.

Akizungumzia nia ya ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba alisema, Mamlaka kama Mdhibiti na Msimamizi wa Mawasiliano nchini, imeona ni vema kutembelea taasisi hizo mbili kwani kuna mambo ya msingi yanayofanywa na taassi hizo yanahusiana moja kwa moja na huduma zinazotolewa na TCRA.

“Lengo la ujio wetu hapa Terminal III nikuangalia katika hatua hizi ambazo ujenzi umekamilika ni mahitaji yapi ambayo bado ili sisi tuongeze ushiriki wetu ili kuyakamilisha hususan katika mifumo ya mawasiliano.” Alsiema Mhandisi Kilaba.

Alisema wakiwa hapo TBIII wamepata fursa ya kuulizia hali ya mawasiliano kama imekamilika ambapo watoa huduma, TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo, Zantel, Halotel na hata Internet kama wako tayari.

“Huduma hizi ni muhimu sana na zinatakiwa ziwe kwenye maeneo kama haya kwa sababu zinawezesha hata kufanya utalii kuwa rahisi, mgei anapoingia hapa na anataka kwenda eneo Fulani la utalii lazima awasiliane, lakini pia TCRA inatoa masafa kwa ajili ya kuongozea ndege zinapotua na kuruka na lengo hasa ni kuhakikisha hakuna muingiliano katika huduma hizo." Alibainisha Mkurugenzi huyo Mkuu wa TCRA.

"Kuja kwetu kumetupa fursa ya kujifunza mengi kama ambavyo watanzania wanaweza kushuhudia kuwa kiwanja hiki ni kizuri, kinapendeza na mawasiliano yapo yanaendelea kukamilishwa na tumejionea hata Wifi point ipo.” Alifafanua Mhandisi Kilaba.

Aidha kuhusu Maktaba mya ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhandisi Kilaba alisema, Maktaba hiyo inatumia huduma za TCRA kwani moja ya huduma zitolewazo ni pamoja na Maktaba mtandao (e-library) na hili ni jambo jema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt.Jones Killimbe alisema, ziara hiyo imekuwa ni ya mafanikio makubwa kwani imewezesha timu nzima ya TCRA, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti, Wajumbe wa Kamati zinazosaidia kutekeleza majukumu kwenye mamlaka kwa pamoja wameelimika sana.

“Kiwanja hiki katika lugha ambayo ningeiazima ni flagship project….ni mradi wa kimkakati wa taifa hili... nikisema kimkakati ni kwasababu mojawapo ya masuala ya kiuchumi ya nchi yetu ni utalii, na nadhani huu utakuwa mlango mkubwa sio dirisha…utakuwa mlango mkubwa wa utalii na mchango wa utalii kwenye uchumi wetu utaongezeka sana.” Alisema Dkt. Killimbe.

Ziara hiyo imewezesha wajumbe kupata maelezo ya kina ya kukamilika kwa huduma mbalimbali kwenye jengo la TBIII hali kadhalika kwenye maktaba ya ksiasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaa,
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (mwenye shati jeupe), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba, (kulia), wajumbe wa Bodi na Kamati ya Maudhui ya TCRA wakiongozwa na Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa jingo la Terminal 3 (TBIII) la kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Juni 21, 2019.
 Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mhandisi Kilaba, wakitembelea eneo la kusubiri abiria la jingo la TBIII kabla ya kuingia ndani ya ndege. 
 Muonekano wa nje wa eneo la kuondokea abiria kwenye jingo jipya la TBIII la kiwanja cha ndege cha Julkius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Ujumbe wa TCRA ukipatiwa maelezo na Mhandisi Barton Komba (kulia), kuhusu wapi abiria anapaswa kuelekea mara tu baada ya kuingia eneo la kuondokea abiria.
 Mandhari ya sehemu ambayo abiria wa kawaida watakuwa wakisubiri kabla ya kupanda ndege.
 Eneo la udhibiti wa Pasipoti mara tu baada ya abiria kuwasili kwenye kiwanja hicho.
 Mhandisi Komba (kushoto), akimpitisha Mkurugenzi Mkuu wa TCRA eneo litakalotumika kudhibiti pasipoti.
 Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Bw. Jacob Tesha, akizunhumza jambo ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya huduma kwenye jingo hilo.
 Eneo la ku chek-inn.
 Picha ya pamoja.
 Msimamizi wa Maktaba mpya na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (eneo la nyaraka za serikali), akitoa maelezo kwa ujumbe wa TCRA ukiongozwa na Mwenyekiti wa bodi, Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba (mwenye nguo za kibuluu), wakati wa ziara ya kutembelea maktaba hiyo.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, TCRA), Bi. Valerie Msoka (kushoto) na mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Bw. Dreck Murusuri, wakiangalia jinsi maktaba ya kielektroniki (e-library)ya Maktaba ya kisasa ya UDSM inavyofanya kazi.
 Mkurugenzi Mkuu, TCRA, Mhandisi James M. Killaba (wapili kulia), akiangalia kwa makini jinsi maktaba ya kielektroniki (e-library) ya Maktaba ya kisasa ya UDSM inavyofanya kazi.
 Mwenyekiti wa bodi, Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba (mwenye nguo za kibuluu), pamoja na ujumbe wakiouongoza, wakiwa kwenye chumba cha maktaba ya kielektroniki (e-library) ya Maktaba hiyo ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Maktaba mpya ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt.Esther Ndenje Sichalwe (katikati), akiongoza ujumbe wa TCRA ulipotembelea maktaba hiyo Juni 21, 2019.
 Dkt. Sichalwe (kulia), akizungumza na Kaimu Mkuu wa Kitenmgo cha Mawasilian, Uhusiano na Elimu kwa Umma, TCRA, Bw. Semu Mewakyanjala, wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi James M. Kilaba, (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi wa Maktaba mpya ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Esther Ndenje Sichalwe (kulia), machapisho mbalimbali yanayoeleza shughuli za Mamlaka hiyo.
 Picha ya pamoja ya ujumbe wa TCRA mara baada ya kutembelea maktaba hiyo.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 22,2019


HALOTEL YAIPIGA JEKI TAIFA STARS AFCON

$
0
0
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa uhusiano kampuni ya simu Halotel Stella Pius wakati akizungumza katika harambee ya kuchangia Taifa Stars iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Halotel ilichangia shilingi Million 10, Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Halotel Hindu Kanyamala na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi. 

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza Afisa uhusiano kampuni ya simu Halotel Stella Pius mara baada ya kuzungumza na kuchangia katika harambee ya kuchangia Taifa Stars iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Halotel ilichangia shilingi Million 10, Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Halotel Hindu Kanyamala na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Susan Paul, wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Halotel katika harambee ya kuchangia timu ya Taifa Stars ambapo kampuni hiyo ilichangia Milioni 10/.

BALOZI JOSEPH SOKOINE AONGOZA WATUMISHI WA MAKAMU WA RAIS KUFANYA USAFI MAKULU DODOMA

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma leo imefanya usafi katika eneo la Makulu jijini Dodoma kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji, NEMC, Wadau mbali mbali wa mazingira pamoja na Wananchi wa Makulu.
Wananchi na Wadau wa Mazingira wakishiriki zoezi la usafi katika eneo la Makulu, Dodoma ambapo taka za mifuko ya plastiki zilipewa kipaumbele, zoezi hili liliandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi Umma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wakazi wa Makulu jijini Dodoma wakiwa na vifaa vyao vya usafi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa zoezi la usafi lililoratibiwa na Ofisi yake ikiwa Sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 
Wananchi na Wadau wa Mazingira wakishiriki zoezi la usafi katika eneo la Makulu, Dodoma ambapo taka za mifuko ya plastiki zilipewa kipaumbele, zoezi hili liliandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi Umma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali, Wadau wa mazingira na Wananchi mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika eneo la Makulu Dodoma, zoezi hilo liliratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali, Wadau wa mazingira na Wananchi mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika eneo la Makulu Dodoma, zoezi hilo liliratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (mwenye kofia) akiongoza watumishi wa ofisi yake pamoja na wananchi wa Makulu, Dodoma kufanya usafi ikiwa sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (mwenye kofia) akiongoza watumishi wa ofisi yake pamoja na wananchi wa Makulu, Dodoma kufanya usafi ikiwa sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SERIKALI KUIMARISHA MAFUNZO KWA WALIM WA MICHEZO-

$
0
0

JOSEPH MPNAGALA-MTWARA

Serikali imesema itaendelea kuimarisha Mafunzo kwa walim wa michezo ili kuweza kuwa na Walim watakaoweza kuibua Vipaji vya wanafunzi Mashuleni na kuweza kusaidia Taifa katika michezo mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi na Prf.Joyce Ndalichako wakati akifunga mafunzo ya Copa cocacola UMISETA yaliyomaliziaka katika Uwanja wa Umoja Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

Prf.Ndalichako amesema michezo ya umiseta imekuwa ikiibua vipaji mbalimbali kutoka kwa vijana na wapo waliofanikiwa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa hivyo serikali itaendelea kuimarisha michezo.

“Tunafaham Kwamba michezo inasaidia kuimarisha afya michezo inasaidia kupunguza na kuepusha kupata magonjwa yasiyoambukiza lakini kwa wanafunzi Michezo inasaidia kuchangamsha akili”amesema PRf Ndalichako.

Naye Meneja Maendeleo ya Biashara Kampuni ya Coca Cola Yassin Hussein amesema ili kuhakikisha Mazingira yanatunzwa kampuni yake imeanzisha kampeni ya Rejesha na Ushinde ambapo Wanafunzi wanashindana kukusanya Chupa za zilizotumika.

“Kampeni yetu ya cocacoLA vijana wameweza kukusanya Chupa za Plastic zilizotumika zoezi ambalo tumelianzisha mwezi June na litamalizika mwezi wa Nane ili kuhakikisha tunatunza mazingira na nchi yetu inabaki salama”amesema Yassin.

Michezo ya Umeseta imeshirikisha Mikoa26 ambapo Fainali zilikutanisha Timu ya Songwe na Ruvuma ambapo Timu ya Ruvuma Ilishinda kwa mikwaju ya penati 10 kwa 9 .

Baadhi ya wanfunzi wa kutoka shule mbalimbali za sekondari wakionesha ishara ya kumalizika kwa mashindano ya Copa Coca Cola ambayo yalimalizika katika Uwanja wa Umoja Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Mkoa wa Ruvuma wakimnyanyua Juu Kipa wa Timu hiyo baada ya Kufanikiwa kupangua Mkwaju wa Mwisho uliyoipa Timu ya Mkoa wa Ruvuma Ushindi.

Washindi wa Promo ya Tigo AFCON wapata baraka za Serikali

$
0
0
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Yusuf Singo (kushoto) akimkabidhi Godfrey Muta (kulia) mbaye ni mmoja wa washindi wa Promosheni ya Soka la Afrika inayoendeshwa na kampuni ya Tigo bendera ya Taifa kwa ajili ya kwenda kushuhudia Michuano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri. Anayeshuhudia katikati ni Afisa Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Yusuf Singo (kushoto) akiwa na baadhi ya washindi wa Promosheni ya Soka la Afrika inayoendeshwa na kampuni ya Tigo muda mfupi baada ya kuwakabidi bendera ya Taifa kwa ajili ya kwenda kushuhudia Michuano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri. Wa kwanza kulia ni Afisa Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf.
 Afisa Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi bendera ya Taifa baadhi ya washindi wa promosheni ya Soka la Afrika watakaokwenda Misri kushuhudia michuano ya mataifa ya Afrika. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Yusuf Singo na kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisael.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Yusuf Singo (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi bendera ya Taifa baadhi ya washindi wa promosheni ya Soka la Afrika watakaokwenda Misri kushuhudia michuano ya mataifa ya Afrika. Kulia ni Afisa Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf na kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisael.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Yusuf Singo (kushoto) akimkabidhi Kalaghe Rashid (kulia) mbaye ni mmoja wa washindi wa Promosheni ya Soka la Afrika inayoendeshwa na kampuni ya Tigo bendera ya Taifa kwa ajili ya kwenda kushuhudia Michuano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri. Anayeshuhudia katikati ni Afisa Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf.




WAZIRI WA UTUMISHI WA UMMA, VIJANA NA JINSIA JAMHURI YA KENYA AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA UTHUBUTU WA UJENZI WA SGR.

$
0
0
Banda la Shirika la Reli Tanzania - TRC lilipo katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma Barani Afrika katika viwanja vya KICC jijini Nairobi nchini Kenya Limepata fursa ya kutembelewa na Waziri wa Utumishi wa Umma,Vijana na Jinsia Mheshimiwa, Dokta Margaret Kobia juni 22, 2019.

Lengo la ziara ya Waziri katika maadhimisho haya kwa nchi za bara la Afrika ni kufahamu majukumu ya taasisi za utumishi wa umma zilizoshiriki,maendeleo na ubunifu unaoleta tija katika nchi zilizoshiriki kutoka nchi tofauti barani Afrika.

Kupitia ziara hiyo Mheshimiwa Waziri alisifu uthubutu alioufanya Mh.Rais Dokta John Pombe Magufuli katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa-SGR.

Pia Waziri amepata fursa ya kufahamu Huduma zitolewazo na TRC pamoja na miradi mikubwa inayosimamiwa na Shirika la Reli yaani Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR,Uboreshaji wa Reli ya kati na miradi mingine kama Ufufuaji wa njia ya reli Tanga, Arusha ba Moshi pamoja na Mradi wa treni za kisada za Mijini ambazo TRC imeanza na jiji la Daresalaam na Dodoma.

Maadhimisho haya ya Utumishi wa umma barani Afrika yaliyobebwa na kauli mbiu Uhusiano kati ya uwezesha vijana na usimamizi masuala ya uhamiaji, kujenga utamaduni wa utawala Bora, matumizi ya Tehama na ubunifu katika utoaji utoaji huduma jumuishi.

Washiriki kutoka Tanzania ni taasisi zilizo chini ya serikali kuu ambapo maadhimisho haya yameandaliwa na kuongozwa na Ofisi ya Rais Utumishi, Taasisi hizo ni zilizoshiriki ni Shirika la reli Tanzania-TRC, Mamlaka ya chakula na Dawa-TFDA, Bohari ya Dawa Tanzania-MSD.

Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika yanatarajia kufungwa juni 23, 2019 katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari  na Uhusiano TRC Bi Jamila Mbarouk  akitoa  Maelezo na ufafanuzi  kwa Waziri wa Wizara ya Utumishi wa Umma, Vijana na Jinsia, Jamhuri ya Kenya  Dkt.Margaret Kobia  (Wa pili kushoto)kuhusu Huduma zitolewazo na TRC pamoja na miradi inayosimamiwa katika maadhimisho  ya wiki ya utumishi wa umma mjini Nairobi nchini Kenya katika viwanja vya KICC  leo juni 22, 2019.
 Mhandisi Tito Mateshi kutoka TRC akitoa  Maelezo  kwa Bi Hytham Amour kuhusu miradi inayosimamiwa na TRC pamoja na huduma zitolewazo katika maadhimisho  ya Wiki  ya wiki ya utumishi wa umma jijini Nairobi nchini katika viwanja vya KICC juni 22, 2019.
Watumishi wa  Shirika la Reli Tanzania -TRC wakimpokea mdau  Bi Lilian John, tayari kwa kumpatia maelezo kuhusu Huduma zitolewazo  pamoja na miradi inayosimamiwa na TRC katika maadhimisho  ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika  yanayoendelea  jijini Nairobi, nchini Kenya juni 22, 2019.
Baadhi ya Wadau jijini Nairobi  walipotembelea banda la Shirika la Reli  Tanzania -TRC kwa ajili ya kupata uelewa kuhusu  Huduma na Miradi inayosimamiwa na TRC katika viwanja vya KICC  jijini Nairobi  nchini Kenya juni 22, 2019.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI BONANZA NA BENKI YA NMB NA WABUNGE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua timu ya Mpira wa kikapu ya Benki ya NMB ambayo ilipambana na timu ya Bunge katika mechi la Bonanza la Benki ya NMB na Bunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha mpira wakati lipoanzisha mechi ya mpira wa kikapu ya Bonanza na Benki ya NMB na Wabunge kati ya timu ya Bunge na NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Bunge wakiwa wamejipanga kabla ya mechi kati yao na timu ya Benki ya NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WATUMISHI NI MUHIMU KUSHIRIKI MICHEZO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni muhimu kwa watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali kwa kuwa inaimarisha afya pamoja na kudumisha mshikamano.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 22, 2019) wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya NMB lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema mbali na kuimarisha afya kwa watumishi na wabunge, pia michezo inasaidia katika kuimarisha mshikamano baina ya benki hiyo pamoja na wateja.Akizungumzia kuhusu utendaji wa benki ya NMB, amesema imekuwa ikishirikiana na Serikali kuwaelimisha wakulima umuhimu wa kufungua akaunti na kujiwekea akiba.

“Benki ya NMB ni benki pekee iliyomudu kufungua matawi hadi maeneo ya vijijini, hivyo kurahisha upatikanaji wa huduma kwa watumishi na wananchi waishio maeneo hayo.”Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya Bunge ilishinda baada ya kuifunga timu ya benki ya NMB magoli matano kwa matatu. 

Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya NMB magoli 25 kwa 18, huku katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya NMB ilishinda baada ya kuifunga Bunge vikapu 52 kwa 51.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za NMB.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI BONANZA LA NMB,AKABIDHI KOMBE TIMU YA BUNGE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kikombe nahodha wa timu ya soka ya Bunge, Cosato Chumi baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya timu ya NMB katika mchi ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. Kushoto ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,wa tatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NMB Bw. Albert Jonkergouw .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto) na wa tatu kulia Kaimu Mkurugenzi wa NMB Bw. Albert Jonkergouw wakimtazama nahodha wa timu ya Soka ya Bunge, Cosato Chumi aliponyanyua kikombe cha ushindi wa mechi ya soka ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. Bunge ilishinda 5 - 3. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Martin Massawe wa NMB akimlamba chenga Abdallah Aman wa Bunge (kushoto) katika mechi ya soka ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 22, 2019. Bunge ilishinda 5-3.
Abdallah Aman wa Bunge (kushoto) akizuia mpira huku akizongwa na Martin Massawe wa Bunge katika mechi ya soka ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 22, 2019. Bunge ilishinda 5-3.

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI MISA TAKATIFU YA MAADHIMISHO YA SHEREHE EKARISTI TAKATIFU KANISA LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Padre Dkt. Alister Makubi, Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam baada ya kushiriki Misa ya Maadhimisho ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu kanisani hapo katika leo Jumapili Juni 23, 2019. Katikati ni Paroko Msaidizi wa kanisa hilo Padre Paul Haule na Mzee wa Kanisa Dkt. Aldehem Meru
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki katika Misa ya Maadhimisho ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Juni 23, 2019

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MKONO WA POLE KWA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR KWA KUFIWA NA MKE WAKE JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) Mikocheni jijini Dar es salaam ambaye amefiwa na mkewe Dkt. Badria Abubaker Gunar aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiomba dua maalumu na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) pamoja na familia yake nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar es salaam kumuombea marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar(Mke wa Naibu katibu mkuu CCM Znz) aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu wa Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa pili wa Rais wa Znz Balozi Sefu Ali Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi  na Viongozi mbalimbali wa  Serikali na Chama cha Mapinduzi wakimuombea dua marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimsikiliza Gavana wa Benki Kuu Profesa Frolence Luoga akizungumza mara baada ya dua maalumu ya kumuombea marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) ambaye pia alikuwa ni mtumishi wa Benki Kuu (BOT) ,aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiwa msibani wakati wa dua maalumu ya kumuombea marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) ambaye pia alikuwa ni mtumishi wa Benki Kuu (BOT) ,aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na Mdau wa Michezo Mzee Kilomoni  pamoja na waombolezaji wengine mara baada ya dua maalumu ya kumuombea marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) ambaye pia alikuwa ni mtumishi wa Benki Kuu (BOT) ,aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) mara baada ya kumpa pole kufuatia kifo cha  mkewe Dkt. Badria Abubaker Gunar Mikocheni Jijini Dar es salaam, aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

RAIS DKT MAGUFULI AHANI MSIBA FAMILIA YA ABBAS TARIMBA LEO JIJINI DAR

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisalimiana na mke wa Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwao Kinondoni ambao hivi karibuni wamefiwa na watoto wao wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendani wa SportPesa Bw. Abbas Tarimba Abbas alipofika kuhani msiba nyumbani kwake Kinondoni Hananasifu jijini Dar es salaam ambapo hivi karibuni wamefiwa na watoto wao wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwake Kinondoni ambaye hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es
salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza na Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwake Kinondoni alipokwenda kuhani msiba ambapo hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki
iliyopita jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimpa mkono wa pole Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwake Kinondoni alipokwenda kuhani msiba ambapo hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwake Kinondoni alipokwenda kuhani msiba ambapo hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es salaam

Vodacom watunukiwa tuzo ya NEEC

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Kassim Majaliwa (Kulia) akimpongeza na kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Rosalynn Mworia (kushoto) kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kuinua wananchi kiuchumi wakati wa semina ya uwezeshaji wananchi kiuchumi uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Rosalynn Mworia akizungumza na wadau mbalimbali wa masuala ya kiuchumi katika semina ya uwezeshaji wananchi kiuchumi iliyofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

MAJALIWA AISIFU NMB KWA KUIUNGANISHA JAMII KWA HUDUMA ZAKE

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Mpira wa Kikapu ya Benki ya NMB – Danford Kisinda baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa vikapu 54-52 dhidi ya timu ya mpira wa Kikapu ya Bunge katika mechi ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma mwishoni mwa juma. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya soka ya Bunge, Cosato Chumi baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya timu ya NMB katika Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma mwishoni mwa juma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Tulia Ackson na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB wakiwa pamoja na timu ya Bunge la  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakifurahia ushindi wa timu za bunge kwenye Bonanza la michezo la NMB na Bunge lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma mwishoni mwa juma.

Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB akishangilia ushindi wa Mpira wa Kikapu baada ya kuwashinda timu ya Bunge kwa Vikapu 54 kwa 52 kwenye Bonanza la michezo la NMB na Bunge lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma mwishoni mwa juma.
 
……………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesifu juhudi za Benki ya NMB kwenye kuunganisha jamii kupitia huduma bora za kibenki, matukio ya michezo na hata misaada mbalimbali nia ikiwa kuona jamii ya kitanzania inashiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa Taifa. 

Alitoa kauli hiyo juzi jijini Dodoma kwenye Bonanza la michezo lililowashirikisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wafanyakazi wa Benki ya NMB. Akizungumzia kuhusu utendaji wa benki ya NMB, amesema imekuwa ikishirikiana na Serikali kuwaelimisha wakulima umuhimu wa kufungua akaunti na kujiwekea akiba. 

“Benki ya NMB ni benki pekee iliyomudu kufungua matawi hadi maeneo ya vijijini, hivyo kurahisishha upatikanaji wa huduma kwa watumishi na wananchi waishio maeneo hayo.” Amesema ni muhimu kwa watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali kwa kuwa inaimarisha afya pamoja na kudumisha mshikamano. 

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya Bunge ilishinda baada ya kuifunga timu ya benki ya NMB magoli matano kwa matatu. Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya NMB magoli 25 kwa 18, huku katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya NMB ilishinda baada ya kuifunga Bunge vikapu 54 kwa 52. 

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za NMB.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images