Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAWA MWENYEJI WA MAFUNZO YA UKAGUZI WA KODI

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akifungua rasmi mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na African Tax Administration Forum (ATAF). Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika
Meneja wa Mafunzo ya Ukaguzi wa Kodi kutoka African Tax Administration Forum (ATAF) Caroline Mutayabarwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na ATAF ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika. Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019.
Baadhi ya Wakaguzi wa Kodi kutoka Mamlaka za Mapato Afrika wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na African Tax Administration Forum (ATAF) ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika. Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019
Wakaguzi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na African Tax Administration Forum (ATAF) ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika. Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya menejimenti ya TRA, wakufunzi na wakaguzi wa kodi mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na ATAF ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika. Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KUKAGUA UJENZI WA DARAJA LA TANZANITE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa daraja linalokatiza baharini na kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipatiwa maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee 

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KUKAGUA UJENZI WA DARAJA LA TANZANITE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa daraja linalokatiza baharini na kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipatiwa maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee 

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KUKAGUA UJENZI WA DARAJA LA TANZANITE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa daraja linalokatiza baharini na kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipatiwa maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee 

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KUKAGUA UJENZI WA DARAJA LA TANZANITE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa daraja linalokatiza baharini na kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipatiwa maelezo ya ujenzi huo na Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Yoosin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee 

WAZIRI MKUU AFUNGUA TAWI LA BENKI YA UWEKEZAJI TANZANIA (TIB )

$
0
0






Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifungua Ofisi na Tawi la Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), katika jengo la PSSSF jijini Dodoma, Juni 24.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe, wakati akifungua Ofisi na Tawi la Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), katika jengo la PSSSF jijini Dodoma, Juni 24.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifungua akaunti katika Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), baada ya kufungua Ofisi na Tawi la Benki, katika jengo la PSSSF jijini Dodoma, Juni 24.2019. Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja Elizabeth Mkondya.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihifadhi fedha baada ya kufungua akaunti katika Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), baada ya kufungua Ofisi na Tawi la Benki ya Benki hiyo, iliyopo katika jengo la PSSSF jijini Dodoma, Juni 24.2019. Kushoto ni mtoa huduma wa fedha, Nasra Namkudai.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kufungua Ofisi na Tawi la Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), katika jengo la PSSSF jijini Dodoma, Juni 24.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji, wakati wa ufunguzi wa Ofisi na Tawi la Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), katika jengo la PSSSF jijini Dodoma,

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA GHALA NA MITAMBO YA GESI YA KAMPUNI YA TAIFA GAS TANZANIA LIMITED KIGAMBONI, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz kuangalia Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo kabla ya kuvizindua huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya kuchakata Gesi ya LPG vya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz alipowasili kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz baada ya kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Hamisi Ramadhani wakisiliza maelezo ya namna mitambo ya kuchakata gesi inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019. PICHA NA IKULU

UNILEVER YAKAMILISHA KAMPENI TOA MKONO WA KA KWA KUSAIDIA YATIMA,WAZEE WASIOJIWEZA

$
0
0
Meneja Bidhaa ya Omo ya Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (kushoto) akimkabidhi msaada wa sabuni, Sukari na Nguo kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto yatima cha Children`s Home Msimbazi, Sista Etienne katika kuhitimisha Kampeni ya Kampuni hiyo ya Toa Mkono wa Ukarimu iliyofanyika Kipindi cha mwezi wa Ramadhani uliomalizika hivi karibuni. . Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Bidhaa ya Omo wa Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (katikati) akimkabidhi msaada wa sabuni, sukari na nguo Ofisa Mfawidhi wa Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge, Jacklina Kanyamwenge katika kuhitimisha kampeni ya kampuni hiyo ya ‘Toa Mkono wa Ukarimu’ iliyofanyika kipindi cha Mwezi wa Ramadhani. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni Nunge, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Christabella Msangi na Nurdin Ally walioambata na meneja huyo.
Mmoja wa wazee wanaoishi katika Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge, Vumilia Chambusho (kulia), akipokea msaada wa baadhi ya vyakula, nguo na sabuni kutoka kwa Meneja Bidhaa ya Omo wa Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (watatu kushoto) vilivyotolewa na Unilever katika kuhitimisha kampeni ya kampuni hiyo ya ‘Toa Mkono wa Ukarimu’ iliyofanyika kipindi cha Mwezi wa Ramadhani. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni hapo, Nunge, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Christabella Msangi na Nurdin Ally walioambata na meneja huyo.
Meneja wa Bidhaa ya Omo wa Kampuni ya Unilever, Upendo Mkusa (kushoto) akisalimiana na baadhi ya wazee wanaoishi katika Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge baada ya kukabidhi msaada wa sabuni, sukari na nguo vilivyotolewa na Unilever katika kuhitimisha kampeni ya kampuni hiyo ya ‘Toa Mkono wa Ukarimu’ iliyofanyika kipindi cha Mwezi wa Ramadhani. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni Nunge, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

KAMBI MAALUM KWA WANAWAKE WENYE MAKOVU,ULEMAVU ULIOTOKANA NA VURUGU MAJUMBANI AU AJALI KUFANYIKA JUMAMOSI HII KISARAWE

$
0
0




KISARAWE PWANI Juni, 2019. Programu ya Reconstructive Women and Children ni jitihada ya ushirikiano kati ya Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam (AKHD), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) pamoja na shirika la kibinadamu la Reconstructing Women International (International Confederation for Plastic, Reconstructive and Aesthetic Surgery) ili kutoa huduma ya upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile au ngozi iliyokakamaa kwa wanawake na watoto wa kike maskini wenye ulemavu uliosababishwa na ukatili wa majumbani, kuungua na ajali.


 Ushirikiano huu unalenga kubadlishana na kuimarisha utaalamu wa upasuaji kwa ajili ya kushughulikia hitaji la kitiba la upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile katika maeneo mbalimbali ya Tanzania na Kanda ya Afrika Mashariki. 


Programu hii ilianzishwa mnamo Januari 2016 ikihusisha wapasuaji kutoka Marekani, Canada na Ulaya wakifanya kazi kwa karibu na wanatiba wa Kitanzania. Tangu hapo, kupitia awamu NNE, operesheni 143 za upasuaji zimefanywa bila gharama yoyote kwa wagonjwa (ambao ni wahanga wa ukatili wa majumbani, kuungua na ajali), na kurejesha utendaji wa kimwili na mwonekano wa wanawake na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. 


Kwa kuwa upasuaji huu  wa kuboresha maumbile, ngozi iliyokakamaa, umeonesha kuboresha kwa kiwango kikubwa maisha ya wale wanaosumbuliwa na unyanyapaa na ulemavu, Hospitali ya Aga Khan na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinayo furaha kushirikiana kwa mara nyingine tena katika mradi huu wa kipekee. 


Kambi kubwa ya uchunguzi ili kuwatambua wagonjwa wenye uhitaji kwa ajili ya awamu ya 5 Hospitali ya Aga Khan  Muhimbili pamoja na shirika la SADAKA network  Tunapanga kuwa na kambi hii kwa mara ya kwanza kabisa wilayani Kisarawe .kambi hii itafanyika  hospitali ya wilaya ya kisarawe na mganga mkuu wa wilaya ya kisarawe atakuwepo  na kambi hii imepewa Baraka zote na Halmashauri ya wilaya ya kisarawe 


Ambapo wanawake na watoto wenye ulemavu mbalimbali wanaalikwa kuhudhuria kambi hii ya tathmini ya awali; wataonwa na wataalamu waliobobea katika upasuaji wa Kubadili na Kuboresha Ngozi/Maumbile iliyokakamaa. 



KWA Mawasiliano 


AKH-D: Olayce S. Lotha, olayce.lotha@akhst.org, Simu: +255-717-516-650 


SD ; Viola Julius ,viola.m@sadakanetwork.com , simu : 0763858029

Benki ya Stanbic yatoa mafunzo kwa Meneja Rasilimali watu

$
0
0
 Mtaalamu wa masuala ya Kiuchumi,  Paulsen Mrina (kulia shati  la blue bahari) akiwaelezea Meneja Rasilimali Watu kutoka kampuni mbali mbali jinsi ya kutunza fedha, katika semina ya kuwawezesha kiuchumi iliyoandaliwa na Benki ya Stanbic Tanzania, Coral Beach Hotel, Dar es Salaam.
Meneja Rasilimali Watu kutoka kampuni mbali mbali wakijadili jambo katika semina kwaajili ya kuwapatia mafunzo ya kuwawezesha kiuchumi, iliyoandaliwa na Benki ya Stanbic Tanzania, Coral Beach Hotel, Dar es Salaam.

NAIBU SPIKA DKT. TULIA AZINDUA KITABU CHA 'VIWANDA: MOVING TANZANIA FORWARD' JIJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimpongeza mwandishi wa kitabu cha “Viwanda: Moving Tanzania Forward”, Pro. Teddy Maliyamkono mbele ya waheshimiwa wabunge, watumishi wa Ofisi ya Bunge na wageni waalikwa (hawapo kwenye picha) katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizindua kitabu cha “Viwanda: Moving Tanzania Forward” mbele ya waheshimiwa wabunge, watumishi wa Ofisi ya Bunge na wageni waalikwa (wote hawapo kwenye picha) katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni mwandishi wa kitabu hicho, Prof. Teddy Maliyamkono 
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na waheshimiwa wabunge, watumishi wa Ofisi ya Bunge na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha “Viwanda: Moving Tanzania Forward” katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA MAADILI NA USALAMA PAMOJA NA KAMATI KUU LUMUMBA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Maadili na Usalama cha chama kilichofanyika katika ofisi ndogo za Makao makuu ya Chama hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. June 26, 2019.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi kilichofanyika katika ofisi ndogo za Makao makuu ya Chama hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. June 26, 2019.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Ali Mohammed Shein mara baada ya kikao cha Maadili na Usalama pamoja na kikao cha Kamati kuu ya Chama hicho  vilivyofanyika katika ofisi ndogo za Makao makuu ya Chama hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. June 26, 2019.
PICHA NA IKULU

Tigo Business yatoa simu 247 na miavuli 100 kwa wamachinga Arusha

$
0
0



Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kati kati) akikabidhi moja ya boksi lenye simu 247 kwa viongozi wa wafanya biashara wadogo wadogo mkoani Arusha maarufu kama Wamachinga. Kulian ni mwenyekiti wa umoja huo Amina Njoka na kushoto ni makamu mwenyekiti Iddi Hussein.
Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kati kati) akikabidhi sehemu ya miavuli 200 kwa viongozi wa wafanya biashara wadogo wadogo mkoani Arusha maarufu kama Wamachinga. Kulian ni mwenyekiti wa umoja huo Amina Njoka na kushoto ni makamu mwenyekiti Iddi Hussein
Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi za simu 247 kwa viongozi wa wafanya biashara wadogo wadogo mkoani Arusha maarufu kama Wamachinga. Kulian ni mwenyekiti wa umoja huo Amina Njoka.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Tigo mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga muda mfupi bada ya kuwakabidhi simu 247 pamoja na miavuli 200 kwa ajili ya kusaidia kuboresha biashara zao jijini Arusha jana.



Kupitia Chama Cha Wamachinga Mkoa wa Arusha, leo tarehe 26/06/2019 kampuni ya Tigo kupiti kitengo chake cha Tigo Business imetoa simu 247 pamoja wa miavuli 100 kwa wateja wake ambao ni wanachama wa umoja huo wa wafanya biashara wadogo wadogo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwakabidi vifaa hivyo kwa wateja hao 247, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo alisema, zawadi hizo ni utaratibu wa kawaida wa kampuni hiyo kuwazawadia na kuwashukuru wateja wake waliopo kwenye vikundi na unalenga kuboresha biashara zao pamoja na mazingira wanayofanyia kazi.

“Leo kampuni ya Tigo inayofuraha kukabidhi vifaa hivi kwa wateja wetu ambao ni wanachama wa Umoja wa Wamachinga hapa mkoani Arusha. Ni utaratibu wetu wa kawaida kuwapa zawadi wateja waaminifu kama hawa na tunaamini vifaa hivi vitawasadia kuboresha biashara zao huku wakifurahia huduma bora kutoka Tigo,” alisema

Lilian alifafanua kuwa, kampuni ya Tigo hutoa zawadi mbali mbali ikiwamo simu za mkononi kwa wateja wa malipo ya baada waliopo kwenye vikundi na ambao hutumia huduma za Tigo wakiwa na mkataba wa miezi 12 au 24.

Ili mteja aweze kunufaika na zawadi hizi anatakiwa kujiandikisha kama mteja wa walipo ya baada (postpaid) na ni lazima awe katika kikundi au kampuni kubwa AU ndogo. Hivyo basi, tunakaribisha vikundi, makampuni pamoja na taasisi kwa ajili ya kupata huduma zetu nzuri na za uhakika za mawasiliano.

Meneja huyo pia aliwataka wanafuaika wa zawadi hizo kuendelea kutumia mtandao wa Tigo na kuongeza kuwa Tigo inajali na kuwekeza kwa wateja na wabia wake wa biashara ili kuhakikisha kuwa watanzania wote wawanufaika na huduma bora za mawasiliano.

Waziri Mkuu afungua Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Dodoma

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mvinyo, katika banda la Benki ya Maendeleo (TIB), kwenye Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Dodoma, lililofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Juni 27.2019. Tokea kushoto ni Meneja Maendeleo ya Biashara (TIB), Joseph Chilambo na Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati (TIB) Patric Mongela.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa mkoba uliyobuniwa na Wajasiriamali wa Kitanzania na Meneja Mzalishaji wa Fay Fashion Gregory Mlay, kwenye Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Dodoma, lililofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Juni 27.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, wakati akikagua mabanda, kwenye Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Dodoma, lililofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Juni 27.2019.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC na Afisa mkuu mpya wa Ufundi kutoa ushirikiano kwa Uongozi kampuni hiyo

$
0
0
 Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC Dkt Omary Nundu akisalimiana na Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania alipotembelea Makuu ya ya Airtel Tanzania yaliyopo jijini Dar es salaam mtaa wa Morocco. Mwenyekiti huyo ameahidi kushirikiana na uongozi kuhakikisha kampuni hiyo inayomilikiwa na watanzania kwa asilimia 49% inaleta tija kwa watanzania.
 Afisa Mkuu wa Ufundi mpya wa Airtel Tanzania Dkt Prospa Mafole (kati) na Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC Dkt Omary Nundu (kulia) wakisalimiana na mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso walipotembelea yaliyopo jijini Dar es salaam mtaa wa Morocco hivi karibuni. Mkuu huyo wa ufundi anaendelea na kazi sasa baada ya kuteuliwa na serikali ili kujiunga na uongozi uliopo wa Airtel kuhakikisha kampuni hiyo inayomilikiwa na watanzania kwa asilimia 49% inatoa huduma bora zaidi na kuipa serikali mwekezaji faida .
 Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC Dkt Omary Nundu (kulia) na Afisa mkuu mpya wa Ufundi Dkt Prospa Mafole wakisalimiana na Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania Sunili Colaso (kushoto) leo walipotembelea yaliyopo jijini Dar es Salaam mtaa wa Morocco. Mwenyekiti bodi na Afisa ufuni Mpya walioteuliwa na serikali kushika nyadhifa hizo wameahidi kushirikiana na uongozi kuhakikisha kampuni hiyo inayomilikiwa na watanzania kwa asilimia 49% inaleta tija kwa watanzania.
Wakwanza tokea kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akifuatiwa na Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC Dkt Omary Nundu na Afisa mkuu mpya wa Ufundi Dkt Prospa Mafole wakiwa kwenye kikao cha ukaribisho mara baada ya kutembelea Makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam mtaa wa Morocco leo na baadhi ya wakuu wavitengo mbalimbali wa Airtel Tanzania.

VIJANA WA KAMBI YA ARIEL WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI VYA IPP ,MAKUMBUSHO YA TAIFA

$
0
0

Watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Simiyu,Mwanza,Mara na Shinyanga wanaoshiriki Kambi ya Ariel 2019 leo Juni 27,2019 wametembelea Vyombo vya Habari vinavyomilikiwa na Kampuni ya IPP Media ambavyo ni ITV,Radio One, Capital Radio,Capital Tv,East Africa Tv ili kujifunza namna wanavyoendesha vipindi na kurusha matangazo.

Vijana na watoto hao pia wametembelea Makumbusho ya Taifa ili kujifunza historia ya mwanadamu na nchi ya Tanzania pamoja na kiwanda cha kutengeneza juisi kinachomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa ili kujionea namna uzalishaji unavyofanyika. 

Ziara hiyo inakuja baada ya watoto hao wanaoshiriki kambi ya Ariel 2019 ya wiki moja iliyoanza Juni 23,2019 jijini Dar es salaam, kujifunza darasani masuala ya VVU/UKIMWI, kukua, ujinsia,ujasiriamali na kujengewa ujasiri na kujiamini ili waweze kutimiza ndoto zao. 

Kambi ya Ariel 'Ariel Camp' inasimamiwa na asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) ambayo inafanya shughuli zake katika mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Simiyu na Mara. 
Kulia ni Mkurugenzi wa Radio One Stereo na Capital Radio ,Deogratius Rweyunga akiwaelezea vijana na watoto kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza na Mara wanaoshiri Ariel Camp 2019 namna wanavyoendesha vipindi vya radio. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mtangazaji wa kipindi cha Yaliyomo Yamo, Hatya Omary akiendelea na kipindi wakati vijana na watoto wa Ariel Camp 2019 walipotembelea studio ya Radio One. 
Meneja Mawasiliano wa asasi ya AGPAHI,Agnes Kabigi akizungumza 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'. Kabigi alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kukaa na watoto na kuwaeleza kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI. 
Kijana akielezea kuhusu VVU na UKIMWI 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'. 
Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Capital Radio, Abdallah Mwaipaya akitoa ufafanuzi namna wanavyoendesha vipindi vya radio. 
Hapa ni Control Room ITV: Kulia Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyoandaa vipindi vya Televisheni. 
Ndani ya chumba cha kurushia matangazo ITV na East Africa Tv: Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyorusha vipindi vya Televisheni. 
Hapa ni chumba cha kusomea taarifa ya habari ITV: Kulia ni Fundi wa ITV, Paul Urio akiwaonesha vijana na watoto namna wanavyoendesha vipindi vya habari. 
Vijana na watoto wakipiga picha na Mtangazaji wa Kipindi cha Habari za saa, Richard Stephen. 
Afisa Elimu Mwandamizi katika Makumbusho ya taifa,Anamery Bagenyi (aliyevaa nguo nyeupe) akielezea historia ya Makumbusho ya taifa yaliyoanzishwa mwaka 1940. Alisema katika Makumbusho hayo kuna maeneo matano ya kujifunza ambayo ni Chimbuko la Mwanadamu,jumba la maonesho ya kihistoria,jumba la michoro ya mapangoni na miamba,jumba la sanaa za kisasa,jumba la kumbukumbu ya ubalozi wa Marekani na Jumba la Baiolojia.
Kushoto aliyenyoosha mkono ni Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Samson Yohana akionesha gari (la kijani) la kwanza kutumiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya Taifa,Samson Yohana akionesha moja ya nyumba za kihistoria.

Vijana na watoto wakipiga picha ya pamoja nje ya jumba la makumbusho lililojengwa mwaka 1940 na Waingereza. 
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Samson Yohana simba aliyekaushwa. 
Vijana na watoto wakiwa katika jumba la makumbusho ya kihistoria. 
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha michoro iliyochorwa mapangoni. 
Vijana na watoto wakifurahia kinyago cha mwanamke anayetwanga vitu huku kabeba mtoto na kashikilia mtoto. 
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha picha ya binadamu aliyejitambua. 
Watoto wakisoma vitabu na kuangalia katuni kwenye vifaa vya kisasa katika Maktaba ya watoto katika makumbusho ya taifa. 
Watoto wakisoma vitabu kwenye Maktaba ya watoto katika makumbusho ya taifa. 
Vijana wakisaga unga wa ulezi kwa kutumia mawe katika makumbusho ya taifa. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 28,2019

Benki ya Azania yazindua Kampeni Ya ‘AMSHA NDOTO’ kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa Watanzania.

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Itembe Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Amsha Ndoto ‘Amsha Ndoto’ yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.Kulia kwake ni Mkurungezi wa Biashara wa Benki ya Azania Rhimo Nyansaho na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Uendeshaji wa Azania Bank, Jane Chinamo mapema leo Jijini Dar es salaam.
Wanahabari wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya AMSHA NDOTO


 Benki ya Azania (ABL) leo imetangaza uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina, ‘Amsha Ndoto’ yenye lengo la kuwahamasisha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili waweze kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.

Kampeni itaendeshwa kwa miezi mitatu, kuanzia 27 Juni 2019 hadi 27 Septemba 2019 na itahusisha wateja wa zamani na wapya ikijikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti(kwa ajili ya kila mmoja) na Watoto Akaunti(kwa ajili ya watoto tu).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa ABL, Charles Itembe, Ili kustahili kupokea zawadi, wateja wanapaswa kuwa na akiba yenye thamani ya TZS 1,000,000 kwenye akaunti zao na kuendelea ili kuwawezesha kustahili kuingia kwenye fainali ya droo na hatimaye kuweza kushinda. Washindi wa 3 watapatikana kila mwezi. Kupitia kampeni hii wateja wataweza kujishindia mpaka mara mbili ya kiwango walichoweka kwenye akaunti, ambapo kiwango hiki cha zawadi huweza kufikia mpaka Shilingi milioni Tatu

Akiongelea kuhusu vigezo vya washiriki, Itembe alisema kuwa wateja ni lazima waweke akiba ya kiasi cha TZS 500,000 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima, na wale watakaoweka akiba kiasi cha TZ 1,000,000 watapewa tokeni zitakazowawezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho itakayowapata washindi.

“Tunawahamasisha watanzania wote, wateja wetu wa sasa na wapya,wazazi na walezi kufungua akaunti hizi ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuongeza mitaji, kulipia kodi za pango na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye”, alisema Itembe, akigusia pia kuwa akaunti hizi zitakuwa fursa ya kuwahimiza kuweka akiba kwa ajili ya .

Promosheni hii, yenye kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde,tumuwezeshe ada ya shule’, itawasilishwa kupitia radio na mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn, Google Display placement na tovuti za ndani. ABL pia imetengeneza tovuti ndogo kwa wateja wapya kujiunga na inaweza kupatikana kupitia linki hii: amshandoto.com.

Masharti na vigezo kuzingatiwa

KAMPUNI YA TOL GASES LIMITED YATANGAZA KUTOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI MOJA KWA WANAHISA WAKE

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMPUNI ya TOL Gases Limited imetangaza kutoa gawio la Sh.bilioni moja kwa wanahisa wake ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo kwa kipindi ha miaka 20 tangu walipoingia kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE).

Hayo yamesemwa leo Juni 28,2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa TOL Gases Limited Daniel Warungu wakati wa Mkutano wa mwaka 2018 wa uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amefafanua kuwa kutokana na mageuzi makubwa ya kiuendaji ambayo yamefanyika katika menejimenti hivi sasa wamekuwa wakijiendesha kwa faida na kwa mwaka wa fedha wa 2018 wamepata faida ambayo imewezesha kuanza kutoa gawio ikiwa ndio mara ya kwanza kufanya hivyo tangu mwaka 1998 walipoingia kwenye Soko la Hisa.

"Kwa kweli hivi sasa tunajivunia kwani tunajiendesha kwa faida, na ndio maana leo tumekutana na wanahisa kutangaza kugawa gawio ambapo hisa moja ni Sh.17.37.Jumla ya gawio ambalo limetengwa kwa wanahisa ni Sh.bilioni moja.

"Tunawashukuru wanahisa wote, menejimenti na bodi ya wakurugenzi kwa namna ambavyo wameshirikiana kwa pamoja kuhakikisha kampuni yetu tunafanya vizuri kwenye kuuza bidhaa zetu katika soko,"amesema Warungu.

Pia amesema katika kuhakikisha wanapata faida walimua kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima na kuongeza uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na matokeo yake leo wanajipongeza kwa mafanikio yanayokwenda sambamba na utoaji wa hisa kwa wanahisa wote.

Kuhusu mikakati yao amesema ni pamoja na kununua mitambo miwili na kuongeza magari kwa ajili ya kusafirisha bidhaa katika nchi za SADC pamoja na Afrika Mashariki na kufafanua katika uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamasisha ujenzi wa viwanda umeisaidia kampuni yao kuongeza idadi ya wateja.

"Tunalo soko la uhakika ndani ya nchi ya Tanzania, lakini pia tunafanya biashara zaidi ya kuuza bidhaa zetu kwenye nchi mbalimbali za Afrika.Hivyo katika kufurahia mafanikio yetu , tunakwenda pamoja na kuweka mikakati ya kujiimarisha zaidi,"amesema Warungu.

Akizungumzia mkutano wa wanahisa amesema , umefanyika kwa mafanikio makubwa na wanahisa wameridhishwa na juhudi ambazo kampuni hiyo inafanya huku wakitoa ushauri na maoni ya namna bora ya kuendelea kutengeza faida kwa miaka mingi ijayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni hiyo Michael Shirima amewahakikishia wanahisa wote kuwa wamejiridhisha na utendaji kazi wa menejimenti ya sasa ambayo inafanya kazi vizuri na wameanza kuona matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

"Tunawapongeza menejimenti yetu, huko nyuma kwa miaka mingi hatukuwa tunafanya vizuri na ndio maana hatujapata gawio lakini safari hii tunapata gawio.Hata hivyo menejimenti tuliiuliza zaidi ya mara moja hili la gawio litakuwa kila mwaka au itakuaje.Wametujibu kuanzia sasa itakuwa ni kila mwaka kwani wanakwenda vizuri"amesema Shirima.

Shirima ametumia nafasi hiyo kueleza kampuni yao inafurahishwa na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyipo nchini na hivyo wataendelea kufanya kazi kadri ya uwezo wao kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kufanikisha kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda.
 Mwenyekiti wa  Bodi ya Kampuni ya TOL Gases Limited Michael Shirima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2018 wa wanahisa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 28,2019
 Mkurugenzi Mtendaji wa TOL Gases Limited Daniel Warungu(wa nne kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa mwaka 2018 wa wanahisa uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa TOL Gases Limited Daniel Warungu akifafanua jambo baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwaka 2018 wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
 Wanahisa wa TOL Gases Limited  wakiendelea kuchambua taarifa ya mkutano mkuu wa mwaka 2018 wa kampuni hiyo uliofanyika leo Dar es Salaam
 Baadhi ya wanahisa wa kampuni ya TOL Gases  Limited wakipitia taarifa ya mkutano wa mwaka 2018 wa wanahisa uliofanyika leo Dar es Salaam

RAIS DK. MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WABUNGE WA SADC NA SPIKA JOB NDUGAI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma ambao wameongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na wageni hao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya Tingatinga na Kinyago Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, alipokutana na na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya picha ya kuchora toka Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, huku akishuhudiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019 PICHA NA IKULU
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images