Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT. HASSAN ABBASI AIPONGEZA PSSSF KWA KUANZA VIZURI KUTEKELEZA MAJUKU YAKE

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MSEMAJI Mkuu wa serikali, Dkt. Hassan Abbasi ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuanza vizuri kutekeleza majukumu yake katika kipindi kifupi tangu kuunganishwa kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 15, 2019 ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati alipotembelewa na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, aliyefuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi.

Kwa takriban wiki nzima, Meneja huyo amekuwa kwenye ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ili kujenga mahusiano ikiwa ni pamoja na kueleza malengo ya Mfuko huo ambao ni mpya baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF kwa lengo la kuboresha utoaji huduma.

“Tunaposikia kuwa watu wameanza kupata mafao yao tena kwa wakati kwakweli ni jambo la faraja kwa serikali kwa hiyo mpeleke salamu zangu kwa watendaji wote, akiwemo mtendaji mkuu wa Mfuko, tunafarijika sana tunapoona kwamba yale malengo ya serikali kuu kuunganisha hii mifuko ili kutoa huduma bora yametimia.” Alisema.

Dkt, Abbasi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Malezeo, pia amempongeza Meneja huyo kwa uamuzi wa kuvitembelea vyombo vya habari kwa lengo la kuelimisha umma na kueleza shughuli za Mfuko kwani hii itasaidia wanachama kujua kinachoendelea kwenye Mfuko wao.

“Huu ni Mfuko mpya, yako maswali mengi yanayozua tashtiti na tashwishwi ambavyo kwa pamoja vinafanya kitu kinaitwa jakamoyo ambayo ni vile mtu anaumia moyoni kumbe anakuwa tu hana taarifa sahihi, hili nalo niwapongeze baada ya kukamilisha zile taratibu za ndani na kuhakikisha wale wastaafu wanapata kile kilicho chao sasa kazi kubwa ni kutoa elimu.” Amefafanua Dkt, Abassi

Aidha Dkt. Abbasi alitoa wito kwa wastaafu na wale wastaafu watarajiwa kutambua kuwa msingi wa pensheni ni kumuhudumia mfanyakazi anapokosa nguvu ya kufanya kazi, ama uzeeni au kutokana na kupata madhara mengine ambayo yatafanya akose nguvu ya kufanya kazi.

“Niwakumbushe watanzia kuwa tuweke pesa benki zile tunazohitaji kutumia leo, kesho au katika kipindi kifupi, lakini mafao ni kwa ajili ya kukusaidia katika maisha ya baadaye, si vema umetumikia nchi, jamii halafu baada ya kustaafu ukaishi maisha ya mashaka.” Aliasa.

Awali Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume alimweleza Dkt. Abassi kuwa amepata fursa ya kutembelea vyombo vya habari ili kujenga na kuendeleza mahusiano ikiwa ni pamoja na kuutambulisha Mfuko huo mpya kwa wadau wa sekta ya habari.

Alisema Mfuko ulianza kutekelez amajukumu yake Agosti 1, 2018 na ndani ya miezi 6 tangu Mfuko uanze kutekeleza majukumu hayo umeweza kulipa malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ile ya kila mwezi kiasi cha shilingi bilioni 880, lakini pia Mfuko unaendelea na zoezi la kuhakiki taarifa za wanachama (wastaafu) ambapo kati ya wastaafu 120,000, elfu 10,000 bado hawajahakikiwa.

“Kwa hiyo tumeeleza kuwa Mfuko umefungua ofisi nchi nzima bara na visiwani na kwa kila mstaafu ambaye bado hajahakiki taarifa zake afike kwenye ofisi ya PSSSF iliyo karibu naye ili atekeleze wajibu huo wa kisheria.” Alifafanua Bi. Chiume.
Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kushoto), akipeana mikono na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Dkt. Abassi jijini Dar es Salaam leo Juni 15, 2019. Bi. Chiume ambaye alikuwa katika ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii jijini Dar es Salaam, amehitimisha ziara hiyo kwa kufanya mazungumzo na Dkt. Abassi.
Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kulia), akizungumza na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, wakati Bi, Chiume alipomtembeleka Dkt. Abassi ofisini kwake jijini Dar es Salaam Juni 15, 2019. 
Dkt. Abbasi (kulia), akimsikiliza mgeni wake. Bi. Eunice Chiume ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Bi. Chiume akiziungumza.
Dkt. Abassi (kulia), akijadiliana jambo na Bi. Eunice Chiume, (katikati), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi ,mara baada ya mazungumzo yao.
Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kushoto), akipeana mikono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF bw. Abdul Njaidi.
Dkt. Abbasi akiwa na wageni wake, Bi. Eunice Chiume (katikati) na Bw. Abdul Njaidi kutoka PSSSF.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 16,2019

SERIKALI IMEPOKEA GAWIO LA SH. BILIONI 6.8 KUTOKA CRDB

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) akiwa ameshika hundi kifani ya Sh. bilioni 6.8 aliyoipokea kama gawio la Serikali kutoka Benki ya CRDB, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dkt. Khatibu Kazungu, kushoto ni Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar Jensen,  wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Bw. Ally Laay na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Abdulmajid Nsekela, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiipongeza Benki ya CRDB, kwa kuwa Benki ya mfano kwa kutoa gawio la jumla ya Sh. bilioni 10 kwa Serikali, mashirika na taasisi za umma zilizowekeza hisa zao katika Benki hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Bw. Ally Laay, akieleza kuhusu Benki yake kutoa mikopo katika mradi wa maendeleo wa umeme wa mto Rufiji na ujenzi wa Reli ya Kisasa yenye kiwango cha kimataifa-SGR, wakati wa hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali, mashirika na taasisi zake la Sh. bilioni 10 , katika ukumbi wa Wizara ya Fedha jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dkt. Khatibu Kazungu (kulia), Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar Jensen (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Bw. Ally Laay (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wengine baada ya Benki ya CRDB kutoa gawio la Sh. bilioni 10 kwa Serikali, mashirika na taasisi mbalimbali za umma, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Bw. Ally Laay, baada ya kupokea gawio kwa niaba ya Serikali, mashirika na taasisi mbalimbali za umma la Sh. bilioni 10, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Dkt. Khatibu Kazungu (kulia), akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela, baada ya hafla ya Benki hiyo kutoa gawio la Sh. bilioni 10 kwa Serikali, mashirika na taasisi mbalimbali za umma,  katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.

***************************

Na Farida Ramadhani na Peter Haule, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  imepokea kiasi cha shilingi bilioni 6.8 ikiwa ni gawio linalotokana na uwekezaji wa asilimia 21 za hisa katika Benki ya CRDB, ikiwa ni sehemu ya shilingi bilioni 10 ambazo benki hiyo imetoa kama gawio kwa mashirika na taasisi mbalimbali za umma zenye hisa katika Benki hiyo kutokana na faida iliyopatikana Mwaka 2018.

Makabidhiano ya mfano wa hundi za gawio hilo yalifanyika jijini Dodoma ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) alipokea gawio hilo kwa niaba ya Serikali na kukabidhi baadhi ya mashirika na taasisi za umma zilizopata gawio kutoka Benki hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Mpango, aliupongeza uongozi wa benki hiyo kwa kurudisha fadhila kwa mwananchi na kuzitaka benki na taasisi zote za fedha nchini kuiga mfano wa benki hiyo kwa maendeleo ya nchi.

“Benki ya CRDB na benki zingine muongeze jitihada ili kuongeza gawio kwa Serikali ili iweze kuwahudumia wanachi katika huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu na maji”,  alieleza Dkt. Mpango  
Alizitaka benki na taasisi za fedha kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa huduma za benki ili waweze kujikomboa kiuchumi na kuiwezesha nchi kupata gawio kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo.

Dkt. Mpango aliipongeza benki hiyo kwa kuwekeza katika teknolojia hasa katika matumizi ya Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroni (GePG) na kuzitaka benki na taasisi zingine za fedha kutumia mfumo huo.

Aidha, Dkt. Mpango alipongeza taasisi na mashirika ya umma yaliyopata gawio kutoka benki hiyo huku akizitaka Serikali za Mitaa nchini kuiga mfano wa Halmashauri za Lindi, Shinyanga na Mbinga ambazo zimepata gawio, ili ziweze kujiendesha na kukuza uchumi wa nchi.

“Serikali za Mitaa zinaweza kufanya njia nyingine mbadala za kujiongezea kipato kama hii ya kuwekeza kwenye Sekta ya fedha “, alisistiza .Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Bw. Ally Laay alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2018, Benki yake ilitengeneza faida ya shilingi bilioni 64.1 baada ya kukatwa kodi ikilinganishwa na faida ya sh. bilioni 36.2 iliyopatikana Mwaka 2017, huku akichagiza mafanikio hayo na matumizi ya mfumo wa Serikali wa malipo kwa njia ya kielektroniki (GePG).

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela Alisema CRDB imewekeza fedha kwenye mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji katika Mto Rufiji mkoani Pwani na kwamba benki yake iko tayari kuwekeza kwenye ujenzi wa miradi mingine ukiwemo  ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa (SGR).

Mashirika na taasisi za umma zilizopokea gawio ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF (Bil. 2.4), Mfuko wa Hifadhi ya Taifa-NSSF (Mil. 111.5), Mfuko wa Mafao kwa Wafanyakazi wa Serikali-GEPF (Mil. 56,7) , Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar-ZSSF (Mil. 6.5)

Mashirika na taasisi nyingine zilizopokea gawio hilo ambalo ni sehemu ya faida ya shilingi bilioni 21 baada ya kodi kwa mwaka 2018 ni  Mfuko wa Maendeleo Lindi -(Mil. 111.5, Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga (Mil. !.3), Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (Mil. 13.3 na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF (Mil.243.5)

Aidha, Chama cha ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi kimepokea gawio la shilingi mili

Benki ya Exim Yapewa Tuzo kwa Uchangiaji wa Damu Nchini

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim Tanzania Bw Stanley Kafu (Kulia) akipokea tuzo maalum kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ikiwa ni utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha suala la uhamasishaji na uchangiaji wa damu salama hapa nchini katika Maadhimisho ya Siku ya Wachangiaji Damu Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania kutoka makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo, Bw Arafat Haji (katikati) wakichangia damu katika Maadhimisho hayo.
Pamoja na wafanyakazi pia baadhi ya wateja wa benki hiyo walijitokeza kwa wingi makao makuu ya benki hiyojijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitolea damu.


  Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine Ulimwenguni katika kuadhimisha Siku ya Wachangiaji Damu Duniani, Benki ya Exim Tanzania imekabidhiwa tuzo maalum kutoka serikalini ikiwa ni utambuzi wa mchango  wa benki hiyo katika kufanikisha suala zima la upatikanaji wa damu salama hapa nchini. 

Benki hiyo imekabidhiwa tuzo hiyo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika Maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha mwishoni mwa wiki iliyopita yakiwa na kauli mbiu ‘Damu Salama Kwa Wote’ 

Akiipongeza benki hiyo kwa ushiriki wake mkubwa kwenye jitihada za upatikanaji wa damu salama hapa nchini, Waziri Ummy ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo pia aliihimiza benki hiyo kuendelea kuwa balozi imara wa damu salama hapa nchini sambamba na kuhamasisha taasisi nyingine na watu binafsi kuungana na benki hiyo katika kufanikisha mpango huo muhimu. 

“Serikali imetenga Sh. bilioni tano katika mwaka wa fedha 2019/20 zitakazotumika kujenga vituo vidogo vya uchangiaji damu salama katika mikoa 12 nchini.’’ Alisema Ummy ambae pia alizindua mashine mpya ‘full automation’ za kupima maambukizi katika damu na za kupima makundi ya damu ambazo zimesimikwa kwenye vituo vya kanda sita ikiwamo Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Kilimanjaro, Mtwara na Mbeya. 

“Tunataka kumfikia kila mtanzania mwenye mahitaji ya damu salama popote alipo tuhakikishe anapata damu salama bila kikwazo chochote. WHO inakadiria idadi ya watu 1000 zipatikane chupa 10 za damu, Watanzania tunakadiriwa tupo milioni 55 tunapaswa kupata asilimia moja ya idadi hiyo, hivyo chupa 550,000 zinahitajika kila mwaka kutosheleza mahitaji,” alisema. 

Akizungumza kuhusiana na tuzo hiyo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu alisema: "Benki ya Exim tumepokea tuzo na heshima hii kutoka serikalini kwa mikono miwili kwa kuwa ni sehemu ya matokeo chanya ya mkakati wa benki ya Exim ya uwajibikaji kwa jamii unaofahamika kama ‘Exim Cares’. Hivyo tuzo na heshima hii ni kama chachu ya sisi kuendelea kujitoa zaidi katika kufanikisha mpango wa damu salama hapa nchini,’’ alisema 

Kwa mujibu wa Bw Kafu, mapema mwezi huu benki hiyo kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) walianza utekelezaji wa pamoja wa mpango wa uchangiaji wa damu uliohusisha matawi yote ya benki hiyo hapa nchini hususani katika mikoa minane ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Tanga, Mtwara na Zanzibar. 

"Sisi ni mojawapo ya taasisi ambazo zinaendesha huduma zake katika sehemu kubwa ya nchi hii na huduma yetu inagusa idadi kubwa ya watu. Tunaguswa na jamii tunayoihudumia na tunaamini jamii yenye afya ni muhimu katika kutimiza malengo yetu. Na hiyo ndio sababu tumeelekeza rasilimali zetu pamoja na maeneo ya ofisi zetu kama kambi za kukusanyia damu,’’ alisema Kafu 

Benki ya Exim imeendelea kuonyesha uwajibikaji wake katika kusaidia sekta ya afya kupitia mipango mbalimbali na miradi ya kijamii. Katika miaka minane iliyopita benki imechangia zaidi ya chupa 1000 za damu katika Benki ya damu taifa.  



NMB KULIPA GAWIO LA SH. BILIONI 33

$
0
0

Benki ya NMB Plc. (NMB), kulipa gawio la Shilingi 66 kwa kila Hisa.

Wanahisa wa Benki ya NMB wameidhinisha kiasi kilichopendekezwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM), uliofanyika mwishoni mwa wiki  jijini Dar es Salaam.

Ikiwa ni matokeo ya utendaji bora na uimara wa nafasi ya mitaji, malipo ya jumla ya gawio la Shilingi Bilioni 33 (sawa na Shilingi 66 kwa kila hisa), yanafanana na sera ya benki ya kulipa moja ya tatu (asilimia 33.3) ya faida la jumla baada ya makato ya kodi (PAT) katika gawio. Hili ni ongezeko la asilimia 3 ukilinganisha na bei ya Shilingi 64 kwa kila hisa iliyolipwa mwaka uliopita. Nia ni kukuza kiwango cha gawio kwa kila hisa, kulingana na utendaji bora wa benki unavyoongezeka.

Benki iliripoti faida ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 142 kabla ya makato ya kodi (PBT), kwa mwaaka wa fedha ulioishia Desemba 31 2018; ambayo ni ongezeko la asilimia 3 kutoka faida ya Shilingi Bilioni 138 iliyopatikana mwaka uliotangulia. Licha ya mafanikio yaliyopatikana, Bodi na Uongozi wa Benki ya NMB umeridhishwa na aina ya mafanikio na mapinduzi chanya katika kipindi cha mwaka.

Mapinduzi hayo ni pamoja na uzinduzi wa NMB KLiK, mikopo ya mshahara - ambayo ni bidhaa ya kwanza ya benki kutoa mkopo kwa njia ya simu. Kuanzishwa kwa Mawakala zaidi ya 6800, wanaoshughulika – pamoja na mambo mengine, ukusanyaji na ulipaji wa kodi, ushuru na mapato ya Serikali za Mitaa katika Halmashauri 180, mapinduzi yanayochangia mzunguko wa pesa kwa mifumo ya kidijitali na kukuza amana. Pia tumeimarisha huduma za kibenki kupitia mtandao ilikuhudumia vizuri zaidi akaunti za makampuni na kuwapa suluhisho zote kamilifu na kufanya miamala ambayo imesababisha ongezeko la wateja kutoka milioni 2.2 hadi milioni 3.1 mwishoni wa mwaka 2018 .

Uimara wa NMB kama taasisi za fedha imepelekea Moody kuipa alama ya B1 ambayo vimethibitisha kuaminiwa kwa Benki ya NMB na wawekezaji wa kimataaifa. Benki imeimarishwa vema na uwiano wa mtaji kwa asilimia 16.5.Hiyo inamaanisha kwamba benki yetu iko salama kabisa kibiashara Mwenyekiti wa Benki, Prof. Joseph Semboja, anabainisha kuwa Bodi inataka kuweka sawa ongezeko la wanahisa, sambamba na kuimarisha biashara ya fedha ndani ya benki katika mpango mkakati wa kukua zaidi kiuchumi.

“Kwa miaka kadhaa sasa NMB imeendelea kuwa imara yenye afya kifedha, lengo ni kuendelea kuimarika zaidi na kubaki hivyo. Ili kufikia mafanikio haya, tunapaswa kuhakikisha tunafanya maamuzi sahihi hasa katika udhibiti wa mabadiliko kwenye mahitaji makuu ya kimtaji,” anasema Mwenyekiti.

“NMB imejipambanua katika kuendelea kusaidia harakati za maendeleo ya uchumi Tanzania na kuvuka kiwango cha sasa cha dira ya uchumi kama kichocheo cha ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi nchini. Tutaendelea kuwa vinara wa hudumaa bora kwa wateja wetu, huku tukiendelea kutimiza wajibu wetu kwa jamii,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw.

NMB imejitolea katika kusaidia ukuaji kiuchumi wa wajasiriamali wadogo na wakati (SME's), hususani wanawake kwa kuwapa mafunzo na elimu ya uwezeshaji katika kuimarisha biashara zao kwa kutambulisha jukwaa jipya la ‘Woman in Banking’ kote nchini. Katika kilimo, NMB tumeboresha jopo la wataalamu wanaojikita zaidi katika Sekta ya KilimoBiashara, ili kuimarisha mnyororo wa thamani unaopewa usaidizi mkubwa na Taasisi ya NMB Foundation, ambayo.

"Sisi ni Benki Bora Tanzania. Ubora wetu ni katika nyanja zote, za utawala, teknolojia ya habari na mfumo mzima unaoifanya NMB kuwa benki salama nchini, huku tukihakikisha amana na akiba zako ziko salama chini yetu," aliongeza. 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NMB  Albert Jonkergouw akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa  wanahisa wa Benki ya NMB uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana.
 

Dk. Kigwangalla kuchangisha fedha za kutokomeza VVU kupitia Mlima Kilimanjaro

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Khamis Kigwangala amesema anatarajia kuandaa utaratibu wa makundi ya watu mbalimbali wakiwamo viongozi mashuhuri na wasanii kupanda mlima Kilimanjaro ili kuchngisha fedha za kuendeleza mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi

Dk. Kigwangala ametoa kauli hivi karibuni mkoani Kilimanjaro wakati akizindua zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro lililoshirikisha zaidi ya watu 80 kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi kwa kupitia kampeni ya ‘Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge 2019’.

Kampeni hiyo ambayo iliyoratibiwa na Mgodi wa dhahabu ya Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kudhibiti Ukimwi nchi (TACAIDS) pia imelenga kutunisha mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF)

Alisema wizara ya maliasili na utalii itaanda utaratibu wa kuhamasisha makundi ya watu mbalimbali ikiwemo wasanii na watu mashuhuri duniani kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi kwani mapambano ya virusi hivyo ni ya watu wote na sio ya serikali pekee.

“Takwimu za maambukizi mapya hususan katika kundi la vijana yanatisha na kwamba zinahitajika jitihada za makusudi kutoka Katika kundi hilo kudhibiti ugonjwa huo.

“Hali ya maambukizi mapya ya VVU yanatisha ni lazima sisi Kama vijana tuwe msitari wa mbele kupambana na hali hii, kwa mwaka nimepanga kupanda Mlima huu na watu mashuhuri ikiwemo wanasiasa na wasanii ili kuchangisha fedha kwaajili ya kudhibiti ugonjwa huu.

“Lakini pia nimefurahi kuona kuwa miongoni mwa wanufaika wa kampeni hii ni wapagazi takribani 150 waliopatiwa mafunzo ya kujilinda na VVU na masuala mbalimbali kuhusu udhibiti wa Ukimwi. Kundi hilo pia limepatiwa mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kuwasaidia wawe na kipato endelevu,” alisema.

Aidha, Mkurugenzi wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko, alisema kila siku watu zaidi ya 200 huambukizwa VVU ambapo Kati yao asilimia 80 ni vijana kwanzia miaka 15-24.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Richard Jordinson, kampeni hiyo imewezesha ukusanyaji wa zaidi ya Sh bilioni 13 tangu ilipoanzishwa miaka 17 iliyopita.

Alisema kampeni ya mwaka huu zaidi ya watu 80 wameshiriki ambapo kati yao 32 watapanda mlima, 28 watauzunguka kwa kutumia baiskeli na watu 17 kutoka nchi mbalimbali wameshiriki kampeni hiyo ya kupanda mlima Kilimanjaro.

“Upandaji huo utachukua siku saba ambapo wameanza kupanda Juni 15 na kushuka Juni 22 mwaka huu,” alisema Alisema tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo miaka 17 iliyopita zaidi ya taasisi binafsi na mashirika 50 yanayotoa misaada na elimu ya Ukimwi nchini yamenufaika na kampeni hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii. Dk. Hamis Kigwangalla (wa pili kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi na washiriki wa kampeni ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kukusanya fedha za kutomomeza VVU nchini. Kampeni hiyo iliyodumu kwa miaka 17 sasa imeratibiwa na Mgodi wa dhahabu GGM na Tacaids
Waziri wa Maliasili na Utalii. Dk. Hamis Kigwangalla (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Richard Jordinson katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kukusanya fedha za kutomomeza maambukizi ya VVU nchini. Zaidi wa wapandaji 80 wameshiriki kampeni hiyo inayoratibiwa na GGM kwa kushirikiana na Tacaids.
Baadhi ya washiriki wa kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro 'Kili challenge 2019' inayoratibiwa na GGM kwa kushirikiana na TACAIDS kwa lengo la kukusanya fedha za kutokomeza maambukizi ya VVU na Ukimwi nchini. Zoezi la upandaji mlima huo limezinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla.

KANISA la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania (EAGT), limfungulia kesi mwenyekiti wao wa udhamini

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

KANISA la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania (EAGT), limemfungulia kesi katika baraza la ardhi mtoto wa marehemu, Mchungaji John Mfuko aliyekuwa Mwenyekiti wa wadhamini wa kanisa hilo, Frida Mfuko kwa madai kuwa amevamia eneo lililopo katika kiwanja namba 154 Kitalu II kilichopo Temeke.

Kesi hiyo yenye namba 127/2019, imefunguliwa na kanisa hilo katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Temeke mbele ya Mwenyekiti wa Baraza hilo, Amina, ambapo mdai namba moja ni EAGT.

Mbali na dhehebu hilo, wadai wengine waliofungua kesi hiyo ni Mchungaji Sara Samson, Wilbroad Adebe na Enosi Ndembeta ambao ni wazee wa kanisa liliko katika eneo linalogombaniwa, ambapo wote wanadai kuwa Frida amevamia eneo hilo.

Kesi hiyo, inatarajiwa kuanza kusikilizwa Julai 19,2019 ambapo Sara na wenzake waliwasilisha zuio wakiomba isikilizwe chini ya hati ya dharura huku Frida akiomba apewe muda wa kuwasilisha utetezi wake.

Aidha, kabla ya kesi hiyo kupelekwa mahakamani, viongozi wa jimbo wa EAGT walifika katika eneo hilo linalogombaniwa na kumtangaza Mchungaji Samson kuwa mchungaji katika kanisa aliloliacha Marehemu Mchungaji John, jambo ambalo limekataliwa na waumini wa kanisa hilo.

Akizungumza hivi karibuni, Frida amesema baba yake ni mmoja wa waanzilishi wa kanisa hilo tangu 1993, baada ya kutokea kwa mgogoro katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) ambapo baba yake, Marehemu Mchungaji Mfuko alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa EAGT hadi pale kifo kilipomkuta Agosti Mosi, 2018.

Amesema Mei 5,2013 wajumbe watatu wa bodi ya wadhamini walikaa kikao na kuidhinisha kuwa kiwanja hicho si mali ya EAGT bali ni mali ya Marehemu Mchungaji John Mfuko na hivyo,wadhamini waliaamua kumilikisha kiwanja hicho. 

"Baraza la wadhamini lilifanikiwa kuandaa nyaraka za kubadilisha hati ya kiwanja hicho na kumilikisha rasimi marehemu na hivyo hati ya kiwanja ikabadilishwa kutoka jina la The Registered Board of Trustees Of EAGT, na kuwekwa jina la Rev John Henry Mfuko mmiliki halali wa kiwanja hichi na shule iliyopo katika kiwanja hicho ambayo pia imesajiliwa kwa jina la marehemu", alisema Frida 

Ameongeza, kabla ya kufariki baba yake alikuwa akihoji viongozi wakuu wa kanisa la EAGT kuhusu tuhuma za kuingiza magari nchini kwa kutumia jina la EAGT ikiwa magari hayo hayapo ndani ya umiliki wa EAGT na ukiwa kuna ukwepaji wa kodi ya Serikali

Aidha, watoto wa marehemu wamelaani kitendo hicho cha kutaka kuwafukuza na kuwanyanganya mali ya baba yao ikiwa viongozi wa EAGT wanajua fika kuwa kiwanja kile pamoja na majengo yaliyopo na shule ni mali ya marehemu Mchungaji Mfuko.

Serengeti Breweries yatangaza mabadiliko ya uongozi wa juu

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini, Serengeti Breweries Limited (SBL) imemteua Mark Ocitti kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya kuchukua nafasi ya Helene Weesie anayeondoka.

Helene amekuwa na SBL kwa miaka minne kuanzia mwaka 2015, kipindi ambacho kampuni imeweza kuzindua bidhaa muhimu zilizosababisha ukuaji wa biashara kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kampuni kupata tuzo za ubunifu na kuongezeka kwa uwekezaji. 
 
Helene anaondoka kwenda kuchukua nafasi nyingine ndani ya Diageo barani Ulaya. Akiwa nchini Tanzania atakumbukwa, bali na mambo mengine, kwa kuibua na kuendeleza vipaji vya ndani ya nchi.

Mkurugenzi mtendaji mpya, Mark Ocitti, kwa sasa anahudumu katika nafasi sawa na hiyo katika kampuni ya Uganda Breweries Limited (UBL) ambayo pia ni sehemu ya kampuni mama ya East Africa Breweries Limited (EABL) inayoongoza kwa uzalishaji wa vinywaji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ocitti, chini ya uongozi wake, UBL imeweza kupiga hatua kubwa katika utendaji wake na kupelekea kukua kwa biashara.

Akizungumzia uteuzi wa Ocitti, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa EABL, Andrew Cowan amesema: “Mark amefanya mageuzi makubwa katika biashara yetu nchini Uganda; ameongeza nafasi yetu kiushindani na kukuza faida ya UBL kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Sina shaka kwamba kutokana na uzoefu wa uongozi wa Mark, maono, pamoja na mipango mikakati yake shupavu, itaifanya biashara ya SBL, inayokua kwa kasi kukua hata zaidi.”
 


SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA MASHINE 62 ZA KUSAFISHIA DAMU KWA WAGONJWA WA FIGO

$
0
0
Na WAMJW- DSM 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yaendelea kusogeza huduma za matibabu ya figo kwa kupokea  mashine 62 za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo na kuzisambaza katika Hospitali za Rufaa za mikoa nchini.

Hayo yamejiri mapema leo katika tukio la kupokea mashine hizo kutoka kwa kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief wakiongozwa na ubalozi wa Saudia Arabia nchini zenye jumla ya shilingi Bilion 1.55, lililoongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Dkt Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea kusambaza na kuboresha huduma hizi na kwa sasa zinapatikana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya KCMC na baadhi ya Hospitali binafsi.

"Sisi kama Serikali tumeendelea kuboresha hizi huduma, kwa sasahivi zinapatikana Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya KCMC na baadhi ya Hospitali binafsi" alisema Dkt. Ndugulile 

Aliendelea kusema kuwa, Serikali inaendelea kuboresha huduma hizi licha ya kuwepo changamoto ya idadi kubwa ya wahitaji wa huduma hizi huku akidai kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuna mashine 42 huku zikifanyika sesheni tatu kwa siku, na zinafanyika kwa siku 6 katika kila wiki, 

Aidha, Dkt Ndugulile amesema kuwa, msaada huo wa vifaa vitavyosambazwa katika mikoa tisa nchini ikiweko mikoa ya Tanga, Mwanza, Kigoma, Kagera, Arusha, Iringa, Mtwara, Unguja na Zanzibar, hali itayosaidia kupunguza gharama kwa kuwasogezea wagonjwa huduma hizo.

Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema kuwa ndani ya miaka mitatu Serikali imefanikiwa kupunguza magonjwa yakuambukiza kwa asilimia 50%, huku akikiri kuwa bado kuna changamoto kubwa katika kukabiliana na magonjwa yasiyo yakuambukiza kama vile kisukari, presha na figo ambayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na mitindo ya maisha.

"Tumepiga hatua kubwa sana katika magonjwa yakuambukiza, ambayo tumeyapunguza kwa asilimia 50% ndani ya miaka mitatu, tumepunguza vifo na maambukizi ya Malaria, lakini tumepunguza vile vile maambukizi ya Ukimwi, sasa changamoto inayotukabili ni magonjwa yasiyo yakuambukiza kama, kisukari, presha na magonjwa ya figo"alisema Dkt Ndugulile. 

Akiongea kwa niaba ya kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Naibu Balozi wa Saudia Arabia nchini Ahmed Bin Saleh Alghamdi ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa jitihada inayoendelea kuchukua katika kutatua changamoto kwenye Sekta ya Afya na ameahidi kuendeleza ushirikiano huo baina ya nchi hizo mbili.
 Baadhi ya mashine za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo zilizotolewa na kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief kwa kuongozwa na ubalozi wa Saudia Arabia nchini, zilizopokelewa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akimshukuru Naibu Balozi wa Saudi Arabia baada ya makabidhiano ya mashine 62 za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo, tukio limefanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile akiteta jambo na Naibu Balozi wa Saudi Arabia Bw. Ahmed Bin Saleh Alghamdi wakati wa makabidhiano wa mashine 62  za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo zilizotolewa na kituo cha King Salman  Humanitarian and Relief, tukio  limefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Naibu Balozi wa Saudi Arabia nchini Bw. Ahmed Bin Saleh Alghamdi akisaini mkataba wa makabidhiano wa mashine 62  za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo zenye thamani ya shilingi Bilion 1.55 zilizopokelewa Leo na Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa tukio la kupokea mashine 62  zakusafishia damu kwa wagonjwa wa figo, tukio limefanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara wahakikishiwa usalama katika Biashara zao.

$
0
0
MKUU wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Jumanne Murilo amewahakikisha usalama wa pesa na mali zao.Akizungumza na  wafanyabiashara katika Jukwaa la business club,Jeshi lake limejipanga imara kuhakikisha wanafanyabiashara hawasumbuliwi na wahalifu.

 Aliwaomba wafanyabiashara mkoani hapa kuhakikisha wanatumia vyema jukwaa la Business Club katika kuhakikisha wanajenga uchumi imara wa nchi.
'"tumejipanga na tunapambana kuzuia uhalifu kabla haujatokea kuliko kukabiliana nao ukishatokea " Murilo alisema.

Alisema wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi bali wahakikishe wanafanya biashara zao kwa uhuru kwakuwa jeshi lake limejipanga vyema kuhakikisha hakuna masuala ya uhalifu.Kwa upande wake,mkuu wa kitengo cha Biashara cha benki ya NMB makao makuu,Donatus Richard alisema benki yao itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kupitia ‘Business Club’

Alisema kupitia elimu watakazokuwa wanatoa kwa wafanyabiashara zitakuwa zikiwasaidia sana wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku.Donatus alisema kwa sasa benki yao itaendelea kuwa karibu na wateja wao na alisema wataendelea kutoa mafunzo mbali mbali kwa wateja wao yakiwemo masuala ya masoko pamoja na kodi.

Alisema semina zao pia zimewasaidia wateja wao kuwa karibu na wateja wenzao ambapo jambo linalodumisha uhusiano mwema katika ufanyaji biashara zao.

Alisema kwa sasa benki yao ipo katika mikakati ya kuwapeleka wafanyabiashara 10 nchini China kwajili ya kuwenda kujifunza mambo ya kibiashara katika tamasha la biashara litakalo fanyika nchini humo katika mwezi wa 10,mwaka huu.Mmoja ya wafanyabiashara,Kejja Misungwi alisema anaiomba benki ya NMB kuhakiksha wanaendelea kutoa semina za mara kwa mara kwa wateja wao jambo ambalo litawasaidia wateja kupata elimu za biashara zitakazowawesha upatakinaji wa faida katika biashara zao.
Mkuu wa kitengo cha Biashara wa NMB Makao Makuu Donatus Richard, akizungumza na wajasiliamali na wafanyabiashara ambao ni wajumbe wa NMB Business Club ya mkoani Mwanza, wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo wajumbe hao,kushoto ni Mwenyekiti wa Club hiyo anayemaliza muda wake Mathiasi Rwechungura na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Godfrey Mzava. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro, akizungumza na wajasiliamali na wafanyabiashara ambao ni wajumbe wa NMB Business Club ya mkoani Mwanza, jinsi walivyojipanga kuwalinda watu,mali na biashara zao wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo wajumbe hao,kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Godfrey Mzava na Mkuu wa kitengo cha Biashara wa NMB Makao Makuu Donatus Richard(kulia).
 

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AKUTANA NA WAWEKEZAJI TOKA UTURUKI

$
0
0
Balozi wa Uturuki akimkabidhi Waziri wa Viwanda zawadi ya mojawapo yabidhaa zinazotengenezwa Uturuki kwa niaba ya ujumbe wa wafanyabiashara

Mheshimiwa Innocent Bashungwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara
pamoja na balozi wa Uturuki

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akizungumza naujumbe wa wafanyabiashara toka nchini Uturuki. Pembeni yake ni Balozi wa Uturuki nchini Mhe Ali Davutaglu

Wafanyabiashara wakimsikiliza kwa makini akiwaeleza kuhusu faida za kuwekeza nchini

………………..
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amekutana na ujumbe wa
wafanyabiashara toka nchini Uturuki katika ofisi za Kiuo cha Uwekezaji
(TIC). 

Ujumbe huo ulioongozwa na balozi wa Uturuki nchini Mheshimiwa Ali
Davutaglu ulihusisha wafanyabiashara wa sekta za ujenzi, utalii, chakula na
viwanda mbalimbali. 

Wafanyabiashara hao walielezea sifa ya Tanzania kuwa na amani kama kivutio
cha wao kutaka kuwekeza nchini na kusema wangependa kufungua ofisi
itakayokuwa kiungo baina ya wafanyabishara wa Uturuki na wale wa Tanzania. 

Mheshimiwa Bashungwa amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba Tanzania ni nchi salama na yenye mazingira rafiki kwa wawekezaji akiahidi kuhakikisha Wizara ya Viwanda na Biashara ikishirikiana kwa ukaribu na taasisi nyingine za Serikali itaharakisha taratibu zote zinazotakiwa ili waanze uwekezaji wao mapema iwezekanavyo. 

Pia aliahidi kuwakutanisha na wafanyabiashara wengine nchini ili wapate kufahamiana na kubadilishana ujuzi.

NAIBU KAMISHNA MKUU TRA ATEMBELEA BANDARI KAVU

$
0
0
Na Veronica Kazimoto

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo ametembelea bandari kavu ya Said Bakhresa (SSB-ICD) na African ICD ambapo amewataka Maofisa Forodha wa Mamlaka hiyo kuzingatia uwajibikaji, weledi na uadilifu wakati wote wanapotimiza majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza na maofisa hao kabla ya kukagua mizigo iliyopo katika bandari hizo, Naibu Kamishna Mkuu huyo amesema kwamba, uzingatiaji wa maadili katika sehemu za kazi utasaidia kuondoa malalamiko na kero kwa walipakodi ambao ni wadau wakuu wa TRA.

“Jukumu la kujenga taswira ya mamlaka ni la kila mtumishi wa TRA. Hivyo, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anafanya kazi bila upendeleo, anawajali wateja ikiwa ni pamoja na kutumia lugha yenye staha, alisema Naibu Kaimshna Mkuu Mbibo.

Kwa upande wake Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Ben Usaje amewasisitiza watumishi hao kutojihusisha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaichafua Mamlaka ya Mapato Tanzania.

“Sote humu ndani tunajua kuwa, kupokea au kutoa rushwa ni kinyume cha sheria ya nchi yetu na yeyote atakayebainika akifanya hivyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Hivyo, hakikisheni mnaepuka kabisa vitendo hivyo vya rushwa kwani vitawasababishia kupoteza kazi na kufikishwa mahakamani”, alisema Usaje. 

Baadhi ya majukumu ya Ofisi za Forodha zilizopo katika bandari kavu hapa nchini ni kuhakikisha kuwa taratibu zote za kuingiza mizigo ndani ya nchi zinafuatwa pamoja na kuhakikisha kwamba kodi stahiki inalipwa na wenye mizigo kabla ya kutoa mizigo yao katika bandari hizo.
 Meneja wa Bandari Kavu ya African ICD, Abeid Said (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu bandari hiyo kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo (wa pili kushoto aliyevaa tai ya mistali) wakati alipotembelea bandarini hapo.
 Afisa Forodha Mfawidhi wa Bandari Kavu ya African ICD, Brian Japheth akitoa maelezo juu ya mizigo iliyopo bandarini hapo kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msafiri Mbibo (wa pili kulia) wakati alipoitembelea bandari hiyo. Kushoto kwake ni Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Ben Usaje.
 Afisa Forodha Mfawidhi wa Bandari Kavu ya Said Bakhresa (SSB-ICD), Caleb Mwangalaba akitoa maelezo mafupi kuhusu bandari hiyo kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msafiri Mbibo (kushoto) wakati alipoitembelea bandari hiyo kuona jinsi inavyofanya kazi.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msafiri Mbibo (aliyevaa tai ya mistali) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Forodha waliopo katika bandari kavu ya African ICD wakati alipoitembelea bandari hiyo. Kushoto kwa Naibu Kamishna Mkuu ni Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Ben Usaje na kulia kwake ni Naibu Kamishna wa Biashara na Uwezeshaji, Godfrey Kitundu. 

Vodacom yazindua duka jipya jijini Tanga

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Kampuni ya Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. . Uzinduzi wa duka hilo ni miongoni umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja katika mikoa mbalimbali nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martin Shigella (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (mkono wa kulia wa mkuu wa mkoa) wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. Uzinduzi wa duka hilo ni miongoni umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja katika mikoa mbalimbali nchini. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Vodacom shop, Micheal Mtawali.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella (Kushoto) akisimkiliza Meneja wa Vodacom Mkoa wa Tanga, Fadhili Linga, (kulia) wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. Aliyesimama katikati ni Meneja wa Vodacom Kanda ya kaskazini, Brigita Stephen. Uzinduzi wa duka hilo umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja wake katika mikoa mbalimbali nchini.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Vodacom na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella (Wanne kutoka kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. Watatu kutoka kulia ni Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen. Uzinduzi wa duka hilo ni miongoni umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja katika mikoa mbalimbali nchini.

ROTARY CLUB UDSM MLIMANI WAPATA RAIS MPYA DK HERI TUNGARAZA

$
0
0
UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI: Rais Mpya wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Dk Heri Tungaraza (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu Lulu Tunu Kaaya (kulia) wakionyesha ishara ya upendo mara baada ya Bi. Catherine Njuguna wa Rotary Club Dar es Salaam Mikocheni (katikati) kumaliza zoezi la makabidhiano kumalizika.
Rais Mpya wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Dk Heri Tungaraza (kushoto) akizungumza machache mara baada ya kutangazwa kuongoza kwa muda wa mwaka mmoja.
Rais Mstaafu wa Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Lulu Tunu Kaaya akizungumza wakati wa halfa ya kumsika Rais Mpya Dk Heri Tungaraza.
Mwanachana wa Rotary Club  Dar es Salaam Mikocheni, Bi. Catherine Njuguna wa Rotary Club Mikocheni (kushoto) akiongea na na Rais Mstaafu Lulu Tunu Kaaya (kulia).
Akivalishwa...
Rais Mstaafu wa Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Lulu Tunu Kaaya (kushoto) akikabidhiwa zawadi na Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi (kulia).
Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi akitoa zawadi.
Wanachama wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam wakipata burudani.
Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi (kushoto) na Edwin Mashayo (kulia).
Rais Mpya wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Dk Heri Tungaraza akimkabidhi zawadi Mwanachana Prof. David Mfinanga ikiwa ni heshima ya kuweza kuifanya club ya UDSM Mlimani kusonga mbele.
Mwanachana wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam Prof. David Mfinanga akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa zawadi.
 Mwanachama wa Rotary Club Catherine Dar North Club akizungumza machache.
Mwanachama wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam Mona Mwakalinga.
Mwanachama wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam Adolpho Mascharenas akizungumza machache.
Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi akitoa wosia kwa uongozi mpya.
Picha ya pamoja na Rais Mpya...
Wanachama wakibadirisha mawazo.
Burudani ikiendelea...
Picha ya pamoja na rais Mpya.

Waziri Kabudi akutana na Balozi Al - Mashaan

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait anayeshughulikia masuala ya Afrika, Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan.

Pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu jinsi ya kuboresha mahusiano yaliyopo katika kati ya Tanzania na Kuwait, nchi ya Kuwait imekuwa ni kati ya wadau muhimu wa Maendeleo hapa nchini kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait(Kuwait Fund). 


Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan
Balozi Mubarak Mohamed Al -Sehaijan pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwait nchini wakisikiliza kwa makini mazungumzo hayo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan (hawapo pichani)
Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan naye akimweleza jambo  Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.)
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan (hawapo pichani)
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan, Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohamed AlSehaijan (wa pili kutoka kulia) pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwaiti na Afisa Mambo ya Nje Bw. Odilo Fidelis (wa pili kutoka kushoto)

TANZANIA YAWAHAKIKISHIA MAZINGIRA BORA WAWEKEZAJI WA KIMAREKANI NCHINI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia wakati wakufunga Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani, ulioandaliwa na Ubalozi wa Marekani Uliopo hapa nchini kwa kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania, ambapo alieleza kuwa Tanzania kwa sasa kuna mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji. Aidha, aliezea kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, imeweka usawa kwa kuwasikiliza wawekezaji wa Ndani na wawekezaji kutoka Nje. 

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akipokea nakala za vitabu vya bajeti ya serikali kutoka kwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ili kujionea mabadiliko ya uwekezaji nchini yalivyoboreshwa.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akimsikiliza kwa makini Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wakifuatilia kwa makini mambo yaliyokuwa yakielezwa na Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi K. Patterson naye akizungumza kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Sehemu ya wageni waliohudhuria kwenye mjadala huo, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Marekani na Ulaya Bw. Jestas Nyamanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki (Mb.) naye akihutubia kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Mhe. Godfrey Mwambe naye akielezea namna kituo hichi kilivyoboresha na kinavyoshirikiana na taasisi nyingine katika kuhakikisha mwekezaji anapokuja nchini hapati shida. 
Juu na Chini ni Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Bw. Godfrey Mwambe (hayupo pichani).


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi K. Patterson 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (wa kwanza kilia)
Prof. Palamagamba John Kabudi, Mhe. Angela Kairuki pamoja na Dkt. Faraji Mnyepe wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa Mjadala wa kwanza wa kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria kwenye mjadala huo

TASAF YAWAJENGEA UELEWA VIONGOZI KUHUSU MAJARIBIO YA UTAMBUZI WA KAYA ZA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI SEHEMU YA PILI MKOANI MTWARA.

$
0
0
Na .Estom Sanga-Mtwara. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeanza mkakati wa kuwajengea uelewa viongozi ,Watendaji na Wawezeshaji katika ngazi ya halmashauri za Wilaya juu ya zoezi la utambuzi wa Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini ili kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa ufanisi mkubwa . 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kilichofanyika mjini Mtwara, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,bwana Ladislaus Mwamanga amesema zoezi hilo linakusudia kuboresha mapungufu yaliyojitokeza kwenye sehemu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango huo inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni na kuwa majaribio hayo ambayo kwa kiwango kikubwa yatatumia njia ya mfumo wa kompyuta yatafanyika katika Halmashauri za wilaya ya Siha,Mtwara na Tandahimba. 

Bwana Mwamanga amesema baada ya kukamilika kwa majaribio hayo, kazi ya kutambua Kaya za Walengwa watakaojumuishwa kwenye Mpango itafanyika nchini kote ili kutekeleza maagizo ya Serikali ya kujumuisha maeneo yote kwenye shughuli za Mpango. Katika Awamu ya Kwanza ya Mpango serikali kupitia TASAF imeweza kutekeleza Mpango huo kwa asilimia 70 ya mitaa/vijiji/shehia na hivyo asilimia 30 iliyosalia itakamishwa katika sehemu ya pili ya Mpango itakayotekelezwa kwa takribani miaka mitano ijayo. 

Akifafanua Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mkazo mkubwa katika sehemu ya pili ya Mpango imewekwa zaidi katika kuhamasisha Walengwa wa Mpango kufanyakazi kwenye miradi ya Maendeleo watakayoiibua na kisha kulipwa ujira ili waweze kujiongezea kipato na kupunguza adha ya umaskini. 

“…tumeweka mkakati bora zaidi ya kutekeleza maagizo ya serikali ya kupunguza dhana ya Walengwa wa Mpango kuwa tegemezi” amesisisitiza bwana Mwamanga. 

Amewahimiza Viongozi,Watendaji na Wawezeshaji kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya utambuzi wa Kaya za Walengwa ili kuondoa uwezekano wa kaya zenye uhitaji kutojumuishwa kwenye Mpango na hivyo kuondoa manung’uniko baada ya kuanza kwa sehemu ya pili ya Mpango unaotarajiwa kuzifikia takribani Kaya milioni 1.3 ikilinganishwa na Kaya Milioni 1.1 zilizoandikishwa katika sehemu ya Kwanza. 

Bwana Mwamanga amesema kutokana na usimamizi thabiti wa Serikali katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, kumekuwa na mafanikio makubwa kwa Kaya za Walengwa kuanza kuboresha maisha yao huku sehemu kubwa ya kaya hizo zikitumia fursa ya kuwemo kwenye Mpango kuanzisha shughuli uzalishaji mali jambo ambalo amesema limeendelea kuvutia Wadau mbalimbali wa Maendeleo kutaka kuchangia zaidi raslimali fedha na Utaalam. 

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara bwana Evold Mmanda amesema TASAF kwa kiwango kikubwa imekuwa kielelezo bora cha kuwafikia wananchi wanaoendelea kuishi katika mazingira ya umaskini kutokana na namna Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini walivyotumia fursa hiyo kupunguza athari za Umaskini. 

Bwana Mmanda amewataka viongozi katika maeneo ya utekelezaji wa shughuli za Mpango kuendelea kuwahamasisha wananchi kuuchukia umaskini kwa vitendo jambo ambalo amesema linawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF(aliyesimama) akizungumza kwenye kikao kazi cha viongozi ,watendaji na wawezeshaji wa majaribio ya utambuzi wa Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika  Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evold Mmanga (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao kazi cha viongozi ,watendaji na wawezeshaji wa majaribio ya utambuzi wa Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika  Mtwara.
 Mtaalamu wa Mafunzo na Uwezeshaji wa TASAF Bi. Mercy Mandawa akitoa maelezo katika kikao kazi cha viongozi,watendaji na wawezeshaji kuhusu utekelezaji wa majaribio ya utambuzi wa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
 Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha kujenga uelewa wa uetekelezaji wa majaribio ya utambuzi wa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini (picha ya juu na chini).

 Picha ya pamoja

MAKAMU WA RAIS AZINDUA HARAMBEE YA KUCHANGIA TIMU YA TAIFA STARS

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Hundi ya Shilingi Milioni 10 kutoka kwa Viongozi wa CRDB Bank ikiwa ni mchango kwa Timu ya Taifa Stars kwenye Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ilioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kuzindua Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ulioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye Jezi Mpya ya Timu ya Taifa Stars ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Jezi hiyo wakati wa Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ilioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachangiaji kwenye Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ilioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuzungumza na msemaji wa Timu ya Simba Haji Manara kwenye Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa Stars ilioyofanyika leo Juni 20, 2019 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 370 zilichangishwa hapo hapo.

Tigo na DStv wazindua kifurushi cha kuangalia michuano ya AFCON

$
0
0
 
Wafanyakazi wa Tigo pamoja na Dstv wakifurahi pamoja muda mfupi baada ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya hizo mbili utakaowawezesha wateja wao kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu.
Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh (kushoto) akiwa na Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo (kati kati) na Mtaalamu wa Huduma za Intaneni wa Tigo Allen Salaita wakipongezana baada ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. 



Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh na kulia ni Mtaalamu wa Huduma za Intaneni wa Tigo Allen Salaita.
Mkuu wa Huduma na bidhaa wa Tigo David Umoh (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni ya Tigo na Dstv utakaowawezesha wateja wa kampuni hizo kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vifurushi vya gharama nafuu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo na kushoto ni Mtaalamu wa Huduma za Intateni wa Tigo Allen Salaita.
 
Wateja wa Tigo na DStv sasa wataweza kufurahia mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika mubashara wakiwa sehemu yeyote na kwa muda wowote, baada ya makampuni haya mawili kuzindua ushirikiano maalum na mahususi ya huduma ya DStv itakayowapa wateja wake fursa ya kutazamaa mechi hizo kupitia DStv Now mobile App kwa gharama nafuu. 

Akizungumzia na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, tMkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema ushirikiano huo na DStv unaendana sambamba na lengo la kampuni hiyo kukuza maisha ya kidijitali kwa kila Mtanzania. . 

“Tunayofuraha ya kuzindua huduma hii maalum ya DStv Now itakayowapa wateja wetu wa Tigo katika msimu huu wa michuano ya Afrika kupata fursa nzuri ya kutazama mechi mtandaoni na kushuhudia timu yao pendwa ya Taifa Stars na timu nyingine zinazoshiriki mashindano haya makubwa barani Afrika,” alisema Umoh. 

Aliongeza, “Kupitia mtandao wetu bora wa 4G, tunaweza kuwahakikishia wateja wetu wanaotumia DStv fursa ya uhakika ya kuunganishwa mubashara na bila usumbufu wowote kuangalia Kombe la Mataifa ya Afrika, kutoka sehemu yeyote na muda wowote kupitia DStv Now App katika vifaa walivyonavyo. Hii ni fursa nzuri pia kwa wale wateja ambao kwa sababu mbalimbali hawatakuwa na nafasi ya kutazama kupitia televisheni zao.” 

Kwa mujibu wa Umoh, Tigo inawapa wateja wake waliounganishwa na DStv nafasi ya kuchagua vifurushi vitatu. Cha kwanza ni kifurushi cha GB 1.5 kwa gharama ya TSH 2000 kwa masaa 24, cha pili ni cha GB 6 kwa gharama ya TSH 7000 kwa siku 7, na kifurushi cha tatu ni ya GB 16 kwa TSH 20,000 tu kwa siku 30. 

Vifurushi hivi maalum na vya gharama nafuu kwa watumiaji wa DStv Now vinapatikana kupitia www.tigosports.co.tz, Tigo Pesa App, na menyu za *147*00# na *148*00#. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, alisema uzuri wa DStv Mobile app ni kwamba inaweza ikafanya kazi katika vifaa aina nne bila nyongeza ya gharama yeyote. 

“Hakutakuwa na gharama ya ziada kutazama DStv kupitia vifaa mbali mbali, kwa sababu gharama zote zinakuwa zimeshalipiwa katika kifurushi cha mwezi cha DStv. Ili kuweza kuangalia mechi za AFCON, wateja wa DStv wanachohitaji kufanya ni kupakua DStv App katika simu janja zao, kompyuta mpakato, tablet au vifaa janja vingine,” alisema Shelukindo. 

Uzuri mwingine wa kipekee ambao mteja anaweza kuupata kupitia huduma hii ni kuwa wateja wa DStv wanapewa uwezo wa kuunganisha hadi vifaa vinne tofauti kwa wakati mmoja kutazama vipindi vya DStv wakati huo televisheni nayo ikiwa nayo imeunganishwa na kuendelea kutumika kuangalia vipindi. 

Shelukindo aliongeza, “Kujiunga na DStv Now wateja wanatakiwa kutembelea now.dstv.com, na kufuata maelekezo ya kuweka jina na neno siri. Baada ya kumaliza hatua hiyo rahisi, watakuwa na uwezo wa kupakua na kuingia katika kifaa janja yeyote na taarifa zao walizoweka na kuanza kutazama mubashara vipindi.” 

Shelukindo aliongeza kuwa, mechi za AFCON zitakuwa zinaonyeshwa kupitia vifurushi vyote vya DStv kuanzia kifurushi cha bei ya chini kabisa mpaka kifurushi cha DStv Premium. “Wateja wa DStv katika vifurushi vyote watakuwa na uwezo wa kufurahia mechi zote 52 ya mashindano haya maarufu ya mpira. Ushirikiano wetu na Tigo umefanya maisha kuwa rahisi kwa sababu inatoa fursa kwa yeyote kufurahia mechi hizi popote pale,” alisema.
 

TANAPA YAWAKUMBUKA WADAU WA UTALII,YAWAPA TUZO WALIOFANYA VIZURI KATIKA UHIFADHI NA UTALII.

$
0
0
Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla akizindua mkataba wa huduma bora kwa mteja wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha .Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -Tanapa ,Kamishna Nsato Marijani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro. Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla akizindua amzezindua Mfumo a uendeshaji wa viwango vya kimataifa (ISO 9001:2015 Quality management system) wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha .Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -Tanapa ,Kamishna Nsato Marijani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro. Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa utalii wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group ,Joseph Kusaga ni miongon mwa waalikwa walioshiriki hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii. Makamishna wasaidizi wa TANAPA wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo. Kamishna Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya TANAPA,Kamishna Nsato Marijani akizungumza wakati wa hafla hiyo.


Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro akizungumza wakati wa hafla hiyo. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji (TBC) Dkt Ayoub Ryoba akiwa na Mkurugenzi wa Channel ten Jafary Aniu pia walikuwa ni miongoni mwa waalikwa katika hafla hiyo. Baadhi ya Makamishna wasaidizi wa Uhifadhi wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi -Mawasiliano TANAPA,Pascal Shelutete akitangaza utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo kwa wadau wa utalii.Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akiwa katika pich ya pamija na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group ,Joseph Kusaga ,Emilian Mallya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa tatu katika kutangaza hifadhi za taifa . Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji ,Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Ryoba (kushoto) ,Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro (kulia). Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adventure baada ya kuibuka mshindi wa Jumla kwa watoa huduma za Utalii katika Hifadhi za Taifa . Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mshindi wa jumla ,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Adventure pamoja na Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -TANAPA ,Kamishna Nsato Marijani na Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jeryy Muro. Washindi wa tuzo za Gold wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Malisili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla.



Na Dixon Busagaga .

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa mara ya kwanza limekabidhi tuzo kwa Wadau mbalimbali wa masuala ya Utalii na Uhifadhi ,tuzo zilizokabidhiwa na Waziri wa Malisili na Utalii jijini Arusha kwa lengo la kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika masuala ya Utalii na Uhifadhi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Maount Meru ,Waziri Dkt Kigwangalla pia amezindua Mfumo wa uendeshaji wa viwango vya kimataifa yaani ISO 9001:2015 Quality management system pamoja na mkataba wa huduma bora kwa mteja .

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na viongozi kutoka kampuni na taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya Utalii na Uhifadhi ,Mgeni rasmi ,Waziri ,Dkt Hamisi Kigwangala aliipongeza TANAPA kwa uamuzi wa kutoa tuzo kwa wadau wa sekta ya utalii hapa nchini.

“Niwapongezeni TANAPA ,Bodi ya wadhamini na Menejenti ya TANAPA mnafanya kazi nzuri sana hasa katika kuisimamia ipasavyo sekta ya utalii, Hongereni sana.”alitoa pongezi hizo Dkt Kigwangalla.

“Nampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwa kuweka mkazo kwenye sekta ya miundombinu na sekta ya anga kwani zimekuwa kichocheo katika ukuaji wa sekta ya utalii,niwahakikishie wadau wa Sekta binafsi katika sekta hii ya utalii, tutaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha lengo ni kuhakikisha tunakuza na kuendeleza sekta hii kwa kasi kubwa kabisa.”aliongeza Dkt Kigwangalla.

Dkt Kigwangalla alisema tuzo walizopata wadau wa sekta ya Utalii kwa kazi nzuri wanazoendelea kufanya ziwe chachu katika kuimarisha ushindani katika utoaji huduma bora katika sekta ya utalii ambapo zitasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu.

“Natoa wito kwa wadau wa sekta ya utalii kuwekeza katika maeneo ya usafiri na malazi kwenye maeneo ya Kusini na Magharibi mwa nchi yetu.”alisema Dkt Kigwangalla.Mjumbe wa Bodi ya TANAPA ,Kamishna Nsato Marijani aliyemwakilisha mwenyekiti wa bodi hiyo,Jenerali George Waitara alisema uzinduzi wa Mkabata wa Huduma kwa Mteja utawezesha utoaji huduma kwa Haraka, ufanisi na kwa wakati ili kuondoa malalamiko na urasimu usio na tija kwa pande zote mbili.

“Sisi kama Bodi tunaahidi kuendelea kusimamia sekta hii kwa kikamilifu ili iwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini.”alisema Kamishna Nsato.
Kwa upande wake KAmishna Mkuu wa Uhifadhi ,Dkt Allan Kijazi alisema TANAPA inatambua mchango mkubwa wa wadau wetu wote katika sekta ya utalii kwa jitihada zote wanazozifanya katika sekta hiyo ikiwemo kuiletea heshima nchi.

“ Tunathamini na tutaendelea kuthamini kila mdau anayefanya kazi na TANAPA,shirika limefanikiwa kuongeza ulinzi wa rasilimali zetu, tutaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwezesha kufikika kwa urahisi katika hifadhi zetu.”alisema Dkt Kijazi .

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa kampuni za Utalii nchini (TATO) Wilbert Chambulo ameishukuru TANAPA kwa tuzo hizo na kwmba shirika hilo limekuwa likijitoa kwa wadau wa utalii hali ambayo imechangia kampuni hizo kukua kiuchumi.

“TANAPA imebadilika sana.nakuahidi Mhe. Waziri Tutaendelea kulinda na kudhitibi uharibufu wa hifadhi zetu na nina kukabidhi magari mawili kwa ajili ya zoezi hilo”alisema Chambulo.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images